SEHEMU YA 503.
Mlipuko wa bomu ulitokea mita chache na waliposimama na hilo ilifanya kuwa bahati yao kwani hawakuuguzwa na moto zaidi ya kurushwa pembenni na presha kubwa ya mlipuko huku vumbi likiwafunika kiasi cha kuwafanya Jin zhe na wanajeshi wake wasione upande wa pili.
Roma maumivu ya majeraha yake aliyasahau kabisa na alichokuwa akiangalia ni Rufi alielala chini akivuja damu na Mage ambaye amesukumwa mbali na mlipuko wa bomu mpaka akapoteza fahamu.
Jin Zhe nia kundi lake walitembea kuwasogelea , mpaka hapo waliamini kwamba washamaliza vita hivyo hakukuwa na haja ya kurusha tena risasi.
“Angalieni kama bado wapo hai?”Alitoa amri
“Yess Boss”
“Niahakikisha nawakata vipande vipande na kisha kuwalisha Papa”Aliongea huku akionyesha hasira kweli kweli , alitamani wasiwe wamekufa ili awape mateso makali.
Wafuasi wake walikuwa na hasira pia ya kiwango cha juu na walisogea mbele ili kuwaangalia maadui zao kama tayari washakufa.
Roma alimwangalia Rufi alielala chini akiugulia maumivu ya kupigwa na risasi na kisha akageuka nyuma na kumwangalia mage alielala chini na alijikuta akijawa na hisia mchanganyikio , hisia za kudharilishwa , hisia za chuki , hasira , kukata tamaa na majonzi, alijihisi ni kama meridian za mwili wake zitapasuka.
Mishipa yake ya damu ilikuwa ikidunda kwa nguvu na kufanya maumivu kuwa makali mno kwani ilikuwa ni kama itampasuka , misuli yake ya mwili pia ilizidi kutanuka na kumfanya kuhisi maumivu makali kwenye miungio ya mifupa.
Sehemu ya kituo katika mwili wake ambayo ndio chanzo cha nguvu zake kiliweza kufunguka kutoka katika kizuizi cha sumu ya vipepeo wa ndoto na mabadiliko hayo yalifanya macho yake kubadilika badilika rangi.
Wale wanajeshi muda ambao walikuwa wakisogea eneo ambalo Roma amesimama walijikuta wakisimama wenyewe mara baada ya kuhisi msisimko mkubwa wa nguvu ya kimauji inayowakaribia na kujikuta kujawa na hofu isiokuwa na kifani na hata eneo lote hali yake ya hewa ilianza kubadilika na mawe madogo yaliaanza kupeperushwa na upepo.
Jin Zhe hatimae aliweza sasa kujua kuna kitu ambacho hakipo sawa , aliinua kicha chake na kuangalia chanzo cha mabadiliko hayo na alijikuta akipagawa mara baada ya kumuona Roma alivyo, kwani macho yake yalikuwa yamegeuka kutoka rangi ya njano na kuwa rangi nyekundu na kuwafanya wazidi kuogopa zaidi na zaidi na kushindwa hata kuchukua maamuzi ya kutumia siraha zao.
Ukweli ni kwamba haikuwa na haja ya Roma kubadilika macho kwani watu waliokuwa mbele yake ni wadhaifu sana , ila wakati huo akili yake alishindwa kuingoza yeye mwenyewe , ule ugonjwa wake ambao siku nyingi ulikuwa ni kama umepotea muda huo ni kama umemrudia upya kutokana na hasira aliokuwa nayo.
Muda uleule wakati wale wanajeshi wakimshangaa Roma alitema mate yaliojaa damu , ndani ya mwili wake ni kama kuna kitu kimepasuka na kumsababishia maumivu mengi, lakini ukweli ni kwamba alikuwa akijaribu kuondoa sumu iliokuwa ipo ndani yake.
Ilimchukua sekunde tu mwili wake wote uliweza kujiponyesha kwa haraka sana na hata risasi zilizokuwa ndani yake hazikuwa na madhara tena na jeraha lake likafunga palepale na sasa alijihisi ni kama nguvu zake zimeongezeka maradufu zaidi.
Kwanini moto?, kwasababu miti , Mawe na radi ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutengeneza moto lakini hata moyo wako unaweza kusababisha moto.
Nishati iliopo kwenye moyo wako unganisha na nishati iliopo kwenye figo zako na kisha malizia na nishati iliopo kwenye kibofu chake ndio trifecta ya kudhibiti moto wa rangi zote.
Ilikuwa ni kama ufunuo katika akili yake , siku zote hakuweza kudhibiti moto wa rangi nyeupe na nyekundu kwasababu hakuwahi kufikiria nguvu zake za kijini zilizojificha katika moyo wake ndio hukamilisha sifa tatu muhimu.
Moto mweupe ulikuwa na nguvu ya kumeza kila kitu , hivyo Roma mara baada ya kupaa ufunuo hu na kujaribu kudhibiti nguvu zake katika moyo , kibofu na figo palepale ile nguvu ilioambatana na vipepeo wa kufikirika iliweza kuisha mara moja na hapo ndipo uwezo wake ukarudi wote tena na zaidi ya kuongezeka.
Lakini licha ya kuwa kwenye mshangao wa kuweza kugundua kitu muhimu sana katika mafunzo yake kwa muda huo hakutaka kwanza kuruhusu mawazo yake yachukue nafasi , bali nafsi yake ilikuwa ikimwambia ua kila mmoja.
Roma palepale aliita nguvu ya kimaandiko na kisha akaunganisha na nguvu ya mbingu na ardhi ambayo ilimpatia ufunuzi wa namna ya kutengeneza moto mweupe na palepale joka la moto liliweza kujitengeneza kwenye mikono yake na hakuwa na muda wa kupoteza tena kwani alilielekeza nini linatakiwa kufanya.
Kilichosikika baada ya hapo ni vilivo na kusaga meno vya wale wanajeshi namna ambavyo walikuwa wakiungua na ndani ya sekunde ishirini tu miili yao iligeuka majivu na muda huo huo akaweza kurejewa na uwezo wake timamu wa kufikiria mara baada ya nguvu ya andiko la urejesho kufunika ugonjwa wake wa ubongo , ugonjwa ambalo aliamini ulipotea kumbe bado ulikuwepo.
Roma palepale alipotea na kuibukia mbele ya Mage ambaye alipoteza fahamu kutokana na mlipuko wa bomu na alijikuta akipata ahueni mara baada ya kuona alikuwa hajaumia sana zaidi ya kupata michubuko tu na palepale alimwingizia nguvu ya kijini na akarejewa na fahamu..
“Roma ume…”Alitaka kuongea lakini Roma alimzuia asiongee na kumuweka chini na kisha akamfuata Rufi kumwangalia maana alijua ndio ambaye alikuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha.
Roma mara baada ya kumkagua alimwona alikuwa amepoteza sana damu kutkana na jeraha la risasi na kumfanya kupauka mno uso na kushindwa hata kupumua vizuri lakini hata hivyo aliamini akimwingizia nguvu ya kijini basi ataweza kumponyesha kwa haraka.
Roma palepale hakutaka kuchelewa aliita nguvu za andiko la urejesho na kuziingiza kwenye mwili wa Rufi ili kuponya majeraha yake pamoja na kumaliza sumu ya risasi lakiini matokeo yake yalimshangaza na kumwacha kuwa na hofu zaidi.
Ijapokuwa kwa nje alionekana akipona , lakini kwa ndani nguvu ya kijini iligoma kumponyesha kabisa ilikuwa ni kama nguvu zake zilikuwa zikikataliwa na nguvu ya aina nyingine na kadri alivyokuwa akijitahidi ilishindikana kabisa.
“Au ni kwasababu kazaliwa na nguvu kubwa ya Yin katika mwili wake?”Alijiuliza Roma kwa mshangao na hapo hapo alijikuta akianza kukusanya doti , ashawahi kumaliza sumu katika mwili wa Rufi na nguvu hio hio lakini aligundua nguvu hio hio ilikuwa ikikataa kumponya viungo vya ndani ya mwili.
“Ir..it’s useless”Rufi alimwangalia Roma kwa taabu huku akijitahidi kuongea akiwa kama mtu aliekata tamaa , alikuwa akimwambia kwamba alichokifanya hakina maana kwani hawezi kupona.
“Huwezi.. huwezi kuniponyesha kwa nguvu zako….”Alijitahidi kuongea lakini kila alipokuwa akijikaza damu zilizidi kumtoka na Roma aliamini huenda kuna mshipa wa damu ambao umepasuka kwa ndani.
Mage baada ya kuona Roma hana anachokifanya alimsogelea kwa haraka kuona kinachoendelea.
“Roma unafanya nini , kama huwezi kumponyesha tatufa namna nyingine ya kumsaidia”Aliongea Mage kwa amri na kumfanya Roma kutoka kwenye mawazo na kuona kweli anapaswa kutafuta mtu mwingine ambaye anaweza kumsaidia
Alijiambia kama kuna mtu atafanikisha kumfanyia upasuaji wa haraka basi kuna uwezekano wa Rufi kupona na hapo hapo jina la Profesa Clark liliibuka kwenye kichwa chake , alijiambia huyo ndio mtu wa pekee ambaye anaweza kumsaidia.
Clark alisomea udaktari kwa sababu ya Roma licha ya kwamba kwa mambo ambayo alikuwa akifanya haikuwa sahihi kumwita dokta lakini alikuwa ameiva sana katika fani hio na alikuwa amezidi madaktari wengi wakubwa duniani.
Clark hakuwa daktari wa kuhudhuria wagonjwa wa kawaida kila siku na kama ataonekana hospitalini badi ni kwa wale wagonjwa ambao wameshindikana au wenye dharula kubwa za kiafya ambazo madaktari wa kawaida hawawezi kupambana nazo.
Roma palepale alisimama na kisha akamgeukia Mage baada ya kuyakusanya mawazo yake na kuyachanganua na kuhitimisha.
“Utanisubiri hapa hapa ninampeleka kwa Clark”Aliongea Roma na Mage hakutaka kubisha wakati huo , hakutaka kuhofia kwamba angebakia mwenyewe katika eneo hilo ila afya ya Rufi ilikuwa kipaumbele.
Roma alijua hawezi kumbeba kwa njia ya kawaida kwani asingeweza kuhimili hivyo alimtengenezea ngaoo ya kijini kama puto na kisha akambeba na kupotea katika eneo hilo la fukwe.
Profesa Clark tokea maswala ya ndoa yake kutoendelea baada ya vifo vya Wolverine , alirejea nyumbani kwao Uingereza kama kawaida na tafiti za madawa nchini Tanzania zilikuwa chini ya wanafunzi wake ambao walikuwa wakiongozwa na Ashley.
Roma akiwa njiani alijua vizuri wapi Clark anafanyia tafiti zake , lakini kwa muda huo atakuwa kwenye jumba lake la kifahari amepumzika kutokana na utofauti wa muda.
Hivyo kwa haraka haraka aliona kumpeleka Rufi moja kwa moja mpaka nyumbani lisingekuwa chaguo bora hivyo aliempeleka Rufi kwenye hospitali ya St Mary’s katika kitengo cha dharula , alitumia dakika tano tu ku’teleport’ kutoka bahari ndogo ya Arafura mpaka London Uingereza.
St Mary’s ilikuwa ni hospitali ambayo inafahamika sana ndani ya London kwa ubora wa huduma zake, Roma alikuwa na mpango kwanza Rufi apatiwe huduma ya dharula na madaktari wa hospitali hio wabobevu na kisha amfuate Clark nyumbani kwake kumleta hapo.
Wakati anatua mbele ya hospitali hio kulikuwa kimya mno kwasababu ni usiku wa kama saa saba kwenda nane hivi.
Wahuhdumu na manesi wa hospitali hio walishangazwa mara baada ya kumuona mwanaume wa kiafrika akiingia akiwa amembeba mwanamke ambaye alikuwa ametapakaa damu., lakini kutokana na taaluma yao hawakushangaa zaidi ya kuchukua maamuzi ya haraka na kumsogelea kwa kumkimbilia huku wakimsogezea kitanda cha hospialini cha mataili na kumfanya Roma amlaze chini taraibu.
“Sir what happened to her?”Aliuliza nsesi akimuuliza Roma nini kimetokea.
“Alipigwa na risasi lakini sasa hivi ameumia viungo vya ndani kutokana na kupigwa na mlipuko wa bomu”Aliongea Roma na kufanya manesi wamwangalie kwa mshituko na walijikuta wakiwa na wasiwasi huku wakiendelea kumsukuma Rufi kuendelea mlango wa chumba cha upasuaji.
“Sir naomba nikuulize wewe ni mtalii au ni raia?”Aliuliza tena nesi mara baada ya Rufi kuingizwa ndani na maswali yake kidogo yalimkasirisha Roma lakini hakutaka kuruhusu hisia zake zimtawale.
“Sisi ni watanzania, kwanini unauliza maswali mengi mtayarisheni kwa ajili ya upasuaji na waiteni madaktari”Aliongea kwa kingereza na kuwafanya wale manesi kumwangalia kwa wasiwasi.
“Grace is doctor Giggs here yet?”Nesi alimuuliza nesi mwenzake akimaanisha je Dokta Giggs hajafika bado.
“Tushampigia simu na amesema anakuja”.
“Sir , tunaomba usubiri nje Dokta Giggs ndio daktari bingwa wa upasuaji ndani ya hospitali hii , atahakikisha anafanya kila liwezekanalo kuokoa hali ya mgonjwa”Aliongea nesi mmoja mzee mzungu ambaye nywele zake zishaanza kubadilika rangi na Roma ilibidi akubali maana kwa muda huo hakuwa na msaada tena hivyo hakutaka kuleta usumbufu.
“Sir kama una wasiwasi sana unaweza kuangalia upasuaji unavyofanyika , zunguka upande wa pili”Aliongea mwanadada ambaye alifahamika kwa jina la Grace.
Lakini kwa muda huo Roma hakuwa na muda wa kuangalia upasuaji huo , alijiambia inawezekana huyo dokta Giggs akawa bingwa lakini imani yake ilikuwa kwa Profesa Clark tu alijiamnbia ndio pekee ambaye anaweza kumuokoa Rufi.
Roma wakati anakaribia kutoka nje , hatimae aliweza kumuona Dokta wa kiume mzungu alievalia Scrub na barakoa akikimbia nduki uelekeao wa chumba cha pasuaji na moja kwa moja Roma alijua atakuwa ndio dokta Giggs mwenyewe, kwani hakuwa peke yake , alikuwa akifuatwa na baadhi ya madaktari wengine ambao Roma alijua watakuwa ni wasaidizi wake.
Dokta yule licha ya kumuona Roma hakujali sana zaidi ya kumpita na Roma alipogueka, alishuhudia akiingia kwenye chumba kile cha upasuaji na Roma alipata ahueni kiduchu ambayo ilimpa ruhusa ya kuondoka katika hilo eneo kumfuata Clark.
Baada ya dakika tatu hatimae Dokta Giggs aliweza kuingia ndani ya chumba cha upasuaji akiwa tayari amevaa Glovuzi na kuruhusu manesi kumvisha gauni maalumu la kufanyia upasuaji.
“What is her condition?”Aliuliza akimaanisha hali yake ikoje huku akimwangalia msichana mwenye kuchanganya rangi akiwa amelazwa kwenye meza ya upasuaji.
“Kuna jeraha la risasi kwenye mgongo wake na pia alipigwa na bomu na kusababisha viungo vya ndani kuharibika , lakini majeraha yake ya nje yanaonekana kutokuwa tatizo, lakini vifaa vimeshindwa kunasa presha ya damu yake”
“What ?! you can’t detect her blood pressure?”Aliuliza kwa mshangao.
“Yes, Doctor Gigg..”Alijibu nesi mmoja mzee akiwa kwenye hali ya wasiwasi.
Upande mwingine, kaskazini mashariki mwa hospitali ni jumba moja la kifahari lililojengwa kwa mtindo wa kasri .
Yalikuwa ndio makazi yake mtoto wa malkia Profesa Clark , ni jumba ambalo limezungukwa na kijani kibichi pande zote na hakuna raia ambaye anaweza kuhoji kwa mtu mmoja kukaa kwenye jumba kubwa kama hilo kutokana na kwamba anatokea kwenye jumba la kifalme.
Licha ya kuwa mtoto aliezaliwa katika koo tajiri sana duniani na yenye nguvu(Roth’schild) lakini maisha yake yalikuwa ya kawaida tofauti sana na watoto wengi wa kitajiri , alikuwa akifanya kazi mchana wote na ifikapo usiku angerudi kwenye jumba lake hilo na kupumzika akiwa peke yake.
Juu ya yote hakuna ambaye alihofia usalama wake , kwani ukiachana na kwamba alikuwa na mafunzo ya kujilinda kwa kupigana lakini pia wengi walikuwa wakimuheshimu kutokana na uwepo wa Hades kwenye maisha yake yeye na mama yake.
Lakini katika siku zote ambazo alihisi kaishi kwa amani bila bughuza siku hio ilikuwa tofuati mara baada ya Roma kutua kwenye nyumba hio upande wa balkoni.
Roma aligonga mlango kwa zaidi ya mara mbili lakini hakukuwa na majibu , hivyo hakutaka kuendelea kugonga tena zaidi ya kuusukuma mlango na kufanya komeo lake la kirembo kuvunjika.
“Who’s there!!?”
Kivuli cha mtu kiliruka kwa ustadi kabisa kutoka kwenye kitanda na mpaka taa inawashwa tayari Clark alionekana kuwa na bastora mkononi ambayo ipo tayari kuachia risasi.
Ijapokuwa alikuwa amelala lakini hisia za kujilinda zilikuwa kubwa mno , hivyo kumfanya kuwa na machale ya haraka,Alijikuta akiwa kwenye mshangao mara baada ya kumuona mwanaume aliesimama mbele yake.
“Roma!!,Why are you here?”Aliuliza mrembo huyo akimaanisha kwanini yupo mahali hapo huku akiweka siraha yake chini na kupumua kwa ahueni
“Clark follow me to St mary’s Hospital! I need you to save someone!”Aiongea akimwambia amfuate mpaka hospitali ya St mary’s kwani kuna mtu wa kumuokoa.
“Kumuokoa mtu?”Alishangaa mwanamke yule alievalia nguo za kulalia lakini kwa mwonekano wa Roma hakutaka kuendelea kuuliza maswali mengi zaidi, alisogelea koti la Burberry kwa haraka na akalivaa n akajiangalia kwenye kioo na kuona yupo sawa.
“Unaweza kunipeleka sasa”Aliongea .
Upande wa hospitalini kwenye chumba cha upasuaji Dokta Giggs alikuwa ameyang’ata meno yake huku akiangalia sura ya Rufi iliopauka akiwa hajitambui.
“Damn it, is she a foreigner?”Aliuliza akimaanisha je sio raia wa nchi hio.
“Mwanaume aliemleta amesema wametokea Tanzania , kwasababu ya haraka hio ndio taarifa iliopo”
“Mambo hayawezi kuwa marahisi hivi , hatuna taarifa zake zote lakini pia ana majeraha ya risasi na yupo kwenye hali hio kwasababu ya kupigwa na bomu”
“Dokta anazidi kupoteza uwezo wake wa kuvuta hewa inabidi tuanze”Aliongea Grace.
“Tumeshindwa hata kunasa presha yake huenda ni kwasababu ya damu kuvuja kwa ndani na hatuwezi kuchukua hatari(risk) wakati sio raia , lakini pia mwanaume aliemleta kakimbia , kama tutamfanyia upasuaji tutalaumiwa kama akipoteza uhai”Aliongea Dokta Giggs na kufanya watu wote kumwangalia kwa mshangao tofauti , lakini hata hivyo walielewa alichokuwa akimaanisha,.
“Hospitali inaweka rekodi ya kila mgonjwa anaeitibiwa hapa na itaharibu taswira kama itafahamika mgonjwa amefia kwenye meza ya upasuaji na isitoshe hatufahamu hata jina la huyu mgonjwa na kwanini ana majeraha ya namna hii , sipo tayari ya kujiingiza kwenye matatizo kama mambo hayatoenda sawa, na nina uhakika kabisa wote wawili hawana hata hela za kulipia gharama za matibabu , kama akifa inabisi sisi wenyewe ndio tulipie gharama zote za matibabu na mnajua kabisa idara yetu haifanyi vizuri kimapato na tutashindwa kujielezea kwa wakurugenzi kwa kupoteza hela za hospitali kwasasabu ya mtanzania ….”Aliongea huku akianza kuvua gloves zake.
“Dokta huwezi kufanya hivi , mgonjwa bado yupo hai na tunapaswa kujitahidi kuyaokoa maisha yake”Aliongea mwanadada aliefahamika kwa jina la Grace, alionekana yeye tu ndio pekee ambaye hakukubaliana na Dokta Giggs na alikuwa na ujasiri wa kusema.
“Grace!!”Nesi aliezeeka aliita kwa namna ya kumtuliza akiwa na hofu kuna ambacho kinaweza kumtokea kwa kubishia maamuzi ya daktari.
Giggs alitoa barakoa yake na kisha akamwangalia Gracke kwa tabasamu lilojaa kejeli.
“You’re the new nurse?”Aliuliza akimaanisha kwamba je yeye ni nesi mpya.
“Dokta Giggs tafadhari usikasirike , Grace ana miaka kumi na nane pekee na yupo ndani ya hii hospitali kwa nusu mwaka pekee , anafanya kazi vizuri lakini bado hana uzoefu wa kutosha”Aliongea nesi aliezeeka.
“Hmph… nina sababu zangu kwa ajili ya kutoendelea na upasuaji wake , ni kupoteza muda wangu tu , kama unataka kuyaokoa maisha yake fanya wewe huo upasuaji na kama huwezi punguza maringo mtoto wa kike , hii ni hospitali na sio kituo cha misaada , Hospitali kama hii inahitai mapato kwa ajili ya kulipa mishahara na kuiendesha pia kihuduma , watu tunaoweza kuwaokoa ni wale wenye uwezo wa kulipia , Kwa umri wako unajua nini maana ya kuendesha hospiali wewe?”
Grace hakuridhika na maneno yake , lakini hakuwa na namna kwasababu hakuwa hata na huo uwezo wa kumsaidia mgonjwa kwani ni nesi wa kawaida.
“Najua wengi wenu mnaweza msikubaliane na mimi lakini lazima tufikirie kimantiki , huyu mgonjwa amepoteza damu nyingi hivyo hawezi kupona , hivyo tusipoteze nguvu zetu na muda kumuokoa , mwambieni yule mtanzania akirudi tumefanya juhudi za kila namna kumsaidia mgonjwa lakini ndio hivyo amefariki”Aliongea na wale wasaidizi wote walitingicha vichwa vyao ,, hata wao wenyewe kwa hali aliokuwa nayo Rufi walijua kabisa kupona kwake ni asilimia kumi tu.
SEHEMU YA 504.
Dokta Giggs alimwangalia kwanza Grace na akamuona anan’gata ng’ata lipsi zake kwa kukosa ujasiri na alitoa tabasamu la kejeli na kisha akageuka na kutoka.
Lakini ile anafungua tu mlango alikumbana na sura za watu wawili , mmoja alikuwa ni mtanzania na mwingine ni mwanamke wa kizungu ambaye hakumgundua mara moja kwa kumwangalia, alikuwa na uzuri ambao ni ethereal na macho yake ya bluu yalikuwa ni ya kustaajabisha.
Kwa uso wake ni kama walikuwa wakiufahamu lakini hawakumkumbuka huenda hawakutaka kuotea, lakini licha ya mwanamke huyo mrembo kuwa katika mavazi ya kihospitali lakini waliamini sio wa hio hospitali.
Daktari aliewafanya kumwangalia kwa mshangao hakuwa mwingine bali ni mtoto wa malkia Catherine afahamikae kwa jina la Clark.
Clark alikuwa akifahamika sana kwa mahospitaloi yote makubwa ambayo yapo ndani ya jiji la London , hivyo mara baada ya kufika hapo ndani alibadilisha haraka mavazi yake na kuvaa Scrubs rangi ya kijani kabla ya kuingia kwenye chumba cha kufanyia upasuaji.
Roma alikuwa ashamwelezea hali ya Rufi wakati wakiwa njiani , hivyo aliingia hapo ndani akielewa kila kitu.
“Giggs are you done with surgery ?”Aliuliza akimuliza dokta Giggs(sio gigi money) kama ndio amekwisha kumaliza kufanya upasuaji.
“Proffessor Clark!!!?”Alijikuta akishituka mara baada ya kusikia sauti yake.
Neno ‘Proffesor Clark’ liliwafanya wafanyakazi wengine wa hospitali hio sasa kuelewa ni kwanini sura ya dokta huyo wa kike alievalia barakoa ilikuwa ikiwajia na kupotea.
Princess Clark kioo cha wanataaluma wengi wa maswala ya kitabibu ndani ya nchi ya Uingereza, hebu subiri , huenda ni dunia nzima.
Giggs alikuwa ni moja ya wanafunzi ambao amefundisha na asingeshindwa kumkumbuka kuokana na kwamba alikuwa vizuri sana kwenye kukariri sura kutokana na akili yake na Giggs alikuwa moja wapo ya wanafunzi wake pendwa.
Na zaidi ya yote Clark alikuwa kama mungu wa kike kwa kila mwanafunzi, alikuwa ni Princess lakini wakati huo akiwa mtafiti namba moja ndani ya jiji lote la London , akiwa vizuri kwenye maswala ya bailojia ya binadamu pamoja na maswala ya siraha za kijeshi.
Alikuwa na vyeo vingi ambavyo hakuna hata mwanasyansi ambaye alikuwa tayari kutaka kulinganishwa nae.
Wote walikuwa kwenye mshngao kwasababu moja , Clark alikuwa ni nadra sana kuonekana hadharani.
Clakr hakufurahishwa na mwonekano wa Giggs kabisa baada ya kumuuliza swali.
“Nipe jibu tafadhari , hali ya mgonjwa ikoje na nini kimetokea wakati wa upasuaji?”
“Uh..teacher … tumefanya kila liwezekanalo lakini moyo wa mgonjwa umeacha kudunda na tayari tulishachelewa kuanza kumfanyia upasuaji kutokana na kupoteza damu nyingi”
“What !!” Roma alihamaki huku akiingiwa na ubaridi usio wa kawaida , ni kama vile amegongwa na nyundo ya utosi , haikuwa kwake tu hata kwa Clark na yeye pia alipatwa na mshangao kwa taarifa hio.
Wale wafanyakazi wengine hakuna alienua mdomo wake kukanusha kauli ya Giggs , waliishia kuinamisha vichwa vyao kwa huzuni, ni kama walikuwa wakiogopa kimwangalia Clark usoni.
“Dokta Clark mgonjwa bado anapumua na hakuna upasuaji uliofanyika , Dokta Giggs alikuwa na wasiwasi kwamba wasingeweza kulipia gharama za matibababu na hakutaka kuchukua risk hivyo akaamua kuacha”Aliongea nesi aliefahamika kwa jina la Grace kwa ujasiri mkubwa na maneno yake ilikuwa ni kama hospitali imepigwa na radi.
Giggs uso wake ulifubaa palepale kwa mshutiko kwani hakutarajia Grace kwenda kinyume na maagizo yake.
“Wewe mwanamke acha kujaribu kukashifu taaluma yangu..”Aliongea akitaka kujitetea lakini Grace alikuwa kama kisiki cha mpingo , moyo wake ulimwambia kumuokoa mgonjwa ndio imani yake na anapapswa kuisimamia.
“Miss Clark I’ve heard about your acomplishments , please save her , she is already at death’s door”
“Bi Clark nimesikia kuhusu mafanikio yako , tafadhari sana muokoe huyu mgonjwa , tayari ashachungulia mlango wa kifo”Grace wa watu mwenye moyo wa kijasiri aliongea na kuwafanya wale wote waliokuwa kimya kama kondoo machinjioni waangaliane wakishindwa kuamini mtoto mdogo kama Grace angekuwa na ujasiri wa namna hio.
Roma palepale alihitaji kwanza kuthibitisha maneno ya Grace , hivyo alitumia mbinu zake za kijini na kisha akam’scan’ Rufi kuona kama bado anapumua na alijiridhisha kwamba yupo hai bado.
Na kwa kupata ufunuo huo kwake ilikuwa sababu tosha ya kumsindikiza Giggs kwanza , alimshikilia shingo palepale na kumnyanyua juu huku akiwa anamkaba.
Giggs ambaye alikuwa kwenye wasiwasi , sasa alijishutikia tu akiwa kwenye kitanzi cha mkono akielea elea huku akipiga miguu huko na kule kama mtu anaekata roho.
“Wewe shetani , wewe ni daktari kweli , leo nakuua mshenzi wewe”aliongea Roma kwa hasira.
“Stop it, this is hospital”
“Acham hapa ni hospitalini”Alifoka Clark
“Hospitalini? Kwahio kama pakiwa hospitalini, ninakwenda kumuua huyu mpuuzi na hakuna wa kunizuia”Aliongea .
“Hii ni hospitalini ukubali au usikubali na mimi kama daktari siwezi kukuangalia ukimuua mtu mbele yangu tena ndani ya hospitali”Aliongea Clark kwa sauti huku akijaribu kumzuia Roma aache kile anachokifanya.
‘Sogea pembeni Clark”
“Sisogei na kama unataka nimuokoe mpenzi wako , acha ukichaa wako”Aliongea na ilikuwa ni kama sasa Roma alielewa alichokuwa akimaanisha na hasira zilishuka palepale na kumrushia kwenye korido nje.
“Roma najua una hasira na kutamani wote wafe na sitojali kama utafanyia nje ya hapa lakini ndani ya hospitali siwezi kuruhusu”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie namna Clark alivyosiriasi na aliona alikuwa akichelewa kumukoa Rufi.
“Clark nakuomba tafadhari muda unaenda , nisaidie kumuokoa siwezi kuruhusu mwanamke mwingine akifa chini ya uangalizi wangu’Aliongea na kauli yake ilimfanya Clark kuelewa.
“Nimekuelewa na nnitajitahidi’Aliongea na kisha akazama ndani kabisa na kuvalishwa gauni kwa ajili ya kuanza kumuokoa Rufi.
Roma yeye alitoka zake ili kwenda kuangalia namna upasuaji unavyofanyika upande wa pili huku akimpia Giggs aliekuwa ameshikilia shingo yake akimwangalia Roma kwa wasiwasi.
Wakati Roma akifika mahali ambapo pametengwa maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa hospitalini kuangalia kile kinachoendelea, upande wa ndani katika meza ya upasuaji Clark alikuwa akianza kuwapa maagizo kwa ufasaha kabla ya upasuaji kuanza.
Wataalamu wa ganzi , watalalamu wa mitambo na wasaidizi wote walikuwa wakionekana kuwa bize kusikiliza kila maagizo yanayotolewa na kuyafanyia kazi kwa haraka na baada ya hali kutulia hatimae alianza kazi.
“Scalpel..”Alinyoosha mkono wake kupewa kisu kuanza kuchana lakini mtaalamu wa ganzi alionyesha wasiwasi.
“Dr Clark mgonjwa tayari keshapoteza fahamu na pia amepoteza damu nyingi kama utampasua ..”
“Najua kwamba presha yake itashuka sana hususani kwa damu iliopotea zaidi eneo la tumboni, hivyo kama kila mmoja wenu ataendana na spidi yangu nina uhakika itakuwa rahisi kurahisisha mchakato mzima ,, tupo kitimu hata hivyo , si wote tunakubalina?”Aliuliza na wote walitingicha vichwa.
“So let’s move it , chop-chop”Aliongea na kuwafanya watu wote ndani ya chumba hiko cha upasuaji hali yao kuamka tena na kushawishika kwamba huenda ni vyema kujaribu.
“The patient’s right lower quandrant has seen massive blood loss so to first start off we must first locate the point of injury before we can cut her open ..”
“Mgonjwa upande wa chini wa kulia umeonyesha kupoteza damu nyingi hivyo kabla hatujaanza lazima tutambue ni eneo lipi limeumia kabla ya kupasua”Aliongea Daktari bingwa Clark huku akivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha akaaanza kazi…………..
“Dokta kapoteza damu nyingi, nakosa ujasiri wa…”Aliongea daktari msaidizi wa kike mara baada ya kuona damu nyingi inayotoka na kumpa ishara ya kuacha hofu.
“Leta spreader na kisha andaa spray ya kusafisha , tutatafuta sehemu iliopata jeraha ..”Aliongea na wakatingisha vichwa kukubali.
Profesa Clark ndani ya muda mchache tu kwa wepesi wa hali ya juu aliweza kufanikisha kuona chanzo cha jeraha ambalo linasababisha damu nyingi kuvuja.
“The patient’s liver is ruptured at three point , S1, S4 and S6”Aliongea akimaanisha ini la mgonjwa limechanika katika sehemu tatu.
“Sehemu tatu?”Walijikuta wakiangaliana kwa mshangao huku wakijikatia tamaa.
“Kama akiendelea hivi hatutoweza kupata muda wa kumaliza kumshona ndani ya muda kwani damu inayovuja katika ini lake itatuletea ukinzani”Aliongea msaidizi..
Upande mwingine nje Roma alikuwa akiona kile ambacho kinaendelea na alikuwa akiomba kila namna Rufi aweze kupona kwani asingeweza kujisamehe kama atapoteza maisha , kwa namna alivyokuwa na wasiwasi hakuwa mfalme Pluto tena yule ambaye kuua ni dakika moja , huyu alikuwa kama binadamu wa kawaida tu ambaye anauguliwa.
“Let us use the patent ductus arteriosus to hold her wound in place !”
“Tutumieni patent ductus arteriosus ili kufanyia kazi majeraha yake”Aliongea Clark mara baada ya kupata wazo.
“Unasemaa..!!”Wote walionyesha kushangaa kama vile hawajamsikia.
“Patent ductus arteriosus”Alirudia.
Timu yote ilikuwa kwenye mshangao kwasababu mbinu hio ya dharula ilihitaji mchakato uchepushaji wa pamoja wa kiumakini wa hali ya juu wa kukata nusu ya mtitirisho wa damu unaoingia kwenye ateri ya ini(hepatic artery) na mshipa wa Cystic(Cystic vein) ili damu isiingie kwenye ini halafu washone majeraha kwa haraka kwa wakati mmoja kwasababu ini limepata majeraha sehemu tatu na kudili na sehemu moja yenyewe ilikuwa ni kazi kubwa na ili mchakato huo ufanikiwe spidi ya hali ya juu sana ya ushonaji inahitajika .
“Tunapoteza muda acheni kushangaa”Aliongea huku akijiamini kile ambacho anakwenda kufanya.
“Hand me the needle kit , thready forty”
“Yes ma’am “
…………….
Kila mmoja alishangazwa na spidi ya profesa Clark , mbinu yake ya kushona kwa haraka iliwaacha mdomo wazi kwani hakutumia nguvu sana, alionekana kuiva kwa kile anachokifanya na ndani ya dakika nne tu alifanikisha kumaliza eneo la kati.
“Blood pressure.!!!”Aliuliza.
“Its out, eighty , sixtty”Aliongea mtaalamu wa ganzi akimaanisha presha ni themanini kwa sitini.
“Nisaidie kushikilia hilo ini , nitaziba sehemu ya tatu”Aliongea na palepale msaidizi aliinua lile ini kujaribu kushikilia lakini walijikuta wakipagawa kwani damu ilifyatuka
“Kwanini kuna damu nyingi inayotoka?”
“Hali sio nzuti , na presha inazidi kuporomoka ,arubaini sasa”Aliongea mtu wa ganzi kwa kupaniki.
“Inabidi kwanza tuipandishe presha na kama jeraha tutaliziba na bado ikaendelea kushuka basi kuna sehemu nyingine imepata jeraha?”
“Kwahio tunatakiwa kufanya nini ?”Aliuliza Grace.
“Allocate the blood funnel, we draw the blood and I will proceed with recycling(Autotranfusion)”Aliongea na kufanya watu wote pia kuchangayikiwa kwani mbinu hio kufanyika kwake ni mara chache na huenda ni mara ya kwanza kufanyika kwenye hio hospitali.
………………..
Ni baada ya masaa kadhaa ya Clark kuonyesha ujuzi wake hatimae aliweza kupata sehemu zote zilizopata majeraha na kuziba kote na damu ilioporuhusiwa kupita tena kwenye ini haikuonekana sehemu inayovuja tena.
“Doctor the patient’s blood presure is now back within normal limit”Sauti ya futaha ilisikika na kufanya kundi lote kupumua kwa ahueni huku wakionyesha furaha zao kupitia macho yao.
Ulikuwa upasuaji uliofanyika ndani ya muda mchache sana na hiko ndio kilichoshangaza na kuona utofauti uliopo kati ya Giggs pamoja na mkufunzi wake.
“Well done everyone “Aliongea kuwapongeza kwa ujasiri waliokuwa nao kumsaidia mpaka akafanikisha na baada ya hapo aligeukia upande wa Roma alipo na kisha akamnyooshea kidole gumba kwamba mambo safi .
Na Roma alijikuta akifurahi na kujiambia Clark hajawahi kumuangusha kila anapopatwa na changamoo kubwa.
“Inaweza kuwa mimi kufeli kwangu mimi kama mkufunzi kwa kuwafundisha maarifa ya kiabibu ila nikashindwa kuwaelesha nini maana ya maadili kama daktari na naamini kupitia tukio la leo mmeweza kujifunza kitu , kama watoa huduma mkumbuke hakuna mgonjwa yoyote ambaye anapaswa kuachwa kufa, mkiwa na mtazamo wenu hupo haitokuwa na utofauti wa kuua mgonjwa mbele ya macho yenu , kama mgonjwa anahitaji huduma na yupo mbele yenu wazo la kwanzo ni kumuokoa na sio kutafuta sababu , kwasababu kazi ya daktari siku zote ni kuokoa maisha kwa mazingira yoyote yale bila kujali aina ya mgonjwa”Aliongea Dokta Clark akijaribu kuwapa shule wale wasaidizi wake.
Mafanikio ya upasuaji huo mgumu uliofanyika usiku huenda ikaacha kumbukumbu kwa wote walioshiriki.
Baada ya kila kitu kumalizika, Clark alimfuata Grace aliekuwa amejikunyata kwenye kona akisinzia kutokana na uchomvu wa kusimama muda mrefu na kisha akamshika mkono.
“Jina lako unaitwa nani?”Aliuliza Clark na kumfanya Grace kushituka kwa haraka huku akiona aibu.
“Naitwa Grace..”
“Grace ni jina zuri mno , ningependa kukushukuru kwa ujasiri ulio uonyesha leo”Aliongea na kumfanya Grace kuinamisha kichwa kwa wasiwasi.
“Hapana daktari , umefanikisha kumuokoa mgonjwa na mimi ni nesi tu..”
“Kama utapenda naomba niwe mwalimu wako kwanzia sasa”Aliongea Clark na kauli yake ilikuwa kama bomu kwa kila mmoa aliemsikia. Grace akiwa mmoja wapo.
Kauli yake iliwafanya kujawa na wivu kwani walielewa nini maana ya kuwa mwalimu chini ya Clark.
Ijapokuwa kimuonekano Grace na Clark wanaweza kuwa katika umri sawa lakini kuwa mwalimu kwa Grace halikuwa tatizo.
Kuwa mwalimu wa Clark haikumaanishaa kwamba kuingia kwenye vipindi vyake akitoa somo chuoni , lakini ilimaanisha kwamba wangeambatana pamoja katika tafiti mbalimbali na kujifunza vitu kwa ukaribu zaidi kama ilivyokuwa kwa Ashley.
“Kama nitakuwa mwanafunzi wako , je nitapata nafasi pia ya kufanya kazi ndani ya hii hospitali?”Aliuliza Grace kwa furaha iliochanganyika na wasiwasi na swali lake lilimshangaza Clark.
“Kwanini unataka kuendelea kubakia hapa?”
“kwasababu nitapamisi hapa na kufanya kazi pamoja na kila mtu na pia napapenda mno , ilikuwa ni kama ndoto yangu kufanya kazi ndani ya hii hospitali”Aliongea kwa sauti ya chini iliojaa aibu na maneno yake yaliwagusa timu nzima na yule nesi aliezeeka alishindwa kuzizuia hisia zake na kutoa machozi ilionekana licha ya kuzeeka alikuwa akimpenda Grace.
“Bila shaka unaweza kufanya kazi hapa na mpaka sasa nadhani tushakubaliana , utakuwa mwanafunzi wangu na siku ambazo upo off utakuja ninakofanyia tafiti au nyumbani kwangu na nitakuwa nakufundisha”
“Really!!?”Grace aliinua kichwa chake kwa msisimko mkubwa wakati akijibu.
“Sure..haha, lakini kama mwanafunzi unatakiwa kuwa tayari na kuwekeza moyo wako wote kwa kile unachojifunza na kama hutofanya vizuri nitakasirika”
“I.. but , I am not smart”Aliongea Grace wa watu akimaanisha kwamba lakini hana akili.
“Kama ungekuwa jiniasi nisingehitaji hata kukufundisha , tabia yako isio ya kichoyo na kumtanguliza mgonjwa kwanza ndio imenifanya nikuone, hata hivyo wewe bado mdogo hivyo kama utaniamini na kufanyia kazi kila ninachokuelekeza nina uhakika utakuwa na kesho inayong’aa”Alimhakikishia Clark.
“Yes doctor Clark I will do my best”Aliongea akimaanisha kwamba atafanya vizuri.
“Umeniita nani?”Aliuliza kwa sauti ya ucheshi.
“Ah..nimesahau namaanisha mwalimu”Aliongea na wote wakacheka na wengine kutabasamu .
Haikuwa tu kwamba Clark alifanya upasuaji wa kushangaza na wa kishujaa lakini pia na bahati ilimwangukia Grace na kupata mwalimu wa viwango.
Waliishia kupompngeza Grace na kumtakia mema katika safari yake ya mafunzo mapya.
Upande mwingine ki asili hakukuwa na haja ya kufikiria sana nini kingempata Giggs kwani kwa tabia alioionyesha ni halali kabisa kupokonywa leseni yake ya udaktari na ndio mwisho wake kutibu na hata hivyo mgonjwa aliemletea dharau ni wa mfalme Pluto ambaye sio kwamba alikuwa na koneksheni bali yeye ndio koneksheni yenyewe hivyo kauli yake moja tu kila kitu kinabadilika.
Hivyo moja kwa moja taarifa zikiwafikia mabosi wa hospitali hio hawatotaka kupewa maagizo mengine zaidi ya kumfukuza.
Baada ya muda mfupi hatimae Rufi alitolewa chumba cha upasuaji na kupelekwa upande wa wagonjwa wa uangalizi wa hali ya juu., Roma mara baada ya kuona angalau hali yake ya ngozi imeimarika alijikuta akivuta pumznni nyingi za ahueni.
“Clark sina maneno halisi ya kuwakilisha shukrani zangu kwako”
“Huna haja ya kunishukuru na kukusaidia nadhani ndio maana nimezaliwa , tokea siku ulipoyaokoa maisha yetu tunaishi kwa kuwa na deni kubwa kwako”
“Unanifanya nione sijaongea kauli sahihi sasa?”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchungu.
“Haha.. wakati nilipo ona mgonjwa ambaye natakiwa kumuokoa nilitamani nisiwe daktari ili isiwe jukumu la kuokoa maisha ya mpenzi wako mwingine”
“Hehe.. wewe ndio daktari pekee ninaekujua na kama si vinginevyo nisingemleta huku kwa haraka”
“Muone sasa unajaribu kubadilisha topiki wakati unajua kabisa ninachojaribu kumaanisha”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.
“Anyway… nakushukuru sana na hongera kwa kupata mwanafunzi mwingine ijapokuwa naona maamuzi yako sio sahihi”Alitania.
“Unaongeaje hivyo , Grace ni mkarimu sana na naamini kama nitamfundisha ndani ya miaka ijayo kutokana na tabia yake basi atakuja kuwa daktari mzuri sana , je unakubaliana na mimi?”
“Lakini unafundishaje mwanafunzi ambaye naona kama mnalingana?”Aliongea na kumfanya ang’ae meno kwa hasira.
“Ninarudi kwenda kulala , isitoshe muda umeenda na inakaribia asubuhi , mgonjwa wako anatakiwa alazwe hapa kwa muda ili kupona na siku mbili au zaidi anaweza akaanza kutembea , mhakikishie kwamba mbinu zangu za ushonaji ni za viwango hivyo asihofie kuona kovu”Aliongea na kisha aliwapa ishara ya kwaheri madaktari na wahudumu na kuondoka.
Roma alisimama kwa muda huku akiwa anapumua sasa vizuri na muda huo mawazo ya Mage nchini Australia yalimrudia.
“Kwa mara nyingine tena naomba uangalizi wa mgonjwa wangu , msiwe na wasiwasi nina kiasi cha pesa kingi kuliko ninavyotumia kwahio muangalieni kwa kiwango cha juu kihuduma kwani ninaondoka mara moja”Aliongea Roma.
Rufi aliumia kwa ajili ya kumuokoa yeye na mpaka hapo alijiambia hawezi tena kumpotezea kama Edna anavyotaka na alijiambia akirudi nyumbani atajua namna ya kumalizana na mke wake , lakini kwanzia muda huo na kuendelea Rufi ni mpenzi wake mwingine katika orodha.
Muda huo wahudumu hakuna ambaye alimuona Roma kama mtu wa kawaida , hivyo walimuhakikishia kwamba Rufi angekuwa salama mpaka atakaporejea.
Roma alitoka hapo hospitalini na kisha aliteleport kurudi Australia , muda ulikuwa umeenda na alipokuwa akiingia kwenye anga la Australia muda nao ulikuwa ukikaribia jioni.
Roma alitokeza nyuma ya Mage aliepiga magoi kuelekea baharini akionyesha kama mtu asie na tumaini na kwa haraka haraka Roma alitambua Mage ana Sali , lakini wakati huo huo akilia kama mtoto alietelekezwa.
Roma alijiambia siku zote mwanamke ni mwanamke tu hata kama ni polisi.
“Babe Mage usiniambie umeshaanza kuwa mchungaji?” Aliuliza Roma na kauli yake ilimshitua Mage na kugeuka haraka huku akisimama.
“Hali ya Rufi inaendeleaje ?”Ndio swali la kwanza ambalo alitaka kusikia kutoka kwa Roma.
“Yupo salama kwasasa na Clark amefanikisha kumuokoa kwa kumfanyia upasuaji, atakaa hospitalini kwa siku kadhaa mpaka atakapokuwa sawa”Aliongea Roma na kumfanya Mage kutoa machozi ya furaha.
“Asante Mungu , Asante sana Mungu , asingepona ningeshindwa kujisamehe maisha yangu yote…”Aliongea na kumfanya Roma amvute kwake na kumkumbatia.