Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Hatariiii
 
Hatari sana
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANO JR

SEASON 17.



SEHEMU YA 481.

Edna ilionyesha hakulala tokea walivyotoka visiwa vya wafu maana alipitiwa na usingizi akiwa ndani ya ofisi kwanzia saa kumi na moja mara baada ya shughuli pevu.

Ilibidi Roma ampatie maagizo Recho aliekuwa akisubiria nje aende nyumbani na yeye angeondoka nae, Recho hakufikiria mara mbili mbili na kuondoka.

Recho tokea siku afanye mapenzi na Roma ile nuksi ilimpotea na kwa kipindi hicho wale wanaume wote ambao walimuomba namba na kisha kumpotezea walirudi kwa kasi , hata mume wake ambaye alimuacha na yeye alianza kumsumbua , lakini Recho hakutaka kurudi alikotoka.

Maisha yake yalishaimarika na hakutaka kufanya kosa tena na katika siku hizo chache aliweza kupata mwanaume ambaye ndio kwanza mapenzi yapo yanaanza , japo Recho hajampenda sana mwanaume huyo kutokana na muda mwingi kufikiria usiku ule akifanya na Roma , lakini hakuwa na namna Roma ni mume wa bosi na huenda akigundulika na Edna basi anaweza kufukuzwa kazi na maisha yake kuwa magumu , hivyo hakufikiria tena kutaka kutoka kimapenzi na Roma , alidharau hisia zake na kisha kusonga mbele na kilichobaki kwenye moyo wake ni ile shukrani kwa Roma kwa kumtolea nuksi na kuna muda akikaa chini anajiuliza ilikuwaje , kwanini mara baada tu ya kufanya mapenzi na Roma wanaume walianza kumuandama maana hakuwa akipumzika na jibu lilikuwa moja tu kwenye kichwa chake , Roma hakuwa mtu wa kawaida.

Edna alipotea usingizi akiwa uchi na ilibidi amvalishe nguo na kumuacha apumzike na alikuja kushituka muda wa saa mbili za usiku, alianza kuzungusha macho na aliweza kumuona Roma amekaa kwenye kiti chake cha ubosi huku akiwa bize na kompyuta yake.

Alijikuta akikumbuka tukio ambalo limetoka na kujihisi aibu nyingi na kuanza kujilaumu kwanini hakujizuia mpaka wakafanyia ndani ya ofisi yake , lakini baada ya kufikiria kwa muda aliona hata hivyo sio jambo baya, haijalishi kama alifanya kwa hiari yake au kwa kulazimishwa hata hivyo alishatoa ahadi ya kufanya tendo la ndoa na Roma baada ya harusi yao lakini yeye ndio alieivunja na hayo ndio matokeo yake.

Alijikuta akiwaza namna hasira zake zilivyompelekesha mpaka akakubari kujumuika kwa chakula cha mchana na Hanson , ilikuwa mara yake ya kwanza kwa hiari yake kumkubalia mwanaume kula nae lakini yote ni zile hasira zake na aliona alifanya ujinga kwani alikwisha kuolewa.

Edna alikaa kwenye sofa huku akimwangalia Roma aliekuwa bize huku mawazo mbalimbali yakipita kwenye kichwa chake na aligundua Roma ni kama anajifanyisha hajamuona licha ya kwamba ameamka , alivaa vizuri nguo zake pamoja na viatu na kisha akasogelea kuangalia ni kipi ambacho kinamfanya kuwa bize.

Alijikuta hasira zikianza kujikusanya baada ya kuona kinachofanyika kwenye tarakishi yake ya kazi.

“Nani kakuambia unaweza kuweka magemu na kucheza kwenye tarakishi yangu ya kazi”Aliongea lakini Roma hakumjibu maada alikuwa bize, maadui watano kwenye gemu walikuwa wakimshambulia na siraha hivyo aling’ata meno kwa hasira na kuanza kuwashushia makombora , kuna mmoja kwenye gemu alijifanya kujificha na alipaa hewani na kwenda kutua mbele yake na kubonyeza batan kwa nguvu na kumpiga ngumi nyingi mfululizo mpaka akafa misheni ikawa imekamilika lakini mshindani wake kwenye gemu alimtumia ujumbe wa kuomba tena mpambano na Roma alimrudishia jibu atulie ndani ya dakika moja anarudi hewani , alikuwa akicheza gemu mubashara na watu wengine.

“Mbona unashangaa wakati umenunua tarakishi yenye uwezo mkubwa kiasi hichi na unaitumia kwa kufanya kazi za ofisi tu, nimeona nikupunguzie hasara..”Aliongea Roma huku akicheka.

“Hey!” Roma alijikuta akipiga mkono kwenye meza mara baada ya Edna kuzima cable ya ukutani na tarakishi kuzima.

“Dear wataniona nimekimbia mchezo , wewe hujui tu hapa nilikuwa nikicheza online nitapigwa penati nikirudi tena hewani”

“Unaonyesha kujutia kisa gemu tu lakini sijawahi kuona ukijutia pale unapomuua mtu”

“Hayo ni mambo mawili tofauti , heshima yangu umeiweka rehani hapa,wataona nimekimbia misheni kwa kuogopa”

“Kama unapenda magemu sana , unaonaje nikikuanzishia kampuni huenda unaweza ukafanya vizuri zaidi na kuleta mafanikio kuliko kucheza kipoteza muda”

“Unajua nini mke wangu , hilo wazo pia sio baya”Aliongea Roma lakini Edna alionekana kama mtu ambaye alikuwa akitaka kusikia Roma akiongea yeye.

“Vipi huna chochote unataka kuniambia?”Aliuliza huku akikosa utulivu , bado alikuwa akiona aibu na kukwepesha macho Roma anapomuangalia usoni.

“Nikuambie nini?”

“Wewe...!” Alimnyooshea kidole huku akiangalia pembeni.

“Oh..! halafu nimejisahau , Muda umeenda na utakuwa na njaa , unaonaje tukienda hotelini kula kabisa , nishampigia simu Bi Wema na kumwambia asituhesabu”Aliongea Roma lakini Edna ni kama kitu ambacho hakupenda kusikia kutoka kwake.

“Mbona kama unanidhihaki”

“Hapana,unamaanisha nini?”

“Unafikiri… nime…nime “

“Umefanyaje..?”

“Uh..!”Edna alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha haikueleweka alikuwa akitaka kuongea nini..

“Nadhani unaniona sina aibu kwasababu nilikukatalia sana lakini mwisho wa siku nikakubalia tena ndani ya ofisi”Aliongea kwa sauti ndogo ambayo haikuwa ya kawaida , ilikuwa mara yake ya kwanza kuongea hivyo huku akiwa anaangalia sakafu kama mtoto wa darasa la saba anaetongozwa.

“Huenda ikawa hivyo ila…..”Alijibu Roma huku akimshangaa na kumfanya Edna ainue uso wake na kumwangalia huku akipotezea aibu zake.

“Huwezi kuongea hivyo , wewe ndio sababu ulikuwa ukitisha mno na..na niliogopa kukukatalia”

“Umenikatisha mwenyewe na sijamaliza kuongea , halafu haijalishi kwasababu nimefurahi na hata hivyo hatujafanya kosa , sisi ni wanandoa na wote tumefurahi, Haina haja ya kuwaza sana sawa”

Edna aliona Roma ana pointi ,ni kweli wamefanyia ofisini lakini kuna haja gani ya kujutia kilichofanyika , kwani amefanya na mume wake hata hivyo alijiambia hio ni bahati mbaya tu kwa siku hio na hawezi kufanya tena ndani ya ofisi yake.

Alivyomuona Roma alivyotulia kuna hisia zilimwambia alionekana kama mtu mzoefu na huenda ashawahi kufanya na michepuko yake ndani ya ofisi za kampuni yake.

“Twende mgahawani tukapate chakula cha usiku tusichelewe kurudi nyumban…”Aliongea Roma huku akiangalia tarakishi iliozimika kwa kujutia hakumaliza misheni yake.

Kwa kiasi flani alijihisi aibu kumpotea kutokana na Roma kutoonyesha kuzingatia sana kile kilichotokea.

“Nywele zangu zimechanguka siwezi kutoka hivi subiri kidogo..”Aliongea na kuanza kuziweka sawa kwa kuzichana na kisha akatoa kibanio na kuzifunga kwa nyuma, ilikuwa siku ya kwanza Roma kumuona Edna akijiweka sawa mbele yake , ilimvutia mno kuangalia kwa macho hasa alivyokuwa siriasi, hakuwa akitumia vipodozi hivyo hakuwa na haja ya kujilemba muda mrefu.

“Mbona unaniangalia hivyo kama ndio mara yako ya kwanza kuniona?”

“Inashangaza sana baadhi ya wanawake wakiolewa wanazidi kupendeza , uzuri wako unanifanya nishindwe kuacha kukuangaliaa, Mrs Edna kama watu wakijua hujapaka chochote usoni watakata tamaa ya kununua vipodozi kwa ajili ya kujipamba kwani watakosa kujiamini”.

“Sweet talker”Aliongea Edna na kisha alichukua mkoba wake na kutangulia mbele.

Muda ulikuwa umeenda hivyo hawakukutana na mfanyakazi yoyote wakati wakitoka.

Waliingia kwenye gari, Roma akiwa dereva na kisha wakaondoka na Roma sehemu ambayo aliona inafaa kwa ajili ya kupata chakula cha usiku ni mikocheni kwaWarioba sehemu ambayo aliweza kufanya maongezi na Nadia, alipenda sehemu hio kwasababu siku ile alifurahia chakula chao.

Dakika chache tu kutokana na kutokuwepo kwa foleni waliweza kuingia ndani ya mgahawa huo wa kisasa na siku hio ilikuwa tofauti na siku ambayo Roma alikaa hapo na Nadia , sehemu ilikuwa haina watu wengi sana na wachache ambao walikuwepo walionekana kuwa wenza pamoja na familia ambazo asilimia kubwa zilikuwa ni wazungu ,wahidi na waarabu.

Edna alipenda mazingira kwasababu hayakuwa na watu wengi na alionekana kuvutia zaidi kwasababu hata zile stress ambazo zilikuwa zikimwendesha ni kama zimepotea na muda huo alikuwa kwenye mood nzuri kweli.

Roma mara baada ya kukaa aliweza kuona mtoto mmoja wa kizungu aliekuwa amebeba mdoli na kumfanya kukumbuka kitu.

“Edna ule mdoli niliokupatia kama zawadi bado upo nao?”

“Yeah..”Alijibu huku akitingisha kichwa na alijua kwanini Roma alimuuliza kwani hata yeye aliweza kuona mtoto wa kizungu alieshikilia mdoli mkubwa.

“Nilijua ungeutupa kwasababu ulikuwa na hasira na mimi , itakuwa kweli nina uwezo mdogo wa kufikiria”Aliongea Roma na Edna alimwangalia bila kujibu huku akijifikira mwenyewe.

Ndio nipo nao lakini niliupiga mateke usiku wa jana wote”.Aliwaza

Ukweli njia nzima Edna alikuwa akiwaza ni kwa namna gani angeweza kusafisha chumba chake na kupunguza baadhi ya vitu ili kuingiza vya Roma , kwani baada ya tukio la siku hio ni muda sahihi wa kulala pamoja lakini kila akikumbuka ana vitu vingi sana vimejaa makabati yote alishindwa kujua kipi angeacha na kipi angetoa.

“Mama…!!!”

Watu wote waliokuwa ndani ya mgahawa walijikuta wakiangalia mlangoni mara baada ya kusikia sauti ya mtoto kuita , hata Roma na Edna waligeuka haraka sana kwani sauti waliitambua.

Alikuwa ni Lanlan ambaye ameingia hapo ndani huku mkononi akiwa ameshikiliwa mfuko wa biscuit.

“Lanlan” Edna alisimama haraka mara baada ya kumuona ni Lanlan na alishangazwa na kuwepo hapo muda huo wa usiku.

Hata Roma mwenyewe alishangaa lakini alifurahi kwa wakati mmoja na hata muda ambao aliweza kusikia sauti yake alihisi mwili ukimsisimka.

Baadhi ya watu walitabasamu kwa jinsi Lanlan alivyom’cute’ na kupendeza na hata baada ya kuona aliekuwa akimwita mama ni Edna walijikuta wakitingisha kichwa na kusema hakika walikuwa wakifanana.

“Lanlan why are you here ? Mommy missed you a lot” Aliongea Edna huku akimbusu shavuni , alikuwa amemmisi kweli licha ya kwamba ni siku tatu tu ambazo hawakuonana kwani walimuacha Songea.

“Lanlan missed you too mommy”Aliongea huku akionyesha furaha kwenye macho yake.

Muda huo huo alionekana mdada mmoja akija mbio mbio na mifuko huku akihema , ilionekana alikuwa akimfukuza Lanlan kwa nyuma na baada ya kuingia kwenye huo mgahawa na kumuona Edna na Roma alijikuta akishika magoti huku akihema kwa tabu.

Edna baada ya kumuona aliweza kumfahamu , alikuwa ni mfanyakazi wa Madam Damasi , mke wa raisi Senga na alimwacha Songea kabla ya kusafiri, Lanlan alitokea kumzoea sana huyo mfanyakazi , hivyo haikushangaza kuwa pamoja.

“Miss Edna!, Lanlan alinizidi spidi ya kukimbia ndio tumefika muda huu kutoka Songea na kuna mzigo kaagiza ndio nimetoka kuuchukua hapo supermarket,Lanlan alivyosema mpo hapa sikuamini hivyo nilipatwa na wasiwasi wakati anakimbia”Aliongea huku akionyesha wasiwasi.

“Usijali Anna , najua Lanlan usingeweza kumzidi spidi”Aliongea Edna huku akitabasamu na Anna alionekana kupata ahueni.

“Umesema babu kasharudi , yupo wapi sasa hivi?”

“Keshatangulia nyumbani na tupo hapa na Frank”Frank alikuwa dereva wa Afande Kweka.

“Okey nimekuelewa , unaweza kujumuika na sisi kwa ajili ya chakula”

“Asante sana lakini Frank yupo anatusubiria..”Aliongea huku akimwangalia Lablan aliemg’ang’ania Edna kwa staili staili ya kuonyesha hakutaka kuondoka kurudi nae.

“Anna unaweza kwenda Lanlan ashafika nitampigia mzee simu”Aliongea Roma na Anna alitingisha kichwa kukubali.

“Goodbye Nanny Anna”Alipunga mkono

“Chubby unaweza kwenda na mlezi wako unamuachaje wakati umekuja nae”Aliongea Roma na kauli yake ilimfanya Edna amwangalie kwa ishara ya kumwambia kaa kimya..

“Mbona unaniangalia hivyo , sijakosea Lanlan kaja na mlezi wake kwanini amtelekeze mara baada tu ya kutuona, huo ni usaliti na isitoshe hata babu yake hajamuaga”

“Lakini Lanlan amemmisi mama yake”Aliongea kwa huruma huku akijificha nyuma ya Edna.

“Lanlan usijali, mama pia amekumisi na tunaenda wote nyumbani” Aliongea Edna na kumfanya Roma ashindwe kuongea chochote na kuchukua Menu, Alimjua Lanlan anapenda sana kulala na Edna hivyo angempeperushia jambo lake ambalo anapanga kichwani ndio maana akapendekeza aondoke na Anna.

Anna mlezi ilibidi kuondoka maana asingeweza kurudi na Lanlan kwani ashakutana na wazazi wake tayari na aliondoka huku akiwa kama ametelekezwa, ijapokuwa alijua Lanlan sio mtoto wa kawaida lakini alishindwa kujua kawezaje kunusa harufu za wazazi wake kutoka mbali.

Kwasababu mhudumu alikuwa amesimama akihitaji oda yao, ilibidi kwanza Edna aagize chakula , lakini mhudumu alijikuta akishangaa baada ya kuona Edna anaagiza chakula kingi.

“Samahani Madam, lakini naona umezidisha”.

“Leta kama nilivyoagiza” Aliongea Edna na mhudumu alishangaa lakini alifanya kama alivyoambiwa na kuondoka.

Edna aliagiza chakula kingi kwasababu ya uwepo wa Roma na Lanlan, kwa alivyokuwa akijua migahawa ya kisasa kuweka chakula cha wastani kisingewatosha kabisa ndio maana akaagiza oda tano , yaani mbili za Roma na mbili za Lanlan na yeye moja.

“Mama kesho nataka kwenda shule , Lanlan amemisi rafiki yake”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie.

“Chubby umepata rafiki?”Aliuliza Roma na kumfanya Lanlan atingishe kichwa.

“Ni msichana au mvulana?”

“Unamuuliza mtoto maswali gani hayo?”

“Kwani vibaya kumjua rafiki wa Lanlan ni wa kike au wa kiume , Wife usiniambie ushaniwazia vibaya maana swali langu halina kasoro”.

“Wewe ndio umewaza vibaya na kama unataka kumfahamu rafiki yake kwanini usiende nae kabisa kesho ukashinde huko ili kumfahamu?”

“Mh!... wanaruhusu wazazi kujumuika na watoto wao shuleni?”

“Ah…!!, ni kila baada ya tarehe ya mwisho wa mwezi”Aliongea Edna.

Baada ya muda waliletewa oda ya vyakula walivyoagizwa na Lanlan mara baada ya kuona msosi misuli ilisimama na haikuwa kwake tu hata kwa Roma ilikuwa hivo hivyo.

Lanlan alimwangalia baba yake na Roma hivyo alimwangalia Lanlan na kumkonyeza , kitendo kile kilimuacha hoi Edna , katika siku zote alizoishi na Lanlan pamoja na Roma utofauti wao ilikuwa mwili tu yaani mmoja mtu mzima na mmoja mdogo.

Lanlan mara baada ya kukabidhiwa sahani yake na kuambiwa aendelee hakutaka kupoteza muda na alianza kupiga msosi kwa spidi zote , huku Roma na yeye akiwa hivyo hivyo.

Wakati mhudumu anawawekea jusi alijikuta akishangazwa na staili yao ya kula, ni mara chache sana kupata wageni wa aina ya Roma , lakini la kushangaza zaidi ni upande wa mtoto.

Edna alijua mhudumu anashangaa lakini alimrudishia tabasamu tu na yeye pia akatabasamu na kisha kuondoka.

“Dear huo ni uharibifu wa chakula sasa na ni dhambi”Aliongea Roma mara baada ya kumuona Edna kula kidogo na kuweka uma chini.

“Malizia chakula chako , kwanini unajali kikiharibika”Aliongea huku akisukumia sahani yake katikati ya meza na kumfanya Lanlan amwangalie.

“Mommny , you cant waste food , Grandfather said that every piece of food is made with the farmers hardwork”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kuona aibu maana ni kama Lanlan anamrekebisha.

“Lanlan lakini mama ameshiba”

“Hivyo ndio ulitakiwa kuongea”Aliongea Roma na kisha akaivuta ile sahani na steki ya nyama iliobakia ilipelekwa yote mdomoni na kutokomea tumboni na kisha akamalizia na kilichobaki.

“Lanlan , wewe ni mtoto mzuri”Aliongea Roma huku akimkonyeza na kumfanya Edna kubetua mdomo.

Muda ule ule wakati wanamalizia chakula mara waliingia wenza wawili , mmoja alikuwa ni mwanaume alievalia kanzu na kirembo kichwani , ambaye alikuwa kama msomali na mwingine alikuwa ni mwanamke lakinni alikuwa amevalia Nikabu hivyo hakuonekana sura.

Walikuwa wakinukia mno na kumfanya Roma kuguna na kusababisha Edna kumwangalia.

Kilichomfanya Roma kuguna ni kutokana na watu walioingia kutokuwa wa kawaida, walikuwa wakitoa Aura ambayo Roma aliweza kuitambua kwa haraka haraka ni majini, lakini sio hivyo tu mwanamke alikuwa na yupo k katika levo ya nafsi na kwa mwanaume alionekana pia alikuwa na mafunzo ya kijini lakini levo yake ilikuwa ni mwishoni mwa levo ya Mzunguko kamili.

Wale wenza walikaa kwenye meza na kutulia huku wakiangalia meza ya Roma, ilionyesha kuna uwezekano walikuwa wakimfatiia lakini muda huo waliona sio sahihi , Roma alijimbia kama wanamfatilia hawatoishia hapo mgahawani tu kama akiondoka watamfauta nyuma na alijihisi mwili wake kumsimsimka.

Muda ule ule na simu ya Edna ilianza kuita na kumfanya aipokee mara baada ya kuona anaepiga ni mama mkwe yaani Blandina.

“Hello , Mama”

“Edna upo na Roma?”

“Ndio , tumemaliza kupata chakula hapa”

“Sophia karudi tokea saa kumi na moja na anawasubiria , hayupo peke yake bali kuna mtu maarufu kaja nae pia anataka muonane kwani kuna kitu anataka muongee”Aliongea Blandina na kumfanyaEdna kuona sio jambo baya hivyo alikata simu na kumuelezea
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANOJR



SEHEMU YA 482.



Baada ya kupata taarifa wanasubiriwa nyumbani hawakutaka kuendelea kukaa , kwani hatahivyo walimaliza rayari kupata chakula , Roma alilipa na alimbeba Lanlan na kuingia kwenye gari.

“Mhh! nahisi wale wenza waliongia sio watu wazuri”Aliongea Edna mara baada ya kuingia kwenye gari.

“Kwanini unasema hivyo?”

“Roma unanitega sio?,nilikuona ukiwaangalia hata wewe kwa macho ya wasiwasi”Aliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu kwa uchungu hakujua Edna angefahamu nia yake.

“Wanaonekana sio wazuri lakini huna haja ya kuwa na wasiwasi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kukaa kimya na safari ya kurudi nyumbani ilianza.

Ulikuwa umbali mrefu lakini kwasababu hakukuwa na foleni muda huo haikuwachukua muda mrefu kufika.

Baada ya kutoka kwenye gari waliweza kupokelewa na Blandina aliekuwa akiwasubiria na alishangaa kumuona Lanlan.

“Grandmaa…”Lanlan alimkimbilia bibi yake na kwenda kumkumbaria miguuni.

“Oh! Lanlan Bibi alikumisi sana, Edna mmemtoa wapi nilijua bado yupo Songea”

“Lanlan alituona njiani , alikuwa na Anna na ndio wamefika leo mjini”Aliongea na kumfanya Blandina kuelewa.

“Sophia anawasubiria , mnapaswa kawenda kuonana na mgeni”Aliongea na Roma na Edna walitangulia na kuingia ndani huku Mama yao akimchukua Lanlan na kwenda kumkabidhi kwa Qiang Xi abadilishwe mavazi pamoja na kuogeshwa.

Baada ya kuingia eneo la sebuleni waliweza kukutana na mwanaume mtu mzima ambaye alikuwa amekaa akiangalia runinga akiwa pamoja na Sophia, alikuwa ni mzungu miaka kama arobaini hivi na Roma na Edna walisalimiana nae na kisha wakaketi.

“Sister huyu ni Director Fabby Lassay kutoka kampuni ya uzalishai wa filamu ya Penguin Production kutoka Afrika ya kusini”Alitambulisha Sophia kwa lugha ya kingereza.

“Mniwie radhi kwa kuwavamia hapa nyumbani , kama alivyosema Miss Sophia nafahamika kwa jina la Fabby Lassay ni Executive Director wa Penguin Production na nipo hapa kwa ajili ya maongezi juu ya ushirikiano wa uandaaji wa filamu:”

“Mr Fabby wewe ni mtu maarufu?”Aliuliza Roma na kumfanya Fabby kutabasamu.

“Mr Roma kama utakuwa mpenzi wa filamu basi jina langu halitokuwa geni , kabla ya kufanya kazi kama Directori katika kampuni ya Penguin nilifanya kazi na Paramaount kama Producer msaidizi na Screen Writer nina kazi nyingi ambazo naweza kusema zinanifanya kuwa mtu maarufu na nishawahi kufanya kazi na Christen atanifahamu pindi utakapomtajia jina langu”

“Okey Mr Fabby kwahio ujio wako hapa ni kutaka kumuhiisha Sophia kwenye filamu au unataka kampuni yetu kuwekeza?”

“Nipo hapa kwa ajili ya kuomba ruhusa kwenu ya kumuhusisha Sophia kwenye filamu kama mhusika mkuu wa kike , nilijaribu kuwasilisha ombi langu kupitia wakala wake lakini majibu nilioyapata ni Miss Sophia kuwa na ratiba ngumu, nilijaribu kuwasiliana na Sophia moja kwa moja na aliniambia kama nyie wawili mtampa ruhusa basi haina haja ya kupitia kwa menejimenti yake wala kampuni”

“Sophia unapenda kuigiza filamu?”Aliuliza Roma huku akmwangalia.

“Hata kama niseme napenda , nina wasiwasi naweza nisifanye vizuri kwanni sina mafunzo maalumu hivyo kuharibu kazi”

“Miss Sophia hilo lisikupe shida , nimeweza kuangalia matamasha yako na nimegundua unafaa kabisa na kwasababu tuna mwezi mzima wa matayarisho tunaweza kukuelekeza na ndani ya muda utakuwa umeelewa namna ya kuwa muhusika mkuu na kuzoea Script na isitoshe stori inaendana sana na mwonekano wako”

“Director kama unadhani Sophia anaweza kufiti kwenye nafasi ya uhusika wa stori basi hatuna haja ya kumzuia , lakini kama mambo yakienda vibaya kutokana na Sophia kukosa uzoefu nadhani hatuwezi kuhusika”

“Hilo lisiwape shida , hatujafanya makosa kumchagua Sophia katika nafasi ya uhusika mkuu na hakuna lawama yoyote kama atashindwa kuendelea”

“Kama ni hivyo nadhani hakuna haja ya kumzuia kwani itakuwa na faida kwake , Lakini Director kuhusu malipo nadhani yanapaswa kuwa ya kuridhisha”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie , yaani hata hawajafikia kwenye hitimisho lakini alishatanguliza maslahi.

“Mr Roma hilo halina shaka kabisa, bajeti ni kubwa hivyo malipo yatakuwa makubwa , lakini pia kwa kulinda heshima yangu katika ‘industry’ siwezi kutoa malipo kidogo”Aliongea na Roma aliridhika , hata hivyo alimuona Director Fabby kuwa mtu siriasi maana kuwasubiri kwa muda mrefu pasipo ya kuondoka sio jambo la kudharau, lakini pia aliwaamini sana Wazungu kwa kujali heshima yao , kama kweli Director amefanya kazi na Christen basi alijua malipo hayatakuwa haba na itamuongezea Sophia umaarufu.

Hakukuwa na maongezi ya ziada hivyo Director aliaga na kuondoka huku taratibu za mikataba zingefuata siku kadhaa zinazofuata kupitia kampuni ya Vexto Media pamoja na menejimenti, Sophia yeye hakuondoka kwasababu ishakuwa tayari usiku.

Baada ya kuongea kwa muda mfupi kama wanafamilia Bi Wema ndio aliekuwa wa kwanza kuaga kwenda kulala.

“Lanlan atalala na mama?”Aliongea Lanlan na kumfanya Roma kung’ata meno kwa kuona Lanlan anamchawia na mbaya zaidi alijitia huruma mbele ya Edna.

“Kibonge utalala na mlezi wako Qiang Xi , huwezi kunipokonya mke wangu”

“Lakini Lanlan hawezi kulala bila mama” Aliongea huku akimwangalia Edna kwa kutia huruma .

“Lanlan usiwe hivyo, utalala na Mama, Sawa mtoto mzuri”Aliongea Edna na kumfanya Lanlan kutabasamu huku akitingisha kichwa na kumwangalia baba yake kana kwamba anamwambia ameshinda.

“Wewe kibonge nyanya nisikilize mimi baba yako kama unataka zawadi”

“Mr Roma nadhani tumuache Lanlan afanye kama anavyotaka, usiku anatabia ya kushituka na kukaa macho nikilala nae na anapaswa kuamka mapema kwenda shule”

“Qiang Xi mbona hujawahi kusema” Aliongea Blandina kwa mshangao.

“Lanlan ndio alivyo tokea nilipoanza kumlea tena imekuwa afadhali tokea aishi na mama yake amekuwa akipata usingizi mapema”

“Ah…!!”Roma alijikuta akikosa neno la kusema na kumfanya Edna amwangalie na kufurahia mwonekano wake.

“Roma lakini kwanini unalazimisha Lanlan akalale na mlezi wake, si nyie mnalala vyumba tofauti au…”

“Mama ni kwamba mimi na Edna tume…”

“Wewe usije ukaongea” Edna alimkatisha huku akitamani amtie Roma ngumi , alishindwa kumuelewa Roma ni mtu wa aina gani anataka kuropoka bila aibu mbele ya mama yake, hakutaka siri ya wao kufanyia ofisini ifahamike.

Roma mara baada ya kuona amekatishwa na Edna alitabasamu na kuonyesha ishara ya kuziba mdomo.

Blandina alishaelewa kilichokuwa kikiendelea hivyo hakutaka kutia neno hata kwa Sophia hivyo hivyo waliishia kutabasamu.

“Sister Edna Hongera sana na kwako Shemeji nadhani unapaswa kutafuta namna ya kushindana na Lanlan”Aliongea Sophia huku akisimama na kumfanya Edna atamani kuwe na shimo atumbukie kwa aibu alizojisikia.

“Hahaha… nyie watoto mnanifurahisha, Roma nadhani uvumilie , Mjukuu wangi Lanlan anapaswa kupata usingizi mapema ili asijekwenda kusinzia shule”

“Grandma is so nice”.

“Lanlan umeelewa nilichoongea?”Aliuliza Blandina kwa mshangao na Lanlan alitingisha kichwa, alionekana ashaanza kukamata baadhi ya maneno ya kiswahili na kuanza kuyaelewa.

“Mjukuu wangu una akili nyingi , utakuja kuwa mtu mkubwa baadae”Aliongea huku akimshika shavu na Lanlan aliishia kutabasamu kwa kutoa meno yake machache nje.

Baada ya Roma kuona amepokonywa mke na mtoto wake , ilibidi kwanza akae sebuleni , hata hivyo kuna kitu alichokuwa akisubiria kwa hamu zote.

Baada ya watu wote kuondoka kwenda kulala, hatimae mwili wake ulianza kusisimka huku vinyweleo kusimama.

“Naona hatimae mmekuja?” Aliwaza kwenye akili yake na kuzima runinga na palepale alipotea na kutokezea nje ya geti , lakini ile anaibukia aliona vivuli vya watu wawili vikipotea kwenye upeo wa macho yake.

Walikuwa ni walewale aliokutana nao kule PalmVillage Restaurant, Roma alijua walikuwa wakitoka hapo ili wasionekane na aliwafuata kwa harufu yao na ndani ya sekunde alikuja kuibukia kwenye fukwe mita kadhaa kutoka nyumbani kwake na hatimae aliweza kukutana na watu wawili waliosimama wakiwa wamempa mgongo.

Roma alitabasamu mara baada ya kugundua wote wawili wamebadilika kimuonekano, walikuwa wamevaa mavazi ya kitamaduni maarufu kama Robes , walionekana kama vile ni wale waigizaji wa filami za kale za mataifa ya Asia, mfano Jumong.

Wote walikuwa wamefunga nywele zao kwa nyuma huku mkononi wakiwa wamshikilia upanga(sword) ambao upo ndani ya Ala kwa kila mmoja.

“Nyie ni wakina nani kwanini mnanifuatilia” Aliongea Roma na wale watu waligeuka na kumwangalia na hapo Roma ndipo alipowaona sasa , walikuwa sio wenye asili ya wasomali tena bali mmoja wa kiume alionekana kama Mchina na wa kike alionekana kama mkorea.

Kwa haraka haraka alijua mwanamke alikuwa mtu mzima kuliko wa kiume na huenda hio ndio ilifanya yeye kuwa na uwezo mkubwa kuliko mwenzake , kwani alikuwa kwenye levo ya Nafsi na mwanaume alikuwa mwishoni mwa levo ya Mzunguko kamili.

Kuna muda Roma alijiuliza Hongmeng ni majini kama majini au ni watu wanaoishi miliki za kijini maana miili yao haikuwa na utofauti na ya binadamu wa kawaida , jambo moja tu la kimaajabu ambalo lilimvutia ni namna ambavyo waliweza kutumia sura za watu ili wasitambulike, ijapokuwa uwezo huo hata Yamata walikuwa nao , lakini kwa jinsi walivyoonekana pale mgahawani walionekana kuwa na uzoefu mkubwa.

“Wewe ni Roma Ramoni?”Aliuliza yule mwanaume.

“Nadhani mpaka kuja nyumbani kwangu mshajua mimi ni nani , kuna haja gani ya kuthitisha?”

“Acha jeuri na jibu maswali yetu kama hutaki kuingia kwenye matatizo na sisi , tunataka kujua kuhusu Monk Tianyi alieuliwa na Yan Buwen”

“Monk Tianyi ndio nani?, sijawapata bado”

“Acha kujifanyisha humjui , tumepata taarifa wewe ndio umemuua Yan Buwen hivyo hutokosa kumfahamu Monk Tianyi”

“Kama ni hivyo kwanini msigemuuliza Omari na kja kwangu”Aliongea Roma, alishajua watu hao ni kutoka Hongmeng kutokana na medali zao za dhahabu walizoning’iniza kiunonni, zilikuwa zikifanana kwa kiasi kikubwa na ile aliochukua kwa monk mweusi aliemteka mke wake.

“Omari tushaongea nae na ndio alietuambia umemuua Yan Buwen kwa kumshushia Radi , je ni kweli unao uwezo wa kudhibiti Radi?”Aliuliza yule mwanaume huku wote wakionyesha shauku kwenye macho yao.

“Kwahio mmeshindwa kumuamini Omari ndio maana mkaja kunitafuta?”

“Tunataka kujua , sio jambo jepesi kwa binadamu wa kawaida kuweza kudhibiti radi kwa kutumia nishati ya mbingu na Ardhi na kama kweli ulikuwa na huo uwezo , kwanini ukamuacha Monk Tianyi akafariki kwa mikono ya Yan Buwen bila kumsadia”

“Kwahio hio mpo hapa kwa ajili ya kulalamika kwasababu Yan Buwen kamuua Monk ambaye alifanya maaamuzi ya kijinga kwa kujiona anao uwezo mkubwa kuliko wa Yan Buwen , mnachoongea ni upumbavu kwanza kwanini niwasaidie”Aliongea Roma.

“Kwahio unatuona sisi ni wapumbavu sio, nadhani kufanikisha kwako kuzijua tamaduni zetu kuna kufanya ujione uko juu sana”

“Kwahio mnasemaje sasa?”Aliongea Roma huku akianza kukosa uvumilivu na yule mwanaume alimzuia yule mwanamke asiendelee kuongea.

“Mr Roma nadhani Monk ndio mwenye makosa kwa kushindwa kukadiria uwezo wake na wa Yan Buwen , Monk Tianyi alikuwa mjumbe ambaye alitumwa kwenye ulimwengu wa kawaida kwa ajili ya kumuwinda Yan Buwen kwa kipindi cha mwezi mzima na juzi ndio tuliweza kugundua taa ya nafsi yake imezima kama ishara ya kifo chake , hivyo tumeagizwa kuja kufuatilia Dhana zake na tunaamini wewe umezichukua hivyo tunazihitaji”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu , Rufi alimweleza katika miliki za kijini ukoo wa Hongmeng licha ya kuwa na nguvu ndani ya taifa la China lakini walikuwa ndio wanaongoza kwa umasikini wa Dhana na baadhi ya dawa za kuwasaidia katika kuvuna nishati za mbingu na Ardhi na hili linajidhihirisha, wamekuja mpaka Tanzania kwa ajili tu ya kutafuta dhana zao basi walionyesha kuwa na uhaba.

“Nadhani hata hilo swali mlipaswa kumuuliza Omari pia, kwanini mnataka kunisumbua?”

“Acha kujiona kijogoo , tunahitaji Dhana zetu, wewe ni mrithi wa Pluto na unao uwezo wa kutumia kanuni za anga hivyo kuna uwezekano ukawa umezificha kwenye parallel space na Omari ameshindwa kugundua”

“Kwahio mnanihisi mimi mwizi si ndio?”

“Tuna kila sababu ya kukuona wewe ni mwizi labda kama utarudisha Dhana zote na tukuache na amani,usije ukajifanya mjanja na kuona hatuwezi kukushughulikia”

“Okey! Yan Buwen aliharibu Dhana zote za Monk kwa kutumia Ant -matter hivyo sijachukua Dhana zenu, nadhani hilo jibu linawatosha”

“Sababu unayotueleza haina mashiko yoyote , zile ni dhana ambazo zimejaa uungu ndani yake na sio ngumu kuyeyuka”

“Kama hamuwezi kuniamini siwezi kuwaamisnisha , jibu langu ndio hilo”

“Inaonekana unaona hatuwezi kukuadabisha sio, nikutahadharishe tu tunatokea Hongmeng na ukishindana na sisi unashindana na jamii yetu yote.”Aliongea yule mwanamke , alionekana kuwa kiburi na aliamini Roma hawezi kuchukua hatua kwasababu wanatokea Hongmeng.

“Kwahio mnanitishia?”Aliongea Roma na kumfanya yule mwanamke kuchomoa upanga wake ambao haukuwa wa kawaida kutokana na Aura yake lakini yule mwenzake alimzuia.

“Senior Dong hatuwezi kupambana nae , anao uwezo mkubwa kuliko wa kwetu ndio maana hatuwezi kuona yupo hatua ipi kwenye mwili wake , tunapaswa kwenda kutoa taarifa kwa Master wafanye maamuzi”Alimtuliza.

“Mr Roma unapaswa kuelewa , bado hatujamalizana na wewe , tunaondoka na kwenda kutoa taarifa na Master mwenyewe atatoa maamuzi , usijione una nguvu huwezi kushindana na wazee wetu wakiamua kukuadabisha”Waliongea na kisha wakajiandaa kuondoka , lakini Roma aliwazuia.

“Sio kwa haraka hizo, mimi bado sitaki muondoke maana hata nyumbani sijawakaribisha kuweka hata baraka kwa kikombe cha chai?”

“Huna sifa ya kuweza kutukaribisha sisi , labda raisi wa taifa hili anaweza angalau kutushawishi”

“Oh! ,, Lakini nikiwaachia mkiondoka na sintofahamu huoni kwamba mnaweza kwenda na kuja na mtu hatari zaidi na ikawa shida kwangu?”

“Hilo lisikupe shida kama haujaiba Dhana zetu Wazee wetu hawawezi kuchukua maamuzi yasio ya busara , unatakiwa kuelewa zile Dhana hazikuwa za Monk bali aliazimishwa na ukoo”

“Okey , basi naomba niwaulize swali, Je kila mmoja ndani ya Hongmeng ana Taa ya uhai wa nafsi yake(Lantern of Soul)”

“Kwanini unatuuliza hivyo?”.

“Kwasababu kuna rafiki yangu mmoja ambaye nilikutana nae , alionekana kubeba medali kama hizo mlizoning’iniza na amesema ametokea Hongmeng , Oh.! tena anamiliki Kisu cha damu ya Joka”Aliongea Roma akimaanisha Blood Dragon Dagger , alikuwa akimzungumzia yule Monk mweusi aliemteka Edna na kumuua.

“Unamaanisha Msaliti Abeo unamfahamu?”Aliongea yule mwanamke huku akionyesha mshangao.

“Kumbe anaitwa Abeo , ndio namfahamu alikuja kwangu akihitaji niwe rafiki yake kwanini mnamuita msaliti”Aliongea Roma na kuwafanya wote kuangaliana.

“Haiwezekani , Abeo hawezi kufanya urafiki na mtu yoyote , ni msaliti kwa Hongmeng kwani aliasi kwa kuhamia kwenye miliki nyingine kutokana na tamaa zake , binadamu wote hamna shukrani , tulimkaribisha na kumuacha ajifunze tamaduni zetu lakini mwisho wa siku akatugeuka kwasababu ya tamaa ya utajiri na nguvu”

“Alikuja kwangu kwasababu nina Vidonge nilivyopatiwa na Master wangu , vinavyonisaidia kwenye kuvuna nishati za mingu na ardhi , hivyo alitaka nibadilishane nae kwa kunipa kisu cha damu ya Dragoni”

“Unamaanisha unavyo Vidonge ambavyo Abeo alikuwa tayari kukupatia dhana yake?”

“Unafikiri nadanganya, vidonge nilibyokuwa navyo vina uwezo wa hali ya juu sana , nadhani hata nyie wenyewe mnaona nipo na miaka ishirini na kitu lakini nimefikia levo za juu”Aliongea Roma , alikuwa akidanganya ili kuwaingiza kwenye mtego anao waandalia.

Dong anaongea ukweli , unaona sisi tuna miaka sabini mpaka saa lakini tupo kwenye levo ya nafsi , nadhani tunapaswa kuhakikisha kupata hivyo vidonge kutoka kwake hata kama ni kumuua”Waliongeleshana kwa kutumia hisia.

Roma hakuwaelewa walichokuwa wakiongea lakini alijua wanawasiliana kwani alihisi msisimko wa hali ya juu.

Naunga mkono hoja, hatuwezi kumruhusu binadamu mweusi kumiliki kitu cha thamani , tukivipata naamini ndani ya muda mfupi tutakuwa levo za juu na hakuna yoyote anaeweza kutuchukulia wa kawaida

Kwahio tunafanyaje?”

Wewe niachie mimi , huyu ni binadamu anawezaje kutushinda viumbe kama sisi ambao tunaweza kufanya chochote”

“Mr Roma vidonge unavyozungumzia ni vya aina gani unaweza kuvielezea?”

“Rangi yake ni njano kama vimeunguzwa na moto mkali ukubwa wake ni kama gororoli”

“Huateng nadhani anazungumzia Poya, vidonge namba moja wanavyomiliki wale wazee wa Kekexil hakika tukivipata lazima tuvunje levo za juu”Waliongeleshana tena kwa njia ya hisia.

“Mr Roma nadhani unazungumzia vidonge maarufu daraja la kwanza vya Poya?”

“Oh! …. Ndio jina lake hilo , Master alinipatia vya kutosha lakini hakuwahi kunielezea jina lake na niliweza kupanda levo bila hata ya usimamizi wake”Aliongea na kuwafanya waangaliane kwa kupeana ishara ya kuridhika.

Huateng kwahio tunafanyaje?”

“Senior Dong nadhani atuonyeshe vilipo, itakuwa rahisi kuvichukua”


Upo sahihi” Waliendelea kuwasiliana na kumfanya Roma azidi kuona mtego wake unafanya kazi.

“Mr Roma unaweza kutuonyesha japo hata kidonge kimoja ili tuweze kuvihakiki”

“Nipo tayari, ninaweza kuwapatia kila mmoja vitatu vitatu , kila kidonge kimoja kitakuwezesha kupanda levo moja”

Roma aliona tayari ndoano yake ishakamata samaki , kuhusu vinavyofanana hakuotea ni kweli alikuwa akijua kuhusu Vidonge na aliweza kujifunza uwepo wake mara baada ya kwenda China katika ngome za Tang kusoma nyaraka za mafunzo ya kijini na utamaduni wa kichina kwa ujumla.

“Tutashukuru sana Mr Roma kama utatupatia , hakika hatuwezi kusahau ukarimu wako?”Aliongea yule mwanamke ambaye mara ya mwisho alionyesha jeuri , lakini kwasababu ya kuwa na tamaa ya kutaka kupanda levo ya juu zaidi , alionyesha kuhiraji kwa hali na mali vidonge vinavyozungumziwa.

Roma katika mazungumzo hayo alikuwa ashaweza kupata mambo mawili , jambo la kwanza alijua kabisa kuhusu Taa ya uhai wa Nafsi na kama wameweza kujua mahali ambapo Monk amekufa ni hapa Tanzania basi ni hakika walitumia hizo Lantern kufatilia.

Alijiambia kama atawauwa wakiwa ndani ya mipaka ya Tanzania basi Hongmeng watafahamu , hivyo mpango wake wa kwanza ni kuwatoa Tanzania na kuwapeleka hata Kenya na kisha angewaua na kuchukua Dhana zao pamoja na vidonge ambavyo ameviona wameficha kifuani na kisha angempelekea Rufi na kuvithaminisha kama vingekuwa na uwezo na usalama na angewapa wanawake wake wameze ili iwarahisishie kupanda levo kwa haraka.

Hayo ndio aliojifunza katika nyaraka alizosoma China, aliamini kama angepata vidonge basi ingekuwa rahisi kwake kurahisisha mafunzo kwa warembo wake na mwisho wa siku wangeweza kufikia levo ya nafsi kwa haraka na angepata amani ya kupata mtoto.

Shida moja ni kwamba hakujua ni kwa namna gani angeweza kupata vidonge , hivyo mpango ulikuwa ni mmoja tu kila atakapokatama kiumbe chochote kutoka Hongmeng angeua na kisha kuiba Dhana pamoja na vidonge.

“Kama mnahitaji kuviona na niwapatie basi mnapaswa kunifuata, kutokana na ubora wake nilivificha mbali na hapa ili watu wenye tamaa wasije kuviiba”

“Tupo tayari kukusindikiza ili mradi utimize ahadi yako ya kutupatia vitatu vitatu”

“Kama mpo tayari nifuateni”Aliongea Roma na kuwafanya waangaliane

“Huateng , tunachukua vyote halafu tunamuua , tukirudi kwenye miliki lazima watunyenyekee”

“Senior , upo sahihi , safari yetu ya dunianni imeleta baraka
”Waliongeleshana tena na kisha walimfuata Roma.

Roma hakujua hata uelekeo , yeye alitambaa kwa spidi kubwa huku akitafua eneo zuri ambalo lingefaa kuwamaliza.

Nani kasema majini hayana tamaa licha ya kuwa na uwezo wa juu wa kufunuliwa mambo mengi, Tamaa ndio udhaifu mkubwa ambao sio binadamu aliewekewa bali kwa kila kiumbe chenye utashi wa akili , asilimia kubwa ya Dhambi zote zinazofanyika chanzo chake ni tamaa na watu hutofautiana viwango vya tamaa kutokana na mazingira , udhaifu wa tamaa unaweza ukalala ndani ya mtu lakini siku atakayopatwa na shida na njia ya haraka ya kutatua shida ikajitokeza basi tamaa huamka na kuzivaa akili , wachache walioweza kuzishinda tamaa ndio wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Roma alikuwa akiwaza hivyo kwenye akili yake huku akitafuta mahali , pazuri na baada ya kusafiri umbali mrefu kwa muda mfupi aliweza kuhisi wapo nje ya Tanzania na kwa haraka haraka akili yake ilimwambia yupo Kenya.

Hili eneo ndio sahihi , kuna mifupa mingi hili eneo yenye roho za chuki zilizolala , nadhani waliokufa hapa wengi sio kwa hiari yao”Aliwaza Roma mara baada ya kutua kwenye moja wapo ya shamba kubwa ndani ya Kenya.

Mchawi hahitaji macho kujua uwepo wa kaburi ,anahitaji uwezo wake wa kichawi kutambua roho za binadamu zilizolala.

Kwa mfano kundi la Takamagahara nido kundi la kichawi kutoka Japani ambalo hutumia roho za wafu waliokufa wakiwa na chuki na hukusanya ile mifupa na kuigeuza kuwa pepo na ndio hutengeneza siraha zao za kichawi.

Katika ulimwengu wa Roho binadamu akifa akiwa na chuki au akifa kifo cha kulazimishwa ni ‘Asset’ kwa wachawi kwasababu roho yake hupatikana kwa urahisi kupitia mifupa yake , ndio maana siku zote waganga wa kienyeji na wachawi hutumia makaburi ya wafu waliokufa kwa chuki katika kazi zao za ulozi au tiba.

“Mr Roma kweli umechagua eneo sahihi , hii sehemu inaonyesha kuwa na roho za binadamu waliokufa kwa kulazimishwa na naona nyingi zimeshikiliwa na mifupa naaminni hili eneo limetengenezwa kwa kazi maalumu”.

Ilikuwa kama Roma alivyofikiria , hili eneo lilionekana kutegenezwa kwani hakuna makaburi kwa juu bali kuna vifusi pekee vyya makaburi na Roma aliweza kuona ndani ya kaburi moja kuna zaidi ya miili ya watu wawili.

“Mr Roma nadhani unapaswa kutonyesha sasa na kutupatia ili kutimiza ahadi yako”.

“Sikuwa na mpango wa kuwaonyesha vidonge, kama mlivyosema hili shamba limetengenezwa kwa ajili ya ibada za kishetani basi sina budi kuongezea na roho zenu hapa?”Aliongea Roma.

“Kwahio ulikuwa ukitudanganya?”

“Pigia mstari , unafikiri mimi ni mjinga niweze kuweka ahadi na watu kama nyie ambao mnaongozwa na tamaa , leo ndio mwisho wenu, kosa kubwa ambalo mmefanya ni kujaribu kunitishia lakini pili kudharau juhudi zangu , mheshindwa kudhibiti raia wenu wanakumbwa na ukichaa halafu bado mnajiita ndio mnaolinda misingi ya Taifa la China , niliwasaidia kuwaondolea adui yenu lakini hamuonyeshi Shukrani , labda vifo vyenu vinaweza kuwa zawadi kwangu”Aliongea Roma na kabla hawajajua cha kufanya Roma alimsogelea Huateng kwa kasi na kuinua mkono wake huku akiita nguvu ya kimaandiko kuielekezea mkononi na kuisha akapiga kibao hewani akiwa amemlenga , Huateng alionekana mzoefu kwani aliweza kukwepa haraka na laiti kingempata kutokaa na levo yake ingekuwa kifo chake.

Na palepale bila ya kuchelewa alitoa upanga wake kwenye Ala na Aura ya upanga wake ilisababisha baadhi ya Roho zilizolala kwenye mifupa kuanza kuamka na Roma aliona hio ni hatari kwani Roho hizo zikitoka kwenye mifupa yake zinageuka kuwa mapepo na kwenda kuvamia watu wenye nguvu chache za ki ulinzi kiroho.

Alichokifanya ni kuachia nguvu ya kijini kulifunika eneo lote ili isitokee Roho hata moja kutoka kwenye mifupa yake.

Upanga wa Huateng uling’aa na kutoa mwanga uliombatana na ukungu kama moshi na mng’ao mithiri ya mwezi.

“Go Xuanshui” Aliongea maneno ya kichina ambayo Roma hakuyaelewa lakini alijua yanavyotamkwa na palepale upanga ulitoa mng’ao zaidi na kumuumiza macho kiasi cha kuyafumba na ile anafumbua aliweza kuona ukuta kama wa barafu mbele yake umejitengeneza kichawi.

Roma alishangaa uwezo huo wa kimajabu uliofanikishwa na siraha ya upanga tu , lakini hata hivyo kwake ukuta huo ulikuwa mwepesi sana kuubomoa. Haukuwa ukuta kama ukuta halisi wa barfu bali ni wa kichawi.

Huateng baada ya kutengeneza ukuta ule , alipata muda na palepale aliongea maneno mengine ya kichina yasioeleweka na palepale kwenye mikono yake iliweza kuonekana Gukini(Guqin), ni aina flanii hivi za gitaa au Zeze ambazo zilitumika sana kipindi cha enzi za kale katika tamaduni za China na mara nyingi huwa na nyuzi saba ambazo hutoa sauti zinazotofautiana, Huateng hakuishia hapo alitoa pia unyonya wa ndege maarufu wa kichawi Phoenix.

Roma alishangaa lakini aliweza kugundua kitu kimoja cha kufurahisha , alishawahi kusikia kuhusu lugha maalumu ambayo majini na watu wanaoabudu vitu vyenye asili ya ushetani hutumia lugha kuingia kwenye mzingo wa Sumeru , kilichomfurahisha Roma ni kwamba hakujua kama unaweza kuiiita Sumeru ukiwa ndani ya bara la Afrika , alijua iliwezekana tu kwa bara la Asia.

“Unapata wapi uthubutu wa kujifanya mjanja mbele yetu”Aliongea Huateng na kisha akajikalisha kwenye hewa kwa kukunja miguu kama vile amekaa chini kwenye mkeka au zulia na kisha akaweka lile gitaa huku akianza kurekebisha zile nyuzi akionyesha anataka kuanza kupiga mziki.

Roma alishindwa kuelewa ni nini anataka kufanya , kwani hakuwahi kufikiria uwepo wa Dhana ya aina hio lakini aliishia kujawa na msisimko wa kutaka kufahamu.

“Tii , Taaa, Tuu….!!” Huateng alidokoa nyuzi moja moja kwa namna ya kupiga akitumia ule unyoya na Roma ndipo alipoweza kujua nini kinatokea.
 
SEHEMU YA 483.

Gukini ilionekana kuwa na muunganiko wa moja kwa moja na nguvu za kijini za Huateng , alikuwa kila akidokoa uzi na ule unyoya mara tatu kulitokea mshale wa kichawi na ulinyooka mahali sawa na Roma aliposimama na mbaya zaidi uliweza kupita kwenye ule ukuta wa barafu bila ya kizuizi.

Roma alifurahishwa mno na hio Dhana alijiambia mwenyewe kwa mfano angempa Edna aimiliki hiyo haitampa shida hata ya kupambana kazi yake ni kucharaza gitaa tu na maadui wanadondoka.

Roma alijiambia Yes, Dhana zote hizo mpaka muda huo ni za kwake na anachotakiwa kufanya ni kuwaua na kuchukua, lakini kabla ya yote lazima aangalie kwanza zinavyotumika.

Roma hakujisumbua hata kukwepa ile mishale , kwani uwezo wake ulikuwa mdogo sana kumdhuru ,hivyo aliita nguvu ya Kimaandiko na kutengeneza ngao na mishale ilipogusana ngao tu ulipotea bila ya kumfikia , ukweli hata kama angeruhusu umchome isingemletea pia shida maana anao uwezo wa kujiponyesha.

Huateng alicharaza gitaa kama mwehu , alianza taratibu taratibu na kuanza kukoleza na alionekana mzoefu mno kwani alitengeneza mziki wa solo wa aina yake , lakini sauti yake ilikuwa ikiamsha siraha za kichawi na kumshambulia Roma , kila alipojitahidi hakuna kilichoonekana kuleta madhara kwa Roma kwani mishale yake ilipotea.

“Inawezekanaje Gukini na unyoya wa Phoenix ushindwe kukudhuru?”Aliongea Dong kwa mshangao kwani hakuamini Roma angekuwa na uwezo mkubwa wa kujikinga.

Dong yule mwanamke palepale alianza kuchezesha elemeti za anga na mkono wake ukatengeneza mpira wa barafu na kuurusha kwa nguvu zote kumlenga Roma.

Roma nae alikusanya nguvu zote kwenye kiganja na lile barafu kabla halijamfikia aliachia wimbi na vikakutana katikati kwenye ule ukuta na ukaporomoka wote.

Wakati Roma anapambana na Dong , Huateng aliendelea kucharaza Zeze lake kama kichaa lakini hata hivyo kila siraha iliomfikia Roma ilikuwa kwake kama upepo kwani haikumdhuru.

Sio kwasababu Dhana zao zilikuwa na uwezo mdogo , lakini ukweli ni kwmaba wao ndio ambao walikuwa na uwezo mdogo wa kuziendesha kwa kiwango chake cha mwisho, ni sawa na kusema kama Roma akaamua kuicharaza Gukini ya Huateng basi angeweza kuleta madhara makubwa kwasababu levo yake ilikuwa kubwa.

“Kimbia”Aliongea Dong akimwamrisha Huategn kukimbia , mpaka hapo alishaona wakiendelea kushindana na Roma wangeishia kupoteza maisha.

Huateng aliona atii kauli ya mwenzake na palepale alijikusanya na kuanza kukimbia kuelekea katikati ya nchi ya Kenya huku Dong akijaribu kupambana na Roma.

Roma aliona huo ni ujinga palepale alianza kufanya kitu cha ajabu ambacho ghafla tu kilitengeneza moto wa njano kama dhahabu kwenye mikono yake na ukawa kama vinyoka nyoka na aliviachia na kumfuata Huateng kwa kasi na vilionyesha kuwa na spidi kuliko ya kwake.

Dong alionyesha mshangao mara baada ya kushuhudia uwezo ule , ulikuwa ni uwezo wa juu kabisa ambao alijua mtu mwenye uwezo huo lazima afikie levo ya kuipita Dhiki na mpaka hapo alijua alikuwa akipambana na mtu wa levo ya juu kuliko yeye , ilikuwa ni kama anapambana na wazee wa miliki ya jamii yake.

Vile vinyoka vyoka vya moto vilianza kumzingira Huateng kwa spidi kali na kutengeneza kama dura huku yeye akiwa katikati , bado hakuwa ameachia zeze lake na alijitahidi kuzuia joto kwa kuendelea kulicharaza kisawa sawa na ule unyoya lakini moto wake ulikuwa mkali kama wa kuyeyushia chuma.

“Sikia nadhani muacha kukimbia kwani mtanifanya niharibu hizo Dhana wakati nazihiraji”Aliongea Roma huku akicheka.

“Mr Roma naomba utusamehe”Aliongea huku akianza kutetemeka ule ujasiri wa kupambana na mtu mwenye uwezo wa kudhibiti moto wa rangi ya njano aliogopa.

Ukweli Roma muda huo alitamani kutumia moto wa rangi nyeupe , lakini alishindwa kuelewa kilichofanyika kwani wakati anapambana na Yan Buwen mwili wake ulikuwa ukitumika tu na mtu anaeishi ndani yake ambaye ana mpango wa kutawala mwili wake.

Hivyo kama ni kujifunza ni machache aliopatia kama kudhibiti moto wa joto la hali ya juu.

Roma mara bada ya kuona ashawadhibiti na hakuna namna ya kukimbia alitengeneza upanga wa moto kwa kuchezesha viganja vya mikono yake huku akiongea maneno yasioeleweka na palepale mapanga mawili yalifyatuka na kuwasogelea kwa kasi na Huateng ndio aliekuwa wa kwanza kunaswa eneo la tumboni na akafuatia Dong.

Roma alijiambia ndio kazi nzuri , aliwasogela huku akiwangaalia kwa tabasasamu la dhihaka.

“Unaweza kutuambia kwanini unataka kutuua , hata kama tulikuonyeshea kiburi lakini hatukua na nia mbaya na wewe”Aliongea yule mwanamke Dong huku akitia huruma.

“Jibu ni rahisi kwanza kabisa mmedharau ukarimu wangu , pili mlianza kunitishia huku mkiamini siwezi kuwafanya chochote kwasababu mnatokea Hongmeng , ngoja niwaambie ukishanikasirisha mimi sina huruma na kuua mimi ni jambo jepesi kuliko kusamehe”

“Huoni kwamba unajiingiza kwenye matatizo , kama wazee watafahamu umehusika na vitu vyote lazima watalipiza kisasi na hutowaweza kwani wapo kwenye levo ya anga kati ya mbingu na Ardhi, nadhani shida yako ni Dhana zetu pamoja na vidonge lakini nakuhakikisha kinachokusubiria ni kikubwa zaidi ya vifo vyetu”’

“Hata kama ningewaacha watu kama nyie mkaondoka , lazima kuna wengine wangekuja kunichokoza tu na kutaka ugomvi na mimi , nitakuwa mjinga kama sitochukua hatua mapema”

“Nakuambia utajutia kitendo chako cha leo”Aliongea Dong.

“Asante kwa kujali , lakini usiwe na wasiwasi nitawatuma wenzako wengine ambao watajaribu kunichokoza ili usiwe mpweke sana”Aliongea Roma na palepale ule upanga uliomchoma eneo la tumboni ulianza kuongezeka ukubwa na alianza kuyeyuka palepale taratibu taratibu na kikawa kifo chake , hivyo hivyo kwa Huateng akapoteza maisha.

Roma alianza kuchukua Dhana zao , alichukua Gitaa na unyoya wake , Upanga ambao uliitwa Xuanshui na kisha aliweza pia kupata pete pamoja na chupa ya vidonge vinavyofanana kabisa na P2 na Roma alipoisoma ile pete aliweza kugundua sasa hio ndio aliotumia Huateng kufungua Sumeru, ilikuwa ni Sumeru Ring .

Roma mara baada ya kuona kazi yake imemalizika hakutaka kubakia hapo tena , hata hivyo halikuwa eneo zuri kutokana na roho za wafu , aliondoka na kurudi Tanzania , alijua fika kwamba muda si mrefu Hongmeng watafatilia vifo vyao , aliwaua Kenya ili wasije wakafahamu kwa haraka kama amehusika , lakini alijua muda si mrefu wataagiza mwingine kuja kwake kwa ajili ya mahojiano na alijisemea akija mwingine anaua tu na kuwaibia.

Mpango wake haukuwa kuwaibia tu , alipanga pia akipata Dhana sahihi basi angezamia ujinini kwenda kuiba vizuri.

Siku iliofuata asubuhi wote waliamkia Chapati za maji ambazo zilipikwa na Mama yake Roma.

“Lanlan hio chapati ya mwisho ni ya kwangu”Aliongea Roma akimwangalia Lanlan ambaye alikuwa kwenye mavazi ya shule na alishangaa siku hio kachelewa.

“Baba hashindani na mtoto kula”Aliongea Lanlan huku Roma akitaka kupeleka mkono kuchukua chapati , lakini Edna alimpiga kwenye kiganja cha mkono.

“Usishindane na mtoto kula , anahitaji kula ashibe ili akue , wewe hata usishibe sio kwamba utakufa”Aliongea Edna

“Haha… Shemeji inabidi ufanye juhudi kwa staili hii Lanlan anaweza kukufunika kabisa”Aliongea Sophia na kumfanya Roma amwangalie kwanza hajazoea Sophia kumuita Shemeji.

“Acha kunitania la sivyo siwezi kukusindikiza kwenda studio kama ulivyoomba”.Aliongea na kumfanya Edna awaangalie na akaanza kumnawisha mikono Lanlan .

“Halafu mbona kachelewa leo kwenda shule?”

“Nitaenda nae leo nataka nikaongee na mwalimu wake nijue maendeleo yake kwa ujumla anavyochangamana na wengine”.

“Sister unahofia kwasababu sio mtoto wa kawaida anaweza kushindwa kuchangamana vizuri?”

“Hilo sihofii kwani Lanlan ni msikivu , ila kuna tahadhari napasawa kuchukuwa”

“Wife usiwe na wasiwasi , haina haja ya kuchukua tahadhari , Lanlan uwezo wake inaonyesha ni kwa ajili ya kujilinda sidhani ni tatizo”.

“Kwahio unanishauri nisiwaambie kuhusu uwezo wake?”

“Haina haja, unapaswa kumuamini kama unavyoniamini, Lanlan ni mtoto wangu na hawezi kuwa wa kawaida”Aliongea Roma na kumfanya Edna kupata ahueni, ukweli kila muda ambao Lanlan anakuwa shuleni anakuwa na wasiwasi mno.

Baada ya Edna kuondoka na Lanlan na Roma na yeye aliondoka akiwa ameambatana na Sophia , mpango wake amfikishe Studio na baada ya hapo amtafute Rufi ampe maelezo kuhusu Dhana na Vidonge alivyoweza kupata.

Roma alikuwa na siku nyingi hajaenda ofisini lakini hata hakujali, siku hio alikuwa na ratiba nyingi alipanga kumtembelea Rose kujua maendeleo yake na baada ya hapo amtafute Amina.

Baada ya kumfikisha Sophia Studio moja kwa moja alianza safari ya kurudi Mikocheni na ilimchukua dakika chache tu aliweza kufika.

Wakati Roma anataka kuingia upande wa lift , aliweza kumuona Rufi akiingia upande wa Supermakert , alimfuata nyuma nyuma lakini mara baada ya kufika katikati akiwa hjamuona Roma , ghafla alisimama huku akionyesha wasiwasi.

Roma aliangalia mbele kwa mshangao na kuona nini tatizo na aliweza kumshuhudia msichana wa kichina alievalia begi akiwa ameshika trey , alikuwa rika la Rufi ki umri.

Kabla yule mwanadada hajageuka nyuma Rufi aligeuza alikotoka na kuanza kukimbia, alimuona Roma mbele yake lakini hakuongea nae na kumpita, kitendo kile kilimshangaza Roma na kumfanya amchunguze yule msichana na alugundua alikuwa binadamu wa kawaida lakini mwenye mafunzo ya kijini tena akiwa levo ya nusu mzunguko.

Alikuwa mrembo haswa na rangi yake nyeupe pamoja na nywele ndefu , ambacho Roma hajapenda ni shepu tu basi lakini sura ilivutia, alikuwa amevalia Haedphone masikioni.

Roma hakuona haja ya kuendelea kumwangalia na aligeuza kumfuata Rufi.Baada ya kupandisha juu kwa lift, mlango wa nje ulionyesha kufunguliwa hivyo aliingia bila ya hodi na kumkuta Rufi amekaa kwenye Sofa.

“Inaonyesha umenifuata , kuna unachotaka nikusaidie”Aliongea Rufi huku akionyesha kuwa siriasi na Roma hakumzoea hivyo ila hakutaka kuleta mbwembwe maana yupo hapo kwa ajili ya kuongea nae vitu vya msingi.

Alimtolea vile vitu vyote alivyowachukulia wale watu wa Hongmeng na kuweka mbele ya Rufi.

“Umevitoa wapi hivi?”Aliuliza Rufi huku akionyesha mshangao. Na Roma alimwelezea kila kitu.

“Umefanya vizuri kuwaua , wanajikuta wana dharau sana binadamu wa kawaida , ningekuwa na uwezo ningewaangamiza wote , Hongmeng sijuo Kekexil wote ni mashetani na hawajawahi kuwa na wema wowote kwa binadamu wanachowaza ni faida tu”Aliongea Rufi huku akionyesha chuki ya wazi wazi.

“Unapaswa kuiona dunia kwa uzuri wake wa nje na sio chuki ndani yake , ukiishi hivyo utaishia kuwa mwenye maumivu”

“Kwa upande wako sawa , kwasababu nao uwezo wa kuamua matokeo ya maisha yako lakini kwangu mimi ni tofauti kabisa , sijawahi kuwa na tumaini maisha yangu yote zaidi ya chuki na maumivu yalioujaza mwili wangu ,siku nitakayopata nafasi nitawarudishia mara mia moja”Aliongea kwa hasira mno na kwa jinsi mudi yake ilivyo Roma alijua mwananemke ambaye Rufi alikuwa akimkimbia huenda anamfahamu, ila hakutaka kuuliza kwa muda huo kwanza , alichokuwa akipanga baada ya hapo ni kumfatilia yule mwanamke na kumjua vizuri , Rufi ashakuwa jukumu lake la kumlinda hivyo alipaswa kuhakikisha anakuwa salama na hivyo kwa kipindi hicho Hongmeng walionyesha kutokuwa na wasiwasi kuvuka bara la Asia , basi aliona kama sio leo au kesho basi keshokutwa wanaweza kunyaka uwepo wa Rufi Tanzania na kutaka kumrudisha.

“Naomba unisamehe kwa kuonyesha hasira zangu mbele yako”Aliongea huku akiwa anaangalia vile vitu kwa namna ya kuvikagua.

“Nafikiri sasa unapendeza zaidi , kuliko kipindi ulivyokuwa ukinitega”Aliongea Roma na kumfanya Rufi atingiche mabega huku akikosa ujasiri wa kumwangalia machoni .

“Hizi zote ni dhana ambazo zipo daraja la pili , nafikiri wamepewa kuja navyo kwa namna ya kuazimwa huo upanga licha ya kutengenezwa kwa chuma kutoka ncha ya Kaskazini lakini pia umezindikwa na nguvu ya barafu ya kichawi , huu unyoya siwezi kuelezea sana ni wa ndege wa Phoenix ukiunganisha na Gukini ni dhana yenye uwezo mkubwa sana kukaribia za daraja la juu kabisa , inaonyesha aliekuwa akitumia uwezo wake wa kuudhibiti ulikuwa mdogo, kuhusu hii pete inatumika kufungulia anga la Sumeru lakini sidhani kama inaweza kufanya kazi kubwa zaidi kutokana na malighafi yake”

“Unamaanisha kuna yenye uwezo zaidi ya hii?”

“Ndio na haitumiki kufungulia anga tu lakini pia inafungua milango mingi ya kiroho”

“Vipi kuhusu hivyo vidonge?”

“Hivi naweza kusema una bahati kubwa kuvipata ,ijapokuwa ni vidongea daraja la mwisho lakini vinauwezo wa kubusti mtu anaeanza mafunzo na kuingia mzunguko kamili kwa urahisi hata pia kuweza kufikia levo ya nafsi , kwa mtu mwenye levo ya juu havina msaada mkubwa , kwa makadirio uwezo wake ni asilimia hamsini tu”

“Hamsini mbona ndogo sana”Aliongea Roma huku akionyesha hajapenda

“Unachukulia kawaida asilimia hamsini, Vidonge katika miliki za kijini ni muhimu zaidi kuliko hata Dhana , kwasababu mimea ambayo hutumika kutengenezea imeshapotea kwenye mazingira yao na mara nyingi huja huku duniani kuitafuta”

Roma aliona ni kweli , kama vidonge hivyo vilikuwa vikisaidia watu kuingia kwenye levo ya Nafsi , basi huko kwenye miliki watakuwa wengi ambao wapo kwenye levo hio na sio vya kudharauliwa hata kidogo.

“Vina athari yoyote?”

“Havina athari kwa ambaye amefikia levo ya nusu mzunguko na kutaka kuingia mzunguko kamili au levo ya Nafsi”Aliongea na kumfanya Roma kuona basi mtu sahihi anaepaswa kumeza ni Magdalena , maana mara ya mwisho wakati anapambana na Yan Buwen alikuwa ashaingia mzunguko kamili.

Wakati Roma anataka kuuliza swali lingine , simu yake ilianza kuita na alipoitoa kuangalia jina la anaepiga alishangaa kuona namba ni mpya , lakini pia haikuwa ya kitanzania kwa uzoefu wake wa kuishi mataifa mengi aliweza kujua ni kutoka Korea Kusini alipokea.

“Hello!”

“Hello”Sauti ilijibu ya kike lakini ilikuwa dhaifu mno.

“Yezi!”Aliita Roma mara baada ya kuifahamu lakini baada ya kuongea hivyo upande wa pili kulianza kusikika vilio na kumfanya Roma kuwa na wasiwasi , ni kweli hajawasiliana na Yezi tokea aondoke , lakini alishangaa amempigia na kuanza kulia.
 
SEHEMU YA 484.

Roma alishangaa mara baada ya simu ile kukatwa, alijaribu kupiga tena lakini haikuunganishwa wala kupokelewa na alijikuta akikata tamaa , lakini pia alipatwa na wasiwasi kwa kujiuliza ni nini kinaendelea.

Sio kwamba walikuwa wamemsahau Yezi , ukweli ni kwamba waliamini angekuwa salama kutokana na uwepo wa babu yake ambaye alimhitajji na mara ya mwisho Edna aliweza kupata taarifa ya babu yake Yezi kuendelea vizuri hivyo hakupata wasiwasi tena.

Roma mara baada ya kukata simu aliwaza kwanza namna ya kumlinda Rufi maana kama watu kutoka miliki zisizoonekana wakifika Tanzania na kumkwapua basi anaweza hata asipate nafasi ya kumsaidia.

“Kuna mtu nitamwagiza na atakuletea Panick Button ambayo ipo kama saa , utavaa mkononi na wakati utakapokuwa kwenye hatari na kuona huwezi nipigia simu hakikisha unabonyeza”Aliongea Roma.

“Una wasiwasi na mimi?”

“Ndio nina wasiwasi , mke wangu kaniambia nikulinde nisipomtii anaweza kuwa na huzuni akisikia umechukuliwa na kurudishwa, labda kama kuna kitu kingine unataka kuniambia”

“Nilidhani utaniuliza”

“Uliekuwa umkimbia ni nani haswa , yule msichana wa kichina ni nani?”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kuwa kimya.

“Anafahamika kwa jina la Luo XiaoXiao nilikutana nae wakati nikiwa kwa wakwe zangu kabla ya kutoroshwa unaweza kusema ni shemejji yangu”Aliiongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Kwahio unamaanisha washafahamu upo Tanzania?”

“Sidhani lakini nina waswasi na kuonekana kwake hapa Tanzani , Luo XiaoXiao ni wa tofauti sana , licha ya baba yake kuwa mkuu wa koo katika miliki zizizoonekana lakini alipenda sana kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa.

“Kama ni hivyo hupaswi kuwa na wasiwasi nitaangalia kama yupo hapa Tanzania kwa sababu gani” Aliongea Roma na Rufi alitingisha kichwa na kukubali na kisha aliaga na kuondoka.

Roma mara baaada ya kusogelea gari alijikuta akitabasamu kifadhuli mara baada ya kuhisi kitu kisichokawaida , lakini hata hivyo hakugeuka nyuma zaidi ya kuingia ndani.

“Jielezee mwenyewe unafanya nini ndani ya gari yangu?” Aliongea Roma huku akivaa mkanda na palepale aliwekewa kisu eneo la shingoni.

Hakuhitaji kugeuka nyuma kufahamu aliekuwa nyuma ni nani , kutoka na na harufu ya marashi kufanana kabisa na ya kike.

Alikuwa ni yuleyule msichana ambaye Rufi alimkimbia na haikueleweka aliwezaje kuzama ndani ya gari pasipo ya kuonekana kwani maegesho ya muda mfupi yalikuwa wazi kiasi kwamba hata watu wa barabarani wanaona.

“Jielezee na wewe kwanini ulikuwa ukinikodotea macho”Sauti ya kike ya kichina iliongea na kumfanya Roma kutabasamu, hakujali kisu kilichowekwa kwenye shingo yake bali alianza kuendesha gari huku akiangalia kioo cha juu.

Alijiambia kazi imerahisishika lakini hata hivyo alipenda ujasiri wa mtoto huyo wa kike ,alijiuliza imekuwaje mpaka akafahamu hilo ni gari lake na kuingia kumsubiria.

“Usiendeshe gari yako kabla hujajibu maswali yangu la sivyo nitakata mshipa wa damu” Aliamrisha huku akizidi kumkandamiza Roma na kile kisu , lakini Roma hakujali aliendelea kuendesha kutoa gari na kuliingiza barabara kuu.

“Hunisikii, nitakuua kweli” Aliongea huku awamu hii akibadili lugha kwenda ya kingereza.

“Umejiteka mwenyewe kwanini nisimamishe gari , wewe ni halali yangu kuanzia sasa”Alitania Roma huku akicheka na aliendesha gari kuelekea Kawe na yule mwanadada aliendelea kumkandamiza na kile kisu kiasi kwamba damu zilianza kutoka , lakini Roma wala hakuogopa.

Baada ya kuendesha na kufika usawa wa Tanganyika Parkers kwenye eneo la bustani ya maua alikata kulia na kuingia Kawe Beach na alienda kusimamisha mita kadhaa kutoka kilipo kiwanda cha kuchakata mchanga na kisha akafungua mlango na kutoka.

Yule mwanaadada wa kichina alikuwa amekasirika mno , kwanza Roma alifurahi baada ya kujua ni aina ya wasichana ambao hajawahi kuua mtu.

“Wewe ni nani?” Kauliza tena na Roma alimwangalia , alikuwa vilevile na mavazi yake lakini awamu hii alikuwa hajaweka Headphone masikionni.

“Mimi ni mwanaume ambaye ulitaka kumteka mchana kweupe”

“Niambie wewe ni nani la sivyo nitakuadabisha , kwanini una nguvu isiokuwa ya kawaida kwenye mwili wako?”

“Na wewe kwanini una nguvu isiokuwa ya kwaida kwenye mwili wako?”

“Jibu swali langu wewe ni nani , kabla sijachukua hatua nyingine wewe binadamu”Aliongea na kumfanya Roma kuona utoto ndani yake.

Roma hakujali sana kuhusu maswali yake bali alitembea kuelekea kwenye fukwe na kwasababu ilikuwa muda wa mchana hapakuwa na watu wengi zaidi ya viti viti vilivyoinamizwa kwenye meza.

Luo XiaoXiao alijikuta akikasirika mno, hakuamini binadamu anaweza kumdharau na alimkimbilia Roma huku akipanga kwenda kumshambulia , lakini wakati anamfikia tu Roma alisongea pembeni na kumfanya kupita kwa kasi na alikosa balansi na kutua kwenye mchanga.

“Kama unataka nikujibu swali lako nieleze kwanini umeweza kugundua gari yangu na kuingia kunisubiria?”Aliongea Roma na kumfanya yule mwanadada kusimama tena huku akionekana kukasirika mno na kutamani kulia , kwani alichokuwa akifanyiwa ni nje ya mategemeo yake, mbaya zaidi mtu anaemchezea ni mtu mweusi ndio maana alikasirika zaidi.

Roma alimchunguza kuanzia chini mpaka juu na kuona namna alivyokabwa na suruali yake aliovaa , alikuwa mwembamba mno licha ya kuwa na sura nzuri.

“You Pervert…!”Aliongea kwa mara nyingine na awamu hii alimsoglea tena Roma na kutaka kumpiga na Roma hakumkwepa aliacha amfikie na kumruhusu kumpiga na kweli aliweza kumpiga na ngumi eneo la kifuani lakini baada ya kumpiga Roma alitoa kilio mwenyewe kwani mkono wake uliumia.

Asilimia kubwa ya watu ambao wapo kwenye levo ya nusu mzuguko hawana uwezo wowote wa kufanya maajabu, ila uwezo wao wa kimapigano wanategemea zaidi nguvu za mikono yao na miguu.

Kwa mfano ukawa na mafuzo ya Kung Fu au Tai Chi na ukawa pia na mafunzo ya kijini na kuifikika levo ya nusu mzunguko faida kubwa utakayopata ni utashi wa hali ya juu lakini kiwango chako cha kutabiri kinaongezeka au kwa lugha ya kimapigano wanaita Kan , kwamba mtu anakuwa na ‘intuition’ ya hali ya juu ya kutabiri adui angefanya nini na wewe unapaswa kufanya nini , lakini pili ni kwamba ngumi ya mtu ambaye yupo kwenye levo ya nusu mzunguko ikimpata binadamu wa kawaida basi inaweza kuwa ndio kifo chake kwani ina ujazo mkubwa sana na hicho ndio kilimwaminisha Luo XiaXiao kuamini angemdhibiti Roma kirahisi.

Jambo moja ambalo lilimchanganya Roma na kutomuuliza Rufi ni kwamba msichana aliekuwa mbele yake alijua kabisa hakuwa na damu halisi ya kijini alionyesha kuwa ni mchanganyiko na huenda anafanana kwa kiasi kikubwa sana na Rufi , lakini kilichomshangaza kama ni hivyo kwanini ?Rufi akadhaliwa na Yin Meridian kiasi cha kumpelekea kushindwa kujifunza mbinu za kijini lakini Luo XiaoXiao alikuwa tofauti.

“Hey niambie umewezaje kugundua gari yangu , huna uwezo wa kupigana na mimi?”

“Kama sina uwezo wa kupigana na wewe baba yangu mzazi huwezi kupigana nae”Aliongea kwa kiburi huku akishika kiganja chake kilichoumia , matendo yao yalifanya watu wawaangalie.

Yule msichana baada ya kuona hawezi kumzidi Roma aliingiza mkono kwenye mfuko wa kibegi chake na kisha akatoa bangiri na kumrushia Roma na aliidaka,Ilikuwa bangiri ya Edna na alishhindwa kuelewa kwanini alikuwa nayo.

“Ulifanya makusudi kuonyesha uwezo wako pale Supermarket ili nikutambue halafu ukapotea ulikuwa na maana gani?”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu, ni kweli alifanya hicho kitendo, ulikuwa mchezo wake , mara baada ya kuona Rufi anamkimbia na kumuona huyo mwanadada yupo kwenye levi ya nusu mzunguko aliachia Aura yake kwa kuisambaza ili yule msichana aweze kutambua uwepo wake na kisha akaifunika tena na nguvu ya kimaandiko.

Katika ulimwengu wa viumbe wanaotumia nguvu za ziada hupenda sana changamoto lakini pia wanaongoza kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na shauku , Roma alijua kwa kufanya vile yule msichana asingeondoka na kujawa na shauku ya kumtafuta mpaka ampate na alijua shauku yake ingekuwa kubwa kwasababu kwanza hapa ni Tanzania na ni mara chache sana kuona watu wa kawaida wanaojifunza mbinu za kuvuna nishati ya mbingu na Ardhi.

“Kwahio unamaanisha uliweza kunitafuta kwa kufuara hii bangiri?”Aliuliza Roma.

“Unaonekana kushangaa, inaonekana hujui mambo mengi licha ya kuwa na vinguvu, nakuambie humuwezi baba yangu mzazi”Kaliongea na Roma aliangalia ile bangiri na kujua Edna atakuwa aliisahau kwenye gari , ilionekana ni sahihi maana kwenye harusi hakuwa ameivaaa lakini alijiuliza ilimtoka lini mkononi na kuwa kwenye gari yake.

Roma aliona ni sahihi kama kweli Luo XiaoXiao aliweza kuipata gari yake kwa kuona hio bangiri kwani yenyewe ilikuwa ya kijini.

“Hili taifa asilimia kubwa nimekutana na watanzania wenye Dhana za daraja la chini na asilimia kubwa nyingi sio za ulinzi bali ni za mvuto na utajiri lakini hio bangiri ndio tofauti kati ya zote , imetengenezwa kwa ajili ya ulinzi na ipo kundi la kati katika Dhana za ulinzi”Aliongea na kumfanya Roma kuona kweli ana hoja na anapaswa kusikilizwa.

“Nimekuelewa”

“Ni zamu yako kujibu maswali yangu , wewe ni nani?, unao uwezo wa kufunika nguvu zako hivyo naamini upo levo ya juu lakini kwanini ukanitega kwa kusambaza Aura yako nikutambue , inaonyesha una kitu unataka kujua kutoka kwangu?”

“Sio mbaya unaonekana una akili”

“Ni jibu”

“Nataka kujua kwanini msichana mrembo wa kichina mwenye mafunzo ya mbingu na Ardhi kuwa hapa Tanzania?”

“Kuwa mkweli acha kuzunguka , najua umevutiwa na mimi?”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Unnaongea nini kuvutiwa na wewe?”

“Kama sio hivyo ni nini, Umevutiwa na mimi kuwa mkweli wewe sio wa kwanza wanaume wengi mnachanganyikiwa na uzuri wangu”

“Hahaha..nishasema nataka kujua kwanini upo Tanzania ukinijibu swali langu nitakuachia”

“Ninasababu mbili za kuwa Tanzania ya kwanza nimekuja kwenye nchi niliozaliwa sababu ya pili nitakujibu mpaka unipe mawasiliano yako”Aliongea na kumfanya Roma ashangae anamaanisha nini kuzaliwa Tanzania mbona hana dalili ya mchanganyiko wa mtu mweusi.

“Acha uongo kama umezaliwa Tanzania , rangi yako ingekuwa inamchanganyiko na kama mama yako ni Mtanzania basi sio wa asili na kama wazazi wako ni wapitaji tu na ukazaliwa Tanzania sidhani kuna haja ya kuwa hapa nchini kwani hili taifa halikuhusu”Aliongea Roma.

“Nadhani ninapaswa kukuomba vitu vingi kutoka kwako nina weza kuzaliwa na mama mweusi lakini nikawa sionyeshi dalili yoyote ya kuzaliwa na mama mweusi hilo litategemeana na nguvu ya baba yangu , una uwezo mkubwa lakini unaonekana kutokujua mambo mengi”Aliongea na kumfanya Roma kuwaza kweli inawezekana au huyo mtoto anamdanganya

“Nitalifuatilia”Aliwaza Roma kwenye akili yake.

“Niambie sababu ya pili”

“Nipe mawasiliano yako”Aliongea na kisha akatoa simu yake na kumnyooshea Roma aweke namba yake.

Roma alijifikira kwa dakika na kisha alichukua ile simu na kuiandika haraka haraka na kisha akamrudishia.

“Unaweza kunijibu sasa”

“Tulia bro tuihakiki isije ikawa plate number” Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu, ni mwanamke ambaye alionekana kuwa mjanja kuliko hata Rufi alivyokutana nae.

Baada ya kuipigia ile namba na kuona inaita alitabasamu.

Anaweza kuwa kwenye levo ya Nafsi au zaidi halafu anaonekana kuwa mjinga , ninaweza kutumia ujinga wake na kufikia levo ya Mzunguko kamili au nusu Mzunguko kwa kufanya nae mapenzi”Aliwaza kwenye akili yake huku akitoa tabasamu na kuisevu ile namba kwa mbwembwe zote.

“Nadhani unapaswa kunijibu wewe binti”Aliongea Roma.

“Kwanini unataka kujua sana sababu ya uwepo wangu hapa Tanzania”

“Sihitaji maswali mengine kutoka kwako nataka majibu”Aliongea Roma huku akiweka usiriasi na kumfanya yule msichana kumwangalia na kisha akatoa kijikadi kwenye mfuko wake na kumrushia Roma na kuanza kutembea kurudi alikotoka.

“Nitakutafuta upokee simu zangu”Aliongea huku akitembea kwa kurudi nyuma nyuma.

Roma alisoma ile kadi na alishangaa mara baada ya kugundua msichana mdogo kama huyo alikuwa ni Director wa kampuni ya kichina ifahamikao kwa jina la Sunda tawi la Tanzania.

Roma mpaka hapo aliamini kuna uwezekano hakuwa Tanzania kwa ajili ya Rufi bali ni kikazi ndio maana akampatia hio kadi.

Roma alisimama kwa dakika kadhaa akimkodolea macho kwa nyuma na alitembea bila ya kugeuka na kumfanya ajiulize maswali mengi , kwanza alisema yupo Tanzania kwasababu mbili , ya kwanza ni kwa ajili ya mama yake ni mtanzania ya pili ni mfanyakazi wa kampuni kama Director, swala la kuwa Director halikuwa na shida ila swala la mama yake kuwa Mtanzania lilifikirisha.

Roma palepale alimkumbuka Zenzhei aliamini angekuwa na majibu , alitoa simu yake na kumpigia Afande Kweka huku akiingia kwenye gari.

“Wewe mtukutu umenikumbuka baada ya kutibua hali ya hewa ya nchi”

“Unamaanisha nini wewe mzee ,nani kutibua hali ya hewa ya nchi?”Aliuliza Roma huku akijifanyisha haelewi Afande Kweka anachojaribu kuongea.

“Kama sio wewe nani anaweza kuyumbisha mifumo ya taifa, Nilijua upo Honeymoon na mke wako kumbe umerudi na kusababisha vifo”

“Mzee unanisingizia kama unamaanisha Mstaafu Kigombola sihusiki na hesabu za vifo nilivyosababisha tokea nirudi ni vitatu”

“Unamaanisha nini vifo vitatu , kuna wengine umeua bila sisi kujua?”

“Nimekupigia nataka kuongea na Bi Zenzhei nadhani upo nae karibu”Aliongea Roma huku akipotezea swali.

“Mr Roma nipo kwenye line”

“Nahitaji kujua kama kuna uwezekano wa….”Roma alijikuta akisita baada ya kuona hajapangilia swali.

“Wa nini Mr Roma”

“Tuseme ninapanga kuzaa mtoto na mwanamke wa Kizungu , je ninao uwezo wa kumfanya mtoto atakaezaliwa kuwa mwafrika bila ya kuonyesha dalili yoyote ya kuwa na mchanganyiko wa rangi kwa kutumia mbinu za kijini?”

“Mr Roma sijui kwanini unauliza hivyo , lakini inawezekana kama huyo mwanamke ni sahihi?”

“Unamaanisha nini kusema mwanamke ni sahihi?”

“Kila mwanamke anazaliwa na kiwango flani cha nishati ya Yin ambacho kinaweza hulandana na Yaksha ndio maana nasema mwanamke sahihi kwani sio wote”

“Yaksha!!, Sijakupata vizuri”

“Mr Roma Yaksha ni aina ya Dhana maalumu ambayo humchagua mwanamke au mwanaume kama tu Jini au binadamu mwenye uwezo mkubwa wa nishati za mbinguna Ardhi anataka kuzaa na binadamu wa kawaida, tuchukulie kwenye mfano wako mwenyewe unataka kuzaa na mwanamke wa Kizungu hivyo hatua ya kwanza unayotakiwa kuchukua ni kutafuta Dhana ya Yaksha na kuilandanisha na mwanamke wa Kizungtu na akipatikana unamvalisha na wakati wa tendo Yaksha itanyonya kiasi kikubwa cha Yang kutoka kwako na kuungana na Yin na kubust uwezo wa mwanamke kuweza kubeba mimba yako na kitakachotokea baada ya hapo mtoto atakaezaliwa atakuwa anafanana na wewe kwa asilimia mia moja kimwonekano, athari kubwa itakayotokea baada ya mwanamke kukuzalia mtoto anakuwa tasa , hivyo Mr Roma kama ndio mpango wako sikushauri”Aliongea Zenzhei na kumfanya Roma kukuna kichwa

“Sina mpango wa kufanya hivyo , nimeuliza kupata maarifa tu hakika kuna vitu vingi sivifahamu”Aliongea.

“Tamaduni za jamii za viumbe wasionekana ni pana kama ilivyo kwa binadamu tu na huwezi kufahamu kila kitu, usijiumize kichwa Mr Roma”

“Okey asante kwa maelezo”Aliogea Roma na kukata simu.

Mpaka hapo aliamini kidogo maneno ya XiaoXiao, aliona kweli kuna mambo mengi hayajui.

Roma aliendesha gari yake taratibu kulitoa upande wa fukwe kuingia barabara kuu , muda ulikuwa umeenda lakini aliona bora aende kazini mara moja , kwani tokea amwachie Tanya majukumu hajawasiliana nae hata mara moja.

Wakati akiwa njiani alipiga simu kwa Sauroni na kumpa maelekezo ya kuwashitua ‘Sleepers agent’ wao waliopo Korea kusini amsaidie kujua nini kinaendelea kwenye familia ya Park Juan, alitaka kuhakikisha kama kuna tatizo lolotea ambalo limempata Yezi.

Roma alijaribu kuendesha kuangalia kama angemuona yule msichana njiani , lakini hakuonekana kwenye upeo wa macho yake na aliamini huenda amepanda gari.

*******

“Zenzhei nadhani ni kama ulivyoongea jana?”

“Ndio Camillius kwa namna jinsi mambo yanavyoenda naamini sina haja ya kuwa na wasiwasi”

“Hahaha.. Zenzhei Roma ni jasiri sana , haogopi kuwachokoza Hongmeng kabisa?”

“Kachukua kila kitu kutoka kwako?”

“Unadhani ni kweli?”

“Nina uhakika Cammilius”

“Unaweza ukawa sahihi , Senga ni mwanangu lakini ni muoga kwenye mambo mengi lakini kwa mjukuu wangu Roma ni tofauti, ninachopenda anafanya kile anachokiamini”Aliongea Afande Kweka.

“Vipi kuhusu ulichoongea nae , nimesikia ukimtajia mambo ya uzazi”

“Camilius nimeshindwa kujua kwanini kauliza swali la namna hio lakini nadhani kuna kitu kimetokea leo”

“Unaamini hivyo?”

“Ndio”

“Hata mimi nadhani, kuna mambo mengi yanamfuata nyuma yake , kuwa na nguvu kubwa ni mzigo mzito”

“Nakubaliana na wewe, lakini kwanini usimwambie kuhusu Lanlan?”

“Hahaha…tena umenikumbusha Lanlan ndio anafanana na mimi babu yake lakini upande mwingine anafanana na mama yangu mzazi , ni mwepesi kushawishika”

“Hapana Camillius nadhani akishakuwa mkubwa atabadilika kwasasa ni mtoto”

“Hata mimi nadhani hivyo , Siwezi kumwambia Roma kuhusu Lanlan hata kama nife kesho , ukweli lazima agundue yeye mwenyewe kama Lanlan ni mtoto wake wa damu”

“Camillius lakini sidhani kama babu yake Lanlan anaweza kurudi?”

“Hilo lisikupe shida kama Lanlan ameweza kumpata baba yake mzazi basi lazima Roma na yeye atamfahamu mtoto wake mwenyewe, Zenzhei hebu fikiria kama tukimwambia Lanlan ni mtoto wake nini kinaweza kutokea?”

“Una busara sana Camillius , lazima atataka kujua mama yake Lanlan yupo wapi na hilo ndio litamchanganya zaidi na kumyumbisha na maadui wnaweza kulichulia kama udhaifu”

“Ndio maana anapaswa kutafuta ukweli yeye mwenyewe , na naamini siku atakayofahamu kuhusu Lanlan ndio atafahamu Seventeen hakufariki na atajue ni wapi alipo”

*******

Edna akiwa kazini kama kawaida mlango wake wa ofisini uligongwa na akaruhusu anaegonga kuingia na alikuwa ni Suzzane na Edna alitabasamu na kumpa ishara ya kuingia.

“Boss habari za harusi yako?”aliongea Suzzane huku akiweka tabasamu la urafiki.

“Nzuri Suzzane , harusi ilienda vizuri nitakuonyesha Vidio yake”.Aliongea Edna huku akitoka kwenye kiti chake na kukaa kwenye Sofa.

“Nitafurahi Madam , nina hamu ya kukuona unavyoonekana kwenye shera”Aliongea na kumfanya Edna kuona aibu kidogo .

“Vipi nadhani umekuja mpaka ofisini kwasababu una kitu muhimu cha kuniambia”

“Ndio boss nina mambo mawili yalionileta yanahusiana na Foundation”Aliongea na kisha alitoa karatasi kwenye mkoba wake na kumpatia Edna ambaye alianza kuzisoma na alijikuta akishangaa mno.

“Suzzane hii Donation mbona ni kiasi kikubwa hivi , nani muhusika?”Aliongea Edna, ijapokuwa Edna ndio mmiliki wa Edna Foundation lakini aliekuwa akiiongoza ni Suzzane , hivyo maswala yote ya taasisi hio ya msaada yalimfikia Suzzane na ndio huyaleta kwa Edna kuyafanyia maamuzi , hata Juma alitibiwa kupitia hio taasisi.

“Mwanzoni hata mimi nilishangaa baada ya mchango huo kuingia kwenye akaunti zetu , lakini wiki iliopita niliweza kupokea jina la muhusika , inaonekana ni Emaar Foundation kutoka Dubai”

“Emaar ..!!!! “Edna alijikuta akiwaza na alijikuta macho yake yakichanua.

“Unamaanisha kampuni inayomilikii jengo la Burj Khalifa?”

“Ndio Madam na huu ndio ujumbe wa barua pepe uliotufikia”aliongea na kisha akampatia kishikwambi na Edna kusoma na alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha.

“Suzzane nadhani watakuwa na sababu , kama hapa wanataka kuonana na mimi sidhani ni tatizo na ndio tutafanya maamuzi tukishafahamu nia zao”Aliongea Edna.

Ilionekana taasisi ya misaada inayomilikiwa na familia ya kiarabu ya Khalifa kutoka Dubai ndio waliotoa Donation(Mchango) ya kiasi kikubwa cha pesa kwenda kwa taasisi ya misaada ya Edna Foundation lakini pia walionyesha walitaka kukutana na Edna kwa ajili ya kikao cha majadiliano na ndio maana Edna aliona mpaka watakapo kutana nao ndio wangejua nini nia yao ya kuchangia kiasi kikubwa cha pesa kwenye taasisi yake.

Edna Foundaton licha ya kwamba kiasi kikubwa cha pesa kilikuwa kikitoka kwa Edna mwenyewe mmiliki lakini watu wa nje waliruhusiwa kuchangia , kwasababu malengo yalikuwa ni kusaidia wale watu wenye uhitajji.

“Niambie na swala la pili”

“Ni kuhusu Najma Madam, mwanzo wa mwezi huu wa nne alituma maombi ya kufuta udhamini wa masomo yake”Aliongea Suzzane na kumfanya Edna kushangaa.

“Kwanini?”

“Hajatoa sababu lakini amekutumia ujumbe kukueleza sababu atakaporudi nchini , taarifa za awali alizoelezea ni kwamba ameacha masomo ndani ya chuo cha Harvard”Aliongea na Edna alijikuta akiwaza.

“Suzzane isije ikawa yupo kwenye matatizo”

“Hapana Madam nilijaribu kuchukua hatua ya kuwasiliana na mwenyeji wake na inasemekana alifanikisha kupata ufadhili mwingine na amehama chuo”Aliongea na kumfanya Edna kuguna.

“Suzzane shida yangu ni kujua kama yupo salama , kuhusu ufadhli kama kapata mwingine sio tatizo , jaribu kuwasiliana na kaka yake uone kama wana mawasiliano na kama yupo salama haina haja ya kuuliza zaidi”.

“Sawa madam” Alijibu suzzane.









SEHEMU YA 485,

Roma ndio aliekuwa wa kwanza kurudi nyumbani na usiku alipanga kumtafuta kwanza Rose na Dorisi kujua maendeleo yao , maana licha ya kwamba ni majirani lakini ni kama waliishi mitaa miwili tofauti.

Baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa alitoka huku akipanga kuanza safari , lakini ile anafika nje tu aliweza kukutana na Edna ambaye anaingia kutokea kazini.

“Mbona kama upo kwenye mtoko mwenzangu” Aliongea Edna kinafiki.

“Mke wangu matendo kwanza na maneno ndio yafuatie” Aliongea Roma na kumsogelea Edna na kumkumbatia.

“Kama kuna sehemu unaenda usiondoke”

“Kwanini!, nilikuwa nikienda kumwangalia Dorisi na Rose mara moja, kuna sehemu unataka twende?”

“Kuna ndugu yako anafanya sherehe ya kuzaliwa leo na ametualika twende pamoja , nimeona sio jambo baya kama tutaenda kwani inakuweka karibu zaidi na ndugu”

“Ni ndugu yupi huyo unamzungumzia?”

“Fredi yule mjanja mjanja aliekuja na kundi la marafiki zake na kuondoka bila ya kushiriki mila kule Songea , nadhani unamkumbuka maana alikuwa wa tofauti familia nzima”Aliogea Edna na kumfanya Roma amkumbuka.

“Unamaanisha yule muuza magari?”

“Ndio huyo na kaniambia nisikose kwenda kwani kaniandalia zawadi ya harusi yangu, unaonaje tunaenda au unaenda kwa Rose na Dorisi?, naweza kwenda hata mwenyewe”Aliongea Edna kimtego na kumfanya Roma asugue pua yake kwanza.

“Sio mbaya kwasababu unataka kwenda lazima na mimi niende”Aliongea huku akiona safari ya kwenda kwa Dorisi imekwama ila alijiambia muda wowote angeweza kwenda.

Baada ya Edna kukubaliana nae aliingia ndani kwa ajili ya kujiandaa na saa kumi na mbili alikuwa ashamaliza na jioni hio alivalia gauni refu la kufunga na mkanda kiunoni , lilikuwa gauni la kawaida kimwonekano lakini lilimpendeza sana kutokana na yeye alivyo.

Roma alivaa jeans na koti la suti na tisheti ndani na ndio aliekuwa wa kwanza kutoka na kutoa gari.

“Mbona umechukua gari hio?”Aliongea Edna mara baada ya kumuona Roma katoa gari ambayo tokea siku aliopewa kama zawadi hakuwahi kuiendesha , ilikuwa ni Lamborgin Urus SUV rangi ya orange.

“Tunaenda kwenye sherehe ambayo imejaa watu wanaopenda show off , Dear we either go big or go home”Aliongea Roma akiwa siriasi na kumfungulia Edna mlango.

Edna alikuwa na magari ya kifahari, lakini hakupenda kuyatembelea sababu ni kutokana na uchache wake ndani ya Tanzania , hivyo kama akitumia wengi wangemwangalia na ndio kitu ambacho hapendi.

“Party inafanyikia wapi?”

“Sijui lakini amesema ni Maple Speed Resort”.

“Mbona mbali hivyo?”

“Unapafahamu?”

“Ndio ni Kisemvule huko kama unapita Kongowe”

“Mhmh!!.. kweli mbali , lakini umepafahamu vipi?”

“Nishawahi kufika kwa kuitwa na Neema..”Aliongea Roma huku akimwelezea namna ambavyo Msechu aliweka rehani gari ya kifahari ya Neema Luwazo na yeye kwenda kuikomboa.

“Mh..! Baba una harakati” Aliongea Edna na kumfanya Roma kutabasamu huku akiwasha chombo na ikanguruma na kumfanya atabasamu, alijiambia ni hivyo tu Tanzania barabara zake hazipo vizuri ila angekuwa anaendesha kwa spidi lakini aliona pia ni hasara sana kuwa na magari hayo kwa hapa Tanzania kwani hayatumiki ipasavyo.

Mama yake Roma na Bi Wema walishangaa kuona wametoka na gari ya aina hio, lakini hawakuuliza hata hivyo walifurahi wanatoka pamoja na alijiambia yeye kazi yake kubwa ni kuhakikisha Lanlan anakula anashiba maana ndio kazi ya bibi kwa wajukuu.

“Ni mbali lakini tunaweza kuchukulia kama muda mzuri wa kupoteza muda na kurelax”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na kushusha kioo kuangalia nje.

Giza lilikuwa lishaingia lakini watu hawakuacha kushangaa gari yao , Lamborgin Urus ni gari ghali, zaidi ya milioni mianne na nusu zilitumika kuliingiza nchini hivyo ilikuwa ni haki kukodolewa macho kwani yalikuwa machache sana.

“Vaa hii?”Aliongea Roma huku akimpatia Edna ile bangiri.

“Ah!… umeitoa wapi nilikuwa nikiitafuta sana bila mafanikio”

“Ilikuwa kwenye gari yangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuvuta pumzi za ahueni.

“Nilikuwa na wasiwasi nimeipoteza , ni kitu cha thamani nilichopewa na familia yako”

“Ni ya thamani ndio na hata mimi sijui wameitoa wapi , ila kazi yake ni kukupa ulinzi kuwa makini usiipoteze”

“Kweli inaweza kunipa ulinzi!?” Aliongea Edna huku akionyesha mshangao.

“Ndio ina nguvu kubwa, ukifanikisha kupanda levo huenda itakuwa rahisi kuitumia na kujua uwezo wake kwasasa ni kama urembo tu lakini bado ni muhimu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuiangalia huku akiivaa.

“Halafu Yezi alipiga simu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia.

“Park Joghyun pia alinipigia leo asubuhi”

“Kweli!! , alikuwa akihitaji nini?”

“Aliniambia hali ya babu yake Yezi imeimarika kwa kiasi kikubwa na ashaanza kurejea kwenye majukumu yake na Yezi pia kashaanza kuendelea na masomo”

“Hajazungumzia kuhuru urithi ambao babu yake amemuahidi?”

“Hajatambulishwa bado kifamilia na hio ndio sababu ambayo amenipigia , wanasema mwisho wa mwezi wa sita katika Anniversary(Kumbukumbu) ya miaka arobaini ya Starmoon Group ndio angekaribishwa rasmi na sisi tunapaswa kuwepo ,.Tena bila kusahau ameniambia kuna kidani ambacho Yezi amekupatia”Aliongea Edna.

“Ndio nina kidani , mara ya kwanza nilipokutana na Yezi alikataa nikimsaidia pesa kuinua biashara yake hivyo nikamwambia anipatie kitu chenye thamani , ndio alinipatia Kidani flani hivi ambacho ndio kitu pekee alichoachiwa na wazazi wake kama utambulisho, kwanini ameulizia wakati tayari washamtambua?”

“Hajaniambia sababu lakini alionyesha ni kitu muhimu sana kwa familia, hivyo siku tukienda usije kukisahau”Aliongea Edna na kumfanya Roma kufikiria kidani kile kinamaana gani kwa familia ya Park Juan , alijua kilikuwa na thamani kutokana na namna kilivyotengenezwa lakini bado shauku yake ilikuwa juu.

Kisemvule ilikuwa mbali , uafadhali pekee ni ile adha ya foleni imeisha kutokana uwepo wa mwendokasi na barabara kupanuliwa.

Baada ya kama lisaa hatimae waliweza kuipita kisemvule na kuingia Maple Speed resorts.

Gari yao ilivutia macho ya watu wengi wakati wanaingia ndani ya eneo hilo, maana licha ya kuonekana mpya lakini ilikuwa ya bei kubwa mno.

Edna alishangazwa na uwepo wa hili eneo na kadri alivyokuwa akilichunguza ndio alijua kwanini liliitwa Maple Speed Resort, kwa jicho la kibiashara aliona ni uwekezaji mzuri kampuni ya Maple wamefanya lakini pia aliona jiji angalau linazidi kupiga hatua.

“Fredi kupenda kwake magari ndio kaamua kufanya Party huku mbali kote?”

“Nadhani pia amechagua kwasababu ni eneo ambalo limejitenga”Aliongea Roma huku akiingiza gari upande wa kulia yalipoegeshwa magari aina tofauti tofauti , ni kama alivyotegemea magari mengi yalionekana ya bei ghali , lakini Gari lao ndio kidogo lilionyesha kufunika karibia magari yote.

Watu walikuwa wamezagaa nje huku wakiongea na kupiga soga , wanawake kwa wanaume na baadhi pia ya wasanii walikuwepo lakini mara baada ya ujio wa Edna na Roma wote walinyamaza na kuwaangalia.

Edna hakupenda sana kukodolewa macho , lakini kama mwanamke alijisikia vizuri namna ya wadada walivyokuwa wakimwangalia kwa wivu.

Roma alijihisi kidume baada ya kupita mbele ya makundi ya watu wakimwangalia mke wake alivyokuwa mrembo, watembea kuelekea upande wa pili wa jengo huku akiwa amemshikilia Edna mkono.

“Nadhani nilipaswa kuvaa jacket kwa juu au kitu chochote kufunika mabega yangu”Aliongea Edna huku akijisikia vibaya maana wanaume walimwangalia kwa macho ya uchu kweli.

“Wife sikudhania wangekuwa wengi hivi ningekushauri kule kule”Aliongea Roma na kisha alivua Blazer yake na kumvalisha.

“Unafanya nini?”

“Vaa hili la kwangu siwezi kuvumilia wakikuangalia kwa matamanio , ushaolewa tayari unapaswa kuwa na aibu kuonyesha baadhi ya sehemu zako za mwili ambazo napaswa kuona mimi tu”Aliongea Roma kitemi.

Edna hakutaka kuvaa kwasababu angeonekana mshamba flani hivi , lakini Roma aliongea ki amri na alimjua tabia yake hashindwei kufanya kitu cha ajabu hivyo aliamua kutulia.

Roma haikuwa mara yake ya kwanza hivyo alimuongoza Edna na kuvuka upande wa pili wa jengo na ile wanaingia upande wa mgahawa wa kisasa kushoto kwao Edna macho yake yaliweza kutua kwa mtu ambaye hakumtegea kumuona hapo na sio kwa Edna tu hata Roma hakutegemea kumuona , alikuwa ni Desmond.,

Desmond alikuwa amesimama karibia na ngazi za kuingilia akiwa anaongea na baadhi ya watu huku akichekelea , alikuwa amevalia suti ya rangi ya bluu na shati bila tai huku mkononi akiwa ameshikilia glass yenye kimiminika cha rangi ya kahawia ndani yake.

Alionekana ni kama alikuwa ametarajia ujio wao , kwani mara tu baada ya kuwaona aliwasogelea na macho yake yalipotua kwa Edna alijihisi moyo wake kuuma ni kama urembo wa Edna kwake umeongezeka mara elfu moja.

“Karibu sana Mr Roma Ramoni , mtoto mpotevu wa Raisi Senga, nimefurahi kuwaona tena wewe na mkeo”Aliongea huku akiweka tabasamu la kinafiki , siku hio alionekana kuchangamka kuliko siku ya mwisho aliokutana na Roma eneo hilo hilo.

“Bro mmefika , karibu sana , Shemeji una meta meta”Aliongea Fred aliewasogelea kwa haraka mara baada ya kuwaona.

“Mbona umechagulia kufanyia sherehe mbali huku”

“Kwasababu hili eneo limetulia na ni pana zaidi lakini pia nadhani mnafahamu mimi ni mfanyabiashara wa magari “Aliongea huku akicheka.

“Desmond huyu ni Bro Roma na huyu ni Edna malkia wa biashara ndani ya Tanzania , Shemeji yangu wa ukweli unamuonaje”Aliongea Fredi na ilionyesha pombe haikuwa mbali na akili yake.

“Sina neno la kuongezea, Hongera kwa kupata Shemeji mzuri namna hii”

“Hizo hongera naomba nizielekeze kwa Bro Roma kwa juhudi kubwa kwani kama sio yeye nisingepata hata nafasi ya kusalimiana na mtu mzito kama Boss Edna , Shemeji karibu sana jisikie huru , huyu ni Desmond…”

“Fred hauna haja ya kututambulisha tunafahamiana nae” Aliongea Roma maana hakutaka kuendelea kusimama na Edna mbele ya Desmond ambaye anamwangalia dada yake kwa macho ya uchu.

Wageni walikuwa wengi na Fredi ilionekana ni mtu wa watu , maana eneo limejaa haswa.

“Mr Roma we meet again”Sauti kutoka nyuma yao ilisikika na kuwafanya wageuke.

“Tusiman!!”Aliongea Roma mara baada ya kumfahamu , alikuwa ni muindonesia alieshindana nae mbio za magari kuikomboa gari ya Neema Luwazo na alishangaa uwepo wake.

Alikuwa amevalia shati la mikono mirefu bila koti pamoja na kofia aina ya Hat na mkononi pia alikuwa ameshikilia kinywaji kwenye glasi.

“Nice to know you still remember me and this must be your lovely wife”

“Ni vizuri sana unanikumbbuka na huyu lazima atakuwa mkeo”Aliongea huku akionyesha kushangazwa na uzuri wa Edna huku akinyoosha mkono wake akimpatia kutaka kusalimiana nae , lakini Roma hakutaka ashikane na Edna kwani aliona kabisa nia yake ni kutaka kubusu kiganja chake na alimvuta Edna na kumrudisha nyuma.

“Niwie radhi Mr Roma nishajisahau tayari nikajua nipo nyumbani”

“Honey ,who is he”Aliuliza Edna na muda huo na Desmond alikuwa tayari ashasogea tena waliposimama na Fredi alikuwa upande mwingine akikaribisha wageni wake.

“Ni mwanachama wa Indonesia Redbull Racing ni dereva wa mbio za magari Formula one”Aliongea Roma na Edna alielewa.

“Mr Tusimani kwanini bado upo hapa , nilijua usharudi nchini kwenu”

“Kwasasa nipo likizo na nimeipenda sana Tanzania hivyo nimevuta muda wa kurudi nyumbani mpaka ligi itakapo anza”

“Mr Roma Tusiman bado hajaridhika na siku ile alivyopoteza pambano kutoka kwako na ameshiriki siku ya leo baada ya kufahamu ujio wako na anaomba umpatie nafasi ya mwisho ya kushindana”

“Ni kweli Mr Roma kama hutojali nitaomba mpambano mmoja tu na baada ya hapo sherehe inaweza kuanza Fredi pia ameridhia”Aliongea Tusimanni huku akionyesha kuwa na mchecheto mno.

“Usije ukaniacha hapa peke yangu” Aliongea Edna kwa tahadhari.

“Napaswa kumsikiliza na isitoshe pia nawakilisha taifa kwa kushindana na mtu mkubwa kama Tusimani”Aliongea Roma

“Mr Roma asante kukubali ombi langu , nadhani tunapaswa kuweka Zawadi atakayopata mshindi”

“Kwanini tusifanye hivi, kwasababu Tusiman wewe umeshinda mapambano mengi tokea ufike hapa Tanzania ,unaonaje ukazibetia hela zote ulizopata na isitoshe wewe ndio umeomba nafasi ya kushindana na Roma”Aliongea Desmond kwa kingerereza na kumfanya Tusimani kukosa ujasiri.

“Acha kuwa mbahili , wewe unafahamika duniani kote na unaheshima kubwa nadhani sio mbaya kama utatoa kiasi kidogo ulichopata hapa Tanzania na isitoshe unajiamini unakwenda kushinda , hupaswi kuwa mbahili namna hio bro”Aliongea na muda huo na Fredi na wageni wengine walikusanyika eneo moja baada ya kusikia Tusimani anataka kushidana na Roma kwenye mbio za magari.

Ilikuwa ni usiku lakini kwasababu eneo hilo limefungwa Spotlight uwezekano wa kufanya mashindano hata usiku wa giza inawezekana kabisa.

Baada ya majadiliano ya muda mfupi Tusimani alikubali kubetia kiasi cha Dola Elfu ishirini na Roma elfu ishirini na makubaliano mshindi ambaye angepatikana hela zote angezitoa kwenda kwa watu wenye uhitaji na Roma hilo hakuona tatizo.

Fredi alimfikishia taarifa Meneja wa Maple kuruhusu uwanja kutumika na Roma alimwangalia kwanza Edna kutaka ruhusa yake.

“Siwezi kushindana bila ruhusa , Unasemaje?”Aliuliza Roma.

‘Unaweza kushindana , pesa ambazo zitakazopatikana hata hivyo hazingii mfukoni mwenu bali ni kwa ajili ya kusaidia wahitaji”Aliongea Edna.

“Nilijua hukutaka nishindane?”

“Ni kabla ya mchango wa hela haujafanyika , kiasi tajwa ni kingi sana na kinaweza kujenga madarasa hata mawili”Aliongea Edna ukweli mara baada ya mwanzo kuona labda mashindano yalikuwa ni ya kuonyesha umwamba hakutaka Roma ashiriki halafu amuache mwenyewe , lakini baada ya kuona hela zinazopatikana zote zingetolewa kwa wahitaji aliona ni mashindano ya maana.

Kwasababu taa zilikuwa zimezimwa walisubiri nusu saa nzima kusubiria zikoleze mwanga kwani Spotlight hazikuwa zikiwaka moja kwa moja kwa mwanga wake wote, zilianza taratibu taratibu mpaka kukolea.

Na muda huo Tusiman na Roma walitumia kuchagua magari watakayotumia kuendesha ambayo yote yalikuwa mali ya kampuni ya Maple.

Tusimani alichagua Ferrari 458 rangi ya njano gari ya milango mwili ambayo injini yake ilikuwa na uwezo mkubwa kuliko gari Roma aliochagua Mc Laren.

Watu walishangilia mno na ilikuwa Party ya aina yake kwani hakuna ambaye alitegemea angeshuhudia mashindano hayo tena muda wa usiku.

Baada ya kila mmoja kukaa kwenye nafasi yake zilihesabiwa sekunde tano kurudi nyuma na ilivyofika sekunde ya sifuri tu.

VROOM!, VROOM!

Wote waliyaondoa magari yao kama mishale na kufanya kelele za kushangilia ziwe juu.

Muda huo huo wakati Roma anaondoka upande wa aliposimama Edna alisogelewa na muhudumu aliebeba Tray la glasi zilizojazwa vilevi pamoja na mvinyo.

Mwanzoni alipokuwa na Roma alionyesha kujiamini na sasa alikuwa peke yake aliona hana usalama na Fredi mwenyewe alionekana kuwa bize kuangalia mashindano na alikuwa ndio kinara wa kupiga makelele.

“Miss care for a glass of drink?”Aliongea yule mhudumu na Edna alitingisha kichwa kidogo kukubali na alimsogela , lakini sasa yule mhudumu alitereza na zile glasi zote kwenye trey kumponyoka na kumwagikia Edna kwani hakuweza kumkwepa kwa haraka.

“Dada samahani, I am sorry” Aliongea huku akiomba kusamehewa , watu wachache waliona hilo tukio lakini kutokana na kuwa bize kuangalia kile kinachoendelea hawakujali sana.

“Haina shida , nionyeshe maliwatoni nikajisafishe”Aliongea Edna maana alikuwa amechafuka na mirangi na alijua angetoa harufu kama asingejifuta na maji.

“Sawa Dada nisamehe sana, nikule nyuma nitakusindikiza”Aliongea na kumfanya Edna ajutie kwani asingeangalia Roma akishinda , aligeuza macho yake na kuangalia kwenye scren za Tv na ilionekana ndio Roma anamaliza mzunguko wa kwanza na kuanza wa pili , kwani jumla ilipaswa kuwa na Lap tatu mpaka mshindi kupatikana.

Aliona akajisafishe haraka haraka na atawahi kuendelea kuangalia , walipita baadhi ya wageni na kisha walizunguka kwa nyuma na kuingia upande wa vyoo na mabafu, eneo lilikuwa la kifahari hivyo kila kitu kilikuwa cha hadhi ya juu na usafi mzuri na ni harufu kwa mbali ya limao ndio alioweza kuhisi kwenye pua zake.

Edna aliingia kwenye korido yenye msururu wa sink nyingi zenye mabomba ya maji na alivuka la kwanza na kwenda kusimama la tatu na akafungua koki na kuanza kuloanisha kitambaa kwa haraka kujifuta rangi nyekundu iliokuwa imemchafua eneo la kifuani.

Wakati akiwa bize kuharakisha kumaliza ili arudi kuangalia shindano , mwanamke mwingine aliekuwa akinukia vizuri aliingia, alikuwa amevalia gauni la rangi nyekundu la mkato wa chini ambalo liliubana mwili wake na kudhihirisha uumbaji.

Yule mwanamke alitembea kimadaha huku akiwa na tabasamu kwenye uso wake na kwenda kusimama nyuma ya Edna na kumfanya amuone kupitia kioo.

“Your skin is so smooth” Aliongea akimaanisha kwamba ngozi ya Edna ni nyororo.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Edna huku akimwangalia kwa mshangao , maana hakuzoea kusifiwa na mtu ambaye hamfahamu tena eneo la chooni.

“Yaani umeshindwa kunifahamu?”Aliuliza na Edna alitingicha kichwa kwamba hamfahamu.

“Mimi nakufahamu sana na pia namjua mume wako vizuri…”Edna alimwangalia vizuri yule mwanamke na sura yake ilikuwa inakuja na kupotea, lakini jambo lingine ambalo lilimtia wasiwasi ni jinsi alivyoingia hapo ndani ni kama amemfuata nyuma ila alijitahidi kujituliza na kujiambie na yeye amekuja toilet lakini mwanamke yule bado hakutoka nyuma ya Edna.

“Unataka nini kutoka kwangu, maana naona kama umenifuata” Aliongea Edna na palepale tabasamu la yule mwanamke lilibadilika na kuwa la kejeli

“Mtoto wangu wa kiume aliweka juhudi nyingi kukupata lakini bado tu ukamkatalia na mimi kama mama yake nikaona nimsaidie..”Aliongea na sasa palepale Edna akili yake ilikaa vizuri.

“Wewe ni madam Kizwe!” Aliongea Edna huku akirudi nyuma kwa mshangao

“Haha.. unaonekana kuwa na akili , nadhani ndio maana Desmond ametokea kukupenda”

“Haiwezekanni…. Nilichojua tayari umekwisha kufa”Aliongea Edna huku akianza kuhisi woga wa ajabu na kutetemeka , lakini Kizwe alianza kucheka.

ITAENDELEA 0687151346 watsapp only contact me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…