Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 523.

Profesa Clark hakujali sana namna ambavyo watu wa nje ya chumba hicho cha upasuaji walivyokuwa na wasiwasi zaidi ya kuwaambia wasaidizi wake kuwa makini na upasuaji.

Mpaka anakuja kumaliza upasuaji hakuna ambaye aliamini kama amefanikiwa kwa asilimia mia moja kuokoa maisha ya Park Juan..

Dokta Lee ambaye aliangalia mchakato mzima wa upasuaji alihisi ni kama vile anaota kwani mambo ambayo alikuwa akifanya Dokta Clark hakuwahi kuyashuhudia na siku hio ilikuwa mara yake ya kwanza.

Kuna baadhi ya taratibu za kiupasuaji aliishia kuzisoma tu kwenye vitabu na hajawahi kuona zikifanyika kwa vitendo , lakini mbele ya Dokta Clark baadhi ya nadharia ambazo amezisoma katika safari yake ya kuwa daktari ameweza kuona mubashara kabisa zikifanyika.

Madaktari na manesi wasaidizi walimhusudu Dokta Clark pia kwa uwezo wake, ilionekana kwao ni kama vile alikuwa amezingatia kila changamoto ambayo ingeweza kujitokea katika upasuaji huo.

Madaktari wote waliofika kuangalia namna upasuaji unavyofanyika walijikuta wakisimamama na kuanza kupiga makofi.

Yezi alifurahi sana kuona babu yake ameweza kuhimili upasuuaji huo mzito kufanyika , upasuaji wa upandikizaji wa viungo viwili kwa wakati mmoja na mpaka hapo shukrani zake zote zilienda kwa Dokta Clark ambaye amemsaidia babu yake.

Katika watu ambao hawakupenda mafanikio ya upasuaji huo kufanikiwa alikuwa ni Park Jonghyun , lakini kwa kinafiki alitoa shukrani kwa madaktari wote waliohusika katika upasuajji.

Baada ya upasuaji kumalizika wanafamilia wote walikubaliana kutafuta mgahawa kwa ajili ya chakula cha usiku.

Kim Jip ambaye aliondoka kwenda kuchukua moyo aliweza kurudi akiwa ameongozana na baadhi ya mabodigadi wa familia ya Park , pamoja na baadhi ya polisi.

Alikuwa kauzu kama kawaida yake na alikuwa tayari ashapata taarifa ya Roma kurudi hospitalini akiwa amefanikisha kuupata moyo uliohitajika.

“Asante sana Mr Roma”aliongea Kim Jip mara baada ya kumsogelea Roma.

“Umeweza kumpata mtu alieigiza sura yako?”

“Hio ndio sababu ambayo imetufanya tuwe hapa Mr Roma , kwa majina naitwa Jang Yoon kiongozi wa idara ya uchugnzi ya kituo kikuu cha polisi Seoul , kulingana na uchunguzi wetu wa mwanzo dereva ambaye alipewa jukumu la kuendesha gari lililobeba moyo amesema wewe ni mtu pekee wa mwisho ambaye uliweza kukutana na mtuhumiwa , hivyo hili ni swali letu kwako , Mtuhumiwa yuko wapi?”

“Si alishakufa, hamkuweza kupata mwili wake? , alijiua yeye mwenyewe kwa sumu”Alijibu Roma huku akionyesha mshangao kidogo.

“Mr Roma tunataka majibu yako ya kweli , wewe ndio uliechukua moyo kutoka kwake hivyo lazima utakuwa umemuona , tafadhari tuambie yuko wapi mtuhumiwa?”

“Oh! Kwahio mnachojaribu kumaanisha ni kwamba hamjaweza kuona mwili wa mtuhumiwa?”

“Sisi ni polisi , unadhani tunaweza kudanganya juu ya hili , Bwana Kim Jip hapa na yeye atapenda kujua nani ambaye amehusika kuigiza sura yake”Aliongea yule polisi wa Kikorea na kumfanya Roma kujilaumu kwa maamuzi yake alioyafanya, mpaka hapo alijua kabisa waliokuwa nyuma ya Kim Jip feki watakuwa waliwahi eneo la tukio na kisha wakaondoa mwili na kwasababu ya kukosekana kwake kesi ni kama imemwangukia yeye.

“Dereva alithibitisha kama alimuona Kim Jip feki na sisi wakati tukiwa tunamuhoji ndio tulipoweza kusikia taarifa ya moyo umeweza kuufikisha hospitalini , kutokana na mlolongo wa matukio tunapata hisia za wewe kuhusika katika hilo, hivyo basi itakuwa vyema kama utakubali kwa hiari yako kuongozana na sisi mpaka kituo cha polisi ili kutoa maelezo yako rasmi”

“Hamuwezi kumchukua bila ya kuwa na ushahidi , Uncle Roma ndio ambaye ameokoa maisha ya babu yangu”Aliongea Yezi akimkingia Roma kifua.

Edna hakujua kinachoendelea kutokana na kwamba hakuwa akifahamu lugha ya Kikorea na ilibidi aombe kutafsriwa na Roma alimweleza kwa ufupi namna tukio lilivyotokea na kumfanya sasa kuelewa na kuwa na wasiwasi.

Jopo lote mpaka hapo waliweza sasa kujua kama ile ajali iliosababisha moyo kuchelewa haikuwa bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango wa watu na hamu yao yote ya kwenda kula ilipotea.

“Mr Roma ni mgeni wa heshima wa ukoo wa Park bila kushahau mchango wake mkubwa aliofanya kwa babu yangu kwa matibabu yake yake ,kapteni Jang nakushauri ufikirie mara mbili unachotaka kufanya”Aliongea Park Jonghyun.

“Bila kuwa na ushahidi wa kueleweka mtu wa mwisho kumuona mtuhudmiwa atageuka kuwa mshukiwa mkubwa wa kile kilichotokea , hivyo naomba ushirikiano wenu kwa jeshi la polisi la jamhuri ya Korea”Aliongea Kapteni Jang.

“Okey hakuna shida , kama unataka kuchukua maelezo yangu basi nitaongozana na wewe , hata mimi pia ninashauku ya kujua mwili umeenda wapi , hivyo nyie endeleeni kwenda kupata chakula na msiwe na wasiwasi”Aliongea Roma na kufanya kundi lote kukubali na Roma aliondoka na polisi.

Upande wa Edna alijua kabisa Roma hakuwa mhusika lakini hakupenda Roma kupelekwa kituo cha polisi.

Roma mara baada ya kuingia kwenye gari la polisi , liliondoshwa na kuelekea upande wa kusini mwa jiji la Seoul na baada umbali kama wa kilomita tatu gari ile ilikunja kulia na ilichukua njia ya pembeni likiachana na barabara kuu na kuingia upande wa viwanda.

“Ofisa Jang inashangaza kituo cha polisi kuwa maeneo haya ya Viwanda?”Aliuliza Roma ambaye muda wote alikuwa ametulia lakini wale mapolisi watatu walipotezea swali lake na gari likaendelea kuserereka

Upande wa Roma aliishia kutabasamu kifedhuli na kisha akakaa kimya kijua mwisho wake ni nini.

Baada ya muda kama dakika tano gari iliingizwa ndani ya eneo lenye ukuta kwa nje, sehemu ambayo ilionekana kuna ujenzi wa kiwanda unaendelea kutokana na uwepo wa magreda ambayo yanaanza kusawazisha ardhi ili kuweka msingi.

“Shuka chini”Aliongea polisi mmoja kwa namna ya kufoka kwa lugha ya kikorea.

“Hatuendi kituo cha polisi?”Aliuliza Roma mara baada ya kukagua mazingira.

“Kituoni kufanya nini?”

“Unamaaisha nini?”

“Kwasababu hapa ndio unakwenda kufia”Alijibu mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Jang.

Polisi wawili ambao walikuwa warefu walimsogelea Roma mara moja , kwa haraka haraka.

Roma aliweza kuona miili yao ilikuwa mikakamavu na kuhisia wanaweza kuwa na mafunzo ya kimapigano.

Lakini upande wa Roma hakuwa na hofu kabisa , kwanza kabisa alikubali kuondoka na polisi hao makusudi kwani alishaona nia yao ovu.

Walianza kumshambulia palepale, lakini kila pigo ambalo walijaribu kumpiga nalo Roma aliishia kukwepa na kumfanya yule polisi ambaye alikuwa kama kiongozi kujiunga pia kwenye kushambulia .

Mmoja wapo alileta teke la hewani la kitaekwondo akidhamiria kumpiga Roma shingoni lakini Roma kwa ustadi kabisa aliweza kukamata mguu wake wa kulia yule bwana na kisha akamzungusha hewani na kumtupia kwenye trekta.

Mwingine alijileta kizembe na Roma kwa kutumia mguu wake wa kushoto alimtegua goti pale na akadondoka chini huku akiugulia maumivu.

Jang Yoon alijawa na kiwewe na palepale alitoa bastora yake na kuikoki akitaka kumshambulia Roma kwani mpaka hapo aliona kabisa hakuna namna wanaweza kushinda kwa kupigana nae bila siraha.

Lakini kabla hata hajafyatua kiganja cha mikono yake kilifikiwa na kupindishwa na bastora ikadondoka chini na Roma akaipiga teke kwenda kutua mbali.

“Nyie watu najua mpo katika kundi moja na yule mwigizaji mwenzenu wa sura , si ndio?”Aliuliza Roma na kuwafanya wale mabwana kushindwa kutoa jibu lakini walikuwa wakikiona kifo chao usiku huo kipo karibu , kwani mtu aliekuwa mbele yao hakuwa wa kawaida.

“Nani kawatuma na mnatafuta nini? Nawapa nafasi ya kujibu la sivyo nitawanyonga mmmoja mmoja mpaka mniambie ukweli”Aliongea Roma lakini wale mapolisi walionekana kutotaka kujibu hivyo Roma alimsogelea mmoja ambaye alikuwa amejipigiza kwenye trekta na kumpiga karate ya uti wa mgongo na kilichosikika ni kuvunjika kwa uti wa mgongo na kufariki palepale.

Wale wawili waliobaki walijikuta wakijawa na hofu na kumuona Roma sio mtu wa kawaida kwa namna alivyommaliza mwenzao kikatili mno.

“Kwasabau wote nyie wawili mpaka muda huu hakuna ambaye amejiua kwa sumu hisia zangu zinaniambia nyie hamna mafunzo ya U’ninja, hivyo ni bora kujieleza mapema kabla sijatekeleza vifo vyenu kama mwenzenu”Aliongea na bado walionekana kusita sita na Roma alimsogelea mmoja kwa spidi na kumsukumia kwenye ukuta kwa nguvu akimnyonga shingo.

“Naomba uniache niondoke… sijui chochote tafadhari … sitaki kufa naomba usiniue”aliongea mwanaume yule kwa namna ya kujitetea.

“Nishakwambia nahitaji majibu ..”Aliongea Roma na palepale hakutaka kuendelea nae kwani alimvunja shingo na kumtupa chini.

Jang Yoon mara baada ya kushuhudia wenzake wote wakiwa wamepoteza maisha kirahisi aliangalia namna ya kukimbia na baada ya kupata upendo alitoka nduki , lakini Roma hakutaka kumpa nafasi na hakutumia uwezo wake wa kijini bali aliokota jiwe na kulivurumisha upande wake na kumpiga nalo mgongonni karibu na kiuno na kudondoka chini palepale huku akigulia maumivu na akamsogelea.

“Nitaongea , nitaongea tafadhari usiniue”Aliongea Jang Yoon huku kila akijaribu kusimama alikuwa akidondoka chini kwa mauamivu.




“Kwanini ulikuwa ukileta ugumu , pengine nisingechafua mikono yangu kwa kuuwa wenzako”Aliongea Roma kwa tabasamu lake la kuogopesha na kumfanya Jang Yoon kuanza kuinua mdomo wake kwa wasiwasi.

“Nime.. nimetokea katika umoja wa siri wa North Buyeo, yalikuwa ni maagizo tuliopewa kutoka kwa viongozi kukuleta hapa na kukuua kwani umeingilia mipango ya jamii yetu “Aliongea na kumfanya Roma kushangaa

“North Buyeo, unaongea ukweli?”

“Ndio , sisi ni Double agent ambao tumepandikizwa katika kituo cha polisi kufanya kazi kwa manufaa ya taasisi”

“Kwa maelezo yako unamaanisha mpo wengi zaidi , huenda kila nyanja ndani ya taifa, si ndiio? Kama ni hivyo wewe nafasi yako katika jamii hio ni ipi?”

“Nafasi yangu ni ya chini lakini sio chini kabisa”

“Nani mwingine anajua kuhusu hii taasisi ambaye yupo ndani ya kituo cha polisi?”

“Sina uhakika lakini mkuu wa kituo cha polisi ni mwanachama pia ambaye yupo ngazi ya kati”

Roma alishangazwa na ufunuo huo, mwanzoni alidhania labda ni kundi tu la maninja ndani ya Korea lakini mpaka hapo alijua kabisa sio kundi bali ni taasisi na kama ni hivyo mizizi yake ndani ya Korea itakuwa mikubwa mno.

Roma hakuwa na matamanio sana na taasisi hio kwasababu haipo nchini kwake na pia sheria hazikumruhusu kuingilia mambo ya binadamu wa kawaida , lakini kilichomfanya kutaka kuingilia ni kwasababu ya Yezi , kama moyo wa upandikizaji umechelewesha na taasisi hio moja kwa moja alijua kabisa hata Yezi pia anaweza kuwa katika hatari akiendelea kuishi Korea.

“Mr Roma ,, je naweza kuondoka?”

“Ndio unaweza kuondoka lakini nitakusindikiza”

“Hapana hapana , nitaenda mwenyewe”Aliongea huku akijikongoja kusimama na kuanza kusogea kuelekea getini , lakini Roma hakuwa na nia ya kumuacha aende hivyo alimsogelea na kummaliza palepale baada ya kumpiga ngumi ya utosini na kwasababu ngumi yake haikuwa ya kawaida kichwa chake kilichanguka paleplae na kumfanya nguo aliovaa kurukiwa na matone ya damu.

“Nilikwambia nitakusindikiza kuna haja gani ya kukimbia, haya umekufa sasa wasalimie kuzimu”Aliongea mwenyewe na kisha palepale akaita nguvu za kijini na kukausha miili yote kimazingara na sehemu ikawa safi bila ya kuacha ushahidi wowote kama kuna watu waliokufa katika hilo eneo,.

Baada ya kumalizana na maiti zao alifungua gari la polisi na kulichunguza na hakuona cha maana na palepale aliita moto wa kijini na gari lile lilipuka kama limetegeshewa bomu , lakini ulipukaji wake haukutoa sauti yoyote kutoka eneo hilo.

Baada ya kumalizana na tatizo hilo dogo alitoa simu yake na kumpigia Edna ,tokea wafike hapo Korea walisajili laini za mitandao ya nchi hio ili kurahisisha mawasiliano.

“Wife kazi imeisha , mpo wapi sasa hivi?”Aliongea Roma kwa kiswahili na Edna alishangazwa na maneno yake na kumwambia sehemu waliopo.

Roma mara baada ya kukata simu alitafuta namba ya simu ya Makedoni na kupiga palepale, aliamini swala kubwa kama hilo la jamii ya siri hawezi kulifanyia kazi yeye mwenyewe bila ya kuhusisha mtaalamu wa maswala ya ujasusi.

“Master Pluto nilikuwa nikipanga kwenda kuoga , unataka nikusaidie nini?”Aliuliza Sauroni upande wa pili mara baada ya simu kupokelewa.

“Nataka kujua kati ya watu wetu ambao wapo Korea kusini , mahsusi walipo ndani ya jiji la Seoul , naweza kuwapataje?”aliuliza Roma.

“Tuna wanajeshi wa kundi la Guerilla lakini wapo Korea ya Kaskazini,kuhusu Seoul sidhani kama kuna uwezekano wa watu wetu kuingia huko bila ya kushitukiwa kwani mipaka yao ina ulinzi wa viwango vya juu sana”Aliongea Makedon na kumfanya Roma kuona ni kweli Korea kaskazini ni mbali kuwaleta watu wake ndani ya Korea kusini.

“Pumbavu , kwanini hakuna watu wowote ambao mmewaweka Korea kusini?”

“Master Pluto nadhani unaelewa kwamba kuna mgogoro kati ya Korea kusini na Korea kaskazini , kama tutaweka watu wetu ndani ya Korea kusini hakuna faida yoyote kwani hakuna misheni ya kufanya , upande wa Korea kaskazini imekuwa rahisi kwani tunafanya na biashara ya siraha katika ukanda huo”Aliongea Roma na hakutaka hata kusikiliza zaidi ya kumpatia maelekezo ya kufatilia maswala ya North Buyeo halafu amtumie kwenye Email yake na kisha akatoweka katika eneo hilo.

Baada ya dakika chache aliweza kutokea katika mgahawa uliojengwa kitamaduni ambao familia ya Gong na ya Park walikuwa wakipata chakula cha usiku na baada ya kuona amerudi walimkaribisha kwa ukaribu na kumuonyesha sehemu kukaa chini kwani hakukuwa na viti.

Upande wa Park Jonghyun mara baada ya kumuona Roma alionyesha mshangao ulioambatana na mshituko na kumfanya Roma amwangalie na kisha kumuonyesha tabasamu la kejeli na kisha akaketi chini , ni kama alikuwa akimwambia kwamba anajua kile ambacho anafanya sirini.




“Mr Rom , unaonyesha haupo vizuri nadhani ni uchomvu wa wiki hii yote , lakini niseme asante sana kwa kumsaidia babu yangu kwani kama sio wewe hatujui nini kingetokea”

“Naamini maneno yako ni ya dhati bwana Jonghyun”aliongea Roma na kukaa katikati ya Edna na Clark,

Clark alikuwa ashabadili mavazi yake na yupo hapo kuungana na kila mmoja kusherehekea mafanikio yake ya kukamilisha upasuaji.

Chakula kiliendelea huku Roma akiwa bize kuongea na Clark ambaye muda wote alikuwa akimshukuru kwa kumsaidia kuokoa taswira yake kama daktari kwa kufanikisha kufikisha moyo ndani ya muda.

Upande wa Edna chakula hata hakikuwa kizuri kabisa kwake kutokana na namna ambavyo Clark anaongea kwa kujibebisha mbele ya mume wake na wivu ulimjaa mno.

Clark usiku huo huo alichukuwa nafasi ya kutoa taarifa anarudi Uingereza siku inayofuatia na jambo hilo lilimfanya Edna kupatwa na ahueni maana aliona kama akiendelea kubakia nchini hapo angeharibu furaha yake.

Baada ya chakula kila mmoja alirejea nyumbani na upande wa Roma na mke wake walirudi katika jumba la Park Juan.

Roma mara baada ya kuingia chumbani haraka alimwambia Edna ampatie Laptop kwanni kuna kitu anataka kufanya na Edna ambae alijinunisha njia nzima alimpatia bila ya kuongea neno.

Roma alielewa kinachomsumbua Edna ni wivu kutokana na namna alivyokuwa akiongea na Clark kwa kutaniana na kujibebisha.

Roma mara baada ya kuchukua laptop hio alifungua haraka haraka na kisha akaunganisha na mtandao kisha akafungua baadhi ya taarifa ambazo zimetumwa na Makedoni kwa njia ya barua pepe yake,alianza ku’scroll’ kwa kusoma kila kitu kwa umakini na alishangazwa mara baada ya kuona mawazo yake yalikuwa sahihi, North Buyeo halikuwa kundi la kawaida la sirii ndani ya Korea kusini.











SEHEMI YA 524.

Msingi wa jamii ya siri inayojiita North Buyeo ulianza zamani sana tokea kipindi cha utawala Goguryeo , wakati ambao Buyeo ilikuwa ipo upande wa Kaskazini mwa bara hilo la Asia.

Katika historia mara baada ya utawala wa Goguryeo kusimikwa rasmi, utawala wa kifalme wa Buyeo ulikufa na kubakia kama kundi la waumini tu ambao walikuwa na matamanio ya kurudisha nchi yao.

Sasa taarifa ambayo Roma alikuwa akisoma ni kwamba North Buyeo ni jamii ya watu ambao walikuwa wakibeba maono ya mababu na kutokana na mipango yao ndani ya taifa la Korea kusini na korea kaskazini walianza kujipenyeza katika nyanja zote za kitaifa.

Roma mara baada ya kusoma taarifa yote aliona ni mgumu sana kumaliza watu wote wanaohusika katika Buyeo licha ya kwamba ni tishio kwa usalama wa Yezi.

Muda huo wakati akiendeea kuwaza , Edna alikuwa ndio anatoka bafuni na kufanya eneo lote la chumba kuwa na harufu nzuri ya Shower gel huku akijifuta maji na taulo na Roma alimwangalia na kuishia kumeza mate kwani urembo wa Edna kwake ni kama unaongezeka kila saa anayomwangalia.

Edna baada ya kuona Roma yupo bize na tarakishi alisogea kuangalia ni kitu gani anasoma na alishangazwa na taarifa hio na kutaka Roma amwelezee kwanini anasoma hio taarifa.

“Norht Buyeo mbona ni kama mambo ya kihistoria kwannii unasoma?”Aliuliza

“Babe Edna , umejuaje ni mambo ya kihistoria?”

“Nakumbuka nishawahi kusoma kitabu kimoja ambacho kimeelezea hio historia , nadhamni unaelewa hobi yangu ya kusoma vitabu ”Aliongea na kumfanya Roma kweli aone inawezekana hata hivyo Edna kama CEO alikuwa akipenda sana kusoma ili kupanua ufahamu wake hususani katika maswala ya kibiashara.

Roma ilibidi mwelezee namna tukio lilivvyotokea masaa kadhaa yaliopita na hisia zake juu ya jamii hio kutishia usalama wa Yezi, Edna alishagaa na kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Ni malengo gani wanayo hio jamii? Ni kheri kama watakuwa adui yako lakini kama wanataka kumdhhuru Park Juan basi haitakuwa salama kwa Yezi kuendelea kuishi hapa”

“Ndio maana kabla hatujarudi Tanzania napaswa kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu hii jamii na kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba Park Jonghyun ni mwanachama pia”Aliongea Roma na Edna alikubaliana nae kwani hakuwa tayari kuona Yezi anapatwa na shida ili hali kwake alikuwa akimchukulia kama mdogo wake.

“Wife una akili nyingi sana , nilidhania huna uelewa wowote kuhusu maswala ya kiihistoria ya nchi za huku, umenizidi hata mimi ambaye leo hii ndio kwanza najua maswala ya Buyeo kuwa katika historia ya kikorea”

“Lakini ni dhahiri simfikii Clark , ana akili nyingi na ana kipaji kikubwa mno?”Aliongea Edna huku akionyesha kabisa bado alikuwa na kisirani..

“Edna mke wangu , kwanini mpaka sasa una wivu, Clark na mimi hakuna kinachoendelea zaidi ya kwamba alikuwa kama mdogo wangu ambaye nilimuona akikuwa mpaka kufikia utu uzima ndio maana anakua huru akiwa mbele yangu”

“Ulimuona?, kama ni hivyo wakati huo wewe ulikuwa na miaka mingapi na yeye alikuwa na mingapi?”

“Yeye alikuwa na miaka kama nane au tisa hivi na mimi nilikuwa na miaka kumi na nne kwenda kumi na tano”

“Kama ni hivyo kwanzia sasa nataka nikuwekeee mipaka , kumuona akikua haimaanishi kwamba ndio umfanye awe mpenzi wako wa utotoni”Aliongea kikauzu na kisha alichukua rimoti na kuwasha Tv.

Na Roma alishindwa kujielezea zaidi maana Edna maneno yake ni kama hayaamini kabisa kila anapomuambia hakuna mahusiano.

Hofu ya Edna ilikuwa ni kwamba Clark ukiachana na kwamba alikuwa mrembo karibia kumfikia yeye , lakini pia alikuwa na akili nyingi na huenda ana msaada mkubwa kwa Roma kuliko yeye mwenyewe hivyo hofu yake ni kupinduliwa .

Wanawake wengine hakuwa na hofu nao kutokana na kwamba walikuwa wa kawaida sana na siku zote wapo chini yake na anaweza kuwamudu lakini kwa Clark ilikuwa tofauti.

Mtu mwingine ambaye alikuwa akiogopa Roma kuanzisha nae mahusiano ni Sophia.

Sophia anaweza asiwe na kitu kikubwa kama yeye , lakini likija swala la uzuri walikuwa wakikaribiana sana na yeye na Edna alikuwa amenuia kwenye moyo wake hatokaa aone mahusiano kati ya Roma na Sophia yanatokea.

Muda huo huo wakati Roma na yeye akijiandaa kwenda kuoga , walisikia mtu akigonga mlangoni na kumfanya Edna amwangalie Roma kwani haikuwa kawaida kwa kugongewa muda huo.

Roma alisogelea mlango na kufungua na aliweza kukutana na mwanaume ambaye amevalia mavazi ya suti yenye nembo maalumu kumtambulisha ni mfanyakazi wa hapo ndani.

“Mr Roma ,Mrs Edna kila kitu kipo sawa?”Aliuliza kwa lugha Kikorea.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma na kumfanya yule bwana kushangaa.

“Mimi ni mlinzi katika hii nyumba na dakika chache zilizopita niliweza kusikia purukushani ikitokea upande huu ndio maana nimewagongea kuona kama mpo sawa”Aliongea

“Kama ni hivo kwanini umeshikilia kisu mkononi na kukificha au upo hapa kwa ajili ya kutuua?”Aliuliza Roma na ku,fanya yule bwana kushangazwa na jambo hilo , kwani hakujua Roma ameonaje kisu aina ya daga alichoshikilia kwani aliificha vyema kwa kukibana na ukuta.

Lakini hata hivyo hakuwa na muda wa kupoteza baada ya kuona mpango wake ushagundulika hivyo alitoa mkono kwa haraka na kuipeleka ile Daga usawa wa kifua cha Roma , lakini Roma kutokana na wepesi wake aliwahi kushikilia mkono wake ulioshikilia kisu na kuupindisha na kumfanya yule bwana kutoa ukulele na kukidondosha chini.

Edna ambaye macho yake yalikuwa kwenye runinga alishangazwa na purukushani hizo na kusimama kwa wasiwasi

“Wewe ni nani? North Buyeo wamekutuma?”aliuliza Roma.

Yule mwanaume alionekana kuchezesha meno yake palepale mara baada ya kuona amekamatika , lakini Roma alitegemea hilo hivyo alimuwahi kwa kumpiga shingoni na kumfanya palepale kupoteza fahamu.

Dakika hio hio Roma aliweza kusikia purukushani zingine zikisikika kutoka juu na mpaka hapo alijua wapo wengi zaidi.

“Edna kuwa makini , ngoja nikamwagalie Yezi inaonekana wapo wengi”Aliongea Roma na kwa haraka alitoka hapo akihofia Yezi anaweza kuwa katika hatari.

Muda uleule aliweza kutokea mbele ya chumba cha Yezi sehemu ambayo ndio aliweza kusikia sauti.

Muda huo Roma aliweza kushuhudia kijakazi wa kike akipigana na kijakazi mwingine wa nyumba hio, alikuwa ni kijakazi afahamikae kwa jina la Eujung msaidizi wake Yezi.

Eujung alionekana kuwa vizuri kwenye mapigano na Roma palepale aliweza kugundua huenda alikuwa na mafunzo ya juu ya Taekweond kwani hata mpinzani wake hakuwa haba lakini alikuwa akionyesha kumdhibiti vizuri.

Eujung hakuwa mzembe baada ya kukwepa mapigo mawili , alipiga sarakasi mzunguzo ambayo ilimpiga yule adui mtama na akadondoka chini na kabla hajamka , Eujeong tayari amekwisha kupiga teke lingine la shingo na kumlegeza kabisa na kumuweka chini ya ulinzi.

Roma alishangazwa na jambo hilo kwani hakutegemea kuona msichana wa kikorea aliekuwa mpole na kijakazi wa familia hio alikuwa na uwezo mkubwa kama huo , aliona huenda yote hio ni mipango ya Park juan babu yake Yezi kuhakikisha mjukuu wake anakuwa chini ya ulinzi mkali.

Eunjung alikosa umakini na adui yake na ghafla tu yule Ninja aliamka kwa mara nyingine na kutaka kumchoma na kisu tumboni na Roma palepele kwa haraka sana alimkaribia kijini na kumzuia kwa kumpiga utosini na palepale alilegea na kudondoka chini na ukawa mwisho wa uhai wake.

“Asante sana Mr Roma kwa msaada wako”Aliongea Eunjung na muda uleule Yezi aliekuwa akitetemeka aliweza kufungua mlango.

“Oh asante umekuja , naogopa mimi”Aliongea Yezi kwa hofu kubwa.

“Upo na Eujung hapa kwanini unapatwa na hofu wakati yupo vizuri kwenye kukulinda?”

“Sikujua hata kama anajua kupigana , babu nilimwambia sitaki mabodigadi na akinniahidi hatoniwekea , lakini inaonekana alinidanganya”

“Usikarisike Miss , Master kafanya yote kwa ajili yako”

“Sio kama nakasirika, asante kwa kuweza kuyaokoa maisha yangu”Aliongea na Eunjung alitingisha kichwa kukubali shukrani yake.

“Kama hapa kumefanyika mashambulizi vipi kuhusu hospitalini?”Aliuliza Eunjung kwa wasiwasi.

Eunjung kuongea hivyo hata Roma aliona uwezekano wa kushambuliwa kwa wakati mmoja hapo nyumbani na hospitalini ni mkubwa , lakini hata hivyo asingeweza kuondoka na kuelekea huko kwani bado usalama wa Yezi na Edna ulikuwa juu yake.

Edna alikuwa katika levo ya mwanzoni katika nusu mzunguko hivyo aliona hata kama anaweza kuweza kujilinda lakini hana uzoefu na kama atakutana na adui ambaye ana siraha kama bastora basi moja kwa moja angemdhuru.

Muda huo huo Edna alitoka na kuja mahali walipo huku akiwa ameshikilia simu ya Roma.

“Hubby simu yako inaita?”Aliongea na Roma alimsogelea na kuichukua na kisha akpokea palepale.

“Mr Roma nimeshangazwa sana kuona mpaka sasa bado upo hai?”Sauti ilisikika kwa lugha ya kikotea.

“Wewe ni nani au ndio nyie North Buyeo?”

“Mhh.. umetisha sana Mr Roma , mbali kabisa na matarajio yangu”

“Unataka nini kutoka kwangu?”

“Labda hujagundua kitu bado lakini kabla hamjarudi hapo nyumbani tayari mpango ulikuwa ushaandaliwa na hospitalini pia kwa wakati mmoja , kwa ajili yako Roma tutahakikisha unaendelea kuburudika kile tulichokupangia”Aliongea mwanaume huyo kwa sauti yake ya besi huku akicheka kicheko cha dharau.

“Nadhani mpango wako ni kulipua hii nyumba si ndio?”

“Upo sahihi , nyumba yote tushatega mabomu ya ukubwa wa C4 yanayotosha kutengeneza wingu kubwa la mlipuko na kuharibu jumba lote”

“Pumbavu zenu nyie wakorea naona mnaona mambo yanaweza kufanikiwa kirahisi hivyo , mnafikiri mnaigiza muvi sio? Hamchoshwi na huo upuuzi wenu?””

“Kama kitu hakivunjiki kuna haja gani ya kukirekebisha, Mr Roma kama hutaki kuona hio nyumba ikilipuka na mkeo pamoja na mdogo wenu Yezi kuangamia basi hakikisha unafanya kama tunavyokuelekeza”ilisikika sauti.

Roma hakuwa na wasiwasi hata hivyo na vitisho vyao kwani alikuwa na uhakika wa kuwakoa Edna na Yezi kwa wakati , lakini bado jambo moja ambalo lilimpa mashaka ni upande wa hospitalini lazima na penyewe kuna mtego ambao umetegwa.

“Mnataka nifanye nini?”

“Ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kutoka mpaka nje na utaona gari aina ya BMW sedani nyeusi , ingia kwenye hio gari na endesha mpaka hoteli ya Myeondong kuna watu watakupokea hapo”Aliongea mwanaume huyo upande wa pili na Roma alikubali.

“Nini kinaendelea, ni watu kutoka North Buyeo?”aliuliza Edna na kumfanya Roma kucheka na kisha alimsogelea sikioni na kumnong’oneza.

“Utafanya kazi?”Aliuliza Edna huku akikunja ndita.

“Hio itategemeana na wewe CEO Edna , una uwezo mkubwa wa kuigiza hata wa kunidanganya mimi kwanini tusifanikiwe”Aliongea Roma ilionyesha kuna mpango ambao walikuwa wakipanga na Edna ni sehemu ya kuukamilisha.

“Kuwa makini sasa , tutaendelea kufuata mpango wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma amshike Edna mashavu kama mtoto na kisha alitoka hilo eneo na kuanza kushuka kwa ngazi kuelekea chini.

“Anaenda wapi?”aliuliza Yezi.

“Tumepewa maagizo kutoka kwa watu waliotuma wauaji hapa na wanataka Roma afuate maagizo yao la sivyo hii nyumba na jengo la hispitali alilolazwa babu yako litalipuka kwani kumetegewa mabomu”

“Kwanini wanataka kufanya kitu kama hicho?”Alilalamika Yezi na muda huo huo mabodigadi waliingia ndani ya nyumba hio na kuizingira huku wakimpa ulinzi Yezi.

Kwasababu walikuwa aneo la juu katika Lounge waliweza kumuona Roma akitokea nje ya geti na kuingia kwenye gari ambayo imegeegeshwa na baada ya kuiwasha kwa kutoa mwanga wa taa palepale ulitokea mlipuko wa aina yake.

“BOOM!!”

“Mama..!! ulikuwa ni mtego”Aliongea Eujung kwa kikorea huku akishindwa kuzuia mshituko wake mara baada ya kuona gari lililipukaRoma akiwa ndani na kuishia kushika mdomo

“Uncle Roma…!!Yezi alijikuta akitoa ukulele akiwa kama mtu ambaye haamini macho yake.

Muda huo huo magari yaliokuwa yapo karibu na hayo maeneo yalianza kulia alarm baada ya mlipuko huo kutokea,

Haikuchukua muda mrefu mara baada ya mlipuko gari nyingine nyeusi kampuni ya Honda ilifika katika hilo eneo na walitoka wanaume waliovalia suti na kuanza kuchunguza gari hio inayowaka moto.

Edna na yeye aliekuwa ameona tukio hilo aliishia kutoa machozi huku akiwa amesimama kama sanamu.
 
SEHEMU YA 525.

Yezi ndio aliekuwa wa kwanza kukurupuka kutoka juu na kukimbia kuelekea nje na walinzi walichelewa kumzuia lakini wakafannikiwa kumkamara akiwa tayari yupo getini na kumzingira.

Ziliongezeka gari nyingne tatu nyeusi aina ya Range na wakatoka wanaume ambao wamevalia suti huku mkononi wakiwa wameshikilia siraha na wakasogelea upande ambao wapo walinzi wa familia ya Park.

Edna na Eunjung na wao waliweza kufika katika eneo hilo na mpaka hapo waliweza kuona hatari inayotaka kutokea kwani maadui walikuwa washaingia ndani ya ukuta tayari.

Walikuwa ni kama kundi la Mafia Gang kutokana na wingi wao na namna walivyovalia na usiriasi uliokuwa kwenye macho yao.

Kiongozi wao,bwana mmoja mwembamba mwenye nywele nyeupe alievalia koti la Leather palepale aliwapa ishara ya kushambulia na ilikuwa ni kama wanaendeshwa kwani waliwasogelea walinzi na kuanza kushambulia kwa spidi , walipiga mateke virungu na wengine walikuwa wameshikilia visu.

Mpala dakika tano zinapita walibakia walinzi wanne tu ambao hawakuwa wamepata majeraha.

“Nyie ni wakina nani?”Aliuliza Eujung akimwangalia mwanaume ambaye nywele zake aliziweka dawa na kuwa za rangi nyeupe.

“Huna haja ya kufahamu sisi ni nani , nyoosheni mikono juu na mwangalie ukuta , tupo hapa kumchukua Yezi pekee”Aliongea na kumfanya Yezi kuwaangalia huku akiwa na machozi mengi yaliosababishwa na majonzi ya kuona Roma kalipukiwa na bomu.

“Huwezi kumchukua ikiwa nipo hai, wekeni umakini wenu wote kwa ulinzi wa Yezi na msiruhusu wamchukue”Aliongea Eujung kijasiri akiwapa maelekezo wale walinzi waliobaki lakini hawakufanya kama alivyoongea zaidi ya kuangaliana kwa sekunde kadhaa na kisha wakanyoosha mikono juu kujisalimisha na wakashikilia ukuta.

“Nyie wapuuzi , kwahio hivi ndio mnavyomlipa Mzee kwa mema yote aliowafanyia?”Aliongea Eujung kwa hasira huku aking’ata meno, mpaka hapo aliona hakuwa na msaada tena na watu waliokuwa mbele yake ni wengi kuweza kupambana nao wote.

Upande wa Yezi licha ya kwamba sasa walinzi wake washamgeuka na kujisalimisha yeye alisimama vilevile bila hofu akiwa kama sanamu, alikuwa kama mtu ambaye amepoteza tumaini la kuendelea kuishi.

Kitendo kile kilimfanya Edna ambaye alikuwa pembeni yake kushangazwa na kujiuliza je yote hayo ni kwasababu ya kushuhudia Roma akilipuka ndani ya gari, je Roma ni mtu muhimu kwake mpaka kuwa katika hali hio.

“Wewe mwanamke ni kichefu chefu , sheria yetu ni kutotaka kuumiza watu wengi zaidi lakini kwasababu unataka kutuzuia umeyataka mwenyewe , mshambulienni kwa risasi tuondoke hapa”aliongea na palepale wanaume wawili ambao walikuwa na bastora walisogea mbele na kuanza kuzirusha kuelekea sehemu aliposimama Eujung.

Eujung hakutaka kufa kizembe , alipiga sarakasi ya haraka kabla hawajavuta triga na aliweza kuwawahi wawili waliokaribu yake na kuwapiga mateke ya kifuani na kudondoka chini.

Kitendo kile kiliwafanya wale wengine kurudi nyuma na kujiunga kwa kumlenga kwa risasi , milio ya bunduki haikuwa mikubwa kutokana na siraha zao kufungwa viwambo vya kuzuia sauti.,

Sasa walichokuja kugundua ni kwamba hakuna risasi yoyote ambayo imeweza kumpata Eujung na yule bwana mwenye nywele nyeupe alishangazwa na jambo hilo lakini sio yeye tu ambaye alikuwa akishangaa hata Eujung hakuamini kama ni kwa uwezo wake ndio amefanikisha kuzikwepa risasi zote na isitokee hata moja kumpata, lakini hakutaka kuupa mshangao wake nafasi , watu waliokuwa mbele yake walikuwa wakijiamini kutokana na kwamba walikuwa na siraha za moto , lakini kwasababu siraha zao hakuna hata moja iliomdhuru aliona kabisa anaweza kuwamudu kuwadhibiti kwani walikuwa dhaifu kwenye mapigano ya bila siraha.

Yule kiongozi hakutaka kuamini kama msichana kijakazi ndio ambaye anawamaliza watu wake , ilikuwa ni ngumu kuamini na alianza kuingiwa na hofu na kuanza kulisogelea geti ili atoke , lakini palepale alijikuta akisimama huku akiingiwa na ubaridi wa uti wa mgongo.

“Nimerudi”Aliongea Roma na palepale alimbutua yule mwanaume kiongozi teke ambalo lilimpeleka chini , lakini licha ya kupigwa bado alikuwa akimwangalia Roma kama mzimu uliofufuka.

“Mzimu..!!!”Alipiga kelele huku akisogea kurudi nyuma.

Upande wa Yezi mara baada ya kumuona Roma alishindwa kujiuzuia na palepale alimkimbilia na kumkumbuatia na hakuishia hapo tu alimpiga mabusu ya shavuni akijisahau Edna yuko mbele yake.

Roma kitendo kile kilimfanya amwangalie Edna kwa wasiwasi , maana matendo ya Yezi ni kama vile ni ya kimapenzi.

“Wife amefanya mwenyewe, kwa kunishitukiza”Roma alijishuku.

Edna yeye alikuwa akijua Roma hajafa na wasiwasi aliokuwa akiuonyesha ni kuweka maigizo tu na hicho ndio ambacho aliambiwa na Roma afanye mara baada ya kunong’onezwa, hivyo kumuona Roma amerudi akiwa hajapata madhara alipata ahueni lakini kitendo cha Yezi kumbusu mume wake aliingiwa na hisia za kuchanganyikiwa.

“Sister Sijamaanisna vibaya , ni kwamba nimeshindwa kuzuia furaha yangu”Aliongea Yezi kwa aibu huku akijitoa kwa Roma na kusogea pembeni.

“Haina haja ya kuwa na aibu unaweza kumbusu utakavyo kwanza ananuka”

“Hey wife unanisemaje vibaya ilihali tunalala wote kitanda kimoja”

“Unanuka moshi ndio , unaonaje kwanza ukamalizana na hao watu maana mpaka sasa hatujui kama hospitalini kwenyewe kupo salama”

“Sidhani kama kuna chochote ambacho kimetokea hospitalini na siamini kama ni kweli wametega mabomu kwani kufanya hivyo sio kazi nyepesi ukilinganisha na ulinzi wa hospitali yenyewe na isitoshe wapo hapa kumchukua Yezi hivyo inamaanisha kwsamba babu yake bado yupo hai”Aliongea Roma

“Kwahio tunafanya nini baada ya hapa?”

“Kilichobaki ni mimi kutafuta bosi wao aliewaagiza kuondoa mzizi kabisa, wakati anatupigia si alisemaa niende Myeondong hoteli naamini hio ndio sehemu nzuri ya kuanzia”aliongea Roma na Edna alielelewa.

“Eujung utafanya maamuzi namna ya kuwafanyia hawa waliobaki hapa ndani, usiwaue kwani wanaweza kusaidia katika uchunguzi”Aliongea Roma na Eujung alitingisha kichwa kukubali.

“Asante sana Mr Roma kwa mara nyingine”Alishukuru Eujung alikuwa akijua kabisa kuna kitu ambacho Roma alifanya wakati akivurumishiwa risasi na Roma alitabasamu na kisha akamuaga Edna na kuondoka katika hilo eneo.

Dakika chache mbele Roma alikuja kutua katika hoteli ya Myeondong , ni hoteli ambayo haikuwa mbali kwani ilikuwa pia ndani ya wilaya ya Gangnam hivyo haikumsumbua Roma kuipata.,

Roma mara baada ya kutua nje ya bustani ya hoteli hii katika eneo la bwawa la kuogelea alianza kuchunguza jengo lote na kuamini kabisa kazi itakuwa ngumu kujua watu wote ambao ni wanachama wa North Buyeo kwasababu hoteli ilikuwa kubwa na ilikuwa na wageni wengine .

Jambo moja tu aliamini linaweza kurahisisha kazi yake ni kuingia kwenye Casino ndani ya hoteli hio.

Ndani ya hoteli hio upande wa vyumba vya chini kabisa ya ardhi ndio Casino kubwa ya kisasa ililikuwepo na ajabu ni kwamba licha ya giza kubwa nje lakini eneo hilo lilikuwa limechangamka sana na watu walikuwa bize wakicheza kamari.

Sera za kikorea zinaruhusu Kamari kuchezwa katika eneo la makasino tu na sio nje ya hapo kwani ni uvunjaji wa sheria huenda ndio maana kulikuwa na watu wengi sana.

Ulimwengu ambao pesa ni mfalme hakuna ambaye anasinsinzia katika hilo eneo na kwao ni kama ndio kwanza kumekucha , kila meza kulikuwa na watu wenye usiriasi wa uso huku macho yao yote yakiwa kwa wanawake warembo ambao ndio dealers(wachezesha kamari).

Ni eneo ambalo lilikuwa na mwanga hafifu , eneo la kisasa ambalo mziki wake ulisikika vizuri katika eneo zima na kutosababisha makelele zaidi ya kutoa burudani , wanawake waliovalia vinguo vifupi walipita huku na huko kufanya huduma, kuna waliokuwa wakitoa huduma ya vinywaji lakini kuna wale ambao walikuwa wakitoa huduma ya miili yao ilimradi kufurahisha wateja , kiasi kwamba hata kama mtu akipoteza kibunda katika kubahatisha asiwe mnyonge sana.

Upande wa kulia katikati ndio sehemu ambay kuna chuba maalumu ambacho kukaa kiongozi wa Kasino ambaye muda wote huangalia kila meza kwa kutumia Kamera zilizofungwa.

Ilikuwa ni kawaida sana kwa viongozi wa Kasino kujua kila mteja wao alieibuka mshindi na yule ambaye aliepoteza hivyo walijua kabisa kila mteja anaeingia na ambaye anatoka na yote hayo yalifanikishwa na teknolojia ya Camera za kisasa.

Sasa katika chumba hicho ambacho kilikuwa na ulinzi mkubwa na ambacho wateja wakawaida hawakupaswa kuingia , alikuwa ameketi bwana mmoja wa makamo kwenye masofa ya kisasa ya Leather akiwa ameshikilia glasi yenye kinywaji cha rangi ya dhahabu ndani yake .

Hakuwa peke yake bali kulikuwepo na wanaume wengine ambao walikuwa pembeni yake wanaofanana kimuonekano na macho yao yote walikuwa wameyaelekeza kwenye meza wakiwa wanacheza karata mchezo maarufu wa Poker.

Kila mmoja ambaye alikuwa ndani ya hiko chumba alikuwa ni mwenye kuashiria kumiliki ukwasi mkubwa , kwani kila kitu chao kilionekana cha thamani kubwa.

“Mr Go kuna simu yako hapa?”Waiter alimletea karibu bwana huyu wa makamo na kumkabidhi simu ambayo inaita.

“Nani anaingilia burudani yangu ya mchezo”Aliongea kwa Kikorea huku akionyesha amechukizwa na simu hio.

“Ni Park Jonghyun”Baada ya kijibiwa hivyo alighairisha kile ambacho anakifanya na kisha akachukua ile simu.

“Huyu mpuuzi mpaka sasa bado ananiamini”Aliongea kabla ya kupokea ile simu huku akitoa tabasamu ambalo liliashiria kutokujali na kujali kwa wakati mmoja.

“Msema sana , bwana Park mambo yanaendaje?”

“Unaniuliza mimi tena , Go Chak uliniambia kabisa mpango wako hakuna ambaye anaweza kuukwepa , vijana wako ni kipi wamefanya?”Sauti ya kufoka na kulalamika kwa wakati mmoja ilisikika upande wa pili na kumfanya bwana aliefahamika kwa jina la Go Chak kukaa vizuri kwenye Sofa.

“Unaongea nini? Vijana wangu ni kipi kimewakuta?”

“Wewe mpumbavu m unashindwaje kuelewa hali uliokuwa nayo , ngoja nikuambie watu wako wote wameweza kudhibitiwa na mpaka sasa umeshindwa kuweza kupata taarifa kutokana na kwamba hakuna aliesalia

Go Chak wewe mpuuzi , narudia watu wako wameweza kudhibitiwa na kijakazi wa familia na sasa wamepelekwa kituo cha polisi na muda sio mrefu naamini watataja makao makuu yako wapi , yaani sio tu umeshindwa kumpata Yezi lakini umeshindwa pia kumdhibiti yule nzi Roma Ramoni, unaniweka katika hatari”Aliongea Park Jonghyun alionekana mpaka muda huo amechafukwa sana.

“Inawezekana vipi?, nimetuma wanajeshi wastaafu wa kitengo cha operesheni maalumu kumaliza kazi , unataka kuniambia watu wote hao wamedhibitiwa?”

“Unauliza majibu sio maswali, nilikuambia usimpuuzie na Kim Jip haya umeshindwa hata kumuua yule mzee na sasa unaniambia hujui kinachoendelea , tokea uwe Chief wa Nothr Buyeo Kikanda huna chochote ambacho umefanya kikatimia , kwanzia sasa mimi na wewe hatukuwahi kuwa na ukaribu wowote”Aliongea na Park jonghyun alipigiza simu ukutani na ikajikata yenyewe

Go Chak na yeye mara baada ya kupewa taarifa hio alijikuta akibeba glasi iliokuwa kwenye meza na kuitupia kwenye ukuta

“Ondokeni hapa mbele yangu”Aliongea kwa kufoka na wale wanaume ambao alikuwa nao walisimama wote na kuondoka kwani walijua kabisa Go Chak akikasirika ni mtu mwingine kabisa.

“Wafanye kila mmoja kuondoka hapa ndani ya Casino , sio mahali salama tena na baada ya kila mmoja kuondoka kusanya nyaraka zote na zifiche , hakikisha huachi ushahidi wa aina yoyote”Aliongea Go Chak akimpa maelekezo Meneja.

“Lakini Mr Go hakuna muda wa kutosha kufanya hivyo”

“Unafikiri ufanisi wa polisi ni kiasi gani ?, kama nitawapa muda wa kufika hapa ni lisaa limoja kamili , hata hivyo tuna watu wetu ndani ya polisi hivyo tunaweza kuwaamini kuwachelewesha kufika hapa , ili mradi watu wetu wakubwa serikalini hakuna ushahidi unao wafunga tunaweza kuepuka lawama zote , fanya kama nilivyokuambia”

“Yes sir”

Dakika chache tu baadhi ya watu waliokuwa wakichezesha kamari palepale waligeuka na kuwa kama wanajeshi na kuanza kuwaondoa watu kutoka nje ya eneo hilo na wale ambao walikuwa wakilalamika kupewa Chip zao waliishia kupigwa mateke na ngumi na kukimbia.

Upande wa Go Chak katika ofisi yake alifungua boksi lake la usalama la kuhifadhia vitu na kisha akasukuma maburungutu yote ya hela kutoka nje na kisha akayakweka kwenye begi na hakuishia hapo tu alitoa na baadhi ya vito vya thamani na kuvikusanya pia.

Chini ya ulinzi wa vijana wake alitoka alianza safari ya kutoka Casino hio kuelekea nje na muda huo karibia watu wote walikuwa washatoka.

Walinzi waliotangulia mbele ya Go Chak kabla hawajatokea kwenye mlango walirudishwa ndani kwa kurushwa na kutua chini kama vile ni kiroba cha mchele.

Go Chak palepale aliinua kichwa chake kuangalia mbele na hapo ndipo alipojikuta akipatwa na ubaridi mara baada ya kumuona Roma.

“Roma Ramoni”Aliongea kwa mshituko.

“Hahaha…. Kuliita jina langu kumenirahisishia kukufahamu wewe ndio kiongozi”Aliongea Roma kwa Kikorea na kumfanya Go Chak kung’ata meno yake kwa hasira na palepale aliwapa ishara vijana wake walioshikilia siraha za moto kumshambulia Roma.

“BANG! BANG…!!”.

Milio ya risasi ililirindima eneo lote na kufanya lifuke moshi, hisia zao ziliwaambia kabisa mtu aliekuwa mbele yao ni hatari hivyo hakupaswa kupigwa na risasi moja ndio maana walishambulia kwa pamoja mfululizo.

Lakini sasa ile wanamaliza risasi zao na kusimamisha mashambulizi walishangaa mbele yao hakuna mtu, Go Chak kabla hata hajaelewa Roma yuko wapi alishangaa akivutwa kwa nyuma na kushikwa shingo na Roma na kuanzwa kukabwa.

“Niambie nani kaagiza mshambulie familia ya Park?”Aliuliza Roma lakini Go Chak aliishia kufurukuta huku akionyesha kabisa hayupo tayari kuongea chochote.

“Nitajie kiongozi wako?”Aliuliza Roma kwa mara ya pili.

Wale walinzi walishidnwa kufanya chochote kutokana na kwamba wenyewe walikuwa kwenye mshituko wakijiuliza imekuwaje mtu waliekuwa wakimshambulia mbele yao ghafla tu yupo nyuma yao.

Roma hakuwa na muda wa kuchelewesha na haraka haraka aliona angechelewa kumhoji Go Chak kwani hakuonyesha nia ya kuongea chochote na hakutaka kukutwa hapo na polisi hivyo alimvunja shingo palepale.

“Kamuua bosi wetu , tumshambulie”Aliongea mmoja wapo wa wale mabodigadi na kuanza kumshambulia Roma , lakini ilimchukua dakika tano tu kuwavunja wote shingo, kwasababu walikuwa wengi hakutaka kuwaacha hapo na kukutwa na polisi hivyo aliwayeyusha na kuwageuza majivu na mtu pekee ambaye hakutaka kumgusa ili kubakia kama ushahidi ni Go Chak.

Roma mara baada ya kukamilisha kazi yake alichukua mkoba alioshikilia Go Chak pamoja na wa meneja na kuangalia ndani na alijikuta akikutana na nyaraka mbalimbali kwenye mkoba wa meneja na alizotoa na kuanza kuzisoma , lakini kati ya nyaraka zote moja wapo ni nyaraka iliosainiwa na Park Jonghyun

Ni nyaraka ambao ilikuwa kama mkataba ambao umesainiwa na Park Jonghyun kwa niaba ya familia yote ambao ulikuwa ukiwapa haki ya uendeshaji wa baadhi ya mali za familia hio , ilikuwa ni rahisi kusema Park jonghyun ameuza sehemu ya mali za kampuni bila ya familia kufahamu.

Roma baada ya kupata ushahidi huo alitabasamu , hivyo alichukua begi lenye nyaraka huku akichana na lile lenye pesa, alijiambia kazi yake mpaka hapo imeisha na ushahidi aliokuwa akitafuta ameupata , hivyo moja kwa moja alipanga kwenda kumuonyesha babu yake Yezi ili kuchukua hatua zaidi juu ya Park Jonghyun.

Roma mara baada ya kusikia purukushani za watu kuingia katika hilo eneo palepale alipotea.

********

Upande mwingine katika makazi ya Park Jonghyun , bwana huyo alishindwa kabisa kukaa chini kwani alikuwa akizunguka huku na huko, kila saa akijifuta jasho , alionyesha kuwa na wasiwasi mno na ilikuwa ni kama kuna taarifa mbaya ambayo anaomba isimfikie.

Muda huo huo msaidzi wake aliingia katika hilo eneo huku akiwa ameshikilia simu.

“Boss tumeweza kupata taarifa kutoka hoteli ya Myeondong, inasemekana polisi baada ya kufika hakukuwa na ushahidi wowote zaidi ya kuonyesha kulikwa na mapigano makali ya kurushiana risasi na Go Chak amekutwa amefariki”Aliongea msaidiizi.

“Nini , amefariki?Wengine wote wako wapi , hususani meneja wake?”Aliuliza kwa kufoka.

“Huneda wakawa wamekufa Sir , kwani magari yapo parking na hawajaonekana kama walitoka”

“Sijali kama wamekufa , lakini vipi kuhusu nyaraka ya siri ya makubaliano yangu na North Buyeo , je wamezipata na zenyewe?”

‘”Mtu wetu ndani ya polisi amesema hakuna nyaraka za aina hio zimepatikana zaidi ya mkoba pekee ambao una pesa, kwa maana hio ni afadhali kwetu kwani uwezekano wa Go Chak kuzificha kabla ya kufa ni mkubwa”

“Sidhani kama inawezekana , hakuna namna Go Chak akaziweza sehemu nyingine tofauti na ndani ya Casino, vipi kuhusu kamera za ulinzi?”

“Hilo ndio tatizo bosi , Kamera za ulinzi zimeonyesha mtu alieingia ndani ya Casino ndani ya muda ni Roma Ramoni”Aliongea msaidizi na kumfanyaPark Jonghyun kupeleka mikono yake kichwani huku akitoa macho.

“Hahaha.. Roma! oh Roma Ramoni !!, ni yeye tena, si alikuwa nyumbani kwanini akawa ndani ya hio hoteli?”

“Ni ngumu kujua kwasasa bosi na tumechelewa , Bosi kama Roma ndio ambaye amezichukua nyaraka na akampelekea Mzee , itakuwa ndio..”

“Itakuwa ndio mwisho wetu , si ndio?”Aliuliza na kumfanya msaidizi wake kutingisha kichwa kwa huzuni kuonyesha kwamba mpaka hapo hawatakuwa na haki tena ya kusogelea kampuni ya Starmoon.

Tena itakuwa ni bahati kwao kama watafanikiwa kutoroka kabla ya kujikuta gerezni na sio hivyo tu hata kama wanaweza kupelekwa gerezani hakuna uhakika kama wanaweza kuendelea kuishi kwani North Buyeo wasingeweza kuwaacha hai na kutoa siri zao.







SEHEMU YA 526.

Baada ya Park Jonghyun kutafakari kidogo , alionekana kupata wazo na kisha akamgeukia msaidizi wake.

“Nenda kwenye ofisi yangu haraka sana , na fungua safebox kwa kutumia nywira za mwaka niliozaliwa na kuunganisha na mwaka wa kampuni ilipoanzishwa na kuna kiasi cha pesa ambacho kinaweza kukutosha wewe na wengine”Aliongea

“Bosi unamaanisha unataka ku..”

“Huu ndio mwisho wetu, mipango yetu yote mmoja baada ya mwingine imefeli , ninachoweza kusema yule mzee ana bahati sana kwa Roma kuweza kuwahi kuja Korea mapema …,Kwa muda mrefu umekuwa ukinifuaa na kutii maagizo yangu , nitakupa kile ambacho unastahili , lakini kwa namna ambavyo utaishi wewe na wengine hilo litakuwa juu yenu”

“Boss kwanini tusiende hadi hospitalini n kuomba msamaha , wewe ni mjukuu wake sidhani kama anaweza kukutupa kabisa bila ya msamaha”

“Unafikiri anaweza kunifanya nini mimi ambaye sina uhusiano wowote wa damu na familia yake? , kwenye macho yake Yezi peke yake ndio ambaye anaweza kuendeleza legacy ya familia , kama nitaenda sasa hivi itakuwa kama misheni ya kujitoa muhanga”

“Kama ni hivyo bosi kwanini usiungane na sisi , namfahamu mtu mmoja ambaye anaingiza vitu nchini kimagendo, anaweza kutusaidia kutorokea nje ya nchi, tunaweza kutafuta kisiwa chochote na kujificha huko , huenda siku moja tukarudi kwenye utukufu wetu”

“Unajidanganya , hivi unajua kwanini yule mzee amewezaje kutawala bara la Asia lote , haha,, biashara za magendo huko kote kuna mizizi yake na nitakamatika kirahisi , kwasasa jiokoe wewe mwenyewe na mimi nitajisaidia mwenyewe, hivyo nenda kabla mambo hayajanikuta kuna kitu kimoja lazima nikifanye”Aliongea na palepale alichukua funguo za gari.

Upande wa msadizi wake , alianza kusita sita lakini palepale alijipa ujasiri na kisha akakimbilai kwenye ngazi ili kuelekea juu kwenye ofisi ya Park jonghyun , lakini kabla hata hajapiga hatua nne kupanda , mlio wa risasi ulisikika palepale na yule msadizi alidondoka chini huku damu zikisambaa na alianza kufurukuta huku macho yake yakionyesha kama vile ni mtu ambaye anakufa kifo ambacho hakutarajia.

Park Jonghyun alieshikilia risasi alimwangalia namna msaidizi wake anavokufa na kisha alitoa tabasamu la kejeli.

“Sikutarajia utakuwa mtiifu namna hii , kama nazama na nyie mnapaswa kuzama “Aliongea huku akionyesha kutojutia kwa kile ambacho amefanya.

*******

Roma kwa haraka haraka alikadiria mpaka muda huo Park Juan atakuwa ameamka na ndio maana hakutaka kwanza kurudi kwa mke wake mpaka kuonana nae.

Roma alitaka kukamilisha kila kitu mapema kabla ya kurudi Tanzania na isitoshe siku zilikuwa zinaenda kwa kasi na nyumbani walimuacha Lanlan ambaye hakupaswa kuendelea kukaa bila ya kuwa na ukaribu wa mama yake na hata kwa Edna mwenyewe alishaona kabisa ashamkumbuka mtoto wake na alikubali kuendelea kubakia hapo nchini kwasababbu ya swala la Yezi tu na kama si vinginevyo heunda angekuwa Tanzania tayari.

Roma akiwa na mkoba wake aliweza kuruhusiwa kuingia katika wodi aliolazwa Park Juan na ilikuwa ni kama alivyotarajia kwani Park Juan aikuwa ashatoka kwenye usingizi wa Ganzi na muda huo hata dripu zishaondolewa na aliwekewa tu nasal prongs ambazo zilimsaidia kupata hawa safi.

Kim Jip kwa namna ambavyo alionekana ni kama vile dakika moja hakuwa akipigana kwa kudhibiti watu ambao walitaka kumdhuru bosi wake.

Mara baada ya Roma kufika hakuongea neno zaidi ya kumtingishia kichwa tu kumuonyesha ishara ya kumkaribisha.

Roma mara baada ya kusalimiana na Park Juan ambaye alionekana kuwa dhaifu mno hata kwenye kuongea, aliamua kutoa kidonge cha kijini kwenye kijimkebe alichokuwa nacho na kisha akamuwekea Park Juan Mdomoni na kisha akakimeza.

Roma aliona kisingeweza kumponyesha kwa haraka hivyo palepale alishika mkono wake na kuanza kumuingizia nguvu ya urejesho na Park Juan alijikuta akitoa macho kwani ni kama alihisi mwili wake ulikuwa ikiingiwa na chaji kwa haraka sana na hata mishono yote ilijifunga na maumivu yalianza kupotea.

Athari chanya za kidonge jumlisha nguvu ya urejesho vilimfanya Park Juan kurejewa na nguvu kabisa kama mtu ambaye amepona kabisa na alishangazwa sana na jambo hilo na haikuwa kwake tu hata kwa Kim Jip alionyesha kushngaaa licha ya kwamba hakuonyesha sana kwenye macho yake kama alikuwa kwenye mshangao.

“Mr Roma wewe ni nani haswa?”Aliuliza Park Juan mara baada ya kutoa mpira wa kupumulia lakini Roma aliishia kutabasamu huku akionyesha hayupo tayari kujielezea zaidi na kuweka siri zake zote hadharani.

“CEO Park kama nilivyokueleza hizi ni mbinu nilizorithishwa , kama unataka kuishi zaidi ya miaka mia ni juu yako kama upo tayari kulipia kwa hilo maana sio bure”

“Nipo tayari , una vidonge vingi zaidi kama hiki ulichonipatia?, kama vipo vingi nitanunua vyote”Aliongea huku akionyesha kuwa na tamaa.

Roma alishangazwa na kauli yake , ijapokuwa ilikuwa kweli kidonge alichompatia kilikuwa cha daraja la chini lakini asingemuuzia vyote .

“Hivi vidonge ni hadhina ya familia yangu , ninavyo vitatu pekee ambavyo vimebakia, unaweza kuwa tajiri dunia nzima lakini huwezi pata kirahisi hivi vidonge , nimeamua kukusaidia kwasababu wewe ni babu yake Yezi”

“Mr Roma nina uhitaji sana na hivyo vidonge angalau vinipe miaka miachache ya kuishi , mjukuu wangu Yezi kuna mambo mengi ambayo hayajui kuhusu kuongoza kampuni na isitoshe maadui hawawezi kumuacha salama. Unaonaje kuhusu hili, taja bei yoyote ambavyo ungependa kuuza na mimi nitanunua”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria.

“Unaonaje kuhusu hili CEO Park , nitakuuzia kidonge kimoja kwa dolla milioni kumi(bilioni ishirini na tatu za kitanzania)?”.

“Kidonge jimoja tu?, kama vipi nipatie vyote kabisa , najua ni kitu cha thamani kubwa , unaonaje kama nitakuongezea milioni ishirini zaidi unipatie vyote?”Aliongea na kumfanya Roma kushikwa na tamaa ya pesa ya haraka namna hio , alijiambia kwa staili hii bora amwambie Sauroni aachane na biashara zake za kutengeneza na kuuza siraha na waanze kutengeneza vidonge na kusambaza dunia nzima.

Lakini mawazo hayo aliona hayawezi kukamilika kutokana na kwamba vidonge hivyo haviwezi kutengenezwa vingi kukidhi mahitaji.

Roma hakutaka kukataa ofa hio ya hela hivyo alitoa vile vilivyobakia na kisha akampatia Park Juan na bwana huyo alifurahi mno kuona Roma amekubali . siku zote ndoto ya tajiri ni kuishi muda mrefu ili kufurahia pesa zake lakini kwasababu hakuna binadamu ambaye anao uwezo wa kurefusha maisha ni jambo ambalo hubakia kama ndoto.

Hivyo kwa mtu kama Park Juan asingeshindwa kutoa kiasi hicho cha pesa ambacho hakifikii hata asilimia moja ya utajiri wake kwa ajili ya kidonge cha kurefusha maisha.

Alimpa ishara kim Jip kumpa cheque(cheki) na akasaini kwa kuandika kiasi cha pesa tajwa alichopaswa kulipa na kisha akampatia Roma , hivyo mpaka muda huo Roma akawa na milioni therathini za kimarekani sawa na zaidi ya bilioni sitini za kitanzania.

Roma mara baada ya kuona sasa mzee huyo hali yake ya afya imekuwa sawa alichukua mkoba aliokuja nao na kisha akatoa nyaraka ambazo Park Juan alipaswa kuziona.

“Hizi nyraka ni halisi na nimezithibitisha lakini naamini unapaswa kuziangalia wewe mwenyewe , siwezi kuongea chochote kwani mimi sio mwanafamilia”Aliongea Roma na akamkabidhi na baada ya Park Juan kupitisha macho sura yake ilikunjamana.

“Nilijua tu huyu mkorofi kuna mambo anafanya , lakini sikuwahi kuwaza kama anaweza kushirikiana na North Buyeo?”

“Unajua kuhusu hawa North Buyeo?”Aliuliza Roma.

“Kwanini nisiwajue , ukweli ni kwamba nimekuwa kwenye mashindano makali na wanachama wote ambao wapo chini ya huu umoja wa siri kwa zaidi ya miaka miwili sasa , lakini licha ya hivyo kutokana na ushawishi wangu hawakuweza kunifanya chochote , lakini bahari mbaya kutokana na afya yangu kudhorota sikuwa na mtu mwingine wa kumuamini zaidi ya park Jonghyun.”

“Unaweza usiwe na ufahamu wa hili Mr Roma , lakini North Buyeo malengo yao makuu ni kuunganisha Korea kusini na Korea kaskazini kuwa nchi moja, huu mwaka kwa hapa Korea ni wa uchaguzi na upande ambao nasapoti ni ambao una ukinzani mkubwa na serikali ya Korea kaskazini ,siku hizi teknolojoia imekuwa kubwa sana, hivyo ukifanya kosa kidogo tu linaweza kupelekea mamia ya watu kuwa hatarini, hawa North Bueyo hapa nchini wanachotaka ni kuchafua nchi na kuiingiza kwenye vita ya pili”Aliongea na kufanya Roma kushangaa na kuona kumbe mambo yote hayo yana muunganiko wa kisiasa ndani yake.

“Kwangu usalama wa Yezi ndio kitu ninachojali , hivyo nakuomba kwa haraka kushughulikia hili na kulimaliza mara moja ukishakuwa tayari”Aliongea na kumfanya Park Juan kutingisha kichwa na kisha palepale alimpa ishara Kim Jip kumpatia nguo zake abadili .

“Kim Jip weka gari tayari , waambie na wengine kwenda nyumbani kwa huyo mwanaharamu na wamlete kwangu”Aliongea

“Aye”

*********

Upande mwingine katika makazi anayo ishi Najma , gari nyeusi aina ya Bernz ilisimama kando ya jengo hilo na kwa haraka haraka aliekuwa akiendesha alitoka nje ya gari na kisha akatoa simu yake na kutafuta namba na kuipiga.

“Vivian , ninajisikia vibaya muda huu , kama hutojali naomba nije tuongee kwa dakika kadhaa”

“Muda umeenda ,najiandaa kulala”Aliongea Najma upande wa pili na kumfanya Park Jonghyun kukunja sura.

“Nipo tayari nje ya Apartment yako , nahitaji kweli kuongea na wewe leo leo , ninaondoka kwenda Ulaya wiki ijayo , hivyo hii inaweza kuwa mara ya mwisho tunaonana”Aliongea kwa kubembeleza na kumfanya Najma aliekuwa ndani akijisomea kufikiria kidogo na kutokana na sauti ya Park Jonghyun ilivyokuwa kinyonge alimuonea huruma hivyo akampa ruhusa ya kupandisha juu.

Dakika chache mbele Park Jonghyn aliweza kufika nje na kugonga mlango na Najma ambaye alivalia gauni la pinki la maua maua na visendo manyoya alifungua mlango na kumkaribisha ndani.

Park Jonghyun mara baada ya kuingia alimchunguza mrembo huyo wa kiafrika kwa macho ya uchu , ijapokuwa yeye alikuwa Mkorea na wanawake wa Kkorea hawakujaaliwa shepu lakini kwa Najma alipenda sana shepu yake.

“Mr Park je kuna kitu kinachokusumbbua , unaonekana kutokuwa vizuri?”aliongea Najma mara baada ya kumkaribisha mwanaume huyo kwenye sofa na kisha kwenda upande wa jiko kuandaa kikombe cha kawahawa ili kumchangamsha.

Upande wa Park Jonghyun alikuwa amekula bata sana na wanawake wa aina tofauti alipokuwa nje ya nchi na ndani ya nchi , lakini kwake ilikuwa mara ya kwanza kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mpole na asie na mambo mengi kama Najma , hisia zake zilikuwa zikimwambia kabisa Najma alikuwa bikra na hio ilimuongezea shauku ya kutaka kuona kama mawazo yake yapo sahihi.

“Vivian vipi kama nisingeanza kukufukuzia , je ungeweza kunipenda wewe mwenyewe licha ya sisi kuwa wa rangi tofauti?””Aliuliza Park Jonghyun na kumfanya Najma kushitushwa na swali lake lakini aliishia kutingisha kichwa kukataa.

“Kwaini iwe hivyo… au ni kwasbabu sitamaniki ? hivi nachukiza sana?”Aliuliza huku akionyesha huzuni ya kukataliwa na mrembo kama Najma.

“Ukweli ni kwamba sio kama nakuchukia au huvutii, kama ni mwanamke yoyote wa rangi yetu angefurahi kupendwa na mwanaume kama wewe , lakini kwangu mimi ni vugumu kufanya hivyo kutokana na kwamba moyo wangu ushampenda mtu mwingine na ndio huyo ambaye ananifanya nishindwe kabisa kumpenda mtu mwingine , nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kupotezea mapenzi yangu kwake lakini nimeshindwa , huenda mtu yoyote anaweza kuniona kama mtu dhaifu lakini ndio hivyo nimeshindwa kumsahau kabisa”Park Jonghyun alijikuta akikunja ngumi na kung’ata meno kwa wakati mmoja.

“Je mtu huyo ni Roma Ramoni?”Aliuliza na Najma alitigisha kichwa kukubalia.

“Nafasi yake katika moyo wangu haiwezi kuzibwa na mtu yoyote”Aliongea na kumfanya Park Jonghyun kusimama na kuanza kucheka kicheko cha uchungu, ni kama lile jibu ambalo hakuwa ametegemea hatimae limewekwa hadharani.

“Roma Ramoni,,, muda wote ni Roma Ramoni , kila kitu ni Roma , nimemkosea nini mimi huyu Roma Ramoni ,mpaka kuharibu maisha yangu”Alianza kuongea kama kichaa na mpaka hapo Najma alijua kabisa amefanya kosa kumtaja.

“Mr Park kwanini .. upo..”

“Kaa Kimya”Aliongea kwa kufoka na palepale alitoka aliposimama na kumsogelea Najma na kisha akambana kwenye kabati la jiko.
 
SEHEMU YA 527.

Najma mpaka hapo alijua alifanya kosa kubwa sana kumruhusu Park Jonghyun kuingia ndani kwake na sio hivyo tu pia kumtaja Roma kama mwanaume anaempenda , lakini alifanya hivyo kwasababu ya kwamba hakuwa akija kama Park Jopnhyun na Roma wana ugomvi.

Kutokana na namna ambavyo ameshikiliwa alishindwa kabisa kujitoa katika mikono ya Park Jonghyun na alishia kuangalia pembeni akikwepa pumzi yake ya moto.

“Biashara zangu zimeharibika , hivyo hivyo maisha yangu yameharibika na kila kitu changu kimechukuliwa kwasababu ya yule mwanaharamu , hebu angalia nilivyo sasa , nimeachwa sina kitu na mwanamke ambaye kwa mara ya kwanza nimetokea kumpenda na yeye amechukuliwa kutoka kwangu na Roma Ramoni , kila saa ni Roma Ramoni kwanini , hebu niambie ana kitu gani cha ziada mnachokipenda?”Aliongea kwa hasira.

Machozi pekee ndio ambayo yalikuwa yakimtoka Najma hakuweza kuongea kuwakilisha kile ambacho anajisikia moyoni.

“Kwanni huongei?, Oh.. itakuwa naogopesha , itakuwa nakutisha si ndio ,, hahaha , sikupanga kuwa hivi , kama ungesema hata uongo huenda ningekuachia , lakini hata wewe mtu wa mwisho ambaye niliweka matumaini yangu unakuwa mkatili kwangu?”Aliongea na hasira zake zilianza kugeuka machozi , alionekana kabis ahakuwa hana tumaini tena.

“Mr Park tafadhari naomba usifanye hivi ,, nini kimetokea? Roma kakufanya nini?”

“Uthithubutu kutaja jina lake mbele yangu”Aliongea huku akionyesha kabisa muda huo ni kama akili haikuwa yake kabisa.

“Kwasababu Roma ameharibu kila kitu changu , nitakurudishia kila kitu , na wewe nakuharibia kama kulipiza”

“Mr Park .. unataka kufanya nini?”Najma ambaye sura yake ni ya kipole ilijawa na majonzi aliuliza kwa kujipa ujasiri , huku hofu ikiwa juu.

“Unafikiri mimi mjinga , inaonyesha kabisa Roma anakujali hivyo nitafanya mapenzi na wewe na kitakachotokea hapa kitamuumiza sana maisha yake yote”

Najma baada ya kusikia hivyo alizidi kuogopa , alizidi kukusanya nguvu zake zote ili kuweza kujitoa katika mikono ya Park Jonghyun lakini alikuwa ameshikiliwa vizuri sana kiasi kwamba hakuwa na namna ya kujiokoa.

Jasho lilianza kumtoka palepale , alishindwa hata kupiga kelele , Park Jonghyun aliongea kwa vitendo pia kwanni palepale alimchania gauni Najma na kumuacha na nguo za ndani pamoja na Bra tu.

Shepu yake ilionona ilikuwa wazi katika macho ya Park Jonghyun , jambo ambalo liliamsha mashetani yake zaidi ya kimatamanio .

“Naomba usinifanyie hivi… hapapna,, arhg tafadhari naomba uache ugh…”Hata kama alitoa kilio ilikuwa ngumu kusikika kwani nyumba hizo zimejengwa kwa mtindo wa soundproff.

Kilio chake kilimfanya Park Jongyun kuwa kama chizi na kuachia kicheko ambacho kilisambaa chumba kizima na kufanya hata sauti yake ya kilio isisikike.

****

Roma aliondoka hospitalini hapo akiwa ndani ya gari ya Park Juan akijiweka kuwa huru kwenye gari hilo mpaka kuanza kupiga miayo ya usingizi.

Upande wa Park Juan alikuwa na nguvu mpya , alikuwa ni kama amezaliwa upya hivyo hata usingizi hakuwa nao zaidi ya furaha ya kwamba anakwenda kuishi maisha marefu tofauti na alivyowaza siku kadhaa zilizopita, alijichukulia kama mzee mwenye bahati sana katika maisha yake.

Upande wa Kim Jip alionekana kuongea na simu kwa dakika kadhaa na kisha akageuka nyuma na kumwangalia bosi wake kumpatia taarifa.

“Sir Tumepotkea taarifa Park Jonghyun amemuua msaidizi wake na mlinzi wake na sasa yupo mafichoni , lakini kwa taarifa zinazoonyesha hajatoka nje ya Gangnam”Aliongea Kim Jip.

“Lazima atakuwa amejua hawezi kutoka bila ya kukamatika , endeleeni kumuwinda mpaka mumpate , nahitaji kujua kila kitu alichofanya bila ya mimi kujua”Aliongea Park Juan na Kim Jip alitingisha kichwa kukubali.

Upande wa Roma mara baada masikio yake kusikia maneno ya Kim Jip alikunja ndita , lakini kwa wakati mmoja kushangazwa na kitendo cha Park Jonghyun kumuua msaidizi wake mwenyewe pamoja na mlinzi wake.

Alijiuliza kama kweli alikuwa ana mpango wa kutoroka kwanini kaamua kumaliza watu wake wa karibu , ilihali huenda wangemsaidia kutoroka , au inamaanisha kwamba hakuwa na mpango wa kutoroka, Roma alijiuliza hayo maswali na palepale alamu ilipiga kwenya ubongo wake.

“Simamisha gari?”Aliongea Roma kwa kushituka na kumfanya dereva kushangazwa na kauli yake ya kibabe lakini alisogeza gari pembeni na kulisimamisha

“Mr Roma kuna tatizo?”Aliuliza Park Juan lakini Roma hakuwa na muda wa kujibu zaidi ya kufungua mlango haraka haraka na kutoka na alienda hadi nyuma ya bustani ambapo watu wa barabarani hawamuoni na kisha akapotea.

Roma alishajua kabisa kutokana na kitendo ambacho amefanya Park Jonghyun basi lazima agefanya zaidi ya hilo hivyo moja kwa moja alioa mtu ambae anaweza kuwa katika hatari ni Najma.

Ilikuwa bahati kwamba alikuwa akijua eneo ambalo anaishi Najma mpaka chumba chake baada ya kumsindikiza Edna kukutana nae na hilo ndio ambalo lilimsaidia kutopata tabu.

Roma mara tu ya kuibukia nje ya jengo la analoishi Najma alitumia uwezo wake wa kijini kuanza kuangalia mazingira ya jengo huku roho yake ikinuia kumtafuta Najma ili kuona kama yupo sawa.

Na palepale alipotea na ile anakuja kuibukia alikuwa juu kabisa ya balkoni ya apartment anayoishia Najma .

Park jonghyun alikuwa ashafanikisha kumlaza chini kwenye sakafu Najma na sasa alikuwa akimpiga mabusu kuanzia kwenye shingo kushuka chini huku akiwa ameshikilia mikono vizuri pamoja na kumbana kiwiliwili cha chini na miguu yake.

Baada ya kulizika na hatua ya kwanza alihamia chini na kisha akavuta Tight nyeupe aliokuwa amevaa na kuichana kabisa na kumfanya sasa kuwa mtupu .

“Hahaha..Vivian you are mine now”Aliongea kwa kingereza huku akizidi kupandishwa na mumkari mara baada ya kuona tunda ambalo halikuwa na dalili ya kumegwa kabisa.

Upande wa Roma aliweza kusikia maneno ya Park Jonghyun na yaliyamfanya kuwa katika hasira ya kiwango cha juu mno na Park Jonghyun aliweza kumuona kutokana na Roma kuingia kwa kufosi mlango.

“Hatimae umekuja wakati ambao sikukutegemea , nilikuwa nikijiandaa kuonja utamu hapa , lakini naona umekuja kuniharibia tena”Aliongea Park Jonghyun mara baada ya kumuona Roma.

Roma hakuwa na haja ya kuwa mpole tena kwa Park Jonghyun , alimsogelea kwa kasi na kisha akamwinua juu juu na kumshikilia shingo yake.

“Kumbuka haya macho , kama ikitokea ukawa mzimu na kurudi kwangu nitakuua tena zaidi ya mara elfu moja”Aliongea Roma na palepale akiwa ameng’ata meno yake kwa hasira alikaza kiganya chake cha mikono na kufanya mshipa mkubwa wa damu kupasuka palepale lakini hakuachia mpaka alipohakikisha Park Jonghyun alipopoteza maisha na alimtupia chini huku damu nyingi zikimtoka kama bomba la maji.

Roma bado ni kama hakuwa ameridhika na kifo chake , hivyo aliweka na mguu kwenye kifua chake na kisha akakanyaga kwa nguvu na kufanya mguu wake kutengeneza unyao kwenye kifua na kiasi flani hali yake ya utulivu ilirudi kawaida na kisha akamsogelea Najma ambaye amelala chini akiwa hana nguo.

Ijapokuwa Park Jonghyun hakufanikiwa kumbaka kutokana na yeye kufika ndani ya muda , lakini bado alikuwa na wasiwasi na hali yake.

Najma tokea aonane na Roma nchini hapo ni kama maisha yake yalibabadilika na hata ile furaha na hali ya kujiamini ilimpotea kabisa na kubakia kama Najma ambaye alikuwa wa miaka kadhaa iliopita.

“Najma…!!”Roma alijaribu kumuita mara baada ya kumkalisha na kumuegamiza kwenye mikono yake , lakini licha ya kwamba Najma alionekana kuwa na fahamu lakini hakuna kitu ambacho alijibu.

“Kila kitu kipo sawa Najma , nimekuja..”Aliogea Roma na kisha akavua jaketi lake na kumvalisha na baada ya kuona amejisitiri alimsimamisha lakini Najma alionekana kama kukosa nguvu na alianza kuzungusha kichwa taratibu huku akiwa na mwonekano usioelezeka.

Alimwangalia Roma kwa muda na palepale alianza kuongea maneno yasioeleweka kwa sekunde na ghafla tu palepale alipoteza fahamu kwenye mikono ya Roma.

“Najma”

Roma alijua huenda baada ya kumuokoa angesimama na kisha kumkumbatia na kuanza kulia , lakini ajabu ilikuwa tofauti na mategemeo yake , hakutegemea kama angepoteza fahamu muda huo huo.

Roma palepale alijikuta akipeleka mkono wake na kushika kiganya chake cha mikono na kumuingizia nguvu ya urejesho isio na kikomo ili kujaribu kuangalia kama kuna tatizo lolote ndani ya mwili wake , lakini alikuja kugundua Najma hakupata majeraha yoyote ya ndani.

“Inawezekanaje akapoteza fahamu..?”Aliwaza Roma na palepale aliona hilo ni swala ambalo hawezi kurekebisha kwa kutumia uwezo wake , Roma palepale alimlaza kwenye sofa na kutafuta gauni kwenye kabati na kisha akamvalisha na kumbeba na akapotea nae na alikuja kutokezea hospitalini na kupokelewa na manesi.

“Sir ana tatizo gani?”Aliuliza nesi wa kikorea huku akijua hajaeleweka kutokana na lugha.

“Alipatwa na mshituko na kupoteza fahamu , nimejaribu kumuamsha lakini meshindikana”Aliongea Roma kwa lugha ya kikorea na alipokelewa haraka na madaktari wa kitengo cha dharula na baada ya kufanyiwa vipimo vya awali walishauri afanyiwe CT scan.

Roma baada ya kuona Najma kashaingizwa kufanyiwa vipimo alitoa simu yake na kukuta kulikuwa na missed call kama tatu kutoka kwa Edna, na moja kwa moja alidhania kabisa mke wake atakuwa kwenye wasiwasi na palepale simu ilianza kuita upya na alipokea.

“Honey uko wapi , kwanini babu yake Yezi ndio amerudi wewe huonekani?”

“Najma amepoteza fahamu na nipo hospitalini saivi , usiwe na wasiwasi hakuna kibaya kinachoweza kunikuta”

“Usiniambie Najma ameba..”

“Hapana ,ilikuwa afadhali nilifika ndani ya muda”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchungu , aliona kama angechelewa hata dakika moja tu basi huenda Najma angenajisiwa na angejilaumu maisha yake yote maana yeye mwenyewe ndio ambaye alikuwa na makosa kwa kumuacha Park jonghyun akiendelea kuishi licha ya kufahamu uovu wake.

“Kama ni hivyo nitamwambia babu yake Yezi ili kusafisha hali , nitajiandaa kukufauta sasa hivi”Aliongea Edna na Roma alitaka kumzuia lakini aliona asifanye hivyo kwani Edna angefikiria mambo mengine .

Haikupita hata nusu saa Edna aliweza kufika hospitalini akiwa amevalia sweta kubwa la manyoya na kujifunga na scarf kwenye shingo kuzuia baridi, alikuwa ameshikilia kijimfuko.

“Njmenunua kahawa njiani, kunywa kidogo kupasha mwili joto”aliongea

Wakorea ni watu wa kahawa na mara nyingi huwa zinauzwa mpaka madukani tena zikiwa za moto kabisa.

Roma alijikuta akifurahishwa na harufu nzuri ya kahawa na baada ya kunywa kidogo iliweza kurudisha mudi yake.

“Ilikuwa siku ngumu kwako leo , rudi mapema ukapumzike”

“Mpaka nione hali ya Najma ikoje, nitakuwa popote ulipo”Aliongea Edna.

“Bado una wasiwasi nikiwa karibu na wanawake wengine?”Aliongea Roma huku akicheka kivivu.

“Nina wasiwasi na hali ya Najma , ni rafiki yangu licha ya yote yaliotokea , hivyo nitakaa hapa mpaka nione kinachoendelea”Aliongea na muda huo huo daktari aliwasogelea akiwa ameshikilia faili kwenye mikono yake.

“Wewe ndio Mr Roma , naitwa Zeng Guozhong mChief daktari wa hospitali , raisi Park alinipigia simu, nisameheni kwa kuchelewa kufika, ndio nimetoka nyumbani , tutafanya kila linawezekana kuhakikisha hali ya mgonjywa inatengemaa , kwasasa naomba mnifuate kwenda kwenye ofisi yangu”Aliongea na kumfanya Roma asitarajie kama Park Juan angechukua hatua ya kumpigia Chief daktari mkuu.

Kwa muda huo alijua kabisa angepaswa kushughulikia maswala ya Park Jonghyun pamoja na North Buyeo hivyo alijuwa yupo bize , lakini lichia ya hivyo aliweza kumuita daktari ambaye ashatoka hospitalini kurudi.

Ndio maana alikuwa mfanyabiashara mkubwa ndani ya bara la Asia kutokana na ushapu wake na uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka

“Dokta Zheng hali ya mgonjwa wetu ipo je , yupo kwenye hatari?”Aliuliza Roma mara baada ya kukaribishwa ndani ya ofisi.

“Hayupo kwenye hatari , lakini hali yake sio rahisi”Aliongea huku akilazimisha tabasamu.

“Nini tatizo?”

“Mr Roma je mgonjwa alifanyiwa kitendo cha ukatili , nesi amesema alikutwa na baadhi ya alama kwenye mwili wake”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa.

“Kuna mtu alikuwa na nia yakumfanyia hivyo lakini niliweza kuzuia kabla haijatokea”

“Haishangazi , je aliweza kugonga kichwa chake kwa namna yoyote wakati wa tukio hilo?”Aliuliza na kumfanya Roma kushangaa lakini aliishia kukumbuka tukio zima namna ambavyo alilikuta.

“Nilimkuta akiwa amekandamizwa kwenye sakafu lakini sijui namna ambavyo aliweza kulazwa chini , inawekzekana akawa amejigonga ndio , hata mwonekano wake alioniangalia nao ni kama vile hanijui”Aliongea Roma kwa kikorea na Edna aliekuwa pembeni aliomba kutafsiriwa na alijikuta akishikwa na huzuni mara abaada ya kusikia kinachoendelea ,

“Mr Roma kwa heshima zote naomba niseme hali ya tatizo la mgonjwa linaweza kuwa nje ya matibabu ya kawaida ambayo sisi madaktari tunaweza kufanya?”

“Unamaanisha nini?”

“Miss Najma amegonga kichwa chake vibaya na kupata majeraha kwenye Cerebral Cortex , ingazwa jeraha sio kubwa sana lakini baadhi ya neva zake zimeharibika l wakati huo huo ufahamu wake umepitia mshituko mkubwa , hivyo utambuzi wake wa fahamu , na kujieleweza vyote havipo sawa,, kwasasa tumempa dawa ya usingizi mara baada ya kuamka.

Kabla ya kuchomwa sindano ya usingizi alikuwa akitetemeka sana huku akitaja neno ‘hapana’kwa nguvu na tulishindwa kuwasiliana nae , hivyo kwa uzoefu wangu naweza kusema amepatwa na ugonjwa wa akili kama PTSD (Post-traumatic stress disorder) au Phobia(Woga maalumu).

Roma alijikuta hata akisahau kumtafsiria Edna kutokana na taarifa hio mbaya na Edna aliona wasiwasi wa Roma na kumwambia amtafisirie na Roma alifanya hivyo kinyonge na kumfanya Edna Chozi kumtoka, hakuamini kama Najma anaweza kuchanganyikiwa kwa tukio la kutaka kubakwa.

“Kwanini iwe hivi?”

“Kwa kawaida ukatili peke yake hauwezi kumfanya mgonjwa kuwa katika hali kama hio , nina makisio Miss Najma alikuwa na msongo mkubwa wa mawazo , hali ambayo ni kama imempelekea kujikatia tamaa na inawezeana alikuwa kwenye uvumilivu wa hali ya juu sana, hivyo mara baada ya kuwa katika hali ya kubakwa alijikatia tamaa na kuruhusu utu wake wa ndani kumpotea na kujizima kabisa”Aliongea daktar Zheng na baada ya kuona Roma bado alikuwa katika hali ya mawazo aliendelea kuuliza swali.

“Mr Roma je mgonjwa alikuwa na matatizo hayo bainishi?”















SEHEMU YA 528.

Roma alijikuta kwanza akinywa kidogo kahawa ambayo ishaanza kupoa iliokuwa kwenye mkono yake , mwanzo ilikuwa tamu lakini wakati huo aliiona ni chungu.

Roma alijua kabisa kuhusu kumkataa Najma kusingemsababishia matatizo makubwa mpaka kujikatia tamaa ya kuishi.

“Dokta je tunamsaidieje sasa , atakuwa hivyo maisha yake yote?”

“Hatuwezi kusema kwa uhakika , labda mgonjwa anaweza kupona yeye mwenyewe lakini kuna uwezekano hali yake kuzidi kuwa mbaya”

Edna mara baada ya kusikia tafsiri alijikuta akikumbuka mazungumzo yake na Najma katika Apartment yake, maneno ya Najma baada ya kujirudi katika kichwa chake , alihihisi ni mwenye hatia na kujiona ni yeye pekee ambaye alikuwa kwenye nafasi ya kumsaidia lakini hakufanya hivyo na kumuacha afanye atakavyo.

Edna hata yeye mwenyewe alianza kujishangaa , kwanini moyo wake ulikuwa ukiuma , kwanini anajisikia huzuni kiasi cha kukosa raha kabisa.

Roma alimuona namna Edna alivyobadilika na aliamua kumshikilia mkono ili kumtuliza na alivyoinua macho yake aliona tayari Dokta Zheng alikwisha kuondoka bila kuelewa ameondoka hapo muda gani.

“Usifikirie sana , hili halijatokea kwasababu yako , sio wewe uliemuagiza Park Jonghyun , sio jambo zuri kujibebesha lawama kwa kitu ambacho hujafanya”

“Najihisi kuwa mwanamke mkatili…”Aliongea Edna huku machozi yakianza kumtoka , kilichomuuma Edna zaidi ni kuona kwamba yeye ni kama alinunua hisia za Najma , kule Tanzania yeye ndio ambaye alimshauri Najma kuondoka kwenye maisha ya Roma na kwenda kuishi Marekani kwa sababu ya kimasomo akiamini kwamba Najma angeweza kumsahau Roma kwa haraka,lakini mambo yaligeuka ndivyo sivyo Najma alionekana kupenda kweli na mapenzi yake kushindwa kumpotea mara moja, hivyo kuwa nchini Marekani ni kama hisia zake zilinunuliwa kwa pesa taslimu na ndio kilichompelekea kujitoa katika ufadhili na kuja kukimbilia mpaka Korea ambako ndio anakuja kupatwa na tatizo ambalo linampelekea uchizi.

“Kama wewe utakuwa mwanamke mkatili basi mimi nitakuwa mwanaume mkatili zaidi kuwahi kuishi katika uso wa dunia, hujafanya kosa lolote , kuna baadhi ya vitu sisi kama binadamu vipo nje ya uwezo wetu , niamini mimi Najma hajawahi kukuchukia”

“Kweli?”

“Ndio”Aliongea Roma na kumfuta machozi kwa kutumia kiganja cha mkono wake

“Twende tukamuangalie Najma anaendeleaje”Aliongea na kumfanya kusita sita lakini alitingisha kichwa kiukubali na akasimama.

Ilikuwa ni usiku bado , hivyo hospitali ilikuwa na ukimya wa hali ya juu sana, walitembea kwenye korido na hatimae kuweza kufika katika wodi ambayo amelazwa Najma , huku akiwa mkononi ametundikiwa dripu.

“Najma ataamka lini?”Aliuliza Edna.

“Sijui , ameishi mwenyewe kwa muda mrefu , hana rafiki wala familia , kama tungekuwa Tanzania angalau kaka yake angekuwa karibu yake na kumsaidia”

“Kama ni hivyo basi tusiondoke , tukae hapa hapa mpaka atakapo amka”Aliongea Edna na Roma alikuwa na mawazo sawa , alikuwa akiwaza kama hali yake ikiendelea hivyo huenda wamtoe hapo na kumpeleka nchi nyingine au kurudi nae Tanzania kabisa kama asingeweza kupona.

Masaa nayo yalipita kwa haraka na hata hivyo muda ulikuwa umeenda hivyo Edna alijikuta akisinzia kwenye bega la Roma huku Roma yeye akiwa macho muda wote , hakuwa na shida kukaa macho muda mrefu kutokana na uwezo wake.

Kulivokucha mtu wa kwanza kuwapigia simu alikuwa ni Park Juan akiulizia hali ya afya ya Najma na kuuliza kama kuna kitu chochote cha kusaidia , lakini kwa hali yake aliokuwa nayo Roma aliona kwamba mzee huyo asingeweza kufanya chochote kama yeye mwenyewe tu ameshindwa.

Saa moja kamili hatimae Najma aliweza kufumbua macho yake , lakini licha ya hivyo mwonekano wake ulikuwa kama wa mtu ambaye hana uelewa wowote kama yupo wapi.

“Najma umeamka , unajisikiaje?”Aliongea Edna lakini Najma aliishia kumwangalia bila ya kutoa jibu , ilikuwa ni kama vile hamjui.

“Kiu…”

“Una kiu , ngoja nikupe maji”Aliongea Edna na kisha akachukua maji ambayo yalipashwa moto kidogo kupunguza ubaridi na kisha akamsaidia kumnywesha.

“Najma vipi hali yako bado unajisikia vibaya?”

“Wewe ni nani?”Aliuliza Najma huku akionyesha kumshangaa Edna.

Edna baada kuulizwa swali hilo alijikuta kikombe kikimponyoka bila ya kujielewa na kudondoka chini huku akiwa ameshikwa na bumbuwazi akiwa kama mtu asieamini.

Upande wa Roma kidogo aliona ni ahueni baada ya kuona hali yake haikuwa mbaya kama alivyotegemea lakini mara baada ya kumuuliza Edna yeye ni nani kauli yake ilishitua moyo wake.

“Najma hautujui sisi?”Aliuliza Roma na kumfanya sasa Najma kuona kumbe kuna mtu mwingine ndani ya hiko chumba.

“Ah…Ondoka , Ondoka ..”alianza kufurukuta kwenye kitanda kama vile mtu ambae ameona kitu cha kutisha mara baada ya kumwangalia Roma.

Roma ilibidi amuwahi na kumshikilia mikono na miguu ili aisje akadondoka chini , lakini hakuacha kupiga makelele.

“Niache …Argg.. Niache mimi ,. Ondoka zako”

“Najma hebu tulia , mimi ni Roma , Roma Ramoni”

“Najma hutujui sisi , usilie”Aliongea Edna akiwa amemshikilai mkonno mwingine kwa namna ya kubembeleza , lakini bado Najma alianza kurusha rusha miguu.

“Roma inabidi uondoke , Inaonekana Najma anakuogopa”Aliongea Edna na kumkumbatia Najma akimshikilia kwa nguvu.

Roma alielewa na kumwangalia Najma kwa wasiwasi na kisha akatoka ndani ya hio wodi. Na ilionekana kuwa kweli , kwani Roma mara baada ya kutoka alitulia na kuishia kumkumbatia Edna na kuanza kuporomosha kilio kama mtoto mdogo.

Muda huo huo na manesi waliweza kufika kwa kukimbia kumsaidia Edna na walikuwa wakiongea kikorea tu jambo ambalo lilimfanya Edna asielewe , hivyo mwanamama mmoja alimshika Edna mkono na kumtoa nje,

“Sir, hali ya mgonjwa kwasasa haijatulia , je daktari hajawaambia msimsogelee kwani angefanyiwa uchunguzi tena , kwanzia sasa kaeni mbali na mgonjwa”Aliongea yule nesi huku akionyesha kuchukizwa kiaina lakini Roma alielewa nesi huyo alikuwa akijali zaidi kuhusu hali ya mgonjwa.

“Nesi kwanini mgonjwa ananiogopa mimi ilihali mke wangu yeye hamuogpi”

“Kutokana na kilichomtokea kusababishwa na wanaume hivyo woga wake anaelekezea kwenu , hivyo kumfanya kuzidi kuwa katika hali hatarishi”Aliongea yule nesi na kumfanya Roma kuhisi maumivu kwenye moyo wake.

Edna alishindwa kuvumilia kumwangalia Najma ambaye alikuwa akihudumiwa na manesi, kadri alivyokuwa akimwangalia alizidi kujibebesha lawama kwa kuona yeye ndio mhusika mkuu wa yote hayo , hata hivyo Najma alikuwa hana kosa , kama kuonana na Roma yeye ndio wa kwanza na hata kumpenda yeye ndio wa kwanza , lakini licha yote yeye ndio akawa mhanga mkubwa wa mapenzi,Roma alikosa hata nguvu za kumfariji Edna tena.

Nusu saa mbele daktari wa wagonjwa wa akili aliweza kufika hapo kwa ajili ya kumchunguza Najma , lakini ilishindikana kwni Najma alikuwa akileta vurugu na mwishowe daktari wa kike aliitwa.

Yezi na Park Juan pia waliweza kufika hapo lakini Najma hakuweza kuwatambua kabisa na Najma alimuogopa hata Park juan licha ya uzee wake.

Yezi kumuona mwalimu wake kuwa katika hali mbaya kama hio alijikuta akishindwa kujizuia na kutoa machozi.

“Vipi tuwataarifau familia yake , nadhani litakuwa jambo zuri kumpa taarifa kaka yake”

“Hapana , nyumbani inaonekana wanajua kabisa Najma anaendelea vizuri , unafikiri tukiwaambia yupo kwenye hali kama hii tutaeleza sababu iliosababisha ni nini”

“Tutafanyeje sasa yupo katika hali hii na kama ikiendelea kubakia hivyo?”

“Kwasababu hawa madaktari wamekusoa suluhu ya tiba yake , naamini Clark anaweza kusaidia katika hili”Aliongea Roma na ikawa imepita hio , Roma aliamini Clark asingekosa suluhisho.

Taarifa zilionyesha Clark tayari alikwisha kupanda ndege , hivyo Roma alikadiria muda ambao Clark angekuwa ashafika na kisha aende akamrudishe tena Korea.

Siku iliofatia mara baada ya hali ya Najma kuendelea vilevile na madaktari wa hospitali hio kubwa kukosa suluhu hakutaka kuendelea kumwangalia Najma akiwa kaenye hali yake hio , hivyo moja kwa moja alienda Uingereza.

Clark alishangazwa na uwezo wa Roma kusafiri anavyotaka ndani ya sekunde tu na alijikuta akianza kupatwa na tamaa na yeye kuutaka kujifunza mbinu za kijini , akijiambia kwamba angeweza kusafiri kwa muda mfupi sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Roma alimweleza Clark njiani juu ya tatizo la Najma hivyo mara baada ya kufika Korea kwasababu daktari mkuu wa hapo alikuwa akimfahamu alipewa ushiriano wa kutosha.

Na kwa upande wa Najma hata baada ya kuonana na Dokta Clark alionyesha pia kutokumfahamu.

Clark alitumia zaidi ya masaa mawii kuwa na mgonjwa kuongea nae na kumchunguza tatizo lake na kisha aliweza kutoka kumpatia majibu Roma.

“Hali yake kwasasa ni ngumu sana kuielewa ,ameamua kufunga baadhi ya kumbukumbu zake na kupatwa na tatizo la woga maalumu kwenda kwa wanaume , kama hali yake isiposhughulikiwa haraka basi moja kwa moja hali yake itakuwa mbaya zaidi”

“Kwahio tunamsaidiaje, madaktari wote wa hapa Korea wameshindwa kuwa na njia”

“Sio kama wameshindwa kuwa na njia , ila ni kwamba hawana uhakika njia ipi inaweza kumfaa , kikawaida kuna matibabu ya aina nyingi kwa mgonjwa kama huyu , kuna tiba ya hypnotherapy , tiba ya utambuzi, tiba ya ulazimishaji , tiba ya kimazingira na nyingine nyingi… ila nitajaribu na tiba ya hypnotherapy , kama nitaweza kugundua ni tatizo ganni linasababisha woga wake basi itakuwa rahisi kuamua matibabu mengine”Aliongea kwa kingereza.

“Ni hatari hio tiba?”Aliuliza Edna.

“Kama itafikia hatua mgonjwa ataonyesha kuwa katika hatari basi tutaghailisha , isitoshe nina uzoefu wa kutosha hivyo usiwe na wasiwasi’Aliongea Clark huku akitabasamu kumtoa Edna wasiwasi.

Baada ya hapo Najma alihamishiwa na kupelekwa katika chumba maalumu cha ukimya na kufayiwa taratibu za mwazo ili kuanza matibabu mengine.

Edna kwanini usirudi kwanza katika makazi ya Park, nadhani itakuwa sawa nikiendelea kubakia hapa , mwambie Yezi asiwe na wasiwasi lazima kutakuwa na njia ya kmsaidia”Aliongea Roma na Edna aliona afanye hivyo kwanza alikuwa akijihisi uchomvu wa aina yake.

“Honey , kama Najma asipopona , utafanya nini?”Aliuliza kabla ya kuondoka.

“Nahusika moja kwa moja kwa hali ambayo amepata , hivyo kama matibabu yatashindikana sina jinsi nitamrudisha Tanzania na kumweleza kaka yake kilichotokea , kama atanichukia sio mbaya , lakini nitaendelea kumhudumia”Aliongea na kumfanya Edna kutoa tabasamu la kulazimisha.

“Muda mwingine inaonekana sahihi kufanya hivyo lakini matokeo yake mzigo unaniegamia mimi”Aliongea Edna na Roma alijua Edna anachojaribu kumaanisha , lakini kwa muda huo hakuwa na cha kuongea zaidi ya kumwambia akapumzike.

Baada ya saa moja kupita Clark alirudi kwa Roma tena kumweleza hali inavoendelea.

“Umefanikiwa?”

“Imeshindikana kabisa , tumejaribu kumwambiea aingie ndani kabisa ya mawazo yake ili kukumbuka matukio yote , lakini alionekana kuwa katika taharuki ya hali ya juu na presha yake kupanda hivyo tukakatisha asije akapatwa na Stroke”

“Clark najua hili sio rahisi kufanya , lakini nakuomba sana umsaidie apone , yupo kwenye miaka ishirini tu na ameteseka sana , itakuwaje akaendelea kuwa hivyo bila ya kukamilisha ndoto zake”Aliongea Roma kwa wasiwasi huku akibembeleza kwa dhati kabisa.

“Kwanini upo na wasiwasi hivyo , lakini mimi hata hunionei huruma hata mara moja”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake kidogo.

“Wewe ni wa tofauti , sisi ni marafiki wazuri sana”

“Marafiki wazuri ,,, yaani baada ya miaka yote hio , na yote nilioyafanya bado to sisi ni marafiki wazuri”Alilalamika huku aking’ata lipsi zake.

“Roma kwanini unanikatili namna hio?”Aliendelea kuongea.

“Clark naomba tuache hii topiki , ni muda mrefu sana sijapata uchomvu na wasiwasi wa namna hii , naomba kwanza tafadhari unisaidie kumrudisha Najma kwenya hali yake ya kawaida”

“The only person in this world who can let the murderous His Majesty Pluto beg is probably me”Aliongea Clark akimaanisha kwamba mtu pakee ambaye anaweza kumfanya Mfalme Pluto muuaji kuomba basi ni yeye.

“Sioni tatizo kukuomba hata hivyo”Aliongea na kumfanya Clakr kutingisha kichwa kumsikitikia .

“Ukweli ni kwamba nishapata wazo la kutatua shida yake”

“Ni wazo gani hilo?”

“Vipi kwanza mkeo hayupo hapa si ndio?”

“Tatizo nini akiwepo , wazo hilo linamuhusu , nimemuambia aende akapumzike”Aliongea Roma na kumfanya Clark kutabasamu kidogo.

“Kumbuka nilichokuambiwa mwanzo , kwamba tunaweza kumtibu kwa njia ya hali ya kimazingira pamoja na tiba lazimishi(compulsive therapy)”

“Ndio nakumbuka , lakini inafanyika vipi?”Aliuliza Roma na Clark alimwonyesha Roma ishara ya kumsogelea karibu amnong’oneze.

“Ah.. ndio maana ukauliza kwanza kama Edna yupo hapa , kumbe tiba yenyewe ni hio”Aliongea Roma huku akionyesha mshangao.

“Hio ndio njia yenyewe ambayo inaweza kumsaidia , najua unaweza kuona haifai hivyo sikulazimishi kwani anaweza akapona mwenyewe siku yoyote , lakini kwa hali yake aliokuwa nayo naamini atazidi kudhorota kadri ziku zitakavyosogea , na isitoshe kama ataendelea kuogopa wanaume basi maisha yake yatakuwa magumu sana”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa , lakini njia yenyewe ilikuwa na changamoto kwani ilibidi yeye ndio afanye kumponyesha Najma.

Unafikiri ni tiba gani hio ambayo Edna hatakiwi kuwepo?”

ITAENDELEA
 
Shukuran sana mkuu
Tuliisubir kwa hamu sana [emoji120]
 
Every man for himself!!! Kaketu kachoshwa na huduma za bure!!!! [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sema nini bro sijapenda umem character roma kama mlugaluga sana hapo hapo ana mwil wa mazoez.nakumbuka nilivokua korea tulikua tunasoma sana stori na mwalimu wetu wa fasihi alikuwa anasema umfanye main character kuwa handsome bhana
 
mkuu hatimaye nimemaliza kusoma kuanzia mwanzo mpaka todate shukhran sana mkuu pia nimeamua kuwafuatilia The greek gods ikiwemo:
Zeus*
Poseidon*
Hermes
Hera
Hades*
Dionysus
Demeter
Apollo*
Ares
Artemis
Athena*
na Aphrodite*
nikagundua hii story bado ni ndefu na na ninashauku ya kuisikia miungu isiyotajwa.
miongo iliyokuwa na nyota hapo juu mkuu singanojr umeshaitaja ninashauku ya kuisikia iliyobakia
 
Mkuu nilipofuatilia kindakindaki nikagundua kwamba
Demeter ni mama wa persephone yaani Edina hvyo basi kuna siri nyingi zimejificha humu.
 
Vilevile moja kati ya siri tusiyoijua uyo anayejiita apollo na huyo the don yaani Athena ni mapacha
 
Kwakusema hayo machache, twasubiri muendelezo wa simulizi yako mkuu singanojr shukhran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…