SEHEMU YA 436
Roma hakutaka kumzuia Yan Buwen kabisa kutokuua familia yake , kwanza ni mambo ambayo hayakuwa yakimhusu na pili familia hio ndio iliomwingiza katika mambo ya kutengeneza siraha za maangamizi ili tu kuweza kushindana na Hongmeng.
Lakini hata hivyo swala la kuua familia yake mwenyewe lilimfanya Roma kuuona Yan Buwenn kiumbe cha hatari sana ambacho kwa namna yoyote ile alitakiwa kumwangamiza hapo hapo kwani kitendo alichokifanya hakuweza kufikiria hata siku moja mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya..
“Nakubali umekuwa chizi kuliko nilivyofikiria , lakini kabla hatujaanza mapambano yetu niambie kwanini ukaamua kuwa adui yangu , maana hakuna siku yoyote ambayo nilishawahi kukuchokoza”Aliuongea Roma
“Haijalishi chochote kwasasa”Alijibu .
“Kweli! Unaweza usiamini lakini swali langu ndio sababu ambayo imenifanya muda wote nisikuchukulie hatua licha ya kunichokoza mara kibao, nadhani unakitaka kifo sasa”
“Hahaha,.. unafikiri unweza kunishinda mimi?”Aliuliza Yan Biuwen lakini Roma hakumjibu , ukweli alichokitaka ni kujua kwanini ghafla tu Yan Buwen akaanza kumuwinda yeye kwani hakuwa na ugomvi nae.
“Nadhani hata hivyo napaswa kukujibu , mwanzoni sikuwa na haja na wewe kabisa , lakini nilikuja kugundua unamiliki kitu cha thamanni ambacho hakikuwa cha kwako , hata hatua yangu ya kufika Tanzania ilikuwa ni kukipata , unaweza ukashangaa labda kwanini nikakaa Tazania kwa ajili ya tafiti zangu lakini ukweli kabla ya kuja Tanzania nilikuwa na makazi mengine bora zaidi kuliko maabara ile ya kipuuzi kule Tanzania , lakini hata hivyo mimi Yan Buen nimekuwa wa kupata kila ninachokitaka katika dunia hii..”Aliongea
“Ulikuwa ukitaka nini kutoka kwangu?, mpaka sasa kama unahitaji Jiwe la kimungu halipo kwenye umiliki wangu, nini unachokitaka kutoka kwangu”
“Huna haja ya kufahamu , lakini kaa ukikumbuka hivi , kifo chako pekee ndicho kitathibitisha kwamba mimi ndio mmiliki pekee wa dunia , I am strongest man in the world”
“Sijawahi kujitangaza mimi kama ni mmoja wapo ya watu wenye nguvu ndani ya dunia hii”Alijibu Roma.
“Lakini kuna watu wanaamini una nguvu kuzidi mtu yoyote ndani ya dunia hii na ndio maana nitaichukua nafasi yako kwa kukuua”Aliongea Yan Buwen.
“Nani anaamini hivyo?”
“Unaongea sana Hades, haijalishi tena kukuambia kwani mpaka sasa wewe ni mfu”Aliongea na palepale nguvu isioelezeka ilianza kumzingira kiasi cha kutengeneza mwanga flani wa rangi ya Cyan lakini ambao haujakolea sana lakini angavu mno kiasi kwamba ulifanya mazingira kuwa na mwanga , Cyan ni mwanga ambao unazalishwa kati ya rangi ya bluu na kijani katika mwimbi ya wevu 490nm kwenda 520nm , inasemekana kwenye anga la sayari ya Uranus ndio imekithiri.
Sasa mwanga ule ulikuwa ukimzunguka huku ukitengeneza kama wingu flani hivi la rangi hio kuanzia chini kwenye miguu mpaka kichwani huku ukiambatana na upepo mkali, kadri nguvu ilivyokuwa ikizunguka ndio anga lote lilivyoanza kucheza cheza kwa kupinda.
Roma alishangazwa kwani ilikuwa ni nguvu sawa kama ya Clone alilopambana nalo siku chache zilizopita lakini awamu hii nguvu hii ilikuwa kubwa mno.
“I am sue you have come into contact with my creations , So please enjoy it while it last”
“Naamini ushakutana na kiumbe changu , hivyo furahia uwezo wangu kadiri unavyodumu”Aliongea kwa kujigamba huku akicheka kama chizi na kusogelea Roma kwa spidi ya mwanga akilenga eneo la moyo wa Roma.
Roma alishajua alichokifanya Yan Buwen ni kutengeneza mbinu ya kucheza na kanuni za anga kwa kutengeneza uzio nyuzi nyuzi sambamba(disorderly Paraller space fabric) ili kwamba hata kama Roma angekuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga kushambulia basi ashindwe.
Hata hivyo aliamini huenda Yan Buwen alimtegemea angeweza kutumia kanuni za anga kushambulia , lakini yeye alitumia mbinu za kijini.
Roma palepale aliita nguvu ya kijini ya kimaandiko na ilitengeneza ngao flani kama kioo na ni muda huo huo Yan Buwen aliweza kumfikia hivyo mgongano wa ngao na nguvu ya Yan Buwen ulitengeneza mtetembo kama wa bomu huku cheche kama za radi zikisambaa eneo lote kutoka kwenye ile ngao ya Roma aliotengeneza.
Mtikisiko ule ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ulisambabisha hata jengo la nyumba hio na ukuta wake kuporomoka chini , lilikuwa ni jambo ambalo lilimshangaza Roma kwani Yan Buwen alikuwa na uwezo mkubwa sana kiasi kwamba ilimshangaza na kujiuliza imekuwaje Yan Buwen kuwa na uwezo mkubwa kiasi hicho kwani mara ya mwisho alionekana kuwa wa kawaida tu.
Yan Buwen mara baada ya kuona pigo lake la kwanza halijafanikiwa alipiga tena kwa mara mbili mfululizo , lakini ngao ya Roma iliuonekana kuwa ngumu , lakini hata hivyo alivyopiga mara ya tatu ilitengeneza uwazi hivyo hakutaka kuchelewasha kwani palepale alilenga ngumi iliojaa mwanga kama wa jiwe la kimungu na kuipitisha kwenye uwazi.
!POW!
Baada ya ngumi ile kumpata vyema Roma kwenye kifua alirushwa kwenda juu kama vile ni mpira huku akizunguka zunguka kwenye hewa na baada ya kufika mwisho alirudi chini kwa spidi lakini palepale alitumia uwezo wake wa kijini kupunguza spidi ya namna anavyoshuka , lakini kabla hajakanyaga Ardhi , Yan Buwen alileta teke lenye nguvu isiokuwa ya kawaida na kwakua alitumia spidi kubwa Roma alizubaa na kushindwa kukwepa.
“Arrgh…”Roma alitoa ukulele mara baada ya kupokea bonge la teke na kwenda kutua kwenye mlima wa mawe yaliorundikwa sehemu moja mara baada ya nyumba ile kubomoka.
Yan Buwen mara baada ya kuona amefanikisha kumpiga mapigo mawiali Roma na kumpeleka chini alipaa juu angani akimwangalia kwa chini.
“Hahaha… naona kupokea kipigo ndio unachoweza pekee , vipi umekuwa mdhaifu kwa kapigo kadogo kutoka kwangu”Aliongea kwa kimandarini akimwangalia Roma aliekuwa akiugulia maumivu chini ya rundo la mawe.
Lakini Roma alivyotaka kusimama vizuri Yan Buwen alimsogelea kutoka juu kama mshale , lakini kabla hajamfikia liliamika jiwe kubwa pembeni na kumlenga Roma.
PUUH!,
Jiwe lilimpiga kisawa sawa Roma na kumfanya kutema damu huku akipiga magoti kwa maumivu.
Alijikuta akipeleka mkono mdomoni na kujifuta huku macho yake yakiwa mekundu kama yanaanza kutoa damu.
Roma alitaitiwa mapema sana tofauti na alivyokuwa akipambana na Poseidon,nguvu aliokuwa nayo Yan Buwen haikuwa ya kitoto.
“Haha.. Etia anaitwa Pluto upuuzi mtupu , wewe ni kichekesho , kwangu nakuona kama kunguni tu ambaye nakuua na vidole , hustahili hata kuwa mshindani wangu pumbavu”Aliongea Yan Buwen na Roma alijitahidi kusimama vizuri baada ya maumivu kupungua.
“Here is my advice for you , I’m reissuing my clone offer , Be my slave and I might let you live”
“Huu ndio ushauri wangu , ninakupatia tena ofa kama nilivyotoa maagizo mwanzo kwa clone langu , kuwa mtumwa wangu na ninaweza kukuacha hai”Aliongea Yan Buwen
“Halafu tena kabla sijasahau , unao warembo wengi , nafikiri pia wanaweza kuwa msaada kwangu nina kwani nina Clones nyingi na zina nyege hatari , itakuwa jambo zuri kama warembo wako watatoa huduma kwao wote , nataka wewe mwenyewe uangalie namna Clones zangu zinavyofanya mapenzi na mademu zako hahahah..”
Kauli yake ni kama ilimfanya Roma aliekuwa amesimama kivulini kurudiwa na nguvu zake zote , kwani hasira zilimpanda kiasi kwmaba zilisambaza nguvu isiokuwa ya kawaida ndani ya eneo lote.
“Unaonekana bado una vinguvu vya kuweza kupambana , ngoja tuone ulichonacho kwa sasa”Aliongea Yan Buwen mara baada ya kuhisi nguvu isiokuwa ya kawaida.
Sasa ukumbuke Roma wakati alivyokuwa akipigana macho yake yalikuwa kawaida kabisa licha ya kwamba yalikuw mekundu , lakini awamu hii Yan Buwen alivyotaja warembo wake na kusikia kuna kopi nyingi zinazofanana nae ,viini vya macho vilibadilika rangi kutoka weusi na kuwa nyekundu na miale kama ya laser.
Yan Buwen mara baada ya kushuhudia Roma kabadilika macho alijikuta ile hali ya kuamini angeweza kushinda pambano ilimpotea mara moja
Roma sasa alikuwa kama nusu shetani kwanza ,alitoa ulimi na kulamba damu zilizokuwa zikimtoka kwenye midomo yake.
“Niliamua kutokuwa siriasi na wewe , kwasababu nilikuwa nikihofia kulikorofisha anga lakini sasa hivi sina haja ya kucheza mchezo wa kitoto na wewe , nitakuonyesha nini maana ya kupigwa na radi harafu na kupona”
“Haha unaongea sana , kuna mtu unajaribu kumsubiria…”Aliongea lakini kabla ya kumaliza sentensi yake palepale aliposimama ni kama alikuwa akivutwa na nguvu isiokuwa ya kawaida kiasi kwamba alikuwa akikosa balansi ya kuendelea kudumu kwenye anga lakini wakati huo huo akihisi mkandamizo ambao sio wa kawaida kabisa , huku Roma akiwa amesimama akimwangalia kwa macho ya hasira.
“Hii ni…”Alijikuta akitoa macho mara baada ya kugundua nguvu ni kama zinapotea mwili wake na kumwangalia Roma kwa mshangao.
Uwezo wa Roma ulikuwa umeongezeka zaidi ya mara ishirini kuliko alivyokuwa akipambana mwanzo , alikuwa ni kama mtu mwingine kabisa.
Wingu lilianza kuzunguka juu kama vile mvua inataka kunyesha na nyota zilizokuwa zikionekana zilibwa na wingu.
BOOM, BOOM, BOOM
Ngurumo kali ilipiga ikiambatana na radi lakini ambayo haikufika chini huku mawingu yakizidi kusuguana na kusababisha umeme.
Roma aliangalia juu angani mara baada ya ngutumo na kuona ahueni na kisha alipiga hatua moja mbele , lakini kilichomkuta Yan Buwen ni kwamba aliporomoka chini huku akianza kukosa hewa, alikuwa ni kama yupo kwenye chumba chenye moshi mwingi.
“Kwanini umekuwa kimya ghafla , nia yako ya kuniua na kuwachukua wanawake wangu ipo wapi , hii ndio nafasi yako ya mwisho ichukue”Aliongea kwa sauti ndogo lakini ni kama ilikuwa ikitoka juu angani kwani ilikuwa kama mwangwi.
Yan Buwen alijitahidi kushindana na nguvu iliokuwa ikizunzuia kutofanya chochote lakini alishindwa.
Upande wa Roma mwenyewe alihisi mabadiliko yasiokuwa ya kawaida ambayo hakuweza kuyatarajia , siku zote alikuwa akiita nguvu za kijini akitaka kupambana lakini sasa hivi sio kama alikuwa akiziita lakini yeye ni kama ndio nguvu zenyewe za kijini na zilikuwa zikiamua kipi cha kufanya.
“Uli ., ulificha uwezo wako kumbe?”Aliongea Yan Buwen kwa shida sana.
“Unatakiwa kujichukulia wa juu kwani siku zote situmiagi uwezo wangu kwa watu wa kawaida ,, ninaweza kukuua bila ya wewe mwenyewe kujua kama umekufa , nina miaka elfu moja sijawahi kuamshwa na kuwa na nguvu kiasi hichi ndani ya uso huu wa dunia”Iliskika sauti ambayo haika sio ya Roma bali ni kama ya kijini inayomtawala ndio inayoongea.
“Acha kujihisi una uwezo mkubwa sijashindwa bado”Aliongea Yan Buwen na palepale alijikakamua kwa uwezo wake wote na kuchomoka kwenye nguvu iliokuwa ikimzuia chini kutopaa na alifika juu hewani na kumfuata Roma kwa namna ya kurusha shambulizi , lakini Roma alitoa tabasamu la kifedhuli nakukunja kiganja na kisha akakifumbua na kurusha kibao juu angani.
BANG!
Yan Buwen alirudishwa kutoka juu kwa spidi isio kuwa ya kawaida na alishindwa kujiongoza na kwenda kuyavamia mawe ya ukuta kiasi kwamba sehemu aliodondoka ilitoa vumbi zito.
“Inaonekana unaweza kufa kwa pigo moja tu”Aliongea Roma lakini nguvu ilianza kujikusanya tena kwenye mwili wa Yan Buwen kwa kupepesa macho tu.
“Inaonekana kwangu nguvu zako ni za aina yake lakini sio kama za kwangu , ninaweza kuzifyonza zote na kuzitoa kwenye mwili wako nakushauri utii amri kama sijakuua kwa zaidi ya mara kumi”Aliongea Roma vile vile huku sauti ikiwa sio kama ya kwake kwani ilikuwa nzito na ya kuogofya mno.
Yan Buwen alijikusanya kwenye vumbi kwani nguvu zake zilikuwa zimemtoka nyingi na huenda angekuwa mfu kwa wakati huo
“Siwezi kukubali kushindwa…”Aliongea kwa hasira na kuamka kama mwanga wa radi.
BOOM!
Ni vipande vipande vya nyama vilivyosambaa angani , ilionekana Roma alimtegemea ndio maana akamtanguliza na shambulio kama la bomu ambalo lilimsabaratisha
Lakini licha ya kusambararika ilionekana nguvu isiokuwa ya kawaida ikikisanya vile vipande vipande vya nyama pamoja na damu yake kwenda sehemu moja pasipo ya kudondoka chini, lakini Roma hakuteka kuruhusu tukio hilo , alirusha tena pigo lingine na kusambaratisha tena, lakini ajabu tena vipande vilikusanyikka kwa spidi kubwa sana ni kitendo cha kupepesa macho tu Yan Buwen alirudi tena kwenye uhai wake na kumfanya Roma kutoa macho.
Lakini kabla hajaamua cha kufanya ni nini , palepale mwili wa Yan Buwen ulibadilika na kufunikwa na suti flani hivi ya aina yake na kumziba mpaka kichwa , ilionekana ilikuwa ni kama ngao
Roma alishangazwa na vazi la Yan Buwen kwani ni kama vile alikuwa akiangalia muvi ya Avenger end game.
“You can’t kill me , I have this..”Aliongea Yan Buwen akiwa amefunikwa kichwa chake kama vile ni Spiderman huku mkononi mwake kukionekana kitu kama kitenesi kikitoa mwanga mkali sana wa mng’ao
“The Godstone,! This whole time it was you?”Aliuliza Roma kwa mshangao usio na kifani huku akimaanisha kwamba kilichomtokea siku ile mpaka kupoteza jiwe hilo la kimungu ,lakini vile vile kule Ufaransa kupoteza teknolojia ya Thanatos , lakini pia kupotea kwa Moses Vampire na Holygrail , mambo yote hayo yalikuwa ni yeye , Roma alijiambia haiwezekani ndio maana alitoa mshangao usio na kifani.
Jambo moja lingine ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba lile jiwe lilikuwa limebadilika ukubwa wake na sasa lilikuwa likitoa mwanga mkali sana unaoumiza macho mweupe lakini mfano wa jua , ni haki kusema kwamba Yan Buwen huenda kajua siri ya jiwe hilo.
Yan Buwen hakueleweka alifanya nini na lile jiwe lakini alilirusha juu angani na likanasa na palepale lilitengeneza shimo nyeusi kubwa ambalo anga lake ni kama linachemka kwa spidi kubwa ni kama unaangalia BlackHole , mwili wake ulivutwa kwa kasi sana na lile shimo na akapotea palepale kwa namna ya kuyeyuka.
Roma alijaribu kuzuia shimo liile lakini nguvu yake ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba ilimrusha mbali kwa kumkataa.
Roma alijikuta akianza kuhema kwa tabu , mpaka hapo aliamini huenda Yan Buwen alitumia jiwe hilo kuweza kuwa na nguvu kama hizo , ilikuwa mantiki kufikiria hivyo , lakini swali aliwezaje kufahamu kanuni za anga kirahisi hivyo kwanni hakuwa na uungu wowote ndani yake
Pumbavu”Aloijikuta akitoa tusu huku aking’ata meno yake kwa hasira kwa kitendo cha Yan Buwen kumkimbia , alijua aliweza kumtoroka kwa kutumia jiwe la kimungu, ijapokuwa miaka mingi lilikuwa chini ya umiliki wake lakini hakuwahi kufikiria jiwe hilo linauwezo mkubwa mpaka wa kutengeneza shimo jeusi angani na kuwa kama njia ya kutoroka.
“Hades usiwaze hatoweza kukushambulia kwa muda hahah..”Ilikuwa ni sauti ambayo inasikika kwenye kichwa chake na kumfanya kutoa macho , ilikuwa ni hali kama ya mtu mwenye ugonjwa wa kuchanganyikiwa.
“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikisikika vyema sasa lakini macho yake hayajatoka kwenye rangi ya uwekundu.
“Hehe .. umenipa jina mwenyewe unaweza kuendelea kuniita kwa jina la nguvu ya kimaandiko naishi ndani ya mwili wako , mimi na wewe ni ndugu wa damu chanda na pete una mwili mzuri sana kwa ajili ya mimi kuishi”Sauti ilisikika kwenye akili yake na kumfanya Roma kushika kichwa kwa namna ya kuchanganyikiwa.
“Achia akili yangu”
“Sawa kwasasa nitakuachia akili yako , lakini kadri unavyozidi kuwa na nguvu ya kijini itafikia siku lazima nitaiongoza akili yako kabisa,mwili wako unanifaa sana ngoja niendelee kulala nikisubiria siku yangu ya kurudi uraiani”Iliongea Sauti na kumfanya Roma ang’ate meno yake kwa hasira na palepale macho yake yalirudi kwenye hali yake ya kawaida na ile sauti ikapotea kwenye akili yake.
Alijikuta jasho likimtoka mno hakuelewa ni nini kinachomtokea hata hivyo ni kweli kabisa wakati anajaribu kupambana na Yan Buwen kwa uwezo wake wote ni kama mwili wake hakua ukiuongoza yeye kwenye mapambano, ni kama akili yake ilikuwa ikifanya kazi nusu na nusu nyingine ilitawaliwa.
Lakini hata hivyo Roma alitabasamu kifedhuli kutokana na kwamba ndani ya mwili wa Yan Buwen wakati alivyokuwa amemshikilia kichawi alimwingizia nguvu ya kijini kwenye mwili wake, kitendo ambacho hata yeye akili yake hakuelewa kwanini alifanya hivyo lakini kwa sauti iliomwongelesha anaelewa kwamba ni mtego.
Aliamini lazima mwili wake Yan Buwen utakuwa kwenye maumiu makali , kwani inaonekana nguvu ya jiwe la kimungu na za kijini haipatani ndio maana wakati anasogelea shimo jeusi tofauti na kumezwa yeye alitupwa mbali kwa ishara kwamba shimo lile linamkataa yeye.
Lakini Roma sauti aliokuwa akiisikia kwenye kichwa chake ilimfanya kuwa na wasiwasi lakini hata hivyo aliamini huenda ni akili yake mwenyewe , hivyo aliamua kupuuzia lakini bado roho yake haikuwa na amani.
“Au kuna athari za kutumia kanuni ya kimaandiko?”Roma alijikuta akianza kuwaza mwenyewe huku akiangalia uharibifu uliofanyika.
“Roma nini kimetokea , wewe ndio umeharibu hizi nyumba zote?”Ilisikika sauti kutoka hewani na kumfanya Roma kuangaliai juu alikuwa ni Omari alieonekana ndio anafika.
“Umewezaje kusafiri umbali mrefu mpaka hapa bila kukasiriha anga?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Kuna namna ya kusafiri pasipo kukasirisha aga , nnimefunzwa huko Hongmeng, pumbavu kabisa nimechelewa daah sijaona pambano”Aliongea huku akiongekana kulalamika.
Njia ambayo anazungumzia Omari ya kusafiri pasipo kukasirisha anga ni kusafiri kwa vituo , yaani unaweza kupaa kwa kilomota kadhaa na kisha ukatulia kwa dakika kumi na tano then unaendelea tena kwa kilomota kadhaa , mpaka ufikie eneo husika , uzuri ni kwamba tu nguvu za kichawi zenyewe zinakupeleka sehemu unayonuia kufika haina haja ya kuwa na ramani kichwani lakini athari kubwa ni kwamba kila kituo lazima kiwe ni maji au bahari, yaani kwa mfano ukatoka Tanzania na madhumuni ya kwenda China basi unatakiwa usafiri na uelekeo wa bahari tu ili kila ukifikisha kilomita kadhaa , unatumbukia majini na kukaa huko kwa dakika kumi na tano na unaibuka tena unasafiri tena kwa kilomita kadhaa halafu unaingia tena majini unajificha ndani ya maji kwa dakika kumi na tano unaibuka tena , ilikuwa ni mbinu ngumu kwani inahitaji ujasiri lakini inakuwezesha kusafiri kwa muda mfupi.
Hivyo kimahesabu ni kwamba Omari alianza safari kabla ya Roma kwani kuna vituo vingi sana ndani ya maji ambavyo lazima Omari alipumzika kabla ya kuendelea na safari.
Hivyo unaweza ukaona jini linaibukia baharini usiku ukashangaa lakini ukweli ni kwamba bahari au ziwa ni njia salama ya majini kusafiri pasipo kukumbana na malipizi ya anga.
“Taarifa za Yan Buwen kuua familia yake zinasambaa sana kuna rafiki yangu hapa China nilianza kufikia kwake na kupata habari hizo , inasemekeana walinzi ndio walitoa habari, Vipi umefanikiwa kumdhibiti”Aliuliza Omari huku akikagua namna eneo lilivyoharibika.
“Amenitoroka bwana”Alijibu Roma kinyonge.
“Hapana , amewezaje kutoroka mbele yako nadhani ni afadhari nimekuja baada ya mapambao kuisha huenda ningekufa hapa hapa, maana huenda ningepatwa na hasira na kushindwa kujizuia mpaka kumpiga ngumi”
“Unashindwa vipi kujizuia au kwasababu mwanamke wako kamtia mimba?”Aliuliza Roma kwa kejeli.Lakini Omari alionekana kutopendezwa na swali lake
“Najua huenda huna hela yoyote na pia mavazi yako yamechafuka , twende kuna sehemu salama ya sisi kwenda kula msoni na kupata hifadhi ya kulala”Aliongea Omari.
“Nani kakuambia sina pakuishi”Aliongea Roma na palepale licheza na anga , kilikuwa ni kitendo kama alichofanya Clelia allisanto wakati akitoa kiboksi cha uwa angani.
“Hades kuna uwezekano na mimi kujifunza namna ya kutunza vitu kwenye anga?”
“Uwezekano huo huna , nina nguvu ya kiuungu ndani yangu ndio maana naweza pia kujifunza kanuni za anga , wewe ni binadamu wa kawaida ambaye umejifunza mbinu za kijini”Aliongea Roma huku akiangalia kipi cha kuchukua kwenye shimo ambalo linatumika kama sehemu ya kuhifadhia vitu kwenye anga , aliachana na pete na kisha akachukua kadi ya benki na passport yake ya kusafiria.
“Hivi ni vibali ambavyo vinaweza kunipatia makazi kwenye hoteli yoyote hapa nchini China pambana kivyako sijakuambia unifuate huku China”Aliongea na kabla hata Omari hajaongea neno , palepale Roma alipotea na kumuacha Omari akiwa kwenye mshangao.
“Pumbavu zako Hades , nimekufuata mpaka China halafu umeniacha nitakupata tu”Aliongea Omari huku akiangalia baiti moja iliofukukiwa na mchanga uliotokana na kuharibika kwa nyumba na alisikitika kidogo na kisha akapotea ndani ya eneo hilo mara baaada ya kusikia magari ya polisi yakisogelea hilo eneo.
Unafikiri sauti iliomuongelesha Roma inatokana na nguvu za kijini anazojifunza , kama kweli ataendelea kupanda levo je nguvu ya kimaandiko itaweza kutawala akili yake , nini kitaendelea tukutane kesho.