Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu singanojr muendelezo linitaisha to the End muwe na Amani
[emoji91][emoji91][emoji91]SEHEMU YA 434.
Ilionekana hata Rose alikuwa akijua swala la Clellia Allisanto kwani hakuonyesha mshangao wowote na hata Roma alitambua Rose alikuwa akifahamu lakini alishangaa kwanini Dorisi hakuweka wazi swala hilo kwake .
Dorisi ilibidi amuelezee Roma kwa kila kitu kilichotokea , jinsi alivyorudi nyumbani kwake na kumkuta mwanamke ndani ya nyumba yake , mwanamke ambaye alijitambulisha kwa jina la Clellia Allisanto.
Mpaka Dorisi anamaliza kusimulia Roma ilimshangaza sana na kujiuliza huyu Clallia Allisanto alikuwa akimtakia nini mpaka kuanza kuzungumza na Dorisi maswala ya kuzaa nae , swala hili lilimshangaza na kumchanganya kwa wakati mmoja , lakini alishangaa zaidi mara baada ya Clellia Allisanto kuweza kutaja jina la Naira ambaye alikuwa rafiki wa utotoni wa Dorisi.
Roma palepale alijikuta kuna swala likimjjia akilini hapo hapo na ni kama alianza kupata majibu ya kile ambacho alikuwa akijiuliza tokea Edna alivyokutana na huyu Clelia Allisanto.
“Nafikiri stori yako inatengeneza ukweli ambao ulikuwa ukiutafuta”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi kumwangalia mpenzi wake kwa wasiwasi.
“Ukweli wa… Unazungumzia Black Card?”Aliuliza Dorisi akiwa kumbukumbu zake sasa zikikaa sawa na Roma alitingisha kichwa.
Ilibidi Rose aeleweshwe kidogo kuhusu Black Card ili aweze kuelewa kile kinachozungumziwa na alijikuta akishangaa mara baada ya kusikia Dorisi alikuwa na kadi ya benki ambayo ilikuwa na uwezo wa kutoa mabilioni ya hela benki , maelezo hayo ni kama hayakuwa ya kuaminika kabisa kwake lakini kilichomshangaza zaidi ni Roma kusema kadi hio imeunganishwa na akaunti ya benki ya The Doni.
Ilikuwa rahisi sana kugundua Dorisi alikuwa akimiliki Black Card kadi ambayo akaunti yake ya banki inamilikiwa na The Doni ambaye ni Athena lakini Clelia huyo huyo akamtembelea Dorisi na kutaja jina la Naira rafiki wa utotoni wa Dorisi hivyo kwa haraka haraka ni kwamba Clelia ndio Athena.
“Dorisi umesema alikuonyesha picha?”
“Ndio alinionyesha picha akiwa amepiga na Naira kwenye mapozi tofauti tofauti , lakini sehemu moja , walionekana kama wapo kwenye chumba cha hospitali au maabara , lakini sehemu ya kisasa zaidi”Aliongea Dorisi na kumfanya Roma kutabasamu.
“Kuna namna moja ya kumtambua Clalia , ile picha ya Naira si upo nayo?”Aliuliza Roma na Dorisi aliitikia kwa kichwa na Roma akampa ishara ya kumwambia akailete na Dorisi alitii haraka sana na kupandisha ngazi na kushuka na picha ile na Roma alimwangalia Naira aliekuwa kwenye picha hio.
Ukweli Roma hata mara ya kwanza alivyoona hio picha kuna kitu kilimwambia huyo mtoto hakuwa kabisa wa kawaida, hakuelewa kwanini alikuwa akimuona kama sio wa kawaida.
Roma alitoa simu yake na kisha kuipiga picha na kumrudishia Dorisi na baada ya kumaliza alitafuta tena namba ya Makedoni.
“Mfalme Pluto unanipigia tena”Ilisikika sauti ya Makedoni upande wa pili lakini waliongea kwa lugha ya kihebrew.
“Nataka ujaribu kutafuta jina la Naira Ryani , nakutumia picha yake kama jina halitokuwa kwenye mfumo wenu wa taarifa kwa teknolojia ambayo Israeli mnayo , haitashindikana kutoweza kupata taarifa zake”Aliongea Roma kwa kiebrania na kuwafanya Rose na Dorisi kuangaliana na kutabasamu.
“Mfalme Pluto nipe dakika moja , nitumie kabisa hio picha kwa Email nitakurudia mara baada ya kupata majibu”Aliongea na Roma alikata simu na kisha akatuma kwa njia ya email ile picha.
“Hubby hio ni lugha gani uliokuwa ukiongea?”Aliuliza Rose. Na kumfanya Roma kutabasamu.
“Ni Hebrew(Kiebrania)”Alijibu Dorisi na kumfanya Roma kutabasamu lakini Rose kushangaa.
“Dorisi unaonekana kukijua kiebrania?”
“Sijui kuzungumza lakini matamshi ya kiebrania nayajua”
“Hubby ilionekana uliishi sehemu nyingi za dunia , uliwezaje kujua lugha ya kiebrania?”
“Mpenzi wako nina historia ndefu sana”Aliongea Roma.
“Nakumbuka wakati unaanza kuja kwenye usaili tulishangazwa na uwezo wako wa kuzungumza lugha nyingi nadhani ndio kigezo kilichotufanya kukupatia kazi , licha ya kwamba maswali mengi ulijibu”Aliongea Dorisi na kumkumbusha Roma kipindi kile.
“Hahah.. Hubby nasikia mkeo alikuacha njiani ukiwa huna hata mia ndio ukaweza kukutana na Dorisi kwa mara ya kwanza na kumuomba hela ya nauli”Aliongea Rose huku akishindwa kuzuia kicheko.
“Naweza kusema kila mmoja wenu nimeweza kukutana nae kwa mtindo wa aina yake”Aliongea Roma huku akianza kukumbuka namna ambavyo aliweza kukutana na Edna mke wake.
Dorisi na Rose walionekana kucheka sana mara Roma alipowaeleza namna ambavyo alianza mahusiano na Nasra hawakuamini kama Nasra alianza kuvuliwa nguo na kubakia uchi bila kujielewa.
Wakati wakiendeleza stori Roma aliweza kupokea simu kutoka kwa Makedoni na kuweka sikioni .
“Mfalme Pluto nimejaribu kutafuta jina Naira Ryani na nimegundua taarifa ambayo sio ya kawaida”.
“Unamaanisha nini taarifa isiokuwa ya kawaida?”
“Kwanza namna ya kuupata ukweli ilikuwa ngumu kidogo , kwani inaonekana taarifa zinazohusiana na huyu Naira ni Top Confidential ndani ya serikali ya Marekani , nimejaribu kuomba ‘Clearence’ kutumia koneksheni zangu na kuweza ku access faili linalohusiana nae , lakini nilichopata kimeniacha mdomo wazi”
“Unanipa shauku Makedoni hebu nielezee ulichoweza kufahamu”
“Naira ni mtoto wa marehemu Ryan Kennedy , Agent mbobevu aliekuwa chini ya kitengo cha CIA chini ya idara ya SID ,mwaka 1990 taarifa zilionyesha Ryan Kennedy alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani na alikuja kupatikana mwaka 2005 , nikatafuta kwa haraka haraka kwanini Ryan alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani ndipo nilipoweza kupata faili la siri sana ambalo lilinishangaza”Aliongea
“Faili linahusiana na nini?”
“Project Pro Human”Aliongea Makedon na kumfanya Roma kukumbuka kitu lakini hakutaka kwanza kuingilia maongezi ya Makedon.
“Project Pro human kwa taarifa hapa nilizonazo inaonekana ilifanyikia ndani ya taifa la Bolivia kwenye msitu wa Amazoni kilomita kadhaa kutoka La paz , ni project ambayo ilianzishwa kwa siri sana na muuza madawa ya kulevya maarufu kutoka Mexico , mfalme Pluto ngoja nikutumie faili kwa njia salama uweze kujisomea mwenyewe”Aliongea Makedoni na Roma alikubali na ndani ya dakika chache tu faili liliweza kumfikia na alifungua na kuanza kusoma na alijikuta akikunja sura .
Ndio kama unakumbuka vizuri Project Pro human iliofanyika nchini Bolivia basi ndio taarifa ambayo alikuwa akisoma Roma , hakukuwa na utofauti mkubwa , Roma aliweza kukumbuka vitu viwili baada ya kusoma ripoti hio , kwanza kabisa ni stori ya Mellisa Luiz , mwanamama ambaye aliwahi kukutana nae ndani ya hoteli ya Kilimanjaro na kumuelezea kila kilichomtokea mpaka kujikuta kuwa na tatoo kwenye mwili wake ambayo ni kama uraia wa visiwa vya wafu, kitu kingine Roma alichoweza kukumbuka ni Carlos ambaye mpaka muda huo anaofikiria alikuwa ni raia wa visiwa vya wafu , alikumbuka kuna kupindi wakati akiwasiliana na Sauroni alimwambia kwamba walikuwa ndani ya jiji la Palermo Italy kwa ajili ya kumuokoa Carlos ambaye alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani.
Dorisi alimwangalia Roma kwa wasiwasi na kutaka kujua ni kipi ameweza kufahamu.
“Roma umeweza kufahamu nini?”Aliuliza Dorisi na ilibidi Roma ampatie simu yake aweze kusoma mwenyewe , hakuwa na haja ya kumficha.
Dorisi kadri alivyokuwa akisoma alijikuta mikono yake ikianza kutetema huku macho yakiongezeka ukubwa , ni kama alichokuwa akiangalia kwenye karatasi hio lilikuwa jambo la kuogopesha sana.
“Rafiki yako hakuwa wa kawaida Dorisi”Aliongea Roma lakini Dorisi alionekawa kufikiria sana, ilibidi na Rose aweze kusoma faili lakini hata hivyo hakuelewa sana kilichozungumziwa.
“Mama na baba itakuwa walikuwa wanafahamu hili ndio maaa ,,, ndio maana,..”Aliongea Dorisi huku akianza kutokwa na machozi.
“Dorisi unaongea nini, kwanini useme hivyo?”
“Licha ya kwamba nilikuwa mdogo lakini nilikuwa nikielewa maisha ya wazazi wa Naira yalikuwa ni ya kujificha sana . Naira hakuruhusiwa hata kuonekana onekana mtaani na mara nyingi tulicheza ndani ya geti na hata shule hakupelekwa…”
Ni kweli kabisa Naira hakusoma wakati alivyokuwa hapa nchini na wazazi wake hawakuwa na maelezo ya moja kwa moja kwanini Naira hakuwa akieonda shule licha ya kuwa na umri mkubwa.
Naira alimzidi Dorisi kwa takribani miaka minne , hivyo ni rahisi kusema Naira alikuwa dada kwa Dorisi tokea kipindi anazaliwa huko jijini Arusha na kwakuwa familia ya Dorisi na ya Ryani na mke wake Epholia walikuwa na ukaribu , hivyo ni kama waliishi kama ndugu na ndio maana wakati Dorisi ni kichanga alikuwa akilelewa na Naira mpaka Dorisi anakuja kuwa mkubwa wa miaka sita mlezi wake mkubwa alikuwa ni Naira , ni kama walikuwa kitu na mdogo wake na Naira alitokea kumpenda sana Dorisi kama mdogo wake.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba licha ya Dorisi kuanza shule upande wa Naira hakuwa amehudhuria kabisa masomo na jukumu la elimu yake lilibakia kwa wazazi wake , lakini licha ya hivyo Naira alikuwa ni moto wa kuotea mbali kwani alikuwa na kichwa chepesi mno kuliko binadamu wa kawaida , ilifikia kipindi hata hakupenda kabisa kufundishwa na wazazi wake na alichohitaji ni vitabu na sio kufundishwa..
Watu hawakuuliza sana maswali ya kwanini Naira hakuchangamana na watu wengine na yote hio ni kutokana alikuwa mtoto wa kizungu na watu hawakuwa wenye kuhoji sana kwani watoto wa kitanzania walikuwa waoga sana kila walipomuona Naira , lakini pia Naira hakuwapenda kutokana na kwamba akili yake ilikuwa ikipevukwa haraka sana , hivvyo ilikuwa ngumu sana kumwambia acheze na watoto ambao akili zao zilikuwa zikipevuka taratibu sana , hivyo maisha ya Naira yaliishia kuwa ya kipweke na mtu aliechangamana nae alikuwa ni Dorisi na hilo ni kutokana alimchukulia kama mdogo wake.
Kipindi Dorisi ndio anaaanza kujitambua ndipo Naira aliweza kuondoka na wazazi wake lakini ndio ambapo Ryani na Epholia walipoweza kumpoteza Naira wakati Naira akikaribia miaka kumi.
Naira alichukuliwa na Athena na kupelekwa makao makuu ya Zeros organisatioa na ni huko ambako Naira aliweza kupata elimu yake ambayo haikuwa rasmi ya chuo , lakini kutokana na uwezo wake usio wa kawaida aliweza kuwa msaada mkubwa sana hata kufumbua baadhi ya mafumbo ya mpango LADO.
Hivyo ni rahisi kusema Naira alishawahi kushiriki kwenye mpango LADO kama mwanasayansi ijapokuwa mpango huo wakati unaaza hakuwepo.
Huenda pia ikawa kweli kupotea kwa wazazi wa Dorisi ni kutokana na kujua historia iliokuwa nyuma ya Naira.
Roma alifikiria swala hilo kwa mantiki na kuona ni jambo ambalo linawezekana na kilichobakia ni kutafuta uthibitisho tu kama kweli wazazi wa Naira walikufa kwasababu walikuwa wakiujua ukweli kuhusu Naira.
“Dorisi kwasasa hupaswi kua na huzuni nakuahidi nitachimba na kuujua ukweli wote”
“Lakini Hubby kama hayo yote ni ya kweli inamaanisha huyu Naira sio wa kawaida na ni jambo la kuwezekana kwa Naira kuwa na urafiki na The Doni”
“Upo sahihi lakini siamini kama huo ndio ukweli wote , kuna sababu kubwa za The Doni kumfanya Naira rafiki yake , huenda anamtumia kwenye mipango yake”Aliongea.
“Unasema Naira atakuwa hatarini?”
“Kwasasa anaweza kuwa salama lakini baadae anaweza kuwa hatarini”Aliongea Roma na kisha Roma alipiga tena simu kwenda kwa Sauroni.
“Mfalme Pluto nadhani hata wewe umeshangaa”
“Naweza kusema hivyo , lakini dunia ni pana sana na yanayoendelea ni mengi hivyo nishazoea, Nataka unisaidie kuangalia ni eneo gani ambalo Naia yupo kwa sasa”Aliongea Roma.
“Hilo nafanyia kazi , lakini taarifa hapa inaonyesha wazazi wake walimpoteza na hawakuweza kufanikiwa kumpata tena , mfalme Pluto hii ni taarifa kubwa nadhani nitakupatia majibu nikipata chochote”Aliongea na Roma alikubali.
Muda ulikuwa umeenda hivyo Roma aliaga kuondoka huku akihidi akirudi China ataendelea kufatili habari zaidi za Naira pamoja na Clielia Allisanto
Ni asubuhi Roma mara baada tu ya kuamka alitafuta namba ya Profesa Clark ili kujua ana majibu ambayo amepata kwani juzi yake kupitia Sauroni aliweza kumpatia kazi ya kumtafuta Yan Buwen ni wapi alikuwa akifanyia mawasiliano.
“Umepata majibu?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Profesa ambaye alikuwa akiachama kuonekana alikuwa na usingizi.
“Ndio inaonyesha alifanya mawasiliano akiwa Beijing China sijui ni upande upi lakini mwelekeo ni upande wa Kaskazini magharibi sijaweza ku’pin point’ sehemu kwani ‘IP adress’ aliotumia sio ya kawaida lakini nina uhakika anahusika hakuna mtu wa kuweza kufanikisha jambo hili tofauti na Yan Buwen”Aliongea Clark.
“Inaonekana kweli aliweza kuondoka hapa nchini muda mrefu”Aliongea Roma.
“Roma unafikiria kufanya iin juu ya hili, maana kila nikifikiria Yan Buwen kuweza kufanikisha kutengeneza kopi yake inanifanya kuamini ni hatari sana”Aliogea Profesa.
“Ndio maana nataka niende China , naamini kuna maabara huo upande wa Kaskazini magharibi”Aliongea Roma.
HatariiiiSEHEMU YA 436
Roma hakutaka kumzuia Yan Buwen kabisa kutokuua familia yake , kwanza ni mambo ambayo hayakuwa yakimhusu na pili familia hio ndio iliomwingiza katika mambo ya kutengeneza siraha za maangamizi ili tu kuweza kushindana na Hongmeng.
Lakini hata hivyo swala la kuua familia yake mwenyewe lilimfanya Roma kuuona Yan Buwenn kiumbe cha hatari sana ambacho kwa namna yoyote ile alitakiwa kumwangamiza hapo hapo kwani kitendo alichokifanya hakuweza kufikiria hata siku moja mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya..
“Nakubali umekuwa chizi kuliko nilivyofikiria , lakini kabla hatujaanza mapambano yetu niambie kwanini ukaamua kuwa adui yangu , maana hakuna siku yoyote ambayo nilishawahi kukuchokoza”Aliuongea Roma
“Haijalishi chochote kwasasa”Alijibu .
“Kweli! Unaweza usiamini lakini swali langu ndio sababu ambayo imenifanya muda wote nisikuchukulie hatua licha ya kunichokoza mara kibao, nadhani unakitaka kifo sasa”
“Hahaha,.. unafikiri unweza kunishinda mimi?”Aliuliza Yan Biuwen lakini Roma hakumjibu , ukweli alichokitaka ni kujua kwanini ghafla tu Yan Buwen akaanza kumuwinda yeye kwani hakuwa na ugomvi nae.
“Nadhani hata hivyo napaswa kukujibu , mwanzoni sikuwa na haja na wewe kabisa , lakini nilikuja kugundua unamiliki kitu cha thamanni ambacho hakikuwa cha kwako , hata hatua yangu ya kufika Tanzania ilikuwa ni kukipata , unaweza ukashangaa labda kwanini nikakaa Tazania kwa ajili ya tafiti zangu lakini ukweli kabla ya kuja Tanzania nilikuwa na makazi mengine bora zaidi kuliko maabara ile ya kipuuzi kule Tanzania , lakini hata hivyo mimi Yan Buen nimekuwa wa kupata kila ninachokitaka katika dunia hii..”Aliongea
“Ulikuwa ukitaka nini kutoka kwangu?, mpaka sasa kama unahitaji Jiwe la kimungu halipo kwenye umiliki wangu, nini unachokitaka kutoka kwangu”
“Huna haja ya kufahamu , lakini kaa ukikumbuka hivi , kifo chako pekee ndicho kitathibitisha kwamba mimi ndio mmiliki pekee wa dunia , I am strongest man in the world”
“Sijawahi kujitangaza mimi kama ni mmoja wapo ya watu wenye nguvu ndani ya dunia hii”Alijibu Roma.
“Lakini kuna watu wanaamini una nguvu kuzidi mtu yoyote ndani ya dunia hii na ndio maana nitaichukua nafasi yako kwa kukuua”Aliongea Yan Buwen.
“Nani anaamini hivyo?”
“Unaongea sana Hades, haijalishi tena kukuambia kwani mpaka sasa wewe ni mfu”Aliongea na palepale nguvu isioelezeka ilianza kumzingira kiasi cha kutengeneza mwanga flani wa rangi ya Cyan lakini ambao haujakolea sana lakini angavu mno kiasi kwamba ulifanya mazingira kuwa na mwanga , Cyan ni mwanga ambao unazalishwa kati ya rangi ya bluu na kijani katika mwimbi ya wevu 490nm kwenda 520nm , inasemekana kwenye anga la sayari ya Uranus ndio imekithiri.
Sasa mwanga ule ulikuwa ukimzunguka huku ukitengeneza kama wingu flani hivi la rangi hio kuanzia chini kwenye miguu mpaka kichwani huku ukiambatana na upepo mkali, kadri nguvu ilivyokuwa ikizunguka ndio anga lote lilivyoanza kucheza cheza kwa kupinda.
Roma alishangazwa kwani ilikuwa ni nguvu sawa kama ya Clone alilopambana nalo siku chache zilizopita lakini awamu hii nguvu hii ilikuwa kubwa mno.
“I am sue you have come into contact with my creations , So please enjoy it while it last”
“Naamini ushakutana na kiumbe changu , hivyo furahia uwezo wangu kadiri unavyodumu”Aliongea kwa kujigamba huku akicheka kama chizi na kusogelea Roma kwa spidi ya mwanga akilenga eneo la moyo wa Roma.
Roma alishajua alichokifanya Yan Buwen ni kutengeneza mbinu ya kucheza na kanuni za anga kwa kutengeneza uzio nyuzi nyuzi sambamba(disorderly Paraller space fabric) ili kwamba hata kama Roma angekuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga kushambulia basi ashindwe.
Hata hivyo aliamini huenda Yan Buwen alimtegemea angeweza kutumia kanuni za anga kushambulia , lakini yeye alitumia mbinu za kijini.
Roma palepale aliita nguvu ya kijini ya kimaandiko na ilitengeneza ngao flani kama kioo na ni muda huo huo Yan Buwen aliweza kumfikia hivyo mgongano wa ngao na nguvu ya Yan Buwen ulitengeneza mtetembo kama wa bomu huku cheche kama za radi zikisambaa eneo lote kutoka kwenye ile ngao ya Roma aliotengeneza.
Mtikisiko ule ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ulisambabisha hata jengo la nyumba hio na ukuta wake kuporomoka chini , lilikuwa ni jambo ambalo lilimshangaza Roma kwani Yan Buwen alikuwa na uwezo mkubwa sana kiasi kwamba ilimshangaza na kujiuliza imekuwaje Yan Buwen kuwa na uwezo mkubwa kiasi hicho kwani mara ya mwisho alionekana kuwa wa kawaida tu.
Yan Buwen mara baada ya kuona pigo lake la kwanza halijafanikiwa alipiga tena kwa mara mbili mfululizo , lakini ngao ya Roma iliuonekana kuwa ngumu , lakini hata hivyo alivyopiga mara ya tatu ilitengeneza uwazi hivyo hakutaka kuchelewasha kwani palepale alilenga ngumi iliojaa mwanga kama wa jiwe la kimungu na kuipitisha kwenye uwazi.
!POW!
Baada ya ngumi ile kumpata vyema Roma kwenye kifua alirushwa kwenda juu kama vile ni mpira huku akizunguka zunguka kwenye hewa na baada ya kufika mwisho alirudi chini kwa spidi lakini palepale alitumia uwezo wake wa kijini kupunguza spidi ya namna anavyoshuka , lakini kabla hajakanyaga Ardhi , Yan Buwen alileta teke lenye nguvu isiokuwa ya kawaida na kwakua alitumia spidi kubwa Roma alizubaa na kushindwa kukwepa.
“Arrgh…”Roma alitoa ukulele mara baada ya kupokea bonge la teke na kwenda kutua kwenye mlima wa mawe yaliorundikwa sehemu moja mara baada ya nyumba ile kubomoka.
Yan Buwen mara baada ya kuona amefanikisha kumpiga mapigo mawiali Roma na kumpeleka chini alipaa juu angani akimwangalia kwa chini.
“Hahaha… naona kupokea kipigo ndio unachoweza pekee , vipi umekuwa mdhaifu kwa kapigo kadogo kutoka kwangu”Aliongea kwa kimandarini akimwangalia Roma aliekuwa akiugulia maumivu chini ya rundo la mawe.
Lakini Roma alivyotaka kusimama vizuri Yan Buwen alimsogelea kutoka juu kama mshale , lakini kabla hajamfikia liliamika jiwe kubwa pembeni na kumlenga Roma.
PUUH!,
Jiwe lilimpiga kisawa sawa Roma na kumfanya kutema damu huku akipiga magoti kwa maumivu.
Alijikuta akipeleka mkono mdomoni na kujifuta huku macho yake yakiwa mekundu kama yanaanza kutoa damu.
Roma alitaitiwa mapema sana tofauti na alivyokuwa akipambana na Poseidon,nguvu aliokuwa nayo Yan Buwen haikuwa ya kitoto.
“Haha.. Etia anaitwa Pluto upuuzi mtupu , wewe ni kichekesho , kwangu nakuona kama kunguni tu ambaye nakuua na vidole , hustahili hata kuwa mshindani wangu pumbavu”Aliongea Yan Buwen na Roma alijitahidi kusimama vizuri baada ya maumivu kupungua.
“Here is my advice for you , I’m reissuing my clone offer , Be my slave and I might let you live”
“Huu ndio ushauri wangu , ninakupatia tena ofa kama nilivyotoa maagizo mwanzo kwa clone langu , kuwa mtumwa wangu na ninaweza kukuacha hai”Aliongea Yan Buwen
“Halafu tena kabla sijasahau , unao warembo wengi , nafikiri pia wanaweza kuwa msaada kwangu nina kwani nina Clones nyingi na zina nyege hatari , itakuwa jambo zuri kama warembo wako watatoa huduma kwao wote , nataka wewe mwenyewe uangalie namna Clones zangu zinavyofanya mapenzi na mademu zako hahahah..”
Kauli yake ni kama ilimfanya Roma aliekuwa amesimama kivulini kurudiwa na nguvu zake zote , kwani hasira zilimpanda kiasi kwmaba zilisambaza nguvu isiokuwa ya kawaida ndani ya eneo lote.
“Unaonekana bado una vinguvu vya kuweza kupambana , ngoja tuone ulichonacho kwa sasa”Aliongea Yan Buwen mara baada ya kuhisi nguvu isiokuwa ya kawaida.
Sasa ukumbuke Roma wakati alivyokuwa akipigana macho yake yalikuwa kawaida kabisa licha ya kwamba yalikuw mekundu , lakini awamu hii Yan Buwen alivyotaja warembo wake na kusikia kuna kopi nyingi zinazofanana nae ,viini vya macho vilibadilika rangi kutoka weusi na kuwa nyekundu na miale kama ya laser.
Yan Buwen mara baada ya kushuhudia Roma kabadilika macho alijikuta ile hali ya kuamini angeweza kushinda pambano ilimpotea mara moja
Roma sasa alikuwa kama nusu shetani kwanza ,alitoa ulimi na kulamba damu zilizokuwa zikimtoka kwenye midomo yake.
“Niliamua kutokuwa siriasi na wewe , kwasababu nilikuwa nikihofia kulikorofisha anga lakini sasa hivi sina haja ya kucheza mchezo wa kitoto na wewe , nitakuonyesha nini maana ya kupigwa na radi harafu na kupona”
“Haha unaongea sana , kuna mtu unajaribu kumsubiria…”Aliongea lakini kabla ya kumaliza sentensi yake palepale aliposimama ni kama alikuwa akivutwa na nguvu isiokuwa ya kawaida kiasi kwamba alikuwa akikosa balansi ya kuendelea kudumu kwenye anga lakini wakati huo huo akihisi mkandamizo ambao sio wa kawaida kabisa , huku Roma akiwa amesimama akimwangalia kwa macho ya hasira.
“Hii ni…”Alijikuta akitoa macho mara baada ya kugundua nguvu ni kama zinapotea mwili wake na kumwangalia Roma kwa mshangao.
Uwezo wa Roma ulikuwa umeongezeka zaidi ya mara ishirini kuliko alivyokuwa akipambana mwanzo , alikuwa ni kama mtu mwingine kabisa.
Wingu lilianza kuzunguka juu kama vile mvua inataka kunyesha na nyota zilizokuwa zikionekana zilibwa na wingu.
BOOM, BOOM, BOOM
Ngurumo kali ilipiga ikiambatana na radi lakini ambayo haikufika chini huku mawingu yakizidi kusuguana na kusababisha umeme.
Roma aliangalia juu angani mara baada ya ngutumo na kuona ahueni na kisha alipiga hatua moja mbele , lakini kilichomkuta Yan Buwen ni kwamba aliporomoka chini huku akianza kukosa hewa, alikuwa ni kama yupo kwenye chumba chenye moshi mwingi.
“Kwanini umekuwa kimya ghafla , nia yako ya kuniua na kuwachukua wanawake wangu ipo wapi , hii ndio nafasi yako ya mwisho ichukue”Aliongea kwa sauti ndogo lakini ni kama ilikuwa ikitoka juu angani kwani ilikuwa kama mwangwi.
Yan Buwen alijitahidi kushindana na nguvu iliokuwa ikizunzuia kutofanya chochote lakini alishindwa.
Upande wa Roma mwenyewe alihisi mabadiliko yasiokuwa ya kawaida ambayo hakuweza kuyatarajia , siku zote alikuwa akiita nguvu za kijini akitaka kupambana lakini sasa hivi sio kama alikuwa akiziita lakini yeye ni kama ndio nguvu zenyewe za kijini na zilikuwa zikiamua kipi cha kufanya.
“Uli ., ulificha uwezo wako kumbe?”Aliongea Yan Buwen kwa shida sana.
“Unatakiwa kujichukulia wa juu kwani siku zote situmiagi uwezo wangu kwa watu wa kawaida ,, ninaweza kukuua bila ya wewe mwenyewe kujua kama umekufa , nina miaka elfu moja sijawahi kuamshwa na kuwa na nguvu kiasi hichi ndani ya uso huu wa dunia”Iliskika sauti ambayo haika sio ya Roma bali ni kama ya kijini inayomtawala ndio inayoongea.
“Acha kujihisi una uwezo mkubwa sijashindwa bado”Aliongea Yan Buwen na palepale alijikakamua kwa uwezo wake wote na kuchomoka kwenye nguvu iliokuwa ikimzuia chini kutopaa na alifika juu hewani na kumfuata Roma kwa namna ya kurusha shambulizi , lakini Roma alitoa tabasamu la kifedhuli nakukunja kiganja na kisha akakifumbua na kurusha kibao juu angani.
BANG!
Yan Buwen alirudishwa kutoka juu kwa spidi isio kuwa ya kawaida na alishindwa kujiongoza na kwenda kuyavamia mawe ya ukuta kiasi kwamba sehemu aliodondoka ilitoa vumbi zito.
“Inaonekana unaweza kufa kwa pigo moja tu”Aliongea Roma lakini nguvu ilianza kujikusanya tena kwenye mwili wa Yan Buwen kwa kupepesa macho tu.
“Inaonekana kwangu nguvu zako ni za aina yake lakini sio kama za kwangu , ninaweza kuzifyonza zote na kuzitoa kwenye mwili wako nakushauri utii amri kama sijakuua kwa zaidi ya mara kumi”Aliongea Roma vile vile huku sauti ikiwa sio kama ya kwake kwani ilikuwa nzito na ya kuogofya mno.
Yan Buwen alijikusanya kwenye vumbi kwani nguvu zake zilikuwa zimemtoka nyingi na huenda angekuwa mfu kwa wakati huo
“Siwezi kukubali kushindwa…”Aliongea kwa hasira na kuamka kama mwanga wa radi.
BOOM!
Ni vipande vipande vya nyama vilivyosambaa angani , ilionekana Roma alimtegemea ndio maana akamtanguliza na shambulio kama la bomu ambalo lilimsabaratisha
Lakini licha ya kusambararika ilionekana nguvu isiokuwa ya kawaida ikikisanya vile vipande vipande vya nyama pamoja na damu yake kwenda sehemu moja pasipo ya kudondoka chini, lakini Roma hakuteka kuruhusu tukio hilo , alirusha tena pigo lingine na kusambaratisha tena, lakini ajabu tena vipande vilikusanyikka kwa spidi kubwa sana ni kitendo cha kupepesa macho tu Yan Buwen alirudi tena kwenye uhai wake na kumfanya Roma kutoa macho.
Lakini kabla hajaamua cha kufanya ni nini , palepale mwili wa Yan Buwen ulibadilika na kufunikwa na suti flani hivi ya aina yake na kumziba mpaka kichwa , ilionekana ilikuwa ni kama ngao
Roma alishangazwa na vazi la Yan Buwen kwani ni kama vile alikuwa akiangalia muvi ya Avenger end game.
“You can’t kill me , I have this..”Aliongea Yan Buwen akiwa amefunikwa kichwa chake kama vile ni Spiderman huku mkononi mwake kukionekana kitu kama kitenesi kikitoa mwanga mkali sana wa mng’ao
“The Godstone,! This whole time it was you?”Aliuliza Roma kwa mshangao usio na kifani huku akimaanisha kwamba kilichomtokea siku ile mpaka kupoteza jiwe hilo la kimungu ,lakini vile vile kule Ufaransa kupoteza teknolojia ya Thanatos , lakini pia kupotea kwa Moses Vampire na Holygrail , mambo yote hayo yalikuwa ni yeye , Roma alijiambia haiwezekani ndio maana alitoa mshangao usio na kifani.
Jambo moja lingine ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba lile jiwe lilikuwa limebadilika ukubwa wake na sasa lilikuwa likitoa mwanga mkali sana unaoumiza macho mweupe lakini mfano wa jua , ni haki kusema kwamba Yan Buwen huenda kajua siri ya jiwe hilo.
Yan Buwen hakueleweka alifanya nini na lile jiwe lakini alilirusha juu angani na likanasa na palepale lilitengeneza shimo nyeusi kubwa ambalo anga lake ni kama linachemka kwa spidi kubwa ni kama unaangalia BlackHole , mwili wake ulivutwa kwa kasi sana na lile shimo na akapotea palepale kwa namna ya kuyeyuka.
Roma alijaribu kuzuia shimo liile lakini nguvu yake ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba ilimrusha mbali kwa kumkataa.
Roma alijikuta akianza kuhema kwa tabu , mpaka hapo aliamini huenda Yan Buwen alitumia jiwe hilo kuweza kuwa na nguvu kama hizo , ilikuwa mantiki kufikiria hivyo , lakini swali aliwezaje kufahamu kanuni za anga kirahisi hivyo kwanni hakuwa na uungu wowote ndani yake
Pumbavu”Aloijikuta akitoa tusu huku aking’ata meno yake kwa hasira kwa kitendo cha Yan Buwen kumkimbia , alijua aliweza kumtoroka kwa kutumia jiwe la kimungu, ijapokuwa miaka mingi lilikuwa chini ya umiliki wake lakini hakuwahi kufikiria jiwe hilo linauwezo mkubwa mpaka wa kutengeneza shimo jeusi angani na kuwa kama njia ya kutoroka.
“Hades usiwaze hatoweza kukushambulia kwa muda hahah..”Ilikuwa ni sauti ambayo inasikika kwenye kichwa chake na kumfanya kutoa macho , ilikuwa ni hali kama ya mtu mwenye ugonjwa wa kuchanganyikiwa.
“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikisikika vyema sasa lakini macho yake hayajatoka kwenye rangi ya uwekundu.
“Hehe .. umenipa jina mwenyewe unaweza kuendelea kuniita kwa jina la nguvu ya kimaandiko naishi ndani ya mwili wako , mimi na wewe ni ndugu wa damu chanda na pete una mwili mzuri sana kwa ajili ya mimi kuishi”Sauti ilisikika kwenye akili yake na kumfanya Roma kushika kichwa kwa namna ya kuchanganyikiwa.
“Achia akili yangu”
“Sawa kwasasa nitakuachia akili yako , lakini kadri unavyozidi kuwa na nguvu ya kijini itafikia siku lazima nitaiongoza akili yako kabisa,mwili wako unanifaa sana ngoja niendelee kulala nikisubiria siku yangu ya kurudi uraiani”Iliongea Sauti na kumfanya Roma ang’ate meno yake kwa hasira na palepale macho yake yalirudi kwenye hali yake ya kawaida na ile sauti ikapotea kwenye akili yake.
Alijikuta jasho likimtoka mno hakuelewa ni nini kinachomtokea hata hivyo ni kweli kabisa wakati anajaribu kupambana na Yan Buwen kwa uwezo wake wote ni kama mwili wake hakua ukiuongoza yeye kwenye mapambano, ni kama akili yake ilikuwa ikifanya kazi nusu na nusu nyingine ilitawaliwa.
Lakini hata hivyo Roma alitabasamu kifedhuli kutokana na kwamba ndani ya mwili wa Yan Buwen wakati alivyokuwa amemshikilia kichawi alimwingizia nguvu ya kijini kwenye mwili wake, kitendo ambacho hata yeye akili yake hakuelewa kwanini alifanya hivyo lakini kwa sauti iliomwongelesha anaelewa kwamba ni mtego.
Aliamini lazima mwili wake Yan Buwen utakuwa kwenye maumiu makali , kwani inaonekana nguvu ya jiwe la kimungu na za kijini haipatani ndio maana wakati anasogelea shimo jeusi tofauti na kumezwa yeye alitupwa mbali kwa ishara kwamba shimo lile linamkataa yeye.
Lakini Roma sauti aliokuwa akiisikia kwenye kichwa chake ilimfanya kuwa na wasiwasi lakini hata hivyo aliamini huenda ni akili yake mwenyewe , hivyo aliamua kupuuzia lakini bado roho yake haikuwa na amani.
“Au kuna athari za kutumia kanuni ya kimaandiko?”Roma alijikuta akianza kuwaza mwenyewe huku akiangalia uharibifu uliofanyika.
“Roma nini kimetokea , wewe ndio umeharibu hizi nyumba zote?”Ilisikika sauti kutoka hewani na kumfanya Roma kuangaliai juu alikuwa ni Omari alieonekana ndio anafika.
“Umewezaje kusafiri umbali mrefu mpaka hapa bila kukasiriha anga?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Kuna namna ya kusafiri pasipo kukasirisha aga , nnimefunzwa huko Hongmeng, pumbavu kabisa nimechelewa daah sijaona pambano”Aliongea huku akiongekana kulalamika.
Njia ambayo anazungumzia Omari ya kusafiri pasipo kukasirisha anga ni kusafiri kwa vituo , yaani unaweza kupaa kwa kilomota kadhaa na kisha ukatulia kwa dakika kumi na tano then unaendelea tena kwa kilomota kadhaa , mpaka ufikie eneo husika , uzuri ni kwamba tu nguvu za kichawi zenyewe zinakupeleka sehemu unayonuia kufika haina haja ya kuwa na ramani kichwani lakini athari kubwa ni kwamba kila kituo lazima kiwe ni maji au bahari, yaani kwa mfano ukatoka Tanzania na madhumuni ya kwenda China basi unatakiwa usafiri na uelekeo wa bahari tu ili kila ukifikisha kilomita kadhaa , unatumbukia majini na kukaa huko kwa dakika kumi na tano na unaibuka tena unasafiri tena kwa kilomita kadhaa halafu unaingia tena majini unajificha ndani ya maji kwa dakika kumi na tano unaibuka tena , ilikuwa ni mbinu ngumu kwani inahitaji ujasiri lakini inakuwezesha kusafiri kwa muda mfupi.
Hivyo kimahesabu ni kwamba Omari alianza safari kabla ya Roma kwani kuna vituo vingi sana ndani ya maji ambavyo lazima Omari alipumzika kabla ya kuendelea na safari.
Hivyo unaweza ukaona jini linaibukia baharini usiku ukashangaa lakini ukweli ni kwamba bahari au ziwa ni njia salama ya majini kusafiri pasipo kukumbana na malipizi ya anga.
“Taarifa za Yan Buwen kuua familia yake zinasambaa sana kuna rafiki yangu hapa China nilianza kufikia kwake na kupata habari hizo , inasemekeana walinzi ndio walitoa habari, Vipi umefanikiwa kumdhibiti”Aliuliza Omari huku akikagua namna eneo lilivyoharibika.
“Amenitoroka bwana”Alijibu Roma kinyonge.
“Hapana , amewezaje kutoroka mbele yako nadhani ni afadhari nimekuja baada ya mapambao kuisha huenda ningekufa hapa hapa, maana huenda ningepatwa na hasira na kushindwa kujizuia mpaka kumpiga ngumi”
“Unashindwa vipi kujizuia au kwasababu mwanamke wako kamtia mimba?”Aliuliza Roma kwa kejeli.Lakini Omari alionekana kutopendezwa na swali lake
“Najua huenda huna hela yoyote na pia mavazi yako yamechafuka , twende kuna sehemu salama ya sisi kwenda kula msoni na kupata hifadhi ya kulala”Aliongea Omari.
“Nani kakuambia sina pakuishi”Aliongea Roma na palepale licheza na anga , kilikuwa ni kitendo kama alichofanya Clelia allisanto wakati akitoa kiboksi cha uwa angani.
“Hades kuna uwezekano na mimi kujifunza namna ya kutunza vitu kwenye anga?”
“Uwezekano huo huna , nina nguvu ya kiuungu ndani yangu ndio maana naweza pia kujifunza kanuni za anga , wewe ni binadamu wa kawaida ambaye umejifunza mbinu za kijini”Aliongea Roma huku akiangalia kipi cha kuchukua kwenye shimo ambalo linatumika kama sehemu ya kuhifadhia vitu kwenye anga , aliachana na pete na kisha akachukua kadi ya benki na passport yake ya kusafiria.
“Hivi ni vibali ambavyo vinaweza kunipatia makazi kwenye hoteli yoyote hapa nchini China pambana kivyako sijakuambia unifuate huku China”Aliongea na kabla hata Omari hajaongea neno , palepale Roma alipotea na kumuacha Omari akiwa kwenye mshangao.
“Pumbavu zako Hades , nimekufuata mpaka China halafu umeniacha nitakupata tu”Aliongea Omari huku akiangalia baiti moja iliofukukiwa na mchanga uliotokana na kuharibika kwa nyumba na alisikitika kidogo na kisha akapotea ndani ya eneo hilo mara baaada ya kusikia magari ya polisi yakisogelea hilo eneo.
Unafikiri sauti iliomuongelesha Roma inatokana na nguvu za kijini anazojifunza , kama kweli ataendelea kupanda levo je nguvu ya kimaandiko itaweza kutawala akili yake , nini kitaendelea tukutane kesho.
Tutajie ivo vigongo twende uko mkuuVipo vigongo vingi.uku ukipata arosto.unaamia kwingine .wala akuna haja ya kuuliza kila ck lini mwendelezo.
Amesema kesho asubuhiKesho ndio leo naona unatuletea miyeyusho tu bwana singanojr..
Kwamba anayeyusha sio? Wacha ajibu kwa vitendo kabla siku haijageuka.Kesho ndio leo naona unatuletea miyeyusho tu bwana singanojr..