NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.
MTUNZI: SINGANOJR.
SEHEMU YA 501.
Siku iliofuata kila mmoja alibeba begi lake na safari ikaanza rasmi , kabla ya kuondoka Roma alibeba makaa ya kuni zilizoungua na kuweka kwenye begi lake na kumfanya Mage kushangazwa na jambo hilo.
“Hubby si utachoka sana , kwanini unabeba hayo makaa , tunaweza kutokuwa na chakula lakini kuwasha moto njiani ni rahisi kwani tuna kiberiti”..
Tokea waanze safari alikuwa hajazoea kumwita Roma mpenzi kutokana na Rufi lakini mara baada ya Roma kupoteza uwezo wkae alijikuta akishindwa kujizuia.
“Haya makaa sio kwa ajili ya kuwashia moto , huko tunakoelekea maji hayatokuwa salama na yamejaa minyoo na sumu na pia hatuna uwezo wa kuyachemsha hivyo njia pekee ni kuondoa sumu yake kwa kutumia mkaa nadhani ni bora zaidi kuliko kuugua njiani kwa kuumwa na matumbo”Alielezea Roma huku akitabasamu.
Roma hakuwa tayari kuona wanawake hao wanapatwa na shida yoyote njiani kwani ingekuwa ngumu sana kutoka kwenye msitu huo kwasababu mwili wake ulikuwa na sumu na asingeweza kuwasaidia pale watakapopatwa na ndio maana alikuwa akichukua kila tahadhari.
Mage hakuwa amelifikiria hilo, hivyo mara baada ya kuelewa hakuuliza tena swali hata hivyo alikuwa mgeni kwenye mambo mengi.
Roma ndio ambaye aliongoza njia huku wakichukua uelekeo wa Kaskazini aliamini ndio upande ambao ungekuwa karibu zaidi na bahari kuliko kurudi walikotoka mwanzo, jua lilishaanza kuunguza licha ya kwamba bado ilikuwa ni asubuhi na kadri walivyokuwa wakisonga mbele Roma alikuwa akichoka mno na kuhema kwa nguvu kama ilivyokuwa kwa Mage na Rufi tu.
Kiasi kidogo cha unyevu nvyevu uliokuwa ukidondoshwa na miti ya msitu huo ulimfanya kuelewa kwanini watu hawakupendelea kuishi kwenye hayo maeneo, ilikuwa ni hali ya kisauna mwanzo mwisho.
Mage na Rufi lipsi zao zilianza kupasuka pasuka kutokona na ukosefu wa maji pamoja na njaa lakini kwa wakati huo walikuwa na wasiwasi zaidi juu ya Roma kutokana na sumu iliokuwa ndani ya mwili wake.
Njia yote waliotembea hakukuwa na maji zaidi ya vichaka tu ambavyo vilikuwa vimekauka kutokaa na hali ya ukame na baada ya kutembea mita kadhaa hatimae waliweza kufika kwene eneo ambalo lilikuwa kama bwawa ambalo limeacha tope tu kwa juu na palepale Roma alikata tawi la mti na kufukua lile tope na ndani ya dakika chache tu maji yalianza kuonekana na kuwafanya waangaliane kwa mshangao.
“Mara nyingi ukikuta sehemu yenye mto au bwawa lililoacha tope kwa juu jua chini yake kuna maji ni kama nadharia lakini naona tumekuwa na bahati”Aliongea na kuwafanya wafurahi.
“Ngoja nikusaidie”Aliongea Mage akiruka upande wa pili na akaanza kumsaidia Roma kupanua shimo kwa kutumia mikono yao, Rufi alijikuta akishangazwa na jambo hilo lakini mara moja na yeye aliungana na wakaanza kutengeneza kijidumbwi ili maji yakusanyike sehemu moja.
“Haina haja ya kunisaidia ninaweza kufanya hivi mwenyewe”aliongea Roma mara baada ya kuona wanachafuka.
“Acha kujifanya mgumu na utuache tukusaidie au unajisikia vibaya kwasababu hauna uwezo wako?”
“Ah..! sijamaanisha hivyo”Aliongea huku akimwangalia na aligundua tayari Mage alishajichafua usoni.
“Babe ushajichafua tayari baada ya kujishika pua yako”Aliongea na kumfanya Mage kweli aone amejichagua baana alijifuta na mkono wakushoto akidhania ni msafi.
Roma alijikuta akiguswa na namna wanawake hao wanavyochakarika , ijapokuwa alichokuwa akifanya sio cha kutumia nguvu nyingi lakini ushirikiano wao ulimfanya kuona kweli ana watu sahihi.
Baada ya kutengeneza kidumbwi maji yalianza kutiririka kutoka pande zote na kujaa.
“Yashajaa tayari lakini tunayatoaje hapa na kuyasafisha kwani yana matope?”
“Hio kazi ngoja niifanye mimi wewe angalia tu”Aliongea Roma na kisha akachukua nguo safi kwenye begi na kuiingiza kwenye kile kidumbwi na kisha akakamua kwenye kontena na baada ya hapo alichukua ule mkaa aliobeba na ndani ya dakika chache tu maji yalionekana kuwa masafi kabisa kwa ajili ya kunywa.
Kitendo kile kiliwafanya Rufi na Mage kushangazwa na mbinu zake za kupambania kuishi kwenye hali ngumu kama hio, baada ya kunywa na kutosheka walijaza ya kutosha kwenye makopo yao na kisha safari ikaendelea.
“Kutokana na Roma kukosa uwezo wake alijitahidi kuwa makini sana na vichaka kabla ya kuwaruhusu kupita , lakini bahai nzuti hawakuweza kukutana na hatari yoyote.
Wakati inafika muda kama wa saa tisa Rufi alijikuta nguvu zikimwishia kutokana na njaa na alitembea kinyonge mno akiwa amechoka kutokana na kukosa mazoezi tofauti na Mage na Roma.
Ilibidi wasimame na kumwangalia alivyokuwa akihema kwa shida akiwa ameshikilia magoti na kuinamisha kichwa chini.
“Hubby nina njaa pia na tokea jana hatujala kitu chochote na tumetembea sana”Aliongea Mage na kumfanya hata Rufi kuona aibu maana alijua Mage ameongea hivyo kwa ajili ya kumsaidia.
Kutokana na changamoto walizopitia yale mawazo ya Mage kumuona Rfufi kama Vixen yaliisha kabisa , alijiambia kama alikuwa hivyo huenda siku ya jana asingemfukuzia wakati anajaribu kumsogelea Roma wakati wa hatari.
Roma alijikuta akitingisha kichwa , alikuwa ashasahau kuwa stamina zao sio imara hivyo hawawezi kuvumilia muda mrefu , hivyo kwa muda huo alipaswa kujua namna ya kupoza njaa yao.
Alijaribu kuzungusha macho kwenye msitu huo kuangalia kama anaweza kuona chochote cha kulika lakini hakuona kitu , lakini baada ya kuangalia kwa umakini mbele aliweza kuona mti ambayo ulikuwa una matunda juu yake.
“Nifuateni”Aliongea na kisha wakaanza kutembea kwenda mbele.
Baada ya kuufikia alijaribu kuangalia mizizi yake kwa kufukua kiasi ili kuuchunguza na kisha alioneana kuridhika na kuchuma baadhi ya matuda yaliokuwa juu yake.
“Huu ni mti wa matundwa mwitu , majani yake yana umbo mviringo na mizizi yake imesambaa kwenda chini ardhini ili kutunza maji , kwa sifa hizo matunda yake ni salama, yanaweza yasiwe matamu lakini hatuna namna jitahidi kula kiasi cha kutosha ili angalau muongeze Vitamin C na huko mbele najua tutapata namna ya kupata chakula”Aliongea Roma na kuwafanya wasifikirie mara mbili na kuanza kula huku wakikunja sura kwa uchachu wake.
Roma na yeye hakuwa nyuma alichukua kiasi kwa ajili yake lakini hata hivyo alijua kwa upande wao wasingeweza kudumu kwa muda mrefu pasipo ya kupata chakula chenye calories.
Safari iliendelea kwa muda mrefu kama masaa manne matano hivi na waliweza kufikia mto na kwasababu ilikuwa tayari ni jioni Roma aliwaambia ni muda wa kuweka kambi hapo kupumzika mpaka siku inayofuata , aliwapa kazi ya kutafuta eneo zuri na yeye alienda kutafuta kitu chochote ambacho kingeweza kuwasevu kama chakula cha usiku.
Baada ya Roma kuwaacha, walienda kukusanya kuni zilizokauka kwa ajili ya kuwasha moto .
Roma alitembea kando ya mto kuangalia namna yoyote ya kuweza kupata kitoweo , hakuwa na kifaa chochote cha kumsaidia kuvua lakini pia hakuwa na uhakika kama huo mto ulikuwa na samaki.
Baada ya kuhangaika kwa dakika kumi na tano hatimawe aliweza kuona nyoka wa majini akiambaa ambaa na alisema huyo huyo anafaa na aliingia majini na kisha akamnyaka mkononi na kumbeba juu huku akipinda pinda na alichokifanya ni kutumia meno yake kunyofoa kichwa chake.
Kikawaida nyoka wa baharini hawakuwa na sumu nyungi na katika hali ambayo kama ni binadamu umekosa kabisa chakula unashauriwa kumkamata na kumtumia kama chakula na isitoshe nyoka wa aina hio wana calories nyingi hivyo kiasi kidogo tu kinaweza kukufanya udumu kwa muda mrefu pasipo ya kuhitaji kula tena.
Baada ya kung’ata kichwa chake alikitema chini , hakuwa na namna kwa muda huo zaidi ya kuwa kama watu walioishi zama za kale.
Roma airudi kuelekea kwenye kambi yao hku akiwa ameshikilia nyoka wake lakini wakati akiwa anakaribia alisikia Mage akitoa ukulele upande wa pili na kumfanya kushituka na kuwahi , ilikuwa ni sehemu ambayo wamewasha moto na nyoka mkubwa alionekana akitoa ulimi wake kama matawi akiwasogelea.
“Kaa mbali kabisa , huyu ni Nyoka wa Australia afahamikae kwa jina la Coastal taipan , ndio nyoka namba moja mwenye sumu dunia nzima na akishambulia ni ngumu kumkwepa”Aliongea Roma na kuwafanya wote kwa pamoja kuondoka ndani ya hilo eneo na kukaa mbali.
Roma hakujiuliza mara mbili alitupia nyoka wa majini pembeni na kisha akaokota tawi na kulitengeneza kama fimbo na kuanza kumshambulia kwa kumlenga kichwani..
Lakini muda ambao alikuwa akitaka kumlenga yule nyoka alishituka na kuruka wakwanza kumlenga Roma na alikuwa amechelewa kwani tayari alishang’atwa kwenye mkono.
“F**ck!”
Alilaani , ijapokuwa alikuwa amejipanga kushambuliwa lakini ilimchukiza kushindwa ujanja mpaka na nyoka , kama ingemtokea kabla hajapoteza uwezo wake angekwepa tu kwa kutumia nguvu zake za kijini na hata kanuni za anga.
Hakuwa tu amepoteza uwezo wake lakini pia hata ubongo wake ulifanya kazi taratibu sana na hakuwa na uwezo wa kuanza kufikiria kanuni za anga na akili yake hio na kugeuza kama siraha.
Roma baada ya kuona ashang’atwa hakuona haja tena ya kutumia ule mti hivyo alitupa na kisha akamrukia yule nyoka na kumshika kichwa chake na kumkaba eneo la shingoni kupelekea yule nyoka kuachama na hio ndio nafasi kwa Roma kwani alishika taya lake na kisha akavuta kwa nguvu na kumfanya achanike katikati kama vile ni kitambaa.
“Hubby uko sawa?”Aliuliza Mage baada ya kuona nyoka alishakufa.
“Usijali nipo sawa siwezi kufa”Aliongea Roma huku akishikilia jeraha lake .
“Ijapokuwa nimepoteza nguvu zangu lakini mwili wangu bado una uwezo mkubwa wa kuvumilia sumu ya aina yoyote ile , hivyo nikipumzika kidogo tu nitakuwa sawa”
Aliongea kuwatoa wasiwasi lakini ukweli Coastal taipan kama atamng’ata binadamu wa kawaida ni ngumu sana kupona ,afiti zinasema nyoka mmoja kimahesabu anaua zaidi ya panya elfu ishirini katika uhai wake kwa kutema sumu yake tu.
Licha ya Roma kusema yupo sawa lakini hali yake ilimfanya Mage kushindwa kujizuia, ule upolisi aliokuwa nao ulishaisha muda na hapo alikuwa kama mwanamke tu ambaye anamtegemea mwanaume.
“Kwani kulikuwa na ulazima gani wakumuua si ungemfukuza tu akaenda zake , tayari upo kwenye hii hali lakini bado unatafuta matatizo mengine”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie kwa huruma na kisha akachukua nyoka wa majini aliemkamata na kisha akampatia Rufi.
Mage baada ya kuona chakula walichoatafutiwa ni nyoka alijikuta hata kilio kikikata ghafla na kuwa katika bumbuwazi.
Upande wa Rufi hakuona shida , huenda ule uchina kwenye damu yake ulimfanya kutokuwa na wasiwasi na aina hio ya chakula.
“Huyo nyoka mmoja atawatosha nyie tu , sina jinsi na giza ndio linaingia zaidi hivyo nadhani atawaondolea njaa..’Aliongea na kumfanya Rufi kugusuwa na kauli yake maana alikuwa akimaanisha kwamba yeye hana haja ya kula hivyo wao ndio wale, ilimgusa zaidi yeye kutokana na kwamba hakuwa na uhusiano wowote na Roma hivyo hakupaswa kumjali zaidi ya Mage.
“Rufi mchome kwenye moto na kisha kwangua ngozi yake na mpasueni mtoe vitu vyote vya ndani na kisha unazungusha kwenye mti na unachoma tena nyama yake , hakikisha inaiva vizuri kwani nyoka wana minyoo wengi msije kutapika”
Mage alijikuta akichuchumaa chini huku akimwangalia Riufi akifanya kazi hio ,ijapokuwa hata wakati alipokuwa kwenye mafunzo ya kipolisi walifundishwa namna mbalimbali za ku’survive’ wakiwa maeneo kama msituni lakini hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa kwenye hali ya uhalisia.
Roma alipumzika kwa zaidi ya lisaa na aliwasaidia kuhakikisha nyoka ameiva vizuri na kumkata kati na kisha akampatia Rufi na Mage.
Ajabu ni kwamba nyama yake ilipofikia pua za Mage ilionekana kunukia vizuri na njaa aliokuwa nayo alijikuta akianza kula mara baada ya kumuona mwenzake anafurahia.
“Roma kula kidogo tu”Aliongea Mage.
“Hapana kutokana na mwili wangu ulivyo naweza kudumu muda mrefu pasipo ya kula “
“Lakini huwezi kukaa na njaa hivyo, kwasasa huna nguvu yoyote na umeng’atwa na nyoka”
“Mage nimesema kula bwana , ngoja nikajaribu kutafuta chochote kama nitabahatika kupata”Aliongea Roma na kisha alisimama na kuondoka katika hilo eneo.
Ukweli ni kwamba alikuwa na njaa tena sana kutokana na kwamba mwili wake umepoteza nguvu na alichokuwa akitegea ni chakula.
“Inaonekana kashaamua sisi tule yote , tuendelee tu”Aliongea Mage huku akimwangalia Rufi na alitingisha kichwa kukubaliana nae.
Nyama ilikuwa ikinukia vizuri lakini bado haikuwa tamu , lakini licha ya hivyo waliendelea kula kwani hawakuwa na namna nyingine ya kupata chakula.
“Has he always been this good to you guys?”Aliuliza Rufi akimaanisha je Roma muda wote ni mwenye kuwafanyia mazuti muda wote.
“Hata mimi sijajua , muda wote ni mwenye kutulinda lakini hata hivyo huu udhoefu umenipa nafasi ya kumjua zaidi”Aliongea Mage na kumfanya Rufi kutingisha kichwa na hakuongeza swali lingine.
Hakuwa nyoka mdogo hivyo nyama iliwatosheleza kwa zaidi ya asilimia themanini kwani baadhi ya vitu vingine hawakuweza kutafuna kutokana na kuwasha.
Muda huo huo walimuona Roma akirudi kwa kukimbia akiwa kifua wazi, kwa mwonekano wake ilionekana kama kuna kitu ambacho amefanikisha kupata lakini walishangazwa kuona amevua shati.
Baada ya kuwafikia ndipo walipoweza kuona kitu alichobeba kina mchanganyiko wa mchanga , walijikuta wakisimama bila ya kumsogelea.
‘Umebeba nini?”AliulizaMage na Roma alitua lile shati lake chini na hapo hapo waliweza kuona wadudu wakipanda kwa juu na kumuogopesha Mage na Rufi.
“Ah..!!”Walitoa mshangao wao huku wakichungulia ndani na ndipo walipogundua ni wadudu wengi waliokuwa kwenye masega .
“Acheni wasiwaso ni masega ya wadudu aina ya mchwa(termites) hawang’ati na ni wazuri mno”Aliongea Roma.
“Mchwa…!!!”Walishangaa ilikuwa mara ya kwanza kwa Mage kuona aina hio ya mchwa.
“Kwanini umewaleta hapa au unataka kutufanya tupatwe na woga?”Aliuliza Rufi na Roma hakujali alikaa chini na kisha akachukua wadudu hao kwenye mkono na kisha akawapeleka wote mdomoni.
“Ah.. wewe,, wewe!!!” alikuwa akitafuna Roma lakini wao ndio waliokuwa wakihisi kutapika lakini Roma aliishia kutabasamu huku akijilamba lamba alionekana kufurahia utamu wao.”
“Mchwa wana protini mara mbili zaidi ya nyama , najua hamuwezi kuwala hivyo nitakula mimi mwenyewe”
“Kama ndio hivyo ungekula huko huko kabla ya kuja hapa na kubeba mpaka masega yao?”Aliongea Mage huku akishikilia shingo yake.
“Haya masega yametengenezwa na mate na mchanga , kikawaida watu wa asili watayachoma motoni na kufanya moshi wake kuwa na harufu ambayo hufukuza mbu, najua hapo mnavumilia maumivu ya kung’atwa ndio maana nikaja nayo”Aliongea na kuwafanya sasa waelewe , ijapokuwa maelezo yake yaliwagusa lakini hawakuvumilia kumuona akitafuna hao wadudu.
Roma hakujali , ukweli ni kwamba alishawahi kuwatafuna wakati wa utoto wake ili kuishi , alijua angeonekana kama kichaa lakini ili apate nguvu za kuwatoa kwenye msitu huo hana budi kufanya hivyo .
Siku ya pili yake ilipowadia walianza safari tena , walishaanza kumzoea Roma hivyo hawakushangazwa zaidi na tabia yake hata pale alipokamata wanyama wadogo wadogo mfano wa Sungura, Panya wakubwa na Kobe wa Australia wote hao waliwafanya chakula.
Tukio moja ambalo liliwafanya kutaka kupoteza fahamu ni pale alipong’ata kichwa cha spider na kukimeza chote.
Siku ya nne hatimae waliweza kufika kwenye fukwe ya bahari ya Arafura upande wa Kaskazini ni eneo ambalo lilikuwa na kiasi kikubwa cha miti aina ya Pandanus ambayo mingine ilikuwa na matunda na mingine haikuwa na matunda.
Wakati wao wakiwa wamepumzika wakifurahia upepo Roma alitengeneza ndoano kwa kutumia miti na uzi na kisha akatafuta jongoo na kumuweka kama chambo na kurudi tena msituni kwenye mto uliokuwa ukimwaga maji ndani ya bahari na kuanza kuvua samaki, asingeweza kuvua baharini kwani mara nyingi hawapatikani kwenye fukwe hivyo mto waliokuja nao kufuatisha aliona ndio mahali salama pa kuvua na alifanikisha kukamata Kambare wawili wakubwa., Roma hakushangazwa kupata samaki wakubwa kama hao kwenye mto wa maji malaini lakini alijiambia huenda ni kutokana kila mahali wanapatikana.
Baada ya kuwarosti kwenye moto na kula waliamka na kuendelea na safari yao huku awamu hii sasa hawakutembea kwenye vichaka bali kwa kufuatisha fukwe ya bahari.
“Mawazo ya kurudi nyumbani yametufanya kushindwa hata kutafuta tena mimea ya vidonge”Aliongea Rufi
“Sidhani kuna haja ya kujisumbua mpaka sasa nimeshindwa kujua namna ya kurudisha nguvu zangu sembuse kuweza kudhibiti moto wa njano wa kutengenezea hivyo vidonge’
“Usijilazimishe sana najua pia moto wa njano ni ngumu sana kudhibiti zaidi hata ya moto mweupe , kwa umri wako naweza kusema nguvu zako ni kubwa mno na inatosha”Aliongea na Roma aliona Rufi anajaribu kumfariji lakini hakutaka kuongezea neno zaidi ya kutembea mbele.
Kutokana na uwepo wa majabali upande wa Fukwe walirudi ndani msituni kuanza kutembea ili kuzunguka watokezee upande wa pili na baada ya kutembea kwa takribani nusu siku waliweza kutokea eneo la tambarare lenye miti mifupi , muda ulikuwa umeenda na hali ya hewa ilikuwa ya baridi mno.
Muda uleule wakati wakipanga kutokezea tena kwenye fukwe mara kwa mbele yao waliweza kuona wazungu waliovalia kombati za jeshi wakiwasogelea kwa kasi kwa kutumia vyombo vya moto ambavyo huwaruhusu kusafiri hata sehemu ambazo sio za barabara ni kama magari flani hivi yanayotumiwa sana sehemu za jangwani.
Roma baada ya kuangalia ivzuri alijua hata vyombo vya moto wanavyotumia ni vya kijeshi.
Walizidi kuwasogelea kwa kasi na walipowakaribia ndipo Roma alipoweza kuona sura zao vizuri , walikuwa na sura ngumu mno zilizojaa usiriasi huku wakiwa na mashine za bunduki kwenye mikono yao.
“Roma wanatulenga sisi?”Aliuliza Mage kwa hofu lakini Roma alishindwa kujibu kwani hata yeye alikuwa na moyo mzito , asingeogopa kama angekuwa na uwezo wake, lakini muda huo hakujuwa namna ya kujilinda kama watu hao wataamua kushambulia.
Mage alikuwa polisi na alikuwa na mafunzo lakini hakuwa na mafunzo ya kupambana na wanajeshi
“Kaeni kimya , tutajua wanataka nini kwetu”Aliongea Roma huku wakizidi kuwasogelea.
Baada ya wanajeshi wale kuwakaribia na kuwazuguka alitokezea mwanaume aliekuwa na ndevu pande zote kiasi cha kufanya mdogo wake kuonekana kwa shida.
“Black skinned peaple Africa or America?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza akisema wati wa ngozi nyeusi je wanatokea Afrika au Amerika
Roma hakuwatambua ni kundi gani wanatokea kutokana na kwamba hakuna taarifa kwenye uniform zao zaidi ya alama ambayo iliashiria walikuwa ni Mercenary , hivyo asingeweza kujitambulisha kwao , aliogopa wasije kuwa maadui zake.
“We’re Tanzanians , our plane crashed so we landed here , what is matter?”Aliongea Roma akidanganya kwamba wao ni watanzania lakini ndege yao ilidondoka na ndio maana wapo hapo.
“Marafiki kutoka Tanzanyia , naamini mmechoka sana mnaonaje mkapumzika hata hivyo sijatarajia kukutana na wanawake warembo kwenye hili eneo , jina langu naitwa Ryan na ni furaha kwangu kuwakaribisha kwenye kambi yetu”Aliongea huku akicheka na kufanya meno yake ya njano kuonekana.
Mage na Rufi waliogopa mno na walijikuta wote wakienda kukaa nyuma ya Roma kwa woga.
“Hubby tunatakiwa kufanya nini?” Aliongea Mage na wale wengine walipiga miluzi kwa furaha wakiwaangalia Rufi na Mage kwa macho ya matamanio.
Roma alijitahidi kurudisha kumbukumbu zake kutafuta jina la kambi ya masenari yenye makazi kwenye ukanda huo na alijikuta sasa akikumbuka, waliokuwa mbele yake ni Grey Marcenaries , alikuwa akijua sana kuhusu taarifa zao ni watu wasiojali utu na ni wenye roho mbaya sana.
SEEHEMU YA 502.
Roma mara baada ya kujua ni hatari gani iliokuwa mbele yake alijua kabisa hana la kufanya , ijapokuwa hakujua ilikuwaje mpaka wakawaona lakini kwa wakati huo aliona jambo la pekee ni kufuatisha kwanza kile wanachotaka.
Aliwageukia Rufi na Mage na kisha aliwapa ishara wasiwe na wasiwasi na waongozane nao na kisha akawageukia wale wanajeshi na kuwaambia waongoze njia.
Wote walipandisha kwenye vyombo hivyo vya moto ambavyo muundo wake ni kama yale matrekta ya kulimia yenye matairi mapana.
Safari ilianza huku wakiwa chini ya ulinzi na ndani ya muda mfupi tu walikuja kutokezea kwenye eneo la fukwe na hapo sasa ndio Roma alielewa , mbele yake meli kubwa ya mizigo ilionekana ikiwa imetia nanga.
Upande wote wa fukwe kulikuwa na walinzi ambao walikuwa wakilinda kwa kuzunguka zunguka pande zote..
Ilikuwa ni meli kubwa ya mizigo na pambeni yake kulikuwa na vessels mbili za ulinzi zilizokaa kulia na kushoto na moja kwa moja Roma aliweza kufahamu hili sio eneo lao la kudumu bali huenda kuna biashara haramu zinazofanyika hapo kutokana na uwepo wa mahema mengi kwenye hio fukwe.
Watu waliokuwa tu nje walikuwa kama therathini kwa haraka haraka kuna ambao walikuwa na sura za kiasia na kuna wazungu pia na Roma alijua hao ni smugglers watu wanaoingiza biadhaa kimagendo nchini Australia kupitia baharini.
Wote walitolewa kwenye chombo kile cha usafiri na kufanya kundi lote kuwaangalia huku macho yao ya kimatamanio yakiwaangalia Rufi na Mage na kufanya wazidi kuwa na hofu , mpaka hapo walijua hawana namna ya kuepuka ubakaji hivyo waliona ni vyema kukaa zaidi karibu na Roma.
Wote waliongozwa mbele na kupelekwa mpaka kwenye hema lenye rangi ya zambarau na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Ryan alinyoosha mtutu wake na kuwaonyesha ishara ya kuingia ndani.
Ni eneo ambalo lilikuwa na mahema kama kumi na tano hivi makubwa yaliosimamishwa kwa mita tano nao kuachana na yalikuwa ni makubwa mno.
“Go in our Tanzanyian friends”Aliongea huku akichapia Tanzania na kuita Tanzanyia.
“Mna mpango gani na sisi?”Aliuliza Roma.
“Tusha mtaarifu bosi wetu na utafahamu mara baada ya kufika”Aliongea na kisha akamsukumzia Roma ndani ya hema hilo na wakaongezeka wanajeshi watatu na kulinda nje
“Inaonyesha hawana mpango wa kutuua lakini pia hawajatupa sababu ya sisi kutufungia humu”Aliongea Mage kwa wasiwasi.
“Amesema kiongozi wao atakuja kutuona , nadhani tutajua mpango wao”Aliongea Roma na kisha akaanza kuangalia mazingia ya hema hilo na alijikuta akikunja sura baada ya kuona maboksi mengi ya mbao yaliochongwa vizuri na kuvutia kwa nje , yalionyesha kanisa yalikuwa na vitu vya thamani ndani yake na namna ambavyo yalipangwa ni kama walikuwa wakiogopa yakidondoka na kuharibika.
Roma aliyasogelea na kisha akafungua moja wapo taratibu sana ili walinzi nje wasisikie na ndani yake aliweza kuona kifaa ambacho kimezungushiwa magazeti , alishangaa kutokana na lugha iliotumika kwenye hayo magazeti lugha ilikuwa ya kichina (mandarin) na moja kwa moja alijiambia huenda ni kitu ambacho kinahusiana na nchi hio.
Baada ya kuondoa lile gazeti alikutana na buble wrap iliozungushiwa kwa juu ili kama kifaa hicho kingedondoka chini kisipasuke kwa urahisi , baada ya kumalizia kutoa sasa alijikuta akishangaa baada ya kuona kilichopo ndani ya boksi.
“This is…”Rufi alijikuta akiziba mdomo kwa mshangao na Roma alimtingishia kichwa kukubaliana nae.
“Ni Porcelaini ya rangi nyeupe na bluu ambayo imedariziwa na mchoto wa mawingu na Dragoni , makadirio ya thamani yake nchini China ni zaidi ya dola milioni kumi”Aliongea Roma na kumfanya sasa Mage kuelewa maana aliona ni kama kikombe cha udongo tu na hata hivyo hakuwa na uelewa na tamaduni za China.
“Are they smuggling relics?””Aliuliza Rufi kwa sauti ya kunong’oneza akimaanisha je wanaingiza mabaki ya vitu vya kale vya thamani nchini Australia kwa njia zisizo halali.
“Naamini kuna zaidi ya mabaki , hebu fikiria kwanini wamekuja kutuweka ndani ya hema lenye vitu vya thamani namna hii , jibu ni kwmaba mahema yote huenda yamejaa, ndio maana wametumia meli kubwa ya mizigo , nina uhakika kama serikali ya China wanaelewa hiki kinachoendelea lazima wangewawinda kwani vitu kama hivi ni vya thamani sana kwao”
Wakati Roma akiendelea kuongea aliweza kusikia sauti yenye ucheshi nje ikiongea na ndani ya muda mfupi tu hema lilifunguliwa na akaingia mwanaume mrefu mchina akiwa amevalia T- shirt iliombana vyema mwili wake , alikuwa yupo na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Ryani.
Alianza kumwangalia Mage na kisha akahamia kwa Rufi na halafu akamgeukia Roma sasa.
“Dude I heard from Ryan that you guys were trapped in this place because your plane crashed?”
“Dude nimesikia kutoka kwa Ryani mmekwama mara baada ya ndege yenu kudondoka?”Aliuliza kwa lugha ya kingereza lakini iliojaa rafudhi ya kichina.,
“Wewe ni mchina?”Aliuliza Roma na kumfanya yule bwana kumwangalia kwa namna ya kumchunguza Roma.
“You don’t look like a spy since you don’t recognise me , I’m leader of the Hydralisk Mercenary group , Jin Zhe , They call me Hydra , Havu you heard about me?”
“Unaonekana sio shushu kwasababu haunifahamu , mimi ni kiongozi wakundi la Masenari la Hydralisk nafahamika kwa jina la Jin Zhe lakini wananiita Hydra , ushawahi kusikia kuhusu mimi?”Aliongea huku akimwangalia Roma kama Cobra alieona binadamu wa kumshambulia.
Roma alitingisha kichwa chake akishiria kwamba hajawahi kumsikia na alikuwa akiongea ukweli kwani hajawahi kuwasikia labda huenda hawakuwa maarufu.
“Haijalishi kama hunifahamu lakini naamini nyie sio hao watu wanaonitafuta”Aliongea na kumfanya Roma sasa kidogo kuwa na ahueni, kwasababu hakuwa akiwajua moja kwa moja alijua sio maadui zake hivyo hakuogopa kama atagundulika ni mfalme Pluto.
“Kwahio unamaanisha utatuacha tuondoke?”Aliuliza Mage.
“Go!?, My beutiful you think too highly of us ..”Aliongea huku akitingisha vidole vyake akimaanisha kwamba wamewadhania ndivyo sivyo kwani hawana mpango wa kuwaachia.
Roma alijikuta akikunja ngumi akijiambia mwenyewe mambo yanaweza yasimalizike vizuri.
“Tumekaa hapa kwa muda mrefu na haya maeneo hakuna watu wanaofika hivyo unaweza kusema ni kwa muda mrefu hatujawhai kuona wanawake warembo kama nyie ,itakuwa ujinga kama nitawaachia muondoke bila mabro kunufaika na uzuri wenu”Aliongea na kumfanya Mage na Rufi kukasirika na kuogopa.
“Huna aibu wewe?”Alilaani Rufi
“Nisamehe sana , ijapokuwa hatuna uhasama na nyie lakini siwezi kujali kwasasa , hali ya kimazingira yenyewe ndio hii, ninachomaanisha msiwe na wasiwasi na muwaburudishe mabro wangu vizuri tu na hakuna kibaya kitakachowakuta”
“Sio tu wewe ni mwizi unaeliibia taifa lako mwenyewe, lakini pia ni mchafu wa tabia”Aliongea Rufi
“Nione aibu hahah….. mnaonekana kabisa nyie ni matajiri ndio maana mnatoka nchini kwenu na kudondoka na ndege na hamuwezi kunielewa mtu kama mimi”Aliongea ilionekana kabisa alikuwa na chuki na taifa lake.
“Unaonekana kama mtu mwenye huzuni , inakufanya uonekane kama mtoto”Aliongea Roma.
“Unasemaje wewe , funga domo lako”Aliongea kwa hasira na kumfanya Roma hata asijali na kuendelea kuongea.
“Inaonyesha kabisa nchi yako imekufanyia mabaya lakini lawama zote unaangushia dunia nzima , angalia sasa ulivyo, unaonekana kama mtu ambaye umekufa huku unatembea , nina uhakika kuna kilichokutokea lakini tofauti na kujitafuta ili kujua ulikosea wapi au kulipiza maadui zako kwa kile walichokufanyia lakini upo hapa ukiwa umejificha unaishi bila amani , kwangu wewe ni Loser na mtu mdhaifu sana”Aliongea Roma kwa kujiamini kama kawaida yake na kumfanya Mchina kukasirika zaidi na zaidi.
“Unajifanya mjuaji sana kwa kuongea , lakini ngoja nikushauri wanaume hatuongei sana bali ngumi yetu ndio inazungumza”Aliongea .
“Boss niwapeleke hawa wanawake kwenye hema lako”
“Haina haja, waondoe wanajeshi wanao linda nje”Aliongea na kisha Ryani mzungu alitoka nje na kuwaambia wale walinzi waondoke na kisha akarudi tena ndani.
“Boss huyu mwanaume na yeye tunamfanya nini maana hana faida kwetu?”Aliuliza tena.
“We have brothers who like to go other way right? , he looks young and tender, give him to them !”
“Tuna mabraza ambao wanapenda mlango wa uani si ndio? , huyu bwana anaonekana mdogo lakini pia ni mpole muondoe hapa ukawapatie”Aliongea na kumfanya Ryan kutabasamu huku meno yake ya njano yakiwa nje nje.
“You have to serve our brothers well .. hehe, I’ll send you there myself”
“Unapaswa kuwahudumia mabraza wetu vizuri … hehe nitakupeleka mwenyewe”Aliongea .
Rufi na Mage walijikuta wakijificha nyuma ya Roma , ni kama washasahau kwamba mwenzao hana nguvu yoyote , Mage alikuwa amekunja ngumi alikuwa akijua kupigana kwasababu ashapitia mafunzo lakini aliogopa siraha zao tu
Ryan alianza kumsogelea Roma kwa ajili ya kumnyanyua ili kumpeleka kwa mabraza , lakini ile anamkaribia Roma alinyanyuka kwa staili matata sana na kupiga viungio vya mkino yake.
‘Arrghh,,,”
Alijikuta akitoa ukulele , ijapokuwa Roma hakuwa na nguvu za kijini lakini haikumaanisha alikuwa hajui kupambana kwa njia za kawaida , alikuwa na mafunzo ya hali ya juu ya Kung Fu na alikuwa akijua mbinu zote za kijeshi na isitoshe mwili wake ulikuwa mwepesi kutokana na kwamba alikuwa amemulikwa na mwanga wa jiwe la kimungu na akaja kuwa Agent 13.
Roma kwa haraka sana alinyanyua bunduki ya Ryani na kisha alimfyatua nayo kwa kumlenga kichwa na muda uleule zile purukusani zilifanya wanajeshi wengine wawili kuingia na Roma hakutaka kuwarembesha , bunduki ilikohoa mara mbili mfululizo na kuwapasua wote vichwa na kudondoka chini.
Mchina alijikuta akishangazwa na uwezo wa Roma na alijikuta hana cha kufanya zaidi ya kukimbia nje huku akiita wenzake .
Roma palepale alichuchumaa na kisha akachomia mikebe ya bunduki za wale wawili aliowaua , alikuwa akijua wapo wengi na mikebe mwili haiwezi kutosha kuwamaliza.
“Roma tunapaswa kufanya nini?”Aliuliza Mage.
“Hawawezi kushambulia hili hema bila ya tahadhari kuna vitu vya thamani vya kutosha hapa na kama vitaharibika watapoteza mamilioni ya pesa”Aliongea Roma
“Pumbavu zako , sijategemea ungekuwa na ujuzi wa hali ya juu namna hio lakini siwezi kukuacha hai , ushaua tayari mabraza wetu watatu lazima ulipie’Aliongea Mchina kwa sauti kubwa nje kwa hasira.
“Roma unaonaje tukuchukua bunduki na wote tukashambulia nina uzoefu mkubwa na tunaweza kuwamaliza”Alishauri Mage.
“Hapana tukifanya hivyo ndio watatuua vizuri kwani ni kama tunawachokoza na watatushambulia na ukumbuke wana siraha nzito”
“Kwahio tunafanya nini , tunasubiria hapa ndani watuue?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kujibu swali lake kwani hakuwa na wazo, kwenye maisha yake hakuwahi kuwa hivyo , kuwa binadamu wa kawaida ni jambo ambalo hajalizoea
Alichukia hali aliokuwa nayo kwani alishindwa kabisa hata kuwalinda wanawake wake ,kwake ilikuwa kama matusi ambayo ni kama yalikuwa yakimkosesha amani.
Muda huo kwa nje hali ilitulia kabisa , ni kama vile wameondoka lakini Roma hisia zake zilimwambia huenda wanawategea kitu hatari zaidi.
Kabla hajajua ni nini kinaendelea nje , vyuma vilirushwa ndani na baada ya kuangalia kwa umakini aligundua ni mabomu ya machozi .
“Ni mabomu ya machozi fumba macho ”Aliongea, katika maisha yake alikuwa ashapitia changamoto kama hizo na ni kama amekumbushiwa nyuma lakini hata hivyo bado hatari ilikuwa nje nje.
“Hatuna chaguo zaidi ya kutoka nje , Mage chukua hio bunduki na wote hakikisheni mnakuwa nyuma yangu”Aliongea Roma.
Muda huo alijiambia sio wa kusita tena bali ni wa kupambana huku akitegemea Mage kidogo angemsaidia kwani alikuwa mwanajeshi na ukichanganya pia alikuwa kwenye levo ya nusu mzunguko , hivyo alikuwa na uhakika anaweza kudondosha watu kumi.
Alijua walikuwa wakisubiriwa nje hivyo aliona haitokuwa busura kama watatumia mlango wa hema kutoka nje
Wote walikuwa wamefumba macho ili moshi usiwaumize na kuwafanya wawashe na macho.
Roma alitumia hisia zake kujaribu kupata kuona namna wanajeshi hao walivyojipanga na palepale aliachia risasi kupitia upande wa nyuma mwa hema na alidondosha watu wawili bila makosa.
“Kimbieni nje”Aliongea Roma na muda ule alijirusha nje huku akitanguliza mdomo wa bunduki mbele na kufanya hema lichanike kwa wepesi na aliweza kubiringita kama pia huku akirusha risasi ambazo hakuna hata moja iliokosa mtu.
Jambo lile liliwafanya kushangazwa mno na kujiuliza huyu ni komandoo au ni nani kwani haikuwa kawaida, sekunde tano tu alikuwa amedondosha watu watano.
Mage alimtoa Rufi na kumwambia akimbilie baharini zaidi huku yeye akimkinga na siraha, lakini palepale yule mchina alionyesha kuwashitukia tayari.
“Mnajaribu kukimbia sio , Never”Aliongea huku akiwapa vijana wake ishara ya kuzunguka nyuma.
Na Mage alikuwa shapu mno kwani alimdodosha Rufi chini na kisha akauegamiza mgongo wake kwa staili ya kuelekea mbele na akaachia risasi mfululizo ambazo ziliwapata watatu na kudondoka chini , hali ile iliwafanya kusogea upande huo kwa tahadhari.
Muda ule ule kuna wanajeshi wengine wanne waliokuwa kwenye gari waliwasogelea kwa spidi na Roma alielala chini alilenga mara mbili tank la mafuta kwa shabaha kuntu kabisa.
“BOOM!!
Gari ililipuka palepale na wanajeshi wanne walikuwa wafu tayari na kumfanya Jin Zhe kuwa kwenye kiwewe akishangazwa na Roma alivyokuwa vizuti kwenye kuchezesha bunduki.
“Back off and take cover!”
Aliongea kwa sauti akiwamrisha warudi nyuma kwani aliogopa wangeshambuliwa na Roma ambaye alikuwa na shabaha ya hali ya juu kwenye matumizi ya siraha hivyo kuogopa wanajeshi wake kufa wengi.
Ndani ya sekunde tu wote walijificha nyuma ya mahema na kwenye mawe , huku wakiwa wamejaaa sumu ya kuua maradufu.
Upande wa Roma risasi zilikuwa zishamwishia tayari , lakini hata hivyo hakuna ilioharibika na aliwaza mbinu ya pili ya kushambulia.
“Mage unafanya nini acheni kukimbia” Aliongea Roma kwani aliona wangeshambuliwa na pale pale Mage alilala chini kwa haraka
Roma baada ya kuona hawako kwenye hatari alisimama na kisha akamrushia bunduki wanajeshi wawili waliokuwa wakitaka kujitokeza kushambilia na palepale alikimbia nduki kumfuata mwanajeshi mwiengine ambae ashakufa achukue bunduki yake.
Mage aliejificha na Rufi chini ya jiwe alinyanyua sura kidogo kuchungulia , hata yeye siraha yake ilishaisha risashi hivyo alitupilia mbali na wanajeshi waliokufa wapo mbali
“Roma kuwa makini..”
Mage alijikuta akiziba mdomo kwa wasiwasi mara baada ya kushuhudia moja wapo ya mwanajeshi ambaye alilipuka kwenye gari bado hakuwa amekufa na alisimama huku akiwa ameshikilia bomu la kurusha na mkono.
Roma alikosa umakini wa kuangalia nyuma yake hivyo hakumuona na yule mwanajeshi hakutaka kuchelewa palepale alirusha lile bomu uelekeo wa Roma lakini alikuwa fasta mara baada ya kusikia kauli ya Mage na aliruka upande mwingine .
“BOOM!”
Lilipuka lakini Roma hakuwa ameenda mbali hivyo nguvu ya wimbi lake ilimpiga na kumfanya adondoke chini akiugulia maumviu.
“Nice one, very nice”Aliongea Jin Zhe
“Ameishiwa na risasi mfuateni tummalize”Aliongea kwa nguvu.
Roma alikuwa amefunikwa na vumbi la mlipuko wa bomu na alikuwa akijihisi kizungu zungu na viungo vya ndani ni kama vilikuwa vikikamuliwa kwa maumivu aliokuwa akisikia.
Lakini alijiambia hana muda wa kusikilizia maumivu na atumie vumbi lilomfunika kama kinga , alijivingirisha kama pia na kusogelea bunduki iliokuwa kushoto kwake
Mlio wa bunduki ulikuwa umesambaa na wale wanajeshi hawakuangalia pa kulenga ili mradi ni eneo ambalo Roma yupo walirusha huko huko na kwa wingi wa risasi ilikuwa ngumu Roma kukwepa zote.
Roma alijikuta aking’ata meno kwa maumivu mara baada ya kugundua ashapigwa risasi ya tumbo na kwenye kigimbi cha mguu
Ijapokuwa mwili wake bado ulikuwa mkomavu lakini haukuwa na ulinzi tena wa nguvu ya kimaandiko ya urejesho kutokana na sumu iliokuwa kwenye mwili wake , hivyo alijihisi dhaifu mno.
Alijikuta akitema damu nyingi huku akisikilizia maumivu makali kutoka tumboni , alijjitahidi kubingirika upande mwingine lakini bado hakuwa na spidi kama ya mwanzo lakini bahati kulikuwa na jiwe kubwa karibu hivyo alilala chini na kujikinga na risasi.
Mage alishindwa kabisa kuvumilia pale alipokuwepo kwani alishuhudia Roma akipigwa na risasi na akitema damu na alitoka kwenye jiwe na kukimbilia upande wa Roma alipo.
“Mage..!!”Aliita Rufi kwa hofu lakini alikuwa ashachelewa na hata yeye alianza kukimbia kuelekea upande wa Roma.
Roma alijua wanamsogelea ili kumsaidia ,lakini aliona kabisa isingeweza kusaidia palepale aliwapa ishaa wasije upande wake lakini Mage alimpotezea na kukimbia kwa spidi na kwenda kutua alipo na Rufi hivyo hivyo aliweza kufika.
“Roma hapa hatuwezi tena kupambana nao , ni wengi na hatuna siraha njia pekee nitumie uwezo wangu kukubeba kukimbia na wewe kuelekea upande ule”Aliongea Mage na Roma aliona wazo sio baya, alijua ni kweli Mage anao uwezo wa kukimbia nae kwa spidi kutokana na uwezo wake.
Roma kabla hajajibu Mage tayari ashamnyanyua kama mtoto na kuanza kukimbia nae huku Rufi akifuatia.
Kitendo kile kiliwaamsha Jin Zhe na wanajeshi wake na kuanza kuwasogelea bila hofu baada ya kujua Roma hana siraha tena na walikuwa wakiwasogelea huku wakirusha risasi.
Rufi baada ya kuona wanashambuliwa mfululizo alibadilisha upande ili kumpa nafasi Mage akimbie akiwa na Roma na Mage alifanikiwa kufikia chini ya jabali lakini ile wanataka kujificha chini Rufi aliwakimbilia tena lakini alishachelewa kwani palepale alipigwa na risasi ya mgongoni na aliishia kutema damu na kudondoka chini.
“Noo…!!”Roma alijikuta akitoa ukulele bila kuamini na alishindwa tena kujificha zaidi ya kutoka kwenye mikono ya Mage na kumsogelea Rufi.
Jin zhe alionekana kufurahishwa na tukio lile na palepale alitoa bomu la kurusha kwa mkono na kuliotoa pin.
Roma alikuwa ashamfikia Rufi na kumshikilia akiwa amepiga magoti.
“Roma kimbiaaa……!!!””Alijikuta akitoa ukulele Mage mara baada ya kuhushudia bomu likiruswa pale walipo na Roma alijikuta akimwachia Rufi na kuangalia lile bomu na palepale macho yake yalibadilika na kuwa ya rangi ya njano.
0687251346 nicheki watsapp .
ITAENDELEA.