Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 439.

Rufi aliwahi kuamka mara tu baada ya kufikishwa hospitalini na kupokelewa na madaktari , ilionekana hakuumia sana zaidi yakupata michubuko kidogo tu jambo ambalo hata Edna lilimshangaza kidogo na kushukuru kwa wakati mmoja.

Baada ya nusu saa ya Edna na Innocent kusubiri nje ya chumba cha wagonjwa wa dharula hatimae waliruhusiwa kuonana na mgonjwa wao ambaye tayari alishazinduka.

Edna baada ya kumuona mgonjwa wake alishangazwa na mwonekano wake , kwanza alikuwa mzuri lakini kitu cha pili alionekana kuwa na rangi mchanganyiko ambayo ilimfanya amuone kama ni Yezi , utofauti pekee kati ya Yezi na mgonjwa wake ni kwenye macho , mwanadada aliekuwa mbele yake alikuwa na macho kidogo ambayo kwa haraka haraka aligundua alikuwa ni mchina.

Edna alimsalimia mgonjwa kwa kuanza na lugha ya kiswalihi na ndipo alipogundua hakuwa akijua lugha ya kiswahili kabisa na ilibidi atumie lugha ya kingereza na hapo ndipo alipomfahamu kwa jina la Rufi Wangsi.

Jambo la kwanza ambalo Edna alitaka kulifahamu kutoka kwa Rufi mara baada ya kuomba msamaha ya kumgonga na gari ilikuwa ni kutaka kujua ndugu zake hapa Tanzania ili waweze kutaarifiwa kufika kumuona lakini jibu ambalo Ruffi alitoa lilimfanya Edna kushangaa.

Kwanza kabisa Rufi alisema hakuwa na wazazi kwani baba yake alikwisha kumtelekeza lakini pia mama yake hakuwa akimfahamu na hata ujio wake hapo Tanzania ilikuwa ni kujaribu kuangalia fursa zinazopatikana aweze kujiendeleza kimaisha.

Maneno ya Rufi yalimshangaza Edna lakini kwa wakati mmoja aliweza kuyaamini kwani Rufi alionekana kabisa hakuwa akidanganya . lakini ukweli ni kwamba Rufi alikuwa akidanganya kwnai ujio wake ndani ya Tanzania sio kwa ajili ya kutafuta maisha bali ni kwa ajili ya kumtafuta mwanaume anaefahamika kwa jina la Roma , mwanaume aliekutana nae ndani ya jiji la Los Angeles.

Haikueleweka mara moja kama Rufi alitokea kumpenda Roma au alikuwa na shauku ya kumjua zaidi kutokana na kuweza kumponyesha sumu iliokuwpo kwenye mwili wake miaka na miaka lakini uhakika ni kwamba Rufi alikuwa akimjua vizuri tu Edna kama mke wa Roma na huenda hata kugongwa na gari ilikuwa sehemu ya mipango yake.

Sasa wakati Roma anafika ndani ya hospitali hio upande wa Innocent alikuwa ashaondoka kwa kupewa maelekezo mengine na Edna , hivyo Edna kutokanna na kuguswa na stori ya Rufi ndipo alipoweza kuwasiliana na Roma na kumwambia kile kilichotokea lakini kubwa zaidi ni kama Edna alitaka na Roma aweze kusikia stori ya Rufi jambo ambalo Rufi alifurahi mno.

Edna alikuwa ni moja ya wanawake wanaoguswa kirahisi na matatizo ya watu hivyo kwa mwonekano wa Rufi kuweza kufanana na wa Yezi , lakini pia udogo wa umri wa Rufi vilimfanya kumuonea huruma , hakujua kwanini Rufi aliamua kuja Tanzania na sio kwenda kwenye mataifa yalioendelea kwa ajili ya kutafuta maisha.

“Kwanini ukaamua kuja Tanzania kutafuta maisha na sio nchi nyingine ambazo zina fursa nyingi?”Aliuliza Edna mara baada ya Rufi kumaliza kuelezea kwa ufupi stori yake ya uongo na kweli.

“Nimechagua kuja Tanzania kwasababu pia naamini ninaweza kumpata mama yangu”Aliongea Rufi na kumshangaza Edna.

“Mama yako ni Mtanzania?”Aliuliza Edna ijapokuwa Rufi alikuwa na rangi mbili ya kiafrika na ya Kiasia lakini hakuweza kudhania Rufi mzazi wake upande wa mama angeweza kuwa mtanzania.

“Ninachofahmu mama ni mtu wa Afrika mashariki , kwa maelezo ya baba mama alinitelekeza mara baada ya kutimiza mwaka mmoja”Aliongea Rufi na kuendelea kumshangaza Edna lakini ndio muda ambao Roma aliweza kufika ndani ya wodi hio.

Roma mara baada ya kuingia hakuamini mwanamke aliekuwa akiongea na mke wake ni Rufi maswali kibao yalimjia , kwanza kabisa mwanamke huyo alianza na kudukua kampuni yake katika mitambo ya kurushia matangazo lakini swala la pili mwanamke huyo huyo ndio majeruhi aliegongwa na gari mke wake , mpangilio wa matukio hayo ulimchanganya kiasi cha kumfanya aanze kuona haiwezekani kuwa bahati mbaya , huenda yote ilikuwa mipango ya Rufi.

Roma mara baada ya kuambiwa na Eda aingie ndani asisimame mlangoni kama sanamu alijikuta akijongea huku macho yake yote yaikuwa kwa Rufi , alikuwa na wasiwasi ni kitu gani ambacho Rufi alikuwa akiongea na Edna lakini kwa muonekano wa Edna aliamini kabisa Rufi hakugusia swala la wao kukutana nchini Marekani.

“Rufi huyu ni mume wangu anaitwa Roma…., Roma huyu ndio muhusika ambaye nimekuambia tumemgonga maeneo ya Kivukoni lakini kwa bahati nzuri hakuumia sana zaidi ya kupata michubuko na kutegua mguu(Soft tissue injury)”Aliongea Edna.

Upande wa Rufi aliishia kumwangalia Roma kwa macho ya kawaida akijifanyisha kama ndio kwanza wanaonana lakini moyoni alijiona mshindi maana kwa macho ya Roma yalivyokuwa yakimwangalia kwa wasiwasi aliona kabisa atakuwa ashapata kujua yeye ndio mdukuzi.

“Pole sana Rufi”

“Asante sana Mr Roma nimefurahi umekuja kuniona”Aliongea Rufi kwa Kingereza.

“Nisingeshindwa kuja hapa wakati mke wangu kipenzi yupo kwenye shida , hivyo usijali sana ujio wangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna amuangalie Roma na kujiuliza kwanini anaongea kauli kama hio , lakini upande wa Rufi aling’ata meno kwa hasira, alijua kauli ya Roma kwake ni kama tahadhari ya kwamba asifanye chochote cha kijinga , alikuwa na akili hivyo kwake ilikuwa rahisi sana kuelewa kauli zenye zaidi ya maana.

Edna ilibidi amuelezee Roma simulii fupi ya maisha ya Rufi kwanini alikuwa Tanzania, hivyo haraka haraka alimwambia kwamba Rufi hakuwa na ndugu hapa Tanzania , pili alikuwa hapo kwa ajili ya kutafuta maisha pamoja na kumtafuta mzazi wake.

Kila alichosema Edna kilimshangaza Roma , kwanza kabisa alishindwa kuelewa kama maneno hayo ni ya kweli , kwani hata mara ya kwanza kukutana na Rufi ilikuwa ni kwasababu mrembo huyo alitaka kumtapeli hivyo haraka haraka Roma aliona kabisa na mke wake kadanganywa , lakini kwasababau hakutaka dhambi alioifanya Marekani ifahamike aliona atulie tu na asubiri muda muafaka aweze kumuonya Rufi kutomfatilia.

“Kwahio Wife unapanga kufanya nini juu ya mgonjwa?”

“Atakua chini ya uangalizi wangu mpaka atakapo pona kabisa na kuendelea na shughuli zake , nitakuwa mkatili nikumuacha msichana kama huyu akiishi bila msaada wowote”

“Unataka kumsaidia kivipi , mimi nashauri tumpe pesa kiasi itakayomsaidia kwenye mambo yake ya kimatibabu , kuhusu mzazi wake sio jukumu letu”Aliongea Roma kwa kingereza.

“Miss naomba tafadhali usinitelekeze… sina msaada wowote wa mtu ninae mjua hapa Tanzania , nataka kumtafuta mzazi wangu lakini sijui pa kuanzia..”Aliongea Rufi huku akianza kutoa machozi na kumfanya Roma akasirishwe na maigizo yake.

Kitendo cha Rufi kutoa machozi mbele yake kilimhuzunisha Edna , alijua msichana mdogo kama huyo alikuwa akipitia wakati mgumu.

“Huna haja ya kutoa machozi Rufi sawa nitakusaidia kwa kila hatua , ijapokuwa itakuwa ngumu kumpata mzazi wako kutokana na humjui hata kwa sura wala sehemu anayoishi , lakini Mungu siku zote ni mkubwa na kwa wakati wake utampata mama yako”Aliongea Edna huku akimpeti peti Rufi kwa kuzishika nywele zake ndefu na kumfanya Roma aone kazi anayo , mke wake kaingia moja kwa moja kwenye mtego pasipo ya yeye kujua.

Muda huo huo Edna simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la mtu anaepiga aligundua ni Recho sekretari wake.

“Boss saa saba kamili una ratiba ya kuonana na muwekezaji kutoka kampuni ya Kiboko Enterprises , naulizia kama ratiba inaendelea kama ilivyopangwa au nifanye mawasiliano kuweka miadi siku nyingine”Aliongea Recho kwenye simu.

“Ninakuja ofisini muda si mrefu , weka miadi afike moja kwa moja ofisini kwangu”Alijibu Edna.

“Sawa Madam”Aliongea Recho na kisha simu ilikatwa na Edna aliangalia muda na kuona zimebaki kama dakika therathini kuweza kuonana na muwekezaji kutoka kampuni ya Kiboko.

“Unaweza kwenda tu kazini nitahakikisha mgonjwa namsaidia kadri ya uwezo wangu”Aliongea Roma mara baada ya Edna kukata simu na Edna alitabasamu na kutingisha kichwa.

“Kama kuna lolote la ziada utaniambia, Rufi nitaenda ofisini mara moja ila baadae nitapitia kukuona sawa?”

“Okey , Asante kwa mara nyingine Miss Edna”

“Usijali”Alijibu Edna na kisha alimuaga Roma na kutoka.

Baada ya Edna kutoka Roma alifungua mlango na kuchungulia nje kuona kama Edna kashatokomea na baada ya kuhakiki Edna ashaondoka kabisa alifunga mlango na kurudi ndani huku akimkazia Rufi macho, lakini Rufi wala hakumhofia kabisa kwanza kabisa alijiegamiza bila wasiwasi.

“Rufi najua kila ulichomuelezea mke wangu ni uongo , hivyo niambie umekuja Tanzania kufanya nini?”Aliongea Roma huku akiweka sura yenye usiriasi na Rufi alitabasamu na kuufanya uzuri wake kuonekana vizuri.

“Wapi unahisi nimeongea uongo?”

“Acha kujibu kwa kuuliza maswali , ni jibu kwanini upo Tanzania?”

“Usiniangalie hivyo bwana unanitisha”

“Rufi naomba unisikilize , mimi na wewe hatudaiani kabisa na najua upo hapa nchini kwa ajili ya kunitafuta ndio maana ukafanya utundu wa kudukua kampuni yangu , hivyo kama shida ni pesa nitakupatia pia nitakusamehe kwa kosa la kudukua mawasiliano ya Tv Chaneli ya kampuni , hivyo nitahitaji ufute Vidio ile , pili uondoke Tanzania”Aliongea Roma akiwa siriasi.

Roma hakutaka kwa namna yoyote kujihusisha kabisa na Rufi , ni kweli alikuwa ashafanya nae ngono lakini siku ile alimchukulia kama kibudurisho tu cha muda na hata hivyo alishakwisha kumlipa kwa kumponyesha sumu iliokuwa mwilini mwake kwa mabadilishano ya kumtoa Bikra hivyo ni kama hakuwa na deni na mrembo huyo , alijaribu kumshawishi Rufi kwa kutumia pesa kwanni aliamini huenda mrembo huyo ndio alichokuwa akihitaji kutoka kwake , hivyo aliamini anaweza kumaliza hilo tatizo kwa kumpa pesa ili mke wake asijue kile alichokifanya na yeye.

Rufi alimwangalia Roma namna anavyoongea na alijikuta akiishia kucheka kwa sauti , kicheko ambacho hakikuonyesha kama ni cha dharau bali kilionyesha ni kama amefurahi kumuona Roma katika muonekano aliokuwa akitegemea , kwake aliona ni kama ushindi.

“Usicheke nipo siriasi Rufi sitaki nilichofanya mimi na wewe kimfikie mke wangu , mpango wako wa kujigongesha uonekane umepata ajali , lakini pia kudukua chaneli yetu hilo nakubali ni mpango safi lakini kwasasa unapaswa usikilize ninachokuambia”.

“Mr Roma Ramoni najua una pesa nyingi sana na kama mpango wangu ni kuhitaji unipatie pesa zako basi nisingekwenda mbali mpaka kutengeneza ajali kwa kutumia gari ya mkeo lakini pia kufanya udukuzi kwenye kituo cha televisheni, ninachotaka ni kingine kabisa na sio pesa”Aliongea Rufi

“Kama hutaki unahitaji nini kutoka kwangu?”

“Swala la kwanza nimefurahi kukuona kwa mara nyingine , tokea ulivyoondoka nilikuwa nilikuwazia sana , hivyo ni ngumu kwa yale ulionitendea kuweza kuyasahau mara moja na kuendelea na maisha yangu, swala la pili nilichomwambia mke wako sijadanganya, najua nilikuambia nilikuwa na babu yangu ni mgonjwa lakini ile ilikuwa ni uongo”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.

“Niambie unachoitaji ni nini ambacho ni zaidi ya pesa”

“Nadhani swali la kwanza uniulize kwanini nilikuwa na sumu nyingi ndani ya mwili wangu , ni wapi nimetokea , kwanini nina ngozi nyeusi na nyeupe , je nilichomwambia mkeo ni sahihi au sio sahihi , unatakiwa kuniuliza maswali ya namna hio”Aliongea Rufi huku akianza kuwa na uso uliokuwa siriasi na kuonyesha namna ya huzuni na kumfanya Roma kuvuta pumzi kidogo.

“Mr Roma Ramoni sipo hapa kwa ajili ya kukugombanisha na mke wako , bali nipo hapa kumtafuta Mama yangu mzazi, nilipokutana na wewe Loss Angeles nilishakufahamu tayari kwa majina yako kamili na wapi unapotokea”Aliongea Rufi na kumfanya Roma kidogo kushangaa lakini Rufi hakumjali zaidi ya kuchukua mkoba wake na kisha akaufungua na kutoa picha na kumpatia Roma.

Roma alishangazwa na picha hio , ilikuwa ni picha ambayo ilipigwa kipindi cha shindano la Kizazi nyota ni picha ambayo alionekaa yeye , Edna mke wake pamoja na Christen Stewart msanii kutoka Marekani.

“Hio picha ndio ilionifanya nikahamia Loss Angeles kutoka New York, sababu kubwa ya kuhamia Loss Angeles ni kuweza kukutana na Miss Christen ili aweze kuniunganisha kwako”Aliongea Rufi na kumfanya Roma kukunja sura.

“Kwanini ulitaka kuonana na Miss Christena na akuunganishe kwangu?”

“Kama nilivyosema nipo hapa nchini kumtafuta Mama yangu mzazi, kuhusu kutaka kuunganishwa kwako ni stori ndefu sana ila kwa ufupi sana sina ndugu huku duniani wala mzazi wa aina yoyote nipo mimi kama mimi Rufi na nimeishi miaka mitano nchini Marekani kwa kurubuni watu, maisha yangu yalikuwa ya maumivu makali na sikuwahi kuwa na amani hata kidogo , kila siku kwangu nilikitamani kifo lakini sikuweza kufa niliishi kwa mateso makali , lakini mpaka leo siamini mateso yangu yote yaliisha mara baada ya kukutana na wewe , uliiponya maumivu nilioishi nayo tokea nikiwa mdogo…..”Alijikuta akiishia njiani na kuanza kulia na kumfanya Roma kuzidi kuchanganyikiwa kwa kutojua namna ya kumsaidia lakini hata hivyo hakutaka kumuamini Rufi moja kwa moja ,alikuwa ashamjua ni mwanamke mjanja lakini kwenye swala la maumivu ni swala la kweli kabisa kwani yeye mwenyewe ndio aliemsaidia kupona.

“Okey haina haja ya kulia tena , kama kweli umekuja hapa kwa ajili ya kumtafuta mama yako kwanini ukamu’approach’ mke wangu , lakini pia kwanini ukadukua Tv Chaneli yetu?”Aliuliza Roma lakini Rufi hakujibu zaidi ya kuinama chini.

Roma alijikuta akimwangalia Rufi kwa namna ya kumwangalia , ijapokuwa msichana huyo alikuwa na urembo wa kupitiliza lakini hakutaka kujihusha nae alikwisha kujiapiza asingeongeza mwanamke mwingine kabisa kwa namna yoyote, lakini hali ya upweke ya Rufi ilimfanya kumuonea hjuruma kwani hisia alizokuwa akipitia mrembo huyo ni hisia ambazo hata yeye mwenyewe amekwisha wahi kupitia , maisha ya kutokuwa na mzazi wa kumtegemea maisha ya kuwa mpweke ni maisha ambayo Roma aliweza kuishi nayo kiwa miaka mingi kabla ya kufanikiwa kuijua familia yake.

“Kama unataka nikusaidie na niruhusu ukae hapa Tanzania lazima utii masharti mawili matatu”Aliongea Roma mara baada ya kumuagizia Chakula na Rufi alimwangalia Roma kwa shauku ya kujua hayo masharti.

“Kwanza kabisa sitaki kujihusisha na wewe kimapenzi , hilo niweke wazi kabisa , sipendi ugomvi na mke wangu , mimi na wewe deni letu liliisha hivyo kama una chembe ya shukrani lazima unaelewa nilichokufanyia usingeweza kufanyiwa na mtu yoyote yule , swala la pili ufute Vidio zote za sisi tukifanya mapenzi, swala la tatu ijulikane kwamba hatujawahi kukutana mahali popote, Je upo tayari kutii masharti?”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kufikiria kidogo na kisha akamwangalia Roma usoni na akaishia kutabasamu kinyonge.

“Nipo tayari”Aliongea

Ushaonja tayari kitumbua changu ni swala la muda tu utanihitaji tena, nitazidi kujenga ukaribu na wewe mpaka unitake mwenyewe, , Rufi Mission accomplished without Hitch hehe..”Alijiwazia kwenye akili yake , ilionekana mpaka hapo alichokuwa amekipanga kimekamilika kwa aslimia mia moja.

Ni kweeli kabisa kwanza kabisa mrembo Rufi baada ya kufika Tanzania na kuchukua Chumba ndani ya hoteli , mpango wake wa kwanza ni kutafuta namna ya kujenga ukaribu na Roma lakini pia na mke wake , hakutaka kutumia mbinu ya kumtishia Roma kwa kutumia Vidio alizorekodi pasipo ya Roma kujua wakati wakifanya mapenzi kutokana na kwamba alishajua Roma sio mtu wa kawaida na angetaka kuzichukua kutoka kwake ingekuwa ni rahisi sana na mpango wake usingefanikiwa , hivyo alichofikiria cha kwanza ni namna ya kuweza kujenga ukaribu na Edna na wakati huo huo akijitambulisha kwa Roma kwa namna ya kipekee , katika kuwaza kwake namna ya kufanikisha jambo lake ndipo moja kwa moja alipopata wazo la kutumia uwezo wake wa akili na taaluma yake.

Rufi n kweli aliishi Marekani kwa miaka mitano na katika miaka yote hio aliweza kujifunza vitu vingi kwa namna isiokuwa rasmi , yaani kwa njia ya mtandao.

Kwanza kabisa alijifunza lugha ya kingereza na kuielewa vizuri na baada ya kukamilisha kujifunza lugha hio alianza kujikita kwenye kujifunza matumizi ya kutumia Kompyuta na ndipo alipochagua somo la Computer Science kwa kuchukua kozi maalumu kwenye mtandao wa Udemy pamoja na alijikita kwenye kujifunza lugha zaidi ya nne za Programing , alijifunza PHP, Python , JavaScript pamoja na C++.

Aliweza kujifunza kwa haraka kutokana na kwamba alikuwa na uwezo mkubwa wa kiakiri wa kukariri vitu na kutovisahau lakini pia kilichomsaidia zaidi ni mara baaada ya kujenga urafiki na moja ya wanafunzi wa chuo cha Columbia.

Njia rahisi ya kupata marafiki ndani ya jiji kubwa kama New York ni ule upekee ambao mtu kwenye jambo husika , kwa mfano kama unao uwezo mkubwa sana wa kucheza na masoko ya hisa basi ni rahisi kupata marafiki wanaopenda maswala ya hisa, kama unapenda maswala ya komputa katika maswala ya ubunifu na ukawa vizuri kwenye kazi yako basi ni rahisi sana kupata marafiki wa kada hio, ijapokuwa Rufi hakuwa amesoma elimu rasmi lakini uwezo wake ndio uliomtambulisha kwa watu waliosoma kutoka vyuo mbalimbali kama Columbia na Queens University.

Baada ya kuiva ndipo alipojiingiza katika kufanya kazi mbalimbali kwenye makapuni kwa njia ya ‘freelancing’ kazi mbalimbali ambazo zilikuwa zikihitaji ujuzi zaidi kuliko vyeti , hivyo njia hio ilimpatia pesa za kulipia kodi na kuishi ndani ya New York, lakini hata hivyo njia hio haikumpatia pesa za kutosha kukidhi kiu yake hivyo ndipo alipoanza kujiingiza kwenye kazi ya kutapeli watu kwanjia mbalimbali na kazi hio ilimpatia pesa nyingi sana kuliko hata ya kupata ‘gig’ mtandaoni.

Roma alijikuta akivuta pumzi mara baada ya Rufi kumuelewa , ijapokuwa aliona swala hilo linaweza kumletea shida mbeleni lakini hakutaka kumnyima Rufi nafasi ya kumtafuta mama yake mzazi , alijiambia mwenyewe moyoni kwmaba atajitahidi kuwa makini ili mazoea yake na Rufi yasiwe na ukaribu zaidi kiasi cha kuwa wapenzi.

Edna mara baada ya kutoka kazini moja kwa moja alikuja hadi hospitalini na Rufi aliomba ruhusa ya kuondoka siku hio hio kwani hakupenda kukaa hapo hospitalini kwa muda mrefu.

“Umefikia wapi hapa Tanzania?”Aliuliza Edna.

“Nilifikia hotelini lakini nimefanikisha kununua Apartmeng kwa msaada wa rafiki yangu”Aliongea Rufi na kumfanya hata Roma kusangaa.

“Kumbe unarafiki hapa Tanzania?”

“Ndio nilikutana nae kupitia mtandao wa Speaky”

Mtandao wa Speaky ni mtandao maarufu ambao unaunganisha watu wa tamaduni nyingi duniani kwa ajili ya kufundishana lugha , kwa mfano kama utahitaji kujifuza kiarabu na pia kuna mtu anataka kujifunza kiswahili basi mtaombana urafiki na kusaidiana kufundishana.

Kwa maelezo ya Rufi rafiki yake ni mwenyeji wa mkoa wa Kahama ambaye anasomea chuo cha CBE, kauli hio ilimfanya Roma kuwa na ahueni kwani aliamini huenda mke wake angemuambia Rufi akakae nyumbani.

Basi ilibidi Rufi awasiliane na rafiki yake , ambaye ndani ya muda mfupi aliweza kufika hospitalini hapo, Roma alishangaa mara baada ya kugundua rafiki aliekuwa akizungumziwa na Rufi alikuwa mwanaume tena kijana ambaye alikuwa Sharobaro kutokana na mavazi yake na mkato wa nywele , alionekana kama kijana muhuni muhuni lakini Roma hakutaka kutoa maoni yake na hata kwa Edna alionyesha wasiwasi lakini upande wa Rufi alionekana kumuamini rafiki yake.

Alikuwa kijana ambaye pia hela ilionekana kuwa sio tatizo kwani alikuwa akiendesha gari nzuri kweli ya kifahari aina ya BMW X6 toleo jipya.

Baada ya Rufi kuondoka , Roma na Edna waliamua kurejea nyumbani huku Edna akimuahidi Rufi atamsaidia kumtafutia namna ya kuishi Tanzania kama mgeni kwani Viza yake alioingia nayo nchini kama mtalii ilionyesha kuisha ndani ya mwezi mmoja.

“Kesho kuna mahari nataka twende pamoja”Aliongea Edna wakati wakiwa kwenye gari na Roma wakielekea nyumbani.

“Nipo tayari kwenda na wewe hata kuzimu mke wangu nitahakikisha naongoza njia kabisa”Aliomgea Roma kwa namna ya utani na kumfanya Edna amshangae Roma na uropokaji wake mpaka kujisikia kucheka.

“Kesho kuna graduation UDSM, Profesa Clark na mimi ni moja ya watu tulioalikwa , lakini pia ndio siku ambayo projekti ya kampuni yangu kwa kushirikiana na chuo itatangazwa rasmi ili kuruhusu wanafunzi wenye sifa za kuomba kushiriki kuanza rasmi, naomba unisindikize kwasababu kwanza wewe ndio upo na ukaribu zaidi na Profesa Clark hivyo itakuwa vizuri kama utamsapoti”

“Okey wifey umeongea pointi , tutahudhuria pamoja siwezi kukuacha uende mwenyewe na maprofesa wakaanze kukodolea macho nitahakikisha wanaelewa nini maana ya mwanmke mrembo kama wewe kuwa ‘taken’”.

“Yaani Roma..”Alijikuta akiongea na kufumba macho.

Ilikuwa ni muda wa usiku baada ya chakula Roma wakati akiwa amekaa sebuleni akicheza na Lanlan simu yake kubwa ilianza kuita kwa kutetema na kumfanya kuitoa ili kuangalia nani aliekuwa akipiga na aligundua namba inayompigia ni kutoka Uingereza , alishangaa kidogo na kisha alitoka nje kwa ajili ya kuipokea

“Who is this?”Aliuliza Roma mara tu baada ya kuipokea .

“Little Roma Roma it’s me” Ilisikika sauti ya kimagizo yenye kuumiza masikio na kumfanya Roma mwili wake kushikwa na msisimko.

“Catherine!!” Aliongea Rima baada ya kuitambua sauti ni ya Catherine mama yake mzazi Profesa Clark , kwani ni yeye pekee ambaye alikuwa akizungumza nae kwa namna ya kitoto na kurudia rudia jina lake.

“Nilikumisi sana kwanini hukunipigia tokea mara ya mwisho tuonane , kila wakati unapenda kuniacha nikiwa na huzuni na hamu ya kukuona tena kila unavyomaliza kunichezea”

“Huna tabia ya kunipigia simu , labda iwe kwa shida maalumu unaonaje ukienda moja kwa moja kwenye shida yako”Aliongea Roma.

“Oh! sikujua unanifahamu hivyo?”

“Kadri utakavyobakia kwenye uhalisia wako nitaendelea kukufahamu”Aliongea na Catherine alitoa kicheko kidogo.

“Roma nadhani ushakutana na Clark huko Tanzania , ameondoka huku bila ya kuaga na kuja huko nataka umrudishe nyumbani haraka”Aliongea Catherine na kumfanya Roma kushangaa hata hivyo alishajua tokea mwanzo kuna kitu hakikuwa sawa kwa Profesa Clark ghafla tu kuja Tanzania kwa ajili ya kazi ya kufindisha.

“Unamaanisha nini kumrudisha nyumbani , mmefanya nini mpaka akawakimbia?”Aliuliza Roma.

“Ameondoka pasipo ya kuaga mara baada ya familia ya Rothchild kumtaka aolewe na mchumba waliomwandaa”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio.
Hatariiii
 
SEHEMU YA 444.​

Edna na Roma mara baada ya kuingia eneo la sebuleni waliweza kukutana na sura nne ngeni ,kulikuwa na mwanaume mwenye kitambi na mwili mkubwa alievalia suti , mwanaume mwingine alikuwa ni mzungu. , wengine wawili walikuwa ni mabodigadi.​

Kuhusu mzungu alikuwa mrefu wa kama inchi sita na nusu , ana nywele nyeupe aina ya blonde akiwa amevalia shati rangi ya pink na suruali ya kitambaa, mwonekano wake ilikuwa ngumu sana kuweza kukadiria umri wake , lakini alikuwa ni kijana kabisa huenda hata Roma akawa mkubwa.​

Roma na Edna mara baada ya kufika eneo hilo la sebuleni yule bwana mweusi mwenye kitambi alisimama, Roma hakumfahamu lakini upande wa Edna alimfahamu huyo mwanaume kwani alikuwa ni mwanasiasa maarufu tu.​

“CEO Edna umerudi?, naomba unisemehe kwa kufanyia ziara ya kushitukiza asubuhi asubuhi”​

“Usijali muheshimiwa karibu sana”Aliongea Edna.​

“Mr Roma nadhani hatujawahi kukutana ana kwa ana , kwa jina naitwa Abasi Nguya ni waziri wa Uwekezaji , biashara na Viwanda”Alijitambulisha.​

“Karibu sana bwana Abasi Nguya”Aliongea Roma lakini Edna macho yake yote yalikuwa kwa mzungu ambaye alikuwa akitoa tabasamu , ilionekana ni kama wameshakutana kabla ya ujiio huo.​

“Mr Maksim? Why are you here?”Aliuliza Edna kwa kingereza akimuuliza bwana mzungu kwanini yupo hapo.​

Roma mara baada ya kuona mke wake anamfahamu huyo mzungu alijiuliza ni wapi wamekutana.​

“Edna unamfahamiana nae?” Aliuliza Roma na kabla hajajibu yule mwanaume alimsogelea Roma.​

“Hello I’m Maksim frome the Klyuchevsky familly in Russia , its honor to visit your home, I met CEO Edna at the international bussiness and economics meeting yerstaday”​

“Habari naitwa Maksim kutoka familia ya Klyuchevsky kutoka Urusi , ni heshima kwangu kutembelea hapa nyumbani kwako , nilikutana na CEO Edna kwenye kikao cha uchumi na biashara za kimataifa siku ya jana”Aliongea yule bwana kabla hajampa nafasi Edna kujibu.​

Roma hakuweza kujua kama siku ya jana kulikuwa na kikao cha aina hio hata hivyo asingejua kwani alikuwa kwenye mgogoro na mke wake.​

“Mr Maksim amekuja mpaka hapa kwa nia ya kuongea na nyie wote juu ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi , nimepewa kazi hii na mheshimiwa raisi kuwa mtu kati kwenye mazungumzo”Aliongea bwana Abasi Nguya.​

“Mazungumzo ya kidiplomasia ndani ya nyumba yangu , mbona kama ni swala ambalo halijakaa sawa”Aliongea Roma.​

“Hapana Mr Roma , inawezekana sehemu hii sio sahihi , lakini serikali haiwezi kufanya maamuzi ya moja kwa moja bila makubaliano kati yako na mke wako kuhusu maswala ya kibiashara , hivyo kauli yako ni muhimu pia kwenye mzungumzo yetu” Baada ya kuongea hivyo Roma aliamua kwenda kukaa na wote wakakaa chini kwa ajili ya mazungumzo.​

Licha ya bwana Maksim kusema kwamba alikuwa ashasikia habari zake , lakini aliihisi bwana huyo alikuwa akimfahamu kwa jina la zaidi ya Roma ,kama si hivyo asingefika nyumbani na kuhusishwa kwenye maswala ambayo mke wake anaweza kufanya maamuzi kama siku zote.​

“Familia anayotokea bwana Maksim ni moja ya familia kubwa ndani ya taifa la Urusi na hata Raisi wa sasa wa Urusi yupo madarakani kutokana na sapoti kubwa kutoka kwenye familia ya bwana Maksim , ndio wameshikilia uchumi wa Nishati ya nyuklia , Gesi asilia na Petroli Urusi yote, Hata hivyo wanajiendesha kwa siri sana ndio maana hawana umaarufu mkubwa”Aliongea Mheshimiwa Nguya na kumfanya Edna kushangazwa na taarifa hio , siku ya jana mara baada ya kukutana nae alimchukulia poa kumbe alikuwa mtu mzito sana.​

Urusi ni nchi ambayo imejaaliwa rasilimali nyingi za kinishati , msingi wa biashara ya Vexto ni uingizaji wa asilimia hamsini za mafuta kutoka nje ya nchi hivyo mazungumzo hayo ya kibiashaa kama yanegeenda sawa ingekuwa ni faida kubwa sana kwa kampuni yake na huenda hata gharama ya mafuta ya Petroli zilizokuwa juu kwa sababbu ya vita kati ya Ukraine na Urusi ingepungua, lakini sio hivyo tu kama kutakuwa na makubaliano ya kibiashara kampuni nyingi ndani ya Afrika mashariki kwa ujumla zingepatwa na ukichaa, Edna alijikuta mwili wake ukimsimsika.​

“Mr Maksin jana hukuzungumzia swala lolote linalohusiana na ushirikiano wa kibiashatra , kwanini iwe leo?”Aliuliza Edna kwa kingereza huku akionyesha shauku kwenye macho yake , hata hivyo Edna alizaliwa kuwa mfanyabiashara hivyo eneo kama hilo lilikuwa la kwake kabisa kutawala.​

“Miss Edna my proposal ties with my background I do not wish to reveal it to the general public right now”​

“Edna Pendekezo langu linafungamana na ubini ambao sitamani kuweka wazi sasa hivi”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa , lakini Maksim alibadilisha mkao na kisha akamwangalia Roma na Edna kwa pamoja.​

“Pendekezo langu nataka kampuni ya Vexto kuvunja mkataba na Princess Clark”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio lakini aliendelea kuongea.​

“Nimekuja hapa nchini kwa ajili ya Clark , Clark ni mchumba wangu na hata mipango ya ndoa yetu ni makubaliano kati ya familia yangu na Rothchild, lakini kutokana na kutokuelewana ndio akaingia mkataba na Kampuni ya Vexto pamoja na serikali ya Tanzania ili tu kuweza kuepuka kufunga ndoa , jambo ambalo ni matusi kwa familia yangu na familia ya kifalme kutoka Wales , hivyo ujio wangu hapa Tanzania ni kwa ajili ya kumrudisha Urusi ili taratibu za ndoa ziendelee”​

Roma maneno hayo hakuyapenda kabisa , ijapokuwa Catherine alishamwambia kwamba Clark alipaswa kuolewa lakini hakujisumbua kuuliza ni familia gani anaozeshwa, lakini alishangaa kujua ni moja ya familia ya Ma oligarch kutoka Urusi.​

Mpaka hapo Roma kuna kitu kilimjia akilini , huenda Clark anatolewa kafara kutokana na yale yanayoendelea ndani ya bara la ulaya , Uingeeza ni kati ya nchi ambazo zinategemea sana rasilimali nishati kutoka Urusi , ukijumlisha na Vita vinavyoendelea huenda ndio ilipelekea Rothchild kutaka kufanya makubaliano ya kibiashara yanayofunganishwa na ndoa, hata hivyo alikuwa akijua familia ya Rothchilds siku zote ilichokuwa ikijali ni pesa sio utu.​

Unapaswa pia kujua kwamba Klyuchevisky ndio wapo nyuma ya chama tawala ndani ya Urusi.​

Edna sasa ndio anajua ujio wa Profesa Clark sio wa kibiashara bali alikuwa akikimbia ndoa, akili yake ilianza kuzunguka kwani maongezi hayo hayakuwa ya kibiashara tu bali yalionekana kama tishio kwa biashara zake , ukizingatia pia kampuni yake ilikuwa ikijihusisha na biashara ya mafuta kutoka Urusi , aliona hata kama hatomwachia Clark kuondoka kwa kuvunja mkataba lakini hakuwa na uwezo wa kuziia swala hilo kwani asingeweza kushindana na familia kubwa kama hio.​

Mkataba wake na Clark ulikuwa ni wa faida kubwa huko mbeleni kama angefanikiwa kutengeneza dawa za magonjwa ambayo yamekuwa yakiangamiza jamii ya Afrika kwa makusudi kabisa kwa ajili ya faida ya Wazungu , lakini hata hivyo upande mwingine wa kibiashara aliamini familia hio ingeweza kumlipa fidia ya kuvunja mkataba.​

Hivyo kama Edna angekataa kuvunja mkataba ni dhahiri kwamba alikuwa akishindana na serikali kubwa zote za bara la Ulaya kwani Rothchild ndio watawala wa bara lote kwanzia Ufaransa ambako kuna tawi lake la kibiashara mpaka Uingereza na Ujerumani, lakini pia Urusi moja kwa moja.​

Edna alijikuta akigeuza kichwa na kumwangalia Roma , aliamini yeye pekee ndio ambaye anaweza kufanya maamuzi kwa wakati huo.​

Ikumbukwe kwamba Edna pia kama angevunja mkataba , sifa ya kampuni yake ingeshuka , kwanni siku ya juzi kwenye mahafali pale Chuo kikuu cha Mlimani dhumuni la mkataba wake na Profesa Clark lilikuwa bayana kwamba ni kusaidia nchi za Afika kujitegemea katika maswala ya utafiti wa utengenezaji wa madawa kwa magonjwa sugu,, jambo ambalo lilipokelewa kwa uchanya na mataifa mengi ya Afrika ambayo yalichoshwa na kunyenyekea wazungu, hivyo kama angevunja mkataba kwa ajili ya pesa ingemletea sifa mbaya na kampuni ingeathirika zaidi.​

“Edna nini mawazo yako juu ya hili”Aliongea Roma lakini Edna alisita kutoa jibu moja kwa moja.​

“Mr Maksim nadhani tuone kwanza masharti yako kwanza juu ya kuhitaji kuvunja mkataba na kampuni yangu , Kama nitakubali moja kwa moja lazima utambue kwamba pesa tu haiwezi kutatua tatizo lakini pia taswira ya kampun itaathirika , nadhani umekuja hapa ukiwa umefanya utafiti na umeona siku tatu hizi baada tu ya kutangaza nia yetu ya utafiti wa madawa hisa za kampuni yangu zilipanda kwa zaidi ya asilimia kumi”Aliongea Edna huku akijitahidi kujituliza ili kutumia akili yake ya kibiashara katika kufanya maamuzi.​

Maksim alibadilisha mkao tena huku akionekana kama mtu alietarajia swali hilo kutoka kwa Edna kwani alitabasamu.​

“Kwanza kabisa kampuni yako Tanzu iliopo ndani ya bara la Ulaya itapata kibali cha kufanya biashara upande wa Mashariki yote ya Ulaya ,Nimefahau kwamba mara ya mwisho ulivyokuwa Ufaransa uliweka wazi nia yako ya kutengeneza mirija ya kibiashara upande huo wa mashariki kwa kujipanua zaidi , lakini licha ya juhudi kubwa ulizoweka hilo halijafanikiwa mpaka sasa hivyo tutafanikisha ndoto yako, Pili biashara ya utafiti wa madawa sugu na mafunzo ya wanasayansi wazawa utaendelea kama kawaida lakini kwa kutumia wataalamu wabobevu ambao watatoka moja kwa moja Urusi nakuziba nafasi ya Profesa Clark na ninakuhakikishia kupitia wataalamu wetu ndani ya miaka mwili utakuwa na mafanikio unayoyata. Tatu na mwisho kabisa , tunajua mpaka sasa kuna mkataba wa kudumu uliosainiwa na Raisi wa awamu ya tatu wa biashara ya mafuta kati ya serikali na kampuni ya Vexto, tunapanga kuongeza kiasi cha mafuta yanayoingia Tanzannia kwa gharama ya nafuu chini ya thamani ya soko, lakini pia kampuni yako itapewa kipaumbele ya kupata malighafi zinazotokana na ‘Petreleum extraction”​

Edna alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha fidia zote zilikuwa ni kubwa kiasi kwamba hakuhitaji kufikiria mara mbili mbili na kama angekubali inamaanisha kwamba angezidi kuwa tajiri , ni kichaa tu ambaye angekataa dili kama hilo , ukizingatia pia kama angevunja mkataba na Clark ilikuwa na faida ya ziada kwake pia kwani angezuia uwezekano wa mahusiano ya kimapenzi kati ya Roma na Profesa Clark..​

Maksim baada ya kushusha bomu hilo la ofa kichaa alikaa kwa kuegamia kabisa , alijua kama kweli Edna ni mfanyabiasha asingeweza kukataa ofa yake.​

“Edna ofa ambazo zimetajwa na bwana Maksim ni kubwa mno na faida yake sio kwako tu bali ni kwa watanzania kwa ujumla na Serikali inaangazia swala hili kwako kwa matarajio chanya kutoka kwako kwani lina faida pia ya kidiplomasia baina ya nchi zetu mbili , huna haja ya kuwa na wasiwasi na Profesa Clark kwani familia yake ishafanya mawasiliano na Profesa ili kusitokee lawama yoyote”Alipigilia msumari waziri Nguya.​

“Kama ofa yenu ni ya kweli basi nita…”​

“Hapana” Roma alimkatisha mke wake baada ya kuona anataka kukubali na kauli yake ilifanya chumba kuwa kimya hata Edna mwenyewe alitetema na kuwa mpole​

“Haya mazungumzo yanapaswa kwanza kukubaliwa na Clark , hata kama atakubali kuvunja mkataba na hataki kuolewa basi nasema hivi hakuna wa kumtoa hapa nchini”Aliongea Roma.​

“Mr Roma nakufahamu kwa jina lingine ambalo hata familia ya Rothchild wanaliogopa kila linapotajwa , lakini hata hivyo haimaanishi kwamba unaweza kufanya maamuzi ambayo yanaingilia maswala ya kisiasa na uchumi wa dunia kwa ujumla wake , una nguvu kubwa lakini hata hivyo sio kama hufuatiliwi , makosa kidogo tu yanaweza kusababisha migogoro mkubwa kati ya Tanzania na mataifa makubwa”​

“Kwahio unanitishia si ndio ?”Aliongea Roma kwa Kingereza huku akisugua vidole vyake vya mikono ambavyo vishaanza kumuwasha.​

“Sikutishii ila nina kuhabarisha , kwa ninavyofahamu pia wewe ni mtoto wa raisi wa taifa hili na pia familia yako imefungamana na jeshi kwa muda mrefu , hivyo siamini kwamba hata wanafamilia wanaweza kukaa chini na kuangalia unaharibu maswala ya Diplomasia ambayo ni maslahi mapana kwa Wananchi”​

“Bwana Maksim nadhani kuna kitu kimoja unapaswa kujua , mimi nikiamua jambo langu kichwani basi hakuna mtu wa kunizuia kulitimiza , sintojali taifa na tafia kuingia kwenye vita kama inaleta maana ya kupata ninachotaka,msimamo wangu siku zote mwenye nguvu anaongoza njia na dhaifu anamfuata mwenye nguvu”Aliongea Roma na kumfanya bwana Maksim sura kumshuka.​

“Kama unakataa mapendekezo yangu nitaihusisha wizara ya mambo ya nje kushughulikia hili swala na nakuhakikisha hili swala halitopita kirahisi kama unavyodhani na sio kwa Tanzania tu lakini pia hata kwa Clark ambaye unajaribu kumkingia kifua , heshima yake aliojijengea ndani ya muda mrefu itaharibika itaharibika ndani ya siku moja”​

Waziri Nguya sofa lilianza kuwa la moto , serikali ilimwamini katika mazungumzo hayo ndio maana akatumwa kama mtu kati , lakini kile anachokiona hapo hakuna namna ya kufikia kwenye makubaliano kwa amani.​

“Roma unafanya nini , unaonaje tukitulia na tukizungumza hili swala bila mtafaruku”Aliongea Edna kwa wasiwasi kwani alimuona Roma kama bomu ambalo lingelipuka muda wowote ,lakini Roma ni kama hajamsikia.​

“Oh tena… CEO Edna kwa taarifa nilizokuwa nazo una madaraka kamili juu ya kampuni ya Vexto , kwanini unataka kushikiliwa kimaamuzi na mume wako kwenye maswala ya kibiashara , hili ni swala linalokuhusu wewe sio Roma , na hata hivyo nimeweza kupata taarifa kwamba upo vizuri sana likija swala la biashara”Aliongea huku akisimama na kutaka kupiga hatua kutoka nje , lakini Roma alitoka kwenye sofa na kumkinga kwa mbele akimzuia asipige hatua, alikasirishwa na kauli yake na kuichukulia kama tusi mbele ya mke wake.​

“Unataka kufanya nini .?.” Aliongea Maksim huku akianza kushangazwa na mabadiliko ya ghafla ya Roma, kwani alikuwa ni kama mtu mwingine kabisa kwa jinsi alivyokuwa na hasira.​

Maksim alimkwepa akitaka kumpita kwa pembeni lakini kabla hajatimiza azma yake Roma alimshika Shingo kwa nyuma na kumfanya Maksim kushindwa kupiga hatua​

“Usijione wa thamani sana tena ndani ya nyumba yangu , hupaswi kabisa hata kukaa meza moja na mimi mbwa wewe ..”Aliongea Roma huku sauti yake ikiwa nzito na palepale alimgeuza kama anachezeshwa Tango na ile anageuka alipigwa ngumi yenye ujazo mkubwa wa nguvu za kijini eneo tumboni na mkono wa Roma ulizama ndani na akauchomoa kwa nguvu na kusababisha damu kusambaa pamoja na nyama nyama.​

“Aaarrggh!!”​

Edna alifumba macho akishindwa kuangalia , Waziri pamoja na mabodigadi walishindwa kuzuia mshangao wao huku na kukimbilia nyuma ya Edna na kusimama.​

Maksim alidondoka chini huku akionekana kushindwa kuzuia maumivu anayoyasikia huku damu zikimtoka mfululizo , lakini Roma alimshika kwenye shingo kwa mara nyingine na kumtupia nje kama furushi akijua kabisa bwana huyo ni wa kufa.​

“Unaweza kutoa taarifa kwa kila kichotokea hapa ndani bila ya kubadilisha neno, na kama itatokea tatizo lolote njoo niambie nitakusaidia nitakusaidia kulirekebisha”Aliongea Roma akimwangalia Waziri Nguya pasipo kujali mikono wake uliojaa mabonge ya damu.​

Edna alishindwa kuhema kwa tukio aliloshuhudia , mwanzoni akili yake ilikuwa kwenye ofa , lakini sasa hivi hakuwa akifikiria kingine zaidi ya kuwa na hofu kwa kile kilichomkuta Mzungu.​

Muda ule ule waziri alipotaka kuongea neno , wote walijikuta wakiangalia nje na kushuhudia kitu ambacho hakikuwa cha kawaida , kwanza Maksim alisimama akionekana mzima kabisa , ni kama hakuguswa kabisa kwani sehemu aliopigwa ngumi na kutobolewa tumbo ilirudi kama kawaida , lakini muda huo huo sura yake ya kizungu ilibadilika na kuanza kutengeneza michirizi ya ukijani uliokolea kwenye macho , huku meno yake yakirefuka na kucha vile vile ziliongezeka ukubwa , ilikuwa picha ya kushanganza na kuwafanya wale mabodigadi wote kurudi nyuma na kumuacha Roma akiwa mbele peke yake​

“Your strength is realy unbeleivable Pluto …”Alisimama huku akionekana kama Vampire na hata tabasamu lake lilitisha mno.​

Roma palepale akili yake ilifanya kazi mara baada ya Maksim kupona kwa haraka sana , lakini pia kucha zake kuchomoza na meno kurefuka na kuwa na mwonekano usiokuwa na utofauti na Vampire.​

“Nimekumbuka ….Wolverines!!!, wewe ni mwendelezo wa kizazi cha White wolf kutoka Urusi , katika familia ya kifalme mliojipatia jina la Wolverines…”Aliongea Roma huku awamu hii akionyesha hali ya kuwa na msisimko usio na kifani ni kama ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na watu wa namna hio.​

“Hahaha.. sasa ushanifahamu hivyo huna cha kunifanya , hatupo kwenye kizazi cha karne ya tano sasa hivi , hilo jina lishapotea na kubakia sisi ambao ni binadamu wa kawaida , tumekuwa watawala wa siri karne na karne ndani ya taifa la Urusi , Sisi ni wafalme wa Nchi zote za mashariki ya Ulaya., ulichokifanya leo kimeingiza Tanzania kwenye orodha ya nchi adui zetu”Aliongea na baada ya kumaliza palepale alipotea mbele kwa namna isioelezeka.​

.​

SEHEMU YA 445​

Roma hakutaka kumfukuzia , hata hivyo alishawahi kusikia habari juu ya jamii ya siri sana iliokuwa imejibatiza kwa jina la Wolverines, lakini hakuwahi kuamini kuhusu stori hizo kwani kwake ilikuwa kama hadithi.​

Wolverines ni jamii kama Vampire ambayo simulizi zake zilisikika sana kati ya karne ya tano mpaka mwishoni mwa karne ya kumi na tano , katika zama hizo waliaminika kuwa binadamu ambao ni jamii ya Vampire , lakini utofauti wao ni kwamba Wolverine hawakuwa wakiathiriwa na mwanga wa jua kama ilivyo kwa Vampires na walikuwa na nguvu kubwa sana kwenye mapambano kuliko hata jamii ya Vampire yenyewe na waliweza kuishi hata nyakati za mchana na hawakutegemea damu ya binadamu kuishi bali wanakunywa damu ya mnyama anaefahamika kwa jina la Wolverine au White Wolf(Mbwa mwitu) na ndio chanzo cha jina lao, inasemekena mbinu pekee ya kuweza kuwaua ni kwa kunyofoa moyo wao.​

Waziri Nguya alihisi ni kama yupo kwenye ndoto ya kutisha , hakuamini angeanza siku kwa kushuhudia kitu cha namna hio , lakini upande wa Edna licha ya kuwa kwenye mshangao , lakini alishindwa hata kutetemeka zaidi ya kuangalia mikono ya Roma iliotapakaa damu ni jambo ambalo kwa mwanamke halivumiliki lakini kwa Edna ilikuwa jambo ambalo ni kama amewahi kuliona kabla.​

“Unaweza kwenda kuripoti kama ulivyoona hapa bila kuacha neno”Aliongea Roma akimwambia mheshimiwa waziri na kisha alipita na kuingia ndani na kwenda kuosha mikono jikoni kwenye sink.​

Edna alijikukta akitembea kwa kusita sita na kwenda kujibwaga kwenye sofa akiwa kama mtu ambaye hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea na hata Roma alivyotoka jikoni aliishia kumwangalia kwa maswali mengi.​

“Nadhani umeona mwenyewe kilichotokea , ijapokuwa mpaka sasa sijui ni kwasababbu ipi familia yake kutaka kumuozesha kwa viumbe wa ajabu ,, lakini siwezi kuruhusu swala hilo litokee”​

“Hivi unajiona unachokifanya mbele yangu?”​

“Nakuambia siwezi kumruhusu Clark kuolewa na wanyama”​

“Acha mambo yako ya kumlinda mwanamke mbele yangu Roma, utanikasirisha”​

“Nisamehe kama kauli yangu inaziumiza hisia zangu lakini huo ndio msimamo wangu , sidhani kwa ulichoshuhudia hata wewe mwenyewe ungekubaliana nacho”Aliongea Roma lakini muda huo huo Bi Wema na Blandina walishuka kutoka juu wakiwa na wasiwasi.​

Na walishangazwa zaidi mara baada ya kuona damu zilizokuwa zimetapakaa karibu na mlango na kutaka kujua nini kimetokea.​

Muda huo huo alipokuwa akitaka kuuliza , sauti ya gari kutoka nje ujio wa mtu zilisikika na mlango palepale ulifunguliwa na alionekana Profesa Clark aliekuwa akihema kwa nguvu.​

Alikuja akiwa amevalia koti la maabara na ilionekana kabisa alitoka kazini muda huo kwa mwonekano wake.​

Aliangalia damu zilizotapakaa na hakujali sana zaidi ya kupita na kumsalimia Blandina na Bi Wema na kisha akasalimiana na Edna aliekuwa akifikicha macho.​

“Kwanini umekuja ukiwa hivyo?”Aliuliza Roma na Profesa aliingiza mkono wake kwenye koti na kuibuka na kijichupa kama vile vya kuhifadhia chanjo(Vials) na kumpatia Roma.​

Ni ‘antidote’ , niliogopa ningechelewesha ndio maana nikaja mwenyewe haraka haraka , unatakiwa kumpatia na kumeza kwa kupitia mdomoni tu”Aliongea na kumshangaza Roma.​

“Umeweza kufanikisha ndani ya muda mfupi hivi?”​

“Damu ya mgonjwa wako nilipoifanyia majaribio niliweza kubaini amewekewa kimiminika ambacho ni kama sumu ambayo inashambbulia DNA za mwili, ni kimiminika ambacho kimetenenezwa kwa kuunganisha DNA na RNA za virusi ishirini na nne,, kimiminika hiko kinafahamika kwa jina la ‘Tribute to Maria’ , ni siraha ya kibailojia ambayo imefanyiwa majaribio nchini Urusi kwenye maabara ya siri ifahamikayo kwa jina la Nicene , mwezi uliopita kuna wanafunzi wangu i waliiuliza maswali baadhi yanayohusina na sayansi ya uundaji wa mchanganyiko wa virusi pamoja na namna Chanjo yuake inavyowezekana kutengenezeka na niliwapa majibu na kushauri wasijaribu kuunda siraha hio kwani ni hatari sana kwa maisha ya binadamu lakini inaonekana waliendelea na kazi yao”​

“Kwanini jina la ‘Tribute to Maria’ na vipi kuhusu hii maabara ya Nicene?”​

“Kwanza kabisa hiki kimiminika kiligundulika kwa mara ya kwanza katika karne ya kumi na moja kihistoria , ulikuwa ni mwendelezo wa tamaduni za kimiminika(Siki) alichopewa Yesu wakati wa kusulubishwa , utofauti ni kwamba Kimiminika hiki na Siki ni vitu viwili tofauti kwani katika karne ya kumi na moja kiliongezewa ubora wenye dhamira tofauti kabisa na kuanzia hapo kikaendelea kuboreshwa na katika Karne ya kumi na sita ndipo kilipobatizwa jina la Kinywaji cha Heshima Kwa Maria kupitia vita baina ya dini ya kikristo na waislamu wa Uturuki.​

Kila mturuki ambaye alikamatwa alilazimishwa kunywa kimiminika hiko kama atakataa kukubali kubatizwa na kuwa mkristo , sasa pale mateka anapolazimishwa kunywa hiko kimiminika wanajeshi(crusaders) walipiga kelele ‘Heshima kwa Maria’(Tribute to Maria) aliemzaa Mwana wa Mungu.​

Baada ya vita uwepo wa kinywaji huo ulipotea kabisa kwa kupigwa marufuku na kanisa la Roma , mpaka miaka ya hivi karibuni kulipogundulika tena kimiminika kilichopewa jina hili hili ambacho wanasayansi waliokuwa chini ya kanisa la Orthodoxy huko Urusi walikipatia jina kwa kuamini ni mwendelezo wa kimiminika kile kile kilichotumiwa katika vita vya kusambaza dini ya kikristo, kuhusu Nicene ni jina la maabara iliokuwa nchini Uturuki ambayo ilihusika kutengenezea kimiminika hicho wakati wa vita na baada ya vita kuisha maabara hio ilihamishiwa nchini Urusi mpaka leo hii na ndio ilioendeleza sayansi ya kutengeneza kimiminika kipya ambacho ni kama siraha ya kibailojia”Aliongea Clark kwa muda mrefu na kumshangaza Edna na Roma kwani maelezo hayo ni kama yalikuwa mapya kwao.​

Ndio kama utakuwa mtu wa historia basi utaweza kugundua jina la Nicene limetokena na jina la Nicaea kwa kilatini kilichotoholewa kutoka lugha ya kigiriki , lakini kwa kiswahili inafahamika kwa jina la Nikea , maana ya jina hilo ni mji wa ushindi ambayo kwa sasa unafahamika kwa jina la Iznik huko Uturuki.​

“Kwahio kama ni kweli hii maabara ipo eneo gani nchini Urusi na wanapata hela ya ufadhili kutoka wapi au ni serikali?”Aliuliza Roma.​

“Hio taarifa ni ya siri na mimi mwenyewe sijui , labda umjaribu rafiki yako Makedon kutoka Mossad nadhani atakuwa na majibu , udhalishwaji wa kimiminika hiko ulipigwa marufuku sana na kanisa la Catholic na Orthodoxy kwa kutumia jina la Maria, lakini licha ya hivyo hakuna kilichobadilika naamini kuna ajenda kubwa ya siri ambayo inaendelea , naweza pia kuamini huenda serikali ya Urusi haihusiki kabisa”​

“Okey nitajaribu kuwasiliana na Makedon aweze kunipa mwanga”Aliongea Roma huku akikuna kichwa.​

“Halafu nimesahau swali moja, kama mtu atakuwa amepatiwa hiko kimimnika kuna uwezekano wa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwani kwa melezo yako naweza kusema ni kirusi”​

“Hakika ni kirusi lakini lakini tunaita kimiminika kutokana na kwamba ni muunganiko wa virusi ishirini na nne vilivyodhalisha majimaji , bahati nzuri ni kwamba kinasambaa kama kirusi cha HIV , lakini naamini kuna uwezekano kikawa kimeongezewa ubora wa kusambaa kwa njia ya hewa ili kutumika kama siraha ya kibailojia inayosambulia Genes”​

“Umesema kuna wanafunzi wako wako waliulizia maswali juu ya hiko kimiminika , je unahisi ndio waliotengeneza ?”​

“Inawezekana kwani kati ya wanafunzi wangu mmoja wapo alikuwa ni mrusi”Aliongea.​

“Hawa wanafunzi wako kila wanapoenda ni kusababisha matatizo tu, kwanini unafundisha vichaa”Aliongea Roma​

“Roma nadhani hata wewe unafahamu ule msemo wa kwamba elimu inapaswa kutolewa kwa watu wote bure na kwa usawa , ndio nilichofanya, sina haki ya kumjaji mwanafunzi wangu anakwenda kufanyia nini elimu anayoipata ili mradi napokea heshima yangu kama mwalimu wao , wakishamaliza elimu yao siwajibiki kwa wanachofanyia elimu yao”​

“Lakini huogopi kwmaa inaweza ikatokea mmoja wapo kukugeuka na kukudhuru?”​

“Unajua nini Roma, licha ya kwamba Yan Buwen amekuwa kichaa lakini mafanikio yake yamenishangaza , likija swala la utafiti wa kisayansi ukimtoa Profesa Shelukindo nadhani ni yeye pekee kidogo anaeweza kunikaribia”​

Edna aliekuwa kimya muda wote aliona akili yake inakuwa nzito , kila siku anavyozidi kuishi na Roma aliweza kufahamu mambo mapya zaidi , huku mengi yakiwa ya kutisha zaidi na mazito kweli kweli..​

“Edna naomba unisamehe…”Aliongea Clark na kumfanya Edna kushangaa kwanini anaombwa msamaha.​

“Nilipishana na gari mbili wakati nakuja hapa , mojawapo ni gari ambayo namfahamu mmiliki wake na alikuja jana nyumbani kwangu , kwa uwepo wa hizi damu hapa naamini Roma ameweza kumfanyia jambo”Aliongea na kumfanya Edna kidogo kukosa neno la kuongea.​

Alijisikia vibaya kuona Mwanamke mwenzake analazimishwa kuozeshwa kwenye familia ya Mashetani .​

“Edna najua ukaribu wangu na Roma unaweza kukufanya ujisikie vibaya lakini naomba nikwambia usiwe na wasiwasi kabisa , sina mpango wa kuwa kidudu mtu kwenye mahusiano yenu , Roma aliniokoa mimi na mama yangu miaka mingi iliopita nikiwa mdogo na kama sio yeye nisingeweza kuwepo kwenye dunia hii , kwangu Roma ni mwokozi wangu , kama unahisi uwepo wangu hapa Tanzania unakufanya usijisikie vizuri niambie tu, sitokasirika nitaondoka mara moja, ninaweza kuagiza wanafunzi wangu na kuendeleza project yetu, Natumaini maisha yako na Roma kuwa yenye furaha…”​

“Inatosha Clark ,hakuna tatizo lolote mimi na Edna tupo sawa kabisa , kinachoniumiza ni hawa Klyuchevsky , bora hata wangekuwa ni Vampire lakini Wolverines , pumbavu kabisa siwezi kuruhusu ukaolewa na hawa viumbe na ukaja kuzaa mdudu, Catherine na familia yako watakuwa vichaa”​

“Usimlaumu sana mama , hana nguvu kubwa juu ya Rothchild miaka iliopita familia ya klyuchevisky walisaidia sana kwenye uchumi wa familia hivyo ni kama kulipa fadhila na hata hivyo sikuwa na mchumba na ni haki yangu kuoelewa. Binafsi nimeonea nisichukulie hili swala kuwa kubwa sana kwani hata kama nitaolewa kwao sio kwa ajili ya kuzaa ila ni kama maonyesho tu”​

“Kwahio unapanga kuolewa kwa hayo maonyesho?”​

“Ndio , ndoa yangu itatatua shida kubwa ya kiuchumi inayoendelea baina ya Urusi na Uingereza katika maswala ya nishati.. Roma nafahamu unajua haya sina haya ya kuelezea zaidi ni wajibu ambao unanihusu”​

Roma alitaka kuongea lakini Edna alimzuia kwa kumshika mkono.​

“Edna unataka kuongea nini?”​

“Mimi sioni tatizo la Maksim kabisa kumuoa , anaweza kuwa tofauti na binadamu lakini ni kijana mzuri , kinachoangaliwa ni moyo wake ulivyo ,mabadiliko yake ya muda mfupi yasiwape uhalali wa kujaji mapenzi yake kwa Clark wala kumsema vibaya Maksim, mimi nadhani Clark ukubali kuolewa tu”Aliongea Edna na kauli yake ilishangaza kila mmoja.​

Roma moja kwa moja alijua Edna hakuwa akipenda uwepo wa Clark ndani ya Tanzania hivyo anapanga kuhakikisha anaondoka moja kwa moja kwa kuoelewa.​

“Edna upo sahihi sana , Roma nadhani nishafikisha kilichonileta hivyo kwaherini”Aliongea Clark na kisha alitoka kwa kukimbilia nje akitoa machozi na ndani ya muda mfupi mngurumo wa gari ulisikika ukififia nje ya geti.​

Blandina na Bi Wema walikaa kimya muda wote , hawakutaka kuingilia swala hilo kwa namna yoyote , waliamini ni maswala ya wao kumalizana wenyewe.​

Roma hata yeye hakupenda kauli ya Edna ambayo imemfanya Clark kuondoka namna hio , alijua lazima muda huo angeenda kulia , alisimama na kutoka eneo la sebuleni na kupandisha kwenye chumba chake.​

“Roma unaweza kukasirika utakavyo lakini sijutii kwa kauli yangu, nipo tayari kufanya chochote ambacho kitalinda amani ya familia yangu”Aliongea na kumfanya Roma kusimama na kumwangalia kisha akatingisha kichwa na kuendelea kwenda juu.​

********​

Upande mwingine ndani ya hoteli ya Johari Rotana katika chumba cha Presidential Suite alionekana Maksim aliesimama kwenye dirisha akiangalia upande wa nje wa jiji huku akiwa ameshikilia glasi ya mvinyo mkononi.​

Alionekana kama mtu ambaye hakuwa ametoka kwenye kupatiwa kibano na Roma mpaka kupoteza vipande vya utumbo mpana , muda huo alikuwa amejifunga taulo mwili mzima akiwa msafi na sura yake ya Kihandsome boy , hakuna mtu ambaye anaweza kuamini kwamba anaweza kubadilika sura na kuwa wa kutisha.​

Nyuma yake alionekana mwanamke wa kizungu ambaye amepiga magoti chini akiangalia mgongo wa bwana Maksim.​

“Boss misheni ulionipa ya kumshawishi kiongozi wa Alshababu kutumia wanajeshi wake imefannikiwa na mpaka sasa wapo tayari mpakani na kombora lilojaa kimiminika cha ‘Tribute To Maria’ lipo kwenye mkao wa utayari kuelekea Tanga, nahitaji oda yako tu kuendelea na misheni”Aliongea na kumfanya Maksim kutabasamu.​

“Kama nilivyotarajia mpango utaenda sawa , Mkuu wa Alshabab kasemaje baada ya kusikia kifo cha mtoto wake?”​

“Yupo ni mwenye hasira kubwa sana na hasira yake imefanya kumshawishi kwa urahisi mpaka kukubali mpango wetu”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli.​

Kama Roma angekuwepo hapo angeweza kumfahamu mara moja huyo mwanamke na huenda asingefanya kosa ile juzi kumruhusu kumtoroka , alikuwa ni Aishapova.​

Mtoto ambaye alikuwa akizungumziwa juu ya kifo chake ni Shedrack Kengeu ambaye halikuwa jina lake halisi, kwanza ni msomali na ni mara chache sana kukutana Msomali anaitwa Shedrack Kengeu, ukweli Shedrack alikuwa mtoto wa kundi la Alshabab ambaye alitumwa Tanzania kwa mishenni maalumu ya kuhakikisha kuna makubalianao ya kibiashara kati ya Kundi la kihalifu la ZoaZoa pamoja Alishabab kupitisha siraha kupitia mipaka ya Tanzania.​

Miezi kadhaa iliopita Samweli Nguluma ambaye ni baba yake Benadetha alikataa kufanya biashara baina ya Alshababu na ZoaZoa kwa kuogopa serikali ya Tanzania kugundua , baada ya Samweli kutokubali dili hilo Alshababu kwa kumtumia Shedrack walimshawishi mke wa bwana Samweli Nguruma afahamikae kwa jina la Zuwena kumsaliti mume wake kwa kumuua na kisha awe mkuu wa kundi hilo na kisha afanye biashara ya kupitisha siraha za kivita kwenda kwa kundi la Alshabab.​

Lakini kabla ya Zuwena kutimiza azma yake ya kumuua mpango wake ulivuja na Samweli Nguluma ndipo aliposhitukia mchezo mapema na kumuwekea mtego, mpango wa Zuwena ni kumuua Samweli nchini Congo siku tatu zilizopita na Samweli alitumia mtego huo huo kumnasa mke wake na ushahidi na hakumpa tena msahama zaidi ya kumchapa Risasi ya kichwa.​

Taarifa ilipomfikia Mika kuhusu mama yake kupigwa risasi nchini Congo na Mzee wake ndipo alipotorokea Bagamoyo , lakini Alshababu hawakukata tamaa mara baada ya mpango A kufeli , hivyo walianzisha mpango B ambao ulikuwa ni kumtumia Mika,​

Shedrack ambaye alipewa jukumu la mipango yote A na B alikuwa tayari na ukaribu sana na Mika kwa muda mrefu kwa kuhakikisha mipango yote inafanyika kwa wakati mmoja na ukweli pia ni Kwamba Shedrack hakuwa Shoga kama Roma alivyomuona bali alikuwa akiigizia ili serikali ya Tanzania isije kufatilia taarifa zake.​

Sasa haikueleweka ilikuwaje mpaka Maksim kuweza kufanya mawasiliano na Kundi hilo la wapiganaji haramu , lakini mara baada ya Mika kumpiga risasi mtoto wa mkuu wa kosi hilo la Alshababu , Aishapova alitoa taarifa kwenda Alshababu kwamba mhusika wa kifo cha Shedrack Kengeu(Jina feki) ameuliwa na Roma.​

Ilionekana kabla ya ujio wa Aishapova Tanzania walikuwa kwenye majadiliano ya siri , lakini ni hakika kwamba mkuu wa kundi hilo baada ya kupata taarifa ya kifo cha mwanae moja kwa moja itakuwa alijenga kisasi na Romampaka kumpelekea kutoa kikosi ambacho kimejificha mpakani Tanza na Kombora la kimiminika cha kirusi kilichopewa jina la Tribute To Maria.​

“Vipi kuhusu Clark?”Aliuliza Maksim kwa kirusi.​

“Princes amerudi nyumbani kwake, kwa uchunguzi niliofanya tumegundua kuna maabara ndani ya nyumba anayoishi”​

“Endeleeni kumfatilia kwa umakini na jiandaeni muda wowote nitatoa maagizo ya kumteka”Aliongea kwa Kirusi.​

“Bosi mpaka sasa nimeshindwa kukuelewa , kwanini unataka sana kumuoa Princess Clark licha ya kuonyesha utomvu wa nidhamu ninavyoona hapaswi kuwa sehemu ya wanafamilia wa Klyuchevsky”​

“Unajua nini kuhusu mimi wewe .. simuoi kwasababu nampenda ila namuona kwasababu ya akili yake …”​

“Akili?”​

“Tumetumia akili nyingi pamoja na muda kutegeneza kirusi cha Tribute to Maria ,, kama mpango wetu ukiweza kufanikiwa hakuna nchi itakayoweza kutengeneza chanjo ndani ya mwaka mmoja , mtu anaeweza kuvuruga kila kitu ni Clark pekee, unachotakiwa kuelewa kirusi hiki kimetengenezwa na mwanafunzi wake ambaye yupo chini yetu na kama huyu Myahudi hatutomdhibiti atatengeneza chanjo ndani ya masaa machache na mpango kufeli”​

“Kwahio unachofanya ni kuweza kumdhibiti asiweze kutengeneza Chanjo?”​

“Upo sahihi , Familia ya Rothchild imekubali Clark aolewe kwa siri na familia yetu kwasababu wanaamini kwamba ataendelea kuwa na msimamo wake wa kutojihusha na utengenezaji wa siraha za kimaangamizi huku wao kuendelea kupata gesi asilia kupitia Nord stream , naweza kusema kwamba wanajidanganya ,Wolverine tuna mbinu nyingi za kuweza kumwendesha binadamu na kutufanyia mambo bila hata yeye kujielewa na huo ndio mpango , ni sawa na kupiga ndege wawili kwa jiwe moja , tutazuia utengenezwaji wa chanjo ya Tribute to Maria lakini pia tutaweza kutumia akili ya Clark kufanikisha uundaji wa siraha nyingine kubwa , Urusi ipo duniani kwa kuwa mbabe wa dunia na sio Wamarekani”Aliongea​

“Boss unazungumzia Totem of Hypnotism katika kukontrol akili yake?”​

“Nadhani unanipata vyema , angekubali kuoelewa na mimi bila shida yoyote nisingefikia huko”​

“Lakini bosi vipi kuhusu Hades , uwezo wake lazima tuuzingatie?”​

“Usiwe na wasiwasi mpango tuliouandaa ni kwa ajili ya kumdhibiti asifanye jambo la kijinga, amenichokoza kwa kunidhalilisha leo lakini nitamlipa kwa kumuelimisha nini maana ya nguvu ya Kluychevsky hata mtangulizi wake hakuwahi kutuchokoza”.​

“Boss huu mpango kama utafanikiwa , tutakuwa ni wakuogopeka sana , mheshmiwa Raisi amekuwa ni mwenye kupinga mipango yetu , lakini baada ya kuona matunda ya mpango lazima atatoa kibali mwenyewe , naahidi nitakuwa mtu wa kwanza kumuua yule mwanamke Lilith, wapuuzi wale wanatusumbua sana , Wolverine lazima tuisimamishe Urusi itawale Dunia tena”Aliongea Aishapovakwa kujigamba.​

ITAENDELEA.​

Ndiooooo
 
SEHEMU YA 446.

Aishapova alionekana kuwa na munkari kweli kwa kuona kwamba muda si mrefu watu wa jamii yao wanakwenda kuwa na nguvu juu ya jamii nyingine katika ulimwengu usio onekana.

Wakati akiendelea kumwangalia bosi wake kwa namna ya kumuhusudu mara akili yake palepale ilifanya kazi na kukumbuka tukio moja.

“Boss siku ya juzi baadhi ya wanajeshi wetu walimnywesha Mtoto wa kundi la ZoaZoa kimiminika cha Tribute to Maria, inawezekana Hades akawa amempeleka kwa Profesa Clark kwa ajili ya kutengenezewa chanjo”

“Unaongea nini?”Alibadilika na kugeuka na teke ambalo lilimpata Aishapova kifuani na kwenda kumtupa kwenye mlango.

“Nena kachuchunguze sasa hivi nini kiliendelea , kama usemayo ni kweli mumteke muda huu na kuondoka nae , usimpatie nafasi akatengeneza chanjo”Aliongea kwa hasira na Aishapoiva aliitikia huku akikohoa damu na kuondoka kwenye chumba hicho .

Upande Mwingine Roma baada ya Clark kuondoka nyumbani kwake alijikuta akiingia kwenye mawazo ya hapa na pale , akifikiria namna ya kutatua tatizo lililokuwa likiendelea , Roma hakuwa na hasira kwa kauli ya mke wake ya kuunga mkono Clark kwenda kuolewa na Maksim aliona Edna alikuwa akijitahidi kufanya maamuzi ambayo hayawezi kuathiri familia , lakini pia hakuwa kwenye nafasi ya kukasirika kwani yeye ndio chanzo cha matatizo yote.

Roma alitoa simu na kisha alimpigia mwanajeshi wa The Eagles aliekuwepo karibu na kisha akampatia Chanjo ile iliotengenezwa na Clark na kumpa maelekezo apeleke nyumbani kwa Benadetha na apatiwe Mika.

Roma mara baada ya kurudi chumbani kwake kwa mara nyingine alizitafuta namba za Makedoni na kisha akafanya mawasiliano moja kwa moja na kumpa maelezo ya kuchunguza kuhusu taarifa za Nicene Lab.

Muda huo huo alimtafuta Tanya awape maagizo kundi lake la Yamata Sect kufanya uchunguzi kwanzia kwenye hoteli ya Bagamoyo one na kujua dhamira ya uwepo wa wanajeshi wa Urusi aliowaua siku ya juzi , aliamini kuna jambo kubwa ambalo lilikuwa linaendelea na alitaka kulifahamu.

Baada ya kumaliza kuwasiliana na Tanya alimpigia Diego na kumpa maagizo ya ulizi wa Profesa Clark kuongezewa , aliamini lazima Maksim angefanya jaribio la kumteka Clark hivyo hakutaka kutoa mwanya huo kufanikiwa.

“Mfalme kuna taarifa nyingine imetufikia?”Aliongea Diego

“Taarifa gani?”

“Kuna tishio la kigaidi ambalo limepangwa kufanywa na kundi la Alshababu kati ya mpaka wa Tanga na mkoa wa pwani , taarifa zinaonyesha wanajeshi hao wanataka kuachia bomu lenye siraha ya kibaiolojia”Aliongea Diego na kumshangaza Roma.

“Unamaanisha Tribute to Maria?”

“Ndio Mfalme Pluto , ni taarifa ambayo tumeipata muda huu hivyo hatujaithibitisha na uchunguzi wetu”

“Imetumwa na nani?”

“Kuhusu mtu alietuma kwetu hajaweka wazi jina lake , ni kama hakutaka kujitambulisha lakini inaonekana nia ni sisi kuchukua hatua”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kidogo.

“Fanyeni kwanza uchunguzi kuthibitisha taarifa hio na juu zaidi tufahamu ni kwanini wanajeshi hawa wanataka kutumia Tanzania kama sehemu ya majaribio, unaweza kumtafuma Omari Tozo akawarahisishia katika uchunguzi, ukikamilisha nakupa ruhusa ya kuamua cha kufanya ili kuhakikisha tukio hilo halifanikiwi na kuleta matatizo kwa raia”

“Sawa mfalme Pluto nakuhakikishia kila kitu kitaenda sawa”Alijibu Diego na Roma alikata simu huku akihema kwa nguvu , alijua tukio hilo lilikuwa likimuunganisha na mwanamke aliekuwa akifahamika kwa jina la Aishapova lakini hata hivyo alimini hakuna kitu kinafanyika bila ya sababu.

Nusu saa mbele aliweza kupokea simu kutoka kwa Makedoni na Roma aliipokea haraka haraka.

“Mfalme Pluto watu wetu wamejaribu kutafuta taarifa zinazohusiana na maabara ya Nicene kupitia mfumo wa utunzaji taarifa wa KGB na tumeweza kufahamu Nicene ni maabara iliofufuliwa upya mwaka 1940 na mwanasayansi aliefukuzwa jeshini chini ya serikali ya Kisoviet , alifukuzwa kutokana na Marekani kuishutumu Urusi kumtumia mwanasayansi huyo kufanya utafiti juu ya siraha za kibaiolojia , hivyo kufukuzwa kwake ilikuwa ni kwa ajili ya kuzima kashfa hio , lakini hata hivyo hakuacha kufanya utafiti wake kwani baada ya kutoka jeshi alifufua maabara ya Nicene kwa kushirikiana na familia ya Kyluchevsky”Aliongea Makedon.

“Kwahio unaamaanisha kwamba familia hio ndio ipo nyuma ya tafiti zinazoendelea ndani ya maabara ya Nicene?”

“Ndio Mfalme Pluto , kutokana na ukubwa na nguvu ya familia hii ni watu wachache sana wanaojua kinachoendelea ndani ya maabara hio , wanafunzi wawili ambao walikuwa chini ya Profesa Clark wanafanya kazi ndani ya hio maabara na kama kweli wanaboresha kimiminika cha Tribute to Maria basi tutakuwa hatarini, labda tu”

“Labda Profesa Clark aweze kutengeneza chanjo si ndio?”Alimalizia Roma.

“Ndio Mfalme , Nadhani Klyuchevsky wanamuhitaji Clark kwa ajenda binafsi na sio kwa ajili ya ndoa, inaonekana kama asipokuwepo upande wao anaweza kuharibu mipango yao ndio maana wametoa pendekezo la ndoa”

“Umefanya vizuri kunipatia taarifa ila kwasasa nataka utafute eneo maabara hio ilipo na kisha umpe taarifa zote Sauroni”

“Mfalme Pluto kwanini unataka kumpa kazi kichwa maji kama Sauroni , hii tunapaswa kuifanyia kazi wenyewe Mossad”

“Wanajeshi wenu hawawezi kushindana na Wolverines kutokana na uwezo wao wa kujiponyesha”

“Lakini Mfalme Pluto hata The Eagels hawawezi , tena hapa tunazungumzia Wolverines na sio Vampires”

“Kama wakishindwa nitaingia kazini mwenyewe na wengine wote waliosambaa sehemu tofauti tofauti nitawapa kazi kikosi cha Expendable”

“Aaa Mfalmeee..Expendable!!, unaonekana kuwa na hasira kuliko nilivyodhania niliamini huwezi kwenda mbali mpaka kuwatumia wanajeshi wa kikosi cha Expendable”

“Walitakiwa kujiandaa mara baada ya kumfanya Clark kuwa kete yao kwenye mchezo wa Chess”

“Mfalme Pluto mpango wako wa mwisho ni upi?”

“Huyu Maksim anaonekana kadhamiria kweli kumuoa Clark , lakini atawezeje kutimiza azma yake kama hatokuwa na familia tena”Aliongea Roma na kumfanya Makedoni upande wa pili kunyamaza , aliamini kabisa alichokuwa akimaanisha Pluto ni kwamba angeua wanafamilia wote wa jamii ya Wolverine.

*******

Upande mwingine ndani ya ikulu ya Mheshimiwa Senga kulikuwa na kikao cha dharula.

Kikao kiliitishwa mara baada ya serikali kupata taarifa za tishio la ugaidi kutoka ubalozi wa Marekani , baada ya taarifa hio kufikia usalama wa taifa vikosi vya uchunguzi vilipewa maagizo ya kufanya uchunguzi wa haraka sana kuithibitisha.

Watu wanne walikuwa wameketi kwenye meza , akiwemo Raisi mwenyewe ,Mheshimiwa waziri mkuu , waziri wa ulinzi , Mkurugezi wa kitengo cha usalama wa taifa , Mkuu wamajeshi na mkuu wa jeshi la polisi.

Mheshimiwa Senga alimpa ishara mkuu wa idara ya kitengo cha usalama wa taifa kutoa maelezo kwa ufupi juu ya kile kinachoendelea.

“Tumeweza kupokea taarifa kutoka ubalozi wa Marekani inayoelezea tishio la kigaidi linalotaka kufanywa upande wa mkoa wa Tanga , kwa maelezo ambayo wametupatia ni kwamba siku mbili zilizopita katika mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo kulitokea tukio la kiharifu ambalo lilipelekea mmiliki wa hoteli ya Bagamoyo one kupoteza maisha”

“Nimesikia kwa muda mrefu juu ya hii hoteli na skendo zake lakini sikuwahi kujua mmiliki wake”Aliongea Afande Tozo.

“Bwana Shedrack Kengeu ndio mmiliki”Alijibu na Mheshimiwa alimpa ishara ya kuendelea.

“Ni kweli kwamba kwa muda mrefu serikali yetu ilikuwa ikifahamu mmiliki kuwa Shedrack Kengeu ,lakini kupitia ubalozi wa Marekani tumeweza kugundua mmiliki wa hoteli ya Bagamoyo one ni mtu mwingine”

“Unamaaisha nini kusema mmiliki ni mtu mwingine”

“Maelezo yanaonyesha Shedrack anaimiliki hoteli ya Bagamoyo One baada ya kupewa nguvu kisheria(Power of Attorney), lakini wamiliki wa hoteli hio ni kampuni ifahamikayo kwa jina Dalai , iliosajiliwa mwaka 2018 katika visiwa vya Shelisheli , baada ya kufatilia kampuni hii ya Dalai imegundulika ni kampuni hewa(Shell Company) ambayo iliuzwa kwa kampuni ya Talhat kutoka Somalia, mmiliki mkuu wa hisa ndani ya kampuni ya Talhat ni Mahmood Tarf ambaye ni mfungwa nchini Botswana”Aliongea na kufanya wote kuangaliana kwani ni kama hawajaelewa.

“Kwahio kwa maelezo yako unataka kumaanisha nini bwana Kizito”Aliuliza Mheshimiwa Waziri mkuu.

“Mahmood kabla ya kukamatwa nchini Botswana alikuwa akihusishwa kuwa mkuu wa kikosi cha wapiganaji wa Alshababu mpaka alipohamisha madaraka yake kwa mdogo wake afahamikae kwa jina la Faruq Tarf , huyu bwana ni mfanyabiashara pia na ameoa mwanamke wa Kitanzania afahamike kwa jina la Zumaridi kutoka Mwanza”

“Maelezo yamekuwa marefu kidogo , tunataka kujua tishio la kiusalama linaungana vipi na Bagamoyo one”Aliongea IGP.

“Zumarid kabla hajahamia nchini Tanzania akitokea Somalia alipokuwa akiishia na mume wake Faruq alishajifungua mtoto wa kiume na hata hivyo hakupewa nafasi ya kurudi nchini na mtoto wake afahamikae kwa jina la Sharf , lakini miaka minne iliopita Sharf aliweza kurudi kwa mama yake Zumarid na kubatizwa kuwa mkristo na kupewa jina la Shedrack Kengeu”.

Baada ya Sharf kukaa nchini kwa jina la Shedrack Kengeu ,mwaka mmoja mbele ndipo ujenzi wa hoteli ya Bagamoyo One ulipo anza na kukamilika mwaka jana , hivyo ukifuatilia muunganiko wote huo utadugnua Sharf baba yake ni mkuu wa kikosi cha Alshababu na kwa uchunguzi uliofanyika hivi karibuni ilionyesha Shedrack Kengeu kuwa na mahusiano ya karibu na kundi la ZoaZoa kutoka Kahama , mahusiano haya yalionekana kuwa na ajenda ambayo ilionyesha Shedrack alikuwa akimshawishi mkuu wa kundi hilo kusaidia kupitisha siraha za kivita kupitia Tanzania kwenda kwenye kambi ya Alshababu ombi ambalo ilionekana halikukubaliwa”

“Hii ni taarifa pia ambayo tumeletewa na Ubalozi kupitia idara ya CIA ,inaoneysha walikuwa wakifuatiia kwa ukaribu sana familia ya Klyuchesky kutoka Urusi na wameweza kugundua familia hio kufanya mawasiliano na mkuu wa kikosi cha Alshababu kwa kumtumia undercover agent afahamikae kwa jina la Aishapova”Aliongea kwa kuonyesha picha ambayo anaonekana Aishapova akiwa amesimama na mwanaume alievalia kanzu, lakinni hata hivyo sura ya mwanaume huyo haikuonekana kwani alijifunga usoni kwa Skafu na kuacha macho tu kuonekana.

Aliweka kituo na akachukua karatasi na kisha kumpatia mheshimiwa Senga na akamalizia kwa wanakikao wote.

“Picha unazoziona hapo Mheshimiwa zimetumwa kwetu kutoka makao makuu ya CIA na hao ni wanajeshi wa kundi la Alshababu wakiwa mpakani kuingia Tanzania na siraha aina ya bomu la kibailojia”

“Alshababu kwanini wanataka kutuchokoza ,hatujawahi kuwa na ugomvi nao?”Aliuliza Afande Tozo

“Waamarekani wanaamini kwamba kutokana na mazungumzo kati ya familia ya Kyluchevsky na Alahababu yalianza kwa muda mrefu , wanaamini kitendo cha kufa kwa Shedrack Kengeu nchini Tanzania yalimwamsha Faruq na kutaka kulipiza kisasi cha mwanae , lakini hata hivyo wanaamini kuna zaidi ya sababu ambayo hwaifahamu mpaka sasa”

“Ineleta maana , ni mara chache sana kwa wanajeshi wa Alshabau kutaka kujiletea uhasama na jeshi letu , lakini huyu Shedrack kwanini amakufa”

“Kwa taarifa tulizoweza kukusanya ni kwamba Shedrack kauliwa na Roma Ramoni , ambaye ndio aliesababisha tukio la kiharifu ndani ya hoteli ya Bagamoyo one , baada ya kufika kumchukua mtoto wa Samweli Nguluma , lakini hata hivyo tukio hilo lilitokea mara baada ya gari lake kutegeshewa bomu na kulipuka, hivyo inaonekana muhusika alikuwa Shedrack na Roma alimuua kwa kulipiza kisasi”

“Roma Ramoni?”Aliuliza mheshimiwa huku akionyesha hali ya mshangao na hasira kuanza kujitengeneza.

“Ndio mheshimiwa, lakini hata hivyo hatuwezi kuamini moja kwa moja kwamba Alshababu wanataka tu kulipiza kisasi inawezekana kuna sababu nyingine ndio maana Klyuchevsky wamehusika”

“Nashindwa kuelewa moja kwa moja , ukijumlisha swala la Profesa Clark na Kifo cha Samweli Nguluma halikai sawa na taarifa tuliokuwa nayo, kama Wamarekani wapo sawa kuhusu Klyuchevsky kufanya mazungumzo na Alshababu kwa muda mrefu basi tunaweza kuamini kuna zaidi ya sababu”

“Mheshimiwa huyu Profesa Clark anahusikaje na familia hii ya Klyuchevsky?”Aliuliza Waziri Wa ulinzi na Mheshimiwa Senga aligundua kweli hakuwa ametoa mwongozo wa kile kilichokuwa kikiendelea.

Lakini palepale mlango wa ofisi hio ulifunguliwa na mwanamama afahamikae kwa jina la Fatuma ambaye alpandishwa cheo kutoka kuwa msemaji wa ikulu mpaka kuwa katibu mkuu wa Ikulu.

“Mheshimiwa Afande Kweka yupo kwenye line anataka kuongea na wewe”Aliongea mwanamama Fatuma na mheshimiwa alimpa ishara ya kumpatia simu.

“Senga nasikia upo kwenye kikao na wakuu waandamizi wa usalama wa nchi”

“Nadhani taarifa imekufikia , tamaa za mjukuu wako zinaingiza nchi kwenye matatizo”Aliongea Raisi Senga.

“Mjukuu wangu au mtoto wako, hata hivyo nimekupigia kukutaarifu kwmaba haina haja ya kuendelea na kikao”Aliongea Afande Kweka.

“Unamaanisha nini haina haja ya kuendelea na kikao?”

“Tayari Mjukuu wangu kashaingia kazini na muda si mrefu utapata taarifa ya tishio la kigaidi kuzimishwa, lazima tukubali kuna utofauti mkubwa kati yako na Roma , wewe wakati unaendelea kufanya vikao yeye tayari anashughulikia tatizo”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Senga kungata meno kwa hasira kwani aliona kama baba yake anamtusi.

ITAENDELEA JMATANO -WATSAPP ME 0687151346

Hivi juma tano c leo? Singanoja, sema kitu, tusubiri au tuvute kete tu
 
AUTHOR : DR SINGANOJR
SPONSORED BY : MIND LINK ENTERTAIMENT.

SEHEMU YA 447
Zilipita dakika kama therathini hivi wakati waheshimiwahao wakiendelea na kikao , mlango wa ukumbi ulifunguliwa na akaingia msaidizi wa Raisi afahamikae kwa jina la Kabwe.
“Mheshimiwa tukio la kigaidi limekuwa neutralized na kikosi cha kundi la Yamata Sect”Aliongea Kabwe kuwafanya waheshimiwa kushangazwa na taarifa hio
“Yamata Sect ndio kundi gani?”
“Yamata Sect ni kundi la kihalifu kutoka Japani ambalo mwaka uliopita mkuu wa kundi hilo alikuwa ni Noriko Okawa , mpaka alipouliwa na Roma Ramoni nchini Japani na madaraka kuhamia kwake”Aliongea Mkurugezi wa kitengo cha usalama wa Taifa na kufanya chumba chote kuwa kimya na kumwangalia.
“Mkurugenzi kundi hili kama ni la Japani imewezekanaje wakahusika kwenye misheni hii?”
“Kwa taarifa tulizo kuwa nazo mpaka sasa kundi hili liliingia Tanzania wiki kadhaa zilizopita kama wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuunga vifaa vya simu kilichopo Kibaha, ujio wao Tanzania nadhani ni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa Familia ya Roma dhidi ya Yan Buwen”Aliongea na wote walionekana kuelewa hata hivyo habari za Yan Buwen hazikuwa mpya.
“Mkurugezi taarifa ya ujio wa hawa Yamata Sect mbona haikufika ofisini kwangu?”
“Mheshimiwa taarifa ya ujio wao tuliweza kuipata siku ya jana baada ya muda mrefu wa uchunguzi”Alijibu Mkurugenzi.
“Kabwe kuna taarifa nyingine?”
“Ndio mheshimiwa, tumeweza pia kupata taarifa ya kikosi cha The Eagles kumkamata jasusi wa siri afahamikae kwajina la Aishapova wa familia ya Kyluchevsky wakati alipokuwa akijaribu kumteka Profesa Clark na wenzake wa tano ambao wanne wote wamekufa hapo hapo”Aliongea na kuwafanya wote kuangaliana.
“Mheshimiwa nadhani kama huyu Aishapova yupo hai tuombe The Eagles watupatie ili tuweze kumuhoji na kujua sababu nyingine ambayo imepelekea kuungana na kikosi cha Alshababu na kutaka kutushambulia”
“Naunga hoja pendekezo la Waziri wa ulinzi , tunaweza kupata majibu yote kwa kumuhoji huyu mwanamke , ili kujua ni mpango gani ambayo Klyuchevsky wanapanga zidi ya Tanzania”Aliongea Waziri mkuu , lakini muda huo huo Katibu wa Ikulu alionekana kuingia tena katika ukumbi hio na kuwafanya viongozi hao kumwangalia kujua kuna taarifa ipi nyingine.
“Mheshimiwa Balozi kutoka Urusi yupo kwenye Line kupitia Vidio call”Aliongea mwanamama huyo na mheshimiwa alimpa ishara ya kuunganishwa nae na ndani ya muda mfupi tu Tv iliokuwa imefungwa ukutani ndani ya ukumbi huo ilionyesha sura ya mheshimiwa Balozi Anneth Kimba.
“Mheshimiwa kikosi cha The Eagles kifahamikacho kwa jina la Expendable kimeanza kufanya mashambulizi zidi ya wanafamilia wa Klyuchevsky, Wizara ya mambo ya nje ya Urusi wametoa malalamiko yao na kutishia kuiwekea vikwazo nchi yetu kwa kukata biashara zote zinazofanyika kati ya Urusi na Afrika Mashariki kama hatutachukua hatua za kumzuia Roma”Aliongea mwanamama huyo mara baada ya kutanguliza salamu za awali na kuwafanya viongozi wote kushangaa
Hakuna alieamini kama Roma angeweza kuchumua mamuzi haraka ya namna hio ambayo ni kama yana athiri diplomasia ya taifa.
“Expendable! ? , ndio kikosi gani hicho?”Aliuliza Mheshimiwa Raisi huku akionekana kukunja ngumi kwa hasira.
“Kwa taarifa chache nilizokuwa nazo hapa mheshimiwa , Kikosi hiki ni cha kijeshi kutoka kundi la The Eagles ambacho pia kina muunganiko wa moja kwa moja na Profesa Clark , Miaka mitano iliopita Profesa Clark alitangaza kamwe tkutojihusisha kutengeneza siraha za aina yoyote za kibailojia lakini hata hivyo aliweza kutengeneza dawa ambayo inasaidia wanajeshi kupona haraka mara wanapopata majeraha lakini moja wapo ya athari ya dawa hio ilifanya miili ya wanajeshi kuwa na nguvu kubwa zisizo za kawaidaa , kutokana na matokeo hayo kikosi hicho kilitolewa katika mjumuisho wa jeshi la kawaida la The Eagles na kuingizwa katika kundi la Ninja lifahamikalo kwa jina la Zero Unity na kupatiwa jina la Expendable , idara nyingi za kijeshi zimewabatiza kikosi hicho kwa majina mengi ikiwamo jina lao maarufu la Assassin from Hell”Aliongea Mkurugenzi kutokea maelezo.
“Kama ni hivyo hili swala lina haribu uhusiano wetu na Urusi ukizingatia tunao ushirikiano mwingi wa kibiashara , Roma anaharibu uhusiano wa kidiplomasia wa hili taifa”Aliongea Raisi Senga kwa hasira.
“ Mheshimiwa nadhani tukiangalia swala hilo kwa mtazamo mwingine kuna faida , Nchi yetu haijawahi kuwa na ushirikiano mzuri sana na taifa la Urusi na sidhani kama washawahi kutuchukulia siriasi”Aliongea Mheshimiwa Waziri.
“Unamaanisha nini?”
“Ninachomaanisha kama serikali ya Urusi imeruhusu familia ya Klyuchevsky kutaka kutulipua na bomu la kibailojia kwa kupitia kikosi cha kigaidi cha Alshababu kuna ushirikiano gani hapo , wao ndio wametuchokoza kwa kuona sisi hatuna umuhimu na wanaweza kufanya wakavyo kwasababu wanajiona taifa kubwa , kama tunataka kuwa na ushirikiano imara na maaifa ya nje lazima kwanza sisi wenyewe tuwe imara kijeshi ili tuogopeke”
“Mheshimiwa Waziri una ujasiri wa hali ya juu sana , tunawezaje kuwa na jeshi kubwa kuzidi urusi ilihali hata siraha tunawategemea”
“Kama hatuna jeshi kubwa kuwazidi ndio watuchokoze , mimi namuunga mkono Roma kwa kuanza kuwashambulia , licha ya kwamba maamuzi yake yalikuwa ya haraka sana na yanaweza kutuathiri, hatuna haja ya kuogopa ili mradi Roma ataendelea kuwa upande wetu”Aliongea Waziri
“Mheshimiwa Waziri kwahio unachomaanisha ni kwamba tuache swala ili kama lilivyo licha ya athari ambazo zinaweza kutokea?”
“Mheshimiw anadhani anachoongea Waziri tunaweza kufikiria mara mbili pia, kwa taarifa za haraka haraka ambazo tulikuwa nazo ni kwamba mtoto wa Samweli Nguluma aliweza kuwekewa Kirusi kifahamikacho kwa jina la Tribute To Maria , kitendo hiki cha siraha hii ya kibailojia kuweza kuingizwa Tanzania bila sisi wenyewe kujua ni udhaifu mkubwa sana kwa taifa , kama swala hili halijaleta athari leo . vipi siku zijazo , lazima tuanzee kufikiria namna ya kujilinda kwa teknolojia zetu na sio kutegemea mabeberu, waliongiza kirusi hiki kwetu ni hawa warusi ambao tunawachukulia kama washirika wetu”
“Nadhani pia uchunguzi ufanyike ili kujua ni kwa namna gani Alshababu wameweza kusogelea mpaka wetu bila majirani zetu kufahamu”Aliongea Afande Tozo.
“Wizara ya ulinzi kwa kuhishirikiana na jeshi pamoja na idara ya usalama wa taifa mfanye uchunguzi ili uweze kufahamuni kwa namna gani kundi hili la Alshababu wakaweza kufanikiwa kuufikia mpaka wetu pasipo majiran zetu kutupa taarifa, kuhusu namna ya kumhoji Aishapova idara ya usalama wa taifa nawapa ruhusa ya kufanya majadiliano na kundi la The Eagles”Aliongea mheshimiwa na kisha palepale akampigia simu waziri wa mambo ya nje kufika ofisini kwake siku hio hio na kikao kikafungwa.
Muda huo huo wakati kikao hiko kikiendelea kilomita kadhaa kutoka ikulu , ndani ya hoteli ya Johari Rotana katika chumba cha Presidential Suite , alionekana Roma akiwa ameketi kwenye sofa huku chini yake kukiwa na mwili wa Maksim ambao unatobo kubwa upande wa kifuani , ilionyesha dhahiri Roma aliunyofoa moyo wa Maksim na kumuua hapo hapo.
Maksim alionekana amekufa kifo ambacho hata yeye menyewe hakukitarajia na kwa maiti yake ilivyokuona ikionekana ni kama alikuwa akishangaa kwanini anauliwa.
Muda huo Roma akiwa ameketi kwenye sofa , mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na akaingia Adeline alievalia suruali na Jeans na kwa hali aliokutana nayo hapo ndani ilimfanya mwili wake kutetema.
“Take care of this , I have some Business in Russia to attend to..”
“Shughulikia hali ya hapa ndani nina maswala yangu nchini Rusia naenda kuyafanyia kazi”Aliongea Roma na palepale akayeyuka na kumfanya Adeline kukosa utulivu.
********
Mji wa kihistoria wa Keswick ulijengwa katika kipindi cha utawala wa Malkia Victoria(Victorian era) kati ya miaka 1800 kwenda 1900 ndani ya nchi ya Uingereza
Juu kabisa ya kilele cha mlima mita kadhaa kutoka Ziwa la Keswick kuna ngome kubwa ya kizamani iliokuwa imesimama imara huku juu ikiwa na bendera ya taifa la UK, usanifu wa jengo hilo uliwakilisha zama za miaka ile iiliopita , lakini licha ya jengo hili kuonekana kama la Zamani kwa upande wa nje lakini ndani yake ni moja ya sehemu nzuri sana yenye kupendeza mno macho kutokana na kazi nyingi za kisanaa zilizotengenezwa na kupamba eneo lote la ndani kuanzia juu kwenye Ceilling mpaka chini kwenye sakafu.
Sasa ndani ya Ngome hii katika eneo la sebuleni alionekana mwanaume mweusi akiwa ameegamia kwenye sofa kivivu huku akiwa anapiga miayo na kugeukia saa iliokuwa ukutani.
Mwanaume huyu alionyesha huko atokako hakukuwa na amani kutokana na hata mavazi yake aliovaa yalikuwa yamejaa madoa mengi yenye damu lakini si hivyo tu juu ya meza kulikuwa na kiroba ambacho kilikuwa kikitoa maji maji kama ya damu.
Muda huo huo wakati mwanaume huyu akiendelelea kupiga miayo huku akiangalia juu kwenye Ceiling Board , mlango wa kuingilia eneo la sebuleni ulifunguliwa.
Alionekana mwanaume mzee wa miaka isiopungua kama sabini hivi , mzungu , alievalia suti ya rangi nyeusi pamoja na saa ya mfukoni mfano wa Henry graves ambayo ameivaa shingoni kwa kutumia Cheni.
Pembani yake alikuwa ameongozana na mwanamke mwenye nywele nyeupe , mzungu pia ambaye mara baada ya kuangalia mtu alieketi kwenye sofa nguo zake zilivyokuwa na madoa ya damu alijikuta akifumba mdomo.
Mwanaume yule mzee na yeye pia alionekana kwenye mshituko kwa kile kilichokuwa mbele yake , lakini alijikuta akuvaa ujasiri na kukohoa kidogo kusafisha koo.
“How rare for you to visit us , You Majesty Pluto , You Haven’t visited us Rothchilds in years”
“Imekuwa nadra sana kwako mfalme Pluto kututembelea haujawahi kututumebelea sisi Rothchild kwa zaidi ya miaka sasa”Aliongea yule mwanaume huku akijaribu kuweka tabasamu ili aonekane kuwa jasiri.
Naam mwanaume ambaye muda wote aliikuwa akipiga miayo , huku akiangalia saa ya ukutani hakuwa mwingine bali ni bwana Roma Ramoni , haikueleweka ni muda gani kafika hapo , lakini ilionekana kabisa ni zaidi ya masaa tokea alivyotoka Tanzania..
“Kwanini nahisi sauti yako ni ya kinafiki na haijafurahishwa na ujio wangu”Aliongea Roma
“Utakuwa unatania Mfalme Pluto ,Familia yetu ya Rothichild inakukaribisha muda wote”Aliongea kwa lugha ya kingereza akiwa amesimama karibu na Roma , lakini upande wa Roma hakuwa na furaha ya kuendeleza mazungumzo juu ya familia hii ambayo alikuwa akijua inajali pesa kuliko kitu chochote.
“Hebu angalia huo mfuko kwanza , ni zawadi yangu kwako”Aliongea Roma akimpa ishara yule mzee kuangalia Kiroba ambachokinavuja damu kwenye meza.
Yule mzee alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha na kisha akampa ishara mwanamke aliekuja nae aite mabodigadi waliokuwa wakilinda nje na ndani ya dakika chache tu waliweza kuingia na kufungua mfuko ule , lakini walijikuta wakitoa macho kwa woga na kurudi nyuma.
Mfuko huo uliokuwa na ukubwa wa kiroba cha Safleti ulikuwa umejaa vichwa na damu ambayo ilikuwa ikitoa halufu isiopendeza kabisa kwenye pua za binadamu yoyote.
“Ware.. Warewolves!?”Aliongea yule mwanaume mara baada ya kuona vichwa vile havikuwa na mwonekano wa kawaida bali ni kama vya wanyama..
Roma hakujali mshutuko wao , alichokifanya ni kusimama na kisha alivua shati lililokuwa na madoa ya damu na kulitupia kwenye sofa na kisha akaendelea kufungua na mkanda wa suruali.
“Imenichukua masaa zaidi ya sita kuua wanafamilia wote wa Klyuchevsky , Hivi vichwa unavyoviona ndio vya wale wanafamilia wenye ushawishi ndani ya familia”Aliongea Roma na kumfanya yule mwanaume kutetemeka
“Mfalme Pluto kwanini umefanya hivi?”
“Nyie si ndio mlipanga kumuozesha Clark kwenda kwa familia ya Klyuchevsky , Sasa wanafamilia wote washapoteza maisha hivyo naamini ndoa hakuna tena”Aliongea Roma na kumfanya yule mzee kukosa nguvu na yule mwanamke kumshikilia kwa haraka sana asije akadondoka.
“Mfalme Pluto naamini unafahamu kwamba kuna makubaliano pamoja na wenzako ya kutoingilia maswala yanayohusu binadamu kabisa , athari za matokeo kwa hiki ulichofanya?”
“Naheshimu makubaliano yaliopo na ni kweli kabisa sipendezwi na maswala ya matafia mengine , lakini hichi kilichotokea ni kwasaabu watu wangu wa karibu wameguswa, Clark ni mwanamke ambaye siku zote alikuwa akiendelea na maisha yake bila kuathiri wengine , nitafumbia macho kwa matendo yenu yote maovu mnayofanya kwa ajili ya kujipatia pesa lakini sitovumilia kuona mambo yenu yanaingilia maswala yangu binafsi”
“Hahaha., Athari !... kwa nilichokifanya leo kama kuna mtu yoyote anataka kulipiza basi namsubiria kwa hamu zote , nitamuua kila mtu ambaye ataingilia mambo yangu , Maneno ya kisiasa hayana athari yoyote kwangu na siku zote nitarudia kusema mwenye nguvu ndio muongoza njia na dhaifu hufuatia .. Oh! tena nimekumbuka hawa watu jamii ya Wolverine imenichukua masaa sita tu kuwaua wote licha ya uwezo wao mkubwa wa mapambano unafikiri binadamu wa kawaida atachukua muda gani kushindana na mimi”Aliongea lakini muda huo huo aliingia mwanaume mwingine mwenye nywele nyeupe , hakuwa mwingine bali ni Edward na baada ya kukutana na hali hio alijikuta akianza kumwangalia Roma kwa wasiwasi na kisha akamgeukia yule mzee.
“Edward nakushauri uishawishi familia yako kuzingatia sana kile wanachokifanya kupata pesa zao , wewe unaweza kuwa rafiki yangu lakini ninao uwezo wa kuiangamiza familia yako bila ya kuangalia nyuma”
“Nilidhania maswala ya kuua kikatili ushayaacha , lakini nadhani nilikufikiria vibaya , Serikali ya Urusi mpaka sasa hivi wamechukua hatua kwa kitendo ulichokifanya na wanaogopa utaenda Bersek kumuua kiongozi wao”Aliongea Edward.
“Ngoja wafanye wanavyotaka ,ninaenda kuoga kwa muda huu fanya mpango uniandalie ndege nataka kurudi nyumbani”Aliongea Roma.
*******
Ni siku nyingine kabisa muda wa asubuhi ndani ya jiji la Dar , Edna alionekana kusimama kwenye Balconi huku macho yake yote yakiangalia baharini na akifurahia kijua cha asubuhi.
Alionekana kuwa na wasiwasi kwenye macho yake, hata hivyo yote hayo ni kutokana na Roma kuondoka siku ya jana asubuhi pasipo kurudi siku nzima mpaka muda huo , ijapokuwa Roma aliaga kwa kusema ataelekea Urusi lakini Edna bado alionekana na wasiwasi na yote hayo ni kutokuwepo kwa maelewano wakati Roma anaondoka mara baada ya kuongea kauli yake ya kutaka Clark aweze kuolewa na Maksim.
Muda huo huo wakati akiendelea kuangalia upande wa baharin geti la jumba lao lilifunguliwa na gari aina ya V8 nyeusi iliingia na kusimama na palepale alitoka mwanamke mnene kidogo ambaye alimfanya Edna atoke kwenye Balconi haraka haraka na kushuka mpaka chini kwa ajili ya kumpokea.
Alikuwa ni mdogo wake Blandina afahamikae kwa jina la Jestina au Mama Nusra , mke wa tajiri Azizi ndio aliefika hapo nyumbani muda huo wa asubuhi akiwa ameshikilia boksi.
Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kumlaki mdogo wake na kupokea lile boksi na kuliweka kwenye meza.
“Edna yaani unashuka mwenyewe kunisalimia , nikajua na Roma angekuja”
“Hajarudi bado?”Alijibu Edna.
“Ooh!... nikajua asharudi tayari, tutaongea baadae kidogo akisharudi maana nimekuja kwa ajili yake”Aliongea na kumfanya Edna kuwaza kwanini Mama Nusra alikuwa na uhakika Roma angerudi siku hio.
Blandina alionekana kufurahi baada ya kutembelewa na mdogo wake , kwani tokea wahamie hapo Jestina hakuwahi kufika , ijapokiuwa waliishia ndani ya jiji moja lakini kila mtu alikuwa bize kiasi cha kutokutembeleana.
Nyumba ilichangamka kwani Soga zilionoga mpaka wakati wa kujipatia kifungua kinywa.
“Jestina umesema umekuja kwa ajili ya Roma , je una uhakika atarudi leo?”
“Asubuhi ya leo nilisikia kutoka kwa mume wangu angerudi leo ,lakini alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi , hivyo hakuwa na uhakika sana”
“Kwanini awe na wasiwasi , kuna jambo ambalo Roma kafanya huko alipoenda?”Aliuliza Blandina.
“Kama kuna taarifa mbaya nsingekuja na furaha kama hivi , siku ya jana Roma alisaidia sana taifa , huenda isingekuwa yeye taifa lingekuwa kwenye matatizo sasa hivi”Aliongea na kuwafanya waangaliane akiwemo Bi Wema.
“Mhm! mbona unaongea kimafumbo mwenzetu , ni nini Roma kafanya kusaidia taifa?”
“Ni siri nilioweza kuijua kwenye kikao kilichofanyika jana nyumbani, ila ngoja niwaambie, kwa maelezo ya mume wangu ni kwamba jana kulikuwa na tishio la kigaidi mkoani Tanga na bahati nzuri magaidi waliweza kufikiwa mapema kabla ya kufanya shambulizi la siraha za kibailojia , lakini hata hivyo inasemekana wanajeshi waliotumwa walichelewa kwani Aslhababu wameweza kuachia bomu moja ambalo lilivamia kijiji cha Mabando wilayani Pangani, lakini hata hivyo hali imedhibitiwa na hakuna madhara kwani mpaka sasa wananchi wote wa kijiji hicho wanapatiwa chanjo ambayo iliwezekana kwa msaada wa Profesa Clark”Aliongea.
“Unamaanisha kirusi chenyewe ndio hicho kinachofahamika kwa jina la Tribute to Maria”
“Yes! kumbe mshapata hizo habari”
“Ndio jana Roma na Profesa Clark walikuwa wakizungumzia kuhusu hiko kirusi”
“Basi ndio hivyo , uzuri ni kwamba licha ya kirusi hiko kuboreshwa kwa kuweza kusambaa kwa njia ya hewa lakini udhaifu wake ni kwamba kinachukua siku tatu mpaka kuonyesha athari katika mwili hivyo Chanjo muda huu zinatolewa kwa wananchi wote wa kijiji cha Mabando na maeneo ya karibu na inatagemewa hadi kesho zoezi litakuwa limemalizika ,kama sio Roma na Profesa Clark huenda kuongetokea ugonjwa wa ajabu Tanzania”
Ndio siku ya jana licha ya kwamba taarifa zilionyesha Yamaa Sct kufanikiwa kuwadhibiti magaidi wa Alshababu lakini inasemekana kuna baadhi yao ambao walivuka mpaka na kuingia Tanzania na kurusha bomu hilo kwenye kijiji kilichokuwepo wilayani Pangani kifahamikacho kwa jina la Mabando, kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba walidhania ni mabomu ya machozi, lakini baada ya taarifa kutolewa kwenye ngazi ya serikali ndipo uchunguzi ulipobaini ni sehemu ya mashambulizi ya siraha za kibailojia ndani ya kijiji hicho na ndipo kulipotolewa rai kwa wananchhi wote kutosafiri nje ya kijiji mpaka waweze kupatiwa chanjo.
Ilikuwa rahisi kwa Profesa Clark kutengeneza chanjo kwani tayari alikwisha kutengeneza chanjo ambayo alipewa Mika.
“Tena nimekumbuka , nasikia kuna bwana mzungu ambaye anafahamika kwa jina la Maksim aliekuja kuwatembelea hapa pamoja na waziri wa Viwanda , sasa nasikia huyo ndio ambaye amejihhusisha na utengenezaji wa Virusi hivyo ambavyo inasemekana athari zake zinafanana kabisa na za Ebola, imekuwa bahati kwamba Profesa Clark yupo hapa nchini na amewasaidia wataalamu katika hospitali ya Muhimbuli kuandaa chanjo ya haraka na kwa maelezo ambayo nimeweza pia kusikia ni kwamba Maksim alitaka kumuoa Clark ili kuzuia asijetengeneza Chanjo tofauti na wao wenyewe”Aliongea kwa kirefu huku akijaribu kuelekeza sifa zote kwa Roma kwa kusema ndio sababu ya ujio Profesa Clark Tanzania na hata kusaidia taifa kuliokoa na janga la mlipuko wa kirusi kinachotokana na kimimnika cha Tribute To Maria.
Sasa maneno ya Jestina yalimfanya Edna kujihisi ni mwenye hatia kwa kauli yake aliomwambia Clark , alijiambia alikuwa mbinafsi kwa kumfikiria Clark vibaya kwa kushauri aweze kwenda kuolewa na Maksim, kumbe mwanaume yule hakuwa na nia ya dhati ya kumuoa bali alitaka kutumizia mipango yake.
Wakati huo wakati akiwaza, mngurumo wa gari kutoka nje ulisikika ikimaanisha kmaba kuna mtu ambaye alikuwa akifika ndani ya nyumba yao .
Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kwenda kuangalia juu ya mgeni anaefika na aligeuka.
“Ni Roma karudi kweli”Kaongea Blandina kwa furaha.

SEHEMU YA 448
Roma aliweza kuchukua masaa kadhaa kuwa angani kwa ndege binafsi ambayo iliandaliwa na Edward.
Alishangaa mara baada ya kuona ndani kwake kulikuwa na ugeni , alisogea hadi sebuleni huku macho yake yote yakimwangalia Edna.
“Roma msalimie kwanza mama yako mdogo”Aliongea Blandina mara baada ya kuona Roma muda wote kamwangalia mke ,ilibidi asalimiane nae, ukweli hakuzoea kusalimia kwa kusema ‘Shikamoo’ kutokana na mazingira aliokulia hivyo alitumia lugha ya kingereza tu kusalimia.
“Babe mbona unaniangalia hivyo bila ya kuongea lolote ? Au ndio furaha ya kuniona nimerudi”Aliongea Roma akimchokoza Edna ambaye alikuwa akimwangalia Roma bila neno.
“Hamna tu nimefurahi umerudi”Alijibu Edna kwa sauti ndogo na kuwafanya Blandina na Mdogo wake kutabasamu.
“Roma nimekuja leo kwasababu babu yako kaniagiza nije nikualike angalau ukamuone , lakini pia anataka kukupa pongezi kwa msaada uliofanya siku ya jana , anataka kupitia msaada wako umshawishi Profesa Clark kuendelea kubakia nchini Tanzania ili kuweza angalau kusaidia wanasayansi wetu waweze kujitegemea katika tafiti mbalimbali ikiwemo za siraha”Aliongea
“Unamaanisha yule mzee Atanasi , bado tu na umri wake ananikumbuka?”
“Baba ni mzee lakini kumbukumbu zake zinafanya kazi vizuri tu na ni mtu wa kufatilia siasa kila siku na anatamanni kuona Tanzania ikipiga hatua kabla ya kifo hakijamchukua , mwenyewe anasema anataka akikutana na Nyerere awe na taarifa nzuri ya kumwambia”Aliongea na kuwafanya kucheka.,
“Kwannini wanataka Profesa kubakia Tanzania , waliweza kumruhusu Yan Buwen kuingia Tanzania mpaka kupatwa na ukichaa na sasa amekuwa tishio la usalama wa familia , Siwezi kumfanya Clakr kubakia hapa Tanzania kama hapendi ,kama wamemshawishi akakataa basi mimi sina sababu ya kuongea nae”Aliongea Roma.
Ndio Jestina aliagizwa hapo nyumbani ili aweze kumshawishi Roma kufika nyumbani kwa Mzee Atanasi kwa ajili ya mazungumzo , lakini kubwa zaidi ni kutaka Clark asaidie kutengeneza wanajeshi kama wa kikosi cha Expandable lakini pia kusaidia wanasayansi wa Tanzania kujiendeleza katika uundaji wa siraha kwa siri.
“Nimekuja tu kukupatia taarifa , hata hivyo kila taifa linampigania Profesa Clark kwa uwezo wake”
“Tanzania kama ilifeli kumshawishi Profesa Shelukindo kuwasaidia katika hilo , hawatoweza kwa Clark ni bora wakaacha kuota ndoto ya mchana na wafanye mpango wa kutuma vijana nje ya nchi kuweza kupata ujuzi”Aliongea Roma na Jestina hakutaka kutia neno , hata hivyo alionyesha kumhofia Roma kwani pia alipata taarifa ya namna alivyoweza kuua wanafamilia wote wa Klyuchevsky.
Baada ya Mama yake mdogo kuondoka akisindikizwa na Mama yake , Roma alimfuata Edna ambaye alikuwa ndani ya chumba chake cha kujisomea alitaka angalau kuongea nae , kwani aliona alikuwa amenuna bila ya kutokujua sababu..
“Vipi Edna kuna jambo lingine nimefanya ambalo limekukwaza?”
“Mh! Hapana najihisi hatia kwa kukukosea?”
“Kwanini , kuna kitu kimetokea, Wife niambie kama kuna mtu kakuchokoza, nitahakikisha halioni jua likizama”
“Sio hivyo, kwanini kila kitu kwako lazima utangulize neno kuua, ni jambo jepesi sana kwako?”
“Nilikuwa natolea mfano kama mtu atakuchokoza , ni mfano tu”
“Mfano! , hivi unafikiri nilishindwa kuona namna Mama Nusra alivokuwa na wasiwasi na wewe hata wa kukuangalia machoni?””Aliongea Edna.
“Roma niambie huko ulipotoka umeua tena?”Aliuliza Edna na kufanya Roma kushindwa kujibu , hata hivyo hakujua kama Edna angefahamu kwamba amefyeka familia nzima ya Maksim , Roma alishawahi kumuahidi Edna kwamba asingeua watu hovvyo hivyo alichokifanya ni kama alienda kinyume na ahadi yake.
“Edna nisamehe , nilichokifanya sikudhania kingekufanya kukasirika lakini nilikuwa na sababu ya kufanya hivyo”
“Yote hayo ni kwasababu ya Clark tu ndio maana unavunja ahadi tuliowekeana, Sitaki uombe msamaha tena , hata hivyo haujanifanyia kosa lolote”Alongea Edna huku sura yake ikijikunja na kuonyesha alikuwa na hasira.
Roma ilibidi ajaribu kumsogelea akitaka kumgusa Edna , lakini hata hivyo aliogopa kwamba angekasirika zaidi, kwa jinsi Roma alivyokuwa akimhofia Edna ni kama sio Mfalme Pluto aliekwenda kuchinja familia nzima ya Wolverine , Edna alikuwa udhaifu wake mkubwa,
“Edna mpenzi wangu…”
“Sitaki uniite hivyo , sistahili kuwa mke wako, ulimwengu wako na wangu ni tofauti , Kwako wewe kuua ni sawa sawa na kupumua , pesa na madaraka kwako wewe unaamini ni kwa wale wanaoweza kuwaua wengine , unaweza kuua watu zaidi ya kumi bila hata ya kuonyesha hatia lakini mimi kushuhudia kifo cha mtu mmoja tu kunaweza kunifanya usiku nisilale vizuri wiki nzima “
“Maadui zako wewe sio binadamu wa kawaida na huenda wananiona sistahili hata kuitwa mkeo , Siwezi kukusaidia kwenye lolote na sina ninachokijua zaidi ya kugombana na wewe kuhusu wanawake wako wengine , I have nothing left to offer , My dignity , my pride and my beliefs are just a piece of fragile paper in front of you , halafu bado nakuona kama mtu wa thamani sana kwangu , naonekana kama mwanamke kichaa , Eh,..”Aliongea huku akianza kutoa machozi na kumfanya Roma kushangaa ,ijapokuwa haikuwa mmara ya kwanza kuuona Edna akiongea hivyo lakini ni mara yake ya kwanza kumuona Edna akionyesha hali ya kutojiamini mbele yake kwa namna ya kujishuku.
“Muda mwingine nahisi wapenzi wako wanafuraha kuliko hata ilivyokwangu mimi ambaye ni mkeo , Hawana sababu ya kujihisi kutokuwa wa thamani kwako ili uwapende, hawana haja ya kuwaza utawatembelea au utarudi nyumbani mapema kama ilivyo kwangu , labda ningekuwa sio mkeo na kuwa kama wao ningekuwa na furaha na mimi”
“Edna usiongee hivyo..”Roma alishindwa kusikiliza na kutoa kauli ya kinyonge.
“Roma naamini yatakuwa maamuzi sahihi kumfanya Clark kuendelea kuwa karibu yako , ndio yeye pekee ambaye ana akili nyingi za kukusaidia hivyo ni wa thamani kwako , ni mrembo na kubwa zaidi anatoka kwenye familia kubwa ya kifalme , Anakupenda mno kiasi kwamba yupo tayari hata kuolewa na shetani kwa ajili yako , hawezi kuota usiku kucha kwaasababu tu eti umeua mtu, wala kuogopeshwa na wanawake wengine , kwasababu hakuna hata mmoja ambaye anaweza kufikia levo zake”
“Edna unaongea nini wewe?”Aliongea Roma huku hasira zikianza kumpanda.
Edna usiku mzima alishinda kuanza kujifananisha na wapenzi wa Roma katika vitu vingi na katika kufikiria alijua hakuna cha ziada ambacho anampatia Roma , hakuwa akimpa kitumbua kama wenzake walivyokuwa wakifanya , hakuwa na akili nyingi kama Clark kwamba angemsaidia kwenye mambo mengi, yaani Edna alijiona kwamba hana chochote cha kumsaidia Roma kwani kama ni hela Roma anazo , kitendo hicho kilimfanya ajione hana thamani kubwa kwenye maisha ya Roma kama ilivyo kwa Clark na hilo ndio swala ambalo lilimkasirisha na kumuona Clark kama tishio kwake , ilikuwa ni maya yake ya kwanza kuanza kujilinganisha na mwanamkie mwingine kwanzia uzuri na vitu vingine.
“Edna nishakuambia wewe kwangu ni wa kipekee na bila wewe nisingekuwa na maisha ya aina hii , kwanini uanze kujihisi hauna thamani kwangu”Aliongea Roma.
“Mimi sijui , labda kwasababu nashindwa kujielewa mimi mwenyewe , naomba unisamehe kama nimekukwaza ninaenda kazini”Aliongea na kisha alitoka kwenye chumba hicho cha kusomea na kuingia kwenye chumba chake na kumuacha Roma ambaye hakujua cha kufanya kumpoza Edna, alijua wanawake hisia zao hubadilika badilika kutokana na mazingira lakini hakutegemea jambo hilo kwa Edna kwani siku zote alimchukulia kama mwanamke anaejiamini kwa kila sekta , lakini mwisho wa siku alijiona yeye ndio mjinga , wanawake wote wanafanana kwa kila kitu likija swala la hisia , Edna alikuwa akilalamika kwa kumchukulia Clark kama mshindani wake.
Roma mara baada ya Edna kuondoka kihasira hasira aliweza kupokea simu kutoka kwa Amina ambako angalau aliweza kupunguza stress zake zote zilizosababishwa na mke wake.
Siku yake iliisha vizuri kwani waliweza kuzurura mchana wote hata walipokuwa eneo la Mlimanni, Roma aliweza kumuona Rufi akiwa pamoja na Mika lakini Rufi yeye hakuweza kumuona Roma.
Muda ambao Roma alirudi nyumbani, mke wake alikuwa asharudi tayari , Roma alikuwa akiwaza siku nzima namna ya kumbebembeleza Edna na kurudi kwenye hali yake ya kawaida na katika kufikiria kwake aliona ni heri siku hio wakienda kupata chakula nje na nyumbani.
Na ndio ambacho Roma alifanya, alivyofika aliwapa taarifa Bi Wema na mama yake kwamba hawatokula chakula cha usiku kwani wnatoka Out na Blandina hakua na kipingamizi kwanza alifurahi kuona mwanae anaweka juhudi kumfurahisha mke wake.
Haikueleweka Roma alimwambia nini Edna huko walikotoka lakini Edna alirudi akiwa na furaha mno , huku kila alipokuwa akimwangalia Roma usoni kwa jicho la huba alikuwa akitabasamu bila sababu..
Kule kukasirika kwa Edna kulikuwa kumeisha kote na hata aliporudi na Chumbani ilimchukua kidogo tu kujilaza kitandani na kupotelea usingizini.
Roma baada ya kuona Edna kalala alirudi kwenye chumba chake kwa ajili ya kubadili mavazi baada ya kuoga , lakini ile anamaliza tu , simu yake ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina la mtu anaempigia aligundua ni Neema Luwazo.
“Hivi wewe mwanaume kwanini huna huruma?”Sauti ya malalamishi ilisikika mara baada tu ya Roma kupokea simu.
“Darling mbona unaongea ukiwa na jaziba hivyo , Donyi kakukasirisha nini?”Aliongea Roma.
“Unao uwezo wa kumtoa out Amina siku nzima lakini pia kubebana na mkeo kule ufukweni lakini umeshindwa hata kunijulia tu hali , hebu niambie ni lini ushawahi kunitoa Out hata mara moja , unanichulia mwepesi kwasababu muda wote nipo kimya , unafikiri nashindwa kuja kukutembea kila siku hapo nyumbani kwako ili nimkasirishe mkeo?” Roma alijikuta akikosa usemi , aliamini huenda Neema Luwazo alimuona akiwa ufukweni na Edna akiwa amembeba mgongoni kimahaba , maana hivyo ndicho walichofanya baada ya kupata chakula cha usiku kwenye mgahawa.
“Neema usiwe na hasira , unajua mwenyewe muda mwingi nakuwa na mambo mengi kichwani lakini pia niliogopa kuja kwako kwa kuhofia uwepo wa mtoto wako Donyi”
“Acha kutafuta sababu zisizokuwa na maana , kama ungekuwa unaogopa sana uwepo wa Donyi kwenye maisha yangu usingenisogelea kabisa . Hata hivyo namshukuru Mugnu sio kwamba nakutegemea kunihudumia , hivyo naomba usije ukanitafuta tena , mimi na wewe basi”Aliongea Neema kwa hasira na kisha akakata simu.
Roma alijikuta akitabasamu kwa uchungu , hata hivyo alijua tu Neema Luwazo aliongea hivyo kwasababu ana hasira na wivu, ilionyesha mwanamke hata awe na kila kitu lakini kwa mwanaume ataishia kuwa dhaifu tu.
Roma alivaa na hakujiuliza mara mbili mbili , kwasababu alijua Edna ashalala muda huo , ilimbidi kwenda nyumbani kwa Neema Luwazo muda huo huo kupitia Balkoni akajaribu kutulizza gubu lake.
Na kweli ile anafika nje ya Balkoni kwenye chumba ambacho kilikuwa cha Neema Luwazo aliona taa bado ipo wazi na kumfanya atabasamu kifedhuli, Roma aliona kabisa maneno ya Neema Luwazo ni mtego tu , kwanza kilichomchekesha hata mlango wa kutokea kwenye Balkoni haukuwa umegufungwa kwa ndani.
Roma baada ya kuingia alimkuta Neema akiwa amejilaza kitandani pasipo kujifunika shuka na nguo za kulalia nyepesi ambazo zilichora umbo lake.
“Umekuja kufanya nini hapa , si nimekuambia mimi na wewe basi”Aliongea lakini Roma macho yake ya kifisi yaliendelea kuchunguza umbile la mrembo Neema.
“Unaniangaliaje hivyo , wakati una mke mrembo wa kuvutia umemuacha nyumbani?”
“Acha hizo basi nishafikta tayari haina haja ya kujifanyisha kama mtoto mdogo, vipi Donyi keshalala?”
“Kashalala huyo muda mrefu tu , Vipi upo hapa kwa ajili ya mchezo au kuna kingine kimekuleta , kwanini unaniambia najifanyisha kama mtoto?”
“Kwa muda huu unafikiri nini kimenileta zaidi ya mchezo , hatuwezi kwenda kutemba sasa hivi ni usiku “Aliongea Roma na kumsogelea karibu na kuanza kumnusa nusa kama mbwa.
“Wewe usiniharakishe nipo na hasira bado?”
“Tunaweza kuendelea ukiwa na hasira , hakuna kinachoharibika “Aliongea Roma huku akipeleka Mkono kwenye sehemu ambazo ndio mashteni ya Neema yanalala.
“Argh..”
Walifukunyuana usiku mzima kiasi kwamba Roma usiku huo alisahau kabisa kurudi nyumbani na ile anashituka ilikuwa saa tatu asubuhi, alijikuta akijikasirikia kwa kupitiwa na usingizi muda mrefu , lakini alijua ashachelewa na upande wa Neema hakujali hata kumuamsha zaidi ya kuandaa kifungua kinywa.
“Donyi yuko wapi?”
“Kafuatwa na mpenzi wake asubuhi na wameondoka?”Aliongea Neema na kumfanya Roma kushangaa kidogo.
“Mpezi wake , sijawahi kusikia Donyi akiwa na mpenzi”
“Kassimu mtoto wa Tajiri Azizi ndio mpenzi wake mwanzoni Donyi alionekana kutompenda , lakini sasa hivi kakolea na leo asubuhi wamechukuana wanaenda Ngorongoro”AliongeaNeema na Roma hakuingizia swali na kuendelea kunywa chai huku wakibadilisha stori nyingine.
Neema kila alipokuwa akimwangalia Roma aliishia kutabasamu , ilionekana alikuwa na kumbukumbu ya kile kilichotokea usiku ndio maana muda wote alionyesha hali kama ndio kwanza anafahamiana na Roma.
Neema Luwazo hakuwa na haja ya kufanya kazi sana kama ilivyokuwa Edna , kwanza walikuwa wakitofautiana namna wanavyofanya biashara , Neema alipenda watu wenye uwezo kumsaidia kufanya kazi zake , huku yeye akidili na baadhi ya maamuzi tu ya kampuni hususani upande wa bodi ya wakurugenzi.
Alikuwa tofauti na Edna ambaye alipenda kufanya kila kitu yeye na kusimamia wafanyakazi wake kwa kila wanachofanya na hata likija swala la ki uwekezaji Edna alikuwa ni mwanamke anae take risk kila fursa inapojitokeza.
Wakati wakiendelea kunywa chai simu ya Roma ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina ni la Edna mke wake na moyo ulienda mbio na kumfanya apokee palepale.
“Sijui upo kwa mwanamke gani muda huu na sitaki hata kujua , lakini kwanini haupo kwenye kikao saa tano hii , Kama hutaki kuendelea kuongoza kampuni ni bora unieleze nitafute mtu mwingine, Acha kunikasirisha Roma”
“Kikao gani , mbona sijui kama kuna kikao?”
“Uko siriasi kweli, Hujapata kusikia kuna kikao cha viongozi wa juu wa kampuni za habari na burudani na wizara?”
“Ndio mara yangu ya kwanza kusikia kuhusu kikao hicho?”
“Kama ni hivyo kwanini umemuajiri Tanya kama Secretary wako.Kwanini hajakuambia swala muhimu kama hilo?”Aliongea Edna huku sauti yake ikioneysha kukasirika.
“Hajaniambia , ni kweli jana sikufika kazini lakini sikujua kuhusu kikao”
“Sawa naomba uwahi ukutane na hawa wageni muhimu wakufahamu”Aliongea Edna na kukata simu na kumfanya Roma kuvuta pumzi
 
SEHEMU YA 449.
Roma mara baada ya simu kukatwa ilibidi kwanza awasiliane na Tanya kujua nini kinaendelea kwani hakuwa hata na taarifa.
“Master ni yapi maagizo yako?”Aliongea Tanya mara baada ya kupokea simu , lakini sauti ya Tanya Roma hakuwa akiizoea kabisa.
“Tanya Boss Edna kasema kuna kikao nimekosa leo , nini kinaendelea ?”
“Ni project ilioandaliwa makao makuu , inayohusisha Semina kwa wafanyakazi wote wa kampuni yetu pamoja na Wizara ya Habari na utamaduni,lakini pia kuna kikao ambacho kilijumuisha wawekezaji kutoka nje ya nchi ambao wanapanga kufanya kazi na sisi , Semina na watu wa Wizara imekwisha isha lakini kikao na wageni kutoka nje ya nchi bado hakijaanza”Aliongea Tanya kwa lugha ya kingereza.
“Sasa kwanini hujanipatia taarifa?”
“Nisamehe sana Master ,nilidhania utakuwa bize ndio maana sikuthubutu kukusumbua”Aliongea huku sauti yake ikiwa na uoga , lakini Roma aliishia kumlaumu Noriko Okawa kwani alimfunza Tanya kuishi kama mtumwa kwa watu ndio maana muda wote ametawaliwa na hofu.
Roma alikata simu na kisha aliagana na Neema Luwazo ambaye ilionekana pia alikuwa akijua kuhusu Semina hio , Roma aliondoka haraka na kurudi nyumbani na kupiga suti ya Tuxedo haraka haraka baada ya kuoga , alipuliza unyunyu alionunuliwa na Edna na kisha akaingia kwenye gai yake ya Lexus ambayo hata namba hakuhangaika kuzibadilisha.
Dakika kadhaa mbele aliwasili ndani ya Posta nje ya jengo la makao makuu ya kampuni na aliweza kushuhudia watu wengi wakitoka kwenye jengo hilo kwa makundi makundi na alihisi amechelewa.
Alitoa simu yake na kisha akatafuta namba ya mke wake na kupiga , lakini iliita kidogo tu na kisha ikakatwa hapo hapo, alijikuta akitabasamu kwa uchungu na kisha akatafuta namba ya Recho na kupiga.
“Nikusaidie nini Roma?”Sauti kutoka kwa Recho ilisikika upande wa pili.
“Acha kujifanyisha hebu niambie Edna yupo wapi?”
“Recho kata simu , tuna shughuli nyingi za kukamilisha leo”Sauti upande wa pili ya Edna ilisikika.
“Roma kuna wageni wameakuja kwa ajili ya kikao na Directors wote wa kampuni , inabidi uje kwenye ukumbi wa mkutano siti yako ilikuwa wazi tokea asubuhi”Aliongea Recho haraka haraka .
Roma sasa alielewa wapi anatakiwa kwenda , hivyo alitoka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya jengo hilo , wafanyakazi siku hizi walikuwa wakimpa heshima yake kutokana na kujua kwamba alikuwa mume wa bosi na sio hivyo tu alikuwa mtoto wa Raisi.
Dakika chache mbele Roma aliweza kuingia ndani ya ukumbi wa mikutano katika ghorofa ya kumi na nane ya jengo hilo linalomilikiwa na mke wake , ambalo ndio makao makuu ya Vexto.
Ndani ya jengo hili katika chumba cha mikutano kulikuwa na meza ndeefu ambayo imejaa watu waliovalia suti , huku mbele yao kukiwa na maiki , makaratasi pamoja na chupa za maji ya uhai ,ilikuwa ni kama kikao cha raisi na mawaziri wake.Edna alikuwa mwisho kabisa wa meza huku akiwa ametulia na sura iliojaaa usiriasi akidhihirisha nini maana ya kuwa bosi.
Muda huo huo mlango ulifunguliwa na akaingia Roma ambaye alimfanya Edna aliekuwa akiangalia karatasi ziliokuwa kwenye meza yake kumwangalia mpaka alipoenda kukaa kwenye siti yake.
Upande wa Roma hakujali sana sura zilizokuwa zikimwangalia , kwanza alikuwa akijiamini , ni hivyo tu hakuwa akizoea ukauzu wa mke wake.
Edna alikuwa na hasira na Roma kwani usiku wa jana tu mambo yao yaliikuwa mazuri mno na alikuwa na huba nae la kiwango cha juu , lakini asubuhi mara baada ya kwenda kwenye chumba chake na kukuta kitanda kimetandikwa na hakikuwa na dalili ya kulaliwa usiku mzima, alijikuta akitoa matusi ya ndani kwa ndani na kumsuta Roma kwa kumlaani.
Kilichomkasirisha zaidi ni mwanaume huyu kushikiliwa na mchepuko kiasi kwamba amesahau hata kuwahi kazini kwenye kikao muhimu.
Roma mara baada ya kukaa aliweka suti yake vizuri na kujiweka sawa na kuanza kuangalia watu wote waliohudhuria hapo ndani na alishangazwa na uwepo wa wazungu , ukimtoa Richie kuna mmoja ambaye hakumpenda kabisa.
Alikuwa ni mwanaume alievalia suti ya rangi ya bluu kampuni ya Armani na tai nyembamba ambayo ilitoa ‘Vibe’ yenye kuelezea uanaume wake hivyo kuwa wa hadhi ya juu , hakuwa mwingine bali ni Hanson mwanaume ambaye siku kadhaa zilizopita aliweza kukutana nae kwenye kusanyiko la wanadarasa wa Edna , mpaka Roma kumzidi kete kwa kuonyesha uthamani wa Henry Graves.
Hanson mara baada ya kukutanisha macho na Roma aliachia tabasamu la furaha.
“Director Roma hatimae ameweza kufika , nilikuwa nikitaka kusema ni jambo gani la kuhuzunisha nisingeonana na wewe kwa mara nyingine”Aliongea na kufanya wale watu ambao hawakuwa wamemfahamu Roma sasa kumfahamu kwamba ndio Director wa kampuni ya Vexto Media.
“Mr Hanson is here as a representative for BMW’s African Division which Explain his attendance today”
“Mr Hanson yupo hapa kama mwakilishi wa kampuni ya BMW upande wa Afrika , Swala linaloelezea kuhudhuria kwake siku ya leo”Aliongea Edna baada ya kuona Roma anamwangalia kwa wasiwasi.
“Oh! Naona , Lakini kumbukumbu zangu zinaniambia kabisa sijawahi kukutana nae kwenye maisha yangu yote , inashangaza sana yeye kunifahamu”Aliongea Roma na kumfanya Hanson kukunja sura alijua ?Roma anamkejeli.
“Mr Roma utakuwa unatania , lakini hata hivyo sijali kujitambulisha kwako kwa mara nyigine , Mara ya mwisho tulikutana kwenye mkusanyiko wa wahitimu wa chuo cha Oxford wiki kadhaa zilizopita ukiwa na boss Edna”Aliongea .
“Okey Okey nimekumbuka nisamehe bwana Hanson , nimependa mtindo wako wa nywele , kwa maisha yangu nilitamani sana kuwa na nywele ndefu za kizungu lakini inanisikitisha kuzaliwa na nywele fupi kama zangu pamoja na hii sura”Aliongea akimtania Hanson maana tofauti na siku kadhaa walizokutana leo alikuwa amepunguza nywele na zikawa fupi mno.
“Kuna joto sana siku hizi ndio maana ufupi wa nywele ni sahihi kwangu , Oh Yeah , tena Director wewe ni mume wa CEO Edna , mahusiano yenu mazuri yamekuwa ni jambo la kuvutia watu wengi sana lakini hata hivyo President Edna anaaminika kwa kujali umakini likija swala la kazi”Aliongea Hanson na kumtupia dongo Roma kwa kuchelewa kwake hata watu walishangaaa pia inakuwaje Edna anesifika kwa uchapa kazi akawa na mume wa aina hio , hawakujali sana cheo cha kuwa mtoto wa Raisi kwani ni jina tu tofauti na pesa.
Edna baada ya kuona mazungumzo hayo yangeenda vibaya alianzisha kikao palepale baada ya kusafisha koo.
Kikao kiliendelea kwa zaidi ya msaa kadhaa mpaka mchana yote jambo ambalo lilimchosha mno Roma , kwani aliishia kusinzia bila ya kuelewa chochote kinachoendelea , ilikuwa afadhali kwake kwani Tanya aliweza kufika mapema na kuchukua kumbukumbu ya kikao chote.
Baada ya kikao kumalizika ilikuwa ni saa tisa za mchana na Roma baada ya kumuona mke wake anaelekea ofisini alifuata nyuma.
Edna baada ya kuingia ofisini kwake alichukua mfuko mkubwa uliokuwa juu ya meza yake na kuingia kwenye chumba cha mapumziko.
Wakati Roma akiwa anapangilia mistari yake kwa ajili ya kumlegeza , Edna alitoka akiwa kwenye mavazi tofauti na yale ya mwanzo na kumfanya Roma kubung’aa , kwani alikuwa amependeza haswa.
Kiuno chembamba kilichochangamshwa na lishepu lililojipangilia upande wa chini ilimfanya Roma damu kumcheka, Edna alimwangalia Roma kwa jinsi macho yake yalivyokuwa ya kifisi na kutoa kicheko cha chini chini ilionekana hata hasira zake zilikuwa za maigizo tu.
“Vipi nimependeza?”Aliuliza Edna huku akijigeuza geuza mbele ya Roma aliekaa kwenye sofa na Roma alitingisha kichwa mara mbili nakumfanya Edna kukunja sura.
“Ndio unamaanisha nini kwa kutingisha kichwa?”
“Mwanaume Gentlemen akitingisha kichwa mara moja inamaanisha kwamba umependeza sana , lakini akitingisha kichwa mara mbili ni kwamba umependeza zaidi ya neno lenyewe mimi nimetingisha mara mbili”Aliongea Roma na kumfanya Edna kupumua kwa afadhali yote hayo ilikuwa ni kutaka kujua kama gauni lake limempendezesha.
“Usiku wa leo tumealikwa katika hafla ya ugawaji wa Tuzo za sanaa zilizoandaliwa na serikali , kutakuwepo wasanii mbalimbali wakubwa na nimepewa heshima ya kutoa Tuzo kwa moja wapo wa wasanii ndio maana lazima nivae nipendeze kuiwakilisha kampuni yangu ya mitindo, linaonekana kidogo kunibana kwenye kiuno lakini muda wa kutafuta gauni lingine sina hata hivyo ilinitumia muda mrefu kuweza kuchagua hili gauni….”Aliongea lakini palepale alijikuta akiwa hewani kwenye mikono mikakamavu ya Roma akiwa amembeba juu juu.,Roma alimpiga mabusu rasha rasha huku akimzungusha.
“Unafanya nini , utaharibu gauni langu bwana?”
“Darling nadhani unapaswa kutafuta gauni lingine , nina wasiwasi na hao masuperstars watakaokuwepo, wanaweza kukomezea mate. Na mimi nitaona wivu”
“Wewe sibadilishi hivi hivi ndio fasheni , kwanza linaniacha wazi kwenye mabega tu, hili ndio linaendana na Red Carpet”Aliongea na kisha alijitoa kwenye mikono ya Roma.
“Sio mbaya umependeza sana mke wangu , lazima nikusindikize ili watakaojaribu kusema ni warembo kuzidi wewe ninawanyofoa makoromeo yao”
“Yaani , huwezi kuongea vizuri mpaka uweke vitisho”
“Natania mke wangu , Oh.. tena babe vipi hauna hasira na mimi tena si ndio?”Aliuliza na kumfanya Edna atingishe kichwa kukubali.
“Sio jambo jipya hata hivyo na najua utafanya tena na tena , inabidi tu nikuzoee hivyo hivyo , nashindwa kujizuia na kuwa na hasira lakini ni kwa muda mfupi tu , hata hivyo umeweza kumuona Hanson kwenye kikao lakini hujaniuliza chochote hivyo naona unaniamini”
“Wifey mimi nakuamini ila yule mpuuzi akikusumbua nitahakikisha na mnyonga”
“Wewe..”Edna aling’ata meno yake kwa hasira na kugeuka na kumfanya Roma kucheka.
“Wifey ukweli licha ya kwsamba hatujaoana kwa muda mrefu lakini ndoa yetu imepitia mambo mengi ambayo wengine wanaweza kuyazungumzia ,Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa mlima kwa wengine kwetu ni vijimlima vidogo vidogo vya kupanda na kushuka , nimefurahi hatuna ugomvi”
“Usijifanyishe hapo na maneno yako , bado hata sijaanza kukuhoji vozuri , Haya uniambie jana usiku umelala wapi?”Aliuliza lakini Roma alianza kufikiria namna ya kujibu.
“Arrgh .. Edna unaharibu viatu vyangu bwana?”Roma alilalamika mara baada ya kukanyagwa na kiatu cha kisigino kwenye viatu vyake vyeusi.
“Kwahio viatu vyako vinathamanni kuliko miguu ?”
“Ulifikiria ukinikanyaga hivyo nitahisi maumivu?”Aliongea
“Subiri uone”Aliongea na kukanyaga kwa nguvu mpaka alipohakikisha ameridhika .
“Inakutosha hio kwa leo ukirudia nitakupa adhabu kali mpaka ukome kutoroka usiku”Aliongea na kisha akaondoka na kurudi kwenye chumba cha kubadili.
*********
Naam ilikuwa ni usiku wa tukio lililopewa jina la Tuzo ya Taifa , Saa moja na nusu ndio muda ambayo Roma na Edna waliweza kufika ndani ya eneo la Mlimani City kwa ajili ya kutii mwaliko wa tuzo hizo.
Roma alikuwa amependeza na suti yake ya Brown Luis Vuiton akiwa na mke wake mrembo pembeni tajiri Edna Adebayo, Kamera ziliwamulika wakati wa kupita kwenye Red Carpet na Edna hakuacha kutabasamu.
Edna alikuwa ameanza kubadilika kidogo katika msimamo wake .zamani alikuwa akigopa sana umaarufu ndio maana hata licha ya kuwa tajiri surayake haikuonekana sana mitandaoni na sio watu wengi waliokuwa wakimjua , hata akaunti kwenye mitandao ya kijamii hana.
Watu waliokuwa wakifika walikuwa wengi , lakini pia siku hio ilikuwa ikiangaziwa na wasanii wengi mno kutokana na uwepo pia wa msanii wa kimataiafa kutoka Ireland.
Baada tu ya Edna na Roma kupita kwenye Red Carpet, Roma aliweza kumuona Recho akiwa ndani ya ukumbi akiongea na mwanamke mmoja mrembo wa Kizungu , lakini hata hivyo hawakumsogelea moja kwa moja kwani walisogelewa na watu mbalimbali na kusalimiana nao , wakiwemo wasanii wakubwa ambao pia walijipendekeza kwa Edna na Roma ili kuweza kupata ufadhili wa nyimbo zao , lakini pia kupewa ‘Airtime’ kwenye Chaneli Tv ya Vexto.
Baada ya kusalimiana na watu kadhaa wakiwemo wafanyabiashara , Recho alimsogelea Edna akiwa na yule mzungu.
“Madam , huyu ni mtoto wa kike wa msanii maarufu kutoka Ireland Marehemu Ms Doleres aliekuwa katika kundi la Cranberries , She and other artist are currentlly on their world tour stop in Tanzania , She insistend an Audience with you” Aliongea Recho , alikuwa vizuri mno kwenye lugha ya kingereza huenda nio credit iliomfanya kuwa Sekretari wa Edna.
Kabla Edna hajatoa jibu kuna mwanamke mrembo mmoja aliekuja kwa namna ya kupaniki na kuwasogelea.
“Oh My God! Nessa!”Aliongea kwa mshituko lakini alijiuzuia.
“Sorry! Let me introduce my self , I’m Dina and it’s pleasure to meet with you”Aliongea kwa kujitambulisha kwa jina la Dina.
Dina ni moja ya wasanii maarufu ndani ya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla , ni moja ya wasanii wa kike wa Tanzania wanaosifika kwa kuwa na sauti nzuri , mwenyewe anajiita kwa jina la Malkia wa Afrika.
Ni kawaida sana kwa msanii kama Dina kushangazwa na uwepo wa Nessa msanii maarufu kutoka Ireland ambaye pia alikubalika sana ndani ya taifa lake kwa kumrithi mama yake marehemu Ms Doleres ambaye alikuwa chini ya Band Maarufu sana enzi za miaka ya tisini ifahamikayo kwa jina la Cranberries.
“Nice to meet you , it’s my first visit to Tanzania so do forgive me , I aren’t so familiar with a lot of peaple here”Aliongea Nessa akimaanisha kwamba ni mara yake ya kwanza kutembelea Tanzania , hivyo hafahamu watu wengi, kauli ile ilimnyong’onyesha kidogo Dina.
Edna ilibidi achukue jukumu la kumtambbulisha Dina kwa Nessa , Edna ijapokuwa hakuwa mpenzi sana wa mziki wa Rock , lakini Ms Doleres aliweza kumfahamu sana hususani na tukio la msanii huo kukutwa amejizamisha kwenye maji ya Swimming Pool ndani ya Hoteli usiku kwa kile kilichodaiwa ni Depression(Sonono)
Upande wa Roma alikunja sura kiasi , alikuwa akimjua vizuri Ms Doleres , lakini mtoto wake kuja Tanzania na kutaka kuongea na mke wake kulimfanya kidogo kuhisi huenda kuna zaidi ya hilo. .
Baada ya watu kutulia hatimae ugawaji wa tuzo uliozaminiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Vexto ulianza rasmi..
“Nilikuona ukiwa huna furaha wakati wa kusalimiana na Nessa , nini tatizo?”Aliuliza Edna mara baada ya kukaa.
“Hakuna tatizo , ni kwamba tu nina mashaka?”
“Mh! Mashaka gani tena?”
“Siwezi kusema , ila kama ningetaja jina la baba yake huenda angeondoka mara moja hapa nchini”Aliongea Roma
“Baba yake!, unamaanisha nini , kwanini aogope kutajwa jina la baba yake?”
“Babe kuna mambo ambayo hayapaswi kabisa kuzungumziwa na yabakie kua siri , Kuna vitu viovu sana vinafanyika ambavyo vina haribu Dunia”Aliongea na Edna alivuta mdomo.
“Unajifanyisha mjuaji , Haya baba endelea kubakia na siri zako”Aliongea Edna na muda huo ukumbi ulibakia kimya na hio ni mara baada ya Nessa kupewa nafasi ya kutumbuiza siku hio kama mgeni wa Heshima.
Ijapokuwa alikuwa na vibao vyake maarufu vinavyotamba duniani , lakini usiku huo alitaka kuimba wimbo wa Dreams ulioimbwa na Band aliokuwepo mama yake ya Cranberries, haikueleweka kwanini alichagua wimbo huo , lakini inasemekeana kila nchi aliopita alikuwa akiimba huo wimbo huenda ilikuwa ni kumuenzi mama yake.
Nessa ijapokuwa hakuwa akimfikia mama yake katika uimbaji , lakini alikuwa na sauti nzuri mno , kwanzia mwanzo wa wimbo huo wa kistaarabu mpaka mwisho aliweza kuteka hisia za watu na sauti yake , lakini kubwa zaidi aliimba kwa hisia mno,Ile anamaliza kila mmoja alisimama na kupiga makofi ya kumshangilia.
“Ana sauti nzuri sana?”Aliongea Edna.
“Hawezi kumzidi Sophia”Alijibu Roma
“Unaongea kama vile ni ndugu yako , kama kweli unaamini Sophia anafanya vizuri kwanini unashindwa hata kutumia muda wako kuwasiliana nae”
“Ah! Ni ndugu yangu ndio kupitia wewe , halafu Daudi alinipa habari kwamba angerudi hivi karibuni Tanzania”
“Atarudi kuzindua albamu yake ya kwanza, yupo Nigeria kwa ajili ya Shooting , sasa hivi hayupo huru kama mwanzo kwani ashakuwa superstar”Aliongea
Baada ya ratiba za mwanzo kumalizika hatimae Ugawaji wa tuzo ulianza mara moja na Edna aliweza kumpatia Tuzo msanii bora wa kike wa mwaka, tunzo ambayo ilienda kwa Dina Queen of Africa..
Baada ya taratibu za tuzo kuisha hatimae Dina ndio aliepewa nafasi ya kutumbuiza kwa ajili ya kufunga tukio hilo , ikiwa imetimu saa sita kwenda saba usiku kutokana na mlolongo wa ratiba yenyewe.
Neema Luwazo pia alikuwepo kwenye mashindano hayo , akiwa amepatiwa pia nafasi ya kumpatia Tunzo msanii chipukizi wa kiume wa mwaka.
Ni muda ambao watu walianza kutawanyika Edna na Nessa walikuwa na maongezi ambayo Nessa alitaka yafanyike usiku huo huo kwani hatochukua muda mrefu.
Sasa mazungumzo hayo yalitakiwa yafanyikie kwenye moja wapo ya mgahawa uliokuwepo eneo hilo hilo la Mlimani , mgahawa ambao mpaka muda huo ulikuwa wazi , Edna ndio aliekuwa wa kwanza kufika ndani ya mgahawa huo akiwa ametangulizana na Roma.
Na kazi ya Nessa kuletwa hapo kwenye mgahawa alipewa Recho,kutoka ulipo ukumbi na huu mgahawa ni umbali mfupi sana kiasi kwamba watu waliokuwa wakitoka kwenye ukumbi wanaonekana.
“Bosi , Bosi….!!”Recho alikuja mbio mbio huku akihema na kumfanya Edna amwangalie Recho kwa namna ya mshangao.
“Kuna nini mbona uko hivyo na mgeni yupo wapi?”
“Kuna mtu kafa…”Aliongea huku akishika moyo wake , akishindwa kupumua vizuri , kauli ile ilimfanya Roma kumwangalia Recho kwa maswali.
“Unamaanisha nini , hebu punguza presha na utueleze nini kinaendelea”
“Dinaaa… Dina kafariki Madam..:”Aliongea huku machozi yakianza kumtoka , muda huo huo kelele za watu kutoka ukumbini zilisikika na kuwafanya Roma na Edna kuchukuana kurudi kwenye ukumbi.
Lakni ni ndani ya muda mchache sana polisi na wenyewe waliweza kufika.
Kwa maelezo ya Recho ni kwamba wakati anarudi kwa ajili ya kumchukua Nessa , alimkuta akiongea na baadhi ya wasanii hivyo alisubiri , lakini haja ndogo ilionekana kumbana sana , hivyo alitumia muda huo kuingia vyoo vya wanawake kwa ajili ya kujisaidia, lakini kitendo tu cha kufungua mlango wa choo kimoja wapo ndipo alipotahamaki kumuona msanii marufu anaefahamika kwa jina la Dina akiwa chini kwenye dimbwi la damu chini ya sink la choo cha kukalia.
Ni tukio la kutisha kutokea katika siku kama hio m ukizingatia kwamba mtu aliepatwa na kifo hicho ni msanii maarufu sana Tanzania.

SEHEMU YA 450.
Dina ni moja ya wasanii wenye umri mkubwa ndani ya taifa la Tanzania , lakini licha ya kuwa na miaka mingi uzuri wake ulikuwa ukifubaa kwa kiwango kidogo mno mpaka muda mwingine mashabiki wake kuhoji mwanamke huyo alikuwa akitumia chakula gani mpaka kuzidi kudumisha uzuri wake na kuonekana kijana zaidi.
Licha ya hivyo alikuwa akipendwa sana na watu kutokana na staili yake ya uimbaji , ashawahi kufanya Kolabo na wasanii wakubwa wa Nigeria akiwemo Tems, Davido na Burna Boy.
Kifo chake cha ghafla hivyo mara baada tu ya kutumbuiza kwa kufunga tukio la usiku wa Tuzo za Taifa , kiliibua maswali na joto kali.
Polisi waliweza kufika haraka haraka na kuweza kupima nini kimeweza kutokea , kwa maelezo ya awali Polisi wameweza kuelezea kwamba sababu ya kifo ni Dina kukatwa na kisu eneo la shingoni kwenye mshipa mkubwa wa kupeleka damu kwenye ubongo , hivyo kumsababishia kupoteza damu nyingi.
Roma aliekuwa karibu na eneo la tukio alijikuta akiguna, aliweza kupiga mahesabu kuanzia muda ambao waliweza kumuacha Dina akiimba stejini mpaka kumaliza ,lakini muda ambayo ameweza kwenda maliwatoni na kukutwa na tukio hilo , aliona kuna vitu haviingiii akilini kwa mlinganisho wa muda.
Polisi walitoa mwili wa Msaniii na Afande Mage aliweza kutangazia pia waandishi kuthibittisha kifo hicho na kuahidi uchunguzi ungefanyika kwa weledi mkubwa ili kubaini nani kahusika na kifo cha Dina ili sheria ichukue mkondo wake.
Wanahabari waliweza kunakiri habari hio kwa munkari ya hali ya juu mnohuku picha nyingi zikipigwa.
“Shuhuda wa kwanza kuona mwili wa Dina alikuwa ni Recho , hivyo alitakiwa kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo , Recho alionekana kuwa na wasiwasi mno , lakini Edna alimtoa hofu kwamba kila kitu kitakuwa sawa aende tu na isitoshe Mage ndio anaeongoza kesi hio.
Wageni waliondoka kwa mshituko mkubwa, huku habari zikisambaa mtandaoni kwa moto wa kifuu , hakuna ambaye ameweza kuamini kama Dina kweli ameweza kufariki mara tu baada ya kumaliza kuimba, ilikuwa ni habari ya kushangaza lakini ya kusikitisha kwa wakati mmoja.
“Edna nitahakikisha Recho anahojiwa ndani ya muda mfupi na kurudi nyumbani mapema”Aliongea Mage.
“Sawa Mage, Recho anaonekana kwenye mshituko mkubwa ni kheri kama hatolala kituoni”
“Usijali baada ya kuchukua maelezo yake na kuruhusiwa nitakutaarifu”AliongeaMage na kumwangalia Roma kwa dakika na kisha aliondoka eneo hilo kwa kupanda Difenda.
Edna alijikuta akivuta pumzi , hata hamu ya kubakia eneo hilo imemwishia, Roma aliona hali aliokuwa nayo mke wake hivyo alimchukua na kumuondoa kwenye eneo hilo na kuanza safari ya kurudi nyumbani.
Dakika chache tu mara baada ya kuingia ndani , simu ya Edna ilianza kuita mfululizo na baada ya kuona jina ni la Mage alipokea haraka haraka.
“Edna nimeona nikupe taarifa usiku huu”
“Nini kimetokea?”
“Tumeweza kupata kisu eneo la tukio ambacho kimeweza kumkata Dina eneo la shingoni na kukuta alama za vidole na tulivyojaribu kuziingiza kwenye mfumo imeonekana ni za Recho”Aliongea na kumfanya Edna kutoa macho.
“Unamaanisha Recho ndio amehusika kumkata Dina na kisu?”
“Inaonekana hivyo , pia hata mkanda wa CCTV zinaoneyesha baada ya Dina kingia chumba cha maliwatoni na Recho pia aliingia na hakuna mtu mwingine alieingia tunashindwa kuthibitisha muhusika kwani hakuna Camera ndani ya vyoo”Aliongea Mage na kumfanya Edna kujikongoja na kukaa kwenye sofa.
Roma alichukua simu haraka haraka kutoka kwenye mikono ya Edna na kuongea na Mage.
“Mage ninaweza kuona mwili wa Marehemu?”
“Ndio , umehifadhiwa hospitali ya Lugalo , ninaweza kuongea na baba na ukapita kuuona ndio naelekea huko sasa hivi”Aliongea na Roma alikata simu mara moja.
“Edna usiwe na wasiwasi naamini Recho hawezi kuhusika katika hili , mpigie simu mwanasheria ili aweze kumuwekea Recho Zamana wakati uchunguzi ukiendelea”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa.
Ilikuwa usiku lakini Roma alijiambia lazima afanye uchunguzi muda huo huo , hata hivyo tokea mwanzo kulikuwa na kitu kinamtekenya mara baada ya kumuona Nessa mtoto wa marehemu Dolores kutoka Ireland.
Dakika chache tu zilimtosha kuweza kufika Lugalo na kukutana na Mage , ambaye alimuongoza moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Forensic, sehemu mwili ulipohifadhiwa kwa muda kabla ya kuingizwa Mochwari.
Roma baada ya kuingia kwenye chumba hicho chenye ubaridi kiasi , aliweza kushuhudia mwili wa Dina ukiwa umelezwa juu ya meza kubwa ya bati ukiwa umefunikwa na shuka nyeupe kwa juu.
Mage alijikuta akiwa na wasiwasi mno na kujiambia kweli mtu akishakufa ndio basi tena , ni ngumu kuamini msanii aliekuwa akipendwa na watu wengi ndani ya Tanzania ndio huyo alielazwa peke yake kwenye chumba cha baridi.
Roma aliweza kuufunua mwili wote na kutoa shuka ambalo limemfunika , huku Mage akisogea taratibu kwa wasiwasi , ijapokuwa alikuwa Polisi lakini kukagua maiti haikuwa fani yake, kwani madaktari wa kipolisi walibobea kwenye upande wa ‘Forensic investigation’ ndio waliokuwa wakihusika na uchunguzi.
“Kwa uchunguzi wa mwanzo uliofanywa na madaktari wamesema kifo chake kimesababishwa na kupoteza damu baada ya kukatwa kwa nguvu eneo la Shingoni kwenye mshipa mkubwa wa damu , vipi unaamini kuna uwezekano wa sababu nyingine ambayo imesababisha kifo chake?”Aliuliza Mage kwa sauti ya chini.
“Hapana , kilichomuua ni kweli ni kukatwa na kisu , lakini naamini kuna uwezekano wa sababu nyingine pia”Aliongea Roma huku akisogea upande wa miguuni na kuanza kugusa mwili huo kwa namna ya kupapasa.
“Kwani lazima umguse hivyo , huwezi kuangalia tu”Aliongea Mage huku akivuta pumzi nyingi na kumfanya Roma kucheka .
“Mage hata kama nina genye kiasi gani siwezi kufanya maiti , ninachofanya hapa ni kuangalia kama kuna kidonda kingine tofauti na cha shingoni”Aliongea Roma.
“Kidonda kingine?, Kwanini kiwe kwenye maeneo kama hayo?”
“Swali zuri , kwasababu hakuna mtu ambaye anaweza kutegemea kidonda kuwepo kwenye hili eneo, Nilitaka kwanza wataalamu wafanye kazi yao na mimi nifanye kazi yangu kutokana na eneo nililotaka kuchunguza kuwa ‘sensitive’,mtu angeweza kuona labda naidhalilisha maiti”Aliongea Roma huku akichanua miguu ya Maiti na kusogeza macho karibu zaidi , maiti yote ilikuwa imevuliwa nguo hivyo ilikuwa kwake rahisi kuchunguza.
Mage bado alikuwa na wasiwasi na alichokuwa akifanya Roma , lakini aliamua kutulia kuendelea kuangalia mwisho wake.
Roma baada ya kuchanua miguu na kuangalia katikati karibu kabisa na sehemu za siri, alimpa ishara Mage kusogea na kuangalia na Mage alijikuta akiziba mdomo kwa mshituko.
Kulikuwa na matundu mawili ambayo yalionyesha kutoa damu ya wastani, yalikuwa madogo kiasi kwamba ilikua ngumu kwa mtu kuyaona hususani kwenye eneo lenyewe.
“Haya ni…”Afande Mage alionekana kukosa neno
“Wew unaonaje?”Aliuliza Roma
“Inaonekana kama ameng’atwa na nyoka , lakini haya matundu ni makubwa kidogo hivyo ni ngumu kusema ni nyoka..”Aliongea Mage kwa mshituko.
“Acha ujinga haya ni meno ya Vampire , Wanajiita wenyewe kwa jina la kingereza Blood Race”
“Unasema..!!”Mage ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia kuhusu Vampires na Roma aliongea hivyo kwa kumdhania Mage ni Magdalena , kwani kuna siku moja Roma alimpatia Magdalena maelezo ya kutosha.
“Naona upo kwenye mshituko na unaweza usiamini ninachokuambia , ila nishawahi kukutana na Vampire miaka kadhaa iliopita”Aliongea lakini Mage alishindwa kuamini , alishawahi kusikia kuhusu Vampiea hata kuona muvi za aina hio , lakini haikuwahi kumuingia akilini kwamba hadhithi hizo ni za kweli.
“Kama kweli unasema ni Vampire kwanini wameng’ata eneo la huko na sio shingoni?”
“Vampire kunyonya damu eneo la shingoni ni uzushi mkubwa sana ambao walieneza wao wenyewe kupitia hadithi na baadhi ya Muvi hio yote ni kuficha namna wanavyoweza kumfyonza binadamu ili wasigundulike uhusika wao na tabia zao, Wenyewe wanaamini damu inatofautiana utamu kutokana na eneo katika mwili , Eneo la shingoni wanapenda pia lakini ni sehemu ambayo ipo wazi sana nadhani hata wewe umeona madaktari hapa wamethibitisha Dina amekufa kwa kukatwa na kisu wakati sababu ni nyingine kabisa , hii ndio mbinu yao”Aliongea. Roma na kuendelea.
“Mishipa yote ya damu maeneo ya mapajani mpaka sehemu za siri ndio sehemu wanazopenda sana , damu inayotoka hapo ni tamu sana , pili ni yenye kujitosheleza, lakini kingine kinachowafanya kupenda ni harufu ya Homoni za kike katika eneo hilo”Aliongea
“Aaah… inatia kinyaa”Aliongea Mage na Roma aliuweka mwili vizuri na kuufunika vna kisha alimwambia Mage waondoke hapo akaanze msako wa kutafuta Vampire halisi ambalo limehusika na kifo cha msannii Dina.
Unafikiri nani kahusika na ni raia gani ambaye ni Vampire
END OF SEASON 15 ,
SEE YOU 0687151346 watsapp nicheki by SINGANOJR - SPONSORED BY MIND LINK ENETERTAINMENT
 
Shusha Nondo nasema shusha vitu mkuu Hades SinganoJr,aka Roma Roman. Tunakufuatilia...hii weekend isipite hivihivi mambo yanazidi kuwa bambam.
 
Huu mji wq Iznik wa Uturuku niliona kwenye filamu ya The OTHOMAN Azam tv Kama sehemu mojawapo ambayo OTHMAN anapataka
 
Back
Top Bottom