singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
- #2,921
SEHEMU YA 523.
Profesa Clark hakujali sana namna ambavyo watu wa nje ya chumba hicho cha upasuaji walivyokuwa na wasiwasi zaidi ya kuwaambia wasaidizi wake kuwa makini na upasuaji.
Mpaka anakuja kumaliza upasuaji hakuna ambaye aliamini kama amefanikiwa kwa asilimia mia moja kuokoa maisha ya Park Juan..
Dokta Lee ambaye aliangalia mchakato mzima wa upasuaji alihisi ni kama vile anaota kwani mambo ambayo alikuwa akifanya Dokta Clark hakuwahi kuyashuhudia na siku hio ilikuwa mara yake ya kwanza.
Kuna baadhi ya taratibu za kiupasuaji aliishia kuzisoma tu kwenye vitabu na hajawahi kuona zikifanyika kwa vitendo , lakini mbele ya Dokta Clark baadhi ya nadharia ambazo amezisoma katika safari yake ya kuwa daktari ameweza kuona mubashara kabisa zikifanyika.
Madaktari na manesi wasaidizi walimhusudu Dokta Clark pia kwa uwezo wake, ilionekana kwao ni kama vile alikuwa amezingatia kila changamoto ambayo ingeweza kujitokea katika upasuaji huo.
Madaktari wote waliofika kuangalia namna upasuaji unavyofanyika walijikuta wakisimamama na kuanza kupiga makofi.
Yezi alifurahi sana kuona babu yake ameweza kuhimili upasuuaji huo mzito kufanyika , upasuaji wa upandikizaji wa viungo viwili kwa wakati mmoja na mpaka hapo shukrani zake zote zilienda kwa Dokta Clark ambaye amemsaidia babu yake.
Katika watu ambao hawakupenda mafanikio ya upasuaji huo kufanikiwa alikuwa ni Park Jonghyun , lakini kwa kinafiki alitoa shukrani kwa madaktari wote waliohusika katika upasuajji.
Baada ya upasuaji kumalizika wanafamilia wote walikubaliana kutafuta mgahawa kwa ajili ya chakula cha usiku.
Kim Jip ambaye aliondoka kwenda kuchukua moyo aliweza kurudi akiwa ameongozana na baadhi ya mabodigadi wa familia ya Park , pamoja na baadhi ya polisi.
Alikuwa kauzu kama kawaida yake na alikuwa tayari ashapata taarifa ya Roma kurudi hospitalini akiwa amefanikisha kuupata moyo uliohitajika.
“Asante sana Mr Roma”aliongea Kim Jip mara baada ya kumsogelea Roma.
“Umeweza kumpata mtu alieigiza sura yako?”
“Hio ndio sababu ambayo imetufanya tuwe hapa Mr Roma , kwa majina naitwa Jang Yoon kiongozi wa idara ya uchugnzi ya kituo kikuu cha polisi Seoul , kulingana na uchunguzi wetu wa mwanzo dereva ambaye alipewa jukumu la kuendesha gari lililobeba moyo amesema wewe ni mtu pekee wa mwisho ambaye uliweza kukutana na mtuhumiwa , hivyo hili ni swali letu kwako , Mtuhumiwa yuko wapi?”
“Si alishakufa, hamkuweza kupata mwili wake? , alijiua yeye mwenyewe kwa sumu”Alijibu Roma huku akionyesha mshangao kidogo.
“Mr Roma tunataka majibu yako ya kweli , wewe ndio uliechukua moyo kutoka kwake hivyo lazima utakuwa umemuona , tafadhari tuambie yuko wapi mtuhumiwa?”
“Oh! Kwahio mnachojaribu kumaanisha ni kwamba hamjaweza kuona mwili wa mtuhumiwa?”
“Sisi ni polisi , unadhani tunaweza kudanganya juu ya hili , Bwana Kim Jip hapa na yeye atapenda kujua nani ambaye amehusika kuigiza sura yake”Aliongea yule polisi wa Kikorea na kumfanya Roma kujilaumu kwa maamuzi yake alioyafanya, mpaka hapo alijua kabisa waliokuwa nyuma ya Kim Jip feki watakuwa waliwahi eneo la tukio na kisha wakaondoa mwili na kwasababu ya kukosekana kwake kesi ni kama imemwangukia yeye.
“Dereva alithibitisha kama alimuona Kim Jip feki na sisi wakati tukiwa tunamuhoji ndio tulipoweza kusikia taarifa ya moyo umeweza kuufikisha hospitalini , kutokana na mlolongo wa matukio tunapata hisia za wewe kuhusika katika hilo, hivyo basi itakuwa vyema kama utakubali kwa hiari yako kuongozana na sisi mpaka kituo cha polisi ili kutoa maelezo yako rasmi”
“Hamuwezi kumchukua bila ya kuwa na ushahidi , Uncle Roma ndio ambaye ameokoa maisha ya babu yangu”Aliongea Yezi akimkingia Roma kifua.
Edna hakujua kinachoendelea kutokana na kwamba hakuwa akifahamu lugha ya Kikorea na ilibidi aombe kutafsriwa na Roma alimweleza kwa ufupi namna tukio lilivyotokea na kumfanya sasa kuelewa na kuwa na wasiwasi.
Jopo lote mpaka hapo waliweza sasa kujua kama ile ajali iliosababisha moyo kuchelewa haikuwa bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango wa watu na hamu yao yote ya kwenda kula ilipotea.
“Mr Roma ni mgeni wa heshima wa ukoo wa Park bila kushahau mchango wake mkubwa aliofanya kwa babu yangu kwa matibabu yake yake ,kapteni Jang nakushauri ufikirie mara mbili unachotaka kufanya”Aliongea Park Jonghyun.
“Bila kuwa na ushahidi wa kueleweka mtu wa mwisho kumuona mtuhudmiwa atageuka kuwa mshukiwa mkubwa wa kile kilichotokea , hivyo naomba ushirikiano wenu kwa jeshi la polisi la jamhuri ya Korea”Aliongea Kapteni Jang.
“Okey hakuna shida , kama unataka kuchukua maelezo yangu basi nitaongozana na wewe , hata mimi pia ninashauku ya kujua mwili umeenda wapi , hivyo nyie endeleeni kwenda kupata chakula na msiwe na wasiwasi”Aliongea Roma na kufanya kundi lote kukubali na Roma aliondoka na polisi.
Upande wa Edna alijua kabisa Roma hakuwa mhusika lakini hakupenda Roma kupelekwa kituo cha polisi.
Roma mara baada ya kuingia kwenye gari la polisi , liliondoshwa na kuelekea upande wa kusini mwa jiji la Seoul na baada umbali kama wa kilomita tatu gari ile ilikunja kulia na ilichukua njia ya pembeni likiachana na barabara kuu na kuingia upande wa viwanda.
“Ofisa Jang inashangaza kituo cha polisi kuwa maeneo haya ya Viwanda?”Aliuliza Roma ambaye muda wote alikuwa ametulia lakini wale mapolisi watatu walipotezea swali lake na gari likaendelea kuserereka
Upande wa Roma aliishia kutabasamu kifedhuli na kisha akakaa kimya kijua mwisho wake ni nini.
Baada ya muda kama dakika tano gari iliingizwa ndani ya eneo lenye ukuta kwa nje, sehemu ambayo ilionekana kuna ujenzi wa kiwanda unaendelea kutokana na uwepo wa magreda ambayo yanaanza kusawazisha ardhi ili kuweka msingi.
“Shuka chini”Aliongea polisi mmoja kwa namna ya kufoka kwa lugha ya kikorea.
“Hatuendi kituo cha polisi?”Aliuliza Roma mara baada ya kukagua mazingira.
“Kituoni kufanya nini?”
“Unamaaisha nini?”
“Kwasababu hapa ndio unakwenda kufia”Alijibu mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Jang.
Polisi wawili ambao walikuwa warefu walimsogelea Roma mara moja , kwa haraka haraka.
Roma aliweza kuona miili yao ilikuwa mikakamavu na kuhisia wanaweza kuwa na mafunzo ya kimapigano.
Lakini upande wa Roma hakuwa na hofu kabisa , kwanza kabisa alikubali kuondoka na polisi hao makusudi kwani alishaona nia yao ovu.
Walianza kumshambulia palepale, lakini kila pigo ambalo walijaribu kumpiga nalo Roma aliishia kukwepa na kumfanya yule polisi ambaye alikuwa kama kiongozi kujiunga pia kwenye kushambulia .
Mmoja wapo alileta teke la hewani la kitaekwondo akidhamiria kumpiga Roma shingoni lakini Roma kwa ustadi kabisa aliweza kukamata mguu wake wa kulia yule bwana na kisha akamzungusha hewani na kumtupia kwenye trekta.
Mwingine alijileta kizembe na Roma kwa kutumia mguu wake wa kushoto alimtegua goti pale na akadondoka chini huku akiugulia maumivu.
Jang Yoon alijawa na kiwewe na palepale alitoa bastora yake na kuikoki akitaka kumshambulia Roma kwani mpaka hapo aliona kabisa hakuna namna wanaweza kushinda kwa kupigana nae bila siraha.
Lakini kabla hata hajafyatua kiganja cha mikono yake kilifikiwa na kupindishwa na bastora ikadondoka chini na Roma akaipiga teke kwenda kutua mbali.
“Nyie watu najua mpo katika kundi moja na yule mwigizaji mwenzenu wa sura , si ndio?”Aliuliza Roma na kuwafanya wale mabwana kushindwa kutoa jibu lakini walikuwa wakikiona kifo chao usiku huo kipo karibu , kwani mtu aliekuwa mbele yao hakuwa wa kawaida.
“Nani kawatuma na mnatafuta nini? Nawapa nafasi ya kujibu la sivyo nitawanyonga mmmoja mmoja mpaka mniambie ukweli”Aliongea Roma lakini wale mapolisi walionekana kutotaka kujibu hivyo Roma alimsogelea mmoja ambaye alikuwa amejipigiza kwenye trekta na kumpiga karate ya uti wa mgongo na kilichosikika ni kuvunjika kwa uti wa mgongo na kufariki palepale.
Wale wawili waliobaki walijikuta wakijawa na hofu na kumuona Roma sio mtu wa kawaida kwa namna alivyommaliza mwenzao kikatili mno.
“Kwasabau wote nyie wawili mpaka muda huu hakuna ambaye amejiua kwa sumu hisia zangu zinaniambia nyie hamna mafunzo ya U’ninja, hivyo ni bora kujieleza mapema kabla sijatekeleza vifo vyenu kama mwenzenu”Aliongea na bado walionekana kusita sita na Roma alimsogelea mmoja kwa spidi na kumsukumia kwenye ukuta kwa nguvu akimnyonga shingo.
“Naomba uniache niondoke… sijui chochote tafadhari … sitaki kufa naomba usiniue”aliongea mwanaume yule kwa namna ya kujitetea.
“Nishakwambia nahitaji majibu ..”Aliongea Roma na palepale hakutaka kuendelea nae kwani alimvunja shingo na kumtupa chini.
Jang Yoon mara baada ya kushuhudia wenzake wote wakiwa wamepoteza maisha kirahisi aliangalia namna ya kukimbia na baada ya kupata upendo alitoka nduki , lakini Roma hakutaka kumpa nafasi na hakutumia uwezo wake wa kijini bali aliokota jiwe na kulivurumisha upande wake na kumpiga nalo mgongonni karibu na kiuno na kudondoka chini palepale huku akigulia maumivu na akamsogelea.
“Nitaongea , nitaongea tafadhari usiniue”Aliongea Jang Yoon huku kila akijaribu kusimama alikuwa akidondoka chini kwa mauamivu.
“Kwanini ulikuwa ukileta ugumu , pengine nisingechafua mikono yangu kwa kuuwa wenzako”Aliongea Roma kwa tabasamu lake la kuogopesha na kumfanya Jang Yoon kuanza kuinua mdomo wake kwa wasiwasi.
“Nime.. nimetokea katika umoja wa siri wa North Buyeo, yalikuwa ni maagizo tuliopewa kutoka kwa viongozi kukuleta hapa na kukuua kwani umeingilia mipango ya jamii yetu “Aliongea na kumfanya Roma kushangaa
“North Buyeo, unaongea ukweli?”
“Ndio , sisi ni Double agent ambao tumepandikizwa katika kituo cha polisi kufanya kazi kwa manufaa ya taasisi”
“Kwa maelezo yako unamaanisha mpo wengi zaidi , huenda kila nyanja ndani ya taifa, si ndiio? Kama ni hivyo wewe nafasi yako katika jamii hio ni ipi?”
“Nafasi yangu ni ya chini lakini sio chini kabisa”
“Nani mwingine anajua kuhusu hii taasisi ambaye yupo ndani ya kituo cha polisi?”
“Sina uhakika lakini mkuu wa kituo cha polisi ni mwanachama pia ambaye yupo ngazi ya kati”
Roma alishangazwa na ufunuo huo, mwanzoni alidhania labda ni kundi tu la maninja ndani ya Korea lakini mpaka hapo alijua kabisa sio kundi bali ni taasisi na kama ni hivyo mizizi yake ndani ya Korea itakuwa mikubwa mno.
Roma hakuwa na matamanio sana na taasisi hio kwasababu haipo nchini kwake na pia sheria hazikumruhusu kuingilia mambo ya binadamu wa kawaida , lakini kilichomfanya kutaka kuingilia ni kwasababu ya Yezi , kama moyo wa upandikizaji umechelewesha na taasisi hio moja kwa moja alijua kabisa hata Yezi pia anaweza kuwa katika hatari akiendelea kuishi Korea.
“Mr Roma ,, je naweza kuondoka?”
“Ndio unaweza kuondoka lakini nitakusindikiza”
“Hapana hapana , nitaenda mwenyewe”Aliongea huku akijikongoja kusimama na kuanza kusogea kuelekea getini , lakini Roma hakuwa na nia ya kumuacha aende hivyo alimsogelea na kummaliza palepale baada ya kumpiga ngumi ya utosini na kwasababu ngumi yake haikuwa ya kawaida kichwa chake kilichanguka paleplae na kumfanya nguo aliovaa kurukiwa na matone ya damu.
“Nilikwambia nitakusindikiza kuna haja gani ya kukimbia, haya umekufa sasa wasalimie kuzimu”Aliongea mwenyewe na kisha palepale akaita nguvu za kijini na kukausha miili yote kimazingara na sehemu ikawa safi bila ya kuacha ushahidi wowote kama kuna watu waliokufa katika hilo eneo,.
Baada ya kumalizana na maiti zao alifungua gari la polisi na kulichunguza na hakuona cha maana na palepale aliita moto wa kijini na gari lile lilipuka kama limetegeshewa bomu , lakini ulipukaji wake haukutoa sauti yoyote kutoka eneo hilo.
Baada ya kumalizana na tatizo hilo dogo alitoa simu yake na kumpigia Edna ,tokea wafike hapo Korea walisajili laini za mitandao ya nchi hio ili kurahisisha mawasiliano.
“Wife kazi imeisha , mpo wapi sasa hivi?”Aliongea Roma kwa kiswahili na Edna alishangazwa na maneno yake na kumwambia sehemu waliopo.
Roma mara baada ya kukata simu alitafuta namba ya simu ya Makedoni na kupiga palepale, aliamini swala kubwa kama hilo la jamii ya siri hawezi kulifanyia kazi yeye mwenyewe bila ya kuhusisha mtaalamu wa maswala ya ujasusi.
“Master Pluto nilikuwa nikipanga kwenda kuoga , unataka nikusaidie nini?”Aliuliza Sauroni upande wa pili mara baada ya simu kupokelewa.
“Nataka kujua kati ya watu wetu ambao wapo Korea kusini , mahsusi walipo ndani ya jiji la Seoul , naweza kuwapataje?”aliuliza Roma.
“Tuna wanajeshi wa kundi la Guerilla lakini wapo Korea ya Kaskazini,kuhusu Seoul sidhani kama kuna uwezekano wa watu wetu kuingia huko bila ya kushitukiwa kwani mipaka yao ina ulinzi wa viwango vya juu sana”Aliongea Makedon na kumfanya Roma kuona ni kweli Korea kaskazini ni mbali kuwaleta watu wake ndani ya Korea kusini.
“Pumbavu , kwanini hakuna watu wowote ambao mmewaweka Korea kusini?”
“Master Pluto nadhani unaelewa kwamba kuna mgogoro kati ya Korea kusini na Korea kaskazini , kama tutaweka watu wetu ndani ya Korea kusini hakuna faida yoyote kwani hakuna misheni ya kufanya , upande wa Korea kaskazini imekuwa rahisi kwani tunafanya na biashara ya siraha katika ukanda huo”Aliongea Roma na hakutaka hata kusikiliza zaidi ya kumpatia maelekezo ya kufatilia maswala ya North Buyeo halafu amtumie kwenye Email yake na kisha akatoweka katika eneo hilo.
Baada ya dakika chache aliweza kutokea katika mgahawa uliojengwa kitamaduni ambao familia ya Gong na ya Park walikuwa wakipata chakula cha usiku na baada ya kuona amerudi walimkaribisha kwa ukaribu na kumuonyesha sehemu kukaa chini kwani hakukuwa na viti.
Upande wa Park Jonghyun mara baada ya kumuona Roma alionyesha mshangao ulioambatana na mshituko na kumfanya Roma amwangalie na kisha kumuonyesha tabasamu la kejeli na kisha akaketi chini , ni kama alikuwa akimwambia kwamba anajua kile ambacho anafanya sirini.
“Mr Rom , unaonyesha haupo vizuri nadhani ni uchomvu wa wiki hii yote , lakini niseme asante sana kwa kumsaidia babu yangu kwani kama sio wewe hatujui nini kingetokea”
“Naamini maneno yako ni ya dhati bwana Jonghyun”aliongea Roma na kukaa katikati ya Edna na Clark,
Clark alikuwa ashabadili mavazi yake na yupo hapo kuungana na kila mmoja kusherehekea mafanikio yake ya kukamilisha upasuaji.
Chakula kiliendelea huku Roma akiwa bize kuongea na Clark ambaye muda wote alikuwa akimshukuru kwa kumsaidia kuokoa taswira yake kama daktari kwa kufanikisha kufikisha moyo ndani ya muda.
Upande wa Edna chakula hata hakikuwa kizuri kabisa kwake kutokana na namna ambavyo Clark anaongea kwa kujibebisha mbele ya mume wake na wivu ulimjaa mno.
Clark usiku huo huo alichukuwa nafasi ya kutoa taarifa anarudi Uingereza siku inayofuatia na jambo hilo lilimfanya Edna kupatwa na ahueni maana aliona kama akiendelea kubakia nchini hapo angeharibu furaha yake.
Baada ya chakula kila mmoja alirejea nyumbani na upande wa Roma na mke wake walirudi katika jumba la Park Juan.
Roma mara baada ya kuingia chumbani haraka alimwambia Edna ampatie Laptop kwanni kuna kitu anataka kufanya na Edna ambae alijinunisha njia nzima alimpatia bila ya kuongea neno.
Roma alielewa kinachomsumbua Edna ni wivu kutokana na namna alivyokuwa akiongea na Clark kwa kutaniana na kujibebisha.
Roma mara baada ya kuchukua laptop hio alifungua haraka haraka na kisha akaunganisha na mtandao kisha akafungua baadhi ya taarifa ambazo zimetumwa na Makedoni kwa njia ya barua pepe yake,alianza ku’scroll’ kwa kusoma kila kitu kwa umakini na alishangazwa mara baada ya kuona mawazo yake yalikuwa sahihi, North Buyeo halikuwa kundi la kawaida la sirii ndani ya Korea kusini.
SEHEMI YA 524.
Msingi wa jamii ya siri inayojiita North Buyeo ulianza zamani sana tokea kipindi cha utawala Goguryeo , wakati ambao Buyeo ilikuwa ipo upande wa Kaskazini mwa bara hilo la Asia.
Katika historia mara baada ya utawala wa Goguryeo kusimikwa rasmi, utawala wa kifalme wa Buyeo ulikufa na kubakia kama kundi la waumini tu ambao walikuwa na matamanio ya kurudisha nchi yao.
Sasa taarifa ambayo Roma alikuwa akisoma ni kwamba North Buyeo ni jamii ya watu ambao walikuwa wakibeba maono ya mababu na kutokana na mipango yao ndani ya taifa la Korea kusini na korea kaskazini walianza kujipenyeza katika nyanja zote za kitaifa.
Roma mara baada ya kusoma taarifa yote aliona ni mgumu sana kumaliza watu wote wanaohusika katika Buyeo licha ya kwamba ni tishio kwa usalama wa Yezi.
Muda huo wakati akiendeea kuwaza , Edna alikuwa ndio anatoka bafuni na kufanya eneo lote la chumba kuwa na harufu nzuri ya Shower gel huku akijifuta maji na taulo na Roma alimwangalia na kuishia kumeza mate kwani urembo wa Edna kwake ni kama unaongezeka kila saa anayomwangalia.
Edna baada ya kuona Roma yupo bize na tarakishi alisogea kuangalia ni kitu gani anasoma na alishangazwa na taarifa hio na kutaka Roma amwelezee kwanini anasoma hio taarifa.
“Norht Buyeo mbona ni kama mambo ya kihistoria kwannii unasoma?”Aliuliza
“Babe Edna , umejuaje ni mambo ya kihistoria?”
“Nakumbuka nishawahi kusoma kitabu kimoja ambacho kimeelezea hio historia , nadhamni unaelewa hobi yangu ya kusoma vitabu ”Aliongea na kumfanya Roma kweli aone inawezekana hata hivyo Edna kama CEO alikuwa akipenda sana kusoma ili kupanua ufahamu wake hususani katika maswala ya kibiashara.
Roma ilibidi mwelezee namna tukio lilivvyotokea masaa kadhaa yaliopita na hisia zake juu ya jamii hio kutishia usalama wa Yezi, Edna alishagaa na kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.
“Ni malengo gani wanayo hio jamii? Ni kheri kama watakuwa adui yako lakini kama wanataka kumdhhuru Park Juan basi haitakuwa salama kwa Yezi kuendelea kuishi hapa”
“Ndio maana kabla hatujarudi Tanzania napaswa kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu hii jamii na kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba Park Jonghyun ni mwanachama pia”Aliongea Roma na Edna alikubaliana nae kwani hakuwa tayari kuona Yezi anapatwa na shida ili hali kwake alikuwa akimchukulia kama mdogo wake.
“Wife una akili nyingi sana , nilidhania huna uelewa wowote kuhusu maswala ya kiihistoria ya nchi za huku, umenizidi hata mimi ambaye leo hii ndio kwanza najua maswala ya Buyeo kuwa katika historia ya kikorea”
“Lakini ni dhahiri simfikii Clark , ana akili nyingi na ana kipaji kikubwa mno?”Aliongea Edna huku akionyesha kabisa bado alikuwa na kisirani..
“Edna mke wangu , kwanini mpaka sasa una wivu, Clark na mimi hakuna kinachoendelea zaidi ya kwamba alikuwa kama mdogo wangu ambaye nilimuona akikuwa mpaka kufikia utu uzima ndio maana anakua huru akiwa mbele yangu”
“Ulimuona?, kama ni hivyo wakati huo wewe ulikuwa na miaka mingapi na yeye alikuwa na mingapi?”
“Yeye alikuwa na miaka kama nane au tisa hivi na mimi nilikuwa na miaka kumi na nne kwenda kumi na tano”
“Kama ni hivyo kwanzia sasa nataka nikuwekeee mipaka , kumuona akikua haimaanishi kwamba ndio umfanye awe mpenzi wako wa utotoni”Aliongea kikauzu na kisha alichukua rimoti na kuwasha Tv.
Na Roma alishindwa kujielezea zaidi maana Edna maneno yake ni kama hayaamini kabisa kila anapomuambia hakuna mahusiano.
Hofu ya Edna ilikuwa ni kwamba Clark ukiachana na kwamba alikuwa mrembo karibia kumfikia yeye , lakini pia alikuwa na akili nyingi na huenda ana msaada mkubwa kwa Roma kuliko yeye mwenyewe hivyo hofu yake ni kupinduliwa .
Wanawake wengine hakuwa na hofu nao kutokana na kwamba walikuwa wa kawaida sana na siku zote wapo chini yake na anaweza kuwamudu lakini kwa Clark ilikuwa tofauti.
Mtu mwingine ambaye alikuwa akiogopa Roma kuanzisha nae mahusiano ni Sophia.
Sophia anaweza asiwe na kitu kikubwa kama yeye , lakini likija swala la uzuri walikuwa wakikaribiana sana na yeye na Edna alikuwa amenuia kwenye moyo wake hatokaa aone mahusiano kati ya Roma na Sophia yanatokea.
Muda huo huo wakati Roma na yeye akijiandaa kwenda kuoga , walisikia mtu akigonga mlangoni na kumfanya Edna amwangalie Roma kwani haikuwa kawaida kwa kugongewa muda huo.
Roma alisogelea mlango na kufungua na aliweza kukutana na mwanaume ambaye amevalia mavazi ya suti yenye nembo maalumu kumtambulisha ni mfanyakazi wa hapo ndani.
“Mr Roma ,Mrs Edna kila kitu kipo sawa?”Aliuliza kwa lugha Kikorea.
“Wewe ni nani?”Aliuliza Roma na kumfanya yule bwana kushangaa.
“Mimi ni mlinzi katika hii nyumba na dakika chache zilizopita niliweza kusikia purukushani ikitokea upande huu ndio maana nimewagongea kuona kama mpo sawa”Aliongea
“Kama ni hivo kwanini umeshikilia kisu mkononi na kukificha au upo hapa kwa ajili ya kutuua?”Aliuliza Roma na ku,fanya yule bwana kushangazwa na jambo hilo , kwani hakujua Roma ameonaje kisu aina ya daga alichoshikilia kwani aliificha vyema kwa kukibana na ukuta.
Lakini hata hivyo hakuwa na muda wa kupoteza baada ya kuona mpango wake ushagundulika hivyo alitoa mkono kwa haraka na kuipeleka ile Daga usawa wa kifua cha Roma , lakini Roma kutokana na wepesi wake aliwahi kushikilia mkono wake ulioshikilia kisu na kuupindisha na kumfanya yule bwana kutoa ukulele na kukidondosha chini.
Edna ambaye macho yake yalikuwa kwenye runinga alishangazwa na purukushani hizo na kusimama kwa wasiwasi
“Wewe ni nani? North Buyeo wamekutuma?”aliuliza Roma.
Yule mwanaume alionekana kuchezesha meno yake palepale mara baada ya kuona amekamatika , lakini Roma alitegemea hilo hivyo alimuwahi kwa kumpiga shingoni na kumfanya palepale kupoteza fahamu.
Dakika hio hio Roma aliweza kusikia purukushani zingine zikisikika kutoka juu na mpaka hapo alijua wapo wengi zaidi.
“Edna kuwa makini , ngoja nikamwagalie Yezi inaonekana wapo wengi”Aliongea Roma na kwa haraka alitoka hapo akihofia Yezi anaweza kuwa katika hatari.
Muda uleule aliweza kutokea mbele ya chumba cha Yezi sehemu ambayo ndio aliweza kusikia sauti.
Muda huo Roma aliweza kushuhudia kijakazi wa kike akipigana na kijakazi mwingine wa nyumba hio, alikuwa ni kijakazi afahamikae kwa jina la Eujung msaidizi wake Yezi.
Eujung alionekana kuwa vizuri kwenye mapigano na Roma palepale aliweza kugundua huenda alikuwa na mafunzo ya juu ya Taekweond kwani hata mpinzani wake hakuwa haba lakini alikuwa akionyesha kumdhibiti vizuri.
Eujung hakuwa mzembe baada ya kukwepa mapigo mawili , alipiga sarakasi mzunguzo ambayo ilimpiga yule adui mtama na akadondoka chini na kabla hajamka , Eujeong tayari amekwisha kupiga teke lingine la shingo na kumlegeza kabisa na kumuweka chini ya ulinzi.
Roma alishangazwa na jambo hilo kwani hakutegemea kuona msichana wa kikorea aliekuwa mpole na kijakazi wa familia hio alikuwa na uwezo mkubwa kama huo , aliona huenda yote hio ni mipango ya Park juan babu yake Yezi kuhakikisha mjukuu wake anakuwa chini ya ulinzi mkali.
Eunjung alikosa umakini na adui yake na ghafla tu yule Ninja aliamka kwa mara nyingine na kutaka kumchoma na kisu tumboni na Roma palepele kwa haraka sana alimkaribia kijini na kumzuia kwa kumpiga utosini na palepale alilegea na kudondoka chini na ukawa mwisho wa uhai wake.
“Asante sana Mr Roma kwa msaada wako”Aliongea Eunjung na muda uleule Yezi aliekuwa akitetemeka aliweza kufungua mlango.
“Oh asante umekuja , naogopa mimi”Aliongea Yezi kwa hofu kubwa.
“Upo na Eujung hapa kwanini unapatwa na hofu wakati yupo vizuri kwenye kukulinda?”
“Sikujua hata kama anajua kupigana , babu nilimwambia sitaki mabodigadi na akinniahidi hatoniwekea , lakini inaonekana alinidanganya”
“Usikarisike Miss , Master kafanya yote kwa ajili yako”
“Sio kama nakasirika, asante kwa kuweza kuyaokoa maisha yangu”Aliongea na Eunjung alitingisha kichwa kukubali shukrani yake.
“Kama hapa kumefanyika mashambulizi vipi kuhusu hospitalini?”Aliuliza Eunjung kwa wasiwasi.
Eunjung kuongea hivyo hata Roma aliona uwezekano wa kushambuliwa kwa wakati mmoja hapo nyumbani na hospitalini ni mkubwa , lakini hata hivyo asingeweza kuondoka na kuelekea huko kwani bado usalama wa Yezi na Edna ulikuwa juu yake.
Edna alikuwa katika levo ya mwanzoni katika nusu mzunguko hivyo aliona hata kama anaweza kuweza kujilinda lakini hana uzoefu na kama atakutana na adui ambaye ana siraha kama bastora basi moja kwa moja angemdhuru.
Muda huo huo Edna alitoka na kuja mahali walipo huku akiwa ameshikilia simu ya Roma.
“Hubby simu yako inaita?”Aliongea na Roma alimsogelea na kuichukua na kisha akpokea palepale.
“Mr Roma nimeshangazwa sana kuona mpaka sasa bado upo hai?”Sauti ilisikika kwa lugha ya kikotea.
“Wewe ni nani au ndio nyie North Buyeo?”
“Mhh.. umetisha sana Mr Roma , mbali kabisa na matarajio yangu”
“Unataka nini kutoka kwangu?”
“Labda hujagundua kitu bado lakini kabla hamjarudi hapo nyumbani tayari mpango ulikuwa ushaandaliwa na hospitalini pia kwa wakati mmoja , kwa ajili yako Roma tutahakikisha unaendelea kuburudika kile tulichokupangia”Aliongea mwanaume huyo kwa sauti yake ya besi huku akicheka kicheko cha dharau.
“Nadhani mpango wako ni kulipua hii nyumba si ndio?”
“Upo sahihi , nyumba yote tushatega mabomu ya ukubwa wa C4 yanayotosha kutengeneza wingu kubwa la mlipuko na kuharibu jumba lote”
“Pumbavu zenu nyie wakorea naona mnaona mambo yanaweza kufanikiwa kirahisi hivyo , mnafikiri mnaigiza muvi sio? Hamchoshwi na huo upuuzi wenu?””
“Kama kitu hakivunjiki kuna haja gani ya kukirekebisha, Mr Roma kama hutaki kuona hio nyumba ikilipuka na mkeo pamoja na mdogo wenu Yezi kuangamia basi hakikisha unafanya kama tunavyokuelekeza”ilisikika sauti.
Roma hakuwa na wasiwasi hata hivyo na vitisho vyao kwani alikuwa na uhakika wa kuwakoa Edna na Yezi kwa wakati , lakini bado jambo moja ambalo lilimpa mashaka ni upande wa hospitalini lazima na penyewe kuna mtego ambao umetegwa.
“Mnataka nifanye nini?”
“Ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kutoka mpaka nje na utaona gari aina ya BMW sedani nyeusi , ingia kwenye hio gari na endesha mpaka hoteli ya Myeondong kuna watu watakupokea hapo”Aliongea mwanaume huyo upande wa pili na Roma alikubali.
“Nini kinaendelea, ni watu kutoka North Buyeo?”aliuliza Edna na kumfanya Roma kucheka na kisha alimsogelea sikioni na kumnong’oneza.
“Utafanya kazi?”Aliuliza Edna huku akikunja ndita.
“Hio itategemeana na wewe CEO Edna , una uwezo mkubwa wa kuigiza hata wa kunidanganya mimi kwanini tusifanikiwe”Aliongea Roma ilionyesha kuna mpango ambao walikuwa wakipanga na Edna ni sehemu ya kuukamilisha.
“Kuwa makini sasa , tutaendelea kufuata mpango wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma amshike Edna mashavu kama mtoto na kisha alitoka hilo eneo na kuanza kushuka kwa ngazi kuelekea chini.
“Anaenda wapi?”aliuliza Yezi.
“Tumepewa maagizo kutoka kwa watu waliotuma wauaji hapa na wanataka Roma afuate maagizo yao la sivyo hii nyumba na jengo la hispitali alilolazwa babu yako litalipuka kwani kumetegewa mabomu”
“Kwanini wanataka kufanya kitu kama hicho?”Alilalamika Yezi na muda huo huo mabodigadi waliingia ndani ya nyumba hio na kuizingira huku wakimpa ulinzi Yezi.
Kwasababu walikuwa aneo la juu katika Lounge waliweza kumuona Roma akitokea nje ya geti na kuingia kwenye gari ambayo imegeegeshwa na baada ya kuiwasha kwa kutoa mwanga wa taa palepale ulitokea mlipuko wa aina yake.
“BOOM!!”
“Mama..!! ulikuwa ni mtego”Aliongea Eujung kwa kikorea huku akishindwa kuzuia mshituko wake mara baada ya kuona gari lililipukaRoma akiwa ndani na kuishia kushika mdomo
“Uncle Roma…!!Yezi alijikuta akitoa ukulele akiwa kama mtu ambaye haamini macho yake.
Muda huo huo magari yaliokuwa yapo karibu na hayo maeneo yalianza kulia alarm baada ya mlipuko huo kutokea,
Haikuchukua muda mrefu mara baada ya mlipuko gari nyingine nyeusi kampuni ya Honda ilifika katika hilo eneo na walitoka wanaume waliovalia suti na kuanza kuchunguza gari hio inayowaka moto.
Edna na yeye aliekuwa ameona tukio hilo aliishia kutoa machozi huku akiwa amesimama kama sanamu.