Simulizi ya Kijasusi: Giza la Wasaliti

Simulizi ya Kijasusi: Giza la Wasaliti

MAANDIKO NA NADHARIA MBALI MBALI ZINA SISITIZA KWAMBA KATIKA MAMBO YOTE NI VYEMA KUSEMA UKWELI, LAKINI KATIKA HAYO SIYO KILA WAKATI NA KATIKA KILA KITU YATUPASWA TUSEME UKWELI…………KWANI YANA MAANA GANI MANENO HAYA MANENO UNGANA NAMI SEHEMU YA KUMI NA NNE
"nasikia vanessa alikuwa ‘SHIMO LA TEWA’ leo anahojiwa vikali na malaika wa kifo pamoja na kile kimama cha nyumba nyeupe" alifungua maongezi hayo pande la mtu lilikuwa limeyaficha macho yake katika miwani na mkononi alikuwa ameshika kimiminika cha mvinyo wa bei mbaya brandi ya ‘Cabernet Sauvignon’
"unasema amehojiwa wapi na nani? mchongo si ulikuwa uishie polisi na vipi maelezo na askari wa kumhoji si tulikuwa tusha mpenyezea kamanda wa mkoa huku akiniahidi hakuna kitakacho haribika imekuwaje tena uniambie ameenda kuhojiwa sijui wapi Kobe acha kunichanganya"aliongea mzee wa makamo ambayo bado mwili wake ulikuwa timamu kwa ratiba ya mazoezi anayozingatia kila siku huku akiwa na sigara kubwa mdomoni
"eeennhh niliambiwa hivyo na yule mtu wetu aliyeko jikoni na alinieleza kuwa watu wetu walikuwa wanahojiwa vikali na watu wa idara ya kupambana na dawa za kulevya na uhamiaji, ila ni vanessa peke yake aliyepelekwa kuhojiwa na idara ya ujasusi tena alikuwa katika mahojiano makali na dada mmoja wana muita malaika wa kifo na mheshimiwa raisi" alisema yule jamaa mwenye jina la kiroboto huku akipiga mafundo mawili ya mvinyo ule ulioanza kumkolea.
"weeee kiroboto umeanza lini kuleta habari za magazeti ya udaku kwangu.....tanzania na kiidara chake cha ujasusi mbona wanafanya maigizo sana haya huyo malaika wa kifo unayemsemea amepata nini kwa mtu wetu"aliongea kwa dharau na majivuno konokono jamaa aliyekuwa amekaa kimya muda wote akiwa sikiliza.
"mpaka raisi anaondoka mle ndani mtu wetu alikuwa hajatapika maelezo yoyote kiufupi aliwakazia sana na hakusema chochote kutuhusu "
"safi sana nimeongea na mkuu na amesema ndani ya masaa matatu mtu wetu atakuwa anaiacha nchi kuelekea visiwa vya Havana-Cuba kupumzika ama jiji la Arusha liwe majivu, kikamshuka yule mmama na sasa ana haha kutafuta bomu lilipotegwa ila amehakikishiwa hata apewe mwezi mzima wa kulitafuta hatolipata na hata akina kapeto nimeambiwa watatoka lisaa limoja baada ya vanessa kuiacha ardhi ya tanzania.
"hahahah kazi nzuri sana nina imani hata chatu anafurahia sana kuwashika pabaya sana yule mama na vibaraka wake sasa baada ya hapo ndiyo ule mpango wa mapinduzi utafutata hahahahaha mimi nikiwa waziri wa fedha najua wewe kobe watakupeleka madini ushindwe tu kumiliki bastola ya dhahabu hahaaha watoto wazuri wote wa hapa mjini watali imba jina lako"watu hao watatu wenye majina ya uficho ya kiroboto,kobe na konokono walikuwa nchi ya jirani ya Rwanda huku wakibwia mvinyo huku wakipiga soga za hapa na pale
********
saa moja lililopita katika ofisi ya idara ya ujasusi, underground ilikuwa na watu watatu tu peke yake na mazingira yalikuwa ya ukimya wakati walinzi wa mheshimiwa raisi na chifu wakijua kuna kikao kinaendelea ofisini, chifu alikuwa amewasha kompyuta yake huku akifatilia kinachoendelea huko chini huku ajenti chiku akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia huko chini akiwa makini kufatlia nyendo za yule binti wakati anafanya mazungumzo na mheshimiwa raisi.
"sina dakika nyingi za kukaa hapa andika majina unikabidhi karatasi" alisema mheshimiwa raisi huku akimkabidhi kalamu na karatasi huku akiwa makini
"mheshimiwa raisi hili jambo ni zito na linahusisha watu wakubwa sana na wengine wako katika serikali yako, nakwambia hivi siyo sababu ya mateso niliyoyapata ila ni kwasababu ya wema kiduchu ulionionesha na kiuhakika mtandao wa dawa za kulevya kwa nchi yetu unaongozwa na mtu mmoja ambaye hata mimi sijawahi kumtia machoni anaitwa ‘VANOSACA’ ila usishangae mtu huyu kuwa na jina hili kwani ukiligeuza unapata maana halisi ila ni mtu hatari na hapa ikulu ashakuja sana tu kiasi cha kutengeneza mtandao wake serikalini huku akiwa na kofia ya ufanyabiashara, biashara zake ni kama kivuli tu ukitaka kumpata angalia video footage za wafanyabiashara wanaoingia ikulu mimi sijawahi kumuona zaidiya kusikia jina la CASANOVA tu kama mkuu lakini mkimpata huyo atawapeleka kwenye mzizi mnaoutaka" alisema Vanesa
"umeniita hapa ili uje uniambie hayo maelezo machache tu ambayo hayajitoshelezi"
"la hasha mheshimiwa mimi wala siyo shemeji yake na makamu wa raisi"
"what.......unasemaje binti?"
"mimi siyo shemeji yake na makamu wa raisi bali wote watatu tulikuwa kwenye misheni, misheni hiyo ilianza kwa kukutana kigoma sijui wakaoana ilikuwa ni kuwapa giza machoni idara ya ujasusi ila mimi ni mzaliwa wa burundi na kwa upande wa mke wa makamu wa raisi, ni mzaliwa wa burundi ila makamu wako wa raisi anatoka nchi jirani ya congo" kulikuwa na kiyoyozi cha kutosha kwenye hilo gari lakini halikuzuia jasho jembamba kumtoka mheshimiwa raisi kwa nimaelezo aliyokuwa anayatoa yule binti ni mazito na watu wale walikuwa jikoni kabisa na kama ni nchi ilikuwa iko uchi bila nguo, kama jasusi mbobevu alijilaumu sana kuto kuyajua hayo tangu mwanzo lakini mwili wake uliingiwa na ubaridi baada ya kukumbuka mchakato mzima wa uchaguzi kwamba kuelekea kura za maoni ndani ya chama alifuatwa na mheshimiwa raisi mstaafu na kwa heshima akamuomba apambanie kiti na huyo bwana akiwa kama makamu wake.
"lakini hilo siyo kubwa sana kushinda hili, hivi unakumbuka oparesheni iliyorudisha maiti mbili za wanajeshi wenu ndiyo oparesheni ya mwisho mliyofanikisha kwa kiasi kikubwa kutuliza amani nchini Congo, kuna watu hawakupenda iwe hivo ndiyo maana mamluki ni wengi serikalini kwako kuliko wazalendo na kwa taarifa tu ninayokupa ni kwamba una siku chache sana za kuvuta pumzi kabla Chatu hajakumeza na ambacho hujui ni kwamba walifanikisha kuiba codes za kuendeshea mitambo ya nyuklia yanayodhalishwa kisiri siri katika maabara za kambi ya jeshi Mafinga na hata mlipuko wa kambi ile na kuibiwa silaha chache ilikuwa geresha tu kuficha kilichotokea nyuma ya pazia."
"wewe binti wewe haya yote umeyapata wapi"
"samahani mama wakati niko kwenye hiki kikundi nilimvutia sana jenerali mstaafu kiasi cha kunifanya niwe mchepuko wake kwa siri sana na alipogundua mimi ni mwenzao hakuwa akifanya siri kuongea na simu za washirika wake mbele yangu na hapo ndipo kulipokuja kutokea mpango wa kukufedhehesha wewe ki madaraka kwa kukupiga matukio huku akishirikiana na mtu mmoja ambaye hakuwahi kumtaja ila anaonekana ana nguvu sana au alishawahi kuwa na nguvu kwenye nchi hii na huyo ndiyo anaemfadhiri huyu jamaa mwenye kitu kingine"
"kitu kingine???......"
"ndiyo.....huyu mtu mwenye nguvu anamfadhiri MUSTAPHA ABD NUR AHMED, ambaye nyie mnamchukulia kama gaidi ila ni zaidi ya gaidi anayetafutwa na serikali ya marekani kwa miongo miwili sasa na kutunzwa kwake katika lile gerezai likuwa ni siri na hata kuondoka kwake gerezani mle pia ilikuwa ni siri na kwa kiasi kikubwa kuna mikono ya watu wazito ilipita ndiyo maana hata kwenye data base yenu ya makampuni hakuna kampuni iliyosajiliwa kutoa huduma za uzibuaji wa mabomba na kama haipo ilipataje tenda ile je wizara na jeshi la magereza halijayatambua haya?" Aliuliza swali tena binti yule na kumuacha mheshimiwa mdomo wazi
"kuna mabomu wameniambia yatalipuka katika jiji hili hebu nisaidie katika hili binti yangu, hebu angalia ni watu wangapiwatapoteza maisha uhawahi kuwaza kama mlipuko huo utatokea ni watoto wangapi watapoteza ndoto zao na maisha yao kwa ujumla, ni mashabiki zako wangapi utawapoteza lifikirie hilo kisha uniambie ni wapi yalipo." Aliongea mheshimiwa raisi kwa sauti ya kusihi
"mimi sijui yalipo ninachokijua nadhani nimekueleza maamuzi ni yako japo sidhani kama itasaidia chatu amekasirika kupata hasara ya kiasi kikubwa cha pesa hivvo hata ukinipeleka bado mabomu yatalipuka na usipofanya hivyo bado atakutia hasara tu kama walivyo zikwapua zile trilioni tano kule katika mapori ya singida......kiufupi unatakiwa uwaze maili nyingi kuweza kuwapata wahusika ukiwa na ushahidi mzito bila hivyo nauona utawala wako ukidondoka na wewe ukizikwa kwa aibu"
"kwahiyo unataka kunambia jenerali mstaafu mzee Chukurubu thomas ndiyo yuko nyuma ya haya masuala" aliuliza mheshimiwa huku akikunja sura
"utakuwa sahihi kwa upande mmoja ila kwa upande mwingine kama uliniskiliza kwa umakini nilikwambia kwamba kuna mtu anawasiliana nae mara kwa mara na huyo ndiyo mkuu wake ambaye ana nguvu na ushawishi mkubwa kwa watumishi wa serikali na vile vile jamii na kama haitoshi fununu zilizopo nikwamba hata huyu mtu ana bosi wake ambaye sio jenerali mstaafu wala kibaraka mwingine anayemfahamu zaidi ya huyu mtu mwenye nguvu katika nchi hii, na kumfikia inabidi uwe umefanya kazi ya ziada sana kwani hata huyo mtu mwenye nguvu sidhani kama kuna mtumishi wako yoyote anaweza kumpata kirahisi labda kama utawapata watu wawili tu jenerali au yule aliyejifanya ni dada angu maana ndiye kiburudisho chake.” Alimaliza huyo binti huku akimuangalia mheshimiwa raisi kwa masikitiko
"nini unaongea wewe binti unataka kusema yule mke wa makamu alikuwa anamsaliti mmewe kwa huyo mtu.........na mbona habari hii haijaletwa mezani kwangu au chifu anatambua hili na akaamua kunyamaza nalo" alijiwazia kwa sauti mheshimiwa raisi.
"mheshimiwa wewe ni mwepesi sana au kusahau habari nilizokupa zimekuchanganya ni hivi tangu wameanza kuishi kwa kujiita mume na mke makamu wako hajawahi kushiriki tendo la ndoa na huyo unayemjua ni mke wake kwasababu huyu makamu wako wa raisi alikuwa hana nguvu ya kusimamisha uume wake baada ya kuchomwa sindano iliyokuwa na dawa kali kiasi cha kuuwa mshipa mkuu wenye kazi ya kupeleka damu kwenyeuume wake na walimuahidi kwamba watampa dawa ili arudie hali yake ya uanaume kamili endapo kama kazi ya kukuangusha ikikamilika ila alifanya kosa moja la mwaka ambalo litamtesa maisha yake yote kwani kiukweli hakuna dawa ya kufanyahivyo na hata wale.watoto walikuwa siyo wake bali ya huyo mtu ndiyo maana huoni hata mmoja akimfanana hata kwa sikio lakini pia bado kuna jambo moja zito huja lifahamu na hilo ndilo linawapa kiburi mpaka kukufanya ukose maamuzi sahihi ni kwamba wanataka kushambulia nchi jirani ya kenya kwa ajili ya kuibua taaruki ili nchi isitawalike huku ukionekana umeshindwa kuongoza na kile ambacho hujui hata huyu spika wa bunge ni mtu wao na wamepanga kumtumia yule mbunge wa kule mkoa wa kusini kupeleka hoja katika hati ya dharura ya kutokuwa na imani na raisi na robo tatu ya wabunge watanunuliwa na watapiga kura ya ndiyo kisha wanakutoa madarakani na baadaya hapo utabaki huna ulinzi utauwawa na baada ya hapo utazikwa kwa aibu badala ya heshima." jasho liliendeleakumwagika japo kuwa kiyoyozi cha gari ile aina ya GMC kikiwa kinaendelea kuweka ubaridi na hewa safi.
***********************************
WALE WOTE WANAOTUFUNDISHA MAANA YA UBINADAMU KUMBE SIYO WANADAMU WENZETU…………. Kumi na nne inaisha hapo tukutane kumi na tano tuone hili jahazi litafika au litazama katikati ya kina cha bahari Tchao
 
“KATIKA KIVULI CHA UKWELI , MARA ZOTE KUNA GIZA LA SIRI AMBALO LIKIFICHULIWA LINAWEZA KUWAANGUSHA FALME NA KUVUNJA MIOYO ISIYOHESABIKA…….. UNATAKA KUJUA NI SIRI ZIPI HIZO TUONGOZANE SEHEMU YA KUMI NA TANO
Endelea………
kwanini uliamua kuhatarisha maisha yako kwa kukubali mateso makali si ungesema tukiwa kule chumba cha mwanzo huenda usingekuwa na vidonda na hata huko gerezani unapoenda sidhani kama utatumikia adhabu kwa raha na sidhani kama watakuhudumia vizuri " alisemahivyo mheshimiwa raisi huku akimuonea huruma binti yule
"hahahaha ilitakiwa iwe hivyo sikiliza mheshimiwa kama nilivyokwambia serikali yako imezungukwa na mamluki nandiyo maana sikutaka kuhatarisha maisha yangu kwa mara ya pili kwa kufunguka kila kitu kwa maana ningejulikana mimi ni jasusi mlaini na ningekufa mapema nilitaka waone ni jinsi gani nilivyokuwa mgumu katika kutoa siri zao ili niendelee kununua pumzi yangu ya bure......mheshimiwa naomba utambue hili na uliweke akilini kwako kuanzia dakika hii na ulisahau hilo neno mara moja na uchukulie sijakwambia" akameza mate kisha akamtazama raisi machoni ili aweze kutazama kilichopo,ebhana eeennnhh macho yake yalisadifu unyama ambao huupati sehemu yoyote zaidi ya shirika la ujasusi la urusi FSB.
"mimi ni jasusi ninayefanya kazi na shirika la ujasusi la urusi lakini pia niliingizwa kwenye idara ya ujasusi ya nchi ya burundi ili tu niweze kuifanya kazi yao kwa usahihi lakini pia nilichukuliwa na CIA kwa ajili ya kazi hii hii wao walikuwa na vyanzo sahihi vilivyofanya wawe mbele ya muda siyo kwamba mkurugenzi wenu wa idara ya ujasusi aliyepita alikuwa halijui hili jambo wakati wewe uko katika kozi yako ya mwisho na CIA, kwa mara ya kwanza nilisikia jina lako katika korido zao kwamba wewe ni mwanamke wa kazi unayefaa kukaa kwenyekiti hicho unachokikalia leo ni kwasababu wewe umewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwapata watu wao.....hivyo usijefikiri uliingia hapo kwa nguvu na akili zako na usidhani katika hatua unazokanyaga usione kama hakuna macho yanayokutazama kutoka kwa hawa CIA, siku utakayo nikabidhi ndiyo siku ambayo nitakuwa nimekamilisha ripoti yangu na nitaishi kwa amani na hata nikifa nitakuwa na amani sana ni hayo tu mheshimiwa" mheshimiwa akafungua mlango nakushusha mguu mmoja chini alivyotaka kushusha mwingine akavutwa mkono wake alipogeuka akakutana na tabasamu pana kutoka kwa yule dada.
"siitwi Vanessa Ndelwa kama rekodi zinavyosema ila naitwa OLIVIER AMIE SANTIANA na hata ukitafuta katika rekodi za idara ya ujasusi ya Burundi(SNR) hauwezi kufanikiwa kuliona jina hili ila ukifungua majalada ya CIA utalipata jina hili ila ningependa kukusaidia kitu cha muhimu sana ukitaka kulipatia ufumbuzi suala la bomu, nyumba namba 54 daraja mbili songea utapata jawabu........siku njema "Queen of hell".
"umejuaje hilo jina wewe mtoto mdogo"
"hahaha ntakwambia nililifahamu vipi mara tu serikali yako itakaponikabidhi kwa ndugu zangu na siyo magereza ya nchini kwao"
DODOMA-TANZANIA
saa 06:45 mchana
"mheshimiwa spika kuna simu yako kutoka ikulu iko kwenye line"
"hallow spika wa bunge hapa na zungumza nani mwenzangu" alikoroma spika kwani ni muda ambao alitoka kupata taarifa zilizomvuruga.
"unazongumza na mkuu wa nchi"
"oooohhh mheshimiwa raisi habari za muda huu"
"si salama sana ila nimekupigia ili nkuambie kwamba itisha kikao cha bunge katika hati ya dharura kisha kuna mbunge atatoa hoja"
"lakini unatambua inakuwa ngumu kuwapa wabunge na vile vile ni juzi juzi tu tumelifunga bunge letu tukufu baada ya kupitisha bajeti kuu ya serikali, hivyo itakuwa ngumu sana kuwapata wabunge wote ili kufikia akidi inayotakiwa na katiba hivyo mheshimiwa kiasi fulani inakuwangumu ila nitajaribu ila kama jambo ni nyeti sana unaweza kulifanyia maanmuzi tu mheshimiwa na likatekelezwa kikamilifu"
"ni suala la kikatiba na bunge lako ndilo linalotakiwa kufanya hivyo na ni haraka iwezekanavyo"
"sikiliza mheshimiwa kama ni suala la kikatiba basi mimi nakushauri ili tusije fanya vitu vya ajabu tukalaumiwa mbele huko na vizazi, ni heri tungesubiri kikao kijacho ili tulifanye jambo kwa usahihi alafu mheshimiwa unajisahu kuwa mimi ni mkuu wa huu mhimili na nina imani unaijua vizuri katiba yetu inasemaje kuhusu mgawanyo wa madaraka hivyo kama bunge tuna uhuru wetu hatupangiwi na mtu yoyote" alisema spika kwa jeuri na kiburi.
"waoooh nimeupenda ujasiri wako ila upo tayari kuwapa notisi ya kuwataarifu wafike bungeni pindi ile hoja yenu ya kutokuwa na imani na raisi itakapopewa mikono ya baraka na wakuu wa genge lenu........" akaiachia sentensi hiyo ielee hewani huku akisikiliza utulivu wa upande wa pili.
"unasemaje wewe naona umechanganyikiwa kwa haya yanayoendelea labda cha kukushauri ni heri uachie madaraka huenda wananchi watakusamehe ila kama ukiendelea kukaza fuvu nikuhakikishie kwamba utatoka na aibu na utadharirika nakwambia na kama huna hoja nkutakie asubuhi njem......." alikatishwa
"usisahau mimi ni mwenyekiti wa chama na kama ulikuwa hujui ninakutaarifu kuwa kutakuwa na kikao cha dharura na wajumbe wa kamati kuu ya chama saa nane hapa ikulu ni chaguo lako kufika ama uingie mitini kama wenzio na hizo jeuri unazojibu uwe unafikiria kwanza kabla hujafungua kinywa chako na kingine labda kama hujui au unajua unajizima data spika wangu, umesahau mimi ndiyo niliyependekeza jina lako na wabunge wakakuchagua kuwa spika kama nilikuwa na uwezo wa kulipeleka jina lako pia utambue ninao uwezo wa kukuvua uanachama na nadhani unaelewa maana yake kwamba hutakuwa spika tena labda huo uspika unao uringia utaufanyia nyumbani kwako" akapima tena utulivu wa upande wa pili na alipogundua kwamba amemshika pabaya spika wa bunge la Tanzania akaendelea kumpa maelekezo.
'nataka kuona ofisi yako inachapisha notisi katika tovuti yabunge na katika akaunti zenu katika mitandao ya kijamii haraka iwezekanavyo nina imani upo hapo Dodoma na ujumbe utawafikia wabunge wote kuhusu dhumuni nadhani maelezo mengine utayapata ukifika kwenye kikao hicho........kama una swali lolote sidhani kama nitakuwa na majibu kwa sasa ila utayapata kwenye kikao nikutakie maandalizi mema" akakata simu
***********
"kiroboto nilishakwambia nini kuhusu kunipigia simu tena kwenye hii namb....."
"nisamehe mkuu ila kiufupi kuna taarifa nimezipata sasa hivi kutoka kwa kile kimama kichawi kwamba niitishe bunge kuna hoja ya dharura itakuja mezani na mbunge na nilipomkatalia alisema atanivua uanachama kwasababu kuna kikao cha kamati kuu ya chama kinaenda kufanyika saa moja kutoka sasa na ninavyokwambia nipo kwenye ndege nasubiri kuondoka na alichonichanganya kabisa anajua sipo upande wake sasa nashindwa kuelewa mambo gani yanyoendelea hapa mkuu nimeona nikuulize wewe moja kwa moja kuliko kumuuliza konokono na kobe nisije kuzua taharuki kama unavyo wajua wataharibu kila kitu."
"hahahaha kiroboto tuliza munkari kila kitu kipo kama mipango ilivyopangwa haya yasikutishe anatapatapa tu na hawezi kupata kitu......kaa utulie uone kitakachofanyika asante kwa taarifa naimani baada ya hapa tutazungumza ulichokipata huko.'
"sawa mkuu umenipa nguvu sana wacha nifike" simu ikakatwa na hapo hapo yule mtu wa upande wa pili akatafuta namba moja kwenye simu yake na alipoipata akaipiga iliita kwa sekende kisha ikapokelewa
"nahitaji kiroboto asilione jua la kesho, hii ndiyo iwe safari yakeya mwisho kuivuta hewa safi hii ya bure"
"hilo limeeleweka mkuu na hata maiti yake pia haitowahi kuonekana popote pale"
"safi sana kefa mkimalizana na hilo kuna kazi moja ya muhimu sana mnatakiwa kuifanya kuna mjinga amerudi tena mjini na kwa jicho langu ninaamini kabisa anataka kufukua makaburi tuliyoyafunika kwa zege nadhani mnakumbuka wale wajinga mlio wa maliza mara tu walivyofikisha ule mzigo sasa kuna mjinga mmoja walimtekenya na akapiga chafya mochwari sasa nahisi anataka kuja kuafukua wenzake aone ni wapi risasi zile ziliwatekenya mpaka hawakupiga chafya kama yeye sasa hivi hata tekenywa nataka mwili wake safari hii uwe kama chandarua."
"bosi nadhani unaelewa hatujawahi kuwa na kazi mbovu....huyu kayakanyaga" alisema kwa sauti kavu na nzito sana.
****************************
MAMBO YANAZIDI KUWA MOTO HAKIKA GIZA LIMETANDA KWA PANDE ZOTE MBILI TUKUTANE SEHEMU YA KUMI NA SITA HUENDA TUKAPATA SULUHISHO AU TATIZO KUONGEZEKA TCHAO
 
"HAKUNA JAMBO LINALOUMA KAMA KUTAMBUA KUWA MTU ULIYEWEKA IMANI YAKO KWAKE, NDIYE ANAKUSALITI KWA SIRI KATIKA GIZA LA UAMINIFU, UKWELI NI KIVULI KINACHOSHINDWA KUFICHIKA MILELE” …………. UNATAKA KUFAHAMU NINI TAFSIRI YA MANENO HAYA NISOME KATIKA SEHEMU YA KUMI NA SITA

IKULU -DAR ES SALAAM
Saa 8:15 mchana
wajumbe wa mkutanano mkuu wa chama walikuwa wameshafika huku wakiwa wamependeza na sare zao za bluu bahari lakini mbali na yote, hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua kiini cha kuitwa kule kwa dharura huku wajumbe waliokuwa mbali na mkoa wa dar es salaam wakilaziimika kukodi ndege za kuwafikisha kwenye mkutano huo, na hakuna aliyeonekana kukosa kwani zoezi hilo liliratibiwa kwa weledi sana huku idara ya ujasusi ikitia mkono wake,
"mheshimiwa raisi tayari wajumbe wameshafika na wako tayari" aliongea katibu wa raisi bi Siaely Mnzava
"sawa, tunaweza kwenda" aliongea raisi huku akisimama tayari kwa safari
"mwewe anatoka.....narudia tena mwewe anatoka kila mtu akae kwenye nafasi yake" ilisikika sauti ya mlinzi mkuu akiwapa maelekezo wenzake wanaotengeneza timu ya kumlinda mheshimiwa raisi, huku wote wakiwa ni makomandoo kutoka idara ya ujasusi ya taifa na walimu ongoza raisi mpaka nje ya mlango wa chumba cha mkutano kisha akawapa ishara ya kusimama nje.
"mheshimiwa raisi una uhakika na hilo jambo......nimeapa kukulinda na usipatwe na tatizo lolote hata kama litahatarisha maisha yangu ila jukumu langu la kwanza ni Hilo" aliongea kwa msisitizo mlinzi mkuu huku akimtazama mheshimiwa raisi.
"nina uhakika......na hakuna jambo baya litakalo tokea na mimi ndiyo raisi, hivyo basi nimekupa amri ya kubaki hapa nje kuna tatizo, ulikula kiapo kunilinda raisi na mimi hapa naingia kama mwenyekiti wa chama hivyo uraisi nauacha hapa mlangoni na nkukumbushe pia mimi ndiyo kiongozi wako siku nyingine ninapokupa amri sihitaji vipingamizi kutoka kwako au la utakuwa na nia yako nyingine" aliongea mheshimiwa raisi kwa utulivu
"samahani mheshimiwa raisi.......ulimi wangu umeteleza bahati mbaya" aliongea hivyo Jerry, mlinzi mkuu wa raisi
"jiangalie sana" alisema mheshimiwa raisi huku akiingia ndani na huku upande mwingine wajumbe wakisimama huku wakiimba nyimbo za chama huku wakimkaribisha mwenyekiti wao, baada ya makaribisho mafupi yaliyodumu baada ya dakika kadhaa bado wajumbe walikuwa kwenye bumbuwazi ni kwanini mkutano umeitishwakwa hiyo namna ya dharura lakini kilichowapa upofu zaidi ni mheshimiwa raisi kuingia akiwa ameambatana na mpambe wake pekee Kanali Juliana ndunduma mwanadada mkakamavu na mwenye uso usiotabirika, aliwaambia waketi kisha akafungua kikao kwa salamu ya chama huku akiweka ajenda mezani
"jamani nimewaita kwa kikao cha dharula ambacho kiukweli naweza kusema ni cha aina yake huku kikibeba ajenda nzito ila zenye kubeba maslahi ya taifa, lakini pia maslahi ya dunia nzima kwa ujumla" alisema hivo huku akiwakagua katika nyuso zao ambazo bado zilionesha kuwa na viulizo, alitabasamu na kuendelea kukazia kwenye yale aliyoamini yatawagusa walengwa.
"taifa lipo katika matishio ambayo nadhani chanzo chake kinazalishwa na sisi wenyewe......ni heri hata wangekuwa wanaatoka nje ya chama chetu, ningesema kuwa huwenda wameishiwa hoja za kiushindani hasa katika majukwaa.......imenishangaza adui kutoka ndani ya chama tena wengine ni wazee wangu kabisa ila matendo mnayofanya nina imani hata kizazi chenu kitakaposikia nina uhakika watawarudi kwa ukatili mkubwa."
"sitaki kuwachosa sana wazee wangu, kaka ,dada na wadogo zangu niende kwenye ajenda za mkutano huu mbao kama nilivyotangulia kusema ni wa aina yake tangu kuanzishwa kwake......ndugu wajumbe napenda kuwajuza na kuwatangazia kwamba makamu wa raisi amekengeuka na kwa lugha nyepesini kuwa AMEASI............"alisema mheshimiwa raisi kwa utulivu ule ule
"haiwezekani haiwezekani hizo ni chuki za kisiasa yule mzee hawezi kuwa na sifa kama unazozisema tangu lini mtu mkubwa kama yule aliyeapa na kuitumikia ofisi yake kwa weledi na uhodari mkubwa ageuke kuwa muasi........mheshimiwa raisi mimi nimekaa kwenye khicho kiti kwa muda wa miaka kumi na sikuwahi kumpa mtu tuhuma nzito kama hizo kama mna tofauti zenu za kisiasa nadhani jambo sahihi ni kutuliza akili na mmalize tofauti zenu" ikazuka minong'ono ya chini chini kuhusu wazungumzaji wale huku wengi wao wakiwa njia panda
"kuna mwingine ana maoni tofauti au anaunga mkono hoja ya mtangulizi wangu, mzee wangu kabisa aliyeuza jina langu na mpaka leo nimekuwa raisi na vile vile mwenyekiti wa chama hiki na amekiongoza vizuri akishirikiana na nyie wajumbe wa mkutano mkuu wa chama chetu."
"hata mimi na ungana na mheshmiwa raisi mstaafu kwamba siyo sahihi kumtangaza yule mzee kama muasi na kiutaratibu alitakiwa kuwa hapa lakini hatumuoni na kinachotushangaza nikwamba hata mawasiliano yake hayapatikani kiufupi tunataka mwenyekiti atuambie mjumbe mwenzetu yupo wapi na kama haitoshi kwanini apotee alafu aje na hoja ya rejareja kwamba ni muasi katika nchi hii yenye amani tunataka maelezo ya kutosha pasipo kuacha shaka vinginevyo sisi wajumbe tutakutambua kama mtu mwenye nia ovu na kama itawezekana tutaongea na sekretarieti ya chama tuone tunafanya jambo gani dhidi ya mwenyekiti mzalimu" alifoka mzee mmoja anaeshika wadhifawa naibu katibu mkuu wa chama na alipomaliza kuongea bado raisi alikuwa katika tabasamu zito sana hali iliyoendelea kuwachanganya wajumbe kwenye mkutano huo huku kukiwa na mgawanyiko wa makundi mawili wale wenye maslahi na makamu wa raisi na pia wale ambao walihitaji kufahamu ni kwanini imefikia hatua ya mjumbe mwenzao kuitwa muasi....walijipa subira ili kufahamu mbivu na mbichi.
"nchi yetu ilighubikwa na majanga hapa katikati kiasi cha kunifanya mimi mwenyewe niingie kazini kutafuta mzizi wa hiki kinachoendelea.....ndugu wajumbe wa mkutano huu mkuu wa chama ambao nimeuitisha kwa dharura na nimewasikia wazee wangu wawili waionipokea kwenye chama na wengine wamenifundisha siasa kabisa, mimi siyo muumini wa siasa za kuchafuana wala kupakana matope....nina uhakika na ninachokisema achilia mbai vitendo mnaweza kujiuliza wenyewe na natambua kuna watu humu ndani mna watu wenu hata viwanja vya ndege mnaweza kuwauliza je? mahakamu waraisi alirejea baada ya kutoka mkutanoni adis ababa, Ethiopia kama jibu ni hapana atakuwa wapi yeye na walinzi wake?" akameza fundo la mate na kisha akaendelea
"lakini natambua wachache wenu hapa mnatambua kinachoendelea na wapi alipojificha makamu wa raisi na bila kupepesa macho wajumbe mlioko katika mkutano huu kuna wengine ni wahaini kabisa wana mpango wa kufanya mapinduzi lakini niwahakikishie hakuna atakayesalia akila kuku kwa mrija wote wenye mipango hiyo ni heri mjisalimishe wenyewe kabla hamjafikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama"aliongea mheshimiwa raisi na kisha kupiga fundo zito la maji
"vile vile watu hao wengine watakuwa humu na ni wa hakikishie kila mtu aliyeshiriki atafikiwa na asije akajitokeza mtu akapiga kifua chake kwa kuwa ni mwanachama wa chama kinachotawala kwamba nitamuonea aibu au labda ni kiongozi mstaafu au bado yuko ofisini akadhani cheo au pesa zake itakuwa kinga dhidi ya kushtakiwa kwake, nadhani mnatambua vyema hakuna ambaye yuko juu ya sheria hivyo utashughulikiwa sawa na mwananchi yoyote yule aliyefanya uhalifu"
"kwahiyo mheshimiwa mwenyekiti umetuita hapa ili ututishe si ndiyo ajenda kuu uliotuitia kwenye kikao hiki cha dharura, naunga mkono maneno yako kwamba nchi yetu ni kisiwa cha amani......na ukumbuke nilikukabidhi nchi ikiwa shwari kabisa ila napata taarifa kutoka huko huko ndani kwamba nchi imekushinda umekuwa ni mtu wa mipasho tu kama unaimba taarabu, sasa umeona maji yamefika shingoni unaanza kutapatapa niliku heshimisha binti nikakutangaza na ukauzika kwa watu kama unaona mambo ni mazito sina haja ya kukumbusha pale chuo kikuu mwalimu wako wa somo la katiba alikufundisha nini juu ya ukomo wa madaraka yaraisi......umetuita hapa na kutupotezea muda ili ututishe na kesho asubuhi tukutane na vichwa vya habari kwenye gazeti ya kuwa umeupiga mkwara mzito, hilo haliwezekani, ila tukitoka hapa itisha mkutano uwaambie watanzania makamu wao wa raisi alipo na mtoe sababu za kumficha na kama haitoshi umuombe msamaha mbele ya waandishi wa habari na ukiona ni vema sana unaweza ukajiuzulu kabisa ili uwapishe wenye siha njema ya uongozi..........tofauti na hapo mimi mwenyewe nitawahamasisha wananchi kuingia barabarani kuja hapa ikulu tukiishinikize serikali yako dhaifu itukabidhi makamu wetu wa raisi au wajumbe wenzangu mnaonaje" aliongea kwa kufoka mheshimiwa raisi mstaafu SAID BENDERA,huku akimaliza kwa kutoa kauli ya kuona idadi ya watu watakaokuwa pamoja nae kwa shutuma kali alizotoa dhidi ya mwenyekiti wao.
"mimi nadhani si vyema tukaparuana humu ndani kwani ni kitu gani hasa kinaendelea, mheshimiwa mwenyekiti maana sisi wengine tumebaki gizani bila mategemeo ya nuru hebu tusaidieni sasa ni nini hatma na ajenda ya kikao hiki" aliongea kwa unyenyekevu sana mheshimiwa waziri mkuu Laurent James ambaye mpaka wakati huo hakuwa akijua kiini cha kikao hiko
"kama nilivyowaambia mwanzo kwamba makamu wa raisi ameasi ni kweli makamu wa raisi na amekengeuka na kuisaliti serikali yake na kabla sijaendelea ndugu wajumbe labda nimuulize swali moja mheshimiwa raisi mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya chama kuwa wakati anamleta makamu wa raisi na kuni tambulisha kwangu na kunishauri niwanie nae kiti cha uraisi akiwa kama mgombea mwenza ulipitia sawa sawa taarifa za mtu huyo? aliuliza mheshimiwa raisi swali lililo mlenga mheshimiwa raisi mstaafu SAID BENDERA.
"Jamani mbona mwenyekiti anajitukana mwenyewe hapa, hajafika kwa waandishi wa habari anaanza kupaniki kiasi hiki, na mimi namueleza kinaga ubaga aliamua kuingia kwenye kamari ambayo alijua itampa faida na umaarufu kwa wananchi lakini nisikufiche binti hiyo uliyocheza ni KAMARI YA AIBU, ni kweli mimi ndiyo nilikuletea makamu wa raisi uweze kuwania naye nafasi katika uchaguzi wa uraisi, wabunge na madiwani ila jina lake lilipendekezwa na ofisi yenu wenyewe baada ya kuwa mmejiridhisha na taarifa zake zote sasa nina kushangaa unaposema nilikuwa najua taarifa zake labda ujitee tu kuwa bosi wako mstaafu alikuficha taarifa za mtu huyo lakini vile vile hukupaswa kuzijua kwa sababu ulikuwa ushasimama kazi hiyo kwa ajili ya nafasi ya kugombea tamaa ilioje." Aliendelea tena
"nilifanya kwa mapenzi ya chama ila najilaumu sana kukuachia kiti na nadhani unaona tamaa yako ilipokufikisha wajumbe karibu robo tatu wana mashaka na hoja zako na kibaya zaidi baada ya kuchanga karata zako umeanza kuwatisha watu umesahau tunaweza kukuvua uanachama na unatambua kabisa bila chama uraisi utaenda kuufanya na ukoo wako." alipigilia msumali raisi mstaafu SAID BENDERA huku akionesha hasira za wazi wazi.
"ni kweli kabisa mzee wangu wakati wa mchakato uliletewa jina na taarifa za makamu kutoka ofisi ya idara ya ujasusi ambayo nilikuwa nafanyia kazi lakini umesahau uchunguzi huweza kuchukua muda mrefu sana mpaka kufikia ukweli wa jambo.....ndugu wajumbe sijaitisha kikao ili tujue nani ana taarifa kuliko mwenzake bali nimewaita ili tujadiliane kuhusu kujazwa kwa nafasi iliyo wazi ya makamu wa raisi na hii ni kutokana na kile nilichomuagiza spika wa bunge kukifanya hiyo kesho" aliongea mheshimiwa raisi kwa utulivu bila kuonesha tashtwitwi yoyote
"binti unatambua unachokifanya siyo sahih......" alikatishwa mzee yule na sauti iliyoja mamlaka na hasira ya mheshimiwa raisi
"ni sahihi kwa nafasi ya makamu wa raisi kuwa wazi, ni sahihi kabisa bunge kumuondoa kwa sababu makamu wa raisi hakuwa mtanzania kama katiba inavyohitaji, makamu wa raisi hakuwavraia wa nchi hii ila alijipenyeza huku akipewa sapoti na washirika wenzake lakini vile vile niliuliza taarifa sahihi za huyu mtu kwa maana imebainikiwa hakuwa raia wa kigeni peke yake bali pia alikuwa jasusi mbobevu kabisa kutoka idara ya huduma za kiusalama za nchi ya congo." ikaibuka minong'onoya wajumbe huku wengi wao wakibaki midomo wazi.
"hapana na haiwezekani msitufanye watoto wadog......"
"uwe unaelewa au huelewi hayo ni yako mzee wangu kaa utulie kama ulijua nimechanga karata mbovu basi makamu wa raisi na washirika wenzie nadhani ndiyo muda wa kuona kauli yako kama ndiyo jibu pekee itakayozunguka vichwani mwao kuwa walicheza 'KAMARI YA AIBU' kabla sijahamia ajenda ya pili nipende kusisitiza kwa upendo kabisa kwamba yeyote aliyehusika katika matukio yaliyotokea na yanayoendelea kutokea kwamba kabla hajajisalimisha basi nimuone akiwaomba watanzania msamaha hadharani kabisa huenda ikasaidia kupungua kwa adhabu yake japo sina hakika na hilo kuliko kufikiwa na watu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama" aliwatazama wajumbe wale kuona wame lipokeaje jambo lile huku wachache wakiwa kama wamechanganyikiwa akapiga fundo la maji kisha akaendelea.
"ndugu zangu wajumbe hoja nyingine iliyotuleta hapa mkutanoni ni hili la kumhus...." alikatishwa baada ya mpambe kumnong'oneza mheshimiwa raisi kuwa chifu alikuwa na jambo la muhimu sana na huenda ikiwa ni ushindi mwingine dhidi ya hujuma za watu wachache huku wengine wakiwa ukumbini.
"mwambie aingie ndani, ijapokuwa anavunja utaratibu ila jambo alilonalo ni la muhimu sana kwa maslahi ya taifa" alisema mheshimiwa raisi huku akijikita kwenye tafakari juu ya haya yanayoendelea huku muda aliopewa na mtu yule ukiwa ukingonina hauwa na jibu la msingi la kumpa alikuja kushtuliwa baada ya kuhisi uwepo wa mtu nyuma ya mabega yake hakuwa mwingine bali chifu wa idara ya ujasusi ya tanzania.
"mkuu panya wameanza kunasa kwenye mitego yetu pasipo kufatwa huko mashimoni" aliongea chifu
"ngoja nimalize hiki kikao utanipa ripoti, kingine spika wabunge asivuke geti la ikulu nadhani unaelewa tafsiri yake"
"naelewa....ila mbona kama utaanzisha taaruki kwa wanachama wa chama chako kwanini tusis....."
"fanya nilichokuagiza mengine niachie mimi" yalikuwa ni mazungumzo mafupi sana ya mheshimiwa raisi na chifu wa idara ya ujasusi, wajumbe wa kamati kuu hawakuambulia hata moja kwa kuwa watu waliokuwa wakizungumza ni watu hodari na makini katika kuficha taarifa ambazo ni muhimu sana. chifu aliondoka huku akiacha maswali mengi kwa wajumbe na raisivwala hakujali alihitimisha kikao kwa maazimio kwamba nafasi ya makamu wa raisi wameliachia bunge ila yeye atapendekeza jina la mtu ambaye anaona ni mzalendo na mwenye weledi katika kuwahudumia wananchi.
wakati wageni wale wakiondoka kwa usafiri waliokuja nao, hali ilikuwa tofauti kwa mheshimiwa spika kwani alikuta wanaume watatu wakiwa katika suti zao nyeusi.
"mbona mnakosa adabu vijana ni nani anawa ingiza kwenye ajira nyeti kama hizi alafu mnajisahau kama mko car wash......alafu walinzi wangu wako wapi hebu ngoja nije kwanza na mkuu wenu anatakiwa aone kazi mnayoifanya sehemu tukufu kama hii, vijana wa siku hizi bhana"aliongea spika huku akipiga hatua kurudi ndani akaonane na mkurugenzi wa ulinzi ikulu ili akampe malalamikoyake.
"sikiliza mzee haina haja ya kupaniki sijui uende kwa nani kuanzia leo sisi ndiyo tumepewa jukumu la kukulinda na wale walinzi wako wamerudishwa kozi hivyo kutokana na haya matishio yanayoilikumba taifa hatuhitaji mtu kama wewe upate madhara....hahaha alafu futa wazo la kurudi huko ndani ulipotoka huoni utajuzalisha, mambo mengine ambayo hayakuwa ya lazima, ingia kwenye gari tukupeleke hotelini" alisema hivo jamaa aliyekuwa na weupe wa kufifia na mwenye mwili mithili ya mcheza mieleka batista"the animal"
"unajua unaongea na mkuu wa mhimili katika taifa hili au unajisahaulisha makusudi kijana, nimeamua kuwasamehe maana ndivyo mlivyolelewa vibaya huko mlikota"
"hahahaha....kati yetu sisi na wewe nani kalelewa vibaya, kumbe we mzee hamnazo" aliongea jamaa mmoja kati ya wale watatu huyu alikuwa mweusi ti na mrefu kupanda hewani muda huo alikuwa anashuka kwenye gari huku kashika bastola nyeusi aina ya colt 45, kuona hivo spika wa bunge koo likamkauka kwa hofu.
"una machaguo mawili uongozane na sisi mpaka hoteli ulipofikia na kisha tukuache upumzike na tutakuwekea ulinzi katika kipindi chote au tuuache mzoga wa mke na watoto wako baharini ukawe chakula cha samaki na familia yako hutaionatena ndiyo inkuwa imeisha hivo chaguo ni lako tamka haraka hatuko hapa kupiga soga na wewe"
**************************
Je atachagua kusuka au kunyoa tuonane sehemu ya kumi na saba kwa majibu sahihi Tchao
 
KATIKA ULIMWENGU WA KIJASUSI HAKUNA ALIYE SALAMA KWA HIYO YAKUPASA KUJITAYARISHA KUKABILIANA NA ADUI ASIYEONEKANA HUKU UKITAFUTA UKWELI KATIKATI YA MAWIMBI YA UONGO…………UNGANA NAMI KATIKA KUTAFUTA UKWELI HUU.
“shida ni nini vijana.......kama mna shida na mimi husikeni na mimi, familia yangu msiiguse tafadhari vijana wangu ila ni nani amewatuma kufanya hivi?" Aliongea spika wa bunge kwa sauti inayo kwama kwama ana kigugumizi
"mbona mzee unakuwa muoga tena wewe si ulikuwa mkali kama pilipili haya iko wapi jeuri yako, kiufupi tusizunguke sana, wewe panda gari tuondoke, utaratibu hauruhusu magari binafsi kuendelea kukaa kwenye maegesho kama hivi" ni kama ubaridi ulipita kwenye moyo wake huku akirudia sentensi yamwisho"gari binafsi" ilibidi azunguke kuangalia namba za usajili wa gari ile akakutana na kibao cha njano alipigwa na butwaa na alikaa chini kwa kukosa nguvu kwani kila kitu kilikuwa kime badilika kumaanisha tayari ameshavuliwa cheo hicho na wenye nguvu"
festo mchukue huyo mzee muda ushatuacha" wakati wamemaliza kumuweka kwenye gari tayari kwa safari walipata ugeni wa chifu kwenye kioo cha dereva"
"huyo mzee yuko wapi" alisema chifu akichungulia ndani na hakuweza kumuona kirahisi kwasababu ya kioo kilicho watenganisha kati ya siti za nyuma na zile za mbele akampa ishara amfungulie mlango wa siti za katikati na punde mlango ulipofunguka walijikuta wame kutanisha macho huku mmoja akiwa kwenye tabasamu na mwingine aliyeonekana kupatwa na msongo wa mawazo
*****
MBEZI BEACH-DAR ES SALAAM
"mtu wetu tumepewa amri kwamba asafirishwe akakutane na tanuru la moto."
"kwahiyo hapo kinyonga unataka saa ngapi tukamkague kama kweli na yeye ana roho tisa kama paka" alisema kwa usongo kinyundo
"hatuna muda wa kupoteza inabidi tujisogeze mitaa ya posta akiikama barabara la nyumbani kwake tuta msindikiza hadi kwake na bahati iliyo nzuri tutamkuta ameshachaa kutoka kwavijana wake wanao mlinda kwani wakati mmoja nilipokuwa na mmega yule mchepuko wa JM aliwahi kunambia kwamba wakuu wetu wana watu zaidi ya mia moja katika idara zote kwenye serikali hii na akaniambia takribani asilimia kubwa ya walinzi wa huyu bwege tunaeenda kumnyamazisha ni watu wetuhivyo kazi itakuwa ni sawa na kumsukuma mlevi"mara hii aliongea kitemi kobelo huku akichomoa bastola yake aina ya bareta yenye rangi nyeusi na kuibusu.
"tuondokeni zetu kwa maana tuna siku ndefu mpigie na yule demu anayejifanya mlokole mwambie awaambie wenzie wawe active maana hii usiku wao ndio watakaoanza kumtembelea yule mgeni wetu kisha sisi tutakuja kumpatia tamasha la bure atakufa huku anafurahi" alisema kefa huku akinyanyuka kwenye moja ya sofa katika nyumba ile iliyokuwa karibu na ufukwe wa bahariya hindi katika eneo la mbezi beach jijini dar essalaam, walikuwa kikazi zaidi na mbali na yote walifanikiwa kupita na mzigo kwani walikwisha letewa vitambulisho feki vikiwaelezea wao kama walinzi wa siri wa mheshimiwa raisi, hivyo walifika jiji la raha na karaha bila kupata usumbufu mwingi barabarani.
****
KISANGURA SECONDARY SCHOOL-SERENGETI
Saa 8:50
"hivi mwalimu janet samahani, una taarifa zozote za kutokufika kwa mwalimu Musa kwa maana nimempigia simu ila sijampata hewani tangu asubuhi" aliuliza huku akilitupia jicho lake katika daftari la mahudhurio kwa mwalimu mkuu na hakuambulia jina lililokuwa linauliziwa, ikiwa ina maana hakufika kazini..
"mwalimu mkuu, nisiwe muongo kwa kweli sijui sababu za kutokufika kwakwe ila ntamuuliza mtu ambaye yuko karibu nae ili aweze kunijuza, kilijili nini kwa siku ya leo mpaka hakufika nafikiri kufikia kesho au hata leo leo nitakupa taarifa mkuu." Alisema mwalimu Janet
"nitashukuru sana, lakini pia pole kwa usumbufu najua siyo kaziyako kufatilia maisha ya mtu ila tafadhari ni kwasababu tumeishi nae vizuri tangu ameanza kufundisha"
"wala usijali mkuu nitalifatilia" alisema hivo huku akiondoka katika ofisi ile na kutazama saa yake na hapo aligutushwa nahamaniko usoni mwake, kwani alijua atawa wahi wanafunzi na kuweza kumuuliza maswali zakaria alikuja kustuka alipohisi kuna mtu nyuma yake naye hakuwa mwingine alikuwa ni mwalimu mkuu.
"Madam janet ni kipi kimekusibu maana umeganda kwa dakika kadhaa ukizama kwenye dimbi la mawazo eeeennnhee hebu niambie ni kitu gani kinasumbua kichwa chako" aliongea mwalimu mkuu kwa sauti ya udadisi.
"aaaaaahhh aaaaahh...hakuna kitu isipokuwa........"
"isipokuwa nini madam janet mbona umepoteza umakini ghafla kama sio yule tuliyeongea nae dakika kadhaa" aliuliza tena mwalimu mkuu kwa upole kabisa huku akihitaji kujua kilicho nyuma ya mabadiliko yale ya ghafla kuna nafsi ilimnong'oneza kwa madam janet kuna kitu anakificha hivyo akaongeza mkazo wa jambo hilo.
"nilifikiri nitawahi kabla ya wanafunzi hawajatawanyika kurejea nyumbani, nilihitaji nimuulize mwanafunzi wa kidato cha tatu Zakaria Magebo maana ndiyo alikuwa rafiki yake pete na kidole, sasa nilivyomkosa nilikuwa na waza na kuwazua wapi ntampata mwanafunzi yule ukizingatia sijawahi kupafahamu kwao mkuu" alitoa maelezo yaliyoanza kumuingia mkuu yule wa shule na hapo ni kama kumbukumbu ilipita na kumgutusha tena mkuu yule wa shule.
"aaaaaahh hata ungewahi usingeweza kumuona Zakaria Magebo kwani mama yake mzazi aliugua ghafla na kisha mjomba wake kuja kumchukua ili wasaidiane kumpeleka katika hospitali ya wilaya kwa matibabu zaidi, maadamu nina namba ya mjomba wake ntawasiliana nae ili atutatulie tatizo hili.......samahani kwa usumbufu madam Janet nkutakie siku njema na kwaheri." alisema mkuu huyo wa shule huku akielekea uelekeo wa nyumbani kwake, huku madam janet naye akishika uelekeo wakuingia senta ya kijiji mahali alipoweka makazi yake.
*****
IKULU- DAR ES SALAAM
Saa 10:40 jioni
"chifu habari ya muda huu, unaweza kuja ikulu hapa sasa hivi" alisema nheshimiwa raisi
"nipo ikulu mkuu, katika ofisi ya katibu mkuu nilikuwa naratibu upatikanaji wa vifaa muhimu kwa ajili ya kazi ya leo mheshimiwa raisi na ndani ya dakika tano nitakuwa ofisini kwako na ripoti Kamili"
"umefanya jambo la maana kwa kupiga hatua hiyo na ndiyo maana mpaka leo sijawahi kujutia kwanini ulikaa hapo kwasababu unafikiria sana nje ya box......lakini mbali na yote hayo umeweza kumshirikisha jenerali?,nasema hivo ili asije akaweka kinyongo na kuonekana unataka kumfelisha kwenye hili jambo"
"mkuu wala usiwaze kuhusu jenerali,huyu ni kijana wangu na pia mbinu za kimedani nimemfundisha mimi na nilipendekeza akasome kozi ya ukomando kipindi hicho angali kijana mdogo kabisa mwenye cheo cha kapteni hivyo hawezi kuweka kinyongo kwa mwalimu na mkufunzi wake katika sanaa ya mapambano ya ana kwa ana, sote tunalenga kuwafikisha wahalifu wote mbele ya sheria na hakuna anayetafuta cheo sote ni wakuu katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hivyo nkuondoe hofu hiyo mheshimiwa kwa mara nyingine tena kwamba tunafanya kwa ajili ya taifa kuwa Salama"
"nisiwe muongo maneno yako yameniondolea uchovu na yameniongeza nguvu......nakuhitaji ofisini kwangu sasa hivi" alisema raisi na kuikata simu huku akitabasamu
*****
Saa 11:00-IKULU DAR ES SALAAM
ofisi ya mheshimiwa raisi ilikuwa imetulia huku ikizungukwa na samani za bei ghali kabisa huku rangi nyeupe ikizungukwa na utepe wa rangi ya dhahabu uliinakisha ofisi hiyo na kuifanya ionekane kama peponi, harufu nzuri na hewa safi viliitawala huku picha ya muasisi wa taifa hili ikiwa imebadikwa kwenye moja ya kuta pamoja na ile ya raisi wa sasa ambayo kiukweli ilisadifu urembo aliojaliwa bi. Gloria steven raisi wa tanzania huku akiwa katika suti nadhifu ya rangi nyeusi,miwani ya macho na ukataji wa nywele zile kwa mtindo wa low cut ulipigilia msumari kuwa mbali na kuwa na vivutio mbalimbali vilivyoliingizia taifa fedha ndefu ila pia ilisadifu kuwa taifa hili lina wanawake wazuri ikiwemo raia namba moja ambaye ni raisi, mbali na hayo ofisi ilikuwa imetulia huku ikiwa na watu saba pekee huku wanne wakiwa ni vijana wa makamo watatu wa jinsia ya kiume na mmoja wa jinsia ya kike, huku watatu wakiwa ni mheshimiwa raisi, chifu na jenerali.
"mheshimiwa walioko mbele yako ndiyo wale vijana wanne ulionitumia ma file yao ili nimtumie jenerali kwa kazi yakusafisha na kuondoa uchafu katika taifa hili" alisema chifu na muda huo huo Jenerali akishtuka kwamba kumbe hata yale majina siyo kwamba chifu ndiyo aliyateua bali yalitoka moja kwa moja ikulu.
"kila kitu kuwahusu wao nadhani kipo kwenye detail zao ndani ya yale mafaili ili kuokoa muda mheshimiwa raisi naomba twende moja kwa moja kwenye mpango kazi" alimaliza chifu
"vijana wangu nimefurahi kuwaona mko vile vile kama nilivyowaacha chuo, naongea hapa nikiwa kama dada yenu ninahitaji msaada wenu nadhani mnaelewa kauli hii? Aliongea mheshimiwa raisi
"ndiyo madam president" walijibu kwa pamoja
"ina maana gani"
"tutamlinda dada yetu na vitu vinavyo mzunguka kwa maslahi ya wadogo zetu"
"vizuri...............ni hivi kuna watu wanaichezea amani tuliyo nayo na kutishia kuleta machafuko, kuna watu wamepotea na kontena la fedha wakati hayo yanaendelea kuna gaidi anatoroshwa mchana kweupe lakini pia kama haitoshi wakaondoka na silaha za kibaiolojia huku mafinga eneo ambalo hata huyu jenerali hajui kama kulikuwa na maabara ya hatari kuliko maelezo na mambo hayo yalifanyika kwa usiri mkubwa sana wakamaliza na hili la ubalozi ambapo kuna wadogo zenu zaidi ya kumi na saba wametangulia.........." aliweka nukta huku chumba kizima kikijipa dakika moja ya kuwakumbuka maofisa waliotangulia mbele za haki.
"Amen............nilihakikisha kila familia inalipwa stahiki zao haraka iwezekanavyo, na kama haitoshi niliweza kufanya kikao na wakuu wa vyombo vya usalama tukakubaliana na tukatengeneza timu kubwa sana ila ilifeli, nilikumbuka tulisahau karata moja yenye umuhimu sana wingi wa watu siyo kuishinda vita, tulisahau kuitumia karata ya maarifa kwani vita hupiganwa kwa maarifa, hawa wazee wamesha tafuna siku nne kati ya kumi na nne hivyo nafasi zao za kazi zipo mikononi mwenu, nataka niwaambie hivi karibuni alikamatwa binti ambaye ukimuona utajua ni mpole na hata mikono yake haijawahi kushika damu hata ile ya kuku" aliongea mheshimiwa raisi huku akiinuka kutoka kwenye kiti na kusimama
"tulipomuhoji vikali aliniambia mimi mwenyewe mambo mengi sana ambayo nataka yafanyiwe utekelezaji wa mara moja na hili litawahusu jenerali na chifu..........vile vile alichokwisha kunieleza ndicho nataka mfanye vijana wangu kwanza kabisa kila mmoja achukue kishkwambi tuzungumze ki vitendo" watu wale ofisini wote walichukua vishkwambi na kuviwasha.
"naombeni mfungue video za faili ya kwanza, kisha mniambie nani ana sura ya kumtilia mashaka miongoni mwa hao watu waliohudhuria mkutano katika hili jengo" kila mtu alikuwa makini katika kutazama video footage zilizopigwa na kamera za ulinzi hapo hapo ikulu na wote walisadiki kwamba hakuna sura ya mashaka, mheshimiwa raisi alitabasamu
"fungueni faili lenye video ya pili" walilikagua huku wengi wakiwa ni wale wale na wachache wakiwa ni sura ngeni napo pia wakaibuka na jibu la kutokuwa na mashaka na yoyote.
"fungueni hilo la mwisho huenda mkawa na jibu jipya" wakaangalia kwa kurudia rudia kwa zaidi ya dakika mbili lakini hakuna aliyepata kuona tofauti na mwisho wakatoa majibu kwamba hakuna wanaye mhisi ijapokuwa vile vile watu hubadilika ila ni ngumu kwa wafanyabiashara hao wakubwa kwani hujua hatma ya pale wanapokuwa matatani huharibu wasifu wa biashara zao na kufilisika vibaya.
"naombeni mfungue hilo faili limeandikwa kivuli cha mbingu" alisema mheshimiwa raisi na wakafungua na kukutana na picha tatu huku ya kwanza ikisadifu mazingira na watu waliokuwa katika video na faili la kwanza huku picha ya mtu aliyevaa kamba nyembamba na iliyo na msalaba kwa mbele, picha hiyo ikiwa imezungushiwa duara jekundu, huku sura yake ikionesha alikuwa akitazama sehemu,
"fungueni faili la pili" nalo pia lilikuwa na picha ya mtu yule yule akiwa amekaa siti za katikati katika mkutano huo, akiwa ndani ya suti nadhifu ila pia macho yake yalielekea kule kule kama picha ya kwanza sema ilihitaji utaalamu wa ziada kuweza kung'amua jambo hilo, nayo pia ilizungushiwa duara kwa rangi nyekundu.
"fungueni na hilo la tatu" walifanya hivo na hapo ndipo midomo iliwaacha vinywa wazi baada ya kuonekana mtu akiwa anasalimiana na katibu mkuu kiongozi balozi Ndumuri Chichi, katika picha hii akiwa na tabasamu pana, picha hiyo nayo ilikuwa imezungushiwa duara kwa rangi nyekundu kama zile za mwanzo.
"mnajua sababu za kuzungushiwa duara jekundu kwa huyo mtu, ni kutokana na taarifa fiche nilizopewa na yule binti na alinieleza uhusika wa huyu mtu kuwa yeye ndiyo msambazaji wa dawa za kulevya ukanda wa afrika mashariki, amejivika vazi la unabii ila gizani kuna mipango mibovu ya kuwahujumu vijana wa taifa hili, mtu huyu ana pesa ndani ya mifumo rasmi na halali lakini pia kuna zingine hizi za dili chafu hazionekani kokote, sasa basi nimewapa kazi hii nyie nendeni mkamchukue hata jioni ya leo sura yake nataka niitazame vizuri" aaliongea raisi huku akiwatazama watu wote mle ndani.
*********************************
Ni nani huyu anayetakiwa akachukuliwe na vijana hawa? Je watafanikiwa kama walivyoagizwa ungana nami katika sehemu ya KUMI NA SABA.Tchao
 
KIROBOTO ANAWEZA KUMSUMBUA SIMBA MARADUFU KULIKO AMBAVYO SIMBA ATAJIHANGAISHA KUMSUMBUA KIROBOTO……….WAHENGA WALISEMA NYANI WENGI HAWAWEZI KUNING’INIA KWENYE TAWI MOJA, TUONGOZANE SEHEMU YA KUMI NA SABA TUPATE KUJUA UNDANI WA MANENO HAYA.
SONGA NAYO……………………..
"mkuu kwanini usimuagize tu IGP akamleta kwani hawa vijana wana kazi ngumu ya kuwatafta magaidi" aliuliza jenerali huku akimtazama mheshimiwa raisi.
"ni swali zuri ila njia unayoitaka kuitumia ni mbovu, makamanda wote wa wilaya za kipolisi karibia zote wanakula pamoja na huyu mtu tena huyo IGP ndiyo usiongee kabisa, kwanini hukuniuliza nimewaita nyie wawili tu, kwanini hujiulizi taarifa za kujulikana kwangu kama nipo pale ofisi ya idara yaujasusi tena nkimuhoji yule binti ziliwafikia maadui hiyo ni picha tosha kwamba tuna wasaliti katika mifumo yetu.Chifu hebu nijuze mtu wetu umempata?"
"mheshimiwa sijampata huyo mtu ila maadamu tuna macho mengi huenda tukapata kitu" chifu akawasha televisheni kubwa na pana iliyokuwa ukutani na kuunganisha na diski mweko iliyokuwa na faili moja kisha akabonyeza na kulifungua kulikuwa na 'video footage' ambayo hakusita kuicheza huku akiiweka katika mtindo wa 'slow motion' na hapo macho yote yalikuwa kwenye televisheni ile
"STOP" alisema luteni kanali Charz Busungu, huku akisimamana kuanza kujongea kwenye televisheni huku akichukua rimoti kutoka mikononi mwa chifu
"kamera zilichezewa........mnaona hapa huyu mlinzi kaangalia hii sehemu huku akichezesha vidole vyake, lakini tuangalie hapa ikiendelea kucheza utaona mlinzi huyu bado kaangalia kule kule huku vidole vikiwa havichezi na hata dakika ni vigumu kujua sekunde zake zilisogezwa mbele mara mbili tuendelee hapa.....unamuona huyu jamaa hapa amejishika kidude cha mawasiliano mboni za macho yake zinanaonesha kuwa bandia na hata yeye siyo mwenyeji wa kazi hizi, chifu utanisaidia huku wengine wanatafuta details zake kwa ufupi tu miminilicho king'amua raisi hayuko salama" kukatokea na ukimya mfupi sana
"hata mimi nimeliona hilo mheshimiwa, akachukua rimoti nakuipeleka hadi kipande cha raisi anataka kuondoka, huyu jamaa namfahamu vizuri tulikuwa wote mafunzoni huko canada na yeye alichukuliwa na warusi na sikuwahi kumuona tena nashangaa kumuona hapa, mimi ni mpenzi wa kuhudhuria kila ziara anayoifanya mheshimiwa raisi, nawatazamaga walinzi wote wa raisi lakini kiukweli sijawahi kuziona hizo sura huenda walivaa 'transmitor wire' hivyo mkuu wa ulinzi hapa ikulu atakuwa na majibu ya kutupatia kama atabanwa vizuri" alisema ASP Richard au kwa jina la uficho "Sorge"
"mimi nadhani aitwe hapa yule mwarabu koko atatusaidia sana kwenye kujua sura zao"
"unamzungumzia "Dolphin" yule demu kapanda bei vibaya sana ila sikatai kuhitajika hapa msaada wake ni muhimu sana ila sijajua kama mheshimiwa raisi atafikiana nae bei" alisisitiza Chiku huku akitoa wasifu wa bei anazotoza mtu yule kulingana na kazi.anayotaka mtu afanyiwe.
"nipe namba yake ya simu nitazungumza naye mimi mwenyewe" alisema kwa msisitizo mheshimiwa raisi na muda huo huo simu yake ilikuwa imewekwa sauti kubwa na chumba kizima kilipata kusikia muito wa namba ile ikiwa ina maanisha iko hewani na upande wa pili simu ilikuwa ikiita
"hallow nani wewe" ililalama sauti ya upande wa pili huku ikionesha mhusika alikuwa katika dimbwi zito la usingizi"
"unaongea na Bi Grolia Steven raisi wa Tanzania sijui naongea na Dolphin" iliongea sauti tulivu na yenye msisitizo
"lete deal haijalishi ni dolphin au la wewe nenda kwenye mpango nina usingizi wa masaa kama mawili kabla yakuendelea na majukumu yangu" raisi akashusha pumzi kwani mbali na kuheshimika na wananchi kwa asilimia kubwa ila alikiri kuwa kuna watu wana viburi vilivyopitiliza hivyo akataka kumuona mtu huyu anafananaje.
"ni hivi nina kazi ambayo inahitaji ujuzi wako na kikubwa zaidi ni kuhusu kamera za ulinzi kuchezewa hivyo nakuhitaji ikulu " alisema mheshimiwa raisi huku akipima utulivu wa upande wapili.
"dola elfu hamsini kwa kazi nzima......ila dola elfu ishirini natano kama kianzio alafu hiyo ishirini na tano nyingine mtaniingizia wakati nimemaliza kazi yenu, nadhani tumeelewana.
"sikiliza binti hiyo ni pesa ndogo kulinganisha na kazi unayoenda kufanya fika ikulu kwanza na pesa yako utaipata hata ukiwa huku"
"waga sifanyi kazi kwa kupewa maelekezo wakati mimi ni wa kwanza kuweka mapendekezo tekeleza kwanza nami nitafika hapo kufanya kazi yako kama una kigugumizi tafuteni mtu mwingine awafanyie kazi yenu........jioni njema mheshimiwa raisi titititi" hiyo ilimaanisha simu imekatwa na upande wa pili kitendo ambacho kilimkera mheshimiwa raisi na kuchukulia jambo hilo kama dharau.
"tusikilizane kama nilivyowaambia mtu wetu wa kwanza kumpata kwa usiku huu ni huyu baba Askofu wa hili kanisa la JEHOVAH AMESHINDA, kisha yeye atatufikisha mpaka kwawatu anaofanya nao kazi, nilikuwa sijawaambia kwanini tumuwinde huyu mtu, kutokana na kumhoji yule mpumbavu aliyetaka kuligeuza bunge kuwa kama sebure ya nyumbani kwake, tulimkamata na tume mbana vilivyo na ametupa ufunguo ambao utatufungulia makufuli mengine, lakina kuna intel pia ya kwamba huko pembezoni mwa Arusha ndipo alipokimbilia mtu hivyo chifu wakati kijana mmoja anafika huko huo mji uwe umepekuliwa vya kutosha, jenerali hakuna mtu kutoka Arusha na wanaoingia watazamwe kwa ukaribu sitaki makosa yatokanayo na uzembe"
"kuhusu ubalozini kuna harufu ya usaliti kila anayekwenda kutafta ukweli anakuta amengojewa vikali na wengi wameishia kurudi maiti, hivyo hii oparesheni sitaki ifeli, ikifeli ina maana kati yetu kuna msaliti na mimi nasemehe vyote ila siyo usaliti na bahati nzuri nyote mnatambua adhabu ya msaliti ni nini?, siwatishii ila niwahakikishie sinaga huruma na mtu aliyeamua kuasi katikati ya oparesheni nadhani tumeelewana, jenerali na chifu mnajua mtafanyaje ila kwa sasa vijana waingie kazini tuko nje ya mud........" ghrrrrr ghhrrrr simu ya mheshimiwa iliita na alipoitazama alikutana na ile ile namba iliyopiga mida ya mchana akapokea.
"nilijua huenda hutapokea simu hii.....hahah.." alikatishwa kicheko chake kwa sauti ya mamlaka.
"nenda kwenye lengo na sema shida yako" ilisikika sauti ikiongea kitemi
"nafikiri siko upande wa kusemea shida ila nadhani muda tuliokubaliana kutoa majibu ndiyo sasa unaweza kuchagua kusuka au kunyoa hahahaha"
"nani alikudanganya serikali yangu inaweza kufanya ujinga kwa kuingia makubaliano na magaidi kama wewe.......hahahaha nikuhakikishie tu hakuna utakachofanya na jiandae kuiona sura yangu hali mpaka kesho utakuwa umepata majibu kutoka kwa washirika wenzako na hata ukikimbilia mbinguni tutakufata huko huko na kukurudisha utumikie adhabu kama wahalifu wengine"
"kwahiyo unanitisha si ndiyo......sijawahi kuona raisi dhaifu na mpumbavu kama wewe unayeruhusu wananchi wako kufa kwa ujinga wake, kwa kuwa umetaka kushindana karibu kwenye'LIGI YA WAUNGWANA'
" nikuhakikishie tu ntaongoza hiyo ligi na ntakushusha daraja na rasmi utachagua kati ya majina mawili haya la kwanza ni Mfungwa na la pili ni marehemu chaguzi ni lako, nikutakie tafakari njema.......titititi"
"hey guys mnaruhusa ya kukamata na kama akileta ubishi usisite kumuondoa yeyote yule anayehusika na kila mmoja aliweke hili akiini kwamba hatakiwi kufa, maisha ya kila mmoja kwenu nihitaji muhimu kwa maslahi ya taifa......mnaweza kwenda na niwatakie utekelezaji mwema wa majukumu hayo" yaikuwa maneno mazito ila yenye kutia hamasa na hali ya kufanya kazikwa vijana wale nao wakatoka na jenerali aliwaambia waongozane nyumbani kwake
******
"jamani karibuni hapa ndiyo nyumbani" alisema jenerali kwa bashasha kubwa huku tabasamu lake ikiendelea kuchanua, nawote watano wakiongozwa na chifu walirudisha tabasamu kubwa huku wakishukuru kwa ukarimu ule wa mwenyeji wao
"jamani hatuna muda wa kupoteza, jenerali kutokana na hawa vijana nawafahamu japo walichaguliwa moja kwa moja kutoka kwa mheshimiwa raisi na kuttoka na na heshima uliyonipa napenda kugawa majukumu kama ifuatavyo."black cobra na angel of death mnatakiwa Arusha mara moja usafiri wa ndege utaondoka na nyinyi mara baada ya hapa kuna dondoo kwamba huenda mtandao wa ugaidi wa Mustapha upo huko ikiwezekana na mustapha mwenyewe maelekezo mengine mmeshapewa jinsi ya kufanya na mheshimiwa raisi"
"Breath of satan tiketi yako ya ndege kuingia bujumburaimeshakatwa na utaingia burundi ukitokea kenya kama mpiga gitaa wa bendi ya watusafi jazz, na taratibu zote zishakaa kwenye msitari na usiku huu huu unatakiwa uwe kenya ili kesho uanze kulipekua jiji la bujumbura na kuwasafisha wahusika kimya kimya akiwemo mke wa makamu wa raisi"
Richard 'Sorge' wewe una kazi moja laini ila ngumu ya kumleta kwetu huyu baba Askofu Theobald kitumbuyo wa hili kanisa la JEHOVAH AMESHINDA, sijaona taarifa zako ila najua nyie wote hapa mnafanana uwezo ijapokuwa chifu amenidokeza kwamba kozi yako ya mwisho ulifanya japan nina uhakika wewe ni mashine ya kazi usiniangushe" alisema chifu huku akimtazama ASP Richard , na kisha akamgeukia the chameleone ambaye mara tu alipofikishwa ikulu akakuta ndiyo muda wale watu wanatoka hivyo aliunganisha mpaka nyumbani kwa jenerali.
"kuna video nimekutumia kwenye email nahitaji unitaftie hao watu nione sura zao na kisha ntakwambia kitu gani cha kufanya sawa binti tangu" aliongea chifu kwa sauti ya chini huku akiwapa ishara kwamba wanaweza kwenda na usafiri wa kila mmoja ushaandaliwa, mipango iliyopangwa wote walihusudu uandaaji huo wa vitendea kazi kwa wakati huku kwa pamoja wakiapa kuto kuiangusha serikali
************************************
PAKA MWENYE NDOTO ZA KUWA SIMBA NI LAZIMA ATAPOTEZA HAMU YA KULA PANYA TUKUTANE SEHEMU YA KUMI NA NANE
 
CLUB 662-DAR ES SALAAM
Saa 03:00 usiku
ndani ya ukumbi wa VIP muda huu sauti tamu ya mziki wa taratibu ulikuwa ukisikika huku kibao kilichokuwa kuwakita kwenye spika kilisindikizwa na maneno matamu
"Commit a crime and I'll be your defender,
Overpower me so that I surrender Hmm,
I wish I could be your saliva,
So that I could taste your lips whenever,
I envy your hipster,
Vile inakushika kwa mapaa,
Kwa kweli manzi umebarikiwa,
Ndio maana tunaimba halleluyah,
I wish I could be your shoe,
I would have such a beautiful view,
And if I was the slit on your dress,
My goal in life would be to aim for the highest,
If only I could be your body lotion,
I would walk with undivided devotion,
Kila siku nakufikiria Ndio maana nasinzia,
Nasinzia nikikuwaza (oh oh)
Nasinzia nikikuwaza (oh oh)
Miaka rudi, miaka nenda (oh oh)
Nasinzia nikikuwaza (oh oh)
Nasinzia nikikuwaza (oh oh)" kibao safi toka kwa msanii kutokanchi jirani kilikonga nyoyo za watu waliokuwa mle ndani huku wakionekana kuwa ni watu wazito sana kiukwasi na vile vile kimamlaka huku wakizungukwa na vijana wenye miilii nayozingatia sawa sawa ratiba ya mazoezi lakini sio hivyo tu katika meza hiyo hiyo kulikuwa na warembo wapatao wanne ambao sura na maumbo yao yalisadifu urembo waliobarikiwa.
"jamani hali ni mbaya tukilegea yatazidi mambo kuwa mabaya zaidi" alisema mzungumzaji huyo aliyeonekana kuwa na hofu na wasiwasi,
"siku zote nakushangaa sana kobe kwanini unakuwa muoga kiasi hiko hujaona hizi sura za kazi au unahisi uwezo wao ni wa mashaka mashaka wewe hujiulizi kwanini Club imechangamka kiasi hiki ni kwa sababu hao wanaume ndiyo wamekuja na mzigo, shusha presha na hakuna hata kijidudu kitakachopitisha kiguu chake kutugusa tena sharubu"aliongea konokono kwamajigambo.
"kwanini mnalumbana kama watoto wadogo tusikilizane..........ule muda wa vitendo dhidi ya maneno ndiyo huu, ni muda wa kupeleka vilio ni muda wa kumuonesha yule mama kwamba hatutanii nimeongea na Mustapha amenambia vijana wameshajisogeza kwenye point tayari kwa kuseti mambo na kesho akiwa ofisini kwake hataamini.......najua wamejiona wajanja sana kumshikilia kiroboto kabla kesho hajaanza kunywa chai nahitaji aanze kupata maiti za watu wake nimetumiwa picha moja ikionesha raisi kuongozana na watu wanne wapya katika msafara wake kuelekea ofisini huku mmoja ni yule niliyewaambia asilione jua la kesho, kuambatana huko kunanipa picha kwamba huo ni mwiba unaotaka kutuchoma hivyo narudia tena ukatwe usiku huu kabla haujaleta madhara"
"diana kazi yako ni kunitaftia taarifa za huyu malaya mweusi, ukishazipata niletee ili nimuandalie mazingira mazuri yakuufaidi mwili wake kabla sijampiga risasi ya upendo afe akinikumbuka na wewe kefa na wenzako hakikisheni mnaniletea kichwa cha huyo mbwa mweusi kabla sijalala mnaweza kwenda" lilikoroma jitu lile lenye miraba minne jeusi na lililopanda hewa huku likijazia kwa misuli mingi naam hakuwa mwingine bali ni jenerali mstaafu wa jeshi Mzee Chukurubu, muda huo alibaki peke yake kwenye kiti upande wa VIP kwenye club ile huku akigida mafunda ya kinywaji kikali kilichokuwa kwenye bilauli ndogo ya chupa brandi ya Glenfiddich's na siku hiyo haikuruhusiwa watu kuonekana eneo hilo la VIP kwani lilikuwa na kikao nyeti sana na hata uondokaji wao haukutia shaka kwani muda wanaondoka kuna wengine walikuwa katika uhusika wa uhudumu na wengine ufanyaji usafi na wachache kama mabaunsa na hakuna aliyeshtukia kwani hata watu waliokuwa upande wa pili nao walikuwa bize na vinywaji vyao.
*******
"NDUGU WATANZANIA WENZANGU, NIMEKAA NA KUTAFAKARI, NIMEPIGA MAGOTI NA KUSALI MBELE ZA MUNGU HUKU NIKIMSHTAKIA KWA KILE ALICHOFANYIWA BINTI YETU, WENGI TUNAMFAHAMU, LAKINI HATUWEZI KULIACHA LIKAPITA HIVI HATA BIBLIA IMESEMA WAZI KWAMBA MUNGU HUWASAIDIA WALE WANAOONESHA JUHUDI, KUKAA KANISANI PEKE YAKE HAITOSHI HIVYO KONDOO WA BWANA NINAOWAONGOZA MIMI PAMOJA NA WATANZANIA TUUNGANE HAPO KESHO SAA 4 ASUBUHI, KWA WINGI WETU TUINGIE BARABARANI TUKIITAFTA AMANI NA UTAWALA ULIO BORA TUANDAMANE MPAKA IKULU TUMSHINIKIZE MHESHIMIWA RAISI AMUACHILIE BINTI YETU MARA MOJA ILI AKAENDELEE KUMSIFU MUNGU...............BWANA YESU APEWE SIFA NA JEHOVAH AMESHINDA HATA KWENYE HILI#FREEVANESSANDELWA." ni moja kati ya post zilizomfikia mheshimiwa raisi kutoka kwa chifu ambaye aliipata dakika moja iliyopita kutoka katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa XY
"huyu njinga nahitaji usiku huu awe na wenzake hapo ofisini kwako na kesho nitakuja kumuona hivyo mwambie jenerali vijana wake wasimpoteze huyo mtu kwani sentensi kutoka kwenye kinywa chake ni za muhimu sana."
"sawa mheshimiwa....nikutakie wakati mwema acha tuingie kazini kidogo"
"akishatiwa mkononi nipigie simu muda wowote kwani ntakuwa nikiisubiri simu hiyo ndiyo nijiegeshe kitandani"
******
ghrrrrr ghrrrr......simu iliita kwa fujo na alipotoa alikutana na jina limeandikwa Chatu hakufanya jambo lingine zaidi ya kuipokea na kuiweka sikioni.
"kwanini umemruhusu Casanova kuanza kufanya vitu vilivyo nje ya mpango wetu, hivi anajua athari baada ya chapisho lake kuzua sintofahamu nina uhakika usiku wa leo serikali itamnyakua kama ilivyofanya kwa kiroboto, ambaye hatujui kama akibanwa korodani ataacha kufunguka mambo yetu"
"mimi nadhani hajakosea lengo ni kuzua taharuki na ndiyo muda wa kubonyeza batani niuzike mji wa Arusha hahahaha"
"una uhakika na hilo unalolisema?"
"iko hivi akimnyakua na kesho ametangaza maandamano atasababisha watu kuona kwamba ni kweli serikali inacheza michezo michafu na sisi ndiyo muda tunawawasha kule arusha na kusababisha hasira kuwaka kwa wapiga kura(wananchi). na hapo tutakuja na ule mpango wa mapinduzi" aliongea kwa majigambo mtu yule alietopea kwenye kile kilevi ila makini kwakila neno alilokuwa anatamka
"yuko wapi kunguni na chawa mpaka sasa sijapata habari zao na kwanini wamesababisha mpaka watu wamestuka na kesho wanapeleka hoja ya dharula ya kumtoa na kumsimika makamu wa raisi mpya, tusipokuwa makini kete zetu muhimuzitaendelea kuliwa na huyo mjinga ana akili na IQ kubwa sana usijisahaulishe kwenye Hilo" aliongea mtu yule mwenye jina la uficho linalofahamika kama Chatu.
"wala usijali nilishamtuma kobelo na kinyundo wakamlinde Casanova, huku kefa na meja tumbaku nimewapa jukumu la kumfuta yule mjinga anayejiita kobra usikuhuu,nadhani niachilie hili suala nitalishughulikia na wewe utakubali" aliongea tena kwa majigambo na mtu yule alipiga tena funda la kinywaji kile.
"hiyo ni hatua nzuri ila umakini uongezeke tafadhari......nkutakie usiku mwema tititititi" aliongea chatu na kukata simu.
*************
SHEIKH AMRI ABEID KARUME STADIUM-ARUSHA
saa 5:15 usiku
usiku huu kulikuwa na maandalizi ya tamasha la Mbuni Fiesta litakalofanyika kesho yake ambalo lilitarajia kuhusisha wasanii kutoka ndani na nje ya nchi na kikubwa zaidi msanii wamidondoko ya Hip Hop Nas Escobar alitarajiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wake, usiku huu vyombo vya usalama navyo vilikuwa macho na sasa doria ilikuwa uwanjani hapo kuhakikisha kila kitu kiko sawa.
"Aroooo wewe ni nani? na unaenda wapi usiku huu kwani hujui kwamba hiri eneo hatakiwi kuonekana mtu? toa hiro rikofiakenge maji wewe naongea na wewe unafunika kichwa, arafukwenye begi umebeba nini? hebu chuchumaa tukukagaue vizuri ukute umebeba mirungi au bangi." iliongea rafudhi ya kikurya kutoka kwa afande yule mwenye cheo cha sajenti aliyekuwa amesimama nyuma ya geti la kuingilia uwanjani
"hapana afande mimi ni moja ya wafanyakazi tuliokuwa tunaliandaa jukwaa sasa nilisahau simu yangu bahati mbaya katika moja ya choo nilipokuwa nabadilisha nguo afande nakitambulisho changu ni hiki"
"tulia wewe unanifundisha mimi kazi, afande choto hebu likaguehilo begi" kufikia hapo mtu yule alipatwa na wasiwasi na kuzipiga hesabu za kuwatoka maafisa wale, kitendo cha afande choto kumsogelea kwa nia ya kumpekua alikutana na teke lililolenga usawa wa tumbo na kwa vile kilikuwa ni kitendo cha ghafla hakuwa amejipanga nacho na lilimpata sawia tumboni ambapo alihisi maumivu na kichefu chefu kwa wakati mmoja, mtu yule kwa spidi kama mkimbiaji raia wa jamaica usain bolt alizihesabu hatua zake ila alipofika kwenye kona alijikuta akipaa hewani kimo cha mbuzi na alipofika chini alijikuta anatoa tusi la nguoni kwani aliufikia mgongo na kupata maumivu makali sana, ulikuwa ni mtama uliopigwa kiustaadi sana na kabla hata hajameza mate akakutana na chuma cha baridi kwenye uso wake na sura ya mwanamke mrembo ikiwa inamtazama katika hali ya kushangaza alijikuta mikono yake imezungusha na mikono migumu na kufungwa pingu kwa nyuma
"nyanyuka turudi huko unakotoka" aliongea kitemi mwanamke yule na mtu yule hakuwa na ujanja zaidi ya kutekeleza walipofika usawa wa geti walikutana na maafande wale wanne waliokuwa doria wakimpa mwenzao huduma, sajenti Marwa alipatwa na mshangao kwani mtu aliyewatoroka muda siyo mrefu sasa alikuwa amerudi akiwa amenyong'onyea kwa maumivu makali yanayosambaa mwilini mwake.
"aroo rire rimtu riromuumiza afande choto si ndiro hiri afande Deusi, reo ritajuta kucheza na serikali, kijana reo utatutajia aliyegundua kombinesheni ya wari na maharage"
"jamani habari za saa hizi, nilitaka kujua kwani ilikuwaje maana nilikuwa upande ule wa pili nkaona kuna mpambano hapa mara nkaona huyu dogo anachomoka kwa kasi nami nilitaka kujua kwanini alikimbia ndipo nilipomdhibiti na nipo nae hapa........naitwa inspekta Saida kutoka makao makuu" aliwapa kitambulisho chake na muda huo wote walikakamaa huku wakipiga saluti na punde tu baada ya hapo walimwelezea mkasahuo.
"tulikague begi tujue lina mini"
itaendelea**
KUCHANIKA KWA JAMVI SIYO MWISHO WA MAZUNGUMZO TUKUTANR SEHEMU INAYOFATA
 
MAISHA YANATUFUNDISHA YA KWAMBA RAFIKI WA TAJIRI SIO TAJIRI ILA RAFIKI WA MWIZI NI MWIZI……….DUNIA SIYO MBAYA ILA WALIMWENGU NDIO WABAYA TUSOMANE TENA KWENYE KIPANDE HIKI.
Tuendelee…………..
wakati analivua begi lile kutoka kwa kijana yule walistaajabu akitokwa na jasho jingi walifungua begi lile lahaula!!! kulikuwa na bomu la kutengeneza lililokuwa litegwe uwanjani hapo, na hapo akatoa simu yake na kulipiga picha huku akiwasiliana na upande wa pili na kuomba wakutane kwenye nyumba waliyopewa kwa ajili ya kazi.
"huyu ninaondoka naye usiku huu atahitajika atufungulie milango kwani kuna mabomu zaidi ya matatu yanatakiwa.kupatikana usiku huu huu kwani kuna tukio nbaya lilipangwa kutokea kesho na niwaombe mfunge vinywa vyenu kwani hatujui hata kwenye jeshi letu nani ni mwema na nani siyo mwema.......nadhani tumeelewana endeleeni kuwa makini mtu mnayemtilia mashaka msimpe nafasi si mmeona alichokifanya huyu" wakaitikia kwa kichwa huku wakiwa katika hali yakuchangamka iliyo changanyikana na hofu
******
USA RIVER-ARUSHA
Saa 5;30 usiku
"mpo wangapi nyie mnao husika na utegaji? aliulizwa kijana yule huku akiwa amechakaa kwa kipigo kikali kilichodumu kwa dakika kumi na tano.
"tupo saba, sisi wategaji tuko wanne na walitugawa katika maeneo ya kimkakati kama mimi nilikuwa nimepewa uwanja wa mpira, mwenzangu mmoja alipewa kazi ya kuidondosha jengo la samsung ila sijajua kama amekwishafika......naumia nipeni dawa basi" aliongea kwa maumivu kijana yule
"MUSTAPHA ABD NUR AHMED yuko wapi ndani ya Arusha hii?"iliuliza kitemi sauti ya luteni kanali Charz
"kuhusu huyo mtu kusema kweli sisi hatujui ila kuna jamaa anaitwa ‘Mohamed mahboob’ ndiye anayetambua ni wapi alipo kwani hata sisi hatujawahi kumuona huyo mtu zaidi ya kumsikia tu kutoka kwa wakuu wetu.........nisaidieni tafadhari misuli inauma." aliendelea kufunguka kijana yule
"mpigie mwenzio simu mwambie kwamba wewe umemaliza ulichoagizwa, umuulize na mahali alipo"ilikoroma tena sauti ile
"hahahaha siwezi kumuuza mdogo wangu nyie kama mnaniua niueni tu ila nilichowaambia kinatosha na hayo mengine hamuwezi kuyapata hahahaha" aliongea kwa jeuri iliyochanganyikana na maumivu anayopitia mwisho alikilaza kichwa chake chini huku akitokwa na mapovu mengi mdomoni yaliyochanganyikana na damu huku ikionesha amejing'ata ulimi
"mmmmmhh hawa watu wana roho mbaya sana ni kwa vile muda ule sikumpa nafasi ila alipopata naona kaamua kuitumia sasa nina ona cha kufanya ni kumtumia hii namba chameleone atujuze yuko wapi? na tupate pia taarifa za huyu mohamed mahboob." aliongea luteni kanali Charz Busungu
"siyo mbaya wacha nimtaarifu na chifu pia kwa tulipofikia" alisema Chiku huku akiiweka simu yake sikioni hazikupita sekunde simu ikapokelewa.
"nambie binti yangu hao ndege mmefanikiwa kuwakusanya na mayai Yao?"
"mwanga upo na ndani ya muda mchache tangu tufike huku kiotani tulifanikiwa kumpata ndege mmoja na yai lake na aliweza kutuambia ni wapi yai la pili linaenda kutagiwa ila alituambia ili kumpata ndege dume anayewafanya watage mayai hayo usiku huu kuna jamaa anaitwa mohamed mahboob ndiye anajua hilo ndege dume lilipo hivyo kwa sasa nataka chameleone anitaftie namba ninayokutumia ili tuweze kumpata ndege wa pili na yai lake" aliongea chiku huku akitumia lugha ya mafumbo ambayo chifu aliielewa vizuri.
"sasa huyo ndege mliye nae mna lolote la kusema naye au mnamsafirisha?"
"kashajisafirisha na kwa hakika hawa jamaa ni makatili sana hakuwa na chochote zaidi ya simu wanayotumia kuwasiliana na anasema wako saba pamoja na huyo mohamed mahboob, kuondika kwake ina maana wamebaki watatu wenye mabomu hivyo chifu mwambie binti mikono ichangamke mpaka asubuhi nahitaji tuwe na mayai yote ili kazi ya kumdaka Mustapha iwe nyepesi" aliongea Chiku akiwa na morali ya hali ya juu
"safi sana......nitahakikisha nalisimamia hili mpaka mwisho baada ya hapa nitawasiliana na jenerali, nkutakie majukumu mema" aliongea chifu na kukata simu na muda huo ukaingia ujumbe wenye namba ya simu na jina ambalo linatakiwa lifanyiwe kazi.
******
"BRO MANSOOR KAMA UMEMALIZA UTANIKUTA MASAI POINT CLUB TWENDE KIA, FANYA HARAKA SANA UTANIKUTA NA HUSSEIN YEYE KASHAMALIZA KWENYE PART GALLERY KULE MAJENGO" ulikuwa ni ujumbe uliosomeka kwenye simu ya mtu aliyetambuika kama Mansoor na bila kupoteza Chiku akawasha gari aina ya BMW X6 na kuitoa nje na bila kuchelewa akatoka luteni Charz Busungu huku akiwa na bunduki mbii moja ikiwa BUL M-5 naCOLT M1911 alizozifunga viwambo vya kuzuia sauti tayari kwa heka heka za usiku huo dakika kumi baadae walikuwa wanaiacha kona ya kuingiia stendi na sasa walikuwa wanaitafuta Masai point club.
MASAI POINT CLUB-ARUSHA
Saa 5;55 usiku
"NIMESHAFIKA SOGEENI HAPA KARIBU NA HEAVY EWEIGHT BAA TUONDOKE"
"TUNATOKA ILA WEWE MJINGA UMETUCHELEWESHA SANA KIASI CHA KUTAKA KUKUFATA FANYA KUSOGEA PARKING" baada ujumbe huo kusomeka chiku na charz walipeana ishara na kisha na kuwasubiri watu wao namuda huo luteni kanali Charz alikuwa amelivaa begi lile na kugeukia upande wa pili huku akiupa mlango wa kutokea mgongo huku akipewa maelekezo na Chiku aliyekuwa makini kuwatazama watu wao.
"wanakuja kaa tayari wakifika tu tunawatia mkononi"
"copy that"
"wewe mjinga umetuweka kinoma noma mpaka bosi mudi alikuwa ashaanza kuwa na wasiwasi na wewe, mdogo wako kanambia tumkute Samsung ili tukamalizie kazi ya KIA alaf mbona ka......." alijikuta ametumbua macho baada ya mtu yule kugeuka na wote wawili walikutana na bastola aina ya BUL-M5 iliyotengenezwa na kampuni ya Bul transmark ya Israel ikiwa imefungwa kiwambo ikiwa inawaangalia na ndiyo muda doria ya jeshi ilikuwa ikipita maeneo yale walijisogeza eneo hilo na muda huo huo alijitokeza Chiku akiwa na bastola yake aina yaCOLT M1911 bila kutegemea vijana wale walijikuta wakipiga magoti mara baada ya kushambuliwa kwa mateke mazito ya mwanamke yule.
"wanafanya nini wale na mbona wana silaha isije ikawa ni moja ya watu tunao watafuta mkuu"
"hebu nendeni mkaniletee wale wote niwahoji mimi mwenyewe" iliongea sauti kavu ya jitu jeusi lilikuwa kwenye gari hilo huku likiwa na cheo cha luteni na vijana wale walikuwa na vyeo vya koplo huku wakiwa na vitambaa vilivyoandika MP, hatua kama kumi na tano kutoka pale waliposimama walisita baada ya kuona vijana wale wamefungwa pingu na wanapekuliwa.
"nyie ni akina nani mnaotoa silaha hadharani tena kwenye maeneo ya maegesho ya club tena bila kificho wala uoga"
"ndivyo mlivyofunzwa huko kwamba watu wakiwa wanafanyakazi zao mnawaingilia si ndiyo"
"mkuu anawahitaji nyinyi wote bila kujali nyinyi ni akina nani kiustaarabu tu tuongozane mpaka kwenye gari" Chiku na Luteni kanali Busungu waliangaliana na kisha Chiku akamjibu.
"rudini mwambieni hivi hatuna muda wa kupoteza akita kakuzungumza na sisi atatukuta ofisini kwa jenerali, Charz tuondoke tumuwahi huyo mwingine"
"usitujibu kijinga hivo wewe malaya mimi sijali wewe ni nani au vipi ila kwa mkuu utafika ana mahojiano na wewe ya muhimu na huyo jamaa hapo........oya malimi fanyeni mambo chaap" kilifutia kitendo cha ghafla cha ngumi kupasua upepo ikiwa ina maana ilimkosa mlengwaji likarushwa buti lilijaa uzitowake na kumkosa chiku na hapo ndipo likafatia tukio la kustaajabisha pyuuu ni mlio wa risasi uliotoka kwenye bastola ya luteni kanali Charz iliyo utoboa mguu wa mmoja ya wale vijana mwenye begi iliyekuwa anatoroka.
"nyie mna vichaa eeennnhh mnakuja kufanya mambo ya ajabu na niwaambie tu angetoroka gaidi hata mmoja mngewaleta nyie hamjui ni jinsi gani jiji hili liko kwenye shida nenda kamwambie mkuu wako akihitaji kuongea na mimi apande vyeo viwili kutoka alipo ndipo aje kuongea na mimi, nyie wajinga amkeni mkatuoneshe mwenzenu" alikoroma luteni kanali Charz huku askari wale wakiganda kumtazama aligeuka na kuwaambia.
"akiwauliza mwambie luteni kanali Charz Busungu ametupa amri ya kuendelea na doria" akaingia kwenye gari huku akikaasiti ya katikati na wale vijana wawili.
"mbona hamjawaleta na mnaona wanaondoka? mmeanza kudharau amri za wakuu wenu si ndiyo" alifoka mzee yule mwenye cheo cha luteni
"mkuu yale ni maji marefu sijawahi kuona luteni kanali akifanyakazi za kukamata kutakuwa na kitu na yule demu ananukia harufu ya ikulu.......mmmhhh mkuu hao siyo watu wa kawaida hata upigaji wake wa risasi unaonesha huyu siyo mtu wa kawaida"aliongea mmoja ya wale wanajeshi
"unataka kusemaje sasa kwamba wale wamekuja kwa kazi maalumu"
"tena mwanzo walisema kwamba kama unataka kuongea nao uende ofisini kwa jenerali" aliongea mtu yule mtu kikakamavu huku akimtazama luteni.
"niende kwa jenerali? wana kichaa nini hebu ingieni tuendelee na Doria" wakaingia kwenye gari baada ya kupiga saluti na kisha kuendelea na doria mitaani.
*******
"mpigie simu mwenzenu kwamba asogee barabarani" aliongea kwa sauti kavu isiyo na masikhara luteni kanali charz
"sawa braza" aliongea kwa maumivu yule kijana aliyetobolewana risasi na walipofika karibu na jengo la Samsung akamfungulia pingu mkono uliokuwa umefungwa na badala yake ikavishwa kwenye mkono wa kuume wa yule mwingine uliokuwa huru na sasa yote ikawa imefungwa, akampa maelekezo kuwa anatakiwa asimame akiwa ameegemea gari na asioneshe taswira yoyote ya kuwa matatizoni.
"salaam alleykum"
"walaikum assalam wa rahmatullahi wabarakatuh"
"hussein na mansoor wapo wapi? ustaadh Othman amenipigia simu na amesema mzigo uliotakiwa uwekwe Jengo la Samsung sasa uwekwe KIA njia kasha kwisha kuisafisha vipi wewe la kwako tayari ushaliweka kul..........." hakumaliza sentensi yake kwani aliguswa na chuma cha baridi akajikuta amevishwa kitu kama bangili nzito huku akiunganishwa na mwenzie.
"Ashraf sijaamini kama ungeniuza namna hii.......hata ustaadh akisikia hato kusamehe nakwambi......" alipigwa na kitu kizito eneo la kichwani kisha mwenzake akapewa jukumu la kumkokota ambapo naye alikuta mwenzake amekwisha sinzia na yeye kabla hajajiuliza alisikia kitu cha baridi kinapita na kisha muda ule ule akausikia usingizi mzito"
"hawa tushuke nao chimbo bado tuna kazi nao ya kutuletea wale wawili nahisi mpka asubuhi yule demu atakuwa ametupa detail za mohamed mahboob si ulimtumia namba na jina la huyo mtu"
itaendelea**
MCHAKA MCHAKA UNAENDELEA, Je unalijua Chimbo? Je watatapika taarifa walizonqzo? Na ustaadh Omary ni nani? Usipate taabu tuungane toleo lijalo usikubali kupitwa na kipande kijacho Tchao
 
“SHERIA NI KAMA NGUZO YA JAMII. INATUUNGANISHA NA KUTUFANYA TUISHI KWA AMANI, KILA KOSA LA KISHERIA LINA GHARAMA YAKE NA MATOKEO YAKE YANAWEZA KUDUMU MAISHA YAKO YOTE”……….UNATAKA KUJUA UNDANI WA NUKUU HII FUATANA NAMI KATIKA TOLEO HILI
SONGA NAYO……..
"ni kweli Charz wacha tufike ila kabla hatujapumzika itabidi watueleze hayo mabomu yalikuwa manne tu au kuna mengine yapo sehemu" alisema hivo Chiku huku akizidi kukanyaga mafuta na hasa ukizingatia ni usiku na barabara ni nyeupe, gari ilizidi kuchanja mbuga kuitafuta USA river na ndani ya dakika ishirini walijikuta wakiwa kwenye uzio wa nyumba waliyopewa kwa ajili ya kazi hizo maalumu.
OYSTER BAY-DAR ES SALAAM
MASAA MAWILI YALIYOPITA.
Majira ya saa tatu na dakika zake, nyumbani kwa Askofu wa kanisa la JEHOVAH AMESHINDA, kulikuwa na ukimya kama wa siku zote lakini mita chache kutoka nyumba Ile kubwa na ya kifahali anaonekana mtu, mweusi wa rangi, mrefu kupanda hewani, kichwa kilifunikwa na kofia nyeusi, mwili wa miraba minne aliyekuwa katika mavazi meusi kama Yale ya mafundi mitambo, huku mikononi akiwa na glavu ngumu na nyeusi vile vile, alisimama na kuiangalia transiforma inayosambaza umeme kwenye mtaa ule na dakika iliyofatia ni mlipuko mdogo wa transfoma Ile huku kukifuatiwa na kiza kizito mtaani pale. Kutawala kwa Giza ilikuwa ni rahisi kwa bwana yule kuhama Mahali pale na kukimbia kwa kasi Kisha akaudandia ukuta wa jumba lile la askofu wa kanisa la JEHOVAH AMESHINDA.
"mzafalu hebu cheki shida ni umeme umekatika hapa tu au mtaa mzima?"
"kote ni Giza mkuu alafu nilisikia mlipuko kwa mbali nahisi transfoma itakuwa imejibu au wauza chips wanachakachua wese"
"jenereta si linafanya kazi?"
"Ila kama nilimsikia kizito akisema liliishiwa mafuta na umeme huku ulikuwa haukatiki ovyo ovyo hivyo tuliona haina haha........ila hata hivyo Kuna dumu Lina mafuta Kule stoo ngoja nikayaweke niliwashe mkuu"
"fanya hivyo" aliongea Jamaa yule mwenye mwili uliokubali ratiba ya mazoezi na hakuwa mwingine bali meja Tumbaku, wakati wao wakiimarisha ulinzi upande wa juu yule mvamizi alionekana akiambaa na ukuta na kutua kama unyoya bila kutoa kishindo ilifurahisha kwa mtindo aliotua nao na kwenda kujibanza na kutuma ujumbe sehemu na hapo hapo alirudishiwa jibu kuwa kila kitu kilikuwa sawa alijisogeza mpaka nyuma ya stoo ile na kumsubiri mtu aliyefahamika kama mzafalu ili aweze kuanza kazi yake ya kuwamaliza walinzi, ilikuwa kazi nzito ila kivyovyote vile ilikuwa lazima amfikie mtu anayemhitaji na punde aliona miale ya tochi ikija katika eneo alilopo huku mtu yule akipiga miluzi tu bila kujua ndiyo itakuwa miluzi ya mwisho kuitoa kabla hajavuta pumzi yake ya mwisho kabla ya kifo.
"hizi funguo na zenyewe ziache weng......" hakumaliza alichotaka kuongea shingo yake ilijaa katika mikono migumu na iliyojaa misuli na hapo alituliza kwa kofi moja la mgongo.
"tulia wewe kenge.....mpo wangapi humu ndani" aliuliza kwa sauti ndogo ila iliyojaa utemi.
"tupo watano tu" alipigwa ngumi kavu ya mgongo mpaka akajikuta anataka kulia.
"siku nyingine ukiwa unaongea na wanaume si vyema kuongea uongo humu ndani mko kumi na nalijua hilo ila nilikuuliza makusudi ili nione kama wewe ni muaminifu ila kumbe siyo na adhabu yako wewe ni kifo" alisema hivo na muda ule kijasho chembamba kikamtoka yule mlinzi na hapo ikasikika mlio wa kitu kuvunjika.....naam ilikuwa ni shingo ya mlinzi imevunjwa vibaya huku mwili ukiwa mbali na uhai, akaibuluza ile maiti nakuificha nyuma ya mlango.punde akasikia vishindo vya mtu akija upande ule wa stoo akabana nyuma ya mlango na kuizima tochi ile.
"oya wewe mzafalu umekuja kulala stoo hebu lete hayo mafuta tuwashe jenereta niistue simu yangu nimtafute mama chanja hehehehe" lakini alisita kupiga hatua kwenda mbele kwani alihisi uwepo wa mtu mle ndani na hapo akapiga moyo konde kwamba huenda mwenzie anatafuta dumu la mafuta ili akawashe jenereta ila nafsi nyingine ilipingana nae kwamba utafutaji ule wa gizani na tochi alikuja nayo huku ya kazi gani? wakati anawasha tochi alihisi kitu kama upepo kimempita na hata alipogeuka hakuona hicho kitu akapuuzia huku akihisi ni upepo unaovuma ndiyo umepita, alipopiga tochi mbele yake alikutana na viatu vya mtu aliyelala alipopiga hatua kuelekea ilipo miguu ile ndipo alipopigwa na butwaa kwani Mzafalu alikuwa chini huku uhai ukiwa mbali nae alipogeuka ili aende kutoa taarifa kwa wenzie alikutana na ngumi kavu na nzito iliyotua kwenye koo na kulipasua mtu yule aliishia kuguna kama mtu aliyepiga mshindo katika tendo la ndoa, mtu yule alidondoka huku akishika shingo yake na sekunde iliyofata aliicezesha miguu yake na kutumbua macho kama amebanwa korodani na kuikata roho. kuona hivyo alijua kuna hesabu ya walinzi nane kabla hajamfikia mlengwa wake akatambaa mpaka kwenye maua makubwa yaliyokuwa karibu na ukuta na punde alimuona mlinzi mmoja aliyekuwa amewasha sigara, sekunde ya kwanza mlinzi yule alikuwa peke yake akijiandaa kuivuta sigara ile sekunde ya pili walikuwa wawili huku mmoja akiwa tofauti na yeye kabla hajafanya chocchote alipigwa pigo hatari la karate na kumuacha akitambarajika chinii huku mwili ukikosa uhai lilikuwa ni pigo baya lilipotua kwenye shingo la mtu yule liliipasua kabisa kiasi cha mtu yule kushindwa kuvuta hewa vizuri na kujikuta dakika chache zilizopita aliivuta pumzi ya uhai na sasa anahangaika kuitafuta na kila akivuta pumzi anajikuta anakifata kifo na mwisho alitulia akiwa hana uhai, hatua ya kwanza ilimkuta ameyaacha maficho yale na kuusogelea ukuta ulio karibu na kona ya kuelekea kwenye maegesho ya magari. alisikia chuma cha baridi kimegusa kisogo chake.
"tulia hivyo hivyo wewe kunguni ukileta ujanja wa aina yoyote sitasita kuumwaga ubongo wako" sauti kavu na iliyojaa utemi ilisema huku ikionesha haina masikhara hata kidogo.
"kwani wewe ni nani unayekaa nyuma kwa wanaume mwenzako unataka kufanya nini" ASP Richard alipima umakini wa mtu yule ila hata hivyo aliambulia ngumi kavu ya mgongo kutoka kwa jitu lile.
"unatakiwa unijibu maswali nitakayo kuuliza na siyo kuniuliza maswali na ukirudia hiyo tabia sitosita kutumbukiza risasi kwenye kichwa chako......kwanza tulia nijihakikishie kama huna silaha kunguni wewe uliyevamia meli ya wagiriki na boxa leo tutakuonesha kwamba kuna ngome hufai kuingia" alisema hivyo huku akianza kumpapasa na hapo ASP Richard koo lilimkauka kwa hofu ya kuingia mikononi mwa adui mapema vile.
"unatoka wapi wewe kunguni waliokutuma hawakukuambia hii ngome haiingiliki leo utatafunwa na mbwa huku ukiwahai.....tembea mbele wewe mtoto wa malaya" aliongea huku akimpiga kofi la shingo huku akiendelea kuweka umakini kwa mtu yule wakati wanatembea simu ya jitu lile iliita kiasi cha kulipotezea umakini na hilo ndilo kosa alilokuwa anasubiri ASP Richard lifanyike ili aweze kusahihisha makosa kitendo cha kuichukua simu na kuiangalia kabla hajapokea alikutana na mkumbo ulio wadondosha kila mtu upande wake huku bastola ikidondoka pembeni na kuliacha jitu likitukana tusi kubwa la nguoni, na kwa wepesi wote waliamka tayari kwa mpambano wa kutumia mikono na hapo ASP Richard alimuonesha kwanini alipewa mkanda mweusi katika sanaa ya mapigano hasa ule wa judo na karate, kwani alimsukumia teke maarufu kwa mchezo wa karate 'ushiro geri' lilimpata jitu lile na kuvunja mbavu zake kiasi cha kulifanya libweke kama mbwa aliyepigwa na mwikowakati akitaka kuiba nyama kwenye sherehe, liliposimama lilikutana na mdomo wa bastola unaliangalia na muda huo huo bastola ilikohoa mara mbili kama chafya ya mtoto mdogo na kwenda kutua kwenye upande wa kushoto wa kifua na kuuondoa uhai wa jitu lile, akaokota bastola ya lile jitu akaitoa magazine na kukuta ina risasi za kutosha, akasonga mbele na kukutanana na uwazi mpana uliokuwa unaunganisha nyumba ile na maegesho ya magari na mpaka muda huo eneo lote lilikuwa giza.
"tulia hivo hivo na ufate maelekezo ntakayokupa" aliongea kitemi ASP Richad huku akiibana bastola kiunoni mwa mlinzi yule aliyekuwa amejibanza karibu na gari huku akiongea na simu na mpenzi wake
"nipeleke hadi chumbani kwa bosi wako na usilete janja janja utajuta kuzaliwa haya songa mbele" walianza kutembea huku mlinzi yule akipitia eneo la jikoni na punde alipofikia kitasa na kukizungusha kikakubali akili ya ASP Richard ilikuwa kazini huku mlango wake wa sita wa fahamu ukiwa unafanya kazi kiasi cha kusikia hata mchekecho wa hatua za sisimizi, kulikuwa na giza sana jikoni na alichokifanya Richard ni kumuuliza ni wapi bosi wake alipo lakini alistaajabu jibu la kejeli la mtu yule.
"unamtaka bosi yupo hapa fungua zipu ukutane naye hahahahaha"
"sawa ngoja nionane nae...." bastola yake ilikohoa mara tatu na mtu yule kabla ya kufika chini alidakwa ili asilete kishindo alilazwa chini huku akikoroma na hapo alimuongeza risasi ya kichwa kumuwahisha huko akawe kuni, mbele kidogo alikutanana korido iliyosheheni kiza na kisha akaamba ambaa kwa hatua zisizotoa sauti, hatua kadhaa mbele alimuona mlinzi mwingine ambaye alimnyatia kwa nyuma, alipobakisha hatua kadhaa kumfikia alichomoa kisu na alipomfikia hakufanya kosa alizamisha kisu kile nyuma usawa wa uti wa mgongo nakumziba sauti kwa mkono wa kushoto alimshikilia hivo hivo mpaka alipokata kauli, punde mlango ulifunguliwa na akatoka Askofu huku akiwa anaongea na simu huku akiwa na bashasha.
"tulia hivo hivo Askofu muovu wewe" na kufumba na kufumbua tayari walikuwa wameifikia sebure na punde umeme ukawaka katika jambo la kustaajabisha ASP Richard alishangaa kuwaona watu anao wafahamu kabisa,
" meja tumbaku na ajenti Diana mnafanya nini kwa huyu muovu? au nanyi mmeasi" aliongea kwa uchungu huku akiwatazama watu wale kwa makini.
"tukuulize wewe umefikaje hapa na nani? aliyekupa ruhusa yakufanya hivi, tangu mwanzo nilikuona mnoko mnoko sana sasal eo unoko utaufanyia huko utakapofika kwa shetani" kufikia hivo wote wawili walitoa bastola zao aina ya Colt 45 nakumnyooshea ASP Richard, bila wasiwasi alimkwida Askofu vizuri huku mdomo wa bastola ukiwa jirani kabisa na sikio lake la kulia.
"kuna watu wana roho mbaya sana umeanza lini kuwasingiziaviongozi wa dini na umefikaje fikaje humu ndani.....ukuteumekuja kufanya ujambazi hapa, polisi wa siku hizi mna njaa sana na utakacho ambulia ni risasi za kutosha mbwa wewe" akiongea ajenti Diana kwa dharau na kejeli
"hahaha eti nimefikaje, kwanza shusheni bastola zenu chini kabla sijamwaga ubongo wa huyu mkuu wenu na sitanii katika hili" alisema kitemi huku akiikandamiza bastola hiyo kwenye kichwa cha Askofu kitemi.
"shusheni vijana wangu......halijui alitendalo muacheni tu" alisema askofu kwa hofu na taharuki huku akiwakazia macho watu wale wawili
"ongoza njia wewe shetani wa pembe moja" waliongozana mpaka wakaupita mlango wa sebureni pale sekunde iliyofata iliwakuta getini huku askofu akiwa amemtanguliza mbele kama ngao huku yeye anarudi kinyume nyume alipofunga geti alimkimbiza askofu mpaka kwenye gari huku akifatwa na mvua ya risasi kama chizi aliigeuza gari ile kwa mwendo wa ajabu nakutokomea mitaa hiyo yenye kukaliwa na watu wenye uwezo kiuchuni kwani hata majengo yalisadifu hivo.
"ningekuwa wewe hivi sasa ningekuwa natafuta sehemu ya kutorokea.......alaf naskia wewe ni askari polisi japo sijajua ni wa kituo gani? ila umefanya kitu utakacho kijutia maisha yako yote au wenzio hawajakueleza kwamba watu kama sisi hatugusiki kiwepesi, bosi wako hajakueleza hilo nakuonea huruma maana ninaona ukipoteza kazi ingali bado kijana mdogo na kingine aliyekutuma ni kama alikuwa hakupendi kwani mpaka sasa maisha yako na kibarua chako kijana wangu kipo rehani na kama, ni pesa wewe sema ni kiasi gani unataka nami nitakuwekea sasa hivi kwenye akaunti yako na nitakusameh...." alikatishwa na sauti nzito.
"nyamaza na utulie mimi sinunuliki kama nyanya sokoni kama wale wajinga, nakupeleka ukaonane na aliyenituma kisha nitawarudia wale paka wako na nakuhakikishia watakutana na 'PUMZI YA KIFO' kaa kwa kutulia wewe ni mhalifu kama walivyo wahalifu wengine na sheria itakushughulikia vilivyo kama inavyowashughulikia wengine " aliongea kwa.msisitizo uliochanganyikana na hasira, huku akiwa makini barabarani.
"hahahaha kijana unaongelea sheria ni kiongozi gani atakayesema nipelekwe mahakamani.....yaani kiufupi unapoteza muda wako bure unaongelea sheria kwa tajiri kama mimi sheria, alafu masikini ndiyo mnataja taja hiyo sheria bwana mdogo acha kukaza fuvu chukua pesa uone kama utaizungumzia tena hiyo sheria, kama watu wameshindwa kufuata sheria za Mungu ije kuwa hizi zinazotungwa na wanada........"
"unanipeleka wapi hapa......hizi si ofisi za....ooohhh Munguwangu" alilalama askofu mara tu baada ya kufika katika ofisi za idara ya ujasusi, kwani anazifahamu kupitia kwa mamluki wanaofanya kazi nae ambao walimdokeza mahali alipopelekwa Vanessa Ndelwa kwa ajili ya kuhojiwa na sasa ndiyo naye alikuwa anapelekwa humo humo ndani.
"unataka kuonana na aliyenituma ambaye kwake pesa zako za sadaka unazowaibia wajinga wajinga kwa mwamvuli wa kanisaa hizo nyingine unazo zitakatisha kupitia madawa ya kulevya kiufupi wewe mzee anayekula pesa zako, anajipaka damu za wale wanaokufa na kuteseka mtaani huku wakiwa hawana nguvu ya kujitaftia kipato kisa tu ni hayo madawa ya kulevya mnayoyauza na ni kuhakikishie watu kama wewe mnapaswa muishie maisha yenu jela mkiteseka kama wanavyoteseka vijana wengine, shuka ukaonane na masikini wanaoitaja taja sheria" aliongea kwa majigambo ASP Richard huku akimvuta mtu wake kuelekea ndani ya jengo huku akimpitisha mlango wa nyuma wa jengo lile na hapo alipokelewa na watu wanne walioonekana kuwa wakakamavu na wasio na uso wa masikhara hata kidogo, wakamvisha gunia Askofu na kumpeleka msobe msobe mpaka selo za chini kabisa wanazoziita 'SHIMO LA TEWA'
"KAZI NZURI SANA KIJANA WANGU" aliongea kwa tabasamu Chifu kwani sasa lile zoezi linaonekana kufanikiwa huku wahusika wakianza kushughulikiwa.
"asante sana chifu ila.........naweza kupata muda tukaongeaofisini kwako.
"bila shaka kijana wangu...........subiri mara moja kuna simu inaingia." aliongea hivo chifu huku akijisogeza pembeni
"ndiyo mkuu, umeshindaje" alianza hivo chifu
"nimeshinda salama ila nipo nje ya jengo lako kama tulivyokubaliana kwamba silali mpaka nimuone huyo wanayemuita CASANOVA" aliongea mheshimiwa raisi huku akianza kutupa miguu kuelekea ofisi ya chifu idarani hapo
*itaendelea
HAYA SASA RAISI AMEFIKA KUONANA NA MTU WAKE KAMA ALIVYOAHIDI, JE ATAKIPATA KILE ANACHOKIHITAJI ILI NCHI IWE SALAMA? Tukutane toleo lijalo kwa majibu zaidi
 
Back
Top Bottom