Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

" hivi sasa ni saa tano na dakika kumi. Na hii ni taarifa ya habari ya saa 24 zilizopita. Msomaji ni charles hilari." sisi wa analog enzi hzo RTD tunakula "maji" ya kienyeji pale kwa mama tabu uwanja wa fisi manzese! Taarifa ilikuwa inarekodiwa halaf tape inawekwa saa 11 alfajiri. Nyie mnajua ndo saa tano kumbe kumekucha mkakutane na misala ya wake zenu huko.
 
Sura inakuja inapotea Edina kutahamaki ni madam kizwe! Mara ukatokea mkono kwenye kioo ukamshika kichwa madam kizwe! Kraach! Mlio wa mifupa ya shingo ikivunjika! "Uwiiii nakufa mara ya piliii!" Yowe lililomtoka madam kizwe! ... ITAENDELEA MWEZI FEBRUARY 2824 ! Subira taurati bab lai
 
Sura inakuja inapotea Edina kutahamaki ni madam kizwe! Mara ukatokea mkono kwenye kioo ukamshika kichwa madam kizwe! Kraach! Mlio wa mifupa ya shingo ikivunjika! "Uwiiii nakufa mara ya piliii!" Yowe lililomtoka madam kizwe! ... ITAENDELEA MWEZI FEBRUARY 2824 ! Subira taurati bab lai
[emoji23][emoji23][emoji23]
Wacha tukae kumsubir mwamba, ni arosto hii zaidi ya sigara
 
Edna alishangaa , ijapokuwa hakuwahi kuwa na ukaribu na Kizwe lakini ashawahi kumuona ana kwa ana , kubadilika kwake na kuwa kama kijana kulimshangaza mno na kuogopesha kwa wakati mmoja.

“The old Kizwe is dead . I have been reborn”Aliongea akimaanisha kwamba Kizwe wa zamani amekwisha kufa na yeye amezaliwa upya.

Edna alikuwa akitetemeka mno na kilichomjia akilini muda huo ni kukimbilia nje na Kizwe alimuacha apite huku akicheka , lakini ile anafikia mlangoni alizuiwa na Desmond.

“Ni wewe..?”Edna alijikuta akianza kuhofia na akili yake ilimwambia huenda kila kitu kimepangwa , kwanzia sherehe kufanyikia huku mbali lakini pia swala la Roma kushindana mbio za magari na yeye kumwagiwa Mvinyo.

“Vipi ,mbona unashangaa kuniona?”Aliongea Desmond huku akiwa ameweka tabasamu la kejeli na kumfanya Edna kurudi nyuma kwa wasiwasi.

“Desmond usije ukathubutu kunifanya chochote , Roma atarudi muda si mrefu na mtakuwa kwenye matatizo”Alitahadharisha Edna.

“Relax , tutamalizana na wewe kabla hata hajamaliza pambano”Aliongea huku akimsogelea karibu na Edna alianza kurudi nyuma nyuma.

“Mume mume wangu atawaua msithubutu kunigusa”Aliongea Edna

“Haha…So what , Tutakufa kwa mikono yake tu hata kama hatutokugusa , hivyo badala ya kufa bila sababu tutajitengenezea sababu”Aliongea Kizwe.

“Edna ,,, nimeisubiria hii siku kwa muda mrefu sana , usijali sana , Roma anahitaji angalau dakika kumi mpaka kuja kukupata , lakini kabla ya muda huo ngoja nikupatie kitu cha kipekee usiku wa leo”Aliongea

“Desmond huwezi kunifanyia hivi , huwezi kufanya hivi”Aliongea Edna na hakuwa na pakukimbilia kwani Desmond ashamshika tayari mkono huku akimsogezea sura yake karibu.

“Desmond hakikisha unafanya haraka nitaondoka baada ya kuifurahia show”Aliongea Kizwe bila aibu , ni kana kwamba Desmond hakuwa mtoto wake kabisa.

“Mama mpango wangu nataka nijipigie taratibu taratibu na muda ambao Roma anafika nashusha wazungu huku anaona”Aliongea huku akiweka tabasamu la kebehi.

“Hehe. kama huo ndio mpango wako basi sina budi kusubiri”Aliongea Kizwe lakini muda ule ule yule muhudumu ambaye alimchafua Edba aliingia.

“Madam , What are your orders?”Aliuliza kwa Kingeereza.

“Jeremy yupo wapi , bado hajafika tu?”Aliuliza kizwe.

“Mheshimiwa atafika hivi punde , tayari wanausalama washawasili”Alijibu na kumfanya Kizwe kuonyesha tabasamu la furaha , alijiambia anakwenda kumkomoa Jeremy kwa Desmond kumla dada yake.

Raisi Jeremy alikuwa nchini Tanzania kuhhudhuria mazishi ya kifo cha Raisi mstaafu wa Tanzania Kigombola , ilionekana walitumia nafasi ya uwepo wake nchini kukamilisha mpango wao.

Desmond alizidi kumkandamiza Edna kwenye ukuta na lile koti ambalo alipewa kuvaa na Roma lishadondoka chini na hivyo mabega yake kuwa wazi

“Desmond tafadhari nakuomba usifanye hivi , mimi ni ..”Edna alianza kushikwa na kigugumizi.

“Wewe ni nani , Sema..?”Aliongea kwa kingereza.

“My…”Edna alishindwa kuongea huku machozi yakimtoka mfululizo huku akimwangalia mwanaume ambaye alionekana kama kichaa mbele yake.

Kizwe mara baada ya kuona Edna anataka kuongea kitu kumwambia Desmond alimsogelea kwa spidi pale waliposimama huku akimwangalia kwa macho yaliojaa sumu.

“Desmond usijali chochote atachokuambia , anajaribu kuvuta muda , usimuamini kabisa”

“Hata mimi nimeona hilo , Edna usijifanye mjanja mimi ni mjuzi likija swala la mitego , uliweza kuwashinda wengine lakini sio mimi na hata kama nikikubaka Roma hawezi kufanya chochote mbele ya baba yangu”Baada ya kusema hivyo alimwinamia Edna akinuia kumpiga kiss kwenye lips , lakini Edna alitumia nguvu kumsukuma na kumkwepa huku akikimbilia kwenye vyoo.

“Mama anajaribu kukimbia” Aliongea Desmond lakini palepale Kizwe alipotea na kwenda kuibukia mbele yake na kumzuia asiingie chooni na kujifungia na kitendo kile cha Kizwe kutokea mbele yake ghafla kilimuogopesha mno Edna.

Desmond hata yeye mwenyewe alishangazwa na uwezo wa mama yake , kwani hakuwahi kumuona akiwa hivyo

“Edna mpenzi, nadhani utii shuruti la sivyo mama yangu hatokuvumilia”

“Hapana Desmond , huwezi kufanya hivyo kwasababu mimi ni dada yako”Aliongea Edna kwa sauti huku akianza kulia kwa kwikwi na Desmond alijikua akisimama akionyesha mshituko lakini Kizwe alishika mikono Edna kwa nguvu na kusimama nyuma yake na kisha akamwangalia Desmond.

“Unafanya nini Desmond , fanya haraka acha kusita sita nakushikilia iwe rahisi”Aliongea Kizwe, alionekana hakubadilika mwili tu lakini hata nafsi yake pia imebadilika.

“Unajifanyisha kunitega , hahaha…, lini ukawa dada yangu , Mama yangu tangu lini akawa na mtoto wa kike”Aliongea Desmond huku akianza kupandwa na jaziba na palepale alimsogelea Edna bila ya huruma na Edna alikosa matumaini na tegemeoo lake muda huo ni Roma , asingetokea basi ndio anakwenda kubakwa na kaka yake lakini ile Desmond anataka kushika mkanda wa gauni..

BOOM!

Lilikuwa wimbi la upepo lililoambatana na rangi ya kijani ambalo lilimkumba Desmond kwa nguvu na kurudishwa kwa kasi na kama sio Kizwe kuwahi kumuachia Edna na kwenda kumzyia basi angegonga kichwa moja kwa moja kwenye Sink.

Rangi ya choo ilibadilika kabisa na kuwa ya kijani na kuambatana na ukungu, Kizwe alijikuta akipagawa na kujiuliza nini kilichotokea.

Edna na yeye alishangaa lakini mkono wake wa kushoto ulikuwa ukitetemeka mno na alipoangalia aliona mwanga ulikuwa ukitoka kwenye ile bangiri ya ajabu, alikumbuka Roma alimwambia ni ya ulinzi lakini hakuamini mpaka muda huo alipofanya maajabu yake na kumuokoa.

Alikumbuka Roma akimwambia aivae na asiivue wakati wakija ndani ya hilo eneo na alimwambia kabisa kwa muda huo ilikuwa kama urembo tu.

Asichokifahamu Edna na Roma pia ni kwamba bangiri ile haikuwa Dhana za kawaida na hata mtu ambaye yupo kwenye levo ya Nafsi hajui namna inavyotumika na sio kwa Roma tu hata kwa Zenzhei mwenyewe hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu hio bangiri.

“Desmond upo sawa?” Aliuliza Kizwe huku akimshikilia Desmond vizui akimwangalia kwa wasiwasii.

“Desmond alijitahidi kusimama mwenyewe na kusaficha damu iliokuwa ikitoka kwenye midomo yake , ilionekana aliumia kwa ndani.

“Niko sawa mama, There is something wrong with that bitch” Aliongea

“Huenda Roma alijua siku moja jambo kama hili lingemtokea?”Aliongea Kizwe huku wakimwangalia Edna ambaye anaishangaa bangiri yake iliomuokoa.

“Kwahio nawezaje kumfikia sasa?”Aliongea huku akionyesha woga wa kupiga hata hatua maana nguvu iliompiga haikuwa ya kawaida kabisa.

Kizwe aling’ata meno yake kwa hasira na kisha akapotea aliposimama Desmond lakini ile anataka kutokea aliposimama Edna bangiri ilitoa tena mwanga wa mng’ao wa kuumiza macho wa kijani kwa nguvu kubwa kiasi cha Edna kufumba macho.

Lakini ujinga aliofanya Kizwe ni kupotezea ule mwanga na kutaka kumsogelea Edna na kumshika na alipigwa na wimbi ambalo sio tu kumrudisha nyuma lakini pia lilimuunguza kwenye mikono kiasi hata nguo aliovaa iliungua na mwanga ulirudi tena kwenye ile bangiri na Edna alionekana kutopata madhara yoyote.Ilionekana ile Dhana ni kama ngao kwa Edna na ilitambua wakati gani alikuwa kwenye hatari.

“Damn it her bangle’s the one causing trouble , I can’t get close either”Aliongea Kizwe kwa hasira huku akimaanisha kwamba nni Bangiri yake ndio inamzuia kutokumsogelea pia.Desmond alijawa na wasiwasi huku akimwangalia Edna na kumuona kama kiumbe cha ajabu.

“Mama hatuna muda wa kutosha na Roma muda wowote atarudi , si ulisema hata kama nikimbaka baba atanilinda , yupo wapi muda huu?”

“Nina uhakika tayari ashakwisha kufika na kama ukitoka nje unaweza kumuona”Aliongea .

“Na vipi kuhusu Edna?”

“Kwanini unajali sana kuhusu yeye , mpango wetu umefeli hivyo ukiulizwa kaelekea wapi wewe jibu hujamuona na hukumfanya chochote na Roma atakosa ushahidi wa kukushambulia mbele ya baba yako”Aliongea kizwe.

“Nadhani kwa hilo nitajua namna ya kufanya mwenyewe”Aliongea Desmond na Kizwe alimwangalia mtoto wake kwa dakika kadhaa na kisha akamwangalia Edna kwa chuki nyingi na kisha palepale alipotea, ilionekana alikimbia hilo eneo.

Desmond mara baada ya mama yake kupotea hakutaka kuruhushu mshangao wake uchukue nafasi kwani angekutwa ndani ya vyoo hivyo vya kike ingekuwa tatizo na asingeweza kujitetea hivyo aliondoka haraka kutoka nje.

Edna alijikuta akivuta pumzi ya ahueni huku akijiegamiza kwenye ukuta , hakuamini alikuwa amepona kwenye adha iliokuwa ikikaribia kumkumba , shukrani kwa Bangiri lake mkononi limeweza kumuokoa.

Desmond mara baada ya kufika nje alijikuta akihema kwa nguvu na kushika magoti yake, ijapokuwa alijitahidi kuwa sawa mbele ya mama yake , lakini alimuona ni wa tofauti kabisa na kila kitu kilikuwa zaidi ya maajabu, alijitahidi kujituliza na kutembea kuelewa alipowaacha watu wengine.

Roma ndio aliekuwa wa kwanza kugusa mstari wa mwisho , hivyo kufanikiwa kushinda na watu walimshangilia , akiwemo Fredi ambaye alimsahau hata Edna , watu wengine pia walimshangilia.

“Mr Roma ninashauku na jambo moja , kwannini unao uwezo mkubwa wa kuendesha magari?”Aliuliza Tusiman.

“Ni sababu gani imekupelekea kuendesha magari?” Aliuliza Roma.

“Kwasababu napenda magari lakini pili ndio fani niiochagua kufanya kwenye maisha yangu”

“Sababu zetu ni tofauti, mimi nikishikilia usukani naendesha kuyaokoa maisha yangu na sio kushinda kama wewe”Aliongea Roma na kumfanya Tusimani kuchangayikiwa kwani hakumuelewa maana Roma kaongea kimafumbo.

Roma alianza kuitafuta sura ya Edna , lakini hakuiona , aliangalia pia kumtafuta Desmond lakini pia hakumuona lakini muda ule ule aliweza kumuona Desmond akitokea upande wa nyuma akirudi kwa kukimbia.

“Nadhani kila mmoja ameweza kufurahia zawadi ya macho niliowaandalia na huu ni muda wa kuanza kile kilichotukusanya leo hii , wote tukusanyike ndani ya ukumbi “Aliongea Fredi huku akiwa na furaha kwani siku yake ilionekana kama ya kipekee mno.

Roma kitendo cha kutokumona Edna kilimfanya kuwa na wasiwasi na alitumia uwezo wake wa kijini kutafuta ndani ya eneo hilo na aliweza kumuona akiwa eneo la maliwatoni , upande ambao Desmond alitokea , alishangazwa na jambo hilo na kuanza kutembea kuelekea upande huo.

Lakini ile anakata tu kona aliweza kukutana na Edna njiani , alimwangalia na kugundua gauni lake limechafuka kwa kuwa na rangi, licha ya kuumizwa na muonekano wa Edna lakini alijitahidi kujituliza , hata hivyo alishatarajia mara tu baada ya kumuona Desmond ndani ya hilo eneo.

“Vipi umefanikiwa kumwambia?”Aliuliza Roma mara baada ya kumfikia na kumfanya Edna ainue macho yake na kumwangalia maana alielewa Roma anachouliza , alikuwa akiuliza amefanikisha kumwambia kama wao ni ndugu.

“Ulikuwa ukijua hili litatokea, inaonekana ilikuwa mpango wao kukushindanisha kwenye mbio za magari ili kukuweka mbali na mimi na kwa mwonekano wako ni kama ulifahamu kinachoendelea , Ulifanya hivyo kwasababu ulifahamu nina hii bangiri na ingenipa ulinzi?”Aliuliza Edna

“Baada ya kumuona hapa nilijua kuna kitu anapanga”

“Ungeniambia sasa na wewe mapema , vipi kama angekuwa na mpango mwingine?”Aliongea Edna huku aking’ata meno kwa hasira maana mpaka muda huo bado hakuwa akiamini kama amepona.

“Ningekuambia anachokipanga ,usingepata ujasiri wa kumuweka wazi na kuendelea kukuangalia na macho yake ya kimatamanio, nilichotaka ni kwanza aondoe mawazo yake ya kipumbavu kwa kuujua ukweli maana hili lisipoisha leo lazima lingejirudia, hata hivyo nilijua ungekuwa salama”.

“Wewe mwanaume ni umenikatili sana unajua nilikuwa kwenye hali ganni?”

“Nimefanya yote kwa faida yako na angalau kwa sasa utaachana na mawazo yako ya kimatarajio”Aliongea akimaanisha kwamba ataachana na mawazo yake ya kusubiria jambo ambalo haliwezi kutokea bila yeye kuchukua hatua.

Na alichoongea Roma ni nusu ukweli , Edna hakuchukua hatua ya kumpigia simu Raisi Jeremy na kusubiria yeye ndio amtafute na amtambue kama mtoto wake na alijua Edna angeendelea kusumbuliwa na Desmond na asingechukua hatua ya kumueleza ukweli.

“Sikuwa hivyo..”

“Unaweza kujidanganya mwenyewe na mtu yoyote ndani ya dunia hii lakini huwezi kunidanganya mimi , siku zote unaigiza kutokujali lakini nina uhakika unamjali Desmond na baba yako na leo nataka nikuambie kwamba Desmond hawezi kubadilika na huenda muda sio mefu nikayakatisha maisha yake”.

“Umekuwa chizi , umuue ? Utaishije Tanzania ukishafanya hivyo?”

“Kitu muhimu kwangu mimi ni wewe kuwa na furaha na mpaka sasa huenda yupo hai kwasababu yako , naogopa kufanya hivyo kwasababu unaweza kunikasirikia”

“Sijui chochote mimi , sitaki hata kufikiria akili yangu sasa hivi imejaa ukungu na nashindwa kabisa kufanya maamuzi sahihi ya kila kitu kilichoppo mbele yangu”Aliongea huku akishindwa kuzielewa hisia zake , tokea arudi kutoka visiwa vya wafu alikuwa akiangalia ujumbe wake umejibiwa lakini wapi , alikuwa akitamani hata ampigie Desmond amuulize kuhusu baba yake lakini angeanzaje, alitaka kujua angalau kidogo kwanini kadi la kliniki wakati mama yake akiwa mjamzito ilionyesha alikuwa na mapacha, lakini alikosa ujasiri wa kufanya hivyo , alitegema kupata majibu kupitia kwa Raisi Jremy lakini vipi kama raisi Jeremy angekataa kumtambua na kusema hana uhusiano nae wowote.

Lakini angefanyaje sasa huo ndio udhaifu wake , alikuwa akijali familia yake kuliko kitu chochote na ndio maana hata mpaka muda huo alikuwa na mawasiliano na Ernest Komwe licha ya yale aliotaka kumfanyia na tena sio kuwa na mawasiliano tu alikuwa bado akiwasaidia na pesa ya matumizi kwa siri, huyo ndio Edna uhusiano wa damu ndio udhaifu wake mkubwa.

“Unajihisi kuchanganyikiwa kwasababu , mbele yako ni kiza na hauna tochi ya kukupa mwanga wa kuona mbele na kama ni hivyo mimi nitakuazimisha tochi yangu ili uweze kuendelea na safari”Aliongea Roma na kumfanya atabasamu huku akishindwa kutoa jibu.

“Unadhani kama nikimuua Desmond itakuchukua siku ngapi kuomboleza ?”

“Hapana , usije ukafanya jambo lolotea la kijinga, Kizwe ineonekana amemualika raisi Jeremy kuja hapa na huenda anaweza kufika muda wowote”

“Unamaanisha nini kuhusu Kizwe!!! ?”Aliuliza kwa mshangao mara baada ya Edna kutaja jina la Kizwe.

“Ndio” huku akikunja sura.

“Ndio alieandaa kila kitu kumsaidia Desmond , anaonekana kuwa kijana zaidi kuliko mara ya mwisho nilivyomuona lakini pia anaonekana kuwa na nguvu na spidi kubwa tofauti na binadamu wa kawaida na alipotea mbele ya macho yangu”

“Hahaha… Yan Buwe realy was extraordinary…”Alicheka Roma , alijua lazima ni matumizi ya Ressutection Fluid , lakini kilichomshangaza kama Kizwe kafufuliwa na kikimiminiika hiko na bado anaonekana kujiendesha mwenyewe kwanini wale wengine walionekana kama misukule.

Jibu ni moja tu kwake lililomjia , huenda aliendelea zaidi na zaidi upande wa teknolojia ya kibailojia , lakini hata hivyo hakuwa na wasiwasi kwani muda huo alikwisha mmaliza, ila kuna hisia zililimjia na alijifariji mwenyewe kwa kujiambia hakuna uwezekano wa Kizwe kuwa kama Yan Buwen na kitu pekee ambacho anapaswa kuhofia labda ni ukakamavu wake tu na kuwa na spidi ya kupigana , lakini sio kutumia kaunini za anga kama ilivyokuwa kwa Clone.

“Vipi utafanya nini , naamini karudi kwa ajili ya kisasi?”aliuliza Edna.

“Simuogopi , unachopaswa ni wewe kujichunga tu ,.. njoo tuondoke hapa turudi kabisa nyumbani huwezi kuendelea ukiwa umechafuka namna hio”Aliongea Roma huku akimshika mkono , lakini bado alionekana kusita sita na Roma aliweza kusoma mawazo yake , huenda alichokuwa akitaka muda huo ni kusubiri Jeremy kufika.

“Kama unataka kumuona mzazi wako basi tufanye hivyo na kama humhitaji katika maisha yako nipo tayari kumuua?”

“Unataka kumuua Raisi , Unatania wewe?”

“Vipi unadhania siwezi, kama sio kwa ajili yako huenda ningeshamuua”Aliongea Roma akikumbuka ile siku kule kigamboni alivyokutana na Raisi Jeremy na kumkwida mbele ya wana usalama wake baada ya kumwambia hana mpango wa kumtambua Edna kama mtoto wake.,

“Twende tu nyumbani , baada ya leo sitaki kuwaona tena”

“Ni ngumu sana , nina uhakika Desmond atakutafuta tena ndio maana natamanni kumaliza tatizo moja kwa moja , lakini unasita sita”

“Roma nisikilize tuondoke”Alibembeleza , ashaona Roma ni mtu mwepesi kuchukua maamuzi bila ya kufikira nini kitatokea baadae ndio maana alitaka kumtoa hapo haraka.

Ile wanakuja kufikia upande wa mbele wa jengo hilo la Maple Resort , msururu wa magari uliingia na wanausalama waliovalia suti walitoka kwenye magari ya mbele na nyuma kwa kasi na kuzagaa eneo lote kila mtu akiangalia upande wake ,

Baada ya dakika kama tano kupita gari iliokuwa katikati ilifunguliwa na alitoka mwanaume mweusi alievalia miwani na kusogela mlango wa gari ya abiria na kisha akafungua mlango na Raisi Jreremy aliweza kutoka na kukanyaga ardhi na kugeuza macho yake mbele na hapo ndipo alipomuona Edna akiwa amesimama na Roma wanamwangalia.
 
SEHEMU YA 487.

Baada ya dakika kama tano kupita gari iliokuwa katikati ilifunguliwa na alitoka mwanaume mweusi alievalia miwani na kusogela mlango wa siti ya abiria na kisha akafungua mlango na Raisi Jreremy aliweza kutoka na kukanyaga ardhi na kugeuza macho yake mbele na hapo ndipo alipomuona Edna akiwa amesimama na Roma wanamwangalia.

Raisi Jeremy kabla hajapiga hatua kusogea mbele alimpa ishara msaidizi wake kumsogelea na kisha aliteta nae jambo na akaitikia kwa ishara na kisha alipiga hatua kusogelea mbele.

Alikuwa ashaanza kuzeeka kwani nywele zake zilikuwa na mvi , lakini licha ya hayo bado alionekana kuwa na afya nzuri.

Haikueleweka kwanini akafanya safari ya dharula mpaka kuja ndani ya hilo eneo kwani ni hakika sherehe ya Fredi haikuwa ikimuhusu.

Macho yake yalififia mara baada ya kugundua Edna alikuwa akiangalia upande mwingine kama vile hakuwa akimtambua na baada ya kuwafikia alisimama.

“Edn…CEO Edna”Aligwaya kwa kutaka kutaja jina la Edna lakini akabadilisha na kutaja jina la CEO.

Wageni ambao walikuwa wamealikwa kwenye sherehe hio walikuwa na shauku ya kujua nini kinaendelea , baadhi yao walikuwa wakimfahamu Raisi Jeremy hivyo mara baada ya kumuona walishangaa kwani ujio wake haukutegemewa , lakini ni kwamba wasichokijua kabla ya ujio wa raisi huyo hapo Maple speed Resort kuna baaadhi ya wanausalama walikwisha kufika mapema kuimaliza protakali za ki ulinzi..

Wengi walishangazwa kuona Raisi Jeremy amesimama mbele ya Roma na Edna, walijua Edna alikuwa mfanyabiashara lakini haiwezekani kama mheshimiwa kaja mahali hapo kwa ajili yake na moja kwa moja waliamini itakuwa ni Desmond mtoto wake.

“Mr President can I help you ?”Aliongea Roma akimaanisha kuna kitu anataka amsaidie huku akionyesha kutopenda kabisa kuongea nae.

“Hongera kwa kuweza kurudi katika familia yako baada ya kupotea kwa muda mrefu , naamini kutokana na baba yako kuwa kiongozi mkubwa wa nchi tutapata nafasi ya kuonana mara kwa mara”.

“Acha kujikweza , mtu kama wewe huwezi kukutana na mimi”Aliongea Roma na kauli yake iliwafanya wanausalama kumwangalia kwa macho ya tahadhari, maana hawajawahi kuona mtu wa kawaida kuongea na raisi vile anavyotaka hata kama sio raisi wa Tanzania walijiambia anapaswa kuheshimiwa.

“Ineonyesha ukoo umepata mrithi mwenye uwezo mkubwa na kujiamini, nimefahamiana na baba yako kwa kipindi kirefu sana na urafiki wangu na yeye ulianza kwasababu yako , lakini mara baada ya kurudi kwako , kila ninapomuuliza kuhusu bahari zako hataki kabisa kunipa majibu ya moja kwa moja”.

“Sijui unaemzungumzia, Mr President nipo hapa na mke wangu kwa ajili ya kushiriki party lakini imeharibika hivyo tunaondoka kama huna lingine la kuongea”Aliongea Roma na kisha akamshika mkono kumuashiria waondoke..

“Subirini kwanza msiondoke”Sauti ya Desmond kutoka nyuma ilisikika na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia , awamu hii alionyesha ile hofu aliokuwa kwenye macho yake imekwisha kumpotea na sasa alikuwa akijiamini ,alikuwa ameshikilia glasi ya mvinyo huku akiwa ameachia tabasamu.

“Nyie wote ni wageni wa heshima ambao mmealikwa kwenye hii sherehe , kwanini ya kuondoka mapema, isitoshe mtu muhimu mheshimiwa yupo hapa nadhani ni fursa pia kwenu”Aliongea Desmond kana kwamba sherehe hio ilikuwa ya kwake.

Raisi Jeremy macho yake yote yalikuwa kwa Desmond , ni kama alikuwa akichunguza kitu flani lakini alishindwa kukiona.

Roma alishindwa kufanya maamuzi na kumwangalia Edna , hata hivyo aliekuwa mbele ni baba yake hivyo alitaka ampe nafasi ya kuamua kubaki au kuondoka , upande wa Edna hakuwa akijiamini kukaa mbele ya mwanaume anaefahamika kama baba yake ambaye hataki hata kumtambua na ni zaidi ya miezi minne alikuwa akijaribu kutuma nyumbe za barua pepe.

“Edna my young sister nadhanni baba kafika hapa kwa haraka kwasababu yako , sidhani unapaswa kuondoka bila ya kuongea nae kwani mnakutana mara moja kwa mwaka”Al;iongea Desmond na kuufanya moyo wa Edna kupiga kite kwani hakutegemea Desmond kuropoka.Roma ilibidi amshikilie mkono mara baada ya kuona Edna anatetemeka.

“Desmond unaongea ujinga gani?”Alifoka Raisi Jeremy huku akianza kubadilika sura lakini na Desmond na yeye alianza kubadilika vilevile.

“Unashangaa nini baba kutotoboa siri yako ulioficha kwa muda mrefu?”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kwanza kuangalia mazingira japo watu walikuwa mbeli na waliposimama , lakini alijua kama angegombana na mtoto wake mbele ya watu ingempunguzia heshima yake kama kiongozi na wasaidizi wake waliona hilo na haraka sana walianza kutawanyisha watu.

“Unapata wapi ujasiri wa kuongea ki mitego mitego mbele yangu?”.

“Usingefika hapa kama hukutaka ukweli ujulikane,baba nilichoongea ni kweli Edna ni mtoto wako na kama naongopa kanusha akiwa mbele yake”

“Kimya …!”Aliongea kwa hasira na muda huo huo alimwita bodygurad wake na kumpa maelekezo ya kughairisha shughuli zote zinazoendelea hapo na kila mmoja atawanyike na swala lile lilifanyika kwa haraka sana , kwani ndani ya dakika chache watu wote washapanda magari na kuondoka na wakabakia wanafamilia.

“Desmond kilichonileta hapa nikutaka kujua kama yule mwanamke ushakutana nae tayari?”Aliongea .

“Mwanamke gani?”

“Mama yako?”

“Haha.. mama ashakufa tayari , Baba huwezi ukaongea hivyo wakati uliongoza raia kuomboleza kifo chake”Aliongea Desmond na hapa ilionyesha kabisa Raisi Jeremy alishakutana na Kizwe.

“Acha kunipotezea muda wewe mtoto , kama hamjaonana usingeongea ujinga wako , ndio sababu moja tu ilionileta hapa la sivyo nisingepoteza muda wangu”Aliongea huku akionyesha kuwa na hasira mno.

“Baba kwanini unaongea kwa hasira namna hio , nadhani uwepo wa mama kwenye maisha yetu ni jambo la kufurahia”

“Unajua nini wewe,nijibu swali langu Kizwe yupo wapi?”

“Baba sijui unachoniuliza ni nini , na laiti ningejua kuhusu kilichomtokea mama yangu nisingepoteza machozi yangu namna ile na nisingeumia moyo wangu kwasababu ya Edna , ndio maana ulikuwa mkali sana kutotaka ni mguse kumbe alikuwa ni mtoto wako wa nje ya ndoa na ulivyoona mama anataka kumfilisi ukaamua kupanga njama za kumuua”

“Wewe mtoto nimekuambia kaa kimya?”Alifoka.

“Kwani nakosea? , haishangazi ndio maana ulinipiga vibao bila ya kunijali , siku zote tumeishi pamoja , mama alikujali sana na kuwa msaidizi wako lakini kwasababu ya mtoto wa nje ya ndoa ukafanya maamuzi ya kumuua”Aliongea huku akitoa tabasamu la hasira.

“Kama kweli ulikuwa ukimjali kwanini hukuwahi kumtambua? Au ulikuwa ukiogopa watu kukunyooshea vidole ,haijalishi wewe ni raisi lakini ni binadamu vilevile haikuwa na haja ya kukaa kimya, unajua najisikiaje baada ya kugundua mwanamke niliekuwa nikimtamani ni mdogo wangu ?”

SLAP!

“Unanipiga tena?, kwanini usiniue tu na ukamalizana na mimi pia moja kwa moja , hata hivyo tayari ushapata mrithi wako”Aliongea huku akionekana kama mtoto mdogo mwenye wivu , kwa umri wake huenda hakupaswa kuwa kama hivyo.

Roma hakutaka kumvumilia Desmond na palepale alimpiga teke na kumfanya adondoke kama furushi, kitendo kile kiliwafanya walinzi kutoa siraha zao haraka na kumnyooshea Roma ,sio kwamba hawakumfahamu Roma alivyo ilikuwa mara ya pili kukutana nae na akafanya vitendo vya hatari kwa mheshimiwa hivyo muda huo walikuwa makini sana na yeye

“Roma usimpige tena”Aliamrisha Raisi Jeremy mara baada ya Roma kutaka kumuongezea lingine.

“Unajua maana ya kupiga , sijampiga bali nimemsukuma tu”Aliongea Roma na kumfanya Jeremy amwangalie kwa macho makali.

“Roma tuondoke”Aliongea Edna kwa kubembeleza alikuwa ashaanza kutokwa na machozi na kumshika mkono Roma na hakutaka kumkatalia aliona ndio anaeumia zaidi.

Desmond alijilazimisha kusimama huku akiugulia maumivu akiwaangalia Roma na Edna wanavyoondoka bila waswasi.

“Raisi Jeremy , unamwachaje mtu kama yule aondoke ilihali kampiga mtoto wako wa kipekee , mrithi wako, unapaswa kuwa kweli raisi wewe kama unamuogopa kinyamkela kama yule”

“Desmond nitakupiga nikuue , kaa kimya , huoni kwamba ukimchokoza zaidi atayakatisha maisha yako”

“Aniue.. Hahaha… kabla hajaniua nitahakikisha namuonja yule malaya hata kama ni ndugu yangu wa damu”Aliongea ilionekana hata hivyo kilevi kilishamkolea ndio maana alikuwa akiongea bila ya kufikiria.

Roma aliweza kusikia lile tusi na alijikuta akisimama kabla hajafungua mlango wa gari na kuingia..

“Nadhani hupendi kuendelea kuishi , unadhani siwezi kukufanya chochote kwasababu upo mbele ya baba yako kwa kumtukana mke wangu?”Aliongea Roma huku hasira zilianza kujitengeneza kiasi kwamba hata macho yake yalitisha.

Lakini kabla hawajaelewa kinachotkea Roma alipotea aliposimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Desmond na kuinyakua shingo yake na kuing’ingiza juu Desmond alijitahidi kujinasua kwenye mkono wa Roma lakini jitihada zake zilikuwa bure , wale walinzi pia walitaka kumuokoa lakini waliogopa kushambulia kwani wangemdhuru na Desmond hivyo walimwangalia Raisi Jeremy kupata amri yake.

Ndio wakati ambao Desmond alijua sasa kifo chake kinaweza kutekelezwa muda wowote na alifanya kosa kumchokoza bila ya kufikiria mara mbili.

“Roma hapana…”

Edna alikimbia na kwenda kumshika Roma tisheti akimzuia asimuue Desmond na ilikuwa bahati kwa Desmond maana alitaka akaze mkono na kumkatisha uhai palepale.

“Usimuue , Roma nakuomba tafadhari usimuue”Aliongea Edna lakini Roma aliendelea kuminya na kumfanya kuanza kurusha miguu kulia na kushoto akionyesha dalili ya kupoteza hewa.

“Edna mwambie aache tafadhari , Desmond hayupo kwenye akili zake timamu kwasasa ndio maana kaongea ujinga na ndio mtoto wangu wa pekee na mrithi niliebakiwa nae sitaki kumpoteza pia”Aliongea na kumfanya Edna amgeukie Jeremy na kumuangalia ‘neno mtoto wangu wa pekee niliebakiwa nae’ lilijirudia mara mbili mbili.

Edna aling’ata meno yake kwa hasira na kisha akamshika mkono wa kushoto Roma.

“Mwachie aondoke”Aliongea.

“Unamaanisha nini nimuachie wakati kakutukana”Aliongea Roma huku akionyesha ishara ya kutotii ombi la Edna.

“Honey …Edna alianza kupasha viganja vya mikono huku akijaribu mbinu za kike kumlegeza.

“Hii ni mara ya mwisho nakuomba , tafadhari….sitokuomba tena naomba usimuue , akirudia tena sitokuomba tena umsamehe”Roma alijikuta akikasirika.

“Una uhakika gani hatorudia , haujamsikia alivyokutukana”Edna alijikuta akishindwa kujua cha kufanya , alimwangalia Raisi Jeremy na kuona yupo kwenye wasiwsi na ameshindwa kuchukua hatua zozote kutokana na kumhofia Roma.

“Roma kama utamuua leo hii siwezi kukusamehe maisha yangu yote”Aliongea Edna na kumfanya Edna kumwangalia kwa mshangao na hakujua hata ni muda gani ameachia mkono wake na kumruhusu Desmond kudondoka chini kama furushi.

“Edna unanitishia kisa hii taka taka , unanitishia mimi mume wako?”

“Hapana …najua nimekosea na sio fair lakini hii ni mara ya mwisho haitorjirudia”Aliongea huku akimuogopa Roma yeye mwenyewe.

“Okey sitomuua”Aliongea Roma na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi za ahueni na kuwapa ishara walinzi kushusha siraha chini na Roma baada ya kuona hivyo alimwangalia tena Desmond aliekuwa amejichanua chali mbele yake akivuta hewa na palepale alimpiga teke lingine sehemu zake za uzazi .

“Ow..!!”Hata sauti haikumtoka kutokana na maumivu alioyasikia na palepale alipoteza fahamu.

“Desmond!!”

Raisi Jeremy alikimbilia alipolala Desmond bila ya kujali tena , Alimshika mabega na kuanza kumtingisha lakini hakukuwa na majibu ya aina yoyote kutoka kwake.

Edna alijikuta akimwangalia Roma kwa mshituko bila ya kuelewa hisia zake , alijua Roma ashakubaliana na ombi lake lakini yamegeuka kuwa mengine.

“Umeomba nisimuue lakini sio kutokumuadhibu kutokana na makosa yake”Aliongea Roma na kisha akamsogelea karibu.

“Una baki au tunaondoka wote?”Aliuliza Roma kibabe na kumfanya ameze mate ya huzuni.

“Kwanini umemfanyia hivyo?”

“Unabaki au unaondoka?”Aliuliza mara nyingine. Na kumfanya Edna amwangalie Mheshimiwa Raisi Jeremy aliechuchumaa huku akiwa ameshikilia Desmond kwa huzuni , alijikuta akiumia ndani kwa ndani kwa kuona hakuna dalili ya kutambulika kama mtoto tena.

Walinzi walipisha njia wenyewe , hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kumfanya Roma chochote kutokana na kutahadharishwa na mheshimiwa mwenyewe , hivyo waliishia kumwangalia Roma na Edna wanaingia kwenye gari.

“Roma kama mwanangu akapatwa na ukilema nitakufanya jambo ambalo hutokaa usahau”Aliongea Raisi Jeremy kwa hasira lakini Roma hakumjali zaidi ya kuingia kwenye gari.

Muda huo huo na wale walinzi walimsogela Mheshimiwa na kisha wakamchukua Desmond na kumuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumuwahisha hospitalini.

Roma aliendesha gari kimya kimya , hakuwa na mudi yoyote ya kuongea na Edna alikosa amani kutokana na ukimya wake , alijua amekosea lakini asingeweza kuona Roma akimuua ndugu yake wa damu mbele yake.

“Bado una hasira na mimi?”Aliuliza.

“No”

“Unazo , Roma naomba tusahau yaliotokea leo , kwanzia leo nawasahau kwenye maisha yangu”

“Usiwazie sana , No means no”

“Unanidanganya acha kujizuia na kama ni kunifokea nifokee yaishe”Aliongea na kumfanya Roma kung’ata meno kwa hasira na kukanyaga padeli na kufanya gari lianze kunguruma kama simba huku likitembea kwa kasi kama mshale.

“Sina haja ya kukufokea , haujafanya chochote kibaya”Alijibu Roma na kumfanya Edna ashindwe kujua nini kingine cha kuongea na aliishia kukaa kimya.

Saa tatu usiku ndio muda ambao waliweza kufika na Blandina alishangaa kuona wamerudi mapema , alitarajia kurudi kwenye saa tano na namna pia Edna alivyonekana kuchafuka , lakini pia nyuso zao zilivyokosa nuru ya furaha ilimshangaza na Edna mara baada ya kusalimia nae alipandisha ngazi.

“Nini kimetokea Roma , mbona mmeondoka mkiwa vizuri na mmerudi mkiwa mmenuniana”

“Hakujatokea kitu Party haikuwa nzuri sana tumeamua kurudi”

“Mh! Naona kabisa mmegombana”Aliongea.

“Mama usiwe na wasiwasi”Aliongea Roma na kisha akapandisha juu kwenye chumba chake na alipoingia alijibwaga kwenye sofa na kuvuta pumzi nyingi huku akiwa amefumba macho.

Zilipita kama nusu saa tu mlango ulifunguliwa na Edna aliingia huku akiwa ashabadili mavazi na kuvaa ya kulalia kitambaa cha hariri , baada ya kumuona Roma amelala kwenye sofa akiwa gizani alijihisi kuumia na kuona huenda alichokifanya kimemkwaza sana .Alitembea taratibu na kwenda kusimama pembeni yake na Roma alifumbua macho na kumwangalia na kisha akayafumba tena.

“Hubby nimekuandalia chakula tayari nikuletee hapa hapa au unashuka tukale wote?”Aliongea Edna huku akijaribu kulegeza sauti awezavyo lakini Roma hakujibu kitu.

“Au unataka kuoga kwanza nitapasha maji yako moto yawe ya uvuguvugu na yatakuweka sawa”

“Huna haja ya kunifurahisha ki makusudi”

“Sio hivy… Sifanyi kimakusudi ni kwasababu napaswa kufanya hivi kama mkeo”Aliongea na kumfanya Roma asimame.

“Ulitakiwa kuniacha nimmalize Desmond moja kwa moja kwanini ukanitishia kutokunisamhehe kwasababu ya yule mpuuzi?”

“Bado una hasira na mimi?”

“Kwannii niwe na hasira na wewe , hasira ni juu yangu mwenyewe najilaumu kwanini nimemuachia kwa kukusikiliza wewe , nishawahi kumsamehe mara ya kwanzo na akarudia na nina uhakika atarudia tena , ulichofanya leo kitakuingiza kwenye matatizo baadae, Sijui kwanini nnimekuwa mjinga na kukusikiliza”Aliongea Roma na kisha akavua tisheti na suruali bila ya kumjali Edna aliesimama na aliingia bafuni na kubamiza mlango kwa nguvu.

Edna alisimama palepale akiwa hajui cha kufanya maana alimuona Roma kuwa mwenye hasira na alijikuta machozi yakianza kujitengeneza.

Roma mara baada ya kuingia bafuni alivua bukta yake na kisha akafungulia bomba la mvua(Shower) na kuacha maji ya mloanishe huku akiwa amefumba macho na kufanya kifua chake kilichojengeka kimazoezi kupanda na kushuka akijitahidi kutuliza hasira zake.

Lakini mlango wa bafuni ulisukumwa na Edna na kumfanya ageuke na kumwangalia.

“Unafanya nini?”Aliuliza Roma kwani alijua Edna hajawahi kufanya kitu kama hicho kwenye maisha yake.

“Kwanini unanifanyia hivyo Roma?”

“Unamaanisha nini?”

“Nimekuomba na kukuomba na nimejitahidi kukujali ili unisamehe , kwanini unashindwa kuacha hili lipite”

“Tutaongea nikimaliza kuoga”

“Hapana..!!, umenisaliti mara kibao lakini mwisho wa siku niliishia kukusamehe , kwanini mimi unanikatili wakati nishakuomba msamaha?”

“Edna nilichotaka kufanya ni kwa ajili yako , kwanini huelewei , Desmond hawezi kubadilika na Jeremy umeshuhudia mwenyewe hana mpango hata wa kukutambua”

“Ndio maana nimesema ni mara ya mwisho , kwanini hunielewi?“Aliongea Edna bila kujali maji ya bomba yanamloanisha.

“Una baba na kaka ambao wewe huwatambui na wao hawakutambui lakini huwezi kupotezea uwepo wao kwenye maisha yako , kwa mfano Denisi ni mara ngapi uliweza kumsamehe na kumuachia , je kama ni mtu mwingine aliekuchokoza ungemwachia na kuondoka?”

“Kwanini nipotezee kila kitu najua hakuna anaenihitaji na Desmond kanikosea lakini kwanini unaona ni kosa kwangu kuwaachia waondoke kwa mara ya mwisho?, ila sawa tu fanya utakavyo mimi ndio ambaye napaswa kukusamehe kila mara unaponisaliti , sawa usinisamehe na mimi nitakusamehe kila unaponikosea”Aliongea na kisha kihasira aligeuka lakini alijikuta akikanyaga sabuni na kuteleza lakini kabla hajatua chini Roma aliwahi kumdaka na maji ndio yalimloanisha kisawa sawa na kufanya nguo kugandia mwili wake.

Roma alimwangalia usoni huku akiwa amebadilika na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

“Unanicheka ?”Aliongea huku akijitahidi kuangalia pembeni akionyesha hajaathirika maana Roma hana nguo.

“Nafikiri ishaongezeka na kuwa kubwa,,”Aliongea na kumfanya Edna kuona aibu za kike,lakini Roma hakuwa na namna ya kumuachia kwa muda kama huo.

Na kilichoendelea kilianzia bafuni huko huko na kuhamia chumbani na ni vilio tu vilivyosambaa kila kona.

Upande mwingine wakati Roma akifurahia uanaume wake kwa kumlaza mke wake mrembo Edna kunako sita kwa sita ndani ya hospitali ya Aghakhan ilikuwa taarifa mbaya kwa raisi Jeremy.

“Mr President we tried our best but we cannot recover his reproductive organs , it has been damaged both internally and externally beyond repair”

“Mheshimiwa tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini hatuwezi kurudisha tena mfumo wa ogani zake za uzazi , zimeharibika nje ndani kiasi cha kutotibika tena”Aliongea dokta kihindi

Ilikuwa taarifa mbaya kupokea huenda katika maisha yake yote , Desmond ndio mtoto wake wa pekee wa kiume ambaye alitarajia kuendeleza kizazi chake , anapokeaje taarifa ya kwamba hawezi tena kuwa mwanaume aliekamilika.

Baada ya kusharabu kauli ya daktari alijiambie hapana , lazima kuwe na namna ya kumuokoa mtoto wake kwa namna yoyote ile.

“Have our medical staff come over to take care him and you prepare plane we are going back”Aliongea akimaanisha kwamba watu wao wa afya waje kumuangalia mgonjwa na mwingine aandae ndege kwani wanarudi Rwanda.













SEHEMU YA 488.

MWEZI MMOJA NYUMA KIGALI.

Ilikuwa ni mtanange wa kibabe kati ya Kizwe na Lekcha , ijapokuwa aliwahi kufunga goli la kwanza kutokana na ukame wa muda mrefu aliokuwa nao , lakini mzunguko wa pili ulidumu kwa muda mrefu.

Huenda mwanafunzi yoyote wa chuo ambaye angesogelea ofisni ya mkufunzi wa fiizikia angesikia kwa nje kile kichokuwa kikiendelea ndani kwani Kizwe alionyesha kutoweza kuhimili hisia na kupiga makelele huku akitaja jina la Kilema.

Baada kama ya nusu saa Lekcha miguu ilimtetema na ilikuwa ni muda ambayo alikuwa akikamilisha mzunguko na alijitupa pembeni huku akihema kama mbwa baada ya kuwashusha wote.

“Kilema wangu , umeimarika sana kwa siku zote ambazo hatukuonana”aliongea.

“Niite Lekcha sio kilema”Aliongea

“Hapana ‘kilema’ ni jina ambalo limekaa kimahaba mpenzi , naomba usinizuie kukuita hivyo kuanzia leo”Aliongea na kumfanya Lekcha kutabasamu kifedhuli, tokea aanze kupata ufadhili kutoka kwa raisi wa taifa la Rwanda maisha yake yalikuwa mazuri na hata ule ukilema ulipotea mbele za macho ya watu kutokana na kupata matibabu mazuri ya viwango.

Hakupenda jina la Kilema kwani lilimkumbusha maisha yake ya nyuma , lakini Kizwe tokea wanaanza mchezo ameng’ang’ania kutaja jina la Kilema mwanzo mwisho, lakini kwa muda huo hakuona shida , alijiambia labda ni kwasababu ndio namna inavyomfanya kupandwa na hisia zaidi.

“Such a bitch”Aliwaza Lekcha kwenye akili yake , ijapokuwa ndio mara yake ya kwanza kukutana na Kizwe mara baada ya kushuhudia kifo chake , lakini ujio wake haukumfurahisha na sio kwamba alikuwa akimpenda.

“Umekuwa mrembo sana Kizwe”Aliongea Lekcha na kumfanya Kizwe kumsogelea na kumkumbatia.

“Nimerudi kwako kwasababu najua ni wewe pekee unaenipenda kwa mapenzi ya dhati”

“Mtu kama mimi mwenye ukilema , unaamini vipi nakupenda?”

“Haijalishi ilimradi nauona upendo wako juu yangu ni wa dhati hilo ndio la muhimu”Aliongea na kumfanya Lekcha kutabasamu.

“Niambie nini kimetokea mpaka ukawa hai na kuwa na mwonekano wa kitoto kama huu huenda na mimi ninaweza kuponyesha huu mguu”.

“Unamaanisha unataka kua kama mimi?”

“Sio kuwa kama wewe nataka kujua nini kimetokea , hivi unajua ni maumivu kiasi gani nimeishi nayo kwa kushuhudia kifo chako , niliishi kwa chuki sana zidi ya aliekuua”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu.

“Niliweza kuishi tena baada ya kufufuliwa na Yan Buwen , ndio aliehusika na mimi kuwa kama hivi”Aliongea.

“Yan Buwen!!!”Aliongea kwa kuhamaki.

“Ndio ambaye amekusaidia?”

“Mbona umeshangaa kama unafahamu jina lake?”Aliuliza.

“Nafahamu jina lake ndio , hakuna mwanasayansi siriasi ambaye hamfahamu , Yan Buwen ni mwanasayansi ambaye alikataa tuzo ya Noble Prize na umaarufu wake ulianzia hapo”Aliongea na kumfanya Kizwe kushangaa kidogo.

“Lekcha unashangaza , unaonyesha kujua mambo mengi na hata nilipopata taarifa umeweza kuwa Profesa wa chuo kikubwa kama hiki nilishangaa na kujiuliza maswali mengi kwanini ulikuwa Tanzania kwenye majalala tena ukiwa raia wa Rwanda?”Aliongea na kumfanya Lekcha kutulia kidogo.

“Nadhani mpaka sasa ushafahamu taarifa zangu si ndio?”

“Nataka uniambie wewe mwenyewe Lekcha haijalishi najua nini kuhusu wewe , ila nataka kusikia kila kitu kutoka kwako ,mara ya mwisho uliniambia siwezi kukutimizia unachotaka kupitia pesa na shauku yangu ndio hio , nataka kukujua kwa udani maana najua wewe sio mtu wa kawaida ambay hukupaswa kuokota makopo”

“Nitakueleza muda muafaka ukiwadia ila ninachoweza kusema adui wako ni adui wangu wa muda mrefu”

“Unataka kumaanisha nini?”Aliongea Kizwe kwa mshangao na Lekcha alisimama na kisha akasogelea droo ya meza na kuivuta na kisha akatoa picha chakavu na kumpatia.

“Huyu ni…”Aliuliza Kizwe kwa mshangao akiangalia picha ya kijana mmoja alievalia mavazi ya kininja.

“Anafahamika kwa jina la Ajent code 13 huyu ndio adui yangu ambaye ni adui yako”

“Sijakuelewa”

“Huyu ajent 13 ni siraha iliotengenezwa na taasisi ya siri ya Zeros organisation na ndio Roma Ramoni adui yako wa sasa”Aliongea na kumfanya Kizwe kushangazwa na maneno ya Lekcha.

“Ndio mtu ambaye alinipatia huu ukilema na ndio adui yangu namba moja na wewe kunikuta Tanzania ni mwendelezo wa kutafuta namna ya kulipiza kisasi changu”Aliendelea kuongea huku awamu hii akionyesha kukasirika na Kizwe alimwangalia kwa mshangao na kuanza kujiuliza Roma ni nani haswa ,kwanini hata kwa Yan Buwen alikuwa na kisasi nae.

Clelia mpenzi wangu nipo njiani naja.. nitamtumia huyu mwanamke kumsogelea Yan Buwen na kupitia yeye nitamuua Hades na kama ulivyosema utanipokea baada ya kukuonyesha uwezo na nguvu zangu”Aliwaza Lecha akitaja jina la Clelia na aligeuza macho yake na kuangalia picha iliokuwa imetundikwa ukutani.

“Lekcha kwanini unaangalia sana hio picha?”Aliuliza Kizwe akiangalia picha iliokuwa ukutani yenye maandishi ya United Nation general Secretary, Clelia Allisanto.

“Kwasababu niliikuta imetundikwa hapo ukutani na inashangaza”

“Inashangaza nini?”

“Wewe huoni umri wa Clelia Allisanto na nafasi yake?”Aliongea na kumfanya Kizwe kuwaza kimantiki sasa , mwanzoni aliangalia uzuri wa mwanamke huyo lakini hakuangalia cheo chake na kweli haiwezekani kwa umri wake kuweza kufanikisha hilo tena akiwa ni mwanamke.

**********

Katika wanawake wake wote ambaye alikuwa amepiga hatua kimafunzo ni Rose pekee na Roma ilimshangaza kwani aliweza kuingia kwenye levo ya nusu mzunguko kwa muda mfupi sana , ijapokuwa ilikuwa levo ya chini katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi , lakini ilikuwa ni hatua kubwa ambayo amefikia na Roma ilibidi ampatie vidonge ambavyo alivichukua mara baada ya kuwaua watu wa hongmeng ili kumuwezesha kupanda levo kwa haraka.

Huwenda sababu ambayo ilimfanya Rose kupanda levo kwa haraka ni kutokana na kutokuwa na kazi ambazo zinamchukulia muda mwingi kama ilivyo kwa wenzake

Kwa mfano Amina alikuwa nyuma sana na yote hayo ni kutokana na majukumu kwani baba yake mzazi alikuwa nje ya nchi na yeye alipaswa kusimamia biashara zake kwa muda kutokana alikuwa akisumbuliwa na magonjwa.

Upande wa Nasra yeye alikuwa bize na ujenzi wa mradi wa Adani hivyo kazi ndani ya kampuni zilikuwa zimeongezeka maradufu.

Jambo moja ambalo lilimshangaza Roma ni juu ya Dorisi pekee, Roma aliona kitu cha ajabu ambacho alihisi huenda Dorisi alivyokutana na mwanamke anaefahamika kwa jina la Clelia Allisanto kuna kitu kilitokea.

Kila alipokuwa akifanya mapenzi na Dorisi alikuwa akijihisi kuchoka mno na ni kama nguvu zake zinanyonywa na kitu kingine Doris alionekana alikuwa akiimarika zaidi kila wanapokutana na hilo ndio ambalo lilimshangaza na kuona Dorisi ndio ambaye hakuwa wa kawaida , lakini hata hivyo hakutiliia sana maanani hisia zake.

Alijiambia kama Dorisi anaimarika kwa kufanya nae mapenzi basi atajitahidi kuhakikisha anamsaidia katika hilo.

Edna ndio pekee ambaye alikuwa kawaida tu , licha ya kwamba alikuwa akichukua mazoezi kila asubuhi lakini Roma hakumruhusu kuanza kwa kuhofia kwamba mwili wake ni mdhaifu mno.

Ijapokuwa Edna hakupenda kuwa nyuma nyuma , lakini hakuwa na jinsi kwasababu Roma ndio mwalimu wake na ilipaswa amsikilize hata kama hakuwa akiridhika na alichofanya ni kuendelea kujitahidi kuchukua mazoezi.

Ni saa tisa mchana siku ya ijumaa Edna na Suzzane walionekana ndani ya hoteli ya Peacock kwa ajili ya miadi na mgeni siku hio.

Edna alishangazwa sana jana yake Suzzane kumpigia simu akielezea kwamba Tajiri Khalifa mwenyekiti wa taasisi ya Emaar Foundation ndio ambaye amefika nchini kwa ajili ya kuonana nae.

Khalifa alikuwa tajiri mkubwa na ilishangazwa na ujio wake , ijapokuwa hata yeye ni tajiri mkubwa lakini kujilinganisha na Khalifa alieanza biashara zaidi ya miaka hamsini iliopita ilikuwa ni kumvunjia heshima.

Ndio maana muda huo wakati wanashuka kwenye gari alikuwa na mchecheto , kwanza kabisa alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini Khalifa kachangia mchango mkubwa kwenye taasisi yake , lakini muda huo uho akataka kuonana nae , hayo ndio maswali ambayo Edna alikuwa nayo na aliamini majibu yake yangeweza kujibika mara baada ya kukutana na mgeni huyo kutoka Taifa la urabuni Abu dhabi.

Kwasababu walikuwa na miadi waliweza kupokelewa na mhudumu na kuwaongoza mpaka kwenye lift na kutokea kwenye Floor za juu kuelekea kwenye chumba ambacho alikuwepo Tajiri khalifa , Edna alikuwa akijiamini kwasababu hakuwa peke yake.

Ila asichokijua ni kwamba Fayezi mtoto wa Tajiiri Khalifa aliuliwa na Roma mara baada ya kutaka kumlazimisha Amina afunge nae ndoa.

Baada ya kufunguliwa mlango na mhudumu mwenye asili ya kiarabu alievalia suti , Edna alishangazwa kukuta sio mtu anaekutana nae bali ni jopo la watu kama ishirini waliojipanga kwenye meza na ajabu ni kwamba mara baada tu ya kuingia wote walisimama kiheshima na kati ya sura alizozifahamu ni moja tu ambaye ni Nadia Alfonso mwanasheria wake.

Upande mwingine Roma akiwa kazini aliweza kupigiwa simu na Afande Kweka , alishangaa kupigiwa simu na huyo mzee babu yake kwani haikuwa kawaida yake.

“Uko wapi wewe mtukutu?”Aliuliza Afande Kweka kama kawaida yake.

“Nipo kazini tena kwenye kikao”

“Kuna mambo nahitaji tuongee lakini pia Zenzhei anaondoka”Aliongea.

“Unamaanisha nini Zenzhei kuondoka”Aliongea Roma na kumpa ishara Tanya ya kuendelea na alichokuwa akijadiliana nae na Tanya alitikisa kichwa na kutoka kwenye ofisi ya Roma.

“Muda wake wa kukaa kwenye ulimwengu wa kawaida ushafika kikomo na anapaswa kurudi kwenye miliki ya Hongmeng , anataka muonane kabla ya kuondoka”Aliongea Afande Kweka na kumshangaza.

“Kwani alikuwa na ukomo wa kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida?”

“Kama unataka majibu ya swali lako hakikisha kabla ya saa kumi na mbili za jioni upo hapa , alipaswa kuondoka jana lakini aliomba kuongezewa masaa mpaka leo jioni”Aliongea Afande na kumfanya Roma kushangaa lakini kwasababu alijua mzee huyo asingejibu maswali yake basi alimuambia anakuja.

Wakati Roma akipokea simu na Edna akikutana na jopo la watu asiowatambua upande mwingine katika mkoa wa Pwani Bagamoyo , Blandina na yeye alikuwa na miadi na mtu ambaye hakuwaza kama atakuja kumtafuta na kuongea nae tokea arudi nchini.

Ukweli mwanamama huyu alijishauri sana kwenda kuonana na mtu huyo tokea alipopata ujumbe wake na yote hayo ni kutokana na kukosa ile hali ya kujiamini.

Alijihisi kuwa mkosaji mbele ya Senga na chochote kilichotokea miaka kadhaa iliopita yeye ndio mkosaji , kwani yeye ndie aliefanya maamuzi ambayo yalikuwa ya ki usaliti , ijapokuwa hakufanya maamuzi hayo ya kiusaliti kwa makusudi lakini haikuwa ikimfanya kutokuwa mkosaji.

Raisi Senga alitaka kuonana na Blandina na muda huo wa mchana wakati Raisi huyo alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa bandari Bagamoyi, alipanga miadi hio ya siri ili mke wake asije kufahamu.

Naam ni ndani ya hoteli ya Bagamoyo Resort ndio sehemu ambayo Blandina alikuwa akipaswa kukutana na mheshimiwa na muda huo alishuka eneo la maegesho, alifika mwenyewe akiendesha hivyo mara baada ya kushuka kutoka kwenye gari alifuatwa na Kabwe msaidizi namba moja wa Raisi Senga na kumuongoza njia.

Kule Jopo linamkaribisha Edna , kule Blandina na Senga , Upande mwingine ni Roma na Zenzhei.
 
SEHEMU YA 489.

Baada ya kufunguliwa mlango na mhudumu mwenye asili ya kiarabu alievalia suti , Edna alishangazwa kukuta sio mtu anaekutana nae bali ni jopo la watu kama ishirini waliojipanga kwenye meza na ajabu ni kwamba mara baada tu ya kuingia wote walisimama kiheshima , kati ya sura alizozifahamu ni moja tu ambaye ni Nadia Alfonso mwanasheria wake.

Edna na Suzzane walihisi wamekosea chumba walichopaswa kuingia na Edna alitoa ishara ya kuomba msamaha kwa kuingilia kikao.

“Karibu sana Madam Persephone” Waliongea wote kwa pamoja kwa lugha ya kingereza na kisha waliinamisha vichwa kuonyesha ishara ya heshima jambo ambalo lilimpagawisha Edna na moyo wake kupiga kwa nguvu , alijihisi ni kama anaota na akishituka ingekuwa ndoto.

Kwa mara ya kwanza alihisi jina la Madam Persephone ambalo alilikuwa akiitwa mara kwa mara bila ya kujua sababu yake alihisi sio la kwake , ule ujasiri aliokuwa nao kwa muda huo ulimpotea na aliishia kuduwaa.

Suzzane pia alikuwa kwenye mshangao asijue nini kinatokea mbele ya macho yake , walikuja hapo kwa minajili ya kukutana na Tajiri Khalifa kutoka Dubai , mtu ambaye alichangia kiasi kikubwa cha pesa katika taasisi ya Edna Foundation na uwepo wao hapo ni kutii wito wa kuonana na tajiri huyo , lakini mambo yanaonyesha kuwa tofauti.

Licha ya kwamba alihisi yupo ndotoni lakini ulikuwa uhalisia na jinsi watu waliokuwa mbele yake walivyokuwa wakimwangalia alijua kabisa walimlenga yeye na ndio ambaye alikuwa akisubiriwa, lakini bado alijiuliza kwanini yeye na ni maigizo gani yanafanyika.

Kwanza chumba kilionekana kilikuwa cha mikutano ndani ya hoteli hii ya Peacock, pili mpangilio wa hapo ndani ulikuwa ni wa kikao muhimu kutokana na watu waliokuwepo , ilikuwa ni meza ndefu ambayo inajumla ya watu kumi kila upande kukamilisha watu ishirini na ni kiti kimoja tu ambacho kilikuwa wazi , kiti cha katikati ambacho huruhusu mkaliaji kuona nyuso za kila mtu aliekuwa mbele yake , ni rahisi kusema ndio kiti cha mwenyekiti kama ni kikao ambacho kinatarajiwa kufanyika.

Watu waliofahamika ambao wapo ni Shekhe Assad , Tajiri Khalifa , Mellisa Luiz , Pastor Cohen , Nadia Alfonso , Zoe Kovacic , Phill Knight na wengine wengi ambao ilionyesha ni wanachama wa Ant- illuminat.

Mwanadada mmoja aliekuwa wa kifilipino , alievalia suti alimsogelea Edna na kuinamisha kichwa mbele yake kwa namna ya heshima na kisha akavuta kiti kilichokuwa wazi na kumuonyesha ishara ya kukaa.

Edna bado aikuwa kwenye mshangao na alishindwa kujua achukue maamuzi , ya kuondoka au abaki na hata aliponyeshwa kiti cha kukaa bado hakupiga hatua kukisogelea maana alijua kukaa kwenye kile kiti ni kama yeye ndio anakwenda kuongoza kile ambacho kingekwenda kuendelea hapo ndani , kitu ambacho hata hakijui ni nini.

“Madam!!!” Suzzane alimshitua Edna ambaye bado alishindwa kufanya chochote licha ya kuonyeshwa kiti cha kukaa.

Edna aliinua uso wake na kuanza kuangalia kila mmoja ambaye yupo ndani ya hiko chumba, kuna wengine alikuwa akiwafahamu na kuna wengine hakuwahi kuwaona popote.

Lakini ghafla tu Edna alitoa tabasamu hafifu kama vile anavyofanyaga akiwa kwenye kampuni yake akiwa na kikao na wafanyakazi wake na alisogelea kile kiti na kuketi na kuwaangalia watu wote waliokuwa hapo ndani kama vile alikuwa akiwajua.

Ni kintendo ambacho hakikumshangaza Suzzane tu lakini kila mmoja kilimuacha na maswali lakini sio hivyo tu pia kiliwafanya kuwa na tumaini.

**********

Roma baada ya kuambiwa na Afande Kweka kwenda kuonana na Zenzhei , hakutaka kuchelewa sana , alikuwa na shauku ya kujua kwanini Zenzhei anataka kurudi Hongmeng baada ya kuishi Tanzania kwa muda mrefu.

Alitaka pia kujua ni jambo gani ambalo Zenzhei alitaka kumwambia , alikuwa na shauku kubwa kutokana na kwamba alikuwa na mpango wa kuivamia Hongmeng siku moja hususani muda huo ambayo alijua kabisa yeye ni adui na jamii hiyo , hivyo alitaka kukusanya kila taarifa iliokuwa ikihusiana na jamii hizo ili kumsaidia huko mbeleni.

Roma alimuaga sekretari wake kwamba anatoka na anagerudi siku iliokuwa inafuata , Tanya alishangaa kutokana na kwamba kuna baadhi ya maamjuzi yalikuwa yakimpasa kuyashughulikia siku hio hio lakini alikosa ujasiri wa kumzuia Master wake.

Ni zaidi ya miezi sasa tokea Tanya achukue majukumu ya Amina kama Secretari na alionekana ashanza kuipenda kazi yake na kuizoea na alikuwa ni msaada mkubwa kwa Roma kwani mambo mengi aliyafanyia kazi.

Muonekano wake ulikuwa umebadilika kwa asilimia mia moja na ilikuwa ngumu kujua ndio anaehusika kuongoza kundi la Yamata kutoka Japani ambalo linamilikiwa na Roma.

Roma alitumia muda machache sana kufika nyumbani kwa babu yake na baada ya kusalimiana na Afande Mstaafu Camilius Kweka ilisalimiana na Zenzhei pia wote walikuwa wamekaa nje kwenye bwawa la kuogelea na ilionekana walikuwa wakiongea.

“Nitawaacha muongee”.

“Camilius haina haja ya kuondoka , ninachoongea na Mr Roma sio kipya kwako”

“Hapana umesubiria muda mrefu na huu ni muda wako, Wewe mtukutu ukimaliza unione kwanza kabla ya kuondoka”Aliongea Afande Kweka na kisha aliondoka eneo hilo.

“Mr Roma samahani kama nimekuchukulia muda wako , muda huu ulipaswa kua kazini”

“Usijali kuhusu hilo , nilipaswa kuja hata jioni lakini kwasababu sikuwa na kitu cha kufanya kazini nimeona nije mapema”Aliongea Romana kumfanya Zenzhei kutingisha kichwa kumuelewa.

Na muda huo mfanyakazi aliwaletea Juisi ya matunda na kuweka mbele yao na kisha akaondoka.

“Mr Roma muda wangu wa kukaa kwenye ulimwengu wa kawaida umeisha”

“Nilipoambiwa unaondoka nimeshangaa , kwani ulikuwa na ukomo wa kuishi Duiani?”

“Nadhani ushawahi kisikia sheria za miliki za kijini juu ya binadamu au viumbe wanaojifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi?”

“Najua watu wa jamii kutoka miliki za kijini na binadamu ambao wamefikia katika levo ya Nafsi hawapaswi kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida”

“Upo sahihi Mr Roma na mimi muda wangu wa kuishi hapa duniani ushafikia ukomo?”

“Lakini uliishi kwa miaka mingi hapa Tanzania na naamini bado ulikuwa kwenye levo ya Nafsi , kwanini unaondoka sasa?”

“Ni stori ndefu Mr Roma ambayo nataka unipe muda wako nikuelezee ili upate kujua nia ya mimi kutaka haya maongezi na wewe”

“Nipo tayari kukusikiliza”Alijibu Roma kwa msisimko na Zenzhei alianza kumuhadhithia Roma kila kitu kuanzia namna ambavyo Zenzhei na familia yake walivyokimbia katika miliki za kijini na kuja katika ulimwengu wa kawaida , alielezea namna ambavyo baba yake mzazi na mama yake mzazi walivyopambana na wajumbe kutoka Hongmeng mpaka kuwaua , aliendelea kuelezea namna ambavyo baba yake alipambana na mtu asieonekana ambaye ndio aliyakatisha maisha ya wazazi wake mbele yake , namna ambavyo alipona , namna ambavyo alijiunga na kundi la kininja la Yamaguchi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa The Doni.(Rejea episode ya 317).

Roma alishangazwa na stori nzima ya Zenzhei na sasa alielewa uwepo wa Zenzhei kwenye maisha ya Afande Kweka ni kutokana na misheni aliopewa na kundi la Yamaguchi kukaa nae karibu.

Roma alikuwa akielewa kuhusu Yamaguchi lakini kwenye maisha yake hakuwahi kulipa umuhimu kundi hilo na yote hayo ni kwasababu aliyachukulia kama makundi mengine tu ya kininja ambayo yalikuwa yakiua kwa ajili ya pesa ,lakini hakufahamu kuna zaidi ya hayo.

“Kwahio kundi la Yamaguchi hawakuweza kukufahamu kama unatokea Hongmeng?”

“Hawakuweza kunifahamu mpaka baadae sana nilipowakatalia misheni ya kumuua Cammilius”

“Ushawahi pewa mishenni ya kumuua Afande Kweka?”

“Ndio lakini sikutekeleza agizo, Camillius nilifahamiana nae kwa muda mrefu tokea mke wake akiwa hai na amenisaidia kwenye mambo mengi ambayo yalinigusa moja kwa moja na kwangu nilimchukulia kama ndugu,nilipomuelezea ukweli juu ya kwanini nipo kwenye maisha yake hakukasirika na aliniacha nifanye chaguzi mimi mwenyewe kumchagua yeye au kundi na mamuzi nilioyafanya ni kumchangua yeye na ndio nilipokuja kuwa mlinzi wake mpaka leo hii”

“Nikupe pole kwa yaliokukuta , lakini bado sijapata jibu la moja kwa moja umeishi miaka mingi ndani ya Tanzania na Hongmeng hawajakusumbua , kwanini sasa hivi?”Aliuliza Roma , alishangaa kwani ni kweli Zenzhei alikuwa kwenye levo ya Nafsi na kwa sheria za Hongmeng hakutakiwa kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida , lakini ajabu ameshaishi miaka mingi sana bila ya kurudishwa.

“Wazee wa Hongmeng hawakufahamu uwepo wangu duniani , walifahamu nimekwisha kufariki miaka mingi iliopita”.

“Lakini mara ya mwisho ulisema ulikuwa na mawasiliano na Hongmeng”

“Ambao wanafahamu uwepo wangu hawakuuweka wazi kwa Wazee wa Hongmeng , ndio maana nikasema Wazee hawakufahamu uwepo wangu duniani”

“Kama ni hivyo naweza kutafsiri ulikuwa na mawasiliano na wajumbe wa Hongmeng pekee na walificha uwepo wako lakini ukawa unaendelea na mawasiliano nao kama ni hivyo naamini kuna sababu wakaamua kuficha uwepo wako”Aliongea Roma.

“Upo sahihi kuna sababu kubwa ya kuficha siri ya uwepo wangu duniani na ni kutokana na ahadi ya faida”

“Ahadi ya faida?”

“Ndio Mr Roma unaweza kusema niliwaahidi kitu chenye faida ili waendelee kunifichia siri ya uwepo wangu hapa Tanzania”

“Kama ni hivyo kwanini sasa hivi wanataka urudi?”

“Kwasababu ahadi sijaitimiza na siwezi kutimiza kutokana na nia yangu ya kulipiza kisasi kwa kile kilichowatokea wazazi wangu, kutokana na kutotimiza ahadi walinitishia mara nyingi kwenda kutoa taarifa kwa Wazee , lakini nilijitahidi kuwa mjanja kwa kuwasubirisha kwa maneno nikisubiria ujio wako”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa ujio wake tena.

“Unamaanisha nini kusubiria ujio wangu?”Aliongea Roma na Zenzhei alitabasamu.

“Kwasababu kuna mtu nilikutana nae miaka iliopita na akaniomba msaada na kisha akaniambia ikiwa ni muda sahihi rudia haya maneno ‘ Damu na Giza ni laana’”Aliongea Zenzei nakumfanya Roma kutoa macho.

“Ulishawahi kukutana na mtangulizi wangu?”Aliuliza Roma akiwa haamini Zenzhei anafahamu hayo maneno kwasababu yalikuwa ni maneno ambayo ni fumbo.

Mara ya mwisho Roma kuongea na Hades wa zamani alimwambia maneno hayo ya fumbo na kumpa maelekezo mtu yoyote ambaye angeyatamka mbele yake anapaswa kumsaidia.

“Mr Roma kukujibu swali , nitasema ndio nilikutana nae mara moja tu na aliniomba msaada wa kumtambua mwalimu”Aliongea na kumfanya Roma kuzidi kujawa na shauku na mshangao kwa wakati mmoja na Zenzhei alijua Roma hakumuelewa hivyo akamwelezea kwa kirefu.

Kwa maelezo ya Zenzhei ni kwamba Hades wa zamani alimuomba msaada wa kumtajia mwalimu ambaye anaweza kufundisha binadamu mbinu za uvunaji wa nishati ya mbingu na ardhi kwa njia ndefu yaani ile ya Maandiko ya urejesho isio na kikomo ambayo ndio hio aliojifunza Roma na mtu ambaye alimtajia ni Tang Chi yaani master wake Roma.

Kwa lugha nyepesi Zenzhei alimpendekeza Tang Chi kwa Hades wa zamanni na Tang Chi akaja kuwa Master wa Roma.

Roma alishangazwa na ufunuo huo wa mambo lakini bado ilimchanganya kwani kwa namna ambavyo alikutana na Tang Chi ilikuwa ni kabla alipokutana na Hades wa zamani , kuna kitu kilimwambia huenda Master Tang Chi aliagizwa na Hades wa zamani kumfundisha yeye mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

Roma alijikuta akikumbuka namna ambavyo alikutana na Master Tang Chi ilikuwa ngumu sana kuamini alikuwa ameagizwa na mtu.

“Mr Roma najua mtangulizi wako hajakuambia mambo mengi na mimi pia sio jukumu langu kukuambia yale ambayo hajakuambia kwani hata hivyo siyajui , nilimpendekeza Tang Chi kwasababu ndio binadamu pekee ambaye nilimfahamu kwa mara ya kwanza kujifunza tamaduni za jamii zisizoonekana na tokea nilipomsaidia hatukuwahi kuonana tena , lakini aliniambia msaada niliompatia ukizaa matunda basi nitayashuhudia kwa macho yangu na ndio ninapaswa kutamka maneno ya Damu na Giza ni laana”Aliongea Zenzhei na kumfanya Roma kukuna kichwa , ni kweli hakuwa akijua mambo mengi kuhusu Hades wa zamani na ilikuwa sawa kutokumuelewa, kwanza mtu mwenyewe aliishi miaka mingi hivyo huenda alikuwa na mipango mingi, Roma alifikiria na alijikuta akivuta pumzi.

“Kama ni hivyo nadhani unapaswa kuniambia shida yako na mimi nitakusaidia”Aliongea Roma na kumfanya Zenzhei kuvuta pumzi.

“Ninarudi Hongmeng kwasababu nahitajika kurudi , lakini naenda kukusubiria, mpaka sasa Mr Roma umekuwa adui namba moja wa Hongmeng na muda na saa yoyote watatoka huko walipo na kuja kukushambulia kabla ya muda huo kufika unapaswa kuwa wa kwanza kuchukua hatua”

“Unamaanisha niende Hongmeng na kupigana nao?”

“Ndio njia pekeee ya wewe kuwa salama na watu wako unaowapenda , mbinu uliojifunza ni hatari zaidi na hakuna mtu wa hongmeng yoyote ambaye amefanikisha kufikia leo ya Kuzaliwa upya”

“Lakini kama nitakuja kupambana Hongmeng watanizidi kwa uwezo wangu niliokuwa nao huu na isitoshe taarifa zinaonyesha ni wengi ambao wameshavuka levo ya Dhiki”

“Kuhusu uwezo wako sina wasiwasi umeweza kufikia levo ya kuipita Dhiki ndani ya umri mdogo sana hivyo natarajia utaenda juu zaidi ndani ya muda mfupi sana , nimekuambia nimevunja ahadi ndio maana Wazee wakagundua uwepo wangu duniani basi kile nilichoahidi nitakupatia wewe”Aliongea.

“Unamaanisha?”

“Mr Roma haikuwa bahati mbaya familia yangu kushambuliwa ni kwasababu ukoo wetu ulimiliki kitu cha thamani sana ambacho Baba na Mama hawakuwa tayari kukiweka wazi”Aliongea na kisha akampatia Roma karatasi.

“Hio karatasi imejaa taarifa ambayo ndio inanifanya nirudi Hongmeng, ndio urithi wa pekee kutoka kwa familia yangu nilioutunza kwa muda mrefu, nakupatia wewe kwasababu ni mtu sahihi wa kuwa nao”Aliongea na kumfanya Roma aifungue ile karatasi na alijikuta akishangaa baada ya kuona ni kanuni ya utengenezaji wa vidonge vya kusaidia mafunzo ya kuvuna nishati ya mbingu na Ardhi.

“Hii ni kanuni ya kutengenezea vidonge vya Poya?”

“Inaonekana ushalifahamu tayari jina lake , jibu ni ndio kama utaweza kufanikisha kutengeneza hivyo vidonge itakuwa rahisi kwako kupanda levo ya juu zaidi na hakuna kiumbe chochote kutoka Hongmeng kitakuwa tishio kwako”Aliongea na kumfanya Roma macho yake kuchanua kwa furaha na kupitia kwa haraka ile katatasi.

“Kwanini hukutengeneza hivi Vidonge wewe na kukuwezesha kupanda levo za juu zaidi na kulipiza kisasi?”

“Mr Roma nimekupatia kanuni tu , uwezekano wa kukamilisha utengenezwaji wa hivyo vidonge haitokuja kuwa rahisi na haikuwa rahisi wangu pia kutengeneza nikiwa hapa duniani na sitoweza kutengeneza nikiwa Hongmeng wewe pekee ndio naamini unaweza kukamilisha”Katika siku ambayo Roma alipata kitu cha thamani basi ni siku hio, hakuamini Zenzhei alikuwa na material muhimu na hamwambii mpaka wakati anaondoka , huenda angemsaidia hata kutafsiri kanuni hio.























SEHEMU YA 490.

Abu Dhabi- UAE.

Ni baada ya mwezi mmoja tokea waanze uchunguzi wa kile ambacho alifanya Chriss , kitendo cha kutaka kumuua Edna, waliamini kabisa majaribio ya kuuwawa kwa Edna ni nje ya malengo ya jumuia yao hio ya siri na ndio maana walitaka kuufahamu ukweli , kwanini Chriss kafanya maamuzi alioyafanya.

Uchunguzi ulikamilika mara baada ya Nadia Alfonso kumuhoji Roma na kupata majibu ya kile kilichotokea na pia kumuhoji Suzzane kwa kile ambacho kilitokea na baada ya kupata maelezo yao na kuona yanafanana waliendelea na uchunguzi wa kutaka kujua zaidi kuhusu Chriss aliishi wapi mara baada ya kuokolewa na Hades wa zamani gerezani katika mikono ya CIA.

Naam sasa ilikuwa ni siku ya ijumaa mara baada ya swala ya mchana muda wa saa tisa katika moja ya makazi ya Tajiri Khalifa ndani ya Abu Dhabi kulikuwa na kikao cha siri sana ambacho kilikuwa kikiendelea.

Ni kikao ambacho hakikuhusisha watu wengi sana ,waliohudhuria ndio mhimili wa umoja huo wa siri ufahamikao kwa jina la Ant Illuminat.

“Mmefikia katika hitimisho?”Aliuliza mwanaume mmoja alievalia kilemba kichwani na kanzu.

“Ndio Shekhe”Alijibu kijana alievalia suti huku akiwa ameshikilia kishikwambi mkonnoni na jibu lake liliwafanya watu sita walioketi kwenye meza ya pembe nne wamwangalie kwa shauku ya kutaka kumsikiliza.

“Unaweza kuendelea”Aliongea mwanaume mwingine alievalia suti na miwani , alikuwa ni mzee ambaye umri wake ulionyesha kuwa mkubwa kutokana na nywele zake kuwa nyeupe.

“Nadia Alfonso alifanikisha kufanya mahojiano na Roma Ramoni juu ya kile kilichotokea na ameweza kutupatia majibu yaliorahisisha uchunguzi”Aliongea na kisha akafanya ‘casting’ ya kishikwambi chake na Screen ya TV ya nch 85 ya kampuni ya Sumsung na palepale ilionekana picha ya ua.

“Mnachokiona kwenye Screen ni ua adimu linalofahamika kwa jina la Blue Ghost Orchid, kwa maelezo ya Mr Roma Ramoni kutoka Tanzania anasema kabla ya Chirss hajamshambulia CEO Edna na Miss Suzzane alitokea mwanamke na akawaokoa na baada ya Chriss kufariki mwanamke huyo aliacha zawasi ya hilo ua , Maelezo haya yanafanana na ya Bi Suzzane ambaye pia tulichukua maelezo yake”Aliongea na kisha akapozi kidogo na kuangalia kishikwambi chake na kwenda ukurasa wa pili.

“Blue Ghost Orchid ni utambuisho wa taasisi ya siri yenye makao makuu nchini Singapore lakini pia ni utambulisho rasmi wa mwanachama baada ya kupokea ua hilo kama zawadi kutoka kwa The Doni”aliongea na kuwafanya wale wazee kuangaliana.

“Kwa maelezo yako tunapaswa kuamini The Doni ndio aliemuokoa CEO Edna si ndio?”Aliuliza na kumfanya kijana yule kutingisha kichwa na kisha akaendelea.

“ Kwa maelezo ya Bi Suzzane na Mr Roma mwanamke aliemuua Chriss ni Clellia Allisanto ambaye ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa”Aliongea na kuwafanya wote kuangaliana.

“Mr Alban unatuambia kwamba aliemuokoa Edna ni Katibu mkuu wa umoja wa mataifa?”Aliuliza mzee mwingine wa kiafrika alievalia suti.

“Tumeshindwa kufikia kwenye hitimisho kutokana na kwamba hakuna namna yoyote ya kuthibitisha kama Clellia Allisanto ni The Doni”Aliongea na kuwafanya waanze kuongeleshana wao kwa wao kwa dakika kadhaa na kisha wakamgeukia.

“Vipi kuhusu Chriss, aliishi wapi mara baada ya kutolewa gerezani na kwanini alitaka kumuua Bi Edna kuna dhamira yoyote mmepata kuifahamu?”.

“Kamati yetu ya uchunguzi iliweza kupokea nyaraka iliotumwa kwetu kwa njia ya barua pepe na mtu ambaye hakujitambulisha jina na imetoa majibu ambayo tumeshindwa kuyahakiki na nitayaweka wazi”Aliongea na kisha alienda kwenye Gmail na kufungua nyaraka iliotumwa na palepale ilionekana kwenye Skrini na kuwafanya wale wazee wenye miwani kuziweka vizuri ili kusoma na wale ambao macho yao yalikuwa imara walikodoa macho.

“Nyaraka hii inaonyesha Chriss aliishi ndani ya Vatican mara baada ya kutolewa gerezani nchini Marekani na alikuwa ni mkutubi wa maktaba Chemba namba 4”Alielezea ile nyaraka na kuwafanya wale wazee kuendelea kushangaa.

“Kuna taarifa yoyote inaonyesha alikuwa na dhamira ya kutaka kumuua Bi Edna?”Aliuliza na Alban alitingisha kichwa kuashiria jibu ni ndio na kisha akapangusha kishikwambi chake na akatoa nyaraka nyingine iliotumwa kwao kama barua mfumo wa portable file(PDF).

“Hii ni barua ambayo tunaamini imeandikwa na Chriss mwenyewe kabla ya kutekeleza misheni ya kutaka kumuua Bi Edna nchini Tanzania na inaonyesha sababu kwanini alifanya maamuzi tofauti na misheni aliopatiwa.”Aliongea na palepale alianza kuisoma.

Kwa maelezo ya barua inaonyesha ni kweli Chriss alikuwa akiishi ndani ya Vatican kwa kipindi chote tokea atoroshwe kwenye gereza chini ya serikali ya kimarekani , anasema kwamba aliishi kwa Dilema ni upande upi anapaswa kuegamia kutokana na mfanano wa malengo ya dunia ijayo kati ya taasisi mbili tofauti yaani hio ya Ant-Illuminat na nyingine ambayo hakuitaja.

Anaendelea kusema maamuzi alioyafanya ni chaguzi alioifanya yeye mwenyewe na barua hio kama wataisoma basi atakuwa tayari amekwisha kufariki na misheni yake imefeli.

Mwisho kabisa anawafunulia kwamba misheni aliopewa kwa ajili ya Ant -illuminat ni kuwajuza kwamba kiongozi wanaemgojea sio yule ambaye wanamfikiria bali ni yule ambaye anapewa ulinzi na yule wanaemfikiria na ushahidi wa maneno yake upo kwenye mchoro wa unabii.

Mwisho kabisa wa barua anasema kama watakuwa wamefanikisha kupata barua yake basi misheni aliopewa na aliemuokoa imekamilika na atapumzika kwa amani akimlenga Hades wa zamani aliempatia misheni.

“Mchoro wa unabii!!??”Walijikuta wakiongea wote kwa wakati mmoja kwani hawajaelewa.

“Barua hii ni ya kweli inetokea kwake kutokana na sahihi na nadhani kabla ya kufikiria mchoto wa unabii tunapaswa kujua kauli yake: ‘yule tunaemfikiria sio mwenyewe bali yule anaelindwa na tunaemfikiria’ tuanzeni na kufumbua kauli yake”Aliongea mwanaume alievalia suti na Collar ya kiuchungaji.

“Albani kuna taarifa nyingine ambayo bado haujatupatia?”

“Hakuna Shekhe”

“Kwasasa uchunguzi wenu uhamie upande wa Clellia Allisanto ili kufahamu kama ndio The Doni, kuhusu kuthibitisha uwepo wa Chriss ndani ya Vatican tutatumia koneksheni tulizokuwa nazo”Aliongea Shekh na Albani alitingisha kichwa kukubali.

“Unaweza kwenda kwasasa , tunapaswa akujadili”Aliongea na kisha Albani aliondoka , haikueleweka alikuwa akitokea kitengo gani ndani ya taasisi hio ya Ant-illuminat lakini ni dhahiri ni sehemu ya kamati ya uchunguzi ilioutwa kutafiti kifo cha Chriss.

“Pastor Cohen nini maoni yako?”Aliuliza Shekhe na kumfanya mzee alievalia suti na kuwa na kipara cha nywele nyeupe kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Mpaka kufikia leo hii ni mengi ambayo yamefanyika na tumejipanua sana ndani ya mabara karibia yote na tuna washirika wengi wa kutuunga mkono kupambana na uovu , lakini licha ya mapambano yetu hatukuwa na kiongozi na wote tunajua tarehe 24 ya mwezi wa nne kwa mujibu wa Kalenda ndio siku ya kumtambua kiongozi wetu , nadhani alichoongea Chriss tunapaswa kukifiria mara mbili ili kupata majawabu lakini pia kuihakikisha kauli yake”Aliongea Paster Cohen kwa lugha ya kingereza.

“Naungana na Pastor Cohen ,nadhani ni wakati sahihi kwanza kuchambua kile alichoandika kwenye barua yake ili tufanye reasoning”Aliongea mwingine.

“Tunaefikiria siku zote kama kiongozi wetu ajae ni mrithi wa Hades ambaye ni Mr Roma Ramoni lakini kama sio yeye kwa kauli ya Chriss je anaemlinda ni nani?”

“Nadhani kujibu swali hilo kwa wepesi ni sisi kujiuliza ni nani wa muhimu kwenye maisha ya Hades mpya?”

“Mke wake ndio muhimu zaidi”

“Upo sahihi Shekhe Assad, nadhani hili pia linatoa majawabu ya kauli ya Chriss kuwa katika Dilema”Aliongea mwingine .

“Kwa haraka haraka inaonyesha Chriss hakuwa akifanya kazi tu kama mkutubi ndani ya Vatican , huenda kuna watu aliokutana nao na kujenga nao mahusiano ambayo yamempelekea kwenye dilema na huenda dilema aliokuwa nayo ni katika kuchagua upande aidha wa kwetu au wa kwao na ni sahihi pia kuamini huenda ndio wamemuonyesha kitu alichokiita mchoro wa unabii”

“Unafikiri huo mchoro wa unabii unahusiana na Edna?”

“Kama Bi Edna anapaswa kuwa kiongozi wa umoja wetu ambaye amechaguliwa na Hades wa zamani nadhani kuna uwezekano mchoro huo wa unabii unamzungumzia na ndio maana Chriss akachagua kutaka kumuua kwa kuagizwa na upande mwingine”

“Lakini kama mchoto unamzungumzia Edna kuwa kiongozi wetu kwanini na The Doni akamuokoa?”.

“Hili ni fumbo gumu , lakini naamini majibu yake tunayo wenyewe”

“Unamaanisha nini Paster Cohen?”

“Wote tunajua namna ambavyo Hades wa zamani alivyomuhusisha Seventeen kwenye mpango LADO, mnafikiri ilikuwa bahati mbaya , Seventeen na Edna ni mapacha tena wa kufanana kabisa na mpaka sasa hatujui Seventeen yuko wapi na tukumbuke yeye ni mwanachama wa ant-illuminat na ndio ambaye alimwingiza Zoe Kovac kwenye uanachama na haikuwa hivyo tu, Seventeen alikuwa na madaraka ya kuchagua mwanachama mpya wa ‘first echelon’ cheo ambacho ni kikubwa katika jumuia yetu na ni madaraka makubwa”

“Lakini wote tunaamini kiongozi wetu amekabidhiwa muhuli na Hades wa zamani , si ndio ulivyosema Shekh Assad namna ya kumtambua?”

“Uko sahihi kwa maelezo ya Hades wa zamani tutamtambua kiongozi kwa kutuonyesha pete ya muhuri(signet ring)?”

“Basi nadhaini hilo ni jibu la hiki tunachojadiliana hapa, kama maneno ya Chriss yapo sahihi na Hades mpya sio mwenye umiliki wa pete yenye muhuri basi mke wake Edna atakuwa nao”

“Upo sahihi ndugu Khalifa , lakini kalenda yetu inatupa muda mchache sana wa kutambua nani mmiliki wa pete hio ya muhuri wa uongozi , kalenda yetu inaonyesha tarehe 24 mwezi wa nne ndio siku ambayo tunapaswa kumtambua kiongozi”Aliongea na kuwafanya watu wote kuingia kwenye mawazo na waliona ana point.

“Nadhani kuna namna moja tu ya kuthibitisha maneno ya Chriss ni ya kweli au ya uongo?”Aliongea Shekhe Assad.

“Unataka kusema nini?”

“Tarehe ishirini na nne ndio siku katika kalenda yetu ya kumtambua kiongozi wetu na Chriss katuachia tayari fumbo na wote tunafahamu mtu muhimu katika maisha ya Hades mpya ni Edna mke wake , nadhani hili ni jibu tosha kwetu, Kama Edna kweli ni kiongozi wetu basi lazima atakuwa na pete ya muhuri wa uongozi na siku hio anapaswa kutuonyesha”Aliongea na kufanya chumba kukaa kimya.

“Wajumbe mnasemaje juu ya wazo la Shekhe Assad?”

“Kama kweli fumbo la Chriss linamuonyesha Edna ndio kiongozi wetu basi lazima atakuwa na muhuri wa uongozi”Alirudia mwingine kauli ileile ya Shekhe Assad.

“Na kama hatokuwa na pete ya muhuri basi tutatambua moja kwa moja yeye sio mlengwa na sio kiongozi wetu na fumbo la Chriss sio sahihi”Aliongea na wote walikubaliana na wazo lake.

“Kama ni hivyo tunafanikishaje kumfanya atuonyeshe pete hio?”Aliuliza Tajiri Khalifa.

“Tunatakiwa kumfanya atuonyeshe na ili hilo lifanikiwe lazima tuwe na mpango, Miss Edna anaweza kuwa na muhuri lakini hana ufahamu wowote kuhusu jumuiya yetu”

“Naunga mkono hoja na matukio mengi yanaonyesha ndio kiongozi wetu na wote hatujui hapa huenda Hades mpya amemkabidhi Edna pete hio kwa maelekezo ya Hades wa zamani”

“Ni kweli kabisa hakuna ambaye anajua nini Hades wa Zamani na Hades mpya waliongea wakati wakukabidhiana urithi , huenda alimwagiza Edna apatiwe muhuli na yeye ndio anaepaswa kumlinda”

“Mimi nina mawazo tofauti , kwa maelezo ya Hades wa Zamani hajamwambia Hades mpya kitu chochote kuhusu Ant illuminat na ameseme yeye mwenyewe angefahamu kitu kimoja kimoja kadri ya muda unavyosonga,tutaomba CEO Edna atuonyeshe muhuri wa uongozi kama kweli anao lakini tusiende na wazo la kuamini kwamba Hades mpya kampatia pete hio ya muhuri wa uongozi, nadhani mpaka sasa tunaelewa kwamba Hades hajamwambia mkewe chochote kuhusu Seventeen kuwa ni pacha wake , unafikiri ingekuwa rahisi kwake kumpatia Muhuri”Aliongea Shekhe na maneno yake yalionekana kuwa na mantiki.

Makubaliano ni tarehe ishirini na nne mwezi wa nne kuonana na Edna ili aonyeshe pete ya muhuri wa uongozi wa jumuia hio ya ant-illuminat.

Naam Edna kukutana na jopo la watu hao kwa kisingizio cha kuonana na Tajiri Khalifa ilikuwa ni mbinu tu, lakini vipi kuhusu hio pete.

ITAENDELEA --- WATASAPP 0687151346 ULIZIA MWENDELEZO
 
Back
Top Bottom