Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Kesho ambayo ndio leo mzee wangu bas wacha tuvumilie saa tatu sio mbali.
 
Nikitaka 2 hours of memories na umoja namba 97 ni kiasi gani
 
Mvumilivu hula mbivu ndio lakini naona mbivu zenyewe zimetepeta tayari mkuu, sijui kuna mtu kalipa cha juu huko whatsap ili tusimwone uku!!!?? Maana ata sielewi, ata usingizi wenyewe unaninyemelea
 
mkuu kama unaona unakuwa bize muda uliotupanga basi uwe unatupia hata mapema aisee alosto [emoji16][emoji16]
 
Ni kumpotezea.tu.akijisikia atatupostia.mana hatukumlazmisha.ni mapenz yake mwenyewe Kwa wanajf.ila mwandish kuwa mwongo mwongo haifai.timiza ahd kadri ulivyoahd,
 
Hakuna asiyependa kupigiwa magoti akiwa kwenye eneo lake.
Hata huyu mwandishi anaona raha kubembelezwa. Ngoja tuendelee kumbembeleza na kumpa muda.
 
SEHEMU YA 414.

Watu wote walishangaa kutokana na kwamba saa yenyewe licha ya kuwa ‘Pocket Watch’ lakini ilionekana kuwa ya kawaida sana na kutokuwa na kitu cha ziada cha kuvutia.

“Hii saa niliishia kuona tu kwenye baadhi ya vitabu , Henry Graves ni saa ya mfukoni ambayo ilitengenezwa miaka mingi iliopita , ijapokuwa inaonekana kuwa kawaida kutokana na umri wake , lakini ni kweli imetengenezwa kwa karati kumi na nane za madini ya dhahabu , ni saa mabayo imetengenezwa kwa ajili ya kudumu muda mrefu, imetengenezwa kati ya mwaka 1932 na 1933, mmarekani anaefahamika kwa jina la Henry Graves alialika moja ya watu maarufu wanaohusika na kutengeneza saa wakati huo na kisha akaelezea wazo lake na saa hii ndipo ilipoweza kutengenezwa , ni moja tu dunia nzima”Aliongea Abaiku na watu wote walishangazwa na taarifa hio.

“Unasema moja tu?, Kama ni hivyo si inamaana ina Zaidi ya miaka tisini tokea kutengenezwa kwake?”Aliuliza Lele .

“Abaiku una uhakika saa hio ni yenyewe?”Aliuliza mwingine huku hali ya hewa ikifanya hata ule msisimko aliokuwa nao Cindy kupotea ghafla , mpaka hapo walipigwa gepu kali.

“I can assure you that it is , The Oxidation matches the era it was from, there is also no evidence of it being replica”

“Nina wahakikishia ni yenyewe , kutu yake inalingana na kipindi cha miaka ilipotengenezwa na hakuna ushahidi kuonyesha kama ni feki”Aliongea

Watu walikuwa wakimuamini sana Abaiku tokea alipokuwa chuo na umaarufu wake haukuishia chuoni tu, Abaiku ameshaalikwa kuwa mwendesha minada na mtambuzi wa vito vya thamani kwenye minada mikubwa duniani , ikiwemo mmoja uliofanyika Ufaransa mwaka 2018 ambao ndio ulimpatia umaarufu..

Edna alianza kukumbuka siku ambayo Roma alimpatia hio saa , alikumbuka Roma akimwambia kwamba aliichukua kutoka kwa Kamishina wa FBI , alijiuliza kama ni hivyo Roma alikuwa akifanya nini ndani ya USA?.

“Ijapokuwa saa hii imeishi kwa miaka Zaidi ya tisini , lakini namna ilivyotengenezwa kwa teknolojjia yake hakuna saa ambayo imeipita , ni moja ya saa inayochanganya sana yenye vifanya kazi Zaidi ya ishirini na nne , hata saa za kisasa ambazo zimetolewa zinaishinda kwenye vitu vichache sana , na ninaweza kukadiria kudumu mpaka mwaka 2100”Aliongea

“Sasa si itakuwa ghali sana?”

“Neno Ghali huwezi kupima thamani ya saa hii , mara ya mwisho iliuzwa kwenye mnada wa Sotheby’s mwaka 2014 kwa Zaidi ya Dollar za kimarekani milioni kumi na moja , ukijumlisha na mfumuko wa bei kama utaiweka kwenye thamani leo hii inaweza kununuliwa kwa Zaidi ya Dollar milioni ishirini na nne ni rahisi kusema huwezi kuikadiria thamani yake”Aliongea Abaiku.

Watu wote walijikuta wakitulia kabisa pasipo kuwa na neno huku wakijiuliza inakuwaje saa hio ya chuma chuma kuwa na thamani kubwa namna hio .

Walijiambia kama Vacheron Constatine ni mfalme wa Saa basi Henry Graves ni Mfalme juu ya Falme.Abaiku mara baada ya kumaliza shauku yake alimsogelea Roma na kuirudisha kwake.

“Mr Roma nisamehe kwa kutoa maelezo marefu , ila nimefurahi sana leo kuiona hii saa , imekuwaje mpaka ikawa mikononi mwako?”

“Niliipata kutoka kwa mtu mmoja huko Marekani , alionekana kutokuwa na shida nayo ndio maana nikaichukua ili kumpa mke wangu kama zawadi”Aliongea Roma.

Ni kweli saa hio ilikuwa ya thamani na Robert Mueller huenda ndio maana akawa anatembea nayo kile anapoenda.

Moja ya msemo wa kizungu katika ujaususi ni ule unaosema . The most Dangerous place is safety place, kwamba sehemu hatarishi Zaidi ni ile sehemu salama na sehemu salama Zaidi ni ile isionekana salama nadhanni ndio maana Robert akawa anatembea nayo mfukoni ili watu wasiweze kumdhania anatembea na kitu cha thamani kubwa kama hicho na ndio ilimpa nafasi Roma kuweza kuipata mara tu baada ya kuisachi kwenye mifuko yake.

Sasa Roma alikuwa ni mtaalamu sana kwenye kugundua vitu vyenye thamani kubwa hivyo mara baada ya kuiona tu aliweza kuifahamu mara moja na ndio maana akaichukua , ijapokuwa alikuwa na pete mfukoni lakini hata saa aliona vyote vinaweza kumfiti mke wake kama zawaidi , lakini tukio la Nasra lilimpa chaguzi ya kipi ampatie kama zawadi ndipo alipoamua kumpatia pete ya Almasi na akabakisha saa kwa ajili ya mke wake Edna , ijapokuwa hakupenda kumpatia Nasra mbele yake lakini alijiambia kwenye nafsi yake ili siku za mbeleni kupunguza migogoro ni bora kile anachowapatia wanawake wake wengine mke wake kuweza kuona , inaweza kuuma mwanzoni lakini ataweza kuzoea mbeleni na kuchukulia kama kawaida, Hata hivyo Roma alikuwa akimpenda Edna kuliko wanawake wote na ndio maana hakuwa na mpango wa kumfanya mwanamke wake yoyote yule kuwa na cheo cha mke.

Baada ya Edna kuipokea saa ile kwa mikono miwili awamu hii na kuirudisha kwenye begi kistaarabu tofauti na siku kadhaa nyuma kutupia tu kwenye mkoba wake alimwangalia Roma kwa wasiwasi.

“Edna is most precious to me in this world , So a priceless artifact like this is the perfect gift for my beloved wife”

“Edna ni wa thamani sana kwangu kwenye ulimwengu huu , hivyo kitu kama hichi cha zamani ambacho gharama yake haihesabiki ni zawadi nzuri kwa mke wangu nimpendaye”Aliongea Roma kwa sauti bila ya wasiwasi na kujiamini kwa hali ya juu, bila shaka alisema kwa sauti kwa ajili ya kila mmoja kusikia na kusanyiko lote lilishangazwa na kuguswa kwa wakati mmoja na maneno yake na kumfanya Hata Edna kuwa mdogo kama piritoni huku akiwa mwekundu kwa aibu iliochanganyika na utamu.

Mwanamke siku zote ni kiumbe anaependa kufanywa wa pekee hususani mbele ya marafiki zake, kuna muda unaweza kusema mwanamke huyu kwasababu ni kauzu sio mwenye kujali kuhusu mambo yasio na maana , lakini ukweli ni kwamba kila mwanamke anapenda kufanywa wa spesho , alichofanya Roma ni kumfanya Edna kuwa na deni la kihisia , ijapokuwa kwamba alijua saa ilikuwa ni ya thamani kubwa lakini alikaa Zaidi ya wiki pasipo kuitolea maelezo, Edna alielewa sasa Roma alimaanisha alivyosema siku ile alikuwa amenuia kumpa zawaidi hio yeye peke yake.

Cindy na Hanson sura zao ziliwashuka hawakuamini tambo zao zilimpa Roma uwanja wa kumpamba mke wake , ni kama wamepigwa kibao cha uso.

Saa yao ya Vacheron Constatin ya paundi milioni tatu haikufua dafu kwa saa ya kilijend kama Henry Graves.

Wale waru ambao walimuona Roma wakawaida sasa walianza kuhisi huenda mwanaume huyo sio wa kawaida ndani ya Tanzania na familia yake inaweza kuwa kubwa na hata kufanya kazi kwenye kampuni ya mke wake huenda kaamua tu kwa ajili ya kupoteza muda..

Umakini ulibadilika na wale ambao hawakumjali Edna mwanzo walimsogelea na kuomba angalau kuangalia saa hio na Edna alimwangalia Roma kwa ishara ya kuomba ruhusa lakini Roma wala hakujali Zaidi ya kuendelea na chakula chake na Edna ilibidi aitoe na awapatie waoshe oshe macho.

Mara palepale wote walimsifia Edna kwa kuweza kupata mwanaume kama Roma ambaye anauwezo wa kumzawaida kitu cha thamani kubwa kama hicho, hawakuwa wajinga walisema kama mtu kaweza kutoa saa ya thamani kubwa bila shaka asingekuwa vibaya mfukoni na ndio maana walitoa sifa zote.

Cindy ambaye siku zote alikuwa akitafuta ushindi alijikuta akipoteza pia , yeye ndio haswa aliemlazimisha Hanson kuja Tanzania kwa ajili ya kumuonyesha Edna tambo kwamba ameolewa kwenye famli aya ya kitajiri , ili kumkomesha kwa kumfanya kuwa katika kivuli chake wakati walipokuwepo chuo , lakini meza zikapinduliwa kibabe na akaendelea kuwa chini ya kivuli , hata ile mudi yote aliokuja nayo ilipotea ghafla.

Muda huo huo wakati wakiendelea kujadiliana mlango ulifunguliwa na bodigadi alievalia suti na walionekana mwanamke na mwanaume watu wazima wakiingia na Hanson ndio aliekuwa wa kwanza kuwasogelea.

“Naamini sijaharibu muda wenu mzuri , mke wangu kalazimisha tufike hapa angalau aweze kusalimiana na mtoto wa dada yake ambaye ni mjomba wangu pia”Aliongea kwa Kingereza na kumfanya Hanson kushangaa.

“Jamani huyu ndio mgeni ambaye nilikutana nae dakika kadhaa zilizopita , anafahamika kwa jina la Azizi Mohamedi ni Tajiri namba mbili Afrika, miezi michache iliopita kampuni yetu kutoka Barcelona iliweza kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni yake , kutokana na utajiri wake watu wengi hapa nchini Tanzania wanamchukulia kama moja ya watu wenye nguvu sana pamoja na familia yake”Aliongea Hanson bila ya kujali sentensi ya mwanzo ya Tajiri huyo kuhusu mke wake kutaka kusalimiana na mtoto wa dada yake.

Tajiri Azizi alikuwa ameambatana na mama yake mdogo Roma , mtoto wa Mzee Atanasi haikueleweka walijua vipi uwepo wake hapo ndani.

Watu wote baada ya kusikia hivyo walijikuta wakifurahishwa kukutana na moja ya Tajiri mkubwa wa Afrika , bwana Azizi.

“Mr Azizi umesema kuna ndugu yako kati yetu?”Aliuliza kwa mshangao kidogo na Tajiri Azizi alitabasamu mara baada ya kumuona Roma na Edna..

“Ndio Roma ni mjomba wangu na mama mdogo kwa mke wangu na ndio ambaye tumekuja kumsalimia kabla ya kuondoka, Mr Hanson nadhani swala lako lile la kibali ni vizuri sana ukijenga koneksheni na Mjomba wangu maana baba yake ndio raisi wa taifa hili kama mtoto wa kwanza, hajafahamika hadharani kwasababu aliungana na familia yake muda si mrefu kwa miaka mingi tokea alivyoondoka, familia yake ina nguvu kwenye mambo mengi ya kisiasa kuliko mimi mfanyabiashara”Aliongea bila ya wasiwasi na kushangaza watu wote na sio yeye tu hata Edna mwenyewe hakutegemea Tajiri Azizi angekweka uhusiano wa Roma na Raisi Senga wazi.

Baada ya kusema hivyo watu wote walijikuta wakishangaa na hata wale waliokuwa wakijiuliza maswali ya Roma ni nani haswa waliweza kutoa sintofahamu zao , walijiambia ndio maana alikuwa na uwezo wa kutoa saa ya thamani kiasi hicho kumbe alikuwa mtoto wa raisi, walijiambia ndio maana Edna akakubali kuolewa nae kumbe alijua alikuwa ni sehemu ya familia kubwa ndani ya Tanzania.

Roma mwenyewe licha ya kuona Azizi anaropoka sana hakujali kwanza alishaongea tayari na maneno yake hawezi kuyarudisha mdomoni mwake.

Jambo moja la uhakika ni kwamba Tajiri Azizi alifanya makusudi kabisa kuweka uhusiano wa Roma wazi , sasa haikueleweka ni kwa utashi wake au kuna mtu aliekuwa nyuma yake.

Baada ya madakika kadhaa ya kusalimiana na baadhi ya wageni hao Tajiri Azizi alitoa sababu isiokuwa na mashiko na kisha waliondoka na mke wake wakiwa kwenye sura za tabasamu na kazi yao ya kumpaisha Roma ilikuwa imeisha.

Edna sasa aliangaliwa kwa macho yasio kawaida na wadada wenzake waliokuwa hapo ndani , kila mmoja alijua ndio maana Edna alikubwali kuolewa , nani angejua mwanaume alieolewa nae kuwa mtoto wa Raisi.

“Edna inaonekana ulifanya chaguzi sahihi kuoelwa kwenye familia kubwa ndani ya Tanzania , Vipi lakini kuna sheria ngumu za kuwa mke wa mtoto wa raisi?”Aliuliza Lele.

“Hakuna sheria , ni kawaida tu hata hivyo wakati tunaona sikujua kama ni mtoto wa raisi”Aliongea Edna na kufanya watu wote wasiweze kuamini kauli yake.

“Babe wakati tunakutana kipindi kile nikiwa mbeba mizigo , haukuona kitu ambacho sio cha kawaida kuhusu mimi ukiachana na uhandsome wangu?”Aliongea Roma kwakingereza na kumfanya Edna kutamani kumchona machoni na uma.

“Endelea kula sitaki kusikia kuhusu maswala ya ubeba mizigo”Aliongea Edna kwa kiswahili.

Ni ndani ya lisaa lingine mbele hatimae waliagana , tukio hilo likuwa la aina yake kwa upande wa Edna na Roma , kwani waliweza kupewa heshina na kila mmoja.

Ijapokuwa Roma hakujali sana kuitwa mtoto wa raisi lakini alifurahi cheo cha jina lake kimemjengea heshima mke wake , Kwake kuitwa mtoto wa raisi wala halikuwa jambo kubwa sana maana hata hivyo yeye ni raisi kwenye nchi yake akitambulika kama mflame, hivyo hakuwa mtu ambaye angeweza kutembea mtaani na kuanza kujisifia , hata hivyo mwanaume anaefahamika kuwa baba yake hakuwahi hata kumchukulia kama mtoto wake.

Hakuna hata mmoja ambaye aliweza kuomba mawasiliano ya Roma lakini wengi wao waliamini kutokana na kufahamiana na Edna , basi ingekuwa rahisi kujenga koneksheni kwa wale ambao walikuwa wakitafuta fursa za ki uwekezaji ndani ya Tanzania.

Wakiwa ndani ya barabara ambayo haikuwa na magari mengi wakielekea nyumbani Edna alijikuta akitoa saa ile kwenye mkoba wake na kuanza kuikagua upya, aligeuza kulia na kushoto na kuchunguza vitendea kazi vilivyokuwa ndani ya saa hio na alijikuta hata yeye mwenyewe kushangaa , huenda siku ile angeinagalia kwa umakini angeigundua kwani ilikuwa na jina kwa ndani.

“Mke wangu bado unataka Pete ya Almasi?”Aliuliza Roma akiweka tabasamu.

“Usinitanie bwana , mimi sio mzoefu sana na mambo ya saa , hususani hizi za zamani maandishi yake yanaonekana kuwa madogo sana na kama usipo angalia kwa umakini huwezi kuona , kama ningefahamu ilikuwa ya thamani hivi nisingeiweka kihasara hasara kwenye mkoba wangu, nilifikiri ulinipa tu kama kunipoza na haikuwa na maana kubwa kama ilivyo kwa ile pete”

“Ile siku nilitaka kukuelezea , lakini hukunipa hata nafasi ya kunisikiliza Zaidi ya kujifungia”Aliongea Roma na kumfanya Edna ajihisi mwenye hatia.

“Yote ni makosa yako ungeniambia mwanzoni kabisa tokea kule Chalinze kama ulikuwa na zawaidi kwa ajili yangu , nilikasirika sana siku ile”Aliongea na Roma alitingisha kichwa huku akimwangalia Edna anavyoifuta futa na kitambaa chake.

“Kwasasa usijali sana thamani yake , ni ya kwako na unaweza kuifanyia maamuzi unayotaka , unaweza kuicha kwenye begi kama mwanzo na utakapotaka kuangalia muda unweza kuitoa na kuangalia muda , sio lazima uihifadhi kama vito vya thamani iichukulie kama saa ya kawaida”

“Siwezi kufanya hivyo , ni ya thamani kubwa na nikiiharibu hata ambaye ameitengeneza anaweza kunilaani huko aliko , siwezi kufanya hivyo”

“Hio ina maisha yake kivyake ikifikia muda wa kuharibika itaharibika vile vile haina haja ya kuitunza kama yai kwani ni saa iliotengenezwa kwa ajili ya kuonyesha muda”Aliongea Roma na Edna alionekana kuridhika.

“Hii ndio zawadi ulioniahidi siku ile?”Aliuliza Edna , alikuwa akikumbuka vyema Roma alishawahi kumuahidi kwamba atakuja kumpa zawaidi ambayo itamfurahisha , ni tabia ya mwanamke kutosahau ahadi ya kupewa zawaidi , ni bora mwanaume kama huna mpango wa kumpa mwanamke wako Zawadi usimuahidi bali umfanyie kama Surprise.

“Hii sio yenyewe , kama nilivyosema zawadi yangu utaipenda tu na nitahakikisha muda si mrefu unaipata”aliongea Roma na kumfanya Edna kufikiria ni zawaidi gani hio ambayo inaandaliwa muda mrefu.

“Unajua kwanini nilichagua kukupa saa na sio pete?”Aliuliza Roma

“Si kwasababau ni ya thamani Zaidi kuliko ile pete?”Aliuliza Edna na Roma aliabasamu

“Hapana , Wakati naichagua hio saa sijawaza kuhusu pesa , kwasababu wewe ni tairi tayari”

“Kama sio uthamani wake nini kingine?”Aliuliza Edna kwa shauku kubwa na Roma alitabasamu na kisha aliendesha kwa mkono mmoja wa kulia huku akitumia wa kushoto kumshika Edna mkono ule ulioshikilia saa.

“Hii saa ina miaka tisini tokea kutegenezwa kwake lakini mpaka sasa bado infafanya kazi na kuonyesha majira , imepita kwenye mikono ya watu huenda ilidondoka na kuokotwa na watu wengine lakini tofauti na kuchubuka juu tu n akua na kutu bado inaendelea kufanya kazi na itaendelea kufanya kazi pasipo kuacha mpaka siku itakapoharibika na kufa moja kwa moja , ufanyaji kazi wa saa hii licha ya kupitia changamoto ndio itakavyokuwa kwa moyo wangu kwako, ilimradi nitaendelea kuishi basi moyo wangu utaendelea kudunda kwa ajili yako, uthamani wake haupo kwenye pesa bali kwenye maana ya Maisha yangu kwako”Aliongea Roma huku akiwa siriasi lakini sauti yake ilisikika vizuri mno na ya kuvutia.

Edna alijikuta akikaa kimya asielewe hata hisia zake na alijikuta akisikilizia namna saa hivyo inavyotembea na mpaka anakuja kushituka kwenye mshangao wake alijikuta macho yake yashafunikwa na machozi.

“Naona umeguswa na maneno yangu , inaweza kuwa nimeongea tu ujinga kwa ajili ya kukupendezesha?”Aliongea Roma akimwangalia Edna

“Unajua mwenyewe sijawahi jihusiha na maswala ya mapenzi tokea nilivyozaliwa , usinielezee maneno yanayonifanya nitoe machozi , nikishindwa kulala usiku je?’Aliongea Edna na kumfanya Roma kucheka sana.

“Kwanini ushindwe kulala , ukitoa machozi ndio unasafisha macho?”

“Kwahio unamaanisha macho yangu ni machafu?”

“Hahaha… sijamaanisha hivyo , unajua watu wanasema kadri unavyotoa machozi ndio macho yanajisafisha ila, kwa wewe babe wangu macho yako ni masafi hata usipotoa machozi na yanang’aa kama kioo , hebu jiangalie kwenye kioo uone yalivyo”Aliongea Roma na kumfanya Edna kujisikia vizuri kweli.

“Unataka kujua historia yangu na Hanson?”Aliuliza Edna.

“Kama inahuzunisha usiniambie?”

“Haihuzunishi na inanifanya kucheka muda mwingine nikikumbuka”Aliongea Edna na kumfanya Roma kutingisha kihcwa amwambie.

Na Edna kwa mara ya kwanza alifunguka namna ambavyo chuoni alikuwa akihusishwa na Hanson kutoka nae kimapenzi , anasema wakati anaanza kozi ya Masters ndio kipindi ambacho Hanson alihamia kwenye chuo chao akitokea Cambridge kwa ajili ya kusomea masomo ya uongozi wa biashara , kutokana na umaarufu wake kipindi hicho na pia kuvutiwa nae ndio aliposikia tu watu wakivumisha kwamba anatoka nae kimapenzi.

Kipindi hicho rafiki yake mkubwa ni Sasha na aliweza kuwa na ukaribu na Hanson kwasababu alikuwa rafiki yake Richie ,, Edna anasema kati ya wanawake ambao walitokea kumpenda sana Hanson ni Cindy lakini kutokana na Hanson kuvutiwa na Edna hakujigangaisha kabisana Cindy ndio maana chuki ya Cindy juu yake ikaibuka.

“Hata hivyo sikuwahi sana kujihusisha na mapenzi , ijapokuwa kuna muda nilionekana kuwa na ukaribu na Hanson lakini ulikuwa ni wa kirafiki pekee na yote ni kutokana na ukaribu wake na Richie pamoja na Sasha, baada ya kuwa na ukaribu kidogo wa muda mrefu alikuja kunifuata siku moja mara baada ya kupata taarifa ya kuhuzunisha kutoka nyumbani kwao Norway na alisema hawezi kuondoka pasipo kuniambia kile anachojisikia na hapo ndipo aliposema kwamba ananipenda sana na alitamani anioe”

“Wow!, Inaonekana sio mbaya sana huko chuoni ulikuwa kidogo haupo siriasi kama ulivyosasa?”Aliongea Roma na Edna alitabasamu na kuendelea.

“Kiasi chake alivyoniambia hivyo nilimkataa na kumwambia sina mapenzi nae jibu ambalo lilimuumiza na aliondoka siku hio hio kurudi kwao na baada ya siku anarudi chuo nilisharudi nyumbani mara baada ya kupokea taarifa ya kuugua kwa ghafla kwa mama yangu na sikurudi tena chuo na hata Master yangu sikuhitimu”Aliongea Edna

“Wakati nilivyoona hutaki hata kunitambulisha kwao nikaona wivu , nikasema huenda mke wangu alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine , inaonekana sio kweli”

“Sio kweli sikuwahi kabisa kuwa na mahusiano nae na nilimsahau kabisa hata nilivyorudi na sikujihusisha kabisa na mwanaume yoyote chuoni hata nilivyorudi”Aliongea Edna kwa kujitetea akisahau kwamba Roma alimtoa bikra.

Baada ya kuongea hatimae muda mchache tu waliweza kuingia ndani ya barabara ya H?aile Selassie.

“Unaweza kuendesha ukiwa umefumba macho?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kushangaa

“Nini?”

“Unaweza kugongana na gari kama umefumba macho yako?”Roma alishangaa lakini aliliishia kujibu.

“Ninaweza kutuisha ndege na kuipaisha macho yangu kwa hisia tu”Aliongea Roma.

“Basi fumba..”Aliongea Edna na Roma hakutaka kuleta ubishi alifanya kama alivyoambiwa na kisha akayafumba huku akiendelea kuendesha gari kwa hisia za kichawi.

Muda ule ule alihisi harufu nzuri ikizidi kujaa kwenye pua zake huku Edna akiwa amemshika bega lake la kushoto , ni lipsi laini za midomo ndio alizohisi kugusa lipsi za midomo yake na sasa kuelewa jaribio analotaka kufanya Edna na hakutaka kuchelewa alitumia mkono mmoja kuendesha gari kwa hisia na kisha mwingine akashika kiuno cha mke wake na kumvutia kwake huku ndimi zao zikipigana kwenye vinjwa vyao

Waliendelea kupigana French Kiss mpaka wanakuja kuachiana zilipita dakika Zaidi ya ishirini na Edna alikuja kushangaa gari likiwa limesimama nje ya geti la nyumbani kwao, kwenye Maisha yake huenda hilo ndio kiss la muda mrefu sana.

“Tumeshafika nyumbani sasa?”Aliongea Roma na Edna aliona aibu za kike huku akikaa vizuri.

“Nilikuwa nikikupa zawadi ya muda mfupi tu , kwanini ukafanya ikawa ya muda mrefu?”

“Ninaweza kusemaje mimi kwa utamu niliojisikia , hata hivyo hizi ni rasha rasha tu , kama tulivyokubaliana tutaendelea Zaidi mara baada ya kufunga ndoa kwa mara nyingine , unaweza kusema hiki ni kionjo cha mboga tu inayochemka”Aliongea Roma.

“Tunafunga ndoa lini?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kutabasamu.

“Una wasiwasi?”

“Yeah kidogo?”

“Wow! Umeanza lini kuwa muwazi mke wangu”

“Ninaona wasiwasi tunaweza kugombana tena na nikaanzisha vita baridi na wewe, hata hivyo tumeoana muda mrefu sina haja ya kukuonea aibu tena”Aliongea na Roma alifikiria kidogo.

“Ni kawaida sana kwa wapenzi na wanandoa kutofautiana baadhi ya nyakati , lakini haimaanishi kwamba upendo wao ndio unakuwa mwisho , Tufunge ndoa yetu ndani ya miezi minne ijayo na siku hio ndio nitakupatia zawaidi ambayo inaipanga kichwani kwangu”Aliongea Roma

Baada ya kuongea kwa muda wakiwa nje wakipanga mipango yao ya ndoa hatimae waliweza kuingiza gari ndani ya geti na kushuka wote kwa pamoja , mwanga wa taa za ndani ulionekana kwa nje ikionyesha bado wanafamilia wengine hawajaenda kulala bado.

Blandina na Bi Wema walikuwa macho kasoro Sophia , Qiang Xi na Lanlan , walijikuta wakiangaliana na kutabasamu mara baada ya kuona namna ambavyo Edna alionyesha kutabasamu kwa furaha na kwa utu uzima wao walijua tu lazima kuna jambbo limetokea na kuwafanya wawili hao kupatana.

Bi Wema na Blandina hawakutaka kumruhusu Edna kuondoka bila ya kusema kilichotokea na Roma aliishia kutabasamu na kisha akapandisha chumbani kwake.

Baada ya dakika kadhaa za Blandina kumtania Edna pamoja na kumdadisi hatimae walimruhusu Kwenda kulala kwani kesho ilikuwa siku ya kazi.

Edna baada ya kuufikia mlango wa chumbani kwake alishikwa mkono na Roma na kisha akaambiwa amfuate na Edna alishangaa lakini aliishia kumfuata Roma na walipandisha juu kabisa ya nyumba hio kwenye paa sehemu maalumu iliotengwa kwa kupumzika.

“Edna kuna kitu ambacho napaswa kukuambia ili uweze kufanya maamuzi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa.

“Ni kitu gani?”

“Kutokana na mwili wangu ulivyo na nguvu za ziada nilizokuwa nazo siwezi kumpa mwanamke wa kawaida ujauzito”Aliongea Roma huku akishika nguzo huku wakipulizwa na upepo mkali unaotoka baharini.

Kauli ya Roma kumwambia kwamba hawezi kumpa mwanamke ujauzito ilimshangaza mno.

*************

Upande mwingine baada ya nusu saa tu kwa Roma kuondoka ndani ya hotei ya Hyatt Kilimanjaro, ilisimama gari aina ya Taksi na kumshusha mwanadada mmoja mrembo sana alievalia suruali na blazia nyeiupe pamoja na miwani ndogo ya macho.

Alikuwa ni mwadada mwenye rangi za kuchanganya , yaani rangi ya kiafrika pamoja na rangi ya kizungu , mathalani kwa kumwangalia macho yake tu na nywele zake utaweza kutambua aidha baba yake au mama yake anaweza kuwa Mchina.

Mwadada huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mrembo Rufi mwanadada ambaye aliweza kukutana na Roma ndani ya jiji la Loss Angeles.

Baada ya kushushwa na taksi hio moja kwa moja aliweza kuingia ndani ya hoteli hio ya kimataifa na kufuata taratibu zote za kupata chumba.

…………

Ni asubuhi ya siku hio Rufi mara baada ya kutoka usingizini na kujisafisha aliingia mtandaoni kwa kutumia simu yake janja na kuanza kutafuta Habari zinazovuma ndani ya Tanzania katika mtandao wa Twitter na ndani ya madakika kadhaa tu ya kupekue pekua alijikuta akitoa tabasamu la ushindi mara baada ya kuona Habari ambayo ni kama hakuitegemea.

“Jina lako ni Roma Ramoni , mtoto wa Raisi wa taifa hili , What twisted Fate kazi yangu ya kukufuatilia imekuwa nyepesi kuliko nilivyodhani”Aliongea kwa tabasamu na kisha alijirusha kitandani kwa furaha.
 
SEHEMU YA 415.

Roma ilibidi ampe Edna kwanza maelezo kwa ufupi kuhusu nguvu anazotumia , hakuziita kwa jina la mbinu za kijini bali yeye aliziita mwenyewe mbinu za Heaven and Earth’ , yaani mbinu za kuvuna nishati kati ya mbingu na Ardhi.

Edna hakushangaa sana kwani mwenyewe alikuwa na mengi ambayo hakuwa akiyajua kuhusu Roma , lakini jambo moja ambalo lilimfanya kushangaa ni swala la Roma kusema kwamba pasipo ya mwanamke kuwa angalau na nguvu hizo hatoweza kubeba mimba yake.

Roma hakumficha Edna juu ya kumwambia Rose na Dorisi na katika maelezo yote sehemu iliomgusa Edna kwa kumuogopesha na kushangaa kwa wakati mmoja ni pale Roma aliposema kwamba kama tu yeye ataweza kujifunza mbinu hizo na kufikia levo za juu anaweza kuishi muda mrefu pasipo kuzeeka.

“Niliamua kumuelezea Rose kwanza kwasababu mwili wake umejengeka kimazoezi , mbinu hizi sio rahisi na hata kama niseme naweza kukuingizia kiasi kwenye mwili wako utashindwa kuhimili”Aliongea Roma na kumfanya Edna kufikiria.

“Kwahio unataka nifanye nini??”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuvuta pumzi mpaka hapo aliona Edna alishaleewa anachojaribu kumuelezea.

“Kwasasa siwezi kusema kuna njia ya moja kwa moja juu ya kujifunza, ijapokuwa hata mimi nimefunzwa lakini njia yangu mimi ni ndefu sana na itachukua miaka mingi mpaka kuipatia , hivyo nafikiria kutafuta maarifa yanayohusiana na mbinu fupi ambayo mtaweza kujifunza na kupanda levo kwa haraka”Aliongea Roma kwa nafsi ya pili wingi akijumuisha wanawake wake.

Roma alimweleza Edna kwanini alichagua kujifunza mbinu za kijini na alimwambia sababu kubwa ni kushindana na sayansi iliowekwa ndani ya mwili wake , yote hayo ikiwa ni kumfanya kuwa na uwezo mkubwa pasipo kutumia sayansi iliowekwa kwenye mwili wake na hatimae kumfanya kuwa binadamu wa kawaida.

Edna alitulia kwa madakika kadhaa akiwa ni mwenye kufikiria kidogo na Roma alimwacha kwa takribani dakika tano zote akiwa pembeni yake.

Edna na yeye aliwaza kama kweli anakwenda kuanza Maisha ya ndoa na Roma basi atafikia hatua ya kuhitaji watoto lakini wakati huo huo hawezi yeye kuzeeka halafu mume wake akawa hazeeki haraka.

“Nifanye nini ili niweze kujifuza?”Aliuliza Edna akimwangalia Roma usoni na Roma mwenyewe alishangazwa na swali hilo kwani hakutarajia Edna kumuelewa kirahisi namna hio.

“Kwasababu sijapata mbinu rahisi ya kurahisisha mafunzo yote , unachotakiwa kufanya nimaandalizi ya mwili wako mpaka wakati nitakapopata mbinu rahisi ya kueleweka”

“Maandalizi ya aina gani ambayo napaswa kufanya?”

“Unapaswa kuchukua mazoezi kila siku asubuhi , ili kuweka viungo vyako imara”

“Mafunzo haya hayataingiliana na ratiba zangu za ofisini ?, kwani unafahamu kampuni kwanugu ndio kila kitu na ni Zaidi ya familia laki moja zinategemea niwalipe mshahara , hivyo nitahitajika muda wote kuwa kazini ili kuhakikisha kampuni inaendelea bila kupatwa na tatizo”Aliongea.

“Huna haja ya kuwazia sana kuhusu mbinu hii kwani haiwezi kabisa kuingilia mambo yako ya kazi, na mafunzo ni ya muda mchache sana kwa siku na unaweza kuyafanya mahali popote , hata hivyo kwasasa siwezi kuongea sana kwani sijapata mbinu za kuyafanya yawe marahisi”Aliongea Roma na Edna alionekana kuelewa kwa kiasi chake, hata hivyo Edna alijiambia hawezi kuwaacha michepuko kujifunza mbinu hizo peke yao , itamaanisha yeye ndio atazeeka na wanawake wengine wa Roma hawatozeeka.



********

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa , muda wa asubuhi wakati Raisi Senga Kweka alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya Kwenda ofisini , mara simu yake iliokuwa pembeni kwenye Dressing table ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Kabwe , moja ya wasaidizi wake ambao anawaamini sana.

“Kabwe kuna nini?”

“Mheshimiwa kuna habari inasambaa mtandaoni”Aliongea Kabwe upande wa pili na kumfanya Raisi Senga kushangaa.

“Habari gani na inahusiana nini na Ikulu?”

“Inakuhusu wewe mheshimiwa..”Aliongea Kabwe na Raisi Jeremy hakutaka maelezo mengi wakati simu ipo ambayo inaweza kuangalia mtandaoni , haraka haraka alifungua moja ya mtandao maarufu na kuangalia kile ambacho kinasambaa, alijikuta akipandwa na Jaziba mara baada ya kuona taarifa hio.

“F**ck!”Alitoa tusi huku akihema kwa nguvu na kurudisha simu yake kwenye meza huku akijiangalia kwenye kioo kwa macho yaliojaa hasira , lakini wakati huo huo mlango wa chumba hicho cha kupumzikia ulifunguliwa na mke wake Damasi au Mama Ashley.

“Mume wangu , mbona uko hivyo?”Aliuliza Damasi kwa wasiwasi mara baada ya kuona mabadiliko ya mume wake kwa kupitia kioo , lakini Senga hakuongea lolote Zaidi ya kumpa ishara aangalie kwenye simu.

Damasi mara baada ya kuchukua simu na kuangalia kile kilichokuwemo alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha kwa wakati mmoja.

“Mme wangu huna haja ya kuwa hivi , nilitarajia hili kutokea na nimekuwa nikikusihi utafute namna ya kulitatua”Aliongea Damasi kwa upole.

“Upo sahihi Mama Ashley , lakini unaamini hili ni sawa? , Kwannii yule mzee siku zote hapendi kunishirikisha kwenye baadhi ya mambo muhimu yanayonihusu na kuchukua maamuzi ambayo yana athari kwa uongozi wangu?”Aliongea huku akipunguza mkabo wa tai.

Taarifa ambayo ilikuwa ikisambaa mtandaoni ilikuwa inayohusiana na uhusiano uliokuwepo kati ya Roma na Raisi Senga , taarifa ilikuwa ikielezea uwepo wa Roma kama mtoto wa kwanza wa Raisi Senga ambaye alimpata na mke wake wa kwanza, taarifa hio ilionekana kutokuwa uzushi na kumkasirisha Raisi Senga kutokana na kwamba alieithibitisha ni Afande Camillius Kweka mwenyewe.

Kwa maana rahisi ni kwamba ni taarifa iliosambazwa mtandaoni s na Afande Kweka mwenyewe akijaribu kumtambua hadharani Roma kama mjukuu wake , hivyo hata kama Raisi Senga atake kuibatilisha hakukua na uwezekano huo na isitoshe Raisi Camilius Kweka ni mwanajeshi mstaafu ambaye alikuwa akiaminika kwenye maswala mengi ya kitaifa.

Damasi mke wa Raisi Senga mwenyewe alishatarajia hilo kutokea na ndio maana siku zote alitamani mume wake kumkubali Roma kama sehemu ya mtoto wake na kumjumuisha katika familia , lakini Senga alionekana kuwa mgumu katika hilo.

“Utafanya nini mume wangu , unapaswa kumtambua Roma kama mtoto wako”

“Damasi mke wangu unasikia unachokiongea, nikishamtambua Roma kama sehemu ya familia yangu ni kwamba nampa ushindi baba wa kumfanya Roma kuwa mrithi wa familia , jambo ambalo sitaki litokee , jambo ambalo hata wewe unajua litaibua migogoro kati ya Denisi na Roma”Aliongea na kumfanyaDamasi kurudi nyuma na kukaa kwenye kitanda.

“Kama hutaki kumtambbua Roma kama mwanao , unanjia ipi nyingine? , Senga mume wangu najua kinachokuumiza ni usaliti aliokufanyia Blandina na hili linaniumiza pia sana , linanifanya nione bado unampenda kuliko mimi mkeo”Aliongea na kumfanya Senga kugeuka.

“Sio kweli Mama Ashley simpendi kabisa yule mwanamke”

“Kama humpendi kwanini unamkataa Roma kama mtoto wako wakati kosa lilikuwa upande wa Mama yake , Unachokifanya ni kumkomoa Blandina kwa kutokumkubali Roma kwasababu unampenda bado na unatamani unachojisikia na yeye apate kuhisi hivyo , Senga niambie kama bado unampenda?”Aliongea huku utulivu wake ukianza kupotea na maneno yake yalionekana kuwa ya kweli ndani yake na kumfanya hata Raisi Senga mwenyewe ajiulize ni sababu ipi ambayo ilikuwa ikimfanya kutokumtambua Roma kama mtoto wake na jibu lilikuwa moja tu kwamba alikuwa akimkasirikia Blandina kwa usaliti wake ndio maana anajaribu kumkomesha kwa kutomtambua mwanae.

“Senga najua ni mengi tulipitia pamoja , najua nilipokutoa Senga , lakini swala la Roma na Blandina sitaki livuruge kile tulichokijenga pamoja , wewe ni Raisi wa nchi hii hebu fikiria siku ikatoka taarifa kwamba umeikataa damu yako , utakuwa unaonyesha mfano wa namna gani kwa jamii kama kiongozi wa juu, serikali yako ipo kidedea kwenye kuhamasisha wanaume kutimiza wajibu wao pasipo kukimbia majukumu , pasipo ya kutelekeza watoto wao , je wewe una utofauti gani na hao walioko mtaani , wanaume ambao wanatelekeza familia zao?, Mume wangu sio kwamba nakufananisha lakini najaribu kukushauri kwamba unapaswa kuwajibika kwa kila kinchotokea kwenye maisha yako kwani ni sehemu ya matokeo ya chaguzi ulikwisha kufanya”Aliongea Damasi na kumfanya Raisi Senga kufikiria kidogo.

“Mke wangu kwahio unanishauri nimpokee Roma kama mtoto wangu?”

“Senga najua ni mapema mno kwako kukubali kila kitu kuwa sawa na kuendelea kuishi kama hakuna kilichotokea , najua ni wakati gani unapitia kuamini kwamba siku zote ulidanganywa , silazimishi moyo wako kumkubali Roma kwani hilo ni swala ambalo lipo nje ya uwezo wangu bali ninachofanya hapa ni kujaribu kulinda taswira yako , una maadui wengi katika siasa na kama utawapa udhaifu wa kukutawala basi hutofikia hata nusu ya malengo uliojiwekea, Ninachotaka wewe ufanye sasa hivi ni kufanya maamuzi ya kisiasa , mambo mengine tuyape muda”Aliongea na Raisi Senga alionekana kufikiria.

“Nitafikiria na nitajua nini cha kufanya , hata hivyo nashukuru kwa ushauri wako huu mzuri Mama Ashley”Aliongea na kumfanya Mama Ashley kumkumbatia kwa kumpiga piga mgongoni.

*****

Upande wa Roma hata yeye aliamshwa na habari hio hio ya yeye kutangazwa kuwa mtoto wa Raisi Senga Kweka , ijapokuwa jambo hilo mwanzoni hakuwahi kulichukulia siriasi lakini ni jambo kubwa mno kwake kutokana na kugusa mpaka watu ambao wanamzunguka.hata hivyo habari za familia yake hakuziweka wazi hata kwa wanawake wake, ni Edna pekee ndie aliekuwa akijua kuwa baba yake ni Raisi Senga.

Moja ya watu ambao waliweza kuona habari hio pia ni Blandina na alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha baada ya kuona mtu alieweka taarifa hio ni babu yake Roma yaani Afande Kweka , kwa haraka haraka aliamini huenda mzee huyo alikuwa akijaribu kumfanya Senga kumkubali Roma kama mwanae.

Roma wala hakujihangaisha kabisa na habari hio na alionekana ni kama haikuwa ikimuhusu, akiwa chumbani kwake alionekana akipiga simu kwa kutumia simu yake ndogo huku namba alizokuwa akitumia zikionekana kutokuwa za kawaida kabisa.

“You Majest Pluto!!!”Ilisikika sauti upande wa pili kwa mshangao.

“Ron habari za siku nyingi”Aliongea Roma huku akikaa kwenye kitanda.

“Mfalme Pluto siamini hatimae umeweza kunipigia, habari zako nilikuwa nikizisikia juu juu kutoka kwa Sauron na sikuamini hata niliposikia umeoa”Iliongea sauti upande wa pili kwa lugha ya kingereza na kumfanya Roma kutabasamu.

“Nisamehe Rona kwa kutokutafuta mapema, alichokuambia Sauroni ni kweli , sasa hivi nina familia”Aliongea.

“Mfalme Pluto huna haja ya kuniomba msamaha najua ulikuwa na sababu za msingi kufanya hivyo ni jambo la kushangaza na kufurahisha sana , natamani siku moja kuiona familia yako ikiwa huku kisiwani kwenye nyumba yako , imepooza sana”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

“Kuhuhusu hilo , ndio sababu ilionifanya nikakupigia , ninapanga kumleta mke wangu huko kwa ajili ya kufunga ndoa ,ijapokuwa nilioa lakini hakuna sherehe ambayo imefanyika”

“Mfalme Pluto nimefurahi kusikia hivyo, nipo tayari kusikiliza maagizo yako na kufanya maandalizi makubwa”Aliongea mwanaume anaeitwa Ron na Roma alianza kumuekeza kila kitu ambacho anatakiwa kufanya kwa sauti ndogo ikiwa kama siri.

“Kuhusu swala la Zawadi ninayopanga kwa ajili ya mke wangu nitamshirikisha Sauron pia kulifanyia hilo kazi”Aliongea Roma.

“Mfalme Pluto nitahakikisha maagizo yako yote yanafanyiwa kazi kwa wakati kabla ya siku ya tukio, raia wako watakuwa ni wenye furaha sana kumuona Malkia Perseephone”

“Asante sana Ron , wasalimie wote hapo kisiwani na nikutakie jioni njema”

“Asante sana Mtukufu Mfalme Pluto , na mimi nakutakia Asubuhi njema”Aliongea Ron na kisha akakata simu.

Roma mara baada ya kumaliza mlango wake ulifunguliwa na Edna alieonekana kujiandaa kabisa kwa ajili ya Kwenda kazini na Roma mara baada ya kumuona alimsogelea na kumkumbatia na Edna hakuleta ubishi, alikubali kukumbatia na mume wake huyo , hata hivyo alishaamua kumkubali kabisa hata kuolewa nae, Roma alishindwa kulala pamoja na Edna kutokana na usumbufu wa Lanlan kutaka kulala na mama yake hivyo Roma kwake haikumsumbua kulala mwenyewe na alijiambia siku ya ndoa yake ikifika Lanlan atalala kwenye chumba chake.

“Babe mbona unaniangalia hivyo?”Aliongea Roma mara baada ya Edna kuonekana kumwangalia Roma usoni kama mtu anaetafuta chunuzsi.

“Nimeona Habari ya Afande Kweka kukutangaza rasmi kama mjukuu wake kutoka kwa mtoto wake Raisi Senga”Aliongea Edna.

“Ndio kinachokupa wasiwasi?”

“Najaribu kusoma mawazo yako kwa kukuangalia usoni”Aliongea Edna kwa sauti ndogo na kumfanya Roma kutabasamu.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi lilikuwa swala la muda tu kutambulika hivyo nishakuwa mwanafamilia tayari”Aliongea Roma na Edna alivuta pumzi nyingi huku akionyesha huzuni kwenye macho yake jambo ambalo lilimfanya Roma kushangaa.

“Mbona umekua mnyonge ghafla?”

“Licha ya Raisi Senga kutokukutambua lakini kuna watu kama Afande Kweka wapo nyuma yako , wakiwa na hiari ya kukutangaza hadharani..”Aliongea Edna.

“Edna kuna jambo ambalo limetokea kati yako na raisi Jeremy?”Aliongea Roma huku akimshika Edna na kumkalisha kitandani.

Roma siku ya pili yake mara baada ya kurudi kutoka Marekani aliweza kupata taarifa juu ya kifo cha Kizwe, jambo ambalo hata halikumshangaza sana wala kujihangaisha nalo.

Kitendo cha Edna kuonyesha huzuni aliona kabisa ni juu ya swala la baba yake , kwani tokea siku agundue kuhusu Raisi Jeremy kuwa baba yake hakupata nafasi hata ya kuongea nae.

“Unakumbuka nilishawahi kukuelezea kuhusu mtu aliewahi kujitambulisha kwa jina la The Protector?”

“Ndio nakumbuka”

“Nilijaribu kutuma ujumbe wa meseji nikiwa na uhakika atakuwa raisi Jeremy , lakini nimesubiria majibu ni zaidi ya wiki mbili sasa”Aliongea Edna kinyongea na Roma alimwonea huruma , alishatambua kwamba Raisi Jeremy hana mpango wa kumtambua Edna kama mtoto wake.

“Edna niambie unataka kuongea na Raisi Jeremy ana kwa ana?”Aliuliza Roma na Edna alishindwa kutoa majibu lakini sura yake ilionyesha alikuwa na uhitaji huo , hata hivyo Roma alikuwa ashamsoma Edna muda mrefu tu , ni mtu ambaye si rahisi kupotezea mtu anaefamika kwa jina la ndugu yake, mfano halisi aliweza kupata juu ya hilo ni siku ambayo alitaka kumuua Ernest Komwe.

Hata hivo Roma aliona ni sahihi kutaka kumtambua baba yake , kwani Edna ni kama hakuwa na ndugu yoyote wa damu , ukiachana na wale wa upande wa mama ambao wapo nchini Marekani, mtu pekee ambaye Edna alikuwa amezoeana nae na kumuita kama ndugu ni Bi Wema , lakini licha ya hivyo uzito wa baba ulikuwa mkubwa mno.

Roma alijiambia hawezi kumsemea Raisi Jeremy kwa kumwambia Edna kwamba hakuwa na mpango wa kumtambua , aliona jambo la maana ni Raisi Jeremy mwenyewe kuongea na Edna na kama ataamua kumkataa awe mbele yake.

Roma alimuahidi Edna kuhakikisha anakutana na baba yake hata kama itakuwa ni kwenda nchini Rwanda.

Baada ya wote kwa pamoja kupata kifungua kinywa , Edna aliondoka kuelekea kazini na hivyo hivyo Roma aliweza kuondoka kuelekea kazini akiwa na Sophia ambaye alitakiwa kufika makao makuu kwa ajili ya kutengeneza shooting ya matangazo.

Roma aliweza kuingia kwenye jengo hilo la kampuni na kupokelewa na Daudi , Wendy pamoja na Amina ambaye ni kama alikuwa akifanya kazi zote za Roma., baada ya kufanya kikao cha muda mfupi katika ukumbi wa mikutano aliingia ndani ya ofisi yake akiwa ametangulizana na Amina.

Amina licha ya kufanya kazi kama Sekretari , alikuwa akifanya kazi pia kama mtangazaji ndani ya kituo cha Vexto Tv .

Kampuni ya Vexto Media ilikuwa imechangamka mno kutokana na uwepo wa wafanyakazi wengi.

“Babe Amina kuna kitu muhimu nataka tuzungumze”Aliongea Roma na kumfanya Amina kumwangalia Roma usoni kwa mshangao kidogo.

“Nipo tayari kukusikiliza mfalme wangu , huna haja ya kuweka uso wako namna hio”Aliongea Amina huku akitembea kimadaha na kwenda kukaa kwenye masofa kwa kukunja nne na kufanya mapaja yake yalionona kwenye suruali kuonekana vyema na kumfanya Roma aliesimama kuangalia mtikisiko na kutabasamu kifedhuli.

“Babe utajisikiaje kama nitakuambia kuna uwezekano wa kuendelea kuwa mzuti hivi hivi pasipo kuzeeka haraka?”Aliongea Roma na kumfanya Amina kushangaa kidogo.

“Ingekuwepo hio teknolojia ningefanya kila linalowezekana kuwa wa kwanza”Aliongea Amina pasipo ya kuchukulia maneno ya Roma Siriasi alijua alikuwa akitania tu.

Nasra na Amina ni wanawake pekee ambao hakuwahi kuwaonyesha upande wake wa pili m ijapokuwa Amina aliweza kugundua Roma hakuwa mtu wa kawaida kutokana na namna alivomuokoa na Fayezi nchini Japani, aliamini huenda Roma alikuwa tu na pesa pamoja na konekesheni.

Amina alikuwa tofauti na Rose ambaye ashawahi kuyashuhudia kabisa mabadiliko ya mwili ya Roma , alikuwa tofauti na Dorisi kwani alishawahi kumona Roma akibadilika nchini Japani , alikuwa tofauti na Edna kwani alishawahi kumuona Roma akibadilika macho na kuwa wa kurisha, alikuwa tofauti na Neema Luwazo kwani Neema alishawahi kushuhudia Roma akipigwa risasi na ikapona hapo hapo kwenye kusanyiko la wafanyabiashara, hivyo hivyo kwa Mage aliweza kumjua Roma kama mtu asiekuwa wa kawaida.

Hata hivyo Nasra pia aliamini Roma hakuwa wa kawaida aliamini alikuwa na historia ya maisha yake ya nyuma ambayo inaweza isiokuwa ya kawaida lakini kama ilivyokuwa kwa wengine wote Nasra na Amina wote walijiambia watampenda Roma hata abadilike na kuwa mdudu.

Kwahio kwa maneno marahisi huenda kati ya wanawake wote ambae hajaweza kushuhudia makubwa ni Nasra peke yake.

Roma hakutaka kuongea sana , bali alichokifanya ni kumuonyesha Amina kwa vitendo juu ya uwezo wake na zoezi rahisi ambalo alifanya ni kugandisha hawani mafaili yote yaliokuwa kwenye meza yake na kumfanya Amina kushangaa.

“Babe hii mbinu…”Kabla hajamaliza sentensi yake palepale simu yake ilianza kuita na alinyanyuka na kuichukua kwenye meza na alipoangalia jina la anaepiga ni Neema Luwazo alijikuta akiguna na kujiuliza kwanini mwanamke huyo akampigia muda huo , lakini hakujali sana alichokifanya ni kupokea na kuweka sikioni.

“Roma nahitaji msaada wako…”Sauti upande wa pili ilisikika ikiwa kwenye hali ya wasiwasi.

“Nipo tayari kukusaidia mrembo , kuna tatizo gani?”

“Unaweza kuja Maple Speed Vibe”Sauti ya Neema luwaza iliskika upande wa pili na kumfanya Roma kushindwa kuelewa maana ya Maple Speed Vibe , lakini ni kama Neema alijua Roma atashindwa kumuelewa hivyo alipatia maelezo mafupi na kumwambia kwamba aende Kisemvule.

“Babaa naona unaitwa kwingine , haya wahi uje kunielezea mazingaombwe ulioyafanya hapa”Aliongea Amina na kumfanya Roma kumkonyeza.

“Tutaongea baadae” Aliongea Roma na kisha alitoweka kwenye ofisi hio huku akimwacha Amina akivuta mdomo.

Dakika arobaini na tano tu alikuwa ndani ya Kisemvule na alipewa maagizo ya kuendelea mbele kuipita stendi ya daladala na ataona bango kubwa la Maple Speed na Roma aliendesha kama nusu kilomita tu hivi aliweza kuona bango hilo ambalo lilikuwa na mshale uliokuwa ukimwelekeza kuingiza gari kushoto mwa barabara.

Roma bila hata ya kufika eneo husika alishajua Maple Speed ni lazima itakuwa sehemu ya uwanja wa mbio za magari maarufu kama Formula one Racing, hata yeye mwenyewe alishangazwa na uwepo wa hili eneo kwani alidhania ndani ya jiji hili mashindano ya mbio za magari hayakupewa kipaumbele sana kama nchi zilizoendelea mfano wa Abu Dhabi na Marekani.

Dakika chache mbele alifika kwenye kizuizi na kuruhusiwa kupita na kuingia eneo ambalo lilikuwa na mandhari nzuri mno kwa jinsi ilivyopendezeshwa na bustani, huku mbele yake akiona jengo kubwa la gorofa kama tatu hivi refu kwenda mbele.

Baada ya kufika mbele kabisa ya jengo hilo aliweza kumuona Neema aliekuwa amesimama akiwa amevalia gauni flani la rangi nyeupe ya mua maua na viatu vya rangi nyeusi huku akiwa ameshikilia mkoba , baada ya kuiona gari ya Roma aliipungia mkono na kuisimamisha huku akiwa na tabasamu.

Roma mara baada ya kutoka alijikuta akishangaa , ijapokuwa eneo hilo halikuwa zuri sana kama baadhi ya maeneo ya mashindano ya magari kama Dubai na Marekani lakini kuwepo kwa eneo hilo ndani ya jii hili la Tanzania ilikuwa ni hatua kubwa.

“Sikudhania Tanzania kuwa na eneo kama hili , hongera kwa uwekezaji mkubwa kwenye mashindano ya magari”Aliongea Roma kwa kutabaamu huku akikagua eneo lote.

Ni eneo ambalo lilikuwa limejengwa barabara za Rami maalumu kwa ajili ya mashindano ya magari ya formula one , kulikuwa na barabara za aina mbili, ya kwanza ilikuwa ni ya magari ya F1 na nyingine Roma kwa kuiangalia tu ilikuwa ni ya magari ya kawaida kwa ajili ya mashindano , huku mbele ya eneo hilo kukiwa na jengo kubwa ambalo lilionekana kama maalumu kwa ajili ya watazamaji pamoja na ‘Timing’.

Eneo lote lilikuwa la tambalae ambalo ni rahisi kuona magari yakiwa yanakimbia katika mizunguko ya barabara.

“Asante sana, Tanzania kwa sasa inapanuka hatuwezi kuangalia mambo haya kuwa kwenye nchi zilizoendelea tu , naweza kusema huu ndio uwekezaji mkubwa ambao nishawahi kufanya”Aliongea Neema mara baada ya kusalimiana kawaida na Neema kutokana na uwepo wa baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakiwazunguka.

“Imekugharimu kiasi gani kujenga hili eneo?”Aliuliza Roma.

“Hapa nilijenga kwa kushirikiana na kampuni ya Toyota ikiwa na hisa asilimia arobaini jumla ya ujenzi wote ni bilioni mia tatu za kitanzania”Aliongea Neema huku wakitembea kuelekea mbele.

Neema alikuwa amependeza kweli , ijapokuwa alikuwa mtu mzima lakini staili ya nywele fupi ilimpendezesha mno huku mwili wake ulionenepa kimpangilio ukimfanya kuonekana kijana.

“Hujaniambia kipi unataka nikusaidie”Aliongea Roma kabla hawajafikia mlango na Neema alisimama.

“Yaani hata sijui kama utaweza kunisaidia , nipo na mdogo wangu wa hiari, mtoto wa Mzee Chino anafahamika kwa jina la Msechu leo asubuhi nilimwazima gari yangu mpya kabisa ya Volkswagen , sasa nipo kazini ananipigia simu anasema gari kaibetia na imehukuliwa”

“Kaibetia kivipi?”

“Kuna moja ya mwendesha magari kutoka Indonesia alikuwa akilala kwenye hoteli yangu, baada ya kukutana na Msechu ndio wakaweka dili la kushindana kuendesha magari kwa mzunguko mmoja, Msechu kaweka gari yangu kama rehani na Mwindonesia kaweka kiasi cha pesa na Msechu alipoteza pambano hivyo gari kuwa chini ya umiliki wa Mwindonesia”Aliongea Neema.

“Nimefikiria namna ya kutatua tatizo hili na kukomboa gari yangu na nafsi yangu imeniambia ni wewe pekee unaeweza kunisaidia kushindana upya na Mwindonesia, sikuwa na uhakika sana nilivyokupigia lakini gari yangu sitaki kuipoteza kwani nimetoa pesa nyingi kuinunua , sina uhakika kama unaweza kuikomboa lakini naamini kuna vitu vingi unavyoweza kufanya ndio maana nikakufikiria kwenye wakati kama huu”Aliongea huku akionyesha huzuni na Roma aliamini huenda gari hio Neema anaipenda sana.

“Okey! Usiwe na wasiwasi nitahakikisha gari yako inarudi kwenye mikono yako”Aliongea Roma na Neema alitabasamu.

“Ni kuonyeshe kwanza magari ya kuchagua au unataka ukutane kwanza na mshindani wako?”Aliuliza.

“Shida yangu sio mshindani , shida ninayotaka kuangalia kwanza ni gari yake anayotumia , hivyo ni vyema kama nitaiona kwanza”Aliongea .

“Kama ni hivyo basi wapo upande ule wanatusubiria”Aliongea Neema na kisha akaanza kutembea kuelekea upande wa nyuma wa jengo hilo ambapo kuna sehemu iliojengewa kwa ajili ya mapumziko.

“Unamdekeza sana mdogo wako , ilikuwaje ukampa gari muhimu kwako na ghali kiasi hicho na akaja kuibetia”

“Nashindwa hata nikueleze vipi , aliniomba gari akatembee asubuhi lakini nashangaa mtu ananipigia simu kwa wasiwasi ananiambia gari kaipoteza kwa Mwindonesia , nilikasirika sana lakini Msechu ni mtu mzima na gari kaipoteza sikua kwenye nafasi ya kumlalamikia bali kurudisha gari yangu”Aliongea na Roma hakutaka kuuliza sana

Baada ya kufika upande wa nyuma hatimae Roma aliweza kuona watu watano wakiwa wamesimama huku wakiongea kwa kucheka huku mwingine akiwa amekaa chini akiwa na huzuni , kwa haraka haraka Roma alitabambua aliekaa atakuwa Msechu lakini sasa ile anawakaribia alijikuta akishangaa kumuona Desmond ndani ya eneo hilo tena akionekana kuwa wa kawaida kama vile hakuna ambacho kimetokea.

Desmond mwenyewe alishangazwa na ujio wa Roma ndani ya eneo hilo , wengine waliokuwepo ni Elvice , Abubakari, Msechu , Mwarabu ambaye amevalia nguo za kushindania kuendesha mbio za magari na mwingine Roma alikuwa ni bwana mweusi mfupi lakini alievalia nguo za bei ghali.
 
SEHEMU YA 416.

Neema alimtambulisha Roma kwa wote pasipo ya kujali kama walikuwa wakimfahamu au Lah, lakini kwa Roma macho yake yalikuwa kwa Desmond alijiuliza kwanini Desmond kuwepo hapa Tanzania ilihali alikuwa kwenye majonzi , lakini hata hivyo Roma alijiambia swala hilo halikuwa likimuhusu.

“Mr Roma naitwa Tusiman nimefurahi kukutana na wewe”Aliongea bwana mmoja ambaye alionekana kuwa mwarabu akimsalimia Roma.

Tusimani alikuwa akijua Neema anakwenda kuleta mtu wa kushindana nae ili kurudisha gari yake , lakini hakuamini mtu ambaye anakwenda kushindana nae ni huyo aliekuwa mbele yake.

“Nimefurahi kukutana na wewe bwana Tusimani”Aliongea Roma huku akipeana mkono na yeye.

Upande wa Desmond alikuwa akimwangalia Roma kwa chuki kweli na hilo hata kwa Neema Luwazo alishaliona.

“Roma nadhani ushawahi kukutana na Demsond , mtoto wa Raisi wa Rwanda?”.

“Nishawahi kukutana nae kwa muda mfupi sana , Mr Desmond naamini haupo hapa Tanzania kwa ajili ya mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Elvice Abubakari na wenzake kumwangalia mwenzao.

“Hata kama nipo hapa kwa ajili ya mkeo ni kipi unaweza kunifanya”Aliongea Desmond.

“Haha.. mara nyingi sipendi maneno , kama unaamini siwezi kufanya chochote fanya kumgusa mke wangu uone kitakachotokea , sitojali kama bado upo kwenye maombolezo ya kifo cha mama yako”.

“Hahahaha… hahaha.. muda si mrefu utakuja kunielewa”Aliongea Desmond lakini Roma alimpotezea huku upande wa Abubakari na Elvice wakionekana kutotaka kuingiza neno kabisa , hawakutaka kununua ugomvi kwani walikuwa wakimuelewa Roma.

“Broo Roma naomba unisaidie kukomboa gari yangu , ukifanikisha nipo tyari kufanya loolote kwa ajili yako tafadhari’”Aliongea Msechu kwa kupasha viganja vya mikono , uchangamfu ulimrejea mara baada ya Roma kufika ndani ya hilo eneo.

“Kipi unaweza kunifanyia?”

“Chochote naweza kukufanyia hata kama ni kuwa chawa wako”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.

Ukweli ni kwamba wote walikuwa washaona habari juu ya Roma kuwa mtoto wa Raisi Senga na ndio maana hata Abubakari na Elvice walikuwa wakijizuia kuongea neno na kuwa wakimya mno, kuna muda walijiambia wangelijua hilo tokea mwanzo wangekuwa kwenye nafasi nzuri na Roma , lakini ukweli hawakuwahi kujua kama Roma anaweza kuwa mtoto wa Raisi , walimuona kama mbeba mizigo ambaye alikuwa na nyota nzuri ya kupendwa na wanawake.

“Msechu kaa pembeni umenipotezea gari langu na sasa hivi unaonga maneno yako marahisi , kama ulikuwa unafahamu unachoweza kufanya ni kuongea tu kwanini ukaaweka gari langu Rehani?”Aliongea Neema , ukweli hakutaka kabisa wawe nrafiki wa karibu kutokaana na mahusano yake na Roma.

“Okey nadhani ni muda wa kwenda kuchagua gari ya kushindana na hii ya bwana Tusiman”Aliongea Roma huku akiangalia gari ya Tusimani eneo hilo, kulikuwa na gari mbili moja aina ya Volkswagen na nyingine ilikuwa ni gari aina ya Lamborgin”

“Mr Tusimani utatumia gari gani kati ya hio Volks na Lamborgin?”Aliuliza Roma na Tusimani alitabasamu na kisha akasogelea gari yake aina aLamborigna na kumweleza Roma atatumia gari hio aina ya Lamborgin na Roma alitabasamu na kisha akamwangalia Neema.

‘Mr Tusiman kama tulivyokubaliana nitaweka kiasi cha Dollar laki moja na kama utashinda utachukua gari pamoja na pesa lakini kama Roma akishinda nitachukua gari yangu”Aliongea Neema.

“Madam usiwe na shaka nipo tayari kupambana na kujinyakulia hio pesa”Aliongea huku akionyesha majigambo , hakuamini kama Roma anaweza kumshinda kwenye kuendesha gari , kwani hio ndio ilikuwa kazi yake miaka na miaka na alikuwa ashafanya mashindano mengi na kupokea medali nyingi, sasa alijiambia kwanini ashindwe na mtu kama Roma ambaye alionekana hata mashindano ya mbio za magari hakuwahi kuyafanya hapo kabla.

Baada ya jibu hilo Neema alivuta pumzi na kisha akamgeukia Roma na kumwambia akamuonyeshe gari ya kuchagua.

Roma aliongozwa na Neema luwazo mpaka ndani ya jengo hilo kubwa katika eneo la gereji ya magari, Roma aliishia kumsifia Neema na aliona mwanamke huyo alikuwa siriasi kwa kile ambacho anakifanya , kwani kulikuwa na magari ya aina mbalimbali kutoka kampuni nyingi , kwa haraka haraka alijua huenda alikuwa akiyakodisha kwa wale ambao walikuwa wakitaka kufanya mashindano kwa namna ya kujifunza.

“Umejitahidi sana Babe Neema”Aliongea Roma huku akipitia magari mengi yaliokuwa mbele yake na alienda kusimama kwenye gari aina ya Toyota Supra rangi ya samawati na kumwambia Neema atachukua gari hio , hata wafanyakazi wa hapo ndani waliotangulizana nae walimshangaa kwani waliona gari hio ni ya kawaida sana, walitegemea Roma kuchukua Lamborgin au Buggat kwa ajili ya kuonyesha ushindani.

Roma kwanini unachagua gari hio ya Toyota , kwanini usichukue nzuri zaidi?”aliuliza Neema kwa wasiwasi.

“Ndio ambalo linafaa , nitakuelezea mara baada ya kuhakikisha nimeshinda na kurudisha gari yako”Aliongea Roma pasipo ya kuwa na wasiwasi na alitoa ishara ya mfanyakazi kumpatia ufunguo wa gari hio na alipopatiwa aliingia ndani na kuliwasha na mngurumo wake tu ulimfanya kutabasamu.

Tusimani mwenyewe alishangaa kwa chaguo la Roma na alijikuta akishindwa kujizuia kucheka , alikuwa mzoefu wa magari na alijiambia hakuna namna ambayo Roma anaweza kumshinda.

“Mr Roma una uhakika unataka kukomboa gari ya Madam au unataka kuendesha kwa kujifurahisha?”Aliuliza Tusimani.

“Hilo swali naomba kulijibu mwishoni kabisa”Aliongea na Tusimani alicheka na kisha akaingia kwenye gari yake.

Roma alianza kupima ukubwa wa barabara hizi maalumu kwa mchezo wa mbio za magari na kutabasamu baada ya kuona ujenzi wake ulikuwa wa kimataifa zaidi.

Ni ndani ya dakika tano mbeleni Roma na Tusimani waliingia kwenye barabara kuanza pambano, walihitaji kuzunguka mara tatu ndio wakamilishe pambano na yule ambaye atawahi kuhakikisha anakamilisha mizungungo yote kwa wakati ndio angekuwa mshindi.

Neema alikuwa na wasiwasi kutokana na Roma gari aliochagua , lakini alijiambia ngoja amuamini Roma , hakuwa tayari kupoteza gari yake hio ya Volkwagen Golf R.

Roma aliendelea kuendesha mdogo mdogo pasipo yakuwa na wasiwasi huku akihakikisha muda wote yupo nyuma ya Lamborgin inayoendeshwa na Tusimani.

Elvice na wenzake walishindwa kuelewa ni jambo gani Roma anajaribu kufanya wani hakuwa akijaribu kumpita kabisa hata pale ambalo alikuwa akipata nafasi.

“Sister unadhani atashinda kweli?”Aliuliza Msechu.

“Naamini atashinda”Aliongea Neema huku macho yake yakikaza upande wa kwenye uwanja huo huku injini za gari zilikuwa zikikoroma kama hazina akili nzuri kiasi kwamba ilifurahisha kusikika , ni kwamba tu eneo lote lilikuwa na ukuta mkubwa la sivyo wananchi waliokuwa maeneo ya karibu wangetamani kuona kile kinachoendelea.

Mzunguko wa kwanza ulimalizika , Roma akiwa nyuma , wakaenda mzunguko wa pili bado Roma akawa nyuma na katika mzunguko wa tatu wakati Tusiman anajaribu kukunja kona na kuongeza spidi alijikuta akipitwa kama upepo na Roma alijikuta aking’ata meno kwa hasira na kujiambia hawezi kushindwa lakini walivyofika kwenye kona nyingine ya V ndio alipojua udhaifu wa gari yake na kujikuta akijilaumu kwanini alisahau kulifikiria hilo.

Mpaka gari inakwenda kumaliza raundi ya tatu Roma alikuwa mbele huku akimwacha Tusiman nyuma kabisa.

Hakuna alieweza kuamini Toyota Supra kufanikiwa kuishinfda gari aina ya Lamborigin Super Trofeo ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mchezaji wa mbio za magari wa kimatiafa bwana Tusiman.

Neema ndio aliekuwa wa kwanza kupiga makofi kwa nguvu mara baada ya kusimamisha gari.

“Mr Roma nikiri kwamba kukudharau kwangu ndio kumenifanya ukanishinda”Aliongea Tusiman akiwa kwenye uso wa kwaida tu , alionekana amekubali kushindwa.

“Kwanini unaongea hivyo?”

“Kwasababu ulionekana kutokuwa mzoefu sikujiuliza kwanini ukachagua gari aina ya Toyota Supra na hapo ndipo nlipokosea , ni kweli Lamborgin ina spidi kubwa kuliko Toyota lakini likija swala la kukata kona Lamnborgin inaonyesha udhaifu mkubwa sana”

“Upo sahihi Lamborgin imetengenezwa kwa ajili ya mashindano ya mbio zisizokuwa na makona na Toyota Supra licha ya kuwa na injini kubwa ya V12 na displacement kubwa lakini haina spidi , nilichokifanya ni kutumia udhaifu wa Lamborgin kushinda , kwani Lamborgin ili ifanikiwe kukata kona kutokana na spidi yake lazima ukanyage breki tofauti na Toyota sina haja ya kukanyaga breki nikikata kona na hili limenisaidia kukushinda”Aliongea Roma na kumfanya Neema na Wengine sasa kuelewa kwanini Roma aliweza kuchangua gari aina ya Toyota Supra na sio gari kama Lamborgin.

“Mr Roma , una heshima yangu , Asante sana kwa kunisaidia kukomboa gari letu kutoka kwa Mr Tusiman”Aliongea Msechu.

“Siku nyingine kama unataka kubeti tumia vitu vyako sio vya wengine , mshukuru Roma katusaidia kuirudisha gari yetu la sivyo nisingekuacha salama”Aliongea Neema huku akisogelea gari yake ya Volks kwa tabasamu pana akishindwa kuamini imerejea mikononi mwake kwa mara nyingine.

Ni baada ya nusu saa mbele wakati Roma akiongea na Neema juu ya nia yake ya kutaka kujifunza mbinu za kijini , Desmond ambaye alikuwa kwenye makasiriko makubwa hata baada ya Roma kushinda aliondoka akiwa kwenye gari yake kwa spidi kuelekea katikati ya jiji.

Ndani ya mdakika kadhaa alikuwa ashafika ndani ya Posta na kuendesha gari kwa kuchukua barabara ya Salenda na alikuja kusimama nje kabisa ya engo la hospitali kubwa ya kimataifa ya MAYA.

Alionekana kuwa makini kweli , kwani baada ya kutoka kwenye gari alianza kugeuka kulia na kushoto kuhakikisha hakukuwepo na watu wanaomfuta na kisha ndipo alipochukua nafasi ya kuingia kabisa ndani ya jengo hilo la hospitali , sasa hakuelewekea alikuwa akienda kumuona nani ndani ya hospitali hio,

******

Wakati siku hio habari kubwa nchini Tanzania kuwa ya Roma kuwa mtoto wa Raisi , upande wa dunia kulikuwa na habari kubwa sana ambayo ilikuwa kama rekodi ya kipekee.

Habari hio ilikuwa ikimuhusisha mwanamke wa kwanza katika historia kushika wadhifa wa kiongozi mkubwa wa UN yaani nafasi ya katibu mkuu.

Clelia Allisanto ndio jina maarufu lililokuwa likisambaa kwenye vyombo vikubwa vya kimataifa vya habari juu ya kuchaguliwa kwake, lilikuwa ni jambo la kihistoria kweli kweli kwani kwa taarifa iliotolewa ni kwamba mwanamke huyu mrembo wa kupindukia kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hio alikuwa akifanya kazi kama Gavana mkuu wa benki ya Dunia kutoka Uswisi.

Lakini licha ya watu wengi kujiuliza maswali na kumtaja mwanamke huyo katika vinywa vyao lakini habari kubwa iliosambazwa ni ile ya uongozi wake hondari katika kipindi chote alichohudumu katika benki ya dunia.

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye mshituko mkubwa wa habari hio alikuwa nni mrembo Dorisi wakati alipokuwa kazini , kwani ndio aliekuwa wa kwanza kuvutiwa na habari hio mara tu baada ya kuiona , yote hayo ni kutokana na kwamba alikuwa akimfahamu mtu aliekuwa akitajwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa katibu mkuu wa Umoja wa kimataifa.

Tokea mara ya mwisho ya Dorisi kukutana na mwanamke huyo hakuwahi kurudi tena licha ya kumuahidi kwamba atarudi , Dorisi alikuwa na woga wa kumuambia Roma kuhusu Clelia Allisanto kutokana na kwamba alipewa onyo la kutokuzungumza kile walichoongea.

Sasa baada ya kuangalia habari hio alijikuta na hofu yake ikiongezeka maradufu jambo la kwanza mwanamke yule alikuwa akimchukulia kama kiumbe cha ajabu na kwake siku ile ilibakia kama ndogo kwenye maisha yake , lakini leo hii kile alichokuwa akijidanganya kuwa ndoto anaona sio ndoto bali ni uhalisia.

“Huyu mwanamke ni nani haswa , kwanini anaonekana kuwa wa ajabu?”Ni swali ambalo liliibuka kwenye kichwa chake.

*******

Katika taarifa ambazo zilimfurahisha Neema ni pale alipoambiwa na Roma kuna mafunzo akiyafanya hatozeeka haraka ,Neema hakutaka kujua maelezo ya ziada yaliokuwepo kwenye mbinu hizo , ila alichotaka ni kuanza mafunzo mara moja , alijua alikuwa kwenye miaka ya mwisho mwisho kuaaga kabisa ujana na kuitwa mama mtu mzima jambo ambalo hakutaka litokee na ni siku nyingi alikuwa akijiambia angekuwa na uwezo wa kuzuia miaka isisogee basi angeweza kufanya hivyo ili tu ngozi yake isifikie hatua ya kukunjamana.

Sasa Roma alimuona kama mkombozi wake mara tu kumpa maelezo mafupi kwamba kuna mbinu za kijini kama atajifunza zitamfanya kutozeeka kwa haraka.

“Roma kwanini hukuniambia mapema nikaanza mazoezi?”Aliuliza Neema huku akijifanya kumlaumu Roma kwa kumchelewesha.

“Wazo la kuwafundisha ndio kwanza limenijia hivi karibuni mara baada ya kujua kutokana na uwezo wangu wangu nilionao siwezi kumpa ujauzito mwanamke wa kawaida”Aliongea Roma na kumfanya Neema kuelewa.

“Nipo tayari kupanga upya ratiba zangu ili mradi niweze kujifunza”Aliongea na umfanya Roma kutabasamu.

“Unaonekana unaupenda sana ujana?”

“Hakuna mwanamke anaependa kuzeeka na sura yake kukunjamana ndio maana leo hii unaona biashara ya vipodozi imekuwa habari ya mjini , wanawake wanajitahidi sana kutunza ngozi zao”Aliongea Neema na kumfanya Roma kuelewa.

“Siwezi kusema kwamba kwasasa unaweza ukajifunza moja kwa moja ila tu unapaswa kujiandaa kwa kufanya mazoezi ya viungo, naamini kutakuwa na njia bora zaidi na fupi ambayo itawafanya kujifunza kwa haraka na kurahisisha mambo”Aliongea Roma na Neema alionekana kusikiliza kwa makini utadhani alikuwa akitaka kusaini mkataba mnono wa kibiashara.

“Nipo tayari kujifunza na katika siku zote ulizonifurahisha mpenzi basi ni leo, nipo tayari kwa kufanya unachokitaka kwa siku ya leo mtoto wa Raisi Senga”Aliongea Neema akiingizia utani na kumfanya Roma kucheka kivivu na kupandwa na mizuka kwa wakati moja , tokea apige Threesome kati ya Dorisi pamoja na Rose hakukutana na mwanamke tena na kwasababu mwili wake muda wote ulikuwa na kiu ya mwanamke alijiambia hawezi kumuacha mrembo huyo akaondoka.
 
SEHEMU YA 417.

Ni muda wa saa kumi na mbili za jioni mara baada ya Roma kupiga show ya kimataifa na mrembo Neema Luwazo katika moja ya hoteli iliokuwa katikati ya jiji, wakati akiwa anaendesha gari kuelekea nyumbani aliweza kupokea simu kutoka kwa Mage na Roma alijikuta akitabasamu huku akioneka pia kukumbuka ahadi aliowekeana na mrembo huyo siku kadhaa zilizopita.

“Babe Mage mambo?”.

“Poa tu”

“Mbona unaongea kinyonge hivyo”

“Unafikiri unayofanya ni mazuri wewe mwanaume , umeenda Marekani umerudi wiki ya pili sasa umeshindwa kunitafuta”Aliongea Mage upande wa pili kwa kulalamika na kumfanya Roma kukunja uso, ni kweli alikuwa ameenda Marekani na kurudi na ikapita takribani wiki sasa hajawahi kuonana na huyu mwanamke na kujikuta akijisikia vibaya.

“Mage sijui namna ya kujitetea mpenzi ni kweli sijaonana na wewe wala kutokuwasiliana kwenye simu lakini haimaanishi nafasi yako kwangu imepungua”

“Kama maneno yako ni ya kweli , kesho mama na baba wanataka uje ujitambulishe”Aliongea Mage.

“Okey! Kesho nitafika”Aliongea Roma.

“Kweli!”

“Nilikuahidi nitakuja kwenu , kwanini nidanganye sasa niambie muda gani mnanitegemea”

“Muda wa jioni…”

“Okey sawa , lakini vipi mbona unaonekana kuwa na furaha hivyo?”

“Ni kwasababu mama alikuwa akikukataa ila sasa hivi amekukubali”Aliongea Mage huku akiachia kicheko kwa mbali.

“Unamaanisha nini kunikataa na kunikubali?”

“Tokea afahamu tuna mahusiano alikuwa akikataa mimi kuendelea na wewe na alidiriki mpaka kunitafutia mwanaume , lakini leo hii mara baada ya kujua wewe ni mtoto wa raisi kakubali moja kwa moja na anataka akuone”aliongea Mage na kumfanya Roma kutabasamu huku akijiambia kumbe Mzee Kweka kitendo alichokifanya kimemrahisishia baadhi ya mambo , alijiambia ngoja atampigia simu kumshukuru kwa kumpa promo mtandaoni.

Lakini Roma pia alijiuliza inamaana Afande Tobwe hakuwa na habari kama yeye alikuwa na uhusiano na familia ya Afande Kweka , Roma alijiambia huenda mzee huyo alijifanyisha kutofahamu maana alikuwa akikumbuka vyema kwamba yeye ndio aliemruhusu kuanzisha mahusiano na Mage..

Roma alikata simu na kisha kuendesha kuelekea nyumbani kwake , baada ya kuingiza gari ndani alitabasamu mara baada ya kuona gari ya mke wake ipo eneo hilo la gereji.

Baada ya kuingia ndani eneo la sebuleni Edna alikuwepo pamoja na Lanlan alieshikilia kishikwambi cha kucholea.

“Babe mbona unaonekana kuwa na furaha sana , Lanlan anakuonyesha kitu gani?”

“Yaani Lanlan ni mtundu kweli, Lanlan muonyeshe baba ulivyochora”Aliongea Edna kwa Kingereza na Lanlan alimsogezea Roma Drawing Pad na kuangalia na alijikuta akitabasamu mara baada ya kuona mchoro wa watu watatu wakiendesha Tembo huku akiandisha majina yao.

“Chubbi kwanini unapenda Tembo sana?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Lanlan.

“Mama pia anapenda Tembo na mama amemfundisha Lanlan kuendesha Tembo”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia Edna na kutabasamu , walijua anachoongea Lanlan huenda ni kumbukumbu za mama yake mzazi lakini bado swali hilo lilikua gumu kwao kwani kwa maelezo ya Qiang Xi Lanlan hakuwa na mama na hata kama angekuwa naye , kwanini waendeshe Tembo mbali na wanyama wote.

“Kuna kila sababu ya kumuanzishia shule”Aliongea Roma.

“Nilitaka pia tujadiliane kuhusu hilo ila wasiwasi wangu ni juu ya uwezo wake usiokuwa wa kawaida”Aliongea Edna huku akimshika shika nywele Lanlan na Roma alikumbuka maelezo ya mke wake juu ya Lanlan alichokifanyaga mara baada ya kuvamiwa wakati alipokuwa Japani.

Sasa Roma licha ya kujua hivyo , lakini hakuwahi kumshuhudia Lanlan yeye mwenyewe akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida lakini hata hivyo alishajua sio mtoto wa kawaida.

“Inaonekana hana shida sana akianza masomo hata hivyo uwezo wake unatokana na akiwa kwenye hatari “

“Naomba nikuulize nguvu zake zinafanna na hizi unazotaka tujifunze?”

“Kwa kiasi flani ninaweza kusema hivyo , yupo kwenye hatua za awali kabisa za mafunzo na kinachomsaidia yeye ni kuzaliwa na mwili usiokuwa wa kawaida , inaonekana hata nguvu zake ameingiziwa sio zile za kujifunza mwenyewe”

“Unamaanisha nini kusema mwili wake sio wa kawaida?”

“Ni maelezo ambayo siwezi kuyalezea kwa kina kwanni yanachanganya , lakini seli za mwili wake unaaweza kusema zimechangamka na hazipo kama za miili ya binadamu wa kawaida”

“Kwahio ndio maana ana uwezo mkubwa wa akili?”Aliiuliza Edna na kumfanya Roma kutingisha kichwa , hata hivyo alishindwa kumuelezea vizuri Lanlan kutokana na yeye mwenyewe kukosa maarifa ya namna mwili wake unavyofanya kazi,

Hata upande wa Edna alipenda sana kujua kwanini Lanlan alikuwa na mabadiliko kwenye mwili wake , lakini alishindwa kupata mahali pa kuulizia maana kama lilivyokuwa jambo hilo geni kwake , alijiambia hata kwa madaktari wanaweza kuona jambo geni.

Kuna muda hata yeye mwenyewe aliwaza ni sababu gani ambayo Mungu amemkusudia mpaka kukutanishwa na watu wasiokuwa wa kawaida , kuanzia Roma halafu Lanlan , aliishia kukosa majibu.

“Huna haja ya kufikiria sana , tunachotakiwa ni kumpeleka shule na kumuelekeza chakufanya Lanlan ni mtoto mwenye akili na anazingatia maagizo tutakayompatia”Aliongea Roma na Edna akatingisha kichwa.

………….

Ni mwisho wa siku nyingine kabisa Roma aliweza kupata nafasi ya kuonana na Mama T pamoja na Afande Tobwe , mambo hayakuwa magumu kama alivyotarajia kwani Mama T alimpokea kwa heshima zote.

Mam T mwanzoni alikuwa akipinga kwa Mage kuendelea na Roma mara baada ya kumuona Roma kama mwanaume wa kawaida sana , lakini mara baada ya kupata taarifa ya Roma kuwa mtoto wa raisi Senga , lakini pia fununu kutoka kwa mume wake juu ya Roma kurithishwa mali za ukoo alijikuta msimamo wake ukikosa sababu na kuishia kumkubali Roma.

Ijapokuwa imani yake ilikuwa ikimwambia kwamba Roma hawezi kuoa wanawake wengi , lakini alijiambia kama Roma atakuwa na maelezo ya kueleweka namna atakavyoishi na mwanae bila kuleta mgogoro na Edna mke wake na kwasababu Mage kashapenda basi hatakuwa na sababu ya kumkataa.

Mabadiliko yake ya ghafla katika msimamo aliokuwa nao hayakumshangaza Mage na Magdalena tu bali hata kwa Afande Tobwe, siku zote Afande Tobwe aliamini mke wake hakuwa mtu wa kunyenyekea watu wenye pesa kwasababu na yeye alikuwa nazo , lakini alijikuta akiamimi hakuwa akimfahamu vizuri mke wake.

Afande Tobwe hakuwa na mpango wa kumuelezea mke wake kwamba Roma alikuwa ni Hades au Pluto na alikuwa na cheo kikubwa kuliko cha kuwa mtoto wa raisi , hakufanya hivyo tokea mwanzo kwasababu uhusika wa Roma kuwa Hades au Pluto ulikuwa ni wa siri sana na ni watu wachache waliokuwa wakifahamu.

Basi Roma aliweza kumuhakikishia Mama T kwamba haitotokea Mage akaishi maisha ya Manyanyaso kutoka kwa Edna na atajitahidi kumpa furaha kadri awezavyo.

Kutokana na kujiamini kwa Roma na kutokuwa na aibu kulimshangaza sana Mama T lakini hakutaka kutia neno kabisa.

Wakati wa maongezi yote Magdalena alikuwepo na alionekana kuwa na furaha juu ya pacha wake Mage, lakini ndani kwa ndani alitamani apate nafasi kama ya Mage.

Baada ya maongezi yaliodumu kwa muda mfupi hatimae Roma alipata nafasi ya kuongea na Magdalena.

Roma alikuwa na mpango huo kichwani tokea jana yake , aliamini huenda Magdalena akampa taarifa chache kuhusu mbinu za kichawi alizojifunza kutoka nchini China Roma aliamini huenda kukawa na mbinu rahisi zaidi tofauti na ya kwake ili kama ataunganisha maarifa aweze kutengeneza njia ambayo itakuwa nyepesi zaidi kuwafundisha wanawake wake.

“Magdalena napanga kuwafundisha Edna juu ya mbinu za kijini”Aliongea Roma na kumfanya Mage kushangaa kidogo.

“Mh! Hilo haliwezekani , mbinu za kijini sio kila mtu anaweza kujifunza”Aliongea.

“Unachoongea ni sahihi lakini mimi naamini kila kitu kinawezekanana nitaegemea upande huo mpaka nipate mbinu ya kurahisisha”Aliongea Roma na kumfanya Magdalena kufikiria.

“Kwahio mpango wako ni upi maana mpaka sasa siwezi kuamini kama jambo hilo linaweza kufanikiwa”

“Ijapokuwa nimejifunza pia mbinu za kijini lakini za kwangu na za kwenu ni tofauti sana , mimi nilienda na ile njia ndefu na ni wengi sana wanatumia njia fupi naamini kama nitapata maelezo kidogo ya mbinu zote mbili yaani njia ndefu na fupi ninaweza kutengeneza mbinu ya kwangu na kurahisisha mafunzo”Aliongea Roma.

“Lakini hayo maelezo unayozungumzia yanapatikana kwenye vitabu na sio rahisi pia kuvipata”

“Wewe ulijifunzia wapi mbinu zako?”

“Nilijifunzia China sehemu moja inaitwa Shushan katika Ngome ya Tang”Aliongea Magdalena.

“Nishawahi kusikia kutoka kwa Master juu ya hii ngome na aliwahi kuniambia kuna pia uwepo wa maktaba ya kuhifadhi mbinu nyingi za kitamaduni za China hususani kwenye Martial Arts”

“Unachoongea ni kweli, Shushani kuna hio maktaba ambayo ipo ndani ya pango , lakini licha ya mimi kudumu ndani ya ngome ya Tang kwa muda mrefu sikubahatika kuingia wala kusoma ‘Scrolls’ zao”Aliongea Mage na kumfanya Roma kufikiria kidogo.

“Magdalena nataka unipeleke China kwenye hio ngome ya Tang”Aliongea Roma na kumfanya Magdalena kutoa macho.

“Uko siriasi?”

“Ndio nataka kwenda huko , jambo hili kwangu lina maana kubwa sana nataka mafunzo yaanze mapema”Aliongea Roma akiwa siriasi na kumfanya Magdalena kuwaza kidogo.

“Nipo tayari kukusaidia ila sina uhakika kama utaruhusiwa na wazee kuingia kwenye mapango wanapohifadhia ‘Scrolls’ za mafunzo ya tamaduni za kichina za Martial Arts”

“Kuhusu hilo usiwaze , ninachotaka ni kwenda huko na nitajua namna gani ya kuwashawishi”Aliongea Roma na kumfanya Magdalena kuvuta pumzi.

“Unataka nikupeleke lini?”

“Kesho kutwa tunaanza safari”.

“Kesho kutwa!!?”

“Ndio, Au haiwezekani?”

“Inawezekana lakini karibu sana na ndio kwanza unaniambia”

“Ajenti Flamingo wewe ni mwanajeshi kwanini unataka kufanya maandalizi kama mwanamke wa kawaida”Aliongea Roma huku akitabasamu.

“Kuna haja gani ya kuniita Ajenti Flamingo , Sijapenda”

“Hahaha,, Afande jiandae kesho kutwa tunaelekea China ila kama hutaki kwa hiari yako nitamuomba Afande Maeda anisindikize yeye”Aliongea Roma huku akiondoka na kumuacha Magdalena akimwangalia kwa macho makali yenye hasira.
 
SEHEMU YA 418.

Roma mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Magdalena hatimae aliaga na kusindikizwa na Mage.

Wakati wakiwa kwenye gari ndipo Roma alipomuelezea Mage mpango wake wa kwenda China na Magdalena kwa ajili ya kufatilia baadhi ya maarifa yanayohusiana na nguvu za kijini.

Mage baada ya kusikia kutoka kwa Roma kuwa anaweza pia kumfundisha mbinu hizo alionekana kufurahi mno huku akiamini anakwenda kuwa kama pacha wake.

Roma mpaka hatua hio aliamini warembo wake wote wapo na hiari ya kujifunza na kilichobaki ni yeye kutafuta namna za kufanya mafunzo hayo kuwa marahisi zaidi ili hatimae waweze kujifunza na kupanda levo za juu na hatimae kutegemea faida mbili kubwa , ya kwanza ni kwamba angeweza kupata watoto bila shida na swala la pili angeweza pia kuwafanya wanawake wake kutozeeka haraka kama ilivyokwake yeye.

Saa mbili kamili ndipo alipoweza kurudi nyumbani kwake na alimwelezea Edna juu ya mpango wake wa kutaka kwenda China kwa ajili ya kufatilia mbinu hizo , Roma alimwelezea Edna kwamba angeenda na Magdalena mpaka mhalai alipokuwa akijifunzia na Edna alionekana kutokuwa na tatizo juu ya hilo.

Magdalena na Omari walikuwa na utofauti kwenye mafunzo yao , Omari yeye alijifunzia kabisa Hongmeng wakati Magdalena akiwa amejifunzia kwenye mazingira ya kawaida huko nchini China sehemu inayofahamika kwa jina la Sichuan katika Dhehebu linalofahamika kwa jina la Tang Sect.

Magdalena yeye alikuwa na nguvu za kichawi lakini kidogo zilikuwa na utofauti na zile za kawaida , kutokana na kwamba alikuwa amechanganya mambo mengi katika mbinu hizo, alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko kwenye mbinu za kijini lakini wakati huo huo akiwa na mafunzo ya aina nyingine ya kichawi zaidi

Siku iliofuata Roma aliweza kwenda kazini kama kawaida na kupokelewa na mrembo wake Amina.

Siku hio mara baada ya Roma kumwelezea Amina juu ya kumfundisha mbinu ambazo zingemfanya kuwa mrembo pasipo kuzeeka , mrembo huyo alionekana kuwa na furaha kweli , ni kama hakuamini maneno ya Roma , lakini mwishowe aliishia kukubali na katika furaha yao hio waliishia kufanya mapenzi ndani ya ofisi.

Muda wa jioni wakati alipokuwa anatoka ofisini alimpigia simu Nasra na walikutana kwenye mgahawa uliokuwa chini ya jengo la Apartment anayoishi na Roma aliongea na Nasra kwa kirefu juu ya mbinu za kijini, Nasra alishangaa kwa maelezo ya Roma mno lakini hata hivyo aliishia kukubali pia kwamba atakuwa tayari kujifunza kama wengine.

Mpaka hapo Roma sasa aliweza kuona wanawake wake wote walikuwa kwenye mstari anaotaka, mstari wa kujifunza mbinu za kijini, alijiambia kama watakuja kupanda levo atakuja kuwa na amani na hatotumia nguvu nyingi kuwalinda kwani watakuwa na uwezo binafsi.

Roma baada ya kumuaga kila mtu wakiwemo wanajeshi wake wa The Eagles hatimae maandalizi ya safari yakaanza rasmi.

********

Naama ikawa ni siku nyingine saa tisa kamili za alasiri ndio muda ambao Roma na Magdalena waliweza kupanda ndege ya Airbus kutoka shirika la ndege la Qatar airways wote wakiwa ndani ya daraja la Uchumi.

Ilikuwa ni safari ndefu kutokana na ndege hio haikuwa ya moja kwa moja , kwani ingepitia Doha Nchini Qatar na kisha wangepanda kwenye ndege ya shirika hilo hilo ya Boeng na kwenda kutua Guanzhou nchini China na hapo ndipo wangepanda ndege kwenda Chengdu, kwa hio ratiba za safari yao ingewachukua masaa zaidi ya kumi na nane wakiwa angani.

Chengdu ni mji mkuu wa jimbo la Sichuani ni moja ya jiji la kupendeza lenye pilika pilika nyingi sana, jiji hili ni mchanganyiko wa majengo ya kihistoria na ya kisasa , huenda tofauti na miji mingine mikubwa ndani ya China na sifa yake kubwa ni uwepo wa vyakula mbalimbali vya kutoa mate ya hamu.

Kuna utofauti mkubwa kati ya majiji makubwa yaliopo Afrika na Chengdu , wachina wenyewe wamejikita zaidi katika kutunza bustani hata katikati ya jiji na hili hufanya eneo kupendeza zaidi na kuwa na hali ya hewa nzuri.

Saa tatu kamili za usiku ndio muda ambao Roma na Magdalena waliweza kutua kwenye uwanja wa ndege wa Chengdu Shuangliu, kama kawaida Roma hakuwa amebeba vitu vingi alikuwa yeye na shati lake na suruali yake tofauti na kwa Magdaelana yeye alikuwa na kijibegi kidogo cha mgongoni.

Kutokana na muda ulikuwa umeenda ilibidi watafute hoteli moja ndani ya eneo hilo kwani kusingekuwa na usafiri wa kuwafikisha milima ya ngome ya Tang kwa muda huo.

Hoteli waliokuja kupata ni iliokuwa karibu kabisa na uwanja huo iliokuwa ikifahamika kwa jina la Hyatt Place Chengdu , shukrani kwa kadi ya Platinum ambayo Roma aliichukua nchini Marekani ndio ilimsaidia kulipia gharama zote na yeye pamoja na Magdalena waliweza kupata kila mmoja chumba chake.

Siku iliofuatia wa kwanza kuamka alikuwa ni Roma na alimgongea Mage kwa ajili ya kujiandaa na kuanza safari , Roma yeye kwa upande wake kwenye hayo maeneo hakuwa na uzoefu mkubwa hivyo ilikuwa ni kama alikuwa akimtegemea Magdalena kuongoza njia.

Magdalena alimaliza kujiandaa na hatimae akakutana na Roma eneo la mgahawahi na kupata kifungua kinywa ili kuianza safari.

“Nisamehe kwa kukusubirisha muda mrefu”Aliongea Magdalena ambaye asubuhi hio alikuwa amevalia blazia nyeupe na jeans ya bluu pamoja na raba , alionekana kupendeza kweli na ngozi yake ya kibantu , kwa mwanamue yoyote anaemwangalia ni ngumu sana kujua alikuwa na mafunzo makubwa ya kimapigano na pia ni mwanajeshi.

“Usijali”Alijbu Roma na kisha akampa ishara ya kuketi na muda huo huo kifungua kinywa kikaandaliwa kwa wote.

Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa ilibidi Roma aulize ni kwa namna gani wanafika huko kwenye ngome ya Tang na Magdalena alimwambia amfuate nyuma nyuma tu na Roma hakujali zaidi na kumfuata.

Baada ya kutembea umbali mfupi walikuja kusimama barabarani kwenye kituo kidogo cha kupandishia abiria na hazikupita hata dakika kumi basi rangi ya kijani lilitokea na kwenda kusimama pembeni yao.

“Magdalena hili basi ndio litatupeleka mpaka huko kwenye Nogme , kwanini tusichukue usafiri binafsi?”Aliongea Roma lakini Mage hakumjali zaidi ya kupanda na kisha akamgeukia.

“Tutashuka kwenye kituo kinachofuata” Aliongea na Roma alitingisha kichwa na kisha akaingia kwenye basi na kuanza kutafuta siti, basi lote lilionekana kutokuwa na vijana bali ni wachina wazee wazee wanaume kwa wanawake wakiwaangalia kwa mshangao kidogo kutokana na ngozi zao na Roma aliishia kuwatingishia vichwa kama salamu na kwenda kukaa kwenye siti ya nyuma kabisa.

“Ngome ya Tang ipo kwenye wilaya inayofahamika kwa jina la Pujiang tungechukua usafiri wa kawaida lakini gharama zingezidi kuwa kubwa”Aliongea Mage na kumfanya Roma kushangaa , hakujua kama Magdalena alikuwa mbahili namna hio , ijapokuwa hata yeye alikuwa mbahili miezi kadhaa nyuma lakini mara baada ya kuanza maisha mapya na Edna , kwake pesa haikuwa tatizo sana.

“Kama shida ni nauli kwanini usingesema ningelipia mimi”

“Swala sio pesa nataka angalau tufike kidogo muda umeenda”Aliongea Mage na kumfanya sasa Roma kuelewa.

“Kwahio tutachukua masaa mangapi kufika?”

“Ni masaa mawili kamili”

“Mbona mapema , Magdalena usiniambie unampango wako kichwani wa kutaka kutumia muda mrefu na mimi , kama ni hivyo tunaweza kurudi tena na kuanza safari upya”Aliongea Roma na kumfanya Magdalena kuona aibu kwani ni kama siri yake iligundulika.

“Mimi ndio mwenyeji acha kuongea ujinga na utafuata kila ninachokuambia”Aliongea.

“Okey! Mwenyeji”Aliongea Roma kwa kutabasamu na safari yao iliendelea kimya kimya huku Roma akijaribu kuangalia mazingira ya nje ya barabara.

Ni muda wa saa nne nne hivi waliweza kushuka kwenye basi mara baada ya kusimama katika kituo kikubwa cha mabasi cha Wilaya ya Pujiang.

Pujjiang ipo kusini mwa jimbo hili la Sichuani na kwasababu ni sehemu ambayo ipo chini ya mlima ilifanya eneo lote kuwa na kijani kizuri na maji ya kutosha huku hali ya hewa ikiwa ya ubaridi kiasi.

Roma mara baada ya kushuka kwenye basi alijaribu kuangalia mazingira ya eneo hilo na kujiuliza ngome hio itakuwa wapi na alijiambia kama angefika mwenyewe huenda asingefanikiwa hata kuiona kwani ni eneo kidogo ambalo linachanganya kwani halikuwa kama kijiji bali lilikuwa limeendelea , ni rahisi kusema kwamba karibia maeneo yote ya China yalikuwa yapo kimjini mjini.

“Hii wilaya unaweza kusema ndio niliokulia, tuelekea upande huo wa kushoto nilishawasiliana na Master nakuja na amesema ataagiza mtu wa kutupokea”Aliongea Magdalena huku akimpita Roma.

Roma kwa kiasi flani aligundua Magdalena alikuwa na wasiwasi kwenye macho yake lakini alishindwa kuuliza , hata hivyo ni watu wachache sana wa rangi yao kuonekana kwenye eneo hilo.

Roma alifuatisha nyuma kwa nyuma upande wa kushoto wakipita kwenye barabara iliojengwa kwa Zege wakiiacha Stendi na ndani ya dakika chache tu waliweza kufika kwenye eneo ambalo lilikuwa ni soko na pilika pilika zilikuwa za kutosha na watu hawakuwajali sana hata hivyo katika jimbo hili kulikuwa na mchanganyiko wa watu wengi kidogo tofauti na maeneo mengine.

Baada ya kukatiza soko hilo na kuibukia upande wa pili hatimae Mage alisogelewa na Mchina mmoja huku akiwa na tabasamu kwenye uso wake.

“Mkubwa , umefika?”Alioongea Kwa lugha ya kimandarini huku akiwa na furaha kumuona Mage na wote waliangaliana na kisha Mage akacheka kidogo na kisha akamgeukia Roma.

“Roma huyu unaweza kusema kwamba alikuwa mdogo kwangu katika mafunzo anafahamika kwa jina la Tang Lizhong , ni mtoto wa mwisho wa mkuu wa ngome anaefahamika kwa jina la Tang Dianshan nimempita mwaka mmoja ki umri, wakati wa mafunzo tulifanya wote kwa kusaidiana vitu vingi”Aliongea Magdalena kwa Kimandarini na kumfanya Roma kushangaa , hakuamini Magdalena anaweza kuongea Kichina vizuri.

“Nimefurahi kukutana na wewe bwana Tang Lizhong”Alijibu pia Roma kwa kichina na kumfanya yule mwana kushangaa kidogo Roma kujua lugha yao.

“Lizhong ngoja nikutambulishe huyu anafahamika kwa jina la Roma Ramoni ni rafiki yangu”Aliongea Magdalena.

“Mkubwa huna haja ya kuigiza ulivyotoa taarifa unakuja na mwanaume moja kwa moja tuliamini hampo kwenye mauhsiano ya kawaida kama ya urafiki tu”Aliongea Tang Lizhong kwa kutania na kisha akamgeukia Roma.

“Mr Roma Ramoni karibu sana tumeweza kusikia sana kuhusu habari zako katika uwezo wako uliokuwa nao kwenye kujifunza mbinu za kijini kutoka Hongmeng, kwenye maisha yangu sikuwahi kufikiria kama nitakuja kukutana na wewe , watu wengi huwa wanakuzungumzia, moja ya sifa kubwa unayafahamaika nayo ni namna ulivyoafanikiwa kujifunza mbinu ndefu ya mafunzo ya kijini , lakini inanishangaza kuona mwili wako kuwa wa kawaida sana kama wa binadamu asie na mafunzo ya aina yoyote”Aliongea Tang Lizhong.

“Sikujua kama nina umaarufu mkubwa ukanda huu , huenda ndio sababu hata mkubwa wako hapa ananihusudu”Aliongea Roma kwa utani na kumfanya Magdalena amkate jicho na aliishia kucheka kwani hakuwahi kumuona Magdalena akiwa hivyo na upande wa Lizhong aliona asiingilie wawili hao mambo yao.

“Gari nimeicha mbele , twendeni sasa ngomeni”Aliongea na wote kwa pamoja walitingishiana vichwa na kufuatishana.

Baada ya kuingia kwenye gari flani aina ya Jeep walikata kona chache na hatimae kuacha mji na kuusogelea msitu uliokuwa mbele yao, ulikuwa ni simtu ambao miti yake mingi ni ile ya aina ya Mi pine.

Roma baada ya kuona gari linaingia ndani ndani kwenye msitu alijikuta akijiambia kama ni mtu wakawaida kuingia sehemu hii hakika kuna uwezekano wa kusimamishwa na walinzi , ilikuwa pia ni sahihi kwake kukisia huenda hata soko hilo chini yake lilitengwa kwa makusudi kabisa ili kufanya ngome hio kutofahamika sana lakini wakati huo wakilitumia kupata mahitaji yao.

Baada ya gari kutembea kwa takribani dakika kumi , hatimae liliweza kutokezea kwenye ardhi nyingine ya uwazi kabisa ambayo ilikuwa na nyumba nyingi zilizojengwa kwenye eneo la tambarare , huku karibia zote zikiwa katika hali ya kufanana.

Eneo hilo lilimfanya Roma kujihisi ni kama alikuwa amesafiri nyuma ya muda ,ijapokuwa kulikuwa na nyumba chache za kisasa lakini hazikuonekana kutokana na majengo mengi ya kizamani kujaa katika hilo eneo.

Mbele kabisa kabla ya kuingia ndani ya hilo eneo kulikuwa na ubao mkubwa uliozeeka wenye maandishi mekundu ya kichina ambayo Roma aliweza kuyaelewa kwa haraka haraka huku yakiambatana na mchoro mfano wa Dragoni, Tang Ancestral Fortress’.

Ijapokuwa nyumba zote kuwa za muundo wa kizamani lakini pia kulikuwa na magari ya kawaida ndani ya eneo hilo katika shepu mbali mbali , kulikuwa na pickups , madogo ya kutembelea ambayo sio mapya sana lakini pia kulikuwa na yale yakubebea mizigo.

“Kuna nyumba nyingi zaidi tofauti na unazoziona hapa na nyumba za kisasa ni za kuhesabika, hili eneo ni kubwa sana na lina watu wengi”Aliongea Magdalena

“Wewe ulikaa wapi wakati ukiwa mafunzoni hapa?”Aliuliza Roma.

“Ngoja kwanza tukutane na Master nitakuonyesha baadae”

Walitoka kwenye gari na kuendelea kutembea mbele huku wakipishana na baadhi ya watu waliokuwa wakiwashangaa watoto kwa wakubwa , wote wakiwa kwenye mavazi ya kitamaduni, kuna wale walioonyesha kumfahamu Magdalena lakini hata hivyo hakuna ambaye alionekana kuanza kumsalimia zaidi walimsalimia Lizhong kwa kumtania kwa lugha yao.

Magdalena alimwambia Roma kuna sheria kali mno , ijapokuwa ameishi miaka mingi lakini hakuwa akiruhusiwa kujichanganya na watu wa jamii zingine na Roma alijikuta akimuonea huruma na aliona huenda mtu ambaye aliongea nae sana wakati wa ukaaji wake ni Lizhong tu pekee.

Baada ya kupita kwenye vijumba hivyo walikuja kusimama mbele kabisa ya nyumba moja ya kizamani yenye muundo wa kupendeza kidogo na Lizhong aliwaongoza na kuingia ndani eneo la sebuleni, mbele yake kulikuwa na jiko moja kubwa ambalo kuni za Misandali zilikuwa zikiungua na kusababisha harufu nzuri.

Tang Lizhong alisimama kwa mbele yao na kisha akakusanya mikono yake kwa mbele kwa namna ya ukaribisho , ilikuwa ni sehemu ya tamaduni za kichina .

“Mkubwa, Mr Roma tafadhari naombeni msubiri kwa dakika kadhaa , Wazee watafika hapa muda si mrefu kwani wapo kwenye maadiliano”Aliongea na kisha akawaonyesha mahali pa kuketi kwenye viti huku wakipata joto kutoka kwenye moto.

“Kuna kikao gani kinachofanyika kwa muda huu?”Aliuliza Roma.

“Tang Sect siku zote imekuwa ni yenye kujitenga sana na watu wa kawaida na ni mara chache sana kukaribisha hata Wachina wenyewe kufika kwenye mipaka yao , sababu kubwa ni kutokana na uwepo wa vitu vingi vya thamani na vya siri sana vinavyohusu mbinu za Uvunaji wa nishati na dhana nyingi za kichawi, hata wewe wameweza kukuruhusu kutokana na umaarufu wako kama Hades , naamini Master’s wote mpaka sasa wapo kwenye kikao maana nilipowasiliana nao niliwaelezea dhumuni lako la kutaka kufika huku”Aliongea Mage

Muda huo huo walifika wanawake wawili waliovalia mavazi yao ya kitamaduni na kuwawekea chai inayonukia , ambayo Roma alishindwa kuelewa ni ya mti gani , huku wakipewa na vijikeki vidogo.

Baada ya wahudumu wale kuondoka sauti za watu wanaongea kwa kutoeleweka kwa lugha ya kichina zilisikika na muda uleule aliingia eneo hilo mwanaume alieotokea upande wa kulia kwao kwenye jengo lingine akiwa amevalia vazi la kitamaduni kama joho rangi ya bluu akiwa amefunga na mshipi kiunoni wa rangi nyekundu.

Alikuwa ni mwanaume mtu mzima ambaye alikuwa na ndevu nyingi mno na masharubu yaliofanya hata midomo yake kujificha.

“Flamingo hatimae umeweza kurudi hapa tokea mwaka mmoja ulivyoondoka baada ya kujiunga na mafunzo ya kijeshi, tulikumisi sana”Aliongea pasipo kumzingatia Roma.

“Asante sana Mjomba”Aliongea Magdalena na kusimama na kisha akatoa salamu kwa kuinamisha kichwa.

“Wewe mtoto mtukutu usie na shukrani , naamini kama sio huyu mpuuzi uliekuja nae usingetia mguu tena hapa”Ilisikika sauti ya kike ikitokea kwenye mlango uleule huku akiwa amevalia joho pia ambalo lina naksi nakshi nyingi.

Alikuwa Mchina mtu mzima kiasi anaeonekana kujiamini kabisa , sura yake pia haikuwa imekunjamana sana kuonyesha kama alikuwa ashaanza kuufikia uzee.

“Master….!”Aliongea Magdalena huku akisimama kwa heshima akimwita mwanamke huyo kwa jina la Master.

Roma baada ya kusikia Magdalena anamwita kwa jina la Master palepale alijua mwanamke huyo atakuwa anaitwa kwa jina la Tang Luyi kwani wakati anaongea na Magdalena alimtajia jina hilo.

Baada ya kumchunguza vizuri aligundua alikuwa kwenye levo ya Mzunguko kamili wa mafunzo ya kijini na Roma aliamini huenda ndio maana ngozi yake ikawa nyororo kwani ni ngumu kuona mwanamke kama huyo wa kuitwa Master halafu bado akawa kijana.

Tang luyi alimwangalia Magdalena kwa namna ya kumchunguza kwanzia juu mpaka chini na alionekana kuridhishwa na jambo fulani na ndipo alipogeuza macho yake kwa Roma na baada ya kumchunguza Roma na kuona hana hata dalili ya msisimko wowote alitoa sonyo huku akikaa chini kwenye kiti cha mbao kwa mbwembwe zote.

Muda huo huo waliongezeka wazee wengine wakiume na kukamilisha idadi yao na kuwa jumla ya nane huku macho yao yote yakimwangalia Roma kwa macho ya dharau kama vile walikuwa wakiona kiumbe cha ajabu.

“Wewe ndio Roma Ramoni kutoka Tanzania unaetokea kwenye ukoo wa Kweka?”Aliuliza yule mzee mmoja ambaye kidogo alionyesha heshima akiwa amevalia joho la rangi ya kijani, Roma alishangaa kwa Afande Kweka kutambulika ndani ya eneo hilo na alijiambia huenda ni kutokana na uwepo wa Zenzhei maana mpaka wakati huo alikuwa akijiuliza ilikuwaje Zenzhei akawa msaidizi wa karibu wa Afande Kweka.

“Lazima utakuwa Master Tang Dianshan naomba unisamehe kwa kuwafanyia ziara ya kushitukiza”Aliongea Roma Roma na yule mzee alivuta pumzi.

“Nimesikia umeweza kujifunza mbinu ndefu ya mafunzo yetu ya kuvuna nishati ya mbingu na Ardhi na umeweza kuingia levo ya nusu mzunguko lakini hata hivyo, sisemi kwamba nakubagua kwa utofauti wako na jamii yetu lakini levo yako ya mafunzo ni ndogo sana kuruhusiwa kuingia kwenye Pango la Scrolls.

Scrolls ni aina flani ya makaratasi yaliokunjwa kunywa kwa staili flani ambayo hutunza maandishi kama kumbukumbu.

“Kwaho ni jambo gani ambalo napaswa kufanya ili kuweza kuingia kwenye pango hilo la kumbukumbu”Aliuliza Roma

“Ukijumlisha taratibu zetu za taifa la China ,lakini pia ndani ya jamii yetu ya Sichuan haturuhusu watu wa tamaduni za nje kuingia kwenye hifadhi ya kumbukumbu zetu tokea zamani , lakini kutokana na mipango ya kuendeleza tamaduni zetu kwa vizazi vingine tulilegeza kidogo sheria na ndio maana hata Magdalena aliweza kujifunza hapa na wengine kutoka mataifa ya Afrika, lakini hata hivyo hakuna mtu hata mmoja ambaye ashajifunza hapa na kuweza kufanikiwa kuingia huko hio yote ni kutokana na kukosa vigezo”

Ili uweze kufikia vigezo ni lazima upitie majaribio ambayo yatafutanya kupima nia yako ,utimamu wako wa akili lakini tujue pia hauna nia mbaya ya kutaka kuona hifadhi zetu kwa malengo ya kifisadi , hii yote ni kuzuia uharifu unaotokana na mbinu hizi za kichawi kwenye jamii ya kawaida”Aliongea.

“Nipo tayari kupitia vigezo vyote”Aliongea Roma.

“Wewe mtukutu ni kipi hapo sasa hujaelewa , anachomaanisha huwezi kufika kwenye maktaba yetu”Aliongea Tang Luyi

“Nimetoka Tanzania mpaka hapa kwa pesa nyingi sana , siwezi kurudi mikono mitupu”Aliongea Roma na kufanya chumba chote kuwa kimya huku wale wazee wa kichina wakitoa msisimko wa nguvu zao za kichawi , lakini kwa Roma aliona kama mchezo wa kitoto sana maana hazikumuathiri kwa chochote.

“Unajifanyisha kijogoo kwasababu unacheo cha kipumbavu kinachoitwa uungu , nikuambie tu hizo mnazoziita kanuni za anga ni upuuzi kwetu na hazina athari yoyote , usijifanye umefanikiwa kumdanganya Flamingo na kukuleta hapa ukadhani na sisi tutakupokea , acha kuota ndoto za mchana na kujifanyisha wewe ni kijogoo mbele yetu”Aliongea Tang luyi kwa majigambo.

“Magdalena Master wako kumbe ni mshamba hivi , nahisi kwa roho yake mbaya alikuwa akikunyanyasa , haishangazi ndio maana ukaamua kuondoka kwenye hili eneo ambalo ni kama limelaaniwa”Aliongea Roma

“Nyamazaaa…”Alifoka kwa hasira Tang Luyi na palepale aliachia nguvu isio ya kawaida ya kijini kuelekea alipokaa Roma.

ITAENDELEA WEEKEND:0687151346 NICHEKI WATSAPP KWA UTARATIBU WA MWENDELEZO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…