Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Huwezi amini nimekutana Edna jamani bonge la pisi Kali alikuwa posta offisini kwake jamani mtoto mzuri
 
SEHEMU YA 495.
Roma alishangazwa na kupatwa na huzuni ya taarifa hio ya kifo kwani siku hio hio ndio walipanga kwenda yeye Edna na Lanlan kumtembelea, kwao ilikuwa ni kama wamechelewa kwenda , lakini hata hivyo hakujilaumu sana kwa kutowahi kwenda kumuona.
Mzee Atanasi ni moja wapo ya wazee waliokula chumvi nyingi na alikuwa akikaribia kutimiza miaka mia moja na moja na kwa uzito wake ndani ya serikali ya Tanzania ni sahihi kuitwa babu wa taifa.
Ndio mwanajeshi pekee aliebaki ambaye alipigania uhuru wa Tanzania pamoja na Raisi Nyerere.
Roma hakuwa na haraka ya kwenda moja kwa moja msibani , alitaka kwanza kumaliza kilichomfikisha hapo na kisha ndio arudi nyumbani na kuelekea huko , ile safari yao ya kwenda kwa ajili ya kusalimia iligeuka na kuwa safari ya kwenda msibani.
Roma baada ya kukata simu kwa kumpa mama yake pole aliwageukia Diego na kuwapa taarifa hio ya msiba na Diego na Bram walimpatia pole.
Roma aligeukia kwa mara ya pili picha iliokuwa ikionekana kwenye skrini , picha ya mwanaume aliefahamika kwa jina la Bikindi , alikuwa ni baba mzazi wa Lekcha na Roma alimkumbuka kwasababu ni moja ya wanasayansi wa Zeros organisaiton aliowaua.
“Mfalme Pluto unamfahamu huyu mwanaume?”Aliuliza Diego na Roma alitingisha kichwa kuashiria anamjua.
“Mmefanikisha kuchunguza taarifa za Joseph Bikindi za hivi karibuni”
“Ndio mfalme Pluto kwa taarifa tulizoweza kupata kutoka Rwanda mpaka miezi michache iliopita alikuwa mkufunzi wa chuo kikuu cha taifa lakini kwa wiki kadhaa sasa ameripotiwa kutoonekana chuoni bila ya taarifa”.
“Endeleeni kumchunguza kwa ukaribu zaidi na sura yake iunganishe na mfumo wetu wa ‘facial recognition’ ili kama itatokea akiwepo Tanzania tuweze kutambua mara moja”Aliongea Roma huku akipata hisia huenda Lekcha alikuwa Tanzania kwa kutafuta namna ya kulipiza kisasi na kwa muda huo ambao Kizwe alionekana kutokuwa wa kawaida aliamini huenda wapo wote na wanajiandaa na mipango ya kulipiza kisasi , hakusahau na Denisi alikuwa hivyo hivyo tu ndio maana alihitaji kuchukua tahadhari mapema.
Jambo lingine ambalo lilimfanya kuwa na wasiwasi ni juu ya Athena ,tokea apewe cheo cha Hades hakuwahi kujionyesha kwake na alikuwa akijua ana mzunguka lakini hakuwa akijua sababu ni ipi ,lakini alijiambia maadamu yupo hai basi kuna siku tu wataonana na atathibitisha maswali yake yote.
“Vipi kuhusu uchunguzi wa Chriss mlikamilisha?”
“Mfalme Pluto taarifa za Chriss imekuwa ngumu sana kuzipata na mpaka sasa hatujapiga hatua lakini kuna jambo moja tu ambalo tulifanikiwa kupata”
“Mmepata nini?”Aliuliza Roma kwa shauku na Diego alitoka ndani ya chumba hiko na ndani ya muda mfupi aliweza kurudi na mfuko wa plastic ambao ndani yake ulionekana kuwa na mkufu uliofungwa na kishaufu cha madini ya almasi.
“Huu ni…”
“Ni mkufu ambao unaonyesha Chriss alikuwa mwanachama wa Freemason”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuchukua na kuangalia vizuri na kweli aliweza kugundua maana ya mchoro uliokuwa kwenye kishaufu(Pendant).
Ijapokuwa sasa ameweza kuanza kupata ukweli wa Chriss alikuwa akitokea jamii ya siri ya freemason lakini ilikuwa ngumu kwake kuweza kuamini kama watu wa jamii hio ya siri ndio walitaka kumuua mke wake na moja kwa moja alijua huenda majibu yapo kwenye mchoro.
Roma ilibidi kwanza amuelezee Diego na Bram kile ambacho alikuwa akitambua kuhusu Chriss.
“Mfalme Pluto hata sisi tunashindwa kuelewa kama Chriss alikuwa mwachama wa Ant- illuminat”
“Kwanini mnaamini hawezi kuwa mwanachama unajua taarifa zote za umoja huo?”
“Ndio mfalme Pluto najua taarifa zote zinazohusiana na umoja wa ant- illuminat na baadhi ya mipango yao ya mbeleni japo mpaka sasa hakuna uthibitisho kwani ni taarifa ambazo ni kama uzushi”
“Ni taarifa gani ambazo unafahamu?”
“Mfalme Pluto ushawahi kusikia kuhusu mpango TASAC?”
“Mpango TASAC!, si huu ulioanzishwa na serikali ya Urusi kuyafanya mataifa ya Afrika kutounga mkono wala kukataa vamizi anazozifanya Raisi wa Urusi nchini Ukraine?”
“Ndio mfalme Pluto lakini ni ngumu kusema mpango TASAC umeanzishwa na Urusi”
“Kwanini?”
“Taarifa za siri za daraja la tatu zinaonyesha mpango TASAC waanzilishi ni Ant- illuminat”Aliongea na kumfanya Roma kuguna ilikuwa habari mpya kwake na huenda angekuwa anafatilia sana maswala ya siasa angekuwa ashaijua , huenda ilikuwa sahihi kwa Christen kumwambia hayuko ‘flexible’ kama mtangulizi wake”
“Uzushi mwingine unaoenezwa kuhusu Ant-illuminat ni juu ya mataifa ya kiarabu kuwekeza zaidi katika mataifa yalioendelea ya kimagharibi katika nyanja ambazo zinagusa moja kwa moja hisia za watu mfano kwenye vilabu vya mpira na kadhalika”Aliongea Bram.
“Na pia ndio kinara wa mapambano ya sarafu ya Dola ya kimarekani kutaka kuiangusha”Aliongezea Diego.
“Inaongekana mnapenda sana uzushi”
“Your Majesty if no Somke no Fire “Aliongea Diego akiingiza msemo ambayo unaoendana na ule wa kiswahili usemao yasemwayo yapo na kama hayapo yaja au penye moshi hapakosi moto.
Roma hakutaka kukaa sana hapo kwani kuna msiba ambao ulikuwa ukimuhusu na mpango wake ni kuunganisha kwanza msibani kujua kile kinachoendelea na kujua taratibu zinazofuatia, hivyo alitoa msisitizo wa usalama zaidi wa watu wake wa karibu kuzingatiwa hususani muda huo ambao alijua na Lekcha ni adui yake mpya alieingia kwenye orodha.
Akiwa garini alijaribu kuwasiliana na mke wake kumuulizia kama kapata taarifa na ilionyesha Edna alikuwa na taarifa na alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kufika msibani pamoja na Bi Wema na Roma alimwambia angemkuta huko huko kwani anatangulia.
Baada ya kufika Masaki nyumbani kwa Tajiri Azizi aliweza kuona watu wengi waliokuwa wakiingia ndani ya nyumba hio na kutoka na pia kulikuwepo na baadhi ya waandishi wa habari.
Kwa haraka haraka Roma alishajua msiba huo ni wa kitaifa hivyo wageni wengi lazima wangefika kutoa salamu zao za pole.
Roma hakuingiza gari ndani ilibidi apaki pembeni kwa kuhofia ndani kusingekuwepo na nafasi na baada ya kuegesha aliingia moja kwa moja ndani na alikuta tayari maturubai yashasimamishwa pamoja na viti ambavyo vilikuwa vikipangwa.
Mtu wa kwanza kuonana nae alikuwa ni Kassimu mtoto mkubwa wa tajiri Azizi ambaye alikuwa akipokea wageni na alimkaribisha Roma na kumpeleka kuonana na mama yake pamoja na wanafamilia wengine.
Dakika chache mbele na Edna aliweza kufika na kutoa pole , msiba haukuwa na vilio sana zaidi ya sura za majonzi tu huenda ni kwasababu mzee huyo kaishi miaka mingi na muda wake umewadia hivyo alipaswa kutangulia mbele za haki .
Ratiba ya msiba ilikuwa ni siku inayofauta mwili kuagwa katika viwanja vya Karimjee na kisha safari ya kuelekea Kilosa kijijini ingeanza ili kumpumzisha Babu Atanasi.
Katika watu ambao walikuja kutoa salamu za pole ni Samweli Nguruma kiongozi wa kundi la ZoaZoa na ilikuwa ni kama amekuja kumtafuta Roma kuongea nae.
Roma alishawahi kuwasiliana na bwana huyo kwa kupitia simu ila hakuwahi kukutana nae ana kwa ana na siku hio ndio waliweza kufahamina kwa mara ya kwanza.
Samweli Nguruma baba yake na Benadetha alikuwa ni kama bosi mtu mwenye kitambi na kipara cha nywele na ilikuwa ngumu kuamini ndio ambaye alikuwa akijihusisha na biashara za magendo lakini hata hivyo Roma hakutaka kumtoa dosari ukizingatia hata Rose hakuwa na mwonekano wa kuongoza kundi la Tembo.
“Mr Roma unamwonaje mtoto wangu Benadetha?”Aliuliza Samweli Nguruma na kumfanya Roma kushangazwa na swali hilo.
Ilikuwa ni saa za mwisho mwisho za kuaga mwili ili safari ya kuelekea Morogoro ianze ndio maana Roma alishangaa.
“Kwanini unauliza hivyo mzee?”.
“Nataka kujua maoni yako, umefanya nae kazi kwa muda mrefu kidogo hivyo sio dhambi kutoa maoni yako unavyomuona na tabia yake kwa ujumla”Roma ijapokuwa muda huo aliona hakupaswa kujibu swali hilo kutokana na muda kutokuwa mzuri lakini aliona ni kheri kujibu kile anachokiona kwa Benadetha.
“Namuona kama msichana mzuri mwenye sheria zake na inaonyesha ashatambua mapema kama mwanamke anataka nini katika maisha yake”Alijibu Roma na kumfanya Samweli nguruma kutabasamu.
“Upo sahihi Benadetha ni binti mwenye msimamo na mara nyingi uwezo wake mkubwa wa kujielewa unanifanya hata mimi baba yake kumhofia”
“Hongera kwa malezi, kwa ninavyomuona atakuja kuwa na maisha yenye furaha sana mbeleni”
“Furaha ya mwanamke inakamilika pale akiridhika na kila kitu kunachomzunguka, asipo ridhika ataishia kutangatanga kukidhi haja ya moyo wake”Aliongea
“Ndio maana nikasema Benadetha atakuja kuwa na furaha kwasababu kama mwanamke ukishafahamu kwenye maisha unataka nini mapema ni rahisi pia kuridhika”
“Upo sahihi Mr Roma lakini ushawahi kujiuliza kwanini kipindi Benadetha alipopelekwa kituoni na mkeo nilitaka wewe ufanye kazi ya kumtoa?”
“Kwanini?””
“Nilijua tayari mkeo ashafahamu hisia za Benadetha kwako”Aliongea na kumfanya Roma ashangae.
“Mzee labda utakuwa haujamfahamu Benadetha vizuri , mimi na yeye hatuna ukaribu huo na hata kama Benadetha anipende mimi kama mwanaume siwezi kumpokea kwani tayari nina mke”Aliongea Roma bila ya wasiwasi.
“Haha.. Mr Roma nimekutana na vijana wengi ila ujasiri wako na kujiamini ni wa viwango”
“Na wewe pia ujasiri wako ni wa viwango kumnadi mtoto wako wa kike kwangu ilihali tayari nina mke sio jambo la kawaida kabisa kwa tamaduni za kiafrika”
“Upo sahihi imenichukua ujasiri kuongea na wewe kuhusu maswala ya binti yangu na nimetidhika pia kama huna nia ya kumfanya kuwa sehem ya wanawake wako”Aliongea na kumfanya Roma kumchanganya na kuona huenda habari za yeye kuwa na wanawake wengi zilikuwa zikifahamika kwa watu wengi.
*********
Tokea kumalizika kwa maziko ya Babu Atanasi siku zilienda haraka haraka mno na katika watu ambao walikuwa wako bize basi ni Roma ,kuna muda alijiambia uwepo wa Lanlan kidogo ulikuwa umesaidia sana kupunguza migogoro yake na Edna.
Kwani kitendo cha Lanlan kung’ang’ania kulala na mama yake ilimpa nafasi Roma ya kila usiku kutembelea wanawake wake kwa zamu na hilo pia lilisaidia sana kuyafatilia maendeleo yao.
Vidonge ambavyo aliweza kuvipata baada ya kuwaua watu wa hongmeng vilisaidia sana katika kumfanikisha Rose kupanda levo na Roma aliona kabisa muda si mrefu Rose angefanikisha kupata ufunuo wa nguvu ya mbingu na Ardhi jinsi ya kutumia elementi zote za dunia.
Katika mafunzo ya kijini kila mmoja alitofautiana na mwenzake katika kupata ufunuo wa namna ya kutengeneza maajabu kwa kutumia elementi za dunnia na hicho ndio ambacho kilimfanya Roma kupatwa na hamu kubwa ya kuwaona wakifikia levo ya kupata ufunuo.
Mage na yeye hakuwa mbali sana na ilionyesha juhudi zake zilionyesha manufaa kwani alianza kuelewa levo ya nusu mzunguko kikamilifu na Roma aliona kabisa muda si mrefu angeweza kuingia levo ya mzunguko na alijiambia kama atafanikisha mpango wake wa kutengeneza vidonge vyenye nguvu basi huenda ndani ya mwaka mmoja kila mmoja anaweza kuingia kwenye levo ya Nafsi na matumaini ya kuweza kupata mtoto yangekuwa juu.
Upande wa Amina msukumo wa ndani zaidi kujifunza mafunzo hayo ni kwa ajili ya kutunza urembo wake na kufanya tahajudi muda mrefu haikuwa kazi kubwa kwake, ,ijapokuwa maendeleo yake yalikuywa ya taratibu lakini alileta matumaini na hata hivyo Roma alifurahi kuona Amina alikuwa mzoefu wa mazoezi ya Yoga na hilo ndio lilirahisisha.
Neema Luwazo ndio ambaye alikuwa akijifunza kwa fujo sana na tamaa kubwa ya kufikia levo za juu na Roma aliona huenda ni kwasababau alikuwa akiukaribia utu uzima ndio maana alitaka kupanda levo kwa haraka ili asiendelee kuzeeka na kubakia na mwonekano wa ujana.
Lakini licha ya fujo alizokuwa nazo za kutaka kujifunza maendeleo yake yalikuwa ni ya taratibu mno kulinganisha na wengine wote kutokana na utu uzima wake kwani ilikuwa rahisi kwa vijana kujifunza na kupanda levo kwa haraka tofauti na watu wazima na Roma ilibidi achukue jukumu la kumtuliza.
“Roma nimeachia majukumu kabisa ya kampuni kwa Alhaji kwa ajili ya kujifunza”Aliongea Neema usiku Roma alipomtembelea.
“Umefanya vizuri lakini unatakiwa kwelewa mbinu hizi huwa zinaendana na utulivu wako wa akili ukiwa na tamaa ya kupanda levo kwa haraka utakosa utambuzi wa kunyaka kila viashiria vinavyokujia wakati wa kufanya Tahajudi na ndio maana nakushauri usichukulie sana hili swala siriasi lifanye kama ni moja wapo ya starehe, kama unavyokaa kwenye Jakuzi ukiwa umeshikilia glasi ya mvinyo ukiyafurahia mafanikio yako”Aliongea Roma nakumfanya Neema kutabasamu.
Na alfajiri Roma alijaribu kufanya nae mafunzo na sasa angalau aliona akili yake ilikuwa imetulia , ilionekana maneno yake ya jana usiku yalikuwa yamefanya kazi.
Upande wa Edna na Nasra maendeleo yao yalikuwa ya kinyonga lakini yalioleta mabadiliko kwenye miili yao.
Zamani Edna alikuwa akimhofia Lanlan kumrukia kutokana na uzito wake lakini kwa kipindi chote alichokuwa akichukua mazoezi alikuwa ameimarika na kumudu hata uzito wa Lanlan vizur.
*******
Ni baada ya wiki moja kupita hatimae Omari na Queen waliweza kufunga ndoa yao rasmi kwa tamaduni za dini ya kiislamu ambazo zilimtaka Queen kubadili dini jambo ambalo Mzee Alex hakupinga, hata hivyo ni Omari pekee ambaye alionyesha kumpenda mtoto wake kwa mapenzi ya dhati licha ya kwamba alikuwa mjamzito hivyo hata swala la Queen kubadili dini kuwekwa mezanni kwake hakuwa na kipingamizi.
Saa tano na nusu za usiku ndio muda ambao Roma na Edna walirudi kutoka kwenye sherehe ya harusi hio ya Omari na Queen na wakati Roma anaingiza gari ndani ya geti alishangazwa kuona nyumba bado inatoa mwanga wa taa kutokea sebuleni kwani kwa muda huo aliamini wanafamilia wote wangekuwa washalala.
Roma usiku huo akiwa njiani alikuwa akipanga kwenda kuburudika na mke wake Edna usiku kucha kwa kuamini muda huo Lanlan angekuwa tayari amekwisha kulala na Qiang Xi.
Lakini sasa ile wanaingia sebuleni lile tumaini lake lote lilipotea baada ya kumkuta Qiang Xi na Lanlan wakiwa wamekaa sebuleni na hata Edna mwenyewe alishangaa kuwakuta hapo kwani muda ulikuuwa umeenda.
“Qiang mbona mpaka muda huu Lanlan hajalala na asubuhi anatakiwa kuwahi kuamka”
“Madam nimejaribu kumfanya alale lakini hana usingizi na anasema anakusubiria”Aliongea Qiang Xi huku akionyesha hali ya uchomvu ilionekana alikuwa akijitahidi kuwa macho kwasababu ya Lanlan na alikuwa amechoka.
“Lanlan kwanini unashindwa kulala?”
“Mama sipati usingizi , Lanlan anataka kulala karibu na mama”Aliongea na kumfanya Roma akunje sura alijiambie kama watoto wake watakuja kuwa kama Lanlan basi maisha yake yangekuwa magumu sana.
Edna alimuonea huruma kuona alikosa usingizi na swala hilo lilikuwa likimsumbua kichwa namna ya kulitatua kuishia kujiuliza kama siku nyingine asingekuwepo na Lanlan angelala vipi.
Upande wa Roma alishajua kwanini Lanlan alikuwa akikosa usingizi , sababu ilikuwa ni kutokana na damu yake kuchemka kila wakati na kumfanya kukosa utulivu wa akili ndio maana alikuwa akikosa usingizi na njia pekee ambayo aliona huenda ingemsaidia Lanlan ni kumfundisha ya mbinu ya kimaandiko ya urejesho ili aweze kudhibiti uwezo wake lakini alimuona Lanlan ni mdogo na hata kama angejaribu kumfundisha kutamka maneno ya maandiko na kuyageuza kuwa nguvu ingekuwa ngumu kwake.
Hivyo suluhisho la muda mfupi ambalo aliona lingefaaa kwa muda huo ni Lanlan kuendelea kulala na Edna mpaka atakapogundua namna ya kumsaidia kupata usingizi bila ya uwepo wa Edna.
Roma mara baada ya kurudi kwenye chumba chake akijiandaa kwenda bafuni kujimwagia maji alale simu yake ilitoa mlio wa ishara ya mwaliko wa mtu kumpigia kwa njia ya Vidio Call.
Baada ya kuangalia inatoka kwa nani aligundua ni Sauron na alijikuta akiwa na shauku ya kumsikia maana ni kama mwezi unakaribia kuisha tokea ampatie Sauroni kazi ya kusambaza vijana kutafuta maeneo walioishi binadamu enzi za kale , maeneo ambayo yalifanikisha ukuaji wa mila na tamaduni za kijamii za mwanzo kabisa(Ancient Civilization) lakini baada ya muda maeneo hayo yakatelekezwa , aliamini upatikanaji wa maeneo hayo ingekuwa rahisi kwake kuweza kupata mimea anayojitaji itakayosaidia katika utengenezaji wa vidonge vya kijini.




SEHEMU YA 496.
Licha ya mwonekano wa kutisha kutokana na mtindo wake wa nywele nyingi alizokuwa nazo kwa upande wa Roma alikuwa ashamzoea na kumuona mtu wa kawaida lakini kwa mwingine huenda mwonekano wa Sauroni ungemkosesha amani hususani wakati anapokuwa siriasi.
Ilionekana muda huo Sauroni upande wa kwao kulikuwa ni mchana maana alionekana ndani ya ofisi huku kwenye meza yake kukiwa na mafaili mengi, huku yeye mwenyewe akiwa amevalia miwani ya kusomea.
Roma mara baada ya kupokea simu na kubadilishana salamu na Sautoni ilibidi amwambie aende moja kwa moja kwani alitaka kulala.
“Mfalme Pluto nishakutumia mafaili yanayohusiana na taarifa ulizo omba kupitia barua pepe yako , tumefanikisha kupata maeneo nane yanayofanana na sifa ulizotupatia”Aliongea Sauroni
“Asante sana Sautoni kwa juhudi zako zilizopelekea kufanikisha , vipi kuna changamoto yoyote uliweza kupata?”
“Sijapata changamoto kubwa mfalme Pluto lakini nina shauku ya kufahamu kwanini unahitaji taarifa za hayo maeneo kwani kwa uelewa wangu hayo maeneo sasa hivi hayakaliwi na binadamu na huenda hata uwepo wa hio mimea ni kwasababu hio na binadamu wa kawaida ambaye angesafiri kwenda kwenye hayo maeneo asingeweza kutoka hai”Aliongea na kumfanya Roma kucheka kidogo
“Maeneo ambayo watu waliishi na sasa hawaishi ndio ambayo ninayatafuta kwani naamini inaweza kufanikisha kupata kile ninachohitaji , najua una shauku lakini nitakuelezea siku nyingine kwasasa taarifa hii ulionitumia nitaipitia na kuanza na mikakati ya kuelekea huko”Aliongea Roma na Sauroni aikubali na kisha akakata mawasiliano
Roma alighairi kwanza kwenda kuoga na kuanza kupitia taarifa ambazo ametumiwa na Sauroni na ilionekana ziliandikwa vizuri ili kueleweka kwa urahisi, ni ‘Document’ ambayo ilikuwa na peji nane ambazo zilikuwa zikielezea maeneo husika ambayo yalikuwa yakikidhi vigezo.
Na mpaka anakuja kumaliza alikwisha kupata sehemu ambayo aliona inafaa kuanzia kutafuta mimea hio lakini kwakuwa hakuwa mzoefu sana alitaka kwanza kusikia maoni kutoka kwa Rufi na kwasababu muda huo ulikuwa ni usiku sana aliona angewasiliana nae asubuhi.
Siku iliofauta jambo la kwanza ilikuwa ni kuwasiliana na Rufi na akamtumia na faili la taarifa alizotumiwa na Sauroni na wote walijikuta wakiachana na baadhi ya maeneo yalio orodheshwa kwa sababu za aina moja, waliachana na eneo la Eveglades ambalo lipo kusini mwa Marekani , Msitu wa Panama , msitu wa Amazoni na maeneo mengine na wakaja kuchagua eneo lililofahamika kwa jina la Arnhem Land ambalo lipo kaskazini mwa bara na nchi ya Australia.
Arnhem Land ni eneo ambalo walichagua kutokana na historia yake kwani sio tu kwamba miaka ya hivi karibuni halikukalika lakini miaka mingi iliopita lilikaliwa na watu wa asili zaidi wa nchi ya Australia na ilikuwa ni eneo ambalo ni kama tamaduni nyingi zilizaliwa na hivyo ndio vigezo ambavyo Rufi alipendekeza.
Eneo ambalo lilikaliwa na watu wa asili na kuzaa tamaduni na mila ndio ambalo lingekuwa na mkusanyiko wa nguvu nyingi za kiroho ambazo zingefanikisha upatikanani wa malighafi za Alchemy.
Roma alikuwa akielewa Australia ilikuwa kusini mwa ncha ya dunia na kwa mwezi huo wa nne kwenda wa tano ni kipindi cha Vuli na kama angevuta muda vuta muda basi mwezi wa sita ingekuwa ni hatari zaidi kwenda kwani ingekuwa ni kipindi cha baridi kali na kwasababu hakuwa akienda mwenyewe alitakiwa pia kuzingatia hali ya kiafnya ya Rufi na ndio maana aijiambia ni kheti kuharakisha kufanya safari na kwenda kutafuta hio mimea na kuanza harakati zingine.
Rufi alikuwa ashakubali kuongozana nae kwani hakuwa na shughuli ya maana ya kufanya Tanzania na maisha yake yalikuwa ya upweke sana na aliona ingekuwa kama utalii kwake kusafiri mpaka Australia.
Tatizo ambalo Roma aliona ni changamoto ambayo alipaswa kuitatua ni kwa mke wake , alijua akimuaga kwamba anaelekea Australia na Rufi angemuwekea ngumu lakini hata hivyo aliona lazima akubaliane na matakwa yake kwani anachokifanya sio kwa faida yake mwenyewe bali ni kwa faida ya wote.
Usiku baada ya Roma kupata chakula aliona ndio wakati muafaka wa kumweleza Edna mpango wake wa kusafiri na Rufi na Roma alimsubiria kwanza Edna amalize kumwandaa Lanlan kwa ajili ya kulala na ndio aongee nae.
Roma mara baada ya kukaa chini na kumuelezea anachopanga mwanzoni hakushangazwa na taarifa hio lakini Roma alipokuja kusema anataka kwenda na Rufi alihisi hatari.
Tokea aanze kuwa na ukaribu zaidi na mume wake alikuwa mwangalifu mno hakutaka Roma aongeze mwanamke kabisa na ndio maana hakutaka mazoea kati ya Rufi na Roma kuongezeka kwani mwisho wake usingekuwa wa kheti kwake.
“Najua unaweza kuona sio sawa mimi kwenda na Rufi lakini hili ni swala ambalo napaswa kulifanya na hata hivyo Arnhem sio sehemu ambayo ipo kiburudani ni kama gereza na kila kitu ni msitu hivyo kwenda na Rufi kule ni kama nampeleka kuzimu, hivyo mke wangu usiwe na wasiwasi na toa ruhusa yako niweze kuondoka nae”Aliongea Roma kwa unyenyekevu baada ya kuona mabadiliko yake.
Edna alifikiria na alionekana kama mtu ambaye amechanganyikiwa, moyo wake siku hizo za karibuni ulikuwa tofauti na zamani, alikuwa tayari kuona Roma akiendelea na wanawake wale wale aliokuwa nao na asione wivu lakini kumuona mwaamke mwingine mpya kwake ilimuuma na kumuogopesha kwa wakati mmoja na hata yeye mwenyewe alijishangaa na hata Roma alivyoweka wazo hilo akili yake ilimwambia na yeye aungane nae ili aweze kumlinda vizuri , lakini alifikiria uwepo wa Lanlan aliona asingeweza kuongozana na Roma na kumuacha peke yake.
Wazo moja tu ambalo lilimjia katika akili yake na kuona ndio njia mbadala ni kumteua mtu mwingine wa kuongozana nae kwenda huko na ingekuwa rahisi kuzuia mahusiano kuibuka zaidi na zaidi
“Nimekubali unaweza kwenda nae lakini lazima uende na mtu mwingine pia”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.
“Mtu mwingine kwenda nae sio tatizo kwangu , nani unaona anafaaa kunisindikiza?”
“Mage”Aliomngea akiwa ni mwenye sura iliojaa usirias na kumfanya Roma moyo wake kupiga kite , alikuwa na mahusiano na Mage lakini alikuwa akiyafanya siri Edna asifahamu.
“Unashangaa nini Mage ndio mtu pekee ambaye unaweza kwenda nae ningewaruhusu mwingine lakini kwa walivyokuwa wadhaifu kwako wasingeweza kukuzuia kufanya jambo la kishenzi?”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.
Roma alikuwa na mahusiano na Mage lakini hakuwahi luyaweka wazi na ndio maana alikuwa kwenye mshangao bara baada ya Edna kutaja mtu wa kuongozana nae kwenda Australia kuwa Mage, hali hio ilimfanya kuvhanganyikiwa yeye mwenyewe kwa kuona Edna alikuwa akifahamu siri yake halafu alikaa kimya.
"Mbona uko hivyo au Mage hafai ?"
"Sio kwamba hafai lakini kuna ulazima wa kutangulizana na mwanamke?"
"Ndio nataka utangulizane na mwanamke tena mwanamke huyo akiwa Mage ndio mtu pekee ambaye anaweza kukuzuia usifanye ujinga na Rufi na ndio sharti langu"Aliongea
"Edna ulifahamu lini?"
"Kuhusu nini?"
"Mimi na Mage tuna mahusiano" Aliongea Roma kwa ujasiri lakini kwa hofu ndani yake na swali lake lilimfanya Edna kucheka kidogo kwa uchungu.
"Hilo swali muulize Mage mwenyewe atakuwa na majibu" Aliomgea Edna na kisha hakutaka mazungumzo zaidi na kuondoka kwenye chumba hiko cha kujisomea na kumuacha Roma bado akiwa kwenye sintofahamu.
Ni kweli alikuwa na mahusiano na Mage lakini siku zote alikosa ujasiri wa kumuweka wazi Edna , lakini alishangaa Edna kutambua juu ya hilo bado lakimi aka kaa kimya bila ya kuzungumza.
Roma alijiuliza Edna alifahamu lini maana kama ingekuwa ni siku hio basi huenda angemnunia siku nzima lakini ajabu walikuwa sawa na hata siki yao iliisha bila shida.
Ila kitendo sasa cha Edna kuondoka wakiwa hawajamaliza mazungumzo alijua lazima angekuwa na hasira na yeye kutokumuambia ukweli lakini hata hivyi asingejuwa namna ya kujitetea kama hajui ni lini ameweza kujua ukweli.
Roma hapohapo aliona majibu ayapate kuroka kwa Mage mwenyewe , muda ulikuwa umeenda lakini alijua lazima Mage atakuwa macho na kweli baada ya simu yake kuita muda mfupi ilipokelewa haraka.
"Babe Mage mbona kama ulikuwa ukisubiria simu yangu"
"Mh ..! Roma vipi kuhusu Edna"
"Edna ana nini?"
"Mama leo kaharibu kila kitu"
"Kaharibu nini??"
"Sijui kaongea nini na Mkeo ila kamwambia kuhusu sisi baada ya Magdalena kakataa mchumba anaetaka kumuoa...."
Kwa maelezo ya Mage ni kwamba mtoto wa waziri wa sayansi na teknolojia afahamikae kwa jina la Jumbe alifika nyumbani kwa Mage na kuweka nia yake wazi ya kutaka kumuoa Magdalena jambo ambalo lilipokelewa kwa mikono miwili na Mama T.
Mwanamama huyu alikuwa ashachoshwa kuona watoto wake wa kike wakikosa ndoa ilihali wakina mama ambao ni marafiki zake watoto wao walikuwa wakiolewa na kuoa kwa sherehe kubwa na yeye kuishia kutoa michango pekee.
Na kilichompa shida zaidi ni kila mara alipofikiria Mage hawezi kuolewa tena kwa kuamua kuwa mchepuko wa Roma jambo ambalo hata mume wake alilibariki hivyo tumaini lake kubwa ilikuwa ni kwa Magdalena.
Alielewa watu wakiona Mage hajaolewa wangemnyooshea vidole na kumsema lakini kwasababu ilikuwa ni kwa ajili ya furaha yake hakutaka kumzuia lakini jambo hilo hilo hakutaka kuona likitokea kwa Magdakena pia na ndio maana Jumbe alupoweka nia yake wazi ya kutaka kumuoa mtoto wake alipokea taarifa hio kwa mikono miwili.
Lakini sasa kilichomshangaza ni baada ya Magdakena kukataa akisema hawezi kuolewa na Jumbe kauli ambayo ilimfanya kuhisi uchizi.
"Magdalena kama humtaki Jumbe inamaana tayari una mchumba kama ni hivyo mlete tumuone na nikiridhika nae nitakuruhusu uolewe nae" Aliongea Mama na kumfanya Mage aliekuwa amekaa upamde wa kushoto kushindwa kuongea chochote na kumuonea huruma dada yake kwani alikuwa akijua kike kilichokuwa kikiendelea kwenye moyo wake.
"Mama sina mchumba ila sipo tayari kuolewa na Jumbe" Alijibu Magdalena na kumfanya Mama T kushindwa hata kuelewa watoto wake wamekumbwa na nini , kwenye maisha ykje alijitahidi kuwalea kimaadili na kutegemea waje kuolewa na kuwa na furaha kakini imegeuka kuwa tofauti .
"Mume wangu mbona huongei chochote jamani hawa watoto wanataka kunitia uchizi?"
Afande Tobwe alikosa cha kusema kabisa kwani alikuwa ashajua muda mrefu sababu ya Magdalena kukataa ndoa na Jumbe , alikumbuka vizuri siku ya Roma alipokuwa akipambana na Yan Buwen namna ambavyo Magdalena alitaka kumuokoa Roma kwa kujitoa Muhanga yeye mwenyewe uhai wake.
Kwanzia kipindi hiko alikuwa akishindwa kujua tatizo la Magdakena linaisha vipi , kwenye maisha yake licha ya kuwa mwanajeshi likija swala ka familia yake alikuwa akizingatia zaidi watoro wake waje kuishi na furaha na ndio maana hata Mage alipo onyesha kuwa na mapenzi na Roma hakusita kumruhusu licha ya kujua Roma ana mke tayari na mwanae angekwenda kuwa mchepuko tu, lakini swala la Magdalena ilikuwa ngumu kumruhusu kuwa na mahusiano na Roma na wakati huo na pacha wake akiwa na mahusiano na Roma.
Jambo hilo kama angeruhusu jamii isingemuelewa na sio hivyo ru hata dini yake ilimzuia kuruhusu kitu kama hiko.
"Magdalena kama huna mahusiano, Jumbe anakufaa usikatae , najua kwa zama za sasa wazazi hawapaswi kuwachaguliwa watoto wao wachumba lakii siku zote mzazi anamuombea mtoro wake kuwa na furaha hivyo kuelewa ni kipi bora kwako , Jumbe anakupenda hivyo hata kama humpendi utajifunza"Aliongea Afande Tobwe kwa usiriasi na kisha akaamka na kuondokaneneo hilo la sebuleni.
Huku nyuma akiacha sura ya Magdalena kuwa katika hali isioelezeka , alitarajia baba yake kumuunga mkono lakini akaishia kumkandamiza kwa.kusimama upande wa mama yake.
Wakati wa mchana Edna alipofika dukani kwa ajili ya kutafuatilia mwenendo wa mauzo ya mavazi alioingiza sokoni kupitia kampuni yake kwa kutumia malighafi mpya ndio alipokutana na Mama T.
Walikuwa hawajaonana muda mrefu tokea Edna asafiri kwa ajili ya harusi yake hivyo waliongea sana huku Mama T akitaka kuona Edna alipendezaje na katika mwendelezo wa stori ndipo Mama T alipojikuta akiropoka kuhusu mtoto wake Mage kuwa na mahusiano na Roma.
Mwanzoni Edna alihisi kuna kitu kinaendelea kati ya Mage na mume wake lakini alikosa ushahidi wa wazi wa kuthibitisha kile anachowazia.
******
Upande mwingine nchini Rwanda mheshimiwa Jeremy alikuwa akizunguka zunguka kwenye ofisi yake huku na huko akionyesha kama mtu mwenye hasira nyingi na hio yote ni mara baada ya kupata taarifa ambazo zilithibitisha Kizwe ndio ambaye alimtorosha Desmond hospitalini wiki kadhaa zilizopita.
Raisi Jeremy mara baada ya kumtoa Desmond Tanzania moja kwa moja alimsafirisha mpaka India kwa ajili ya matibabu , hakuwa akiamini maneno ya daktari wa Tanzania kwamba mtoto wake hawezi kupona kiungo chake cha uzazi na ndio maana alikuwa radhi kufanya lolote kwa ajili ya mtoto wake huyo na isitoshe ndio ambaye alikuwa ni mrithi wake akitaratjia siku za usoni kumwachia nchi aiendeshe , lakini akajiuliza kama Demsond hatokuwa na uanaume wake je angeweza kuendesha nchi kisawasawa na jibu lilikuwa hapana.
Upande wa Desmond mara baada ya kushituka katika kupoteza fahamu na kujua hakuwa na uwezo tena wa kumfanya chochote mwanamke wakiwa kitandani alilia sana na kuomboleza na maumivu yake yalikuwa ni zaidi ya siku aliopokea taarifa za kifo cha mama yake.
Mpaka muda huo alijiona hakuwa ni wa thamani tena kama mwanaume na ndio maana alijawa na huzuni isiokuwa ya kifani huku lawama zote akimwangushia baba yake mzazi ,kwani aliamini kama sio matendo yake basi huenda asingepatwa na kadhia hio.
Ilikuwa ni adhabu kubwa mno ambayo Roma alikuwa amemfanyia , ilikuwa ni zaidi ya kifo kwake na hakujiona wa thamani kabisa.
Hata pale raisi Jeremy alipomtembelea katika wodi aliolazwa hakutaka kumuona kabisa na alitangaza waziwazi kwamba anamchukia na hali ilio iliamsha sana huzuni kwa Raisi Jeremy ,hakujua ni kwa namna gani angemsaidia mtoto wake kupona kwani alishakuwa tayari Eunuch ,kwa mtazamo wake hata kama angetaka kulipiza kisasi kwa Roma asingeweza na pia ingekuwa laana kwake kushindana na mkwe wake.
Kuna muda aliona huenda matendo yake ndio yaliokuwa yakimfikisha katika hali kama hio, alikuwa na mafanikio katika uongozi wake lakini likija swala la familia alikuwa amefeli pakubwa na alijiona kama mtu ambaye hakuwa na bahati.
Madaktari wa kihindi walijitahidi kufanya juhudi za kila namna ili kumponyesha Desmond tatizo lake lakini majibu hayakuwa na tofauti sana na yale ambayo yalitolewa Tanzania.
Kwa ufupi ni kwamba mtoto wake hakuwa mwanaume mwenye makali tena , taarifa ambayo ilikuwa mbaya sana na kuishia kumlaani Roma kwa kumfanyia hivyo mtoto wake.
Wakati akiendelea kutafakari namna gani ya kumsaidia Desmond akiwa nchini India kwa siri, ndipo alipopokea taarifa za Desmond kutoweka hospitalini kwa hali isiokuwa ya kueleweka jambo ambalo lilimshangaza mno na sio kwake tu hata vitengo vya ulinzi vya hospitali vilishangazwa na jambo hilo kwani hakukuwa na Kamera yoyote ilionasa tukio la Desmond kutoroshwa na kitu kingine zaidi ni kwamba CCTV Kamera zote zilikuwa zikifanya kazi.
Kwa maelezo hayo mafupi alioyapata Raisi Jeremy alijua moja kwa moja Kizwe atakuwa anahusika katika hilo.
Tokea siku ambayo aliweza kupata taarifa za Kizwe kuwa hai kutoka kwa Linda ilimshangaza sana Raisi Jeremy kwani ilikuwa ni taarifa ambayo kwake ni kama anaambiwa mfu kafufuka , alishuhudia yeye mwenyewe kifo cha mke wake na kumuona akizikwa inakuwaje akawa hai.
Linda hata yeye mwenyewe alishindwa kuamini kama Kizwe alikuwa hai , aliweza kupata kuigundua sura ya Kizwe siku kadhaa wakiwa wanafanya uchunguzi ndani ya chuo cha taifa cha Rwanda mara baada ya Lekcha kupotea na walipoangalia kamera za Chuo ndio walipoweza kuona sura ya mwanamke anaefanana na Kizwe kabisa akiwa katika ujana.
Tena inasemekana wakati Kizwe anaondoka na Lekcha katika chuo hicho Kizwe aliangalia Kamera ya ulinzi na kisha akatabasamu kifedhuli na kutamka maneno kwa namna ya kuonyesha ishara za midomo yake, alifanya hivyo kama mtu ambaye aliamini kabisa Footage za sura yake zingemfikia Jeremy.
Katika rekodi hio ya camera Kizwe alikuwa akionyesha ishara kama ya kumtahadharisha Jeremy kwa kumwambia kwamba anarudi kulipiza kisasi.
Baada ya taarifa ya mwanamke anaefanana na Kizwe kumfikia raisi Jeremy kwanza kabisa hakuamini na aliweza kupitia hatua zote tano za mshituko ili kujibu hali ya taarifa hio na baada ya masaa mengi ya kufikiria ndio uamuzi wa kufukuliwa kaburi(exhumation) la Kizwe kwa siri sana ufanyike nyakati za usiku kazi ambayo iliongozwa na Linda.
Na ilichukua siku tatu kwa mchakato wote kumalizika na mara baada ya raisi Jeremy kuwekewa majibu mezani alijikuta akipagawa , mwili ambao ulifukiwa haukuwa wa mke wake Kizwe kwani vinasaba vilithibtisha hilo.
Sio kwake tu ambaye alishangazwa na hilo lakini hata Linda pia alishangaa na kutaka kuthibitisha hilo na hapo ndipo walipoanza kuwasiliana na wanasayansi na vitengo vya serikali nyingine ili kuweza kuthibitisha uwezekano wa mtu aliefariki kufufuka na katika majibu mengi ambayo walipokea moja wapo ni kesi ya siri sana iliomtokea raisi mstaafu wa China lakini kesi hio hio ikajirudia nchini Tanzania baada ya mwili mtoto wa tajiri wa makampuni ya Maya kuonekana akiwa hai mara baada ya kifo chake kuthibitishwa.
Taarifa zilikusanywa kwa kutumia idara za kitelijensia na zilipomfikia Raisi Jeremy ndipo alipotambua sasa jina la mwanasayansi Yan Buwen ambaye alikuwa amepewa hifadhi ya kufanya majaribio yake nchini Tanzania.
Intellijensia ya Rwanda iliweka kila kitu wazi na kweli Yan Buwen wakati wa maombolezo ya kifo cha Firsr lady alionekana kuingia nchini Rwanda , muunganiko huo wa matukio ndio ulikamilisha uchunguzi wa kuamini Kizwe alikuwa hai bado na aliehusika kumrudisha hai ni Yan Buwen.
Na Raisi Jeremy alijiona mjinga kwa kuona alizidiwa akili na mke wake na hata kitendo cha Lekcha kumbakisha hai ulikuwa pia ni mpango uliosukwa , hatari aliweza kuiona mbele yake na kuanza kumuogopa Mwanamke aliekuwa ni mke wake na hata ulinzi wake aliongeza maradufu huku akihakikisha Desmond mtoto wake hafahamu ukweli wowote kuhusu hilo.
Asichokijua raisi Jeremy ni kwamba Desmond ndio moja wapo ya watu walioshuhudia mama yake mzazi akifufuliwa na Yan Buwen na hata nyakati za maombolezo ya taifa alikuwa akijifanyisha tu kuwa na huzuni.
Baada ya kifo cha raisi Kigombola pamoja na Yan Buwen Raisi Jeremy alipata unafuu na safari yake ya kuhudhuria maziko ya raisi Kigombola ilikuwa na sababu ya ziada ambayo ni kuona uwezekano wowote ambao ungemkutanisha na mke wake.
Siku ambayo Fredi aliandaa Party ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na Edna na Roma kualikwa ndio siku ambayo pia hata yeye mwenyewe aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa Kizwe akimwambia afike Maple speed Resort kama anataka kuonana nae.
Lakini Kizwe hakuwa na mpango wa kuonana na Jeremy bali aliandaa mpango wa kumfanya Jeremy kushuhudia Kaka akimbaka mdogo wake kwa macho yake lakini kwa bahati mbaya mpango wake huo ukaja kufeli mara baada ya bangili aliovalishwa Edna kuingilia kati na matokeo yake ni Desmond kuharibiwa uanaume wake.
Sasa zikawa zimepita siku kadhaa tokea Desmond apotee nchini India huku akiamini moja kwa moja muhusika ni Kizwe ambaye amebadilika na kuwa wa tofauti sana , sio tu kwamba alikuwa amefufuka lakini pia akarudi ujana.
Asubuhi hio aliokuwa akizunguka katika ofisi yake ni mara baada ya Kizwe kumthibitishia Jeremy kwamba yupo na Desmond na ajiandae kuachia uongozi wa nchi , kauli ya Kizwe kwake ilikuwa kama ya vitisho na ndio maana alikuwa na hasira na kuzunguka huku na huko huku akikosa namna ya kumshughulikia mwanamke huyo ambaye muda huo hakumuona kama mke wake tena bali alimuona kama shetani.
Mbaya zaidi aliogopa kwa kuamini na Desmond atakuwa amejazwa ujinga na mama yake kwa wakati huo .
Ilikuwa kama laana kwake kwa baba wa familia kushindana na familia yake na jambo hilo lilimkosesha amani kabisa.
ITAENDELEA.
Hatimaye nimefika kwenye arosto sasa singano huna baya
 
SEHEMU YA 497.
NORTH POLE(NCHA YA KASKAZINI).
Ni katika maabara ambayo ipo ndani ya Manuari katika ncha ya kaskazini ya dunia ,alionekana Lekcha ambaye amevalia koti zito rangi nyeupe ambalo liliziba hadi miguu yake , lilikuwa ni koti maalumu la kimaabara na alikuwa amekaa kwenye kirefu kinachozunguka kwa mtindo wa kuchanua miguu.
Kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana ni ngumu sana kumtambua kama ni yule Lekcha aliekuwa Tanzania akijifanyisha kuwa muokota makopo.
Macho yake yote yalikuwa yapo kwenye skrini kubwa iliokuwa mbele yake huku vidole vyake akivichezesha kwenye batani ambazo zilikuwa ni za kupangusha , Data mbalimbali zilionekana kupanda na kushuka kwenye Skrini na kila alipokuwa akigusa kitufe cha Enter kanuni za kikemia zilizoungana ungana ungana zilionekana zikizunguka.
Taarifa zilizokuwa mbele yake zilikuwa ni za juu sana katika maswala ya kisayansi na tehama , ni taarifa ambazo nyingine zilionekana ni gunduzi ambazo hazijawekwa hadharani bado.
Kwa muonekano wake ni kama vile alikuwa mbele ya muda kwani vitu ambavyo alikuwa akifanya vilikuwa vikipita uwezo wa binadamu wa kawaida kufikiria.
Aliendelea kuchezesha vidole vyake kwenye touch on screen keyboard kwa haraka haraka sana huku akijilamba lamba lipsi zake na baada ya kumaliza alifumba macho na kisha akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akagusa batani ya Enter kwa mara nyingine na akafumbua macho yake na alivyoangalia kwenye Skrini macho yake yalichanua huku akionyesha msisimko wa furaha.
“That’s right … That’s right …mmm , yes you don’t say , You may be dead but I must say , you’re fucking genius”Aliongea huku akionyesha mshangao , alikuwa akimaanisha anaweza kusema Yan Buwen amekufa lakini amekubali ana uwezo mkubwa wa akili..
Muda huo mkao wake ulikuwa ni wa kuchanua miguuu na kwa mtu ambaye yupo nyuma yake asingeweza kugundua kuna mtu mwingine ndani ya eneo hilo.
Wakati Lekcha akiwa bize kutumia ubongo wake kuchambua data za kitaarifa alizoacha Yan Buwen upande wa kizwe alikuwa amejichimbia chini ya kiti alichokalia Lekcha akiwa ameshikilia rungu ya Lekcha na kuendelea kuipa joto la mdomo, alionekana alikuwa akimbusti Lekcha.
Sasa baada ya kusikia Lekcha anaongea yeye mwenyewe ndio ilimfanya Kizwe kuamsha kichwa na kumwangalia usoni kutaka kujua nini kimempa msisimko wa furaha.
“What is it!, A break through discovery?”Aliuliza akimaanisha kwamba ameweza kugundua kitu.
“Nishati ya Ant- matter ina matumizi mengi kiasi ambacho sikuweza kudhania”Alimjibu huku akiachia tabasamu lililojaa kebehi ndani yake na hilo ndio jibu pekee ambalo amempatia Kizwe.
Muda huo huo wakati wakiongeleshana, mlango wa kuingilia eneo hilo la maabara ulifunguliwa na alionekana Desmond ambaye amevalia jaketi la rangi nyeusi maarufu kama Black windbreaker huku akiwa na mwokano ambao haukuonyesha kujali kile kilichokuwa kikiendelea hapo ndani.
Alimwangalia mama yake aliepiga magoti katikati ya miguu ya Lekcha na kisha akatoa tabasamu la kejeli na kupotezea kile kinachofanyika.
“Roma is about to leave Tanzania”Aliongea akimaanisha kwamba Roma anakaribia kuondoka Tanzania.
Baada ya Kizwe kusikia sauti ya Desmond alisimama na kisha alichukua gauni lake na kulivaa bila wasiwasi kwani muda wote huo aliokuwa akifanya kazi alikuwa hana nguo yoyote mwilini na wala hakuona shida.
Yan Buwen aliweza kufanikisha kufufua mwili wa Kizwe lakini alionyesha kuna kitu alishindwa kukirudisha upya , Kizwe alipoteza ule utu na hisia zote kama mzazi na hata Desmond licha ya kumfahamu kama mtoto wake lakini alimchukulia kama msela na kwa Desmond hivyo hivyo alimuona mwanamke huyo sio mama yake kabisa kwani mabadiliko hayakuwa tu kimwonekano bali mpaka kitabia.
“Taarifa ilionifikia inaonyesha anatoka Tanzania kwa ndege ya kawaida kwenda Brisbane Australia”Aliongea Desmond mara baada ya Lekcha kumwangalia.
“Anatumia ndege?”Aliuliza hivyo akimaanisha kutokana na uwezo wake asingepaswa kutumia ndege zaidi ya kuteleport.
“Ndio na katika safari yake yupo na Mage Tobwe mtoto wa Kanali wa jeshi la Tanzania lakini pia ameambatana na msichana mwingine anaefahamika kwa jina la Rufi ambaye taarifa zake hazikupatikan”Aliongea .
“My , my he’s quite the gentlemen . As long as he is not coming to the North pole , I say we let him be”Aliongea akimaanisha kwamba kwasababu sio kwamba anakuja ncha ya kaskazini sehemu waliopo basi hawana budi kumuacha.
“Hauna shauku anaenda Australia kufanya nini?”
“Nina uhakika ni jambo ambalo halituhusu”Alijibu na kumfanya Kizwe ambaye ashamaliza kuvaa nguo zake kumgeukia Lekcha.
“Acha kuwa mjinga , kwanini tusitumie nafasi hii akiwa mbali kuwateka wanawake wake na kisha kumtishia nao”Aliongea Kizwe
“Unaongeea upumbavu. kama unaamini kuteka wanawake wake ndio kutaleta majibu ya unachokitafuta basi naweza kusema unajaribu kudharau uwezo wake au unataka kurudia makosa alioyafanya Yan Buwen , hukumbuki alivyoagiza watu wakamuue Queen, licha ya kwamba alikuwa mbali huko Ulaya aliweza kurudi kwa haraka na kuwaokoa”Aliongea.
“Tutaenda sisi wenyewe kuwakamata na sio hao Cyborgs, nina uhakika tunaweza kufanikisha hata kuteka wawili”Aliongea Kizwe na kumfanya Lekcha kutingisha kichwa kwa namna ya kusikitika.
“Mpaka sasa hatujui ni namna gani aliweza kumuua Yan Buwen , tunaweza kufanikisha kwenda Tanzania na kuwateka wanawake wake na kuwaua lakini Roma bado akawa hai ni kitendo hicho cha kujitakia kifo cha mapema”
“Kwahio unamaanisha tusifanye chochote?”
“Ndio maana yake, muda bado sana na hatuwezi kumshambulia, ngoja tujijenge zaidi na zaidi , Yan Buwen alikosea kwa kujiamini kupitiliza na hicho ndio kilimgharimu ,ijapokuwa alipanga namna ya kujirudisha hai lakini bado alikuwa amechelewa na kumfanya Roma aweze kugundua udhaifu wake wote , siraha pekee ambayo kwasasa tunaweza kuitumia kwa faida kwetu ni kwamba Roma bado hajui uwezo wetu halisi na nini tunamwandalia na kama tutaenda sasa hivi ni kama kujidhihirisha kwake na atachukua hatua ya kujihami”Baada ya kumaliza ngonjera zake aligeukia Skrini kwa mara nyingine huku akikagua data zinazoonekana.
“Kabla ya kuona haya maendeleo ya sayansi mawazo yangu yote yalikuwa ni kulipiza kisasi kwa yale alionifanyia mimi na baba yangu , lakini kwa sasa kisasi sio jambo tu ambalo linanifanya niwe hapa bali ni mipango yangu mikubwa zaidi zidi ya dunia, kama tukimuacha akiendelea kuwa hai ni hakika anaweza kunizuia nisifanikishe kileinachokiwazia…..
Kwa sasa tunapaswa kutulia kwanza bila ya kuchukua hatua na muda ambao tutafanya mashambulizi ni ya kummaliza moja kwa moja”Aliongea Lekcha kwa kujiamini alijiambia mwenyewe njia pekee ya kumshinda Roma sio kwenda kichwa kichwa bali ni kwa mahesabu makali sana , hakutaka kufanya makosa ambayo Yan Buwen alifanya na kubwa zaidi baada ya kushuhudia ukuu wa kile alichokuwa akifanya Yan Buwen hata yale mawazo ya kulipiza kisasi yalipotea na tamaa ya kitu kikubwa zaidi ilijijenga na alijiambis Roma kumkata mguu na kumuua na baba yake yaikuwa ni malipo ya kile ambacho ameweza kupata muda huo , hakutaka kuruhusu kisasi kichukue nafasi kwani ndio udhaifu mkubwa wa kushindwa na adui.
“Kuna watu wengi duniani ambao ni maadui zake na wanaandaa mipango ya kummaliza , Yan Buwen na yeye licha ya kuwa na nguvu kubwa lakini alifeli pia ,je unafikiri na sisi tutafanikiwa?”Aliuliza Desmond.
“Yan Buwen is nothing ,in the end he died in my hands , There is no room for failure .Only those who had thought a few steps ahead will receive the final victory”Aliongea huku akisimama kutoka kwenye kiti na alichokuwa akimaanisha ni kwamba Yan Buwen hakuwa kitu kwani mwishowe amekufa kwa mikono yake na kwake hakuna nafasi ya kufeli na watu ambao wapo mbele ya muda siku zote ndio washindi.
“Mpaka sasa nimeweza kuchimba kwa asilimia tisini na tisa kumbukumbu zake zote na kukusanya taarifa zinazohusiana na namna ya kulitumia jiwe la Kimungu na kwanzia sasa nitahakihisha narithi nguvu zake zote na kudhizibiti pamoja na kuboresha zaidi na Roma siku ambayo atakutana na mimi lazima aombe huruma yangu”Aliongea kwa kujigamba , chuki ambayo aliokuwa nayo Kizwe zidi ya Roma kusikia maneno ya Lekcha ilimfanya moyo wake kusuuzika mno.
“Kwahio unamaanisha tutarajie mambo makubwa zaidi?”
“Yap kwasasa tumuache kwanza afurahie maisha kwa kipindi kifupi huku sisi tukiendelea kumfatilia tukiwa gizani, niwahakikishe siku ambayo atakuja kuniona itakuwa ndio mwisho wa maisha yake”
“Natamani sana huo muda ufike”Aliongea Desmond na kisha akageuka kutaka kuondoka.
“Desmond unaondoka kweli?”Aliuliza Kizwe
“Sina cha kufanya hapa napaswa kurudi Rwanda”Aliongea na kumfanya Kizwe kumuonea huruma.
Baada ya mpango wao kufeli Denisi ndio ambaye alimfikisha hapo kwa ajili ya kufanyiwa matibabu ambayo yalichukua wiki moja na kiungo chake cha mwili kupona.
Tatizo la Desmond lilikuwa dogo sana , kama Yan Buwen alifanikisha kumponyesha Lekcha mguu wake mbovu kwa kucheza na DNA zake za mwili sembuse Desmond ambaye tududu yake ndogo iliolala.
Alichokifanya Lekcha mara baada ya Demsond kufikishwa hapo ni kumdunga sindano ya kiowevu cha teknonolojia ya Acceleration Growth ambayo ilivumbuliwa na kampuni ya Maya nchini Canada.
Teknolojia ambayo mara baada ya Yan Buwen kuipata aliongezea ubora zaidi kiasi kwamba ilifanya kazi ya kubadilisha seli za mwili zilizozeeka na kuweka mpya na ndiio maana Kizwe mwonekano wake ukabadilika na kuwa kijana zaidi na hiko ndio ambacho Desmond alifanyiwa zile seli ambazo Roma aliziua katika dushe yake zilibadishwa na kuwekewa mpya ambazo zilikuwa na nguvu zaidi.
Sasa kwasabab tayari alishapona na uanaume wake kurudi hakutaka kuendelea kuishi ndani ya hio Manuari akimwangalia mama yake mzazi akifanyana na Lekcha bila ya aibu.
Lakini hata hivyo hakuwa na majuto tena , alivyoletwa sio anavyoondoka na alijihisi kama mtu ambaye amezaliwa upya na msukumo wake wa kuishi ulikuwa ni ule wa kuona maadui zake wote wakifa mbele ya macho yake.
“Yeye na Denisi itawachukua muda mrefu sana kufanikisha kudhibiti nguvu ya jiwe la Kimungu kwa asilimia kubwa na nimeweza kugundua katika kumbukumbu za Yan Buwen kuna uwezekano wa kutengeneza jiwe lingine lenye robo ya nishati yote ambayo ipo kwenye jiwe halisi”Aliongea na kwa haraka haraka ilifanya kueleweka sasa kwamba Yan Buwen wakati alipokuwa Tanzania aliweza kutoa nguvu nusu yake na kutengeneza jiwe lingine.
Kwahio kwa lugha nyepesi Lekcha alibakiwa na jiwe ambalo lina nguvu nusu na ile ya Awali kabla Roma hajalipoteza.
“Kwahio unamaanisha.”
“Kikubwa kuhusu jiwe hili la kimungu ni nishati yake tu , kwa nje inaonekana kama vile ni jiwe lakini yote hio ni teknolojia ambayo imetumika kutrap(Kunasa) nishati ya ant-matter ndani yake ni teknolojia ambayo kama binadamu wakipata ufunuo basi huenda vichaa wanaweza kuwa wengi na ukawa mwisho wa dunia”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu .
“Kizwe wewe kazi yako kubwa ni kuniburudisha wakati nikijijenga ki uwezo na visasi vyako vyote nitalipa mimi”Aliongea
“I thought you were going to call me a bitch”
“Haha…in fact you are my favourite bitch..”Aliongea na palepale alimshika mkono na kumvutia kwake na kuanza kumpapasa na kadri muda ulivyososogea ndio miguno ya kimahaba ilivyozidi kutawala.
*******
Australia – Arnhem Land.
Licha ya kwamba haikuwa mwezi wa sita, mwezi wa baridi kali lakini katika ardhi ya bara mwa Arnhem hali ya hewa ilikuwa tofauti na maeneo mengi ya mwambao wa pwani.
Eneo lote lilikuwa likichukua zaidi ya kilomita za mraba elfu nane ,Arnhem hali yake ya hewa ilikuwa ni ile ya Ki’savanna na kipindi cha kiangazi jua lilikuwa likipiga kweli kweli na eneo kuwa na joto kali mno.
Ndio eneo la kale zaidi la kihistoria katika bara lote la Australia na ndio sehemu ambayo ilikuwa na maeneo mengi ambayo haya kusapoti maisha
Na watu wa asili wa Australia(Aboriginal) licha ya kuyakimbia maeneo mengi lakini kulikuwa na ushahidi mwingi wa kihistoria unaoturudisha nyuma zaidi ya miaka elfu hamsini iliopita.
Licha ya eneo hili kutokuwa na hali ya hewa ya kufanya watu kupendelea kuishi lakini bado watu walikuwepo , maendeleo ya viwanda ambayo yalifanywa na nchi ya Australia katika maeneo ya mijini yalifanya maeneo hayo kuwa ya kitalii zaidi ndani ya nchi na hilo lilifanya watu wale wa asili zaidi kuendelea kuishi katika hayo maeneo na kufurahia faida zinazotokana na wale wanaotembelea.
Ni kama hapa Tanzania ufananishe na makabila kama vile wamasai au Hadzabe ambao bado wanaishi kitamaduni na maeneo yake kufanya kuwa kivutiio basi ni kama ilivyo ndani ya eneo la Arnhem.
Ni eneo ambalo lilifaa kutembelea zaidi kuliko kuishi na mazingira yake hayakuwa ya kuvutia bali yalikuwa yakishangaza zaidi na ni hatarishi vilevile , ukiingia ndani ndani zaidi huko misituni kuna wanyama wengi wakali huishi huko.
Wakati baadhi ya watalii wakiendelea kushangaza macho yao chini , angani ilionekana ndege ndogo ya wastani , ni ndege ambayo ilikuwa chini ya Roma na kabla hajaanza safari yake kutoka Tanzani alikuwa ashatoa taarifa ya ndege hio kusafiri mpaka Brisbane kwani ndio ambayo ilitakiwa kuwachukuwa na kuwapeleka Arnhem Land.

“We’ve now entered the hinterlands, highland grassland , two hundred and seventy meters above sea level , the temperature on the ground is ninety-three Fahrenheit. The Plane now will begin its descend”Alisikika rubani akimaanisha kwamba washaingia upande wa bara, nyanda za juu nyikani, mita mia mbili na sabini kutoka usawa wa bahari , nyuzi joto 330 C(930F) katika ardhi na ndege itaanza kushuka.Baada ya kutoa ripoti hio alisubiria maelekezo kutoka kwa Roma.
Wakati huo kwenye kajichumba ndani ya ndege hio alionekana Mage ambaye miguu yake yote imezunguka kiuno cha Roma na kujifunga nyuma huku upande wa Roma akiwa amesimama akiwa anacheza boringo , kwa jinsi Mage alivyokuwa akionekana ni kama vile dunia ilikuwa ikimuadhibu.
Upande wa Rufi alikuwa peke yake na macho yake yote yalikuwa nje kuangalia mandhari na hakutaka kufuatilia kinachoendelea upande wa pili kwani kilimtia wivu na muwashwasha kama mwanamke.
Hata hivyo alijua nia ya Edna kumfanya Mage aambatane nao kwenye safari hio yote ilikuwa ni kumuweka Roma chini ya uangalizi ili kusitokee kitendo chaochote cha kufanyika matendo ya ki usaliti.
Roma mwenyewe aliondoka Tanzania akiwa hajamalizana na mke wake , alikuwa amemnunia lakini kwasababu safari ilishakaribia hakutaka kupoteza muda sana kumbembeleza kikubwa tu ni kwamba alishapatiwa ruhusa na ndio maana akaja na Mage.
Baada ya taarifa kutoka kwa Rubani ilibidi Roma aghailishe kile alichokuwa akifanya na kisha akatoka huko na kuja kuungana na Rufi.
Wote walikuwa wamevalia mavazi aina ya Camo, ni mavazi flani ya mchanganyiko wa rangi ambayo yanafanana na yale yanayovaliwa na wanajeshi.
Rubani aliwapa taarifa ili wajiandae kujirusha kwenda msituni kwani ndege hio isingekuwa na uwezo wa kutua chini , Mage alikuwa polisi lakini kwenye maisha yake hakuwahi kufikiria kama angekuja kujiusha kutoka kwenye ndge kwani waliofanya mara nyingi kama hivyo ni wanajeshi.
“Hatuwezi kumwambia Rubani aishushe ndege hadi chini”Aliongea kwa wasiwasi kiasi cha kujionea aibu maana alikuwa mwanajeshi halafu anashindwa hata na Rufi ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi.
“Haiwezekani ndege kutua, ardhi haijanyooka na chini kuna miti mirefu njia pekee salama ya kushuka ni kwa kutumia parashuti na nishaandaa kila kitu kwa ajjili ya kujirusha”Aliongea Roma
“Ndio maana Edna akanichagua kuja huku inaonekana hanipendi kabisa”Aliongea kwa kulalama na kumfanya Roma acheke.
“Nilishakuambia huku sio kwa ajili ya utalii bali ni kama kwenye mateso”Aliongea Roma huku akicheka ijapokuwa angepaa tu na kwenda kutua chini lakini kutokana na kumiss sana kuruka kutoka kwenye ndege kijeshi aliona afanye kama binadamu wa kawaida.
“Pilot open the hatch”Aliongea akimaanisha afungeu mlango mara baada ya kuhakikisha wote wapo tayari na palepale mlango wa ndege mkiani ulifunguka na kufanya upepo mwingi kuingia ndani na mabegi yao ndio yaliokuwa ya kwanza kushuka kwenda chini.
Safe trip Your Majesty Pluto”Sauti ya Rubani ilisikika ikimtakia safari njema na palepale Roma alimpa ishara Rufi aanze kuruka na bila ya wasiwasi alisogea na kisha akajirusha chini , hakuwa muoga na alikuwa na mchecheto mno.
Baada ya Rufi kuondoka Roma alimshika kiuno Mage vizuri na kisha alimsukuma mbele na wote wakadondoka kuelekewa chini.





SEHEMU YA 498.
Mage alifumba macho huku akisikilizia upepo na mapigo yake ya moyo kudunda kwa nguvu alikuja kuyafungua mara baada ya kuhisi walikuwa wakielea na upepo umepungua na alipoangalia Parashuti lilikuwa tayari lishajifungua.
“Bado unaogopa?”Aliuliza Roma kwa sauti kubwa kwani upepo ulikuwa mwingi na Mage aliangalia chini pasipo kujibu na kadri walivyokuwa wakishuka chini ndio miti ilivyozidi kuongezeka ukubwa na nyasi nyingi zilizokauka kuonekana vizuri zaidi.
Sekunde chache mbele waliweza kugusa ardhi na kumfanya Mage kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.
Rufi alikuwa tayari alkwisha kutua umbali kiasi kutoka walipotua wao na alikuwa ameshika kiuno pasipo ya kuwa na habari na parashuti lake lililojibwaga kwenye nyasi.
“Ningejua ningekuja na Miwani ya jua sio kwa kuungua huku macho”Aliongea Rufi maana muda huo jua lilikuwa likipiga sio mchezo iikuwa kipindi cha Vuli lakini kulikuwa na jua kali.
Roma aliokota mabegi yao ambayo ndio yalianza kudondoka chini na kisha kila mmoja akampatia la kwake na begi lake tu ndio kiasi lilikuwa zito kwani alibeba chakula na Rufi na Mage wao walikuwa hawajaweka vitu ndani kwani walitegemea kuhifadhi vitu watakavyopata kwa ajili ya kutengeneza vidonge vya kijini.
Mage alihisi joto kali kwenye mwili wake kiasi kwamba ni kama hali ya hewa ilimkataa na alichokifanya ni kuruhusu nguvu zake za kijini kutawala mwili wake ili kupoza na Roma aligundua hilo.
“Jitahidi usitumie kiwango kikubwa cha nguvu zako zote kujipozesha maana haijulikani tutakaa kwa muda gani kwenye hili eneo kwani ni mpaka tupate tulivyokuja kutafuta”
Ukweli Roma alimkataza kutumia uwezo wake aliopata ili mwili wake upate mazoezi ya ziada katika safari hio ili asije kuwa mnyonge wakati atakapo ingia katika levo ya Mzunguko kamil.i
Baada ya kutoa baadhi ya maelekezo aliwaambiwa wamsubiri na alienda kukusanya parashuti la Rufi na kisha akalitandaza chini sehemu inayonekana vizuri kutoka juu angani na kuchukua mawe na mchanga na kulizuia ili upepo usije kulipeperusha.
“Roma unafanya nini?”Aliuliza Rufi
“Ni alama kwa ajili ya ndege endapo ikiwa ni wakati wakuondoka , lakini pia ni alama ya mwanzo watu na rahisisha mambo ili kama tukifuatwa basi iwe rahisi kuona hii alama”Aliongea Roma na kumfanya Rufi sasa kuelewa na hata Mage pia kuelewa
Hawakuwa na vifaa vyovyote vya mawasiliano kwani safari yenyewe haikuwa na maandalizi makubwa na Roma alijiambia hata kama wangebeba vifaa hivyo visingefanya kazi kwenye eneo hilo kwasababu ya mtandao lakini vilevile chaji isingedumu sana , hivyo simu walikuwa nazo lakini ni kama za kupigia picha.
“Tunaachukua uelekeo upi kutoka hapa?”Aliongea Mage mara baada ya kuangalia ardhi yote iliokuwa ikitanuka kwenda mbali ,sio nyuma wala mbele hakuona mwisho zaidi ya miti na miinuko na sauti ya ndege , eneo hilo lilikuwa kama mbuga kwa mwonekano wake ni kama vile walikuwa katikati ya Serengeti lakini utofauti mkubwa wa eneo hilo ni ule ukavu wake kwani nyasi nyingi zilikaushwa na jua na ilikuwa dhahiri mvua haikunyesha kwa kipindi kirefu.
“Hapa inabidi tuanze kwa kuelekea Kaskazini maeneo ya katikati, asilimia kubwa ya wenyeji wanaishi katika mwambao wa pwani na kama tutakosa huko katikati basi tunaweza kuchukulia kama utalii tu”
“Ah.. unaitaje utalii na jua lote hili , haya ni zaidi ya mateso”Aliongea Mage alikuwa mtoto wa kishua ambaye maisha yake yote alizoea kukaa kwenye kiyoyozi hivyo kukumbana na joto la namna hio ni kama vile yupo jijini Dar, kwake ni zaidi ya mateso.Roma alimshika shavu na kisha akamsukuma mbele atangulie.
Matendo yao yalimfanya Rufi kuona wivu kwani walikuwa wakionyesheana mapenzi waziwazi bila hata ya kujali uwepo wake ,mbaya zaidi Rufi hakuwa amezoeana sana na Mage na mara nyingi waliongea lugha ya kiswahili ambayo hakuwa hata akiifahamu vizuri.
Walianza kutembea huku jua la mchana wa saa tisa likiwachakaza vibaya na kumfanya Mage kuanza kujutia kukubali kuja eneo hilo kwani alihisi kama vile alikuwa kwenye jangwa , kila alipokuwa akitembea kidogo alikunywa maji ili kujipoza .
Rufi na yeye aliishia kufuta jasho na mkono wake tu huku macho yake yote yakiwa ardhini kutafuta mimea ambayo ingekuwa sahihi katika kutengenezea dawa hizo , umakini wake ulimfanya Roma kuvutiwa na aliona huenda alikuwa akijitahidi kufanya yote hayo ili kumsaidia apande levo na mwishowe aje kulipiza kisasi chake na kuwa huru.
Baada ya kutembea kwa umbali wa kama kilomita tatu waliweza kufika juu ya kijimlima na kujitupa kwenye kivuli kwa ajili ya kupumzika na Rufi na Mage walitoa maji na kunywa.
“Roma huna kiu m chukua unywe kidog?”Aliongea Mage.
“Nyie kunyweni tu na msione labda nahofia kuyamaliza mwili wangu ninaweza kuendesha na kumaliza kiu pale inaponitokea”Aliongea Roma kwa lugha ya kingereza ili Rufi asipate shida ya kutafsri.
“Kwa jinsi unavyoongea unafanya sasa nikuone kama sio binadamu”Aliweka maoni yake Rufi huku akitabasamu.
Mage alikuwa mzuri na alijaaliwa umbo lakini upande wa Rufi alikuwa na kasura ka upole sana na mwili kiportable na jinsi jua lilivyompiga na rangi yake ya mchangayiko aliiva kama yai la kisasa na kumfanya kupendeza zaidi.
Baada ya kupumzika kwa dakika kama kumi na tano Roma ndio aliekuwa wa kwanza kusimama.
“Tutembeeni zaidi kwenda mbele kufikia lile bonde naamini kuna mto , tutatafuta eneo la mbali kidogo kupumzika”
“Kwanini tusiende kupumzika karibu kabisa na mto?”
“Tishio kubwa la Arnhem ni uwepo wa Mamba wakubwa maarufu kama Baru , kuna zaidi ya Mamba laki moja wanaoishi mitoni wenye meno marefu na wanaweza kukumeza mzima mzima na usinekane hata ukucha”Aliongea Roma na kuwafanya miili yao kusisimka kwa ubaridi wa uoga na kumfanya Roma kutamani kuwachceka.
“Msiwe na waswasi nitakuwa wa kwanza kufahamu uwepo wa Mamba hata kilomita kadhaa, hatuwezi pia kupumzika karibu na mto kwasababu ya uwepo wa Scorpion na mbu wengi,”
“Australia ndio makazi ya zaidi ya aina ishirini na moja ya Nyoka wenye sumu kali, tokea tunaanza safari nililikuwa nikijitahidi kuwa makini hivyo na nyie pia mnapaswa kuangalia kulia na kushoto”Alitahadharisha Roma
“Roma kwanini unajua mambo mengi kuhusu hili eneo?”Aliuliza Rufi na kumfanya hata Mage mwenyewe ashangae. Na Roma aliishia kutabasamu.
“Nimekulia mazingira hatarishi zaidi ya hili eneo wakati nikiwa nafahamika kwa jina la Thirteen , nishawahi kukaa kwa siku therathini na moja peke yangu katika milima ya Siberrian hivyo ninaweza kusema likija swala la ku’survive’ mimi ni mjuzi na maisha yangu yamenifanya niweze kujifunza Flora na fauna (wanyama na mimea)ya maeneo mengi duniani kwa namna ya kukariri ili kujihami ninapokuwa kwenye maeneo hatarishi lakini pia kufahamu ni mmea upi napaswa kutumia kama chakula na ni mnyama gani napaswa kuwinda na vilevile ni tahadhari gani napaswa kuchukua.
Aliendelea kuwahadithia njia nzima huku wakitembea kulifuata bonde ambalo waliamini uwepo wa mto.
Baada ya kutembea sana hatimae walikaribia karibu zaidi na kweli waliweza kuona mto unaotiririsha maji kiasi.
Muda uleule Rufi macho yake yalichanua mara baada ya kuona kitu ambacho walikuwa wakitafuta na alimpita Roma kwa haraka kusogea mbele lakini Roma palepale kwa spidi alimvuta na kumrudisha nyuma.
Mage mara baada ya kuona kwanini Roma kafanya vile mwili wake ulimsisimka baada ya kuona bonge la Mamba aina ya Baru likiwasogelea.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI:ISSAI SINGANO)SINGANOJR)

SEHEMU YA 499.
Roma alikuwa na uwezo wa kuwabeba wote na kurudi mjini kwa ajili ya kulala na tena asubuhi wakarudi kuendeleza utafutati , lakini kwa maelezo ya Rufi ni kwamba mimea mingi ya ajabu huwa inaonekana katika vipindi tofauti vya siku.
Kwa mfano kuna mimea ambayo ilikuwa ikionekana asubuhi asubuhi wakati jua likiwa linachomoza na kuna ile pia ambayo ilikuwa ikionekana usiku sana wakati wa mbalamwezi na kuna ambayo huonekana wakati wa jua linapozama.
Hivyo ili kuweza kufanikisha kupata aina yote ya mimea hio ya ajabu katika nyika hio ya Arnhem kwanza kabisa walipaswa kuwepo kwa vipindi vyote.
Sasa wakati wanafikia bonde karibu na mto tayari jua ndio linaelekea kuzama upande wa magharibi na ndio maana Rufi aliweza kuona mti ambao alishawahi kuona katika miliki za kijini.
Sasa ule mchecheto wa kukimbilia mbele ulimfanya asiwe makini na Roma ndipo alimposogelea na kumrudisha nyuma kwa haraka.
“Nishakuambia mtembee nyuma yangu muda wote”Aliongea Roma lakini Rufi bado hakuelewa nini ambacho Roma alikuwa akimaanisha lakini muda uleule majani yalianza kucheza cheza na sekunde mbele ndipo waliposikia mngurumo wa mnyama mkubwa akiwasogelea , alikuwa ni Mamba mkubwa mno akiwasogelea kwa kasi ya ajabu licha ya kuwa na mwili mkubwa.
Hali ile ilimfanya Mage kushikwa na ubaridi wa woga kwani ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia Mamba mkubwa aina ya Baru , Rufi awamu hii alikosa ujasiri na kukimbilia kujificha nyuma ya Mage huku akitetemeka.
Roma aliacha limfikie na ile linataka kumtia meno miguuni aliachia nguvu ya kijini ambayo ilikuwa kama wimbi la upepo na kumbeba mzima mzima yule Mamba na kurudishwa nyuma kwa kasi na kwenda kutua kwenye mti kiasi kwamba ule mkia wake kupinda , lakini licha ya pigo lile bado hakupoteza maisha bali aliamka tena na kuamsha mashambulizi.
“Pumbavu huyu mnyama anaroho ngumu sana ,nilijua pigo moja lakawaida linaweza kumuua”Aliongea Roma huku akimwangalia yule Mamba akimsogelea kwa mara nyingine japo awamu hii hakuwa na kasi zaidi kuliko mwanzo na Roma hakutaka kulipa nafasi tena ya kumpotezea muda ali’chaneli nguvu nyingi zaidi na lilibebwa mzobemzobe na kwenda kujigonga kwenye tawi na lilipodondoka chini lilitingishika kidogo tu na kutulia likiacha meno yake wazi na Roma alitabasamu na kuanza kupiga mluzi kwa furaha.
“Unapata wapi ujasiri wa kupiga mluzi kwenye hali ya hatari kama hii?”Aliongea Mage kwa kulalamika.
“Nilitaka kwanza niwaonyeshe nini maana ya hatari kwenye hili eneo , nishawambia kuna zaidi ya Mamba laki moja hivyo mnapaswa kuwa makini na kila chanzo cha maji mnachokikaribia”
“Rufi kuna kitu uliona kwenye huo mti?”
“Ndio”
“Huu mti kama sijakosea ni aina ya Eucalyptus lakini majani yake yapo tofauti kidogo na pia magamba yake ni ya rangi ya zambarau”Aliongea Roma akiuelezea mti uliokuwa mbele yao”
“Hapana huu ni m’cardinal ni miti ambayo ni adimu sana ndani ya ulimwengu wa kijini na inatengenezea pia vidonge vya kijini vya gredi ya chini”Aliongea mti uliokuwa mbele yao ni miti flani kama ile ambayo hutumika sana kipindi cha Christmasi unaweza kuita Christmas tree.
“Unasema miti pia inaweza kutengeneza dawa , mbona itakuwa ngumu kubeba”
“Hii miti mbona ipo mingi sana Tanzania?”Aliuliza Mage.
“Mage hii miti inaweza ikawa kweli ipo Tanzania lakini haina sifa ya kutengeneza vidonge , kinachoufanya mti huu kuwa na ubora zaidi ya kule kwetu nyumbani ni kwamba huu upo kwenye eneo la kihistoria, hili eneo licha ya kuonekana kama nyika lakini lina historia pana za kimila”Alichokuwa akimaanisha Roma ni kwamba mazingira ya eneo mmea ulipo ndio inaamua uwezo wake , Arnhem ni eneo la kihisitoria ambalo matambiko mengi yalifanyika hivyo kuna kiwango kikubwa cha nguvu za kiroho.
“Rufi kwahio tunachukua majani yake au tunafanyaje?”
“Kwa huu hatuhitaji majani wala mizizi mikubwa bali unachukua manyoya ya mizizi ambayo ni nyuzi nyuzi ambazo hazijaenda chini sana ardhini”Aliongea na kumfanya Roma kuona kila kitu kinasheria zake lakini hata hivyo hakujali zaidi ya kufanya kama alivyoambiwa na kuanza kuchimba na kuchukua vinyuzi nyuzi vya mti huo.
Roma baada ya kupata mafanikio ya mwanzo alijikuta akipata tumaini ya kupata kitu kikubwa zaidi kwani ndio kwanza wamefika.
Siku hio ya kwanza hawakupata shida yoyote ya kusumbuliwa na mnyama na baada ya giza kuingia walitafuta pango ambalo waliona ni salama na kisha wakajaza upepo godoro(air matress) lao na kuupiga usingizi , Roma hakulala kuhakikisha kila mmoja anakuwa salama.
Asubuhi asubuhi kulivyokucha wakati wanataka kujiandaa kuamka kuwahi kutafuta miti inayoota jua Rufi aliweza kuona mmea flani unaotambaa chini na kujifunga funga funga kwa kamba , ni mmea ambao ulikuwa na tabia ya kuchanua usiku maua yake na ikipita asubuhi tu yale maua yananyauka na kudondoka(Dragon knot plant), Roma baada ya kupewa maelekezo hakutaka kujiuliza mara mbilimbili alikusanya kila kitu na kutupia kwenye mkoba .
Siku ya pili ilipita siku ya tatu waliendelea kuzunguka kilomita na kilomita kusaka mimea kwani mpaka kipindi hicho hawakuwa wamepata ile mimea ambayo ingeweza kutengeneza vidonge ya uwezo wa juu lakini licha ya hivyo bado alikuwa na mimea mingi.
Roma kwakuwa alikuwa na Pete ya kufungua anga la Sumeru aliitumia kutupia baadhi ili kupunguza uzito.
Siku ya nne ilipita na yenyewe kwa haraka, Mage na Rufi ni kama sasa washaanza kuzoea kulala vichakani kwani hawakumtegea Roma tena kutafuta mahali salama pakulala
Siku ya tano chakula kilikiwa kishaisha na kilichobaki maji tu, Roma alipendekeza asubuhi awaache hapo na kisha aende mjini kununua mahitaji na kurudi lakini Mage alipendekeza Roma atafute namna ya kuwasiliana na ndege waliokuja nayo kuwafuata ili kurudi mjini maana ashachoka kukaa polini kama ngedere..
Ni muda wa usiku wakati Roma akitaka kuyafumba macho yake ili kupumzisha ubongo mara alihisi msuguano wa hewa ukiongezeka kuzunguka eneo walilokuwepo kiasi cha kufanya mwili wake kusisimka na alisimama haraka kwa tahadhari.
Aliachia utashi wake kutawaliwa na nguvu ya kijini ili kuweza kutambua hatari iliokuwa ikimkaribia na palepale alipotea na kisha akaibukia mita kadhaa mbele.
“Wewe ni nani?”Aliuliza kwa sauti.
Rufi na Mage baada ya kuona Roma kaondoka kwa haraka na wao walitoka kwenye godoro na kusogea upande wake kujua nini kinaendelea.
Muda ule ule alitokea mtu kutoka angani mwenye nywele zake za njano ndefu mno kiasi ambacho sio cha kawaida alikuwa kama mzimu uliofufuka na nguo zake ziilikuwa za kitamaduni zaidi kama zile walizokuwa wakivaa warumi enzi hizo na sura yake haikuonekana kutokana na kuvaa Mask kama kinyago ya chuma(Cloack).
Roma alijikuta akikunja ngumi yake sio kwa hasira bali kwa hofu, hisia zake ni kama zilikuwa zikimwambia mtu ambaye yuko mbele yake ana nguvu kuliko za kwake.
“Who the hell are you?”Aliuliza kwa mara ya pili Roma kwa sauti ambayo ilisambaa kwa kasi kutokana na usiku.
“My identity is not important , the important thing is that you know that you’re no match against me”Aliongea akimaanisha kwamba ubini wake sio muhimu lakini jambo la muhimu ni yeye kuelewa kwamba hana uwezo wa kupambana nae.
Mage na Rufi walijikuta wakishikana kwa woga na kwa muda huo hawakuwa na chakufanya kwani hawakuwa na nguvu yoyote kusema kwamba wangeweza kumsaidia Roma , kitu pekee ambacho walikuwa nacho ni wasiwasi zidi yake.
“Nimeweza kukupata baada ya kukutafuta kwa siku tano mfululizo na nimepoteza muda mwingi sana , hivyo nitakupa chaguzi mbili ili tusipotezeane muda, chaguzi ya kwanza salimisha andiko la urejesho usio na kikomo kwa hiari yako, chaguzi ya pili nimimie mwili wako na kuutawala na kisha nichukue mwenyewe kwa lazima, chaguzi ya pili ni hatari zaidi kwani nitakuvua nguvu zako zote”Aliongea
Roma alikuwa amekasirika sio mchezo , kwenye maisha yake alikuwa akichukia sana uchokozi wa waziwazi na watu wenye kupenda majigambo , ijapokuwa mtu aliekuwa mbele yake alionekana huenda akawa na uwezo mkubwa kuliko wa kwake lakini siku zote hakuwa na hofu ya kupambana ni bora afe kwenye ulingo kuliko kukimbia.
Msuguano wa hewa ambao alisababisha yule mtu haukuwa wa kawaida kabisa na hili lilimfanya Roma kushindwa kujua anakwenda kupambana na mtu gani kwani hakutaka kujidhihirisha kwa kujitambulisha.
Roma alijiambia huenda angekuwa na uwezo wa kudhibiti radi kama alivyofanya mtu ambaye upo kwenye mwili wake angekuwa na uhakika wa kushinda.
Akiwa amekunja sura aliwageukia Rufi na Mage na kuwaangalia namna waliyyokuwa na wasiwasi ,
“Kimbieni kadri ya uwezo wenu wote muondoke hili eneo , sitokuwa na uwezo wa kuwalinda mkibakia hapa”Aliongea Roma na Mage alitaka kuongea neno lakini Rufi mara moja alishamwelewa Roma alichokuwa akimaanisha hivyo alimshika Mage mkono na kumvuta na wakaanza kukimbia kwenda mbele zaidi gizani, hawakujali tena kama kuna wanyama wakali au nyoka ambao wanaweza kuwadhuru.
Kadri walivyozidi kwenda mbali zaidi ilimfanya Roma kupata ahueni alijua kama wangebakia kwenye hilo eneo asingeweza kupambana na wakati huo huo akawa anatoa ulinzi.
Kitu kingine alijua lazima mtu aliekuwa mbele yake ametokea kati ya jamii za kichina za Hongmeng kwasababu alikuwa na uelewa na mbinu yake ya urejesho ya kimaandiko isiokuwa na kikomo , hivyo kwa haraka haraka alijiambia kama akiliamsha akashindwa pambano moja kwa moja angejaribu kutumia kanunzi za anga ili kuwashitua miungu wenzake waje kumsaidia kwani mtu huyo kuja mpaka Australia ilikuwa ni kuvunja vipengele vya kikanuni vilivyopo kwenye The gods treaty.
“Unajaribu kutumia kanuni za anga ili kuwataarifau wenzako?”Aliuliza yule mwanaume kwa lugha ya kingereza huku akionyesha utulivu wa hali ya juu na hilo tu lilimpa hofu Roma.
“Kama unapanga utumie mbinu hizo siwezi kukupa nafasi”Aliongea na palepale alianza kunung’unika kwa lugha isiokuwa ikieleweka na palepale Roma alihisi ubaridi wa hali ya juu mno ukimzunguka pande zote , alijitahidi kutumia akili yake kihisia ili kugundua ni mbinu gani imetumika na alipokuja kuigundua alijikuta akitoa macho.
“Dark Ice soul!!”
Roma alitoa mshangao mara baada ya kugundua mtu alievalia Mask mbele yake alikuwa akitumia mbinu ya Dark ice Soul , alikuwa akiitambua kutokana na kwamba katika maongezi yake na Zenzhei kabla ya kuanza safari kuelekea miliki za kijini, Dark Ice soul ni mbinu ambayo hutumiwa na wazee wa Hongmeng.
“Haha.. naona uko vizuri kwenye kuelewa kwa haraka , ndani ya huu mduara mbinu zako za anga hazifanyi kazi hivyo hakuna yoyote ambaye anaweza kuja kukusaidia”Aliongea kwa cheko la kebehi.
“Wewe ni sehemu ya wazee wa Hongmeng?”.
“Unauliza sana maswali , ninakupa nafasi ya mwisho jisalimishe kwangu na unipatie ninachotaka “
“Njoo uchukue kama una uwezo huo”Aliongea Roma kwa kiburi akimaanisha kwamba hakuwa tayari kujisalimisha.
“Very well , you asked for this”Aliongea akimaanisha kwamba vizuri sana kwa aliloomba.
Yule mwanaume baada ya kusema vile aliinua mikono yake kama vile wale waongoza kwaya kanisani wanavyofanya na aliipopandisha kwenda juu na kushusha chini na kisha alitoa tamko la kijini.
“Mvua nyota barafu , Mazingahombwe …!!!!”
Aliongea na palepale Roma aliona vitu kama vinyota vyota vilivyokuwa kwenye mfumo wa barafu vikiamka kutoka ardhini na kumsogelea kwa kasi.
Rufi na Mage waliokuwa mbali walichokishuhudia ni kama vile wanaona vimulimuli(firefly) wakitoa mwanga mweupe kwa kuamka kimakundi.
Roma mpaka hapo aliona kabisa mtu aliekuwa mbele yake kwanza kabisa hakuwa na hofu na kwa kumsoma kimawazo tu aligundua huenda anadhaau uwezo wake kwa kuona hana lolote la kumfanya hivyo njia ya pekee ambayo aliona ingemuokoa hapo ni kutumia kanuni za anga.
“Unseal , Space barrier!!!”
Aliongea kwa nguvu huku akichezesha vidole na palepale ulitokea mlipuko wa aina yake huku eneo alilosimama anga lake ni kama vile linacheza cheza na vile vinyota vyota vya barafu vilianza kukusanywa sehemu moja katika anga msambo(Pareller space).
Lakini yule mvaa Mask alitoa tabasamu la kejeli akimwangalia Roma alichokuwa akifanya na alishusha tena mikono yake kutoka juu kama anaimbisha kwaya na viliamka vinyota vingine vingi sana na kumvaa Roma na vilianza kutengenza nguvu ya mvutano ya kiasi kikubwa mpaka kumpelekea Roma kuhisi maumivu makali, ilikuwa ni kama vile nguvu zake zinafyonzwa na mwili wake kugeuka barafu.
Kwa staili hio alijua huenda mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ashaipita tayari levo ya Dhiki na kufanikisha kuweza kudhibiti elementi za maji na moto katika dunia, ilikuwa levo ambayo Roma hakuwa amefikia licha ya kwamba wote walikuwa kwenye levo moja.
“Umekuwa na akili kutegemea zaidi kanuni za anga kuliko mbinu za kijini , ngoja nikuambie hufikii hata nusu ya uwezo wangu na sio wewe tu hata mtangulizi wako Hades hawezi hata kunisogelea”Aliongea na kumfanya ?Roma apandwe na hasira maradufu na palepale alibadili mbinu na kurudi kwenye mbinu za kijini na kuita moto wa njano na kufanya eneo lote kuwa na mwanga kama vile msitu unaungua huku akidhamiria kuyeyusha hali ya baridi iliokuwa imemzingira maana ilikuwa ikimkosesha pumzi.
Baada ya kuona zoezi la kwanza lilifanikiwa alitumia tena kanuni za anga na kisha akaunganisha na ule moto kuyeyusha vile vinyota ambavyo amekusanya katika anga msambo.
“Space Tremor!!!”
Aliongea kwa nguvu na anga lilianza kutetemeka kama vile ni nguo ilio loana inayotingishwa ili kukausha maji yake na vile vinyota vilirudi chini na palepale akaachia moto mkari ili kuviyeyusha na kilichosikika ni mlipuko mkubwa ambao ulimrudisha nyuma yeye mwenyewe huku akihisi maumivu ya kiwango kikubwa mno ilikuwa ni kama yule mtu alikuwa amemwekea mtego.
“Nishakuambia kanuni zako za anga hapa haziwezi kufanya kazi kwa ufanisi hata wa asilimia hamsini , jifunze kukubali kushindwa”Aliongea lakini Roma alikuwa na kiburi cha kuzaliwa hivyo hakuwa akikubali kama alishindwa na alianza kujikusanya upya lakini yule bwana aliona ni kama anapotezewa muda.
“Nitakupiga pigo moja lakini nitahakikisha hupotezi maisha kutokana na uhitaji wangu wa hilo andiko la urejesho, Ngoja kwanza ni kuonjeshe nguvu ya vipepeo wa kufikirika wa rangi ya pinki”
Roma mara baada ya kusikia anaandaliwa pigo hakutaka hilo litokee na alicho kifanya ni kukusanya uwezo wake wote ili kujitengenezea ngao kwani hakujua hata hao vipepeo wa rangi ya pinki ni nini na yule bwana aliona hilo na kisha akatoa cheko.
“Unachofanya hakitokusaidia?”Aliongea Roma na palepale kitu cha kwanza alihisi kitu kama upepo ulioambatana na harufu nzuri ya marashi yasioelezeka ukimpuliza lakini ghafla mbele yake hakumuona tena yule bwana bali alichoweza kuona mauza uza ya kundi kubwa la vipepeo wakimsogelea kwa kasi.
“Arghiiiiiii…”
Roma alijikuta akitoa kilio cha juu huku akijihisi mwili wake kutawaliwa na nguvu isiokuwa ikielezeka ambayo ni kama inaziba ufasaha wa mtiririko wa nguvu zake za mbingu na ardhi , hata nguvu ya andiko la urejesho ilionekana kufeli kudhibiti nguvu hio ya kichawi iliokuwa ikimtawala , alijihisi kama vile ni mgonjwa wa ugonwa ambao muda si mrefu ungemuua, Alijitahidi kudhibtii uwezo wake wa kufikiria lakini alishindwa na palepale alikosa mhimili na kudondoka chini.
Hata Mage aliekuwa mbali aliweza kuona Roma akishindwa na kudondoka mzima mizma , lilikuwa tukio la mara ya pili Roma akidhibitwa kwa staili ya ajabu , mara ya kwanza ni pale Yan Buwen alipomzimisha Roma na mara ya pili ndio hio ambayo ameweza kiona.
Rufi alimshikilia mkono Mage ili asifanye maamuzi ya kijinga na kumsogelea Roma , lakini alishindwa kuhimili uwezo wa Mage na alijikuta akimwachia huku yeye mwenyewe akikosa nguvu.
“Mage usiende utakufa”Aliongea kwa kingereza lakini Mage hakumsikiliza alitimua mbio kumsogelea Roma bila kujali hatari.
“Wanawake wako wanonekana kweli ni waadilifu , bado tu wanapata ujasiri wa kukufuata ili hali upo kwenye hatua za mwisho”Aliongea mara baada ya kuona Rufi na Mage wanarudi , Rufi alikuwa akimfukuzia Mage kumzuia asimsogelee Roma kwani ingekuwa ni hatari na Mage alikuwa akimkimbilia Romakwa kuona kwamba hawezi kumwangalia akifa bila ya kufanya kitu.
Roma alijitahidi kuamsha kinywa chake amwambie Mage asisogee lakini nguvu zilikuwa zikimwishia , alijitahidi kuita nguvu zake za kijini lakini uwezo huo ni kama hana kwani nguvu ya ajabu iliouvaa mwili wake ni kama vile ilizifunga.
“Mage nenda mbali usisogee…’Alijikakamua kwa mara ya mwisho kumzuia kwa kuongea.
“Acha kupoteza sauti yako , waage kabisa nikumalize nina mambo mengi ya kuhangaika nayo baada ya hapa, nakuahidi nitawaacha hai kwani kuua mwanamke asie na nguvu ni tusi kwangu , kubali kunipa ninachohitaji tumalizane au nichukue kwa nguvu”
Aliongea kwa dharau na palepale alitoka aliposimama na kumsogelea Roma kwa kasi huku akinuia kwenye Roho yake kumzimisha kabisa.
“BAM”
Ni kama vile kioo cha dirisha kinavyogongwa na bunduki au kupasuliwa ndio mlio uliosikika na palepale kilionekana kitu kama mshale ukimkosa kosa yule bwana mwenye Mask na kumfanya asimame kwa kiwewe asimsogelee Roma na ule ukuta wake aliotengeneza kumfanya Roma ashindwe kutumia kanuni za anga ulibomoka.
Lilikuwa ni pigo ambalo sio Roma ambaye amelifanya na alikuwa na mshangao ni nani ambaye amemsaidia lakini mtu mwenyewe hata hivyo hakuonekana , hata kwa yule bwana mwenye Mask alionekana kuwa kwenye mshangao vilevile kama Roma.
“Wewe ni nani , kama una uwezo mkubwa kuzidi wangu jionyeshe’Aliongea yule bwana mwenye Mask.
“Unajua kabisa huna uwezo wa kushindana na mimi na sitaki kukushambulia zaidi, kwanini usiachane na maigizo yako na ukatoweka kabla sijawaita miungu wengine”Sauti yenye mwangi ambayo haikueleweka ilikuwa ya mwanamke au mwanaume ilisikika na kumfanya yule bwana mwenye Mask kutetemeka ni dhahiri alikuwa aking’ata meno yake kwa hasira baada ya pambano lake kuingiliwa, alimwangalia Roma kwa hasira sana.
“Consider yourself Lucky”Aliongea akimaanisha ajichukulie mwenye bahati huku akimwangalia na hakuonekana kutaka kufanya shambulio lingine zaidi ya kupotea katika hilo eneo.
Na Roma ambae alikuwa amelala chini alianza kuhisi msuguano wa hewa ukipotea na hapo hapo alijua kabisa watakuwa washaondoka , yule bwana na mtu mwingine ambae alimpatia msaada kabla hajakutana na kifo chake.
Mage na Rufi baada ya kuona ameondoka walimkimbilia Roma na kumbeba na kumfanya aegamie huku akiwa kama vile ni mlevi aliepewa pombe za kienyeji(gongo) maana alikuwa akifumaba macho na kuyafumbua kama vile ni taa mbovu inayoungua.
“Ongea chochote Roma jamanii , nini kimekutokea?”Alianza kuongea huku akiangua kilio na kumfanya Roma ananyanyue mkono wake kivivu akitaka kumfuta machozi
“Usilie nipo sawa”Aliongea lakini Mage aliekuwa kwenye hofu aliudisha mkono wake chini.
“Uko hivi halafu unasema upo sawa , nini kimekupata unaniogopesha mwenzio”
Ijapokuwa ilikuwa mara ya pili kumuona Roma akidondoka mzima mzima na kuwa kwenye hali mbaya lakini hio ilikuwa ni kama mara ya kwanza kwake na ndio maana alikuwa hofu.
“Nadhani nimepuliziwa harufu ya sumu , sina nguvu yoyote na kichwa ni kizito mno nashindwa hata kuita nguvu zangu… , Daah nilijua kwenye maisha yangu hakuna sumu ambayo inaweza kunidhuru”Aliongea kwa mafadhaiko.na Rufi baada ya kusikia kauli yake alimsogelea ili kumkagua nini kimempata.
“Kuna mbinu yoyote ambayo alitaja wakati wa kukushambulia?”
“Ndio , amesema amesema ananionyesha Vipepeo wa kufikirika”
“Aaah.. Daah”Alimaka Rufi huku akisimama na kuziba mdomo kwa mshangao mkubwa na kumfanya Roma kukunja sura.
“Una ufahamu na hiko kitu?”Aliuliza lakini Rufi alishindwa kujibu kutokana na mshangao.






SEHEMU YA 500
NCHA YA KASKAZINI.
Ijapokuwa ilikuwa ni usiku nchini Australia upande wa Ncha ya kaskazini mwa dunia ilikuwa ni mchana wa saa sita lakini anga lilionekana kama saa kumi za alfajiri na nyota waliweza kuonekana angani kwa wepesi zaidi.
Eneo hilo kama ilivyokuwa Kusini mwa cha ya dunia ni aneo ambalo halikuwa likipata jua la kutosha na ndio maana muda wote kubakia sehemu yenye barafu nyingi na hata mchanga wake ulikuwa ni wa barafu na pale jua linapoonekana ni kama lile la asubuhi asubuhi ambalo linachomoza mara moja na kisha kupotea.
Katika mwinuko mmoja wa barafu(Iceberg) alionekana mtu ambaye alikuwa amesimama huku macho yake yote yakiangalia angani huku gauni lake la rangi nyeusi la malighafi ya halili liliishia kupulizwa na upepo kulia na kushoto kama ilivyokuwa kwa nwele zake.
Licha ya eneo hilo kuwa na ubaridi wa zaidi ya nyuzi joto hasi therathini lakini ngozi yake haikuonekana kuathirika sana na kufanya urembo wake usio tamithilika kuonekana vyema chini ya mwanga wa mbalamwezi
“Mwanamke huyo alionekana kuwa makini kufikiria jambo huku macho yake yote akiangalia angani kwa namna flani hivi kama kuna kitu ambacho alikuwa akiangalia kwa matamanio makubwa.
Muda huo huo nyuma yake alitua kutoka angani mwanaume alievalia Mask , alikuwa ni mwanaume yule yule aliekuwa akipambana na Roma Australia .
“That Hades boy is incompetent. Are you really sure he is the man in your prophecy?”
“Yule Hades mvulana hana uwezo kabisa , una uhakika ndio mwanaume ambaye yupo kwenye unabii wako?”Aliongea kwa sauti nzito akimwangalia yule mwanamke mrembo aliempa mgongo.
Athena hakugeuza sura yake kumwangalia yule mwanaume na aliendelea kuangalia juu angani kama vile mtu ambaye amekumbuka kitu flani ambacho kinamtia huzuni.
“He is not dead?”Sauti yake tamu ilisikika akiuliza kwamba je hajafa.
“Ni katoto kapuuzi sana, nilichokifanya ni kuonyesha theruthi moja tu ya mbinu zangu lakini tayari kashajikatia tamaa , nina uhakika hawezi kuwa tishio kwetu Hongmeng na hata ulipojitokeza kumsaidia alionyesha kupata ahueni kwani ni kama alishajua ndio mwisho wa maisha yake, Kwasasa ameumia lakini kutokana na nguvu ya andiko la Urejesho inawezekana hatokufa lakini sidhani kama atakuwa na uwezo tena”Aliongea huku akionekana kama mtu ambaye anajivunia kile alichomfanyia Roma.
“All is well as long as he is alive”Aliongea akimaanisha kwamba yote ni mema ilimradi tu hajafa na kisha akaendelea kuongea.
“There should be no errors in my prophecy , In the future some things need to be done to tweek the entire situation into reality”
“Hakuna makosa yoyote kwenye unabii wangu , siku za baadae baadhi ya vitu vinatakiwa kufanyika ili kufanya hali yote kuwa uhalisia”
“I’ve heard the king, saying that any failure to your prophecy are your own fault , Why can’t you just admit that you suck at prophecies”
“Nimesikia kutoka kwa mfalme akisema kufeli kwa unabii wako ni makosa yako mwenyewe, kwanini usikubali tu kuwa upo vibaya kwenye maswala ya kinabii”Aliongea
“Wewe mpumbavuu..!!!”Aliongea na palepale vitu vyote vilikuwa vikiwazunguka vilianza kucheza cheza kama vile ni boti iliyoeleela kwenye maji,
Mtikisiko wa ule mlima wa barafu ulianza kubomoka wote na kuwa unga unga wa barafu na yule bwana mwenye Mask baada ya kuona jambo hilo la kuogofya aliruka kurudi nyuma asijefukiwa na mchanga huo lakini palepale Athena alimfuata kwa spidi na kumkanyaga kifuani kwa kumuwekea mguu.
“Nimekosea madam , tafadhari naomba unisamehe”Alijitahidi kuongea kwani nguvu uliokuwa imembana haikuwa ya kawaida na ule ukijogoo wote ulitoweka.
Kwenye maisha yake hakuwahi kushuhudia uwezo halisi wa Athena na alijua fika akileta mchezo anaweza kuyeyushwa mara moja na ndio maana alijishusha mapema.
Kingine ilionekana saikolojia yake ya woga zidi ya Athena ilichukua nafasi yake na ndio maana alishindwa hata kujibu mashambulizi na kutulia kama kuku anaesubiria kuchinjwa , Athena aliemkanyaga alimwangalia kwa kejeli na macho yake ya kiini cha bluu lakini licha ya hivyo urembo wake ulidhihirika zaidi na zaidi.
“Know your place , Your King may not even stand chance against me and yet you are here spewing nonsense ? if this happen again next time I will make sure to turn you into dust”
“Ifahamu nafasi yako , mfalme wako anaweza asipate hata nafasi ya kushindana na mimi lakini bado upo hapa unaongea ujinga , hili likitokea tena nitahakikisha na kugeuza vumbi”Aliongea na kumuondolea mguu.
“Nilikuwa mjinga sana … sirudii tena … sirudii mimi”
Aliongea huku akipiga magoti haraka haraka na kupiga kichwa chake kwenye barafu na Athena aliachana nae na kisha akageuka na kuangalia upande wa pili kama kuna kitu anachokichunguza.
“Simama”Aliongea na bwana yule mwenye maski alisimama haraka kama mwanajeshi.
“Kazi yako kwanzia sasa ni kutafuta na kurekodi alama zote za kiuungu zilizoachwa na makabila yaliotambulika kama miungu ya enzi duniani kote kwa niaba yangu , kazi yako nyingine ni kuhakikisha unafatilia kinachofanyika ndani ya ile maabara nahitaji taarifa za kila siku juu ya maendeleo yao katika matumizi ya jiwe la kimungu na usije ukachukua hatua bila ya maagizo yangu”Aliongea na kumfanya yule mwanaume kutingisha kichwa.
Alichouwa akimaanisha Athena akisema alama za kiuungu ni kama zile ambazo zimeachwa na watu wa Sumeria , miungu ya Misri kama vile Odini na mingine mingi ambayo iliishi kikabila katika maeneo tofauti tofauti duniani kote , sasa haikueleweka kwanini alikuwa akitafuta hizo alama lakini huyi bwana mwenye mask alipewa kazi ya kuzitafuta na kuzirekodi kwa niaba ya Athena.
“Madam bado nimechanganyikiwa kidogo , ukiachana na wewe miungu wengine kama Poseidon na Apollo hawana uwezo wa kupambana na wazee wa Hongmeng pamoja na jamii nyingine zilizojificha , hilo pia sio kwao tu hata kwa Ares na Venus hawawezi hata kusimama kushindana na waliofikia levo ya Nafsi , kwanini umeweka juhudi zako zote kuelewa nguvu ya jiwe la kimungu ili kuwafufua ndugu zako ambao ni wa kawaida?, naamini hata kama waje kufufuka hawawezi kuwa na msaada kwako”Aliuliza na kumfanya Athena kutoa kicheko kikubwa kwa sekunde kadhaa na kisha akamgeukia na kumwangalia kama kituko.
“Unachotaka kumaanisha ni kwamba ukiachana na mimi na Zeus wengine wote hawana thamani si ndio?”Aliuliza na kumfanya yule bwana kutojibu swali lake.
Aliuliza kutokana na uelewa wake, kwani Hongmeng wote walikuwa wakimwogopa Athena tu na kama sio yeye huenda wangeshatoka kwenye miliki zao na kusambaa duniani kote na kuiba hadhina nyingi zenye thamani na hata Roma kwa muda huo angekuwa ashakufa muda na asingekuwepo kule Australia akitafuta malighafi.
“Kama unaamini uwezo wetu tuliokuwa nao ndio wa mwisho kabisa basi nikujibu umekosea , nitakuwa mkweli kwako , kwasasa tulichobakiwa nacho ni namna ya kutumia kanuni za anga pekee na ukiachana namna ambavyo napambana, mimi mwenyewe nimebakiwa na nusu ya uwezo wangu na wengine wote ambao ni dhaifu kuliko mimi na Zeus, uwezo wao ni chini ya asilimia ishirini”Aliongea na kumfanya yule mwanaume kurudi nyuma akionyesha mshangao.
“Unamaanisha?”
“Mbona unaonekana kama huamini?”Aliuliza Athena
“Sio hivyo madam … kama wewe umesema hivyo basi naamini ni kwel”Aliongea kwa hofu na kumfanya Athena kutabasamu.
“Huna haja ya kujilazimisha kuniamini nilichoongea , tokea siku ambayo tulikanyaga ardhi ya dunia nguvu zetu zilikuwa zikipungua kila siku mpaka kufikia hatua ambayo ni kama tunalingana na binadamu wakawaida”Aliongea huku akameza mate na kisha akaendelea.
“This is a humiliatition to us and this is where it hurts most , Not many are willing to bring that up, funnly the friars in Hongmeng had realy thought that we’re only truly capable of this”.
“Hili ni lenye kutudhalilisha na hili ndio linauma zaidi , sio wengi ambao wanapata ujasiri wa kuliongea wazi wazi lakini inachekesha kuona wafia mila(majini) wa Hongmeng wanafikiri uwezo wetu tuliokuwa nao ndio mwisho”Aliongea na kisha akapozi kidogo na kuendelea huku akigeuza uso wake na kuangalia juu angani.
“It won’t be long until I create the thing I desire most , Soon enouph the renaissance of the gods will take place”
“Haitochukua muda mrefu nitaenda kutengeneza kile kitu ninachokitamani sana , hivi punde tu mwamko wa miungu utaanza “Aliongea akiwa na sura yenye usiriasi na ni kama vile kuna watu aliokuwa akiwaongelesha angani kutokana na mwonekano wake.
“Hades kadri unavyopanda levo ndio nafasi ya unabii kutimia inakuwa kubwa , endelea na juhudi hizo hizo”Aliwaza Athena bila ya kueleweka alikuwa akimaanisha nini kusema Hades kadri anavyopanda levo ndio anavyozidi kuufanya unabii utimize lakini huenda ndio maana akamtengeneza yeye mwenyewe.
Sasa unachotakiwa kuelewa nikielezea Athena akitaja miungu anamaanisha watu wote waliotoka katika sayari nyingine na kuja duniani na ndio hao ambao anaelekeza kwamba muda si mrefu wataamka na kuchukua hatamu ya dunia.
Unafikiri atafanikiwa
********.
Huko Arnhem mambo hayakuwa mazuri sana kwa Roma kwani alikuwa bado akihangaika kuita nguvu zake za kijini lakini haziji kabisa , alikuwa ni kama binadamu wa kawaida tu.
Mage ambaye amekaa chini ya shina la mti alimwangalia huku akiwa na wasiwasi mwingi mno na kuomba Roma uwezo wake urudi , alijiambia kama akikosa uwezo wake wangefanya nini maana hawakuwa na kifaa chochote cha mawasiliano na kama wangeamua kutembea kurudi mjini ni zaidi ya kilomita na kilomita.
Rufi na yeye alikuwa kwenye wasiwasi akimwangalia Roma kwahali ya huzuni mno na alikosa kufanya chochote cha kumsaidia.
“Vipi bado imeshindikana?”Aliuliza Mage baada ya Roma kufumbua macho , alikuwa akijaribu kufanya tahajudi kuona angepata uwezo wa kuondoa nguvu ya sumu vipepeo iliokuwa kwenye mwili wake.
“Nimeshindwa kabisa kuita nguvu ya mbingu na ardhi , nahisi kama vile kiini cha uhifadhi wa nguvu zangu kufungwa , njia za mtiriko wa nishati ya mwili zinaonekana kusinyaa na mwili wangu umekuwa mdhaifu mno”Aliongea kwa huzuni.
“Kwahio unamaanisha kwamba umekuwa binadamu wa kawaida?”Aliuliza Rufi na kumfanya Roma amwangalie.
“Hii sumu ya vipepeo wa kufikirika ni kweli haiponi?”
“Mimi sijui , lakini nishawahi kusoma taarifa chache kuhusu maelezo yake na kwa ninavyojua ni sumu ambayo imetengenezwa na wadudu waliokuwepo enzi za kale sana jamii ya vipepeo ambao kwasasa wamepotea duniani , mtumiaji anachokifanya ni kuigeuza sumu hii na kuwa kama moshi wenye harufu ya kuvutia na pale unapovutiwa na harufu hio na kuivuta moja kwa moja inaenda kuleng neva za mwili na mtu aliekusudia uivute akiwa na nguvu kubwa za kijini basi moja kwa moja inaelekea katikati ya mwili sehemu ambayo ndio chanzo cha uwezo wako wote na kufunga moja kwa moja na ndio maana katika miliki za kijini sumu hii inatumika kutolea adhabu majini yanayo asi”
“Sio mbaya sana lakini , najihisi sasa hivi nimekuwa kama binadamu wa kawaida, hizi hisia sijawahi kuwa nazo kwenye maisha yangu”Aliongea huku akicheka.
“Unachekaje kwenye hali kama hio uliokuwa nayo , unachotakiwa kuelewa mpaka sasa upo sawa kwasababu ya mwili wako lakini kwa wengine huenda mpaka sasa wangekuwa wamepooza kabisa mwili”Kauli ya Rufi ilimfanya Mage atamani kulia na kumwonea huruma.
“Rufi kwahio unamaanisha hakuna namna yoyote ya kuiondoa mwili mwangu?”
“Katika nyaraka nilizosoma hakuna sehemu ilionyesha naman ya kuondoa , mpaka sasa naamini uliepambana nae alikuwa akikuogopa sana na ndio maana akaambua kutumia sumu kali kukudhibiti ,inaonekana hakutaka umzidi kwa namna yoyote”Aliongea na Roma aliona kauli ya Rufi ni sahihi , alijiambia kama sio mtu wa ajabu ambaye alitokea na kumsaidia basi hueda angeshakufa.
Aliamini kwa kufanywa binadamu wa kawaida basi muda sio mrefu mtu yule angerudi na kutaka nguvu yake ya andiko mbaya zaidi ni kwamba mtu yule hakuweza kumuona sura na alishindwa kuwa na uhakika kama alikuwa akitokea miliki za hongmeng au lah licha ya kuwa na uwezo ambao alielezewa na Zenzheu.
Hata hivyo Roma hakuwa kwenye nafasi ya kukata tamaa alijiambia lazima kuna namna ya kuondoa sumu hio mwilini na nguvu zake kurudi upya , alijiambia tena kama ni suluhisho linatakiwa kuwa la mapema , kwani alikuwa na maadui wengi.
Alifikiria na kujiambia kama atakosa msaada basi angewauliza hata Christen au Clark kujaribu mbinu za kawaida kumsaidia , hakutaka kukata tamaa ilihali tumaini bado lipo.
Roma aliwaangalia Rufi na Mage waliokuwa kwenye huzuni na Mage na Rufi wenyewe walimwangalia Roma na kushindwa kuongea lolote zaidi ya kukaa kimya katika hali hio ya giza.
“Kwasababu kwasasa hatuwezi kutatua tatizo langu , malengo yetu ya kwanza iwe ni kutoka humu nyikani , ningekuwa bado na uwezo wangu isingekuwa tatizo lakini kwasababu mambo yashabadilika haitokuwa rahisi kwani hatuna vifaa vya mawasiliao kusema tutaweza kuomba msaada lakini pia chakula ndio hiko kishaisha na hatuwezi kukaa chini kusubiria watu waje kututafuta , hapa inabidi safari yetu iwe ni kutembea kwa kulenga uelekeo ambao utatukutanisha na bahari kwa haraka labda tukiwa njiani tunaweza kukutana na mtu ambaye atatusaidia kurudi nyumbani, msiwe na wasiwasi kwani nina uzoefu wa haya maisha hivyo naamini tutatoka salama na mnisamehe kwa kuwaingiza kwenye jambo hili gumu , kwasasa hakuna namna bali safari yetu ya kujikomboa inakwenda kuwa ya mateso makubwa”
“Roma wewe…”Rufi alishindwa hata kuongea , ijapokuwa alifahamu fika alichongea ni kweli lakini kuwaambia wanakwenda kuteseka hakupenda lakini hata hivyo alifarijika kuona Roma hajakata tamaa.
“Kwanini unaniangalia kwa namna hio Mage, ngoja niwaambie kadri nitakavyokuwa naishi siwezi kukata tamaa kabisa, naamini tutaweza kupata suluhisho tu”Aliongea na kumfanya Mage kuguswa na maneno yake , huyo ndio mwanaume ambaye alikuwa akiomba katika maisha yake ajitokeze , mwanaume ambaye hayumbishwi na changamoto.
Kwa mwanamke anaweza kumpenda mwanaume ambaye ni wa kawaida ambaye hata hela hana lakini hawezi kumvumilia mwanaume ambaye hana malengo na muelekeo ambaye ana visirani pale mambo yanapokuwia magumu.
Muda huo wa Mage kujiwazia alijiambia hatokuwa mbaya pia kama atakufa na mpenzi wake akiwa hapo wamekumbatiana na ni muda wake muafaka kuteseka akiwa na mwanaume anaempenda huenda penzi lao likashamiri zaidi na zaidi.
“Mage acha kuniangalia kwa macho yako malegevu , mnaonanye mkarudi kulala kesho haitokuwa rahisi kwani tutatembea bila kupumzika kurudi pwani , naamini inaweza kutuchukua angalau siku tano mpaka kutoboa hivyo lazima tukusanye kila nguvu tuliokuwa nayo”
“Mhmh..!”Waliguna wote kwa kuambizana lakini waliishia kuitikia kwa vichwa vyao na kisha wakarudi eneo lao kwa ajili ya kulala.
Wakati wakiwa wamepotelea usingizini upande wa Roma hakutaka hata kulazimisha usingizi , licha ya kufikiria namna ya kurudisha uwezo wake kwa kuondoa sumu iliopo mwilini , lakini pia aikuwa na hofu kama adui yake akirudi.
Lakini licha ya mawazo mengi , alijiambia hana la kufanya kwa muda huo na ambalo lingetokea mbeleni ya safari basi hana budi kupambana kiume kuyaokoa maisha yake na ya warembo waliolala.
Unaonaje , ngoja lekcha ajue mwamba hana nguvu zozote uone
Tukutane kesho.

ITAENDELEA.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR.

SEHEMU YA 501.

Siku iliofuata kila mmoja alibeba begi lake na safari ikaanza rasmi , kabla ya kuondoka Roma alibeba makaa ya kuni zilizoungua na kuweka kwenye begi lake na kumfanya Mage kushangazwa na jambo hilo.
“Hubby si utachoka sana , kwanini unabeba hayo makaa , tunaweza kutokuwa na chakula lakini kuwasha moto njiani ni rahisi kwani tuna kiberiti”..
Tokea waanze safari alikuwa hajazoea kumwita Roma mpenzi kutokana na Rufi lakini mara baada ya Roma kupoteza uwezo wkae alijikuta akishindwa kujizuia.
“Haya makaa sio kwa ajili ya kuwashia moto , huko tunakoelekea maji hayatokuwa salama na yamejaa minyoo na sumu na pia hatuna uwezo wa kuyachemsha hivyo njia pekee ni kuondoa sumu yake kwa kutumia mkaa nadhani ni bora zaidi kuliko kuugua njiani kwa kuumwa na matumbo”Alielezea Roma huku akitabasamu.
Roma hakuwa tayari kuona wanawake hao wanapatwa na shida yoyote njiani kwani ingekuwa ngumu sana kutoka kwenye msitu huo kwasababu mwili wake ulikuwa na sumu na asingeweza kuwasaidia pale watakapopatwa na ndio maana alikuwa akichukua kila tahadhari.
Mage hakuwa amelifikiria hilo, hivyo mara baada ya kuelewa hakuuliza tena swali hata hivyo alikuwa mgeni kwenye mambo mengi.
Roma ndio ambaye aliongoza njia huku wakichukua uelekeo wa Kaskazini aliamini ndio upande ambao ungekuwa karibu zaidi na bahari kuliko kurudi walikotoka mwanzo, jua lilishaanza kuunguza licha ya kwamba bado ilikuwa ni asubuhi na kadri walivyokuwa wakisonga mbele Roma alikuwa akichoka mno na kuhema kwa nguvu kama ilivyokuwa kwa Mage na Rufi tu.
Kiasi kidogo cha unyevu nvyevu uliokuwa ukidondoshwa na miti ya msitu huo ulimfanya kuelewa kwanini watu hawakupendelea kuishi kwenye hayo maeneo, ilikuwa ni hali ya kisauna mwanzo mwisho.
Mage na Rufi lipsi zao zilianza kupasuka pasuka kutokona na ukosefu wa maji pamoja na njaa lakini kwa wakati huo walikuwa na wasiwasi zaidi juu ya Roma kutokana na sumu iliokuwa ndani ya mwili wake.
Njia yote waliotembea hakukuwa na maji zaidi ya vichaka tu ambavyo vilikuwa vimekauka kutokaa na hali ya ukame na baada ya kutembea mita kadhaa hatimae waliweza kufika kwene eneo ambalo lilikuwa kama bwawa ambalo limeacha tope tu kwa juu na palepale Roma alikata tawi la mti na kufukua lile tope na ndani ya dakika chache tu maji yalianza kuonekana na kuwafanya waangaliane kwa mshangao.
“Mara nyingi ukikuta sehemu yenye mto au bwawa lililoacha tope kwa juu jua chini yake kuna maji ni kama nadharia lakini naona tumekuwa na bahati”Aliongea na kuwafanya wafurahi.
“Ngoja nikusaidie”Aliongea Mage akiruka upande wa pili na akaanza kumsaidia Roma kupanua shimo kwa kutumia mikono yao, Rufi alijikuta akishangazwa na jambo hilo lakini mara moja na yeye aliungana na wakaanza kutengeneza kijidumbwi ili maji yakusanyike sehemu moja.
“Haina haja ya kunisaidia ninaweza kufanya hivi mwenyewe”aliongea Roma mara baada ya kuona wanachafuka.
“Acha kujifanya mgumu na utuache tukusaidie au unajisikia vibaya kwasababu hauna uwezo wako?”
“Ah..! sijamaanisha hivyo”Aliongea huku akimwangalia na aligundua tayari Mage alishajichafua usoni.
“Babe ushajichafua tayari baada ya kujishika pua yako”Aliongea na kumfanya Mage kweli aone amejichagua baana alijifuta na mkono wakushoto akidhania ni msafi.
Roma alijikuta akiguswa na namna wanawake hao wanavyochakarika , ijapokuwa alichokuwa akifanya sio cha kutumia nguvu nyingi lakini ushirikiano wao ulimfanya kuona kweli ana watu sahihi.
Baada ya kutengeneza kidumbwi maji yalianza kutiririka kutoka pande zote na kujaa.
“Yashajaa tayari lakini tunayatoaje hapa na kuyasafisha kwani yana matope?”
“Hio kazi ngoja niifanye mimi wewe angalia tu”Aliongea Roma na kisha akachukua nguo safi kwenye begi na kuiingiza kwenye kile kidumbwi na kisha akakamua kwenye kontena na baada ya hapo alichukua ule mkaa aliobeba na ndani ya dakika chache tu maji yalionekana kuwa masafi kabisa kwa ajili ya kunywa.
Kitendo kile kiliwafanya Rufi na Mage kushangazwa na mbinu zake za kupambania kuishi kwenye hali ngumu kama hio, baada ya kunywa na kutosheka walijaza ya kutosha kwenye makopo yao na kisha safari ikaendelea.
“Kutokana na Roma kukosa uwezo wake alijitahidi kuwa makini sana na vichaka kabla ya kuwaruhusu kupita , lakini bahai nzuti hawakuweza kukutana na hatari yoyote.
Wakati inafika muda kama wa saa tisa Rufi alijikuta nguvu zikimwishia kutokana na njaa na alitembea kinyonge mno akiwa amechoka kutokana na kukosa mazoezi tofauti na Mage na Roma.
Ilibidi wasimame na kumwangalia alivyokuwa akihema kwa shida akiwa ameshikilia magoti na kuinamisha kichwa chini.
“Hubby nina njaa pia na tokea jana hatujala kitu chochote na tumetembea sana”Aliongea Mage na kumfanya hata Rufi kuona aibu maana alijua Mage ameongea hivyo kwa ajili ya kumsaidia.
Kutokana na changamoto walizopitia yale mawazo ya Mage kumuona Rfufi kama Vixen yaliisha kabisa , alijiambia kama alikuwa hivyo huenda siku ya jana asingemfukuzia wakati anajaribu kumsogelea Roma wakati wa hatari.
Roma alijikuta akitingisha kichwa , alikuwa ashasahau kuwa stamina zao sio imara hivyo hawawezi kuvumilia muda mrefu , hivyo kwa muda huo alipaswa kujua namna ya kupoza njaa yao.
Alijaribu kuzungusha macho kwenye msitu huo kuangalia kama anaweza kuona chochote cha kulika lakini hakuona kitu , lakini baada ya kuangalia kwa umakini mbele aliweza kuona mti ambayo ulikuwa una matunda juu yake.
“Nifuateni”Aliongea na kisha wakaanza kutembea kwenda mbele.
Baada ya kuufikia alijaribu kuangalia mizizi yake kwa kufukua kiasi ili kuuchunguza na kisha alioneana kuridhika na kuchuma baadhi ya matuda yaliokuwa juu yake.
“Huu ni mti wa matundwa mwitu , majani yake yana umbo mviringo na mizizi yake imesambaa kwenda chini ardhini ili kutunza maji , kwa sifa hizo matunda yake ni salama, yanaweza yasiwe matamu lakini hatuna namna jitahidi kula kiasi cha kutosha ili angalau muongeze Vitamin C na huko mbele najua tutapata namna ya kupata chakula”Aliongea Roma na kuwafanya wasifikirie mara mbili na kuanza kula huku wakikunja sura kwa uchachu wake.
Roma na yeye hakuwa nyuma alichukua kiasi kwa ajili yake lakini hata hivyo alijua kwa upande wao wasingeweza kudumu kwa muda mrefu pasipo ya kupata chakula chenye calories.
Safari iliendelea kwa muda mrefu kama masaa manne matano hivi na waliweza kufikia mto na kwasababu ilikuwa tayari ni jioni Roma aliwaambia ni muda wa kuweka kambi hapo kupumzika mpaka siku inayofuata , aliwapa kazi ya kutafuta eneo zuri na yeye alienda kutafuta kitu chochote ambacho kingeweza kuwasevu kama chakula cha usiku.
Baada ya Roma kuwaacha, walienda kukusanya kuni zilizokauka kwa ajili ya kuwasha moto .
Roma alitembea kando ya mto kuangalia namna yoyote ya kuweza kupata kitoweo , hakuwa na kifaa chochote cha kumsaidia kuvua lakini pia hakuwa na uhakika kama huo mto ulikuwa na samaki.
Baada ya kuhangaika kwa dakika kumi na tano hatimawe aliweza kuona nyoka wa majini akiambaa ambaa na alisema huyo huyo anafaa na aliingia majini na kisha akamnyaka mkononi na kumbeba juu huku akipinda pinda na alichokifanya ni kutumia meno yake kunyofoa kichwa chake.
Kikawaida nyoka wa baharini hawakuwa na sumu nyungi na katika hali ambayo kama ni binadamu umekosa kabisa chakula unashauriwa kumkamata na kumtumia kama chakula na isitoshe nyoka wa aina hio wana calories nyingi hivyo kiasi kidogo tu kinaweza kukufanya udumu kwa muda mrefu pasipo ya kuhitaji kula tena.
Baada ya kung’ata kichwa chake alikitema chini , hakuwa na namna kwa muda huo zaidi ya kuwa kama watu walioishi zama za kale.
Roma airudi kuelekea kwenye kambi yao hku akiwa ameshikilia nyoka wake lakini wakati akiwa anakaribia alisikia Mage akitoa ukulele upande wa pili na kumfanya kushituka na kuwahi , ilikuwa ni sehemu ambayo wamewasha moto na nyoka mkubwa alionekana akitoa ulimi wake kama matawi akiwasogelea.
“Kaa mbali kabisa , huyu ni Nyoka wa Australia afahamikae kwa jina la Coastal taipan , ndio nyoka namba moja mwenye sumu dunia nzima na akishambulia ni ngumu kumkwepa”Aliongea Roma na kuwafanya wote kwa pamoja kuondoka ndani ya hilo eneo na kukaa mbali.
Roma hakujiuliza mara mbili alitupia nyoka wa majini pembeni na kisha akaokota tawi na kulitengeneza kama fimbo na kuanza kumshambulia kwa kumlenga kichwani..
Lakini muda ambao alikuwa akitaka kumlenga yule nyoka alishituka na kuruka wakwanza kumlenga Roma na alikuwa amechelewa kwani tayari alishang’atwa kwenye mkono.
“F**ck!”
Alilaani , ijapokuwa alikuwa amejipanga kushambuliwa lakini ilimchukiza kushindwa ujanja mpaka na nyoka , kama ingemtokea kabla hajapoteza uwezo wake angekwepa tu kwa kutumia nguvu zake za kijini na hata kanuni za anga.
Hakuwa tu amepoteza uwezo wake lakini pia hata ubongo wake ulifanya kazi taratibu sana na hakuwa na uwezo wa kuanza kufikiria kanuni za anga na akili yake hio na kugeuza kama siraha.
Roma baada ya kuona ashang’atwa hakuona haja tena ya kutumia ule mti hivyo alitupa na kisha akamrukia yule nyoka na kumshika kichwa chake na kumkaba eneo la shingoni kupelekea yule nyoka kuachama na hio ndio nafasi kwa Roma kwani alishika taya lake na kisha akavuta kwa nguvu na kumfanya achanike katikati kama vile ni kitambaa.
“Hubby uko sawa?”Aliuliza Mage baada ya kuona nyoka alishakufa.
“Usijali nipo sawa siwezi kufa”Aliongea Roma huku akishikilia jeraha lake .
“Ijapokuwa nimepoteza nguvu zangu lakini mwili wangu bado una uwezo mkubwa wa kuvumilia sumu ya aina yoyote ile , hivyo nikipumzika kidogo tu nitakuwa sawa”
Aliongea kuwatoa wasiwasi lakini ukweli Coastal taipan kama atamng’ata binadamu wa kawaida ni ngumu sana kupona ,afiti zinasema nyoka mmoja kimahesabu anaua zaidi ya panya elfu ishirini katika uhai wake kwa kutema sumu yake tu.
Licha ya Roma kusema yupo sawa lakini hali yake ilimfanya Mage kushindwa kujizuia, ule upolisi aliokuwa nao ulishaisha muda na hapo alikuwa kama mwanamke tu ambaye anamtegemea mwanaume.
“Kwani kulikuwa na ulazima gani wakumuua si ungemfukuza tu akaenda zake , tayari upo kwenye hii hali lakini bado unatafuta matatizo mengine”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie kwa huruma na kisha akachukua nyoka wa majini aliemkamata na kisha akampatia Rufi.
Mage baada ya kuona chakula walichoatafutiwa ni nyoka alijikuta hata kilio kikikata ghafla na kuwa katika bumbuwazi.
Upande wa Rufi hakuona shida , huenda ule uchina kwenye damu yake ulimfanya kutokuwa na wasiwasi na aina hio ya chakula.
“Huyo nyoka mmoja atawatosha nyie tu , sina jinsi na giza ndio linaingia zaidi hivyo nadhani atawaondolea njaa..’Aliongea na kumfanya Rufi kugusuwa na kauli yake maana alikuwa akimaanisha kwamba yeye hana haja ya kula hivyo wao ndio wale, ilimgusa zaidi yeye kutokana na kwamba hakuwa na uhusiano wowote na Roma hivyo hakupaswa kumjali zaidi ya Mage.
“Rufi mchome kwenye moto na kisha kwangua ngozi yake na mpasueni mtoe vitu vyote vya ndani na kisha unazungusha kwenye mti na unachoma tena nyama yake , hakikisha inaiva vizuri kwani nyoka wana minyoo wengi msije kutapika”
Mage alijikuta akichuchumaa chini huku akimwangalia Riufi akifanya kazi hio ,ijapokuwa hata wakati alipokuwa kwenye mafunzo ya kipolisi walifundishwa namna mbalimbali za ku’survive’ wakiwa maeneo kama msituni lakini hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa kwenye hali ya uhalisia.
Roma alipumzika kwa zaidi ya lisaa na aliwasaidia kuhakikisha nyoka ameiva vizuri na kumkata kati na kisha akampatia Rufi na Mage.
Ajabu ni kwamba nyama yake ilipofikia pua za Mage ilionekana kunukia vizuri na njaa aliokuwa nayo alijikuta akianza kula mara baada ya kumuona mwenzake anafurahia.
“Roma kula kidogo tu”Aliongea Mage.
“Hapana kutokana na mwili wangu ulivyo naweza kudumu muda mrefu pasipo ya kula “
“Lakini huwezi kukaa na njaa hivyo, kwasasa huna nguvu yoyote na umeng’atwa na nyoka”
“Mage nimesema kula bwana , ngoja nikajaribu kutafuta chochote kama nitabahatika kupata”Aliongea Roma na kisha alisimama na kuondoka katika hilo eneo.
Ukweli ni kwamba alikuwa na njaa tena sana kutokana na kwamba mwili wake umepoteza nguvu na alichokuwa akitegea ni chakula.
“Inaonekana kashaamua sisi tule yote , tuendelee tu”Aliongea Mage huku akimwangalia Rufi na alitingisha kichwa kukubaliana nae.
Nyama ilikuwa ikinukia vizuri lakini bado haikuwa tamu , lakini licha ya hivyo waliendelea kula kwani hawakuwa na namna nyingine ya kupata chakula.
“Has he always been this good to you guys?”Aliuliza Rufi akimaanisha je Roma muda wote ni mwenye kuwafanyia mazuti muda wote.
“Hata mimi sijajua , muda wote ni mwenye kutulinda lakini hata hivyo huu udhoefu umenipa nafasi ya kumjua zaidi”Aliongea Mage na kumfanya Rufi kutingisha kichwa na hakuongeza swali lingine.
Hakuwa nyoka mdogo hivyo nyama iliwatosheleza kwa zaidi ya asilimia themanini kwani baadhi ya vitu vingine hawakuweza kutafuna kutokana na kuwasha.
Muda huo huo walimuona Roma akirudi kwa kukimbia akiwa kifua wazi, kwa mwonekano wake ilionekana kama kuna kitu ambacho amefanikisha kupata lakini walishangazwa kuona amevua shati.
Baada ya kuwafikia ndipo walipoweza kuona kitu alichobeba kina mchanganyiko wa mchanga , walijikuta wakisimama bila ya kumsogelea.
‘Umebeba nini?”AliulizaMage na Roma alitua lile shati lake chini na hapo hapo waliweza kuona wadudu wakipanda kwa juu na kumuogopesha Mage na Rufi.
“Ah..!!”Walitoa mshangao wao huku wakichungulia ndani na ndipo walipogundua ni wadudu wengi waliokuwa kwenye masega .
“Acheni wasiwaso ni masega ya wadudu aina ya mchwa(termites) hawang’ati na ni wazuri mno”Aliongea Roma.
“Mchwa…!!!”Walishangaa ilikuwa mara ya kwanza kwa Mage kuona aina hio ya mchwa.
“Kwanini umewaleta hapa au unataka kutufanya tupatwe na woga?”Aliuliza Rufi na Roma hakujali alikaa chini na kisha akachukua wadudu hao kwenye mkono na kisha akawapeleka wote mdomoni.
“Ah.. wewe,, wewe!!!” alikuwa akitafuna Roma lakini wao ndio waliokuwa wakihisi kutapika lakini Roma aliishia kutabasamu huku akijilamba lamba alionekana kufurahia utamu wao.”
“Mchwa wana protini mara mbili zaidi ya nyama , najua hamuwezi kuwala hivyo nitakula mimi mwenyewe”
“Kama ndio hivyo ungekula huko huko kabla ya kuja hapa na kubeba mpaka masega yao?”Aliongea Mage huku akishikilia shingo yake.
“Haya masega yametengenezwa na mate na mchanga , kikawaida watu wa asili watayachoma motoni na kufanya moshi wake kuwa na harufu ambayo hufukuza mbu, najua hapo mnavumilia maumivu ya kung’atwa ndio maana nikaja nayo”Aliongea na kuwafanya sasa waelewe , ijapokuwa maelezo yake yaliwagusa lakini hawakuvumilia kumuona akitafuna hao wadudu.
Roma hakujali , ukweli ni kwamba alishawahi kuwatafuna wakati wa utoto wake ili kuishi , alijua angeonekana kama kichaa lakini ili apate nguvu za kuwatoa kwenye msitu huo hana budi kufanya hivyo .
Siku ya pili yake ilipowadia walianza safari tena , walishaanza kumzoea Roma hivyo hawakushangazwa zaidi na tabia yake hata pale alipokamata wanyama wadogo wadogo mfano wa Sungura, Panya wakubwa na Kobe wa Australia wote hao waliwafanya chakula.
Tukio moja ambalo liliwafanya kutaka kupoteza fahamu ni pale alipong’ata kichwa cha spider na kukimeza chote.
Siku ya nne hatimae waliweza kufika kwenye fukwe ya bahari ya Arafura upande wa Kaskazini ni eneo ambalo lilikuwa na kiasi kikubwa cha miti aina ya Pandanus ambayo mingine ilikuwa na matunda na mingine haikuwa na matunda.
Wakati wao wakiwa wamepumzika wakifurahia upepo Roma alitengeneza ndoano kwa kutumia miti na uzi na kisha akatafuta jongoo na kumuweka kama chambo na kurudi tena msituni kwenye mto uliokuwa ukimwaga maji ndani ya bahari na kuanza kuvua samaki, asingeweza kuvua baharini kwani mara nyingi hawapatikani kwenye fukwe hivyo mto waliokuja nao kufuatisha aliona ndio mahali salama pa kuvua na alifanikisha kukamata Kambare wawili wakubwa., Roma hakushangazwa kupata samaki wakubwa kama hao kwenye mto wa maji malaini lakini alijiambia huenda ni kutokana kila mahali wanapatikana.
Baada ya kuwarosti kwenye moto na kula waliamka na kuendelea na safari yao huku awamu hii sasa hawakutembea kwenye vichaka bali kwa kufuatisha fukwe ya bahari.
“Mawazo ya kurudi nyumbani yametufanya kushindwa hata kutafuta tena mimea ya vidonge”Aliongea Rufi
“Sidhani kuna haja ya kujisumbua mpaka sasa nimeshindwa kujua namna ya kurudisha nguvu zangu sembuse kuweza kudhibiti moto wa njano wa kutengenezea hivyo vidonge’
“Usijilazimishe sana najua pia moto wa njano ni ngumu sana kudhibiti zaidi hata ya moto mweupe , kwa umri wako naweza kusema nguvu zako ni kubwa mno na inatosha”Aliongea na Roma aliona Rufi anajaribu kumfariji lakini hakutaka kuongezea neno zaidi ya kutembea mbele.
Kutokana na uwepo wa majabali upande wa Fukwe walirudi ndani msituni kuanza kutembea ili kuzunguka watokezee upande wa pili na baada ya kutembea kwa takribani nusu siku waliweza kutokea eneo la tambarare lenye miti mifupi , muda ulikuwa umeenda na hali ya hewa ilikuwa ya baridi mno.
Muda uleule wakati wakipanga kutokezea tena kwenye fukwe mara kwa mbele yao waliweza kuona wazungu waliovalia kombati za jeshi wakiwasogelea kwa kasi kwa kutumia vyombo vya moto ambavyo huwaruhusu kusafiri hata sehemu ambazo sio za barabara ni kama magari flani hivi yanayotumiwa sana sehemu za jangwani.
Roma baada ya kuangalia ivzuri alijua hata vyombo vya moto wanavyotumia ni vya kijeshi.
Walizidi kuwasogelea kwa kasi na walipowakaribia ndipo Roma alipoweza kuona sura zao vizuri , walikuwa na sura ngumu mno zilizojaa usiriasi huku wakiwa na mashine za bunduki kwenye mikono yao.
“Roma wanatulenga sisi?”Aliuliza Mage kwa hofu lakini Roma alishindwa kujibu kwani hata yeye alikuwa na moyo mzito , asingeogopa kama angekuwa na uwezo wake, lakini muda huo hakujuwa namna ya kujilinda kama watu hao wataamua kushambulia.
Mage alikuwa polisi na alikuwa na mafunzo lakini hakuwa na mafunzo ya kupambana na wanajeshi
“Kaeni kimya , tutajua wanataka nini kwetu”Aliongea Roma huku wakizidi kuwasogelea.
Baada ya wanajeshi wale kuwakaribia na kuwazuguka alitokezea mwanaume aliekuwa na ndevu pande zote kiasi cha kufanya mdogo wake kuonekana kwa shida.
“Black skinned peaple Africa or America?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza akisema wati wa ngozi nyeusi je wanatokea Afrika au Amerika
Roma hakuwatambua ni kundi gani wanatokea kutokana na kwamba hakuna taarifa kwenye uniform zao zaidi ya alama ambayo iliashiria walikuwa ni Mercenary , hivyo asingeweza kujitambulisha kwao , aliogopa wasije kuwa maadui zake.
“We’re Tanzanians , our plane crashed so we landed here , what is matter?”Aliongea Roma akidanganya kwamba wao ni watanzania lakini ndege yao ilidondoka na ndio maana wapo hapo.
“Marafiki kutoka Tanzanyia , naamini mmechoka sana mnaonaje mkapumzika hata hivyo sijatarajia kukutana na wanawake warembo kwenye hili eneo , jina langu naitwa Ryan na ni furaha kwangu kuwakaribisha kwenye kambi yetu”Aliongea huku akicheka na kufanya meno yake ya njano kuonekana.
Mage na Rufi waliogopa mno na walijikuta wote wakienda kukaa nyuma ya Roma kwa woga.
“Hubby tunatakiwa kufanya nini?” Aliongea Mage na wale wengine walipiga miluzi kwa furaha wakiwaangalia Rufi na Mage kwa macho ya matamanio.
Roma alijitahidi kurudisha kumbukumbu zake kutafuta jina la kambi ya masenari yenye makazi kwenye ukanda huo na alijikuta sasa akikumbuka, waliokuwa mbele yake ni Grey Marcenaries , alikuwa akijua sana kuhusu taarifa zao ni watu wasiojali utu na ni wenye roho mbaya sana.





SEEHEMU YA 502.
Roma mara baada ya kujua ni hatari gani iliokuwa mbele yake alijua kabisa hana la kufanya , ijapokuwa hakujua ilikuwaje mpaka wakawaona lakini kwa wakati huo aliona jambo la pekee ni kufuatisha kwanza kile wanachotaka.
Aliwageukia Rufi na Mage na kisha aliwapa ishara wasiwe na wasiwasi na waongozane nao na kisha akawageukia wale wanajeshi na kuwaambia waongoze njia.
Wote walipandisha kwenye vyombo hivyo vya moto ambavyo muundo wake ni kama yale matrekta ya kulimia yenye matairi mapana.
Safari ilianza huku wakiwa chini ya ulinzi na ndani ya muda mfupi tu walikuja kutokezea kwenye eneo la fukwe na hapo sasa ndio Roma alielewa , mbele yake meli kubwa ya mizigo ilionekana ikiwa imetia nanga.
Upande wote wa fukwe kulikuwa na walinzi ambao walikuwa wakilinda kwa kuzunguka zunguka pande zote..
Ilikuwa ni meli kubwa ya mizigo na pambeni yake kulikuwa na vessels mbili za ulinzi zilizokaa kulia na kushoto na moja kwa moja Roma aliweza kufahamu hili sio eneo lao la kudumu bali huenda kuna biashara haramu zinazofanyika hapo kutokana na uwepo wa mahema mengi kwenye hio fukwe.
Watu waliokuwa tu nje walikuwa kama therathini kwa haraka haraka kuna ambao walikuwa na sura za kiasia na kuna wazungu pia na Roma alijua hao ni smugglers watu wanaoingiza biadhaa kimagendo nchini Australia kupitia baharini.
Wote walitolewa kwenye chombo kile cha usafiri na kufanya kundi lote kuwaangalia huku macho yao ya kimatamanio yakiwaangalia Rufi na Mage na kufanya wazidi kuwa na hofu , mpaka hapo walijua hawana namna ya kuepuka ubakaji hivyo waliona ni vyema kukaa zaidi karibu na Roma.
Wote waliongozwa mbele na kupelekwa mpaka kwenye hema lenye rangi ya zambarau na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Ryan alinyoosha mtutu wake na kuwaonyesha ishara ya kuingia ndani.
Ni eneo ambalo lilikuwa na mahema kama kumi na tano hivi makubwa yaliosimamishwa kwa mita tano nao kuachana na yalikuwa ni makubwa mno.
“Go in our Tanzanyian friends”Aliongea huku akichapia Tanzania na kuita Tanzanyia.
“Mna mpango gani na sisi?”Aliuliza Roma.
“Tusha mtaarifu bosi wetu na utafahamu mara baada ya kufika”Aliongea na kisha akamsukumzia Roma ndani ya hema hilo na wakaongezeka wanajeshi watatu na kulinda nje
“Inaonyesha hawana mpango wa kutuua lakini pia hawajatupa sababu ya sisi kutufungia humu”Aliongea Mage kwa wasiwasi.
“Amesema kiongozi wao atakuja kutuona , nadhani tutajua mpango wao”Aliongea Roma na kisha akaanza kuangalia mazingia ya hema hilo na alijikuta akikunja sura baada ya kuona maboksi mengi ya mbao yaliochongwa vizuri na kuvutia kwa nje , yalionyesha kanisa yalikuwa na vitu vya thamani ndani yake na namna ambavyo yalipangwa ni kama walikuwa wakiogopa yakidondoka na kuharibika.
Roma aliyasogelea na kisha akafungua moja wapo taratibu sana ili walinzi nje wasisikie na ndani yake aliweza kuona kifaa ambacho kimezungushiwa magazeti , alishangaa kutokana na lugha iliotumika kwenye hayo magazeti lugha ilikuwa ya kichina (mandarin) na moja kwa moja alijiambia huenda ni kitu ambacho kinahusiana na nchi hio.
Baada ya kuondoa lile gazeti alikutana na buble wrap iliozungushiwa kwa juu ili kama kifaa hicho kingedondoka chini kisipasuke kwa urahisi , baada ya kumalizia kutoa sasa alijikuta akishangaa baada ya kuona kilichopo ndani ya boksi.
“This is…”Rufi alijikuta akiziba mdomo kwa mshangao na Roma alimtingishia kichwa kukubaliana nae.
“Ni Porcelaini ya rangi nyeupe na bluu ambayo imedariziwa na mchoto wa mawingu na Dragoni , makadirio ya thamani yake nchini China ni zaidi ya dola milioni kumi”Aliongea Roma na kumfanya sasa Mage kuelewa maana aliona ni kama kikombe cha udongo tu na hata hivyo hakuwa na uelewa na tamaduni za China.
“Are they smuggling relics?””Aliuliza Rufi kwa sauti ya kunong’oneza akimaanisha je wanaingiza mabaki ya vitu vya kale vya thamani nchini Australia kwa njia zisizo halali.
“Naamini kuna zaidi ya mabaki , hebu fikiria kwanini wamekuja kutuweka ndani ya hema lenye vitu vya thamani namna hii , jibu ni kwmaba mahema yote huenda yamejaa, ndio maana wametumia meli kubwa ya mizigo , nina uhakika kama serikali ya China wanaelewa hiki kinachoendelea lazima wangewawinda kwani vitu kama hivi ni vya thamani sana kwao”
Wakati Roma akiendelea kuongea aliweza kusikia sauti yenye ucheshi nje ikiongea na ndani ya muda mfupi tu hema lilifunguliwa na akaingia mwanaume mrefu mchina akiwa amevalia T- shirt iliombana vyema mwili wake , alikuwa yupo na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Ryani.
Alianza kumwangalia Mage na kisha akahamia kwa Rufi na halafu akamgeukia Roma sasa.
“Dude I heard from Ryan that you guys were trapped in this place because your plane crashed?”
“Dude nimesikia kutoka kwa Ryani mmekwama mara baada ya ndege yenu kudondoka?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza lakini iliojaa rafudhi ya kichina.,
“Wewe ni mchina?”Aliuliza Roma na kumfanya yule bwana kumwangalia kwa namna ya kumchunguza Roma.
“You don’t look like a spy since you don’t recognise me , I’m leader of the Hydralisk Mercenary group , Jin Zhe , They call me Hydra , Havu you heard about me?”
“Unaonekana sio shushu kwasababu haunifahamu , mimi ni kiongozi wakundi la Masenari la Hydralisk nafahamika kwa jina la Jin Zhe lakini wananiita Hydra , ushawahi kusikia kuhusu mimi?”Aliongea huku akimwangalia Roma kama Cobra alieona binadamu wa kumshambulia.
Roma alitingisha kichwa chake akishiria kwamba hajawahi kumsikia na alikuwa akiongea ukweli kwani hajawahi kuwasikia labda huenda hawakuwa maarufu.
“Haijalishi kama hunifahamu lakini naamini nyie sio hao watu wanaonitafuta”Aliongea na kumfanya Roma sasa kidogo kuwa na ahueni, kwasababu hakuwa akiwajua moja kwa moja alijua sio maadui zake hivyo hakuogopa kama atagundulika ni mfalme Pluto.
“Kwahio unamaanisha utatuacha tuondoke?”Aliuliza Mage.
“Go!?, My beutiful you think too highly of us ..”Aliongea huku akitingisha vidole vyake akimaanisha kwamba wamewadhania ndivyo sivyo kwani hawana mpango wa kuwaachia.
Roma alijikuta akikunja ngumi akijiambia mwenyewe mambo yanaweza yasimalizike vizuri.
“Tumekaa hapa kwa muda mrefu na haya maeneo hakuna watu wanaofika hivyo unaweza kusema ni kwa muda mrefu hatujawhai kuona wanawake warembo kama nyie ,itakuwa ujinga kama nitawaachia muondoke bila mabro kunufaika na uzuri wenu”Aliongea na kumfanya Mage na Rufi kukasirika na kuogopa.
“Huna aibu wewe?”Alilaani Rufi
“Nisamehe sana , ijapokuwa hatuna uhasama na nyie lakini siwezi kujali kwasasa , hali ya kimazingira yenyewe ndio hii, ninachomaanisha msiwe na wasiwasi na muwaburudishe mabro wangu vizuri tu na hakuna kibaya kitakachowakuta”
“Sio tu wewe ni mwizi unaeliibia taifa lako mwenyewe, lakini pia ni mchafu wa tabia”Aliongea Rufi
“Nione aibu hahah….. mnaonekana kabisa nyie ni matajiri ndio maana mnatoka nchini kwenu na kudondoka na ndege na hamuwezi kunielewa mtu kama mimi”Aliongea ilionekana kabisa alikuwa na chuki na taifa lake.
“Unaonekana kama mtu mwenye huzuni , inakufanya uonekane kama mtoto”Aliongea Roma.
“Unasemaje wewe , funga domo lako”Aliongea kwa hasira na kumfanya Roma hata asijali na kuendelea kuongea.
“Inaonyesha kabisa nchi yako imekufanyia mabaya lakini lawama zote unaangushia dunia nzima , angalia sasa ulivyo, unaonekana kama mtu ambaye umekufa huku unatembea , nina uhakika kuna kilichokutokea lakini tofauti na kujitafuta ili kujua ulikosea wapi au kulipiza maadui zako kwa kile walichokufanyia lakini upo hapa ukiwa umejificha unaishi bila amani , kwangu wewe ni Loser na mtu mdhaifu sana”Aliongea Roma kwa kujiamini kama kawaida yake na kumfanya Mchina kukasirika zaidi na zaidi.
“Unajifanya mjuaji sana kwa kuongea , lakini ngoja nikushauri wanaume hatuongei sana bali ngumi yetu ndio inazungumza”Aliongea .
“Boss niwapeleke hawa wanawake kwenye hema lako”
“Haina haja, waondoe wanajeshi wanao linda nje”Aliongea na kisha Ryani mzungu alitoka nje na kuwaambia wale walinzi waondoke na kisha akarudi tena ndani.
“Boss huyu mwanaume na yeye tunamfanya nini maana hana faida kwetu?”Aliuliza tena.
“We have brothers who like to go other way right? , he looks young and tender, give him to them !”
“Tuna mabraza ambao wanapenda mlango wa uani si ndio? , huyu bwana anaonekana mdogo lakini pia ni mpole muondoe hapa ukawapatie”Aliongea na kumfanya Ryan kutabasamu huku meno yake ya njano yakiwa nje nje.
“You have to serve our brothers well .. hehe, I’ll send you there myself”
“Unapaswa kuwahudumia mabraza wetu vizuri … hehe nitakupeleka mwenyewe”Aliongea .
Rufi na Mage walijikuta wakijificha nyuma ya Roma , ni kama washasahau kwamba mwenzao hana nguvu yoyote , Mage alikuwa amekunja ngumi alikuwa akijua kupigana kwasababu ashapitia mafunzo lakini aliogopa siraha zao tu
Ryan alianza kumsogelea Roma kwa ajili ya kumnyanyua ili kumpeleka kwa mabraza , lakini ile anamkaribia Roma alinyanyuka kwa staili matata sana na kupiga viungio vya mkino yake.
‘Arrghh,,,”
Alijikuta akitoa ukulele , ijapokuwa Roma hakuwa na nguvu za kijini lakini haikumaanisha alikuwa hajui kupambana kwa njia za kawaida , alikuwa na mafunzo ya hali ya juu ya Kung Fu na alikuwa akijua mbinu zote za kijeshi na isitoshe mwili wake ulikuwa mwepesi kutokana na kwamba alikuwa amemulikwa na mwanga wa jiwe la kimungu na akaja kuwa Agent 13.
Roma kwa haraka sana alinyanyua bunduki ya Ryani na kisha alimfyatua nayo kwa kumlenga kichwa na muda uleule zile purukusani zilifanya wanajeshi wengine wawili kuingia na Roma hakutaka kuwarembesha , bunduki ilikohoa mara mbili mfululizo na kuwapasua wote vichwa na kudondoka chini.
Mchina alijikuta akishangazwa na uwezo wa Roma na alijikuta hana cha kufanya zaidi ya kukimbia nje huku akiita wenzake .
Roma palepale alichuchumaa na kisha akachomia mikebe ya bunduki za wale wawili aliowaua , alikuwa akijua wapo wengi na mikebe mwili haiwezi kutosha kuwamaliza.
“Roma tunapaswa kufanya nini?”Aliuliza Mage.
“Hawawezi kushambulia hili hema bila ya tahadhari kuna vitu vya thamani vya kutosha hapa na kama vitaharibika watapoteza mamilioni ya pesa”Aliongea Roma
“Pumbavu zako , sijategemea ungekuwa na ujuzi wa hali ya juu namna hio lakini siwezi kukuacha hai , ushaua tayari mabraza wetu watatu lazima ulipie’Aliongea Mchina kwa sauti kubwa nje kwa hasira.
“Roma unaonaje tukuchukua bunduki na wote tukashambulia nina uzoefu mkubwa na tunaweza kuwamaliza”Alishauri Mage.
“Hapana tukifanya hivyo ndio watatuua vizuri kwani ni kama tunawachokoza na watatushambulia na ukumbuke wana siraha nzito”
“Kwahio tunafanya nini , tunasubiria hapa ndani watuue?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kujibu swali lake kwani hakuwa na wazo, kwenye maisha yake hakuwahi kuwa hivyo , kuwa binadamu wa kawaida ni jambo ambalo hajalizoea
Alichukia hali aliokuwa nayo kwani alishindwa kabisa hata kuwalinda wanawake wake ,kwake ilikuwa kama matusi ambayo ni kama yalikuwa yakimkosesha amani.
Muda huo kwa nje hali ilitulia kabisa , ni kama vile wameondoka lakini Roma hisia zake zilimwambia huenda wanawategea kitu hatari zaidi.
Kabla hajajua ni nini kinaendelea nje , vyuma vilirushwa ndani na baada ya kuangalia kwa umakini aligundua ni mabomu ya machozi .
“Ni mabomu ya machozi fumba macho ”Aliongea, katika maisha yake alikuwa ashapitia changamoto kama hizo na ni kama amekumbushiwa nyuma lakini hata hivyo bado hatari ilikuwa nje nje.
“Hatuna chaguo zaidi ya kutoka nje , Mage chukua hio bunduki na wote hakikisheni mnakuwa nyuma yangu”Aliongea Roma.
Muda huo alijiambia sio wa kusita tena bali ni wa kupambana huku akitegemea Mage kidogo angemsaidia kwani alikuwa mwanajeshi na ukichanganya pia alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko , hivyo alikuwa na uhakika anaweza kudondosha watu kumi.
Alijua walikuwa wakisubiriwa nje hivyo aliona haitokuwa busura kama watatumia mlango wa hema kutoka nje
Wote walikuwa wamefumba macho ili moshi usiwaumize na kuwafanya wawashe na macho.
Roma alitumia hisia zake kujaribu kupata kuona namna wanajeshi hao walivyojipanga na palepale aliachia risasi kupitia upande wa nyuma mwa hema na alidondosha watu wawili bila makosa.
“Kimbieni nje”Aliongea Roma na muda ule alijirusha nje huku akitanguliza mdomo wa bunduki mbele na kufanya hema lichanike kwa wepesi na aliweza kubiringita kama pia huku akirusha risasi ambazo hakuna hata moja iliokosa mtu.
Jambo lile liliwafanya kushangazwa mno na kujiuliza huyu ni komandoo au ni nani kwani haikuwa kawaida, sekunde tano tu alikuwa amedondosha watu watano.
Mage alimtoa Rufi na kumwambia akimbilie baharini zaidi huku yeye akimkinga na siraha, lakini palepale yule mchina alionyesha kuwashitukia tayari.
“Mnajaribu kukimbia sio , Never”Aliongea huku akiwapa vijana wake ishara ya kuzunguka nyuma.
Na Mage alikuwa shapu mno kwani alimdodosha Rufi chini na kisha akauegamiza mgongo wake kwa staili ya kuelekea mbele na akaachia risasi mfululizo ambazo ziliwapata watatu na kudondoka chini , hali ile iliwafanya kusogea upande huo kwa tahadhari.
Muda ule ule kuna wanajeshi wengine wanne waliokuwa kwenye gari waliwasogelea kwa spidi na Roma alielala chini alilenga mara mbili tank la mafuta kwa shabaha kuntu kabisa.
“BOOM!!
Gari ililipuka palepale na wanajeshi wanne walikuwa wafu tayari na kumfanya Jin Zhe kuwa kwenye kiwewe akishangazwa na Roma alivyokuwa vizuti kwenye kuchezesha bunduki.
“Back off and take cover!”
Aliongea kwa sauti akiwamrisha warudi nyuma kwani aliogopa wangeshambuliwa na Roma ambaye alikuwa na shabaha ya hali ya juu kwenye matumizi ya siraha hivyo kuogopa wanajeshi wake kufa wengi.
Ndani ya sekunde tu wote walijificha nyuma ya mahema na kwenye mawe , huku wakiwa wamejaaa sumu ya kuua maradufu.
Upande wa Roma risasi zilikuwa zishamwishia tayari , lakini hata hivyo hakuna ilioharibika na aliwaza mbinu ya pili ya kushambulia.
“Mage unafanya nini acheni kukimbia” Aliongea Roma kwani aliona wangeshambuliwa na pale pale Mage alilala chini kwa haraka
Roma baada ya kuona hawako kwenye hatari alisimama na kisha akamrushia bunduki wanajeshi wawili waliokuwa wakitaka kujitokeza kushambilia na palepale alikimbia nduki kumfuata mwanajeshi mwiengine ambae ashakufa achukue bunduki yake.
Mage aliejificha na Rufi chini ya jiwe alinyanyua sura kidogo kuchungulia , hata yeye siraha yake ilishaisha risashi hivyo alitupilia mbali na wanajeshi waliokufa wapo mbali
“Roma kuwa makini..”
Mage alijikuta akiziba mdomo kwa wasiwasi mara baada ya kushuhudia moja wapo ya mwanajeshi ambaye alilipuka kwenye gari bado hakuwa amekufa na alisimama huku akiwa ameshikilia bomu la kurusha na mkono.
Roma alikosa umakini wa kuangalia nyuma yake hivyo hakumuona na yule mwanajeshi hakutaka kuchelewa palepale alirusha lile bomu uelekeo wa Roma lakini alikuwa fasta mara baada ya kusikia kauli ya Mage na aliruka upande mwingine .
“BOOM!”
Lilipuka lakini Roma hakuwa ameenda mbali hivyo nguvu ya wimbi lake ilimpiga na kumfanya adondoke chini akiugulia maumviu.
“Nice one, very nice”Aliongea Jin Zhe
“Ameishiwa na risasi mfuateni tummalize”Aliongea kwa nguvu.
Roma alikuwa amefunikwa na vumbi la mlipuko wa bomu na alikuwa akijihisi kizungu zungu na viungo vya ndani ni kama vilikuwa vikikamuliwa kwa maumivu aliokuwa akisikia.
Lakini alijiambia hana muda wa kusikilizia maumivu na atumie vumbi lilomfunika kama kinga , alijivingirisha kama pia na kusogelea bunduki iliokuwa kushoto kwake
Mlio wa bunduki ulikuwa umesambaa na wale wanajeshi hawakuangalia pa kulenga ili mradi ni eneo ambalo Roma yupo walirusha huko huko na kwa wingi wa risasi ilikuwa ngumu Roma kukwepa zote.
Roma alijikuta aking’ata meno kwa maumivu mara baada ya kugundua ashapigwa risasi ya tumbo na kwenye kigimbi cha mguu
Ijapokuwa mwili wake bado ulikuwa mkomavu lakini haukuwa na ulinzi tena wa nguvu ya kimaandiko ya urejesho kutokana na sumu iliokuwa kwenye mwili wake , hivyo alijihisi dhaifu mno.
Alijikuta akitema damu nyingi huku akisikilizia maumivu makali kutoka tumboni , alijjitahidi kubingirika upande mwingine lakini bado hakuwa na spidi kama ya mwanzo lakini bahati kulikuwa na jiwe kubwa karibu hivyo alilala chini na kujikinga na risasi.
Mage alishindwa kabisa kuvumilia pale alipokuwepo kwani alishuhudia Roma akipigwa na risasi na akitema damu na alitoka kwenye jiwe na kukimbilia upande wa Roma alipo.
“Mage..!!”Aliita Rufi kwa hofu lakini alikuwa ashachelewa na hata yeye alianza kukimbia kuelekea upande wa Roma.
Roma alijua wanamsogelea ili kumsaidia ,lakini aliona kabisa isingeweza kusaidia palepale aliwapa ishaa wasije upande wake lakini Mage alimpotezea na kukimbia kwa spidi na kwenda kutua alipo na Rufi hivyo hivyo aliweza kufika.
“Roma hapa hatuwezi tena kupambana nao , ni wengi na hatuna siraha njia pekee nitumie uwezo wangu kukubeba kukimbia na wewe kuelekea upande ule”Aliongea Mage na Roma aliona wazo sio baya, alijua ni kweli Mage anao uwezo wa kukimbia nae kwa spidi kutokana na uwezo wake.
Roma kabla hajajibu Mage tayari ashamnyanyua kama mtoto na kuanza kukimbia nae huku Rufi akifuatia.
Kitendo kile kiliwaamsha Jin Zhe na wanajeshi wake na kuanza kuwasogelea bila hofu baada ya kujua Roma hana siraha tena na walikuwa wakiwasogelea huku wakirusha risasi.
Rufi baada ya kuona wanashambuliwa mfululizo alibadilisha upande ili kumpa nafasi Mage akimbie akiwa na Roma na Mage alifanikiwa kufikia chini ya jabali lakini ile wanataka kujificha chini Rufi aliwakimbilia tena lakini alishachelewa kwani palepale alipigwa na risasi ya mgongoni na aliishia kutema damu na kudondoka chini.
“Noo…!!”Roma alijikuta akitoa ukulele bila kuamini na alishindwa tena kujificha zaidi ya kutoka kwenye mikono ya Mage na kumsogelea Rufi.
Jin zhe alionekana kufurahishwa na tukio lile na palepale alitoa bomu la kurusha kwa mkono na kuliotoa pin.
Roma alikuwa ashamfikia Rufi na kumshikilia akiwa amepiga magoti.
“Roma kimbiaaa……!!!””Alijikuta akitoa ukulele Mage mara baada ya kuhushudia bomu likiruswa pale walipo na Roma alijikuta akimwachia Rufi na kuangalia lile bomu na palepale macho yake yalibadilika na kuwa ya rangi ya njano.

0687251346 nicheki watsapp .

ITAENDELEA.
 
Kwa nini ulimlipa cash pasipo kuhakiki kama ni mzinguaji?

Waandishi wote wa story nusu nusu huku wakikusanya hela ktk group huwa ni wezi tu.

Nikushauri tu uwe unalipia story iliyokamilika hapo utakuwa hujaibiwa.
hapo umenena mzee, hata mimi uwa napenda kununua story ikiwa imekamilika. nalipa, unanipa mzigo tunamalizana. kuna jamaa mmoja alikuwa anauza story, nikajua imeikamilika! nikalipia; si nikashangaa katuma hadithi nusu. nikamuuliza, mzee mbona unatuma mzigo nusu?! akajibu, bado naandika. aliniboa mpaka leo. kwanza sipendi arosto, sasa nalipia na arosto juu, ni ujinga.
 
Jamaa anazingua mnooo katutelekeza mpaka kwenye group lake kule na tumelipia ana kera
Mkuu hata sioni msingi wa malalamishi yako maana kama ulifuata maelekezo niliotoa kule na umelipia kwanini ukose mwendelezo huku wengine wanaupata
 
Ni ujinga kabisa kulipia kitu ambacho hakijakamilika.
it's all about choices kwasababu maelezo yanajitosheleza mwenzako kalipia 2500 tu kusapoti juhudi huku akipata urahisi wa kupata mwendelezo huna haki ya kusema ni ujinga.
Endelea kusubiri mwendelezo hapa wanaotusapoti kwa kidogo wataendelea kufanya hivyo
 
Mkuu hata sioni msingi wa malalamishi yako maana kama ulifuata maelekezo niliotoa kule na umelipia kwanini ukose mwendelezo huku wengine wanaupata
Labda kama Una magroup tofaut tofaut Ile nilipo mm unatuma mwendelezo kwa kujisikia mnooo na umefunga comment unadhani tutakwambiaje
 
Back
Top Bottom