Asali ya limao
Member
- Dec 27, 2018
- 57
- 104
- Thread starter
- #61
"Watu hujifunza kutoka kwa makosa yao, lakini wengine hujifunza kutoka kwa makosa ya wengine………na Siri nyingi za gizani zinazofichwa ila zinapoanza kufichuliwa, kila mtu anakuwa na hatia.” Eeeeebbhna eeennhh kwani ina maana gani hii nukuu hebu tufunue pazia tuone kulikoni?
Endelea……..
"ila jeshi la polisi chini ya huyu mzee lilikuwa limepwaya Sana rushwa na dawa za kulevya zilikuwa kweupe, utekaji ndiyo usiseme ukija kwenye suala la utekaji ndiyo kabisa kikubwa tumuombee apumzike aendako huenda Mungu amesaidia kumuondoa." Aliongea kijana mmoja aliyeonekana kuwa makini kupitia Vichwa vingine vya magazeti.
"eebhana eeeennnhhh kumbe Kuna mauaji mengine nyumbani kwa Askofu wa kabisa la JEHOVAH AMESHINDA na yeye mwenyewe Askofu hajulikani alipo, nini kinaendelea" alizungumza yule kijana Tena.
*******
Haya yakiendelea nchini Tanzania, Burundi Hali ilikuwa hivyo hivyo huku magazeti Yakipambwa na picha ya bastola na pasi ya kusafiria ya Thobias Chumvinyingi huku kukipambwa na maneno ya kifaransa kuwa huyu ndiyo muuaji wa.mfanyakazi wa hoteli ya Roca Golf na anatafutwa na vyombo vya ulinzi na usalama, hasa idara ya ujasusi nchini humo SNR, huku akikolezwa kwa maandishi ya mtu hatari na jasusi kutoka Tanzania huku kukitolewa tahadhari kwa maeneo ya mkusanyiko wa watu wengi huku donge nono la dola 25000 zikiahidiwa kutolewa kwa atakaye fanikishwa kukamatwa kwake, hayo yote aliyaona kapteni Jumanne baada ya kuazima gazeti, safari haikuwa ndefu sana hatimaye daladala waliyokuwa wameipanda iliwasili kwenye mji wa Gatumba, mara baada ya kushuka hakutaka kuonekana kama mgeni haraka alisogelea maegesho ya Taxi na kumfata mzee mmoja aliyekuwa akisubiri abiria kwani hisia zake zilimtuma hivo.
"kijana wangu hujambo, tunaelekea wapi" alianzisha mazungumzo mzee yule huku akilitia moto gari lake moto kuingia barabarani
"sijambo msee, nipeleke belvedere tafadhari nkapate kifungua kinywa" aliongea kapteni Jumanne, rafudhi yake ilimfanya ageuze kioo cha katikati ili kumuona vizuri sura ya abiria wake akatabasamu.
"kwa mara ya kwanza tangu nianze kazi hii sikuwahi kupata abiria anayetoka katika taifa la kenya.......japo mama angu ni mtu wa huko na bahati mbaya alifariki tungali watoto wadogo na hatukufanikiwa kufika huko hata angalau tuwajue ndugu zetu wengine, ila kusikia sauti nimefarijika sana naitwa cliff sibomana" alimaliza na kutaja jina lake huku tabasamu lake likiwa lile lile, muda huo walikuwa wakiyapita majengo kadhaa ya jiji lile huku wakisindikizwa na mziki wa mahadhi ya hip hop kutoka kwa mwanamziki Tupac Shakur na kibao chake cha 'My block' kilichomfanya kapteni Jumanne atabasamu na kukumbuka maisha yake mtaani hasa pale kwenye mstari wa mwisho wa 'verse' ya pili " i close my eyes and picture home for my block"
"msee mbona ka iko wewe hufananii na hii mughizi"alisema hivo kapteni jumanne huku akitupa na swaga ili aendelee kuvuna pointi tatu kwa mzee huyo
"hahaha vijana tatizo mnahisi sisi hatupendezwi na mahadhi haya na nyie ndiyo mna haki ya kusikiliza, usisahau hata mimi nilikuwa kijana kama ulivyo, tena mimi huenda nilikuwa zaidiyako pengine, burundi hii nimeizunguka nikila bata kweli kweli, nilitaka kufika nairobi maana naskia ni jiji la raha na gharama afrika mashariki hii.....ila sikufanikiwa kwa sababu nilipata msala mzito ulinimaliza kila kitu nimedondokea huku kusogeza siku" alisema mzee yule kwa bashasha huku akimaliza kwa sauti ya masikitiko.
"pole sana mzee japo sijui kilichokupata ila inaonekana hakikuwa chema ila naamini kina kuhuzunisha kila ukikikumbuka" alisema kapteni jumanne kwa udadisi
"ni stori ndefu kijana wangu ila kiufupi nilifungwa jela kwa kosa lisilo langu na huwezi amini waliofanya hilo kosa walikuja kutoa ushahidi dhidi yangu na walinikandamiza kweli kweli nilibaki nikipigwa na butwaa kwenye kizimba mwisho wa siku nikaiona milango ya gereza na mimi kumezwa humo kwa muda wa miaka kumi na tano......maadam upo jiji hili siku moja ntakusimulia labda nkuachie anuani yangu kijana, alafu tushafika mg hahawa ndiyo huo hapo mbele." akampa kikadi kilichoonesha anuani ya mzee yule dereva taxi, na muda huo alikuwa ashafika katika mgahawa huo, wakaagana na kapteni Jumanne akisogelea moja ya Meza na muda uliofata alikuwa ameshaketi na mhudumu alikuwa mbele yake kupokea oda ya chakula kutoka kwa mteja huku akitumia lugha ya kifaransa ambayo ilijibiwa vizuri na kapteni Jumanne.
"karibu chakula kaka mzuri" aliuliza yule Dada kwa lugha Ile Ileya kifaransa huku akitabasamu.
"Asante Dada mzuri" alisema huku Akitabasamu huku sekunde ya pili akikivuta kijiko na kwanza kuishambulia supu Ile ya kuku na maandazi matatu yaliyokuwa kwenye sahani ndani ya dakika kumi alikuwa mbele ya Meza ya malipo.
"Samahani naweza kufanya malipo kwa kadi" aliuliza kapteniJumanne.
"bila shaka mashine ni hiyo hapo" kauli Ile ilikuwa kama taa yakijani kwa kapteni Jumanne, naye hakusita kuchanja kadi yake aliyokuwa ameisunda katika mahali ambapo palikuwa Salama zaidi hasa ukizingatia alitambua madhara ya safari za usiku, baada ya kupata kifungua kinywa Sasa mwili wake ulikuwa umeanza kurudisha utimamu wake kitu kilichobakia ilikuwa nikuondoa uchovu na kukutana na Thobias Chumvinyingi, alielewa kichwa chake kisha kuwa dili na kukutana maeneo ya watu itakuwa ngumu
"atakuwa wapi huyu mtu" alijiwazia kapteni Jumanne alichekecha akili kwa sababu hakuwa na Ramani ya wapi pa kuanzia. Suluhisho aliona akapumzike kwanza Kisha aanze kaziya kumtafuta mwenyeji wake
******
TSS HQ- DAR ES SALAAM
Saa 2:30 asubuhi
Ni asubuhi nyingine, ofisi hii ilikuwa na pilika pilika huku wanausalama katika ofisi hii walikuwa bize kiasi kwamba hakuna ambaye alikuwa amesimama bila kazi hata chifu mwenyewe ambaye ndiyo bosi wao alikuwa bize akitazama taarifa za mtu aliyefikishwa alfajili ya siku hiyo, faili hili lilikuwa na rangi nyekundu na yenye maandishi meusi yenye nyota tatu katikati, huku yakikolezwa na maandishi meusi 'TOP SECRET', Punde simu ya mezani ilitoa mlio kumaanisha kulikuwa na simu inaingia, akanyanyua mkono wa simu Ile na kuiweka sikioni huku umakini wake ukiendelea kutazama taarifa zilizomo ndani ya faili lile.
"samahani Chifu, kuna wageni wako wanahitaji kukuona" ilisikika sauti nyonyoro wa katibu muhtasi wake Mwanamama Caroline chakachaka.
"waambie waje saa 7 za mchana Sasa hivi Nina kazi na usisahau mheshimiwa raisi atakuwa hapa muda wowote" aliongea chifu huku akionekana kukereka.
"ni jenerali yuko na wale watu wa siku Ile" alisema Tena yule mwanamama mweupe wa rangi, macho makubwa, nywele kazitengeneza mtindo wa fidofido huku akibeba umbo la kuvutia ambalo kwa umri wake wa miaka 45 ni Nadra sana kumkuta nalo mwanamke wa umri wake, midomo mipana iliyowatoa udenda wavnaume kibao ila ndiyo hivo hawakuwa na namna ya kukubaliana na ukweli kwamba kujisogeza kwake ni kukisogelea kifo kwani mwanamke yule ni mke wa ndoa wa Chifu, miiko ya kazi ilikuwa pale pale na miaka yote aliyofanya kazi kama katibu muhtasi wa mkurugenzi wa idara ya ujasusi hakuwahi kuleta mazoea au majivuno kisa tu bosi ni mmewe.
"ooooohh waruhusu na waambie waingie tafadhari, Tena wamefika wakati muafaka" japo alikuwa kazini Ila kibinadamu roho yake ilisononeka kufoka Tena kwa mtu mzima kama yule, alimezea na alijua wapi ataenda kuomba msamaha na muda huohuo aliingia jenerali akiwa katika vazi lake nadhifu huku kofia yake ikipambwa na nyota nne, huku nyuma yake akifuatiwa na mtu aliyevaa suti nadhifu ya rangi ya bluu bahari kwa umbile alikuwa mwanamke ila tembea yake ilimsadifu ni mtu wa Aina gani hakuwa mwingine Bali ni Chausiku Deusi huku nyuma yake pande la mtu lilikuwa katika gwanda za jeshi, naam alikuwa katika gwanda zilizomtambulisha kama komandoo wajeshi la wananchi huku bawa la ndege katika kifua chake upande wa kulia lilisadifu kuwa mtu huyu amefuzu mafunzo ya juu katika medani za kijeshi, kofia ya zambarau na vyeo mabegani vilimsadifu kuwa yeye ni Nani? katika jeshi, kwa Hakika asubuhi hii alipendeza kiasi cha kumfanya chifu atabasamu, kwani hakutarajia kama angeshangazwa kiasi hiko, baada ya kufunga mlango wote walikakamaa na kutoa heshima mbele ya chifu mpaka jenerali na yote ni kwa sababu Chifu ni bosi wao wote.
"karibuni mketi.....niseme tu ugeni went umenipa faraja na niseme tu mmefika wakati sahihi" aliongea chifu huku akiwataza wote kwa umakini
"jenerali tangu mwanzo nilikueleza hii kazi ni ngumu na hapa nilikuwa napitia taarifa za huyu akofu wa kanisa la 'JEHOVAH AMESHINDA', aiseee taarifa zake zimenisisimua Sana yaani hapa nilikuwa nawaza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinakwama wapi mpaka kufumba macho na watu hawa kuifanya hii nchi kama ghetto Lao la kufanyia uchafu wao, Katika taarifa zilizomo humo ndani…….jenerali, watu wangu walioko idara ya uhamiaji wameweka rekodi Sawa kwamba Jamaa siyo raia wa nchi hii"
"whaaaaat!!!! Hebu chifu tuwekane Sawa kwenye Hilo" aliongea jenerali kwa kupigwa na butwaa ila pia katika namna ya kutafuta ufafanuzi.
"ni kweli kabisa Jamaa siyo raia wa nchi hii japo alivihadaa vyombo vya ulinzi na usala ila Jamaa ni mzaliwa halisi wa nchi ya............Ghrrrr Ghrrrrr......aaaahhh sorry ni simu yamheshimiwa raisi" aliongea chifu huku akipokea simu Ile iliyotoa maelekezo kuwa dakika chache kutoka pale angekuwaofisini kwa chifu na haikusubiri kujibiwa.
NIMEJIKUTA HATA MIMI NIKITAMANI KUJUA HUYU JAMAA NI RAIA WA WAPI? JE HII SIMU ILIYOINGIA HIVI SASA ITALETA TATIZO JIPYA AU INA KITU GANI?? TUKUTANE TENA TOLEO LIJALO.Tchao