“NIKIANGALIA NYUMA YANGU NAONA WINGU ZITO LA GIZA ILA NIKITAZAMA MBELE YANGU NAONA MWANGAZA WA MATUMAINI”……….TUFUATANE ILI TULIKIMBIE GIZA HILI
MUTAMBU-BURUNDI
Saa 8:47usiku
Ni mji ulioko nje ya jiji la Bujumbura kilomita 33.0 Sawa na mwendo wa dakika 45 kwa saa kwa wale waliokuwa na usafiri wa magari, ni mji uliokuwa kimya Sana kiasi kumaanisha wakazi wake wametopea katika usingizi mzito, muda huu alishuka bwana Thobias Chumvinyingi katikati ya mji huu na kutelekeza gari aliloliiba katika nyumba moja iliyokuwa haIkiliwi na mtu katika pori dogo katika mpaka wa kuingia jijini Bujumbura na mji wa Rumonge, Kisha akafungua tenki la mafuta na kuwasha kiberiti cha gesi ambacho kilikuwa kwenye mfuko wa suruali yake ya dengirizi kwani ukiondoa kadi ya Benki aliyoisunda mfuko wa nyuma nyaraka nyingine ikiwemo pasi ya kusafiria ilisahaulika mikononi mwa watu wale waliomvamia usiku alistuka Sana alipojisachi na kukumbuka simu ameisahau juu ya Meza ndogo iliyo jirani na kitanda alichokuwa amelalia katika chumba cha hoteli Ile, baada ya kuiwasha moto gari Ile Aina ya Toyota Mark II aliyoiiba katika moja ya maegesho bubu ya jiji lile la Bujumbura ambayo mlinzi wake alikuwa amelala usingizi wa pono.
Sasa lilikuwa likiteketea kuficha ushahidi wa yeye kuwepo katika mji huo alizipiga hatua ndefu ndefu na Sasa alikuwa Almanza kuziona taa za mji ule lengo lake ilikuwa ni kufika katika nyumba ya siri ya moja ya maafisa waandamizi wa ubalozini hapo aliyekuwa anahusika na jukumu la ulinzi wa ubalozini pale, ilibaki umbali wa mite Mia moja kabla hajaifikia nyumba Ile aliamua kuuvaa uhusika wake kama afisa usalama na jasusi, akazunguka mtaa wa nyuma na kuangalia mazingira yaliompokea kwa utulivu akausogelea ukuta ule na kuukwea na kujivuta hadi juu ambalo alichungulia ndani na kupokelewa na mazingira yalioonekana kutokupewa matunzo kwa muda mrefu. Akajivuta na kutua kama unyoya wa kuku bila kutoa sauti akaanza kunyata kwa kuambaa na ukuta Giza lilimpa faida na lilipozoea macho yake ilikuwa kama aonavyo mchana sekunde ya kwanza ilipita akiwa amebana pale pale, sekunde ya pili alikuwa anacheza na kitasa cha mlango wa kutoka nje kupitia upande ule wa nyuma, akafanikiwa kuingia na kukutana kiza totoro, alipiga hatua ya kwanza kuifata korido akafanikiwa na sekunde iliyofata alitaka kuifata swichi ili kuwasha taa alifanikiwa kuifikia kitendo cha mwanga kujitokeza alipigwa na butwaa kukutana na mdomo wa bastola Aina ya Taurus PT-109 iliwa imefungwa kiwambo, alijikuta anatetemeka na Koo kumkauka, alijilaumu kwa kila kosa analolifanya linamgharimu, alijiona ni binadamu mwenye mkosi kuliko wote,
"wewe ni Nani? na unafanya nini hapa na Nani amekutuma Kuja usiku huu hapa?" sauti nzito na kavu ilivunja ukimya kwa Kiswahili kilichonyooka , hii ilimpa ahueni kidogo kukutana na mtanzania mwenzake
"Mimi ni Thobias Chumvinyingi ni afisa wa ubalozi huu uliolipuliwa na nilikuja hapa kutafta hifadhi" sentensi hiyo ilichakatwa kwa sekunde kadhaa Kisha kikafuatia kitendo cha kustaajabisha kwani mtu yule aliirudisha silaha kiunoni Kisha akamhadaa kwa kumpa mkono ambalo thobias bila kujua akajuani Ishara ya Amani naye akaupeleka sekunde Ile ulidakwa na mikono imara na kuvuta kwa nguvu Kisha akapigwa kichwa kwenye mwamba wa pua kitu kilichomfanya apige yowe la hofu, kabla maumivu hayajapoa alipokea makonde Mawili ya mbavu yaliyomfanya aangaike kuvuta pumzi huku akisikilizia maumivu.
"nyie ndiyo wasaliti tunaowatafuta na Leo utanieleza kila kitu kilichotokea mshenzi wewe nilijua mtakuja huku" alifoka Tena yule mtu kwa gadhabu kama nyati aliyejeruhiwa
"nisikilize ndugu yangu mimi nimefika jijini hapa massa mawili na......" Akataka kufunguka ila akajikatiza na kukumbuka sheria namba moja ya ujasusi kuwa haitakiwi kumuamini mtu yoyote yule hata kivuli chake kwani kinaweza kukukimbia akiwa kwenye matatizo, lakini alishtukia amepigwa Kofi Zito lililomfanya ahisi kichefu chefu na kuona rangi rangi machoni mwake.
"mbona unanipiga Tena ndugu yangu" alilalama mwanaume yule aliyeona ameyakanyaga, akamtazama mtu yule mikononi mwake na kuona Pete inayofanana na Ile aliyomuona nayo Kapteni Jumanne Saidi.
"Leo Utanitajia wasaliti wote Simama juu nyani wewe" alifoka Tena mtu yule na hapo akatoa bastola kiunoni mwake nakuinyoosha usawa wa kichwa cha Thobias huku akimsachi mifukoni katika namna iliyompatia maumivu kila kiganja cha mtu yule kilipopita kwa namna ya kumsachi, alihusudu kuwa yule mtu alikuwa hatari kuliko wale aliowakimbia
"haya nambie watu unao shirikiana nao kulihujumu taifa" alibaki njia panda kujibu kwani bado hakujua yule mtu yuko upande gani, ila alijipa matumaini kwa rafudhi ya mtu yule ambaye hakuiona sura yake vizuri kwani ilifunikwa kwa kofia na barakoa nyeusi ikibakiza macho tu yaliyotoa taswira ya unyama ulioko ndani ya mtu huyu, Kuona hivo ilibidi aulize kitu kuona kama ni mmoja wa mtu aliyeko upande wao.
"siku ya jumamosi kule chuoni Zanzibar maafisa wote watarajiwa walitakiwa kula pilau la kachumbari lililochanganywa na nyama ya Bata mzinga na siku ya kuapishwa tulikula kiapo cha kuwa waaminifu na wazalendo na kulinda Siri za nchi ikiwa ni pamoja kufichua, kutafuta na kuchakata taarifa zinazohatarisha usalama wa nchi iwe ndani au nje ya nchi na kumtii raia namba moja wa nchi yetu" alijaribu kutia kidole kwenye maji kuona kama ni saizi ya miguu yake kuyavuka.
"Hilo ni jambo dogo Sana, hivi hutambui wapo watu wanakula kiapo na bado Kuna wasaliti na umesahau sheria ya kwanza uliyoambiwa siku ya kwanza uliyokuwa mafunzoni, hiyo Mimi naitekeleza kama sheria zingine za nchi na Mungu, tusipotezeane muda kwa hadithi nyepesi wenzako wake wapi? Safari hii alibwata huku akiikandamiza kabisa bastola Ile kichwani.
"wasalimie kuzim....." Alikatishwa na Jina lililotajwa kwa sauti ndogo
"ukikutana na Kapteni Jumanne Saidi mwambie Hali ni mbaya Sana jijini Bujumbura" aliongea kwa kukata Tamaa na sekunde Ile Ile alishangaa bastola imeshushwa chini
"umemfahamu vipi Kapteni jumanne Saidi" hakuwa na huyana zaidi ya kujitambulisha na kumsimulia tangu alivyoanza naye safari jijini Dar es salaam na kuachania katika uwanja wa ndegewa Jomo Kenyata.
"ndugu ni heri kusafiri ukiwa na matumaini kuliko kufika" aliongea hivyo ASP Richard huku Akivua barakoa na kofia, akamsimulia jinsi alivyoutumia usafiri wa gari huku Mara kadhaa akikutana na vizuizi hivyo alifanikiwa kupita kwani nyaraka zake zilionesha akielekea rumonge kupeleka gari hiyo kwa tajiri mmoja hivyo kuepuka kushtukiwa na watu wabaya miongoni mwa Askari waliokuwa kwenye vizuizi.
"tangu umeingia jiji la Bujumbura Kuna kitu gani umegundua" alitupa swali Hilo kuelekea kwa thobias chumvinyingi
"tangu nimefika roho yangu imewindwa na nimeishia kuponea chupuchupu tu" alisema thobias chumvinyingi kwa masikitiko.
BABATI-MANYARA
Saa 9:03 usiku.
wakati watanzania wengine wakiwa wamelala, kuna watu katikavyombo vya ulinzi na usalama walikuwa macho na sasa walikuwa wana muuwinda mtu ambaye ana hatarisha usalama wa nchi na yuko mita kadhaa kutoka wao walipo katika nyumba yake ya kulala wageni.taarifa za uwepo wa mtu huyu zilithibitishwa baada ya kunaswa sura yake na kamera za siri zilizopachikwa na idara ya ujasusi lengo kuu hasa ni kuiweka nchi katika hali ya ushwari kila siku ieandayo kwa mungu, taarifa walizozipata kutoka Arusha ya kuwa wamefanikiwa kuyapata mabomu yale ambayo yalitakiwa Yazuie kesho yake watu kutoka na kuingia ili Yale mengine yakitarajia kuwazika asubuhi Ile wakazi wa jiji lile ule muda punde tu baada ya tamasha kuanza ilikuwa ni kazi iliyotukuka ya The chameleone hasa ukizingatia hakukuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutafuta mtu ambaye atafanya kazi bila kuwa mamluki, neno uaminifu likiwa limepotea kwa watu wa juu kabisa wa vyombo vya ulinzi na usalama kama jenerali wa jeshi, chifu wa idara yaujasusi na hata raisi mwenyewe hakutambui yupi yupo upande wake yupi ni mamluki, sasa walipeana ishara waanze kuingia katika uzio wa nyumba ile ya kulala wageni ulinzi ulikuwa wa kawaida, lakini wakaghairi na kuamua kutumia njia ya kawaida huku silaha zao kiunoni zilikuwa ziko tayari kukohoa na kuondoka na pumzi ya mtu.
" kaka Habari" alimsalimia luteni kanali Charz, mlinzi wa getini
"sogeeni hatua kumi alafu mjieleze nyie ni akina nani na mnataka nini" ulikuwa ni mkwara wa mlinzi aliyekuwa getini.
"tunataka chumba tukapumzike mimi na mume wangu" aliongeakwa sauti nyororo huku akimlalia kifuani luteni charz kitu kilichomfanya mwili kumsisimka kwani joto mwanana la chiku lilitaka kuamsha hisia zake za tangu miaka kadhaa ya ujana wake......akamezea kwani alikuwa na kazi mbele yake ambayo ilitakiwa kukamilishwa kabla ya alfajiri.
"watu wengine bhana mtu unakutana naye barabarani huko humjui umeshajipachika cheo cha mke haya bhana mna bahati Sana kimebakia kimoja tu tatizo sijajua kama mna pesa ya kukichukua" alibwabwaja Tena yule mlinzi huku safari hii akitikisa kiberiti huku akimtazama luteni kanali Charz.
"kwani ni bei gani hiyo ambayo siwezi kuilipa Kisha nikaufurahia usiku na mrembo kama huyu" alizungumza kwaj euri ya pesa luteni kanali Charz
"kimebakia cha laki mbili bosi teeth teeeh" alirudia tena mlinziyule huku akijichekesha kinafiki.
"Sawa tunalipa wapi hapa au mapokezi" aliuliza Tena luteni kanali Charz.
"mapokezi mkuu, Tena ngoja tuongozane ili nikawaoneshe" walifika mapokezi na kumkuta Binti wa makamo akiwa amejiegesha huku akipambana na kero za mbu na baridi
"mamaaaaa......kumbe ni wewe nilidhani nyoka au limdudu " wote waliishia kucheka huku Binti yule akijiweka sawa
"wewe mrembo acha uwoga hehehehe si nikuoe tu nikufundishe ujasiri" alisema mlinzi huku mate ya uchu yakimdondoka baadaya kuona paja la kinyaturu lililokuwa jeupe, kupanda kwa sketi ndiyo kulimnyanyasa kihisia.
"koma mshenzi wewe nakupeleka wapi mtu sura kama unanizomea....hebu acha ujinga wako mimi niwahudumie watu wakajivinjari.....umewaambia kimebakia kimoja na bei yake" aliongea yule Dada huku akiwa amekasirika kutaniwa na mlinziyule ambaye kwa ni ushahidi Tosha kuwa sura yake ilikuwa inatumika kutishia watoto katika mtaa anaokaa ambapo huwenda mtoto amegoma kula, kuoga na hata kulala wakilisikia Jina la Majuto basi hutekeleza kile alichokuwa anagomea kukifanyia utekelezaji.
"upo na mkurugenzi husikii ananukia pesa" alichombeza kipambe mlinzi yule.
"mwaka huu utautafuta uchawa na usipate nyani wewe....achaneni na huyo kaka unaweza kulipia tu, huyo anawalia unit zenu za usingizi Hana lolote ona jisura lake" alibwata Tena yule Dada huku akimnanga mlinzi yule ajulikanaye kama Majuto
"Sina cash ila si hata kwa kadi nalipia?" Alimuuliza Dada yule huku akimtazama machine.
"bila shaka kaka angu mashine hiyo hapo" aliongea yule Dada huku akiweka machine ya kuchanjia kadi. Alipomaliza utaratibu wa malipo ukaja utaratibu wa kusaini ambapo chiku alilivuta daftari lile na Kisha kuandika Jina la JACOB FRANK akaandika taratibu taarifa nyingine huku muda huo luteni kanali Charz akijifanya kumbusu Chiku huku jicho lake kama LA mwewe liki ya peruzi Yale majina ya wageni wa siku hiyo kwa umakini mkubwa, ndiyo aliamua kutumia njia Ile kuwazuga mlinzi na Dada yule wa mapokezi waliofikiri watu wale walikuwa wanajifanya wanapendana Sana takribani dakika tatu zilitosha kupata kile walichokitafuta,Naam kwa namna Mohamed mahboob alivyojifanya kuwahadaa wanausala kwa kujifanya raia mwema hata akiwa hotelini kwake kwa kuandika Jina kama mgeni ndivyo alivyowasogeza karibu na bahati nzuri ni kwamba chumba Chao kilikuwa kwenye mstari wa vymba vilivyokuwa ghorofa ya tatu, jumbo lililo wastaajabishani kutoliona Jina la Shaban Chakupewa, wakati taarifa zinasema ndiye mlinzi wake wa mwisho waliishia kutabasamu na kuanza kuzipanda ngazi kwa pupa, wakakipita chumba kile kilicholaliwa na windo lao, mlango wa pili kutoka kile ndiyo kilikuwa chumba Chao.
"walipoingia ndani ya chumba kile kipana chenye kitanda cha Sita kwa Sita, jokofu dogo lililokuwa na chupa ya mvinyo Brandi ya pearly Bay, juu kulikuwa na feni yenye mapanga boi marefu huku chini kukiwa na zulia jekundu, chumba kilitamanisha kwani kilipambwa kwa mapazia mazito ya rangi ya pinki iliyochanyikana na weupe kwenye baadhi ya michoro katika mapazia Yale, Hakika chumba kiliendana na bei waliyotoa kiufupi hawakupigwa kama wasemavyo vijana wa mjini. Chiku alizima taa punde tu baada ya kufunga mlango, shiiiiiiii ni ishara ambayo luteni kanali charz aliielewa kwani haraka alitoa simu yake na kuiweka upande wa kamera ili kutafuta kamera za Siri kama zimetegwa hotelini humu huku Chiku akitoa combo kinachotambua uwepo wa vinasa sauti, zoezi Lao lilidumu ndani ya dakika tano kwa weledi wa Hali ya juu kuhofia kuharibu mpango, Naam ukafatia muda wa maigizo.
"aaaaaaissshhh mume wangu taratibu baba" ilisikika sauti ya mwanamke kwenye hoteli Ile ya MOMA'S
"hapo hapo mme wangu.....nakojoa nakojoaaa baba sikuachi nimesema sikuachi" alilalama mwanamke kwa sauti huku kelele za kitanda zikiwa nyingi kiasi cha kuwa kero kwa wateja wengine kiasi cha kupiga simu mapokezi kuwasaidia kuondosha kero hiyo mmoja wao akiwa Mohamed mahboob mwenyewe, Dada wa mapokezi alifika na kugonga lahaula! Chumba alichokipiga hodi aligundua ni kile cha wateja waliokichukua dakika kumi na tano zilizopita.
"kaka.......kaka fungua" aliongea Dada wa mapokezi
"Nani wewe unayesumbua starehe za watu......aaahhh kuharibiana tu utamu" muda huo alijifanya anavaa suruali, lakini ukweli ni kwamba hakuwa ametoa chochote aliulegeza mkanda na kifungo cha suruali yake Kisha akaiachia wakati anashuka kitandani Kisha kuidaka kabla haijafika chini na sekunde iliyofata alikuwa mlangoni huku akiweka sura ya kuonekana kana Kwanba kachukizwa na kitu.
"Kuna shida gani wewe Dada unagonga gonga Milango au mmepanga mimi nisiifaidi hela yangu si ndiyo? Aliongea kwa sauti ya kukoroma huku akikunja sura.
"kaka wateja wanalalamika mnawapigia kelele na wao wamepumzika"aliongea yule Binti kwa unyenyekevu.
"kwani Mimi nimewazuia wanawake wao wasipige kelele kama kuna anayechukia aje humu aone kinachofanya apige kelele hehehe"alimalizia kwa kicheko huku akimwangalia yule Dada
"kaka kuwa mstaarabu basi heshimu basi usingizi wa majirani zako" alilalama Tena yule Dada huku akionekana kuanza kuchukia.
"Sema basi na wewe kama unataka tuumalize usiku tukiwa mrembo acha pang'ang'a nyingi eeeennh" alisema hivo huku akiupeleka mkono wake kwenye shavu la yule mhudumu.
"Tena unikome usichukulie kila mtu ni Malaya ohooooo....tutaharibiana Sasa hivi ngojea uone, ms*nge wewe nisubiri hapo nkuletee hela yako alipayuka yule Dada huku akianza kupiga hatua mapokezi kana kwamba amesahau kitu, alivyoishia kwenye ngazi alijitokeza Mohamed kutoka chumbani kwake huku akiwa na bastola kiunoni, akamkuta yule bwana amesimama pale.
"nimekuja kuona hicho kinachopigisha kelele kama ulivyosema bwana mkubwa" aliongea Mohamed akiwa umeuweka uso wakazi, Hakika luteni kanali Charz aliuhusudu uwezo wa the chameleone katika kucheza na kompyuta pamoja na uchoraji wa picha kwani picha waliyotumia ilifanana na mtu aliyesimama mbele Yao, kitu kilichowastaajabisha ni umbile dogo la mtu yule katika picha lakini Sasa lilikuwa mbele ya luteni kanali Charz
"hahahaha dunia Ina mambo kweli nilijua atakuja mkeo ili sinema inoge......umekuja wewe hebu Rudi kamlete mkeo wewe utazame kama filamu hahaha" alisema hivyo kebehi kwa lengola kumpandisha hasira adui yake ili aingie kichwa kichwa.
"kafiri mkubwa wewe ingia ndani nkufundishe adabu unapoongea na wanaume wenzio mzungu wa reli wewe" alifoka huku akifunua Shati na kumuonesha bastola na muda huo huo alimsukuma luteni charz kurudi ndani, alipoingia yeye aliurudishia mlango na kuufunga kabisa ila alivyogeuka alistaajabu kukutana na midomo miwili ya bastola Zilizofungwa viwambo vya kuzia sauti vikimtazama, alitamani ardhi ipasuke aungie alijilaumu kuingia kwenye mtego ule kiwepesi namna Ile
"tupa silaha yako chini na piga magoti weka mikono kichwani" iliongea kitemi sauti ya mwanadada chiku huku Mohamed akiwa Hana namna zaidi ya kutii amri hakuamini kama angekamatwa kama kuku Tena akiwa kwenye nyumbaxaliyojenga mwenyewe, alipigwa take la mgongo na kudondokea kifua huku akipiga yowe la hofu.
"Tulia wewe mshenzi....nkakufunze kuongea na wanaume kwakuwa wewe umeshindwa kunifunza kuongea na wanaume" aliongea luteni kanali Charz huku akimsimamisha na sekunde iliyofata mlango ulipigwa take huku luteni kanali Charz akimpiga kikumbo Mohamed mahbobo na wote walidondoka chini, kuhama Kwao ni kama kulisaidia kwani mvua ya risasi ilichimba pale chini huku mpigaji akiwa amekusudia kuwamaliza wote huku yeye akiingia kwa mtindo wa kuzunguka kama tairi na hata yeye alikoswa na risasi zilizotumwa kwa lengo la kumuondoa shabani chakupewa kutoka kwenye bastola aliyoishika kikamilifu Chiku, muda huo mohamed akapigwa kabali huku akiwekwea bastola kichwani.
"mwambie mwenzio ajisalimishe au nikumwage ubongo" kuna kitu Luteni kanali Charz alijifunza kutoka kwa mohamed.......hofu ya kifo! alijikuta anatabasamu kwani alikwishaujua udhaifu wa mateka wake.
"shebby weka silaha chini......watanimaliza shusha silaha tumesha wahiwa" alipayuka mohamed huku kijasho chembamba kikimtoka wakati huo huo alijitokeza shaban chakupewa akiwa amenyanyua mikono na kuitupa silaha chini wakati chiku anajiandaa kumdhibiti alijitokeza yule mdada wa mapokezi akiwa na mlinzi wa getini na hapo hapo ikawa nafasi ya pekee kwa shaban kutoroka ndani mle, alifanikiwa kipita mlangoni ila akiwa na maumivu makali kwani risasi mbili zilizotumwa pamoja zilimuingia katika mfupa wa bega lake la kushoto, pamoja na maumivu ila alizikwea ngazi kwa uharaka na kupotea eneo lile.
********
"SIMBA WENYE NJAA KALI WALIVAMIA BOMA LA MTEMI NA KUONDOKA NA MTEMI NA MIMI NIMEPATA MAJERAHA NARUDI SAITI KWA AJILI YA KUJIAGUA ILA HAWA WATU NI HATARI SANA MKUU TUSIPOANGALIA WATAIFIKIA MBONI YA JICHO"
itaendelea******
JE NINI KITAJIRI KATIKA TOLEO LIJALO? Usikae mbali na simulizi hii……….MCHANA MWEMA