SEHEMU YA 487.
Baada ya dakika kama tano kupita gari iliokuwa katikati ilifunguliwa na alitoka mwanaume mweusi alievalia miwani na kusogela mlango wa siti ya abiria na kisha akafungua mlango na Raisi Jreremy aliweza kutoka na kukanyaga ardhi na kugeuza macho yake mbele na hapo ndipo alipomuona Edna akiwa amesimama na Roma wanamwangalia.
Raisi Jeremy kabla hajapiga hatua kusogea mbele alimpa ishara msaidizi wake kumsogelea na kisha aliteta nae jambo na akaitikia kwa ishara na kisha alipiga hatua kusogelea mbele.
Alikuwa ashaanza kuzeeka kwani nywele zake zilikuwa na mvi , lakini licha ya hayo bado alionekana kuwa na afya nzuri.
Haikueleweka kwanini akafanya safari ya dharula mpaka kuja ndani ya hilo eneo kwani ni hakika sherehe ya Fredi haikuwa ikimuhusu.
Macho yake yalififia mara baada ya kugundua Edna alikuwa akiangalia upande mwingine kama vile hakuwa akimtambua na baada ya kuwafikia alisimama.
“Edn…CEO Edna”Aligwaya kwa kutaka kutaja jina la Edna lakini akabadilisha na kutaja jina la CEO.
Wageni ambao walikuwa wamealikwa kwenye sherehe hio walikuwa na shauku ya kujua nini kinaendelea , baadhi yao walikuwa wakimfahamu Raisi Jeremy hivyo mara baada ya kumuona walishangaa kwani ujio wake haukutegemewa , lakini ni kwamba wasichokijua kabla ya ujio wa raisi huyo hapo Maple speed Resort kuna baaadhi ya wanausalama walikwisha kufika mapema kuimaliza protakali za ki ulinzi..
Wengi walishangazwa kuona Raisi Jeremy amesimama mbele ya Roma na Edna, walijua Edna alikuwa mfanyabiashara lakini haiwezekani kama mheshimiwa kaja mahali hapo kwa ajili yake na moja kwa moja waliamini itakuwa ni Desmond mtoto wake.
“Mr President can I help you ?”Aliongea Roma akimaanisha kuna kitu anataka amsaidie huku akionyesha kutopenda kabisa kuongea nae.
“Hongera kwa kuweza kurudi katika familia yako baada ya kupotea kwa muda mrefu , naamini kutokana na baba yako kuwa kiongozi mkubwa wa nchi tutapata nafasi ya kuonana mara kwa mara”.
“Acha kujikweza , mtu kama wewe huwezi kukutana na mimi”Aliongea Roma na kauli yake iliwafanya wanausalama kumwangalia kwa macho ya tahadhari, maana hawajawahi kuona mtu wa kawaida kuongea na raisi vile anavyotaka hata kama sio raisi wa Tanzania walijiambia anapaswa kuheshimiwa.
“Ineonyesha ukoo umepata mrithi mwenye uwezo mkubwa na kujiamini, nimefahamiana na baba yako kwa kipindi kirefu sana na urafiki wangu na yeye ulianza kwasababu yako , lakini mara baada ya kurudi kwako , kila ninapomuuliza kuhusu bahari zako hataki kabisa kunipa majibu ya moja kwa moja”.
“Sijui unaemzungumzia, Mr President nipo hapa na mke wangu kwa ajili ya kushiriki party lakini imeharibika hivyo tunaondoka kama huna lingine la kuongea”Aliongea Roma na kisha akamshika mkono kumuashiria waondoke..
“Subirini kwanza msiondoke”Sauti ya Desmond kutoka nyuma ilisikika na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia , awamu hii alionyesha ile hofu aliokuwa kwenye macho yake imekwisha kumpotea na sasa alikuwa akijiamini ,alikuwa ameshikilia glasi ya mvinyo huku akiwa ameachia tabasamu.
“Nyie wote ni wageni wa heshima ambao mmealikwa kwenye hii sherehe , kwanini ya kuondoka mapema, isitoshe mtu muhimu mheshimiwa yupo hapa nadhani ni fursa pia kwenu”Aliongea Desmond kana kwamba sherehe hio ilikuwa ya kwake.
Raisi Jeremy macho yake yote yalikuwa kwa Desmond , ni kama alikuwa akichunguza kitu flani lakini alishindwa kukiona.
Roma alishindwa kufanya maamuzi na kumwangalia Edna , hata hivyo aliekuwa mbele ni baba yake hivyo alitaka ampe nafasi ya kuamua kubaki au kuondoka , upande wa Edna hakuwa akijiamini kukaa mbele ya mwanaume anaefahamika kama baba yake ambaye hataki hata kumtambua na ni zaidi ya miezi minne alikuwa akijaribu kutuma nyumbe za barua pepe.
“Edna my young sister nadhanni baba kafika hapa kwa haraka kwasababu yako , sidhani unapaswa kuondoka bila ya kuongea nae kwani mnakutana mara moja kwa mwaka”Al;iongea Desmond na kuufanya moyo wa Edna kupiga kite kwani hakutegemea Desmond kuropoka.Roma ilibidi amshikilie mkono mara baada ya kuona Edna anatetemeka.
“Desmond unaongea ujinga gani?”Alifoka Raisi Jeremy huku akianza kubadilika sura lakini na Desmond na yeye alianza kubadilika vilevile.
“Unashangaa nini baba kutotoboa siri yako ulioficha kwa muda mrefu?”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kwanza kuangalia mazingira japo watu walikuwa mbeli na waliposimama , lakini alijua kama angegombana na mtoto wake mbele ya watu ingempunguzia heshima yake kama kiongozi na wasaidizi wake waliona hilo na haraka sana walianza kutawanyisha watu.
“Unapata wapi ujasiri wa kuongea ki mitego mitego mbele yangu?”.
“Usingefika hapa kama hukutaka ukweli ujulikane,baba nilichoongea ni kweli Edna ni mtoto wako na kama naongopa kanusha akiwa mbele yake”
“Kimya …!”Aliongea kwa hasira na muda huo huo alimwita bodygurad wake na kumpa maelekezo ya kughairisha shughuli zote zinazoendelea hapo na kila mmoja atawanyike na swala lile lilifanyika kwa haraka sana , kwani ndani ya dakika chache watu wote washapanda magari na kuondoka na wakabakia wanafamilia.
“Desmond kilichonileta hapa nikutaka kujua kama yule mwanamke ushakutana nae tayari?”Aliongea .
“Mwanamke gani?”
“Mama yako?”
“Haha.. mama ashakufa tayari , Baba huwezi ukaongea hivyo wakati uliongoza raia kuomboleza kifo chake”Aliongea Desmond na hapa ilionyesha kabisa Raisi Jeremy alishakutana na Kizwe.
“Acha kunipotezea muda wewe mtoto , kama hamjaonana usingeongea ujinga wako , ndio sababu moja tu ilionileta hapa la sivyo nisingepoteza muda wangu”Aliongea huku akionyesha kuwa na hasira mno.
“Baba kwanini unaongea kwa hasira namna hio , nadhani uwepo wa mama kwenye maisha yetu ni jambo la kufurahia”
“Unajua nini wewe,nijibu swali langu Kizwe yupo wapi?”
“Baba sijui unachoniuliza ni nini , na laiti ningejua kuhusu kilichomtokea mama yangu nisingepoteza machozi yangu namna ile na nisingeumia moyo wangu kwasababu ya Edna , ndio maana ulikuwa mkali sana kutotaka ni mguse kumbe alikuwa ni mtoto wako wa nje ya ndoa na ulivyoona mama anataka kumfilisi ukaamua kupanga njama za kumuua”
“Wewe mtoto nimekuambia kaa kimya?”Alifoka.
“Kwani nakosea? , haishangazi ndio maana ulinipiga vibao bila ya kunijali , siku zote tumeishi pamoja , mama alikujali sana na kuwa msaidizi wako lakini kwasababu ya mtoto wa nje ya ndoa ukafanya maamuzi ya kumuua”Aliongea huku akitoa tabasamu la hasira.
“Kama kweli ulikuwa ukimjali kwanini hukuwahi kumtambua? Au ulikuwa ukiogopa watu kukunyooshea vidole ,haijalishi wewe ni raisi lakini ni binadamu vilevile haikuwa na haja ya kukaa kimya, unajua najisikiaje baada ya kugundua mwanamke niliekuwa nikimtamani ni mdogo wangu ?”
SLAP!
“Unanipiga tena?, kwanini usiniue tu na ukamalizana na mimi pia moja kwa moja , hata hivyo tayari ushapata mrithi wako”Aliongea huku akionekana kama mtoto mdogo mwenye wivu , kwa umri wake huenda hakupaswa kuwa kama hivyo.
Roma hakutaka kumvumilia Desmond na palepale alimpiga teke na kumfanya adondoke kama furushi, kitendo kile kiliwafanya walinzi kutoa siraha zao haraka na kumnyooshea Roma ,sio kwamba hawakumfahamu Roma alivyo ilikuwa mara ya pili kukutana nae na akafanya vitendo vya hatari kwa mheshimiwa hivyo muda huo walikuwa makini sana na yeye
“Roma usimpige tena”Aliamrisha Raisi Jeremy mara baada ya Roma kutaka kumuongezea lingine.
“Unajua maana ya kupiga , sijampiga bali nimemsukuma tu”Aliongea Roma na kumfanya Jeremy amwangalie kwa macho makali.
“Roma tuondoke”Aliongea Edna kwa kubembeleza alikuwa ashaanza kutokwa na machozi na kumshika mkono Roma na hakutaka kumkatalia aliona ndio anaeumia zaidi.
Desmond alijilazimisha kusimama huku akiugulia maumivu akiwaangalia Roma na Edna wanavyoondoka bila waswasi.
“Raisi Jeremy , unamwachaje mtu kama yule aondoke ilihali kampiga mtoto wako wa kipekee , mrithi wako, unapaswa kuwa kweli raisi wewe kama unamuogopa kinyamkela kama yule”
“Desmond nitakupiga nikuue , kaa kimya , huoni kwamba ukimchokoza zaidi atayakatisha maisha yako”
“Aniue.. Hahaha… kabla hajaniua nitahakikisha namuonja yule malaya hata kama ni ndugu yangu wa damu”Aliongea ilionekana hata hivyo kilevi kilishamkolea ndio maana alikuwa akiongea bila ya kufikiria.
Roma aliweza kusikia lile tusi na alijikuta akisimama kabla hajafungua mlango wa gari na kuingia..
“Nadhani hupendi kuendelea kuishi , unadhani siwezi kukufanya chochote kwasababu upo mbele ya baba yako kwa kumtukana mke wangu?”Aliongea Roma huku hasira zilianza kujitengeneza kiasi kwamba hata macho yake yalitisha.
Lakini kabla hawajaelewa kinachotkea Roma alipotea aliposimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Desmond na kuinyakua shingo yake na kuing’ingiza juu Desmond alijitahidi kujinasua kwenye mkono wa Roma lakini jitihada zake zilikuwa bure , wale walinzi pia walitaka kumuokoa lakini waliogopa kushambulia kwani wangemdhuru na Desmond hivyo walimwangalia Raisi Jeremy kupata amri yake.
Ndio wakati ambao Desmond alijua sasa kifo chake kinaweza kutekelezwa muda wowote na alifanya kosa kumchokoza bila ya kufikiria mara mbili.
“Roma hapana…”
Edna alikimbia na kwenda kumshika Roma tisheti akimzuia asimuue Desmond na ilikuwa bahati kwa Desmond maana alitaka akaze mkono na kumkatisha uhai palepale.
“Usimuue , Roma nakuomba tafadhari usimuue”Aliongea Edna lakini Roma aliendelea kuminya na kumfanya kuanza kurusha miguu kulia na kushoto akionyesha dalili ya kupoteza hewa.
“Edna mwambie aache tafadhari , Desmond hayupo kwenye akili zake timamu kwasasa ndio maana kaongea ujinga na ndio mtoto wangu wa pekee na mrithi niliebakiwa nae sitaki kumpoteza pia”Aliongea na kumfanya Edna amgeukie Jeremy na kumuangalia ‘neno mtoto wangu wa pekee niliebakiwa nae’ lilijirudia mara mbili mbili.
Edna aling’ata meno yake kwa hasira na kisha akamshika mkono wa kushoto Roma.
“Mwachie aondoke”Aliongea.
“Unamaanisha nini nimuachie wakati kakutukana”Aliongea Roma huku akionyesha ishara ya kutotii ombi la Edna.
“Honey …Edna alianza kupasha viganja vya mikono huku akijaribu mbinu za kike kumlegeza.
“Hii ni mara ya mwisho nakuomba , tafadhari….sitokuomba tena naomba usimuue , akirudia tena sitokuomba tena umsamehe”Roma alijikuta akikasirika.
“Una uhakika gani hatorudia , haujamsikia alivyokutukana”Edna alijikuta akishindwa kujua cha kufanya , alimwangalia Raisi Jeremy na kuona yupo kwenye wasiwsi na ameshindwa kuchukua hatua zozote kutokana na kumhofia Roma.
“Roma kama utamuua leo hii siwezi kukusamehe maisha yangu yote”Aliongea Edna na kumfanya Edna kumwangalia kwa mshangao na hakujua hata ni muda gani ameachia mkono wake na kumruhusu Desmond kudondoka chini kama furushi.
“Edna unanitishia kisa hii taka taka , unanitishia mimi mume wako?”
“Hapana …najua nimekosea na sio fair lakini hii ni mara ya mwisho haitorjirudia”Aliongea huku akimuogopa Roma yeye mwenyewe.
“Okey sitomuua”Aliongea Roma na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi za ahueni na kuwapa ishara walinzi kushusha siraha chini na Roma baada ya kuona hivyo alimwangalia tena Desmond aliekuwa amejichanua chali mbele yake akivuta hewa na palepale alimpiga teke lingine sehemu zake za uzazi .
“Ow..!!”Hata sauti haikumtoka kutokana na maumivu alioyasikia na palepale alipoteza fahamu.
“Desmond!!”
Raisi Jeremy alikimbilia alipolala Desmond bila ya kujali tena , Alimshika mabega na kuanza kumtingisha lakini hakukuwa na majibu ya aina yoyote kutoka kwake.
Edna alijikuta akimwangalia Roma kwa mshituko bila ya kuelewa hisia zake , alijua Roma ashakubaliana na ombi lake lakini yamegeuka kuwa mengine.
“Umeomba nisimuue lakini sio kutokumuadhibu kutokana na makosa yake”Aliongea Roma na kisha akamsogelea karibu.
“Una baki au tunaondoka wote?”Aliuliza Roma kibabe na kumfanya ameze mate ya huzuni.
“Kwanini umemfanyia hivyo?”
“Unabaki au unaondoka?”Aliuliza mara nyingine. Na kumfanya Edna amwangalie Mheshimiwa Raisi Jeremy aliechuchumaa huku akiwa ameshikilia Desmond kwa huzuni , alijikuta akiumia ndani kwa ndani kwa kuona hakuna dalili ya kutambulika kama mtoto tena.
Walinzi walipisha njia wenyewe , hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kumfanya Roma chochote kutokana na kutahadharishwa na mheshimiwa mwenyewe , hivyo waliishia kumwangalia Roma na Edna wanaingia kwenye gari.
“Roma kama mwanangu akapatwa na ukilema nitakufanya jambo ambalo hutokaa usahau”Aliongea Raisi Jeremy kwa hasira lakini Roma hakumjali zaidi ya kuingia kwenye gari.
Muda huo huo na wale walinzi walimsogela Mheshimiwa na kisha wakamchukua Desmond na kumuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumuwahisha hospitalini.
Roma aliendesha gari kimya kimya , hakuwa na mudi yoyote ya kuongea na Edna alikosa amani kutokana na ukimya wake , alijua amekosea lakini asingeweza kuona Roma akimuua ndugu yake wa damu mbele yake.
“Bado una hasira na mimi?”Aliuliza.
“No”
“Unazo , Roma naomba tusahau yaliotokea leo , kwanzia leo nawasahau kwenye maisha yangu”
“Usiwazie sana , No means no”
“Unanidanganya acha kujizuia na kama ni kunifokea nifokee yaishe”Aliongea na kumfanya Roma kung’ata meno kwa hasira na kukanyaga padeli na kufanya gari lianze kunguruma kama simba huku likitembea kwa kasi kama mshale.
“Sina haja ya kukufokea , haujafanya chochote kibaya”Alijibu Roma na kumfanya Edna ashindwe kujua nini kingine cha kuongea na aliishia kukaa kimya.
Saa tatu usiku ndio muda ambao waliweza kufika na Blandina alishangaa kuona wamerudi mapema , alitarajia kurudi kwenye saa tano na namna pia Edna alivyonekana kuchafuka , lakini pia nyuso zao zilivyokosa nuru ya furaha ilimshangaza na Edna mara baada ya kusalimia nae alipandisha ngazi.
“Nini kimetokea Roma , mbona mmeondoka mkiwa vizuri na mmerudi mkiwa mmenuniana”
“Hakujatokea kitu Party haikuwa nzuri sana tumeamua kurudi”
“Mh! Naona kabisa mmegombana”Aliongea.
“Mama usiwe na wasiwasi”Aliongea Roma na kisha akapandisha juu kwenye chumba chake na alipoingia alijibwaga kwenye sofa na kuvuta pumzi nyingi huku akiwa amefumba macho.
Zilipita kama nusu saa tu mlango ulifunguliwa na Edna aliingia huku akiwa ashabadili mavazi na kuvaa ya kulalia kitambaa cha hariri , baada ya kumuona Roma amelala kwenye sofa akiwa gizani alijihisi kuumia na kuona huenda alichokifanya kimemkwaza sana .Alitembea taratibu na kwenda kusimama pembeni yake na Roma alifumbua macho na kumwangalia na kisha akayafumba tena.
“Hubby nimekuandalia chakula tayari nikuletee hapa hapa au unashuka tukale wote?”Aliongea Edna huku akijaribu kulegeza sauti awezavyo lakini Roma hakujibu kitu.
“Au unataka kuoga kwanza nitapasha maji yako moto yawe ya uvuguvugu na yatakuweka sawa”
“Huna haja ya kunifurahisha ki makusudi”
“Sio hivy… Sifanyi kimakusudi ni kwasababu napaswa kufanya hivi kama mkeo”Aliongea na kumfanya Roma asimame.
“Ulitakiwa kuniacha nimmalize Desmond moja kwa moja kwanini ukanitishia kutokunisamhehe kwasababu ya yule mpuuzi?”
“Bado una hasira na mimi?”
“Kwannii niwe na hasira na wewe , hasira ni juu yangu mwenyewe najilaumu kwanini nimemuachia kwa kukusikiliza wewe , nishawahi kumsamehe mara ya kwanzo na akarudia na nina uhakika atarudia tena , ulichofanya leo kitakuingiza kwenye matatizo baadae, Sijui kwanini nnimekuwa mjinga na kukusikiliza”Aliongea Roma na kisha akavua tisheti na suruali bila ya kumjali Edna aliesimama na aliingia bafuni na kubamiza mlango kwa nguvu.
Edna alisimama palepale akiwa hajui cha kufanya maana alimuona Roma kuwa mwenye hasira na alijikuta machozi yakianza kujitengeneza.
Roma mara baada ya kuingia bafuni alivua bukta yake na kisha akafungulia bomba la mvua(Shower) na kuacha maji ya mloanishe huku akiwa amefumba macho na kufanya kifua chake kilichojengeka kimazoezi kupanda na kushuka akijitahidi kutuliza hasira zake.
Lakini mlango wa bafuni ulisukumwa na Edna na kumfanya ageuke na kumwangalia.
“Unafanya nini?”Aliuliza Roma kwani alijua Edna hajawahi kufanya kitu kama hicho kwenye maisha yake.
“Kwanini unanifanyia hivyo Roma?”
“Unamaanisha nini?”
“Nimekuomba na kukuomba na nimejitahidi kukujali ili unisamehe , kwanini unashindwa kuacha hili lipite”
“Tutaongea nikimaliza kuoga”
“Hapana..!!, umenisaliti mara kibao lakini mwisho wa siku niliishia kukusamehe , kwanini mimi unanikatili wakati nishakuomba msamaha?”
“Edna nilichotaka kufanya ni kwa ajili yako , kwanini huelewei , Desmond hawezi kubadilika na Jeremy umeshuhudia mwenyewe hana mpango hata wa kukutambua”
“Ndio maana nimesema ni mara ya mwisho , kwanini hunielewi?“Aliongea Edna bila kujali maji ya bomba yanamloanisha.
“Una baba na kaka ambao wewe huwatambui na wao hawakutambui lakini huwezi kupotezea uwepo wao kwenye maisha yako , kwa mfano Denisi ni mara ngapi uliweza kumsamehe na kumuachia , je kama ni mtu mwingine aliekuchokoza ungemwachia na kuondoka?”
“Kwanini nipotezee kila kitu najua hakuna anaenihitaji na Desmond kanikosea lakini kwanini unaona ni kosa kwangu kuwaachia waondoke kwa mara ya mwisho?, ila sawa tu fanya utakavyo mimi ndio ambaye napaswa kukusamehe kila mara unaponisaliti , sawa usinisamehe na mimi nitakusamehe kila unaponikosea”Aliongea na kisha kihasira aligeuka lakini alijikuta akikanyaga sabuni na kuteleza lakini kabla hajatua chini Roma aliwahi kumdaka na maji ndio yalimloanisha kisawa sawa na kufanya nguo kugandia mwili wake.
Roma alimwangalia usoni huku akiwa amebadilika na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
“Unanicheka ?”Aliongea huku akijitahidi kuangalia pembeni akionyesha hajaathirika maana Roma hana nguo.
“Nafikiri ishaongezeka na kuwa kubwa,,”Aliongea na kumfanya Edna kuona aibu za kike,lakini Roma hakuwa na namna ya kumuachia kwa muda kama huo.
Na kilichoendelea kilianzia bafuni huko huko na kuhamia chumbani na ni vilio tu vilivyosambaa kila kona.
Upande mwingine wakati Roma akifurahia uanaume wake kwa kumlaza mke wake mrembo Edna kunako sita kwa sita ndani ya hospitali ya Aghakhan ilikuwa taarifa mbaya kwa raisi Jeremy.
“Mr President we tried our best but we cannot recover his reproductive organs , it has been damaged both internally and externally beyond repair”
“Mheshimiwa tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini hatuwezi kurudisha tena mfumo wa ogani zake za uzazi , zimeharibika nje ndani kiasi cha kutotibika tena”Aliongea dokta kihindi
Ilikuwa taarifa mbaya kupokea huenda katika maisha yake yote , Desmond ndio mtoto wake wa pekee wa kiume ambaye alitarajia kuendeleza kizazi chake , anapokeaje taarifa ya kwamba hawezi tena kuwa mwanaume aliekamilika.
Baada ya kusharabu kauli ya daktari alijiambie hapana , lazima kuwe na namna ya kumuokoa mtoto wake kwa namna yoyote ile.
“Have our medical staff come over to take care him and you prepare plane we are going back”Aliongea akimaanisha kwamba watu wao wa afya waje kumuangalia mgonjwa na mwingine aandae ndege kwani wanarudi Rwanda.
SEHEMU YA 488.
MWEZI MMOJA NYUMA KIGALI.
Ilikuwa ni mtanange wa kibabe kati ya Kizwe na Lekcha , ijapokuwa aliwahi kufunga goli la kwanza kutokana na ukame wa muda mrefu aliokuwa nao , lakini mzunguko wa pili ulidumu kwa muda mrefu.
Huenda mwanafunzi yoyote wa chuo ambaye angesogelea ofisni ya mkufunzi wa fiizikia angesikia kwa nje kile kichokuwa kikiendelea ndani kwani Kizwe alionyesha kutoweza kuhimili hisia na kupiga makelele huku akitaja jina la Kilema.
Baada kama ya nusu saa Lekcha miguu ilimtetema na ilikuwa ni muda ambayo alikuwa akikamilisha mzunguko na alijitupa pembeni huku akihema kama mbwa baada ya kuwashusha wote.
“Kilema wangu , umeimarika sana kwa siku zote ambazo hatukuonana”aliongea.
“Niite Lekcha sio kilema”Aliongea
“Hapana ‘kilema’ ni jina ambalo limekaa kimahaba mpenzi , naomba usinizuie kukuita hivyo kuanzia leo”Aliongea na kumfanya Lekcha kutabasamu kifedhuli, tokea aanze kupata ufadhili kutoka kwa raisi wa taifa la Rwanda maisha yake yalikuwa mazuri na hata ule ukilema ulipotea mbele za macho ya watu kutokana na kupata matibabu mazuri ya viwango.
Hakupenda jina la Kilema kwani lilimkumbusha maisha yake ya nyuma , lakini Kizwe tokea wanaanza mchezo ameng’ang’ania kutaja jina la Kilema mwanzo mwisho, lakini kwa muda huo hakuona shida , alijiambia labda ni kwasababu ndio namna inavyomfanya kupandwa na hisia zaidi.
“Such a bitch”Aliwaza Lekcha kwenye akili yake , ijapokuwa ndio mara yake ya kwanza kukutana na Kizwe mara baada ya kushuhudia kifo chake , lakini ujio wake haukumfurahisha na sio kwamba alikuwa akimpenda.
“Umekuwa mrembo sana Kizwe”Aliongea Lekcha na kumfanya Kizwe kumsogelea na kumkumbatia.
“Nimerudi kwako kwasababu najua ni wewe pekee unaenipenda kwa mapenzi ya dhati”
“Mtu kama mimi mwenye ukilema , unaamini vipi nakupenda?”
“Haijalishi ilimradi nauona upendo wako juu yangu ni wa dhati hilo ndio la muhimu”Aliongea na kumfanya Lekcha kutabasamu.
“Niambie nini kimetokea mpaka ukawa hai na kuwa na mwonekano wa kitoto kama huu huenda na mimi ninaweza kuponyesha huu mguu”.
“Unamaanisha unataka kua kama mimi?”
“Sio kuwa kama wewe nataka kujua nini kimetokea , hivi unajua ni maumivu kiasi gani nimeishi nayo kwa kushuhudia kifo chako , niliishi kwa chuki sana zidi ya aliekuua”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu.
“Niliweza kuishi tena baada ya kufufuliwa na Yan Buwen , ndio aliehusika na mimi kuwa kama hivi”Aliongea.
“Yan Buwen!!!”Aliongea kwa kuhamaki.
“Ndio ambaye amekusaidia?”
“Mbona umeshangaa kama unafahamu jina lake?”Aliuliza.
“Nafahamu jina lake ndio , hakuna mwanasayansi siriasi ambaye hamfahamu , Yan Buwen ni mwanasayansi ambaye alikataa tuzo ya Noble Prize na umaarufu wake ulianzia hapo”Aliongea na kumfanya Kizwe kushangaa kidogo.
“Lekcha unashangaza , unaonyesha kujua mambo mengi na hata nilipopata taarifa umeweza kuwa Profesa wa chuo kikubwa kama hiki nilishangaa na kujiuliza maswali mengi kwanini ulikuwa Tanzania kwenye majalala tena ukiwa raia wa Rwanda?”Aliongea na kumfanya Lekcha kutulia kidogo.
“Nadhani mpaka sasa ushafahamu taarifa zangu si ndio?”
“Nataka uniambie wewe mwenyewe Lekcha haijalishi najua nini kuhusu wewe , ila nataka kusikia kila kitu kutoka kwako ,mara ya mwisho uliniambia siwezi kukutimizia unachotaka kupitia pesa na shauku yangu ndio hio , nataka kukujua kwa udani maana najua wewe sio mtu wa kawaida ambay hukupaswa kuokota makopo”
“Nitakueleza muda muafaka ukiwadia ila ninachoweza kusema adui wako ni adui wangu wa muda mrefu”
“Unataka kumaanisha nini?”Aliongea Kizwe kwa mshangao na Lekcha alisimama na kisha akasogelea droo ya meza na kuivuta na kisha akatoa picha chakavu na kumpatia.
“Huyu ni…”Aliuliza Kizwe kwa mshangao akiangalia picha ya kijana mmoja alievalia mavazi ya kininja.
“Anafahamika kwa jina la Ajent code 13 huyu ndio adui yangu ambaye ni adui yako”
“Sijakuelewa”
“Huyu ajent 13 ni siraha iliotengenezwa na taasisi ya siri ya Zeros organisation na ndio Roma Ramoni adui yako wa sasa”Aliongea na kumfanya Kizwe kushangazwa na maneno ya Lekcha.
“Ndio mtu ambaye alinipatia huu ukilema na ndio adui yangu namba moja na wewe kunikuta Tanzania ni mwendelezo wa kutafuta namna ya kulipiza kisasi changu”Aliendelea kuongea huku awamu hii akionyesha kukasirika na Kizwe alimwangalia kwa mshangao na kuanza kujiuliza Roma ni nani haswa ,kwanini hata kwa Yan Buwen alikuwa na kisasi nae.
“Clelia mpenzi wangu nipo njiani naja.. nitamtumia huyu mwanamke kumsogelea Yan Buwen na kupitia yeye nitamuua Hades na kama ulivyosema utanipokea baada ya kukuonyesha uwezo na nguvu zangu”Aliwaza Lecha akitaja jina la Clelia na aligeuza macho yake na kuangalia picha iliokuwa imetundikwa ukutani.
“Lekcha kwanini unaangalia sana hio picha?”Aliuliza Kizwe akiangalia picha iliokuwa ukutani yenye maandishi ya United Nation general Secretary, Clelia Allisanto.
“Kwasababu niliikuta imetundikwa hapo ukutani na inashangaza”
“Inashangaza nini?”
“Wewe huoni umri wa Clelia Allisanto na nafasi yake?”Aliongea na kumfanya Kizwe kuwaza kimantiki sasa , mwanzoni aliangalia uzuri wa mwanamke huyo lakini hakuangalia cheo chake na kweli haiwezekani kwa umri wake kuweza kufanikisha hilo tena akiwa ni mwanamke.
**********
Katika wanawake wake wote ambaye alikuwa amepiga hatua kimafunzo ni Rose pekee na Roma ilimshangaza kwani aliweza kuingia kwenye levo ya nusu mzunguko kwa muda mfupi sana , ijapokuwa ilikuwa levo ya chini katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi , lakini ilikuwa ni hatua kubwa ambayo amefikia na Roma ilibidi ampatie vidonge ambavyo alivichukua mara baada ya kuwaua watu wa hongmeng ili kumuwezesha kupanda levo kwa haraka.
Huwenda sababu ambayo ilimfanya Rose kupanda levo kwa haraka ni kutokana na kutokuwa na kazi ambazo zinamchukulia muda mwingi kama ilivyo kwa wenzake
Kwa mfano Amina alikuwa nyuma sana na yote hayo ni kutokana na majukumu kwani baba yake mzazi alikuwa nje ya nchi na yeye alipaswa kusimamia biashara zake kwa muda kutokana alikuwa akisumbuliwa na magonjwa.
Upande wa Nasra yeye alikuwa bize na ujenzi wa mradi wa Adani hivyo kazi ndani ya kampuni zilikuwa zimeongezeka maradufu.
Jambo moja ambalo lilimshangaza Roma ni juu ya Dorisi pekee, Roma aliona kitu cha ajabu ambacho alihisi huenda Dorisi alivyokutana na mwanamke anaefahamika kwa jina la Clelia Allisanto kuna kitu kilitokea.
Kila alipokuwa akifanya mapenzi na Dorisi alikuwa akijihisi kuchoka mno na ni kama nguvu zake zinanyonywa na kitu kingine Doris alionekana alikuwa akiimarika zaidi kila wanapokutana na hilo ndio ambalo lilimshangaza na kuona Dorisi ndio ambaye hakuwa wa kawaida , lakini hata hivyo hakutiliia sana maanani hisia zake.
Alijiambia kama Dorisi anaimarika kwa kufanya nae mapenzi basi atajitahidi kuhakikisha anamsaidia katika hilo.
Edna ndio pekee ambaye alikuwa kawaida tu , licha ya kwamba alikuwa akichukua mazoezi kila asubuhi lakini Roma hakumruhusu kuanza kwa kuhofia kwamba mwili wake ni mdhaifu mno.
Ijapokuwa Edna hakupenda kuwa nyuma nyuma , lakini hakuwa na jinsi kwasababu Roma ndio mwalimu wake na ilipaswa amsikilize hata kama hakuwa akiridhika na alichofanya ni kuendelea kujitahidi kuchukua mazoezi.
Ni saa tisa mchana siku ya ijumaa Edna na Suzzane walionekana ndani ya hoteli ya Peacock kwa ajili ya miadi na mgeni siku hio.
Edna alishangazwa sana jana yake Suzzane kumpigia simu akielezea kwamba Tajiri Khalifa mwenyekiti wa taasisi ya Emaar Foundation ndio ambaye amefika nchini kwa ajili ya kuonana nae.
Khalifa alikuwa tajiri mkubwa na ilishangazwa na ujio wake , ijapokuwa hata yeye ni tajiri mkubwa lakini kujilinganisha na Khalifa alieanza biashara zaidi ya miaka hamsini iliopita ilikuwa ni kumvunjia heshima.
Ndio maana muda huo wakati wanashuka kwenye gari alikuwa na mchecheto , kwanza kabisa alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini Khalifa kachangia mchango mkubwa kwenye taasisi yake , lakini muda huo uho akataka kuonana nae , hayo ndio maswali ambayo Edna alikuwa nayo na aliamini majibu yake yangeweza kujibika mara baada ya kukutana na mgeni huyo kutoka Taifa la urabuni Abu dhabi.
Kwasababu walikuwa na miadi waliweza kupokelewa na mhudumu na kuwaongoza mpaka kwenye lift na kutokea kwenye Floor za juu kuelekea kwenye chumba ambacho alikuwepo Tajiri khalifa , Edna alikuwa akijiamini kwasababu hakuwa peke yake.
Ila asichokijua ni kwamba Fayezi mtoto wa Tajiiri Khalifa aliuliwa na Roma mara baada ya kutaka kumlazimisha Amina afunge nae ndoa.
Baada ya kufunguliwa mlango na mhudumu mwenye asili ya kiarabu alievalia suti , Edna alishangazwa kukuta sio mtu anaekutana nae bali ni jopo la watu kama ishirini waliojipanga kwenye meza na ajabu ni kwamba mara baada tu ya kuingia wote walisimama kiheshima na kati ya sura alizozifahamu ni moja tu ambaye ni Nadia Alfonso mwanasheria wake.
Upande mwingine Roma akiwa kazini aliweza kupigiwa simu na Afande Kweka , alishangaa kupigiwa simu na huyo mzee babu yake kwani haikuwa kawaida yake.
“Uko wapi wewe mtukutu?”Aliuliza Afande Kweka kama kawaida yake.
“Nipo kazini tena kwenye kikao”
“Kuna mambo nahitaji tuongee lakini pia Zenzhei anaondoka”Aliongea.
“Unamaanisha nini Zenzhei kuondoka”Aliongea Roma na kumpa ishara Tanya ya kuendelea na alichokuwa akijadiliana nae na Tanya alitikisa kichwa na kutoka kwenye ofisi ya Roma.
“Muda wake wa kukaa kwenye ulimwengu wa kawaida ushafika kikomo na anapaswa kurudi kwenye miliki ya Hongmeng , anataka muonane kabla ya kuondoka”Aliongea Afande Kweka na kumshangaza.
“Kwani alikuwa na ukomo wa kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida?”
“Kama unataka majibu ya swali lako hakikisha kabla ya saa kumi na mbili za jioni upo hapa , alipaswa kuondoka jana lakini aliomba kuongezewa masaa mpaka leo jioni”Aliongea Afande na kumfanya Roma kushangaa lakini kwasababu alijua mzee huyo asingejibu maswali yake basi alimuambia anakuja.
Wakati Roma akipokea simu na Edna akikutana na jopo la watu asiowatambua upande mwingine katika mkoa wa Pwani Bagamoyo , Blandina na yeye alikuwa na miadi na mtu ambaye hakuwaza kama atakuja kumtafuta na kuongea nae tokea arudi nchini.
Ukweli mwanamama huyu alijishauri sana kwenda kuonana na mtu huyo tokea alipopata ujumbe wake na yote hayo ni kutokana na kukosa ile hali ya kujiamini.
Alijihisi kuwa mkosaji mbele ya Senga na chochote kilichotokea miaka kadhaa iliopita yeye ndio mkosaji , kwani yeye ndie aliefanya maamuzi ambayo yalikuwa ya ki usaliti , ijapokuwa hakufanya maamuzi hayo ya kiusaliti kwa makusudi lakini haikuwa ikimfanya kutokuwa mkosaji.
Raisi Senga alitaka kuonana na Blandina na muda huo wa mchana wakati Raisi huyo alipokuwa kwenye ziara ya mradi wa bandari Bagamoyi, alipanga miadi hio ya siri ili mke wake asije kufahamu.
Naam ni ndani ya hoteli ya Bagamoyo Resort ndio sehemu ambayo Blandina alikuwa akipaswa kukutana na mheshimiwa na muda huo alishuka eneo la maegesho, alifika mwenyewe akiendesha hivyo mara baada ya kushuka kutoka kwenye gari alifuatwa na Kabwe msaidizi namba moja wa Raisi Senga na kumuongoza njia.
Kule Jopo linamkaribisha Edna , kule Blandina na Senga , Upande mwingine ni Roma na Zenzhei.