Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 274
Roma hakutaka kumdhuru Raisi Jeremy , alichokifanya ni kujaribu kumuonya tu na ndio maana baada ya walinzi kuingia alimwachia na kisha kutoka , walinzi walitaka kumzuia Roma , lakini Raisi Jeremy aliwapa ishara ya kumuacha aondoke zake.
Mazungumzo yalianza kwenye muda wa saa kumi na mbili hivyo mpaka Roma kumaliza kuongea na raisi Jeremy ilikuwa ni saa kumi na nusu ikimaanisha kwamba wametumia lisaa limoja kumaliza maongezi yao.
Roma hakutaka kurudi moja kwa moja nyumbani, mudi yake haikuwa nzuri kwani maongezi yanayomhusu Seventeen mara nyingi yanapozungumziwa huwa yanaharibu kabisa mudi yake na anakuwa mwenye mawazo na ndio maana alijiambia atafute sehemu tulivu kwa hapo Kigamboni kwa ajili ya kutuliza kichwa.
Mikadi Beach ndio sehemu ambayo aliona inamfaa kwa kupotezea muda, hakuwahi kufika ila alitumia uwezo wa gari yake kutafuta uelekeo na ndani ya dakika moja tu alikuwa ashakaribia.
“Kaka samahani nipo hapa kwa ajili ya kuwa peke yangu sihitaji kampani”Ilisikika sauti ya mwanamke mrembo ndani ya fukwe hii ya Mikadi, mwanamke ambaye kwa siku hio alionekana kama kivutio kwa wanaume wengi waliokuwepo hapo na kwa jinsi mwanadada huyu alivyokuwa akilalamika ni dhahiri kabisa kwamba amesumbuliwa na wanaume wengi sana tokea ajipumzishe, na hii lilidhihirika kwani alimkataa mwanaume aliehisi uwepo wake pembeni yake pasipo kumwangalia usoni , kwani muda huo mrembo huyu alikuwa amejifunika usoni na kofia yake aina ya Hat huku akiwa ameegamia kwenye viti vilivyojengwa ndani ya eneo hili kwa ajili ya mapumziko.
“Babe Nasra inaonekana Mungu ndio kanileta hili eneo”Aliongea Roma na kumfanya mrembo yule kutoa ile kofia na kumwangalia mwanaume eliekuwa mbele yake , mwaaume ambaye alimkataa sekunde kadhaa zilizopita kwa kumdhania kuwa ni walewale wanaume ambao walikuwa wakimsumbua , ndio alikuwa ni Nasra.
“Roma! , Unafanya nini hapa?”Nasra aliuliza kwa mshangao huku akimwangalia Roma aliekuwa mbele yake , ni kama hakutegemea kabisa kumuona na mapigo ya moyo wake yalienda mbio.
“Oya nadhani yule ndio mwenye mali wazee”Sauti upande wa pili ilisikika kwenye meza ambayo imekaliwa na vijana wanne ambao walikuwa wapo hapo Ufukweni kupunga upepo kwa siku hio ya Wikiend.
“Daah! Wanawake bwana , kama ni kweli basi hawa viumbe sio wa kueleweka kabisa yaani ananikataa mwanaume Hb kama mimi halafu awe na mwanaume kama yule”Aliongea mwanaume mmoja kuunga mada na alionekana alikuwa ametupia ndoano kwa Nasra na akachomolewa na sasa yupo kwenye mshangao baada ya kuona Nasra anatoka ushirikiano kwa mwanaume ambaye hakuwa na mwonekano mzuri kama wake.
“Haha.. hivi viumbe wewe achana navyo kabisa Abduli, kila mtu na bahati yake”Aliongea na kufanya wenzake kucheka na kisha waliendelea kuangaliia upande ambako mwanaume ambaye hawakumfahamu akiongea na mrembo waliemshindwa.
Upande wa Nasra alionekana kutomtegemea kabisa Roma eneo hilo na ndio maana alishangaa uwepo wake.
Nasra Baada ya kumsindikiza rafiki yake Najma kuondoka kuelekea masomoni nchini Marekani hakulala nyumbani kwake kabisa , akili yake haikuwa imetulia na alikuwa kwenye mawazo na ndio maana aliamua kutafuta sehemu ya kutulia na , sehemu ambayo aliona inafaa ni Mikadi Lodge na ndio maana hata Roma jana yake alivyoenda nyumbani kwa Nasra hakumkukuta.
“Babe Nasra unajua ni kwa kiasi gani nimekutafuta?”Aliongea Roma huku akikaa kwenye kiti cha pembeni na Nasra muda wote alikuwa akimwangalia Roma , ni kama mambo mengi yalikuwa yakipita kwenye kichwa chake na hakuwa na namna ya kuelezea.
“Roma naomba uondoke”Aliongea Nasra kwa sauti ya chini na kumfanya Roma kutabasamu aliona mrembo huyu bado yupo na hasira na yeye na hilo hakujali hata kidogo na alijiambia huo ndio muda mzuri wa kuyajenga.
*******
Upande mwingine Edna alionekana akipitia karatasi zilizokuwa kwenye mikono yake , swala la Kampuni ya Maya bado lilikuwa likimuumiza sana kichwa na hii yote ni mara baada ya kugundua kuwa jina la kampuni hio lipo kwenye orodha ya kampuni zilizoorodheshwa kwenye nyaraka ambayo mama yake ameacha nyuma , orodha ya kampuni ambayo aliitafsiri kama sehemu ya malipizo ya kisasi ambacho alikuwa nacho mama yake Raheli na yeye mwenyewe hakufahamu ni kisasi juu ya nini.
Alijiambia lazima kuna kitu kilitokea kati ya kampuni hii ya Maya na mama yake na ndio maana ilikuwa kwenye orodha , lakini mpaka muda huo hakuwa akifahamu ni muunganiko wa namna gani ambao upo na ndio maana alijiambia ni lazima atumie akili zake zote na rasilimali alizokuwa nazo kutafuta muunganiko huo.
Alijikuta akiangalia baadhi ya vitabu vilivyopangwa kwenye chumba hiki ambacho kilikuwa ni kama ofisi ya mama yake hapo kabla na kujikuta akiingia kwenye mawazo, ukweli akili yake ilikuwa imekwama kabisa kwani licha ya kwamba Suzzane amemtumia baadhi ya taarifa kwa kile kinachoendelea kwenye kampuni ya Maya lakini bado hakukuwa na muunganiko na kwa jinsi alivyokuawa akiangalia Shelf hizo zilizojaa vitabu ambavyo mama yake siku zte alikuwa akisoma ni kama alikuwa akitafuta wazo jipya.
Kampuni ya Maya ni kampuni ambayo inajihusiha na mambo mengi na hii ni kutokana na kuwa na ‘Subsidiaries’ nyingi ndani ya taifa la Afrika , ni kampuni ambayo ina makao makuu yake nchini India na inawekwa na majarida mbalimbali ulimwengu kama moja ya kampuni kubwa sana ambayo inaongoza katika maswala ya utafiti na utengenezaji wa madawa duniani na moja ya mafanikio yake makubwa yalitokana na kufanikiwa kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa Ebola kupitia kituo chake cha utafiti kilichopo ndani ya taifa la Canada.
Mwaka 2001 ndio mwaka ambao walifungua tawi la kampuni yao hapa Tanzania na moja ya sababu kubwa ya mwanzilishi wa kampuni hii kupenda kufungua tawi hapa Tanzania ni kutokana na kwamba mke wake mkubwa alikuwa ni Mtanzania hivyo ni kama alifungua tawi hilo kwa heshima ya mke wake kuwa raia wa Tanzania.
Maya Hubat licha ya kwamba alikuwa mhindi , lakini pia alikuwa akilipenda sana Taifa la Tanzania na mara nyingi amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Tanzania hasa upande wa tiba , kwani mara nyingi alionekana akichangia sana michango katika hospitali nyingi lakini jambo kubwa pia kwa Kampuni ya Maya pia wanazo hospitali maarufu sana ambazo zimetapakaa kwenye mikoa yote mikubwa Tanzania.
Hivyo ni rahisi kusema kwamba heshima ya Mzee Maya imetokana na michango yake lakini pia uwekezaji wake hapa Tanzania,maswala hayo yote Edna alikuwa akiyafahamu na hata nyaraka zilizokuwa kwenye meza yake zilikuwa zikisema hivyo , alisoma kila kitu kilichokuwa kikihusiana na kampni ya Maya lakini hakuishia kwa kampuni ya Maya tu , lakini pia alisoma na mwanzilishi wa makampuni haya ya Maya na nia zake zote za kupendelea taifa la Tanzania katika maswala ya uwekezaji , lakini licha ya Edna kusoma nia halisi ya Mzee Maya kwa hapa Tanzania katika swala la uwekezaji , aliona kuna jambo ambalo bado halikai sawa, ni kweli kwamba Mzee Maya ameoa Tazania na mara nyingi amekuwa mtu wa kujinasibu kama moja ya watu wanaolipenda tafai la Tanzania kwani limempatia mke bora , lakini hata hivyo aliamini ni kama jambo la ziada kwa hayo yote , Edna alikuwa mfanyabiashara na siku zpte ukifikiria kibiashara Zaidi utajua kwamba kuna baadhi ya uwekezaji hata kama una mapenzi mengi na taifa husika huwezi kuufanya kwani hauwezi kukuletea faida Zaidi ya hasara na hili ndio aliliona kwa kampuni hii ya Maya , Mzee Hubati kuna uwekezaji ambao amefanya hakuona tija yake na kama yeye ndio mwamuzi mkuu basi asingejihangaisha kabisa katika kuwekeza hapa nchini na hili ndio lilimfanya aone kuna Zaidi ya sababu katika juhudi za kiuwekezaji kwa Mzee Hubati na alitaka kuzifahamu.
Edna wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo , akili yake ilikuja kutua kwene moja ya kitabu kilichokuwa kikionekana wazi upande w akushoto kwenye shelf , kitabu ambacho mara baada ya kukiona alikumbuka mama yake mara nyingi alimuona akiwa amekishikilia akikisioma enzi za uhai wake, alikiangalia kwa dakika kadhaa kabla ya kufanya maamuzi ya kunyanyuka alipokuwa amekaa na kukisogelea na kukitoa kwenye shelfu na kurudi nacho kwenye meza yake na kuketi kwa ajili ya kukifungua na kuanza kukisoma , alikuwa akitamani kujua ni kitu gani ambacho mama yake alikuwa akikisoma mara kwa mara.
“One of her favourite book”Aliwaza kwenye kichwa chake akisema kwamba moja ya kitabu pendwa cha mama yake huku akigeuza geuza, baada ya dakika kadhaa ya kukigeuza aliamua kukifungua.
“Kumbe mama alikuwa ni mpenzi wa Mashairi?”Aliwaza Edna baada ya kugundua kuwa kitabu ambacho amekishikilia kina mkusanyiko wa mashairi ambayo yamewahi kuwandikwa duniani, ukweli mwanzoni hakuwa akijua kitabu hiko kilikuwa kikihusiana na nini kutokana na kutokuwa na kava ambalo lilikuwa likielezea nini kimeandikwa ndani yake , hivyo baada ya kufungua ndio aligundua kumbe ni kitabu ambacho kilikuwa kikihusu mashairi.
Edna wakati anafungua ukurasa wa pili kuna kitu kilidondka chini na kumfanya akiangalie na alikuja kugundua ilikuwa ni picha , aliweka kitabu chini na kuiinua na kuishikilia na kukuta sura ambayo inakuja na kupotea kwenye kichwa chake ni kama mtu aliekuwa kwenye picha alikuwa akimfahamu lakini hakuwa akikumbuka amemuona wapi, aligeuza nyuma ya picha hio na kuona kuna maandishi yalioandikwa.
“Sonnet 116 by Shakespeare , I dedicate it to you Rahel My Love”Ndio mwanzo wa maneno yaliosomeka juu ya picha alioshikilia Edna , maandishi ambayo yalikuwa yakimaanisha kwamba “Najitolea kukupa shairi hili mpenzi wangu Rahel, shairi la Sonnet 116 kutoka kwa mtunzi Williams Shakespeare.
Edna alijikuta akshangaa na hisia zake tayari zilimwambia mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni mpenzi wa mama yake na moyo wake ulipiga kite , kwani maandishi yaliofuatiwa yanayohusiana na shairi hilo yalidhihirisha upendo wa dhati sana kutoka kwa mwanaume aliekuwa kwenye picha kwenda kwa Rahel mama yake.
“This guy could be my father”Aliongea Edna akimaanisha kwamba mtu aliekuwa kwenye picha anaweza kuwa ndio baba yake.




SEHEMU YA 275
Saa moja na nusu ndio muda ambao Roma alirejea nyumbani , alionekana mudi yake imerudi na hio yote ni kutokana na kwamba yeye na Nasra mapenzi yao yamerudi kama zamani na ashatuliza hasira zote za mrembo huyo na mipango yao ya kwenda kijijini ilikuwa ikiendelea na zilikuwa zimebaki takribani wiki mbili mpaka kufikia siku yenyewe.
Mama yake Roma siku hio alionekana hakuwa nyumbani, lakini hakujali sana , Edna alionekana kuwa sebuleni akiwa ameketi pamoja na Yezi , Sophia na Bi Wema na walionekana walikuwa wakipiga soga na Roma alitabasamu kuona wanaendana vizuri na mke wake yupo kwenye hali ya kuchangamka.
Ukweli ni kwamba Edna hakumjua mwanaume aliekuwa kwenye picha , ni kweli sura yake ilikuwa ikija na kupotea lakini hakuweza kuitambua na kukumbuka aliiona wapi , hivyo hakutaka kusumbua kichwa chake , kuna hisia ambazo zilikuwa zikimwambia kuwa mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni baba yake , lakini aliamua kupotezea , kwanza hakuwa na mpango kabisa wa kumfahamu baba yake na alijiambia labda baba mwenyewe ndio amtafute yeye , mrembo huyu hakujua kuwa mume wake Roma Ramoni alikuwa na maongezi mchana huo na baba yake mzazi , baba ambaye amemkataa mbele ya mume wake.
Sasa Edna aliona asiendelee kukaa zake chumba cha kujisomea na aungane na wanafamilia sebuleni.
“Roma jumatatu Yezi anatarajjia kuanza kufanya usaili Kwenda chuo , unapaswa kumsindikiza”Aliongea Edna na Roma alishangaa kidogo , ukweli mara nyingi ni kama Yezi alikuwa akimwepuka hivyo hakupata wasaa mwingi wa kuongea nae tokea warudi Ufarnsa na kumkuta nyumbani.
“Yezi umepata chuo gani?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Yezi , lakini Yezi alikuwa ni kama anamshangaa Roma.
Ukweli ni kwamba Yezi alikuwa akiangalia kicheni ambacho kipo kwenye shingo ya Roma na hii ni baada ya Roma kuinama wakati wa kukaa na ndipo kiliponekena , kidani ambacho yeye alimpatia kama zawadi, jambo lile kwake limemgusa sana kwani hakuamini kama Roma anaweza kuthamini zawadi yake na kuivaa shingoni.
“Mbona hunijibu unaniangalia tu”
“Kapata UDSM , yaani wewe Yezi ni mwanafamilia lakini umeshndwa hata kufuatilia maendeleao yake”Aliongea Edna na kumfanya Bi Wema kutabasamu namna Edna anavyomkosoa Roma na Roma lilimwingia kweli , kwani ni kweli hakuwa akifatilia sana maendeleo ya Yezi na ndio maana hata hakufahamu ni chuo gani ambacho Yezi amepata lakini ni wakati gani amabo Yezi kaanza kufanya maombi.
“Ni sawa tu Sister Edna , Anko ana mambo mengi”aliongea Yezi kwa namna ya kumtetea Roma na Edna alitaka kuongea neno ila alijiambia ngoja anyamaze.
“Okey wife Yezi mimi nitampeleka chuo siku ya jumatatu na kuhakikisha kafanya usaili”Aliongea Roma na Yezi alitabasamu.
“Simuoni mama, kaenda wapi?”Aliuliza Roma.
“Kaenda kumsalimia MzeeAtanasi, baba yake”Alijibu Edna na Roma alitingisha kichwa kuashiria kwamba ameelewa.
********
Kila mmoja alitamani kusikia jibu litakalotoka kwa Sheikh Assad , swali ambalo ameulizwa na Zoe Kovac kwanini Hades wa Zamani aliamua kujidhihirsha kwake ilihali hakufanya hivyo kwa wengine kama vile Pastor Cohen ambaye alionekana kuwa ni mtu muhimu katika mipango yake.
“Sababu ya Hades wa zamani kujionyesha kwangu , huenda ikawa ni kutokana na kazi kubwa ambayo alinipatia kuliko watu wote mliopo hapa ndani na wale ambao hampo hapa ndani , najua kila mtu amefanya kazi ambayo ina mchango mkubwa katika mipango ya Hades wa zamani kwa kila mtu na nafasi yake , lakini kwa upande wangu kazi yangu ilikuwa kubwa mno na nilikataa kuifanya mpaka ajionyeshe kwangu”
“Unamaanisha kwamba Hades , alikupa kazi kubwa kiasi kwamba ulikataa kuifanya na ukataka kwanza ajionyeshe kwako?”Aliuliza Pastor Cohen , ukweli ni kwamba hakujua kama kuna mtu ambaye anaweza kumzidi yeye kwa kufanya kazi ngumu , misheni zote ambazo zinaendelea mpaka kwa wakati huo Pastor Cohen aliamini zilianzia upande wake.
“Ndio kazi alionipa ilikuwa ngumu katika utekelezaji wake , kwani ilikuwa ni ya hatari , ya kujishusha, kudharaulika nahata kuonekana kichaa muda mwingine , hivyo ilihitaji uvumilivu mwingi”Aliongea.
“Ni kazi gani ambayo alikupatia ?”Aliuliza Afande Kweka aliekuwa kimya muda wote akigusa gusa ndevu zake zenye mvi.
“Najua wengi wenu hapa mnaamini kwamba nyie wote ni wanachama lakini hamjawahi kufahamu mpo kwenye chama gani mpaka mkaitwa kuwa wanachama na hii ndio ajenda kubwa ambayo imenileta hapa Afrika na kupitia Ajenda hio mtaweza kuelewa ni ipi kazi yangu ambayo nilikuwa nikifanya tokea nifike ndani ya mataifa ya Uarabuni”Aliongea na kisha akavuta pumzi ili kuendelea.
“We Are Ant-Illiminat Society”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa kwani ni kama hawakumuelewa kasoro upande wa Cohen.
“Nadhani sio mara yenu ya kwanza kusikia neno ‘Illuminat’ lakini ni mara yenu ya kwanza kusikia neno Ant-Illuminat?”Aliuliza Sheikh Assad na kunfanya wote hapo ndani kuangaliana , ni kweli walikuwa wakisikia juu ya neno Illuminat , lakini hawakuwahi kusikia neno la Ant-Illuminat.
Ant-Illuminat ni neno ambalo linamaana ya kinyume na neno lenyewe la Illuminat , yaani wapingaji wa jamii ya siri ya Illuminat ndio chama ambacho sheikh Assad alikuwa akizungumzia.
“Lazima tuelewe historia ya Illuminat kabla ya kuwa mwanachama halisi wa Ant-Illuminat , lakini sio hivyo tu ili uweze kuwa mmoja wapo wa jamii hii ya siri itakubidi kwanza ujue kila kitu kuhusu Illuminat na hii ndio kazi yangu ambayo nilipewa na Hades, kazi ya kujiunga na Illuminat.
“Your are Illuminat?”Aliuliza Mellisa kwa mshangoa.
“Yes , I am”Pastor Cohen alishangaa.
“But I am also Ant-Illuminat”Aliongea.
Mpaka hapo ni kama sasa wanaanza kupata picha ya kwanini Sheikh Assad alisema kazi yake ni ngumu sana kuliko wengine wote.
“Sheikh tupo kwenye kiza mpaka sasa , na nadhani litakuwa jambo jema kama utatuweka wazi , ili kila mmoja wetu apate kuelewa.”Aliongea Pastor Cohen na kumfanya Sheikh Assad kukubali na kuanza kuelezea.
Kwa maelezo yake ni kwamba baada ya kuokolewa na Hades wa Zamani na kupelekewa nchini Saudi Arabia kitu cha kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha Sheikh Assad kutoka kwenye hatia ya kutafutwa na CIA Pamoja na FBI na hilo kutokana na kwamba Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa upande wa mataifa ya kiarabu , hivyo kuongea na serikali ya Marekani kwa ajili ya kumfutia kesi Profesa Assad lilikuwa jambo jepesi sana ,h na serikali ya Saudi iliweza kufanya hivyo kutokana na uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya mfalme wa Saudi na Hades wa zamani.
Anasema baada ya kuisha kwa kesi hio ndio mwanzo wa kazi mpya ambayo alipewa kuikamilihsha naHades ama moja ya misheni yake na kazi yenyewe ilikuwa ni juu ya kujiunga na jamii ya siri ya Freemason.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba Illuminati ipo ndani ya ufreemason , hivyo kujiunga kwake ndani ya jamii hii ilikuwa ni kwa ajili ya kazi moja tu , kutambua wanachama wote waliokuwa na asili ya Illuminat na hio ilikuwa kazi ngumu sana kwake kutokana na usiri wa jamii hizi.
Sheikh Assad baada ya kufanikiwa kujiunga na jamii hio alipewa kazi nyingine ya kushawishi mataifa ya kiarabu kuanza uwekezaji nje ya mipaka yake, hii haikuhusisha serikali tu bali mpaka kwa sekta binafsi, kwahio kazi hioi ilikuwa ikimaanisha kwamba ashawishi matajiri ambao wapo kwenye serikali za kiarabu kuanza kuwekeza kwenye mataifa makubwa , hususani yale yenye uchumi mkubwa , ikumbukwe mataifa ya kiarabu kwa asilimia kubwa wamejaaliwa utajiri wa mafuta hivyo kuwa na matajiri wengi ambao hawakufahamika kabisa duniani, hivyo kazi ya Assad ilikuwa ni kushawishi sasa hao matajiri.
Anasema kwamba licha ya kwamba ilichukua muda mwingi kufanikiwa kwa asilimia kubwa , lakini jambo hilo liliwezekana, kwani mpaka muda huo ni makampuni mengi ya kiarabu yameweza kushikilia taasisi nyingi duniani kwa kuzimiliki, ikiwemo vilabu vingi vya mpira kama vile Man City Club na PSG , kampuni za kimitandao kama vile Twitter na maeneo mengi muhimu ambayo yangeweza kuongeza ushawishi wa mataifa ya Kiarabu ulimwenguni.
“Kwanini Hades alichagua Zaidi mataifa ya kiarabu na akaacha mataifa mengine?”Swali zuri sana Zoe.
“Hades wa zamani anaamini kwamba roho nyingi ambazo zilivamia miili ya binadamu hazijatawala sana bara la Asia, hivyo kama Athena ataweza kufanikiwa katika mipango yake ni rahisi kwa sisi kutekeleza mpango wa dharula”Aliongea na kuwafanya wasielewe tena.
“Najua hamuwezi kuelewa maana ya maneno yangu , ila mtaelewa kadri siku zitakavyoendelea kusogea , kwasasasa hatua tunayokwenda kuanza nayo ni kuhakikisha tunatambua miungu yote kumi na mbili”
“Unamaanisha miungu yote kumi na mbili ya kigiriki?”Aliuliza Zoe kwa shauku.
“Ndio najua kwasasa tunamfahamu Artemis , Appolo na Hades na hatumfahamu Athena ni nani na kavaa mwili upi , hatumfahamu Poeseido nani na kavaa mwili upi , hivyo hivyo kwa Aphrodite ,Hermes , Ares na wengine”Aliongea.
“Sheikh Assad ,kuna umuhimu gani wa kufahamu hii miungu na kwanini Hades asingeweza kutuonyesha moja kwa moja kwani ni ndugu zake?”Aliuliza Nadia Alfonso na mrembo huyu aliekuwa kimya muda wote sasa alionekana kuelewa somo.
“Hades wa zamani katupatia kama ‘Assignment’ nah io inamaana kubwa sana kwetu katika kushindana na Athena na miungu mingine lakini hata hivyo Hades hatuwezi kutuambia”Aliongea.
“Roma anaifahamu miungu mingine?”Aliuliza Nadia kwamara nyingine.
“He is God , So he is aware of them and most of all there is god`s treaty?”Aliongea.
“God`s treaty?”
“Ndio kuna mkataba ambao wamesaini miungu yote kumi na mbili”Aliongea.
“Unahusiana na nini?”Aliuliza Pastor Cohen.
“Mambo mengi ambayo siyajui lakini jambo moja ninalojua kwa uhakika ni kwamba mkataba huo pia ulikuwa ukiwazuia miungu kutotajana wala kutoa siri juu ya miili waliovaa labda kwa matukio maalumu pekee”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa.

ALUTA CONTINUARA

CONTACT :0687151346 WATSAPP
275 duh!
Mbombo jilipo.
 
SEHEMU YA 274
Roma hakutaka kumdhuru Raisi Jeremy , alichokifanya ni kujaribu kumuonya tu na ndio maana baada ya walinzi kuingia alimwachia na kisha kutoka , walinzi walitaka kumzuia Roma , lakini Raisi Jeremy aliwapa ishara ya kumuacha aondoke zake.
Mazungumzo yalianza kwenye muda wa saa kumi na mbili hivyo mpaka Roma kumaliza kuongea na raisi Jeremy ilikuwa ni saa kumi na nusu ikimaanisha kwamba wametumia lisaa limoja kumaliza maongezi yao.
Roma hakutaka kurudi moja kwa moja nyumbani, mudi yake haikuwa nzuri kwani maongezi yanayomhusu Seventeen mara nyingi yanapozungumziwa huwa yanaharibu kabisa mudi yake na anakuwa mwenye mawazo na ndio maana alijiambia atafute sehemu tulivu kwa hapo Kigamboni kwa ajili ya kutuliza kichwa.
Mikadi Beach ndio sehemu ambayo aliona inamfaa kwa kupotezea muda, hakuwahi kufika ila alitumia uwezo wa gari yake kutafuta uelekeo na ndani ya dakika moja tu alikuwa ashakaribia.
“Kaka samahani nipo hapa kwa ajili ya kuwa peke yangu sihitaji kampani”Ilisikika sauti ya mwanamke mrembo ndani ya fukwe hii ya Mikadi, mwanamke ambaye kwa siku hio alionekana kama kivutio kwa wanaume wengi waliokuwepo hapo na kwa jinsi mwanadada huyu alivyokuwa akilalamika ni dhahiri kabisa kwamba amesumbuliwa na wanaume wengi sana tokea ajipumzishe, na hii lilidhihirika kwani alimkataa mwanaume aliehisi uwepo wake pembeni yake pasipo kumwangalia usoni , kwani muda huo mrembo huyu alikuwa amejifunika usoni na kofia yake aina ya Hat huku akiwa ameegamia kwenye viti vilivyojengwa ndani ya eneo hili kwa ajili ya mapumziko.
“Babe Nasra inaonekana Mungu ndio kanileta hili eneo”Aliongea Roma na kumfanya mrembo yule kutoa ile kofia na kumwangalia mwanaume eliekuwa mbele yake , mwaaume ambaye alimkataa sekunde kadhaa zilizopita kwa kumdhania kuwa ni walewale wanaume ambao walikuwa wakimsumbua , ndio alikuwa ni Nasra.
“Roma! , Unafanya nini hapa?”Nasra aliuliza kwa mshangao huku akimwangalia Roma aliekuwa mbele yake , ni kama hakutegemea kabisa kumuona na mapigo ya moyo wake yalienda mbio.
“Oya nadhani yule ndio mwenye mali wazee”Sauti upande wa pili ilisikika kwenye meza ambayo imekaliwa na vijana wanne ambao walikuwa wapo hapo Ufukweni kupunga upepo kwa siku hio ya Wikiend.
“Daah! Wanawake bwana , kama ni kweli basi hawa viumbe sio wa kueleweka kabisa yaani ananikataa mwanaume Hb kama mimi halafu awe na mwanaume kama yule”Aliongea mwanaume mmoja kuunga mada na alionekana alikuwa ametupia ndoano kwa Nasra na akachomolewa na sasa yupo kwenye mshangao baada ya kuona Nasra anatoka ushirikiano kwa mwanaume ambaye hakuwa na mwonekano mzuri kama wake.
“Haha.. hivi viumbe wewe achana navyo kabisa Abduli, kila mtu na bahati yake”Aliongea na kufanya wenzake kucheka na kisha waliendelea kuangaliia upande ambako mwanaume ambaye hawakumfahamu akiongea na mrembo waliemshindwa.
Upande wa Nasra alionekana kutomtegemea kabisa Roma eneo hilo na ndio maana alishangaa uwepo wake.
Nasra Baada ya kumsindikiza rafiki yake Najma kuondoka kuelekea masomoni nchini Marekani hakulala nyumbani kwake kabisa , akili yake haikuwa imetulia na alikuwa kwenye mawazo na ndio maana aliamua kutafuta sehemu ya kutulia na , sehemu ambayo aliona inafaa ni Mikadi Lodge na ndio maana hata Roma jana yake alivyoenda nyumbani kwa Nasra hakumkukuta.
“Babe Nasra unajua ni kwa kiasi gani nimekutafuta?”Aliongea Roma huku akikaa kwenye kiti cha pembeni na Nasra muda wote alikuwa akimwangalia Roma , ni kama mambo mengi yalikuwa yakipita kwenye kichwa chake na hakuwa na namna ya kuelezea.
“Roma naomba uondoke”Aliongea Nasra kwa sauti ya chini na kumfanya Roma kutabasamu aliona mrembo huyu bado yupo na hasira na yeye na hilo hakujali hata kidogo na alijiambia huo ndio muda mzuri wa kuyajenga.
*******
Upande mwingine Edna alionekana akipitia karatasi zilizokuwa kwenye mikono yake , swala la Kampuni ya Maya bado lilikuwa likimuumiza sana kichwa na hii yote ni mara baada ya kugundua kuwa jina la kampuni hio lipo kwenye orodha ya kampuni zilizoorodheshwa kwenye nyaraka ambayo mama yake ameacha nyuma , orodha ya kampuni ambayo aliitafsiri kama sehemu ya malipizo ya kisasi ambacho alikuwa nacho mama yake Raheli na yeye mwenyewe hakufahamu ni kisasi juu ya nini.
Alijiambia lazima kuna kitu kilitokea kati ya kampuni hii ya Maya na mama yake na ndio maana ilikuwa kwenye orodha , lakini mpaka muda huo hakuwa akifahamu ni muunganiko wa namna gani ambao upo na ndio maana alijiambia ni lazima atumie akili zake zote na rasilimali alizokuwa nazo kutafuta muunganiko huo.
Alijikuta akiangalia baadhi ya vitabu vilivyopangwa kwenye chumba hiki ambacho kilikuwa ni kama ofisi ya mama yake hapo kabla na kujikuta akiingia kwenye mawazo, ukweli akili yake ilikuwa imekwama kabisa kwani licha ya kwamba Suzzane amemtumia baadhi ya taarifa kwa kile kinachoendelea kwenye kampuni ya Maya lakini bado hakukuwa na muunganiko na kwa jinsi alivyokuawa akiangalia Shelf hizo zilizojaa vitabu ambavyo mama yake siku zte alikuwa akisoma ni kama alikuwa akitafuta wazo jipya.
Kampuni ya Maya ni kampuni ambayo inajihusiha na mambo mengi na hii ni kutokana na kuwa na ‘Subsidiaries’ nyingi ndani ya taifa la Afrika , ni kampuni ambayo ina makao makuu yake nchini India na inawekwa na majarida mbalimbali ulimwengu kama moja ya kampuni kubwa sana ambayo inaongoza katika maswala ya utafiti na utengenezaji wa madawa duniani na moja ya mafanikio yake makubwa yalitokana na kufanikiwa kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa Ebola kupitia kituo chake cha utafiti kilichopo ndani ya taifa la Canada.
Mwaka 2001 ndio mwaka ambao walifungua tawi la kampuni yao hapa Tanzania na moja ya sababu kubwa ya mwanzilishi wa kampuni hii kupenda kufungua tawi hapa Tanzania ni kutokana na kwamba mke wake mkubwa alikuwa ni Mtanzania hivyo ni kama alifungua tawi hilo kwa heshima ya mke wake kuwa raia wa Tanzania.
Maya Hubat licha ya kwamba alikuwa mhindi , lakini pia alikuwa akilipenda sana Taifa la Tanzania na mara nyingi amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Tanzania hasa upande wa tiba , kwani mara nyingi alionekana akichangia sana michango katika hospitali nyingi lakini jambo kubwa pia kwa Kampuni ya Maya pia wanazo hospitali maarufu sana ambazo zimetapakaa kwenye mikoa yote mikubwa Tanzania.
Hivyo ni rahisi kusema kwamba heshima ya Mzee Maya imetokana na michango yake lakini pia uwekezaji wake hapa Tanzania,maswala hayo yote Edna alikuwa akiyafahamu na hata nyaraka zilizokuwa kwenye meza yake zilikuwa zikisema hivyo , alisoma kila kitu kilichokuwa kikihusiana na kampni ya Maya lakini hakuishia kwa kampuni ya Maya tu , lakini pia alisoma na mwanzilishi wa makampuni haya ya Maya na nia zake zote za kupendelea taifa la Tanzania katika maswala ya uwekezaji , lakini licha ya Edna kusoma nia halisi ya Mzee Maya kwa hapa Tanzania katika swala la uwekezaji , aliona kuna jambo ambalo bado halikai sawa, ni kweli kwamba Mzee Maya ameoa Tazania na mara nyingi amekuwa mtu wa kujinasibu kama moja ya watu wanaolipenda tafai la Tanzania kwani limempatia mke bora , lakini hata hivyo aliamini ni kama jambo la ziada kwa hayo yote , Edna alikuwa mfanyabiashara na siku zpte ukifikiria kibiashara Zaidi utajua kwamba kuna baadhi ya uwekezaji hata kama una mapenzi mengi na taifa husika huwezi kuufanya kwani hauwezi kukuletea faida Zaidi ya hasara na hili ndio aliliona kwa kampuni hii ya Maya , Mzee Hubati kuna uwekezaji ambao amefanya hakuona tija yake na kama yeye ndio mwamuzi mkuu basi asingejihangaisha kabisa katika kuwekeza hapa nchini na hili ndio lilimfanya aone kuna Zaidi ya sababu katika juhudi za kiuwekezaji kwa Mzee Hubati na alitaka kuzifahamu.
Edna wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo , akili yake ilikuja kutua kwene moja ya kitabu kilichokuwa kikionekana wazi upande w akushoto kwenye shelf , kitabu ambacho mara baada ya kukiona alikumbuka mama yake mara nyingi alimuona akiwa amekishikilia akikisioma enzi za uhai wake, alikiangalia kwa dakika kadhaa kabla ya kufanya maamuzi ya kunyanyuka alipokuwa amekaa na kukisogelea na kukitoa kwenye shelfu na kurudi nacho kwenye meza yake na kuketi kwa ajili ya kukifungua na kuanza kukisoma , alikuwa akitamani kujua ni kitu gani ambacho mama yake alikuwa akikisoma mara kwa mara.
“One of her favourite book”Aliwaza kwenye kichwa chake akisema kwamba moja ya kitabu pendwa cha mama yake huku akigeuza geuza, baada ya dakika kadhaa ya kukigeuza aliamua kukifungua.
“Kumbe mama alikuwa ni mpenzi wa Mashairi?”Aliwaza Edna baada ya kugundua kuwa kitabu ambacho amekishikilia kina mkusanyiko wa mashairi ambayo yamewahi kuwandikwa duniani, ukweli mwanzoni hakuwa akijua kitabu hiko kilikuwa kikihusiana na nini kutokana na kutokuwa na kava ambalo lilikuwa likielezea nini kimeandikwa ndani yake , hivyo baada ya kufungua ndio aligundua kumbe ni kitabu ambacho kilikuwa kikihusu mashairi.
Edna wakati anafungua ukurasa wa pili kuna kitu kilidondka chini na kumfanya akiangalie na alikuja kugundua ilikuwa ni picha , aliweka kitabu chini na kuiinua na kuishikilia na kukuta sura ambayo inakuja na kupotea kwenye kichwa chake ni kama mtu aliekuwa kwenye picha alikuwa akimfahamu lakini hakuwa akikumbuka amemuona wapi, aligeuza nyuma ya picha hio na kuona kuna maandishi yalioandikwa.
“Sonnet 116 by Shakespeare , I dedicate it to you Rahel My Love”Ndio mwanzo wa maneno yaliosomeka juu ya picha alioshikilia Edna , maandishi ambayo yalikuwa yakimaanisha kwamba “Najitolea kukupa shairi hili mpenzi wangu Rahel, shairi la Sonnet 116 kutoka kwa mtunzi Williams Shakespeare.
Edna alijikuta akshangaa na hisia zake tayari zilimwambia mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni mpenzi wa mama yake na moyo wake ulipiga kite , kwani maandishi yaliofuatiwa yanayohusiana na shairi hilo yalidhihirisha upendo wa dhati sana kutoka kwa mwanaume aliekuwa kwenye picha kwenda kwa Rahel mama yake.
“This guy could be my father”Aliongea Edna akimaanisha kwamba mtu aliekuwa kwenye picha anaweza kuwa ndio baba yake.




SEHEMU YA 275
Saa moja na nusu ndio muda ambao Roma alirejea nyumbani , alionekana mudi yake imerudi na hio yote ni kutokana na kwamba yeye na Nasra mapenzi yao yamerudi kama zamani na ashatuliza hasira zote za mrembo huyo na mipango yao ya kwenda kijijini ilikuwa ikiendelea na zilikuwa zimebaki takribani wiki mbili mpaka kufikia siku yenyewe.
Mama yake Roma siku hio alionekana hakuwa nyumbani, lakini hakujali sana , Edna alionekana kuwa sebuleni akiwa ameketi pamoja na Yezi , Sophia na Bi Wema na walionekana walikuwa wakipiga soga na Roma alitabasamu kuona wanaendana vizuri na mke wake yupo kwenye hali ya kuchangamka.
Ukweli ni kwamba Edna hakumjua mwanaume aliekuwa kwenye picha , ni kweli sura yake ilikuwa ikija na kupotea lakini hakuweza kuitambua na kukumbuka aliiona wapi , hivyo hakutaka kusumbua kichwa chake , kuna hisia ambazo zilikuwa zikimwambia kuwa mwanaume aliekuwa kwenye picha alikuwa ni baba yake , lakini aliamua kupotezea , kwanza hakuwa na mpango kabisa wa kumfahamu baba yake na alijiambia labda baba mwenyewe ndio amtafute yeye , mrembo huyu hakujua kuwa mume wake Roma Ramoni alikuwa na maongezi mchana huo na baba yake mzazi , baba ambaye amemkataa mbele ya mume wake.
Sasa Edna aliona asiendelee kukaa zake chumba cha kujisomea na aungane na wanafamilia sebuleni.
“Roma jumatatu Yezi anatarajjia kuanza kufanya usaili Kwenda chuo , unapaswa kumsindikiza”Aliongea Edna na Roma alishangaa kidogo , ukweli mara nyingi ni kama Yezi alikuwa akimwepuka hivyo hakupata wasaa mwingi wa kuongea nae tokea warudi Ufarnsa na kumkuta nyumbani.
“Yezi umepata chuo gani?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Yezi , lakini Yezi alikuwa ni kama anamshangaa Roma.
Ukweli ni kwamba Yezi alikuwa akiangalia kicheni ambacho kipo kwenye shingo ya Roma na hii ni baada ya Roma kuinama wakati wa kukaa na ndipo kiliponekena , kidani ambacho yeye alimpatia kama zawadi, jambo lile kwake limemgusa sana kwani hakuamini kama Roma anaweza kuthamini zawadi yake na kuivaa shingoni.
“Mbona hunijibu unaniangalia tu”
“Kapata UDSM , yaani wewe Yezi ni mwanafamilia lakini umeshndwa hata kufuatilia maendeleao yake”Aliongea Edna na kumfanya Bi Wema kutabasamu namna Edna anavyomkosoa Roma na Roma lilimwingia kweli , kwani ni kweli hakuwa akifatilia sana maendeleo ya Yezi na ndio maana hata hakufahamu ni chuo gani ambacho Yezi amepata lakini ni wakati gani amabo Yezi kaanza kufanya maombi.
“Ni sawa tu Sister Edna , Anko ana mambo mengi”aliongea Yezi kwa namna ya kumtetea Roma na Edna alitaka kuongea neno ila alijiambia ngoja anyamaze.
“Okey wife Yezi mimi nitampeleka chuo siku ya jumatatu na kuhakikisha kafanya usaili”Aliongea Roma na Yezi alitabasamu.
“Simuoni mama, kaenda wapi?”Aliuliza Roma.
“Kaenda kumsalimia MzeeAtanasi, baba yake”Alijibu Edna na Roma alitingisha kichwa kuashiria kwamba ameelewa.
********
Kila mmoja alitamani kusikia jibu litakalotoka kwa Sheikh Assad , swali ambalo ameulizwa na Zoe Kovac kwanini Hades wa Zamani aliamua kujidhihirsha kwake ilihali hakufanya hivyo kwa wengine kama vile Pastor Cohen ambaye alionekana kuwa ni mtu muhimu katika mipango yake.
“Sababu ya Hades wa zamani kujionyesha kwangu , huenda ikawa ni kutokana na kazi kubwa ambayo alinipatia kuliko watu wote mliopo hapa ndani na wale ambao hampo hapa ndani , najua kila mtu amefanya kazi ambayo ina mchango mkubwa katika mipango ya Hades wa zamani kwa kila mtu na nafasi yake , lakini kwa upande wangu kazi yangu ilikuwa kubwa mno na nilikataa kuifanya mpaka ajionyeshe kwangu”
“Unamaanisha kwamba Hades , alikupa kazi kubwa kiasi kwamba ulikataa kuifanya na ukataka kwanza ajionyeshe kwako?”Aliuliza Pastor Cohen , ukweli ni kwamba hakujua kama kuna mtu ambaye anaweza kumzidi yeye kwa kufanya kazi ngumu , misheni zote ambazo zinaendelea mpaka kwa wakati huo Pastor Cohen aliamini zilianzia upande wake.
“Ndio kazi alionipa ilikuwa ngumu katika utekelezaji wake , kwani ilikuwa ni ya hatari , ya kujishusha, kudharaulika nahata kuonekana kichaa muda mwingine , hivyo ilihitaji uvumilivu mwingi”Aliongea.
“Ni kazi gani ambayo alikupatia ?”Aliuliza Afande Kweka aliekuwa kimya muda wote akigusa gusa ndevu zake zenye mvi.
“Najua wengi wenu hapa mnaamini kwamba nyie wote ni wanachama lakini hamjawahi kufahamu mpo kwenye chama gani mpaka mkaitwa kuwa wanachama na hii ndio ajenda kubwa ambayo imenileta hapa Afrika na kupitia Ajenda hio mtaweza kuelewa ni ipi kazi yangu ambayo nilikuwa nikifanya tokea nifike ndani ya mataifa ya Uarabuni”Aliongea na kisha akavuta pumzi ili kuendelea.
“We Are Ant-Illiminat Society”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa kwani ni kama hawakumuelewa kasoro upande wa Cohen.
“Nadhani sio mara yenu ya kwanza kusikia neno ‘Illuminat’ lakini ni mara yenu ya kwanza kusikia neno Ant-Illuminat?”Aliuliza Sheikh Assad na kunfanya wote hapo ndani kuangaliana , ni kweli walikuwa wakisikia juu ya neno Illuminat , lakini hawakuwahi kusikia neno la Ant-Illuminat.
Ant-Illuminat ni neno ambalo linamaana ya kinyume na neno lenyewe la Illuminat , yaani wapingaji wa jamii ya siri ya Illuminat ndio chama ambacho sheikh Assad alikuwa akizungumzia.
“Lazima tuelewe historia ya Illuminat kabla ya kuwa mwanachama halisi wa Ant-Illuminat , lakini sio hivyo tu ili uweze kuwa mmoja wapo wa jamii hii ya siri itakubidi kwanza ujue kila kitu kuhusu Illuminat na hii ndio kazi yangu ambayo nilipewa na Hades, kazi ya kujiunga na Illuminat.
“Your are Illuminat?”Aliuliza Mellisa kwa mshangoa.
“Yes , I am”Pastor Cohen alishangaa.
“But I am also Ant-Illuminat”Aliongea.
Mpaka hapo ni kama sasa wanaanza kupata picha ya kwanini Sheikh Assad alisema kazi yake ni ngumu sana kuliko wengine wote.
“Sheikh tupo kwenye kiza mpaka sasa , na nadhani litakuwa jambo jema kama utatuweka wazi , ili kila mmoja wetu apate kuelewa.”Aliongea Pastor Cohen na kumfanya Sheikh Assad kukubali na kuanza kuelezea.
Kwa maelezo yake ni kwamba baada ya kuokolewa na Hades wa Zamani na kupelekewa nchini Saudi Arabia kitu cha kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kumsafisha Sheikh Assad kutoka kwenye hatia ya kutafutwa na CIA Pamoja na FBI na hilo kutokana na kwamba Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa upande wa mataifa ya kiarabu , hivyo kuongea na serikali ya Marekani kwa ajili ya kumfutia kesi Profesa Assad lilikuwa jambo jepesi sana ,h na serikali ya Saudi iliweza kufanya hivyo kutokana na uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya mfalme wa Saudi na Hades wa zamani.
Anasema baada ya kuisha kwa kesi hio ndio mwanzo wa kazi mpya ambayo alipewa kuikamilihsha naHades ama moja ya misheni yake na kazi yenyewe ilikuwa ni juu ya kujiunga na jamii ya siri ya Freemason.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba Illuminati ipo ndani ya ufreemason , hivyo kujiunga kwake ndani ya jamii hii ilikuwa ni kwa ajili ya kazi moja tu , kutambua wanachama wote waliokuwa na asili ya Illuminat na hio ilikuwa kazi ngumu sana kwake kutokana na usiri wa jamii hizi.
Sheikh Assad baada ya kufanikiwa kujiunga na jamii hio alipewa kazi nyingine ya kushawishi mataifa ya kiarabu kuanza uwekezaji nje ya mipaka yake, hii haikuhusisha serikali tu bali mpaka kwa sekta binafsi, kwahio kazi hioi ilikuwa ikimaanisha kwamba ashawishi matajiri ambao wapo kwenye serikali za kiarabu kuanza kuwekeza kwenye mataifa makubwa , hususani yale yenye uchumi mkubwa , ikumbukwe mataifa ya kiarabu kwa asilimia kubwa wamejaaliwa utajiri wa mafuta hivyo kuwa na matajiri wengi ambao hawakufahamika kabisa duniani, hivyo kazi ya Assad ilikuwa ni kushawishi sasa hao matajiri.
Anasema kwamba licha ya kwamba ilichukua muda mwingi kufanikiwa kwa asilimia kubwa , lakini jambo hilo liliwezekana, kwani mpaka muda huo ni makampuni mengi ya kiarabu yameweza kushikilia taasisi nyingi duniani kwa kuzimiliki, ikiwemo vilabu vingi vya mpira kama vile Man City Club na PSG , kampuni za kimitandao kama vile Twitter na maeneo mengi muhimu ambayo yangeweza kuongeza ushawishi wa mataifa ya Kiarabu ulimwenguni.
“Kwanini Hades alichagua Zaidi mataifa ya kiarabu na akaacha mataifa mengine?”Swali zuri sana Zoe.
“Hades wa zamani anaamini kwamba roho nyingi ambazo zilivamia miili ya binadamu hazijatawala sana bara la Asia, hivyo kama Athena ataweza kufanikiwa katika mipango yake ni rahisi kwa sisi kutekeleza mpango wa dharula”Aliongea na kuwafanya wasielewe tena.
“Najua hamuwezi kuelewa maana ya maneno yangu , ila mtaelewa kadri siku zitakavyoendelea kusogea , kwasasasa hatua tunayokwenda kuanza nayo ni kuhakikisha tunatambua miungu yote kumi na mbili”
“Unamaanisha miungu yote kumi na mbili ya kigiriki?”Aliuliza Zoe kwa shauku.
“Ndio najua kwasasa tunamfahamu Artemis , Appolo na Hades na hatumfahamu Athena ni nani na kavaa mwili upi , hatumfahamu Poeseido nani na kavaa mwili upi , hivyo hivyo kwa Aphrodite ,Hermes , Ares na wengine”Aliongea.
“Sheikh Assad ,kuna umuhimu gani wa kufahamu hii miungu na kwanini Hades asingeweza kutuonyesha moja kwa moja kwani ni ndugu zake?”Aliuliza Nadia Alfonso na mrembo huyu aliekuwa kimya muda wote sasa alionekana kuelewa somo.
“Hades wa zamani katupatia kama ‘Assignment’ nah io inamaana kubwa sana kwetu katika kushindana na Athena na miungu mingine lakini hata hivyo Hades hatuwezi kutuambia”Aliongea.
“Roma anaifahamu miungu mingine?”Aliuliza Nadia kwamara nyingine.
“He is God , So he is aware of them and most of all there is god`s treaty?”Aliongea.
“God`s treaty?”
“Ndio kuna mkataba ambao wamesaini miungu yote kumi na mbili”Aliongea.
“Unahusiana na nini?”Aliuliza Pastor Cohen.
“Mambo mengi ambayo siyajui lakini jambo moja ninalojua kwa uhakika ni kwamba mkataba huo pia ulikuwa ukiwazuia miungu kutotajana wala kutoa siri juu ya miili waliovaa labda kwa matukio maalumu pekee”Aliongea na kufanya kila mmoja kushangaa.

ALUTA CONTINUARA

CONTACT :0687151346 WATSAPP
Shekhe wa Vatican kakutana na Padri wa Maka😳😳
 
SEHEMU YA 598B.

NORTH POLE.

Ni katika ncha ya kaskazini ya dunia chini ya kofia ya barafu kulikuwa na eneo jipya kabisa ambalo linafanya kazi.

Ni eneo ambalo lilikuwa na nusu ya muundo kama ambalo alikuwa akifanyia kazi Yan Buwen na Lekcha.

Kulikuwa na vifaa vingi ambavyo havikuwa vya kawaida vyenye uwezo mkubwa wa akili bandia vikifanya kazi kwa mipangilio maalumu ya kimfumo , vikifanya ukaguzi wa baadhi ya taarifa na kisha kudhidhibiti kwa wakati mmoja.

Katikati ndani ya eneo hilo lenye upana mkubwa kama ukumbi kulikuwa na kifaa kikubwa ambacho kipo kwa mfumo wa duara lakini kilichotengenezwa na barafu tupu, kifaa hiki kilikuwa kikielea angani huku chini yake kukiwa na mwanga uliokuwa ukimulika chini kwenye sakafu bila kusambaa .

Juu kabisa ya kifaa hicho kulikuwa na matundu ambayo yalikuwa kama mabomba ambayo yalikuwa yakitoa nishati ya Ant- matter, kwa macho ya haraka haraka ilikuwa ni kama vile kuna kitendo cha mchakato wa uwiano uliokuwa ukifanyika , kifaa hichi ni rahisi kusema kilikuwa na muundo kama wa satilaiti za angani kwa kiasi kikubwa.

Eneo hilo lilikuwa na baridi sio ya kawaida kiasi kamba kila kitu ambacho kilikuwa katika hali ya maji kiliganda.

Kwenye kitanda ambacho kilikuwa kimejaa barafu alikuwa amelala mwanaume aliekuwa amevalia Mask na mavazi meusi huku akiangalia runinga iliokuwa upande wa kulia kwake.

Bwana huyo hakuonyesha kupendezwa wala kujali vifaa hivyo vya kiteknoloiia ambavyo vimetengenezwa na binadamu wa kawaida katiika ufanyaji kazi wake lakini licha ya hivyo hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuwepo hapo kama mlinzi , ukiachana na kazi yake ya kukusanya taarifa alipaswa kuishi hapo hapo bila ya kuondoka.

Haikujalisha ni mtukutu kiasi gani lakini hakuthubutu kukiuka maagizo ya Athena.

Ghafla tu akiwa amejilaza kivivu alitokeza mwanamke alievalia skirt katikati ya maabara hio na kumfanya bwana mwenye Mask kuamka haraka haraka na kushuka chini na kusimama kiheshima.

“You’re here , everything is normal , Gaia ‘s heart is gradually recovering..”Aliongea kwa heshima akisema kwamba kila kitu kipo sawa na moyo wa Gaia kwa taratibu sana unaanza kupona.

Uso wa Athena ambao ilikuwa ngumu kuuona tokea apate moyo wa Gaia ulionekana kutokuwa na aina yoyote ya hisia na kama kawaida alikuwa mtu siriasi asiekuwa na utani.

“I know”

Aliongea akimaanisha kwamba anajua na kumfanya yule bwana mwenye Mask kucheka huku akiwa amekakamaa.

“Unastahili kweli kuitwa mungu wa busara , hivi vifaa vinafanya kazi nzuri zaidi kuliko alivyotengeneza Yan Buwen , Naira na Joseph Bikindi , kama sio kwa ratiba zako kuwa ngumu sidhani kama wangeweza kuhimili kwa muda mrefu”Aliongea na Athena hakumwangalia usoni zaidi ya kuanza kukagua taarifa zilizokuwa zikionekana kwenye Skrini ambazo zilikuwa zikiterememsha unyevunyevu.

“Kama ningewaachia kufanyia kazi kila kitu wangeweza kuelewa kanuni za ki utendaji , kuweza kutengeneza mwenyewe ilikuwa ni kwa taratibu za kiusalama”

“Ndio, hakika umekuwa na umakini mkubwa ..”Aliongea huku akionyesha kuwa na mashaka ya kuendelea kuongea lakini alivuta pumzi na kuzishsuha na kisha akaendelea.

“Malkia kwanini tusichukue pia zile Clones ambazo ametengeneza Yan Buwen, alichukua muda mrefu kukamilisha je zimegeuka na kuwa hazina thamani?”

“Nina maana yangu kwa clones zile kutengenezwa na kutokuzitumia kwa muda huu , ilikuwa ni kwa ajili ya kuziunganisha pamoja na moyo wa Gaia utakapo pona ili uweze kukusanya nguvu zote za kiuungu katika pande zote za dunia wakati ukiingia katika hatua ya kufufuka , hii itasaidia sana katika kufua baadhi ya ndugu zangu wengine waliokufa ili kutoa msaada zaidi katika ukamilifu wa moyo wa Gaia, yule mpuuzi Yan Buwen hakuwahi kuwa mtiifu kwangu alipoteza nishati kubwa ya kiuungu iliokuwa ndani ya jiwe la kimungu lakini hata hivyo utukutu wake umesaidia mpango wangu kuwa bora zaidi , kadri moyo wa Gaia utakavyoendelea kunyonya damu ya Titan mchakato wake wa kupona utakamilika”

“Oh …!!”

Bwana mwenye Mask alijikuta akielewa lakini kwa wakati mmoja akichukia , kama angejua baadhi ya vitu havikuwa na umuhimu kwanini alifanya kazi kubwa ya kuvihamisha ili hali katika ufufuzi huo kulihitajika vitu vichache.

“Nakuona kama hujaridhika na namna ambavyo nakabiliana na hili swala?”Aliongea Athena.

“Kwanini nisiridhike Malkia , nina shaku tu juu ya kila kitu”

“Hmmp … nilijua upo hapa kama mlinzi ndio maana nikaamua kukupatia baadhi ya taarifa”

Kwa namna ambavyo mwanmke huyo hakuonyesha kumheshimu, bwana mwenye Mask aliishia kumlaani ndani kwa ndani katika moyo wake , alijiambia kama angekuwa na uwezo wa kupambana nae basi angekuwa ashamuua muda mrefu.

“Malkia Athena , nilikuwa na wasiwasi juu ya kitu kimoja , tafadhari naomba unipe majibu”

“Ongea”

“Yule Josephi Bikindi anajua uwepo wako na naamini anaweza kuotea uwepo wa hii maabara , kwasasa anashindana na Hades , je kama taarifa zetu zitavuja haitotuletea matatizo?”Aliongea na kumfanya Athena kutoa kicheko hafifu.

“Umekosea , hajawahi kujua mimi naishi?”

“Una maanisha nini?, si atakuwa na taarifa za kumbukumbu za Yan Buwen?”

“Upo sahihi lakini bado yeye sio Yan Buwen halisi hivyo hawezi kupata taarifa zote, angeweza kupata kila kitu kama tu Chip ile iliundwa kwa ajili ya ubongo wake , lakini kwasababu iilikuwa ni kwaajili ya Yan Buwen taarifa ambazo anapata ni chache sana, kilichoweza kumuwezesha kupata kila taarifa ni kwa kutumia kompyuta na taarifa ambazo zipo katika chip sio zile ambazo zina mkanganyiko nikimaanisha zile za kihisia hawezi kuzipata.”Aliongea na kumfanya Bwana mwenye Mask kuwa katika mshangao.

“Yan Buwen ni tofauti na Joseph , yeye aliibadilisha nguvu ya Ant-Matter na kujibadilisha yeye mwenyewe kwa kujitengeneza mwili wa nishati na kadri anavyoweza kuvaa miili ya wengine ndio nguvu zake zinavyozidi kuongezeka, baada ya kujibadilisha ndio alifanya kitendo kile cha kuuvaa mwili wa Denisi na kumfanya apate hisia zake zote na baadhi ya taarifa na ndio kitu kilichomfanya kuwa na uwezo mkubwa na kufaidika kiduchu na tafiti za Yan Buwen”

“Yule kilema anaonekana kuwa na akili sana , lakini akishagunduliwa na Hades mbinu zake lazima atamezwa na kile chungu chake”Aliongea Bwana mwenye Mask.

Upande wa Athena alikuwa akiangalia moyo wa Gaia uliokuwa ukionekana katika Skrini ukicheza cheza kwa kuonyesha hali ya kupata nguvu na kumfanya kutoa tabasamu hafifu , ilionekana mipango yake ilikuwa ikienda kama alivyopanga.

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuuponyesha kwanza kwa kuhakikisha ile damu ya Titani inafanya kazi na hatua ya pili ni ya kuufufua kwa kunyonya nguvu za kiuungu katika kila pande za Dunia.

Je unadhani hilo linafanikiwa vipi na kuna athari zozote katika dunia katika mchakato huo?

SEHEMU YA 599.

“Hapana… Roma usifanye hivyo hapana”

Alikuwa ni Edna ambaye alikurupuka usingizini huku akitoa maneno hayo.

Alijikuta akihema kwa nguvu huku akikaa kitako katika kitanda , Edna bila kujijua alijikuta akishika shavu lake kwa wasiwasi , alikuwa akitokwa na jasho jingi sana kiasi cha kuloanisha shingo yake.

“Bora ni ndoto”

Aliongea kwa sauti ya chini akivuta punzi ya ahueni huku akigeuza macho yake na kuangalia saa ya mshale iliokuwa ikitembea na ilionekana tayari ishafika saa kumi na moja za alfajiri.

Alishusha macho yake kulia na kushoto na kuona Roma bado hakuwa amerudi.

Edna alijikua akikunja ndita huku akiwa na hisia ambazo hakuweza kuzielewa , jana alikumbuka aliagwa kwa kuambiwa kulikuwa na watu wanaotumia nguvu za mbingu na ardhi ambao walikuwa wakipigana na isingechukua muda mrefu lakini mpaka muda huo hakuwa amerudi.

Baada ya Edna kufikiria kwa muda aliamua kuiambia nafsi yake Roma ana nguvu sana na hawezi kuwa katika hatari , hivyo hisia za wasiwasi anazopitia muda huo anapaswa kuzipotezea.

Katika maisha yake mama yake alishawahi kumwambai kwamba ukiota kitu kibaya kinatokea basi katika uhalisia ni kinyume chake , hivyo aliamini licha ya kuota ndoto mbaya kuhusu Roma basi kinyume chake atakuwa sawa.

Baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha aligeuza sura yake na kumwangalia Lanlan ambaye alikuwa amelela usingizi mnono bila habari na kushika mashavu yake kwa namna ya kuyapungusa kwa upendo.

Lanlan alikuwa amelala huku mdomo wake ukiwa wazi na kilichomfanya Edna kutabasamu ni namna ambavyo mate yake yalikuwa yameloanisha shuka.

Kama ingekuwa ni mate ya mtu mwingine ambayo yameloanisha shuka huenda angejisikia vibaya sana lakini kwa mtoto wake aliona ni kitu cha kufurahisha .

Edna alijua hakuwahi kuzaa lakini alijiambia alikuwa tayari kuzaa na kuweza kulea na hakupaswa kuhofia kwa hilo kwani kwa Lanlan alijiona alikuwa akianza kupatia malezi.

Baada ya kuona hajisikii kuendelea kulala alitoka kitandani na kisha akaingia bafuni na kuoga maji ya moto na kubadilisha mavazi yake na kuvaa gauni la kawaida sana la kinyumbani.

Zamani alikuwa mwangalifu sana kwenye mavazi ambayo alikuwa akivaa lakini baada ya kujifunza mbinu za kijini alikuwa akivaa chochote ambacho kilikuwa na uwezo wa kumsitiri bila ya kuwazia.

Kutokana na Iringa kuwa na baridi kwa muda huo hakuna ambaye alikuwa macho hivyo alitoa laptop yake na kuingia katika mfumo wa Vexto wa kiutendaji .

Alitumia madaraka yake makubwa kuingia kwenye Server za kampuni kutafuta data ndani ya matawi ya kampuni yake katika mataifa mbalimbali.

Ijapokuwa inajulikana kwamba Ernest Komwe alikuwa amepewa nafasi ya kuwa CEO , haikumaanisha kwamba alikuwa amempa madaraka yote, hata timu yake ya Athena ilikuwa chini yake pekee na Ernest hakuwa akifahamu uwepo wake.

Kazi ya kitengo cha Athena ilikuwa ni kama kitengo cha CIA , na walikuwa wakifanya kazi ya kukusafanya taarifa zote ambazo zilikuwa zikihusiana na kampuni tanzu zote za Vexto dunia nzima.

Edna alifanya baadhi ya taarifa za kampuni kuwa siri kwa ajili ya kuilinda , alikuwa amestaafu lakini hakutaka kuona kampuni yake ikiingia katika matatizo , isitoshe ilikuwa ni urithi pekee ambao alikuwa amechiwa na wazazi wake.

Alitengemea usimamizi wake wa kampuni kuja kutofautina sana na wa Ernest Komwe na hili hakutaka kuingilia kutokana na kujua kila mtu alikuwa na mtazamo binafsi na sera katika kukabiliana na mambo , lakini alikuwa na haki ya kumrekebisha pale anapoona kinachofanyika kinaenda kinyume na sera kuu ya kampuni.

Mpaka anakuja kumaliza kusoma baadhi ya nyaraka nje kulikuwa kumeshakucha vizuri na watu wa nyumba hio walionekana wakianza kuwa bize.

Aliangalia saa na kuona ametumia zaidi ya masaa matatu na muda umeenda hivyo alimsogelea Lanlan na kisha akamuasha huku akimbeba juu juu na kumfanya Lanlan kuikumbatia shingo ya mama yake huku akiwa amefumba macho yake.

“Lanlan umejichafua na mate mwili mzima , ninaenda kukuogesha”

“Mommy kwani muda wa kifungua kinywa tayari?”

“Unajua kuwaza kula tu , haya vua kwanza hizi nguo za kulalia”Aliongea huku akimsaidia kuvua.

Baada ya kumvua nguo mwili wake wote ulikuwa wazi na kuonyesha nyama nyama kutokana na ukibonge wake .

Ilikuwa ni ngumu kuamini mtoto mdogo kama huyo alikuwa na uwezo wa kushindana na mtu mzima na kumzidi nguvu.

Edna alikuwa akipenda sana kumuogesha Lanlan , sababu moja kubwa ni namna mwili wa Lanlan ulivyokuwa mlaini kwa kuugusa , haikushangaza Roma kupenda mara nyingi kufinya mashavu ya Lanlan kwani ni hisia ambazo alikuwa akipata,

Baada ya kuogeshwa na kuvalishwa nguo safi pamoja na sweta Lanlan kwa furaha zote alitoka chumbani na kukimbili nje kwa ajili ya kutafuta msosi.

Ijapokuwa hakuwa amemuona baba yake, lakini kitendo cha Roma kupotea mara kwa mara kilimfanya kuzoea na kutokuuliza hata pale asipomuona.

Edna alikuwa akijiuliza ni kwa namna gani anakwenda kumueleza Afande Kweka juu ya kutokuwepo kwa Roma. Na alijiambia labda hakupaswa kuelezea chochote na kukaa kimya tu.

Lakini mara baada ya kufika katika dining hall , Edna aliona huenda hakupaswa kuelezea chochote , hali ya kimazingira ya eneo hilo ilikuwa tulivu mno huku baadhi ya sura zikionekana kuwa katika hali ya kimawazo.

Kilichomshangaza ni uwingi wa watu waliokuwa wapo eneo la sebuleni muda huo wa saa tatu kwenda saa nne, , mgeni mmoja wapo ya aliekuwa akimfahamu alikuwa ni Tajiri Aziz na alishangazwa kumuona akiwa katika eneo hilo.

“Edna umeamka , nilikuwa nikitaka kuagiza mtu aje awaite , Roma amerudi?”Aliuliza Afande Kweka mara baada ya kusalimia.

“Tokea aondoke usiku hajarudi , babu umejuaje aliondoka?”

“Tumepokea taarifa kutoka Rwanda Raisi Jeremy jana alishambuliwa na gaidi ambaye ametokea upande wa Yan Buwen , imekuwa bahati Raisi Jeremy hajapata majeraha baada ya kusaidiwa ki ulinzi na watu wake , taarifa pia zimesema Roma ndio moja wapo ya watu waliokuwa wakipambana na gaidi hilo”

Edna mara baada ya kusikia habari hio alijikuta moyo wake ukipia kite, hakuamini alichohisi Roma usiku kilihusiana na baba yake mzazi kushambuliwa, alishukuru kusikia Raisi Jeremy alikuwa salama.

“Edna Raisi Jeremy ni mzima wa afya hajapatwa majeraha ya aina yoyote,ila ameniagiza kuja hapa kutoa taarifa ya kile kilichotokea”Aliongea tajiri Azizi.

“Edna usiwe na wasiwasi tunaamini Roma atakuwa salama , nadhani wewe mwenyewe unamjua vizuri likija swala la mapambano?”Aliongea Afande Kweka akijaribu kumtuliza Edna ambaye alianza kuwa na wasiwasi na hata kwa Edna alipunguza wasiwasi wake na kujiambia Roma ana nguvu na hawezi kushindwa na gaidi.

“Afande kilichonileta hapa ni jambo lingine kabisa ambalo pia linahusian ana tukio la jana na ndio maana jeremy ameniambia nilifikishe mimi mwenyewe na isingekuwa vizuri kutoa taarifa kwa njia ya simu”

“Unaweza kutuweka wazi Aziz”Aliongea na kumfanya tajiri Azizi kuwa na wasiwasi kidogo na kugeuza shingo yake kulia na kushoto kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akikagua.

“Ni kuhusu Denisi”

“Denisi !! nini kimemtokea?”

“Kulingana na maelezo ya Raisi Jeremy Gaidi ambae amemshambulia alikuwa ni Denisi kimuonekano na Roma mwenyewe ameweza kushuhudia kila kitu na alikiri mwenyewe sio Denisi , hivyo ni rahisi kusema Denisi hatunae tena…”Aliongea

“Krang !!!”

Ni sahani ya udongo ilioweza kusikika ikidondoka chini na kuwafanya watu wote kugeuuza shingo zao na hapo ndipo walipomuona Damasi akiwa amesimama huku akitetemeka na kutoa macho.

“Mama .. Ashley !!!..Madam”

Waliongea wote kwa pamoja lakini palepale Damasi alidondoka chini na kupoteza fahamu , ilikuwa bahati aliweza kuwahiwa kushikilia na hakugonga kichwa chini.

******

Baada ya muda kupita hatimae aliweza kufumbua macho yake taratibu na kuangalia anga kupitia upenyo uliokuwepo katikati ya matawi ya miti.

Masikio yake yalihisi kupulizwa na upepo usio kuwa na nguvu sana huku pua zake zikiweza kunusa harufu ya majani.

Sophia bado alikuwa akihisi maumivu kiasi katika kifua chake na aligeuza shingo yake palepale nakuangalia pembeni na aliweza kumuona Roma ambaye alikuwa ameegamia kwenye mti mrefu akimwangalia.

“Roma..!”Sophia aliiita kwa mshangao na kwa haraka sana alipeleka mkono na kuanza kujikagua , alionyesha alikuwa na kumbukumbu zote ya kile kilichotokea , lakini alishangaa kuona alikuwa amepona.

Baada ya kujua Roma ndio ambaye amemponyesha na yupo salama palepale alianza kujisikia vizuri na kushukuru ndani kwa ndani.

Alikaa kitako na kuanza kuangalia mazingira ya msitu huo uliokuwa na miti na vichaka vizito mno na kujikuta akishangaa.

“Bro Roma hapa ni wapi ?”Aliuliza kwani mara ya mwisho alikumbuka alikuwa Shushani, lakini alijikuta akishangaa mara baada ya kumuona Roma akitingisha kichwa kwa ishara ya kukakataa huku akiwa na macho ya huzuni ndani yake.

“Sijui chochote hapa ni wapi, ninachokumbuka mara ya mwisho tulikuwa Shushan na wakati nikijaribu kukuchukua ili kuondoka na wewe mnara uliokuwa ukipigwa na radi ulituvuta kwa kasi na kutumeza ,ile nguvu ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba nilishindwa kushindana nayo , lakini cha ajabu mara baada ya kuvutwa kufumba na kufumbua tulikuja kudondokea , kwasababu ulikuwa na majeraha ilinibidi kukuponyesha kwanza na kukusubiri uamke ili tujue tunafanya nini”

“Unamaanisha ule mnara wa kukamata mapepo?”

“Sophia unaujua ule mnara jina lake, je unajua nini kimetokea?”Aliuliza Roma huku akiwa na tumani mara baada ya Sophia kuonyesha kuujua.

“Sijui sana ila wakati najifunza maswala ya Kung fu niliweza kupewa baadhi ya maelezo kuhusu ule mnara na inasemekana una historia kubwa sana licha ya kwamba hakuna taarifa zozote zinazoelezea namna ulivyojengwa na nani alijenga , unaitwa Demon Lock Tower, licha ya wengi kujua jina lake lakini hakuna ambae anajua kazi yake ni nini na kuna makisio ya hapa na pale tu”Aliongea Sophia

“Kama ni hivyo basi tuna tatizo kubwa lipo mbele yetu , hili eneo nimejaribu kulichunguza na linaonekana sio la kawaida na kuna vitu vingi vya kutisha”

“Nini tatizo , mbona sioni chochote cha kutisha naona ni msitu tu wa miti wenye mandhari nzuri”Aliongea Sophia huku akizungusha kichwa chake kulia na kushoto akijaribu kukagua mazingira.

“Bado hujaelewa kinachoendelea ndio maana , hili eneo sio la kawaida , kila kitu kinaweza kuonekana kawaida lakini sio kama unavyodhania, nimejaribu kuchunguza kwanzia hapa na maeneo ya karibu na nimegundua vitu vingi vya ajabu , nimeshindwa kuita uwezo wangu wote wa kijini, nguvu ya kiroho katika hili eneo ni ndogo mno na mawasiliano yangu kati ya mbingu na Ardhi ni ya kiwango cha chini , ni rahisi kusema hata nitake kupaa hapa na kukutoa siwezi kufanya lolote , nimejaribu kupaa kwenda juu zaidi angani lakini ni kama hapo juu kuna kizuizi kwani nimeshindwa kupita kwenda juu zadii na nimerudishwa chini”Aliongea Roma huku akionyesha wasiwsi.

Sophia alipoambiwa kuna tatizo kubwa lipo mbele yake alikuwa na wasiwasi lakini mara baada ya kupewa maelezo wasiwasi wake uliondoka na kumwangailia Roma kwa tabasamu.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , tunaweza kutembea hapa huku tukitafuta namna ya kurudi”

“Unaonekana una matumaini makubwa , sijui nikuambie uwezo wako ni mdogo kuelewa au una bahati?”

“Kwani una haraka sana ya kutaka kurudi?”

“Ndio nina haraka sana ya kurudi , hapa sijui ni wapi na hisia zangu zinaniambia nipo nje ya mfumo wa dunia ya kawaida , naogopa kitu kibaya kikitokea nyumbani na kuwafanya watu wazidi kuwa na wasiwasi na dada yako anaweza kuwa na mawazo”

“Oh… upo sahihi tufanye haraka tutafute namna ya kurudi maana ni kweli sister Edna na wengine wote watakuwa katika hali ya wasiwasi”Aliongea lakini bado hakuonyesha kuwa na wasiwasi na kumfanya Roma amwangalie.

“Sophia wewe huna wasiwasi?, naamini kama taarifa zitawafikia wazazi wako watakuwa na wasiwasi mno na wanaweza kutumia kila njia kukutafuta”

“Najua ndio watakuwa na wasiwasi ,,,lakini kwasasa nina furaha maana nipo na wewe”Aliongea huku akishindwa hata kuamini ni yeye alietamka maneno hayo na alijikuta akiona aibu na kuangalia chini.

Roma alijiambia msichana huyo aliekuwa katika mavazi ya kitamaduni ya wachina alionekana vizuri akiwa na aibu za kike, kama kuna watu wangekuwa wanawaona wangesema Roma anatongoza Monk wa kike.

“Ila Sophia kwanini ukaamua kuwa mjinga , hata kama ulipanga kumchanganya kwa muda yule gaidi usingechukua hatua ya hatari namna ile , hupaswi kufanyia utani mwili wako, kama sio mimi kukuponyesha haraka ingekuwa ndio mwisho wako”

“Najua nilifanya kitu cha hatari ,, nitakuwa makini siku nyingine”Aliongea na kumfanya Roma amsogelee na kumzodoa na kidole kwenye uso.

“Kadri siku zinavyosogea ndio unazidi kuwa mjinga , haishangazi wewe na Edna kutokuwa na undugu wa damu maana mnatofautiana sana kwenye kufikiri, kama ni Edna asingefanya kitendo cha kijinga namna ile”Aliongea na kumfanya Sophia kujisikia vibaya kutokana na mtu anaempenda kumlinganisha na mwingine na kuona yeye ni mjinga

“Mama yangu siku zote ananiambia mimi nina akili na kipaji kikubwa cha kuelewa mambo , mimi sio mjinga kama unavyosema”

“Okey , usikasirike ni maneno tu hayo, kwasasa umeshapona hivyo inabidi tuanze kutembea siwezi kukubeba na kupaa kwani hakuna uwezekano huo na nikitumia kiasi kidogo cha nguvu kilichobaki kitanifanya kushindwa kukulinda katika hali ya hatari”Aliongea na kumfanya Sophia kutabasamu.

Yeye hakujali walikuwa wapi na hata wasitoke ilimradi tu alikuwa na Roma katika eneo hilo.

Msitu huo ulikuwa mkubwa mno na hawakuelewa kama upande ambao wanatembea ndio karibu na maeneo ya watu, ukweli ni kwamba hawakuwa hata na uhakika kama katika eneo hilo kulikuwa na watu wanaoishi maana imepita siku tatu kamili wanalala na kuamka bila ya kuweza kuona dalili yoyote ya kukutana na mtu, mbaya zaidi Roma hakuwa na uwezo wa kwenda juu angani na kuangalia uelekeo maana ilikuwa ni kama vile anga limefungwa.

Katika siku zote tatu Roma alikuwa akijaribu kulisoma eneo hilo ili kuelewa mazingira yake yakoje na jambo moja ambalo aliweza kugundua ni kwamba huenda eneo hilo likawa ni dunia.

Jambo ambalo liliweza kurahisisha safari yao ni uwepo wa ndege pamoja na baadhi ya wanyama na safari ilikuwa rahisi tofauti hata na Roma alivyoenda Australia akiwa na Mage na Rufi maana huku waliweza kupata wanyama wengi na kuwa’roast’ kwenye moto.

Ijapokuwa Roma hakuwahi kuingia darasani lakini alikuwa amesoma vitabu vingi na alifaidika zaidi kutokana na kuwana uwezo mkubwa wa kukariri hivyo katika eneo hilo aliweza kuelewa bailojia yake kwa haraka.

Roma aliweza kugundua asilimia kubwa ya wanyama waliokuwa ndani ya msitu huo katika hilo eneo walikuwa na sifa nyingi na wanyama ambao katika histoia ya dunia walikwisha kupotea , viumbe hao walikuwa na tabia za ki’palenteoloji’ na zile zilizokuwa zikielezwa kaika vitabu.

Kwa maneno mengine muonekano wa viumbe hao aliokuwa akiwaona ni wale ambao ni wa zamani sana huenda kabla haa binadamu hajaanza kuwepo katika uso wa dunia.

Hata miti ambayo ilikuwa ikionekana katika hilo eneo ilikuwa mikubwa sana kuliko isivyokuwa kawaida na mingine mingi hakuwa hata akiielewa ipo katika jamii ipi ya majina.

Baada ya kutembea kwa umbali kiasi Roma aliweza kuona mti wa aina yake ambao ulimfanya kutoa macho , ulikuwa ni mti ambao ulikuwa na majani mapana huku juu ukiwa na maua mengi yaliokaa kama vipasa sauti.

“Bro… vipi kuhusu huu mti, mbona unashangaza sana?”Aliuliza Sophia.

“Nadhani tumeingia katika eneo ambalo limejitenga kabisa na dunia” aliongea na kumfanya Sophia kushangaa kwani tokea safari yao kuanza mpaka kufikia hapo ilikuwa ni ya kushangaa katika vitu vingi sana alivyoona na hata baadhi ya wanyama waliokutana nao walimshangaza sana na alitamani hata kuwa na simu yake kupiga picha maana alijiambia kama angetoka hapo na kuhadithia huko duniani hakuna ambaye angemuamini.

“Nina uhakika mti huu ni kutoka familia ya kundi la miti la Cycadaceae ambao ulithibitishwa kupotea duniani , wanasayansi wanaamini kwamba aina huu ya mmea ulipotea miaka milioni sitini iliopita katika kipindi cha Crateceous(Kipindi cha miamba chaki), ukweli ni kwamba hili eneo kila mmea wake na viumbe vyake vyote ni vya kuanzia miaka elfu ishirini kurudi nyuma , naogopa kwamba inaweza kuwa zaidi ya tunavyodhania kinachotungojea huko mbele.”

Maelezo ya Roma yalimshangaza mno Sophia hakuweza kujaribu kuwaza miaka milioni sitini ilikuwaje katika dunia.

Dakika hio hio kuna kitu kilimfanya Roma kusimama kwa ghafla na kumshika Sophia kiuo na kupaa nae kwenda mbele.

“Kuna tatizo mbele hivyo tulia kimya”Aliongea Roma kwa sauti ya chini.















SEHEMU YA 600.

Kabla hata ya Sophia kuweza kujua kilichotokea alikuwa tayari ashapaa na Roma kwa umbali mfupi kwenda mbele na wakatua nyuma ya kichaka na kujificha.

Katika sehemu ya wazi iliokuwa na miti mifupi na ardhi ya mawe mawe isiokuwa na majani marefu kulikuwa na mapigano yanaendelea.

Waliweza kuona madubwana matatu yaliokuwa mbele yao waliokuwa na miili mikubwa waliovalia mavazi ya ngozi huku misuli ya miili yao ikiwa inaonekana kama mafundo fundo ya miti na sura zao zilikuwa mbaya mno na za kutisha , madubwana hao walionekana wakijaribu kumshambulia kijana mdogo ambaye alikuwa na mwonekano wa kawaida kabisa , alikuwa na mwonekano wa kiarabu akiwa amevalia kanzu yenye rangi ya ugoro.

Kilichomshangaza Roma kuhusu huyo kijana ni muonekano wake wa nywele kuwa za rangi ya Zambarau iliokolea na hata kiini cha macho yake yalikuwa hivyo hivyo.

Roma aliweza kushuhudia wale madubwana watu ambao walikuwa na miili ya kutisha walikuwa wakijaribu kupambana na yule kijana kwa namna ambavyo ni kama vile hawakuwa wakimuona , ilikuwa ni kama vile walikuwa wakitumia hisia katika kupambana na licha ya miili yao kuwa mikubwa walikuwa ni wepesi mno na aina ya mashambulizi yao hayakuwa ya kawaida kabisa , kwani walikuwa ni kama vile wanasali na mawe yaliamka na kumshambulia yule kijana.

Yule kijana ambaye alikuwa na mwoenano wa kiarabu alikuwa akipambana kwa kutumia karatasi flani hivi za feni za mkono za kujipepea ambalo alikuwa amelishikilia mkononi na kulikuwa na moshi flani wa rangi ya zambarau mwingi ambao ulikuwa ukimtoka mdomoni na kuupepea kuelekea upande wa wale watu wasio kuwa wa kawaida, lakini licha ya hivyo alionekana kuzidiwa kwani alikuwa peke yake na waliokuwa wakimshambulia ni zaidi ya watu watatu

Kilichomfanya Roma kushangazwa zaidi na wale majitu ni kwamba alishindwa kujua ni mbinu gani wanatumia katika kupambana lakini kwa staili yao alijua kabisa walikuwa na nguvu za ziada kama za kwake , lakini kwa wakati mmoja alijua hawakuwa na uwezo mkubwa kama wa kwake

“Bro ni wakina nani wale , kwanini wanaonekana kuvaa mavazi ya tamaduni za zamani?”Aliuliza Sophia ambaye alikuwa ameziba mdomo kwa mshangao.

“Mimi najuaje , wanaonekana ni watu ambao wanavuna nishati za mbingu na ardhi lakini nguvu zao zinaonekana kuwa za kipekee , licha ya hivyo nadhani hili ni jambo zuri ambalo tumeweza kuona , angalau tunajua sasa kuna watu wanaoishi katika hili eneo”Aliongea Roma huku akipata tumaini

“Kwahio unataa kujitokeza , vipi kama wakitushambulia?”

“Lazima nijitokeze , angalau tunapaswa kujua hili eneo ni wapi na kwanini lipo hivi , lakini kwasababu wanapigana tunapaswa kuchagua upande sahihi , wale wenye miili mikubwa wanaonekana sio wa kawaida lakini mashambulizi yao ni ya kimuunganiko na kwa mtazamo wangu wataweza kumuua yule kijana wa zambarau kama itaendelea kama hivi”

“Kama ni hivyo ni nani sasa tunapaswa kumsaidia?”

“Usiwe mjinga , pale tunaepaswa kumsaidia ni yule kijana , tutatoa msaada sehemu unapohitajika”

“Oh.. “Sophia aliona ameuliza swali la kijinga na kuishia kukosa neno la kuongea zaidi.

Roma alitabasamu kifedhuli na kisha alimshika Sophia na kujitokeza kwa haraka sana mbele yao.

Wale watu mara baada ya kuona kuna watu wamejitokeza ghafla tu walijikuta wakiacha wanachokifanya na kuwaangalia kwa mshituko huku wakishangazwa na aina ya mavazi yao na mwonekan.

Mavazi ya Roma na Sophia yalikuwa yakionekana ya tofauti kabisa na ya kwao ndio maana wlaionekana kushangaa.

“Nyie ni wakina nani?”Waliuliza wote kwa pamoja kwa kutumia lugha ya kingereza na jambo hilo lilimshangaza lakini kumfurahisha Roma kwa wakati mmoja kwa kuona mawasiliano yasingekuwa shida katika hilo eneo.

“Msiwe na wasiwasi kuhusu sisi , tumejikuta tu tupo mahali hapa bila ya kuelewa tumefikaje , hivyo tunahitaji kuwaliza hapa ni wapi , hatuna mpango wa kuingilia mnachokifanya”Aliongea Roma kwa lugh aya kingereza na kuwafanya wale wote kushangazwa na maneno yake na kumwangalia Roma

“Kwahio na wewe ni mgeni hapa? , kama unataka kujua hapa ni wapi kaeni hapo msubiri kwanza tumalizane na huyu mtoto ndio tutakuambia unayotaka”Baada ya kuongea palepale waliachana nao na kisha waliendelea kupigana na yule kijana mwenye nywele za Zambarau.

Upande wa Roma hakuwa na mpango wa kuendelea kuangalia hivyo alimsogea mmoja wapo aliekuwa amempa mgongo na kumpiga ngumi yenye ujazo mkubwa akidhamiria kumvunja kabisa viungo vya mwili lakini kitu ambacho kilimshangaza Roma ni kwamba hakuweza kumdhuru zaidi ya kumrusha kwenda mbele tu.

“Pumbavu yaani wewe ni mgeni halafu unajaribu kutuchokoza sisi!”Aliongea mmoja wapo kwa hasira sana huku akimwagalia mwenzao ambae alijigonga kwenye kisiki mara baada ya kupigwa na Roma.

Roma alijikuta akishangaa kwanza mkono wake kwani alihisi maumivu baada ya kugusana na mfupa wa mgongo wa yule bwana , Roma hakutaka kutumia nguvu za kijini kupambana nae aliamini nguvu ya mkono wake ingektosha kuwaadhibu watu hao lakini matokeo yake ni nje ya mararajio.

“Unatafuta kufa kabla hata hujajua hapa ni wapi!”Aliongea yule bwana aliepigwa ngumi na aliangalia mkono wake ambao ulianza kutoa mn’gao wa ajabu na palepale alipigiza ngumi yake kwenye ardhi na kusababisha kuamka vumbi na mtetembo wa ardhi

Roma mara baada ya kuona sio kama alivyowadhania watu hao palepale aliita moto wa njano kwenye mkono wake na kupaa juu kidogo akidhamiria kuwaunguza.

“Tatizo hilo”

Waliongea kwa mshangao huku wakiona ule moto ukibadilika na kuwa vinyoka nyoka.

“Moto wa njano!!!Wewe ni nani haswa?”Waliongea kwa mshangao ni kama vile walikuwa na uelewa na anachokifanya Roma

“This guy is evil , retreat now”Waliongea wale watu wakionyesha hofu na hawakuwa na muda wa kubakia hapo kwani walianza kukimbia na Roma palepale hakutaka kuwaacha hivyo aliunganisha na moto mweupe na kutengeneza vijoka vya moto na kuvituma upande wao kuwafukuzia .

Wale watu mara baada ya kuona moto wa kimaajabu ukiwakaribia kuwaunguza palepale walifunikwa na mwaga wa njano na kupotea kwenye macho ya Roma.

Roma alijikuta akishangazwa na jambo lile na alijua kabisa wale watu wamepotelea chini ardhini na kutoroka lakini alijikuta akiikubali spidi yao kwani ilikuwa kubwa mno.

“Kwanini unanisaidia?”Aliuliza yule kijana mwenye nywele za Zambarau mara baada ya majitu yale ya sura mbaya kupotea.

“Ni rahisi sana kwasababu wewe ndo uliokuwa dhaifu , kwa kukupa lazima utataka kunipa shukrani hivyo nikiuliza maswali ni lazima utanijbu , hio ndio sababu”

“Unajuaje kama mimi sio mtu mbaya na naweza kukushukuru baada ya kunisaida?”Aliognea huku akipindisha midogo yake akionekana kama hakupenda kusaidiwa.

“Muonekano wako wa ngozi inaonyesha kabisa wewe sio mtu mbaya”Aliongea na kumfanya yule kijana kutoa kicheko huku akionekana kuwaza na alibadilisha macho yake na kumwangalia Sophia.

“Unachekesha sana lakini kwa bahati mbaya ni kwamba siwezi kukushukuru kwasababu umenisaidia “Aliongea kwa kujiamini.

“Kwanini unakuwa mgumu kuelewa, kama sio Roma kukusaidia wale watu ni hakika wangekuua”Aliingilia Sophia huku akikunja sura.

“Mna uhakika gani kama wangeweza kunia , sikuweza hata kutumia uwezo wangu wote na kubadilika na kuwa pepo , wale ni majini pepo gredi ya tatu hivyo hawawezi kunishinda”

Roma alijikuta akishangazwa na kauli yake , hakuelewa nini maana ya kubadilika na kuwa pepo pamoja na gredi ya tatu ni nini lakini alielewa kuhusu neno majini.

“Napaswa kuondoka sasa hivi , kama nilivyosema siwezi kuwasiadia kwa chochote”Aliongea kijeuri na kugeuka akitaka kuondoka.

“Naona anakiburi sana , sina chaguo lingine kama ni hivyo”Aliongea Roma akimwangalia Sophia na palepale alipotea mbele ya Sophia na alikuja kuibukia mbele ya yule kijana na kumzuia.

“Vipi , unataka kupigana na mimi , hey wewe ni mgeni hapa hivyo napaswa kukuonya , kuweza kuwashinda wale madubwana haimaanishi kwamba unaweza kupigana na mimi , mpaka sasa ushamkasirisha mmiliki wa hili eneo , kama utanichokoza hapa jua tu kwamba utakuwa umeanzisha ugomvi na mtu mwingine ambaye hutikuwa na uwezo wa kushindana nae, nawashaurni mtafute mahali pakujificha kabla hamjakamatwa”

“Nilijua wewe ndio unataka kupigana na mimi kwa kuanza kuondoka kumbe muda wote ulikuwa ukijaribu kujifanyisha tu kuwa na uwezo wa juu”Aliongea Roma na palepale alimshika mkono lakini yule kijana palepale alifanya maamuzi ya haraka na kufyatua feni lake lile la karatasi na palepale alitoa moshi wa rangi ya Zambarau kupitia mdomo na kuusambaza na kile kipepeo lakini ilionekana kutomwathiri Roma.

Roma alijiambia huyu kayataka mwenyewe hivyo hakutaka kumchelewesha kwani palepale alimshika shingo yake na kuiminya kwa nguvu.

“Nachukia sana mtu anapojaribu kunitishia na vitu ambavyo havipo , ijapokuwa sijui hapa ni wapi , simuogopi mtu yoyote , hivyo unapaswa kuniambia mwenyewe hapa ni wapi, wewe ni nani , niambie kila ninachopaswa kujua kabla sijakuua na kisha kutafuta wengine na kuwauliza”Aliongea Roma kibabe

“Unajaribu kunitishia mimi … wewe mgeni ,, nitakuonyesha nini maanaya ya nguvu ya pepo ndani yangu”Aliongea kwa hasira na pale macho yake yalibadilika na kuonekana yakiwaka moto huku yakitoa moshi wa rangi ya Zambarau kwa wingi na palepale Roma alijihisi ni kama vile anapatwa na hisia za ajabu ambazo ni hasi na muda uleule tu yule kijana sura yake ilibadilika na kuwa ya kutisha mno kama ya mnyama.

Roma aliweza kuhisi msisimko wa ajabu wa giza uliokuwa ukitoka katika mwili wa kijana huyo mwenye sura mbaya..

Sophia ambaye alikuwa karibu alijikuta akishidnwa kuendelea kusimama katika lile eneo na kutimua nduki akimuacha Roma mwenyewe.

Roma alijiambia hicho ndio maana ya Pepo la ndani , kama ni hivyo kweli pepo hilo lilikuwa likitisha mno.

Roma kitu pekee ambacho aliona kinaweza kuwa na nguvu ya kushindana na mapepo ni moto wa rangi ya bluu pekee na palepale aliuita na ukajitokeza kwenye mkono wake na yule bwana palepale alirudi nyuma kwa hofu.

“Blue true firee!!”Aliongea kwa mshangao na palepale sura yake iliweza kurudi katika hali ya kawaida.

“BroMgeni hakika una uwezo mkubwa sana kuliko wa kwangu , nisamehe kwa kukuchukulia wa kawaida , unaonaje tukikaa chini na kuongea vizuri”Alianza kujitetea

“Nilikudhania ni mtu wa heshima lakini mawazo yangu yamekuwa tofauti , umebeba sura ya kipole tu?”

Baada ya Rona kuona mtu huyo amesalimu amri alizima moto wake na kisha akampa ishara Sophia aliekuwa akiangalia kwa mbali kusogea

“Kwasababu nyie ni wageni hapa lazima kuna kitu kilichowatokea ndio maana mkajikuta mpo huku si ndio?”Aliuliza na kuwafanya Roma na Sophia kuitikia kwa kichwa.

“Elezeeni kidogo kilichowakuta ili nijue namna ya kuwaeleza, maana nyie sio wa kwanza kufika huku”Aliongea na Roma palepale alielezea kwa haraka haraka na kumfanya yule bwana kutoa tabasamu la uchungu.

“Huo ni mnara ambao hata huku upo unaitwa kwa majina tofauti tofauti kulingana na lugha ya sehemu husika lakini jina lake maarufu ni Toshia au Tongtian”

“Tongtian !! , kule unafahamika kwa jina la Demonic lock”

“Ni sawa tu kwasababu hakuna binadamu ambaye anajua jina lake halisi na alieutengeneza huku ndio tunajua historia yake, kuwarahisishia tu kwa kuanza kujibu maswali yenu hili eneo ni ulimwengu wa mapepo na nyie sio watu wa kwanza kufika huku, kila kipindi flani kuna watu wapya wanaokuja huku kwa bahati mbaya au bila kujielewa , wanaokuja ndani ya hili eneo wanakuja na tamaduni mbalimbali pamoja na lugha na ndio maana mmebaatika kukutana na sisi ambao tunazungumza kingereza , lakini huku kila lugha na utamaduni upo, hakuna lugha wala tamaduni kubwa kuliko nyingine”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa na kutokuelewa kwa wakati mmoja.

“Kwahio unasema huu ni ulimwengu wa Mapepo kama ni hivyo je huku mnaishi madubwana?”

“Ndio ila ni tofauti kidogo , sisi ni aina nyingine ya majini , kwa mfano mimi tu ni jini ambaye nina mafunzo ya kuvuna pepo alielala ndani yangu , wale watatu mliowaona hapa wale ndio madubwana halisi ambao wao katika hatua za mwanzo za kuwa binadamu , katika huu ulimwengu asilimia kubwa ni majini ambayo hayana muonekano wa kibinadamu na wachache ndio kama sisi ambao ni wavunaji wa nishati hasi kati ya mbingu na ardhi , tukiachana na hayo kwa jina naitwa Moli, kuna mambo mengi ya kuewaeleza kuhusu huu ulimwengu hivyo tutaongea taratibu taratibu ili mnielewe lakini niwaambie tu kabisa ukishaingia huku ndio basi tena hakuna kutoka”

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha hakuna ambaye alishawahi kuingia huku na akarudi alikotoka, hata wale wenye nguvu kubwa sana mpaka levo ya tisa ya kuvuna nishati ya kuyapa mapepo nguvu walijaribu kutoka wakashindwa”Aliongea na kumfanya Roma na Sophia kuangaliana kwa mshangao.

ITAENDELEA
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANO JR



SEASON 21

SEHEMU YA 601.

Moli alijitahidi kupotezea hofu ya kumuogopa Roma na kisha akaanza kuwaelezea kuhusu eneo hilo lilivyo.

Kwa maelezo yake ni kwamba eneo hilo lilikuwa likiiitwa ulimwengu wa mapepo kutokana na kwamba viumbe ambao walikuwa wakipatikana hapo ni wale majini ambao walikuwa wakijifunza mbinu za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi ili kulipa nguvu pepo la ndani(inner demon) kutawala mwili.

Inaaminika kwamba kila binadamu au kila kiumbe ana pepo lililo ndani yake na ndio pepo hio ambalo huibua hisia hasi katika roho ya kiumbe , kwa mfano wa hisia hasi ni kama chuki husda na wivu na mengineyo ya mfano huo.

Sasa kuna aina mbili za kuvuna nishati za mbingu na ardhi aina ya kwanza ni ile ya kulishinda pepo la ndani na hatimae kuweza kupata ufunuo wa siri za ulimwengu na aina ya pili ni kwenda kinyume chake yaani kulipa nguvu pepo la ndani ili kukutawala na kukufunulia siriza ulimwengu.

Aina hizi mbili za uvunaji wa nishati ndio ambazo zinatofautisha majini, kuna majini ambao wanawachukia binadamu na kuwaona ni viumbe dhaifu na kuna wale ambao wanaheshimu binadamu , asilimia kubwa ya majini wabaya wanaochukia binadamu ndio ambao wanajifunza mbinu za nishiti za kuamsha pepo la ndani(inner demon).

Sasa hapo zama za kale baada ya majini wanaojifunza mbinu za kuamsha pepo kuonekana ni hatari kwa binadamu walitokea kutenganishwa kwa kutolewa katika ulimwengu wa majini wa kawaida na kutengwa katika ulimwengu mwingine ambao haukuwa wa kawaida , ulimwengu ambao ilikuwa ni ngumu kuweza kuwasiliana na binadamu tofauti na majini ambayo yanavuna nishati kwa ajili ya kushinda pepo la ndani.

Yaani kwa maneno marahisi wale majini wazuri kama wa Hongmeng , Panas na Kekexil hawa wanavuna nishati kwa staili ambayo ni kwa ajili ya kushinda hisia zao hasi na hatimae kufunuliwa wasio yajua, ni kama mtu anavyosali au kuswali na Mungu wake ndio kinachotokea.

Ulimwengu huo sasa wa majini yanayoenda kinyumena njia za kawaida ndio ukapewa jina la Demonic Realm, yaani ulimwengu wa majini mapepo.

Njia pekee ambayo iliwekwa kwa ajili ya kusafiri kuingia katika ulimwengu huo ni kupitia minara au majengo maalumu ambayo kazi yake ni kuvuta kila aina ya nguvu kubwa ya kipepo katika dunia ambayo binadamu hawezi kuhimili.

Moli anasema katika watu ambao waliweza kuingia katika ulimwengu huo kila mtu aliingia kwa staili yake , kuna ambao waliingia kupitia minara iliokaa kimajengo na kuna wengine ambao waliingia kwa njia ambazo hazikuwa zikieleweka na kushindwa kupata majibu.

Mnara inayozungumziwa hapa ni mfano wa ile ya kuongozea meli au ndege sio minara ya simu, mara nyingi inajengwa kama nyumba flani hivi kwenda juu na hata ule wa Shushani ulikuwa hivyo hivyo ila tu ni kwamba ulitofautiana na minara mingine ya kichina ya kitamaduni.

Kwa duniani kuna uwezekano wa kuwa na njia nyingi za kuingia katika ulimwengu huo lakini ukiwa ndani ya ulimwengu huo wa Kidemonic njia ya kutoka nje ni moja tu ambayo ni Mnara wa Mbingu.

Hivyo ilikuwa ni rahisi kusema ulimwengu huo ni wa viumbe hatari visivyokuwa na huruma kutokana na namna yao ya kujifunza mbinu ya kuvuna nishati ilikuwa ikiendana kinyume na ile ya kawaida na kuwapelekea kupandwa na mashetani .

Sasa Moli anamwambia Roma kwamba ili aweze kutoka hapo ndani lazima autafute huo mnara wa mbingu ambao upo katikati ya ziwa na aweze kupitia mapigo tisini na tisa ya radi rangi ya zambarau na bluu ndio aweze kutoka.

Inaaminika kwamba mapigo hayo ya Radi tisini na tisa hayakufanana na yale mapigo tisa ya duniani , mapigo hayo katika ulimwengu huo huwa yana athari za kipekee sana ya nguvu za giza kama vile nishati za giza na nguvu ya kiroho ya giza.

Anasema imepita zaidi ya miaka elfu kumi na haijawahi kutokea jini lolote ambalo liliweza kufaulu kupigwa na mapigo tisini na tisa ya radi na kuweza kutoka katika ulimwengu huo au kupona.

Hivyo kutokana na hilo kila kiumbe kilichoingia katika ulimwengu huo pamoja na majini yenyewe ya pepo yaliokuwepo yalikubali kwamba hakuna namna ya kuweza kutoka katika ulimwengu huo kupitia huo mnara labda kwa njia nyingine ambayo bado haijagunduliwa.

“Hii sehemu ambayo tupo sasa ni Msitu Giza aneo ambalo linamilikiwa na Mbweha wa Jade, ukienda kaskazini mbali huko kuna koo nne za kimajini katika msitu wa Mianzi Zambarau , ukienda mbali mashariki huko unakutana na ukoo wa Mazimwi hatari, eneo ambalo linafahamika kama Bonde Joka ambao ukoo wenyewe unafahamika kwa jina la koo ya Joka kuu.

“Bro mimi nina miaka mia tatu hivyo inanifanya kuwa mkubwa kwako, hivyo mimi kama kaka yako ninakushauri kwamba ijapokuwa una nguvu kubwa za kimaajabu kuliko mimi haziwezi kuwa kubwa kuliko wakuu wa koo husika”Aliongea Moli akimpa Roma tahadhari.

Sophia alionekana kuogopa sana kutokana na maelezo hayo na mbaya zaidi aliposikia kuhusu uwepo wa majini wenye nguvu zaidi ya Roma.

“Je unajua miliki za kijini nje ya hapa kama vile Hongmeng , Kekexil na Panas?”Aliuliza Roma ambaye hakuwa katika hali ya woga hata kidogo.

“Nishawahi kusikia kuhusu Hongmeng na inasemekeana ni miliki ya majini wadhaifu tu wa kawaida kuhusu sehemu zingine sijapata maarifa huenda ni kutokana na nguvu yao kuwa ndogo”

“Kwahio unasema kwamba ulimwengu huu ndio wenye nguvu zaidi kuliko wa majini ya maeneo mengine”

“Inaweza kuwa kweli au isiwe kweli , lakini unapaswa kuelewa kwamba hii sehemu ilikuwepo miaka zaidi ya elfu hamsini iliopita kabla hata kwa ujio wa wale viumbe kutoka sayari nyingine waliojiita miugnu miaka elfu ishirini iliopita, kuna sehemu nyingine ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuwafanya binadamu kuwa salama, sisi tunaamini kwamba roho ya kiumbe chochote haipotei hivyo kama kweli miaka iliopita kabla ya ujio wa binadamu kulikuwa na wanyama wakubwa na wakali kama inavyohadithiwa basi roho zao zitakuwa zimeshikiliwa katika upenyo maalumu kama hili eneo?”

Roma alielewa baadhi ya maneno ya Moli , ilikuwa ni kweli kabisa miugu walikuja miaka elfu ishirini iliopita na katika kipindi hicho binadamu walikuwa wakiishi kawaida na hakukuwa na majini katika uso wa dunia hivyo moja kwa moja ni kwamba ulimwengu wa majini kama huo ulikuwepo kabla yao.

Kuhusu roho za wanyama wakubwa wakali waliokuwepo alijikuta akianza kuhishi huenda ni kweli kutokana na kumiliki Cauldron ambayo ndani yake ilikuwa na roho ya mnyama mwenye nguvu.

Roma alimuonea huruma Sophia kwa kuja nae katika eneo hilo la hatari , kuhusu Lekcha alijiambia ni haki yake kukamatwa katika ulimwengu huu kwasababu nguvu ya nishati ya ant-matter ilikuwa ni tishio sana lakini huku akiomba isitokee Lekcha kuweza kupata namna ya kujiongezea nguvu akiwa katika eneo hili kwani anaweza kumpa changamoto kutokana na kwamba hakuwa na uwezo wake kamili.

Baada ya maongezi ya muda, Moli aliangalia anga na kuona tayari lishakuwa jeusi na hakutaka kuulizwa maswali mengine .

“Bro Roma nimekuja katika huu msitu kwa ajili ya kutafuta mmea adimu , hapa ni eneo la mpakani na sikutegemea kukutana na yale majitu , ila kwa kunisaidia kwako lazima kutakuwa kumewaamsha wamiliki wa hili eneo , hivyo angalau unapaswa kuwa makini katika eneo hilo lote la Mbweha wa Jade, najua mpango wako ni kutaka kwenda kuona mnara lakini nakushauri kama mnataka kuwa salama tafuteni uelekeo wa Ziwa la mbingu”

“Kwa maelezo ambayo umenipatia haiwezi kunisumbua kwenye kutafuta uelekeo na safari ikawa ndefu?”

“Ni kheri safari yenu iwe ndefu kuliko kukamatwa na walinzi wa jumba la Mbweha wa Jade , mkuu wao anafahamika kwa jina la Mbweha wa anga wa mikia tisa na ndio ambaye ana uwezo mkubwa sana katika hili eneo kimapambano , yupo juu katika daraja la tisa huku akilindwa na mapepo wa anga therathini na sita na majitu kama mlioyaona hapa 72 hivyo fikirieni mara mbilimbili”

Roma aliweza kuelewa uvunaji wa nishati katika huo ulimwengu ulikuwa umegawanyika katika madaraja tisa na kila baada ya kupita madaraja matatu ilimaanisha nguvu na zenyewe zinaongezeka.

Kwasababu wote walikuwa na muonekano mbaya basi wanapofikia katika levo ya tatu tu ndio huweza kupata maumbo ya kibinadamu.

Unapaswa kuelewa katika ulimwengu binadamu ndio kiumbe ambaye ana muonekano mzuri kuliko aina yoyote ile ya kiumbe na asilimia kubwa ya hawa viumbe wasioonekana wenye miili mibaya ndoto yao ni kuwa na miili ya kibinadamu na hata hapo mwanzo ilisemekana majini yalikuwa yakiwaonea wivu binadamu kwa kuwa na maumbo mazuri ya kuvutia ndio maana majini mabaya wakawa wanawaingia binadamu na kuwatawala kiroho.

Katika mafunzo ya kawaida ya kijini ili kuweza kuwa na uwezo wa kujitengenezea mwili wa kibinadamu sharti ni kuingia katika levo ya Nafsi.

Kwa maelezo ya Moli alielewa kwamba katika hilo eneo hakukuwa na levo ya kuipita dhiki kutokana na kukosekana kwa radi za mapigo tisa.

Kundi la kwanza la majini ambalo uwezo wao ni wa kawaida ni kuanzia daraja la kwanza mpaka la tatu , kundi la kati ni kwanzia daraja la nne mpaka la sita , kundi hili lilikuwa la watu wachache zaidi, kundi la mwisho ni kuanzia saba ndio waliitwa majini pepo ya anga au mashetani pepo wa anga”

Roma hakutaka sana kujali kuhusu uwepo wa Mbweha wa anga wa mikia tisa na isitoshe kwa maelezo ya Moli hakuna ambaye alikuwa akimfahamu vizuri na kingine inasemekana alikuwa tofauti sana na majini na hakuwa ni mwenye kujali sana , wasiwasi wa Roma muda huo ni namna ya kutoka katika ulimwengu huo tu kwa namna yoyote ile.

Roma aliagana na Moli kisha yeye na Sophia walianza kutembea kuelekea upande wa Kaskazini , kulingana na maelezo ya Moli mji wa kwanza watakao kutana nao ni Mji wa Wingu Jeupe , ambao ndio mji mkubwa zaidi ndani ya miliki ya Mbweha wa Jade na itawachukua siku tatu katika kutembea.

Walipewa taarifa nyingine ya kutafuta mawe maalumu ndani ya mji huo ambayo yanaitwa kama mawe ya kiroho ambayo hutumika kama hela au njia ya kibiashara.

Roma hakutaka kutumia njia ya pemeni kama ambavyo ameelekeza Moli maana kutokana na maelekezo yake njia rahisi kufikia ziwa la mbingu ambapo kuna mnara ni kupitia ndani ya jiji la Wingu jeupe.

*******

Siku tatu ziliweza kupita na taratibu za maombolezo ya kifo cha Denisi ziliweza kufanyika ndani ya Iringa, haikuwa na maana ya kwenda Songea kwa ajili ya kuomboleza msiba kutokana na kwamba hakukuwa na mwili wa kuzika , hivyo kilichofanyika ni ibada ya kawaida tu kupitia kanisa la kikatoliki na kuruhusu jamaa na marafiki kutoa salamu za pole.

Licha ya maombolezo hayo, wanafamilia hao walikuwa katika hali ya wasiwasi kuhusu Roma , katika siku hizo tatu waliweza kupewa taarifa zote kutokea China kuhusu kupotea kwa Roma na Sophia kupitia mnara.

Ilikuwa ngumu kuamini kwa tukio hilo lakini kutokana na maajabu aliokuwa akifanya Roma iliwafanya kuamini kwamba ni kweli wameweza kupotea.

Asilimua kubwa ya wana ukoo waliogopa zaidi kupotea kwa Roma kwani alikuwa ni kama ashakuwa mhimili kwa ukoo wao kwa yale ambayo yametokea hivi karibuni , waliogopa maadui zao kuwachukulia hatua na kujaribu kuwayumbisha kwani kupotea kwa Roma ilimaanisha uwiano wa kinguvu kubadilika , hatua za awali walizochukua ni kufanya jambo hilo kuwa siri ya familia.

Afande Kweka alionekana kuchoka kweli kutokana na kutopata usingizi kwa zaidi ya siku tatu mfululizo , katika eneo la sebuleni alikuwa amekaa pembeni ya raisi Senga pamoja na Damasi ambaye macho yake yalikuwa yamevimba na mbele kabisa alikuwa amekaa Blandina mama yake Roma pamoja na Edna aliempakata Lanlan.

Kushoto kwao kulikuwa na mgeni ambaye ni mchina alievalia mavazi ya kitamaduni , alifahamika kwa jina la Abbess Yumiao na ndio aliekuwa ni mkuu wa Dhehebu la Shushani na ndio aliefika hapo kutoa taarifa.

Wageni wengine walikuwa ni wazazi wa Sophia , Balozi Athumani pamoja na mke wake.

“Tuliweza kutafuta kuzunguka eneo lote la Shushani lakini hatukuweza kupata chochote , tunaomba radhi kwa hilo “Aliongea yule Master.

“Na amini mmefanya kazi kwa jitihada kubwa , hata hivyo unaonekana ulikuwa ukimpenda Sophia hivyo haiwezekani ukakubali apotee kirahisi”Aliongea Afande Kweka kwa kingereza.

“Jamani Sophia wangu mimi,……”

Mama yake Sophia alikuwa akitoa machozi na kuwafanya watu wote waliokuwa hapo ndani kumuonea huruma.

“Sophia atakuwa sawa naamini yupo na Roma na mimi namwamini atamrudisha akiwa salama, huna haja ya kuendelea kulia, Roma ni mwanangu na imani yangu inaniambia atarudi salama”Aliongea Blandina akijaribu kumpoza Mama Sophia lakini wakati huo huo na yeye akitoa machozi , ilikuwa ni kama alikuwa akijifariji.

“Blandina haina haja ya kuendelea kulia , hatujapokea taarifa mbaya, naamini ataweza kurudi muda si mrefu”Aliongea Raisi Senga huku akimwangalia Damasi ambaye muda wote alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.

“Upo sahihi mwanangu Roma atakuwa sawa ,naamini hilo..”Aliongea huku akifuta machozi.

“Okey kwasasa tutaliacha hili kwa jeshi letu kitengo cha wachawi , Master Yumiao na kitengo cha jeshi la Wachawi kutoka china cha Yellow Flame iron Brigade na wao ndio watatupa taarifa ya kile kinachoendelea, Senga umefanya vizuri kwa kuongea na uongozi wa serikali ya china kwa kuruhusu wanajeshi wetu kuweka kambi katika dhehebu la Shushani naamini muda wowote wataweza kupata fununu”Aliongea Afande Kweka na Raisi Senga alitingisha kichwa.

















SEHEMU YA 602.

Siku tatu ziliweza kuwawezesha kutoka katika Msitu wa Giza , ijapokuwa ulimwengu huo ulikuwa ni ardhi ambayo haijagawanyika lakini eneo lilikuwa kubwa mno.

Roma kadri ambavo alikuwa akitembea ndio uvumilivu wake ulizidi kupungua na ili kurahisisha safari aliweza kutumia nguvu yake ya kijini kujaribu kupaa kwa kuruka ruka ruka kama chumba ili kufupisha safari.

Inasemekena mwishoni mwa eneo hilo kulikuwepo na bahari isio na mwisho ambayo mito yote katika eneo hilo humwaga maji yake na kwa maelezo ya Moli ni kwamba wasafiri washawahi kusafiri lakini hawakuwahi kufika mwisho na kuona ardhi ndio maana wakaipa jina la Bahari sio na mwisho.

Mto ambao ulikuwa ukipita katika jiji la Wingu jeupe ulikuwa na upana wa kilomita moja au zaidi na kwasababu ya mvuke uliokuwa ukitoka pamoja na Ukungu ilifanya jiji hilo kuitwa Jiji la wingu Jeupe kutokana na kwa mbali liliweza kuonekana nyumba zilizofunikwa na wingu.

Kilichomshangaza Roma na Sophia ni kwamba licha ya eneo hili kuwa la majini lakini miundo mbinu yao ilikuwa ni ya kawaida kabisa kama ya binadamu, kulikuwa na kila aina ya staili ya usanifu wa nyumba karibia tamaduni zote na mpangilio wake ulikuwa ni wa kueleweka kwani kulia na kushoto kulikuwa na nyumba huku katikati kukiwa na barabara,

Halikuwa aneo kama ulimwengu wa kawaida kutokana na kukosa ule ukisasa, lakini hata hivyo haikushangaza sana kwani kuna watu wengi ambao walikuwa wakiingia katika ulimwengu huo kutoka dunia ya kawaida na kuleta ustaarabu wa aina tofauto tofauti.

Kwa muonekano wa eneo hilo ni kama vile majini hao hawakuwa na tamaa ya kuujenga mji kuwa wa kisasa zaidi na sababu ya moja kwa moja haikueleweka na isitoshe Roma hakuwa na taarifa za kutosha.

Tokea kuumbwa kwa binadamu aliweza kupewa mamlaka ya kutawala viumbe vyote hata wale wasiokuwa wakionekana huenda ndio maana kila kitu majini yalichofanya kilikuwa kikiendana na binadamu wa kawaida.

“Bro tunaingia hivi hivi tu bila tahadhari , vipi kama wakitushambulia?”Aliuliza Sophia aliekuwa akiangalia jiji hilo kwa wasiwasi kupitia mlimani.

“Tunapaswa kuingia ndio hata kama watakuwa ni wakali zidi yetu , kwanza kabisa bado siamini maneno yote alioongea Moli hivyo lazima nifike katika mnara huo na kujionea mwenyewe kwani ndio njia pekee ya sisi kutoka huku, pili kama alivyotuambia lazima tutafute mawe ya kiroho ili kuweza kununua wanyama wa kijini ili tuweze kusafiri kwa urahisi na kutoka katika hilo eneo”

Kwa maelezo ya Moli ili kuishi katika eneo hilo hakuhitajika pesa bali mawe ya kiroho ndio hutumika kama njia ya biashara.

“Bora uwezo wangu ungekuwa mkubwa , kwa staili hii ninakwenda kuwa mzigo tu kwako”

“Hivi unajua siku zote sisi wanaume hatupendi wanawake wenye nguvu , tunapenda mwanamke ambae ni tegemezi, hakuna mwanaume ambaye atakupenda kaa una nguvu kumzidi na huna unachomtegemea”

“Sidhani ni kweli, kama ni hivyo kwanini mpaka leo hii hujaweza kuzikubali hisia zangu”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta hewa kwa nguvu.

“Hilo limetokea wapi katika muda kama huu? , aisee naona unazidi kuwa mwanamke jasiri”

“Unataka niwe muoga , nishakaa chini na kufikiria tayari , kama kweli hatuwezi kutoka huku , hakuna wa kujali maswala ya kimaadili, hivyo matatizo yetu yote yatatatulika kirahisi”Aliongea akimaanisha kwamba kama hawawezi kutoka inamaana yeye na Roma wanaweza kuwa wapenzi.

Roma hakuteka kuendelea kusikiliza maneno ya Sophia na aliishia kumwambia waanze safari ya kuingia ndani ya jiji hilo na Sophia hakutaka kuendelea kuongea kwani aliogopa kumkasirisha.

Haikuwachukua dakika nyingi hatimae waliweza kuingia katika mji huo huku wakiangaliwa na majini hao kwa macho yasiokuwa ya kawaida .

Katika ulimwengu huo elimu haikupewa kipaumbele , kinachopewa kipaumbele ni mafunzo ya uvunaji wa nisahti pekee na kufika katike levo ya kuweza kuwa na mwili wa kibinadamu.

Jini ambalo halina mwili wa binadamu mara nyingi huonekana dhaifu sana na hufanya kazi za kitumwa.

Cha kuwashangaza zaidi ni kwamba ndani ya eneo hilo kulikuwa na wanyama wa ajabu sana ambao walikuwa wakitumika kama vile ni farasi , hakukuonekana magari na vifaa vingine , maisha yao yalikuwa ni yale ya kikale zaidi.

Kila kitu kilionekana kuwa kipya kwa Sophia , lakini kwa namna moja ni kama anafanya utalii.

Ni muda huo huo wakati wakipita katika jengo ambalo lilikuwa limefunikwa na ngozi nyingi kwa nje alionekana mwanamke jini aliekuwa katika mwili wa kibinadamu akiwaangalia , alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa na mwonekano wa kiarabu.

Alikuwa amevaa gauni refu ambalo lilikuwa na mkato wa kuacha shingo wazi huku akiwa amevaa cheni kubwa za madini ya dhahabu tupu ambazo zilikuwa ni za kuwaka waka.

“Wewe mwanaume wa kibinadamu nadhani wewe ni mgeni”Aliongea yule mwanamke kwa lugha ya kingereza lakini rafudhi yake haikuwa ni ya kunyooka , Roma aliamini huenda alikuwa akizungumza lugha nyingine tofauti na kingereza.

“Nimekuja huku bila ya kujielewa , nadhani unaweza kuniona mgeni”

“Unaonekana sio wa kawaida , karibia ya wote walioweza kukamatwa na mnara ni kwasababu ya aina moja”

“Inaonekana watu wengi wamekuja huku kabla yangu , tumeingia hapa lakini hakuna ambaye ametuongelesha zaidi ya kuangaliwa tu, ni kama jambbo ambalo limezoeleka”

“Upo sahihi , siwezi kusema kuna binadamu wengi lakini binadamu wanakuja mara kwa mara , nyie mnaweza kuwa binadamu lakini hapa hamchukuliwi kama alien , jina langu naitwa Mei , je tunakuitaje”

“Niite Roma Ramoni”

“Oh.. Braza Romaa,,!!!”

Aliongea huku akimsogelea Roma karibu kabisa huku akisuguanisha manyonyo yake na kifua cha Roma kwa staili ya kumtega.

“Braza Roma kwasababu ushakuja huku unapaswa kuyachukulia maisha kawaida , unaonaje ukiingia ndani na kuungana na wengine kula raha”Aliongea na kumfanya Roma kuangalia jengo hilo na kuweza kugundua nini kinafanyika huko ndani.

“Kwahio hata huku mna madanguro?”Aliuliza wakati huo Sophia alionekana kuwa na aibu kwa namna ambavyo Mei alikuwa akijigusanisha manyonyo yake na Roma.

“Kuna tatizo gani juu ya hilo , majini pia yana hisia , unadhani ni binadamu tu ambao wanapaswa kuuza miili yao na sisi majini hatuwezi?”Aliuliza lakiini Roma alipotezea.

“Nimeambiwa kwamba hela katika ulimwengu huu ni mawe ya kiroho kutoka bahari isio na mwisho , sina hayo mawe hivyo siwezi kutoa malipo hata kama nikiingia”

“Roma..!!”Aliita Sophia kwa hasira na kumfanya Roma amwangalie.

“Huwezi kuingia nae huyo , kwanini unataka kufanya hivyo wakati una mke anakusubiria?”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasamu kwa uchungu , hakuelewa ni kwanini sasa hivi ndio anaanza kuwaza kuondoka katika hilo eneo.

“Lakini si ndio maana nimesema sina mawe ya kiroho”

“Wewe…:!!”

“Hakuna shida , unaweza kupata hayo mawe hata baadae , unachotakiwa unaweza kujiandikisha na kupata huduma na kisha utalipia baadae”

“Ah.. kwahio hamuogopi kwamba naweza kukimbia bila kuwalipa”Aliuliza Roma.

“Haishangazi ndio maana nasema wewe ni mgeni hapa , hili ni jiji la Wingu Jeupe na Bwana Mkuu Baiju ni sehemu ya majini pepo 36 ambaye anapendelewa sana na jenerali mkuu wa Jade, hivyo yoyote ambaye atashindwa kulipia deni lake atakutana na kifo cha maumivu”Aliongea Mei na kumfanya Roma kuelewa na sasa kusita sita.

“Basi nitapita, sijui namna ya kutengeneza hela hapa , sitaki kufa kifo cha maumivu kwa kushindwa kulipa deni , unaonaje ukiniambia sehemu ambayo naweza kupata hayo mawe pamoja na majini wanyama wa kusafiria?”Aliongea na kumfanya jini pepo Mei kufikiria kidogo.

“Braza Roma kama unahitaji hayo mawe unaonaje tukifanya biashara?”

“Niambie hio biashara”

“Huyu mwanamke hawezi kuishi kwa muda mrefu ndani ya ulimwengu huu na jini pepo lolote lenye mwili wa kibinadamu linaweza kumuua , huwezi kumlinda hivyo unaonaje tukibadilishana, mimi nitakupa mawe na yeye atabakia hapa katika Danguro langu na kutoa huduma kwa wateja , anaweza pia kuweza kulipwa bonasi ya Mawe na kuendelea kuishi”

Roma mara baada ya kusikia biashara hio alielewa ndio maana mwanamke huyo aliwasogelea , kumbe alikuwa na lake jambo la kutaka kumchukua Sophia kwa ajili ya biashara, alijiambia hauzwi mwtu hapa.

Sophia mara baada ya kusikia anataka kuuzwa alimsogelea Roma na kujibana kwake kwa hofu.

Roma alijaribu kumtuliza Sophia na kumwambia hakuna kibaya ambacho kinaweza kumpata.

Roma hakuwa tayari kumuuza Sophia kwa ajili ya kujipatia mawe, hivyo alimwambia Mei kwamba wanaondokana watajua mbele kwa mbele.

Upande wa yule jini pepo wa kike baada ya kuagana nao aliwaangalia na kutoa tabasabasamu lisilokuwa la kawaida na palepale baada ya kuwaona wametokomea upande wa mbele alibadilika na kuwa mwewe na kisha akapaa na kuondoka.

Roma baada ya kuelewa baadhi ya mitaa hio walipita pamoja na kuja kutokezea katika soko na hapo ndipo aliposhangaa kuona watu mbalimbali wakiongea lugha wanazozijua , ilikuwa rahisi kwake kuwasiliana kutokana na kujua lugha nyingii.

Roma aliulizia bei ya wanyama wa kusafiria na alipotajiwa ndio alipogundua wale wanaosafiri kwa kasi tena kwa kupaa walikuwa ghali sana na wale wa chini wanaofananana na nguruwe au Kenge walikuwa ndio wa bei rahisi.,

Hivyo ilikuweza kuwapata hao wanyama alipaswa kukusanya mawe mengi ya kiroho.

Inasemekana mawe hayo hupatikana katika bahari isio na mwisho na wale ambao wanaoenda kuyatafuta huwa ni kama wanaenda vitani kwani kuna viumbe wakali sana chini bahari ambao wanapaswa kupigana nao na kisha kuweza kuchukua mawe hayo.

Hivyo upatikanaji wake ulikuwani mdogo sana ndani ya hilo eneo na ndio maana yalikuwa ni adimu na thamani kubwa.

Roma alitamani kuwa kibaka na kuibia baadhi ya majini ndani ya hilo eneo lakini alijizuia kwa kuamini huenda angeweza kukasirisha mamlaka na kujiingiza katika matatizo.

Jiji la Wingu jeupe halikuwa na vurugu kama alivyodhania , ilikuwa ni sehemu iliokuwa na utulivu na kila mtu alikuwa na mambo yake , ijapokuwa walikuwa wakikodolewa macho lakini hawakujali na kuendelea na safari.

Baada ya kutoka nje ya jiji hilo waliweza kufikia kijimlima ambacho kilikuwa kikiwapa uwezo wa kuona upande wa chini wa bonde , ilikuwa ni eneo ambalo lilikuwa na mwonekano mzuri mno.

Roma paepale alitaka kumshika Sophia ili apae nae mpaka upande wa chini wa bonde hilo lakini aliweza kuhisi kundi la watu wakija upande wao.

Dakika chache tu ilikuwa ni kama hisia zilivyomwambia kwani waliweza kusogelewa na watu ambao walikuwa wamepanda juu ya wanyama kama Kenge(Thunder Lizard) na kuwazuia kwa mbele.

Wanyama hao walikuwa ni warefu mno na wanene waliokuwa wamepakwa rangi ya dhahabu kwa juu huku wakiwa na mapembe makubwa , walikuwa wakitisha lakini walikuwa ni wapole mno kutokna na uwezo wao mdogo wa akili , walikuwa wakishambulia na mapembo yao tu hivyo ndio maana mara nyingi yalipendelewa kutumiwa kama nyenzo ya usafiri.

“Mnaonekana wageni ,Je nyie ni wapya katika hili eneo?”Aliuliza mmoja wapo , walikuwa wakiwaangalia kwa ujeuri wa hali ya juu.

Aliekuwa akiwaongoza alikuwa amevalia Vest ya ngozi ya chui na uso wake ulikuwa mpana na umekaa kama chapati huku mdono ukiwa kama kijishimo, licha ya kubahatka kuwa na mwili wa kibinadamu lakini alikuwa mbaya wa sura mno na Roma alijiambia huenda hio ndio sura mbaya ya kibinadamu alioweza kuona katika maisha yake.

“Sisi ni wageni ndio , je kuna kitu chochote mnataka kutoka kwetu?”Alijibu Roma akiwa mpole maana alishagundua walikuwa na uwezo mkubwa kama Moli.

“Mnaweza kupita katika hili eneo lakini kabla ya hapo mnapaswa kulipia ushuru”Aliongea huku akitoa tabasamu.

Roma alijikuta akiwaza , hakuamini mpango wake wa mwanzo wa kutaka kuiba sasa umegeuka na yeye ndio anataka kuibiwa , alitamani kupaa na Sophia katika hilo eneo na kuwakwepa lakini aliona hilo sio chaguo bora.

“Jamani kama kweli mnatuona sisi ni wapya na tumewajibu hivyo mnawezaje kutaka ushuru ilihali hatuna mawe ya kiroho , kwanini msitusamehe kwa leo”

“Binadamu siku zote hamkosagi maneno nyie , kama tusipokusanya ushuru tunawezaje kupata hela , kama huna unaweza kulipia kwa kumtoa huyo mwanamke na wewe kuondoka , isitoshe hana nguvu zozote za ziada na atakuwa mzigo kwako”

“Nilijua ni Madanguro pekee ndio ambayo yanaweza kufanya biashara waziwazi , nadhani mambo ni ya kimkanganyiko sana ndani ya hili eneo”

“Madanguro gani, mimi ndio mkuu wa hili eneo kwenda kule chini na kila mtu ananijua jina langu mimi Baba Huja , unatakiwa kujifikiria mara mbilimbili la sivyo nitaruhusu hawa Kenge wetu kuwala nyama”Roma alijikuta akikunja sura lakini hata hivyo hakutaka kuogopeshwa na maneno yake maana aliona kama ni kupambana nao angeweza kuwaua wote.

“Hamtaki kutupisha ilihali tunaomba kwa upole , basi sawa hata hivyo nilikuwa nikitafuta mtu wakumuibia ,Shukeni kutoka kwenye hao wanyama wenu na mtoe mawe yenu yote ya kiroho na nitawatunuku kifo cha kistaarabu”

“Hahahaa… mmemsikia ? Binadamu mgeni anapanga kutuibia sisi , hivi hata unajua nani mkuu wa hili eneo lote”

Roma hakutaka kupoteza muda palepale alisogelea jini lililokuwa karibu yake kwa kasi kubwa na kulipiga ngumi na kusababisha liteme damu kutokana na baadhi ya viungo vyake kuharibika.

Baada ya kulishambulia na ngumi ile palepale liligeuka na kuwa kama kifaru huku ikionekana ameacha shimo katika ngozi yake.

Wale hawakutajarajia kama Roma anaweza kupigana , kwanza alikuwa na spidi kubwa kiasi cha kuwashangaza , yule jini aliegeuka kifaru alidondoka chini palepale na kufariki.

“Muueni”Aliongea kwa nguvu yule bwana Huji akiwaamrisha aliokuja nao na wote kwa pamoja walimwangalia Roma kwa macho makali.
 
SEHEMU YA 603.

Wale majini walionyesha hasira za hali ya juu kutokana na kushuhudia mwenzao akipoteza maisha na palepale waliruka kutoka kwenye wale wanyama na kumsogelea Roma kwa spidi na kuanza kumshambulia.

Uwezo wao wa kimapigano mara nyingi ulitegemea zaidi kipaji na ulijumuisha upepo , mawe ,moto na barafu, mbinu zao hazikuwa chini na zile za majini ya kawaida pamoja na binadamu wanaojifunza mbinu za mbingu na ardhi

Roma hakuweza kukwepa mapigo yao kwani alijua akijiwekea ngao ndio ambavyo atazidi kupoteza nguvu zake kwa kiwango kikubwa hivyo alichokifanya ni kuita moto wa rangi nyeipe kujaribu kuwaunguza lakini ni kama walionekana walikuwa na mbinu za kuhimili moto huo sababu walianza kuongezeka ukubwa na kubadilika miili yao

Roma mara baada ya kuona mbinu hio haiwezi kufanya kazi palepale alifungua anga ya Sumeru na kuvuta Dagger ya damu ya Dragoni alioiiba kwa majini ya Hongmeng na kushambulia nayo.

Yale majini mara baada ya kuona kile kisu waliweza kukifahamu na walionyesha hofu lakini Roma hakujali kwani ndani ya dakika chache alikuwa ameshawafyeka, kisu hicho kilikuwa na tabia kwamba jeraha lake ilikuwa ni ngumu kupona lenyewe kwa haraka hivyo iliwapelekea kupoteza damu kwa haraka sana na kupoteza nguvu.

Jini pepo pekee ambalo lilikuwa limebakia ni yule kiongizi wao na baada ya kuona wenzake wote wamekufa alijikuta akipandwa na hasira maradufu.

“Nitakuuua !”Aliongea na palepale mkononni kwake kiliokana kisu cha kumeta meta na kumsogelea nacho Roma kwa kasi kwa ajili ya kumchoma , lakini Roma alionekana kuwa mwepesi kwani alimkwepa na akachukulia faida wepesi wake na kupeleka kisu chake nyuma lakini Huja alionekana kuwa na hisia kali kwani kwa wepesi aliosogea pembeni na kikapita.

Baada ya kuona hakuwa na uwezo wa kumshinda Roma alimwangalia kwa wasiwasi.

“Una bahati sana..”Aliongea akitaka kukimbia lakini Roma hakutaka kumruhusu aondoke na akaite wengine, palepale alimsogelea kwa kasi na kumchoma na kisu eneo la bega na muda huo huo akaita moto wa rangi nyeupe na kuanza kumuunguza lakini alionekana kuwa mjanja kwani palepale alipotea mbele ya Roma kwa kukimbia kwa spidi kubwa na kumfanya Roma ashindwe kumfukuzia kwa kuhofia kumuacha Sophia.

Baada ya kuwadhibiti wote kulibakia wale wanyama ambao walikuwa wamebeba mizigo aina ya viroba na Roma alimwambia Sophia aache woga na aanze kukagua kutafuta vitu ambavyo vinaweza kwuasaidia mbele ya safari.

Baada ya kukagua kwa dakika kadhaa Roma aliweza kukuta mawe ya kiroho yaliokuwa yakizungumziwa , yalikuwa ni mawe ya aina yake yalikuwa meupe sana huku ndani yake kukiwa na kitu cha rangi nyekundu kilichokuwa kikionekana, ni kama vile madini ya Almasi kwa nje na kwa ndani wekundu wake ni kama wa madini ya Rubi laini kitu pekee cha tofauti kuhusu mawe hayo yalikuwa yakipiga shoti ukishika mkononi.

Roma alijaribu kuyachunguza na kugundua kile kiini cha ndani kilikuwa ndio nguvu ya kiroho yenyewe kwani alijaribu kutumia uwezo wake kunyonya nguvu yake na kweli ndani ya dakika alihisi msisimko wa aina yake ukimwingia mwilini kama vile alikuwa akivuna nishati za mbinu na ardhi na ndani ya dakika chache tu kile kiini kilipotea.

Sasa wakati akiwa anaendelea kusachi Kenge wa mwisho aliekuwa na mzigo mkubwa ndipo alipoweza kugundua ndani yake kulikuwa na msichana mdogo aliekuwa amebebwa na alikurupuka palepale mara baada ya kiroba kile kufunguliwa.

“Naombeni msiniue waliniteka”Aliongea kwa kupiga kelele na kumfanya Sophia amsogelee kwa haraka.

“Hatuwezi kukuua usigope”Aliongea Sophia akijaribu kumtuliza , alikuwa na mwonekano wa kirembo mno na kwa haraka haraka sura yake ni kama vile ni mhindu.

“Nadhani ndio kwa mara ya kwanza ameweza kuupata huu mwili wake , nguvu zake ni za chini mno kuliko wengine”Aliongea Roma mara baada ya kumchunguza.

“Ndio nimeingia daraja la tatu la kupata mwili”Aliongea lakini upande wa Roma kuna kitu ambacho sio cha kawaida ambacho alikuwa akikiona kwa msichana huyo lakini hakutaka kujifanya mjuaji sana kwani hata hivyo mbinu hizo zilikuwa zikifanyika kinyume tofauti na yeye.

Majini ili kuweza kuishi walihitajika sana kuwa na nguvu kuliko hata wanavyokula chakula ili tu kuendeleza kudumisha miili yao.

Inasemekana wale ambao wanakaribia kuingia katika levo ya Nafsi hutengwa mahali palipotulia sehemu maalumu na hupewa jiwe la ndoto linalofanana na yai na kisha hulikalia na kulipa joto huku wakiendelea kutahajudi kwa muda mrefu na wakati wakianza kupokea miili yao huwa sio kwa chaguzi zao , kinachoanza kuonekana kwao ni kama ndoto wanaona sura ya mtu mbele yao na huyo mtu ndio mwili wao na kinachofanyika ni kuhakikisha wanapandisha nguvu zao mpaka kuweza kuumiliki .

“Unaitwa nani?”Aliuliza Sophia , alionekana kupata furaha mara baada ya kupata msichana mpole ambaye anaweza kumuuliza maswali.

“Naitwa Aoli, nilikuwa nikielekea katika mji wa Mto Wa Anga karibu na ziwa la mbingu ninakoishi lakini nikaja kukutana na hawa majini pepo wa gredi ya juu na kunikamata”

Maelezo yake yaliwafahamisha kabisa ni dhahiri walikuwa wamemteka kwa ajili ya kwenda kumuuza kwenye Danguro

“Unaonda karibu na Ziwa la Mbingu ?!!”Aliuliza Sophia huku akiwa na furaha kwani hata wao ndio walikuwa wanaelekea.

“Nina uhakika utakuwa unaijua njia ya mkato ,unaonaje tukiongozana pamoja kuelekea huko?”

“Sophia itakuwa hatari kama tukimruhusu akaungana na sisi , nitapaswa kulinda watu wawili kwa wakati mmoja”Aliongea Roma , alimuona msichana huyo wa kijini kuwa mrembo lakini uwezo wake wa kijini ulikuwa wa chini sana na hata yeye mwanzoni alishangaa kwani hakutegemea jini kuwa na mwili na nguvu zake kuwa za chini.

“Sio kweli, huyu yupo kwenye daraja la tatu ambalo ni sawa na levo ya Nafsi hivyo uwezo wake ni mkubwa kuliko wa kwangu na anaweza kujilinda , isitoshe kama tukimuacha hapa si wale watu watarudi na kumchukua tena na kuingia hatarini”Aliongea na kumfanya Roma kukosa neno alikuwa sahihi anaweza kuwa katika hatari lakini alihofia kuongozana na mtu asiemjua.

“Master mimi ni jini wa kawaida tu nisie na uwezo mkubwa , kama tutakuwa katika hatari unapaswa kumlinda mwenzako , sitokuwa na makasiriko zidi yako kwa kutokunilinda , ninajua njia ya karibu kuelekea Ziwa la Mbingu na itawachukua muda mchache kufika mkiwa chini ya uongozi wangu , nyie si wageni nitaendelea pia kuwaelezea baadhi ya mambo msio ya jua”

Roma alijiambia alikuwa na akili , kwani maneno yake yalikuwa yakivutia, ni kweli hawakuwa wakijua njia na mambo mengi pia kuhusu huo ulimwengu hawakuwa wakifahamu.

Sophia mara baada ya kuona Roma anawaza sana alimsogelea na kumwambia kwa taratibu kwamba hakuna ambaye ataweza kumshinda huko njiani hivyo waondoke nae kwani anatia huruma na Roma alitingisha kichwa kukubal.

******

Katika ulimwengu huo huo upande mwingine kando ya ziwa ambalo limezungukwa na msitu wa Mianzi Zambarau alionekana mwanaume ambaye alikuwa na nywele za rangi nyeupe kama mvi hivi , alikuwa amevaa kanzu ya Rangi ya Zambarau huku akiwa na ushanga mkubwa kwenye shingo yake kama Rozari iliotengenezwa na madini ya Jade, alikuwa ni bwana ambaye alikuwa na mwonekano wa kichina na muda huo alikuwa ameegamia kwenye jiwe huku akiwa ameshikilia ufito wa muanzi uliokuwa na kamba ambayo iimeingia majini , alionekana alikuwa akivua samaki.

Nyuma yake kulikuwa na nyumba ambayo ilikuwa imejengwa na Mianzi tupu iliokuwa ikifuka moshi.

Mtu huyo alionekana kuwa katika hali ya raha akifurahia kile alichokuwa akifanya, huku mkono wake wa kulia akiwa ameshikilia kifaa kama kikombe kilichotengenezwa kwa mianzi , ilionekana ni kifaa ambacho kilikuwa na kinywaji ndani yake kwani alikuwa akipeleka mdomoni na kunywa kwa kila baada ya dakika tatu huku akipiga mluzi akionekana kama anaimba.

Dakika hio hio pua yake ilicheza akiwa kama mtu ambaye alikuwa amenusaharufu nzuri na palepale alttupia pembeni ile fimbo na kukimbia kuelekea upande wa kwenye kile kijumba lakini kabla hata hajafika mwanaume mwingine alionekana akitoka katika hicho kijumba akiwa mkononi ameshikilia kibuyu cha mvinyo kama chungu vile , mwanaume huyo pia alikuwa ni mchina ila yeye akiwani mwenye nywele nyeusi.

“Inanukia vizuri “Aliongea yule bwana mwenye nywele nyeupe huku akipeleka pua yake kwenye kile chungu na kunusa huku akionyesha hali ya kufurahi.

“Braza Chi kama nilivyotegemea , inaonekana uwezo wako wa kutengeneza mvinyo ni wa hali ya juu sana , uko vizuri sana katika utengenezaji wa pombe , hii ndio uliniambia unatengeneza kabla ya mvinyo eh?”Yule bwana mwenye nywele nyeusi alishika udevu wake kama vile anautelezesha na mkono na kisha akamwangalia yule mwanaume mwenye udevu wa mvi kwa tabasamu.

“Wang Han Manasaba wa enzi ya Tang hapo zama za kale kama alivyoimba katika ushairi wa Liangzhou, ndipo vikombe vya Jade vilipojaa Divai, sauti ya mtirriko wa pipa ikawaambia na ondokeni…. nimekuandalia huu mvinyo kwa ajili yako, je Braza Zao umeandaa vikombe vya Jade?”Aliongea na kumfanya yule bwana kuanza kuwaza kuhusu Shairi hilo , walionekana ni kama vile walikuwa wakiongea kimafumbo kukumbushiana mambo ya kale hata hivyo alikumbushia ushairi wa Wang Han kuoka enzi ya Tang.

“Braza Chi nimejaribu kuvitafuta vikombe hivyo ila sijavipata , niliwaagiza ndugu zangu Mao Tai na Du Kang kwenda kutafuta katika milima ya Qillian lakini hawakuweza kupata , walivyoleta ni kutoka mlima ya Kunlun , je tunaweza kutumia hata hivyo?”

Mwanaume alieitwa kwa jina la Braza Chi alivuta pumzi na kuzishusha huku akimwangalia Braza Zao..

“Inasikitisha sana lakini sio mbaya tutatumia hivyo hivyo”

Yule mzee Zao mwenye nywele nyeupe alitoa tabasamu pana la furaha huku macho yake yote yakiangalia chungu kilichojaa mvinyo.

Na dakika ileile alionekana ameshikilia vikombe viwili vya Jade ambavyo haikueleweka amevitolea wapi na kuviweka katika meza ya jiwe lililochongwa.

Dakika hio hio wakati akitaka kuchota mvinyo kwa ajili ya kujaza kikombe kingine aliweza kutokeza mbele yao mtu mwingine aliekuwa amevalia kanzu na mwenye nywele za Zambarau, alikuwa ni Moli.

“Kaka Zao je umemuomba Master Chi kukutengenezea kilevi , nimeweza kunusa harufu yake hata nilipokuwa mbali”Moli aliangalia kwa macho ya tamaa chungu kilichokuwa kimejaa mvinyo.

“Bro umekuja muda muafaka , Master Chi ndio amenitengenezea huu mvinyo na sasa upo tayari , njoo ukae na wewe uionje radha yake lakini Du Kang yule mtukutu ameniletea vikombe viwili tu vya Jade kutoka milima ya Kunlun hivyo itakubidi utumie kikombe cha Muanzi.

Walikuwa wakifuata tamaduni za kichina , wenyewe wanaamini utamu wa mvinyo hutofautiana na kikombe ambacho huandaliwa , kikombe cha Jade ndio kinachofanya Mvinyo kuwa mtamu zaidi.

Upande wa Moli alionekana kuwaelewa vizuri kwani hata yeye alikuwa akizungumza lugha ya kichina tena kile cha kale.

Baada ya kuwekewa mvinyo kwenye kikombe chake cha mti na kuonja alijikuta macho yake yakichanua kwa utamu.

“Master Chi wewe ni kaka yangu wa ukweli kuanzia sasa , licha ya kuwa mgeni kwenye huu ulimwengu lakini umeweza kumfanya kaka yangu Zao kulia mara kibao kupitia mvinyo wako”Aliongea na Master Chi alijikuta akicheka.

“Braza Moli ni mara chache sana kukutana na marafiki wazuri kwenye maisha yetu , sikuweza kudhania ninaweza kukutana na mtu ambaye tunafanana kwenye vitu vingi , mwanzoni nilikuwa nishaachana kabisa na mambo ya pombe lakini baada ya kukutana na nyie mabraza nimekosa uvumilivu”

“Eh..!!”

“Braza Chi kabla yako nilikuwa na Moli tu kama ndugu yangu lakini hajui chochote kuhusu maswala ya kutengeneza pombe na anajali sana kukusanya mimea , waliochini yangu wengine wanachojua ni kuvuna nishaiti za mbingu na ardhi , nilikuwa nimeboreka sana kabla haujaja”

“Bwana wetu mkuu wa majini ya kishetani na mmiliki wa Msitu wa Mianzi Zambarau , wewe ndio kiongozi wa majini ya kishetani na unasifika kwa uwezo wako mkuu ndani ya ulimwengu huu lakini ajabu ukaagiza majini ya Gredi ya chini kukutafutia vikombe vya Jade , naamini ni kwasabbau tu wanakuheshimu ndio maana hawakuwa na jinsi , wenzetu wakisikia ulichokifanya wataishia kucheka”

“Hata sijali , yule Mbweha kutoka Jumba la Jade mwenyewe ana mambo ya kipuuzi tu kama mimi , ni mkubwa kuliko mimi na pia ni mzuri zaidi ya wale minyoo katoka Korongo la Joka ,lakini akili yao muda wote ni kuwaza namna ya kutoka ndani ya huu ulimwengu na wasivyojua wanapoteza nguvu na hela zao kwa ajili ya mambo ya kipuuzi”Aliongea huku akitingisha mabega.

“Tuachane nao na tufurahie maisha yetu kwa kunywa mvinyo , Braza Zao unaonaje?”Aliongea Master Chi huku akiinua kikombe chake cha Jade.

“Vizuri sana , sijawahi kukutana na mtu kama wewe unaefurahia sana pombe”Aliongea na palepale alijaza na cha kwake na wakagongesheana na kuendelea kunywa kwa furaha.

“Braza Zao nimetoka Msitu wa Giza na kidogo tu niingie matatizoni lakini kwa bahati nzuri kuna mgeni ambaye ni binadamu alienisaidia”

“Eh… kuna mtu mwingine amefika tena? , haukutumia kadi yangu? , ila sidhani kama wale watu wa miliki ya Mbweha wa Jade wanaweza kukudhuru ilihali wanakujua upo chini yangu “

“Nilitaka kupambana nao lakini wakati nataka kuitoa ndio walitokea hao binadamu na kunisaidia”Aliongea na kisha akamgeukia Master Chi.

“Master Chi sidhani kama ushawahi kusikia binadamu anaevuna nishati za mbingu na ardhi katika ulimwengu wa nje … jina lake anaitwa Roma Ramoni”Aliongea na palepale macho ya Master Chi yalibadilika na kuwa makali






SEHEMU YA 604.

Moli mara baada ya kuona mshangao wa Master Chi palepale alikumbuka namna ambavyo Roma aliweza kutengeneza vinyoka nyoka vya moto.

“Nilijua tu , alikuwa akitumia mbinu za moto katika kushambulia lakini sijawahi kusikia mtu yoyte ambaye ashawahi kufanya hibyo , Roma alikuwa a uwezo wa kuwasha Dragoni za moto bila tabu yoyote na palepale nilikumbuka mbinu zako Master unazotumia zinafanana”

Bwana Zao alijikuta akishangazwa na jambo hilo baada ya kusikia maelezo yote ya Moli.

“Master Chi je huyo ni mwanafunzi wako?”Aliuliza na kumfanya Master Chi kutoa pumzi nyingi huku uso wake ukiwa ni ngumu kuusoma na kisha akapeleka kikombe chake cha mvinyo mdomoni na kunywa pafu moja.

“Huyu mtu siwezi kusema alikuwa ni mwanafunzi wangu bali tulishawahi kukutana na kufahamiana, naamini hili limepangwa kutokea .. nililazmishwa kuja huku kwasababu nilikuwa nikitaka kuuliwa , je na yeye ndio kilichomtokea kama mimi?”Aliuliz lakini swali lake lilimlenga yeye mwenyewe.

“Moli kama wewe ulikuwa ushaona ana tumia mbinu sawa na za Braza Chi kwanini usingekuja nae hapa?”Aliuliza Bwana Zao huku akionyesha kutopenda.

“Sikuwa nikijua kama anafahamiana na Master Chi , isitoshe mpaka sasa una mtegemea zaidi Master Chi kwa ajili ya Mashindano ya Mbingu, sikutaka kuvujisha taarifa za uwepo wake ila nilimshawishi kuja na mimi katika msitu wa Mianzi Zambarau kwa zaidi ya mara mbili lakini alikataa na kusema yeye safari yake ni kuelekea katika Ziwa La Mbingu hivyo nilimuacha kwani sikutaka kuingilia mambo yake”



“Kama hivyo ni kweli basi sasa hivi naweza kukisia atakuwa kwenye miliki ya Mbweha wa Jade , Braza Chi ninaweza kukusindikiza kwenda katika jumba la Mbweha wa anga mikia tisa kama unataka kumfuata”Aliongea Mzee Zao na kumfanya Master Chi kuwaza kwa dakika kadhaa.

“Yupo imara sana na sidhani kama uwezo wake ni wa chini kuliko wa kwangu kulingana na maneno ya Zimo , Majini hata hivyo hayawezi kuonyesha nguvu zao zote , naamini atakuwa sawa . isitoshe hawezi kufika katika mnara wa Mbingu kabla mashindano ya Mbingu kumalizika , tutakuwa na uwezo wa kukutana nae tukielekea katika Ziwa la mbingu”Aliongea Master Chi na kumfanya Zao kutoa kicheko hafifu.

“Unaonekana upo makini kweli , kama ni hivyo kwanini tusipige mkupuo mwingine wa kinywaji chetu , bado ipo ya kutosha , tunaweza kuongezea maana kilevi chake sio kikali sana”

‘Tutakynywa kutosheka leo hakuna namna”Aliongea huku akijiambia atajua mwenyewe huyo mtukutu wa maka mingi iliopita , hakutaka kujishughulisha na kile ambacho kitamtokea na pia hakuwa na nguvu ya kumjali katika mazingira kama hayo , hivyo anapaswa kunywa kujigalagaza.

Moli ambaye hakuwa mnywaji sana aliishia kutingisha kichwa chake huku akiwa ni kama anawaonea huruma kwa ulevi wao.

******

Roma alikuwa na uhukika yule jini Huja angekwenda kuleta wenzake hivyo alichokifanya ni kumbeba Aoli pamoja na Sophia na kisha akapaa nao ili kwenda umbali mrefu kutoka katika eneo hilo.

Roma hakutaka kumuacha nyuma ilihali alikuwa ashakubali kuongozana nae na isitoshe pia uwezo wake ulionekana kuwa mdogo.

Roma licha ya roho yake kujiambia muda wowote watakamatwa lakini hakutaka kujisumbua kuhusu hilo , alijiambia atapambana na kila ambalo litakuwa mbele yake.

Baada ya kuweza kupita kilima hatimae waliweza kufika sasa katika ardhi ya tambarare , katika eneo hilo kitu pekee ambacho aliona atumie kuweza kurahishisha safari ni mbinu nyingine ambayo alijifunzaga iliokuwa ikitofautiana na mbinu za kijini , ilikuwa ni Qinggong .

Roma hakuwa akitembea bali alikuwa akikimbia huku akiruka ruka kwenda mbele kama vile ni chui anaejaribu kufukuzia swala, kuhusu Aoli alikuwa akipambana kuweza kumfukuzia Roma bila kuchoka asiachwe mbali.

Baada ya kupumzika walianza kutembea taratibu taratibu na Sophia alimuuliza Aoli mwonekano wake wa mwazno kabla ya kuwa na mwili wa kibinadamu ulikuwa vipi lakini Aoli alionekna kuona aibu.

Majini ni viumbe ambao wanachukia sana miili yao wanayo zaliwa nayo na ndio maana mara nyingi hata kama wakipambana na adui wakiona ni mkubwa kiliko wao wanaacha na kukimbia.

Mbinu pekee ya kuweza kutumia nguvu zao zote ni lazima wabadilike maumbo yao.

Roma yeye hakufuatilia mazungumzo yao na aliuliza mara chache kuhusu taarifa ambazo alikuwa akihitaji tu kwa ajili ya kumsaidia kufika mwisho wa safari yake.

“Mister Roma je unapanga kutoka kwenye huu ulimwengu kupitia Manara?”Aliuliza Aoli lakini Roma aliona mrembo huyo wa kijini anauliza swali ambalo lipo wazi.

“Nadhani siendi huko kucheza eti, nasikia lakini radi inayotokea katika huo mnara ni ngumu sana kuhimili?”Aliuliza Roma na Aoli alionekana kushangaa kidogo.

“Mr Roma utanisamehe kwa uongeaji wangu wa moja kwa moja , licha ya kwamba uwezo wako unakaribiana na majini pepo ya anga na Majini Shetani ya anga haiwezekani kabisa kuweza kuhimili mapigo tisini na tisa ya mpangilio wa radi”

“Kila mtu ananiambia haiwezekani , ninapaswa kuondoka katika huu ulimwengu , nitafanya lisilowezekana kuwezekana”

“Hakika unaonekana ni jasiri mno , lakini nakuasa kuwa makini usijjilazimishe sana kama utaweza kupata nafasiya kuingia katika huo mnara la sivyo utakufa”

“Unamaanisha nini kupata nafasi , huo mnara sio kila mtu ambaye anaweza kuufikia?”

“Ndio , Mnara wa mbingu haupo wazi kwa kila mtu , mara nyingi unakuwa umezigingwa na radi ya zambarau, ukiwa umefungwa haitokuwa rahisi kuweza kuufikia na kuupanda isitoshe sehemu ya kuingilia kwenye mnara inafunguka mara moja tu kila baada ya miaka sitini”

“Miaka sitini!!?”Roma alitoa mshangao huku akipandisha sauti yake wakati akiuliza.

“Kwahio unamaanisha napaswa nisubiri kwa miaka sitini mpaka niweze kutoka?”Aliuliza na kumfanya Aoli kutoa tabasamu.

“Una bahati kubwa mnara huo mwaka huu unatimiza miaka sitini tokea kufunguka kwake maara ya mwisho , hivyo ndani ya mwezi ujao utafnguka kwa mara nyingine”Aliongea na kumfanya Roma macho yake kuchanua kwa furaha.

“Kama ni hivyo basi naweza kusema nimekuja huku ndani ya muda muafaka”

“Ndio lakini ..”Aoli alionekana kupumua kwanza.

“Lakini nini?”

“Unapaswa kukidhi vigezo kama unataka kuingia ndani ya mnara huo , vigezo ni mpaka ushinde Mashindano ya Vita ya mbingu”

“Mashindano ya Vita ya Mbingu unamaanisha nini?”Aliuliza Sophia akionekana kushangaa.



“Ili kukuelewesha vizuri napaswa kukuelezea stori ilivyo tokea mwanzo , ukiachana na mawe ya kiroho ambayo yanachimbwa chini ya bahari , sehemu nyingine ambayo ina nguvu za kiroho ni ndani ya mnara huo ambao upo juu ya Ziwa , nishati hio inatokana na Radi inayopiga ndani ya hilo eneo , floor ya kwanza ya mnara huo haina radi lakini kwasababu ya uwepo wa kiwango cha juu cha nishati ya kiroho kuna mimea adimu sana inakuwa hapo ndani , ni mimea amayo inatafutwa sana na wakuu wote wa huu ulimwengu , kuna pia hazina za kiroho ambazo hupatikana katika hilo eneo , hizo hazina pamoja na mimea husaidia sana katika kupanda levo kwenye uvunaji wa nishati ya mbingu na ardhi , lakini kutokana na hilo katika Floor hio mara nyingi inageuka kama eneo la machinjio.

Miaka elfu kumi iliopita wakuu wote wa majini waliweza kuona kwamba wanazidi kupungua siku hadi siku kama wataendelea kuchinjana kila baada ya mnara huo kufunguka ili tu kuingia , hawakutaka mbinu zao za kuvuna nishati kupotea hivyo ili kurudisha tumaini kwa ulimwengu huu yakawekwa makubaliano kwa kila upande kutuma wawakilishi kila baada ya miaka sitini kushindania nafasi ya kuingia katika mnara huo na kuweza kupata hio mimea na baadhi ya hazina hizo , kupitia mashindano hayo hakukuwa na haja ya watu kufa kwani anaeshinda ndio anaeingia , ni shindano pia ambalo limeandaliwa kwa ajili ya kuongeza spidi ya watu kujifunza mbinu za kijini ili kila miaka sitini inapokaribia waweze kupata nafasi ya kushindana , kwa mwaka huu lazima shindano hili lifanyike

Huu ulimwengu umegawanyika katika miliki kubwa tatu ambazo zilijigawa miaka mingi iliopita, kuna miliki ya Mbweha wa Jade , Miliki ya msitu wa Mianzi zambarau na Bonde la Joka”

Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo alijiambia kweli hawa majini sio wa kuchezea, wanaonekana kuwaza mbali sana mpaka kuandaa mashindano hayo.

“Kwahio unamaanisha kama nitalazimisha kuingia ndani ya huo mnara nitashambuliwa na hizo nguvu tatu si ndio?”

“Hilo sio tatizo , kuna baadhi ya majini wengine wanajitegemea lakini kutokana na koo tatu kuwa na washindani wenye nguvu sana , basi mara nyingi wale wanaopenda kushindana kwa kujitemgea wanakosa ujasiri”

“Bro Roma kama kweli wapo levo ya daraja la tisa si inamaanisha uwezo wao ni mkubwa kuliko wa kwako?”Aliuliza Sophia.

“Kama hao viongozi watatu wa juu kila koo wapo kwanini wasipigane wao kwa wao mpaka kutuma wawakilishi?”

“Hao watatu waliweza kupata umaarufu wao miaka mingi iliopita na wanajua fika , kama watapambana wenyewe kwa wenyewe inaweza ikachukua hata mwaka na asipatikane mshindi hivyo mnara utafunga ndio maana wanatuma wawakilishi , sheria ya mashindano ni kwa wale tu ambao hawakuwahi kushidana , yaani majini wapya ambao wanataka kupata umaarufu na heshima , mara nyingi wanaonda kupamban ni wale walio katika levo ya Pepo wa anga na shetani wa anga”

Roma mara baada ya kusikiliza maelezo hayo alipata kitu cha kufanya lakini kwa wakati mmoja alikuwa na mgogoro wa nafsi.

Alijiambia anaweza akashinda kama tu ataweza kuwa mwakilishi wa moja wapo ya koo , lakini kama ataingia peke yake nafasi ya kushinda inaweza kua ndogo au isiwezekane kabisa na itambidi kusubiria miaka sitini ijayo kuweza kuingia tena.

Roma tokea aingia katika huo ulimwengu bado hajakutana na jini ambalo lipo levo ya daraja la saba lakini Moli mwenyewe ambaye uwezo wake ulikuwa ni wa chini alionekana kuwa ni hatari, hivyo Roma alikosa kujiamini kama ataweza kushinda hao majini ambao watakuwa katika daraja la saba ,nane na tisa.

“Aoli katika mashindano yaliopita nani alishinda pambano?”

“Ni Majoka mawili kutoka Bonde la Joka na ukiachana na lililopita na la nyuma yake zaidi walishinda hao hao , hao Drago ni majini ambao wapo chini ya mkuu wa majini Majoka na washindi hao wote kwa sasa wana vyeo vikubwa , mmoja ni Joka mjumbe wa shetani , Joka Mjumbe wa upepo na Joka Mjumbe wa ngurumo, ndio watawala ambao hata mkuu wao hawagusi kabisa kutokana na uwezo wao lakini licha ya hivyo bado wanatuogopa sisi majini tuliopo chini ya Bwana wetu mzuri, Mbweha wa mikia tisa”

“Kwa jinsi unavhyoongea ni kama vile umekutana na kiongozi mkuu wa Mbweha wa Jade?”Aliongea Roma huku akicheka.

“Bwana wetu ni jini pekee lenye muonekano mzuri kuliko kitu chochote ndani ya ulimwengu huu , urembo wake hakuna ambaye ashawahi kuufikia wala kuufananisha na kitu”Aliongea akijaribu kumsifia.

Roma hakutaka kupingana nae maana hata hivyo bado hajakutana na huyo mrembo anaeitwa Mbweha wa mikia tisa.

“Hata awe mrembo vipi hawezi kumfikia mke wangu”Aliwaza Roma huku hisia za kumkumbuka mke wake Edna zikimvaa na kuzidi kupatwa na hali ya kutaka kurudi duniani.

Dakika hio hio wakati Roma akimuwazia Edna alijikuta akishituka mara baada ya kuhisi mkandamizo wa hewa wa aina yake unatokea upande wa kusini.

Ilikuwa ni kufumba na kufumbua mwanaume aliweza kuonekana mbele akiwa angani amepanda ndege mkubwa mno wa rangi nyeupe na kwa jinsi ambavyo alikuwa akipepea alifanya upepo kupeperusha majaini.

Ndege huyo alikuwa akifanana sana na Shakwe wa baharini lakini yeye alikuwa mkubwa mno na kwa jinsi ambavyo alikuwa akipaa ilimshangaza sana Roma.

Roma alijiambia kama angekuwa na uwezo wa kupaa ndege mkubwa kama huyo basu ingemrahisishia kuzunguka katika miliki yote ndani ya muda mfupi.

Wakati Roma akimtamani yule ndege upande wa mwanaume huyo alikuwa akimwangalia Roma kwa chuki, na kitendo cha kuona Roma hamwangalii ilimfanya kutoa tabasamu la kifedhuli.

“Nadhani utakuwa ndio wewe binadamu mgeni mwenye uwezo wa kijini?”Aliuliza mwanaume huyo , alikuwa na nywele ndefu mno ambazo zilikuwa zikifika kiunoni za rangi ya kahawia, alikuwa amezifunga na kitambaa chekundu na kufanya mkia wake kupiga piga mgongoni.

Aoli alionyesha hofu na aliweza kujificha nyuma ya Roma kwa Woga ni kama vile mtu anapomuona mtu wa heshima.

“Mister Roma huyo ni Bwana mkuu wa jiji loote la Wingu jeupe , ni moja wapo ya majini therathini na sita ya uwezo wa anga anaitwa Baiju

Ni Roma pekee ambaye alikuwa akiweza kumwangalia moja kwa moja machoni , mkandamizo wake wa hewa ulikuwa mkubwa mno kwa mtu wa kawaida kumwangalia .

“Wewe upo katika daraja la tatu , kwanini umeongozana na hawa binadamu?”Aliuliza akimwangalia Aoli kwa hasira.

Aoli alionekana kutetemeka mno akikosa ujasiri wa kuongea .

“Tushaondoka katika mji wako tayari, je umenifuata mpaka huku ili angalau niongeze muda wangu wa kukaa”Aliongea Roma mara baada ya kumtuliza Aoli.

“Una maneno marahisi mno , umewaua watu wangu na kisha ukamjeruhi generali wangu Huja , nilitaka kupotezea lakini kilichoniuzi ukaamua na kuiba na mawe yao ya kiroho , unanichukuliaje kwa mfano kama unaweza kuondoka kirahisi”Aliongea na Roma kama kawaida alitoa tabasamu la kifedhuli.

“Nilijnua tu, inawezekanaje Huja akateka msichana mdogo na kumbeba kwenye kiroba hivi hivi , kumbe wana sapoti zote kutoka kwako?”

“Kuteka nini , sijui chochote kuhusu hilo , ninachojua ni kwamba nakudai uhai wako”Dakika hio hio alioongea aliruka kutoka kwenye ndege wake na kisha akampiga Roma teka la kifua.

Jini Baiju uwezo wake wa kijini ulikuwa katika daraja la nane ambao ulikuwa ukichukuliwa ni wajuu kati ya majini therathini na sita ya uwezo wa anga , wakati alipokuwa akiita nguvu zake za kijini miti ilianza kuyumba kutokana na upepo mwingi ulikuwa ukijikusanya na haikuwa miti tu hata mawe yalianza kuruka

Roma aliwaambia Sophia na Aoli kukimbia huku akikwepa shambulio la kwamba la wimbi la upepo na palepale aliita moto wa rangi nyeupe na kuungannisha na wa njano kwenye mikono yake.

Baiju uso wake ulibadilika mara baada ya kuona mpira wa moto huo lakini hata hivyo hakuonyesha kuuhofia.

Kwa jini la uwezo wake moto wa rangi nyupe na wa njano haukuwa na uwezo wa kumpa majeraha makubwa , alichopaswa kufanya ni kujikinga tu na nishati ya mbingu na ardhi.

Roma alianza kumrushia mipira ya moto kwa spidi zote lakini Baiju alikuwa mtaalmu mno wa kukwepa na kujikinga kwa wakati mmoja, baada ya kuona amekwepa sana palepale mkono wake uliadilika na kuwa kama mkuki mrefu wenye kumeta meta huku ukiwa na ncha kali isokuwa ya kawaida.

Roma palepale aliweza kukumbuka katika maneno ya Aoli aliomwambia ni kwamba majini yakifikia katika levo flani ya juu yanakuwa na uwezo wa kubadilisha viungo vyao kuwa siraha kutokana na kujiunganisha na vyuma , haijalishi muonekano wao ukoje lakini siraha hizo zilikuwa na urofauti kabisa na viungo vya mwili.

Aoli pia alimwambia kwamba majini ya kipepo hayana uwezo wa kutengeneza Dhana kama majini ya kawaida lakini siraha zao hazikuwa za kupuuzwa hata kidogo na isitoshe hata kama ikiharibika inaweza kurudi katika umbo lake.

“Nguvu yako ya moto haiwezi kuhimili nguvu ya panga zangu za upepo”Aliongea huku akitoa kicheko na alipigisha hewani ile siraha yake na palepale kulidhalishwa visu vya aina nyingi kwa wakati mmoja ambavyo vilikuwa vikiambaa kwa upepo tu kumshambulia Roma.

Roma hakutaka kuleta masikhara kukinga visu hivyo na mwili wake, hivyo palepale aliita nguvu ya kijini na kujaribu kuvizuia huku akivikwepa kwa spidi kubwa kwa sarakasi za kila namna , kuna kingine manusura kimtoboe kichwani lakini aliwahi kukwepesha kichwa na kikaambulia nywele.

Roma wakati huo aliweza kuelewa kitu, kadri visu hivyo vilivyo kuwa vikikata upepo na kutoa ile sauti yake ya Swiii.. vilikuwa vikisababisha mapigo yake ya moyo kwenda mbio mno.

“Pumbavu kabisa , hizi sauti zina matatizo gani”Alilaaani Roma maana ni kama mishipa ya damu inataka kumpasuka.

Roma palepale aliweza kugundua nini tatizo mara baada ya kuona tabasamu la kifedhuli la Baiju.

Tofauti na kuwa na makali hatari kama viwembe , suati zao za mkato wa hewa zilikuwa zikitegneneza mtetemo(vibration) ambazo zilikuwa na madhara kwa nguvu ya kijini iliokuwa ndani ya mtu

Roma kama mwili wake ulikuwa dhaifi angeweza kutema damu palepale.

“Unathubutu vipi kutumia mbinu zako hizo za hila”

Roma alikuwa amekasirika kiwango cha rami , wakati akiwa anasukumia mbali vile visu kwa kutumia nguvu ya mbingu na ardhi , palepale aliiita donge la Maji kubwa kama kitenesi kwenye mkono wake na baada ya kuliachia hewani Donge lile liligeuka barafu na kupasuka pasuka kama cheche na kuanza kumeza sauti ya mawimbi ya visu.

Baiju alionekana kushangazwa na kitendo hicho , hakuamini kama Roma alikuwa na uwezo wa kuita maji ya kiroho na kuyagandisha.

“Huu ni uchawi ,,, hio ni mbinu gani umetumia katika mafunzo yako?”Aliongea kwa kujiwazia na mpaka hapo aliona kabisa hakuna matumaini kwa shambulio lake la visu, hivyo aliamua kutumia mkuki wake kuanza kumsogelea Roma na kumshambulia nao.

Alionekana alikuwa na mpango wa kumuua kabisa Roma na pigo moja lakini upande wa Roma alionekana kutoa tabasamu lakifedhuli.

“Nilikuwa nikisubiri ufanye shambulio la aina hio”Aliongea Roma na palepale alichezesha mikono yake na kulitokea mng’ao kama wa moshi na palepale alimsogelea Baiju kwa spidi kubwa na kushika ncha ya ule mkuki wake na palepale barafu ilianza kusambaa kutoka katika ncha ya mkono wake na kuanza kumsogelea Baiju na kumfunika kwa kasi ya ajuu mno.

Baiju alijikuta akitoa ukulele kutokana na baridi kali aliokuwa akiisikia mwilini na alijitahidi kuvuta ule mkuki kutoka kwa Roma lakini ulikuwa umeshikiliwa vyema.

Sophia aliekuwa akiona mbali alijikuta akiruka ruka kwa kushangilia mara baada ya kuona matumaini ya Roma kushinda.

“Aoli angalia Bro Roma anashinda , Bwana wenu wa mji hana uwezo wa kumshinda , kwa staili hii naamini Bro Roma anaweza kuingia katika mnara , wewe unaonaje?”

Sophia alishindwa kuona mabadiliko ya ghafla ya Aoli huku macho yake yakiangalia namna ambavyo Baiju aligeuka barafu kwa ghafla.

“Huenda anaweza kuwa na kaji uwezo ..”Aliongea huku akitabasamu ki ovu na palepale alisogea kwa spidi kuelekea sehemu ambayo Roma na Baiju wanapambana , Sophia alitaka kumzuia lakini ile anataka kumshika ni hewa tu aliweza kushika kwani Aoli alikuwa na spidi ya hali ya juu na ilimfanya na yeye kuanza kumkimbiza

Baiju alijikuta akianza kutoa matusi kwa kutokuwa makini na kuanza kushindwa pambano kirahisi namna hio , Roma palepale hakutaka kumchelewesha alitaka kuinguza roho yake na moto wa Bluu kwani ulikuwa tayari ushajitengeneza katika mkono.

“Umekuja mwenyewe kwangu na sikuwa na kinyongo chochote na wewe lakini hata hivyo sitaki kusumbuana na mtu kama wewe hivyo nitakupeleka moja kwa moja kuzimu”aliongea Roma

“Huwezi kuniua ,,, Bwana wangu hawezi kukuruhusu uniue na atakuua wewe”Aliongea huku akishindwa kuzungusha chingo yake kutokana na kukabwa na barafu.

Roma hakutaka kusumbuka na maneno yake na ndio alikuwa akianza kutaka kuruhusu mpira ule wa moto wa rangi ya bliuu kuelekea kwake lakini ghafla tu mikono yake iliokuwa imeshikilia ule mpira wa moto ilifungwa fungwa na kamba ndeefu ya nguo ya hariri kwa nguvu kiasi cha kushindwa kudhibiti ule moto na palepale ulizimika.

Alijikuta akishangazwa na kitendo hicho kwani aliamini mtu pekee ambaye anaweza kuuzima moto wake ni mwenye uwezo mkubwa kuliko wa kwake.

Roma alijikuta jasho likimtoka na palepale kwa haraka sana aligeuza shngo yake na kuangalia nani ambaye amemshambulia kwa ghafla sana.

Roma mara baada ya kuangalia alijikuta akishikwa na mshituko mara baada ya kuona aliefanya hivyo ni Aoli na hata kamba ya hariri iliokuwa imemshikilia ilikuwa ikitoka kwake.

“Baiju alijikuta akisogea pembeni haraka sana na kujiifcha mara baada ya mkuki wake kuachiwa., lakini wakati huo huo alijikuta akipauka uso mara baada ya kumuona Aoli.

“Bwana wangu …. Bwana wangu…!!!”

Sophia alijikuta akisimama ghafla mara aada ya kushitukia tukio lile na aliishia kuachama tu.

Upande wa Roma akili yake ni kama ilikosa kufanya kazi kwa muda na hisia zake zilikuwa ni kama mtu ambaye alikuwa akiamini ukweli flani na sasa anaambiwa huo ni uongo.

“Wewe ni nani haswa?”Aliuliza Roma na kumfanya Aoli kumwangalia kwa dharau na palepale kama vile anamulikwa na tochi usoni na haraka sana mwili wa Aoli ulibadilika kabisa na kuwa mwanamke mwingine kabisa aliekuwa ni mrembo wa ajabu.

Mwanamke ambaye alikuwa mbele yake alikuwa amevalia mavazi ya hariri nyeupe huku yakiwa na kamba kamba zilizokuwa zimejiachia kama vile ni Ribon huku zikipepewa na upepo , nywele zake zilikuwa ndefu na nyeusi zikiwa zimefungwa na kitambaa .

Kwa jinsi ambavyo alikuwa akimwangalia Roma ni kama anamtega , ijapokuwa mavazi yae yalikuwa ya kawaida sana lakini uzuri wake haukujificha.

Hakukuwa na maneno sahihi ya kumwelezea kwani alikuwa ni kama uso wake unabadilika badilika na kuzidi kuwa mzuri , mbaya zaidi eneo lote lilijaa marashi ya aina yake ambayo yalitamanisha pua.

“Mister Roma mimi ndio mkuu wa miliki yote ya eneo la Mbweha wa Jade na jumba la kimalkia, naitwa Aoline , Nice to meet you”Aliongea huku akibadilisha muonekano wake na kuweka tabasamu la kiheshima , kwa namna ambavyo alikuwa akimwangalia Roma ni kama vile anamwambia naomba unipende.

ITAENDELEA.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA



MTUNZI :SINGANOJR.

WATSAPP: 0687151346.



SEHEMU YA 605.

Baiju miguu yake katika vigoti ililelegea palepale mara baada ya kujua mwanamke ambaye hakuwa amemtambua ni Aoiline mkuu wake.

“Bwana wangu , sikujua kama upo hapa tafadhari naomba unisamehe”Aliongea kwa kutetemeka huku akiwa amemsujudia chini , hakuwa tena yule mwenye kiburi.

Aoiline aliachana na Roma na kisha alimsogelea Baiju kwa hatua hafifu huku uso wake ukiwa ni ule wa kichokozi , hakuonyesha kabisa kuwa na hasira.

“Baiju nimepewa ripoti kwamba unakusanya kiwango kikubwa cha mawe ya kiroho kupitia Madanguro , ukiichukulia faida kwa mimi kutokuwa makini na maswala hayo , inaonekana umeweza kuteka majini wanawake kwa tamaa zako”

“Bwana wangu wananisingizia tu , waliochini yangu ndio ambao wamefanya kosa hilo kwa kunipatia rushwa , nitahakikisha nina wahukumu vifo nikirudi”Aliongea Baiju huku akionekana kutengeneza kisingizio.

“Hata mimi naona , kwa hio unasema mimi ndio mkosaji hapa kwa kusingizia si ndio?”Aliongea huku kitingishcha kichwa chake kama mtu ambaye anajaribu kumwelewa.

Baiju alitaka kutingisha kichwa kujaribu kujitetea kwamba hakupaswa kumbebesha lawama zote lakini hakuweza kufanya chochote wala kukubali kama ana kosa na uso wake ulibadilika rangi na kuwa mwekundu kutokana na presha ambayo ilikuwa ikijiandaa kumkumba.

“Umekuwa na mimi kwa zaidi ya miaka mia mbili , nimekufanya uwe Bwana wa mji wangu wa Wingu Jeupe na ukapokea tani na tani za mawe ya kiroho kutoka katika maghala ya mji na watu wengi wakakuonea wivu lakini bado ukaamua kukusanya zaidi Mawe ya kiroho kupitiia Danguro , Ingekuwa ni sawa kama tu ungekuwa ukidanganya hao ambao walikuwa wakipenda kufanya kazi chini yako lakini ukathubutu kuteka wale ambao wanajaribu kupita katika mji wetu , hivi unadhani mimi siwezi kuishi bila wewe , unafikiri mimi ni mwepesi kudanganywa?”

Jasho la baridi lilimtoka Baiju na kuloanisha nguo zake na aliishia kutingisha kichwa chake akiwa amekiinamisha chini akishindwa hata kumwangalia Aoiline.

“Bwana wangu, Sikuwa nikifikiri sawa sawa , tafadhari naomba unisamehe kwa dhambi nilizoafanya kwa zaidi ya karne moja”

“Sawa”Aliongea huku akikusanya nguo za mkono wake na kutingisha kichwa.

“Itakuwa ni ukatili kama sitoweza kukupa nafasi , nitakusamehe kwa kuwateka wasichana wa kijini nyuma ya mgongo wangu”Aliongea na kumfanya Baiju kufurahiswa na maneno yake huku akitaka kuanza kusujudu kwa mara nyingine lakini Aoiline alimkatisha.

“Lakini hata hivyo napaswa kukuadhibu kwa jambo moja”

“Ah..!”Alitoa sauti huku sura yake akipeleka chini kwa mara nyingine akiwa kama amechanganyikiwa.

“Watu wako hususani Huji wameniteka siku ya leo na wakaniingiza kwenye kiroba ,… ningekuwa mrembo wa kukuingizia hela ndani ya Danguro leo kama sio Mr Roma kunisaidia”

Hio ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Baiju na sasa aliweza kuelewa kwanini Aoiline alibadilisha mwonekanno wake , kila kitu kilikuwa ni mtego wa kumkamata na ufisadi wake.

Ingekuwa afadhari kama angekamata wanawake wengine lakini sasa alikuwa amemsaliti hata Bwana wake hakukuwa na sababu ya kuachwa hai.

Dakika hio alivyojaribu kuunganisha Dot katika akili yake , Baiju alijiambia hakukuwa na faida yoyote ya yeye kuomba kusamehewa au kujitetea na anapaswa kufanya kitu chochote kile ili kuweza kukimbia na kutoka katika hio miliki, alijiambia kama ataweza kufika katika Korongo la Joka , Mfalme wa Majoka lazima angemlinda kwani alikuwa ni jini mwenye uwezo mkubwa wa kimapambano katika levo ya nane.

Baada ya kupatwa na mawazo hayo hakutaka tena kuchelewa, palepale aliita kwa hisia ndege wake mweupe kwa ajili ya kumshambulia Aioline .

Ndege mweupe na yeye akasikia kuitwa na mkuu wake , na palepale lilitoa kilio kikubwa cha juu huku likipiga piga mabawa yake kumsogelea Aoiline moja kwa moja.

Aoline hakuonakana yule mpole tena kwani alibadilika na alikuwa na uso wa kikauzu usio kuwa wa kawaida na kwa Roma ni kama alikuwa akimuona Edna party two, ilikuwa ni kama vile hewa iliokuwa ikimzunguka imeganda.

“Wewe mjinga , unathubutu vipi kujaribu kunipinga mimi?”Aliongea kwa nguvu na palepale kulitokea mwanga kama nguzo mbili nyuma ya gauni lake na nguo moja ya mwanga ilimshikilia yule ndege kwa kumfunga funga.

Roma aliangalia kwa ukaribu zile nguzo zilizokaa kama kamba kamba na palepale ndipo alipogundua ni mikia na pale ndipo alipojihakikishia kweli huyo ni jini ambaye alikuwa akiitwa Mbweha wa mikia tisa.

Mikia yake ilikuwa ni mirefu mno na haikuwa ya kawaida , ilikuwa ni kama boriti au nguzo.

Yule ndege licha ya Roma kumuona mkubwa lakini mbele ya ile mikia alionekana kuwa mdogo mno kwani alikamatwa na akawa hafurukuti kabisa.

Ndege yule alianza kutapa tapa kama vile kuku ambaye anapoteza uhai na ndani ya dakika tu damu zilionekana kuruka juu , ilionekana alikuwa amekamuliwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha viungo vyake kuharibika na hata manyonya yake yalianza kusambaa angani.

Sophia alishindwa kabisa kuangalia kitendo kile lakini kwa Roma alikuwa akiona kitu kile kama hasara kwani yule ndege alimpenda na kujiambia angalau kabla ya kutoka katika ulimwengu huo amwendeshe hata mara moja.

Wakati Aoiline akidili na ndege Baiju alikuwa ashakimbia kwa kupaa umbali mrefu kidogo , lakini bahati mbaya kwake ni kwamba mkia mwingine wa Aoiline ulikuwa ukimfukuzia na ulikuwa ukiongezeka urefu kadri alivyokuwa akikimbia kwenda mbali..

Roma ni jambo lingine ambalo lilimshangaza kwani hakuamini kama mkia huo ungekuwa na uwezo wa kuongezeka urefu na kusafiri umbali mrefu tena kwa haraka sana.

Ni kufumba na kufumbua tu Baiju alipigwa na mkia ule kwa nguvu mara baada ya kusogelewa na alijikuta akitema damu kutokana na kichapo.

“Rudi”

Ule mkia ulimviringa Baiju kufumba na kufumbua tu na kumvuta nyuma na kisha kumrudisha ardhini mbele ya Aoiline na dakika ileile ulipotea katika macho yao , ilikuwa ni kama vile haukuonekana kwani licha ya urefu wake ulirudi ndani ya mwili wa Aoiline kwa spidi kubwa mno.

Roma alijikuta akitengeneza sauti kupitia ulimi wake , Roma alikuwa akijua mwanamke huyo alikuwa na mikia tisa na ameonyesha mwili tu na kilichotokea sio cha kawaida.

Pengine siraha yake kubwa ni hio mikia na kama atapambana nae basi atakuwa ni moja ya washindani hatari ambao ashawahi kukutana nao kwani angekuwa na uwezo wa kujikinga na wakati huo huo akishambulia.

Kwa spidi yake hio na nguvu zake za kijini aliona kabisa hata yeye hakuwa akimuweza kimapambano kabisa, na hakutaka kujiona yeye ni mkubwa zaidi hivyo alikubali Aoiline alikuwa ni levo ya juu kuliko yeye.

Baiju alijikuta amepauka mno kwa woga , alikuwa tyari amekwisha kujikatia tamaa katika kukimbia na aliishia kusujudu kadri awezavyo na kujaribu kuomba kuhurumiwa , lakini licha ya kujitetea huko kulifanya tabasamu la kikatili la Aoiline kuzidi kutisha.

“Bwana nimetenda dhambi zidi yako , unaweza kuondoa nguvu zangu zote za kijini na kunigeuza kuwa mnyama lakini tafadhari naomba usinie , naomba unisamehe”

“Siku zote nilikuwa mpole sana kwa viongozi kama nyie , kwanini nikuondolee nguvu zako za kijini ?,Baiju je utanisaidia jambo moja?”

“I’m willing to redeem myself!”Aliongea

“Great”

Kufumba na kufumbua Aoline alikuwa nyuma ya Baiju na kuishika shingo yake na palepale mkandamizo wa hali ya juu ulianza kumtoka.

“Sophia kuwa makini”

Aliongea Roma na palepale alimsogelea Sophia na kumzingira na nguvu ya kijini kwani tayari ashajua ni nini kinachokwenda kutokea .

Aoiline alikuwa akipanga kumkandamiza na nguvu yake ili kuweza kutawala uwezo wake hivyo kutokana na mkandamizio mkubwa ambao alikuwa akijaribu kutoa Aoiline ilikuwa ngumu kwa Sophia kuweza kuhimili na angetema damu kwani mara nyingi inakuwa kama vile ni mlipoko wa bomu.

Ilikuwa ni kama vile mwanamke huyo mrembo amegeuka na kuwa mungu wa huo ulimwengu kwani macho yake yalikuwa yamebadilika kabisa na kile kiini cheusi kilikuwa kimempotea kwenye macho na jicho likabakia jeupe kama vile ni barafu.

Dakika ileile Aoiline alifumbua mdomo wake na meno yake yaliongezeka urefu kama Vampire na kuyapelekea katika shingo ya Baiju na kumng’ata.

Baiju sura yake mwanzo ilikuwa imepinda kutokana na mkandamizo mkubwa lakini mara baada ya kung’atwa mwili wake ulibonyea palepale .

Sophia aliekuwa nyuma ya Roma hakuweza kupata ujasiri wa kuangalia kile kinachotokea kwani iliogopesha , upande wa Roma alikuwa katika bumbuwazi kwa kile kinachotokea

Alijiambia swala la kunyonya damu ni la kawaida kwani kilichofanyika ni kujaribu kunyonya nguvu za lile jini lakini hakutegemea mwanamke mrembo kama huyo ndio ambaye anafanya kitendo hicho.

Kile kitendo huenda angekuwa ni binadamu wa kawaida ambaye anaangalia angepoteza fahamu palepale , Sophia kwa kiasi hakuwa wa kawaida kwani alikuwa ashaishi na Roma na kuzoea baadhi ya mambo ya ajabu ya namna hio.

Dakika chache tu mwili wa Baiju ulibadilika na Akawa Kunguru mkubwa ambaye ameoza huku mifupa yake ikianza kuonekana na Aoiline alimsukumia mbali maiti ile ya Kunguru na kuanza kuilamba midomo yake kwa damu zilizokuwa pembeni, alikuwa ni kama vile analamba asali kwa jinsi alivyonekana kufurahia.

Baada ya mkandamizo wa hewa kuondoka ndio aligeuza macho yake kwa Roma huku akiachia mkandamizo wa kawaida kama vile alikuwa akijaribu kumuogopesha Roma.

“Mr Roma huna haja ya kuniangalia hivyo na kuniona kama mchawi mnyonya damu , nimefanya hivi kwa zaidi ya miaka elfu moja , hatima yake ilikuwa ni kifo hata hivyo , kwanini nisimtumie kama kirutubisho , Au naongea uongo?”

Roma alikuwa akianza kuwa na wasiwasi juu yake , hata kama alionekana kuwa mrembo wa kuita lakini matendo yake na uwezo wake wa kijini ulimpa mashaka makubwa na kushindwa kuijua nia yake halisi juu yao.

“Nadhani tunapaswa kuendelea na safari yetu maana ushamaliza maswala yako”Aliongea Roma na kisha akamwangaliaSophia akimwambia waanze safari ya kuondoka hapo haraka iwezekanayvyo.

Sophia hakuwa na shida na alikubali kuondoka , yule Aoiline ambaye alitaka kuwa nae karibu hakumtaka tena maana alikuwa akitisha.

Aoiline palepale alitoa tabasamu la kifedhuli na kufumba na kufumbua alikuwa mbele ya Roma na kuwazuia wasiondoke.

“Mr Roma tupo karibu na jumba langu la kimalkia kwanini msiende kupunzima kwa muda”

“Hakuna shida sana juu ya hilo , safari yetu ni kuelekea kando ya ziwa la Mbingu”Aliongea Roma huku akijaribu kutafuta upenyo wa kumpita.

“Hata kama nimekudanganya kuhusu ubini wangu , lakini sikuwa nikidanganya kuhusu mambo mengine , kuna zaidi ya wiki tatu mpaka kwa mnara kufunguka , kwenda huko ni kupoteza muda wako tu”

“Mimi naweza kutokuwa na akili kama wewe lakini siwezi kuwa kichaa kabisa na kuanza kupigana na mtu kama wewe ambaye umeishi maisha marefu , lazima una nia nyingine hivyo acha kuzunguka zunguka”Aliongea Roma mpaka hapo alijua mwanamke huyo hakuwa na nia ya kuwaruhusu waondoke kirahisi.

“Mr Roma sisi majini tunaweza kufikiria pia na sio wanafiki kama binadamu , mosi nimekuja huku kwasababu nimesikia taarifa kutoka kwa watu wangu ndio maana nimekuja kujionea mwenyewekama ni kweli Baiju alikuwa akitenda mambo ya kifisadi, kitu kingine pia waliniambia kwamba kuna binadamu wageni ambao wameweza kufika katika ulimwengu wetu , Watu watatu ambao ulipigana nao katika msitu wamekuongelea vibaya sana lakini sikuwachukulia siriasi na sina nia ya kuwalipizia kisasi kwa uliowafanyia”

“Lakini bado siamini mtu kama wewe unaweza tu kunialika kwako kwa ajili ya kupumzika”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu.

“Nimeongea vya kutosha je tunaongozana au hatuongozani”

“Hatuongozani”Aliongea Roma kwa sauti huku akitingisha kichwa chake kukataa kusisitizia msimamo wake.

Aoiline alitoa pumzi ya kukatishwa tamaa huku akimwangalia Roma kwa masikito.

“Kama hutaki kuongozana na mimi basi sina budi kukulazimisha”Baada ya kuongea hivyo msisimko aliokuwa ukitoa ulibadilika kabisa na macho yake hayakuwa mazuri tena kwani yalibadilika na kuwa ya chuki.

Roma alishindwa kuelewa chuki yake inatokana na nini , aliajiambia kwanini kumbadilikia namna hio ndani ya dakika tu wakati hajamchokoza.

Roma palepale alimsukumia mbali Sophia ili tu asije akapata madhara na baada ya kumuona ameenda mbali zaidi aliita nguvu zake za kijini ili kuweza kuhimiri mkandamizio uliokuwa ukitolewa na Aoiline.

Dakika hio hio Aoiline muonekano wake wa kirembo ulikuwa umebadilika na kuwa kama vile ni jitu kubwa la kutawala , macho yake yalikuwa ni kama yale ya kutaka mtu yoyote anaemuona kumsujudia.

Roma hakutaka kumruuhusu msichana kama huyo kuendelea kumkandamiza , hakutaka tena kulinda nguvu yake ya kijini isipotee na alimsogelea Aoiline kwa nguvu zake zote.

Mpira wa moto wa bluu ulionekana katika mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto ulitegneneza maji ya kiroho ya kuosha uovu.

Aoiline alitoa tabasamu la kejeli kama vile alikuwa akidharau kile anachotaka kufanya.

Awamu hio hakutoa mikia yake bali nguo yake ilianza kutengeneza kamba kama Ribbon kutoka kwenye nguo yake ya hariri akidhamiria kupigana na hio .

Roma hakutaka kujali mbinu yake ambayo anataka kutumia na dhamira yake ilikuwa ni kutaka kumchapa na maji ya kiroho akiamini hata tone lake linaweza kumletea madhara.

Lakini nguo yake ile haikuwa nguo kama nguo kwani ilikuwa ikidhalisha kiwango kikubwa cha nishaiti isiokuwa ya kawaida na kadri ilivyokuwa ikipepea kuelekea upande wa Roma ni kama ilikuwa ikimzuia asimfikie.

Roma alijikuta akishangazwa na uwezo wake , aliweza kujua mtu anaepambana nae ndio yupo katika levo ya juu kabisa ya daraja la tisa la mafunzo ya kijini ya kuita pepo.

Kutokana na mkandamizio wake kuwa mkubwa Roma alijikuta akiamini huenda hata Athena akashindwa kabisa kudili nae.

Kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao mpizani wake Roma alianza kupoteza pambano mapema kabla hata hajaanza kushambulia kwani alishindwa hata kubadilisha nguvu zake kuleta faida katika kushambulia.

Aoiline hakuonyesha kutumia nguvu yoyote alikuwa ni kama vile anacheza na zile kamba za nguo zake za hariri na alianza kuzifanya zipeperuke hewani na zilikuwa zikitoa nguvu kubwa mno .

Roma palepale aliweza kufikiria huenda mbinu yake haikuwa ikitegemea muundo au nguvu bali alikuwa akitegemea akili yake na ufahamu . mpaka hapo alijua kwamba ulimwengu huo wenyewe ulikuwa kikwazo kwake hivyo hakuwa na namna ya kumshinda.
 
SEHEMU YA 325

Tanya alieleza kile alichokuwa akijua kuhusu jiwe la kimungu , licha ya kwamba maelezo yake hayakufikia ukweli halisia juu ya jiwe hilo , lakini ilitosha kumfanya Edna kushangazwa mno , kilichomashangaza Zaidi ni pale alipoweza kusikia kwamba Underwold duniani kote wanawinda jiwe hilo.

“Kama utaamua kulipima kwa uthamani wa kiwango cha pesa , linaweza kuwa na thamani kiasi gani?”

“Siwezi kufanya makadirio , lakini tokea nimeanza kuliwinda kwa maagizo ya Master , walikuwepo watu ambao walitaka kulipia Zaidi ya Dollar Bilioni nne kupata umiliki wake”Aliongea Tanya na kumfanya Edna kuzidi kushangaa.

“Kwahio mpaka sasa jiwe hili analo Roma?”

“Ndio , mtu pekee ambaye ana umiliki wa jiwe hilo ni Master Roma”Aliongea Tanya na Edna alivuta pumzi, mpaka hapo aliamini kuna siri nyingi sana za kuzifahamu juu ya Roma , yaani mtu anakaa na kitu cha thamani namna hio , lakini haonyeshi hata dalili ya wasiwasi, aliendelea pia kukumbuka Roma alikuwa na mapesa mengi sana ndani ya Swiss Union Bank.

“Sasa ikawaje leo hii wewe ndio unanipokea?”Aliuliza Edna swali la muhimu na kumfanya Tanya kunyamaza kidogo kwa muda na kisha ndipo alipoanza kuelezea namna ambavyo Roma alifika nchini Japani akakutana na Seventeen feki, mpaka alipopewa sumu , Tanya kwakuwa aliahidi kuelezea kila kitu ili kupata msahama kutoka kwaEdna , alijitahidi kuweka kila kitu wazi.

Na mpaka Tanya anamaliza kuongea upande wa Edna aliona ni kama alikuwa akisikiliza simulizi tamu kutoka kwa mwandishi SinganoJr , hakuamini siku chache ambazo Roma alikuwa nchini Japani alisababisha maafa makubwa , lakini sio hivyo tu aliweza kuchukua kundi laYamata Sect na kugeuza maadui zake kuwa watumwa wake.

“Kwahio wewe ndio mkuu wa Yamata Sect?”Aliuliza Edna huku gari ikizidi kutembea kusonga mbele na muda wote Tanya alikuwa amepiga magoti.

“Mkuu ni Master Roma , mimi namuwakilisha tu , ila kundi lote la Yamata Sect ni lake mara baada ya kumuua Master Okawa”

“Hili kundi lenu lina thamani kiasi gani na linajihusisha na nini kwa ujumla?”Aliuliza Edna na kumfanya Tanya kukaa kimya kwa dakika akiwa ni mwenye kufikiria.

Nipo na malikia napaswa kueleza kila kitu kundi hili pia ni la kwake”Aliwaza Tanya na kuelezea kila kitu ambacho Yamata Sect wanafanya na alijikuta akimpa ishara Tanya ya kutoendelea , kwani katika vitu tajwa kuna vingine pia vilikuwa ni vitendo vya kiharamu kabisa , kama vile uuzaji wa madawa ya kulevya , lakini Edna alishindwa kumjaji Roma , kwanza kabisa alikuwa akifahamu Rose alikuwa akijihusisha na madawa ya kulevya na Roma ndio aliekuwa akimsaidia kabisa kwenye biashara hiyo , kwahio kwake haikumshangaza kusikia kundi la Yamata Sect ambalo umiliki wake umehamia kwa mume wake kujihusiha na vitu vingi ambavyo si halali katika kipimio cha Sheria.

Dakika kadhaa mbele hatimae Gari zilisimama kwenye jengo la hoteli ya nyota tano pembezoni mwa fukwe katika jiji hili kubwa la Hongkong lenye majengo mengi marefu , ambayo yamejengwa kwa usanifu wa hali ya juu kabisa , ilikuwa ni usiku lakini kupendeza kwa jiji kulidhihirika Zaidi na Edna alijikuta akitamani Tanzania nchi yake kufikia levo hio.

“Madam karibu kwenye hoteli tuliokuandalia , sehemu hii utakuwa salama na utaweza kupata mahitaji yote”Aliongea Tanya na Edna alitabasamu na kushuka kwenye gari.

Dakika chache mbele Edna aliweza kupelekwa mpaka kwenye chumba ambacho ameandaliwa , kilikuwa ni chumba kikubwa mno cha kifahari ambacho kina hadhi ya kulala Raisi(Presidential Suite) , licha ya kwamba Edna amelala kwenye chumba cha hadhi ya Presidendtial Suite , lakini uzuri wa chumba hiko ulimshangaza mno.

Wahudumu watano walikuwa wamesimama mbele yake , wakionekana kusubiria maelekezo kutoka kwa Edna , huku na Tanya pia akiwepo , Edna aliwaangalia wahudumu hao na kutabasamu.

“Nitahitaji huduma ya chakula baada ya lisaa kupita”Aliongea Edna na wahudumu wale waliinamisha vichwa vyao kwa heshima na kisha kwa mstari walitembea kutoka kwenye hiko chumba.

“Tanya kwakua Roma alikusamehe , basi na mimi nimekusamehe , unaweza kuwa na amani na siku ya kesho nitahitaji usafiri”Aliongea Edna na kumfanya Tanya kutabasamu na kupiga tena magoti na kushukuru. Na kumfanya Edna kutabasamu na kumpa ishara ya kunyanyuka.

……………….

Ni siku nyingine muda wa asubuhi , Edna aliweza kuamka mapema sana siku hio kama ilivyokuwa kawaida yake na alikuwa ashajiandaa kabisa kwa kuoga na sasa alikuwa ameketi kwenye masofa akipitia karatasi za maswala ya kazi alizokuja nazo.

Alitumia muda takribani lisaa limoja kupitia karatasi hizo mpaka pale simu yake ya chumba ilipoanza kuita na aliisogelea na kuinyanyua na kisha kuweka mkonga sikioni.

“Madam kuna mgeni hapa mapokezi anaomba ruhusa ya kupata kifungua kinywa na wewe”Ilisikika sati ya muhudumu kutoka mapokezi na kumfanya Edna kushangaa ni mtu gani ambaye anataka kupata kifungua kinywa na yeye.

“Amejitambulisha kwa jina gani?”

“Anafahamika kwa jina la Clark Stephanie”Edna baada ya kusikia jina hilo alimkumbuka Profesa Clark kwani alikuwa akimtambua.

“Okey nitaonana nae baada ya dakika kumi na tano” Aliongea Edna kwa Kingereza na kisha kukata simu.

Dakika kumi na tano Edna alikuwa amependeza mno na sasa alikuwa akishuka kwa kutumia Lift akielekea kwenye mgahawa wa kisasa uliokuwa ndani ya hoteli hii ya nyota tano inayofahamika kwa jina la Yams Hotel.

Edna baada tu ya kutoka kwenye lift ni kama alikuwa akisubiriwa , kwani aliweza kupokelewa na Tanya , alievalia suti ya rangi ya Bluu , alikuwa amependeza haswa na kwa jinsi ambavyo alisimama mara baada ya kumuona Edna , ilimfanya mrembo Edna kutabasamu.

“Tanya nitaondoka Kwenda kwenye kikao Regency Hotel baada ya lisaa muda huu nina mgeni ambaye napaswa kuonana nae”Aliongea Edna.

“Nina taarifa nao Madam , nipo hapa kukusindikiza mpaka mgahawani”Aliongea Tanya kwa heshima na kumfanya Edna kushangaa kidogo na kisha kutingisha kichwa akimpa ishara Tanya ya kuongoza njia.

Edna aliweza kufika kwneye mgahawa wa kisasa kabisa uliokuwa ndani ya hoteli hii , ilikuwa ni sehemu ambayo ina mpangilio wa kisasa sana na kumfanya Edna kuona nchini Hongkong watu wapo siriasi na biasahara za hoteli.

Watu walikuwa wachache sana na muda huo ilikuwa ni saa mbili za asubuhi Kwenda saa mbili na nusu na Edna alikuwa na Ratiba ya Kwenda kukutana na Viongozi wa kampuni ya Yamakuza pamoja na Maple kwa ajili ya kuzungumzia kuhusu swala ambalo limejitokeza , ila aliona sio mbaya kukutana na Clark.

Edna aliweza kupelekwa mpaka kwenye meza ambayo ilikuwa na watu wawili , wote wakiwa ni wazungu , mmoja akiwa mwanaume mwingine akiwa ni mwanamke , mzungu wa kike alikuwa akimfahamu kama Priofesa Clark lakini kuhusu mwanaume mara baada ya kumwangalia vizuri, palepale kumbukumbu zake zilimpeleka Ufaransa.

“Ednaaa.. Welcomee!”Aliongea Profesa Clark kwa bashasha na kunyanyuka na kukumbatiana na Edna.

“Miss Edna Let me say that I am very happy to meet you for the second time even though I did not have the chance to talk to you in the first time , I’m known by the name of Edward from the Rothchild family. Miss Clark here is my cousin”

“Miss Edna , naomba niseme kwamba ninayofuraha ya kukutana na wewe kwa mara ya pili ijapokuwa mara ya kwanza hatukuweza kuongea , nafahamika kwa jina la Edward kutoka familia ya Rothchild”Aliongea Edward kwa kujiamini sana , asubuhi hio alikuwa ametupia suti iliomkaa vyema mwilini na kwa kuangalia tu ni hakika kwamba suti hio ilikuwa ya bei kubwa.

“I remember your face , but I didn’t think you were from the Rothchild family , I’m also happy to see you Mr Edward”

“Naikumbuka sura yako , lakini sikudhania kama unatokea katika familia ya Rothchild , nafurahi pia kukuona Mr Edward”Aliongea Edna.

Ukweli Edna alikuwa kwenye mshangao ndani kwa ndani , hakudhania mwanaume huyu ambaye alimuoana kwa mara ya kwanza Ufaransa alikuwa akitokea kwenye familia maarufu ya Rothchild.

Edna alikuwa akisikia sana kuhusu familia ya Rothchild na hii yote ni kutokana na kwamba alisomea Ulaya na siku zote alizosikia kuhusu familia hii ni kwamba ilikuwa ikitawala Ulaya na baadhi ya mabara katika Nyanja za maswala ya kifedha, sasa kuonana na mmoja ya mwanafamilia kutoka kwa familia hio jambo hili lilimfanya kushangaa na kuona ni bahati pia kwa wakati mmoja lakini wakati huo huo akishangaa kumbe Clark alikuwa ndugu wa karibu na familia hiio, Sasa Edna baada ya kuketi , aliwaza kama Ednward alikuwa akitokea kwenye familia hio yenye nguvu ndani ya bara la Ulaya je mwanamke aliekuwa naye siku ile alikuwa nani.

“Clark sikudhania pia una undugu wa karibu na familia ya Rothchild”Aliongea Edna kwa tabasamu na kumfanya Clark kutabasamu.

“Mama Yangu , Malkia Catherine aliolewa kwenye familia ya Rothchild hivyo inanifanya kuwa binadamu kwa Edward”Aliongea Clark na kumfanya Edna kutingisha kichwa akiashiria kuelewa.

Baada ya kuongea hapa na pale hatimae chai nzito iliandaliwa , sasa unachotakiwa kuelewa hapa chai sio kama chai ambayo tunakunywa sisi walalahoi , chai na chapati mbili , Hapana , bali walichokuwa wakila wenzetu hawa ni kama chakula cha mchana.

“Miss Edna, Mr Roma amenipigia simu ya ujio wako Hongkong , lakini kabla ya kupiga kwake simu pia tulikuwa tukielewa swala linaloendelea kati ya kampuni ya Yamakuza na Kampuni ya Aba na hili ndio maana nilimtumia Binamu yangu ili niweze kuonana na wewe hapa kabla ya kuelekea kwenye kikao”Aliongea Edward na kumfanya Edna kushangaa kidogo na kuona kumbe Roma alikuwa akijali mambo yake na kuchukua hatua mpaka ya kumpigia Edward.

“Ndio naweza kusema kampuni ya Yamakuza imeingia kwenye mgogoro na kampuni ya Aba Group , jambo ambalo linaathiri kampuni yangu moja kwa moja kutokana na mkataba niliosaini”Aliongea Edna huku akikata kipande cha nyama kwa kutumia kisu.

“Nadhani bado Yamakuza hawajakupatia maelezo ya kile kilichotokea, ukweli ni kwamba kampuni ya Aba wanayohaki ya kufungua madai yao katika mahakama ya usulihishi wa maswala ya wizi wa teknolojia”Aliongea Clark na kumfanya Edna kushangaa.

“Lakini mgunduzi wa teknoloji a hii ametokea kampuni ya Yamakuza?”

“Ni kweli unachozungumza lakini kwenye maswala ya kisayansi kuna mambo mengi huwa yanatokea , Morri mgunduzi wa sayansi hii ambaye ni mwanafuzni wangu , katika tafiti alizozifanya alishikirikiana na mwanasayansi mwenzake anaefahamika kwa jina la Ye Chen kutoka China , naweza kusema kwamba Teknolojia hii imekuwa ‘Co founded’ na wote wawili”Aliongea Profesa Clark.

“Kwahio unachomaanisha huyu Ye Chen yupo ndani ya kampuni ya Aba Group?”Aliuliza Edna kwa mshangao.

“Ndio , Ye Cheni kabla ya kuachana na taasisi ya utafiti ambavyo ipo chini ya Yamakuza , aliajiliwa mara moja na kampuni ya utafiti ya Aba ,yenye makao makuu yake hapa Hongkong na kuanzia siku hio kampuni ya Aba iliianza kufanyia kazi teknolojia hio ya malighafi mpya, kwahio swala hili lina mvutano mkubwa, Ye Chen anayo haki ya kumiliki teknolojia hio , lakini pia Morri pia anayo haki ya kumiliki teknolojia hio , hivyo mpaka sasa naweza kusema kwamba ni haki kwa kampuni ya Aba kupitia Ye Cheni kufungua madai yao mahakamani”Aliongea Clark na kumfanya Edna kuvuta pumzi nyingi , mpaka hapo aliona swala hili linakwenda kuwa gumu sana na kama hali itaendelea hivyo mpaka mwisho wa mwezi huu wa kumi ulioanza basi anaweza kupoteza kiasi kikubwa sana cha pesa kama hasara.

“Miss Edna ujio wangu wa kuja mahali hapa ni kuangalia namna yakutatua hili swala , lakini pia kwa upande wangu kunufaika na mazungumzo haya ya kibiashara, na nikuhakikishe kwamba mimi ndio mtu pekee ambaye naweza kufanikisha usuluhishi wa hili swala”Aliongea Edward.

“Naomba kusikiliza mapendekezo yako juu ya namna unavyotaka kusuluhisha hili swala”Aliongea Edna na kumfanya Edward kufuta midomo yake na kitambaa na kisha kunywa juisi kidogo.

“Njia moja kuu ya kumaliza hili swala ni wewe kukutana na mmiliki wa makampuni ya Aba Group nikisema mmiliki simaanishi mwenyekiti wa kampuni au CEO namaanisha ‘Major Share holder’ wa makampuni yote ya Aba , huyu ndio mtu pekee mwenye nguvu Zaidi ndani ya kampuni”Aliongea Edward na kumfanya Edna kushangaa kidogo.

“Nampataje huyu mmiliki?”

“Hio ndio kazi yangu Miss Edna , lakini kabla ya kuanza mchakato wa kuweza kuongea na mmiliki napaswa kwanza kuweka na mimi faida ambayo nataka kutoka kwako”Aliongea Edward.

“Unahitaji nini kutoka kwangu?”

“JR Group”Aliongea Edward na kumfanya Edna kutoa macho.

ITAENDELEA JUMANNE HAPPY WEEKEND


0687151346 WATSAPP NICHEKI NIKUPE MUENDELEZO
Master Singanojr, yapo baadhi ya maeneo una skip. Mfano Episode ya 316, 317 na 319; zote hizo umeziruka ilhali umezitaja kabisa, yaani zipo blank. Tafadhali proof read EP numbers.
 
Back
Top Bottom