singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
-
- #2,741
SEHEMU YA 489.
Baada ya kufunguliwa mlango na mhudumu mwenye asili ya kiarabu alievalia suti , Edna alishangazwa kukuta sio mtu anaekutana nae bali ni jopo la watu kama ishirini waliojipanga kwenye meza na ajabu ni kwamba mara baada tu ya kuingia wote walisimama kiheshima , kati ya sura alizozifahamu ni moja tu ambaye ni Nadia Alfonso mwanasheria wake.
Edna na Suzzane walihisi wamekosea chumba walichopaswa kuingia na Edna alitoa ishara ya kuomba msamaha kwa kuingilia kikao.
βKaribu sana Madam Persephoneβ Waliongea wote kwa pamoja kwa lugha ya kingereza na kisha waliinamisha vichwa kuonyesha ishara ya heshima jambo ambalo lilimpagawisha Edna na moyo wake kupiga kwa nguvu , alijihisi ni kama anaota na akishituka ingekuwa ndoto.
Kwa mara ya kwanza alihisi jina la Madam Persephone ambalo alilikuwa akiitwa mara kwa mara bila ya kujua sababu yake alihisi sio la kwake , ule ujasiri aliokuwa nao kwa muda huo ulimpotea na aliishia kuduwaa.
Suzzane pia alikuwa kwenye mshangao asijue nini kinatokea mbele ya macho yake , walikuja hapo kwa minajili ya kukutana na Tajiri Khalifa kutoka Dubai , mtu ambaye alichangia kiasi kikubwa cha pesa katika taasisi ya Edna Foundation na uwepo wao hapo ni kutii wito wa kuonana na tajiri huyo , lakini mambo yanaonyesha kuwa tofauti.
Licha ya kwamba alihisi yupo ndotoni lakini ulikuwa uhalisia na jinsi watu waliokuwa mbele yake walivyokuwa wakimwangalia alijua kabisa walimlenga yeye na ndio ambaye alikuwa akisubiriwa, lakini bado alijiuliza kwanini yeye na ni maigizo gani yanafanyika.
Kwanza chumba kilionekana kilikuwa cha mikutano ndani ya hoteli hii ya Peacock, pili mpangilio wa hapo ndani ulikuwa ni wa kikao muhimu kutokana na watu waliokuwepo , ilikuwa ni meza ndefu ambayo inajumla ya watu kumi kila upande kukamilisha watu ishirini na ni kiti kimoja tu ambacho kilikuwa wazi , kiti cha katikati ambacho huruhusu mkaliaji kuona nyuso za kila mtu aliekuwa mbele yake , ni rahisi kusema ndio kiti cha mwenyekiti kama ni kikao ambacho kinatarajiwa kufanyika.
Watu waliofahamika ambao wapo ni Shekhe Assad , Tajiri Khalifa , Mellisa Luiz , Pastor Cohen , Nadia Alfonso , Zoe Kovacic , Phill Knight na wengine wengi ambao ilionyesha ni wanachama wa Ant- illuminat.
Mwanadada mmoja aliekuwa wa kifilipino , alievalia suti alimsogelea Edna na kuinamisha kichwa mbele yake kwa namna ya heshima na kisha akavuta kiti kilichokuwa wazi na kumuonyesha ishara ya kukaa.
Edna bado aikuwa kwenye mshangao na alishindwa kujua achukue maamuzi , ya kuondoka au abaki na hata aliponyeshwa kiti cha kukaa bado hakupiga hatua kukisogelea maana alijua kukaa kwenye kile kiti ni kama yeye ndio anakwenda kuongoza kile ambacho kingekwenda kuendelea hapo ndani , kitu ambacho hata hakijui ni nini.
βMadam!!!β Suzzane alimshitua Edna ambaye bado alishindwa kufanya chochote licha ya kuonyeshwa kiti cha kukaa.
Edna aliinua uso wake na kuanza kuangalia kila mmoja ambaye yupo ndani ya hiko chumba, kuna wengine alikuwa akiwafahamu na kuna wengine hakuwahi kuwaona popote.
Lakini ghafla tu Edna alitoa tabasamu hafifu kama vile anavyofanyaga akiwa kwenye kampuni yake akiwa na kikao na wafanyakazi wake na alisogelea kile kiti na kuketi na kuwaangalia watu wote waliokuwa hapo ndani kama vile alikuwa akiwajua.
Ni kintendo ambacho hakikumshangaza Suzzane tu lakini kila mmoja kilimuacha na maswali lakini sio hivyo tu pia kiliwafanya kuwa na tumaini.
**********
Roma baada ya kuambiwa na Afande Kweka kwenda kuonana na Zenzhei , hakutaka kuchelewa sana , alikuwa na shauku ya kujua kwanini Zenzhei anataka kurudi Hongmeng baada ya kuishi Tanzania kwa muda mrefu.
Alitaka pia kujua ni jambo gani ambalo Zenzhei alitaka kumwambia , alikuwa na shauku kubwa kutokana na kwamba alikuwa na mpango wa kuivamia Hongmeng siku moja hususani muda huo ambayo alijua kabisa yeye ni adui na jamii hiyo , hivyo alitaka kukusanya kila taarifa iliokuwa ikihusiana na jamii hizo ili kumsaidia huko mbeleni.
Roma alimuaga sekretari wake kwamba anatoka na anagerudi siku iliokuwa inafuata , Tanya alishangaa kutokana na kwamba kuna baadhi ya maamjuzi yalikuwa yakimpasa kuyashughulikia siku hio hio lakini alikosa ujasiri wa kumzuia Master wake.
Ni zaidi ya miezi sasa tokea Tanya achukue majukumu ya Amina kama Secretari na alionekana ashanza kuipenda kazi yake na kuizoea na alikuwa ni msaada mkubwa kwa Roma kwani mambo mengi aliyafanyia kazi.
Muonekano wake ulikuwa umebadilika kwa asilimia mia moja na ilikuwa ngumu kujua ndio anaehusika kuongoza kundi la Yamata kutoka Japani ambalo linamilikiwa na Roma.
Roma alitumia muda machache sana kufika nyumbani kwa babu yake na baada ya kusalimiana na Afande Mstaafu Camilius Kweka ilisalimiana na Zenzhei pia wote walikuwa wamekaa nje kwenye bwawa la kuogelea na ilionekana walikuwa wakiongea.
βNitawaacha muongeeβ.
βCamilius haina haja ya kuondoka , ninachoongea na Mr Roma sio kipya kwakoβ
βHapana umesubiria muda mrefu na huu ni muda wako, Wewe mtukutu ukimaliza unione kwanza kabla ya kuondokaβAliongea Afande Kweka na kisha aliondoka eneo hilo.
βMr Roma samahani kama nimekuchukulia muda wako , muda huu ulipaswa kua kaziniβ
βUsijali kuhusu hilo , nilipaswa kuja hata jioni lakini kwasababu sikuwa na kitu cha kufanya kazini nimeona nije mapemaβAliongea Romana kumfanya Zenzhei kutingisha kichwa kumuelewa.
Na muda huo mfanyakazi aliwaletea Juisi ya matunda na kuweka mbele yao na kisha akaondoka.
βMr Roma muda wangu wa kukaa kwenye ulimwengu wa kawaida umeishaβ
βNilipoambiwa unaondoka nimeshangaa , kwani ulikuwa na ukomo wa kuishi Duiani?β
βNadhani ushawahi kisikia sheria za miliki za kijini juu ya binadamu au viumbe wanaojifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi?β
βNajua watu wa jamii kutoka miliki za kijini na binadamu ambao wamefikia katika levo ya Nafsi hawapaswi kuishi kwenye ulimwengu wa kawaidaβ
βUpo sahihi Mr Roma na mimi muda wangu wa kuishi hapa duniani ushafikia ukomo?β
βLakini uliishi kwa miaka mingi hapa Tanzania na naamini bado ulikuwa kwenye levo ya Nafsi , kwanini unaondoka sasa?β
βNi stori ndefu Mr Roma ambayo nataka unipe muda wako nikuelezee ili upate kujua nia ya mimi kutaka haya maongezi na weweβ
βNipo tayari kukusikilizaβAlijibu Roma kwa msisimko na Zenzhei alianza kumuhadhithia Roma kila kitu kuanzia namna ambavyo Zenzhei na familia yake walivyokimbia katika miliki za kijini na kuja katika ulimwengu wa kawaida , alielezea namna ambavyo baba yake mzazi na mama yake mzazi walivyopambana na wajumbe kutoka Hongmeng mpaka kuwaua , aliendelea kuelezea namna ambavyo baba yake alipambana na mtu asieonekana ambaye ndio aliyakatisha maisha ya wazazi wake mbele yake , namna ambavyo alipona , namna ambavyo alijiunga na kundi la kininja la Yamaguchi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa The Doni.(Rejea episode ya 317).
Roma alishangazwa na stori nzima ya Zenzhei na sasa alielewa uwepo wa Zenzhei kwenye maisha ya Afande Kweka ni kutokana na misheni aliopewa na kundi la Yamaguchi kukaa nae karibu.
Roma alikuwa akielewa kuhusu Yamaguchi lakini kwenye maisha yake hakuwahi kulipa umuhimu kundi hilo na yote hayo ni kwasababu aliyachukulia kama makundi mengine tu ya kininja ambayo yalikuwa yakiua kwa ajili ya pesa ,lakini hakufahamu kuna zaidi ya hayo.
βKwahio kundi la Yamaguchi hawakuweza kukufahamu kama unatokea Hongmeng?β
βHawakuweza kunifahamu mpaka baadae sana nilipowakatalia misheni ya kumuua Cammiliusβ
βUshawahi pewa mishenni ya kumuua Afande Kweka?β
βNdio lakini sikutekeleza agizo, Camillius nilifahamiana nae kwa muda mrefu tokea mke wake akiwa hai na amenisaidia kwenye mambo mengi ambayo yalinigusa moja kwa moja na kwangu nilimchukulia kama ndugu,nilipomuelezea ukweli juu ya kwanini nipo kwenye maisha yake hakukasirika na aliniacha nifanye chaguzi mimi mwenyewe kumchagua yeye au kundi na mamuzi nilioyafanya ni kumchangua yeye na ndio nilipokuja kuwa mlinzi wake mpaka leo hiiβ
βNikupe pole kwa yaliokukuta , lakini bado sijapata jibu la moja kwa moja umeishi miaka mingi ndani ya Tanzania na Hongmeng hawajakusumbua , kwanini sasa hivi?βAliuliza Roma , alishangaa kwani ni kweli Zenzhei alikuwa kwenye levo ya Nafsi na kwa sheria za Hongmeng hakutakiwa kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida , lakini ajabu ameshaishi miaka mingi sana bila ya kurudishwa.
βWazee wa Hongmeng hawakufahamu uwepo wangu duniani , walifahamu nimekwisha kufariki miaka mingi iliopitaβ.
βLakini mara ya mwisho ulisema ulikuwa na mawasiliano na Hongmengβ
βAmbao wanafahamu uwepo wangu hawakuuweka wazi kwa Wazee wa Hongmeng , ndio maana nikasema Wazee hawakufahamu uwepo wangu dunianiβ
βKama ni hivyo naweza kutafsiri ulikuwa na mawasiliano na wajumbe wa Hongmeng pekee na walificha uwepo wako lakini ukawa unaendelea na mawasiliano nao kama ni hivyo naamini kuna sababu wakaamua kuficha uwepo wakoβAliongea Roma.
βUpo sahihi kuna sababu kubwa ya kuficha siri ya uwepo wangu duniani na ni kutokana na ahadi ya faidaβ
βAhadi ya faida?β
βNdio Mr Roma unaweza kusema niliwaahidi kitu chenye faida ili waendelee kunifichia siri ya uwepo wangu hapa Tanzaniaβ
βKama ni hivyo kwanini sasa hivi wanataka urudi?β
βKwasababu ahadi sijaitimiza na siwezi kutimiza kutokana na nia yangu ya kulipiza kisasi kwa kile kilichowatokea wazazi wangu, kutokana na kutotimiza ahadi walinitishia mara nyingi kwenda kutoa taarifa kwa Wazee , lakini nilijitahidi kuwa mjanja kwa kuwasubirisha kwa maneno nikisubiria ujio wakoβAliongea na kumfanya Roma kushangaa ujio wake tena.
βUnamaanisha nini kusubiria ujio wangu?βAliongea Roma na Zenzhei alitabasamu.
βKwasababu kuna mtu nilikutana nae miaka iliopita na akaniomba msaada na kisha akaniambia ikiwa ni muda sahihi rudia haya maneno β Damu na Giza ni laanaββAliongea Zenzei nakumfanya Roma kutoa macho.
βUlishawahi kukutana na mtangulizi wangu?βAliuliza Roma akiwa haamini Zenzhei anafahamu hayo maneno kwasababu yalikuwa ni maneno ambayo ni fumbo.
Mara ya mwisho Roma kuongea na Hades wa zamani alimwambia maneno hayo ya fumbo na kumpa maelekezo mtu yoyote ambaye angeyatamka mbele yake anapaswa kumsaidia.
βMr Roma kukujibu swali , nitasema ndio nilikutana nae mara moja tu na aliniomba msaada wa kumtambua mwalimuβAliongea na kumfanya Roma kuzidi kujawa na shauku na mshangao kwa wakati mmoja na Zenzhei alijua Roma hakumuelewa hivyo akamwelezea kwa kirefu.
Kwa maelezo ya Zenzhei ni kwamba Hades wa zamani alimuomba msaada wa kumtajia mwalimu ambaye anaweza kufundisha binadamu mbinu za uvunaji wa nishati ya mbingu na ardhi kwa njia ndefu yaani ile ya Maandiko ya urejesho isio na kikomo ambayo ndio hio aliojifunza Roma na mtu ambaye alimtajia ni Tang Chi yaani master wake Roma.
Kwa lugha nyepesi Zenzhei alimpendekeza Tang Chi kwa Hades wa zamanni na Tang Chi akaja kuwa Master wa Roma.
Roma alishangazwa na ufunuo huo wa mambo lakini bado ilimchanganya kwani kwa namna ambavyo alikutana na Tang Chi ilikuwa ni kabla alipokutana na Hades wa zamani , kuna kitu kilimwambia huenda Master Tang Chi aliagizwa na Hades wa zamani kumfundisha yeye mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
Roma alijikuta akikumbuka namna ambavyo alikutana na Master Tang Chi ilikuwa ngumu sana kuamini alikuwa ameagizwa na mtu.
βMr Roma najua mtangulizi wako hajakuambia mambo mengi na mimi pia sio jukumu langu kukuambia yale ambayo hajakuambia kwani hata hivyo siyajui , nilimpendekeza Tang Chi kwasababu ndio binadamu pekee ambaye nilimfahamu kwa mara ya kwanza kujifunza tamaduni za jamii zisizoonekana na tokea nilipomsaidia hatukuwahi kuonana tena , lakini aliniambia msaada niliompatia ukizaa matunda basi nitayashuhudia kwa macho yangu na ndio ninapaswa kutamka maneno ya Damu na Giza ni laanaβAliongea Zenzhei na kumfanya Roma kukuna kichwa , ni kweli hakuwa akijua mambo mengi kuhusu Hades wa zamani na ilikuwa sawa kutokumuelewa, kwanza mtu mwenyewe aliishi miaka mingi hivyo huenda alikuwa na mipango mingi, Roma alifikiria na alijikuta akivuta pumzi.
βKama ni hivyo nadhani unapaswa kuniambia shida yako na mimi nitakusaidiaβAliongea Roma na kumfanya Zenzhei kuvuta pumzi.
βNinarudi Hongmeng kwasababu nahitajika kurudi , lakini naenda kukusubiria, mpaka sasa Mr Roma umekuwa adui namba moja wa Hongmeng na muda na saa yoyote watatoka huko walipo na kuja kukushambulia kabla ya muda huo kufika unapaswa kuwa wa kwanza kuchukua hatuaβ
βUnamaanisha niende Hongmeng na kupigana nao?β
βNdio njia pekeee ya wewe kuwa salama na watu wako unaowapenda , mbinu uliojifunza ni hatari zaidi na hakuna mtu wa hongmeng yoyote ambaye amefanikisha kufikia leo ya Kuzaliwa upyaβ
βLakini kama nitakuja kupambana Hongmeng watanizidi kwa uwezo wangu niliokuwa nao huu na isitoshe taarifa zinaonyesha ni wengi ambao wameshavuka levo ya Dhikiβ
βKuhusu uwezo wako sina wasiwasi umeweza kufikia levo ya kuipita Dhiki ndani ya umri mdogo sana hivyo natarajia utaenda juu zaidi ndani ya muda mfupi sana , nimekuambia nimevunja ahadi ndio maana Wazee wakagundua uwepo wangu duniani basi kile nilichoahidi nitakupatia weweβAliongea.
βUnamaanisha?β
βMr Roma haikuwa bahati mbaya familia yangu kushambuliwa ni kwasababu ukoo wetu ulimiliki kitu cha thamani sana ambacho Baba na Mama hawakuwa tayari kukiweka waziβAliongea na kisha akampatia Roma karatasi.
βHio karatasi imejaa taarifa ambayo ndio inanifanya nirudi Hongmeng, ndio urithi wa pekee kutoka kwa familia yangu nilioutunza kwa muda mrefu, nakupatia wewe kwasababu ni mtu sahihi wa kuwa naoβAliongea na kumfanya Roma aifungue ile karatasi na alijikuta akishangaa baada ya kuona ni kanuni ya utengenezaji wa vidonge vya kusaidia mafunzo ya kuvuna nishati ya mbingu na Ardhi.
βHii ni kanuni ya kutengenezea vidonge vya Poya?β
βInaonekana ushalifahamu tayari jina lake , jibu ni ndio kama utaweza kufanikisha kutengeneza hivyo vidonge itakuwa rahisi kwako kupanda levo ya juu zaidi na hakuna kiumbe chochote kutoka Hongmeng kitakuwa tishio kwakoβAliongea na kumfanya Roma macho yake kuchanua kwa furaha na kupitia kwa haraka ile katatasi.
βKwanini hukutengeneza hivi Vidonge wewe na kukuwezesha kupanda levo za juu zaidi na kulipiza kisasi?β
βMr Roma nimekupatia kanuni tu , uwezekano wa kukamilisha utengenezwaji wa hivyo vidonge haitokuja kuwa rahisi na haikuwa rahisi wangu pia kutengeneza nikiwa hapa duniani na sitoweza kutengeneza nikiwa Hongmeng wewe pekee ndio naamini unaweza kukamilishaβKatika siku ambayo Roma alipata kitu cha thamani basi ni siku hio, hakuamini Zenzhei alikuwa na material muhimu na hamwambii mpaka wakati anaondoka , huenda angemsaidia hata kutafsiri kanuni hio.
SEHEMU YA 490.
Abu Dhabi- UAE.
Ni baada ya mwezi mmoja tokea waanze uchunguzi wa kile ambacho alifanya Chriss , kitendo cha kutaka kumuua Edna, waliamini kabisa majaribio ya kuuwawa kwa Edna ni nje ya malengo ya jumuia yao hio ya siri na ndio maana walitaka kuufahamu ukweli , kwanini Chriss kafanya maamuzi alioyafanya.
Uchunguzi ulikamilika mara baada ya Nadia Alfonso kumuhoji Roma na kupata majibu ya kile kilichotokea na pia kumuhoji Suzzane kwa kile ambacho kilitokea na baada ya kupata maelezo yao na kuona yanafanana waliendelea na uchunguzi wa kutaka kujua zaidi kuhusu Chriss aliishi wapi mara baada ya kuokolewa na Hades wa zamani gerezani katika mikono ya CIA.
Naam sasa ilikuwa ni siku ya ijumaa mara baada ya swala ya mchana muda wa saa tisa katika moja ya makazi ya Tajiri Khalifa ndani ya Abu Dhabi kulikuwa na kikao cha siri sana ambacho kilikuwa kikiendelea.
Ni kikao ambacho hakikuhusisha watu wengi sana ,waliohudhuria ndio mhimili wa umoja huo wa siri ufahamikao kwa jina la Ant Illuminat.
βMmefikia katika hitimisho?βAliuliza mwanaume mmoja alievalia kilemba kichwani na kanzu.
βNdio ShekheβAlijibu kijana alievalia suti huku akiwa ameshikilia kishikwambi mkonnoni na jibu lake liliwafanya watu sita walioketi kwenye meza ya pembe nne wamwangalie kwa shauku ya kutaka kumsikiliza.
βUnaweza kuendeleaβAliongea mwanaume mwingine alievalia suti na miwani , alikuwa ni mzee ambaye umri wake ulionyesha kuwa mkubwa kutokana na nywele zake kuwa nyeupe.
βNadia Alfonso alifanikisha kufanya mahojiano na Roma Ramoni juu ya kile kilichotokea na ameweza kutupatia majibu yaliorahisisha uchunguziβAliongea na kisha akafanya βcastingβ ya kishikwambi chake na Screen ya TV ya nch 85 ya kampuni ya Sumsung na palepale ilionekana picha ya ua.
βMnachokiona kwenye Screen ni ua adimu linalofahamika kwa jina la Blue Ghost Orchid, kwa maelezo ya Mr Roma Ramoni kutoka Tanzania anasema kabla ya Chirss hajamshambulia CEO Edna na Miss Suzzane alitokea mwanamke na akawaokoa na baada ya Chriss kufariki mwanamke huyo aliacha zawasi ya hilo ua , Maelezo haya yanafanana na ya Bi Suzzane ambaye pia tulichukua maelezo yakeβAliongea na kisha akapozi kidogo na kuangalia kishikwambi chake na kwenda ukurasa wa pili.
βBlue Ghost Orchid ni utambuisho wa taasisi ya siri yenye makao makuu nchini Singapore lakini pia ni utambulisho rasmi wa mwanachama baada ya kupokea ua hilo kama zawadi kutoka kwa The Doniβaliongea na kuwafanya wale wazee kuangaliana.
βKwa maelezo yako tunapaswa kuamini The Doni ndio aliemuokoa CEO Edna si ndio?βAliuliza na kumfanya kijana yule kutingisha kichwa na kisha akaendelea.
β Kwa maelezo ya Bi Suzzane na Mr Roma mwanamke aliemuua Chriss ni Clellia Allisanto ambaye ni katibu mkuu wa umoja wa mataifaβAliongea na kuwafanya wote kuangaliana.
βMr Alban unatuambia kwamba aliemuokoa Edna ni Katibu mkuu wa umoja wa mataifa?βAliuliza mzee mwingine wa kiafrika alievalia suti.
βTumeshindwa kufikia kwenye hitimisho kutokana na kwamba hakuna namna yoyote ya kuthibitisha kama Clellia Allisanto ni The DoniβAliongea na kuwafanya waanze kuongeleshana wao kwa wao kwa dakika kadhaa na kisha wakamgeukia.
βVipi kuhusu Chriss, aliishi wapi mara baada ya kutolewa gerezani na kwanini alitaka kumuua Bi Edna kuna dhamira yoyote mmepata kuifahamu?β.
βKamati yetu ya uchunguzi iliweza kupokea nyaraka iliotumwa kwetu kwa njia ya barua pepe na mtu ambaye hakujitambulisha jina na imetoa majibu ambayo tumeshindwa kuyahakiki na nitayaweka waziβAliongea na kisha alienda kwenye Gmail na kufungua nyaraka iliotumwa na palepale ilionekana kwenye Skrini na kuwafanya wale wazee wenye miwani kuziweka vizuri ili kusoma na wale ambao macho yao yalikuwa imara walikodoa macho.
βNyaraka hii inaonyesha Chriss aliishi ndani ya Vatican mara baada ya kutolewa gerezani nchini Marekani na alikuwa ni mkutubi wa maktaba Chemba namba 4βAlielezea ile nyaraka na kuwafanya wale wazee kuendelea kushangaa.
βKuna taarifa yoyote inaonyesha alikuwa na dhamira ya kutaka kumuua Bi Edna?βAliuliza na Alban alitingisha kichwa kuashiria jibu ni ndio na kisha akapangusha kishikwambi chake na akatoa nyaraka nyingine iliotumwa kwao kama barua mfumo wa portable file(PDF).
βHii ni barua ambayo tunaamini imeandikwa na Chriss mwenyewe kabla ya kutekeleza misheni ya kutaka kumuua Bi Edna nchini Tanzania na inaonyesha sababu kwanini alifanya maamuzi tofauti na misheni aliopatiwa.βAliongea na palepale alianza kuisoma.
Kwa maelezo ya barua inaonyesha ni kweli Chriss alikuwa akiishi ndani ya Vatican kwa kipindi chote tokea atoroshwe kwenye gereza chini ya serikali ya kimarekani , anasema kwamba aliishi kwa Dilema ni upande upi anapaswa kuegamia kutokana na mfanano wa malengo ya dunia ijayo kati ya taasisi mbili tofauti yaani hio ya Ant-Illuminat na nyingine ambayo hakuitaja.
Anaendelea kusema maamuzi alioyafanya ni chaguzi alioifanya yeye mwenyewe na barua hio kama wataisoma basi atakuwa tayari amekwisha kufariki na misheni yake imefeli.
Mwisho kabisa anawafunulia kwamba misheni aliopewa kwa ajili ya Ant -illuminat ni kuwajuza kwamba kiongozi wanaemgojea sio yule ambaye wanamfikiria bali ni yule ambaye anapewa ulinzi na yule wanaemfikiria na ushahidi wa maneno yake upo kwenye mchoro wa unabii.
Mwisho kabisa wa barua anasema kama watakuwa wamefanikisha kupata barua yake basi misheni aliopewa na aliemuokoa imekamilika na atapumzika kwa amani akimlenga Hades wa zamani aliempatia misheni.
βMchoro wa unabii!!??βWalijikuta wakiongea wote kwa wakati mmoja kwani hawajaelewa.
βBarua hii ni ya kweli inetokea kwake kutokana na sahihi na nadhani kabla ya kufikiria mchoto wa unabii tunapaswa kujua kauli yake: βyule tunaemfikiria sio mwenyewe bali yule anaelindwa na tunaemfikiriaβ tuanzeni na kufumbua kauli yakeβAliongea mwanaume alievalia suti na Collar ya kiuchungaji.
βAlbani kuna taarifa nyingine ambayo bado haujatupatia?β
βHakuna Shekheβ
βKwasasa uchunguzi wenu uhamie upande wa Clellia Allisanto ili kufahamu kama ndio The Doni, kuhusu kuthibitisha uwepo wa Chriss ndani ya Vatican tutatumia koneksheni tulizokuwa nazoβAliongea Shekh na Albani alitingisha kichwa kukubali.
βUnaweza kwenda kwasasa , tunapaswa akujadiliβAliongea na kisha Albani aliondoka , haikueleweka alikuwa akitokea kitengo gani ndani ya taasisi hio ya Ant-illuminat lakini ni dhahiri ni sehemu ya kamati ya uchunguzi ilioutwa kutafiti kifo cha Chriss.
βPastor Cohen nini maoni yako?βAliuliza Shekhe na kumfanya mzee alievalia suti na kuwa na kipara cha nywele nyeupe kuvuta pumzi na kuzishusha.
βMpaka kufikia leo hii ni mengi ambayo yamefanyika na tumejipanua sana ndani ya mabara karibia yote na tuna washirika wengi wa kutuunga mkono kupambana na uovu , lakini licha ya mapambano yetu hatukuwa na kiongozi na wote tunajua tarehe 24 ya mwezi wa nne kwa mujibu wa Kalenda ndio siku ya kumtambua kiongozi wetu , nadhani alichoongea Chriss tunapaswa kukifiria mara mbili ili kupata majawabu lakini pia kuihakikisha kauli yakeβAliongea Paster Cohen kwa lugha ya kingereza.
βNaungana na Pastor Cohen ,nadhani ni wakati sahihi kwanza kuchambua kile alichoandika kwenye barua yake ili tufanye reasoningβAliongea mwingine.
βTunaefikiria siku zote kama kiongozi wetu ajae ni mrithi wa Hades ambaye ni Mr Roma Ramoni lakini kama sio yeye kwa kauli ya Chriss je anaemlinda ni nani?β
βNadhani kujibu swali hilo kwa wepesi ni sisi kujiuliza ni nani wa muhimu kwenye maisha ya Hades mpya?β
βMke wake ndio muhimu zaidiβ
βUpo sahihi Shekhe Assad, nadhani hili pia linatoa majawabu ya kauli ya Chriss kuwa katika DilemaβAliongea mwingine .
βKwa haraka haraka inaonyesha Chriss hakuwa akifanya kazi tu kama mkutubi ndani ya Vatican , huenda kuna watu aliokutana nao na kujenga nao mahusiano ambayo yamempelekea kwenye dilema na huenda dilema aliokuwa nayo ni katika kuchagua upande aidha wa kwetu au wa kwao na ni sahihi pia kuamini huenda ndio wamemuonyesha kitu alichokiita mchoro wa unabiiβ
βUnafikiri huo mchoro wa unabii unahusiana na Edna?β
βKama Bi Edna anapaswa kuwa kiongozi wa umoja wetu ambaye amechaguliwa na Hades wa zamani nadhani kuna uwezekano mchoro huo wa unabii unamzungumzia na ndio maana Chriss akachagua kutaka kumuua kwa kuagizwa na upande mwingineβ
βLakini kama mchoto unamzungumzia Edna kuwa kiongozi wetu kwanini na The Doni akamuokoa?β.
βHili ni fumbo gumu , lakini naamini majibu yake tunayo wenyeweβ
βUnamaanisha nini Paster Cohen?β
βWote tunajua namna ambavyo Hades wa zamani alivyomuhusisha Seventeen kwenye mpango LADO, mnafikiri ilikuwa bahati mbaya , Seventeen na Edna ni mapacha tena wa kufanana kabisa na mpaka sasa hatujui Seventeen yuko wapi na tukumbuke yeye ni mwanachama wa ant-illuminat na ndio ambaye alimwingiza Zoe Kovac kwenye uanachama na haikuwa hivyo tu, Seventeen alikuwa na madaraka ya kuchagua mwanachama mpya wa βfirst echelonβ cheo ambacho ni kikubwa katika jumuia yetu na ni madaraka makubwaβ
βLakini wote tunaamini kiongozi wetu amekabidhiwa muhuli na Hades wa zamani , si ndio ulivyosema Shekh Assad namna ya kumtambua?β
βUko sahihi kwa maelezo ya Hades wa zamani tutamtambua kiongozi kwa kutuonyesha pete ya muhuri(signet ring)?β
βBasi nadhaini hilo ni jibu la hiki tunachojadiliana hapa, kama maneno ya Chriss yapo sahihi na Hades mpya sio mwenye umiliki wa pete yenye muhuri basi mke wake Edna atakuwa naoβ
βUpo sahihi ndugu Khalifa , lakini kalenda yetu inatupa muda mchache sana wa kutambua nani mmiliki wa pete hio ya muhuri wa uongozi , kalenda yetu inaonyesha tarehe 24 mwezi wa nne ndio siku ambayo tunapaswa kumtambua kiongoziβAliongea na kuwafanya watu wote kuingia kwenye mawazo na waliona ana point.
βNadhani kuna namna moja tu ya kuthibitisha maneno ya Chriss ni ya kweli au ya uongo?βAliongea Shekhe Assad.
βUnataka kusema nini?β
βTarehe ishirini na nne ndio siku katika kalenda yetu ya kumtambua kiongozi wetu na Chriss katuachia tayari fumbo na wote tunafahamu mtu muhimu katika maisha ya Hades mpya ni Edna mke wake , nadhani hili ni jibu tosha kwetu, Kama Edna kweli ni kiongozi wetu basi lazima atakuwa na pete ya muhuri wa uongozi na siku hio anapaswa kutuonyeshaβAliongea na kufanya chumba kukaa kimya.
βWajumbe mnasemaje juu ya wazo la Shekhe Assad?β
βKama kweli fumbo la Chriss linamuonyesha Edna ndio kiongozi wetu basi lazima atakuwa na muhuri wa uongoziβAlirudia mwingine kauli ileile ya Shekhe Assad.
βNa kama hatokuwa na pete ya muhuri basi tutatambua moja kwa moja yeye sio mlengwa na sio kiongozi wetu na fumbo la Chriss sio sahihiβAliongea na wote walikubaliana na wazo lake.
βKama ni hivyo tunafanikishaje kumfanya atuonyeshe pete hio?βAliuliza Tajiri Khalifa.
βTunatakiwa kumfanya atuonyeshe na ili hilo lifanikiwe lazima tuwe na mpango, Miss Edna anaweza kuwa na muhuri lakini hana ufahamu wowote kuhusu jumuiya yetuβ
βNaunga mkono hoja na matukio mengi yanaonyesha ndio kiongozi wetu na wote hatujui hapa huenda Hades mpya amemkabidhi Edna pete hio kwa maelekezo ya Hades wa zamaniβ
βNi kweli kabisa hakuna ambaye anajua nini Hades wa Zamani na Hades mpya waliongea wakati wakukabidhiana urithi , huenda alimwagiza Edna apatiwe muhuli na yeye ndio anaepaswa kumlindaβ
βMimi nina mawazo tofauti , kwa maelezo ya Hades wa Zamani hajamwambia Hades mpya kitu chochote kuhusu Ant illuminat na ameseme yeye mwenyewe angefahamu kitu kimoja kimoja kadri ya muda unavyosonga,tutaomba CEO Edna atuonyeshe muhuri wa uongozi kama kweli anao lakini tusiende na wazo la kuamini kwamba Hades mpya kampatia pete hio ya muhuri wa uongozi, nadhani mpaka sasa tunaelewa kwamba Hades hajamwambia mkewe chochote kuhusu Seventeen kuwa ni pacha wake , unafikiri ingekuwa rahisi kwake kumpatia MuhuriβAliongea Shekhe na maneno yake yalionekana kuwa na mantiki.
Makubaliano ni tarehe ishirini na nne mwezi wa nne kuonana na Edna ili aonyeshe pete ya muhuri wa uongozi wa jumuia hio ya ant-illuminat.
Naam Edna kukutana na jopo la watu hao kwa kisingizio cha kuonana na Tajiri Khalifa ilikuwa ni mbinu tu, lakini vipi kuhusu hio pete.
SEHEMU YA 491.
ROME β ITALY- Miezi miwili iliopita.
Ni miezi miwili iliopita mashariki mwa jiji la Rome katika moja ya jengo la makumbusho ya kitaifa usiku wa saa mbili na nusu kwenda tatu kulikuwa na kikao cha watu wazito.
Ni watu wazito haswa kutokana na itifaki za ki usalama ambazo zilikuwa zimekwisha kuchukuliwa , jengo hilo lilikuwa kikitumika kama la makumbusho na mara nyingi muda wote linakuwa wazi mpaka saa nne za usiku kuruhusu watu , lakini siku hio jengo hilo lenye muundo wa kikale lilifungwa kwanzia muda wa saa kumi za jioni.
Ilikuwa ni sehemu sahihi sana kwa kufanyia mikutano ya siri kutokana na muundo wa jengo lenyewe lakini kitu kingine barabara ya kuingia ndani ya hili jengo haikuwa na pilikapilika nyingi kama barabara za katikati ya jiji.
Sasa usiku ndani ya vyumba vya Ardhi ndani ya jengo hili kulikuwa na kikao ambacho hakikujumuisha watu wengi sana , jumla ya watu waliokuwa wakifanya kikao walikuwa ni wanne tu, watatu wote walikuwa wamevalia suruali nyeusi na mashati ya rangi ya bluu iliokolea na kuvaa na Collar ambazo kwa harakaraka ziliwatambulisha kama wachungaji.
Mtu mmoja pekee ndio ambaye alivalia suti pamoja na tai , mwanga wa hapo ndani haukuwa mkali sana kutokana na taa zake za rangi ya njano zilizokuwa zikiendana na muundoo wa chumba.
βBarrack nadhani unaelewa sipendezwi na vikao vya dharulaβAliongea mzungu mmoja ambaye umri wake kwa haraka haraka ni kama miaka sabini hivi.
βAndre siwezi kusahau jambo muhimu kama hilo , lakini leo tulipaswa kuonana kwa dharula na nimefarijika mmeweza kutii wito kwa harakaβAliongea yule mwanaume ambaye amevalia suti na tai akiwaangalia wale wenzake ambao walionyesha kuwa ni wachungaji au mapadri..
βNini kimetokea?β
βNi kuhusu Chriss mkutubi wetu ambae alienda Tanzania kwa maagizo yetuβAliongea na kuwafanya wale wachungaji kuangaliana lakini mwanaume alieitwa kwa jina la Andre alionyesha utofauti.
βNini kimetokea kuhusu Chriss , makubaliano yetu ajiingize ndani ya jumuia ya Ant Illuminat ili kupata kujua kila kitu kinachoendeleaβ
βPastor Michal hiko ndio ambacho kimenifanya kuitisha hiki kikao cha dharula , taarifa zilizonifikia mpaka sasa Chriss amefaikiβAiongea mwanaume aliefahamika kwa jina la Barrack na kimya kilitawala.
βNini kimetokea? Je amegundulika ni shushu wetu?β
βHilo haliwezekani ndio maana nahitaji kusikia kutoka kwenu wote,sisi wanne ndio tunajua kuhusu Chriss na Pastor Andre ulihusika kumbadilisha Chriss na kuwa double agent kazi ambayo ilichukuwa muda mrefu na hata aliporudi kuwa chini yangu ulinihakikishia ni Asset ya faida kwetu na ndio maana nilimsamehe na kumpa nafasi nyingineβ
βMr Barrack tunataka kusikia nini kimepelekea kifo cha Chriss?βAliongea mchungaji michael.
βTaarifa nilizopata inaonyesha alienda kinyume na misheni aliopewa na Hades wa zamanni ndani ya Ant illuminat na akamshambulia Edna Adebayo mke wa HadesβAliongea na kufanya wote kumaka lakini Andre muonekano wake haukutafsirika na Barrack aligundua hilo.
βAndre mbona unaonekana kutoshangaa?β
βChriss alipaswa kunitafuta mara baada ya misheniβAliongea Andr.
βUnamaanisha nini Andreβ
βNi mimi niliewasiliana nae dakika za mwisho kabisa na kumwambia misheni imebadilikaβ
βKwanini?β
βWameniambia kama hatuwezi kubadili unabii tunaweza kubadili matokeoβAliongea na kuwafanya wenzake wote kushindwa kumuelewa.
βNilipokea ujumbe kutoka kwa baraza la 33rd degree ya kumbadilishia Chriss misheni yake na wakati nawasiliana nae aliniambia ashafika eneo la tukio na muda si mrefu angekutana na Edna Adebayoβ
βMbona mimi ndio niliwasiliana nae na kumbadilishia misheni siku moja kabla nini kinaendelea?βAliwaza ndugu Barrack.
βAndre ni watu gani hao?β
βPrior of sion, wanajua kila kitu ambacho tunakifanya na mipango yetu na hata kifo cha Chriss waliniambia wao wenyewe muhusika mkuu ni Minervaβ
βAthena ndio aliemuua Chriss?βAliuliza Barrack huku akionyesha wasiwasi.
βHivyo ndio walivyoniambiaβ
βPapa Andre , ulishawahi kunihadithia umekutana na Athena ana kwa ana nadhani huu ndio muda wa kutuambia anafanana vipi? Je ni kweli Clelia Allisanto ndio yeye?βAliuliza kwa kutanguliza jina la Pope Mwanzoni.
βClellia Alisanto katibu wa umoja wa mataifa sio Minerva bali Athena anatumia Clone nina uhakika na hiloβ
βI knew itβAliongea akimaanisha kwamba alijua tu.
Naam mwanaume anaefahamika kwa jina la Barrack ni raisi mstaafu waMarekani na Andre ni Pope , wawili ni Michale ambaye cheo chake haikuwa wazi na pia John cheo chake haikuwa waz.
*********
MASAA KADHAA NYUMA
Ni muda wa saa sita usiku mara baada ya Roma kuondoka nyumbanni na kwenda kuzamia nyumbani kwa Nasra kwa kupitia balkoni, muda huo huo katika chumba chake alionekana mtu mwingine akiibukia na kuanza kuangalia mazingira ya hapo ndani na mara baada ya kuridhika aliingia kwenye chumba anacholala Roma na kuwasha taa na baada ya kuona kitanda hakina mtu alitabasamu kwa kebehi.
βKulikuwa na haja gani ya kufanya sherehe kubwa na kutuharibia maua kama unakuja kulala mwenyeweβAliongea kwa lugha ya chini huku akigeuka nyuma.
Alikuwa ni Hermes au Prince Raphaeli ambaye mwezi mmoja nyuma alimuokoa Denisi kwa kumdhibiti Roma kupitia ndoto.
Baada ya kukagua chumba cha Roma kwa dakika kadhaa alitoka kwenye chumba hiko na kuingia kwenye korido na ndani ya dakika chache tu aliibukia kwenye chumba cha Edna.
Baada ya kuingia ndani ya chumba hicho hakuacha kuangalia mandhari ya chumba kizima na kisha akahamia kwenye kitanda na kumwangalia Edna na Lanlan ambao wamelala fofo,
βHades unaishi na mtoto wako lakini mpaka muda huu umeshindwa kumfahamu, aliesema huna akili kweli kapatiaβAlijiwazia huku akimwangalia Lanlan aliemuwekea Edna mguu kwenye shingo.
βAthena sijui ananitakia nini , Hades akiniona namwangalia mke wake namna hii lazima ataniua, inabidi nifanye haraka kilichonileta na kuondokaβAlijiwazia mwenyewe na kisha akanyanyuma mkono wake na kumnyooshea Edna kama vile anamwombea na muda uleule Edna alianza kutingisha kichwa kama vile mtu ambaye yupo ndotoni na Hermes alidumu vilevile kwa dakika kama tano na kisha akaonyesha kuridhika na akageuza macho kwa Lanlan na kumnyooshea mkono kama alivyofanya kwa Edna na Lanlan alianza kutafuna tafuna kwa kasi kama vile kuna kitu analishwa na Hermes alitabasamu na kisha akaondoa mkonno wake.
βPersephone , kwanzia kesho utafanya mambo yako yote bila kujielewa chini ya udhibiti wangu ukiwa ndotoniβAliongea huku akimwangalia Edna kwa dakika na kisha akafungua mlango wa kutokezea kwenye balkoni na palepale alipotea kufumba na kufumbua.
*********
βMadam Persephone tusamehe kwa kukufanyia hii surprise , yote yamefanyika kwa kuzingatia itifaki za kiusalama wa kuficha kile ambacho kinakwenda kuzungumziwa hapa ndani, nadhani upo kwenye mshituko lakini kabla ya kuendelea na hatua ya pili tutaomba utoe wasiwasi kabisa na kama kila kitu kikienda sawa huenda sisi wote tukawa chini yakoβAliongea Shekh Assad na Edna alishindwa kujibu chochote na alishangaa pia uwepo wa Nadia Alfonso.
βKwa majina yangu naitwa Ally Assad na ndio msemaji mkuu wa hili jopo lote la watu waliopo mbele yako na Kabla ya kujitambulisha kwako mmoja mmoja na kukuelezea dhumuni la uwepo wetu hapa ndani tunataka ututhibitishie kwa kutuonyesha pete ya muhuri unaokutambulisha kama kiongozi wetuβAliongea.
βShekhe Ally Assad unaweza kuketiβAliongea Edna bila wasiwasi na Shekh Assad alikaa chini na watu wote walimwangalia Edna kwa shauku ya kile ambacho anakwenda kufanya.
Edna hakuonekana kuongea chochote zaidi ya kuchukua mkoba wake na kutoa kijiboksi kidogo cha rangi nyeusi , ni viboksi flani kama vile vya kuwekea pete au mkufu.
Kitendo kile cha kushikiria kile kiboksi kabla hata ya kukifungua kiliwafanya watu wote hapo ndani kuwa na mchecheto wa aina yake.
βKwasababu wote mmekuja kukutana na mimi leo hii , basi sina budi kuwadhirihirishia kwenu muhuri ambao unanitambulisha kama kiongozi wenuβAiongea Edna akiwa kama sio yeye vile na kisha akafungua kile kiboksi na ndani yake ilionekana pete ambayo kwa kuiangalia tu haikuwa ya kawaida, ilikuwa na mchoro juu yake ulionakshiwa kwa madini ya shaba , mchoro ulikuwa kama vile ni tunda ambalo limekatwa kwa mshazari katikati sasa ule muonnekano wake wa ndani ndio ulifanana na hio pete.
Edna aliitoa na kuishikilia mkononi na kisha kwa mbwembwe zote aliingiza kidoleni katika mkono wake wa kulia na akaunyoosha juu ule mkono kuelekezea ule upande wa pete kuonekana kwa watu waliokaribu.
βShekh Ally Assad hii ni Signet ring inatumika kama muhuri na ni kwa muda mrefu haijatumika , unaweza kuiangalia kwa ukaribu kuona kama mchoro wake unafanana na muhuri unaonitambulisha kama kiongozi wenuβAliongea Edna na Shekhe Ally Assad aliangalia kwa umakini ile pete na alijikuta akipatwa na mshangao usiokuwa wa kawaida na palepale aliwageukia wenzake wote na kuwapa ishara ya kuashiria ndio muhuri wenyewe na wote kwa pamoja walisimamaa na kuinamisha vichwa chini kwa mara nyingine.
βKaribu sana Malkia wetu PersephoneβWaliongea kwa mara nyingine baada ya kusimama na Edna alinyoosha mkono juu kuwazuia na akawaambia waketi chini na walitiii.
Suzzane na Nadia walikuwa na mshangao kwani hawakutegemea kutokutana na upinzani kutoka kwa Edna , lakini alionyesha kana kwamba watu waliopo mbele yake anawafahamu mbaya zaidi aliongea kimadaraka.
βLeo nimejitambulisha kwenu kikalenda , lakini muda wangu wa kuwaongoza bado , mpaka muda utakapokuwa sahihi nitawatafuta, kwasasa Shekh Assad ataendelea kuongoza jumuia yetu kwa niaba yangu na malengo yote yanapaswa kutimia kabla ya siku ya kurudi kwanguβAliongea na kuwafanya kuonyesha sura za kutoelewa maana ya maneno.
*********
Blandna alijikuta akishangaa mara baada ya kuambiwa na raisi Senga kuhusu Roma kile alichomfanyia Desmond mtoto wa raisi Jeremy, hakujua jambo hilo kama limetokea kwani Roma na Edna hawakumwambia.
Usiku wa juzi walivyorudi alijua kabisa kuna jambo ambalo limetokea lakini hakuhoji sana kwani Roma alimwambia hakukuwa na tatizo na ni sherehe tu ambayo haikuwa nzuri.
Na yeye alipotezea baada ya kuwaona Edna na Roma asubuhi walikuwa wamepatana na ile hali ya kununiana ilikuwa imeisha na ndio maana hakuhoji sana.
βKwahio hiki ndio ambacho ulitaka kuongea na mimi?βAliuliza Blandina
βKuna lingine ambalo ulitarajia kusikia kutoka kwangu , nimekuita hapa kukuambia kile alichokifanya mtoto wako ili umuonye kwani akiendelea kuchafua amani ya nchi yangu nitamchukulia hatuaβAliongea na kumfanya Blandina kumwangalia Senga kwa huzuni.
βKwanini unamwita mtoto wangu peke yangu Senga , Wewe sio mtoto wako? Au ni kwasababu amebadilisha jina na kuitwa Roma ndio kinachokupa shida ya kumtambua, Senga najua huwezi kunisamehe lakini Roma bado ataendelea kuwa mtoto wakoβ
βKimya!!!, wewe na Roma kwangu mlishakufa na ndege na sitaki kuhusika na maisha yenu , ninachotaka kutoka kwako ni kumuonya Roma aache kuharibu diplomasia ya nchiβ
βSenga tangu lini ukawa mnafiki wa hisia zako mwenyewe?β
βUnamaanisha nini?βAliongea Raisi Senga huku awamu hii akionyesha kakarisika maradufu.
βManeno yako yapo tofauti na hisia zako Senga, unafikiria sijui kinachoendelea kwenye moyo wako , ulifikiri nitashindwa kujua kile unachojisikia , sijakusahau Sengaβ
βKimyya , Blandina naomba usinikasirishe zaidi kukaa na mimi chumba kimoja usijipe ujasiri wa kuongea unavyojisikia , wakati ule ulishapita na sasa nimekuwa raisi kwa juhudu zangu wakati wewe ukijifichaβ
βKinachokusumbua Senga ni kwasababu Roma ana nguvu zaidi kuliko wewe , uwezo wake na nguvu zake zinakufanya ujihisi huwezi kuwa baba mbele yake, Senga acha kuishi kwa mateso unapaswa kuachilia baadhi ya mambo megine yasahaulike kwenye moyo wakoβ
βKuna vitu naweza kusahau , lakini siwezi kumsahau mwanamke alienisalitiβAliongea na kumfanhya Blandina kuanza kutokwa na machozi.
Muda huo maongezi yao walikuwa wakiyafanyia ndani ya chumba cha hoteli hivyo ilikuwa ngumu kwa mtu wa nje kujua kile ambacho kinaongelewa na ilikuwa mara ya kwanza kwa Senga na Blandina kukutana wakiwa peke yao tokea arudi Tanzania na huenda ni mwanzo mzuri wa mapatano.
βNajua Senga huwezi kusahau na huwezi kunisamehe lakini upendo wangu kwako hakuwahi kupotea kwa miaka yote ambayo hukuweza kufahamu nipo haiβ
βBlandina acha kuwa mnafiki mbele yangu utanikasirisha , nimekuja hapa kukuonya kuhusu Roma kuingilia amani ya taifaβ
βUna uhakika ndio kitu pekee ambacho ulitaka kuniambia mpaka kutaka kuongea na mimi kwa kujificha ficha?βAliuliza na kumfanya Senga amwangalie Blandina huku akikosa neno la kuongea.
Alichoongea Blandina ni ukweli mtupu, kama kweli alitaka kumuonya tu kuhusu Roma haikuwa na haja ya kumuita hotelini kwenye chumba cha Presidontial Suite tena kwa siri.
Blandina alimwangalia kwa muda namna ambavyo amekosa neno la kuongea na kisha akaangalia mkoba wake na akauchukua.
βKwa mra ya kwanza nimefurahi kukuona kwa ukaribu Senga, nitamwonya Roma kutokuingilia uongozi wakoβAliongea na kisha alisogelea mlango akitaka kutoka.
βSubiri..!!!βAliongea na kumfanya Blandina kusimama na kugeuka na Senga aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti na ilionekana kuna kitu anatoa.
SEHEMU YA 492
Roma hakujua kinachoendelea kabisa na baada ya kutoka kwa Afande Kweka hakupitia nyumbani kabisa , akili yake ilimwambia aende kuonana na Rufi kwanza kuongea nae kuhusu kanuni aliopewa na Zenzhei ya kutengeneza vidonge vya nguvu za kijini , alikuwa na muwashawasha wa kufahamu kama Rufi angeweza kuelewa kanuni zote.
Dakika chache mbele mara baada ya kuendesha gari aliweza kufunga breki chini ya jengo la apartment anapoishi Rufi na alitoka kwenye gari na kuzisogelea lift.
Baadaya kuingia kwenye lift na kubonyeza kitufe cha floor husika simu yake ilitoa mtetemo wa ujumbe wa meseji ulioingia ,alifungua na kuona ni ujumbe ulitoka kwa Xiao Xiao na aliupotezea palepal.
Ilikuwa ni siku zaidi ya mbili msichana huyo wa kichina hakukata tamaa kutuma jumbe za kumsalimia Roma na nyingine za kuchombeza lakini Roma hakujibu hata moja , hakutaka matatizo na mke wake lakini pia alijua akiwa na ukaribu na msichana huyo itakuwa rahisi kwa Rufi uwepo wake hapa Tanzania kufahamika kwa wepesi , hivyo alijiambia anapaswa kumuepuka kwa nguvu zote.
Baada ya kutoka kwenye lift alibonyeza kengere na mlango kwa ndani ulifunguliwa na Rufi ambaye amevalia tisheti ya jezi ya Man U huku mkononi akiwa ameshikilia juisi ya matunda.Alitabasamu na kumpa ishara ya kuingia na Roma alifanya hivyo.
βInaonekana unapenda sana mambo ya kompyuta , kwa mwonekano wako ulipaswa kujifunza vitu vilaini vilaini visivyotumia akili nyingiβAliongea Roma mara baada ya kuona tarakishi ikionyesha namba namba ambazo hata hakuelewa.
βKompyuta naipenda kwasababu nahisi kama dunia yote naiona , nimejifunza mambo mengi sana na kwasasa najaribu kutafuta Proffesional Hacjer anielekeze baadhi ya mambo madogo madogoβ
βKwahio unataka kuwa mdukuzi , haupendezi kabisa kwa fani hio?ββ
βKipi kinanipendeza? Au kutapeli watu ndio kazi nzuri inayonifaaa?βAliongea na Roma hakumjibu na aliishia kumwangalia tu kuona kama ana shida yoyote kwani tokea amuache mara ya mwisho hakuwasiliana nae kabisa na kumpa habari za Xiao Xiao msichana wa kichina aliemkimbia.
βUnaendelejeaje, ulitoka kweli humu na kwenda kutembea?β
βNaogopa hata kwenda Supermarket na hofia naweza kukutana nae tenaβ Aliongea huku akijibwaga kwenye sofa kivivu na kumfanya Roma amuonee huruma.
βUnapaswa kutoka bila ya kuhofia chochote hakuna mtu yoyote wa kuja Tanzania na kukufosi urudi ilihali mimi nipoβ.
βAh .. najua unaweza kunilinda lakini hawatoacha kuja mara kwa mara lazima watalazimisha nirudi sitaki kukuongezea zaidi matatizoβ
βNishakuambia usiwe na wasiwasi juu ya hilo nimefuatilia taarifa za msichana uliekuwa unamkimbia yupo Tanzania kikaziβ
βKweli?β
βUnafikiri nakudanganya? , umeacha lini kutokuniamini?βAliongea Roma na kumfanya Rufi kutabasamu na kushindwa kuongea chochote na Roma aliona apotezee mada hio na kwenda moja kwa moja kwa kile kilichomleta.
βNimekuja kukuuliza namna ya kutengeneza vidongeβ
βUnataka kutengeneza vidonge!?β
βKwanini unaonyesha kushangaa ,ushasema mwenyewe vidonge ni muhimu katika kusaidia kupanda levo naweza nisihitaji mimi lakini warembo wangu nataka niwapatie ili viwasaidieβ
βNdio vidonge ni muhimu sana kwa wanaoanza mafunzo , lakini kuna mahitaji yake na kanuni za kutengenezaβ
βNdio maana nimekuja kwako nataka kujua hayo mahitajiβAliongea Roma na kumfanya Rufi kufikiria kidogo.
βKama kweli una nia ya kutengeneza vidonge. kuna changamoto tatu ambazo unapaswa kuzivuka , Changamoto ya kwanza lazima upate mimea ambayo hutumika kutengenezea, hii sio rahisi kwasababu mimea hio ni adimu sana kupatikana na hata ile ambayo inatengeneza vidonge vya thamani kubwa imepotea kabisa, katika miliki za kijini kwenyewe huwezi kuipata hio mimea na ndio maana licha ya uwepo wa wenye ujuzi mkubwa wa kutengeneza wameishia kutengeneza vidonge vya kawaida tuβ
βLakini umesema kuna wanaokuja huku duniani kutafuta hio mimea ?β
βNdio kuna wanaosafiri mpaka duniani kwa ajili ya kutafuta mimea ya kutengenezea vidonge lakini mara nyingi huishia maeneo ya karibu na bara la Asia , kwani wengi wao wanasema wanaogopa kuvunja sheria za the gods treatyβ
βKama ni hivyo basi uwezekano wa kupata hio mimea upo ,ninachotakiwa kufanya ni kutuma watu wangu wajaribu kufatilia, je ni wapi ambapo unaamini mimea hio inawezekana kupatikana?β
βSina uhakika ila marra nyingi ni sehemu ambazo ustaarabu wa kale ulianzia kama vile Misri na maeneo mengine kama hayoβAliongea na kumfanya Roma kutingisha kichwa kumuelewa.
βVipi kuhusu changamoto inayofuatia?β
βThat is even harder , You would need a high Quality CauldronβAliongea akimaanisha kwamba changamoto ya pili ni ngumu zaidi kwasababu atahitajika kuwa na Cauldron.
βCauldron?βRoma aliuliza.
βNdio Cauldron ni Dhana ambayo ipo mfano wa chungu kikubwa ambacho kimetengenezwa kwa madini maalumu ambayo yalipatikana enzi za kale,ni madini ambayo yana uwezo wa kuhimili kiwango kikubwa cha joto , kwa uelewa wangu katika miliki za kijini vipo vitano tu hivyo vyungu , Kekexil wanavyo vitatu ,ukoo wa wakwe zangu wanacho kimoja na Hongmeng wenyewe wanacho kimoja , kama kuna jamii nyingine ambazo wana aina hio ya chungu kinaweza kuwa nje ya matumizi hivyo haitokuwa rahisiβ
βChangamoto ya tatu ni kuweza kudhibiti moto wa njano na mweupe ambao ndio hutumika kutengenezea hivyo vidonge kwa joto kubwa sana zaidi ya joto la kuyeyushia chuma na kubalansi na Chungu hikoβChungu kinachozungumziwa hapo ni cha kijini ambacho ni kama Cauldron
βChangamoto ya tatu ya kudhibiti moto wa rangi ya njano na mweupe sio tatizoβ
βUnamaanisha unao uwezo huo?βaliuliza huku akionyesha mshangao na Roma alitingisha kichwa.
βKwanini hujazungumzia kuhusu andiko la kanuni za kutengenezea hizo dwa?βAliuliza Roma akimaanisha andiko la kanuni alilopatiwa na Zenzhei.
βKila koo ina kanuni zake , lakini ilisemekana mwanzoni Hongmeng walikuwa na andiko la kanuni ambayo hutengeneza vidonge vyenye uwezo mkubwa sana ,lakini bahati mbaya andiko hilo lilipotea, ndio ninachojua japo sina uhakika,lakini hilo lisikupe shida haina haja ya kuwa na hizo kanuni kikubwa ni namna ya kudhibiti joto la moto wa kichawi mweupe na wa njano ukishafanikisha kupata hiko ChunguβAliongea
βNitakuwa naendelea kuvuna nishati huku nikisubiria watu wangu waweze kutafuta hayo maeneo uliozungumzia , unaonaje kama wakifanikisha unisindikizeβ
βMimi? , unamaanisha twende pamoja?β
βNdio ,najua itakuwa usumbufu lakini siwezi kujua mimea inayohitajika nikienda mwenyeweβ
βLakini inawezekana ikawa ni mbali na Tanzani misituni hukoβ
βUsiwe na wasiwasi nishaishi sana msituni hivyo nina uzoefu wa kutoshaβAliongea Roma.
βMimi sina tatizo lakini vipi mkeo anaweza akakasirika?βAliongea kwa sauti ndogo huku akiona aibu.
Na kabla Roma hajajibu simu yake ilianza kuita na aliitoa na kuangalia mtu anaempigia na alishangaa ni Bi Wema , alipokea harakaharaka na kuweka sikioni.
βMr Roma nadhani Miss Edna kapatwa na tatizoβ
βUnamaanisha nini kapatwa na tatizo Bi Wema , nini kimetokea?β
βAmerudi kutoka kazini saa kumi kamili za jioni na akasema ana usingizi , amelala mpaka muda huu na nimejaribu kumuamsha haamki , Lanlan na yeye amejaribu kumuamsha kwa nguvu lakini hajashitukaβAliongea Bi Wema huku sauti yake ikionyesha wasiwasi na kumfanya Roma kuguna.
βAna pumua?β
βNdio kifua kinapanda na kushuka ndio hivyo haamki , nadhani ni vyema ukarudi umuangalie nina wasiwasi kwani sio kawaida mtu kulala na kushindwa kuamkaβAliongea Bi Wema na kumfanya Roma apumue kidogo kwa ahueni.
βNakuja sasa hivi Bi WemaβAliongea Roma na kisha akata simu.
βNadhani mke wangu kapatwa na tatizo , ngoja niwahiβAliongea Roma na Rufi alitingisha kichwa .
******
Afande CammiliusKweka alionekana kuathirika sana na taarifa ya Zenzhei kutaka kurudi Hongmeng , alijitahidi kuonyesha kuwa sawa lakini ukweli alikuwa akiumia kiume lakini hakuwa na uwezo wowote wa kumzuia kutoondoka kwani asingeweza kumlinda zidi ya Hongmeng.
βZenzhei niseme asante sanaβAliongea Afande Kweka kwa sauti hafifu na muda huo ni kama masaa mawili mara baada ya Roma kuondoka.
βCamillius kwanini unanishukuru?β
βAsante sana kwa kwa kujjifanya kuwa mzee mbele ya macho ya watu ili mradi unilinde bila watu kukushitukia , asante kwa kufanya kazi za hapa kama vile ni mfanyakazi wa ndani , asante sana kwa kumfanya mke wangu kipindi kile kufa kifo cha amaniβAliongea Afande Kweka huku macho yakiwa makundu na hata Zenzhei mwenyewe alishindwa kujizuia na kudondosha chozi.
βHupaswi kusema hivyo Cammilius ulikuwa ni wajibu wanguβ
βHapana, nimekukatili sana kwa kipindi chote ulichokuwa na mimi lakini bado nikakosa aibu na kuwa mbinafsi na kukufanya uendelee kuwa karibu yanguβ
βCamillius usiongee hivyo nilikuwa na furaha kuishi na weweβ
βZenzhei matumaini yangu ni kwamba hutonichukia , najua kwanini ulikaa na mimi kwa miaka mingi sana lakini nilishindwa kufanya chochote juu ya hisia zako kutokana na kukosa ujasiri , nilishindwa kuzipokea na mpaka sasa nashindwa kuzipokea licha ya uzee huuβAliongea afande Kweka na kumfanya Zenzhei kufumba macho yake huku machozi yakimtoka.
Ni kweli alikuwa akimpenda Afande Camillius Kweka tokea mara ya kwanza walipokutana , lakini licha ya kuonyesha hisia zake kwa mzee huyo hakuchukua hatua yoyote na yeye kukosa ujasiri wa kuchukua hatua zaidi.
βCamilius kabla sijaondoka nitarudi kwenye mwonekano wangu wa mwanzo wakati tunakutana nadhani itakufanya usijione mwenye hatiaβ Aliongea Zenzhei na palepale mwili wake ulibadilika taratibu ,ilikuwa ikishangaza mno kwani ndani ya nusu dakika alibadilila na kuwa msichana kama wa miaka ishirini na nne mwanamwali , ilikuwa ni sahihi kusema alikuwa akifanana kabisa na Xiao Xiao japo yeye kidogo alikuwa na umbo la kuvutia na huenda angekutana na Roma angefanya jambo la kueleweka.
Ilionekana ili kuishi na Afande Kweka ilibidi ajizeeshe ili kuficha ujini wake , kwani kama asingefanya hivyo angebakia kuwa msichana mdogo ilihali Afande Kweka alikuwa anazeeka.
βNakumbuka mara ya kwanza tulipokutana Sudani ulikuwa na miaka hamsini CamiliusβAliongea Zenzhei na sio sura tu iliobadilika hata sauti yake pia ilikuwa imebadilika.
βHaha.. bado urembo wako uko vilevile hakujabadilika chochoteβAliongea huku akitoa kicheko chenye machungu na kumfanya Zenzhei kutabasamu akikosa neno.
βNadhani hii ni kwaheri ya moja kwa moja, naamini siku ukirudi nitakuwa tayari nimeshakufaβaliendelea kuongea na kumfanya Zenzhei kuingiwa na huzuni.
βKwaheri ya kuonana Camiliusβ Aliongea Zenzhei.
βKwaheri ya kuonana Zenzhei hakikisha unakuwa na maisha ya furaha na kutafuta mtu anaekupendaβ
βAsante sana CamiliusβAliongea na kisha wakaangaliana usoni kwa madaki kakadhaa na Zenzhei alikosa ujasiri wa kuendelea kusimama mbele ya Camilius na palepale alipotea kwenye macho yake.Na hio ndio safari ya Zenzhei kurudi ujinini ikaanza rasmi.