Simulizi ya Kijasusi: Giza la Wasaliti

Simulizi ya Kijasusi: Giza la Wasaliti

"Tofauti kati ya mpelelezi mzuri na mpelelezi mbaya siyo kama wataweza kupata taarifa, bali ni kama wataweza kutoka hai."
Fredrick Forsyth (2010)
Nimeanza na nukuu hii inaweza isiwe na ukaribu sana na maana ya kipande hiki ila kadri utakavyokisoma ndivyo utagundua kwamba kazi ya ujasusi siyo kazi ya lelemama, ungana nami na unisome
Endelea………….
"mbona mmenigeuka dakika za mwishoni ndugu zangu, hata wewe Diane ni wa kunifanya hivi mbali na kuishi muda wote ulimwengu ukitambua mimi na wewe ni mke na mme haya ndiyo malipo, Mbali na kujifunika Shuka moja Leo unan..." Alikatishwa na Kofi Zito.
"nyamaza hanisi wewe umejifunika Shuka moja na Nani?.....hahahaha Revocatus Bigirimana umesahau kuwa tangu tumekaa pamoja hujawahi kusikia kilio changu kitandani Leo unataka nikusamehe fine nakupa ofa."aliongea mwanamke yule huku akimsogelea karibu
"nipe hiyo ofa na nitaitekeleza kikamilifu niko chini ya miguu yako" mwanamke yule alitabasamu Kisha akamtazama kuanzia juu mpaka chini
"una uhakika utaweza nitaka chokwambia ufanye" aliongea yule mrembo huku akiongea kwa madaha, wakati mazungumzo yakiwa yamepamba moto Richard alikuwa amekwisha ingia ndani kupitia mlango wa nyuma ambapo alikutana na maiti mbili za walinzi zikiwa hazina uhai akaendelea kunyata mpaka alipofika karibu na korido akanyanyua macho yake na kukutana na 'main switch' akatulia hapo
"ukisimamisha uume wako Sasa hivi mimi nitakuacha uishi ila ukishindwa utatangulia mbele za haki 'former Vice president na sijui ni Nani atakayetangaza kifo chako maana hakuna atakayekupa heshima yoyote siyo Congo ambao wameshakukana wala Tanzania, hivyo tuoneshe hapa wewe ni mwanamme kweli au Ashura mwenye ndevu" mstari huo wa mwisho uliyafanya majitu Yale yaliokuwa yamesimama kucheka kicheko Kikali Kisha yakawa yanamtazama kwa usongo, mtu yule jasho likamvuja huku akiwa Hana tumaini la kupona kabisa.
"hahahaha nadhani umeshindwa kuonesha jinsia yako hivyo kama makubaliano yetu yanavyosema una dakika moja ya kutubu dhambi zako half Men half woman" alisema huku akimtazama kwa tabasamu la kikatili na sekunde hiyo hiyo umeme kwenye nyumba ile ulizima na bila kusita mtu yule alijirusha kando huku mvua ya risasi ikimfata, huku miguno ya maumivu ikifuatia.
"madam go....go" alisema mmoja ya wale watu huku akiugulia maumivu katika shingo lake Mara baada ya kuchanwa na kitu chenye ncha kali.
"Hatoki mtu humu ila mnatakiwa kurudisha namba kwa aliyealeta duniani"
"hahahaha nakueleza wewe nyani mweusi hutamaliza dakika tano ukivuta pumz...." alikatishwa kauli mara baada ya risasi iliyotumwa kwenye kichwa cha yule bwana kuondoka na uhai wake alipotazama mbele alimuona aliyekuwa makamu wa raisi wa Tanzania huku akiwa anatetemeka kwa kukosa matumaini ya kupona alijikutaa anaropoka.
"naaaani wewe......."
"JOHNY WALKER" ilisema sauti kavu huku ikiwa imeweka umakini na mashaka kwamba kama siye mlengwa basi tahadhari zote zilichukuliwa
"umetumwa na Chifu kuhusu habari za kifo cha balozi Calistus Daniel Chacha......actually usistaajabu kwamba kwanini nilikuwa makamu wa raisi ila taarifa ninazo,nikweli kabisa mambo haya yametokea chini ya utawala wetu lakini nilitumwana shirika lenu la ujasusi kwa ajili ya kupata dondoo, ni bahati mbaya sana nilishindwa kupata taarifa kwa muda sahihi na kuzifikisha kwenu ila haikuwa bahati mbaya ilibidi yatokee ili wasiweze kushtuka kinachoendelea kwani unaelewa kabisa adhabu inayomhusu msaliti .
"kwanini unaniambia haya wakati bado unahesabiwa kuwa msaliti siyo kwa nchi yako au yetu? aliuliza tena ASP Richard.
"hahahah mimi ni wa kufa tu na sioni tthamani ya kuishi wale watu ni wanyama sana wamenifanya nisijue radha ya uchi wa mwanamke, tazama hapa ungechelewa dakika moja tu yule mwanamke asingesita kuni mwaga ubongo......tusipoteze muda ndugu yangu nnachojua ni vifo vya wale wafanyakazi wa ubalozi ila kuhusu balozi kifo chake bado ni fumbo zito, hao wengine wameuawa kwa kuchomwa na visindano vidogo vyenye sumu shingoni na kazi hiyo ilifanywa kwa weledi wahali ya juu na mabinti wazuri wa kike ambao wakipita mbeleyako hauchomoi nakwambia ndugu yangu na walipewa mafunzo na master mmoja wa kijapan anaitwa 'SHINJI NAGASAKI' kwa ushirikiano na 'EX SPY MASTER'
"whaaat......Shinji Nagasaki anahusikaje na hii mikasa kwahiyo na chifu mstaafu anahujumu taifa aliloapa kulilinda mpaka pumzi yake ya mwisho dah nauona ugumu kwenye hili" alilalama ASP Richard
"wala hakuna ugumu wowote ikiwa wote hao ni vijidudu tu ila kuna kiumbe anaitwa 'MEDUSA' huyo anaogopwa vibaya na watu ijapokuwa sijawahi kumuona ila ana roho mbaya Sana huwezi amini kwenye ngome yake anafuga nyoka wakali na wenye sumu kali na amewachukua katika msitu wa Amazon huko America kusini pia anamiliki samaki walio na sumu kali Aina ya 'Fugu' ambao aliletewa na Masta Shinji kutoka Japan na ndiyo sumu yake ilitumika kuwaondoa ndugu zako ni sumu hatari ambayo inapatikana kwenye sehemu za Siri za samaki hao inayopelekea mapigo ya moyo kufeli na kupelekea kifo ndani ya muda mfupi"
"mmmmhhh mbona watu hawa ni wakatili kiasi hiki namfahamu Sana masta Shinji ni mtu mkatili Sana hata tulipokuwa 'dojo' alikuwa na kasumba moja kwamba akikuona umeingiza karibu roho tatu ya mapigo kutoka kwa mpinzani wako basi hukutakiwa kubaki na pumzi kwa maana utapewa siku saba za mapumziko kisha utajikuta unapewa siku moja za kufanya mazoezi ya mwisho kabla hujamkabili yeye mwenyewe na kiufupi waga ni kama wakala wa kifo kwa maana hakuna hata ngumi moja unaweza kuingiza katika mwili wake, ana pigo moja linaitwa 'fugu fist' Hilo hata aje mganga gani huponi utakohoa damu mpaka Giza linaingia machoni kwako" alisema sorge huku akiweka umakini kwa mtu aliyekaa mbele yake.
"ukiachana na hii kuna kali zaidi na kuna watu kibao 'chini ya kochi juu ya zuria jekundu, hakika mtatokwa na machozi kwani mmeshtuka tayari ugonjwa ushakuwa mkubwa"
"una maana gani? Kusema hivo" aliuliza sorge
"Mimi nilichokupa ni kile nilichokuwa nacho kifuani mengine utayapata kwa Malaya mmoja anaitwa 'VANILLA' anapatikana 'Club handkerchief,Sinza"
"mmmmhhh kwahiyo unataka kusema kwamba kitovu cha yote haya ni hapa na watu hawa wanafanya haya kwa madhumuni gani? Ikiwa nchi yao iko Salama." Aliuliza kwa udadisi Sorge
"hakuna kitu kingine zaidi ya maslahi tu, unajua nchi yenu Ina rasilimali nyingi na pesa ni tamu ila haya yote ni geresha tu, 'KISASI' ndiyo kirusi kinachotafuna ukimpata huyu ex spy Master atakwambia undani wa hili Mimi najua hiko tu nachukulia kama hatujakutana mimi na wew katika Maisha haya....." Alisema makamu wa raisi aliyeondolewa madarakani huku akikatishwa na Ishara ya kunyamaza na hapo hapo sorge akashuhudia tukio la kikatili Sana kwani Alimshuhudia mtu aliyekuwa akiongea nae akitupwa chini na kuwa maiti, risasi mbili kutoka kwenye bastola Aina ya barreta ilitosha kumuachia matundu mawili kifuani katika mwili ule uliokuwa juu ya dimbwi la damu, haraka akachumpa na kutafuta maficho nyuma ya kochi nako zilimfata risasi kama mvua Kisha kukawa kimya kwa muda wa dakika moja Kisha akasikia Mchakato wa miguu Kuja sebureni pale kutokea mlango wa jikoni akatazama pembeni akaona kuna ua kwenye stuli ndogo akalivuta na kulirusha upande mwingine ili kumzubaisha adui ila halikufanikiwa kwani lilipasuka hewani kabla alijafika upande mwingine na Kisha risasi tatu zilichana upepo na kugonga ukuta Kisha likatokea tukio la ajabu kwani yule mtu alipiga yowe la hofu kwa kutupwa juu na kudondoka akiwa maiti Kisha akaona umbo la kike likiishilia kwenye kona ya kuingilia jikoni nae akamuungia mkia kwani alisikia sauti ya muungurumo wa pikipiki na Kisha mafuta mengi yalikanyagwa na kutokomea na hapohapo hisia zikamkuna kwamba pikipiki ile aliipita muda Fulani ikiwa imepaki mita Mia mbili kutoka nyumba hiyo na Sasa mbona haikutoa muungurumo wakati inafika hapo, akashtuka kwenye lindi la mawazo na akili ya kipelelezi zikarudi kazini na punde tu akaanza kuzikagua zile maiti na kwanza na ile ya jitu lile lilikuwa linashambulia kutokea jikoni, ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni kitambulisho cha idara ya ujasusi ya Burundi, SNR na alikwenda kwa Jina la 'ERIC KINYEREBANA' na kuonekana pia na bastola ambayo kwa uelewa wake itakuwa ni mali ya serikali hiyo.
"ebwana eeeennhh serikali inaingiaje kwenye hili au ndiyo maana hata utoaji wao wa taarifa za ubalozi na imekuwa tatizo pia kutoa ushirikiano kuhusu vifo vya majasusi wanaofika nchini humo kwa ajili ya uchunguzi." Alijiwazia huku akiendelea kuikagua na maiti ile nyingine hapo alikutana ajabu linguine lililomfanya agande huku akijiuliza imekuwaje kuwaje'THIERRY FRANCINE ' ndiyo Jina lililosomeka Katika kitambulisho kilicho mtambulisha kama sajenti wa jeshi la Burundi alibaki akipigwa na butwaa huku mdomo ukiwa wazi, vyombo vya ulinzi na usalama vinaingiaje hapa akajipa jibu kuwa kuna watu kadhaa ndani ya Burundi wanalihujumu taifa la Tanzania, haraka akachukua simu yake na kupiga picha maiti zile na kupotea eneo Hilo huku akibaki na dukuduku kwamba ni Nani alifanya mauaji ya afisa yule wa idara ya ujasusi ikiwa Thobias Chumvinyingi alibakia 'MUTAMBU' na umbo lililofanya hivo ni la jinsia ya kike.
"nitakujua tu hakuna linalo shindikana chini ya jua" alisemahuku akitabasamu na kupotea eneo Hilo kwa namna ambayo hata eneo halikuwa na kumbukumbu ya uwepo wa mtu
*****************************
Kama wasemavyo waswahili kuwa 'usiku wa deni hauchelewi kukucha, lakini kauli hii ilichukuliwa tofauti na idara ya ujasusi ya Tanzania, baada ya kuchakata taarifa ya kilichojiri nchini Burundi, vijana walipewa taa ya kijani kuendesha oparesheni ya kuwatafuta watu wawili hatari Sana nao ni mkuu wa idara ya ujasusi ya nchi hiyo pamoja na Shinji Nagasaki huku lengo likiwa ni kuwafuta ili kukwamisha jitihada za hujuma hukoKisha hawa walioko ndani watashughulikiwa kiulalo ulalo.
**************
CLUB HANDKERCHIEF-SINZA.
Saa 7:30 usiku.
Eneo zima lilikuwa limetapaka wanawake wa kila rika na umbo, lengo Lao kubwa ilikuwa ni kujipatia ridhiki kupitia sehemu zao nyeti wzilizokuwa wamepewa bure na muumba wao, Mbali na jinsia ile pia kulikuwa na jinsia ya kiume huku wakionekana kuchangamkiwa na wadada wale hasa eneo lile la nje mita chache kutoka Barabarani, Mbali na kundi Hilo pia lilikuwepo kundi jingine la waliokuwa wamefika eneo Hilo kwa lengo la kusuuza makoo kwa vinywaji mbalimbali hawa tunaweza kuwaita wateja wa haa ile huku kundi jingine lilikuwa la wafanyabiashara waliokuwa na biashara ndogo ndogo kama sigara,pipi nk, Leo eneo lilipata ugeni wa kijana wa makamo, mwenye mwili mkakamavu, mrefu kupanda hewani na mwenye mwili uliojazia kwa mazoezi lakini pia mweusi wa rangi huku akiwa na kofia nyeusi kichwani ya tangu nyeusi miguuni alikuwa amevaa safari buti ya rangi ya kaki iliyoendana na tisheti iliyomchora vizuri mwili wake suruali nyeusi ya dengrizi ilitosha kukamilisha utanashati wa kijana huyu wa makamo, hakuwa mwingine Bali luteni kanali Charz na alikuwa pale kwasababu ya taarifa iliyotoka kwa mwenzao juu ya kilichotokea nchini Burundi.
"karibu baby,elfu kumi yako unaenda kunit*mb@ Cha fasta, Fifte hadi asubuhi si unaona nilivyo" aliinadi biashara yake huku akijigeuza na kulitingisha kalio lake kubwa lililokuwa ndani ya kigauni kifupi kilichombana na kumchora umbile lake lilikatwa na kiuno chembamba, Charz alimtazama na kumeza mate kwanza.
"una bahati niko kazini vinginevyo ningekutafuna" aliwaza hivyo Charz huku macho yakiwa yanatazamana kwa tofauti ya sentimita kadhaa tu.
"nashukuru, Nina shida na 'Vanilla' naweza kumpata wapi kwa Sasa" alisema Charz huku akimtazama mwanamke yule aliyeko mbele yake.
"msyuuu yaani unatoka huko unakuja kuniulizia mwanamke mwingine, una dharau Sana wewe mwanaume Sasa Vanilla unayemsemea ananishinda nini hili si la mchina kitu Og kabisa" alimaka yule mwanamke.
"ntakulipa kwa kuniitia nizungumze naye mimi" alisema Charz huku akimtazama mwanamke yule maeneo ya shingoni, msichana yule alimtazama Kisha kutazama eneo alilotazamwana kwa aibu akamaka Tena.
"hiiii we kaka vipi kuchunguliana wewe si unamtaka Vanilla ila wanaume mna Tamaa kama fisi" alisema hivo huku akianza kuondoka lakini alishikwa mkono na Charz akataka kupayuka ila akakatishwa na sauti ya mtu aliyemshika.
"naitwa Charz ni boyfriend wa Vanilla, nilikuwa nje ya nchi kwa muda ndiyo nimerejea, simpati kwenye simu katika kuulizia ulizia nikaambiwa anapatikana hapa." Alidanganya Charz
"makubwa, kwa Ninavyokuona kwa Sasa huna hadhi ya kusimama na huyo unayemuita Vanilla huku anajulikana kama'Malikia wa ukahaba' huyo anachukuliwa na migari ya bei mbaya, unajisumbua tu kuhangaika na mtu ambaye kwa Sasa si saizi yako wewe zungumza nikakupe mapenzi" alisema yule mwanamke kwa kubenua mdomo na kuzungusha upande ule mwingine kuangaza kama kuna kichwa cha fasta hata hivyo alijikuta ameganda
"nitakupa laki moja cash ukiniletea huyo mwanamke"aliunguruma Luteni kanali Charz.
"makubwa!....nishakuwa kuwadi Sasa ngoja nikuitie nikukute hapa" alizipiga hatua yule mwanamke huku akiziacha sehemu zake za nyuma zikitetemeka kama zimemwagiwa maji ya baridi, baada ya muda, walirudi wanawake wawili ambao walifanana kwa kila kitu isipokuwa kimo na sura kwani mmoja alikuwa mweupe huyu alikuwa ni yule aliyepewa kazi ya kumtafta mwanamke mwenye Jina la vanilla.
"haya mtu wako huyu hapa nipe changu nikale vichwa huko" alisema yule Dada huku akinyoosha mkono kumaanisha awekewe pesa, muda wote Vanilla alikuwa anashangaa tu
"hebu kuweni siriasi.....Bella nini kinaendelea hapa" aliuliza kwa hamaki huku akionekana kukereka na yanayoendelea, ilibidi luteni kanali Charz apunguze wahanga kwa kumlipa yule mwanamke aliyezipiga hatua huku akibaki na Vanilla,
"Habari yako Vanilla, nilikuwa nahitaji huduma ya kuupitisha usiku na mrembo ambaye ni wewe" Alitupia maneno Charz
"one million cash" alisema hivo yule mwanamke huku akitabasamu kwa dharau.
" no problem tuondoke Sasa" alisema charz huku akiwa anataka kuanza kupiga hatua.
"weeee si kiivyo....naweka oda ya chumba mimi mwenyewe na tunaondoka kwa bolt.....oooohhh shit Leo boyfriend wangu kashaniambia atanitumia usafiri" alishtuka baada ya kuhisi uwepo wa mtu mbele yake
"samahani kaka Leo haita wezekana labda uje kesho" alisema yule Dada huku akiangaza huku na huko, Luteni kanali Charz akatumia sekunde kadhaa katika kumtathimini mwanamke aliyeko mbele yake na hapo alimeza mate na kukiri Jina Vanilla halikukosea njia, rangi ya weusi unaoteleza, kiuno chembamba kilichobeba makalio yaliyoshiba nyama za kutosha huku hips zikimfanya aonekane mrembo, mtindo wa nywele zake ulisadifu uzuri aliojaliwa na Mungu, sauti nyororo na yenye kuvutia ilikuwa silaha yake katika kuwanyang'anya wanaume pesa kwahiari yao wenyewe pasipo kutishiwa kwa maneno au silaha.
"kwanini isiwezekane mrembo basi nitaongeza two million over your emergency"
“Hapana kwakweli kwa leo haitowezekana hivyo nakuomba uende Kisha kesho uje hapa mida kama hii Sawa" alisema huku akianza kuzitupa hatua kuondoka pale nje
"siyo kirahisi hivo tutaongozana wote Vanilla" alisema kwa sauti kavu na yenye mamlaka.
"unataka nini labda kutoka kwangu,nakuhurumia kwani bwana angu akijua hili unalotaka kufanya utakuwa maiti ndani ya saa 72 hivyo naomba usitishe na upotee hapa” aliongea vanilla kwa sauti ndogo ila yenye msisitizo
"hivi unadhani nimekuja kucheza hapa na sirudii Tena kuongea twende kwenye ile Crown nyeusi pale na usifanye ujanja wowote" aliongea kitemi huku alimuonesha bastola iliyokuwa imwesundwa kwenye kiuno na wote wakaingia kwenye gari na kuanza kuiacha kumbi ile ya starehe huku muelekeo ukiwa bagamoyo kwa kuwa hakukuwa na magari mengi barabarani kwa mwendo wa dakika 30 walikuwa tayari wamefika katika nyumba ya siri ya idara ya ujasusi.
"Mimi siyo mtu mbaya na usichukulie kama nimekuteka nyara kuna muda demkokrasia inapofeli ubabe unatumika, hata hivyo Nina vitu vichache tu vya kuzungumza na wewe kabla ya kukurejesha ukaendelee na miadi yako"alisema Charz huku akikaa kwenye moja ya sofa lililokuwa pale sebuleni.
"ni mazungumzo gani ambayo tunaoneshana bastola kuna usalama kweli.....nishatekwa Vanilla mimi" alilalamika Dada yule huku akiwa ameinamisha kichwa huku mikono kaiweka kichwani"
"sikiliza Binti mazungumzo baina yangu na wewe yatakuwa ya amani ikiwa utaridhia hivyo ila pia yatakuwa mabaya kwako na ngozi yako hiyo nzuri inayokupa pesa"
"mmmhhhh.....mazungumzo gani hayo na wewe, na mtu sikujui tumekutana leo, kingine sijui chochote zaidi ya kuuza mwili wangu labda na historia yangu fupi tu itakayokuchekesha nakukuhuzunisha" alisema yule Dada anayeitwa vanilla huku safari hii akiinua kichwa chake kumtazama mtu alikaa mbele yake.
"Vanilla mtu asiyekujua akikusikiliza anaweza kusema wewe ni Binti mpole na mstaarabu Sana ila upande wako wa pili hautazamiki una madeni mengi Sana na usiku huu unaweza kuuita 'USIKU WA DENI' kwani mmoja wa watu ulio na deni nao ni hili taifa na mimi nimetumwa Kuja kulichukua deni Hilo" alisema Charz huku akiweka uso wa kazi.
"Deni.....deni gani nadaiwa, sikiliza kaka utakuwa umekosea mimi Sina deni la mtu yoyote kuanzia benki hadi vikoba Sasa sijajua unavyosema umekuja kukusanya deni kwangu utakuwa umekosea" alisema vanilla huku akirusha mikono kana kwamba amekereka.
"SHYROSE MASANJA' Binti wa mzee 'MASANJA BUNDARA LUMWECHA' uliyezaliwa mwaka 1995 huko hospital ya wilaya ya magu na kupata elimu huko kabla ya kupachikwa ujauzito na 'JUMA ULEDI' dereva bodaboda, na ulifukuzwa kwenu na ndoto za kupata elimu ziliyeyuka ungali uko kidato cha tatu, siyo Juma Uledi peke yake aliyekuwa akiiona nguo yako ya ndani Bali hata bwana DERRICK MWAKIPESE' aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika mtaa wenu pale buzuruga alikujua nje na ndani ya mwili wako. REHEMA JUMA' Binti yako mwenye umri wa miaka minne na mwanafunzi wa shule ya awali, 'DON BOSCO' unamsomesha kwa Siri Sana chini ya mwamvuli wa'STELLA RWEYEMAMU'
itaendelea
Unataka kumfahamu vizuri Vanilla basi tukutane toleo lijalo,
NB: napenda kutanguliza samahani ni wazi kama mwanandishi nilikiuka miiko ya uandishi kwa kuleta kitu chenye mapungufu lakini hiyo yote ni presha na kiu ya simulizi hii kutoka kwenu nyinyi nakiri wazi kwamba toleo lililopita lina makosa mengi sana na niseme hapa kwamba halitojitokeza tena sababu kuu ni kama nilivyosema huku uchovu na wingi wa kazi kwenye maisha halisi unachangia.Tchao
 
huyu mtunzi sahivi anazingua tu mwanzo alianza kwa kasi nzuri vipande vya kutosha ila baada ya kupata wafuasi ndo wanajifanya wana mambo mengi hadi ameanza kunata eti kipande kimoja tena kifupi na hadi tubembeleze na kulia lia ndo aturushie kimoja..
Usiseme hivo maana ni mara ngapi nimekuwa nikitoa taarifa humu ndani lakini vile vile siyo kwamba muda wote nakuwa huru nimeishika simu kuwapostia humu toleo ila pale nnapopata nafasi basi nakuwa nafanya hivo hata mara mbili hivyo usinichoke mapema hiyo bado nakuhitaji sana kama hadhira
 
"Huwezi kudanganya tabasamu, huwezi kudanganya mkono wa salamu, na huwezi kudanganya maisha………unabisha fatana nami”
TUENDELEE………….
Binti yako mwenye umri wa miaka minne na mwanafunzi wa shule ya awali, 'DON BOSCO' unamsomesha kwa Siri Sana chini ya mwamvuli wa 'STELLA RWEYEMAMU' mama yako mdogo aliyeachiwa ziwa na mama yako 'REGINA RWEYEMAMU' unajua kwanini nakueleza yote hay.........." Alikatishwa na yule Dada
"weeee usiiongelee Familia yangu wala kujaribu kuigusa ntakuua nakwambia" alisema yule mrembo kwa Shari
"Mara hii unanitishia kifo, sikiliza 'QUEEN MASANJA' nakujua wewe ni mhusika wa mauaji ya baadhi ya maafisa wa ubalozi pale Burundi, wiki kadhaa nyuma na umetumika kama kiunganishi cha kuwarahisishia wauaji kazi, unamjua mtu mmoja anaitwa KHATIB GONGO,?
"mmmhhh...hapan...hapana simfahamu mtu huyu ni Nani kwanza na wewe ni nani?" Aliuliza vanilla huku akionekana kuwa na hamaki.
"niite Charz itapendeza, ila katika mwanzo wa mazungumzo yetu nilikwambia huu ni usiku wa deni na ninayekusanya madeni hayo ni mimi na katika yote pia nakujua Queen wewe ni muigizaji mzuri na hata Mara zote umekuwa ukiyeyuka kwenye eneo la tukio bila kushtukiwa, Sasa nisikilize kwa makini tarehe 17 mwezi wa 5 ulienda kufanya nini Burundi?" Aliongea vile vile kwa sauti kavu huku akiwa vile vile mtulivu na makini.
"Burundi mmmmmhhh hapana sijawahi kwenda kwenye nchi hiyo tangu nizaliwe" aliongea vile akiwa kwenye mshtuko
"hahahaha Queen ukiwa muongo uwe na kumbukumbu ngoja nikukumbushe labda kweli umesahau" alisema Charz huku akivuta bahasha iliyokuwa juu ya Meza na kutoa picha mbili zenye ukubwa wa A4 na kumtupia upande aliokuwepo Vanilla.
"'Queen Masanja' Jina ulilopewa na wazazi ila dunia ya uhalifu ikakubatiza Jina jipya la 'Vanilla' nambie huyo kwenye picha hiyo hapo juu ni Nani?"
"hizi picha mimi sizifahamu kabisa na hata sijui unachoniuliza" alisema hivo vanilla huku sura yake ikiwa ni ile ile kavu.
"acha niendelee kukuvumilia maana nikibadilika Nina uhakika hakuna atakaye kutamani Tena hata kwa shilingi elfu mojahakuna atakaye kupatia ili tu ukidhi mahitaji yako achilia mtoto wako kuwa chokoraa, hivyo jiangalie Sana kinywa chako" alionya Charz huku akiwa anamsoma saikolojia mwanamke yule.
"ni kweli namjua na nilimjua kupitia kwa bwana angu, na alinidokeza kuwa ni mfanyabiashara mwenzake lakini kuna siku walikutana wote wakiwa na haraka kiasi cha kudondosha diski mweko chini kwenye zulia niliiokota na kuihifadhi mpaka nilipomaliza kufanya usafi kwa bahati kuna mmoja wa walinzi alikuja kuazima kompyuta ili amsaidie mdogo wake kuomba nafasi kujiunga na jeshi la polisi na mimi kwa haraka nilihitaji kuona kilichomo kwenye diski mweko ile baada ya kompyuta kuwakana diski mweko kusoma nilijikuta nikipigwa na butwaa kiasi cha kusahau uwepo wa yule mlinzi aliyekuwa katika mavazi ya suti nyeusi, mshtuko ule ulimvuta na yeye akajikuta amegandisha macho kwenye kioo kile na haraka akachomoa diski mweko ile na kisha kunitazama, nilitaka kusema kitu ila alinipa ishara ya kunyamaza na kuniambia hiyo ni siri kubwa sana ambayo sikutakiwa kuiona kwa macho yangu wala kuiweka katika kumbukumbu zangu akaniambia anakuja akaondoka na ile diski mweko pamoja na ile kompyuta kitu kilichoniacha kwenye sintofahamu kusema ukwel......" alikatishwa kwa mara ya kwanza tangu aanze kutoa maelezo yake.
"majina yake ni nani huyo askari aliyechukuwa vitu hivyo na je? alikurudishia vitu hivo? " aliuliza huku akiweka umakini kwa mwanamke yule kwa namna ya udadisi.
"namkumbuka tu kwa jina moja tu la Tonny, na alinirudishia vitu vile baada ya dakika 5 tu na wala hakunisemesha tena" alisema mwanamke yule kwa sauti ya utulivu
"huyu Tonny unayemzungumzia yuko wapi kwa sasa?" alitupa swali jingine huku akijiweka sawa katika kochi alilokuwa amelikalia luteni kanali Charz.
"mimi sifahamu kwa sasa alipo ila ninachojua ni kwamba ile ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kumuona, na hata bwana angu siku ile alirejea baada ya saa 1 akiwa kama mtu aliye changanyikiwa na hata alipoingia ndani moja kwa moja alianza kutazama kuanzia sakafuni na kwenye meza na nilimuona akitabasamu baada ya kuiona diski mweko hiyo mezani ila alipoinua macho na kunitazama nikiwa nimesimama kwenye ngazi ya nyumba ile tabasamu lilipotea huku akinitupia swali ikiwa kama diski ile nimeweza kuitumia ndipo nilipomjibu nimeiokota na kuiweka kwenye meza na wala sijajua hata kilichomo huku nikimuuliza ni diski mweko ndiyo iliyomrudisha au kuna kingine, ila alinijibu kuwa alikuwa na wasiwasi na mali yake na alipewa taarifa kuwa nimeingiza mwanaume ndani na alikuja kwa madhumuni ya kufumania ila matokeo yake kumbe ni uongo tu wa watu wanao tuonea wivu lakini mimi nilijua huu ni uongo tu ila diski mweko ndiyo iliyomrudisha nyumbani muda ule." aliongezea Queen huku akiwa ana mtazama mtu aliyekuwa mbele yake.
''huyo bwana ako hujawahi kumgusia juu ya kuto kuonekana kwa huyo Tonny?" alitupa tena swali luteni kanali Charz
"niliwahi kumgusia siku tatu mbele juu ya kutokuonekana kwa mtu yule ambaye alikuwa kama kiongozi wa ulinzi pale kwake, lakini hakunipa jawabu la kueleweka isipokuwa alisema tu kuwa amepangiwa kazi nyingine, nilinyamaza huku nikiwa na dukuduku moyoni na kesho yake baada ya kuondoka nilimfata mmoja wa walinzi na kumuuliza kulikoni mwenzao amepotelea wapi akanijibu kuwa yupo gereza la ukonga kwa kesi ya ugaidi aliyounganishwa na wasomali fulani waliokamatwa huko mkuranga huku wakuu wakisema alikuwa akishirikiana nao kutoa siri za nchi na kupanga kulipua baadhi ya maeneo ikiwemo kambi ya jeshi iitwayo mgulani.......nilinyamaza kwasababu hayakuwa yakinihusu ila kiukweli kauli ya bwana angu na hii kiukweli zilinichanganya sana kiasi cha kuhisi kuna mchezo umefanyika" alitoa maelezo hayo mwanamke huyo kwa masikitiko
"kwani huyo bwana ako ni nani?" alisema luteni kanali Charz huku akiachia swali lililompa mshtuko mwanamke yule kiasi cha kuanza kuiona hofu machoni mwake na hapo akaunganisha swali lingine.
'utakuwa jasusi wa kwanza muoga kiasi cha kushindwa kumtaja mwanaume anayemuona utupu wake karibia kila siku ijapokuwa amejificha kwenye kivuli cha ukahaba ila serikali imekuweka makusudi ili ukusanye taarifa kuhusu watu fulani pale na ndiyo nazihitaji kwa sasa achana na hayo mengine nataka uniambie uliona nini kwenye ile diski mweko?"
"hahahaha wewe jamaa ni noma sana sijawahi kukusikia hapo kabla ila naamini wewe ni miongoni mwa silaha za mwisho za chifu........ni hivi diski mweko ilikuwa na vitu vichache visivyo na muunganiko ndiyo maana mpaka leo ripoti haijafika mezani kwa chifu kwahiyo hata nikikueleza bado hutapata muunganiko mzuri wa kutufikisha kwenye suluhisho ila ndani ya sik......"
"nipe jina la huyo mtu hayo mengine tayari wewe hujiulizi nimefikaje hapa.....muda hautoshi kuna kazi natakiwa nikaifanye usiku huu kabla giza halijaondoka na ukumbuke mme wako anakusubiri ukampe uroda atakao msimulia shetani wakiwa wanaota moto huko kuzimu
"anaitwa balozi STEVEN KWASU......yule katibu mkuu kiongozi na ndiyo msaidizi wa raisi kupitia kwa makatibu wa wizara zote na wako chini yake nadhani umepata hiko ulichokihitaji japo sina uhakika wa maisha yangu huko niendako ila kama nisipofnikisha nadhani familia yangu itaumia sana kunikosa hasa mwanangu" alimaliza kwa sauti ya masikitiko huku akidondosha chozi huku akiinamisha kichwa, alijikuta ameshikwa na mikono imara kwenye kidevu chake kabla ya kupanguswa chozi lile lililokuwa likiishia kwa kitambaa laini alichokuwa kimeshikwa na luteni kanali Charz.
'nikuahidi tu kuwa utakuwa salama na ntakulinda na hakuna chochote kibaya kitakukuta sio wewe wala familia yako niamin ikwenye hilo 'QUEEN'"
itaendelea
Mambo yanazidi kufunguka huku wahalifu wakianza kufunuliwa, Je usalama wa Queen ni kweli utakuwa wa 100% kama alivyohaidiwa? Usiumize kichwa tukutane toleo lijalo
 
SI AJABU KUWAKUTA WATU WAKIONGEA KIMYA KIMYA NA KWA UHARAKA KATIKA KIZA KABLA HAKUJAPAMBAZUKA…….NI BORA KUWA SIMBA KWA SIKU MOJA KULIKO KUWA KONDOO MAISHA YAKO YOTE.
Endelea…………….
nikuahidi tu kuwa utakuwa salama na ntakulinda na hakuna chochote kibaya kitakukuta sio wewe wala familia yako niamini kwenye hilo 'QUEEN'" alisema luteni kanali Charz kwa sauti ya utulivu ila yenye msisitizo.
"mmmmhhhh wewe unaongea tu kwasababu hujui hatari iliyopo mbele.......hawa watu ni hatari lakini nashukuru hata nimepata mtu wa kunifariji kwa sababu sina matumaini ya kuliona jua la kesho Charz" alilalama tena Queen
"haya nieleze ulikutana na 'KHATIB GONGO' kwa madhumuni yapi na usijaribu kunificha kwa sababu haita kusaidia kwani ndiyo itaongeza tatizo na ndiyo maana nikaomba uniambie ukweli ili iwe salama kwako ili uweze kuvuta hii pumzi ya bure.
"ni kweli kabisa namfahamu mtu huyu kwa kuwa kwa namna moja au nyingine ndiye aliyenisaidia kuingia kwenye idara ya ujasusi........nakwambia hivi kwa sababu natambua muda wowote naweza kuwa marehemu kuanzia sasa hivyo natembea na kifo changu kila ninapo piga hatua na kiufupi huyu ndiye aliyekuwa opareta mkubwa wa oparesheni zote ndani ya idara vile vile huyu ndiye aliyewauza wale maafisa kumi na saba wa ubalozi, japo idarani anajulikana kama mkuu wa oparesheni zote za nje ya nchi ila huyu cheo chake halisi ni mkuu wa ulinzi wa raisi na waga anafanya mambo yake nje ya ile ofisi yake na yule aliyeko pale ni kivuli chake nikiwa na maana ya msaidizi wake, na tarehe 17 ya mwezi wa tano nilikwenda burundi ili kuhakikisha mambo yanakaa sawa pamoja na kuzivusha zile pesa zilizoibiwa kwani mkuu wao alikuwa akizihitaji na hata tulivyofikisha ule mzigo wenzangu wote walitangulia mbele za haki isipokuwa mimi na ni kwa vile kuna kazi moja nilitakiwa kuikamilisha nayo ni ya hatari sana ilikuwa ya kumuondoa waziri mkuu, huyu na hiyo nilipewa na mtu ambaye mpaka leo sauti ile inajirudia kichwani Charz" alisema Queen.
"ni sauti ya nani huyo? ambayo haitoki kwenye fikra zako" aliuliza charz kwa udadisi
"ni ya mtu ambaye kivuli ndiyo rafiki yake na giza ndiyo uwanja wake, hata mimi sijawahi kuiona sura yake wala umbile lake ila anaonekana ni mtu hatari sana na watu wanamuogopa ikiwemo hata huyo 'KHATIB GONGO' unajua ni kwasababu vitu hivi vinatokea na vinakuwa nje ya uwezo wako.............mamluki niwengi sana kuanzia ngazi ya juu hadi huko chini kabisa na tumeshtuka tayari kumekucha ila mshukuru tu yule mama yuko'smart' sana sijajua nani yuko nyuma yake ila kama angechelewa angeambulia aibu kubwa sana.
"kila kitu ni akili Queen, ili uweze kushinda vita ni lazima uweze kujua kwa mapana windo lako utajua mahali gani ukimshambulia unammaliza nguvu adui" alisema Charz huku safari hii akitoa mche wa sigara aina ya chesterfield na kukiwasha na kuvuta pafu kubwa la moshina kulitoa kitu kilichopelekea mpaka Queen kukohoa baada ya kuuvuta moshi ule.
"zima bwana sigara, mimi nina mzio na vitu hivi.......samahani kama nitakuwa nakuharibia starehe yako" alisema hivo huku akiichukua sigara ile na kuizima kwenye kibakuli mezani pale na hapo walijikuta waakigonganisha macho na Charz, Queen aliachia tabasamu
"kwanini ulichagua kazi hii ya hatari kijana mzuri kama wewe, ulitakiwa uwe na kazi zingine umetulia ofisini huku ukiilea familia yako kuliko hizi kazi za kuziweka rehani roho zetu" alisema Queen huku tabasamu likiwa vile vile mara hii alijilamba kabisa na papi za mdomo zilizokuwa nene kiasi cha kumuongezea uzuri ambao hata Charz alikiri kuwa mwanamke yule alikuwa mzuri akaachana na mawazo yale machafu nakurudisha utimamu
"mimi naamini ni kazi nzuri kwa sababu nimechagua kuwa na imani nayo na ninaishi kwa imani hiyo hiyo kwa sababu bila hiyo siwezi fanya chochote, hivyo ni kitu kinachonifanya niwe na wewe hapa"
"ni sahihi unachokisema ila kiukweli tunaweza kuwa na vitu tunavyovihitaji, kama mimi nilichagua upande ambao haukuwa sahihi kwa vile kwa wakati huo tuliamini kwenye nia kuna njia, ni imani yangu kuwa mimi na wewe leo hatujakutana kwa bahati mbaya" alisema Vanilla akilegeza macho yake
"hahahaha watu wote unao waona wana amini katika vile wanavyoviona ni sahihi kwao ila…."alikatishwa na binti yule
"shida ni kwamba watu tunao shughulika nao ni wabaya kuliko wale ambavo unafikiria" aliendelea kusema huku sauti na midomo yake ikiwa imelegea
"nadhani muda umekimbia tunaweza kuongozana na nikakuacha sehemu utakayopata usafiri wa kwenda huko kwenye miadi yako na nikushukuru kwa taarifa ulizonipa" alisema charz huku akisimama
"ni sawa ila natambua kuwa nikiwa hapa nakuwa salama unaweza kwenda na ukibahatika kutoka salama huko uendako utanikuta hapa kwani sioni tumaini la kuishi kwa vile nitasafirishwa mpaka kuzimu tafadhari naomba nikusubiri hapa" luteni kanali Charz alibaki akimtazama Queen kiasi cha kumfanya avunje ukimya.
"natambua bado unatumia ile kanuni ya kwamba'katika mapambano ya nguvu usiwahi kumuamini mtu yeyote si ndiyo Charz, haina shida tunaenda ila tambua damu yangu ikimwagika itakuwa juu yako" aliongea mwanamke yule huku akijizoa zoa toka kwenye kochi kiasi cha kufanya nguo yake ya ndani kuonekana.
"kulikimbia tatizo inaweza kuwa motisha kwa namna moja au nyingine, ila kulikabili tatizo ndiyo njia pekee ya kuyashinda haya yote" alisema tena luteni kanali Charz huku akianza kuzipiga hatua kuuelekea mlango na hapo kikatokea kitendo ambacho hakukitegemea kwani mwanamke yule alijilaza kwenye kochi huku akionesha nia yake ya kuto kuondoka kwa vitendo.
"natambua ulifuzu vyema mafunzo, kiasi cha kukufanya upate nafasi ya kuishi mpaka leo......by the way nkutakie usiku mwema Queen tutaonana asubuhi, usifanye kitu chochote cha kipuuzi tafadhari na usimuamini mtu yoyote naamini hutakuwa na matumizi na simu yako nikabidhi na hiyo ndiyo itakuwa salama yako" alisema Charz huku akitokomea kuelekea kwenye maegesho na kisha kupotea hilo eneo.
*************
MUTAMBU-BURUNDI
saa 7;45 usiku
ni usiku mzito sana ndani ya mji huu uliopakana na jiji mji mkuuwa nchi hiyo Bujumbura, gari aina ya Toyota Crown Majesty ilikuwa ikipita mitaa kadhaa ya mji huo huku ikiwa mwendo wa taratibu na punde dereva wa gari hilo akazima taa huku akiacha litembee polepole kwa spidi ya 20km/h na alipofika usawa fulani wenye giza alisimamisha na kuizima gari lile kisha akashuka na kuanza kutembea kwa tahadhari akilielekea geti la nyumba moja wapo iliyokuwa imezimwa taa kwa nje.
"ina maana Thobi hajawasha taa za nje mpaka sasa hivi usiku mnene nyumba imetopea kwenye giza zito kiasi hiki," fikra zake zilimtongoza kiasi cha kumfanya apime utulivu kwa hatua zake sekunde ya kwanza ilipita bila tashtwitwi yoyote ya hatari kwani mtaa ulikuwa kimya ila sekunde ya pili haikupita hivi hivi kwani teke lilikusudia kuikanyaga shingo yake lilichana upepo huku yeye akiinama kidogo na kumchota mtama mtu yule lakini aliambulia patupu kabla hajafanya chochote alijikuta akipata maumivu kifuani kwa kukanyagwa na guu zito la mtu yule asiyejulikana, lilimsogeza pembeni kiasi cha kuanza kuhisi kwamba kama asipofanya jitihada jitu lile litamuondoa.
"unakuja kufanya mchezo kwenye nchi za watu amka uje upambane wewe si mwanaume simama upambanie roho yako komredi usiwe kama yule mwenzako sijui mlimu ajiri vipi hata shoga angemchakaza hahahaha simama wewe malaya wa kiume ningetaka ningekuua kwa risasi ila ni aibu sana kuwaua mashoga kwa risasi maana ni upotevu wa shabaha nitamrahisishia mungu kazi kwa kuivunja shingo ya shoga kama wewe na utaungana na shoga mwenzako huko motoni mkaendeleze ushetani wenu huk......." kabla lile jitu jeusi na lenye ndevu halijamaliza kauli yajke lilisombwa na risasi mbili zilizotua nyuma ya mgongo wake na kulitupa chini likiwa halina uhai kitu kilicho mstaajabisha tena ASP Richard na hapo alijitupa pembeni huku macho yake yakilikagua eneo hilo, kabla ya kuthibitisha kilichomuondoa duniani mtu yule ni risasi kutoka kwa mdunguaji kwani eneo zima lilikuwa kimya kiasi cha kutokuwa na kashikashi za watembea kwa miguu wala magari hasa ukizingatia muda huo ilikuwa tayari ishakuwa usiku mnene, alijipa utulivu kabla ya kusikia kitu cha baridi kikimgusa kisogoni.
"SIMAMA HIVYO HIVYO NA USILETE UJANJA WOWOTE KOMREDI, HUNA UJANJA WEWE NI MAITI INAYOPUMUA HIVYO FATA UTARATIBU NITAKAOKUPA ILI UENDELEE KUNUNUA PUMZI YAKO UNAYOINUNUA KWA GHARAMA ZAKO MWENYEWE"aliongea kitemi kiasi cha kumfanya ASP Richard kushikwa na hofu huku koo likimkauka na kujilaumu kwanini hakuchanga karata zake vizuri ukiachilia hayo bado alikuwa anaitafakari sauti hiyo kama alishawahi kuisikia sehemu alishindwa kuuliza maana alikuwa amempa mgongo mtu yule, anayeongea kiswahili kilichonyooka akajipa utulivu huku akiiweka akiliyake kazini.
"wewe ni nani unayevizia watu kama kibaka, alafu wewe ni muoga kama mbweha tu" alijaribisha kutikisa kiberit richardsorge.
"nyamaza kimya hayawani mkubwa ukiendelea ntamrahishia kazi malaika mtoa roho shezi baazazi mkubwa"
itaendelea***
Je ni nani huyo anayezungumza kiswahili kilichonyooka katika nchi za kigeni? Je ataweza kuchomoka au ndiyo safari yake itaishia katika taifa la ugenini? Tukutane toleo lijalo
 
alisema kwakiswahili kilichonyooka huku ikifuatia na ngumi kavu mgongonimwa Richard huku akimsukuma atembee hilo likawa kosa kwani Sorge alijifanya amejikwaa ili kuvuta umakini wa mtu yule naye akahadaika na sekunde iliyofata mtu yule alijikuta akielea hewani huku silaha yake ikiwa mbali na yeye, mapigo kadhaa yalimfata huko huko ila aliyakwepa kwa wepesi kama unyoya kwa kujiviringisha kisha alitua kwa mguu mmoja huku mkono wake akiutanguliza chini ni hapo Sorge alihamaki baada ya kukutana na sura anayoifahamu sana kuanzia kambini walipokutana huku mtu huyo akiwa mkufunzi wake baadae akaja kusikia mtu huyo alifukuzwa kwa utovu wa nidhamu.
"ni wewe kanali sentonyo ndo umeibukia upande usioutakia mema nchi yetu" alisema hivo Sorge huku akiongeza umakini kwani mtu aliyekuwa mbele yake ni zaidi ya neno hatari.
"tulia wewe mtoto wa malay* unaongelea nini mimi nimechagua pesa uzalendo mnaolilia na yule bibi yenu mtauona kwa vitendo mkiwa mmebakiza sekunde thelathini mkiwa mnahesabu kila pumzi yenu ya mwisho."
"kumbe kuna watu wazima hovyo kiasi hiki kwanini hukutulia ustaafu ukalee wajukuu zako.....kwa heshima tu piga magoti na ujisalimishe" aliongea tena akimwangalia mzee yule kwenye giza lile lililokuwa linafukuzwa na mwanga hafifu wa taa ya umeme kutoka nyumba iliyokuwa mita kadhaa kutoka pale waliposimama mafahali wale waliokuwa wakiangaliana kwa uchu.
"hahahahha na wewe unaleta ngonjera kama yule marehemu uliyemuacha ndani nasikitika kwamba hutaiona maiti yake ila mtakutana huko huko kuzimu msimuliane ukatili wa vifo vyenu...muda wa kupiga stori umeisha wasalimie kuzimu" alimaliza huku akirusha makonde mazito yaliyochana upepo na kumfanya mkwepaji aone akizembea kweli utabiri utatimia, akarudi nyuma hatua kadhaa kupanga hesabu zake vizuri........alikosea!........alikosea! kwani sekunde zisizo pungua thelathini alijikuta akielea hewani huku akitoa yowe la hofu.
"leo nitakufundisha kwanini fisi miguu yake ya mbele ni mirefu kuliko ya nyuma we mtoto wa malay*" hapo kulifatiwa na mateke mazito yalichana upepo, Sorge aliinama na katika namna ya ufundi na akamchota mtama uliomtupa mtu yule na kisha kutulia mgongo kiasi cha kubweka kama mbwa koko, jitu lile punde liliibuka na bastola iliyokuwa limeisunda kwenye soksi yake ya mguu wa kushoto.
"huna sababu ya kuishi wewe nyau mweusi ulidhani nitakukubalia ushinde, kutwa ukinipasha mwili wangu joto risasi mbili zitafanya maiti yako isitizamike, kenge wewe haya tuma salamu kwa watu wawili kabla maiti yako haijawa chakula cha mamba wakali" alifoka mtu yule huku akiuma meno kwa hasira
"kwa watu waoga kama wewe unayebweka kama mbwa.............ya pili kwa wahujumu wote wa serikali yaTanzania na vibaraka wote kwani kiama chenu kimekaribia"
"kawasimulia huko kuwa hivi sasa mke wako ataenda kuwa mjane na wiki mbili zijazo atakuwa anani bembeleza kitandani FACUND................" ghafla umeme ukikatika mtaa ule na kutanda giza huku mlio wa cheche za transfoma iliyozima huku kukifatia na milio mitatu tofaui, Ndiyo kwani sauti ya kwanza ya mlio kama chafya ya mtoto iliendana sambamba na sauti ya miguno ya maumivu na yowe la mtu aliyekuwa ameshindwa kupiga hesabu zake vizuri na sauti ya tatu ni mlio mbaya wa risasi iliyochana upepo, kisha kukawa kimya, kuashiria kila mtu anamvizia adui yake, mbali na hayo yote bunduki ile iliyotoa mlio wa chafya ya mtoto ilizipiga chafya hizo mara tatu zikifutiwa na yowe la hofu lililoambana na kupaa hewani na kisha kutulia.
"kamanda tuondoke hapa tuko nje ya muda asubuhi inatakiwa itukute tumeshavuka ngara" sauti nzito yenye mamlaka ilikoroma huku kukifatiwa na watu wale kutoweka mahali pale, kapteni jumanne saidi pamoja na Sorge waliondoka eneo hilo.

SNR HQ-BURUNDI
Saa 8:25 usiku
simu inapigwa katika eneo la vyoo vya ofisi moja iliyo ndani yajengo la makao makuu ya idara ya ujasusi nchini Burundi.
"muda wowote kuanzia sasa ngoma inaweza kupasuka na nchi ikawa uchi kweupe ila kwa taarifa tu kuna maiti mbili kutoka kwa majirani zimegundulika jirani na ubalozi na kinachotia shaka ni yule mtu aliyekuwa akitafutwa na idara kwa siku nzima amekutwa akining'inia juu ya jengo huku maiti yake pia ikikutwa na matundu ya risasi acha hilo hili ndiyo litakustua, kanali mmoja kutoka huku naye alikuwa kwenye msitari wa kumlaki bwana mawinguni kwani naye alichezea mvua ya risasi na kisha mwili wake kutoweka na kisha kuibukia mochwari za hospitali ya taifa"
"whaaaaaat!!!,,,,,,,,,,nini kinachoendelea ina maana mkurugenzi halioni hili au ana mkono na ametia baraka kwenye hili?" aliuliza swali mtu aliyeonekana kama ana mamlka fulani
"siwezi kusema ndiyo au hapana kwa sababu kwa binadamu yote yanawezekana na sheria namba moja ni kuto kumuamini mtu yoyote ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe" alisema mpigaji
"fatilia kila kitu na walau nipe ripoti ya kilichojiri kesho asubuhi..........TITITI"simu ile ilikatwa huku ikiacha maelekezo ambayo yalibakisha saa chache kabla hayajatolewa ufafanuzi na mpigaji wa simu aliyekuwa ndani ya jengo la idara hiyo nyeti kisha mtu huyo akatoka ndani humo na kurudi katika kiti alichokuwa amekikalia huku akijikita kwenye kuchakata taarifa zitakazotolewa maelezo asubuhi kwa mkuu wake hakujua kuwa mita kadhaa kutoka katika ofisi yake kuna watu sita walikuwa wakiyasikiliza mazungumzo yale yaliowafanya wasisimke kiasi cha kuadhimia watu wale waliokuwa wamepigiana simu kutokuliona jua laa kesho hii ilimaanisha walikuwa wameshapewa hukumu ya kifo bila hata kupewa notisi
*******************
POSTA-DAR ES SALAAM
Saa 12:00 asubuhi
ilikuwa ni asubuhi nyingine iliyolifukuza giza na kuukaribisha mwanga kutamalaki, jogoo wakiwika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na kona zingine za nchi ya tanzania, muda huo huo ulizoeleka ya kwamba mtangazaji wa redio atawapitisha katika kurasa za magazeti.
"mama johnson hebu niwashie redio nisikilize kulikoni katika hii nchi iliyojaa mizengwe"
"hebu huko usinisumbue......hizo habari zitatulisha badalau amke ukatafute pesa kama wanaume wenzakokutwa unahangaika na mimi" alisema mwanamke yule huku akimgeuzia mgongo
"funga bakuli lako na niwashie redio kabla sijakutia tatuu hapo usoni uone faida ninayopata nkisikiliza uchambuzi wa kurasa za magazeti."
"haya......stesheni gani mume wangu"
"weka mawimbi Fm kama siku zote na harakisha ole wako niikute habari ishachambuliwa nusu utanitambua" alikoroma mwanaume yule
"hebu nawe usinitishe bwana habari habari hadi unanyima amani haya sasa sikiliza habari zako hizo......utadhani mjumbe wa nyumba kumi" aliongea mama yule huku akilifunga tenge lake vizuri tayari kwa safari ya jikoni ndani ya nyumba hiyo."
"hujui ulisemalo mke wangu" akiwa katika tafakuri fupi huku macho yake yakitua kwenye mgongo wa mkewe akakatishwa na habari iliyokuwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la
"GAZETI LA TAA YA JAMII KATIKA HABARI PICHA LINAANDIKA MAUAJI DAR ES SALAAM NA BUJUMBURA HAPATOSHI!!!" alisema kwa mbwembwe za kiandishi wa habari huku akiwaacha wasikilizaji kwa sekunde kama siyo dakika kadhaa wakitafakari ni kitu gani kinaendelea.
"inasemekana kuna fukuto linalo endelea kama siyo mapinduzi katika moja ya nchi ni kuvunja uhusiano wa kidiplomasia, wahusika katika suala hili vigogo wazito katika majiji haya wadaiwa kuhusika, jitahada za kumpata waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki zagonga mwamba ,Habari kamili utaipata katika ukurasa wa pili...........gazeti la habari moto lenyewe limepambwa na habari picha ikimuonesha Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa kwenye mkutano na wakuu wa vyombo vya usalama huku kichwa cha habari kikikolezwa kwa wino mwekundu na maneno 'SAFARI HII WAMEYATIMBA!!! kina nani hao jipatie nakala yako katika ukurasa wa pili na wat atu upate kujua undani wa habari hii '"
"Kumbe kuna mambo yanaendelea chini chini na sisi tupo kama vipofu mme wangu" aliongea mke wa jamaa yule huku akiacha kufagia na kuganda kwa sekunde kadhaa huku akimuangalia mme wake
"mambo kama haya huwezi kuyatambua kwa sababu mitandao imewaziba macho na fikra zenu mmekuwa kama wenda wazimu kutwa kucha umbea mara huyu kalala na huyu sijui huyu kala kitimoto siku ya mfungo wa Ramadhani.......inasaidia nini katika kukujenga kiuchumi na fikra kama mpigania uchumi mke wangu" aliongea kwa msisitizo huku akionekana kukereka bwana yule
"sasa nimekuuliza vizuri unanijibu kwa kunifokea..........wewe umeamka na mimi si bure ngoja nikaoshe vyombo maana huchelewi kunipiga" aliongea. mwanamke yule huku akijifunga tenge lake huku akifata uelekeo wa jikoni ndani ya nyumba ile.
"wanawake wengine ni wapumbavu sana yeye anadhania kishinda mtandaoni ni sifa........unaweza kutembea kwa mwili wako unaonekana mzima wa afya kumbe ulishakufa kifikra na mawazo shenzi kabisa nijiendee kazini nikiendelea kukaa hapa nitamzaba vibao" alijisemea yule jamaa huku akiamka kitandani pale na dakika kadhaa mbele alikuwa ndani ya vazi nadhifu lililo chafuka vyeo mabegani, akakisogelea kioo kilichokuwa katikati ya kabati kubwa la nguo na taswira ya pande la mtu ikajichora na tabasamu likaonekana upande wa pili wa kioo hata hivo halikudumu sana kwani lilipotea baada ya sekunde zisizozidi kumi.baada ya simu yake kutoa mlio.
"usipite ofisini kwako nyoosha ikulu moja kwa moja na sihitaji maswali tititititi,,,,,,,,,,,,,"
*itaendelea
Ni bora kusafiri kwa matumaini kuliko kufika, tukutane toleo lijalo kwani kuna mengi utajiuliza ni nani mtu huyu anayeamshwa na taarifa za magazeti? Je ataweza kupambana na waasi wanaosemekana kuharibu amani? Tukutane toleo lijalo.Tcaho
 
Inatosha...
Wapeleke wasap ukavute mkwanja...
Mjini shule.......
 
Sasa mimi na wewe nani masikini?
Mimi ninauwezo wa kumungisha buku buku kila kipande apate za kujisogeza
Wewe tajiri huna hata buku, umuunge mshikaji anajipinda kuleta burudani ?
kwani ww una uhakika gani kama mtunzi ana njaa ya hela hizo bukubuku unazojitapa unazo..tuliza kijambio ww na vp kama mtunzi yupo vizuri kiuchumi amejitosha sasa ww nani umpangie hobby zake kwenye maisha yake.?
 
NAPENDA NIWASHUKURU WATU WOTE MNAOIFATILIA NA KUISOMA SIMULIZI HII KARIBU KILA SIKU TANGU IMEANZA KURUKA KATIKA JUKWAA HILI LAKINI VILE VILE SISI SOTE LENGO LETU NI KUBURUDIKA NA KUELIMIKA KUPITIA SANAA, MALUMBANO NA MITAZAMO YA TOFAUTI HAITUJENGI NI KWELI UPANDE MMOJA UNAWEZA KUWA NA HOJA SAHIHI KWANBA IFIKE MUDA MTUNZI NAYE AFAIDIKE NA KAZI YAKE VILE VILE KUNA UPANDE UNAOSEMA KUPITIA HOJA ZAO KWAMBA NI HOBBY YANGU NI SAHIHI KABISA HOJA ZAO ZOTE ZINA AKSI NIA NA MATEGEMEO YANGU KUPITIA KAZI HIYO NAMI NITATIMIZA WAJIBU WANGU KWENU KAMA MNAVYOHITAJI ILI KUONDOA HUU MGOGORO NA NAIMANI PANDE ZOTE MBILI ZITAPATA MAJIBU YA KILE WALICHOKIWASILISHA KWENYE HOJA ZAO.
 
“Mazingira si kitu kinachotokea nje yetu; ni sehemu yetu. Hatupaswi kufikiria juu ya kuokoa dunia tu, bali kutafuta njia ya kuishi kwa usawa na dunia."
Sadhguru
TUENDELEE TULIPOISHIA……………….
sauti nzito na yenye mamlaka ilikoroma
"mmmhhhh kuna nini.........siku ngumu imeanza asubuhi yote hii Mungu nitangulie" akapitisha sekunde kadhaa akiwa kwenye tafakuri nzito na kisha akajongea hadi mlangoni na kutokomea nje na hapo alimkuta dereva wake na mlinzi wake wakimsubiri, walipomuona walikakamaa na kutoa salamu ya heshima kwa kupiga saluti akaitikia na kuingia kwenye siti ya katikati tayari kwa safari ya kwenda ikulu geti lilifunguliwa na mtu yule aliyeonekana kuwa afisa wa ngazi za juu wa jeshi la polisi, wakati hayo yakiendelea meza mbalimbali za kuuzia magazeti zilikuwa zimezungukwa na watu huku mijadala mbali mbali ikiwa ni ile iliyoibuliwa na habari zilizokuwa kwenye vichwa vya habari katika ukurasa wa mbele wa magazeti pendwa mawili.
"Muda mwingine serikali inajifanya ni pumbavu ili kuwapumbaza wa pumbavu wanaofikiria wanai pumbaza yenyewe" aliongea mzee mmoja kiasi cha kuwafanya watu wote kugeuka
"kwanini unasema hivyo mzee wangu ikiwa nchi yetu kwa sasa inaghubikwa na matukio ya kutisha na kila taarifa zinapotoka hazina majibu kamili mara leo hivi kesho unasikia mara IGP ameuawa haiingii akilini hata kidogo mtu kama yule ajiue kwa kipi ulinzi anao tena wa kutosha hii inanifanya niamini kuna kitu hakipo sawa nchini" alihoji kijana mmoja huku akimtazama mzee yule akiwa ametengeneza hoja zake.
"kho kho kho sikiliza kijana umeanza vizuri ila umemaliza vibaya iko hivi usiwe na pupa na papara kuamini kila kinachopenya kwenye ngome za masikio yako na siyo wewe peke yako hata nyie wengine" alisema hivo huku akiwatupia macho watu wale kwa zamu nao waliishia kucheka tu na wengine wakimdhihaki kuwa mzee yule ameikimbia familia yake huko kijijini na amekuja kusumbua watu mjini.
"ndiyo tatizo la kizazi hiki chenye papara na ujuaji mwingi ila hakijui chochote ndiyo maana leo hii kuna matangazo ya kuongeza nguvu za kiume kuliko kizazi chochote kile..........iko hivi uongo una tabia ya kupanda ndege na kulifikia eneo la tukio tofauti na ukweli unao panda baiskeli na hakika huchelewa kufika ila unapofika tukioni uongo huona aibu na kutoweka kila kitu hubaki kweupe kama jua la saa tisa kila kitu kitakuwa wazi na hii ndiyo imani na hasira ya serikali hii" hakusubiri maswali katika mjadala ule alipotea eneo lile na mjadala ukazuka tena kuhusu mzee yule mwenye maneno mazito na ya kusisimua huku wengine wakimshuku ni afisa usalama wa taifa huku wengine wakikanusha huku wakijiapiza kumfahamu mzee huyo kama mshona viatu mtaa wa nyuma na aliitelekeza familia yake huko mbalizi mbeya na kukimbilia mjini.wengine wakaenda mbali kuwa huenda ni mchawi na ndiye anayewasumbua usiku wasilale kwa amani.
Wakati hao wakiendelea na mjadala huo mzee yule alikuwa akinunua salio na kisha kupiga simu sehemu ikaita kwa dakika kadhaa na kukatwa kisha ukaingia ujumbe.
"MAKUMBUSHO SAA 4 ASUBUHI, KAUNDA SUTI, ID UTAIKUTA GETINI JINA LAKO 012 titititi" simu ikakatwa na kumuachia tabasamu mzee huyo, halikuwa tabasamu la mahaba au tabasamu la furaha bali tabasamu la kikatili.
"mwandishi hakukosea kusema wameya kanyaga nawaonea huruma wale wote waliochagua maumivu ya majuto watakufa wakijutia kutochagua maumivu ya nidhamu napenda ninachokiona" alijiwazia mzee yule
BUJUMBURA-BURUNDI
Saa 1:25 asubuhi
Kama yalivyo andika magazeti ya nchini Tanzania,ndivyo ilivyokuwa nchini humo huko magazeti kama all Africa na The Africans ilikuwa kama vichwa vyake vimehaririwa na mwandishi mmoja kwani maudhui ni yale yale huku magazeti yakipambwa na picha za maiti mbili jirani na ulipo ubalozi wa nchi ya Tanzania nchini burundi lakini pia kukiwa na picha ndogo ya mkuu wa jeshi la polisi nchini humo huku maswali yakiwa lukuki vichwani mwa wananchi lakini pia viongozi waandamizi katika nchini hiyo kwani ni wiki kadhaa tangu yatokee mauaji na kulipuliwa jengo hilo huku ikisemekana balozi pia ameuwawa, leo tena wanaamshwa na habari hiyo nzito ya kuuwawa kwa watu wale huku mmoja akionekana ni yule aliyekuwa akitafutwa kwa donge nono asubuhi, huku mwingine akisemekana ni mtanzania mwanajeshi mwenye cheo cha luteni usu huku akionekana ni mtu aliyefuzu mafunzo na mbinu za kimedani.
SNR HQ-BUJUMBURA
Saa 3:45
"Good Morning Mr President........." aliongea kwa unyenyekevu mtu yule aliyeonekana kama bosi katika ofisi ile
"what is going on..........i appointed you not to just sit and wait for cosmetics reports, my country is in chaos and nothing is ongoing, ask yourself Director how many times i tell you to act smart and you still repeat those mother https://jamii.app/JFUserGuide*ng mistakes" aliunguruma mheshimiwa raisi
"sorry boss but preliminary investigation shows that Tanzanian try to.........." alikatishwa asiendelee kuongea na mtu yule aliyeonekana ni bosi wake na raisi wa nchi hiyo
"listen carefully you son of b*tch, now i prove that your the most incompetent Director of intelligence in this country, let me tell you one thing if lift your *ss up there and i will drag it down here and just remember one thing you have 12 hours to come with answers or select any prison that you will be comfortable Mr.Director titititi"
"Ooops....." alishusha pumzi ndefu huku jasho likimmwagika.
***********************
NIPENDE KUTOA SHUKRANI TOKA MWANZO WA SIMULIZI HII HADI HIVI SASA ILIPOFIKIA NA NICHUKUE FURSA HII KUSEMA YA KWAMBA KWA TSHS 1000 UTAWEZA KUPATA VIPANDE VILIVYOBAKIA VYA SIMULIZI HII.
TUKUTANE PM KWA ATAKAYEHITAJI
Tchao.
 
"what is going on..........i appointed you not to just sit and wait for cosmetics reports, my country is in chaos and nothing is ongoing, ask yourself Director how many times i tell you to act smart and you still repeat those mother Where We Dare To Talk Openly mistakes" aliunguruma mheshimiwa raisi
"sorry boss but preliminary investigation shows that Tanzanian try to.........." alikatishwa asiendelee kuongea na mtu yule aliyeonekana ni bosi wake na raisi wa nchi hiyo
"listen carefully you son of b*tch, now i prove that your the most incompetent Director of intelligence in this country, let me tell you one thing if lift your *ss up there and i will drag it down here and just remember one thing you have 12 hours to come with answers or select any prison that you will be comfortable Mr.Director titititi"
"Ooops....." alishusha pumzi ndefu huku jasho likimmwagika.
***********************
NIPENDE KUTOA SHUKRANI TOKA MWANZO WA SIMULIZI HII HADI HIVI SASA ILIPOFIKIA NA NICHUKUE FURSA HII KUSEMA YA KWAMBA KWA TSHS 1000 UTAWEZA KUPATA VIPANDE VILIVYOBAKIA VYA SIMULIZI HII.
TUKUTANE PM KWA ATAKAYEHITAJI
Tchao.
Mkuu weka mawasiliano yako iwe rahisi kukupata...ili tuweze kupata huduma
 
Back
Top Bottom