SEHEMU YA 415.
Roma ilibidi ampe Edna kwanza maelezo kwa ufupi kuhusu nguvu anazotumia , hakuziita kwa jina la mbinu za kijini bali yeye aliziita mwenyewe mbinu za Heaven and Earth’ , yaani mbinu za kuvuna nishati kati ya mbingu na Ardhi.
Edna hakushangaa sana kwani mwenyewe alikuwa na mengi ambayo hakuwa akiyajua kuhusu Roma , lakini jambo moja ambalo lilimfanya kushangaa ni swala la Roma kusema kwamba pasipo ya mwanamke kuwa angalau na nguvu hizo hatoweza kubeba mimba yake.
Roma hakumficha Edna juu ya kumwambia Rose na Dorisi na katika maelezo yote sehemu iliomgusa Edna kwa kumuogopesha na kushangaa kwa wakati mmoja ni pale Roma aliposema kwamba kama tu yeye ataweza kujifunza mbinu hizo na kufikia levo za juu anaweza kuishi muda mrefu pasipo kuzeeka.
“Niliamua kumuelezea Rose kwanza kwasababu mwili wake umejengeka kimazoezi , mbinu hizi sio rahisi na hata kama niseme naweza kukuingizia kiasi kwenye mwili wako utashindwa kuhimili”Aliongea Roma na kumfanya Edna kufikiria.
“Kwahio unataka nifanye nini??”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuvuta pumzi mpaka hapo aliona Edna alishaleewa anachojaribu kumuelezea.
“Kwasasa siwezi kusema kuna njia ya moja kwa moja juu ya kujifunza, ijapokuwa hata mimi nimefunzwa lakini njia yangu mimi ni ndefu sana na itachukua miaka mingi mpaka kuipatia , hivyo nafikiria kutafuta maarifa yanayohusiana na mbinu fupi ambayo mtaweza kujifunza na kupanda levo kwa haraka”Aliongea Roma kwa nafsi ya pili wingi akijumuisha wanawake wake.
Roma alimweleza Edna kwanini alichagua kujifunza mbinu za kijini na alimwambia sababu kubwa ni kushindana na sayansi iliowekwa ndani ya mwili wake , yote hayo ikiwa ni kumfanya kuwa na uwezo mkubwa pasipo kutumia sayansi iliowekwa kwenye mwili wake na hatimae kumfanya kuwa binadamu wa kawaida.
Edna alitulia kwa madakika kadhaa akiwa ni mwenye kufikiria kidogo na Roma alimwacha kwa takribani dakika tano zote akiwa pembeni yake.
Edna na yeye aliwaza kama kweli anakwenda kuanza Maisha ya ndoa na Roma basi atafikia hatua ya kuhitaji watoto lakini wakati huo huo hawezi yeye kuzeeka halafu mume wake akawa hazeeki haraka.
“Nifanye nini ili niweze kujifuza?”Aliuliza Edna akimwangalia Roma usoni na Roma mwenyewe alishangazwa na swali hilo kwani hakutarajia Edna kumuelewa kirahisi namna hio.
“Kwasababu sijapata mbinu rahisi ya kurahisisha mafunzo yote , unachotakiwa kufanya nimaandalizi ya mwili wako mpaka wakati nitakapopata mbinu rahisi ya kueleweka”
“Maandalizi ya aina gani ambayo napaswa kufanya?”
“Unapaswa kuchukua mazoezi kila siku asubuhi , ili kuweka viungo vyako imara”
“Mafunzo haya hayataingiliana na ratiba zangu za ofisini ?, kwani unafahamu kampuni kwanugu ndio kila kitu na ni Zaidi ya familia laki moja zinategemea niwalipe mshahara , hivyo nitahitajika muda wote kuwa kazini ili kuhakikisha kampuni inaendelea bila kupatwa na tatizo”Aliongea.
“Huna haja ya kuwazia sana kuhusu mbinu hii kwani haiwezi kabisa kuingilia mambo yako ya kazi, na mafunzo ni ya muda mchache sana kwa siku na unaweza kuyafanya mahali popote , hata hivyo kwasasa siwezi kuongea sana kwani sijapata mbinu za kuyafanya yawe marahisi”Aliongea Roma na Edna alionekana kuelewa kwa kiasi chake, hata hivyo Edna alijiambia hawezi kuwaacha michepuko kujifunza mbinu hizo peke yao , itamaanisha yeye ndio atazeeka na wanawake wengine wa Roma hawatozeeka.
********
Ilikuwa ni siku nyingine kabisa , muda wa asubuhi wakati Raisi Senga Kweka alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya Kwenda ofisini , mara simu yake iliokuwa pembeni kwenye Dressing table ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Kabwe , moja ya wasaidizi wake ambao anawaamini sana.
“Kabwe kuna nini?”
“Mheshimiwa kuna habari inasambaa mtandaoni”Aliongea Kabwe upande wa pili na kumfanya Raisi Senga kushangaa.
“Habari gani na inahusiana nini na Ikulu?”
“Inakuhusu wewe mheshimiwa..”Aliongea Kabwe na Raisi Jeremy hakutaka maelezo mengi wakati simu ipo ambayo inaweza kuangalia mtandaoni , haraka haraka alifungua moja ya mtandao maarufu na kuangalia kile ambacho kinasambaa, alijikuta akipandwa na Jaziba mara baada ya kuona taarifa hio.
“F**ck!”Alitoa tusi huku akihema kwa nguvu na kurudisha simu yake kwenye meza huku akijiangalia kwenye kioo kwa macho yaliojaa hasira , lakini wakati huo huo mlango wa chumba hicho cha kupumzikia ulifunguliwa na mke wake Damasi au Mama Ashley.
“Mume wangu , mbona uko hivyo?”Aliuliza Damasi kwa wasiwasi mara baada ya kuona mabadiliko ya mume wake kwa kupitia kioo , lakini Senga hakuongea lolote Zaidi ya kumpa ishara aangalie kwenye simu.
Damasi mara baada ya kuchukua simu na kuangalia kile kilichokuwemo alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha kwa wakati mmoja.
“Mme wangu huna haja ya kuwa hivi , nilitarajia hili kutokea na nimekuwa nikikusihi utafute namna ya kulitatua”Aliongea Damasi kwa upole.
“Upo sahihi Mama Ashley , lakini unaamini hili ni sawa? , Kwannii yule mzee siku zote hapendi kunishirikisha kwenye baadhi ya mambo muhimu yanayonihusu na kuchukua maamuzi ambayo yana athari kwa uongozi wangu?”Aliongea huku akipunguza mkabo wa tai.
Taarifa ambayo ilikuwa ikisambaa mtandaoni ilikuwa inayohusiana na uhusiano uliokuwepo kati ya Roma na Raisi Senga , taarifa ilikuwa ikielezea uwepo wa Roma kama mtoto wa kwanza wa Raisi Senga ambaye alimpata na mke wake wa kwanza, taarifa hio ilionekana kutokuwa uzushi na kumkasirisha Raisi Senga kutokana na kwamba alieithibitisha ni Afande Camillius Kweka mwenyewe.
Kwa maana rahisi ni kwamba ni taarifa iliosambazwa mtandaoni s na Afande Kweka mwenyewe akijaribu kumtambua hadharani Roma kama mjukuu wake , hivyo hata kama Raisi Senga atake kuibatilisha hakukua na uwezekano huo na isitoshe Raisi Camilius Kweka ni mwanajeshi mstaafu ambaye alikuwa akiaminika kwenye maswala mengi ya kitaifa.
Damasi mke wa Raisi Senga mwenyewe alishatarajia hilo kutokea na ndio maana siku zote alitamani mume wake kumkubali Roma kama sehemu ya mtoto wake na kumjumuisha katika familia , lakini Senga alionekana kuwa mgumu katika hilo.
“Utafanya nini mume wangu , unapaswa kumtambua Roma kama mtoto wako”
“Damasi mke wangu unasikia unachokiongea, nikishamtambua Roma kama sehemu ya familia yangu ni kwamba nampa ushindi baba wa kumfanya Roma kuwa mrithi wa familia , jambo ambalo sitaki litokee , jambo ambalo hata wewe unajua litaibua migogoro kati ya Denisi na Roma”Aliongea na kumfanyaDamasi kurudi nyuma na kukaa kwenye kitanda.
“Kama hutaki kumtambbua Roma kama mwanao , unanjia ipi nyingine? , Senga mume wangu najua kinachokuumiza ni usaliti aliokufanyia Blandina na hili linaniumiza pia sana , linanifanya nione bado unampenda kuliko mimi mkeo”Aliongea na kumfanya Senga kugeuka.
“Sio kweli Mama Ashley simpendi kabisa yule mwanamke”
“Kama humpendi kwanini unamkataa Roma kama mtoto wako wakati kosa lilikuwa upande wa Mama yake , Unachokifanya ni kumkomoa Blandina kwa kutokumkubali Roma kwasababu unampenda bado na unatamani unachojisikia na yeye apate kuhisi hivyo , Senga niambie kama bado unampenda?”Aliongea huku utulivu wake ukianza kupotea na maneno yake yalionekana kuwa ya kweli ndani yake na kumfanya hata Raisi Senga mwenyewe ajiulize ni sababu ipi ambayo ilikuwa ikimfanya kutokumtambua Roma kama mtoto wake na jibu lilikuwa moja tu kwamba alikuwa akimkasirikia Blandina kwa usaliti wake ndio maana anajaribu kumkomesha kwa kutomtambua mwanae.
“Senga najua ni mengi tulipitia pamoja , najua nilipokutoa Senga , lakini swala la Roma na Blandina sitaki livuruge kile tulichokijenga pamoja , wewe ni Raisi wa nchi hii hebu fikiria siku ikatoka taarifa kwamba umeikataa damu yako , utakuwa unaonyesha mfano wa namna gani kwa jamii kama kiongozi wa juu, serikali yako ipo kidedea kwenye kuhamasisha wanaume kutimiza wajibu wao pasipo kukimbia majukumu , pasipo ya kutelekeza watoto wao , je wewe una utofauti gani na hao walioko mtaani , wanaume ambao wanatelekeza familia zao?, Mume wangu sio kwamba nakufananisha lakini najaribu kukushauri kwamba unapaswa kuwajibika kwa kila kinchotokea kwenye maisha yako kwani ni sehemu ya matokeo ya chaguzi ulikwisha kufanya”Aliongea Damasi na kumfanya Raisi Senga kufikiria kidogo.
“Mke wangu kwahio unanishauri nimpokee Roma kama mtoto wangu?”
“Senga najua ni mapema mno kwako kukubali kila kitu kuwa sawa na kuendelea kuishi kama hakuna kilichotokea , najua ni wakati gani unapitia kuamini kwamba siku zote ulidanganywa , silazimishi moyo wako kumkubali Roma kwani hilo ni swala ambalo lipo nje ya uwezo wangu bali ninachofanya hapa ni kujaribu kulinda taswira yako , una maadui wengi katika siasa na kama utawapa udhaifu wa kukutawala basi hutofikia hata nusu ya malengo uliojiwekea, Ninachotaka wewe ufanye sasa hivi ni kufanya maamuzi ya kisiasa , mambo mengine tuyape muda”Aliongea na Raisi Senga alionekana kufikiria.
“Nitafikiria na nitajua nini cha kufanya , hata hivyo nashukuru kwa ushauri wako huu mzuri Mama Ashley”Aliongea na kumfanya Mama Ashley kumkumbatia kwa kumpiga piga mgongoni.
*****
Upande wa Roma hata yeye aliamshwa na habari hio hio ya yeye kutangazwa kuwa mtoto wa Raisi Senga Kweka , ijapokuwa jambo hilo mwanzoni hakuwahi kulichukulia siriasi lakini ni jambo kubwa mno kwake kutokana na kugusa mpaka watu ambao wanamzunguka.hata hivyo habari za familia yake hakuziweka wazi hata kwa wanawake wake, ni Edna pekee ndie aliekuwa akijua kuwa baba yake ni Raisi Senga.
Moja ya watu ambao waliweza kuona habari hio pia ni Blandina na alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha baada ya kuona mtu alieweka taarifa hio ni babu yake Roma yaani Afande Kweka , kwa haraka haraka aliamini huenda mzee huyo alikuwa akijaribu kumfanya Senga kumkubali Roma kama mwanae.
Roma wala hakujihangaisha kabisa na habari hio na alionekana ni kama haikuwa ikimuhusu, akiwa chumbani kwake alionekana akipiga simu kwa kutumia simu yake ndogo huku namba alizokuwa akitumia zikionekana kutokuwa za kawaida kabisa.
“You Majest Pluto!!!”Ilisikika sauti upande wa pili kwa mshangao.
“Ron habari za siku nyingi”Aliongea Roma huku akikaa kwenye kitanda.
“Mfalme Pluto siamini hatimae umeweza kunipigia, habari zako nilikuwa nikizisikia juu juu kutoka kwa Sauron na sikuamini hata niliposikia umeoa”Iliongea sauti upande wa pili kwa lugha ya kingereza na kumfanya Roma kutabasamu.
“Nisamehe Rona kwa kutokutafuta mapema, alichokuambia Sauroni ni kweli , sasa hivi nina familia”Aliongea.
“Mfalme Pluto huna haja ya kuniomba msamaha najua ulikuwa na sababu za msingi kufanya hivyo ni jambo la kushangaza na kufurahisha sana , natamani siku moja kuiona familia yako ikiwa huku kisiwani kwenye nyumba yako , imepooza sana”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.
“Kuhuhusu hilo , ndio sababu ilionifanya nikakupigia , ninapanga kumleta mke wangu huko kwa ajili ya kufunga ndoa ,ijapokuwa nilioa lakini hakuna sherehe ambayo imefanyika”
“Mfalme Pluto nimefurahi kusikia hivyo, nipo tayari kusikiliza maagizo yako na kufanya maandalizi makubwa”Aliongea mwanaume anaeitwa Ron na Roma alianza kumuekeza kila kitu ambacho anatakiwa kufanya kwa sauti ndogo ikiwa kama siri.
“Kuhusu swala la Zawadi ninayopanga kwa ajili ya mke wangu nitamshirikisha Sauron pia kulifanyia hilo kazi”Aliongea Roma.
“Mfalme Pluto nitahakikisha maagizo yako yote yanafanyiwa kazi kwa wakati kabla ya siku ya tukio, raia wako watakuwa ni wenye furaha sana kumuona Malkia Perseephone”
“Asante sana Ron , wasalimie wote hapo kisiwani na nikutakie jioni njema”
“Asante sana Mtukufu Mfalme Pluto , na mimi nakutakia Asubuhi njema”Aliongea Ron na kisha akakata simu.
Roma mara baada ya kumaliza mlango wake ulifunguliwa na Edna alieonekana kujiandaa kabisa kwa ajili ya Kwenda kazini na Roma mara baada ya kumuona alimsogelea na kumkumbatia na Edna hakuleta ubishi, alikubali kukumbatia na mume wake huyo , hata hivyo alishaamua kumkubali kabisa hata kuolewa nae, Roma alishindwa kulala pamoja na Edna kutokana na usumbufu wa Lanlan kutaka kulala na mama yake hivyo Roma kwake haikumsumbua kulala mwenyewe na alijiambia siku ya ndoa yake ikifika Lanlan atalala kwenye chumba chake.
“Babe mbona unaniangalia hivyo?”Aliongea Roma mara baada ya Edna kuonekana kumwangalia Roma usoni kama mtu anaetafuta chunuzsi.
“Nimeona Habari ya Afande Kweka kukutangaza rasmi kama mjukuu wake kutoka kwa mtoto wake Raisi Senga”Aliongea Edna.
“Ndio kinachokupa wasiwasi?”
“Najaribu kusoma mawazo yako kwa kukuangalia usoni”Aliongea Edna kwa sauti ndogo na kumfanya Roma kutabasamu.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi lilikuwa swala la muda tu kutambulika hivyo nishakuwa mwanafamilia tayari”Aliongea Roma na Edna alivuta pumzi nyingi huku akionyesha huzuni kwenye macho yake jambo ambalo lilimfanya Roma kushangaa.
“Mbona umekua mnyonge ghafla?”
“Licha ya Raisi Senga kutokukutambua lakini kuna watu kama Afande Kweka wapo nyuma yako , wakiwa na hiari ya kukutangaza hadharani..”Aliongea Edna.
“Edna kuna jambo ambalo limetokea kati yako na raisi Jeremy?”Aliongea Roma huku akimshika Edna na kumkalisha kitandani.
Roma siku ya pili yake mara baada ya kurudi kutoka Marekani aliweza kupata taarifa juu ya kifo cha Kizwe, jambo ambalo hata halikumshangaza sana wala kujihangaisha nalo.
Kitendo cha Edna kuonyesha huzuni aliona kabisa ni juu ya swala la baba yake , kwani tokea siku agundue kuhusu Raisi Jeremy kuwa baba yake hakupata nafasi hata ya kuongea nae.
“Unakumbuka nilishawahi kukuelezea kuhusu mtu aliewahi kujitambulisha kwa jina la The Protector?”
“Ndio nakumbuka”
“Nilijaribu kutuma ujumbe wa meseji nikiwa na uhakika atakuwa raisi Jeremy , lakini nimesubiria majibu ni zaidi ya wiki mbili sasa”Aliongea Edna kinyongea na Roma alimwonea huruma , alishatambua kwamba Raisi Jeremy hana mpango wa kumtambua Edna kama mtoto wake.
“Edna niambie unataka kuongea na Raisi Jeremy ana kwa ana?”Aliuliza Roma na Edna alishindwa kutoa majibu lakini sura yake ilionyesha alikuwa na uhitaji huo , hata hivyo Roma alikuwa ashamsoma Edna muda mrefu tu , ni mtu ambaye si rahisi kupotezea mtu anaefamika kwa jina la ndugu yake, mfano halisi aliweza kupata juu ya hilo ni siku ambayo alitaka kumuua Ernest Komwe.
Hata hivo Roma aliona ni sahihi kutaka kumtambua baba yake , kwani Edna ni kama hakuwa na ndugu yoyote wa damu , ukiachana na wale wa upande wa mama ambao wapo nchini Marekani, mtu pekee ambaye Edna alikuwa amezoeana nae na kumuita kama ndugu ni Bi Wema , lakini licha ya hivyo uzito wa baba ulikuwa mkubwa mno.
Roma alijiambia hawezi kumsemea Raisi Jeremy kwa kumwambia Edna kwamba hakuwa na mpango wa kumtambua , aliona jambo la maana ni Raisi Jeremy mwenyewe kuongea na Edna na kama ataamua kumkataa awe mbele yake.
Roma alimuahidi Edna kuhakikisha anakutana na baba yake hata kama itakuwa ni kwenda nchini Rwanda.
Baada ya wote kwa pamoja kupata kifungua kinywa , Edna aliondoka kuelekea kazini na hivyo hivyo Roma aliweza kuondoka kuelekea kazini akiwa na Sophia ambaye alitakiwa kufika makao makuu kwa ajili ya kutengeneza shooting ya matangazo.
Roma aliweza kuingia kwenye jengo hilo la kampuni na kupokelewa na Daudi , Wendy pamoja na Amina ambaye ni kama alikuwa akifanya kazi zote za Roma., baada ya kufanya kikao cha muda mfupi katika ukumbi wa mikutano aliingia ndani ya ofisi yake akiwa ametangulizana na Amina.
Amina licha ya kufanya kazi kama Sekretari , alikuwa akifanya kazi pia kama mtangazaji ndani ya kituo cha Vexto Tv .
Kampuni ya Vexto Media ilikuwa imechangamka mno kutokana na uwepo wa wafanyakazi wengi.
“Babe Amina kuna kitu muhimu nataka tuzungumze”Aliongea Roma na kumfanya Amina kumwangalia Roma usoni kwa mshangao kidogo.
“Nipo tayari kukusikiliza mfalme wangu , huna haja ya kuweka uso wako namna hio”Aliongea Amina huku akitembea kimadaha na kwenda kukaa kwenye masofa kwa kukunja nne na kufanya mapaja yake yalionona kwenye suruali kuonekana vyema na kumfanya Roma aliesimama kuangalia mtikisiko na kutabasamu kifedhuli.
“Babe utajisikiaje kama nitakuambia kuna uwezekano wa kuendelea kuwa mzuti hivi hivi pasipo kuzeeka haraka?”Aliongea Roma na kumfanya Amina kushangaa kidogo.
“Ingekuwepo hio teknolojia ningefanya kila linalowezekana kuwa wa kwanza”Aliongea Amina pasipo ya kuchukulia maneno ya Roma Siriasi alijua alikuwa akitania tu.
Nasra na Amina ni wanawake pekee ambao hakuwahi kuwaonyesha upande wake wa pili m ijapokuwa Amina aliweza kugundua Roma hakuwa mtu wa kawaida kutokana na namna alivomuokoa na Fayezi nchini Japani, aliamini huenda Roma alikuwa tu na pesa pamoja na konekesheni.
Amina alikuwa tofauti na Rose ambaye ashawahi kuyashuhudia kabisa mabadiliko ya mwili ya Roma , alikuwa tofauti na Dorisi kwani alishawahi kumona Roma akibadilika nchini Japani , alikuwa tofauti na Edna kwani alishawahi kumuona Roma akibadilika macho na kuwa wa kurisha, alikuwa tofauti na Neema Luwazo kwani Neema alishawahi kushuhudia Roma akipigwa risasi na ikapona hapo hapo kwenye kusanyiko la wafanyabiashara, hivyo hivyo kwa Mage aliweza kumjua Roma kama mtu asiekuwa wa kawaida.
Hata hivyo Nasra pia aliamini Roma hakuwa wa kawaida aliamini alikuwa na historia ya maisha yake ya nyuma ambayo inaweza isiokuwa ya kawaida lakini kama ilivyokuwa kwa wengine wote Nasra na Amina wote walijiambia watampenda Roma hata abadilike na kuwa mdudu.
Kwahio kwa maneno marahisi huenda kati ya wanawake wote ambae hajaweza kushuhudia makubwa ni Nasra peke yake.
Roma hakutaka kuongea sana , bali alichokifanya ni kumuonyesha Amina kwa vitendo juu ya uwezo wake na zoezi rahisi ambalo alifanya ni kugandisha hawani mafaili yote yaliokuwa kwenye meza yake na kumfanya Amina kushangaa.
“Babe hii mbinu…”Kabla hajamaliza sentensi yake palepale simu yake ilianza kuita na alinyanyuka na kuichukua kwenye meza na alipoangalia jina la anaepiga ni Neema Luwazo alijikuta akiguna na kujiuliza kwanini mwanamke huyo akampigia muda huo , lakini hakujali sana alichokifanya ni kupokea na kuweka sikioni.
“Roma nahitaji msaada wako…”Sauti upande wa pili ilisikika ikiwa kwenye hali ya wasiwasi.
“Nipo tayari kukusaidia mrembo , kuna tatizo gani?”
“Unaweza kuja Maple Speed Vibe”Sauti ya Neema luwaza iliskika upande wa pili na kumfanya Roma kushindwa kuelewa maana ya Maple Speed Vibe , lakini ni kama Neema alijua Roma atashindwa kumuelewa hivyo alipatia maelezo mafupi na kumwambia kwamba aende Kisemvule.
“Babaa naona unaitwa kwingine , haya wahi uje kunielezea mazingaombwe ulioyafanya hapa”Aliongea Amina na kumfanya Roma kumkonyeza.
“Tutaongea baadae” Aliongea Roma na kisha alitoweka kwenye ofisi hio huku akimwacha Amina akivuta mdomo.
Dakika arobaini na tano tu alikuwa ndani ya Kisemvule na alipewa maagizo ya kuendelea mbele kuipita stendi ya daladala na ataona bango kubwa la Maple Speed na Roma aliendesha kama nusu kilomita tu hivi aliweza kuona bango hilo ambalo lilikuwa na mshale uliokuwa ukimwelekeza kuingiza gari kushoto mwa barabara.
Roma bila hata ya kufika eneo husika alishajua Maple Speed ni lazima itakuwa sehemu ya uwanja wa mbio za magari maarufu kama Formula one Racing, hata yeye mwenyewe alishangazwa na uwepo wa hili eneo kwani alidhania ndani ya jiji hili mashindano ya mbio za magari hayakupewa kipaumbele sana kama nchi zilizoendelea mfano wa Abu Dhabi na Marekani.
Dakika chache mbele alifika kwenye kizuizi na kuruhusiwa kupita na kuingia eneo ambalo lilikuwa na mandhari nzuri mno kwa jinsi ilivyopendezeshwa na bustani, huku mbele yake akiona jengo kubwa la gorofa kama tatu hivi refu kwenda mbele.
Baada ya kufika mbele kabisa ya jengo hilo aliweza kumuona Neema aliekuwa amesimama akiwa amevalia gauni flani la rangi nyeupe ya mua maua na viatu vya rangi nyeusi huku akiwa ameshikilia mkoba , baada ya kuiona gari ya Roma aliipungia mkono na kuisimamisha huku akiwa na tabasamu.
Roma mara baada ya kutoka alijikuta akishangaa , ijapokuwa eneo hilo halikuwa zuri sana kama baadhi ya maeneo ya mashindano ya magari kama Dubai na Marekani lakini kuwepo kwa eneo hilo ndani ya jii hili la Tanzania ilikuwa ni hatua kubwa.
“Sikudhania Tanzania kuwa na eneo kama hili , hongera kwa uwekezaji mkubwa kwenye mashindano ya magari”Aliongea Roma kwa kutabaamu huku akikagua eneo lote.
Ni eneo ambalo lilikuwa limejengwa barabara za Rami maalumu kwa ajili ya mashindano ya magari ya formula one , kulikuwa na barabara za aina mbili, ya kwanza ilikuwa ni ya magari ya F1 na nyingine Roma kwa kuiangalia tu ilikuwa ni ya magari ya kawaida kwa ajili ya mashindano , huku mbele ya eneo hilo kukiwa na jengo kubwa ambalo lilionekana kama maalumu kwa ajili ya watazamaji pamoja na ‘Timing’.
Eneo lote lilikuwa la tambalae ambalo ni rahisi kuona magari yakiwa yanakimbia katika mizunguko ya barabara.
“Asante sana, Tanzania kwa sasa inapanuka hatuwezi kuangalia mambo haya kuwa kwenye nchi zilizoendelea tu , naweza kusema huu ndio uwekezaji mkubwa ambao nishawahi kufanya”Aliongea Neema mara baada ya kusalimiana kawaida na Neema kutokana na uwepo wa baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakiwazunguka.
“Imekugharimu kiasi gani kujenga hili eneo?”Aliuliza Roma.
“Hapa nilijenga kwa kushirikiana na kampuni ya Toyota ikiwa na hisa asilimia arobaini jumla ya ujenzi wote ni bilioni mia tatu za kitanzania”Aliongea Neema huku wakitembea kuelekea mbele.
Neema alikuwa amependeza kweli , ijapokuwa alikuwa mtu mzima lakini staili ya nywele fupi ilimpendezesha mno huku mwili wake ulionenepa kimpangilio ukimfanya kuonekana kijana.
“Hujaniambia kipi unataka nikusaidie”Aliongea Roma kabla hawajafikia mlango na Neema alisimama.
“Yaani hata sijui kama utaweza kunisaidia , nipo na mdogo wangu wa hiari, mtoto wa Mzee Chino anafahamika kwa jina la Msechu leo asubuhi nilimwazima gari yangu mpya kabisa ya Volkswagen , sasa nipo kazini ananipigia simu anasema gari kaibetia na imehukuliwa”
“Kaibetia kivipi?”
“Kuna moja ya mwendesha magari kutoka Indonesia alikuwa akilala kwenye hoteli yangu, baada ya kukutana na Msechu ndio wakaweka dili la kushindana kuendesha magari kwa mzunguko mmoja, Msechu kaweka gari yangu kama rehani na Mwindonesia kaweka kiasi cha pesa na Msechu alipoteza pambano hivyo gari kuwa chini ya umiliki wa Mwindonesia”Aliongea Neema.
“Nimefikiria namna ya kutatua tatizo hili na kukomboa gari yangu na nafsi yangu imeniambia ni wewe pekee unaeweza kunisaidia kushindana upya na Mwindonesia, sikuwa na uhakika sana nilivyokupigia lakini gari yangu sitaki kuipoteza kwani nimetoa pesa nyingi kuinunua , sina uhakika kama unaweza kuikomboa lakini naamini kuna vitu vingi unavyoweza kufanya ndio maana nikakufikiria kwenye wakati kama huu”Aliongea huku akionyesha huzuni na Roma aliamini huenda gari hio Neema anaipenda sana.
“Okey! Usiwe na wasiwasi nitahakikisha gari yako inarudi kwenye mikono yako”Aliongea Roma na Neema alitabasamu.
“Ni kuonyeshe kwanza magari ya kuchagua au unataka ukutane kwanza na mshindani wako?”Aliuliza.
“Shida yangu sio mshindani , shida ninayotaka kuangalia kwanza ni gari yake anayotumia , hivyo ni vyema kama nitaiona kwanza”Aliongea .
“Kama ni hivyo basi wapo upande ule wanatusubiria”Aliongea Neema na kisha akaanza kutembea kuelekea upande wa nyuma wa jengo hilo ambapo kuna sehemu iliojengewa kwa ajili ya mapumziko.
“Unamdekeza sana mdogo wako , ilikuwaje ukampa gari muhimu kwako na ghali kiasi hicho na akaja kuibetia”
“Nashindwa hata nikueleze vipi , aliniomba gari akatembee asubuhi lakini nashangaa mtu ananipigia simu kwa wasiwasi ananiambia gari kaipoteza kwa Mwindonesia , nilikasirika sana lakini Msechu ni mtu mzima na gari kaipoteza sikua kwenye nafasi ya kumlalamikia bali kurudisha gari yangu”Aliongea na Roma hakutaka kuuliza sana
Baada ya kufika upande wa nyuma hatimae Roma aliweza kuona watu watano wakiwa wamesimama huku wakiongea kwa kucheka huku mwingine akiwa amekaa chini akiwa na huzuni , kwa haraka haraka Roma alitabambua aliekaa atakuwa Msechu lakini sasa ile anawakaribia alijikuta akishangaa kumuona Desmond ndani ya eneo hilo tena akionekana kuwa wa kawaida kama vile hakuna ambacho kimetokea.
Desmond mwenyewe alishangazwa na ujio wa Roma ndani ya eneo hilo , wengine waliokuwepo ni Elvice , Abubakari, Msechu , Mwarabu ambaye amevalia nguo za kushindania kuendesha mbio za magari na mwingine Roma alikuwa ni bwana mweusi mfupi lakini alievalia nguo za bei ghali.