Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaruka sana kwenye group,,umeruka vipande 9nishafanya marekebisho
Toka 620 ulipoishia umeanza 629 leoUnaruka sana kwenye group,,umeruka vipande 9
Vivian = Najma, why kabadilisha jina, tutajua huko mbele[emoji3][emoji3][emoji3]SEHEMU YA 505
“Umepitia mengi sana katika siku hizi chache na ni makosa yangu kuwafanya wote kupitia maumivu makali na mateso , nakuahidi nitafanya kila kitu kuhakikisha kitu kama hiki hakitokei tena’Aliongea Roma akijitahidi kumfariji Mage.
“Alright … Kwahio tunafanya nini sasa hivi , tunarudi nyumbani?”Aliuliza Mage na kumfanya Roma kwanza ageukia mahema yaliokuwa hapo na kabla hajatoa jibu alijikuta akihisi nguvu ya ziada ikitoka kwenye moja wapo ya hema.
“Hii nguvu…”Roma alitaka kuongea na kisha akamgeukia Mage.
“Nifuate”Aliongea na kisha walienda kuingia kwenye hema ambalo lilikuwa katikati kabisa , ndio hema ambalo Roma aligundua linatoa msisimko wa nguvu ambayo haikuwa ya kawaida.
Mage alikuwa kwenye mshangao kwani hakujua kwanini Roma alionyesha kuwa na mchecheto , baada ya kuingia ndani ya hema hilo eneo la katikati kulikuwa na kreti kubwa la mbao ya Mwaloni(oakwood), lilikuwa ni kreti ambalo lina urefu wa makadirio ya zaidi ya mita moja upana na urefu wake na ndio pekee ambalo lilikuwa kubwa ndani ya hema hilo.
“Hubby unajaribu kuangalia nini kwenye hilo Kreti”Aliuliza Mage kwa shauku kwani namna ambavyo Roma analifungua ni kama kuna kitu alikuwa akifahamu kipo ndani yake.
“Kama hisia zangu zipo sahihi , hiki ndio kitu ambacho nilikuwa nikitafuta sana muda wote”Aliongea
“Huh..?”Mage alionekana kuchanganyikiwa
Na muda huo huo Roma alifanikisha kubanjua loki ya kreti hilo kwa mkono mmoja na kutoa karatasi ya juu na kufanya kilichomo ndani kuonekana.
Mbele yao kulionekana Cauldron ya shaba (Sufuria kubwa au jungu la shaba), kaika kuta za Cauldron kulikuwa na naksi za kisanifu za bamba ambazo zimechorwa kama mchoro na wembamba sana kama vile ni uzi wa hariri.
Cauldron ya Shaba ilionyesha kushinda jaribio la muda kwa namna ambavyo kutu yake haikuwa ya kiwango kikubwa , lilikuwa kama sufuria kubwa la chuma kigumu ambalo kwa kuangalia tu lilistaajabisha na heunda ungejiuliza matumizi yake ni yapi.
“Kwasababu wakati nafika hapa nilikuwa nimepoteza uwezo wangu ndio maana nilishindwa kugundua uwepo wake , kwa nje unaweza kuona ni lisufuria tu la chuma lakini linatoa nguvu isiokuwa ya kawaida”Aliongea Roma kumwelezesha Mage ambaye alikuwa akishangaa shangaa.
“Kama nitakuwa sahihi katika kuotea basi naamini hiki ndio kitu ambacho Rufi aliniambia nitafute , chombo ambacho kina uwezo wa kuhimili moto mweupe na wa njano”Aliongea Roma na kumfanya Mage kushangaa ,tokea ajifunze mbinu za kijini maneno kama hayo hayakumchanganya kabisa.
“Kwa maana hii naamini ndio maana tulitaka kufa , kumbe kuna kitu cha thamani kilikuwepo karibu yetu”Aliongea Mage.
“Hata wewe umegundua hilo?”
“Ndio na kama ulivyosema ni sahihi basi tunaweza kusema misheni yetu imetimia”
“Lakini sina uhakika wa asilimia mia moja kama ndio kitu chenyewe ambacyo Rufi alikuwa akizungumzia , inabidi athibitishe mara baada ya kupona, kwasasa nitatafuta watu waje kukibeba na kukipeleka makao makuu”
“Unamaanisha nini kusema makao makuu?”Aliuliza na kumfanya Roma kuanza kuelezea kuhusu visiwa vya wafu na mpaka anamaliza ndio sasa Mage alipoelewa ndio mahali ambapo ndoa yake na Edna ilifanyika na aliikuta akionyesha hali kidogo ya huzuni.
“Usiwe hivyo niliwaalika lakini mkaamua kutohudhuria na isitoshe kama siku mkitaka kwenda nitawapeleka”
“Kwanini tusiende nacho Tanzania?”
“Tungefanya hivyo lakini mtu alievaa maski alienishambulia na mtu mwingine mwenye nguvu sana alienisaidia wote bado taarifa zao hatuna , kama wameweza kuja Australia basi inamaanisha kwamba na nyumbani itakuwa ni hatari zaidi, kama tutakipoteza hiki basi itakuwa hasara kwa maumivu yote tuliopitia”Aliongea Roma na kumfanya sasa Mage kuelewa.
Baada ya kukagua baadhi ya vitu vingine na kuona havikuwa sana na maana kwao waliacha na Roma alifanya mawasiliano na Makedoni kutuma maveterans kuja kuchukua mzigo wake na vitu vyote ambavyo vipo hapo ,ma vinavyohusiana na serikali ya China virudishwe kwa wahusika na ambavyo havikuwahusu vikahifadhiwe visiwa vya wafu.
Sababu ambayo Roma hakutaka kumtaarifu Sauroni kuleta wanajeshi wa The Eagles ni kutokana na kwamba vitu vya hapo vilikuwa na thamani kubwa na asilimia kubwa ya wanajeshi wake hawakuwa na uelewa navyo , hivyo kwa kutumia watu wa Mossad wenye ujasiri ingekuwa rahisi zaidi na salama , kwani kwa haraka haraka mizigo yote hapo huenda thamani yake ni dola bilioni moja.
Kuhusu Cauldron alipanga kwanza ikahifadhiwe kwenye ngome yake katika visiwa vya wafu mpaka atakapo fanya maamuzi mengine.
Baada ya kufanya mawasiliano Roma moja kwa moja alimchukua Mage na kumrudhiisha mjini na akampandisha kwenye ndege kuelekea Tanzania na baada ya ndege kupaa yeye aliondoka Australia na akarudi tena London kwa ajili ya Rufi.
Roma baada ya kufika ndani ya hospitali ya St mary’s alipewa maelekezo ya wodi aliopo Rufi , alikuwa alishatolewa muda tu kwenye wodi ya uangalizi wa karibu na kupelekwa katika wodi ya VIP.
Roma mara baada ya kufungua mlango aliweza kumuona, na sasa alionekana kurudiwa na fahamu na hata ule urembo wake kumrudia.
“Hey .. usinyanyuke utaumiza majeraha yako , kwanini unahangaika kama unakutana na raisi”Aliongea Roma mara baada ya Rufi kujitahidi kuamka haraka kiuoga woga mara baada ya kumuona Roma.
“Nilisikia ulinileta ndani ya hii hospitali usiku manane , na ukamleta daktari bingwa namba moja duniani kunitibu , nataka nikushukuru..”Aliongea kwa wasiwasi kama vile Roma alikuwa mgeni kwake.
“Kuna kipi cha kunishukuru sasa , hilo ndio jambo ambalo nilipaswa kufanya”Aliongea Roma kwa sauti ya chini na kumfanya Rufi kugnudua mabadiliko ya sauti yake tofauti na alivyokuwa akimwongelesha siku kadhaa zilizopita , sauti hio ilikuwa ni ya kujali.
“Vipi uko sawa?”Aliuliza Rufi. na kumfanya Roma ashindwe kujibu swali hilo mara moja maana aliona yeye ndio ambaye alipaswa kuuliza , alijikuta hisia mchanganyiko ziki uvaa moyo wake.
Ijapokuwa Roma alimsaidia kupona kwake kwa kumleta ndani ya hospitali hio , lakini kile alichokifanya kwa ajili yake na Mage ni jambo la kijasiri ambalo mtu yoyote asingeweza kufanya , Rufi alijitolea kupigwa risasi ili kuruhusu wao wasiweze kushambuliwa.
“Kwahio nini kiliokea baada ya hapo?”Aliuliza baada ya kumuona Roma amepiga kimya.
Na Roma alishituka na kuanza kumwelezea namna ambavyo amefanikisha kupata Cauldroni iliotengenezwa kwa madini ya shaba na kumfanya kushangaa.
“Lakini haikupaswa kuwa ya shaba , kama kuna nguvu ndani yake basi nina uhakika ilitumika kutengenezea vidonge na makadirio yangu kama yatakuwa sahihi huenda ina mwonekano wa rangi ya shaba kwasababu kimeishi muda mrefu sana , nina uhakika hakukuwa na teknolojia kubwa yakutengeneza jungu kubwa la kijini namna hio kwa kutumia shaba kwani teknolojia ilikuwa bado ndogo”Aliongea.
Cauldron ni Artifact ambayo ilitegenezwa miaka mingi sana iliopita huenda ziaid ya miaka elfu mbili, sasa kwa ukubwa wake ilikuwa ngumu kuamini kwamba kuna watu duniani waliotengeneza Cauldron ya madini ya shaba kwa ukubwa huo , kwani teknolojia ya kipindi hiko ilikuwa ndogo mno.,
“Kwasasa usiwe na wasiwasi sana , ukishapona nitakupeleka ili ukaone na kuthibitisha”Aliongea Roma na mara baada ya kumaliza alichaneli nguvu ya andiko ya urejesho katika mwili wa Rufi ili kumrahisishia kumponyesha majeraha ya nje ya mshono wake.
“Kwasasa nipo sawa , nadhani ni muda wako sasa wa kurejea Tanzania , naamini familia yako itakuwa na wasiwasi kwani tuliondoka muda mrefu”Aliongea Rufi na maneno yake yalimfanya Roma kweli kukumbuka nyumbani ,alimkumbuka sana mke wake na mtoto wake lakini pia pamoja na mama yake mzazi.
Roma alifanya maamuzi ya haraka na kisha akamwambia Rufi kupumzika hapo hoospitalini angalau kwa wiki mbili na ndipo angerudi kumchukua na kumrudisha Tanzania.
Roma hakutumia ndege tena kurudi nyumbani na isitoshe hakujisumbua hata kubadilisha mavazi hivyo moja kwa moja aliondoka Uingereza kwa mavazi yale yale ambavyo yalikuwa yamechafuka na damu, slijiambia ataoga akishafika.
Tanzania ilikuwa ni asubuhi ya siku ya ijumaa wiki mbili tokea Roma kuondoka , ndani ya nyumba yake alionekana Edna ambaye alikuwa hajavaa chochoe miguuni licha ya kuonekana na mavazi ya kutokea akifukuzana na Lanlan huku akiwa ameshikilia sweta mkononi.
“Lanlan if you don’t come over mummy gonna be really mad, come on”
“Lanlan usipokuja hapa mama atakasirika , njoo haraka?”Aliongea Edna akimwangalia Lanlan ambaye amevalia sare za shule bila ya sweta , sasa Edna alikuwa akitaka kumvalisha sweta lakini Lanlan hataki.
“No! Lanlan hates that , no more clothes it’s warm”Aliongea kimaanisha kwamba anachukia sweta na hataki nguo nyingine kwani kuna joto.
Kwasababbu ilikuwa ni asubuhi Edna aliona Lanlan anapaswa kuvaa sweta , lakini upande wa Lanlan kutokana na mwili wake ulivyo hakuhitaji sweta.
“Lanlan acha kuwa mbishi na nisikilize mama yako kama unataka watoto wengine wakupende”
“Kama ni hivyo Lanlan haendi shule na nitasubiri mpaka baridi iishe”Aliongea na kumfanya Edna ashindwe kujua cha kufanya alikuwa akitamani kumfokea lakini hakutaka kumfanya anune asubuhi asubuhi kwani alikuwa akimlea kama yai.
“Edna mwache avae hivyo hivyo kama hataki hilo sweta”Aliongea Blandina ambaye alikuwa akitokea nje.
Wakati Roma anaondoka Blandina alikuwa nyumbani kwao na sasa kwasababu baba yake mzazi alishafariki asingeweza kukaa katika nyumba ya Tajiri Azizi, ukiachana na hela alizovuna akiwa mke wa raisi. lakini pia katika urithi alipokea asilimia nyingi sana za hisa ambazo mmiliki wake alikuwa baba yake katika makampuni ambayo yanaongozwa na tairi Azizi hivyo angeweza kuishi mahali popote pale , lakini alishindwa kufanya hvyo kwani angeenda kuwa mpweke , hivyo mahali sahihi ilikuwa ni nyumbani kwa mtoto wake Roma.
“Lakini mama muda huu ni asubuhi na kuna baridi , nina wasiwasi anaweza akashikwa na shida ya kifua”
“Mh..!, Edna haina haja ya kumchukulia Lanlan kama mtoto wa kawaida ili hali sio wa kawaida , hata asipovaa hilo sweta na hali ya hewa ya jiji hawezi kupatwa na shida yoyote”Aliongea na Edna aliona amsikilize mama mkwe.
Muda huo huo wakati wakiongea upande wa nje ndio Roma alikuwa akifika , akiwa na mavazi yake yaleyale yaliochafuka na kugandiana damu.
“Son, kwanini unaonekana hivyo?”Aliongea Blandina kwa mshangao mara baada ya Roma kuingia ndani, Edna na yeye baada ya kumuona Roma akiwa na madoa doa alijikuta akikunja sura.
“Hio ni damu kwenye shati lako?”Aliuliza lakini alijikuta akijawa na aibu mara baada ya kufanyiwa kitendo ambacho hakukitegemea , Roma alimsogelea bila ya kumjibu na kumkumbatia.
Alijikuta akitaka kutoa ukulele kutokana na harufu mchanganyiko iliokuwa ikimtoka Roma iliochanganyika na harufu ya msituni baharini na damu.
“Mwaah..!! babe wife nimerudi”Aliongea Roma bila aibu pasipo ya kujali mama yake yupo kwani haikuwa kumkumbatia tu bali mpaka kumpiga busu la shavuni.
“Ni vyema umerudi , lakini kwanini unataka kuniua kwa kunikosesha pumzi asubuhi asubuhi?”Aliuliza Edna huku akijiangalia mavazi yake ambayo tayari alikuwa na mpango wa kuyatumia siku hio.
“Hehe.. nimefurahi kuwaona wote ni wazima wa afya”Aliongea Roma huku akimsogelea Lanlan kumshika lakini alimkimbia.
“Chubby unamkimbiaje baba yako wakati ndio amerudi?”
“Bad daddy , My name is not chubby”Aliongea na kumfanya Roma kutamani kucheka , alidhania Lanlana alishazoea jina lake la utani kumbe bado.
Roma hakutaka kubakia hapo zaidi , baada ya kumsalimia na mama yake pamoja na Bi Wena na Qiang Xi alianza kupandisha juu lakini aliishai katikati na kugeuka nyuma.
“Wife unaonaje ukaja kunisugua mgongo?”
“Screw you!!’(Kwenda huko)Aliongea Edna kijeuri akionyesha hayupo tayari na kuwafanya wengine kuangaliana na kujiuliza kuna nini kinaendelea maana Edna bado alionyesha kutokuwa kwenye hali ya kawaida ya kufurahia mume kurudi.
“Blandina unafikiri nini kimemtokea?”Aliuliza Bi Wema kwa wasiwasi na kumfanya Blandina kuwaza kidogo.
“Nashindwa kufahamu, lakini kama kuna tatizo ambalo limewatokea wengine alioambatana nao nadhani asingeweza kurudi nyumbanni mapema , hisia zangu zinaniambia kuna kitu amefanya akiwa mbali na nyumbani”
Edna yeye hakujali, kwanza nguo zake muda huo ni kama zimechafuliwa na alitaka kutoka nazo , hivyo alipandisha juu kwa ajili ya kuzibadilisha na wakati akibadilisha mawazo ya kumpeleka Lanlan siku hio shule yalikatika na kujiambia bora ampigie simu mwalimu wake kumwombea ruhusa ili akae chini apate kusikiliza nini kimemtokea Roma mpaka akarudi na damu kwenye nguo zake.
Baada ya Roma kuoga vizuri na kubadili mavazi hatimae aliweza kushuka chini akiwa anasubiriwa na watu waliojawa na shauku kubwa ya kumsikiliza kile ambacho kimetokea na safari yake kwa ujumla imekuwaje.
Roma mara baada ya kuketi alianza kuelezea hatua moja moja namna ambavyo waliweza kufika msitu wa Arnhem , namna ambavyo walishambuliwa na mtu asiejulikana na kumpelekea kupoteza uwezo wake kwa muda na mpaka waliposhambuliwa na kundi la masenari wa kundi la Hydralisk mpaka kupelekea Rufi kupigwa risasi.
Ijapokuwa alionekana kueleezea kwa sauti ya kawaida kama mtu ambaye anachukulia kilichotokea kawaida , lakini kila mmoja alishangazwa na kadhia waliopitia.
Katika stori nzima kila mmoja aliweza kumkubali Rufi kwa namna ambavyo alijitahidi kujitolea kulinda wengine.
“Huyu msichana Rufi ni mwenye roho nzuri sana , kama sio yeye huenda wewe au Mage mngepatwa na matatiz”Aliongea Blandina kwa wasiwasi.
“Nakubaliana na wewe , hata mimi siku ya kwanza kumuona amefika hapa nyumbani nilishamuona ni msichana mzuri sana mwenye ujasiri”Aliongea Bi Wema huku akimwangalia Edna kwa tahadhari.
“Roma unaonaje akishapona umualike nyumbani ili angalau tuweze kupata nae chakula na kumfahamu zaidi , Edna unaonaje juu ya hilo?”
Edna hata yeye aliguswa na ujasiri wa Rufi lakini kwa namna ambavyo Blandina alionekana kumkubali ilimfanya kupata ukakasi kidogo.
Kitendo cha Rufi kujitolea kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya Roma na Mage haikuwa cha kawaida na kilimfanya Edna ashindwe kukataa pendekezo lililotolewa, hata hivyo angekataa isingekuwa na maana kwani alijua ukiburi wa Roma akiwa ameamua la kwake kichwani.
“Okey mama hakuna tatizo”Aliishia kujibu Edna na mpango ukawa ni Rufi kukaribishwa nyumbani kwa ajili ya kupata chakula na familia ya Roma.
Je Bi Wema ndio siku ya kumfahamu Rufi kama mtoto wake?
SEHEMU YA 506.
SEOUL-REPUBLIC OF KOREA
Jumba la kifahari la wamiliki wa kampuni kubwa ya Starmoon , familia ya Park ilikuwa ni kielelezo tosha cha kuonyesha utajiri wao ndani ya eneo lote la Gangnam ndani ya jiji la Seoul nchini Korea kusini.
Familia ya Park ilikuwa ndio moja wapo ya familia ambazo zimefanya vizuri sana katika maswala ya uwekezaji katika bara la Asia lote , hususanni kwa mzee mwenyewe mmiliki.
CEO Park Juan alikuuwa shujaa ambaye mafanikio yake yanatazamwa kwa jicho la kipekee zaidi kwa mchango wake alioufanya katika ukuaji wa uchumi wa Korea kusini.
Lakini wahenga wanasema kifo hakimsubiri mtu na hili ndio jambo kubwa ambalo lilikuwa likienea kwa kasi ndani ya jamii za kitajiri(Chaebol) mara baada ya familia kuweka wazi juu ya Park Kuan mwenyekiti na raisi wa makampuni ya Starmoon kuwa na ugonjwa wa saratanni ya ini.
Tajiri akifariki au pale anapokumbwa na ugonjwa ambao utampelekea kifo ndani ya muda mchache wengi hawatozungumzia kifo wala ugonjwa na hilo ndio jambo ambalo lilikuwa likiendelea.
Habari kubwa ilikuwa ni nani ambaye anakwenda kurithi kampuni ya mabilioni ya tajiri huyo mara baada ya kufariki kwake , kwani kwa hali ambayo alikuwa nayo wengi waliamini asingechukua muda mrefu kuendelea kuishi.
Waandishi wa habari na watu ambao walikuwa wakipendelea sana kufatilia habari za kibiashara walikuwa wakitoa michanganuo yao na uchambuzi wa kila mwanafamilia na asilimia zake katika kurithi kampuni.
Katika majina ambayo yalikuwa yakizungumziwa yalijumuisha mtoto wa pili wa tajiri huyo aliefahamika kwa jina la Park Jiki , mtoto wake wa kike afahamikae kwa jina la Park Jiyeon na mtoto wake mwingine wa kumlea afahamikae kwa jina la Park Jonghyun.
Kitu ambacho kila mmoja hakuweza kufahamu wala kuotea ni pale Park Juani kuagiza mtu kwenda mpaka nchini Tanzania kwa ajili ya kumrudisha nyumbani mjukuu wake wa mtoto wake wa kwanza.
Wengi wao bara baada ya kupata habari hio waliona kuruhusiwa kwa mtoto ambaye amekaa sana nje ya taifa la Korea kurithi kampuni kubwa kama hio ni jambo ambalo haliwezekani na hata kama maamuzi kama hayo yatafanyika basi ni ya kijinga. lakini hata hivyo hakuna ambaye alikuwa akijua ni maamuzi gani ya mwisho mwisho ambayo Park Juan angefanya kuhusiana na mtu ambaye angefaa kumrithi, hivyo habari nyingi zilikuwa za makisio kutokana na uadifu wa kila mwanafamilia.
Unajua katika mataifa yalioendelea kuendesha kampuni sio swala la kuamka na kwenda kazini tu , hasa kwa kampunni kubwa kama Starmoon, swala la Park Juan kuwa mgonjwa lilikuwa jambo la kufatiliwa na wengi kwasababu kuu moja, kampuni ya Starmoon ni public company na ina raia wengi ambao wamewekeza hisa zao na ili siku zote waendelee kupata faida lazima wajue kila kitu kinachoendelea si ndani ya kampuni tu lakini mpaka ndani ya familia.
Wananchi wa mataifa yalioendelea kama Korea wengi wao elimu yao ni ya viwango vya juu na si ajabu kumkuta mwanamke wa miaka themanini akifuatilia maswala ya uchumi wa kampuni flani ndani ya taifa ili kuwekeza.
Sasa ndani ya jumba la kifahari la familia ya Park katika chumba kikubwa kilichokuwa floor ya tatu juu kabisa alionekana mwanamke wa kikorea mzuri wa wastani , kijana kiasi alievalia mavazi ya ukijakazi akiingia ndani ya chumba upande wa kushoto.
Kilikuwa ni chumba kikubwa mno ambacho kimepambwa kwa mapambo ya kileo yalioendana na mpangilio wa thamani za gharama kwanzia chini mpaka juu darini, kilikuwa mpaka na hadubini katikati ambayo hutumika kwa ajili ya kuangalia nyota.
Yule kijakazi mara baada ya kuingia alionyesha heshima kwa kuinamisha kichwa chake mbele ya kitanda kikubwa cha sita kwa sita ambacho kimewekwa eneo la katikati ya chumba na juu yake alionekana msichana aliejilaza kivivu kwenye kitanda.
Ni msichana alievalia mavazi ya kulalia yenye vidoti doti vya rangi ya pinki na nyekundu na kwa staili aliolala alionyesha kabisa hana mpango wa kuamka licha ya muda kuonyesha umeenda sana tokea kulivyokucha.
“Miss Yezi kifungua kinywa kipo tayari , tafadhari naomba uamke, kama utaendelea kulala utachelewa kwenda darasani”Aliongea kwa kikorea huku akichanganya na kingereza na Yezi aliekuwa amelala alimsikia vizuri tu lakini hakufumbua macho.
Kwa kipindi chote ambacho alikaa Korea alikuwa ashaanza kuelewa kikorea licha ya kwamba mdomo ulikuwa mzito kuzungumza.
Tokea alipofika Korea aliweza kutafutiwa mwalimu ambaye si tu alimfundisha kikorea lakini pia alimfundisha na lugha ya kingereza rasmi.
Yezi alikuwa akiandaliwa kwa aili ya kurithi kampuni kubwa ya Starmoon hivyo ilikuwa ni mantiki kuweza kuelewa vizuri kingereza na Kikorea, yale maisha yake aliozoea nchini Tanzania yalibadilika kwa kiwango kikubwa sana kwani kila akiamka alikuwa amepangiwa ratiba ya kufanya hiki na kile mpaka jua linapozama.
“Eunjung nimechoka naomba uniache nilale kidogo”Aliongea Yezi
“Young miss!!, Mwalimu Vivian ametoa taarifa kwamba jana hukumaliza ratiba yako yote ya mafunzo na kaniambia kama utaendelea kuwa hivi atampigia simu CEO na wewe mwenyewe unaelewa tokea urudi CEO afya yake imeimarika sana na hata siku ya jana amefanikisha kutembea mwenyewe umbali mrefu na hata daktari amesema kwasasa ugonjwa wake utategemea na hisia zake , hivyo kama atasikia taarifa za utoro wako na kulala muda wote naamini atakasirishwa sana na tabia yako”Aliongea mwanadada aliefahamika kwa jina la Eunjung na kauli yake ilimfanya Yezi kushikwa na hairia na kisha kujinyanyua kutoka kitandani.
Alionekana kupendeza zaidi na zaidi kuliko alivyokuwa Tanzania , ijapokuwa mwili wake ulionyesha dalili za kukonda lakini aliimarika katika mambo mengi.
“Nadhani kwasasa unajua kwanini nakuita muuaji mwenye tabasamu, kila siku unaniamsha kwa kunitafutia sababu ya kunifanya nijione ni mwenye hatia”
“Hapana Miss , sio hivyo , mimi ni kijakazi tu wa hapa na najitahidi kutimiza majukumu yangu , sikutaka tu kukuona ukiendelea kumsubirisha mwalimu wako Vivian nadhani unajua hasira zake za karibu”Baada ya kukumbuka ukali wa mwalimu wake alijikuta akianza kuharakisha mambo.
Wakati anarudishwa Korea kwa ajili ya kuonana na babu yake ambaye alikuwa na kinyongo nae kadri siku zilivyosogea hatimae sasa taratibu alianza kujiona kama mwanafamilia.
Na kwasababu hio familia ya Park ni kama familia za kitajiri nyingi ambazo zilikuwa na sheria kali, na kwa mtoto kama Yezi alipaswa kuzifuatisha, kwaYezi ilikuwa ni lazima zaidi ili kumfanya kuweza kufahamu zaidi tamaduni za kikorea , hivyo kwa maneno marahisi alikuwa na mengi ya kujifunza na ndio maana Park Juan alihakikisha Yezi anapata mwalimu mzuri
Na hapo ndipo alipokuja kuajiriwa mwalimu ambae ana Advanced Diploma ya lugha na fedha , ambaye ana uwezo wa kuzungumza lugha tatu , Kiswahili , Kingereza na kikorea., alikuwa ni mwalimu wa kike mpole mrembo sana aliefahamika kwa jina la Vivian.
Na kwa kile alichokifahamu Rufi ni kwamba mwalimu wake ni msomi kutoka chuo maarufu duniani cha Harvard na jambo la kushangaza zaidi kuhusu mwalimu wake ni kwamba alikuwa amezaliwa nchini Tanzania , akakulia nchini Tanzania na ndipo alipoenda masomoni Harvard na kupata ajira nchini Korea.
Mwalimu Vivian kutokana na tabia yake ya ukali na usiriasi ilimfanya kupata pointi za kutosha kutoka kwa babuu yake Yezi na kuona ni mtu sahihi ambaye anaweza akamfundisha Yezi.
Mwanzoni Yezi alionyesha kuwa na furaha mara baada ya kufahamiana na mwalimu Vivian kutokana na kwamba alikuwa mbongo lakini mara baada ya masomo kuanza ndipo alianza kumchoka kutokana na ukali wake linapokuja swala la kujifunza lugha na maswala ya uongozi wa biashara.
Baada ya kujisafisha kwa haraka ili kumuwahi mwalimu Vivian , alivaa nguo zake safi na kisha akavuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akamfuana Eunjung kwenda chini.
Nyumba hio kubwa hakuna mtoto wa Park Juan anaeishi kwani wote walikuwa wakubwa na ni wenye familia zao , hivyo mwanafamilia pekee aliebaki ni Park Juan yeye mwenyewe pamoja na Yezi mara baada ya kurudi.
Wakati huo upande wa eneo la chini sebuleni alionekana mwanamke alievalia Blazer ya rangi nyeusi , ambaye ana nywele ndefu alizofunga nyuma na kibanio, hakuwa mkorea bali alikuwa mwafrika wa rangi nyeupe ambayo imefifia , huenda kutokana na hali ya hewa ya ubaridi ya jiji la Seoul kwa nyakati hizo.
Alikuwa amekaa kwa kujiamini sana akiwa amekunja nne na mkononi alikuwa ameshikilia jarida flani la maswala ya uchumi na siasa akipitia pitia.
Baada ya kusikia vishindo vya hatua kutoka juu , aliizungusha shingo yake na kugeuka na kisha akatoa tabasamu la kupendezesha sana uso wake uliojaa haiba ya upole , uzuri wa huyo mwanadada huenda angekuwepo tanzania angekuwa habari ya mjini na kilichombeba si tu kwamba alikuwa mzuri wa sura lakini pia alionekana kuwa na mapozi ya watu waliostaarabika.
“Yezi kwasababu umelala kwa muda mrefu leo , nitahakikisha masomo yetu ya leo tunayafidia na muda wako wa mapumziko”Aliongea kwa sauti yake tamu ambayo iliharibiwa na matamshi ya lugha ya kikorea.
“Mwalimu Vivian naomba tupunguze spidi , kwa staili hio nitachoka sana”Alilalamika Yezi.
“Sio kuchoka ila wewe ni mtoro na fanya haraka upate kifungua kinywa na kisha tuendelee na kujifunza kingereza kuanzia pale tulipoishia siku ya jana na baada ya hapo nitakupa zoezi la kufanya”Aliongea na Yezi ashamjua hivyo hakuitikia zaidi ya kukaa kwenye meza na kuangalia vyakula mbalimbali vilivyoandaliwa kwa ajili yake tu, hakuwa yule Yezi tena mkaanga chipsi au Yatima huyu alikuwa Yezi mwingine ambaye huenda Tanzania angebatizwa jina la mtoto wa kishua.
Yezi alikunywa kiasi cha supu akijua sio ya moto na alijikuta akiitema chini na kuichafua kwenye nguo zake na kuanza kujifuta na mkono.
“Usijifute na mkono tumia tishu”Alifoka Vivian.
“Kwanini unakula pasipo kujali ustaarabu, mpaka sasa unatakiwa kuelewa utakuwa na vikao vingi baada ya kupewa kampuni pamoja na kuhudhuria matukio mengi na watu wazito wazito hivyo kila unachokifanya lazima kionyeshe namna gani umestaarabika”Aliongea Vivian kwa kuelekeza.
Eujung hakuingilia, alikuwa kimya akimwangalia Yezi aliekuwa akihangaika kutafuta napkin na palepale alimpa ishara kijakazi mwingine aliesimama kwenye meza ili kumpatia Yezi tishue ajifute.
Yaani licha ya kwamba alikuwa akila mwenyewe lakini wadada warembo vijakazi wa nyumba hio walikuwa wamejipanga msururu wakimwangalia namna ambavyo alikuwa akila chakula, na huo ndio utaratibu wa familia nyingi za kitajiri ndani ya Korea , wakati wanafamilia wakipata chakula wafanyakazi hata kumi utakuta wamejipanga mstari wakiwaangalia wanakula ili ikitokea wanahitaji kitu waweze kuwahudumia kwa haraka.
“Mwalimu Viviani wote sisi tumezaliwa Bongo , haina haja ya kuwa mkali kiasi hicho , yale maisha ya uswahilini unaelewa wewe mwenyewe , halafu ukiendelea kukasirika sura yako inakunjamana na utapoteza urembo wako ohoo…”Aliongea kwa kiswahili kile kile cha kitanzania kabisa na kuwafanya wahudumu wasimwelewe ameongea nini lakini kwa Vivian alielewa kila kitu.
“Sio kama nakuwa mkali ila nakuelekeza namna ya kuwa mstaarabu , sitaki watu waanze kukuzungumzia vibaya kama moja ya watoto wa familia ya Park na kuanza kusema taifa langu vibaya na isitoshe walionipa kazi ya kukufunza wana mategemeo makubwa juu yangu”
“Sura ya kimalaika lakini roho ya kishetani”Aliongea Yezi chini chini ili Viviani asimsikie.
“Nasikia maneno yako ya kunilaani , halafu nikukumbushe mara nyingine usitumie lugha ya kiswahili mbele yangu , ni kingereza na kikorea ndio lugha unazopaswa kuzungumza ili ulimi wako uwe mlaini.
“Sawa nimekuelewa mwalimu, lakini naomba nikuulize swali?”
“Uliza?”
“Umekaa kwa muda gani Marekani?”Aliuliza Yezi.
“Mh.. nadhani kama miezi sita kwenda saba hivi”Aliongea.
“Miezi sita , Wow!! inaonekana una uwezo mkubwa, umeweza kujifunza kuongea kingereza fasaha ndani ya miezi sita na kupewa cheti cha heshima?”Aliongea na akamfanya Vivian kucheka kidogo na kisha akaongea.
“Wakati nilipokuwa Tanzania nilikuwa nikisomea mtandaoni na nilichukua kozi nyingi za lugha ya kingereza na Kikorea na Harvard nilienda kupata kutambulika kitaaluma tu”Aliongea.
“Lakini bado upo juu na hata kama utamuuliza babu kuhusu wewe ni dhahiri atakuwa na mawazo sawa na ya kwangu”Aliongea Yezi akijaribu kumpamba pamba mwalimu wake.
“Unafikiri unaweza kunifanya nipunguze ukali kwa kunipamba?”
“Ah,,! kwanza mwalimu Vivian nina maswali mengi juu yako na mpaka sasa nashangaa kwanini umeamua kuwa mwalimu , kwa mwonekano wako wa kirembo naamini kuna wanaume wengi mabachela ambao wangeweza kukuoa , kwanini unapoteza ujana wako kwa kuwa mwalimu wa mtoto mtukutu kama mimi?”
“Yezi malizia muda unasonga , unapaswa kuelewa mimi kuwepo hapa kukufundisha nipo field niliopewa na profesa wangu na nikikamilisha mafunzo yako kwa kupata uzoefu narudi Marekani kuendelea na masomo yangu ya Masters , kwahio usinipe wakati mgumu wa mimi pia kukamilisha kazi yangu”
“Masters?Mwalimu Vivian nakushauri usijifanye hivyo ni kupoteza muda kama mwanamke , wewe ni mrembo na ni rahisi kuolewa na mwanaume aliefanikiwa na ukayafurahia maisha yako”
“Wewe mtukutu mwenye maneno mengi , umekazania mwanaume mwanaume , mimi kwangu kwasasa nachagua masomo kuliko mwanaume”Aliongea huku akimzodoa.
“Acha kunifanyia hivyo mimi sio mtoto?”
“Katika macho yangu wewe ni mtoto tu”Aliongea na kumfanya Yezi kutoa ulimi wake nje akimchokoza mwalimuwa wake.
“Lakini bado mwalimu Vivian mimi sikuelewi, kwahio mpaka muda huu huna hata mpenzi kama hutaki ndoa?”
“Hakika sina mpenzi na sitafuti kuwa na mpenzi wala ndoa?”Aliongea Vivian huku akionyesha kukunja sura na kwa jinsi anavyoongea ni kama wale wanawake ambao wameumizwa kwenye mahusiano.
Unganisha doti imfahamu Vivian ni nani…
ITAENDELEA
Mkuu singanojr, weekend murua sana Leo!Vivian = Najma, why kabadilisha jina, tutajua huko mbele[emoji3][emoji3][emoji3]
Hao wanalalamika huko kwa group kuwa unazingua.it's all about choices kwasababu maelezo yanajitosheleza mwenzako kalipia 2500 tu kusapoti juhudi huku akipata urahisi wa kupata mwendelezo huna haki ya kusema ni ujinga.
Endelea kusubiri mwendelezo hapa wanaotusapoti kwa kidogo wataendelea kufanya hivyo
Mbongo kwenye Ubora wakoHao wanalalamika huko kwa group kuwa unazingua.
Wamekuamini wakajuinga na group ila unawaacha na arosto nyingi japo wamekulipa.
Ikiwa wewe sio mzinguaji hawawezi kukulalamikia ikiwa unawapa kitu mfululizo.
Nimeamua kutokuingia kwa group kwa sababu ya malalamiko yao hao waliolipia, ni heri nibaki na arosto hapa hapa, nikiona hawalalamiki basi na mie nitaingia kwa group [emoji23]
Hujanijibu bosiMbongo kwenye Ubora wako