SEHEMU YA 444.
Edna na Roma mara baada ya kuingia eneo la sebuleni waliweza kukutana na sura nne ngeni ,kulikuwa na mwanaume mwenye kitambi na mwili mkubwa alievalia suti , mwanaume mwingine alikuwa ni mzungu. , wengine wawili walikuwa ni mabodigadi.
Kuhusu mzungu alikuwa mrefu wa kama inchi sita na nusu , ana nywele nyeupe aina ya blonde akiwa amevalia shati rangi ya pink na suruali ya kitambaa, mwonekano wake ilikuwa ngumu sana kuweza kukadiria umri wake , lakini alikuwa ni kijana kabisa huenda hata Roma akawa mkubwa.
Roma na Edna mara baada ya kufika eneo hilo la sebuleni yule bwana mweusi mwenye kitambi alisimama, Roma hakumfahamu lakini upande wa Edna alimfahamu huyo mwanaume kwani alikuwa ni mwanasiasa maarufu tu.
“CEO Edna umerudi?, naomba unisemehe kwa kufanyia ziara ya kushitukiza asubuhi asubuhi”
“Usijali muheshimiwa karibu sana”Aliongea Edna.
“Mr Roma nadhani hatujawahi kukutana ana kwa ana , kwa jina naitwa Abasi Nguya ni waziri wa Uwekezaji , biashara na Viwanda”Alijitambulisha.
“Karibu sana bwana Abasi Nguya”Aliongea Roma lakini Edna macho yake yote yalikuwa kwa mzungu ambaye alikuwa akitoa tabasamu , ilionekana ni kama wameshakutana kabla ya ujiio huo.
“Mr Maksim? Why are you here?”Aliuliza Edna kwa kingereza akimuuliza bwana mzungu kwanini yupo hapo.
Roma mara baada ya kuona mke wake anamfahamu huyo mzungu alijiuliza ni wapi wamekutana.
“Edna unamfahamiana nae?” Aliuliza Roma na kabla hajajibu yule mwanaume alimsogelea Roma.
“Hello I’m Maksim frome the Klyuchevsky familly in Russia , its honor to visit your home, I met CEO Edna at the international bussiness and economics meeting yerstaday”
“Habari naitwa Maksim kutoka familia ya Klyuchevsky kutoka Urusi , ni heshima kwangu kutembelea hapa nyumbani kwako , nilikutana na CEO Edna kwenye kikao cha uchumi na biashara za kimataifa siku ya jana”Aliongea yule bwana kabla hajampa nafasi Edna kujibu.
Roma hakuweza kujua kama siku ya jana kulikuwa na kikao cha aina hio hata hivyo asingejua kwani alikuwa kwenye mgogoro na mke wake.
“Mr Maksim amekuja mpaka hapa kwa nia ya kuongea na nyie wote juu ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi , nimepewa kazi hii na mheshimiwa raisi kuwa mtu kati kwenye mazungumzo”Aliongea bwana Abasi Nguya.
“Mazungumzo ya kidiplomasia ndani ya nyumba yangu , mbona kama ni swala ambalo halijakaa sawa”Aliongea Roma.
“Hapana Mr Roma , inawezekana sehemu hii sio sahihi , lakini serikali haiwezi kufanya maamuzi ya moja kwa moja bila makubaliano kati yako na mke wako kuhusu maswala ya kibiashara , hivyo kauli yako ni muhimu pia kwenye mzungumzo yetu” Baada ya kuongea hivyo Roma aliamua kwenda kukaa na wote wakakaa chini kwa ajili ya mazungumzo.
Licha ya bwana Maksim kusema kwamba alikuwa ashasikia habari zake , lakini aliihisi bwana huyo alikuwa akimfahamu kwa jina la zaidi ya Roma ,kama si hivyo asingefika nyumbani na kuhusishwa kwenye maswala ambayo mke wake anaweza kufanya maamuzi kama siku zote.
“Familia anayotokea bwana Maksim ni moja ya familia kubwa ndani ya taifa la Urusi na hata Raisi wa sasa wa Urusi yupo madarakani kutokana na sapoti kubwa kutoka kwenye familia ya bwana Maksim , ndio wameshikilia uchumi wa Nishati ya nyuklia , Gesi asilia na Petroli Urusi yote, Hata hivyo wanajiendesha kwa siri sana ndio maana hawana umaarufu mkubwa”Aliongea Mheshimiwa Nguya na kumfanya Edna kushangazwa na taarifa hio , siku ya jana mara baada ya kukutana nae alimchukulia poa kumbe alikuwa mtu mzito sana.
Urusi ni nchi ambayo imejaaliwa rasilimali nyingi za kinishati , msingi wa biashara ya Vexto ni uingizaji wa asilimia hamsini za mafuta kutoka nje ya nchi hivyo mazungumzo hayo ya kibiashaa kama yanegeenda sawa ingekuwa ni faida kubwa sana kwa kampuni yake na huenda hata gharama ya mafuta ya Petroli zilizokuwa juu kwa sababbu ya vita kati ya Ukraine na Urusi ingepungua, lakini sio hivyo tu kama kutakuwa na makubaliano ya kibiashara kampuni nyingi ndani ya Afrika mashariki kwa ujumla zingepatwa na ukichaa, Edna alijikuta mwili wake ukimsimsika.
“Mr Maksin jana hukuzungumzia swala lolote linalohusiana na ushirikiano wa kibiashatra , kwanini iwe leo?”Aliuliza Edna kwa kingereza huku akionyesha shauku kwenye macho yake , hata hivyo Edna alizaliwa kuwa mfanyabiashara hivyo eneo kama hilo lilikuwa la kwake kabisa kutawala.
“Miss Edna my proposal ties with my background I do not wish to reveal it to the general public right now”
“Edna Pendekezo langu linafungamana na ubini ambao sitamani kuweka wazi sasa hivi”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa , lakini Maksim alibadilisha mkao na kisha akamwangalia Roma na Edna kwa pamoja.
“Pendekezo langu nataka kampuni ya Vexto kuvunja mkataba na Princess Clark”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio lakini aliendelea kuongea.
“Nimekuja hapa nchini kwa ajili ya Clark , Clark ni mchumba wangu na hata mipango ya ndoa yetu ni makubaliano kati ya familia yangu na Rothchild, lakini kutokana na kutokuelewana ndio akaingia mkataba na Kampuni ya Vexto pamoja na serikali ya Tanzania ili tu kuweza kuepuka kufunga ndoa , jambo ambalo ni matusi kwa familia yangu na familia ya kifalme kutoka Wales , hivyo ujio wangu hapa Tanzania ni kwa ajili ya kumrudisha Urusi ili taratibu za ndoa ziendelee”
Roma maneno hayo hakuyapenda kabisa , ijapokuwa Catherine alishamwambia kwamba Clark alipaswa kuolewa lakini hakujisumbua kuuliza ni familia gani anaozeshwa, lakini alishangaa kujua ni moja ya familia ya Ma oligarch kutoka Urusi.
Mpaka hapo Roma kuna kitu kilimjia akilini , huenda Clark anatolewa kafara kutokana na yale yanayoendelea ndani ya bara la ulaya , Uingeeza ni kati ya nchi ambazo zinategemea sana rasilimali nishati kutoka Urusi , ukijumlisha na Vita vinavyoendelea huenda ndio ilipelekea Rothchild kutaka kufanya makubaliano ya kibiashara yanayofunganishwa na ndoa, hata hivyo alikuwa akijua familia ya Rothchilds siku zote ilichokuwa ikijali ni pesa sio utu.
Unapaswa pia kujua kwamba Klyuchevisky ndio wapo nyuma ya chama tawala ndani ya Urusi.
Edna sasa ndio anajua ujio wa Profesa Clark sio wa kibiashara bali alikuwa akikimbia ndoa, akili yake ilianza kuzunguka kwani maongezi hayo hayakuwa ya kibiashara tu bali yalionekana kama tishio kwa biashara zake , ukizingatia pia kampuni yake ilikuwa ikijihusisha na biashara ya mafuta kutoka Urusi , aliona hata kama hatomwachia Clark kuondoka kwa kuvunja mkataba lakini hakuwa na uwezo wa kuziia swala hilo kwani asingeweza kushindana na familia kubwa kama hio.
Mkataba wake na Clark ulikuwa ni wa faida kubwa huko mbeleni kama angefanikiwa kutengeneza dawa za magonjwa ambayo yamekuwa yakiangamiza jamii ya Afrika kwa makusudi kabisa kwa ajili ya faida ya Wazungu , lakini hata hivyo upande mwingine wa kibiashara aliamini familia hio ingeweza kumlipa fidia ya kuvunja mkataba.
Hivyo kama Edna angekataa kuvunja mkataba ni dhahiri kwamba alikuwa akishindana na serikali kubwa zote za bara la Ulaya kwani Rothchild ndio watawala wa bara lote kwanzia Ufaransa ambako kuna tawi lake la kibiashara mpaka Uingereza na Ujerumani, lakini pia Urusi moja kwa moja.
Edna alijikuta akigeuza kichwa na kumwangalia Roma , aliamini yeye pekee ndio ambaye anaweza kufanya maamuzi kwa wakati huo.
Ikumbukwe kwamba Edna pia kama angevunja mkataba , sifa ya kampuni yake ingeshuka , kwanni siku ya juzi kwenye mahafali pale Chuo kikuu cha Mlimani dhumuni la mkataba wake na Profesa Clark lilikuwa bayana kwamba ni kusaidia nchi za Afika kujitegemea katika maswala ya utafiti wa utengenezaji wa madawa kwa magonjwa sugu,, jambo ambalo lilipokelewa kwa uchanya na mataifa mengi ya Afrika ambayo yalichoshwa na kunyenyekea wazungu, hivyo kama angevunja mkataba kwa ajili ya pesa ingemletea sifa mbaya na kampuni ingeathirika zaidi.
“Edna nini mawazo yako juu ya hili”Aliongea Roma lakini Edna alisita kutoa jibu moja kwa moja.
“Mr Maksim nadhani tuone kwanza masharti yako kwanza juu ya kuhitaji kuvunja mkataba na kampuni yangu , Kama nitakubali moja kwa moja lazima utambue kwamba pesa tu haiwezi kutatua tatizo lakini pia taswira ya kampun itaathirika , nadhani umekuja hapa ukiwa umefanya utafiti na umeona siku tatu hizi baada tu ya kutangaza nia yetu ya utafiti wa madawa hisa za kampuni yangu zilipanda kwa zaidi ya asilimia kumi”Aliongea Edna huku akijitahidi kujituliza ili kutumia akili yake ya kibiashara katika kufanya maamuzi.
Maksim alibadilisha mkao tena huku akionekana kama mtu alietarajia swali hilo kutoka kwa Edna kwani alitabasamu.
“Kwanza kabisa kampuni yako Tanzu iliopo ndani ya bara la Ulaya itapata kibali cha kufanya biashara upande wa Mashariki yote ya Ulaya ,Nimefahau kwamba mara ya mwisho ulivyokuwa Ufaransa uliweka wazi nia yako ya kutengeneza mirija ya kibiashara upande huo wa mashariki kwa kujipanua zaidi , lakini licha ya juhudi kubwa ulizoweka hilo halijafanikiwa mpaka sasa hivyo tutafanikisha ndoto yako, Pili biashara ya utafiti wa madawa sugu na mafunzo ya wanasayansi wazawa utaendelea kama kawaida lakini kwa kutumia wataalamu wabobevu ambao watatoka moja kwa moja Urusi nakuziba nafasi ya Profesa Clark na ninakuhakikishia kupitia wataalamu wetu ndani ya miaka mwili utakuwa na mafanikio unayoyata. Tatu na mwisho kabisa , tunajua mpaka sasa kuna mkataba wa kudumu uliosainiwa na Raisi wa awamu ya tatu wa biashara ya mafuta kati ya serikali na kampuni ya Vexto, tunapanga kuongeza kiasi cha mafuta yanayoingia Tanzannia kwa gharama ya nafuu chini ya thamani ya soko, lakini pia kampuni yako itapewa kipaumbele ya kupata malighafi zinazotokana na ‘Petreleum extraction”
Edna alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha fidia zote zilikuwa ni kubwa kiasi kwamba hakuhitaji kufikiria mara mbili mbili na kama angekubali inamaanisha kwamba angezidi kuwa tajiri , ni kichaa tu ambaye angekataa dili kama hilo , ukizingatia pia kama angevunja mkataba na Clark ilikuwa na faida ya ziada kwake pia kwani angezuia uwezekano wa mahusiano ya kimapenzi kati ya Roma na Profesa Clark..
Maksim baada ya kushusha bomu hilo la ofa kichaa alikaa kwa kuegamia kabisa , alijua kama kweli Edna ni mfanyabiasha asingeweza kukataa ofa yake.
“Edna ofa ambazo zimetajwa na bwana Maksim ni kubwa mno na faida yake sio kwako tu bali ni kwa watanzania kwa ujumla na Serikali inaangazia swala hili kwako kwa matarajio chanya kutoka kwako kwani lina faida pia ya kidiplomasia baina ya nchi zetu mbili , huna haja ya kuwa na wasiwasi na Profesa Clark kwani familia yake ishafanya mawasiliano na Profesa ili kusitokee lawama yoyote”Alipigilia msumari waziri Nguya.
“Kama ofa yenu ni ya kweli basi nita…”
“Hapana” Roma alimkatisha mke wake baada ya kuona anataka kukubali na kauli yake ilifanya chumba kuwa kimya hata Edna mwenyewe alitetema na kuwa mpole
“Haya mazungumzo yanapaswa kwanza kukubaliwa na Clark , hata kama atakubali kuvunja mkataba na hataki kuolewa basi nasema hivi hakuna wa kumtoa hapa nchini”Aliongea Roma.
“Mr Roma nakufahamu kwa jina lingine ambalo hata familia ya Rothchild wanaliogopa kila linapotajwa , lakini hata hivyo haimaanishi kwamba unaweza kufanya maamuzi ambayo yanaingilia maswala ya kisiasa na uchumi wa dunia kwa ujumla wake , una nguvu kubwa lakini hata hivyo sio kama hufuatiliwi , makosa kidogo tu yanaweza kusababisha migogoro mkubwa kati ya Tanzania na mataifa makubwa”
“Kwahio unanitishia si ndio ?”Aliongea Roma kwa Kingereza huku akisugua vidole vyake vya mikono ambavyo vishaanza kumuwasha.
“Sikutishii ila nina kuhabarisha , kwa ninavyofahamu pia wewe ni mtoto wa raisi wa taifa hili na pia familia yako imefungamana na jeshi kwa muda mrefu , hivyo siamini kwamba hata wanafamilia wanaweza kukaa chini na kuangalia unaharibu maswala ya Diplomasia ambayo ni maslahi mapana kwa Wananchi”
“Bwana Maksim nadhani kuna kitu kimoja unapaswa kujua , mimi nikiamua jambo langu kichwani basi hakuna mtu wa kunizuia kulitimiza , sintojali taifa na tafia kuingia kwenye vita kama inaleta maana ya kupata ninachotaka,msimamo wangu siku zote mwenye nguvu anaongoza njia na dhaifu anamfuata mwenye nguvu”Aliongea Roma na kumfanya bwana Maksim sura kumshuka.
“Kama unakataa mapendekezo yangu nitaihusisha wizara ya mambo ya nje kushughulikia hili swala na nakuhakikisha hili swala halitopita kirahisi kama unavyodhani na sio kwa Tanzania tu lakini pia hata kwa Clark ambaye unajaribu kumkingia kifua , heshima yake aliojijengea ndani ya muda mrefu itaharibika itaharibika ndani ya siku moja”
Waziri Nguya sofa lilianza kuwa la moto , serikali ilimwamini katika mazungumzo hayo ndio maana akatumwa kama mtu kati , lakini kile anachokiona hapo hakuna namna ya kufikia kwenye makubaliano kwa amani.
“Roma unafanya nini , unaonaje tukitulia na tukizungumza hili swala bila mtafaruku”Aliongea Edna kwa wasiwasi kwani alimuona Roma kama bomu ambalo lingelipuka muda wowote ,lakini Roma ni kama hajamsikia.
“Oh tena… CEO Edna kwa taarifa nilizokuwa nazo una madaraka kamili juu ya kampuni ya Vexto , kwanini unataka kushikiliwa kimaamuzi na mume wako kwenye maswala ya kibiashara , hili ni swala linalokuhusu wewe sio Roma , na hata hivyo nimeweza kupata taarifa kwamba upo vizuri sana likija swala la biashara”Aliongea huku akisimama na kutaka kupiga hatua kutoka nje , lakini Roma alitoka kwenye sofa na kumkinga kwa mbele akimzuia asipige hatua, alikasirishwa na kauli yake na kuichukulia kama tusi mbele ya mke wake.
“Unataka kufanya nini .?.” Aliongea Maksim huku akianza kushangazwa na mabadiliko ya ghafla ya Roma, kwani alikuwa ni kama mtu mwingine kabisa kwa jinsi alivyokuwa na hasira.
Maksim alimkwepa akitaka kumpita kwa pembeni lakini kabla hajatimiza azma yake Roma alimshika Shingo kwa nyuma na kumfanya Maksim kushindwa kupiga hatua
“Usijione wa thamani sana tena ndani ya nyumba yangu , hupaswi kabisa hata kukaa meza moja na mimi mbwa wewe ..”Aliongea Roma huku sauti yake ikiwa nzito na palepale alimgeuza kama anachezeshwa Tango na ile anageuka alipigwa ngumi yenye ujazo mkubwa wa nguvu za kijini eneo tumboni na mkono wa Roma ulizama ndani na akauchomoa kwa nguvu na kusababisha damu kusambaa pamoja na nyama nyama.
“Aaarrggh!!”
Edna alifumba macho akishindwa kuangalia , Waziri pamoja na mabodigadi walishindwa kuzuia mshangao wao huku na kukimbilia nyuma ya Edna na kusimama.
Maksim alidondoka chini huku akionekana kushindwa kuzuia maumivu anayoyasikia huku damu zikimtoka mfululizo , lakini Roma alimshika kwenye shingo kwa mara nyingine na kumtupia nje kama furushi akijua kabisa bwana huyo ni wa kufa.
“Unaweza kutoa taarifa kwa kila kichotokea hapa ndani bila ya kubadilisha neno, na kama itatokea tatizo lolote njoo niambie nitakusaidia nitakusaidia kulirekebisha”Aliongea Roma akimwangalia Waziri Nguya pasipo kujali mikono wake uliojaa mabonge ya damu.
Edna alishindwa kuhema kwa tukio aliloshuhudia , mwanzoni akili yake ilikuwa kwenye ofa , lakini sasa hivi hakuwa akifikiria kingine zaidi ya kuwa na hofu kwa kile kilichomkuta Mzungu.
Muda ule ule waziri alipotaka kuongea neno , wote walijikuta wakiangalia nje na kushuhudia kitu ambacho hakikuwa cha kawaida , kwanza Maksim alisimama akionekana mzima kabisa , ni kama hakuguswa kabisa kwani sehemu aliopigwa ngumi na kutobolewa tumbo ilirudi kama kawaida , lakini muda huo huo sura yake ya kizungu ilibadilika na kuanza kutengeneza michirizi ya ukijani uliokolea kwenye macho , huku meno yake yakirefuka na kucha vile vile ziliongezeka ukubwa , ilikuwa picha ya kushanganza na kuwafanya wale mabodigadi wote kurudi nyuma na kumuacha Roma akiwa mbele peke yake
“Your strength is realy unbeleivable Pluto …”Alisimama huku akionekana kama Vampire na hata tabasamu lake lilitisha mno.
Roma palepale akili yake ilifanya kazi mara baada ya Maksim kupona kwa haraka sana , lakini pia kucha zake kuchomoza na meno kurefuka na kuwa na mwonekano usiokuwa na utofauti na Vampire.
“Nimekumbuka ….Wolverines!!!, wewe ni mwendelezo wa kizazi cha White wolf kutoka Urusi , katika familia ya kifalme mliojipatia jina la Wolverines…”Aliongea Roma huku awamu hii akionyesha hali ya kuwa na msisimko usio na kifani ni kama ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na watu wa namna hio.
“Hahaha.. sasa ushanifahamu hivyo huna cha kunifanya , hatupo kwenye kizazi cha karne ya tano sasa hivi , hilo jina lishapotea na kubakia sisi ambao ni binadamu wa kawaida , tumekuwa watawala wa siri karne na karne ndani ya taifa la Urusi , Sisi ni wafalme wa Nchi zote za mashariki ya Ulaya., ulichokifanya leo kimeingiza Tanzania kwenye orodha ya nchi adui zetu”Aliongea na baada ya kumaliza palepale alipotea mbele kwa namna isioelezeka.
.
SEHEMU YA 445
Roma hakutaka kumfukuzia , hata hivyo alishawahi kusikia habari juu ya jamii ya siri sana iliokuwa imejibatiza kwa jina la Wolverines, lakini hakuwahi kuamini kuhusu stori hizo kwani kwake ilikuwa kama hadithi.
Wolverines ni jamii kama Vampire ambayo simulizi zake zilisikika sana kati ya karne ya tano mpaka mwishoni mwa karne ya kumi na tano , katika zama hizo waliaminika kuwa binadamu ambao ni jamii ya Vampire , lakini utofauti wao ni kwamba Wolverine hawakuwa wakiathiriwa na mwanga wa jua kama ilivyo kwa Vampires na walikuwa na nguvu kubwa sana kwenye mapambano kuliko hata jamii ya Vampire yenyewe na waliweza kuishi hata nyakati za mchana na hawakutegemea damu ya binadamu kuishi bali wanakunywa damu ya mnyama anaefahamika kwa jina la Wolverine au White Wolf(Mbwa mwitu) na ndio chanzo cha jina lao, inasemekena mbinu pekee ya kuweza kuwaua ni kwa kunyofoa moyo wao.
Waziri Nguya alihisi ni kama yupo kwenye ndoto ya kutisha , hakuamini angeanza siku kwa kushuhudia kitu cha namna hio , lakini upande wa Edna licha ya kuwa kwenye mshangao , lakini alishindwa hata kutetemeka zaidi ya kuangalia mikono ya Roma iliotapakaa damu ni jambo ambalo kwa mwanamke halivumiliki lakini kwa Edna ilikuwa jambo ambalo ni kama amewahi kuliona kabla.
“Unaweza kwenda kuripoti kama ulivyoona hapa bila kuacha neno”Aliongea Roma akimwambia mheshimiwa waziri na kisha alipita na kuingia ndani na kwenda kuosha mikono jikoni kwenye sink.
Edna alijikukta akitembea kwa kusita sita na kwenda kujibwaga kwenye sofa akiwa kama mtu ambaye hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea na hata Roma alivyotoka jikoni aliishia kumwangalia kwa maswali mengi.
“Nadhani umeona mwenyewe kilichotokea , ijapokuwa mpaka sasa sijui ni kwasababbu ipi familia yake kutaka kumuozesha kwa viumbe wa ajabu ,, lakini siwezi kuruhusu swala hilo litokee”
“Hivi unajiona unachokifanya mbele yangu?”
“Nakuambia siwezi kumruhusu Clark kuolewa na wanyama”
“Acha mambo yako ya kumlinda mwanamke mbele yangu Roma, utanikasirisha”
“Nisamehe kama kauli yangu inaziumiza hisia zangu lakini huo ndio msimamo wangu , sidhani kwa ulichoshuhudia hata wewe mwenyewe ungekubaliana nacho”Aliongea Roma lakini muda huo huo Bi Wema na Blandina walishuka kutoka juu wakiwa na wasiwasi.
Na walishangazwa zaidi mara baada ya kuona damu zilizokuwa zimetapakaa karibu na mlango na kutaka kujua nini kimetokea.
Muda huo huo alipokuwa akitaka kuuliza , sauti ya gari kutoka nje ujio wa mtu zilisikika na mlango palepale ulifunguliwa na alionekana Profesa Clark aliekuwa akihema kwa nguvu.
Alikuja akiwa amevalia koti la maabara na ilionekana kabisa alitoka kazini muda huo kwa mwonekano wake.
Aliangalia damu zilizotapakaa na hakujali sana zaidi ya kupita na kumsalimia Blandina na Bi Wema na kisha akasalimiana na Edna aliekuwa akifikicha macho.
“Kwanini umekuja ukiwa hivyo?”Aliuliza Roma na Profesa aliingiza mkono wake kwenye koti na kuibuka na kijichupa kama vile vya kuhifadhia chanjo(Vials) na kumpatia Roma.
Ni ‘antidote’ , niliogopa ningechelewesha ndio maana nikaja mwenyewe haraka haraka , unatakiwa kumpatia na kumeza kwa kupitia mdomoni tu”Aliongea na kumshangaza Roma.
“Umeweza kufanikisha ndani ya muda mfupi hivi?”
“Damu ya mgonjwa wako nilipoifanyia majaribio niliweza kubaini amewekewa kimiminika ambacho ni kama sumu ambayo inashambbulia DNA za mwili, ni kimiminika ambacho kimetenenezwa kwa kuunganisha DNA na RNA za virusi ishirini na nne,, kimiminika hiko kinafahamika kwa jina la ‘Tribute to Maria’ , ni siraha ya kibailojia ambayo imefanyiwa majaribio nchini Urusi kwenye maabara ya siri ifahamikayo kwa jina la Nicene , mwezi uliopita kuna wanafunzi wangu i waliiuliza maswali baadhi yanayohusina na sayansi ya uundaji wa mchanganyiko wa virusi pamoja na namna Chanjo yuake inavyowezekana kutengenezeka na niliwapa majibu na kushauri wasijaribu kuunda siraha hio kwani ni hatari sana kwa maisha ya binadamu lakini inaonekana waliendelea na kazi yao”
“Kwanini jina la ‘Tribute to Maria’ na vipi kuhusu hii maabara ya Nicene?”
“Kwanza kabisa hiki kimiminika kiligundulika kwa mara ya kwanza katika karne ya kumi na moja kihistoria , ulikuwa ni mwendelezo wa tamaduni za kimiminika(Siki) alichopewa Yesu wakati wa kusulubishwa , utofauti ni kwamba Kimiminika hiki na Siki ni vitu viwili tofauti kwani katika karne ya kumi na moja kiliongezewa ubora wenye dhamira tofauti kabisa na kuanzia hapo kikaendelea kuboreshwa na katika Karne ya kumi na sita ndipo kilipobatizwa jina la Kinywaji cha Heshima Kwa Maria kupitia vita baina ya dini ya kikristo na waislamu wa Uturuki.
Kila mturuki ambaye alikamatwa alilazimishwa kunywa kimiminika hiko kama atakataa kukubali kubatizwa na kuwa mkristo , sasa pale mateka anapolazimishwa kunywa hiko kimiminika wanajeshi(crusaders) walipiga kelele ‘Heshima kwa Maria’(Tribute to Maria) aliemzaa Mwana wa Mungu.
Baada ya vita uwepo wa kinywaji huo ulipotea kabisa kwa kupigwa marufuku na kanisa la Roma , mpaka miaka ya hivi karibuni kulipogundulika tena kimiminika kilichopewa jina hili hili ambacho wanasayansi waliokuwa chini ya kanisa la Orthodoxy huko Urusi walikipatia jina kwa kuamini ni mwendelezo wa kimiminika kile kile kilichotumiwa katika vita vya kusambaza dini ya kikristo, kuhusu Nicene ni jina la maabara iliokuwa nchini Uturuki ambayo ilihusika kutengenezea kimiminika hicho wakati wa vita na baada ya vita kuisha maabara hio ilihamishiwa nchini Urusi mpaka leo hii na ndio ilioendeleza sayansi ya kutengeneza kimiminika kipya ambacho ni kama siraha ya kibailojia”Aliongea Clark kwa muda mrefu na kumshangaza Edna na Roma kwani maelezo hayo ni kama yalikuwa mapya kwao.
Ndio kama utakuwa mtu wa historia basi utaweza kugundua jina la Nicene limetokena na jina la Nicaea kwa kilatini kilichotoholewa kutoka lugha ya kigiriki , lakini kwa kiswahili inafahamika kwa jina la Nikea , maana ya jina hilo ni mji wa ushindi ambayo kwa sasa unafahamika kwa jina la Iznik huko Uturuki.
“Kwahio kama ni kweli hii maabara ipo eneo gani nchini Urusi na wanapata hela ya ufadhili kutoka wapi au ni serikali?”Aliuliza Roma.
“Hio taarifa ni ya siri na mimi mwenyewe sijui , labda umjaribu rafiki yako Makedon kutoka Mossad nadhani atakuwa na majibu , udhalishwaji wa kimiminika hiko ulipigwa marufuku sana na kanisa la Catholic na Orthodoxy kwa kutumia jina la Maria, lakini licha ya hivyo hakuna kilichobadilika naamini kuna ajenda kubwa ya siri ambayo inaendelea , naweza pia kuamini huenda serikali ya Urusi haihusiki kabisa”
“Okey nitajaribu kuwasiliana na Makedon aweze kunipa mwanga”Aliongea Roma huku akikuna kichwa.
“Halafu nimesahau swali moja, kama mtu atakuwa amepatiwa hiko kimimnika kuna uwezekano wa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwani kwa melezo yako naweza kusema ni kirusi”
“Hakika ni kirusi lakini lakini tunaita kimiminika kutokana na kwamba ni muunganiko wa virusi ishirini na nne vilivyodhalisha majimaji , bahati nzuri ni kwamba kinasambaa kama kirusi cha HIV , lakini naamini kuna uwezekano kikawa kimeongezewa ubora wa kusambaa kwa njia ya hewa ili kutumika kama siraha ya kibailojia inayosambulia Genes”
“Umesema kuna wanafunzi wako wako waliulizia maswali juu ya hiko kimiminika , je unahisi ndio waliotengeneza ?”
“Inawezekana kwani kati ya wanafunzi wangu mmoja wapo alikuwa ni mrusi”Aliongea.
“Hawa wanafunzi wako kila wanapoenda ni kusababisha matatizo tu, kwanini unafundisha vichaa”Aliongea Roma
“Roma nadhani hata wewe unafahamu ule msemo wa kwamba elimu inapaswa kutolewa kwa watu wote bure na kwa usawa , ndio nilichofanya, sina haki ya kumjaji mwanafunzi wangu anakwenda kufanyia nini elimu anayoipata ili mradi napokea heshima yangu kama mwalimu wao , wakishamaliza elimu yao siwajibiki kwa wanachofanyia elimu yao”
“Lakini huogopi kwmaa inaweza ikatokea mmoja wapo kukugeuka na kukudhuru?”
“Unajua nini Roma, licha ya kwamba Yan Buwen amekuwa kichaa lakini mafanikio yake yamenishangaza , likija swala la utafiti wa kisayansi ukimtoa Profesa Shelukindo nadhani ni yeye pekee kidogo anaeweza kunikaribia”
Edna aliekuwa kimya muda wote aliona akili yake inakuwa nzito , kila siku anavyozidi kuishi na Roma aliweza kufahamu mambo mapya zaidi , huku mengi yakiwa ya kutisha zaidi na mazito kweli kweli..
“Edna naomba unisamehe…”Aliongea Clark na kumfanya Edna kushangaa kwanini anaombwa msamaha.
“Nilipishana na gari mbili wakati nakuja hapa , mojawapo ni gari ambayo namfahamu mmiliki wake na alikuja jana nyumbani kwangu , kwa uwepo wa hizi damu hapa naamini Roma ameweza kumfanyia jambo”Aliongea na kumfanya Edna kidogo kukosa neno la kuongea.
Alijisikia vibaya kuona Mwanamke mwenzake analazimishwa kuozeshwa kwenye familia ya Mashetani .
“Edna najua ukaribu wangu na Roma unaweza kukufanya ujisikie vibaya lakini naomba nikwambia usiwe na wasiwasi kabisa , sina mpango wa kuwa kidudu mtu kwenye mahusiano yenu , Roma aliniokoa mimi na mama yangu miaka mingi iliopita nikiwa mdogo na kama sio yeye nisingeweza kuwepo kwenye dunia hii , kwangu Roma ni mwokozi wangu , kama unahisi uwepo wangu hapa Tanzania unakufanya usijisikie vizuri niambie tu, sitokasirika nitaondoka mara moja, ninaweza kuagiza wanafunzi wangu na kuendeleza project yetu, Natumaini maisha yako na Roma kuwa yenye furaha…”
“Inatosha Clark ,hakuna tatizo lolote mimi na Edna tupo sawa kabisa , kinachoniumiza ni hawa Klyuchevsky , bora hata wangekuwa ni Vampire lakini Wolverines , pumbavu kabisa siwezi kuruhusu ukaolewa na hawa viumbe na ukaja kuzaa mdudu, Catherine na familia yako watakuwa vichaa”
“Usimlaumu sana mama , hana nguvu kubwa juu ya Rothchild miaka iliopita familia ya klyuchevisky walisaidia sana kwenye uchumi wa familia hivyo ni kama kulipa fadhila na hata hivyo sikuwa na mchumba na ni haki yangu kuoelewa. Binafsi nimeonea nisichukulie hili swala kuwa kubwa sana kwani hata kama nitaolewa kwao sio kwa ajili ya kuzaa ila ni kama maonyesho tu”
“Kwahio unapanga kuolewa kwa hayo maonyesho?”
“Ndio , ndoa yangu itatatua shida kubwa ya kiuchumi inayoendelea baina ya Urusi na Uingereza katika maswala ya nishati.. Roma nafahamu unajua haya sina haya ya kuelezea zaidi ni wajibu ambao unanihusu”
Roma alitaka kuongea lakini Edna alimzuia kwa kumshika mkono.
“Edna unataka kuongea nini?”
“Mimi sioni tatizo la Maksim kabisa kumuoa , anaweza kuwa tofauti na binadamu lakini ni kijana mzuri , kinachoangaliwa ni moyo wake ulivyo ,mabadiliko yake ya muda mfupi yasiwape uhalali wa kujaji mapenzi yake kwa Clark wala kumsema vibaya Maksim, mimi nadhani Clark ukubali kuolewa tu”Aliongea Edna na kauli yake ilishangaza kila mmoja.
Roma moja kwa moja alijua Edna hakuwa akipenda uwepo wa Clark ndani ya Tanzania hivyo anapanga kuhakikisha anaondoka moja kwa moja kwa kuoelewa.
“Edna upo sahihi sana , Roma nadhani nishafikisha kilichonileta hivyo kwaherini”Aliongea Clark na kisha alitoka kwa kukimbilia nje akitoa machozi na ndani ya muda mfupi mngurumo wa gari ulisikika ukififia nje ya geti.
Blandina na Bi Wema walikaa kimya muda wote , hawakutaka kuingilia swala hilo kwa namna yoyote , waliamini ni maswala ya wao kumalizana wenyewe.
Roma hata yeye hakupenda kauli ya Edna ambayo imemfanya Clark kuondoka namna hio , alijua lazima muda huo angeenda kulia , alisimama na kutoka eneo la sebuleni na kupandisha kwenye chumba chake.
“Roma unaweza kukasirika utakavyo lakini sijutii kwa kauli yangu, nipo tayari kufanya chochote ambacho kitalinda amani ya familia yangu”Aliongea na kumfanya Roma kusimama na kumwangalia kisha akatingisha kichwa na kuendelea kwenda juu.
********
Upande mwingine ndani ya hoteli ya Johari Rotana katika chumba cha Presidential Suite alionekana Maksim aliesimama kwenye dirisha akiangalia upande wa nje wa jiji huku akiwa ameshikilia glasi ya mvinyo mkononi.
Alionekana kama mtu ambaye hakuwa ametoka kwenye kupatiwa kibano na Roma mpaka kupoteza vipande vya utumbo mpana , muda huo alikuwa amejifunga taulo mwili mzima akiwa msafi na sura yake ya Kihandsome boy , hakuna mtu ambaye anaweza kuamini kwamba anaweza kubadilika sura na kuwa wa kutisha.
Nyuma yake alionekana mwanamke wa kizungu ambaye amepiga magoti chini akiangalia mgongo wa bwana Maksim.
“Boss misheni ulionipa ya kumshawishi kiongozi wa Alshababu kutumia wanajeshi wake imefannikiwa na mpaka sasa wapo tayari mpakani na kombora lilojaa kimiminika cha ‘Tribute To Maria’ lipo kwenye mkao wa utayari kuelekea Tanga, nahitaji oda yako tu kuendelea na misheni”Aliongea na kumfanya Maksim kutabasamu.
“Kama nilivyotarajia mpango utaenda sawa , Mkuu wa Alshabab kasemaje baada ya kusikia kifo cha mtoto wake?”
“Yupo ni mwenye hasira kubwa sana na hasira yake imefanya kumshawishi kwa urahisi mpaka kukubali mpango wetu”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli.
Kama Roma angekuwepo hapo angeweza kumfahamu mara moja huyo mwanamke na huenda asingefanya kosa ile juzi kumruhusu kumtoroka , alikuwa ni Aishapova.
Mtoto ambaye alikuwa akizungumziwa juu ya kifo chake ni Shedrack Kengeu ambaye halikuwa jina lake halisi, kwanza ni msomali na ni mara chache sana kukutana Msomali anaitwa Shedrack Kengeu, ukweli Shedrack alikuwa mtoto wa kundi la Alshabab ambaye alitumwa Tanzania kwa mishenni maalumu ya kuhakikisha kuna makubalianao ya kibiashara kati ya Kundi la kihalifu la ZoaZoa pamoja Alishabab kupitisha siraha kupitia mipaka ya Tanzania.
Miezi kadhaa iliopita Samweli Nguluma ambaye ni baba yake Benadetha alikataa kufanya biashara baina ya Alshababu na ZoaZoa kwa kuogopa serikali ya Tanzania kugundua , baada ya Samweli kutokubali dili hilo Alshababu kwa kumtumia Shedrack walimshawishi mke wa bwana Samweli Nguruma afahamikae kwa jina la Zuwena kumsaliti mume wake kwa kumuua na kisha awe mkuu wa kundi hilo na kisha afanye biashara ya kupitisha siraha za kivita kwenda kwa kundi la Alshabab.
Lakini kabla ya Zuwena kutimiza azma yake ya kumuua mpango wake ulivuja na Samweli Nguluma ndipo aliposhitukia mchezo mapema na kumuwekea mtego, mpango wa Zuwena ni kumuua Samweli nchini Congo siku tatu zilizopita na Samweli alitumia mtego huo huo kumnasa mke wake na ushahidi na hakumpa tena msahama zaidi ya kumchapa Risasi ya kichwa.
Taarifa ilipomfikia Mika kuhusu mama yake kupigwa risasi nchini Congo na Mzee wake ndipo alipotorokea Bagamoyo , lakini Alshababu hawakukata tamaa mara baada ya mpango A kufeli , hivyo walianzisha mpango B ambao ulikuwa ni kumtumia Mika,
Shedrack ambaye alipewa jukumu la mipango yote A na B alikuwa tayari na ukaribu sana na Mika kwa muda mrefu kwa kuhakikisha mipango yote inafanyika kwa wakati mmoja na ukweli pia ni Kwamba Shedrack hakuwa Shoga kama Roma alivyomuona bali alikuwa akiigizia ili serikali ya Tanzania isije kufatilia taarifa zake.
Sasa haikueleweka ilikuwaje mpaka Maksim kuweza kufanya mawasiliano na Kundi hilo la wapiganaji haramu , lakini mara baada ya Mika kumpiga risasi mtoto wa mkuu wa kosi hilo la Alshababu , Aishapova alitoa taarifa kwenda Alshababu kwamba mhusika wa kifo cha Shedrack Kengeu(Jina feki) ameuliwa na Roma.
Ilionekana kabla ya ujio wa Aishapova Tanzania walikuwa kwenye majadiliano ya siri , lakini ni hakika kwamba mkuu wa kundi hilo baada ya kupata taarifa ya kifo cha mwanae moja kwa moja itakuwa alijenga kisasi na Romampaka kumpelekea kutoa kikosi ambacho kimejificha mpakani Tanza na Kombora la kimiminika cha kirusi kilichopewa jina la Tribute To Maria.
“Vipi kuhusu Clark?”Aliuliza Maksim kwa kirusi.
“Princes amerudi nyumbani kwake, kwa uchunguzi niliofanya tumegundua kuna maabara ndani ya nyumba anayoishi”
“Endeleeni kumfatilia kwa umakini na jiandaeni muda wowote nitatoa maagizo ya kumteka”Aliongea kwa Kirusi.
“Bosi mpaka sasa nimeshindwa kukuelewa , kwanini unataka sana kumuoa Princess Clark licha ya kuonyesha utomvu wa nidhamu ninavyoona hapaswi kuwa sehemu ya wanafamilia wa Klyuchevsky”
“Unajua nini kuhusu mimi wewe .. simuoi kwasababu nampenda ila namuona kwasababu ya akili yake …”
“Akili?”
“Tumetumia akili nyingi pamoja na muda kutegeneza kirusi cha Tribute to Maria ,, kama mpango wetu ukiweza kufanikiwa hakuna nchi itakayoweza kutengeneza chanjo ndani ya mwaka mmoja , mtu anaeweza kuvuruga kila kitu ni Clark pekee, unachotakiwa kuelewa kirusi hiki kimetengenezwa na mwanafunzi wake ambaye yupo chini yetu na kama huyu Myahudi hatutomdhibiti atatengeneza chanjo ndani ya masaa machache na mpango kufeli”
“Kwahio unachofanya ni kuweza kumdhibiti asiweze kutengeneza Chanjo?”
“Upo sahihi , Familia ya Rothchild imekubali Clark aolewe kwa siri na familia yetu kwasababu wanaamini kwamba ataendelea kuwa na msimamo wake wa kutojihusha na utengenezaji wa siraha za kimaangamizi huku wao kuendelea kupata gesi asilia kupitia Nord stream , naweza kusema kwamba wanajidanganya ,Wolverine tuna mbinu nyingi za kuweza kumwendesha binadamu na kutufanyia mambo bila hata yeye kujielewa na huo ndio mpango , ni sawa na kupiga ndege wawili kwa jiwe moja , tutazuia utengenezwaji wa chanjo ya Tribute to Maria lakini pia tutaweza kutumia akili ya Clark kufanikisha uundaji wa siraha nyingine kubwa , Urusi ipo duniani kwa kuwa mbabe wa dunia na sio Wamarekani”Aliongea
“Boss unazungumzia Totem of Hypnotism katika kukontrol akili yake?”
“Nadhani unanipata vyema , angekubali kuoelewa na mimi bila shida yoyote nisingefikia huko”
“Lakini bosi vipi kuhusu Hades , uwezo wake lazima tuuzingatie?”
“Usiwe na wasiwasi mpango tuliouandaa ni kwa ajili ya kumdhibiti asifanye jambo la kijinga, amenichokoza kwa kunidhalilisha leo lakini nitamlipa kwa kumuelimisha nini maana ya nguvu ya Kluychevsky hata mtangulizi wake hakuwahi kutuchokoza”.
“Boss huu mpango kama utafanikiwa , tutakuwa ni wakuogopeka sana , mheshmiwa Raisi amekuwa ni mwenye kupinga mipango yetu , lakini baada ya kuona matunda ya mpango lazima atatoa kibali mwenyewe , naahidi nitakuwa mtu wa kwanza kumuua yule mwanamke Lilith, wapuuzi wale wanatusumbua sana , Wolverine lazima tuisimamishe Urusi itawale Dunia tena”Aliongea Aishapovakwa kujigamba.
ITAENDELEA.