kip-korir
JF-Expert Member
- Sep 5, 2023
- 275
- 467
275 duh!SEHEMU YA 274
Roma hakutaka kumdhuru Raisi Jeremy , alichokifanya ni kujaribu kumuonya tu na ndio maana baada ya walinzi kuingia alimwachia na kisha kutoka , walinzi walitaka kumzuia Roma , lakini Raisi Jeremy aliwapa ishara ya kumuacha aondoke zake.
Mazungumzo yalianza kwenye muda wa saa kumi na mbili hivyo mpaka Roma kumaliza kuongea na raisi Jeremy ilikuwa ni saa kumi na nusu ikimaanisha kwamba wametumia lisaa limoja kumaliza maongezi yao.
Roma hakutaka kurudi moja kwa moja nyumbani, mudi yake haikuwa nzuri kwani maongezi yanayomhusu Seventeen mara nyingi yanapozungumziwa huwa yanaharibu kabisa mudi yake na anakuwa mwenye mawazo na ndio maana alijiambia atafute sehemu tulivu kwa hapo Kigamboni kwa ajili ya kutuliza kichwa.
Mikadi Beach ndio sehemu ambayo aliona inamfaa kwa kupotezea muda, hakuwahi kufika ila alitumia uwezo wa gari yake kutafuta uelekeo na ndani ya dakika moja tu alikuwa ashakaribia.
“Kaka samahani nipo hapa kwa ajili ya kuwa peke yangu sihitaji kampani”Ilisikika sauti ya mwanamke mrembo ndani ya fukwe hii ya Mikadi, mwanamke ambaye kwa siku hio alionekana kama kivutio kwa wanaume wengi waliokuwepo hapo na kwa jinsi mwanadada huyu alivyokuwa akilalamika ni dhahiri kabisa kwamba amesumbuliwa na wanaume wengi sana tokea ajipumzishe, na hii lilidhihirika kwani alimkataa mwanaume aliehisi uwepo wake pembeni yake pasipo kumwangalia usoni , kwani muda huo mrembo huyu alikuwa amejifunika usoni na kofia yake aina ya Hat huku akiwa ameegamia kwenye viti vilivyojengwa ndani ya eneo hili kwa ajili ya mapumziko.
“Babe Nasra inaonekana Mungu ndio kanileta hili eneo”Aliongea Roma na kumfanya mrembo yule kutoa ile kofia na kumwangalia mwanaume eliekuwa mbele yake , mwaaume ambaye alimkataa sekunde kadhaa zilizopita kwa kumdhania kuwa ni walewale wanaume ambao walikuwa wakimsumbua , ndio alikuwa ni Nasra.
“Roma! , Unafanya nini hapa?”Nasra aliuliza kwa mshangao huku akimwangalia Roma aliekuwa mbele yake , ni kama hakutegemea kabisa kumuona na mapigo ya moyo wake yalienda mbio.
“Oya nadhani yule ndio mwenye mali wazee”Sauti upande wa pili ilisikika kwenye meza ambayo imekaliwa na vijana wanne ambao walikuwa wapo hapo Ufukweni kupunga upepo kwa siku hio ya Wikiend.
“Daah! Wanawake bwana , kama ni kweli basi hawa viumbe sio wa kueleweka kabisa yaani ananikataa mwanaume Hb kama mimi halafu awe na mwanaume kama yule”Aliongea mwanaume mmoja kuunga mada na alionekana alikuwa ametupia ndoano kwa Nasra na akachomolewa na sasa yupo kwenye mshangao baada ya kuona Nasra anatoka ushirikiano kwa mwanaume ambaye hakuwa na mwonekano mzuri kama wake.
“Haha.. hivi viumbe wewe achana navyo kabisa Abduli, kila mtu na bahati yake”Aliongea na kufanya wenzake kucheka na kisha waliendelea kuangaliia upande ambako mwanaume ambaye hawakumfahamu akiongea na mrembo waliemshindwa.
Upande wa Nasra alionekana kutomtegemea kabisa Roma eneo hilo na ndio maana alishangaa uwepo wake.
Nasra Baada ya kumsindikiza rafiki yake Najma kuondoka kuelekea masomoni nchini Marekani hakulala nyumbani kwake kabisa , akili yake haikuwa imetulia na alikuwa kwenye mawazo na ndio maana aliamua kutafuta sehemu ya kutulia na , sehemu ambayo aliona inafaa ni Mikadi Lodge na ndio maana hata Roma jana yake alivyoenda nyumbani kwa Nasra hakumkukuta.
“Babe Nasra unajua ni kwa kiasi gani nimekutafuta?”Aliongea Roma huku akikaa kwenye kiti cha pembeni na Nasra muda wote alikuwa akimwangalia Roma , ni kama mambo mengi yalikuwa yakipita kwenye kichwa chake na hakuwa na namna ya kuelezea.
“Roma naomba uondoke”Aliongea Nasra kwa sauti ya chini na kumfanya Roma kutabasamu aliona mrembo huyu bado yupo na hasira na yeye na hilo hakujali hata kidogo na alijiambia huo ndio muda mzuri wa kuyajenga.
*******
Upande mwingine Edna alionekana akipitia karatasi zilizokuwa kwenye mikono yake , swala la Kampuni ya Maya bado lilikuwa likimuumiza sana kichwa na hii yote ni mara baada ya kugundua kuwa jina la kampuni hio lipo kwenye orodha ya kampuni zilizoorodheshwa kwenye nyaraka ambayo mama yake ameacha nyuma , orodha ya kampuni ambayo aliitafsiri kama sehemu ya malipizo ya kisasi ambacho alikuwa nacho mama yake Raheli na yeye mwenyewe hakufahamu ni kisasi juu ya nini.
Alijiambia lazima kuna kitu kilitokea kati ya kampuni hii ya Maya na mama yake na ndio maana ilikuwa kwenye orodha , lakini mpaka muda huo hakuwa akifahamu ni muunganiko wa namna gani ambao upo na ndio maana alijiambia ni lazima atumie akili zake zote na rasilimali alizokuwa nazo kutafuta muunganiko huo.
Alijikuta akiangalia baadhi ya vitabu vilivyopangwa kwenye chumba hiki ambacho kilikuwa ni kama ofisi ya mama yake hapo kabla na kujikuta akiingia kwenye mawazo, ukweli akili yake ilikuwa imekwama kabisa kwani licha ya kwamba Suzzane amemtumia baadhi ya taarifa kwa kile kinachoendelea kwenye kampuni ya Maya lakini bado hakukuwa na muunganiko na kwa jinsi alivyokuawa akiangalia Shelf hizo zilizojaa vitabu ambavyo mama yake siku zte alikuwa akisoma ni kama alikuwa akitafuta wazo jipya.
Kampuni ya Maya ni kampuni ambayo inajihusiha na mambo mengi na hii ni kutokana na kuwa na ‘Subsidiaries’ nyingi ndani ya taifa la Afrika , ni kampuni ambayo ina makao makuu yake nchini India na inawekwa na majarida mbalimbali ulimwengu kama moja ya kampuni kubwa sana ambayo inaongoza katika maswala ya utafiti na utengenezaji wa madawa duniani na moja ya mafanikio yake makubwa yalitokana na kufanikiwa kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa Ebola kupitia kituo chake cha utafiti kilichopo ndani ya taifa la Canada.
Mwaka 2001 ndio mwaka ambao walifungua tawi la kampuni yao hapa Tanzania na moja ya sababu kubwa ya mwanzilishi wa kampuni hii kupenda kufungua tawi hapa Tanzania ni kutokana na kwamba mke wake mkubwa alikuwa ni Mtanzania hivyo ni kama alifungua tawi hilo kwa heshima ya mke wake kuwa raia wa Tanzania.
Maya Hubat licha ya kwamba alikuwa mhindi , lakini pia alikuwa akilipenda sana Taifa la Tanzania na mara nyingi amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Tanzania hasa upande wa tiba , kwani mara nyingi alionekana akichangia sana michango katika hospitali nyingi lakini jambo kubwa pia kwa Kampuni ya Maya pia wanazo hospitali maarufu sana ambazo zimetapakaa kwenye mikoa yote mikubwa Tanzania.
Hivyo ni rahisi kusema kwamba heshima ya Mzee Maya imetokana na michango yake lakini pia uwekezaji wake hapa Tanzania,maswala hayo yote Edna alikuwa akiyafahamu na hata nyaraka zilizokuwa kwenye meza yake zilikuwa zikisema hivyo , alisoma kila kitu kilichokuwa kikihusiana na kampni ya Maya lakini hakuishia kwa kampuni ya Maya tu , lakini pia alisoma na mwanzilishi wa makampuni haya ya Maya na nia zake zote za kupendelea taifa la Tanzania katika maswala ya uwekezaji , lakini licha ya Edna kusoma nia halisi ya Mzee Maya kwa hapa Tanzania katika swala la uwekezaji , aliona kuna jambo ambalo bado halikai sawa, ni kweli kwamba Mzee Maya ameoa Tazania na mara nyingi amekuwa mtu wa kujinasibu kama moja ya watu wanaolipenda tafai la Tanzania kwani limempatia mke bora , lakini hata hivyo aliamini ni kama jambo la ziada kwa hayo yote , Edna alikuwa mfanyabiashara na siku zpte ukifikiria kibiashara Zaidi utajua kwamba kuna baadhi ya uwekezaji hata kama una mapenzi mengi na taifa husika huwezi kuufanya kwani hauwezi kukuletea faida Zaidi ya hasara na hili ndio aliliona kwa kampuni hii ya Maya , Mzee Hubati kuna uwekezaji ambao amefanya hakuona tija yake na kama yeye ndio mwamuzi mkuu basi asingejihangaisha kabisa katika kuwekeza hapa nchini na hili ndio lilimfanya aone kuna Zaidi ya sababu katika juhudi za kiuwekezaji kwa Mzee Hubati na alitaka kuzifahamu.
Edna wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo , akili yake ilikuja kutua kwene moja ya kitabu kilichokuwa kikionekana wazi upande w akushoto kwenye shelf , kitabu ambacho mara baada ya kukiona alikumbuka mama yake mara nyingi alimuona akiwa amekishikilia akikisioma enzi za uhai wake, alikiangalia kwa dakika kadhaa kabla ya kufanya maamuzi ya kunyanyuka alipokuwa amekaa na kukisogelea na kukitoa kwenye shelfu na kurudi nacho kwenye meza yake na kuketi kwa ajili ya kukifungua na kuanza kukisoma , alikuwa akitamani kujua ni kitu gani ambacho mama yake alikuwa akikisoma mara kwa mara.
“One of her favourite book”Aliwaza kwenye kichwa chake akisema kwamba moja ya kitabu pendwa cha mama yake huku akigeuza geuza, baada ya dakika kadhaa ya kukigeuza aliamua kukifungua.
“Kumbe mama alikuwa ni mpenzi wa Mashairi?”Aliwaza Edna baada ya kugundua kuwa kitabu ambacho amekishikilia kina mkusanyiko wa mashairi ambayo yamewahi kuwandikwa duniani, ukweli mwanzoni hakuwa akijua kitabu hiko kilikuwa kikihusiana na nini kutokana na kutokuwa na kava ambalo lilikuwa likielezea nini kimeandikwa ndani yake , hivyo baada ya kufungua ndio aligundua kumbe ni kitabu ambacho kilikuwa kikihusu mashairi.
Edna wakati anafungua ukurasa wa pili kuna kitu kilidondka chini na kumfanya akiangalie na alikuja kugundua ilikuwa ni picha , aliweka kitabu chini na kuiinua na kuishikilia na kukuta sura ambayo inakuja na kupotea kwenye kichwa chake ni kama mtu aliekuwa kwenye picha alikuwa akimfahamu lakini hakuwa akikumbuka amemuona wapi, aligeuza nyuma ya picha hio na kuona kuna maandishi yalioandikwa.
“Sonnet 116 by Shakespeare , I dedicate it to you Rahel My Love”Ndio mwanzo wa maneno yaliosomeka juu ya picha alioshikilia Edna , maandishi ambayo yalikuwa yakimaanisha kwamba “Najitolea kukupa shairi hili mpenzi wangu Rahel, shairi la Sonnet 116 kutoka kwa mtunzi Williams Shakespeare.
Edna alijikuta akshangaa na hisia zake tayari zilimwambia mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni mpenzi wa mama yake na moyo wake ulipiga kite , kwani maandishi yaliofuatiwa yanayohusiana na shairi hilo yalidhihirisha upendo wa dhati sana kutoka kwa mwanaume aliekuwa kwenye picha kwenda kwa Rahel mama yake.
“This guy could be my father”Aliongea Edna akimaanisha kwamba mtu aliekuwa kwenye picha anaweza kuwa ndio baba yake.
SEHEMU YA 275
Saa moja na nusu ndio muda ambao Roma alirejea nyumbani , alionekana mudi yake imerudi na hio yote ni kutokana na kwamba yeye na Nasra mapenzi yao yamerudi kama zamani na ashatuliza hasira zote za mrembo huyo na mipango yao ya kwenda kijijini ilikuwa ikiendelea na zilikuwa zimebaki takribani wiki mbili mpaka kufikia siku yenyewe.
Mama yake Roma siku hio alionekana hakuwa nyumbani, lakini hakujali sana , Edna alionekana kuwa sebuleni akiwa ameketi pamoja na Yezi , Sophia na Bi Wema na walionekana walikuwa wakipiga soga na Roma alitabasamu kuona wanaendana vizuri na mke wake yupo kwenye hali ya kuchangamka.
Ukweli ni kwamba Edna hakumjua mwanaume aliekuwa kwenye picha , ni kweli sura yake ilikuwa ikija na kupotea lakini hakuweza kuitambua na kukumbuka aliiona wapi , hivyo hakutaka kusumbua kichwa chake , kuna hisia ambazo zilikuwa zikimwambia kuwa mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni baba yake , lakini aliamua kupotezea , kwanza hakuwa na mpango kabisa wa kumfahamu baba yake na alijiambia labda baba mwenyewe ndio amtafute yeye , mrembo huyu hakujua kuwa mume wake Roma Ramoni alikuwa na maongezi mchana huo na baba yake mzazi , baba ambaye amemkataa mbele ya mume wake.
Sasa Edna aliona asiendelee kukaa zake chumba cha kujisomea na aungane na wanafamilia sebuleni.
“Roma jumatatu Yezi anatarajjia kuanza kufanya usaili Kwenda chuo , unapaswa kumsindikiza”Aliongea Edna na Roma alishangaa kidogo , ukweli mara nyingi ni kama Yezi alikuwa akimwepuka hivyo hakupata wasaa mwingi wa kuongea nae tokea warudi Ufarnsa na kumkuta nyumbani.
“Yezi umepata chuo gani?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Yezi , lakini Yezi alikuwa ni kama anamshangaa Roma.
Ukweli ni kwamba Yezi alikuwa akiangalia kicheni ambacho kipo kwenye shingo ya Roma na hii ni baada ya Roma kuinama wakati wa kukaa na ndipo kiliponekena , kidani ambacho yeye alimpatia kama zawadi, jambo lile kwake limemgusa sana kwani hakuamini kama Roma anaweza kuthamini zawadi yake na kuivaa shingoni.
“Mbona hunijibu unaniangalia tu”
“Kapata UDSM , yaani wewe Yezi ni mwanafamilia lakini umeshndwa hata kufuatilia maendeleao yake”Aliongea Edna na kumfanya Bi Wema kutabasamu namna Edna anavyomkosoa Roma na Roma lilimwingia kweli , kwani ni kweli hakuwa akifatilia sana maendeleo ya Yezi na ndio maana hata hakufahamu ni chuo gani ambacho Yezi amepata lakini ni wakati gani amabo Yezi kaanza kufanya maombi.
“Ni sawa tu Sister Edna , Anko ana mambo mengi”aliongea Yezi kwa namna ya kumtetea Roma na Edna alitaka kuongea neno ila alijiambia ngoja anyamaze.
“Okey wife Yezi mimi nitampeleka chuo siku ya jumatatu na kuhakikisha kafanya usaili”Aliongea Roma na Yezi alitabasamu.
“Simuoni mama, kaenda wapi?”Aliuliza Roma.
“Kaenda kumsalimia MzeeAtanasi, baba yake”Alijibu Edna na Roma alitingisha kichwa kuashiria kwamba ameelewa.
********
Kila mmoja alitamani kusikia jibu litakalotoka kwa Sheikh Assad , swali ambalo ameulizwa na Zoe Kovac kwanini Hades wa Zamani aliamua kujidhihirsha kwake ilihali hakufanya hivyo kwa wengine kama vile Pastor Cohen ambaye alionekana kuwa ni mtu muhimu katika mipango yake.
“Sababu ya Hades wa zamani kujionyesha kwangu , huenda ikawa ni kutokana na kazi kubwa ambayo alinipatia kuliko watu wote mliopo hapa ndani na wale ambao hampo hapa ndani , najua kila mtu amefanya kazi ambayo ina mchango mkubwa katika mipango ya Hades wa zamani kwa kila mtu na nafasi yake , lakini kwa upande wangu kazi yangu ilikuwa kubwa mno na nilikataa kuifanya mpaka ajionyeshe kwangu”
“Unamaanisha kwamba Hades , alikupa kazi kubwa kiasi kwamba ulikataa kuifanya na ukataka kwanza ajionyeshe kwako?”Aliuliza Pastor Cohen , ukweli ni kwamba hakujua kama kuna mtu ambaye anaweza kumzidi yeye kwa kufanya kazi ngumu , misheni zote ambazo zinaendelea mpaka kwa wakati huo Pastor Cohen aliamini zilianzia upande wake.
“Ndio kazi alionipa ilikuwa ngumu katika utekelezaji wake , kwani ilikuwa ni ya hatari , ya kujishusha, kudharaulika nahata kuonekana kichaa muda mwingine , hivyo ilihitaji uvumilivu mwingi”Aliongea.
“Ni kazi gani ambayo alikupatia ?”Aliuliza Afande Kweka aliekuwa kimya muda wote akigusa gusa ndevu zake zenye mvi.
“Najua wengi wenu hapa mnaamini kwamba nyie wote ni wanachama lakini hamjawahi kufahamu mpo kwenye chama gani mpaka mkaitwa kuwa wanachama na hii ndio ajenda kubwa ambayo imenileta hapa Afrika na kupitia Ajenda hio mtaweza kuelewa ni ipi kazi yangu ambayo nilikuwa nikifanya tokea nifike ndani ya mataifa ya Uarabuni”Aliongea na kisha akavuta pumzi ili kuendelea.
“We Are Ant-Illiminat Society”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa kwani ni kama hawakumuelewa kasoro upande wa Cohen.
“Nadhani sio mara yenu ya kwanza kusikia neno ‘Illuminat’ lakini ni mara yenu ya kwanza kusikia neno Ant-Illuminat?”Aliuliza Sheikh Assad na kunfanya wote hapo ndani kuangaliana , ni kweli walikuwa wakisikia juu ya neno Illuminat , lakini hawakuwahi kusikia neno la Ant-Illuminat.
Ant-Illuminat ni neno ambalo linamaana ya kinyume na neno lenyewe la Illuminat , yaani wapingaji wa jamii ya siri ya Illuminat ndio chama ambacho sheikh Assad alikuwa akizungumzia.
“Lazima tuelewe historia ya Illuminat kabla ya kuwa mwanachama halisi wa Ant-Illuminat , lakini sio hivyo tu ili uweze kuwa mmoja wapo wa jamii hii ya siri itakubidi kwanza ujue kila kitu kuhusu Illuminat na hii ndio kazi yangu ambayo nilipewa na Hades, kazi ya kujiunga na Illuminat.
“Your are Illuminat?”Aliuliza Mellisa kwa mshangoa.
“Yes , I am”Pastor Cohen alishangaa.
“But I am also Ant-Illuminat”Aliongea.
Mpaka hapo ni kama sasa wanaanza kupata picha ya kwanini Sheikh Assad alisema kazi yake ni ngumu sana kuliko wengine wote.
“Sheikh tupo kwenye kiza mpaka sasa , na nadhani litakuwa jambo jema kama utatuweka wazi , ili kila mmoja wetu apate kuelewa.”Aliongea Pastor Cohen na kumfanya Sheikh Assad kukubali na kuanza kuelezea.
Kwa maelezo yake ni kwamba baada ya kuokolewa na Hades wa Zamani na kupelekewa nchini Saudi Arabia kitu cha kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha Sheikh Assad kutoka kwenye hatia ya kutafutwa na CIA Pamoja na FBI na hilo kutokana na kwamba Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa upande wa mataifa ya kiarabu , hivyo kuongea na serikali ya Marekani kwa ajili ya kumfutia kesi Profesa Assad lilikuwa jambo jepesi sana ,h na serikali ya Saudi iliweza kufanya hivyo kutokana na uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya mfalme wa Saudi na Hades wa zamani.
Anasema baada ya kuisha kwa kesi hio ndio mwanzo wa kazi mpya ambayo alipewa kuikamilihsha naHades ama moja ya misheni yake na kazi yenyewe ilikuwa ni juu ya kujiunga na jamii ya siri ya Freemason.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba Illuminati ipo ndani ya ufreemason , hivyo kujiunga kwake ndani ya jamii hii ilikuwa ni kwa ajili ya kazi moja tu , kutambua wanachama wote waliokuwa na asili ya Illuminat na hio ilikuwa kazi ngumu sana kwake kutokana na usiri wa jamii hizi.
Sheikh Assad baada ya kufanikiwa kujiunga na jamii hio alipewa kazi nyingine ya kushawishi mataifa ya kiarabu kuanza uwekezaji nje ya mipaka yake, hii haikuhusisha serikali tu bali mpaka kwa sekta binafsi, kwahio kazi hioi ilikuwa ikimaanisha kwamba ashawishi matajiri ambao wapo kwenye serikali za kiarabu kuanza kuwekeza kwenye mataifa makubwa , hususani yale yenye uchumi mkubwa , ikumbukwe mataifa ya kiarabu kwa asilimia kubwa wamejaaliwa utajiri wa mafuta hivyo kuwa na matajiri wengi ambao hawakufahamika kabisa duniani, hivyo kazi ya Assad ilikuwa ni kushawishi sasa hao matajiri.
Anasema kwamba licha ya kwamba ilichukua muda mwingi kufanikiwa kwa asilimia kubwa , lakini jambo hilo liliwezekana, kwani mpaka muda huo ni makampuni mengi ya kiarabu yameweza kushikilia taasisi nyingi duniani kwa kuzimiliki, ikiwemo vilabu vingi vya mpira kama vile Man City Club na PSG , kampuni za kimitandao kama vile Twitter na maeneo mengi muhimu ambayo yangeweza kuongeza ushawishi wa mataifa ya Kiarabu ulimwenguni.
“Kwanini Hades alichagua Zaidi mataifa ya kiarabu na akaacha mataifa mengine?”Swali zuri sana Zoe.
“Hades wa zamani anaamini kwamba roho nyingi ambazo zilivamia miili ya binadamu hazijatawala sana bara la Asia, hivyo kama Athena ataweza kufanikiwa katika mipango yake ni rahisi kwa sisi kutekeleza mpango wa dharula”Aliongea na kuwafanya wasielewe tena.
“Najua hamuwezi kuelewa maana ya maneno yangu , ila mtaelewa kadri siku zitakavyoendelea kusogea , kwasasasa hatua tunayokwenda kuanza nayo ni kuhakikisha tunatambua miungu yote kumi na mbili”
“Unamaanisha miungu yote kumi na mbili ya kigiriki?”Aliuliza Zoe kwa shauku.
“Ndio najua kwasasa tunamfahamu Artemis , Appolo na Hades na hatumfahamu Athena ni nani na kavaa mwili upi , hatumfahamu Poeseido nani na kavaa mwili upi , hivyo hivyo kwa Aphrodite ,Hermes , Ares na wengine”Aliongea.
“Sheikh Assad ,kuna umuhimu gani wa kufahamu hii miungu na kwanini Hades asingeweza kutuonyesha moja kwa moja kwani ni ndugu zake?”Aliuliza Nadia Alfonso na mrembo huyu aliekuwa kimya muda wote sasa alionekana kuelewa somo.
“Hades wa zamani katupatia kama ‘Assignment’ nah io inamaana kubwa sana kwetu katika kushindana na Athena na miungu mingine lakini hata hivyo Hades hatuwezi kutuambia”Aliongea.
“Roma anaifahamu miungu mingine?”Aliuliza Nadia kwamara nyingine.
“He is God , So he is aware of them and most of all there is god`s treaty?”Aliongea.
“God`s treaty?”
“Ndio kuna mkataba ambao wamesaini miungu yote kumi na mbili”Aliongea.
“Unahusiana na nini?”Aliuliza Pastor Cohen.
“Mambo mengi ambayo siyajui lakini jambo moja ninalojua kwa uhakika ni kwamba mkataba huo pia ulikuwa ukiwazuia miungu kutotajana wala kutoa siri juu ya miili waliovaa labda kwa matukio maalumu pekee”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa.
ALUTA CONTINUARA
CONTACT :0687151346 WATSAPP
Mbombo jilipo.