Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 434.

Ilionekana hata Rose alikuwa akijua swala la Clellia Allisanto kwani hakuonyesha mshangao wowote na hata Roma alitambua Rose alikuwa akifahamu lakini alishangaa kwanini Dorisi hakuweka wazi swala hilo kwake .

Dorisi ilibidi amuelezee Roma kwa kila kitu kilichotokea , jinsi alivyorudi nyumbani kwake na kumkuta mwanamke ndani ya nyumba yake , mwanamke ambaye alijitambulisha kwa jina la Clellia Allisanto.

Mpaka Dorisi anamaliza kusimulia Roma ilimshangaza sana na kujiuliza huyu Clallia Allisanto alikuwa akimtakia nini mpaka kuanza kuzungumza na Dorisi maswala ya kuzaa nae , swala hili lilimshangaza na kumchanganya kwa wakati mmoja , lakini alishangaa zaidi mara baada ya Clellia Allisanto kuweza kutaja jina la Naira ambaye alikuwa rafiki wa utotoni wa Dorisi.

Roma palepale alijikuta kuna swala likimjjia akilini hapo hapo na ni kama alianza kupata majibu ya kile ambacho alikuwa akijiuliza tokea Edna alivyokutana na huyu Clelia Allisanto.

“Nafikiri stori yako inatengeneza ukweli ambao ulikuwa ukiutafuta”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi kumwangalia mpenzi wake kwa wasiwasi.

“Ukweli wa… Unazungumzia Black Card?”Aliuliza Dorisi akiwa kumbukumbu zake sasa zikikaa sawa na Roma alitingisha kichwa.

Ilibidi Rose aeleweshwe kidogo kuhusu Black Card ili aweze kuelewa kile kinachozungumziwa na alijikuta akishangaa mara baada ya kusikia Dorisi alikuwa na kadi ya benki ambayo ilikuwa na uwezo wa kutoa mabilioni ya hela benki , maelezo hayo ni kama hayakuwa ya kuaminika kabisa kwake lakini kilichomshangaza zaidi ni Roma kusema kadi hio imeunganishwa na akaunti ya benki ya The Doni.

Ilikuwa rahisi sana kugundua Dorisi alikuwa akimiliki Black Card kadi ambayo akaunti yake ya banki inamilikiwa na The Doni ambaye ni Athena lakini Clelia huyo huyo akamtembelea Dorisi na kutaja jina la Naira rafiki wa utotoni wa Dorisi hivyo kwa haraka haraka ni kwamba Clelia ndio Athena.

“Dorisi umesema alikuonyesha picha?”

“Ndio alinionyesha picha akiwa amepiga na Naira kwenye mapozi tofauti tofauti , lakini sehemu moja , walionekana kama wapo kwenye chumba cha hospitali au maabara , lakini sehemu ya kisasa zaidi”Aliongea Dorisi na kumfanya Roma kutabasamu.

“Kuna namna moja ya kumtambua Clalia , ile picha ya Naira si upo nayo?”Aliuliza Roma na Dorisi aliitikia kwa kichwa na Roma akampa ishara ya kumwambia akailete na Dorisi alitii haraka sana na kupandisha ngazi na kushuka na picha ile na Roma alimwangalia Naira aliekuwa kwenye picha hio.

Ukweli Roma hata mara ya kwanza alivyoona hio picha kuna kitu kilimwambia huyo mtoto hakuwa kabisa wa kawaida, hakuelewa kwanini alikuwa akimuona kama sio wa kawaida.

Roma alitoa simu yake na kisha kuipiga picha na kumrudishia Dorisi na baada ya kumaliza alitafuta tena namba ya Makedoni.

“Mfalme Pluto unanipigia tena”Ilisikika sauti ya Makedoni upande wa pili lakini waliongea kwa lugha ya kihebrew.

“Nataka ujaribu kutafuta jina la Naira Ryani , nakutumia picha yake kama jina halitokuwa kwenye mfumo wenu wa taarifa kwa teknolojia ambayo Israeli mnayo , haitashindikana kutoweza kupata taarifa zake”Aliongea Roma kwa kiebrania na kuwafanya Rose na Dorisi kuangaliana na kutabasamu.

“Mfalme Pluto nipe dakika moja , nitumie kabisa hio picha kwa Email nitakurudia mara baada ya kupata majibu”Aliongea na Roma alikata simu na kisha akatuma kwa njia ya email ile picha.

“Hubby hio ni lugha gani uliokuwa ukiongea?”Aliuliza Rose. Na kumfanya Roma kutabasamu.

“Ni Hebrew(Kiebrania)”Alijibu Dorisi na kumfanya Roma kutabasamu lakini Rose kushangaa.

“Dorisi unaonekana kukijua kiebrania?”

“Sijui kuzungumza lakini matamshi ya kiebrania nayajua”

“Hubby ilionekana uliishi sehemu nyingi za dunia , uliwezaje kujua lugha ya kiebrania?”

“Mpenzi wako nina historia ndefu sana”Aliongea Roma.

“Nakumbuka wakati unaanza kuja kwenye usaili tulishangazwa na uwezo wako wa kuzungumza lugha nyingi nadhani ndio kigezo kilichotufanya kukupatia kazi , licha ya kwamba maswali mengi ulijibu”Aliongea Dorisi na kumkumbusha Roma kipindi kile.

“Hahah.. Hubby nasikia mkeo alikuacha njiani ukiwa huna hata mia ndio ukaweza kukutana na Dorisi kwa mara ya kwanza na kumuomba hela ya nauli”Aliongea Rose huku akishindwa kuzuia kicheko.

“Naweza kusema kila mmoja wenu nimeweza kukutana nae kwa mtindo wa aina yake”Aliongea Roma huku akianza kukumbuka namna ambavyo aliweza kukutana na Edna mke wake.

Dorisi na Rose walionekana kucheka sana mara Roma alipowaeleza namna ambavyo alianza mahusiano na Nasra hawakuamini kama Nasra alianza kuvuliwa nguo na kubakia uchi bila kujielewa.

Wakati wakiendeleza stori Roma aliweza kupokea simu kutoka kwa Makedoni na kuweka sikioni .

“Mfalme Pluto nimejaribu kutafuta jina Naira Ryani na nimegundua taarifa ambayo sio ya kawaida”.

“Unamaanisha nini taarifa isiokuwa ya kawaida?”

“Kwanza namna ya kuupata ukweli ilikuwa ngumu kidogo , kwani inaonekana taarifa zinazohusiana na huyu Naira ni Top Confidential ndani ya serikali ya Marekani , nimejaribu kuomba ‘Clearence’ kutumia koneksheni zangu na kuweza ku access faili linalohusiana nae , lakini nilichopata kimeniacha mdomo wazi”

“Unanipa shauku Makedoni hebu nielezee ulichoweza kufahamu”

“Naira ni mtoto wa marehemu Ryan Kennedy , Agent mbobevu aliekuwa chini ya kitengo cha CIA chini ya idara ya SID ,mwaka 1990 taarifa zilionyesha Ryan Kennedy alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani na alikuja kupatikana mwaka 2005 , nikatafuta kwa haraka haraka kwanini Ryan alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani ndipo nilipoweza kupata faili la siri sana ambalo lilinishangaza”Aliongea

“Faili linahusiana na nini?”

“Project Pro Human”Aliongea Makedon na kumfanya Roma kukumbuka kitu lakini hakutaka kwanza kuingilia maongezi ya Makedon.

“Project Pro human kwa taarifa hapa nilizonazo inaonekana ilifanyikia ndani ya taifa la Bolivia kwenye msitu wa Amazoni kilomita kadhaa kutoka La paz , ni project ambayo ilianzishwa kwa siri sana na muuza madawa ya kulevya maarufu kutoka Mexico , mfalme Pluto ngoja nikutumie faili kwa njia salama uweze kujisomea mwenyewe”Aliongea Makedoni na Roma alikubali na ndani ya dakika chache tu faili liliweza kumfikia na alifungua na kuanza kusoma na alijikuta akikunja sura .

Ndio kama unakumbuka vizuri Project Pro human iliofanyika nchini Bolivia basi ndio taarifa ambayo alikuwa akisoma Roma , hakukuwa na utofauti mkubwa , Roma aliweza kukumbuka vitu viwili baada ya kusoma ripoti hio , kwanza kabisa ni stori ya Mellisa Luiz , mwanamama ambaye aliwahi kukutana nae ndani ya hoteli ya Kilimanjaro na kumuelezea kila kilichomtokea mpaka kujikuta kuwa na tatoo kwenye mwili wake ambayo ni kama uraia wa visiwa vya wafu, kitu kingine Roma alichoweza kukumbuka ni Carlos ambaye mpaka muda huo anaofikiria alikuwa ni raia wa visiwa vya wafu , alikumbuka kuna kupindi wakati akiwasiliana na Sauroni alimwambia kwamba walikuwa ndani ya jiji la Palermo Italy kwa ajili ya kumuokoa Carlos ambaye alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani.

Dorisi alimwangalia Roma kwa wasiwasi na kutaka kujua ni kipi ameweza kufahamu.

“Roma umeweza kufahamu nini?”Aliuliza Dorisi na ilibidi Roma ampatie simu yake aweze kusoma mwenyewe , hakuwa na haja ya kumficha.

Dorisi kadri alivyokuwa akisoma alijikuta mikono yake ikianza kutetema huku macho yakiongezeka ukubwa , ni kama alichokuwa akiangalia kwenye karatasi hio lilikuwa jambo la kuogopesha sana.

“Rafiki yako hakuwa wa kawaida Dorisi”Aliongea Roma lakini Dorisi alionekawa kufikiria sana, ilibidi na Rose aweze kusoma faili lakini hata hivyo hakuelewa sana kilichozungumziwa.

“Mama na baba itakuwa walikuwa wanafahamu hili ndio maaa ,,, ndio maana,..”Aliongea Dorisi huku akianza kutokwa na machozi.

“Dorisi unaongea nini, kwanini useme hivyo?”

“Licha ya kwamba nilikuwa mdogo lakini nilikuwa nikielewa maisha ya wazazi wa Naira yalikuwa ni ya kujificha sana . Naira hakuruhusiwa hata kuonekana onekana mtaani na mara nyingi tulicheza ndani ya geti na hata shule hakupelekwa…”

Ni kweli kabisa Naira hakusoma wakati alivyokuwa hapa nchini na wazazi wake hawakuwa na maelezo ya moja kwa moja kwanini Naira hakuwa akieonda shule licha ya kuwa na umri mkubwa.

Naira alimzidi Dorisi kwa takribani miaka minne , hivyo ni rahisi kusema Naira alikuwa dada kwa Dorisi tokea kipindi anazaliwa huko jijini Arusha na kwakuwa familia ya Dorisi na ya Ryani na mke wake Epholia walikuwa na ukaribu , hivyo ni kama waliishi kama ndugu na ndio maana wakati Dorisi ni kichanga alikuwa akilelewa na Naira mpaka Dorisi anakuja kuwa mkubwa wa miaka sita mlezi wake mkubwa alikuwa ni Naira , ni kama walikuwa kitu na mdogo wake na Naira alitokea kumpenda sana Dorisi kama mdogo wake.

Lakini jambo la kushangaza ni kwamba licha ya Dorisi kuanza shule upande wa Naira hakuwa amehudhuria kabisa masomo na jukumu la elimu yake lilibakia kwa wazazi wake , lakini licha ya hivyo Naira alikuwa ni moto wa kuotea mbali kwani alikuwa na kichwa chepesi mno kuliko binadamu wa kawaida , ilifikia kipindi hata hakupenda kabisa kufundishwa na wazazi wake na alichohitaji ni vitabu na sio kufundishwa..

Watu hawakuuliza sana maswali ya kwanini Naira hakuchangamana na watu wengine na yote hio ni kutokana alikuwa mtoto wa kizungu na watu hawakuwa wenye kuhoji sana kwani watoto wa kitanzania walikuwa waoga sana kila walipomuona Naira , lakini pia Naira hakuwapenda kutokana na kwamba akili yake ilikuwa ikipevukwa haraka sana , hivvyo ilikuwa ngumu sana kumwambia acheze na watoto ambao akili zao zilikuwa zikipevuka taratibu sana , hivyo maisha ya Naira yaliishia kuwa ya kipweke na mtu aliechangamana nae alikuwa ni Dorisi na hilo ni kutokana alimchukulia kama mdogo wake.

Kipindi Dorisi ndio anaaanza kujitambua ndipo Naira aliweza kuondoka na wazazi wake lakini ndio ambapo Ryani na Epholia walipoweza kumpoteza Naira wakati Naira akikaribia miaka kumi.

Naira alichukuliwa na Athena na kupelekwa makao makuu ya Zeros organisatioa na ni huko ambako Naira aliweza kupata elimu yake ambayo haikuwa rasmi ya chuo , lakini kutokana na uwezo wake usio wa kawaida aliweza kuwa msaada mkubwa sana hata kufumbua baadhi ya mafumbo ya mpango LADO.

Hivyo ni rahisi kusema Naira alishawahi kushiriki kwenye mpango LADO kama mwanasayansi ijapokuwa mpango huo wakati unaaza hakuwepo.

Huenda pia ikawa kweli kupotea kwa wazazi wa Dorisi ni kutokana na kujua historia iliokuwa nyuma ya Naira.

Roma alifikiria swala hilo kwa mantiki na kuona ni jambo ambalo linawezekana na kilichobakia ni kutafuta uthibitisho tu kama kweli wazazi wa Naira walikufa kwasababu walikuwa wakiujua ukweli kuhusu Naira.

“Dorisi kwasasa hupaswi kua na huzuni nakuahidi nitachimba na kuujua ukweli wote”

“Lakini Hubby kama hayo yote ni ya kweli inamaanisha huyu Naira sio wa kawaida na ni jambo la kuwezekana kwa Naira kuwa na urafiki na The Doni”

“Upo sahihi lakini siamini kama huo ndio ukweli wote , kuna sababu kubwa za The Doni kumfanya Naira rafiki yake , huenda anamtumia kwenye mipango yake”Aliongea.

“Unasema Naira atakuwa hatarini?”

“Kwasasa anaweza kuwa salama lakini baadae anaweza kuwa hatarini”Aliongea Roma na kisha Roma alipiga tena simu kwenda kwa Sauroni.

“Mfalme Pluto nadhani hata wewe umeshangaa”

“Naweza kusema hivyo , lakini dunia ni pana sana na yanayoendelea ni mengi hivyo nishazoea, Nataka unisaidie kuangalia ni eneo gani ambalo Naia yupo kwa sasa”Aliongea Roma.

“Hilo nafanyia kazi , lakini taarifa hapa inaonyesha wazazi wake walimpoteza na hawakuweza kufanikiwa kumpata tena , mfalme Pluto hii ni taarifa kubwa nadhani nitakupatia majibu nikipata chochote”Aliongea na Roma alikubali.

Muda ulikuwa umeenda hivyo Roma aliaga kuondoka huku akihidi akirudi China ataendelea kufatili habari zaidi za Naira pamoja na Clielia Allisanto

Ni asubuhi Roma mara baada tu ya kuamka alitafuta namba ya Profesa Clark ili kujua ana majibu ambayo amepata kwani juzi yake kupitia Sauroni aliweza kumpatia kazi ya kumtafuta Yan Buwen ni wapi alikuwa akifanyia mawasiliano.

“Umepata majibu?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Profesa ambaye alikuwa akiachama kuonekana alikuwa na usingizi.

“Ndio inaonyesha alifanya mawasiliano akiwa Beijing China sijui ni upande upi lakini mwelekeo ni upande wa Kaskazini magharibi sijaweza ku’pin point’ sehemu kwani ‘IP adress’ aliotumia sio ya kawaida lakini nina uhakika anahusika hakuna mtu wa kuweza kufanikisha jambo hili tofauti na Yan Buwen”Aliongea Clark.

“Inaonekana kweli aliweza kuondoka hapa nchini muda mrefu”Aliongea Roma.

“Roma unafikiria kufanya iin juu ya hili, maana kila nikifikiria Yan Buwen kuweza kufanikisha kutengeneza kopi yake inanifanya kuamini ni hatari sana”Aliogea Profesa.

“Ndio maana nataka niende China , naamini kuna maabara huo upande wa Kaskazini magharibi”Aliongea Roma.
 
SEHEMU YA 435.

Roma mara baada ya kumaliza kuwasiliana na Profesa Clark alisalimiana na familia yake pasipo kumsahau Lanlan.

Ukweli kadri alivyokuwa akimuona Lanlan ndani ya nyumba ni kama alikuwa akipata nguvu zaidi ya kupambana na kumlinda kwa namna yoyote ile , alishaamua kumlea yeye na Edna hivyo alikuwa na jukumu la kumpa maisha mazuri baadae.

“Ukirudi nataka tukamwandikishe Lanlan aanze masomo”Aliongea Edna mara baada ya kumaliza kunywa chai na Roma aliona ni kweli alichokuwa akiongea Edna kwani ni mwezi wa pili ulikuwa ukikaribia.

“Nitachukua siku mbili kwenda na kurudi na nitapata majibu baada ya hapo , nikirudi tutaenda wote kumpeleka shule”Aliongea Roma n Aedna alionekana kuridhika , alimwinamia Lanlan na kumbusu kichwani na kisha akaondoka huku Blandiina mama yake akimwambia awe makini.

Roma safari yake ya kwanza ilikuwa ni kwenda kwenye kampuni ya Vexto Media kwanza kutokana na Amina kwenda kumsaidia baba yake baadhi ya majukumu kwenye kampuni yao.

Roma mara baada ya kufika kwenye kampuni alishangazwa na uwepo wa Tanya akimsubiria eneo la mapokezi kwani hakuwa na taarifa kama amefika nchini,alisalimiana kwanza na Daudi na baadhi ya wafanyakazi wengine na kisha moja kwa moja alielekea ofisini kwake huku akimpa ishara ya Tanya kumfuata.

Roma alimpa maelezo Tanya baadhi ya Yamata Sect kufika Tanzania kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kutokana na kwamba aliona wangekuwa na uwezo mkubwa kuliko wanajeshi wake ili hata ikitokea kopi yake ikivamia watu wake wa karibu kidogo kuwe na asilimia za usalama.

Sasa Roma hakutarajia kama Tanya angeweza kufika mwenyewe nchini Tanzania.

“Mmeingiaje Tanzania?”Aliuliza Roma mara baada ya kuketi kwenye kiti chake cha kibosi.

“Mfalme Pluto , tumeingia kama wafanyakazi wa mradi kutoka Japani”Aliongea Tanya na kumfanya Roma kutabasamu.

“Okey napanga kwenda China kumtafuta Yan Buwen , lakini taarifa za mwanzo zinaonyesha alifanya mawasiliano upande wa Kaskazini magharibi , je kutakuwa na eneo upande huo ambalo kuna maabara?”Aliuliza Roma.

“Ndio kuna maabara ya muda mrefu ya kisasa ambayo ipo msituni kwenye kambi ya kijeshi , nadhani huenda ndio hio, kuna kipindi tulishawahi kufanya misheni eneo hiloo”Aliongea Tanya na kumfanya Roma kuhisi huenda Yan Buwen kafanya mawasiliano kupitia hilo eneo.

“Nadhani linaweza kuwa hilo eneo , ila uhakika wa moja kwa moja sina , nitajua namna ya kumpata tu”Aliongea Roma.

“Mfalme Pluto naamini hata mimi utampata Yan Buwen na utamuangamiza , siamini kama uwezo wake ni mkubwa kuliko wako”Aliongea Tanya na kumfanya Roma kushangazwa na maneno ya Tanya kuonyesha kumuamini..

“Una amini hivyo?”

“Ndio Mfalme Pluto , Naamini uwezo wako ni mkubwa sana na Yan Buwen amechokoza moto”.

“Okey ni kheri kwamba unaniamini, kwasababu ushafika hapa Tanzania nataka unisaidie na baadhi ya majukumu yangu hapa ofisini , nilikuwa na msaidizi lakini biashaara za familia yake zinamuhitaji zaidi nadhani utaweza kufanikisha baadhi ya majukumu”Aliongea Roma.

“Ndio Mfalme Pluto nitahakikisha nakusaidia majukumu yote , mpaka utakaporudi na ukitaka niendelee kuishi hapa Tanzania kwa ajili yako nipo tayari ”Aliongea Tanya na kumfanya Roma kutungisha kichwa hata hivyo Tanya siku hio alikuwa amependeza kuliko siku zote , alivalia kibosi kidogo na hakuonekana kama Ninja wa kudni la Yamata Sect , alionekana alikuwa akitendea vyema nafasi yake ya ubosi ndani ya kundi.

Muda huo huo Roma akiwa anaongea na Tanya mlango wake uligongwa na Roma alimpa ishara ya kufungua na alionekana Omari Tozo alievalia tisheti na Jeans akiingia hapo ndani huku akiwa na shauku kubwa, kwa kumwangalia tu Roma alijua Omari atakuwa na taarifa juu ya yeye kupambana na Clone yake.

Omari alimwangalia kwanza Tanya kwa namna ya kumchunguza urembo wake na kisha akamwangalia Roma na kwa jinsi alivyonekana ni kama alikuwa akiambia akili yake Hades ameshindikana , lakini hata hivyo Roma alijua hakuna ukweli wowote wa kile anachofikiria Omari kwani Tanya ni mfanyakazi wake tu ndani ya kundi la Yamata Sect.

“Master nitaenda kuendelea na majukumu , kama kuna lolote utaniambia”Aliongea Tanya.

“Unaweza ukaanza hata kesho , nitawasiliana na Amina aje akuelekeze baadhi ya kazi zilizokuwa zikifanyika”Aliongea Roma.

“Nitaanza leo leo Master nimekuja hapa nchini kukusaidia na sio kustarehe”Aliongea na Roma hakutaka kumzuia kama alikuwa na nia ya kufanya kazi siku hio hio , hata hivyo Tanya alionekana akijitahidi sana kumfurahisha tokea amuokoe kwa bosi wake Noriko Okawa ambaye alikuwa akimnyanyasa Kingono , itoshe pia kusema Tanya alikuwa amelelewa maisha tofauti na wanawake wengine , yeye alilelewa kutii hivyo ni ngumu sana kumtoa kwenye jambo ambalo linamwambia anachokifanya ni kwa ajili ya bosi wake.

“Vipi umekuja hapa kwa ajili ya kunielezea maendeleo ya hatua uliopiga kwenye mahusiano yako?”Aliuliza Roma kiutani mara baada ya Tanya kutoka.

“Huenda ningekuwa na uwezo mkubwa kama wewe angekuwa tayari yupo kwenye himaya yangu , nipo hapa baada ya kusikia habari za mapambano yako na kopi yako”Aliongea na kumfanya Roma kukunja sura hakuamini Omari angeweza kupata taarifa zake mapema hivyo , lakini hakushangaa pia kwani bwana huyo alikuwa akifanya kazi ndani ya kitengo cha usalama wa taifa hivyo macho yake siku zote yalikuwa ni juu ya Yan Buwen , huenda waliamini ili kumpata Yan Buwen ni kumfatilia Roma.

“Kwahio kilicho kuleta ni kuthibitisha kama kuna kopi yangu au kuna lingine?”

“Kuna lingine, wote tunamfatilia Yan Buwen hivyo kila hatua ninayofikia lazime nikupe mrejesho , huenda nikakurahishia kazi”Aliongea Omari huku akikaa kwenye masofa.

“Haya nielezee ulichongundua , nadhani sasa hivi unaonekana hata mshangao wa kuona maabara ya kisasa umekwishia na akili yako inafanya kazi vizuri”.

“Kuna haja gani ya kuzungumzia yaliopita , ilikuwa ni haki yangu kushangaa kwani ni mara yangu ya kwanza kuona sehemu nzuri kama ile”

“Okey acha kulalamika , niambia kilichokuleta ofisini kwangu maana ninataka kwenda China”

“Kama ni kumfuata Yan Buwen China haitokuwa rahisi kumpata , nimeshafanya mawasiliano kuona kama kuna uwezekano wa kuwepo kwenye moja wapo za maabara za kijeshi , lakini ripoti niliopata inaonyesha Yan Buwen sababu ya kuja kuweka kambi Tanzania ni kutokana na kufukuzwa China”Aliongea Omari.

“Hilo linawezekana na nimelifikiria , kama ulivyosema Hongmeng wanahofia uwepo wa Yan Buwen ndani ya China hivyo ni lazima viongozi wa ju wa kiserikali kumfukuza”Aliongea Roma.

“Kama unafahamu hilo kwanini bado unahitaji kwenda China?”

“Yan Buwen anaweza akawa amefukuzwa China lakini haimaanishi kwa uwezo aliokuwa nao sasa hivi akaogopa kukaa China, nitampata tu hata kama itanilazimu kuisambaratisha familia yake yote kama hatajionyesha kwangu”

“Huwezi kufanya hivyo Roma , utajisababishia uhasama na taifa la China , familia ya Yan Buwen ni moja wapo ya familia zenye nguvu ndani ya taifa hilo licha ya kwamba hawana muungano wa moja kwa moja na Hongmeng”

“Nimekuelezea ninachopanga kufanya na sio kuomba ushauri wako , yeye ndio kanianza hivyo hata nikimaliza familia yake hakuna wa kunizuia”Aliongea Roma huku akiweka uso siriasi kwenye macho yake.

Baada ya dakika kadhaa mbele ya Omari kuondoka Roma alimpa maagizo Tanya kuhakikisha anawasiliana na Ninja waliopo China kumpatia uelekeo wa sehemu familia ya Yan Buwen inapoishi , Roma aliamini njia moja ya kumpata Yan Buwen ni kupitia familia yake.

********

Ukoo wa Yan nchini China ulikuwa ukipatikana kusini mwa jiji la Beijig , jumba lilionekana kujengwa miaka mingi nyuma lilizungukwa na ukuta mkubwa wa mawe kwa nje ambao mimea flani ya kutambaa yalikuwa yameuziba kiasi cha kufanya kuonekana wote wa kijani.

Ndani ya jumba hilo walinzi waliovalia mavazi ya suti pamoja na siraha nzito za moto walionekana wakizunguka huku na huko wakihakikisha ulinzi , walionekana ni kama vile walikuwa kwenye tishio la hatari kwa namna ambavyo walikuwa makini.

Sasa muda wa saa mbili na nusu za usiku ndio Roma alipotua ndani ya hili eneo, ndani kabisa kiasi kwamba aliwashtua walinzi kwanni hawakuelewa namna alivyoingia.

“Wewe ni nani?” walinzi wale walikoki siraha zao na kumwelekezea Roma ambaye ndio kwanza kafika hapo kutokea Tanzania kwa kutumia mbinu zake za kijini, Roma hakuogopa tena kusafiri kwa umbali mrefu kwa njia za kuteleport kwani tayari alishapitia mapigo tisa ya mpangilio wa radi, hivyo hakuwa na hofu tena na alihakikisha anatii sheria zote ili asilikasirishe anga.

Zaidi ya Askari therathini wa ki ulinzi walikusanyika mara baada ya mwenzao kutoa makelele ya kuvamiwa na mtu mweusi.

Licha ya mmoja wao kuuliza yeye ni nani , hakuonyesha haja kabisa ya kujibu na wawili kati yao pasipo ya kutumia siraha walimsogelea kwa kasi kwa namna ya kumshambulia kwa ngumu , lakini Roma pasipo ya kusogea aliinua mkono wake na kuwakinga na lakini nguvu kidogo aliotumia iliwafanya kurudishwa nyuma na kwenda kujipigiza kwenye sanamu lililokuwa ndani ya hilo eneo.

Ilikuwa usiku lakini giza halikumzuia kutoyaona mazingira yote , walinzi wale mara baada ya kumuona mtu huyu mweusi alieingia hapo ndani kuwa tishio kwao kwa namna ambavyo aliwadhibiti wenzao walianza kumshambulia kwa risasi mfululizo , lakini risasi zote ziliiishia kudondoka chini pasipo ya kumfikia.

Milio ile ya bunduki ilikurupusha familia nzima iliokuwa ndani na kwa maelezo ya kundi la Yamata inasemekeana siku hio ukoo mzima ulikuwa na kikao cha kifamilia huenda ndio maana hata walinzi walikuwa wengi.

Alionekana mzee mmoja wa kichina akitoka akiwa na nguo za kulalia huku nyuma yake akiwa anafuatiwa na wajukuu na watu wazima wanawake na wanaume, jambo hilo lilimfurahisha Roma kweli, kwani alijiambia kama ataua mmoja mmoja hapo ndani anao uhakika lazima Yan Buwen atajitokeza.

Wote walimwangalia Roma kwa wasiwasi , pamoja na walinzi ambao walionekana kumshangaa mwanaume aliewavamia kwani hakuna risasi waliorusha ambayo ilionekana kufanya kazi mbele yake.

“Wewe ndio Roma Ramoni?”Aliuliza yule mzee wa kichina kwa lugha ya kingereza”

“Na wewe ni Yan Qintiang?”Aliuliza Roma kwa lugha ya kimandarini na kufanya yule mzee kukunja sura kidogo.

Roma hakutegemea kwa mzee kama huyo kumfahamu , alijua huenda Yan Buwen amewatahadharisha ujio wake , ndio maana wakamfahamu.

“Mh! Inaonekana huna hata heshima kwa wakubwa , umekuja ndani ya nchi yetu na kuingia nyumbani kwangu na kuanza kuchafua Amani , unajiamini kwa lipi?”Aliongea yule Mzee.

“Sijaja hapa kusikiliza malalamishi yako ya kipuuzi ilihali unaonekana kufahamu kilichonileta , ninachotaka ni kujua mjukuu wako asie na thamani anaefahamika kwa jina la Yan Buen yuko wapi?”Aliongea Roma.

Yan Qintian kwa maelezo ya Tanya ni kwmaba alikuwa ndio kiongozi mkubwa na alikuwa ndio babu wa familai hio, alikuwa mfanyabaishara mkubwa lakini asilimia kubwa za biashara zilikuwa zikisimamiwa na watoto wake pamoja na mjukuu wake mkubwa ambaye anafahamika kwa jina la Yan Buxue.

“Kwanini nikwambie alipo?”Aliongea Yan Qiantian huku akionyesha kidogo wasiwasi kutokana na nguvu ya kijini ambayo Roma alikuwa akisambaza.

Roma hakujali kumjibu , bali aliinua mkono wake kutoka aliposimama kuelekea upande wao na palepale nguvu isiokuwa ya kawaida ilimvuta Yan Buxue mdogo wake Yan Buwen na kwenda kutua mbele ya Roma.

Kilikuwa ni kitendo kilichowaacha wote mdomo wazi , kwani haikueleweka Roma alifanikishaje jambo hilo.

“Pengine unadhani nimetoka Tanzania mpaka hapa kwa ajili ya kubembelezana na mtu kama wewe , mjukuu wako kanichokoza kwenye nchi yangu na nipo hapa kwa ajili ya kisasi , niambie alipo la sivyo nitahakikisha kila mwanafamilia anakufa mmoja mmoja wewe mwenyewe ukishuhudia”Aliongea Roma na kwa kutumia kisigino cha kiatu alimkanyaga Yan Buxue kwenye mkono kwa nguvu na kumfanya kutoa ukulele usiokuwa wa kawaida kiasi cha kumfanya babu yake kuwa na wasiwasi.

“Haina haja ya kutuuliza sisi maana hatujuia eneo alipo , ni kweli juzi alikuja hapa nyumbani lakini aliondoka pasipo ya kutuambia anaelekea wapi”Aliongea

“Kwahio hilo ndio jibu lako , nadhani mnaniacha bila chaguo na kuwalazimisha kuongea ukweli”Aliongea Roma na kisha alimkanyaga tena Yan Buxue kwenye paja la mguu kwa nguvu huku akitumia mkono wake kumkaba shingo kichawi.

“Nitahakikisha nakutesa mpaka kifo chako kama babu yako hatoniambia ni wapi Yan Buwen alipo”Aliongea Roma

“Mpigeni risasi “Aliongea mwanaume mmoja aliekuwa upande wa kushoto aliekuwa wa makamo na walinzi wale walipopewa ruhusa walianza kushambbulia tena , lakini matokeo yake hakukuwa hata na risasi ambayo ilimpata Roma kwa mara nyingine na waliishia kurudi nyuma kwa woga.

Lakini Roma hakuishia hapo hapo alimwangalia mwanaume alietoa maagizo ya kushambuliwa na kumpaisha kichawi kwenda angani na kisha akamwachia akiwa hawani na kujipigiza chini na ni mifupa tu iliosikika kuvunjika.

“Mjombaa..!!!”Walijikuta wanafamilia baadhi wakiita kwa pamoja kwa hofu huku wengine wakitoa machozi.

“Wewe.. wewe kweli ni shetani kama tulivyosikia taarifa zako , huwezi kuua watu ndani ya taifa letu kwa kujisikia tu kufanya hivyo nakuhakikisha hutotoka hapa salama”

“Alitaka kuniua mimi kwanza , nichokifanya ni kumrudishia”Aliongea Roma pasipo ya wasiwasi huku mwanaume alieitwa mjomba akifurukuta kwa maumivu chini akionyesha kukata roho

Arggh…!!!, Babu naomba umwambie , mwambie kaka alipo , huyu mtu hana utani ataniua”Aliongea Yan Buxue kwa mara nyingine huku akionyesha hali ya maumivu kwani Roma alizidi kumkandamiza chini kwa kiatu

Yan Qintian alijikuta akikunja mkono wake kwa hasira na kufumba macho kwa dakika kadhaa.

“Okey naomba umuachie nitakumbia ni wapi Yan Buwen alipo”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

“Hicho ndio nilichokuwa nikitaka , kulikuwa na haja gani mpaka ukanifanya kumuua mtoto wako , haya ongea ni wapi alipo haraka kabla sijaua mwingine”

“Buwen alikuja siku chache zilizopita na kuniambia kakamilisha misheni iliompeleka Tanzania na karudi kwenye makazi yake…”Kabla hajamalizia sentensi yake alijikuta akihisi kupaliwa huku akishika shingo yake na kufanya wajukuu zake kumshikilia na kuita jina lake kwa woga.

“Babu umenikatisha tamaa sana , kwanini umekuwa mrahisi kutaka kutaja mahali nilipo licha ya kukuambia ni siri kati yetu.”Ilisikika sauti ikijaza eneo lote lakini pasipo ya mtu kuonekana.

Roma kutokana na uwezo mkubwa wa masikio yake alikumja sura na kuangalia juu angani na aliweza kushuhudia kama anga lilikuwa likichemka kwenye eneo ambalo lilitengeneza shimo, lilikuwa jambo la kushangaza mno kwake.

Lakini palepale ile sehemu ambayo ilikuwa ni kama inechemka ilimtema chini Yan Buwen ambaye alienda kutua ndani ya eneo hilo..

Roma alishangazwa na mwonekano wa Yan Buwen na kuna hisia zilimwambia huenda Yan Buwena kabla ya kuja Tanzania alikuwa na makazi mengine sehemu nyingine kabisa na huenda ikawa nje ya China.

“Kaka.. Kaka … niokoe nakufa”Aliongea Yan Buxue akimnyooshea mkono Yan Buwen aliekuwa mita kadhaa kutoka kwake.

“Inanishangaza mtu mdhaifu kama wewe bado unaendelea kuishi”Aliongea Yan Buwen huku akionyesha hana nia yoyote ya kumsaidia kwani alimwangalia mdogo wake kama kituko.

Alimwangalia Roma kwa namna ya kumchunguza na kisha akamsogelea kwa spidi lakini hakumshambulia , alichokifanya kiliwashangaza familia yote na kuwaacha mdomo wazi huku wengine machozi yakiwabubujika

Kwani alipasua kichwa cha mdogo wake Yan Buxue na kufanya ubongo wake kusambararika palepale.

Kitendo kile kilimfanya hata Roma mwenyewe kusahngaa , hakuamini Yan Buwen angechukua hatua ya kumuua mdogo wake mbele ya familia yake.

“Aaah.. Buwen unafanya nini tenaa..?”Aliongea Yan Qintian huku akijilazimisha kusimama vizuri kwani alikuwa kwenye mshituko.

“Hii dunia watu wadhaifu dhaifu kama yeye hawapaswi kuishi, nimemua kuongeza nafasi ndani ya dunia kwa kuondoa kiumbe dhaifu kisichostahili kuishi”Aliongea

“Huyu ni.. ni.. mdogo wako , Mdogo wako kwanini umemuaa?”Aliongea mzee wa watu huku pumzi zikianza kukata.

“Hahah… eti mdogo wangu , ukoo huu wa Yan siku zote mtaishi kunitegemea mimi lakini mkitishiwa kidogo tu mnataka kutoa siri zote zinazonihusu , wote hamna thamani kwangu na nitawaua wote”Aliongea

“Yan Buwen unapaswa kuongea kwa heshima sisi ni wakubwa zako”Aliongea Mzee mmoja kwa kufoka.

Lakini Yan Buwen alipotea aliposimama na ile anakuja kutokezea alikuwa mbele ya mlinzi mmoja alieshikilia siraha yake kihasara hasara na kumpokonya na kuanza kuwamiminia ndugu zake risasi bila hata ya kuwa na huruma.

BANG! BANG! BANG!

Wanafamilia wote mmoja mmoja alidondoka chini na kupoteza maisha kwani risasi zililengwa kwa umakini mkubwa kiasi kwamba kila inaempata ni kwenye kichwa

“Hahaha… hahahaha…. Hahahahaha….. nitaunda familia mpya yenye watu wa kutawala viumbe wote dhaifu”Yan Buwen baada ya kuhakikisha kila mwanafamilai yupo chini, alijikuta akicheka kama chizi na kumfanya Roma aliekuwa akishuhudia kitendo hicho kukunja sura na kuona huenda uwezo alioweza kupataYan Buwen umembadilisha na kuwa kichaa.

Wale walinzi baada ya kuona hali hio , walikimbia wote mmoja mmoja baada ya kushuhudia Yan Buwen akimaliza familia yake yote. .

Baada ya kuona wale waliokuwa wakikata Roho wametulia chini kwa kupoteza maisha akiwemo babu yake Yan Qiantian, alipiga miayo miwili kama mtu mwenye njaa na kisha akatupa ile siraha chini na kumgeukia Roma.

“Alright it’s quit now , I have been waitng for this day for long time”Aliongea akimaanisha sasa hali imekuwa tulivu na alikuwa akisubiria hio siku kwa muda
 
SEHEMU YA 436

Roma hakutaka kumzuia Yan Buwen kabisa kutokuua familia yake , kwanza ni mambo ambayo hayakuwa yakimhusu na pili familia hio ndio iliomwingiza katika mambo ya kutengeneza siraha za maangamizi ili tu kuweza kushindana na Hongmeng.

Lakini hata hivyo swala la kuua familia yake mwenyewe lilimfanya Roma kuuona Yan Buwenn kiumbe cha hatari sana ambacho kwa namna yoyote ile alitakiwa kumwangamiza hapo hapo kwani kitendo alichokifanya hakuweza kufikiria hata siku moja mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya..

“Nakubali umekuwa chizi kuliko nilivyofikiria , lakini kabla hatujaanza mapambano yetu niambie kwanini ukaamua kuwa adui yangu , maana hakuna siku yoyote ambayo nilishawahi kukuchokoza”Aliuongea Roma

“Haijalishi chochote kwasasa”Alijibu .

“Kweli! Unaweza usiamini lakini swali langu ndio sababu ambayo imenifanya muda wote nisikuchukulie hatua licha ya kunichokoza mara kibao, nadhani unakitaka kifo sasa”

“Hahaha,.. unafikiri unweza kunishinda mimi?”Aliuliza Yan Biuwen lakini Roma hakumjibu , ukweli alichokitaka ni kujua kwanini ghafla tu Yan Buwen akaanza kumuwinda yeye kwani hakuwa na ugomvi nae.

“Nadhani hata hivyo napaswa kukujibu , mwanzoni sikuwa na haja na wewe kabisa , lakini nilikuja kugundua unamiliki kitu cha thamanni ambacho hakikuwa cha kwako , hata hatua yangu ya kufika Tanzania ilikuwa ni kukipata , unaweza ukashangaa labda kwanini nikakaa Tazania kwa ajili ya tafiti zangu lakini ukweli kabla ya kuja Tanzania nilikuwa na makazi mengine bora zaidi kuliko maabara ile ya kipuuzi kule Tanzania , lakini hata hivyo mimi Yan Buen nimekuwa wa kupata kila ninachokitaka katika dunia hii..”Aliongea

“Ulikuwa ukitaka nini kutoka kwangu?, mpaka sasa kama unahitaji Jiwe la kimungu halipo kwenye umiliki wangu, nini unachokitaka kutoka kwangu”

“Huna haja ya kufahamu , lakini kaa ukikumbuka hivi , kifo chako pekee ndicho kitathibitisha kwamba mimi ndio mmiliki pekee wa dunia , I am strongest man in the world”

“Sijawahi kujitangaza mimi kama ni mmoja wapo ya watu wenye nguvu ndani ya dunia hii”Alijibu Roma.

“Lakini kuna watu wanaamini una nguvu kuzidi mtu yoyote ndani ya dunia hii na ndio maana nitaichukua nafasi yako kwa kukuua”Aliongea Yan Buwen.

“Nani anaamini hivyo?”

“Unaongea sana Hades, haijalishi tena kukuambia kwani mpaka sasa wewe ni mfu”Aliongea na palepale nguvu isioelezeka ilianza kumzingira kiasi cha kutengeneza mwanga flani wa rangi ya Cyan lakini ambao haujakolea sana lakini angavu mno kiasi kwamba ulifanya mazingira kuwa na mwanga , Cyan ni mwanga ambao unazalishwa kati ya rangi ya bluu na kijani katika mwimbi ya wevu 490nm kwenda 520nm , inasemekana kwenye anga la sayari ya Uranus ndio imekithiri.

Sasa mwanga ule ulikuwa ukimzunguka huku ukitengeneza kama wingu flani hivi la rangi hio kuanzia chini kwenye miguu mpaka kichwani huku ukiambatana na upepo mkali, kadri nguvu ilivyokuwa ikizunguka ndio anga lote lilivyoanza kucheza cheza kwa kupinda.

Roma alishangazwa kwani ilikuwa ni nguvu sawa kama ya Clone alilopambana nalo siku chache zilizopita lakini awamu hii nguvu hii ilikuwa kubwa mno.

“I am sue you have come into contact with my creations , So please enjoy it while it last”

“Naamini ushakutana na kiumbe changu , hivyo furahia uwezo wangu kadiri unavyodumu”Aliongea kwa kujigamba huku akicheka kama chizi na kusogelea Roma kwa spidi ya mwanga akilenga eneo la moyo wa Roma.

Roma alishajua alichokifanya Yan Buwen ni kutengeneza mbinu ya kucheza na kanuni za anga kwa kutengeneza uzio nyuzi nyuzi sambamba(disorderly Paraller space fabric) ili kwamba hata kama Roma angekuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga kushambulia basi ashindwe.

Hata hivyo aliamini huenda Yan Buwen alimtegemea angeweza kutumia kanuni za anga kushambulia , lakini yeye alitumia mbinu za kijini.

Roma palepale aliita nguvu ya kijini ya kimaandiko na ilitengeneza ngao flani kama kioo na ni muda huo huo Yan Buwen aliweza kumfikia hivyo mgongano wa ngao na nguvu ya Yan Buwen ulitengeneza mtetembo kama wa bomu huku cheche kama za radi zikisambaa eneo lote kutoka kwenye ile ngao ya Roma aliotengeneza.

Mtikisiko ule ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ulisambabisha hata jengo la nyumba hio na ukuta wake kuporomoka chini , lilikuwa ni jambo ambalo lilimshangaza Roma kwani Yan Buwen alikuwa na uwezo mkubwa sana kiasi kwamba ilimshangaza na kujiuliza imekuwaje Yan Buwen kuwa na uwezo mkubwa kiasi hicho kwani mara ya mwisho alionekana kuwa wa kawaida tu.

Yan Buwen mara baada ya kuona pigo lake la kwanza halijafanikiwa alipiga tena kwa mara mbili mfululizo , lakini ngao ya Roma iliuonekana kuwa ngumu , lakini hata hivyo alivyopiga mara ya tatu ilitengeneza uwazi hivyo hakutaka kuchelewasha kwani palepale alilenga ngumi iliojaa mwanga kama wa jiwe la kimungu na kuipitisha kwenye uwazi.

!POW!

Baada ya ngumi ile kumpata vyema Roma kwenye kifua alirushwa kwenda juu kama vile ni mpira huku akizunguka zunguka kwenye hewa na baada ya kufika mwisho alirudi chini kwa spidi lakini palepale alitumia uwezo wake wa kijini kupunguza spidi ya namna anavyoshuka , lakini kabla hajakanyaga Ardhi , Yan Buwen alileta teke lenye nguvu isiokuwa ya kawaida na kwakua alitumia spidi kubwa Roma alizubaa na kushindwa kukwepa.

“Arrgh…”Roma alitoa ukulele mara baada ya kupokea bonge la teke na kwenda kutua kwenye mlima wa mawe yaliorundikwa sehemu moja mara baada ya nyumba ile kubomoka.

Yan Buwen mara baada ya kuona amefanikisha kumpiga mapigo mawiali Roma na kumpeleka chini alipaa juu angani akimwangalia kwa chini.

“Hahaha… naona kupokea kipigo ndio unachoweza pekee , vipi umekuwa mdhaifu kwa kapigo kadogo kutoka kwangu”Aliongea kwa kimandarini akimwangalia Roma aliekuwa akiugulia maumivu chini ya rundo la mawe.

Lakini Roma alivyotaka kusimama vizuri Yan Buwen alimsogelea kutoka juu kama mshale , lakini kabla hajamfikia liliamika jiwe kubwa pembeni na kumlenga Roma.

PUUH!,

Jiwe lilimpiga kisawa sawa Roma na kumfanya kutema damu huku akipiga magoti kwa maumivu.

Alijikuta akipeleka mkono mdomoni na kujifuta huku macho yake yakiwa mekundu kama yanaanza kutoa damu.

Roma alitaitiwa mapema sana tofauti na alivyokuwa akipambana na Poseidon,nguvu aliokuwa nayo Yan Buwen haikuwa ya kitoto.

“Haha.. Etia anaitwa Pluto upuuzi mtupu , wewe ni kichekesho , kwangu nakuona kama kunguni tu ambaye nakuua na vidole , hustahili hata kuwa mshindani wangu pumbavu”Aliongea Yan Buwen na Roma alijitahidi kusimama vizuri baada ya maumivu kupungua.

“Here is my advice for you , I’m reissuing my clone offer , Be my slave and I might let you live”

“Huu ndio ushauri wangu , ninakupatia tena ofa kama nilivyotoa maagizo mwanzo kwa clone langu , kuwa mtumwa wangu na ninaweza kukuacha hai”Aliongea Yan Buwen

“Halafu tena kabla sijasahau , unao warembo wengi , nafikiri pia wanaweza kuwa msaada kwangu nina kwani nina Clones nyingi na zina nyege hatari , itakuwa jambo zuri kama warembo wako watatoa huduma kwao wote , nataka wewe mwenyewe uangalie namna Clones zangu zinavyofanya mapenzi na mademu zako hahahah..”

Kauli yake ni kama ilimfanya Roma aliekuwa amesimama kivulini kurudiwa na nguvu zake zote , kwani hasira zilimpanda kiasi kwmaba zilisambaza nguvu isiokuwa ya kawaida ndani ya eneo lote.

“Unaonekana bado una vinguvu vya kuweza kupambana , ngoja tuone ulichonacho kwa sasa”Aliongea Yan Buwen mara baada ya kuhisi nguvu isiokuwa ya kawaida.

Sasa ukumbuke Roma wakati alivyokuwa akipigana macho yake yalikuwa kawaida kabisa licha ya kwamba yalikuw mekundu , lakini awamu hii Yan Buwen alivyotaja warembo wake na kusikia kuna kopi nyingi zinazofanana nae ,viini vya macho vilibadilika rangi kutoka weusi na kuwa nyekundu na miale kama ya laser.

Yan Buwen mara baada ya kushuhudia Roma kabadilika macho alijikuta ile hali ya kuamini angeweza kushinda pambano ilimpotea mara moja

Roma sasa alikuwa kama nusu shetani kwanza ,alitoa ulimi na kulamba damu zilizokuwa zikimtoka kwenye midomo yake.

“Niliamua kutokuwa siriasi na wewe , kwasababu nilikuwa nikihofia kulikorofisha anga lakini sasa hivi sina haja ya kucheza mchezo wa kitoto na wewe , nitakuonyesha nini maana ya kupigwa na radi harafu na kupona”

“Haha unaongea sana , kuna mtu unajaribu kumsubiria…”Aliongea lakini kabla ya kumaliza sentensi yake palepale aliposimama ni kama alikuwa akivutwa na nguvu isiokuwa ya kawaida kiasi kwamba alikuwa akikosa balansi ya kuendelea kudumu kwenye anga lakini wakati huo huo akihisi mkandamizo ambao sio wa kawaida kabisa , huku Roma akiwa amesimama akimwangalia kwa macho ya hasira.

“Hii ni…”Alijikuta akitoa macho mara baada ya kugundua nguvu ni kama zinapotea mwili wake na kumwangalia Roma kwa mshangao.

Uwezo wa Roma ulikuwa umeongezeka zaidi ya mara ishirini kuliko alivyokuwa akipambana mwanzo , alikuwa ni kama mtu mwingine kabisa.

Wingu lilianza kuzunguka juu kama vile mvua inataka kunyesha na nyota zilizokuwa zikionekana zilibwa na wingu.

BOOM, BOOM, BOOM

Ngurumo kali ilipiga ikiambatana na radi lakini ambayo haikufika chini huku mawingu yakizidi kusuguana na kusababisha umeme.

Roma aliangalia juu angani mara baada ya ngutumo na kuona ahueni na kisha alipiga hatua moja mbele , lakini kilichomkuta Yan Buwen ni kwamba aliporomoka chini huku akianza kukosa hewa, alikuwa ni kama yupo kwenye chumba chenye moshi mwingi.

“Kwanini umekuwa kimya ghafla , nia yako ya kuniua na kuwachukua wanawake wangu ipo wapi , hii ndio nafasi yako ya mwisho ichukue”Aliongea kwa sauti ndogo lakini ni kama ilikuwa ikitoka juu angani kwani ilikuwa kama mwangwi.

Yan Buwen alijitahidi kushindana na nguvu iliokuwa ikizunzuia kutofanya chochote lakini alishindwa.

Upande wa Roma mwenyewe alihisi mabadiliko yasiokuwa ya kawaida ambayo hakuweza kuyatarajia , siku zote alikuwa akiita nguvu za kijini akitaka kupambana lakini sasa hivi sio kama alikuwa akiziita lakini yeye ni kama ndio nguvu zenyewe za kijini na zilikuwa zikiamua kipi cha kufanya.

“Uli ., ulificha uwezo wako kumbe?”Aliongea Yan Buwen kwa shida sana.

“Unatakiwa kujichukulia wa juu kwani siku zote situmiagi uwezo wangu kwa watu wa kawaida ,, ninaweza kukuua bila ya wewe mwenyewe kujua kama umekufa , nina miaka elfu moja sijawahi kuamshwa na kuwa na nguvu kiasi hichi ndani ya uso huu wa dunia”Iliskika sauti ambayo haika sio ya Roma bali ni kama ya kijini inayomtawala ndio inayoongea.

“Acha kujihisi una uwezo mkubwa sijashindwa bado”Aliongea Yan Buwen na palepale alijikakamua kwa uwezo wake wote na kuchomoka kwenye nguvu iliokuwa ikimzuia chini kutopaa na alifika juu hewani na kumfuata Roma kwa namna ya kurusha shambulizi , lakini Roma alitoa tabasamu la kifedhuli nakukunja kiganja na kisha akakifumbua na kurusha kibao juu angani.

BANG!

Yan Buwen alirudishwa kutoka juu kwa spidi isio kuwa ya kawaida na alishindwa kujiongoza na kwenda kuyavamia mawe ya ukuta kiasi kwamba sehemu aliodondoka ilitoa vumbi zito.

“Inaonekana unaweza kufa kwa pigo moja tu”Aliongea Roma lakini nguvu ilianza kujikusanya tena kwenye mwili wa Yan Buwen kwa kupepesa macho tu.

“Inaonekana kwangu nguvu zako ni za aina yake lakini sio kama za kwangu , ninaweza kuzifyonza zote na kuzitoa kwenye mwili wako nakushauri utii amri kama sijakuua kwa zaidi ya mara kumi”Aliongea Roma vile vile huku sauti ikiwa sio kama ya kwake kwani ilikuwa nzito na ya kuogofya mno.

Yan Buwen alijikusanya kwenye vumbi kwani nguvu zake zilikuwa zimemtoka nyingi na huenda angekuwa mfu kwa wakati huo

“Siwezi kukubali kushindwa…”Aliongea kwa hasira na kuamka kama mwanga wa radi.

BOOM!

Ni vipande vipande vya nyama vilivyosambaa angani , ilionekana Roma alimtegemea ndio maana akamtanguliza na shambulio kama la bomu ambalo lilimsabaratisha

Lakini licha ya kusambararika ilionekana nguvu isiokuwa ya kawaida ikikisanya vile vipande vipande vya nyama pamoja na damu yake kwenda sehemu moja pasipo ya kudondoka chini, lakini Roma hakuteka kuruhusu tukio hilo , alirusha tena pigo lingine na kusambaratisha tena, lakini ajabu tena vipande vilikusanyikka kwa spidi kubwa sana ni kitendo cha kupepesa macho tu Yan Buwen alirudi tena kwenye uhai wake na kumfanya Roma kutoa macho.

Lakini kabla hajaamua cha kufanya ni nini , palepale mwili wa Yan Buwen ulibadilika na kufunikwa na suti flani hivi ya aina yake na kumziba mpaka kichwa , ilionekana ilikuwa ni kama ngao

Roma alishangazwa na vazi la Yan Buwen kwani ni kama vile alikuwa akiangalia muvi ya Avenger end game.

“You can’t kill me , I have this..”Aliongea Yan Buwen akiwa amefunikwa kichwa chake kama vile ni Spiderman huku mkononi mwake kukionekana kitu kama kitenesi kikitoa mwanga mkali sana wa mng’ao

“The Godstone,! This whole time it was you?”Aliuliza Roma kwa mshangao usio na kifani huku akimaanisha kwamba kilichomtokea siku ile mpaka kupoteza jiwe hilo la kimungu ,lakini vile vile kule Ufaransa kupoteza teknolojia ya Thanatos , lakini pia kupotea kwa Moses Vampire na Holygrail , mambo yote hayo yalikuwa ni yeye , Roma alijiambia haiwezekani ndio maana alitoa mshangao usio na kifani.

Jambo moja lingine ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba lile jiwe lilikuwa limebadilika ukubwa wake na sasa lilikuwa likitoa mwanga mkali sana unaoumiza macho mweupe lakini mfano wa jua , ni haki kusema kwamba Yan Buwen huenda kajua siri ya jiwe hilo.

Yan Buwen hakueleweka alifanya nini na lile jiwe lakini alilirusha juu angani na likanasa na palepale lilitengeneza shimo nyeusi kubwa ambalo anga lake ni kama linachemka kwa spidi kubwa ni kama unaangalia BlackHole , mwili wake ulivutwa kwa kasi sana na lile shimo na akapotea palepale kwa namna ya kuyeyuka.

Roma alijaribu kuzuia shimo liile lakini nguvu yake ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba ilimrusha mbali kwa kumkataa.

Roma alijikuta akianza kuhema kwa tabu , mpaka hapo aliamini huenda Yan Buwen alitumia jiwe hilo kuweza kuwa na nguvu kama hizo , ilikuwa mantiki kufikiria hivyo , lakini swali aliwezaje kufahamu kanuni za anga kirahisi hivyo kwanni hakuwa na uungu wowote ndani yake

Pumbavu”Aloijikuta akitoa tusu huku aking’ata meno yake kwa hasira kwa kitendo cha Yan Buwen kumkimbia , alijua aliweza kumtoroka kwa kutumia jiwe la kimungu, ijapokuwa miaka mingi lilikuwa chini ya umiliki wake lakini hakuwahi kufikiria jiwe hilo linauwezo mkubwa mpaka wa kutengeneza shimo jeusi angani na kuwa kama njia ya kutoroka.

“Hades usiwaze hatoweza kukushambulia kwa muda hahah..”Ilikuwa ni sauti ambayo inasikika kwenye kichwa chake na kumfanya kutoa macho , ilikuwa ni hali kama ya mtu mwenye ugonjwa wa kuchanganyikiwa.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikisikika vyema sasa lakini macho yake hayajatoka kwenye rangi ya uwekundu.

“Hehe .. umenipa jina mwenyewe unaweza kuendelea kuniita kwa jina la nguvu ya kimaandiko naishi ndani ya mwili wako , mimi na wewe ni ndugu wa damu chanda na pete una mwili mzuri sana kwa ajili ya mimi kuishi”Sauti ilisikika kwenye akili yake na kumfanya Roma kushika kichwa kwa namna ya kuchanganyikiwa.

“Achia akili yangu”

“Sawa kwasasa nitakuachia akili yako , lakini kadri unavyozidi kuwa na nguvu ya kijini itafikia siku lazima nitaiongoza akili yako kabisa,mwili wako unanifaa sana ngoja niendelee kulala nikisubiria siku yangu ya kurudi uraiani”Iliongea Sauti na kumfanya Roma ang’ate meno yake kwa hasira na palepale macho yake yalirudi kwenye hali yake ya kawaida na ile sauti ikapotea kwenye akili yake.

Alijikuta jasho likimtoka mno hakuelewa ni nini kinachomtokea hata hivyo ni kweli kabisa wakati anajaribu kupambana na Yan Buwen kwa uwezo wake wote ni kama mwili wake hakua ukiuongoza yeye kwenye mapambano, ni kama akili yake ilikuwa ikifanya kazi nusu na nusu nyingine ilitawaliwa.

Lakini hata hivyo Roma alitabasamu kifedhuli kutokana na kwamba ndani ya mwili wa Yan Buwen wakati alivyokuwa amemshikilia kichawi alimwingizia nguvu ya kijini kwenye mwili wake, kitendo ambacho hata yeye akili yake hakuelewa kwanini alifanya hivyo lakini kwa sauti iliomwongelesha anaelewa kwamba ni mtego.

Aliamini lazima mwili wake Yan Buwen utakuwa kwenye maumiu makali , kwani inaonekana nguvu ya jiwe la kimungu na za kijini haipatani ndio maana wakati anasogelea shimo jeusi tofauti na kumezwa yeye alitupwa mbali kwa ishara kwamba shimo lile linamkataa yeye.

Lakini Roma sauti aliokuwa akiisikia kwenye kichwa chake ilimfanya kuwa na wasiwasi lakini hata hivyo aliamini huenda ni akili yake mwenyewe , hivyo aliamua kupuuzia lakini bado roho yake haikuwa na amani.

“Au kuna athari za kutumia kanuni ya kimaandiko?”Roma alijikuta akianza kuwaza mwenyewe huku akiangalia uharibifu uliofanyika.

“Roma nini kimetokea , wewe ndio umeharibu hizi nyumba zote?”Ilisikika sauti kutoka hewani na kumfanya Roma kuangaliai juu alikuwa ni Omari alieonekana ndio anafika.

“Umewezaje kusafiri umbali mrefu mpaka hapa bila kukasiriha anga?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

“Kuna namna ya kusafiri pasipo kukasirisha aga , nnimefunzwa huko Hongmeng, pumbavu kabisa nimechelewa daah sijaona pambano”Aliongea huku akiongekana kulalamika.

Njia ambayo anazungumzia Omari ya kusafiri pasipo kukasirisha anga ni kusafiri kwa vituo , yaani unaweza kupaa kwa kilomota kadhaa na kisha ukatulia kwa dakika kumi na tano then unaendelea tena kwa kilomota kadhaa , mpaka ufikie eneo husika , uzuri ni kwamba tu nguvu za kichawi zenyewe zinakupeleka sehemu unayonuia kufika haina haja ya kuwa na ramani kichwani lakini athari kubwa ni kwamba kila kituo lazima kiwe ni maji au bahari, yaani kwa mfano ukatoka Tanzania na madhumuni ya kwenda China basi unatakiwa usafiri na uelekeo wa bahari tu ili kila ukifikisha kilomita kadhaa , unatumbukia majini na kukaa huko kwa dakika kumi na tano na unaibuka tena unasafiri tena kwa kilomita kadhaa halafu unaingia tena majini unajificha ndani ya maji kwa dakika kumi na tano unaibuka tena , ilikuwa ni mbinu ngumu kwani inahitaji ujasiri lakini inakuwezesha kusafiri kwa muda mfupi.

Hivyo kimahesabu ni kwamba Omari alianza safari kabla ya Roma kwani kuna vituo vingi sana ndani ya maji ambavyo lazima Omari alipumzika kabla ya kuendelea na safari.

Hivyo unaweza ukaona jini linaibukia baharini usiku ukashangaa lakini ukweli ni kwamba bahari au ziwa ni njia salama ya majini kusafiri pasipo kukumbana na malipizi ya anga.

“Taarifa za Yan Buwen kuua familia yake zinasambaa sana kuna rafiki yangu hapa China nilianza kufikia kwake na kupata habari hizo , inasemekeana walinzi ndio walitoa habari, Vipi umefanikiwa kumdhibiti”Aliuliza Omari huku akikagua namna eneo lilivyoharibika.

“Amenitoroka bwana”Alijibu Roma kinyonge.

“Hapana , amewezaje kutoroka mbele yako nadhani ni afadhari nimekuja baada ya mapambao kuisha huenda ningekufa hapa hapa, maana huenda ningepatwa na hasira na kushindwa kujizuia mpaka kumpiga ngumi”

“Unashindwa vipi kujizuia au kwasababu mwanamke wako kamtia mimba?”Aliuliza Roma kwa kejeli.Lakini Omari alionekana kutopendezwa na swali lake

“Najua huenda huna hela yoyote na pia mavazi yako yamechafuka , twende kuna sehemu salama ya sisi kwenda kula msoni na kupata hifadhi ya kulala”Aliongea Omari.

“Nani kakuambia sina pakuishi”Aliongea Roma na palepale licheza na anga , kilikuwa ni kitendo kama alichofanya Clelia allisanto wakati akitoa kiboksi cha uwa angani.

“Hades kuna uwezekano na mimi kujifunza namna ya kutunza vitu kwenye anga?”

“Uwezekano huo huna , nina nguvu ya kiuungu ndani yangu ndio maana naweza pia kujifunza kanuni za anga , wewe ni binadamu wa kawaida ambaye umejifunza mbinu za kijini”Aliongea Roma huku akiangalia kipi cha kuchukua kwenye shimo ambalo linatumika kama sehemu ya kuhifadhia vitu kwenye anga , aliachana na pete na kisha akachukua kadi ya benki na passport yake ya kusafiria.

“Hivi ni vibali ambavyo vinaweza kunipatia makazi kwenye hoteli yoyote hapa nchini China pambana kivyako sijakuambia unifuate huku China”Aliongea na kabla hata Omari hajaongea neno , palepale Roma alipotea na kumuacha Omari akiwa kwenye mshangao.

“Pumbavu zako Hades , nimekufuata mpaka China halafu umeniacha nitakupata tu”Aliongea Omari huku akiangalia baiti moja iliofukukiwa na mchanga uliotokana na kuharibika kwa nyumba na alisikitika kidogo na kisha akapotea ndani ya eneo hilo mara baaada ya kusikia magari ya polisi yakisogelea hilo eneo.

Unafikiri sauti iliomuongelesha Roma inatokana na nguvu za kijini anazojifunza , kama kweli ataendelea kupanda levo je nguvu ya kimaandiko itaweza kutawala akili yake , nini kitaendelea tukutane kesho.
 
SEHEMU YA 437.

Ni usiku huo huo baada ya kumuacha Omari kwenye nyumba ya Yan Buwen ilioharibiwa , Roma alionekana tena ndani ya eneo maarufu sana ndani ya Beijing ambalo hukaliwa na wanasiasa pamoja na wakuu wa jeshi, ni sehemu ambayo inafahamika kwa jina la Xijiao Villas.

Sasa Roma haikueleweka alikuwa akifanya nini ndani ya eneo hilo lakini alitembea na barabara iliokuwa ikitenganisha majumba hayo yenye kuta ndefu kwa nje na alienda kusimama kwenye geti la nyumba namba 32 , ni nyumba ambayo ilikuwa mwishoni kabisa mwa barabara lakini pia iliokuwa karibu zaidi na fukwe.

Eneo hilo muda huo lilikuwa tulivu mno na ni magari machache sana ambayo yalikuwa yakipita , lakini kutokana na mtaa huo kuwa wa hadhi ya juu mwanga haukuwa mkali sana lakini ulimulika vizuri eneo lote.

Roma mara baada ya kusimama nje ya geti hilo taa zake zilizima halafu zikawaka na kumfanya akunje sura kwani aligundua taa hizo zilikuwa ni otomatiki.

Aliangalia kamera zilizofungwa juu kabisa kwa dakika na kisha akabonyeza kitufe cha kengere kama mara tatu na kisha akatulia na zilipita dakika kama mbilitu hivi sauti kutoka ndani ilisikika sehemu ile ya kubonyezea , ilionekana walipo ndani walikuwa wakimuona.

“Wewe mtu mweusi ni nani na unataka nini muda huu?”Ilisikika sauti kutoka ndani ya mwanaume mwenye besi lakini aliezungumza kwa lugha ya Kimandarini.

“Mimi mwanaume mweusi ni Roma Ramoni , nipo hapa kulipiza kisasi”Aliongea Roma huku akiweka sura yake kuikaribia Kamera.

“Wewe ni kichaa ondoka kabla hatua nyingine hazijachukuliwa”Ilisikika sauti mara nyingine na Roma alitabasamu kifedhuli na kisha aliharibu kibonyezeo cha kengele , lakini pia kamera zote pamoja na taa za nje na kukawa giza.

Dakika chache tu mara baada ya kufanya uharibifu huo mlango mdogo ulifunguliwa haraka sana na wanaume waliovalia kombati za jeshi lakini wakiwa na mitutu iliiomwelekezea.

Ni kama Roma alikuwa akisubiria kitendo hicho kwani walivyotokeza tu alinyanyua mkono wake na kuachia nguvu ya kijini isiokuwa ya kawaida na kuwafanya wale wanajeshi kurudishwa ndani kwa namna isiolezeka kwani walipepesuka na wawili walikwenda kutua kwenye ‘Fountain’ ya maji na Roma aliingia bila wasiwasi ndani ya eneo hilo na alishangazwa na uwepo wa wanajeshi wengi waliokuwa wakilinda.

Naona Afande Yang amechukua tahadharai , inaonekana katarajia ujio wangu”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake huku akikagua mazingira pasipo kujali mitutu ya bunduki iliokuwa imemwangalia.

“Simama hapo hapo , la sivyo tutashambulia mara moja”

“Okey kabla sijatii maagizo yenu , shida yangu ya kwanza ni kuonana na bosi wenu muiteni hapa nje la sivyo nitawaua wote”Aliongea Roma kwa Kichina na wale wanajeshi waliangaliana lakini muda ule ule mwanaume wa makamo rika lake mchina alionekana akitokezea mbele , alikuwa amevaa kombati za jeshi ambazo baada ya Roma kukagua kwa haraka haraka aligundua bwana huyo alikuwa na nyota tatu ikimaanisha ni Kapteni wa jeshi.

“Mr Roma Ramoni tumetarajia utafika kututembelea lakini hatukurarajia utafika usiku sana, wasamehe vijana wangu kwa ukaribisho usio na ukarimu, kwa jina naitwa Yang Chen marehemu Afande Yang Gonming ni babu yangu”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Umesema Marehemu?”Aliuliza Roma kwa mshangao na Yang Chen alionekana kidogo kuwa kwenye hali ya huzuni.

“Inaonekana Mr Roma taarifa zimechelewa kukufikia , babu yetu na mkuu wa ukoo Afande Gongming siku ya leo asubuhi ametutoka”Aliongea lakini muda ule ule walionekana wanawake watatu na mwanaume mmoja waliovalia mavazi ya kuomboleza wakija lile eneo.

Na moja kwa mmoja Roma aliamini huenda ni kweli familia hii ipo kwenye maombolezo , lakini alishangazwa na kufa mapema kwa Yang Gongming kabla hajalipa kisasi chake.Wanawake wale walimwangalia Roma huku wakionekana kuwa na wasiwasi.

“Okey Kapteni Yang Chen nadhani nimechelewa kufika kuchukua kiasasi changu nitawaacha muendelee kuomboleza kwa amani lakini naamini huenda ukamrithi babu yako hivyo nikusihi ukae mbali na maisha yangu la sivyo siku nyingine nikirudi hapa nitalipiza kisasi kupitia kwako”Aliongea na kumfanya Yang Chen kumwangalia Roma kwa wasiwasi lakini palepale aliwapa ishara wanajeshi pamoja na wale watu waliongezeka kuondoka na kumuacha yeye na mgeni.

Na ndani ya dakika tu wote waliondoka na akabakia Roma na Yang Chen

“Mr Roma Ramoni kabla babu hajafariki mara ya mwisho niliweza kupata nafasi ya kuongea nae na alionekana kujutuia makosa yake alioyafanya na ameniambia nisirudie makosa alioyafanya”

“Amekuambia amefaya makosa gani?”

“Ndio kosa lake kubwa ni kumsaidia Yan Buwen na kuwa na nguvu kubwa ambayo anaaamini imemfanya kuwa kichaa hivyo wasiwasi wake ni usalama juu ya sisi ambao tumebakia”Aliongea

“Kwahio babu yako kamsaidia Yan Buwen kuwa na uwezo mkubwa na amekufa akiwa na wasiwasi juu ya usalama wenu dhidi ya Yan Buwen,, amepata wapi ujasiri wa kufa na kuwaachia mzigo?”Aliuliza Roma.

“Naweza kusema hivyo , lakini nimejipanga kwa namna yoyote kukabiliana na Yan Buwen kama atajitokeza na kuonyesha nia ya kutaka kudhuru familia yangu kama alivyofanya kwa familia yake , Mr Roma naomba umsamehe babu yangu kwa makosa yote alioyafanya ili apumzike kwa amani”

“Ningemsamehe babu yako kama angekufa baada ya kukutana na mimi , lakini kwasababu amechagua kufa kabla ya kuniomba msamaha hatna haja ya kuyabeba makosa yake”Aliongea Roma na kisha aligeuka na kuytoka eneo hilo lakini ile anafika nje tu aliweza kukutana na Omari ambaye alionekana ndio kwanza anafika.

“Nilijua tu ungekuja huku”

“Kwahio ulikuwa ukinifuatilia , si nilikuambia kila mtu afanye kilichomleta huku”

“Lazima nikufuate kwani wewe ndio njia pekee ya mimi kuweza kupambana na Yan Buwen”Aliongea Omari na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli.

“Kwannini hukuniambia Afande Yang alishakufa mpaka ukanifanya kupoteza muda wangu wa kuja mpaka huku?”

“Nilitaka kukuambia muda ule lakini ukanitoroka , taarifa niliipata mara baada ya kufika hapa China”

“Kwahio unanilaumu kwa kukuacha?”

“Ndio maana yake , siku nyingine ujifunze kuangalia nia nzuri za watu , nimekufuata Hadi China nikiwa na wasiwasi huenda Yan Buwen akakuua na maiti yako ikapotelea huku huku China “Aliongea kiutani na kumfanya Roma kumpita na kusonga mbele.

Ukweli ni kwamba Omari aliagizwa ili kutoa taarifa ya kile kinachoendelea China.

*********

Ni siku iliofuata Roma alipanda ndege ya kurudi nchini Tanzania, hakuwa na haja ya kuendelea kukaa China tena, alikuwa kidogo na amani kwani aliamini kwa mtego wa nguvu za kijini alioweka kwenye mwili wa Yan Buwen ungemfanya kutorudi hivi karibuni mpaka aatakapojiponyesha hivyo aliamini ni kheri kurudi nyumbani kuwa karibu na familia yake.

Omari Tozo yeye alionekana kubakia China na Roma wala hakujali sana kurudi nae , kwani kwanza hakuwa amekuja nae.

Baada ya kukaa hewani kwa muda mrefu hatimae aliweza kufika ndani ya uwanja wa ndege jijini Dar es salaam ikiwa ni usiku wa saa moja , haku itaarifu familia yake kwamba anarudi hivyo hakuna ambaye alikuwa amefika kumpokea , alitumia usafiri wa kawaida wa teksi ambao ulimpeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwake Ununio.

Baada ya kulipa nauli alitoka na kuingia ndani , kwa jinsi ambavyo anaonekana ni kama vile hakuwa akitokea China alikuwa na mavazi yale yale aliotoka nayo siku tatu tatu zilizopita.

“Dadiii…..”Mtu wa kwanza kumuona Roma alikuwa ni Lanlan ambaye alikuwa nyuma ya nyumba pamoja na Qiang Xi wakimpa mbwa chakula,.Roma alifurahi kumuona Lanlan na kumbeba juu juu.

“Dadi.. zawadi ya Lanlan iko wapi?”

“Dadi leo hii hajasahau kumletea zawadi Chubby”Aliongea Roma na pale pale kwa kutumia kanuni za anga alifungua shimo ambalo ni kama mfuko wa kuhifadhia vitu(Space pocket).

Kitendo kile kilimfanya Lanlan kutoa macho baada ya kuona alichokifanya baba yake ni kama alitaka na yeye afundishwe.

Roma hakujali mshangao wa Lanlan kwanza alicheka na kisha alivuta boksi kubwa lililonekana likielea angani na kisha akampatia Lanlan amaye alionekana kuwa kwenye shauku kubwa ni kipi ambacho baba yake anampatia kama zawadi.

“Okey Chuby hii ndio zawadi yako , tutaenda kuiona ndani ukiwa na mama”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan ambaye alionekana kujawa na shauku kukubali kwa kichwa na Qiang Xi alimsaidia Roma kubeba boksi na wote wakaingia ndani.

Roma mara baada ya kufika eneo la sebuleni alishangazwa na uwepo kundi la wanawake ambao walionekana kupiga stori , alijikuta akijiuliza ukaribu huo wa kufika nyumbani umeanza lini kwani hata Neema Luwazo alikuwepo.

Edna alionekana kutokea jikoni akiwa amejifunga khanga kiunoni alionekana kuwa bize na maswala ya upishi.

Wanawake wake wote walionekana kumwangalia kwa kutabasamu lakini ni Edna tu aliemwangalia kwa ukauzu.

“Edna my wife mbona umevuta sura hivyo au hujafurahi kumuona mumeo nimerudi salama salimini”Aliongea Roma huku akiwa anamshusha Lanlan chini.

“Wewe ndio umevuta sura”Aliongea Edna na kisha alimwangalia Lanlan aliekuwa akijaribu kubeba boksi ambalo ameshikilia Qiang Xi na kufanya wenzake kucheka kwa jibu la Edna.

“Niliwaambia mimi atarudi haina haja ya kuwa na wasiwasi na hamkuniamini si huyo hapa sasa hivi”Aliongea Neema Luwazo akionekana kuwashushua wenzake.

“Tulichotaka ni uthibitisho, hatukuwa na wasiwasi lakini taarifa yako ilituchanganya maana ilikaa kimbea zaidi”Aliongea Nasra aliekuwa pembeni yake na Neema alionekana kama ameumbuliwa na kumpiga Nasra kibao mapajani na kuwafanya kucheka, kitendo ambacho kilimfanya Roma kushangaa maana aliona hali ya urafiki kati ya wanawake wake , ukweli hakuelewa kama Edna alikuwa akipenda uwepo wa wanawake hao ila alishindwa kumsoma mara moja kile anachokifikiria.

“Roma umerudi tumekuwa na wasiwasi na usalama wako, lakini kidogo tulitulia mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afande Kweka kwamba upo salama”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kidogo kushangaa huyo mzee kapata wapi taarifa zake , alijikuta akimtukana ndani kwa ndani Omari alijua huenda ndio alievujisha taarifa zake Tanzania.

“ My Dear Roma inaonekana maisha yako hapa Tanzania yanasisimua mno”Ilisikika sauti ikitokea upande wa jikoni ikiongea kwa kutumia liugha ya kingereza na kumfanya Roma kushangazwa na uwepo wa Profesa Clark ndanni ya nyumba yake , alijiuliza mwanamke huyo kafika saa ngapi na anafanya nini Tanzania.

“Clark kwanini upo hapa?”Aliuliza Roma kwa kingereza.

“Nitakaa hapa Tanzania kwa muda”Aliongea

“Unamaanisha nini kukaa Tanzania kwa muda?”

“Profesa Clark yupo hapa Tanzania kwa ajili ya kazi maalumu ya ushirikiano kati ya chuo kikuu cha Dar es salaam na kampuni yangu , tunapanga kufungua maabara itakayohusisha majaribio na mafunzo ya utafiti wa dawa”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.

“Unapanga kujiingiza kwenye biashara ya madawa?”Aliongea Roma kwa kuuliza kwani biashara za Edna hazikuwa zikihusisha kabisa maswala ya madawa.

“Mwanzoni sikuwa na wazo la kuanzisha kampuni itakayohusisha maswala ya madawa lakini nilipopata kusikia wazo kutoka kwa Profesa Clark nilivutiwa , hata hivyo nafanya biashara hio kusaidia Afrika, Profesa Clark kaamua kujitolea kwa ajili ya kuchagua kundi la wanafunzi ambao watakuwa chini ya mkataba wa ushirikiano kati ya serikali na Vexto, hivyo mafunzo yatadumu kwa mwaka mmoja”Aliongea

“Mwaka mmoja!?”Roma alijikuta akikuna kichwa hakuamini mwanamke huyu anaweza kuja kukaa Afrika kwa zaidi ya mwaka mzima, haikueleweka kwanini alikuwa na wasiwasi na ujio wa Profesa hapa nchini.

“Mr Dear Roma am I not welcomed here?”Aliuliz Clark kwama je hakaribishwi Tanzania.

“Sio kama hukaribishwi nimeshangazwa na kuja Tanzania kwa project ya dawa tu, ni jambo ambalo sio kawaida yako”

“Nani kakuambia Project ni ya kawaida wakati nimeiruhusu mimi?”Aliongea Edna huku akionyesha kutopendezwa na kauli yake.

“Babe wife usikasirike , nimekosea kauli yangu , Project kama hizi za madawa mara nyingi ni kwa ajili ya kuisaidia jamii”Aliongea lakini Edna alionekana kutoridhika na jibu lake.

“Waliotakiwa kufika ni wanafunzi wake , lakini mambo yakabadilika hivyo akaamua kuja yeye”

Ukweli ni kwamba siku chache nyuma Edna aliweza kupokea Email kutoka kwa Profesa Clark iliokuwa na wazo la kuanzisha maabara ambayo itahususha utafiti wa dawa za ARV , kwa maelezo ya Profesa Clark ni kwamba dawa ambazo zinatakiwa kufanyiwa utafiti sio kwa ajili ya kurefusha maisha bali ni tiba kamili ya ugonjwa huo , Edna hakuamini baada ya kusoma Emaili hio ndio maana alifanya mawasiliano ya moja kwa moja na Profesa Clark.

Na pendekezo la Profesa Clark alitaka kufundisha watanzania wenyewe juu ya kufanyia utafiti wao wenyewe hatimae kuja kutengeneza hio dawa, huku yeye akiwa kama mtu aliewezesha tu pasipo kugundulika kama ndio mgunduzi , haikueleweka kwanini aliamua kutotaka kuwa mtu aliehusika kugundua dawa hio bali alitaka taasisi ya utafiti wa dawa ambayo itafunguliwa kwa ubia kati ya serikali na kampuni ya Vexto ndio waweze kuja kutangaza dawa hio kama itakuja kuonyesha ufanisi katika majaribio.

Hivyo mwanzoni Profesa alitaka kutuma kwanza wanafunzi wake kuja kuanza mafunzo ndani ya chuo kikuu cha Dar es salam kwa wanafunzi watakao chaguliwa , lakini siku mbili zilizopita Edna alipata kutaarifiwa kwamba mafunzo atayaongoza mwenyewe, sasa mawasiliano hayo yalibakia kuwa siri kati ya Edna na Profesa clark pekee, kwahio ilikuwa ni kama surprise kwa Roma.

“Najua Roma utakuwa kwenye mshangao , kwani juzi niliwasiliana na wewe nikiwa UK lakini nilitaka iwe kama Surprise kwako”Aliongea lakini Roma alishindwa kujua cha kujibu hata hivyo kuna kitu kilimwambia kuna jambo linaendelea ndio maana Profesa Clark akaja Tanzania ghafla na kutaka kukaa mwaka mzima haikumwingilia akilini Clark anaemjua akae tu Tanzania na kuacha maabara yake ya viwango vya juu iliopo Uingereza.

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale Roma alienda kwenye chumba chake kwa ajili ya kubadilisha Mavazi na kuoga huku Edna akimsaidia Lanlan kufungua Zawadi na kila mmoja alishangaa kwani Roma alimletea Lanlan Drone ya kisasa mno.

Lanlan alijikuta akiruka ruka kwa furaha kwa zawadi alioletewa , kwani wakati alipokuwa akicheza gemu kuna misheni ambayo alikuwa akiipenda sana , misheni ya kushambulia Adui kwa kuendesha Drone , sasa baada ya kuona amenunuliwa Drone ki uhalisia ni kama ndoto zake zimetimia na anakwenda kufanya mishezi zake mubashara, utofauti ni kwamba Drone alioletewa Lanlan ilikuwa ni ya kupigia picha na sio ya kurushia watu mabomu kama ilivyokuwa kwenye gemu.

Edna mwenyewe aliona furaha aliokuwa nayo Lanlan na alishindwa kujua kwanini Roma aligundua Lanlan angependa Drone,

Ilibidi siku hio Bi Wema na Edna kupika chakula cha kutosha kwa ajili ya wageni waliokuwepo na saa tatu kamili za usiku mara baada ya chakula kila mmoja aliaga na kurudi kwenye nyumba zao.

Upande wa Profesa alifuatwa na dereva na kupelekwa kwenye hoteli ambayo amefikia.

Baada ya Roma kumuona Edna anapandisha juu kwenda kwenye chumba cha kujisomea Roma alitupa rimoti pembeni na kisha alipandisha kumfuata huko huko.

“Vipi tena mwenzetu?”Aliuliza Edna Edna akimwangalia Roma .

“Nimekuja kuongea na wewe kuona labda una hasira na mimi”

“Nini?”

“Nahisi kama inaonekana nilikuwa nikifahamu Neema alikuwa akiishi huku , lakini pia nikaomba na Amina kuishi na Nasra , unaweza kuniona labda nimeamua kuwaleta wote pamoja ili kushindana na wewe”Aliongea Roma , ukweli ni kwamba Edna wakati wa chakula alionekana kunyamaza mno ni kama hakuwa na amani ndio maana Roma aliona aongee nae.

“Kama ndio unachofikiria basi nikujibu kwamba umekosea , kuna baadhi ya vitu haviwezi kuniathiri hata kama ionekane nalazimishwa, unaonekana wewe ndio huna amani ndio maana umeanzisha haya maongezi”

“Upo sahihi umeona kilichopo ndani ya moyo wangu , nadhani kuwa na mke mwenye akili kuna faida na hasara zake”Aliongea Roma na kumfanya Edna kufurahi kusifiwa kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , yote haya huenda ni makosa yetu wote nusu kwa nusu na hatuwezi kufikiria yaliopita zaidi kukubali matokeo na kusonga mbele , sikasirishwi na uwepo wao kwenye nyumba yangu wala kuwa majirani , nadhani hata wewe umeona mimi na Bi Wema ndio tumeandaa chakula , naweza pia kuwa mkarimu hata kwa wanawake wenzangu”Aliongea Edna.

“Wewe kuwa mkarimu kwa namna hii ndio kinachonifanya kidogo niwe na wasiwasi na kukosa amani”Aliongea Roma na kumfanya Edna kutabasamu kidogo na kisha kumsogelea karibu , huku Roma akiwa na wasiwasi ni nini Edna anataka kufanya kwani alimkaribia kabisa na miili yao kugusana.

“Kwanini… Unanionea huruma kuzungukwa na wanawake wako?”Aliongea Edna akimnong’oneza Roma kwenye sikio kiasi cha kuhisi pumzi yake kwenye sikio kwa namna ya kumpuliza.

“Ah.. kila siku nilikuwa ni mwenye kukuonea huruma sana kiasi cha kukosa amani , yote hayo ni kwasababu ya matendo yangu”Alijibu kwa kubabaika mara baada ya kugundua kusudio la Edna ni kumnongoneza na sio kama alichofikiria.

“Basi nataka wasiwasi wako na huruma yako juu yangu izidi kuongezeka ili mpango wangu ufanikiwe wa kuhakikisha hatia yako ya kurudi usiku ukitoka kwa wanawake wako ikutafune kwa kiwango cha juu ndio utaelewa matendo yako si sahihi kwa mimi mkeo”.

“Nilijua tu huwezi kuwa mkarimu bila ya kuwa na ajenda ya siri”

“Mama ameniambia wanaume wa aina yako mnabadilika sio kwa kutumia nguvu bali ni kwa kuonyeshwa sababu yenye ushawishi , kadri nitakavyo kuonyeshea ukarimu na kukujali ndivyo hatia itakavyozidi kukutafuna na mwisho wa siku utabadilika ,inaonekna mama yako anakufahamu vizuri licha ya kutokulea”Aliongea Edna.

“Mama ndio kakuambia hivyo?”Aliongea Roma kwa mshangao lakini Edna hakumjibu zaidi ya kupitisha mikono yake kwenye kiuno cha Roma kwa kukumbatia na kisha akajilaza kifuani.

“Babe nilikumisi sana…”Aliongea Edna akijibebisha lakini kwa namna sauti yake ilivyotoka ilimfanya Roma kujihisi kama alikuwa kwenye mbingu ya saba.
 
SEHEMU YA 438.

Ni siku iliofuata Roma alienda kazini kama kawaida na kupokelewa na Tanya ambaye tayari wafanyakazi wote walishamtambua kama sekretari wa Roma akiwa amerithi nafasi ya Amina ambaye ameenda kumsaidia baba yake majukumu kwani alitoa taarfa ya kuwa nje kimatibabu.

Sasa wafanyakazi walikuwa wakishangaa Roma aliwezaje kuajiri ghafla tu mrembo kutoka Japani ambaye alionekana kuwa na akili nyingi kichwani , kwani kila kazi iliomfikia Tanya ilifanyiwa maamuzi ya haraka na zile ambazo zilikuwa zikimhitaji bosi wake aweze kuzitolea maelezo aliweka kwenye meza ya Roma ili akirudi kazini azifanyie kazi Tanya alifanya kazi kwa umakini kwani alitaka bosi wake akirudi ampatie sifa.

Daudi na Wendy hawakuwweza kutoa maoni yao juu ya uwepo wa Tanya, hata hivyo wangesema nini kwani Roma ni mume wa bosi wao Edna , walichokifanya ni kumpa heshma yake Roma kwani kupendwa na mwanamke tajiri na mrembo kama Edna lilikuwa jambo kubwa sana, lakini pia hata hivyo Roma jina lake lishakuwa kubwa uraiani kwani alikuwa akitambulika kama mtoto wa Raisi Senga , lakini pia alikuwa mmoja ya wanafamilia ambao wanaarajiwa kurithi mali za familia ya Afande Kweka.

Asubuhi hio Roma mara baada ya kupitia rundo la mafaili yaliokuwa kwenye meza huku Tanya akiwa mbele yake , muda huo huo mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na akaingia Daudi ambaye alionekana kuwa mwenye haraka.

“Vipi mbona unahema hivvyo juu juu?”Aliuliza Roma huku akikunja sura.

“Director kumetokea tatizo kwenye mitambo yetu ya kurushia matangazo”Aliongea.

“Matatizo gani?”

“Inaonekana tumedukuliwa”Aliongea Daudi na kumfanya Roma kukaza sura na kushangazwa na kauli hio na kujiuliza nani wa kuwa na ujasiri wa kudukua mitambo yao ya kurushia matangazo.

Daudi palepale alichukua Rimoti na kuwasha runinga na kuweka Vexto Tv na kilichoonekana kwenye TV kilimfanya Roma kukunja sura, ilikuwa ni kama Chaneli yao imebadilika na kuwa ya Kichina kwani ni nyimbo za lugha ya kichina tu zilizokuwa zikionekana.

“Director aliedukua mitambo yetu ameingiza nyimbo za Kichina tu ambazo zinajibadilisha kila mmoja ukiisha , wataalamu wamejaribu kurudisha mitambo kwenye mfumo lakini wameshindwa kabisa”Aliongea Daudi na kumfanya Roma kusimama na kumwambia waongozane kwenda kwenye chumba cha mitambo ya kurushia matangazo

Dakika tatu tu ziliwafikisha kwenye chumba ambacho kina mitambo na kukutana wataalamu wanahangaika na Tarakishi kurudisha matangazo kwenye ukawaida.

“Nini kimetokea?”

“Kuna mwingiliano wa Frequency za mawasiliano na satilaiti na mfumo mwingine , kwa haraka haraka tunaweza kuamini kwamba mifumo yetu imedukuliwa”Aliongea Mwanaume mmoja ambaye ndio mkuu wa kitengo hiko.

Roma alishika kiuno na kuona jambo hilo ni kama lililotokea kule kwenye jengo la FBI baada ya Mossad kudukua Frequency za mawasiliano na kuonyesha Vido ya mtoto wa Robert Mueller na mama yake wakinyanduana.

Haraka haraka Roma aliamini aliefanikisha hilo lazima atakuwa na uelewa wa juu wa maswala ya komputa hususani kwenye mawasiliano kwani viwango vya ulinzi vilizingatiwa wakati wa kufuma mfumo wote.

“Nipeni jjibu moja kama mnaweza kutatua tatizo au Lah?”Alingea Roma na wale wataalamu walitetemeka na kukosa majibu.

Roma palepale alikumbuka kuna profesa Clark , huenda akafanikisha kutatua shinda hio , hivyo pale pale alipiga simu na kumuuliza yuko wapi na alijibiwa mara moja kwamba yupo ndani ya wizara ya Elimu.

“Kuna tatizo kwenye mfumo wetu wa matangazo , chaneli zinaonyesha nyimbo za kiasia tu hivyo naweza kusema tumedukuliwa , je unaweza kufika na kutusaidia”Aliongea Roma kwa Kingereza.

“Bila shaka nakuja sasa hivi”Aliongea Profesa na Roma alipumua baada ya kukata simu.

Nusu saa mbeleni Profesa Clark aliweza kufika ndani ya kampuni ya Vexto Media na kuingia kwenye chumba hiko hiko cha mawasiliano na kisha alitoa tarakishi yake ya mapakato aliokuja nayo , ambayo haikuonyesha ilikuwa ni ya kampuni gani , lakini jubu la haraka haraka inawezekana ameitengeneza mwenyewe.

Alichomeka HDMI waya kutoka kwenye CPU iliokuwa ikidhibiti mfumo wa urushaji wa matangazo na satilaiti na palepale alifungua ‘Powershell’ na kuanza kuandika mwenyewe kwa lugha isioeleweka kiasi cha kuwafanya wale wataalamu kutoshindwa kuelewa anaandika nini na ndani ya dakika mbili tu alishafanikisha na Daudi na Wendy walikuwa ndio wakwanza kushangalia na kumfanya Roma kutabasamu kwa uwezo aliokuwa nao Profesa.

“Naomba karatasi”Aliongea Profesa na palepale alichomoa karamu yake iliokuwa kwenye mfuko wa suruali ya kitambaa aliovalia na kisha kuandika kitu kwenye karatasi ile na kisha akaendelea kuchezesha vidole kwenye tarakishi kwa dakika moja nyingine na kisha alitabasamu.

“Nadhani muhusika nishampata naweza kusema anaonekana kuwa na akili , lakini hata hivyo kuna mambo anaonekana hajayazingatia kwenye udukuzi wake , hivyo naweza kuamini kama ni mdukuzi basi ni wa kiwango cha kati au kakosa mafunzo maalumu ya kujilinda , hili ndio eneo ambalo IP Adress ya tarakishi yake ilipo , hivyo naamini pia na yeye yupo eneo hilo”Aliongea Profesa na kisha akampatia Roma.

“Clark kama haitokuchukulia muda wako nisaidie kutuwekea ulinzi kwenye mfumo wetu ili siku za baadae swala kama hili lisijirudie”Aliongea Roma kwani alimwamini sana Profesa Clark kwa uwezo wake.

“Actually hicho ndio nilichofanya hapa niliingiza tu mfumo wangu wa ulinzi na kuzuia mwingiliano wa mawasiliano yake na mitambo yenu”Aliongea na kuwafanya wale watanzania waliokuwa ndio wamepewa jukumu zima la mambo ya IT kushangaa.

“Wazungu wana akili bwana , sidhani tungefanikisha hili kwa muda mfupi kama yeye”Mmoja wapo alijiwazia huku akimwangalia Profesa kwa namna ya kumhusudu.

Watu baadhi walimfahamu Profesa kama mmoja ya watu wa heshima sana huko duniani na hata ujio wake hapo ndani uliwashangaza lakini kwasababu walikuwa kwenye tatizo hawakuweza kuongea lolote.

“Kwahio unamaaisha hakuna tena uwezekano wa udukuzi kufanikiwa kwenye mitambo yetu?”Aliuliza Roma.

“Pigia mstari mpendwa wangu Roma Ramoni”Aliongea huku akiichomoa tratakishi yake mapakato kutoka kwenye CPU na kuirudisha kwenye begi, lakini kauli yake iliwafanya Daudi na Wendy pamoja na wale wengine kuangaliana kwani ilionyesha Roma na huyu Profesa wa heshima kubwa walikuwa na ukaribu, waliishia kumkubali bosi wao ndani kwa ndani.

“Vipi hutaki kumkamata mdukuzi wenu?”Aliongea Profesa na kumfanya Roma kuangalia eneo husika.

“Director nitatuma taarifa polisi , kwani udukuzi ni kinyume na sheria”Aliongea Daudi.

“Haina haja nitaenda mwenyewe kumkamata”Aliongea Roma na kumfanya Clark kutabasamu ni kama alijua Roma angejibu hivyo.

***************

Upande mwingine asubuhi hio Edna hakufika moja kwa moja kazini bali alianza kutembelea baadhi ya miradi iliokuwa ikisimamiwa na kampuni yake kupitia Vexto Constructors.

Na mradi wa mwisho kutembelea ulikuwa ni wa Adani ambao ulikuwa kwenye hatua za mwisho za ‘evaluation’ ili mwendelezo wa ujenzi kuanza , baada ya kuongea na injinia mkuu ndipo safari yake ya kurudi ilianza.

Kwenye gari asubuhi hio hakuwa akiendesha yeye bali dereva wake wa kampuni ndio aliekuwa akifanya kazi hio ya kumuendesha na hata gari walilotumia sio la kwake bali ni Rangerover ya kampuni.

Sasa wakati wanakaribia kuingia barabara ya kutokea kivukoni kukaribia kituo cha mabasi ya mwendo kasi , posta ya zamani ghafla dereva alikanyaga breki kwa nguvu kiasi kwamba Edna alirushwa mbele na kurudishwa kwenye kiti kutokana na kuvaa mkanda , lakini hata hivyo Innocent ambaye ndio Dereva alionekana kuhaha kwani tayari alikwisha kugonga mtu.

Edna ndio aliekuwa wa kwanza kuelewa kinachoendelea na alifungua mlango haraka haraka na kutoka pasipo kujali sana watu waliokuwa wakianza kuzuguka , Innocent na yeye alionekana kuchanganyikiwa lakini baada ya kupewa maagizo kwa kufoikewa na Edna ndipo alipozinduka.

Edna aligundua mtu aliegongwa na gari yake alikuwa msichana ambaye alionekana kuwa kama mchina , lakini kutokana na kwamba alipoteza fahamu hakutaka kujiuliza uliza maswali ,walimbeba na kumuingiza kwenye gari haraka na safari ya hospitali ilianza.

Bahati ni kwamba ni michubuko tu iliomdhuru , ilionekana Innocent alifunga breki kabla ya kumkaribia kabisa hivyo ni kama walimpushi.

Dakika chache mbele waliweza kufika hopsitali ya Aghakhani na kupokelewa na manesi na kupelekewa kwenye chumba cha uangalizi wa dharula.

*****

Roma aliweza kutoka kwenye jengo hilo la kampuni akiwa peke yake kuelekea sehemu ambayo kwa maelekezo ya Profesa Clark ndipo anapopatikana mdukuzi wao.

Dakika chache mbele aliweza kufika nje ya jengo la hoteli ya Kilimanjaro na aliingia ndani , tena wakati huo anafika ndio muda ambao ajali ya gari la mke wake kumgonga mtu lilitokea mita kadhaa kutoka ilipo hoteli hio lakini Roma hakujua kwani hakuwa na taarifa.

Baada ya kuegesha gari alitoa simu yake iliokua ikionyesha uelekeo wa Ramani huku ikiwa ni kidoti chekundu , kidoti kilichoahiria sehemu tarakishi iliohusika kudukulia mitambo yao ilipo.

Roma baada ya kuangalia kidoti alitabasamu baada ya kuona alikuwa sehemu sahihi na alikuwa mita kadhaa tu kuweza kufikia eneo husika , alikuwa ni kama akicheza gemu la magari kuonyesha mwisho wa safari yake.

“Nikikumata utanitambua”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake huku akitembea

Alifuata mshale huo mpaka kufika mapokezi, lakini muda ule ule simu yake ndogo ilitoa mlio kuashiria inaita na aliangalia anaepiga na kugundua ni Afande Mage.

“Ingia kabisa nipo eneo la mapokezi”Aliongea Roma akimpa maelekezo Mage na ndani ya muda mfupi tu Mage alievalia gwanda za polisi aliweza kumfikia Roma.

Roma aliamini angeweza kufika hotelini hapo kwa ajili ya kumkamata muhalifu lakini bila msaada wa polisi asingeweza kuruhusiwa kufanya uchunguzi wa kumpata muhalifu ndio maana aliona msaada wa Mage kuwepo.

Mage kwakua alishapewa malekezo ya kile kilichotokea moja kwa moja alijjitambbulisha kama polisi kwa kutoa kitambulisho na wahudumu walimruhusu na Roma alitabasamu na wote waliingia kwenye lift huku bado macho yao yakiangalia mshale unaosogelea kidoti chekundu.

Walikuja kutokea kwenye floor namba tatu ya jengo hilo na Roma alitembea kwa kuhesabu vyumba huku nyuma yao wakiambatana na mhudumu aliekuwa na wasiwasi mno.

“Tumefika”Aliongea Roma kwa kutabasamu huku akimwonyesha Mage na ni kweli mshale ulionyesha wamefika mwisho kwa maana kwamba mlango namba 54 ndio sehemu mdukuzi wao alipo.

Mage hakujiuliza mara mbili mbili , aligonga mlango kwa zaidi ya mara tatu lakini ilionyesha hakukuwa na majibu na palepale alimgeukia mhudumu.

“Tunahiraji Master Card ili kufungua hiki chumba”Aliongea Mage na mhudumu alitoa simu haraka haraka na kupiga huku akionyesha hali ya wasiwasi , lakini muda ule ule mwanaume alievalia suti na bango kwenye eneo la mfuko wa suti yake aliwafikia na kujitambulisha kama Floor manager na yupo tayari kutoa msaada.

“Ndugu Meneja tunataka kufungua huu mlango na inaonekana muhusika hayupo maana tumegonga bila mafanikio”Aliongea Roma na bwana yule wa makamo alitoa kadi ambayo ilikuwa na uwezo wa kufungua milango yote na kisha akaweka sehemu husika na mlango ukafunguka.

“Lakini Roma hakuruhusu mtu yoyote kuingia kasoro ya Mage”Iliokuwa ni amri ya kipolisi hivyo kila mmoja alitii maagizo.

Ni chumba kikubwa cha Presidential Suite See view , mpaka hapo Roma aliifahamu muhusika atakuwa ni mwenye pesa, wakati Mage akionekana kukagua uwepo wa mtu hapo ndani mpaka bafuni , Roma alvutiwa na tarakishi mpakato iliofunikwa , aliisogelea na kisha akaiinua kwa juu lakini ajabu ni kwamba ilikuwa wazi lakini ilikuwa ikichezesha Vidio kwa kurudia tudia. Sasa Vidio yenyewe ilimuacha hoi na kutoa macho kama kabanwa na mlango na kujikuta akijikalia kwenye sofa.

“Shi**t ni Rufii”Roma alijikuta akitamka kinyonge jina la mrembo ambaye alilala nae nchini Marekani ndani ya jiji la Los Angeles , alijua ni yeye kwani tarakishi hio ilikuwa ikionyesha vidio ambayo anamnyandua alijiambi alaifanya la maana kuja mwenyewe maana kwa jinsi sura yake ilivyokuwa ikionekana ingekuwa balaa ingefika kwenye mikono ya adui yake.

“Inaonekana mhalifu tumemkosa hapa? Hakuna dalili yoyote ya uwepo wa mtu”Aliongea Mage huku akisogelea sehemu alipoketi Roma.

“Huyu ni..”Mage aliziba mdomo kwa kutoamini kile kinachoendelea lakini muda ule ule simu kubwa ya Roma ilianza kuita na alipoangalia jina ni mke wake aliekuwa akipiga na ilibidi apokee palepale.

Lakini mara baada ya Roma kupokea na kusikiliza , palepale alitoka kwenye mshangao na kumwangalia Mage ambaye alionekana kuangalia Vidio hio huku akikunja sura na Roma alifunga ile laptop.

“Nishamjua muhusika , nitaondoka na hii laptop mtu mwingine asiruhusiwe kufanya upekuzi mpaka nitakaporudi”

“Lazima uongee hivyo , umezidi kuwa muhuni sana Roma nani angejua inawezekana mtu kukurekodi pasipo ya wewe mwenyewe kufahamu Looh?”Aliongea Mage kwa kejeli huku akibetua mdomo.

“Mage nitakuelezea nikirudi kilichotokea sasa hivi ngoja niwahi hospitalini , Edna kaniambia kapata ajali muda si mrefu na yupo Aghakani”Aliongea Roma na kumfanya mage kumwangalia Roma kwa wasiwasi.

“Kaumia?”

“Hapana kagonga mtu ndio alivyoniambia”Aliongea Roma na Magea alimwambia anaweza kwenda atajua cha kufanya.

Roma alitoka haraka haraka huku akishindwa kuamini mdukuaji alikuwa ni mwanamke Rufi , alijikuta akijicheka mwenyewe kwa kujidharau na alijiuliza ilikuwaje siku ile hakujua kama kuna kamera mle ndani, haraka haraka alijua huenda Rufi kamfuata Tanzania , alijiambia kama kweli amefuatwa basi ana kesi ya kujibu kwa mke wake kama Video hio itamfikia.

“Lazima nimpate Rufi kabla hajakutana na mke wangu au kumtumia hii Vidio najua yote hii ilikuwa mipango yake kutaka kunionyesha kwamba yupo hapa nchini”Aliwaza Roma huku akiingia kwenye gari lake na kuliondosha.

Dakika chache mbele alikuwa ashafika eneo la hospitali na kumpigia Edna kujua yupo upande upi , baada ya kupata uelekeo moja kwa moja alielekea mpaka kwenye chumba cha wodi na kisha alisukuma mlango na kuingia ndani.

Na hapo ndipo alipomshuhudia mdukuzi wake akiongea na mke wake Edna , akiwa mzima, mpaka hapo alijiambia amezidiwa ujanja.

ITAENDELEA
MAWASILIANO YA WATSAPP NI 0687151346
 
Back
Top Bottom