Mkuu mwendelezo badoLeo naelta mwendekezo stay tuned
MwendelezoLeo naelta mwendekezo stay tuned
Mmmh.SEHEMU YA 456.
Ni mwezi mmoja sasa umepita hakuna kubwa ambalo lilitoke, Rose alikuwa tayari ashaanza kujifunza mafunzo ya kijini na alionekana kuwa na matokeo mazuri kwa kutumia mbinu ambayo Roma aliweza kuelekeza.
Upande wa wanawake wengine Roma aliweza kumuelekeza mmoja mmoja namna ya kufanya ‘Meditation’ ili kuweza kupata ‘Reveletion’ au ufunuo juu ya mbinu za kuvuna nishati kati ya mbingu na ardhi.
Ni Edna pekee ambaye alikuwa hajaanza bado na yote hio ni kutokana na Roma kuona mwili wa Edna haukuwa tayari kuhimili hivyo ilimbidi aendelee kufanya mazoezi, alikuwa na wasiwasi kuzidiwa na wenzake lakini kwasababu Roma alimwambia hakuwa tayari ilibidi amsikilize.
Sophia na yeye umaarufu ulizidi kuongezeka mara baada ya kutoa albamu yake ya kwanza ambayo ilikuwa na nyimbo zilizofanya vizuri sana na wale waliomtabiria mema kuridhishwa na matokeo , lakini hata hivyo wanasema siku zote matarajio ni mazuri kuliko matokeo hivyo kuna wale ambao pia hawakuridhishwa kwa aina yake , lakini mzani uliegamia upande wa walioridhika.
Naam ilikuwa ni siku ya Jumamosi ya tarehe ishirini ya mwezi wa pili , siku hio kulikuwa na hafla fupi ya kumpongeza Sophia kwa mafanikio yake ya kimuziki lakini kubwa zaidi siku hio pia ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa , hivyo nyumbani kwa Edna na Roma kulikuwa na sherehe ambayo ilijumuisha watu wachache sana ,mathalani ndugu wa kifamilia ambao walijumuika kwa chakula cha cha mchana.
Ni muda wa saa saba kamili ndani ye aneo la bustani walionekana watu mbalimbali waliokuwa wameketi huku wakiongea kwa vicheko, alikuwepo Neema Luwazo na mtoto wake Donyi , Nasra ,Tajiri Azizi na mke wake pamoja na Kassimu mtoto wa Tajiri Azizi wengine waliokuwepo ni Roma Edna , Bi Wema bila ya kumsahau Lanlan ambaye alikuwa kivutio zaidi.
Baada ya nusu saa kupita alifika Omari Tozo ambaye alikuwa ameambatana na Queen ambaye tumbo lake lilikuwa lishaanza kujitokeza kutokana na ujauzito.
Roma ilikuwa mara yake ya pili kukutana na Queen , mara ya kwanza ilikuwa ni ndani ya hospitali ya Aghakani na ilikuwa kipindi ambacho alikuwa akiongea na Sauroni juu ya mwanamke anaefahamika kwa jina la Zoe Kovac , hivyo baada ya kumuona mrembo yule ndio mwanamke aliekuwa akimsumbua Omari , lakini mwanamke pia ambaye alikuwa na mimba ya Yan Buwen alishangaa , lakini kubwa zaidi alishangaa mara baada ya kufahamu Queen ni mtoto wa Mzee Alex.
Upande wa Queen pia alimkumbuka Roma , lakini awamu hii alionyesha aibu kidogo kuliko kipindi kile na huenda ni kutokana na ujauzito wake.
Omari alionekana kuwa na furaha , ijapokuwa Queen hakuwa amemkubali Omari kwa ajili ya ndoa , lakini walikubaliana kuwa marafiki na Omari alionekana kufa kuoza kwa mrembo Queen hivyo licha ya kwamba Queen alikuwa na mimba ya mwanaume mwingine , lakini alitaka kumuoa hivyo hivyo na kutaka mimba hio iwe ya kwake lakini Queen bado alikuwa na tumaini kwamba Yan Buwen wake angekuja kumrudia.
Blandina alifurahi sana mara baada ya kujua Omari alikuwa rafiki yake Roma , hakujua namna walivyokutana lakini alipenda urafiki wao isitoshe Omari alikuwa mtoto wa familia ya mkuu wa majeshi hivyo ilikuwa faida kwa Roma kuzungukwa na marafiki ambao wanaweza kumsaidia hata Tajiri Azizi alionyesha kufurahishwa na ukaribu wa Roma na Omari.
Edna mwenyewe alishangazwa na ukaribu wa hao wawili, ijapkuwa alitaka kujua namna walivyokutana , lakini alijiambia Omari na Roma hawana utofauti mkubwa , kwanza wote hawakuwa na aibu na ni waongeaji sana na mawazo ya Edna yalikuwa kama wa wengine tu walimuona Omari kutokuwa na aibu kama ilivyokuwa kwa Roma na alichekesha kila alipokuwa akiongea na ni kama alitawala maongezi , huku asilimia kubwa akimsifia Queen kuwa mrembo kuliko ya Edna.
Ilikuwa ni familia kamili hivyo kwa Sophia alifurahi uwepo wa kila mmoja aliefika kwa ajili yake ,ijapokuwa familia yake ilikuwa nchini Japani lakini alihisi watu waliokuwa wakimzunguka kwake ni familia tosha kabisa.
Stori mbalimbali ziliingiziwa, Donyi na Kassimu walionyesha walikuwa kwenye penzi moto moto hivyo ilikuwa ni jambo ambalo lilizungumziwa pia na ukizingatia Jestina na Tajiri Azizi walikuwepo, pamoja na Neema Luwazo ambaye muda si mrefu angekuwa na undugu utakaounganishwa na ndoa
Ilikuwa rahisi kwa tajiri Azizi kumkumbali Donyi katika familia , kwanza kabisa Kassimu ndio angekuwa mrithi wa familia , lakini pia upande wa Donyi alikuwa mrithi wa mali za mama yake hivyo walilandana kwa kiasi kikubwa kwa kuzingatia kwamba siku zote mtoto wa tajiri anamuoa mtoto wa tajiri mwenzake na ni mara chache tajiri kuolewa na masikini ni ukweli mchungu lakini ndio ilivyo.
Asilimia kubwa ya maongezi pia zilikuwa sifa kwenda kwa Edna
Wakati Stori zikiendelea geti lilifunguliwa na ikaingia gari aina ya V8 ya rangi nyeusi na alishuka Denisi kwenye gari hio huku akiwa ameshikilia furushi la mua Waridi ya rangi tofauti tofauti , ilioneysha alikuwa na taarifa ya kilichokuwa kikiendelea hapo ndani.
Ujio wake ambao haukuwa na mwaliko ulifanya watu kuwa kimya lakini hata hivyo Denisi hakuonyesha hali ya kutokujiamini zaidi ya kuwasogelea na kusaliamiana na kila mmoja na mwisho kabisa akamsogelea Sophia na kumkabidhi yale maua aina ya Roses fresh plant, Sophia hakupenda ila alipokea hivyo hivyo.
“Denisi hayo ni maua mengi sana umeweza kununua nadhani ni pesa nyingi umetumia nilitamani na mimi kumnunulia mpenzi wangu Queen kama zawadi lakini hela sina”Aiongea Omari.
“Bwana Omari unasema kwamba unashindwa kununua maua kama hayo , mbona thamani yake ni ndogo sana”Aliongea Tajiri Azizi
“Mzee nadhani hujaulizia bei ya haya maua hivi karibuni yamekuwa ghari mno na wenye bustani wengi wamekuwa wakiyasafarisha kwenda nje ya nchi kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa”
“Hilo naelewa kuna mmoja wa rafiki yangu ni kweli hivi karibuni aliongea kwamba maua ya Waridi yamepanda bei sana sehemu nyingi za dunia , hivyo uhitaji wake kuwa mkubwa na thamani kupanda , lakini hata hivyo sio lazima kumzawadia unaempenda na maua ya Waridi kwani kuna aina yingi za maua ambazo zinawakilisha upendo pia”Aliongea
“Imekuwa ngumu kwa hapa Tanzania kuweza kuhifadhi maua na Watanzania wengi hawajachangamka juu ya uthamani wa maua , kuna siku nilipotembelea Thailland na Singapore nilishangazwa na mashamba makubwa ya maua ya Roses , ilinitamanisha na kampuni yangu ya Maple kuwa na shamba moja lakini Watanzania wengi sio wenye kuzingatia kupeana zawadi za maua”Aliongea Neema , ilikuwa sawa kuongea hivyo kwani alikuwa mfanya biashara na siku zote wafanyabiashara kila kinachomzunguka anakiangalia kwa namna ya fursa.
Lakini ilikuwa ukweli kwamba ni mara chache sana watanzania kupeana zawadi za maua kama Zawadi, wanawake wengi wa Afrika wanachopenda zaidi ni pesa , pesa na pesa tena au vitu vya thamani kubwa maua watakwambia waachie Nyuki , yaani una mpenzi wako yupo Manzese ndani ndani huko umbebee zawadi ya maua unaachwa siku hio hio.
Kwa wenzetu ni tofauti sana lakini hata hapa Tanzania ustaarabu huo upo lakini kwa watu wachache sana , ndio maana ukitembelea majiji makubwa kama Paris , Guanzhou au Seoul utakuta bustani zipo kila kona katikati ya jiji na uzaji wa maua ni biashara nzuri tu.
Chakula kiliandaliwa na wahudumu waliopewa tenda ya kazi hio ,walikuwa ni wafanyakazi kutoka moja ya hoteli ambayo ilikuwa chini ya umiliki wa Edna.
Baada ya kufurahia chakula pamoja mpaka kumaliza , Denisi alisimama na kisha akamsogelea Sophia.
“Sophia nimekuletea zawadi nyingine , hizi siku chache sitokuwepo Tanzania kwa ajili ya misheni maalumu hivyo naomba nikupatie leo hii hii katika siku yako maalumu ya kuzaliwa”Aliongea Denisi bila ya aibu mbele ya watu wote na kufanya kimya kitawale.
Kilikuwa ni kiboksi cha rangi nyeusi ambacho kwa haraka haraka mtu angegundua ndani yake kulikuwa na nini.
“Asante sana kwa zawadi , lakini siwezi kuipokea”Aliongea Sophia huku akiangalia kiboksi ambacho ndani yake kama hakikuwa na mkufu wa dhahabu basi ni saa au Pete.
Watu wote walikuwa kimya kuangalia namna tukio hilo linavyochukua nafasi yake , lakini hata hivyo walishangazwa na namna ya Denisi asivyokuwa na aibu , lakini kwa wakati mmoja walishangazwa na namna Sophia alivyokataa zawadi ile.
“Denisi unaboa sana ,inaonyesha kwenye maswala ya wanawake upo kama mimi tu na Roma hapa anatushinda kwenye vitu vingi..”Aliongea Omari kama kawaida yake ya kuvunja ukimya.
Denisi mara baada ya kusikia maneno yale alimgeukia Roma na kumwangalia kwa muda mfupi kisha akamgeukia Sophia kwa mara nyingine.
“Sophia sijui ni sababu gani ambayo inakufanya unikatae tumejuana kwa muda mrefu sana na tumepitia mengi na hata ulivyonikataa kipindi kile niliona labda ni kwasababu haukuwa tayari , lakini vipi kuhusu sasa huna sababbu yoyote ya kunikataa kwani hata mpenzi huna, nini kinakuzuia kufanya maamuzi”Aliongea Denisi bila kujali kuna watu wazima waliokuwa wamezunguka.
Ukweli ni kwamba Sophia alimkataa mara nyingi Denisi na sio mara mooja tu ni zaidi ya mara mbili , kilichokuwa kikimuuma sana Denisi ni kwamba Sophia sababu kubwa iliokuwa ikimpelekea kumkataa ni Roma.
Ikumbukwe Denisi na Sophia walishawahi kufanya mafunzo pamoja na Kung Fu Nchini China katika moja ya Temple maarufu na huko ndipo walipofahamiana na hata Denisi kuweka hisia zake wazi kwa mara ya kwanza na ndio mara ya kwanza ambayo Sophia alimkataa Denisi.
Sophia alikuwa na hasira kwani aliona ni kama Denisi anamdhalilisha mbele ya kundi la watu.
“Sababu kubwa ni kwamba sikupendi Denisi”Aliongea Sophia na kauli yake ilikuwa ikionyesha kukasirika na Edna alijikuta na yeye kuona Denisi anavuka mipaka na aliona aingilie.
“Denisi huwezi kumlazimisha Sophia akupende , hivyo usimsumbue tena”Aliongea Edna.
“Denisi nadhani alichoongea Shemeji yako ni sahihi , Sophia hakupendi na huwezi kumlazimisha na hata hivyo ana ndoto nyingi za kutimiza hivyo nadhani ni sababu pia ya kutotaka kujihusha na mapenzi”Aliongea Blandina.
“Mimi siamini hio ndio sababu kubwa”Aliongea Denisi na kufanya watu kumwangalia kwa shauku , huku wengi wao wakisisimkwa na mwili kwani hali haikuwa ya kawaida na walishangazwa na ukiburi na kujiamini kwa Denisi.
“Naamini Sophia kuna mtu anampenda ndio maana hataki kunikubalia”Aliongea Denisi huku akimwangalia Roma.
Ndio Denisi anajua Sophia anampenda Roma na Sophia mwenyewe ndio aliemwmabia hivyo , na ilionekana hata ujio wake siku hio ulikuwa ni kutaka kumchokoza Roma mbele ya Edna mke wake , lakini pia mbele ya wazazi wa Roma.
Denisi alikuwa akijua fika Sophia hakuwa na uhusiano wa kindugu na Edna licha ya kwamba watu waliwachukulia kama dada na mdogo wake , mwanzoni ingeweza kufahamika Edna ni dada kamili wa damu kwa Sophia lakini mara baada ya Marehemu Adebayo kujulikana hakuwa na uwezo wakumzalisha mwanamke hivyo moja kwa moja ni kwamba Edna na Sophia ni wa damu tofauti na kama ni udada basi ni ule wa hiari ,sasa yote hayo Dennisi alikuwa akiyajua na aliamini huenda Sophia mapenzi yake juu ya Roma ni ya siri na Edna hayafahamu , hivyo kufahamu kuna kajisherehe aliona yes ndio nafasi nzuri ya kumfanya Sophia aweke wazi kile anachojaribu kuficha.
Sasa kitendo cha Denisi kuongea vile halafu akamwangalia Roma ni kama alikuwa akitoa majibu.
Watu wote walimwangalia Roma na kisha wakamgeukia Sophia wakisubiria jibu .
“Hapana! Msisikilize kwani sina mwanaume ninaempenda kwa sasa nikwamba tu sitaki kuwa na mahusiano na Denisi kwani hana vigezo ninavyovitaka”Aliongea Sophia ili kutuliza ile hali.
Edna alimwangalia Sophia kwa namna ya kumchunguza na kisha akamgeukia Roma aliekuwa kimya na kumwangalia
“Hii topic na tuachane nayo na Sophia usimzingatie sana Denisi na akiendelea na ujinga nitahakikisha anamwaga damu hapa ndani kabla ya kuondoka , Denisi usinichokoze kwasababu unahisi siwezi kukufanya chochote kwasababu kuna wazazi hapa”Aliongea Roma akiwa siriasi
“Roma usiongee hivyo Denisi ni mdogo wako?”Aliongea Blandina
“Jamani jamani mbona tulikuwa tukicheka hapa na kufurahi nadhani tuachane na habari za kuuana kwa sasa”Aliongea Jestina mke wa tajiri Azizi na Roma alibakia kimya lakini Omari alijikuta akipata msisimko kwa mtifuano wa Roma na Denisi ndugu wa damu.
Kasimu yeye alionekana kuwa na wasiwasi na alimpa ishara baba yake kuongea neno ili kutuliza hali ilioanza kubadilika.
Lakini Tajiri Azizi hakutaka kusimama upande wowote na hio yote ni kutokana na kwamba alikuwa akifahamika kama tajri lakini yote hio ni kutokana na kuweza kuoa katika familia ya Mzee Atanasi ambaye alikuwa na utajiri mkubwa ni rahisi kusema kwamba nusu ya mali alizokuwa akiendesha ni za Blandina na nusu ni za mke wake na familia , hivyo hakutaka kujiingiza kwenye ugomvi wa Denisi na Roma kwani pia alikuwa akijua siku zote Denisi ni chaguo la baba yake Raisi Senga kuliko Roma ambaye alikuwa chaguo la babu yake Afande Camillius Kweka.
Denis alifungua kile kiboksi na kuonyesha kilichokuwepo ndani na pete mbili za madini ya Platinum zilionekana ziking’aa sana zikiashiria ni za bei ghali.
“Sophia nataka uniambie sababu ambayo inakupelekea kunikataa”Aliongea Denisi kwa mara nyingine lakini muda ule ule chupa ilirushwa kuelekea upande wake kupiga kile kiboksi lakini Denisi alikuwa mwepesi kwani palepale aliizuia na ikadondoka chini na kupasuka.
Alierusha hakuwa mwingine bali ni Roma Ramoni na alionekana kuanza kukosa uvumilivu uwepo wa Denisi.
“Denisi ondoka nyumbani kwangu la sivyo nitakutoa kwa nguvu”Aliongea Roma kwa amri kali na kufanya watu kuingiwa na ubaridi
“Usiniharakishe na nitaondoka kama unavyotaka lakini lazima nithibitishe jambo moja”Aliongea na kisha palepale alimwinamia Sophia aliekuwa ameketi.
“Sophia sitokulazimisha tena nikitoka hapa lakini nataka uapie kwa mbingu na Ardhi mbele ya kila mmoja kama humpendi Roma”Aliongea kwa sauti na kila mmoja aliweza kusikia na kuwafanya kuvuta pumzi na kumwangalia Sophia kwa jibu ambalo anakwenda kutoa.
SEHEMU YA 457
Kwenye watu waliokuwa na wasiwasi muda huo alikuwa ni Blandina , ni kama alikuwa akitabiri kuna jambo baya sana linakwenda kutokea hapo ndani ,alitamani amwambie Denisi aondoke lakini hakuwa na uwezo huo , lakini pia aliogopa hasira aliokuwa nayo Roma kwani ilidhihirika kwa kila mmoja.
Uzuri ni kwamba muda huu Lanlan alikuwa upande mwingine akicheza na Qiang Xi kwa kutumia Drone yake hivyo hakuona kinachoendelea hapo.
Lakini wengine wote walionyesha wasiwasi , Neema licha ya kwamba alikuwa akimpenda Roma lakini hakuwahi kumuona akiwa na hasira namna hio na sio kwake tu kwa wengine wote walitulia kimya huku wakiomba Roma asichukue hatua yoyote.
Upande wa Sophia sura ilishabadilika na kuwa nyekundu , ni kweli alikuwa akimpenda sana Roma hivyo alishindwa kutamka kama hakuwa akimpenda Roma waziwazi , kila alipokuwa akijaribu kuongea alikosa nguvu na alijua kabisa Denisi siku hio alipanga kumkomesha.
“Nikijibu simpendi si itamaanisha lazima niachane nae kabisa na kujikatia tamaa , lakini hata hivyo sio kama naweza kupata nafasi ya kumfungukia kama nampenda , kwanini nashindwa kujielezea mbele yake kwamba simpendi na hali hii ikaisha?”Maswali yalipita kwenye kichwa cha Sophia, tokea siku anafika kuishi na Roma mpango ulikuwa ni kuwa mke wa pili na si vinginevyo na mapenzi yake aliyaficha kwa kumchukulia Roma kama kaka yake , lakini ukwelia alikuwa akimpenda mno
Ukimya wa Sophia na mwonekano wake ulifanya kila mmoja kujua kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya moyo wake , lakini hata hivyo ilikuwa kawaida kwa Roma kupendwa na wanawake wengi na sio jambo jipya na hata muda huo alikuwa amezungukwana wachumba , lakini swala la Sophia lilikuwa na utofauti kwani Edna na Sophia walitambulika kama dada na kaka na ndio maana hali ya hewa ilikuwa yenye ubaridi licha ya kwamba jiji la Dar es salaam lilikuwa na joto.
Edna mapigo ya moyo wake yalikuwa yanadunda kwa kasi , kwenye moyo wake alishajiapiza siku Roma akitoka kimahusiano na Sophia hatoangalia nyuma na wataachana kwa namna yoyote ile.
Ukweli ni kwamba alikuwa ni mwanamke mvumilivu lakini kwa kile kilichokuwa kikiendelea hapo ndani kama nimwanamke ambaye anaendeshwa na hisia asingeweza kuendelea kukubali yanayoendelea kwani ni kama udhalilishaji, alimchukia hata Denisi alieanzisha hio mada ghafla.
Edna sio kwamba hakujua kama Sophia hampendi Roma alikuwa akijua sana tu tokea siku aliogundua Sophia na Roma walimdanganya ka kujifanyisha ni ndugu lakini vile vile mara baada ya kusikia habari za ndoa kutoka kwa mama yake Sophia , lakini aliamini kwa kumchukulia Sophia kama mdogo wake ingemfanya Sophia kutojihusisha kabisa kimapenzi na Roma, huo ndio mtazamo wake na ni kweli Sophia alijitahidi kyaficha mahaba yake kwa Roma ili asilete mgogoro na Edna.
Edna alijikuta akipunguza wasiwasi mara baada ya kuhisi mkono wake umeshikwa chini ya meza na aligundua ni Roma aliekuwa amemshika na aliinua macho na kumwangalia na Roma alitumia ishara ya kumwambia kwamba asiwe na wasiwasi.
Edna alijua Roma alikuwa akijaribu kumfariji lakini haikuwa ikisaidia kwani wote walikuwa wakihitaji kusikia majibu kutoka kwa Sophia, lakini kubwa zaidi alijua kwamba alikuwa akiujua ukweli na alishindwa kumlaumu Sophia katika hilo kwani swala lakumpenda mtu ni swala ambalo lipo nje ya uwezo wa mtu.
“Sophia nadhani kimya chako ni jibu tosha ila nashindwa kuwaelewa nyie wanawake mnampendea nini huyu mtu kwanza kabisa sio muaminifu na amezungukwa na michepuko kibao lakini bado tu mnampenda”
“Huna haja ya kumsema vibaya Bro Roma na kingine sio lazima nikujibu kwa kila unachouliza kwani wewe sio msemaji wa maisha yangu na jibu nishakupa kwamba sipo tayari kuwa kwenye mahusiano na wewe”Aliongea Sophia kwa hasira.
“Hahaha… au nipo kizamanni inashangaza sana wanawake kumg’ang’ania mtu ambaye sio mwaminifu na kuacha yule anaewapenda kweli”
Aliongea, wakati wengine wakitaka kujua mwisho wa mazungumzo hayo Edna na Neema wenyewe walijiuliza kwanini wametokea kumpenda Roma licha ya kwamba alikuwa sio mwaminifu maana maeneno ya Denisi yalikuwa ya kweli ni kwamba tu aliyazungumza wakati ambao sio sahihi.
Roma aliamua kupunguza hasira zake kwanza na kukaa kimya huku akionyesha kufikiria namna ya kutatua hali hio.
“Denisi hivyo ndio mahusiano yalivyo na pia ndivyo wanawake walivyo na hupaswi kuwaelewa sana , inaonyesha ulikuwa na ukaribu na Sophia wa muda mrefu lakini hio isikupe sababu ya kwamba akupende licha ya kwamba wewe unampenda”
“Kaa kimya wewe chongo unajua ninni kwanza”Aliongea Denisi
“Ndio sijui kitu kwasababu hata mwanamke ninaempenda ananikataa licha ya kwamba nimekamilika na familia yangu ni kubwa pia , lakini naelewa sababu kwanini Sophia hakupendi”Aliongea
“Oh! Hebu nieleweshe”
“Ni rahisi sana , hutakiwi kumfosi licha ya kwamba alikukataa , kama kweli unampenda furaha yake ingekuwa kipaumbele, ni kama mimi tu ijapokuwa Queen amekuwa akinikataa lakini sikumlazimisha zaidi ya kwamba nilitamani aendeelee kuwa na furaha , sijui Roma ana wanawake wangapi na ni mwaminifu kwa kiasi gani lakini naamini kwa tabia yako ya kulazimisha vitu hata visivyokupenda hakuna mwanamke ambaye anaweza kukuvumilia”Aliongea Omari.
“Kaa kimya na acha kuwa mnafiki , unaongea hivyo kwasababu Roma ni rafiki yako”
“Haha.. wewe ni nani wa kuniambia ninyamaze unajifanyisha mjuaji lakini kichwani huna kitu”Aliongea Omari.
“Unaongea kishari unataka ngumi sio?”
“Acha ukijogoo Denisi , wewe ni mtoto sana kwangu”Aliongea
“Haha.. Omari usijifanyishe kwasababu baba yako ana cheo serikalini uone kwamba siwezi kufundisha adabu , Wewe huna cha kunitishia mimi”
“Jamani mnisamehe ninakwenda kuharibu wakati huu mzuri lakini hili lipuuzi siwezi kulivumilia tena”Aliongea Omari huku akionyesha kupandwa na hasira.
Mpaka hapo ugomvi ulihama kutoka kwa Roma kwenda kwa Omari na walianza kutunishiana misuli , Omari alisimama vile vile Denisi alimsogelea huku wote wakionyesha kuwa na hasira.
Omari hakumpenda Denisi kutoka na ukaribu wake na yan Buwen ambaye alikuwa ni adui yake namba moja na Denisi hakumpenda Omari kutokana na kuwa na ukaribu na Roma ambaye ni adui yake namba moja.
Omari alikuwa na nguvu za kijini levo ya Nafsi lakini Denisi vilevile mwili wake ulikuwa umefanyiwa sayansi na Yan Buwen hivyo kama ni kupigana ingekuwa ngumu kutabiri mshindi.
Omari akikasirishwa anakuwa mtu mwingine kabisa na alijiambia siku hio hamuachi salama Denisi na palepale alimpiga Denisi ngumi ya kifua na kumrudisha nyuma.
Kitendo kile kiliwafanya watu wote kusimama na kurudi nyuma huku macho yakimwangalia Roma na Tajiri Azizi pamoja na Kasimu waamue ugomvi kwani ndio waliokuwa wanaume , lakini Roma alikuwa amekaa ametulia akiangalia kwa hamu kile kinachokwenda kutokea , upande wa tajiri Azizi hakuwa na nguvu za kuamulia na Kassimu hivyo hivyo hakutaka kununua ugomvi wa watu wazima.
Denisi baada ya kurudi nyuma mara baada ya kupigwa ngumi ambayo haikuwa na madhara kwake , Omari hakutaka kumchelewesha alikuja na teke la hewani akidhamiria kumpiga Denisi kwenye mbavu lakini Denisi alikuwa ametarajia pigo lake kwani alidaka mguu wake na mkono mmoja huku akitabasamu kifedhuli.
“Unapata wapi ujasiri wa kupambana na mimi na vinguvu vyako vya kijini ulivyokuwa navyo”Aliongea Denisi na palepale kwa mkono wa kushoto alimfyatua Omari kwa kumrusha juu kupitia mguu wake aliokuwa ameushikilia.
Lakini Omari alitua salama kwani alitumia uwezo wa kijini kujikontrol , lakini hata hivyo alihamaki kwani uwezo wa Denisi ulikuwa mkubwa.
“Naona matokeo ya Yan Buwen kuufanyia mwili wako majaribio imekufanya kuimarika sana”Aliongea Omari kwa kebehi.
“Ushaanza kujitetea sasa”Aliongea Denisi huku akimpa ishara Omari kuja tena na pigo lingine , ilionekana ni kama amekuja sehemu hio kuamsha ugomvi kwani alionyesha mchecheto mno.
Queen alikuwa na wasiwasi mno kwa kile kinachoendelea na kujiuliza Denisi ana uhusiano gani na Yan Buwen na haikuwa kwake tu kila mmoja hakudhania mambo yangebadilika mpaka kufikia hapo na yote hayo ni ujio wa Denisi ndio uliovuruga kila kitu.
“Roma famya kuwaamulia bwana sio vizuri kuangalia watu wazima wakipigana mbele yetu”Aliongea Tajiri Azizi.
“Denisi acheni mnachokifanya mara moja huoni mnajidhalilisha nyie ni watu wazima”Aliongea Blandina lakini Denisi alionyesha hakuwa tayari kuliacha hilo lipite , hata hivyo ujio wake hapo ndani ulikuwa ni kutafuta ugomvi ili amkomeshe Roma ,lakini kwasabau Omari ameamua kujiingiza alijiambia ni kheri aanze nae kwanza hata hivyo Yan Buwen alikuwa akifahamu Omari ni zao la Hongmen na yupo uraini kwa misheni ya kumfatilia hivyo Denisi alijiambia akimuua huyu atajiongezea credit mbele ya Yan Buwen.
“Vipi umeufyata mkia?”Aliuliza Denisi kwa dharau na kumfanya Omari kupandwa na jaziba zaidi kwani kwenye maisha yake hakupenda dharau lakini pia Denisi alikuwa mtoto mdogo sana kwake.
“Nitakuonyesha mbwa wewe”Aliongea Omari na palepale alishika jicho lake la kushoto kwa namna ya kuliziba na alipotoa mkono jicho lilikuwa mkononi.
Kitendo kile kilimuogofya mno Queen lakini pia wengine wote walishangazwa na tukio lile ,ijappokuwa watu wengi walikuwa wakijiuliza ni kwa namna gani Omari aliweza kupona jicho lake kabisa lakini kulitoa ilikuwa tukio la ajabu mno.
Roma alijikuta mwili ukimsisimka , alikuwa akijua nini maana ya Omari kufanya vile.
Omari uwezo wake uliongezeka mara mbili yake na upande wa Denisi ni kama na yeye alifunguliwa uwezo wake wote na muda huo huo walianza kushambuliana kwa kasi kiasi kwamba ni Roma pekee aliekuwa na uwezo wa kuona namna wanavyo pambana ila wengine wote macho yao yalikuwa ya kibinadamu hivyo spidi waliokuwa wakitumia iliwafanya kuona vivuli tu na upepo ukipeperusha maua.
Omari alirusha ngumi wa haraka sana kumlenga Denisi maeneo mbalimbali ya mwili , alikuwa akitumia spidi kubwa sana lakini Denisi na yeye hakuwa vibaya kwenye kupangua.
Wanafamilia waijikuta wakiwa kwenye mshituko kwa mabadiliko hayo , ijapokuwa walishindwa kujua nani atashinda kutokana na kutoweza kuona namna ngumi zinavyotembea lakini namna walivyokuwa wakipambana ilichanganya.
“Roma waamulie bwana, mwisho wao utakuwa mbaya na mmoja anaweza kuumia na ikawa shida nyingine”Aliongea Tajiri Azizi kwa namna ya kumuamrisha Roma.
“Unafikiri nani atapoteza pambanno”Aliongea Roma kwa namna ya kuonyesha kwamba alikuwa akifurahia kinachoendelea hata hivyo matukio ya aina hio kwake yalikuwa yakawaida sana.
“Mdogo wako anaweza kuwa kwenye hatari , Omari ni kama jini”Aliongea Tajiri Azizi.
“Sio kweli Omari ndio atazidiwa”Alijibu na kuwafanya kushangaa , walikaa upande wa Denisi kutokana na namna Omari alivyotoa jicho lake kwa namna ya kimazingara hivyo walimuona Omari kama kiumbe cha ajabu.
Kitendo kile kilimfanya hata Queen kuzidi kutokumpenda Omari na kuanza kumuogopa alijiambia kheri yake Yan Buwen baba wa mtoto wake ambaye yupo tumboni.
Muda ule ule Omari alipigwa ngumi nzito ambayo ilimpata kifuani karibu na bega na kumfanya kwenda kudondoka mita kadhaa kutoka ilipo Swimming pool na hapo ndipo walipoona shati alilovaa Omari lilikwisha kuchanika upande mmoja.
Pigo lile lilimfanya sasa Roma aone uwezo halisi wa Denisi maana Omari alionyesha kushindwa kumhimili licha ya kwamba uwezo wake wa nguvu za kijini ulikuwa mkubwa.
Omari alijinyanyua kwa kujilazimisha na kusimama wima huku akitema damu , pigo alilipigwa na Denisi lilionyesha kupelekea viongo vya ndani kuathirika.
“Bado unataka kuendelea?”Aliuliza Denisi.
“Sikuwa makini ndio maana nikashindwa kukwepa ngumi yako , nisogelee tena kama unajihisi una uwezo mkubwa”Aliongea Omari huku akionyesha hali ya kutotaka kushindwa.
“Nadhani unakitafuta kifo kabisa ngoja nikumalizie kabisa nisibakiwe na deni”Aliongea huku akionyesha hali ya kuwa na hasira mno.
“Jamani inatosha sasa mtaumizana zaidi mkiendelea hivyo”Aliongea Blandina huku sauti yake ikiwa ya kitetetemshi alionyesha wasiwasi usiokuwa na kifani na alitaka Roma awazuie wasiendelee.
“Bro Roma wazuie wasiendelee”Aliongea Sophia ambaye sasa alianza kujawa na wasiwasi.
Upande wa tajiri Azizi na mke wake walijikuta hata wakijutia kuja kwenye hafla hio kwani waliamini kama kuna jambo lolote baya litakalotokea lazima wangetakiwa kutoa maelezo.
“Roma Omari ni rafiki yako , kwanini usimsaidie”Aliongea Tajiri Azizi, ukweli hakuwa na uwezo wa kumlazimisha Roma kwani alikuwa akijua hakuwa mtu wa kawiada na vile vile alikuwa akisikia habari kwmaba Omari pia hakuwa mtu wa kawaida na ndio maana hata mabadiliko hayo hakushangaa sana lakini alihofia matokeo.
“Naweza nikaingilia hapa , lakini ikanipelekea kumuumiza kabisa Denisi na wote hapa mnaweza kunilaumu kwa kusema nimempiga mdogo wangu mimi lawama sitaki”Aliongea Roma
“Roma waamulie sitojali kitakachotokea una sapoti yote kutoka kwangu”Aliongea Blandina na kumfanya Roma atabasamu ndio alichokuwa akitaka hivho , alipanga muda wote kama ni kumuua Denisi angalau apate sapoti kwa mama yake mzazi.
“Mama lakini naweza kumuaa kabisa kutokana na nguvu zake ambazo sio za kawaida”Aliongea Roma na Blandina alitaka kuongea kitu lakini mdogo wake alimzuia.
“Dada kwa mwonekano wa Denisi sidhani ni wakati wa kumuonea huruma, inaonekana hata akili sio yake tena , angalia alivyo”Aliongea mke wa tajiri Azizi.
“Najua lakini Denisi na Roma ni ndugu ..”
Mapigano sasa yalibadilika na ilikuwa ni Roma na Denisi sasa na Omari ilibidi atulie pembenni akiugulia maumivu , purukushani hizi zilimfanya hata Lanlan na Qiang Xi kufika eneo la tukio na Lanlan alisogea mbele kabisa huku akiwa amekodoa macho akishuhudia mtanange
Lanlan ndio aliekuwa akiona kabisa kile kilichokuwa kikiendelea , alikuwa na macho ambayo hayakuwa ya kwaida hivyo aliweza kuona namna baba yake anavyopigana na baba yake mdogo na alionyesha kufurahishwa na tukio hilo na kumfanya Edna kuwa na wasiwasi.
Roma alishangazwa na kitu kimoja kuhusu Denisi , ilionysha ni kama hakuwa kwenye akili yake timamu ni kama miezi kadhaa alioweza kumuadhibu akiwa na maambukizi ya kirusi cha Wolverine, alitafsiri kama athari zilizotokea kwa sayansi iliofanywa ndani ya mwili wake na Yan Buwen au alihisi huenda akili yake ilikuwa ikitawalia na Yan Buwen kwani Denisi alikuwa hana huruma kabisa kwenye macho yake na alimwangalia Roma kama Simba aliekuwa mbele ya kitoeo.
Inaawezekana kabisa kwa Yan Buwen kufanya hivyo, teknolojia ilikuwa kubwa sana na mtu kufanyiwa upasuaji na kuwekewa Chip ndani ya ubongo haikuhitaji utaalamu mkubwa na ni mchakato unachokua mwezi tu kukamilika.
Roma alijiambia lazima Yan Buwen alichukua tahadhari kila anapotengeneza mwanajeshi kwa kuwawekea sayansi ambayo ingemuewezesha kuwaendesha atakavyo na hicho ndicho kilichoonekana kwa Denisi.
Mpaka hapa Roma alijiambia hana namna zaidi ya kumuua Denisi kwani asipofanya hivyo anaweza kuwa hatari zaidi kwa usalama wa familia yake maana sasa Denisi hakuwa binadamu bali alikuwa ni kama Drone ya kijeshi inayoendeshwa kwa ajili ya kushambulia
“Roma kama usingekuja kunisaidia nilikuwa na mpango wa kuchapa Raba”Aliongea Omari akikubali kushindwa.
“Niliamini ungepambana mpaka pumzi yako ya mwisho?”
“Wewe hayo ni maamuzi ya watu wapumbavu , ninapenda maisha yangu na isitoshe Queen sijamuoa bado”Aliongea Omari.
Denisi alimsogelea Roma kwa kasi na Roma hakutaka kumpa nafasi yakumfikia na yeye alimsogelea na alipomkaribia aliachia teke ambalo lilimpiga Denisi kwenye tumbo.
Ijapokuwa Denisi alikuwa na uwezo mkubwa kutokana na uwezo aliopewa na Yan Buwen lakini hakuwa akimfikia Roma hata kwa Robo ya uwezo wake..
Teke lile lilimrusha mbali na kwenda kutua kwenye ukuta , lakini hakutaka kukata tamaa aliamka tena na kumsogeleaRoma kwa kasi huku nguvu ya ajabu ikianza kumzingira Denisi na palepale Roma alihisi kitu kisichokuwa cha kawaida ilikuwa ni nguvu ambayo hata Yan Buwen alitumia katika kupambana.
Nguvu inayotokea kwenye Godstone , ni nguvu ambayo Drogba alikuwa nayo na Clone ilikuwa nayo pia lakini kwa Denisi ilikuwa kubwa zaidi.
Roma baada ya kuona nguvu ya Denisi imejiongeza maradufu hakutaka kuzembea na yeye aliita nguvu ya kijini ya kimaandiko na kisha alitengeneza ngao kama kioo na kuisukumia aliposimama Denisi, upande wa Denisi alifanya hivyo hivyo aliachia pigo ambalo ni kama mwanga wa Radi kuelekea upande wa Roma hivyo ngao ya Roma ilikutana na shambulizi la Denisi.
Roma hakutaka kumchelewesha alikusanya nguvu ya kijini na kutengeneza shambulizo ambalo lilikuwa kama kimbunga cha mvuke na kusukumiza upande wa Denisi.
Ile ngao ilizuia pigo la Denisi na ikaruhusu shambulizi la Roma kumsogelea Denisi kwa kasi na alionekana kuchelewa kulizuia kwanni palepale upepo ambao ulikuwa kama mvuke ulimzingira kwa kasi na akawa katikati, Denisi alijikuta akitoa kelele akiashiria kuhisi maumivu makali ya kuungua , lakini licha ya hivyo Roma hakumuonea huruma na kadri nafsi yake ilivyokuwa ikinuia ndio maumivu yalivyokuwa yakizidi kumuathiri Denisi.
Ilishangaza kwa waliokuwa wakiangalia kwani hakuna walichoweza kuona zaidi ya kumuona Denisi akililia huku akitoa machozi makali ya kuhisi maumivu.
“Roma naomba umuache….”Blandina alijikuta akitoa machozi kwa tukio lile aliamini lolote litakalomtokea Denisi angewajibika na kila kitu kingebadilik.
Roma alijiambia hana haja ya kuacha na hakutaka kumuacha Denisi hai , aliamini kufanya hivyo ndio kujiweka hatari zaidi kwa Yan Buwen kuzidi kuwa na nguvu.
Watu wote walishangazwa na tukio lile na kujikuta wakitamani Roma aache anachokifanya lakini Lanlan alipiga makofi ya Shangwe huku akimwigiza Roma kwa kila alichokuwa akifanya, akizungusha mikono alikuwa akifanya hivyo hivyo kwake haikuwa hofu bali fursa ya kujifunza.
Edna baada ya kuona kitendo kile alimsogelea Lanlan kwa namna ya kutaka kumzuia asiige kinachofanyika lakini aligusa hewa kwani Lanlan alimkimbia na kwenda kusimama upande mwingine na Edna alipotaka kumfuata Sophia alimzuia na kumwambia amuache.
Denisi mara baada ya kuona hawezi kusogea kutokana na nguvu isiokuwa ya kawaida kumshika miguu huku akijihisi kuungua alijikuta bila ya kupenda akipiga magoti huku akitoa machozi ya maumivu na Roma alitabasamu kifedhuli kwani ndio alichotaka
Lakini sasa muda ule ule Denisi alisimama kwa mara nyingine na upande wa Roma kila alipojaribu kuitwa nguvu za kijini alishindwa kabisa hivyo hata kile kimbunga cha kijini cha mvuke kiliacha kumzunguka Denisi.
Muda ule ule wakati akijaribu kuita nguvu za kijini alishindwa kabisa na aliweza kushuhudia Denisi akitoka aliposimama na kumsogelea Blandina mama yake kwa spidi ya ajabu na kumlenga na ngumi kali kifuani eneo la sehemu unapokaa moyo na ngumi ile kuchangua kifua na damu kusambaa huku Blandina akitupwa mbali.
“Mamaa..!!”Roma alijikuta akitoa ukulele mara baada ya kushuhudia Denisi akimuua mama yake mbele yake huku yeye akishindwa kufanya chochote.
SEHEMU YA 458.
Ukweli ni kwamba alichokuwa akikiona Roma sio uhalisia kwamba kilikuwa kikitendeka , watu wote walishangaa kwanini alikuwa vile , Denisi hata yeye alishangazwa na mabadiliko ya Roma lakini hakutaka kujiuliza mara mbilimbili kwani alitoweka palepale baada ya kupata mwanya.
Wakati Denisi alivyokimbia Roma hakuweza hata kutambua nini kinatokea , lakini kile alichokuwa akiona sio uhalisia na alikuwa akiongea mwenyewe kama vile mtu aliechanganyikiwa ghafla.
“Roma unafanya nini?”Omari alikosa uvumilivu na kumsogelea Roma lakini Roma hakujibu zaidi ya kuendelea kuwa kimya na kuongea mwenyewe huku maneno yake yasisikike.
Watu wote walijikuta wakianza kujawa na wasiwasi kwa kile kinachomtokea Roma kwani Denisi ashakimbia lakini Roma alibakia kama amechanganyikiwa.
Roma aliendelea kumuona mama yake akiwa amepoteza maisha kwenye akili yake huku akiwa amelala chini na Denisi kupotea.
“Mama…!”Aliita huku akisogea mbele akitaka kumshika mama yake lakini palepale alipotaka kumkaribia tu kwa kumgusa alitoweka na kujikuta akishika ukuta na hapo hapo akili yake ilirudi kwenye uhalisia na baada ya kugeuka aliposimama mama yake alijikuta akivuta pumzi ya ahueni huku akijidharau na aliweza kugundua ilikuwa ni ‘Illusion’ na alichokuwa akiona ni uhalisia mdanganyifu.
Edna na Lanlan ndio waliokuwa wa kwanza kumkimbilia na kumshika na Roma aligeuza macho yake na kuwaaangali.
“Hubby nini kimekutokea?”Edna aliuliza huku akimwangalia Roma huku machozi yakianza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake.
Roma alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kumshika Lanlan kwenye kichwa.
“Nipo sawa kuna kitu kimenitokea ila nimekuwa sawa”Aliongea .
Roma maumivu aliosikia aliposhuhudia Blandina mama yake akipoteza maisha mbele yake yalikuwa yasio ya mfano na mpaka hapo alijua ni kwa kiasi gani alikuwa akimpenda mama yake.
Kila mmoja alivuta pumzi ya ahuenni mara baada ya kuona hakuna aliekufa hapo ndani kwani ingekuwa tatizo lingine kabisa , Roma aliangalia juu angani kwa dakika kadhaa na kisha akawageukia.
“Nitarudi muda si mrefu kuna mtu napaswa kuonana nae mnaweza kusahau kilichotokea hapa na kuendelea kama kawaida”Aliongea Roma na hakusubiri jibu palepale alipotea na kumfanya Lanlan kutoa macho.
Dakika chache mbele Roma alikuja kuonekana Bagamoyo nyuma ya kituo cha afya na alitembea kwenye tifutifu ya mchanga kwenda mbele akikatisha eneo la shule ya msingikwa mbele na alikuja kusimama mara baada ya kuona mzungu mwanaume aliekuwa ameweka Headphone masikioni akiwa amechutama mbele ya bwawa la samaki ambalo limezingirwa na magugu.
Alikuwa ni mwanaume alievalia suti ya rangi nyeusi na tai nyekundu huku akiwa na nywele zake nyeupe (Blonde hair).
Kwa mwonekano wake ilionyesha dhahiri hakuwa mtu wa hilo eneo na ni mgeni ambaye alionekana kama kuvutiwa na mazingira na alikuwa amempa Roma mgongo huku akionyesha kuburudika na mziki uliokuwa ukisikika kwenye Headphone kutokana na namna alivyokuwa akitingisha kichwa.
Roma alimsogelea yule mwanaume wa kizungu taratibu na alipomfikia alimvua zile Headphone .
“Hey..!”Yule mwanaume aligeuka nyuma huku akionyesha kukasirishwa na kitendo cha kuvuliwa Headphone zake
“Nani kakwambia unaweza kunivua Headphone zangu kabla ya mziki haujamalizika?”Aliongea kwa Kijerumani.
Roma hakumjali zaidi ya kuzivaa zile Headphone ili kusikiliza mziki wenyewe na alitumia kama dakika moja na kisha alizivua huku yule mwanaume akimwangalia kwa namna ya kumchunguza kwanzia juu mpaka chini.
“Toccata and Fugue in D Minor by Bach”Aliongea Roma nakumfanya yule mzungu kushangaa.
“You know this piece?”Aliuliza akimaanisha kwamba anaufahamu huo wimbo.
“Ndio”Alijibu Roma
“Sio mbaya mtu yoyote anaelewa huo wimbo lazima aelewe maana halisi ya uhai”Aliongea kwa Kijerumanni.
“Sijasema na uelewa”
“Lakini inaonyesha unaupenda”Aliongea lakini Roma hakumjali zaidi.
“Naona una uwezo usiokuwa wa kawaida mpaka kufanikiwa kunitengenezea ‘Illusion’ ya kifo cha mama yangu kwa kuitawala akili yangu”Aliongea Roma akionyesha kwamba kitendo kilichomtokea dakika kadhaa zilizopita kilisababishwa na huyo mzungu.
“It wasn’t illusion”Aliongea huku sauti yake ikibadilika na kuwa nzito zaidi kuliko mwanzo akimaanisha kwamba alichokiona Roma haikuwa mazingira danganyifu.
“Oh! What’s that then?”Aliuliza kama sio mazingira danganyifu nini.
“Ni ndoto ambayo imetokea kwenye fahamu zako”
“Ndoto . Huh!. inaonyesha upo sahihi”Aliongea Roma
“Inaonyesha tayari umekwisha kunifahamu?”Aliuliza kwa kingereza.
“Haikuwa ngumu kwangu kukufahamu kutokana na Aura yako , licha ya kwamba ni mara yetu ya kwanza kuonana, lakini inashangaza kwanini mmoja wapo wa miungu kumi na mbili, Hermes(Mercury) akawa Vampire na isitoshe wewe ndio mwenye akili kuliko wenzako wote”
Roma pia alionyesha kushangaa na kujiuliza kuna sababu gani ya Hermes kujitokeza kwake tena kwa kipindi hicho.
Athena anaweza kuaminika kwa busara zake lakini kwa Hermes alisifika kama mchunga kondoo(sheepherd) na aliaminika kwa kuwa na mitego mingi.
Hermes katika historia ya miungu ya kigirika alifahamika kama mungu wa biashara , msafiri , mwizi , mhuni, tapeli na mpenda michezo lakini pia alifahamika kama mjumbe kati ya binadamu na miungu ya ugiriki kwasababu ya kupenda kusafiri kusafiri , kwa mfano anaweza kufika Tanzania watu wakataka kutuma salamu kwenda kwa Athena basi angewaambia kwamba wamlipe kiasi flani cha pesa na angefikisha maombi yao lakini moyoni hakuwa na mpango wa kufikisha maombi bali alifanya utapeli tu ni kama baadhi ya wachungaji wanavyowadanganya waumini walipe sadaka ili wapate magari, alikuwa pia akifahamika kwa kuupenda mziki ,ukisikia the first Song katika historia ni kutoka kwa Hermes
Roma ilikuwa mara yake ya kwanza kumfahamu na aliweza kumtambua kutokana na Aura yake na hata kuja hapo alifuata harufu(Scent).
“Nilishawahi kusikia kwamba unao uwezo wa kudhibiti miungu yote kupitia ndoto inaonyesha una uwezo mkubwa kuliko nilivyotegemea , sikuamini kwamba ungeweza kuniathiri kwa kiasi kikubwa”Aliongea Roma.
“Ni rahisi sana kila kiumbe chenye uhai lazima kiwe na mawazo na ukishakuwa na mawazo lazima uweze kuota ndoto ,hivyo ninao uwezo hata wa kutawala akili za mnyama kwa kutumia ndoto”Aliongea,
“Upo sahihi penye mawazo hapakosi ndoto”Aliongea Roma na yule mzungu alitabasamu.
“Now that we know that we’re on the same side can I have my headphones back , the newly appointed Hades”
“Sasa ushajua tupo upande mmoja nirudishie Headphone zangu , Hades mpya uliechaguliwa”Aliongea awamu hii kwa kingereza lakini Roma aliamua kukaa kwenye gogo pembeni yake na Hermes alitaka kumpokonya Roma zile Headphone lakini Roma alikwepesha mkono.
“Unafanya nini nirudishie mali yangu”
“Mpaka uniambie kwanini umemsaidia Denisi kutoroka?”Aliuliza Roma akitaka kujua kwanini huyo mzungu kaharibu mpango wake wa kumuua Denisi.
“Unataka kuujua ukwel?”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa kukubali.
“Kama upo tayari kuniambia, nataka kuufahamu ukweli”
“Hauwezi kuniamini hata nikikuambia hata hivyo mimi ni mungu wa wezi na muongo”
“Nina akili zangu hivyo nitajua ukweli mwenyewe”Aliongea na Hermes ilibidi amwinamie sikioni na kumnong’oneza na Roma alijikuta akitoa macho huku sura yake kubadilika.
“Siku nyingine ukinichokoza siwezi kukuachia kirahisi kwa sababu zako kipuuzi”Aliongea Roma huku akisimama
“Nilijua tu hutoamini?”Aliongea lakini Roma hakujali zaidi ya kuondoka akimwacha amesimama asiamini macho yake Headphone zake za thamani kubwa zinaondoka na Roma.
“Hey! Hades are you a robber?”Aliuliza kwamba Roma ni mwizi.
“Umenichokoza mwenyewe kwa kuruhusu adui yangu kunitoroka hii ni kama fidia na sababbu yako najua ni ya uongo hivyo kama unazitaka njoo uzichukue kwenye mikono yangu”Aliongea na kumfanya Hermes kumwangalia kwamshangao
“Una uhakika gani nimedanganya?’Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli huku akimwangalia kwa namna isioelezeka anafikiria nini kwenye kichwa chake.
Mwanaume aliekuwa akiongea na Roma ni yule yule tuliemuona nchini Ujerumani akiitana na Athena kaka na dada , lakini ni yule yule ambaye alikuwa akiongea ndani ya kanisa na Snejder.
Jina lake halisi ni Prince Raphaeli na Count Dogba alieuliwa na Roma ni mtoto wake, na yeye ni Vampire.
Unafikiri kaja kulipiza kisasi
Itaendelea . Nicheki watsapp 0687151346
Safari hii umetupunja KAMANDA SAURONISEHEMU YA 456.

This time kazingua katuma iliyopita ndeeeeefu alafu kipande kifupi tu cha leo.Safari hii umetupunja KAMANDA SAURONI
Bure ni gharama jamaaa angu.. tungekuwa na vibunda ingekuw tushalipia now twaperuzi tu...Walisema subira huvuta heri. Wewe mwandishi unatuumiza matumbo. Wiki inapita bila post. Haya makubwa; eti nimebanwa.
Nimejiuliza Sasa umesubscribe huu Uzi kwa lengo gani kusoma Mara mbili mbili au ?Akiendelea kukaa kimya hivi ntawapostia yote hapa maana kwenye group lake amepost sehemu ndefu subirieni
Achana nae atawasumbua wengine ndivyo tulivyo waafrika tunapenda sana kupigiwa magoti kwa vitu vidogo mwanzoni hakuwa bize ila sasa baada ya fan base kuwa kubwa kawa bize sikatai kabisa kuwa ni haki yake kupata kile ambacho kinastahili anapokosea anawapa ahadi za uongo pia mara atarudia siyo poa.Akiendelea kukaa kimya hivi ntawapostia yote hapa maana kwenye group lake amepost sehemu ndefu subirieni