SEHEMU YA 678.
Ilikuwa rahisi sana kwa jini mwenye uwezo mkubwa kutengeneza pango , ukweli ni kwamba viumbe wenye uwezo mkubwa enzi hizo ndio walihusika zaidi katika kutengeneza mapango , dunia ya leo ina mapango mengi ambayo ujenzi wake aidha ulifahamika kuwa wa binadamu au mengine hayafahamiki kama ujenzi wake ulifanywa na binadamu kutokana na kukosa ushahidi.
Roma mara baada ya kuingia kwenye pango hili alijua kabisa kama mtu wa kawaida angekuja katika eneo hili angeshangazwa na angekosa ushahidi wa moja kwa moja kama pango hilo limetengenezwa na binadamu.
Roma kitendo cha kuingia ndani tu aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikitoka kwenye hilo pango na eneo lote lilikuwa limezingirwa na vifaa mbalimbali ikiwemo vitu kama vibuyu vilivyotengenezwa kwa madini ya Jade , kwenye chupa hizo kulikuwa na maji ya chemchemu.
Maji ya Chemchem pia ni maji ambayo ni mhimu sana kwa majini na ndio maji adimu sana duniani lakini ya thamani sana kwa majini.
Yaani baadhi ya vitu Rufi alivyomwelezea kwamba vinapatikana katika ulimwengu wa kijini , kwenye kona ya pango hilo kulikuwa kumesimamishwa chuma cha aina mbalimbali ikiwemo chuma kisichopata kutu(Frosty iron) na chumba ambacho ni kigumu(Fire iron) au kwa kiswahili sanifu tunaita chuma cha pua.
Utofauti wa aina ya chuma hicho ni mkubwa sana ni aina ya chuma adimu sana ambacho hutumika kutengenezea Dhana za kijini hivyo huwezi kupata katika dunia ya kawaida labda ujinini.
Kama Master Wadudu angekuwa na uwezo pamoja na kuwa na Chungu kama cha Roma basi angekuwa ashatengeneza dhana za ajabu mno.
Wakati Roma akiendelea kukagua mazingira aliweza kuona kitu kingine ambacho kilifanya macho yake kuchanua , pembeni kabisa kwenye kona kulikuwa na furushi la mifupa na kwa haraka haraka tu aliweza kugundua mifupa ile lazima itakuwa ya wanawake.
“Hio mifupa ni ya nini?”Aliuliza Roma.
“Master hio ni mifupa ya wanawake ambao niliwatumia kuwalisha wadudu wangu “
Roma alijikuta akikunja sura ashawahi sikia kuhusu majini ambayo hutumia mbinu ya kupanda levo kwa kutumia damu na nyama za binadamu.
Aina ya majini ambao hutumia mbinu hio walikuwa ni wa tofauti kabisa na wale ambao amekutana nao kawenye ulimwengu wa majini pepo, majini wazuri ndio wale ambao hushinda laana ya kipepo iliondani yao na wale majini wabaya ni wale ambao wanaipa laana nguvu hao ndio wale wa dunia ya kijini pepo.
Kuhusu majini wanaonyonya damu pamoja na nyama hawa ni aina ya majini ambao hupenda sana kujihusisha na walozi au wachawi na mara nyingi huua binadamu kichawi ili kutumia damu yao kuweza kujiongezea nguvu.
Sasa majini ni kheri kutoa utajiri wa dhahabu na pesa kuliko kukosa nguvu za kijini kwao kitu cha thamani ni nguvu ya kijini na sio pesa na ndio maana hutajirisha binadamu wenye tamaa ili mradi tu watakuwa na uwezo wa kuwahakikishia uwezo wa kupata damu na nyama huku wao wakiwapa utajiri.
“Master nataka kugundua mbinu nzuri ya mafunzo ya kijjini , hi mbinu nilipatiwa na Master wangu , ijapokuwa nataka kujifunza lakini kipindi hichi ni tofauti na miaka ya zamani kwani ni ngumu sana kutumia mbinu za kawaida kuingia hata levo ya nafsi , tafadhari namba uchukue kila kitu lakini uniachia uhai wangu”
“Nipatie majina ya viongozi wakubwa wa umoja wa North Buyeo”Aliongea na Master Wadudu alitingisha kichwa na palepale alitumia pete iliokuwa kidoleni na kilionekana kitabu kidogo kikijitokeza bila ya kueleweka kimetokea wapi.
“Kumbe na wewe unatumia pete kuhifadhi vitu , naamini utakuwa na vitu vizuri zaidi umeficha”Aliongea Roma huku akichukua kile kitabu.
Master Wadudu palepale alishikwa na wasiwasi mara baada ya siri yake kufichuka lakini kutokana na woga wake palepale alitoa ile pete na kumkabidhi Roma akitarajia amuache awe hai.
Roma alitumia uwezo wake kukagua ukubwa wa hifadhi ya pete hio na alikuja kugundua ukubwa wake ni mara mbili zaidi ya kwake na alifananisha na ukubwa wa hifadhi ya pete ya Sophia.
Ndio, Sophia wakati alipokuwa ulimwengu wa kijini Pepo alipewa Zawadi na Aoiline ya pete ya madini ya Dhahabu na Rubi ni pete ambayo ukimuona ameivaa utaona ni ya kirembo lakini ni ya kijini na hutumika katika kuhifadhia vitu kimazingara lakini wakati mmoja pia kumuongezea mvuto.
Ndani ya hifadhi ya Master wadudu katika pete hio kulikuwa na mimea adimu sana na Roma alifurahi na kujiambia angeitumia katika kutengenezea vidonge vingi tu vya daraja la juu ambayo hata ulimwengu wa kijini hawawezi kuwa navyo.
“Master nimekupatia kila kitu , je naweza kundoka sasa hivi , naapia siwezi kuwadhuru wengine tena na sitajitokeza mbele yako milele”
“Kabla ya kuondoka unapaswa kuacha kitu kimoja”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la kifedhuli.
“Nini?”Aliongea huku akianza kujisachi kama ana kitu kingine cha thamani lakini alikuja kugundua alikuwa na ushanga tu ndio amebakia nao.
“Namaanisha unatakiwa kuacha uhai wako hapa hapa”Aliongea Roma na kumfanya Master Wadudu kupiga kelele ya hofu.
“Master kwanini unaenda kinyume na ahdi yako , umesema ninachotakiwa kukupatia…”
“Mimi sio Master wala Shujaa , ninachojua mnafiki kama wewe na mtu mchawi hustahili kuendelea kuishi”Aliongea Roma na mpaka hapo Master Wadudu alijua kabisa alishajiingiza kwenye mtego wa Roma.
Alitaka kukimbia lakini Roma hakumpatia nafasi hio na katika hatua ya kupambania uhai wake palepale kucha za mikono yake zilianza kurefuka huku mwili wake ukianza kuzingirwa na moshi mwingi pamoja na upepo , alionekana alikuwa akitafuta mbinu ya kukimbia lakini Roma alitumia nguvu yake ya kijini akiunganisha na ile aliovuna kutoka kwa chungu na kuisharabu nguvu yote ya Master Wadudu.
“Nitakutafuta hata kama nitakuwa pepo …”
Kabla hajamaliza sentensi yake ya laana mwili wake palepale ulilipuka kama bomu na Roma hakutaka hata kumpa nafasi ya kuwa pepo kwani Roma alitumia nguvu ya Cauldron kuinyonya roho yake na ndio ukawa mwisho wake.
Nguvu yake yote ya kijini ilimwingia Roma palepale na iligeuzwa kuwa yake na nguvu ya andiko la urejesho.
Roma alishangazwa na jambo hilo , mwanzoni hakutaka hata kufnyonza nguvu yake lakini alishangaa nguvu yake ya kijini kufanya kazi kama sumaki na kunasa nguvu zote za Master Wadudu na kuzifanya kuwa za kwake.
Hio kwake ilimaanisha kwamba hakuhitaji tena chungu chake kutaka kufyoza nguvu za wengine. Lakini hata hivyo Roma aliamini pengine uwezo wa Master Wadudu ulikuwa mdogo sana kuliko wa kwake ndio maana umevutwa kirahisi na kubadilishwa kuwa wa kwake.
Roma mara baada ya kummaliza Master Wadudu palepale alianza kukusanya utajiri.
Ilionekana alikuwa amekusanya sana , ukiachana na madini ya dhahabu yaliokuwepo lakini pia kulikuwa na masanduku ya Dollar ambazo zilikuwa zimepangiliwa , ilionekana wakati akiwa kama kiongozi wa North Buyeo alikuwa akijikusanyia mali tu.
Roma alikaa chini kabisa na kuanza kuhesabu thamani ya utajiri kwa haraka haraka kijini na ndani ya lisaa limoja tu alikuwa ashamaliza na aliweza kukadiria utajiri wote wa Master Wadudu ni zaidi ya dollar za kimarekani bilioni moja.
Jambo hilo lilimfurahisha Roma kutokana na kwamba siku chache zilizopita alimpa maelekezo Ron kuuzia Tanzania mafuta nusu bei ambapo jumla ya gharama yake ni zaidi ya bilioni moja za kimarekani , hivyo ni kama amerudisha pale palipopungua.
Roma alijiambia hakika nguvu ya kutoa ni kubwa , ukitoa kidogo unapewa kikubwa zaidi, maana sio kwamba tu amepata utajiri bali alipata vitu vingi zaidi vya thamani.
Kwa Roma inaweza kuwa kama utani lakini katika ulimwengu wa kiroho nguvu ya kutoa ni kubwa mno , Asante ya Dhati katika ulimwengu wa kiroho bila kujali ni upande wa giza au wa nuru ni Akiba, ndio maana sadaka inayomfikia mhitaji moja kwa moja ina nguvu zaidi kuliko ile ambayo inamfikia mtu asie na uhitaji.
Kwa mfano kumpa sadaka mtu ambaye hana uhitaji sadaka yako haina maana kwasababu maana ya sadaka katika ulimwengu wa kiroho inatafutwa ile Asante ya Dhati na sio ile ya kinafiki , yaani sadaka inayoenda mahali sahihi haipotei bali hugeuzwa na kuwa kitu kingine, ndio maana katia dunia ya leo hata wale wahalifu na matajiri wanaotumia majini au mbinu zisizohalali kupata utajiri hutoa sadaka, kile kitendo hakifanyiki kumuonyesha mtu ana roho nzuri bali ni uwekezaji wa kupata mara mbili, japo wengine hawafanyi kama uwekezaji.
Roma aliangalia baadhi ya majina ya wanachama wa North Buyeo na alichoweza kuona ni majina ya watu hata asiowajua na familia ya Gong ambayo alikuwa akiishuku yenyewe haikuwa katika orodha.
Roma hakuwa na mpango wa kuwaua , alichotaka ni kujua kama kuna mtu wa karibu na Yezi na hakuona, hivyo kuhusu hao wengina alijua kwasababu kiongozi wao amekufa basi ni lazima watapambana wao kwa wao ili kugombea nafasi na ni maswala ya kiserikali ambayo hayakuwa yakimuhusu.
Roma aliangalia utajiri uliokuwa nyuma yake na alijikuta akitoa kicheko cha furaha na alianza kukusanya kila kitu na kuhifadhi kwa mbinu za kijini huku akikariri baadhi ya dhana ambazo hakuzijua ili kwenda kumuuliza Rufi.
Wakati akiendelea kuchangua changua baadhi ya vitu alikuja kukutana na tunda la rangi nyekundu kama damu ambalo lilikuwa limehifadhiwa kwenye chupa ya Jade.
Roma hakujua tunda lile maana yake ni nini na palepale alichukua kitabu ambacho kilikuwa kikielezea aina mbalimbali ya mimea na kusoma jina lake na alijikuta akitoa kicheko cha ushindi na palepale alilichukua na kulitupia kwenye hifadhi.
Roma hakuchunguza vitu vingine na aliendelea kutupia kwenye hifadhi ya pete mpaka alipohakikisha pango lote limekuwa tupu aliondoka na palepale alitumia nguvu za kijini kuharibu pango lile na palepale ni kama vile kumegonga radi na eneo lote la mlipa lilititia kwenda chini na kufanya maji kuanza kufunika lile eneo kama vile ni Tsunami na hakutaka kuangalia kitakachotokea zaidi ya kuondoka.
Hali ya hatari ndani ya jiji la Seoul ilikwisha kudhibitiwa na mabomu yote yaliweza kugunduliwa na vifaa vya teknolojia ya hali ya juu , ingekuwa ni Tanzania ingechukua muda lakini kwa Korea kusini taifa lililopiga hatua ilikuwa rahisi sana.
Kutokana na tukio hilo la kigaidi harusi iliopangwa kufanyikia ndani ya matempo hayo ya Jogyesa ilionekana kabisa hakuna dalili ya kufanyikia hapo.
Ni dakika chache tu Park Juan alikuwa akimaliza kuongea na simu na kwa kumwangalia tu ilionekan taarifa haikuwa nzuri , yaani alipewa maagizo ya harusi kutofanyikia katika eneo hilo.
“Sir nadhani hatuwezi kufanya chochote kwa sasa , isitoshe hakuna alietegemea hili kutokea , tunaweza kufanya sherehe hii siku nyingine tu”Aliongea Kim Yang.
“Ndio Babu hatuwezi kuharakisha na kubadilisha eneo la harusi isitoshe dharula imekwisha hivyo hivyo ndoa haitokuwa na baraka kufanyika kesho”Aliongea Yezi akipigilia msumari , aliona atumie nafasi hio ndoa hio kughairishwa.
Upande mwingine Kim Jip wala hakuonyesha mabadiliko yoyote alikuwa ametulia kama vile hakuna kilichotokea.
Park Juan mara baada ya kuona furaha ya Yezi aliweza kukumbuka kitu na palepale aling’ata meno yake kwa hasira.
“Hapana , tushaalika watu tayari na maandalizi yamekamilika , kesho ni siku nzuri pia hivyo ndoa itafanyika kama ilivyopangwa”Aliongea
Watu wote walishangaa lakini hata hivyo hakuna ambaye alimshangaa kuongea hivyo isitoshe walikuwa wakimjua kwa kuwa na isimamo.
“Babu kwanini una haraka ya kutaka niolewe , kwanza simpendi huyo Kim Jip mimi”Aliongea Yezi.
“Kimya!, kwanini unaongea hivyo hapa”
“Nadhani haishangazi kwa Yezi kutompenda Kim Jip , ni sawa tu , isitoshe ndoa nyingi katika familia kama za kwetu, ndoa ni kwa ajili ya sitara tu”
“Yezi unapaswa kushukuru familia ya wakwe zako ni waungwana , utaelewa nini wajibu wako kama mrithi wangu wewe?”Aliongea Babu yake.
“Ninawachukia sana”Aliongea kwa hasira na kisha akakakimbilia juu huku Eujung akimfatilia kwa nyuma akionyesha wasiwasi.
Kim Jip ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kuangalia upande wa ngazi na macho yake yalionyesha hali flani isiokuwa ikielezeka.
“Baba kwasababu hatuwezi kutumia Jogyesa , nitafute eneo lingine?”aliuliza Park Jiyeon mtoto wa kike wa Mzee Park.
Tokea tukio la Park Jonghyun litokee familia yote ilikuwa imeshika adabu na hakuna alieleta kiburi mbele ya baba yao, ijapokuwa hawakuridhika na maamuzi ya kumchagua Yezi kama mrithi lakini hakuna ambaye aliongea neno.
“Wasiliana na wageni wote na waambia sherehe itafanyikia katika ukumbi wa hoteli yetu ya Starmoon, hamisha kila kitu na hakikisha maandalizi yanafanikiwa usiku huu huu”Aliongea na Park Jiyeon aliitikia na palepale waliondoa na mume wake kwa ajili ya kufanya maandalizi.
Juu chumbani kwa Yezi alikuwa akionyesha hasira zake waziwazi kwa kupiga piga kitanda na mito , Eujung aliishia kusimama kwenye mlango huku akimwangalia Yezi tu bila ya kuongea chochote , isitoshe ashajua hata kama akiongea asingemsikiliza.
Dakika ileile Yezi alifunga nywele zake vizuri na kisha akasogelea simu yake .
“Miss , unampigia nani?”
“Nampigia Bro Roma nione kama amerudi , nataka anitoe hapa nimechoka”Aliongea .
******
Upande mwingine tokea tukio litokee Clark alikuwa amekaa kwenye hoteli katika balkon akiwa ameshikilia kishikwambi chake , alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu akimsubiria Roma , kuna hata wanaume wa Kikorea waliionyesha ishara za kumchombeza lakini hakuwa na habari nao.
Clark hakuwa na wasiwasi na usalama wa Roma kwani alikuwa akimjua tokea alipokuwa mdogo na aliamini angeweza kushinda kila gumu lililopo mbele yake.
Wakati akiendelea kuachama kwa njaa hatiimae mtu alitokeza mbele yake hewani na kutua mbele yake na baada ya kuangalia vizuri alikuwa ni Roma.
“Roma!!”
Dakika ileile aliweza kuhisia mabadiliko ya Roma , aliona kitu tofauti kabisa kutokana na muonekano wake.
“Babe umeponyesha uwezo wako na umerudi!!?”aliongea kwa kuhamaki na kumfanya Roma kucheka na kisha kumbusu mdomoni.
“I gained a lot this time , Honey it was a blessing in disguise , I think God really likes me”Aliongea Roma akimaannisha kwamba amepata vingi awamu hio na kusema pengine ilikuwa ni baraka iliojificha na anadhani Mungu anampenda sana.
“Haraka niambie nini kimetokea”Aliongea Clark kwa furaha.
Roma hakuwa na haja ya kumficha kwani ndio aliehusika na mafanikio hayo na kumfanya Clark kuwa katika hali ya mshangao.
“Yule Zihao ,,, namaanisha Master Wadudu ni mzuri kwenye kuigiza aisee”
“Ni kwasababu ya dhana yake ya Jani la Upofu , kwasasa naweza kutumia hii dhana kuficha uwezo wangu , ninaweza pia kubadilisha muonekano wangu ninavyotaka”
Muda ambao Roma alitaka kuongea simu yake ilianza kuita na alipokea palepale mara baada ya kugundua inatokea kwa Yezi.
“Yezi nini tatizo”Aliuliza Roma.
“Bro ,,, uko sawa?”
“Ndio niko sawa”Alijibu Roma huku akitoa tabasamu baada ya kuona Yezi alikuwa akimjali licha ya kumpotezea ile asubuhi.
“Nimefurahi kusikia hivyo , lakini naomba uje unitoa huku , mimi sitaki kuolewa na Kim Jip , babu amesema anabadilisha ukumbi na ndoa inapaswa kufanyika kama ilivyopangwa , mimi kweli sitaki kuolewa nae jamanii..”
“Yezi mimi ni mtu wa nje tu ya familia na siwezi kuingilia , ijapokuwa nakujali lakini hio ni familia yako , babu yako hawezi kufanya maamuzi ambayo yatakuathiri , anachofanya ni kuhakikisha unakuwa na kila kitu chake , hebu jaribu kuzingatia na hisia zake pia , jitahidi kumfahamu Kim Jip sio mtu mbaya na utatokea kumpenda”
“Mimi sitaki kusikia hivyo , kwanini kila mtu hanielewei , Roma nakuchukia sana na wewe”
Upande wa pili Yezi alitupia simu chini na ikapasuka pasuka
“Una uhakika hutojutia , hata kama hutaki kuzipokea hisia zkae lakini hupaswi kumlazimisha kuolewa na mtu asiempenda”Aliongea Clark
“Ukweli ni kwamba sijui kama hisia za Yezi juu yangu ni za kweli , knna muda anaonekana kama mtoto na kuna muda anaonekana kama mtu mzima , itakuwaje hapo baadae kama akishakuwa na akili za kiutu uzima akija kugundua maamuzi alioyafanya yalikuwa ya kimhemko , atanilaumu sana kwa kubadilisha maiiha yake , wakati nilipoanzisha mahusiano na Sophia , Edna aliniambia mimi ni zaidi ya mnyama na niliona yupo sahihi kabisa … sidhani ni hatia ya namna gani itanipaa kama nikifanya hivyo pia kwa Yezi”
“Mwisho wa siku bado unajali hisia za Edna licha ya kwamba ndoa yenu ipo ukingoni na huachi kumuwazia , inasikitisha sana”
“Hapana sio hivyo , yaani nashindwa kujiondoa na hatia , muda mwingine najiuliza mtu kama mimi nilifanikisha vipi kuuteka moyo wako , kuwa na mahusiano na mimi ni hatari pia kwani nina maadui ambao wengine wanaonekana na wengine hawaonekani , kumjumuisha na Yezi ni kumuweka katika hatari … hiki ni kitabu ambacho nimekipata kutoka kwa kiongizi wa North Buyeo na hakuna mwanafamilia yoyote ambaye ni mwachachama , hivyo ijapokuwa najua kabisa hampendi Kim Jip ila sitaki kuzuia ndoa yao , najua kabisa atakuja kuwa na maisha ya amani”
Clark ijapokuwa alimuonea huruma Yezi lakini hakutaka kumlizimisha kutoka kimapenzi na Yezi na aliishia kumkumbatia na kisha walipandisha juu kwenda kuona chumbani kwao kwend akuona ni vitu vya aina gani Roma alipata.
“Clark wewe hebu tangulia kwanza kwenda chumbani , nataka kurudi Tanzania kumuuliza Rufi baadhi ya kitu nilichokipata ili anithibitishie , nitarudi nikimaliza”Aliongea Roma mara baada ya kufika mlangoni