Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 62
Inategemea msimamo wa watu waliyoishuhudia ajali hiyo. Watu wengi usahau kumshughulikia majeruhi na badala yake kumvamia dereva na gari lake kwa mawe na marungu, jambo ambalo huatarisha maisha ya watu wawili badala ya mmoja. Akijua hayo Joram hakuona kama aliwajibika kumlaumu dereva wa ajali hiyo au la.
“Imetokea saa ngapi ajali hii?” aliuliza akimkazia macho msemaji baada ya kuyaondoa juu ya majeruhi.
“Kama nusu saa iliyopita.”
“Kwa nini hukupiga simu hospitali?”
“Kweli! Kwanini sikupiga hospitali?” mtu huyo alijiuliza kwa sauti. “Pengine nilichanganyikiwa kwani ajali hii nusura itukumbe wote. Tulikuwa tukitembea bega kwa bega. Mara…”
“Usijali. Nitakusaidia,” Joram alimkatiza. “Tumpeleke wapi? Muhimbili au hospitali yoyote iliyo karibu?”
“Nadhani popote. Yuko mahututi sana.”
Wakashirikiana kumwinua na kumwingiza garini, mlango wa nyuma. Wakamlaza juu ya kiti kwa uangalifu. Kisha Joram na yule mtu wa pili wakapanda mbele na kuondoka.
Wakati Joram akijitayarisha kukanyaga mafuta kikamilifu, kama inavyomstahili dereva yeyote ampelekaye mgonjwa hospitali, alilazimika kusita mara alipoguswa na kitu baridi kisogoni. “Huna haja ya kwenda hospitali yoyote. Siumwi…” ilifuata sauti nzito ya mtu yule ambaye hapo nyuma kidogo alikuwa akikoroma kwa maumivu. Joram alipogeuka kumtazama alikutana na domo la bastola kubwa ikimwangalia. Aliyeishikilia ni yule aliyekuwa mgonjwa. Alikuwa akimtazama Joram kwa dhihaka ingawa uso wake ulikuwa mkavu uliokunjamana. Tabasamu la kuchukiza likautokea uso huo na kuruhusu meno machafu kutokeza hadharani. “Tumekupata au sio? Leo huna hila Joram,” ilifuata sauti ya mtu huyo.
Kabla Joram hajajua afanye nini alihisi kutekenywa ubavuni. Alipogeuka alikutana na mtutu mwingine wa bastola ukimkuna, bastola ambayo ilishikiliwa na yule mtu wa pili ambaye kitambo tu alikuwa akibembeleza kwa sauti ya huruma. Kama mwenzake, huyu pia alikuwa akichekelea. Tofauti ndogo ni kwamba tabasamu la huyo halikuwa la kuchukiza kama mwenzake. Lilikuwa la kawaida. Na meno yake yalikuwa meupe. “Ndiyo, Joram Kiango, mpelelezi mashuhuri. Umo mikononi mwa Nunda. Umeingia kirahisi kuliko nilivyokutegemea. U wapi ule ushujaa ambao inasemekana unao? Labda