Huyu Hades aka Roma Romoni keshaanza kuniharibu aisee, kanijaza ujasiri wa kumfuata mdada wa watu kwenye Dualis yake na kumsalimia na kisha kumwambia nimekuona dada na nimevutiwa nawe nikaona si vibaya kuja kukusalimia, kwa majina naitwa Putin lkn sio Putin mpiga mabomu mimi ni Putin wa Tz mpenda amani, dada akatabasamu kwa kucheka kidogo, nikamwambia kama hautajali samahani. Kisimu changu hakijawahi kuwa na namba ya mrembo kama wewe kama hautajali naomba angalau na mimi simu yangu kwa mara ya kwanza iwe na namba ya mrembo kama wewe tafadhali. Bila hiyana nikapewa namba, mambo yote haya shukraní kwa Hades