Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Amani iwe nawe mkuu hades/Pluto/roma/baba lanlan/mzee wa kuzichakata tamu za warembo/ singanojr ikukupendeza basi tukumbuke sisi wadau wako hapa jukwaani.
 
Nitaweka mwendelezo saa nne usiku inshallah...mimi ndio nawajibika kutoa mwendelezo hapa maana ndio nimeanzisha uzi... mtu mwingine kuweka mwendelezo hapa ni kuharibu uzi na hasara zake ni kwamba simulizi hii haitofika mwisho hapa.
Kwasababu nikileta mwendelezo ni vipande vingi basi mnivumilie nisipokuwa hewani maana natingwa muda mwingine
572- 575 Hamna
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware


SEHEMU YA 676.
Kutokana na kuelewa uwezo wa Roma ni kama mzigo aliokuwa nao kifuani umeshuka , lakini hata hivyo Jamali hakuwa na uelewa wa uwezo wote wa Roma.
“Kumbe ni wewe… hata kama uliweza kuhimili ulozi wangu bado tu nikwambie huniwezi , ni mjinga pekee ambaye anaweza kuingia kwenye himaya yangu kwa hiari”Aliongea Abbess Yu Lian mara baada ya kumfahamu Roma.
“Hii samaki nyama yake ni tamu lakini ana mifupa mingi”Aliongea Roma akimpotezea Abbess na kisha alitupa ile samaki pembeni huku akijilamba midomo.
“Hivi unanisikiliza?”Aliuliza Abbess kwa mara ya pili na palepale Mason alimsogelea Abbess na kumnong’oneza jambo.
“Kiongozi , nafikiri anajaribu kusema … ameogelea mpaka hapa”Aliongea Mason kwa Kingereza.
“Bullshit , inawezekanaje mtu kuogelea kwa zaidi ya masaa manne kufukuzia boti … hebu acheni kuniangalia muueni”Aliongea kwa kufoka na dakika hio hio Hao , Mason na Hwang Suyeon walianza kumrushia Roma risasi .
Cheche za moto zilitoka kwenye bunduki na kutua kwenye mwili wa Roma lakini hazikuonyesha athari yoyote , jambo ambalo lilimkasirisha Roma ni kwamba boksa yake ilikuwa ikichanika na kumuacha kabisa uchi na palepale , isitoshe hio ni boksa alionunuliwa na Edna.
Roma alisomsogelea Hao kwa spidi kubwa kiasi cha bwana huyo kushindwa kushituka mapema na ilikuwa ni kufumba na kufumbua tu shingo yake ilivunjwa palepale na kudondoka chini na huo ndio ukawa mwisho wake.
Roma hakupoteza hata sekunde kwani palepale alimpiga kibao Hwang Suyeon na mkono mwingine wa kushoto , kilikuwa ni kibao kikubwa mno ambacho kilichangua fuvu lake kama vile amegongwa na gari na palepale alidondoka chini huku kichwa kikiwa na ufa na huo ndio ukawa mwisho wake .
Hofu iliwashika Abbess Yu Lian na Mason baada ya kuangalia mashambulizi hayo ya sekunde tano ambayo yamefanya na wenzao kufa kikatili sana.
Roma hakutaka kujali mshangao wake na palepale aliinua mguu wake na kumpiga nao mzungu Mason sehemu za siri na ni damu tu zilizomtoka na Roma hakuishia hapo tu baada ya kumpiga teke la sehemu za siri aliimuongezea na la tumbo na kufanya mwili wake kuruka juu na kugonga kwenye chuma na mpaka alipokuja kutua chini utumbo wote na maini vilikuwa nje.
Jamali kidogo tu azimie kwa tukio lile huku Zhang Ru akiwa tayari ashapoteza fahamu muda mrefu sana mara baada ya kurukiwa na jicho la Hwang Suyeon kwenye miguu yake.
Yu Lian alijikuta akimeza mate mengi ya woga akiwa anatetemeka na alianza kurudi nyuma huku akitingisha kichwa chake mara nyingi.
“Usinisogee …”
Dakika hio wanajeshi walianza kuongezeka mara baada ya kusikia purukushani lakini mara baada ya kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea walijikuta wakipaniki na kupigwa na bumbuwazi.
Roma aliwapotezea na kisha alimsogelea kiongozii wao Yu Lian.
“Wewe ndio kiongozi wa North Buyeo?”Aliuliza Roma na Abbess Yu Lian alitingicha kichwa
“Umetoa wapi ujasiri wa kuchukua Sarira Kabla yangu , wewe unastahili kifo cha maumivu lakini kama utanipatia faili linalohusiana na huu umoja wenu , nitahakikisha kifo chako kitakuwa cha haraka”
Roma alitaka kufanya uchunguzi yakinifu kuhusu umoja huo wa North Bueyeo ili auzimishe kabisa kabla ya kuondoka kutokana na hofu ya Yezi kuingia kwenye matatizo.
“Kwahio na wewe ulikuwa ukihitaji Sariras?, Haha,, huogopi mabomu ndani ya Seoul yatalipuka baada ya mimi kufa , hata kama wamepata baadhi yao lakini hawawezi kuyapata yote ndani ya muda mfupi mpaka muda h…”
“Nenda kuzimu wewe …”Aliongea Roma na palepale alimchapa kibao.
“Watu ndani ya dunia hii wanakufa kila siku , kwanini nijali vifo vya raia wachache , hao sio wazazi wangu hebu acha kuongea ujinga , unanipa faili au hunipi?”
Yu Lian aliishia kubung’aa na alijikuta macho yake yakipita kwenye maiti zilizokufa vibaya sana kama vile zimekumbana na ajali na woga ulianza kumuingia na kwenda kusambaa mgongoni.
Alikuwa ashajua mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa ni mkatili sana na asingeweza kujali maisha ya raia.
“Nitahesabu mpaka tatu , kama usiponipatia faili nitachomoa kidole kimoja kimoja ..”Aliongea Roma na palepale alimshika Abbess mkono na kushika kidole gumba na kukivunja na kisha akakivuta.
“Argh…!!!”Alijikuta akitoa ukulele wa aina yake.
Wanajeshi walikuwa wakitaka kumshambulia Roma lakini walikuwa na woga na mara baada ya kuona kiongozi wao anachofanyiwa palepale wote walikimbia.
“Master naomba uniokoe” Abbess Aliongea kwa sauti kubwa akimwita Master wake na jambo lile lilimshangaza Roma
Roma kabla hajajua ni Master Gani anaitwa aliweza kusikia miguno ya wanajeshi ambao walikimbilia nje.
Roma palepale aligeuka na macho yake yaliweza kuona kitu cha kushangaza , kulikuwa na kundi la wadudu wa ajabu ambao walikuwa wakipiga kelele na kuwashambulia wale wanajeshi kwa kasi ya ajabu mno , walikuwa ni wengi kiasi kwamba ndani ya sekunde chache tu wale wanajeshi wote walishapoteza uhai na nyama zao zilishalika tayari na kubakiwa na mifupa tu.
Kitendo kile kilimfanya Yu Lian macho yake kuchanua huku upande wa Jamali akipatwa na hofu na kile kilichotokea .
“Haha…. Hamna thamani yoyote nyie wapuuzi ni bora kuwapa lishe watoto wangu kuliko nyie”
Sauti ambayo Roma aliweza kijua iliweza kusikika kutoka nje ikiongea kwa lugha ya Kikorea na kuchanganya na kichina na dakika hio hio aliweza kuonekana Monk kibonge akiingia.
Alikuwa ni Master Zihao , Monk ambaye alikuwa akifatishana na Abbes yu Lian na pia yeye alifahamika kama naibu mkuu kiongozi wa ushirika wa Kibuddha.
“Sijajua ni wapi umetokea lakini unakitafuta kifo kuingilia mipango yangu”Aliongea mara baada ya kumwangalia Roma.
“Ndio maana nilishangaa kwanini North Buyeo kumteka Clark wakati kiongozi wao ni dhaifu , kumbe wewe ndio kiongozi mwenyewe , aisee wewe mwanaume ni msiri”Aliongea Roma
Roma alikuwa katika mshangao ndio , hata kama hakuwa na uwezo wa kutumia uwezo wake wa kijini lakini alikuwa akihisi kabisa mkandamizo wa ajabu uliokuwa ukimtoka Master Zihao alionekana kuwa na nguvu za kijini.
Lakini sasa kilichomshangaza ni kwamba kule hotelini alishindwa kuhisia chochote mpaka baada ya Mzee huyu kuachilia uwezo wake ambao ulikuwa mkubwa zaidi ya levo ya Nafsi.
Roma alijiuliza au huyu Monk atakuwa na dhana ambayo inamsaidia kuficha uwezo wake , vinginevyo asingeweza kuishi Korea Kusini kwani angekuwa ana kiuka sheria.
“Haha… kama ndio umenijua ndio nini sasa , uwezo wako wa kimwili ni wa ajabu mno kitu amabcho sijawahi ona kama nitawalisha watoto wangu na damu yako pamoja na nyama yako nina uhakika watafaidikika”Aliongea akimaanisha wale wadudu.
“Una nguvu za kijini hivyo lazima utakuwa unajua kwamba kuwepo nje ya mipaka ya China na Hongmeng unavunja sheria”
“Ndio maana nakwenda kukuua kirahisi , najua mambo mengi kuliko wewe”Aliongea Master Zihao.
“Ndio Master naomba uniokoe”Aliongea Yu Lian ambaye alikwua kwenye mchecheto mara baada ya kumuona , alikuwa hata amesahau maumivu yake.
“Huna thamani kwangu tena , nimekulisha Virutubisho vya kutosha hivyo mwili wako utakuwa umejaa virutubisho ambavyo vitakuwa na faida kwa watoto wangu , nyie wote wawili mtakuwa ni chakula”Aliongea na palepale kundi la wale wadudu wakubwa wenye umbo kama la Mende lakini ukubwa wao ni mara nne zaidi ya Mende na walikuwa wengi mno.
Ni ndani ya dakika chache tu mwili wa Roma na wa Abbes Yu Lian ulifunikwa na wale wadudu wa rangi nyeusi na kuwafanya wasionekane kabisa miili wao.
Roma aliishia kutoa tabasamu la kifedhuli na palepale aliamua kutumia kanuni za anga kushindana na Zihao , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa mkubwa ziadi ya levo ya Nafsi.
Roma palepale aliwatoa wale mende kutumia kanuni ya anga na wote wakamvamia Abbess.
Abbess Yu Lian alikuwa akitoa kilio cha kusaga meno kwa maumivu ya kung’atwa na wadudu wale wa kichawi na kabla hajapoteza uhai alimwangalia Master wake kwa mara ya mwisho kana kwamba anamuuliza kwanini amemfanyia hivyo na palepale alidondoka chini na kupoteza uhai lakini Master Zihao hakuonyesha kumjali kabisa na alimwangalia Roma kwa mshangao.
“”Huh.. hio ndio mbinu niliosikia katika hadithi ya kanuni za anga , wewe ni sehemu ya miungu?”Aliuliza kwa mshangao na dakika ileile Roma alitumia kanuni za anga na palepale Zhang Ru na Jamali walipaishwa na kutolewa ndani ya eneo hilo na kwenda kutua nje na kutokana wanajeshi walikuwa wakipambania uhai wao hawakuwajali sana.
Muda huo huo Roma alijitengenezea kizuizi kujizingira mwili wake na kisha akafutika na kuibukia mbele ya Zihao akinuia kumuua kabla hata hajafanya shambulizi lingine.
Ilikuwa bahati mbaya Zihao alkuwa amejiandaa na ghafla tu kundi lingine la wadudu liliibuka kutoka kusikojulikana , kundi hilo lilikuwa tofauti kidogo walikuwa na miili kama kidole gumba ukubwa wake na walikuwa ni wa rangi ya kijani.
Na Roma alishangaa mara baada ya wadudu wale kufanikiwa kupita katika kizuizi chake na kuanza kumng’ata.
“Hio ndio mbinu pekee uliokuwa nayo?, unathubutu vipi kujiita mungu , wadudu wangu maarufu kwa jina la Ziwu wa kijani wana nguvu ya kijini ya kupita kwenye kizuizi chochote kilichoteongenezwa kwa kanuni za anga”Aliongea kwa majigambo.
Roma alielewa mara baada ya kung’atwa , wadudu hao walikuwa wana sumu kali sana ambayo walikuwa wakijaribu kuiingiza kwenye mwili wake.
“Hii mbinu hakika ni ya kichawi”Aliongea Roma
Kama isingekuwa uwezo wake wa kimwili angekuwa ashakufa palepale kutokana na sumu kali.
Dakika hio hio Roma alitumia kanuni ya anga na kuwalipiua wale wadudu na kisha akamsogelea Zihao kumshambulia
“Hujaathirika na sumu ya wadudu wangu , wewe ni mnyama?”Aliongea kwa mshangao.
Ijapokuwa uwezo wake wa kijini haukuwa mkubwa sana lakini sumu ya wadudu hao ilikuwa na uwezo wa kuua hata jini mwenye uwezo mkubwa kuliko yeye.
“Haha,.. ulidhani unaweza kunishinda na hawa kunguni wako?”
Baada ya kuona Roma anazidi kumshambulia na kanuni za anga palepale alizidisha kutuma wadudu wa rangi Tofauti tofatui ili kumpa muda.
Zihao mara baada ya kuona tukio lile aliona kabisa hapa kuna uwezekano wa miungu kuja na kumshambulia hivyo aliona ni muhimu kukamilisha pambano mapema au pengine akimbie.
“Sumu ya Spider elfu moja”Aliongea na palepale nguvu zake za kijini zilibadilika na kutengeneza wadudu wa rangi ya Spider ambao walikuwa wakivuma kiasi cha kuumiza masikio na walikuwa wakubwa mno saizi ya kiganja cha mkono.
Roma hakutaka kujisumbua kujilinda na wadudu hao kutokana na kujua sumu yao haiwezi kumuathiri lakini palepale wale Spider walilipuka kama bomu mbele yake .
“Pumbavu kabisa ulikuwa mtego”Aliongea Roma kwa hasira mara baada ya mlipuko ule kumrudisha nyuma sana mbali na Zihao na muda huu wote walikuwa wanashambuliana wakie eneo la nje na Jamali alikuwa amehamia yeye na Zhang Ru aliepoteza fahamu kwenye boti.
“Nitaondoka na Sarirah , tutaonana siku nyingine”Aliongea Zihao huku akicheka mara baada ya kuona mpango wake umefanikiwa.
Roma palepale alijua kama atamuacha amtoroke na akaficha uwezo wake wa kijini basi itakuwa ngumu kumpata , isitoshe alikuwa amepitia mengi mpaka kuja hapo kwa ajili ya kutafuta kitu ambacho kitaweza kuishinda nguvu ya roho ya mnyama iliokuwa ndani yake , mnyama wa maafa hivyo Roma hakuwa tayari kuona moyo wa Kibuddha ukiondoka kwenye upeo wa macho yake.
Roma palepale hasira zilimvaa na macho yake yalianza kubadilika rangi kama taa ya umeme.
“Unapata wapi ujasiri wa kutaka kuniibia, mtu yoyote ambaye anataka kuiba kitu changu lazima afe”Aliongea Roma kwa nguvu na palepale aliachia uwezo wake wa kijini.
Alijiambia inamaana gani kuua watu zaidi ya elfu moja kama tu anashindwa kumzuia mtu mmoja.
Dakika ileile kufumba na kufumbua nguvu zake zilibadilika na kuungana na nguvu ya andiko la urejesho huku nguvu ya chungu ikianza kufurukuta ndani yake.
“Wewe mpuuzi nitadili na wewe mara baada ya kuipata Sairra”Aliongea Roma kimoyo moyo.
Roma alitumia kiwango cha hasira zake na nguvu ya Divine Light na palepale akaweza kufanikisha kutawala nguvu zake za kijini.
“Simama hapo hapo”Aliongea Roma na kufumba na kufumbua alikuwa ashampita Zihao ambaye alikuwa akikimbia.
Zihao aligeuka upande mwingine kutaka kukimbia huku akipatwa na hofu kubwa sana lakini Roma alitoa tabasamu la kifedhuli na palepale Roma alibadilisha nguvu zake za kijini na kuwa kama mkono na kumshikilia Zihao.
 
SEHEMU YA 677.
Master Zihao alitumia kila aina ya mbinu ili kuchoropoka lakni nguvu yake ya kijini ilikuwa ndogo mno kulinganisha na ya Roma na alijikuta damu nyingi zilianza kumtoka kwenye midomo yake na aligeuka na kumwangalia Roma kwa hofu kubwa.
“Una nguvu za kijini? … hapana ,, haiwezekani , nguvu zako za kijini naona kabisa ni mwisho wa kukamilisha mzunguko wa kutawala elementi za maji?”Aliongea Master Zihao kwa mshangao mkubwa.
Kwa uelewa wa Zihao ni kwamba radi ya mapigo tisa kwasababu ni hadithi tu basi aliamini pengine Roma atakuwa katila levo mwishoni mwa kufanikisha kutawala maji.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba kutokana na ugumu wa kuipita levo ya Dhiki , yaani kufanikisha kupitia mapigo tisa ya radi majini wengi wana mbinu nyingine ya mkato ambayo huiita levo ya kuiepuka Dhiki , kwa mfano wakishafikia mwishonni mwa levo ya nafsi huanza kujifunza mbinu za kutawala elemeti za maji na moto kwa njia nyingine.
Ni rahisi jini au mtu ambaye yupo kwenye levo ya kuipita Dhiki kutawala nguvu ya moto na maji na hii ni kutokana ile radi inawaongezea nguvu nyingi sana za kijini lakini kwa mtu wa levo ya Nafsi basi anachokifanya ni kukusanya nguvu nyingi za kijini ili kuweza kutawala moto na maji jambo ambalo hutumia jitihada kubwa sana kuliko yule ambaye amepitia mapigo ya radi.
Sasa kwa upande wa Roma ukishaivuka levo ya Dhiki kinachofuatia baada ya hapo ni kujikusanyia nguvu kubwa sana kwa kupitia mapigo zaidi na zaidi ya radi, kwa mfano yataanza mapigo tisa na kisha yataenda mapigo tisini na tisa na kuendelea kwa mfumo wa kinamba hivyo hivyo mpaka mwisho.
Hivyo Roma nguvu yake sio ya mapigo tisa ya radi bali nguvu yake ilikuwa ni ya mapigo tisini na tisa ya radi hivyo alikuwa na uwezo wa juu sana.
Sasa hapo ukijumlisha nguvu ya andiko , nguvu ya roho ya mnyama wa maafa inatengeneza mzunguko kamili wa levo ya kuipita dhiki ya mapigo tisini na tisa ya radi ambayo ni sawa na cheo cha Master ndani ya ulimwengu wa kijini.
Sasa kutokana na Roma kutokuwa na uwezo wa kutawala nguvu zake zote za kijini , uwezo aliosambaza unafanana na ule wa levo ya nafsi ya jini au mtu mwenye uwezo wa kutawala elementi za maji bila kuipita dhiki yaani mtu aliepita levo ya kuiepuka dhiki na ndio maana Zihao alimhisia hivyo levo yake.
Roma hakujisumbbua kabisa kumjibu zihao kwani kadri muda ulivyokuwa ukisogea ni kama uwezo wake ukishuka kutokana na roho ya mnyama pia ilikuwa ikipambana kuuteka uwezo wake wa kijini hivyo alitaka kummaliza palepale.
Roma palepale mara baada ya kiona muda wowote akili yake inaweza kumezwa alifanya haraka sana na kukishikilia kile kiboksi chenye moyo wa kibuddha ndani yake na kukivutia kwake na dakika ileile kilipasuka vipande vipande na kufanya ule moyo kuelea angani mbele ya Roma huku ukitoa mng’ao wa rangi nyekundu.
Baada ya nguvu yake halisi kumfikia Roma nguvu ya roho ya mnyama ilianza kufurukuta zaidi kwa hasira kana kwamba inahofia Roma atatumia uwezo wote wa moyo huo na kumshinda.
Roma uwezo wake wa kifikra palepale uliimarika mara baada ya kuanza kutumia uwezo wake wa kijini , na alifurahishwa na nguvu kubwa ya Sairira na kilichomshangaza Roma ni kwamba moyo ule ulikuwa na nguvu ya kijini kubwa mno, ilikuwa ni kama kifaa ambacho kimehifadhia nguvu ya majini na alithibitisha hilo mara baada ya kuona ile rangi yake ya dhahabu imebadilika kabisa na kuwa kitu kingine, ni kama vile kaa la moto.
Dakika ileile swali liliibuka katika kichwa cha Roma na kujiuliza kifaa hicho anatumiaje sasa?.
Roma mara baada ya kuona Zihao alikuwa akitetemeka aliona kabisa hata yeye pengine hatokuwa na uwezo wa kujua namna kinavyotumika hivyo Roma palepale alishikilia ile dhana na kisha akapanua mdomo wake na kuimeza.
Ijapokuwa kilikuwa kikubwa sana lakini Roma alitumia nguvu ya kijini kupanua njia na kilifanikiwa kupita , mwanzoni Roma hakuweza kuhisia chochote lakini mara baada ya moyo ule kutua tumboni alichaneli nguvu ya andiko la urejesho kwenda tumboni na kuanza kunyonya nguvu yake na palepale kitu cha kushangaza kilitokea.
Nguvu ya andiko la urejesho ilikuwa kama daraja kupitisha nguvu ya kijini iliokuwa ndani ya ule moyo kwenda kwenye mwili wake na kufanya uwezo wake kuongezeka maradufu , Roma alijihisi ni kama nafsi yake iliokuwa imempotea imeanza kumrudia na ndani ya dakika chache ile hali ya roho ya mnyama kufurukuta ndani yake ilipotea kabisa kwa kuzidiwa na nguvu ya sarira.
Roma alijikuta akitoa pumzi nzito ya ushindi na alijiambia kumbe Monk na wenyewe kuna muda wana manufaa , maana kwa maelezo ni kwamba inasemekena nguvu ya kijini iliokuwa imewekwa kwenye moyo huo ni ya Monk ambaye alijifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi na kabla ya kifo chake ndio alihifadhi nguvu yake kwenye huo moyo.
Unapaswa kuelewa kwamba ijapokuwa majini wanaishi muda mrefu lakini vilevile wanakufa baada ya muda flani na hilo lipo pia kwa inadamu ambao wanajifunza mbinu za kijini hata wanapofikisha levo za juu hawatoishi muda mrefu kabla ya kufa.
Kwa maneno marahisi ni kwamba mpaka leo hii hakuna kiumbe chochote duniani ambacho kimefanikiwa kukishinda kifo na kwa majini wenyewe licha ya baadhi yao kuwa na nguvu kubwa za kijini lakini nguvu zile huwezi kumrithisha mtu.
Yaani kwa mfano jini kwa hiari yake haliwezi kumrithisha mtoto wake kuwa katika levo ya kuipita dhiki na ndio maana kadri siku zilivyosonga majini yanapoteza ule uwezo wao kwa sababu wale Master ambao ni kama mhimili wa nguvu zao hupoteza maisha na nguvu zao pia hupotea na hata kama ikitokea dhana kama moyo huo wa Kibuddha na wakahifadhi nguvu zao za kijini hakuna jini lolote ambalo lishafanikiwa kutumia nguvu yake kutokana na kwamba wanakosa mbinu ya Andiko la urejesho , mbinu ambayo ndio msingi wa kutumia nishati ya mwingine kwa kuigeuza na kuwa yako na ndio Roma mbinu aliokuwa akitumia.
Sasa Roma alijikuta akihema kwa furaha sasa maana alikuwa akitumia nguvu yake ya kijini bila ya kuwa na wasiwasi ya chungu kutawala akili yake tena.
Roma palepale alikunja ngumi yake kwa nguvu na kisha alianza kunyonya nguvu ya roho ya mnyama na kuingiza katika himaya yake na kubadilika na kuwa nguvu hio kutoka nguvu ya kipepepo na kuwa nguvu ya andiko la urejesho isio na kikomo.
Mpaka Roma anamaliza kuipunguza nguvu ya roho ya mnyama alijikuta akipatwa na hali ambayo ni kama vile dunia yote ipo chini yake , yaani kila alipokuwa akinyonya ni kama vile akili yake inatoboa zaidi kwenda angani.
Ndio, kadri unavyopanda levo za kijini uwezo wa kufikiri unakuwa sio flat(tambarare) bali hunyanyuka na kutengeneza mlima ni kama vile helicopter inavyopanda hewani ndio ambavyo Roma alikuwa akijisikia , yaani akili yake inapanuka zaidi na zaidi na kwa wakati huo Roma ssa kila kitu ni kama alikuwa akikiangalia kwa chini hii ndio inaitwa sasa kutoboa mbingu.
Sasa ijapokuwa dhana ya Chaos Cauldron ilikuwa na nguvu lakini ilikuwa ni kama mnyama ambaye amefungwa kamba, Roma alikuwa na uwezo hata wa kuiacha hio dhana lakini aliona kwasababu haina athari yoyote kwake aliona ataitumia kama ATM ya kujiongezea nguvu.
Kutokana na tukio hilo Roma aliona pengine anapswa kukusanya dhana nyingi nyingi na kisha angezimeza na kujiongezea nguvu zaidi na zaidi.
Baada ya kuingiwa na furaha ya mafanikio Roma sasa alianza kujihisi kuwa katika hali ya majigambo bila hata ya kupenda maana ndio side effect (athari)ya nguvu za kijini.
Upande wa Zihao alikuwa katika hali ya hofu mno , alikuwa ameshikiliwa na nguvu ya kijini hivyo hakuwa na uwezo wa kuchoropka , ijapokuwa alikuwa akiamini Sarira ni kitu cha thamani kubwa lakini hakujua kwanini Roma aliimeza , mpango wake ni kuiba na kisha kwenda kuifanyia utafiti namna ya kutumia nguvu yake lakini sasa alishapoteza dhana hio muhimu hivyo ambacho alikuwa akiwaza ni kutoroka tu ndani ya eneo hilo akiwa hai kwani alishindwa kumjua Roma ni nani haswa mpaka kuwa na uwezo mkubwa.
“Unauwezo mkubwa sana uliovuka vizuizi vyote Master , naomba unisamehe kwa kuwa mjinga , tafadhari naomba uniachilie niende”Aliongea Zihao akijaribu kumsifia Roma ili tu asamehewe.
“Jibu maswali yangu yote kwanza bila kunidanganya na nitafikiria kama nitakuacha hai au nikuue”Aliongea Roma.
“Tafadhari uliza?”
Zihao kwa wakati huo alijiambbia ni kheri kujibu kila kitu kwa ukweli wote ili mradi tu aweze kuachwa hai.
“Wewe ni nani , unatokea wapi , kwanini wewe ndio kiongozi wa umoja wa North Bueyeo , kwanini uliiba Sarira na pia umetumia mbinu gani kuficha uwezo wako wa kijini?”Aliuliza Roma aswali mfululizo
“Master Jina langu halisi nafahamika kama Master Insect , Zihao ni jina feki tu , mimi ni jini daraja la tatu kutoka Hongmeng , miaka miamoja iliopita nilikuwa mjumbe kutoka Hongmeng wakati nilipokuwa nikisafiri katika maeneo ya China nilipata Dhana ya kimababu kutoka mlima wa Kunlun, ni siraha ambayo niliipa jina la Jani la Upofu, hii Dhana ina uwezo wa kumfanya mtu yoyote au jini mwenye nguvu ya kijini kuificha na kuonekana kama binadamu wa kawaida na sio hivyo tu inaweza pia kubadilisha muonekano wa mtu na kuwa mtu mwingine kabisa , hata watu ambao wana nguvu kubwa ya kijini hawawezi kunigundua kwa namna yoyote ile na hapo ndio nilipotoroka ulimwengu wa kijini na kuja kuishi katika dunia ya kawaida nje ya China”
Roma mara baada ya kumsikia ni kama alishajua a anachomaanisha , Roma alikuwa akijua kwamba huku dunia ya kawaida kuna maliasili nyingi ambazo ni muhimu kwa majini kuliko hata katika ulimwengu wao.
Master Zihao anasema mara baada ya kutoka katika ulimwengu wa kijini alikuja kufika nchini Korea na hapo ndipo alipokutana na kuongizi wa umoja wa North Buyeo ambaye alimpa koneksheni ya kutembelea pande za dunia na kuanza kukusanya maliasili nyingi sana kutumia nguvu yake.
Anasema alitumia zaidi ya miaka mia moja kupanua umoja wa North Buyeo huku akimtumia kiongozi kama vile ni puppet tu katika kujitambulisha lakini yeye ndio mwenye nguvu , na alitembea kila kona ya dunia na kukusanya pesa pamoja na kuiba vinavyowezekana.
Anasema kupitia North Buyeo aliweza kutumia njia mkato ya mafunzo na kufanikiwa kupita levo ya kuiepuka Dhiki na kufanikisha kutawala moto wa rangi ya njano lakini ilionekana kuwa ngumu kwake kupanda levo zaidi kama wale ambao wamepitia Dhiki.
Kitu alichohitaji ilikuwa ni moyo wa Kibuddha , ijapokuwa alikuwa mjuzi kwenye kuroga na kutupia laana alikuwa pia ni muumini wa dini ya Kibuddha hivyo shauku yake ya kutaka kutumia nguvu ya kibuddha kupanda levo zaidi ilimvaa na hapo ndipo alipotaka kuiba Sarira ili kuifanyia tafiti na kisha kutumia nguvu yake.
Na ndio kwa bahati mbaya Roma ambaye alihitaji Sarira ndio aliharibu mpango wake.
“Kwahio kwa manneo yako umekusanya utajiri mwingi kwa miaka yote hio si ndio?”Aliuliza Roma mara baada ya kusikia maneno yake na Jini Master Insect au Master Wadudu alionekana kuelewa swali la Roma.
“Ndio Master , Nina hazina kubwa sana , kama unaitaka nitakuruhusu uichukue lakini uniahidi hutoniua”
“Unaonekana unauelewa mkubwa , sasa ninachotaka pia sio hazina tu nataka na hio Dhana ya Jani la Upofu na baada ya hapo nipatie orodha ya wanachama wote wa umoja wa North Buyeo …kingine kwasas nadhani sijafikiria zaidi nipe kwanza hivyo”
Master Wadudu kidogo tu atoe kilio alitaka kumpa Roma kila kitu lakini alionekana kutaka kuchukua hata kile ambacho ni muhimu zadii kwake
Lakini hata hivyo Master Wadudu aliona ni kheri kuishi kuliko kung’ang’ania mali , ijapokuwa ingekuwa ngumu kwake kuficha uwezo wake wa kijini bila ya kuwa na Janni la Upofu alichopaswa kufanya ni kujizuia kutotomia uwezo wake wa kijini kwa namna yoyote ile isitoshe mapambano yao yalionekana kutovuta ‘attention’ ya miungu mingine au majini.
Upande wa Roma aliamini akipata jani hilo la upofu basi itakuwa ni kama Dhana aliopoteza Hades wa zamani inafyofahamika kama Helmet of invicibility.
Kama ilivyokuwa jina lake , dhana hio ilikuwa ikifanana na jani pana la mti lakini lenyewe sio jani kama jani bali ni kifaa kilichotengenezwa kwa madini ya Dhababu kinachofanana na jani, ijapokuwa ilikuwa ni dhana ya daraja la kati ya kijini lakini uwezo wake ulikuwa mkubwa sana
Kwa namna yoyote ile namna utakavyoibeba dhana hio kwa mfano kwa kupitia njia ya pete ya kijini au kuiweka mfukoni ingefanya jini lolote au mtu mwenye nguvu za kijini uwezo wake kutokuonekana na kuwa binadamu wa kawaida tu kama Selemani(Jokes).
Kitu kilichomfanya Roma kufurahi ni kwamba jani hilo la upofu lilikuwa na uwezo wa kuwachanganya wengine na kuwafanya waone uwezo wake wa kijini ni mdogo, kwa mfano anaweza kupunguza uwezo wa kijini anaosambaza na kufikia levo ya nafsi hivyo aliona atakuwa anayatega majini yatakayomshambulia kwa kujifanyisha yupo levo ya nafsi.
Roma palepale alijaribisha na kushusha uwezo wake wa kijini ili kuonekana kama vile ndio ameipita dhiki ya mapigo tisa ya radi kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa majini pepo na alionekana kuridhika na ufanisi wake.
Roma palepale alimfuata Jamali pasipo kumwachilia Master Wadudu na kisha akamponyesha kwa kutumia nguvu ya kijini na kutoa risasi kwenye mguu wake.
“Usikumbuke chochote kilichotokea leo hii hapa , ninaweza kukuokoa lakini vilevle ninaweza kukuua , chukua mateka na warudishe Korea , kuna kitu napaswa kufanya”Aliongea Roma.
Roma alipotezea muonekano wa Jamali, muonekano wa shukrani na kisha akampa maagizo Master Wadudu kumpeleka kwenda kuona hazina yake.
Kitendo cha Master Wadudu kupoteza jani lake la upofu palepale sura yake ilibadilika kabisa na akawa mzee sana na Roma alijiambia muonekano wake unamfiti sana na jina lake la Master Wadudu maana alikuwa akitisha.
Hazina ya Master Wadudu alikuwa ameijenga katika kisiwa kisichokaliwa na watu ndani ya Korea , lilikuwa eneo lake binafsi na ndani ya mlima wa kisiwa hicho ndio kulikuwa na hazina ya utajiri wake.
“Master hizi zote ndio maliasili nilizokusanya kwa miaka yote , hapa kuna mimea , kuna matunda , kuna chuma, maji ya chemchem , hivi ni vitu ambavyo nimetumia kuwalisha wadudu wangu na vyote vinavyobakia ni…”
Master Wadudu alianza kuelezea hazina yake yote na alitembea kuelekea ndani kabisa ya pango na kufungua mlango wa chuma cha Bronze kwa kutumia nguvu ya kijini, yaani ukiangalia kama vile hakuna mlango lakini mara baada ya kutumia nguvu ya kijini mlango ulionekana.
 
SEHEMU YA 678.
Ilikuwa rahisi sana kwa jini mwenye uwezo mkubwa kutengeneza pango , ukweli ni kwamba viumbe wenye uwezo mkubwa enzi hizo ndio walihusika zaidi katika kutengeneza mapango , dunia ya leo ina mapango mengi ambayo ujenzi wake aidha ulifahamika kuwa wa binadamu au mengine hayafahamiki kama ujenzi wake ulifanywa na binadamu kutokana na kukosa ushahidi.
Roma mara baada ya kuingia kwenye pango hili alijua kabisa kama mtu wa kawaida angekuja katika eneo hili angeshangazwa na angekosa ushahidi wa moja kwa moja kama pango hilo limetengenezwa na binadamu.
Roma kitendo cha kuingia ndani tu aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikitoka kwenye hilo pango na eneo lote lilikuwa limezingirwa na vifaa mbalimbali ikiwemo vitu kama vibuyu vilivyotengenezwa kwa madini ya Jade , kwenye chupa hizo kulikuwa na maji ya chemchemu.
Maji ya Chemchem pia ni maji ambayo ni mhimu sana kwa majini na ndio maji adimu sana duniani lakini ya thamani sana kwa majini.
Yaani baadhi ya vitu Rufi alivyomwelezea kwamba vinapatikana katika ulimwengu wa kijini , kwenye kona ya pango hilo kulikuwa kumesimamishwa chuma cha aina mbalimbali ikiwemo chuma kisichopata kutu(Frosty iron) na chumba ambacho ni kigumu(Fire iron) au kwa kiswahili sanifu tunaita chuma cha pua.
Utofauti wa aina ya chuma hicho ni mkubwa sana ni aina ya chuma adimu sana ambacho hutumika kutengenezea Dhana za kijini hivyo huwezi kupata katika dunia ya kawaida labda ujinini.
Kama Master Wadudu angekuwa na uwezo pamoja na kuwa na Chungu kama cha Roma basi angekuwa ashatengeneza dhana za ajabu mno.
Wakati Roma akiendelea kukagua mazingira aliweza kuona kitu kingine ambacho kilifanya macho yake kuchanua , pembeni kabisa kwenye kona kulikuwa na furushi la mifupa na kwa haraka haraka tu aliweza kugundua mifupa ile lazima itakuwa ya wanawake.
“Hio mifupa ni ya nini?”Aliuliza Roma.
“Master hio ni mifupa ya wanawake ambao niliwatumia kuwalisha wadudu wangu “
Roma alijikuta akikunja sura ashawahi sikia kuhusu majini ambayo hutumia mbinu ya kupanda levo kwa kutumia damu na nyama za binadamu.
Aina ya majini ambao hutumia mbinu hio walikuwa ni wa tofauti kabisa na wale ambao amekutana nao kawenye ulimwengu wa majini pepo, majini wazuri ndio wale ambao hushinda laana ya kipepo iliondani yao na wale majini wabaya ni wale ambao wanaipa laana nguvu hao ndio wale wa dunia ya kijini pepo.
Kuhusu majini wanaonyonya damu pamoja na nyama hawa ni aina ya majini ambao hupenda sana kujihusisha na walozi au wachawi na mara nyingi huua binadamu kichawi ili kutumia damu yao kuweza kujiongezea nguvu.
Sasa majini ni kheri kutoa utajiri wa dhahabu na pesa kuliko kukosa nguvu za kijini kwao kitu cha thamani ni nguvu ya kijini na sio pesa na ndio maana hutajirisha binadamu wenye tamaa ili mradi tu watakuwa na uwezo wa kuwahakikishia uwezo wa kupata damu na nyama huku wao wakiwapa utajiri.
“Master nataka kugundua mbinu nzuri ya mafunzo ya kijjini , hi mbinu nilipatiwa na Master wangu , ijapokuwa nataka kujifunza lakini kipindi hichi ni tofauti na miaka ya zamani kwani ni ngumu sana kutumia mbinu za kawaida kuingia hata levo ya nafsi , tafadhari namba uchukue kila kitu lakini uniachia uhai wangu”
“Nipatie majina ya viongozi wakubwa wa umoja wa North Buyeo”Aliongea na Master Wadudu alitingisha kichwa na palepale alitumia pete iliokuwa kidoleni na kilionekana kitabu kidogo kikijitokeza bila ya kueleweka kimetokea wapi.
“Kumbe na wewe unatumia pete kuhifadhi vitu , naamini utakuwa na vitu vizuri zaidi umeficha”Aliongea Roma huku akichukua kile kitabu.
Master Wadudu palepale alishikwa na wasiwasi mara baada ya siri yake kufichuka lakini kutokana na woga wake palepale alitoa ile pete na kumkabidhi Roma akitarajia amuache awe hai.
Roma alitumia uwezo wake kukagua ukubwa wa hifadhi ya pete hio na alikuja kugundua ukubwa wake ni mara mbili zaidi ya kwake na alifananisha na ukubwa wa hifadhi ya pete ya Sophia.
Ndio, Sophia wakati alipokuwa ulimwengu wa kijini Pepo alipewa Zawadi na Aoiline ya pete ya madini ya Dhahabu na Rubi ni pete ambayo ukimuona ameivaa utaona ni ya kirembo lakini ni ya kijini na hutumika katika kuhifadhia vitu kimazingara lakini wakati mmoja pia kumuongezea mvuto.
Ndani ya hifadhi ya Master wadudu katika pete hio kulikuwa na mimea adimu sana na Roma alifurahi na kujiambia angeitumia katika kutengenezea vidonge vingi tu vya daraja la juu ambayo hata ulimwengu wa kijini hawawezi kuwa navyo.
“Master nimekupatia kila kitu , je naweza kundoka sasa hivi , naapia siwezi kuwadhuru wengine tena na sitajitokeza mbele yako milele”
“Kabla ya kuondoka unapaswa kuacha kitu kimoja”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la kifedhuli.
“Nini?”Aliongea huku akianza kujisachi kama ana kitu kingine cha thamani lakini alikuja kugundua alikuwa na ushanga tu ndio amebakia nao.
“Namaanisha unatakiwa kuacha uhai wako hapa hapa”Aliongea Roma na kumfanya Master Wadudu kupiga kelele ya hofu.
“Master kwanini unaenda kinyume na ahdi yako , umesema ninachotakiwa kukupatia…”
“Mimi sio Master wala Shujaa , ninachojua mnafiki kama wewe na mtu mchawi hustahili kuendelea kuishi”Aliongea Roma na mpaka hapo Master Wadudu alijua kabisa alishajiingiza kwenye mtego wa Roma.
Alitaka kukimbia lakini Roma hakumpatia nafasi hio na katika hatua ya kupambania uhai wake palepale kucha za mikono yake zilianza kurefuka huku mwili wake ukianza kuzingirwa na moshi mwingi pamoja na upepo , alionekana alikuwa akitafuta mbinu ya kukimbia lakini Roma alitumia nguvu yake ya kijini akiunganisha na ile aliovuna kutoka kwa chungu na kuisharabu nguvu yote ya Master Wadudu.
“Nitakutafuta hata kama nitakuwa pepo …”
Kabla hajamaliza sentensi yake ya laana mwili wake palepale ulilipuka kama bomu na Roma hakutaka hata kumpa nafasi ya kuwa pepo kwani Roma alitumia nguvu ya Cauldron kuinyonya roho yake na ndio ukawa mwisho wake.
Nguvu yake yote ya kijini ilimwingia Roma palepale na iligeuzwa kuwa yake na nguvu ya andiko la urejesho.
Roma alishangazwa na jambo hilo , mwanzoni hakutaka hata kufnyonza nguvu yake lakini alishangaa nguvu yake ya kijini kufanya kazi kama sumaki na kunasa nguvu zote za Master Wadudu na kuzifanya kuwa za kwake.
Hio kwake ilimaanisha kwamba hakuhitaji tena chungu chake kutaka kufyoza nguvu za wengine. Lakini hata hivyo Roma aliamini pengine uwezo wa Master Wadudu ulikuwa mdogo sana kuliko wa kwake ndio maana umevutwa kirahisi na kubadilishwa kuwa wa kwake.
Roma mara baada ya kummaliza Master Wadudu palepale alianza kukusanya utajiri.
Ilionekana alikuwa amekusanya sana , ukiachana na madini ya dhahabu yaliokuwepo lakini pia kulikuwa na masanduku ya Dollar ambazo zilikuwa zimepangiliwa , ilionekana wakati akiwa kama kiongozi wa North Buyeo alikuwa akijikusanyia mali tu.
Roma alikaa chini kabisa na kuanza kuhesabu thamani ya utajiri kwa haraka haraka kijini na ndani ya lisaa limoja tu alikuwa ashamaliza na aliweza kukadiria utajiri wote wa Master Wadudu ni zaidi ya dollar za kimarekani bilioni moja.
Jambo hilo lilimfurahisha Roma kutokana na kwamba siku chache zilizopita alimpa maelekezo Ron kuuzia Tanzania mafuta nusu bei ambapo jumla ya gharama yake ni zaidi ya bilioni moja za kimarekani , hivyo ni kama amerudisha pale palipopungua.
Roma alijiambia hakika nguvu ya kutoa ni kubwa , ukitoa kidogo unapewa kikubwa zaidi, maana sio kwamba tu amepata utajiri bali alipata vitu vingi zaidi vya thamani.
Kwa Roma inaweza kuwa kama utani lakini katika ulimwengu wa kiroho nguvu ya kutoa ni kubwa mno , Asante ya Dhati katika ulimwengu wa kiroho bila kujali ni upande wa giza au wa nuru ni Akiba, ndio maana sadaka inayomfikia mhitaji moja kwa moja ina nguvu zaidi kuliko ile ambayo inamfikia mtu asie na uhitaji.
Kwa mfano kumpa sadaka mtu ambaye hana uhitaji sadaka yako haina maana kwasababu maana ya sadaka katika ulimwengu wa kiroho inatafutwa ile Asante ya Dhati na sio ile ya kinafiki , yaani sadaka inayoenda mahali sahihi haipotei bali hugeuzwa na kuwa kitu kingine, ndio maana katia dunia ya leo hata wale wahalifu na matajiri wanaotumia majini au mbinu zisizohalali kupata utajiri hutoa sadaka, kile kitendo hakifanyiki kumuonyesha mtu ana roho nzuri bali ni uwekezaji wa kupata mara mbili, japo wengine hawafanyi kama uwekezaji.
Roma aliangalia baadhi ya majina ya wanachama wa North Buyeo na alichoweza kuona ni majina ya watu hata asiowajua na familia ya Gong ambayo alikuwa akiishuku yenyewe haikuwa katika orodha.
Roma hakuwa na mpango wa kuwaua , alichotaka ni kujua kama kuna mtu wa karibu na Yezi na hakuona, hivyo kuhusu hao wengina alijua kwasababu kiongozi wao amekufa basi ni lazima watapambana wao kwa wao ili kugombea nafasi na ni maswala ya kiserikali ambayo hayakuwa yakimuhusu.
Roma aliangalia utajiri uliokuwa nyuma yake na alijikuta akitoa kicheko cha furaha na alianza kukusanya kila kitu na kuhifadhi kwa mbinu za kijini huku akikariri baadhi ya dhana ambazo hakuzijua ili kwenda kumuuliza Rufi.
Wakati akiendelea kuchangua changua baadhi ya vitu alikuja kukutana na tunda la rangi nyekundu kama damu ambalo lilikuwa limehifadhiwa kwenye chupa ya Jade.
Roma hakujua tunda lile maana yake ni nini na palepale alichukua kitabu ambacho kilikuwa kikielezea aina mbalimbali ya mimea na kusoma jina lake na alijikuta akitoa kicheko cha ushindi na palepale alilichukua na kulitupia kwenye hifadhi.
Roma hakuchunguza vitu vingine na aliendelea kutupia kwenye hifadhi ya pete mpaka alipohakikisha pango lote limekuwa tupu aliondoka na palepale alitumia nguvu za kijini kuharibu pango lile na palepale ni kama vile kumegonga radi na eneo lote la mlipa lilititia kwenda chini na kufanya maji kuanza kufunika lile eneo kama vile ni Tsunami na hakutaka kuangalia kitakachotokea zaidi ya kuondoka.
Hali ya hatari ndani ya jiji la Seoul ilikwisha kudhibitiwa na mabomu yote yaliweza kugunduliwa na vifaa vya teknolojia ya hali ya juu , ingekuwa ni Tanzania ingechukua muda lakini kwa Korea kusini taifa lililopiga hatua ilikuwa rahisi sana.
Kutokana na tukio hilo la kigaidi harusi iliopangwa kufanyikia ndani ya matempo hayo ya Jogyesa ilionekana kabisa hakuna dalili ya kufanyikia hapo.
Ni dakika chache tu Park Juan alikuwa akimaliza kuongea na simu na kwa kumwangalia tu ilionekan taarifa haikuwa nzuri , yaani alipewa maagizo ya harusi kutofanyikia katika eneo hilo.
“Sir nadhani hatuwezi kufanya chochote kwa sasa , isitoshe hakuna alietegemea hili kutokea , tunaweza kufanya sherehe hii siku nyingine tu”Aliongea Kim Yang.
“Ndio Babu hatuwezi kuharakisha na kubadilisha eneo la harusi isitoshe dharula imekwisha hivyo hivyo ndoa haitokuwa na baraka kufanyika kesho”Aliongea Yezi akipigilia msumari , aliona atumie nafasi hio ndoa hio kughairishwa.
Upande mwingine Kim Jip wala hakuonyesha mabadiliko yoyote alikuwa ametulia kama vile hakuna kilichotokea.
Park Juan mara baada ya kuona furaha ya Yezi aliweza kukumbuka kitu na palepale aling’ata meno yake kwa hasira.
“Hapana , tushaalika watu tayari na maandalizi yamekamilika , kesho ni siku nzuri pia hivyo ndoa itafanyika kama ilivyopangwa”Aliongea
Watu wote walishangaa lakini hata hivyo hakuna ambaye alimshangaa kuongea hivyo isitoshe walikuwa wakimjua kwa kuwa na isimamo.
“Babu kwanini una haraka ya kutaka niolewe , kwanza simpendi huyo Kim Jip mimi”Aliongea Yezi.
“Kimya!, kwanini unaongea hivyo hapa”
“Nadhani haishangazi kwa Yezi kutompenda Kim Jip , ni sawa tu , isitoshe ndoa nyingi katika familia kama za kwetu, ndoa ni kwa ajili ya sitara tu”
“Yezi unapaswa kushukuru familia ya wakwe zako ni waungwana , utaelewa nini wajibu wako kama mrithi wangu wewe?”Aliongea Babu yake.
“Ninawachukia sana”Aliongea kwa hasira na kisha akakakimbilia juu huku Eujung akimfatilia kwa nyuma akionyesha wasiwasi.
Kim Jip ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kuangalia upande wa ngazi na macho yake yalionyesha hali flani isiokuwa ikielezeka.
“Baba kwasababu hatuwezi kutumia Jogyesa , nitafute eneo lingine?”aliuliza Park Jiyeon mtoto wa kike wa Mzee Park.
Tokea tukio la Park Jonghyun litokee familia yote ilikuwa imeshika adabu na hakuna alieleta kiburi mbele ya baba yao, ijapokuwa hawakuridhika na maamuzi ya kumchagua Yezi kama mrithi lakini hakuna ambaye aliongea neno.
“Wasiliana na wageni wote na waambia sherehe itafanyikia katika ukumbi wa hoteli yetu ya Starmoon, hamisha kila kitu na hakikisha maandalizi yanafanikiwa usiku huu huu”Aliongea na Park Jiyeon aliitikia na palepale waliondoa na mume wake kwa ajili ya kufanya maandalizi.
Juu chumbani kwa Yezi alikuwa akionyesha hasira zake waziwazi kwa kupiga piga kitanda na mito , Eujung aliishia kusimama kwenye mlango huku akimwangalia Yezi tu bila ya kuongea chochote , isitoshe ashajua hata kama akiongea asingemsikiliza.
Dakika ileile Yezi alifunga nywele zake vizuri na kisha akasogelea simu yake .
“Miss , unampigia nani?”
“Nampigia Bro Roma nione kama amerudi , nataka anitoe hapa nimechoka”Aliongea .
******
Upande mwingine tokea tukio litokee Clark alikuwa amekaa kwenye hoteli katika balkon akiwa ameshikilia kishikwambi chake , alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu akimsubiria Roma , kuna hata wanaume wa Kikorea waliionyesha ishara za kumchombeza lakini hakuwa na habari nao.
Clark hakuwa na wasiwasi na usalama wa Roma kwani alikuwa akimjua tokea alipokuwa mdogo na aliamini angeweza kushinda kila gumu lililopo mbele yake.
Wakati akiendelea kuachama kwa njaa hatiimae mtu alitokeza mbele yake hewani na kutua mbele yake na baada ya kuangalia vizuri alikuwa ni Roma.
“Roma!!”
Dakika ileile aliweza kuhisia mabadiliko ya Roma , aliona kitu tofauti kabisa kutokana na muonekano wake.
“Babe umeponyesha uwezo wako na umerudi!!?”aliongea kwa kuhamaki na kumfanya Roma kucheka na kisha kumbusu mdomoni.
“I gained a lot this time , Honey it was a blessing in disguise , I think God really likes me”Aliongea Roma akimaannisha kwamba amepata vingi awamu hio na kusema pengine ilikuwa ni baraka iliojificha na anadhani Mungu anampenda sana.
“Haraka niambie nini kimetokea”Aliongea Clark kwa furaha.
Roma hakuwa na haja ya kumficha kwani ndio aliehusika na mafanikio hayo na kumfanya Clark kuwa katika hali ya mshangao.
“Yule Zihao ,,, namaanisha Master Wadudu ni mzuri kwenye kuigiza aisee”
“Ni kwasababu ya dhana yake ya Jani la Upofu , kwasasa naweza kutumia hii dhana kuficha uwezo wangu , ninaweza pia kubadilisha muonekano wangu ninavyotaka”
Muda ambao Roma alitaka kuongea simu yake ilianza kuita na alipokea palepale mara baada ya kugundua inatokea kwa Yezi.
“Yezi nini tatizo”Aliuliza Roma.
“Bro ,,, uko sawa?”
“Ndio niko sawa”Alijibu Roma huku akitoa tabasamu baada ya kuona Yezi alikuwa akimjali licha ya kumpotezea ile asubuhi.
“Nimefurahi kusikia hivyo , lakini naomba uje unitoa huku , mimi sitaki kuolewa na Kim Jip , babu amesema anabadilisha ukumbi na ndoa inapaswa kufanyika kama ilivyopangwa , mimi kweli sitaki kuolewa nae jamanii..”
“Yezi mimi ni mtu wa nje tu ya familia na siwezi kuingilia , ijapokuwa nakujali lakini hio ni familia yako , babu yako hawezi kufanya maamuzi ambayo yatakuathiri , anachofanya ni kuhakikisha unakuwa na kila kitu chake , hebu jaribu kuzingatia na hisia zake pia , jitahidi kumfahamu Kim Jip sio mtu mbaya na utatokea kumpenda”
“Mimi sitaki kusikia hivyo , kwanini kila mtu hanielewei , Roma nakuchukia sana na wewe”
Upande wa pili Yezi alitupia simu chini na ikapasuka pasuka
“Una uhakika hutojutia , hata kama hutaki kuzipokea hisia zkae lakini hupaswi kumlazimisha kuolewa na mtu asiempenda”Aliongea Clark
“Ukweli ni kwamba sijui kama hisia za Yezi juu yangu ni za kweli , knna muda anaonekana kama mtoto na kuna muda anaonekana kama mtu mzima , itakuwaje hapo baadae kama akishakuwa na akili za kiutu uzima akija kugundua maamuzi alioyafanya yalikuwa ya kimhemko , atanilaumu sana kwa kubadilisha maiiha yake , wakati nilipoanzisha mahusiano na Sophia , Edna aliniambia mimi ni zaidi ya mnyama na niliona yupo sahihi kabisa … sidhani ni hatia ya namna gani itanipaa kama nikifanya hivyo pia kwa Yezi”
“Mwisho wa siku bado unajali hisia za Edna licha ya kwamba ndoa yenu ipo ukingoni na huachi kumuwazia , inasikitisha sana”
“Hapana sio hivyo , yaani nashindwa kujiondoa na hatia , muda mwingine najiuliza mtu kama mimi nilifanikisha vipi kuuteka moyo wako , kuwa na mahusiano na mimi ni hatari pia kwani nina maadui ambao wengine wanaonekana na wengine hawaonekani , kumjumuisha na Yezi ni kumuweka katika hatari … hiki ni kitabu ambacho nimekipata kutoka kwa kiongizi wa North Buyeo na hakuna mwanafamilia yoyote ambaye ni mwachachama , hivyo ijapokuwa najua kabisa hampendi Kim Jip ila sitaki kuzuia ndoa yao , najua kabisa atakuja kuwa na maisha ya amani”
Clark ijapokuwa alimuonea huruma Yezi lakini hakutaka kumlizimisha kutoka kimapenzi na Yezi na aliishia kumkumbatia na kisha walipandisha juu kwenda kuona chumbani kwao kwend akuona ni vitu vya aina gani Roma alipata.
“Clark wewe hebu tangulia kwanza kwenda chumbani , nataka kurudi Tanzania kumuuliza Rufi baadhi ya kitu nilichokipata ili anithibitishie , nitarudi nikimaliza”Aliongea Roma mara baada ya kufika mlangoni
 
Back
Top Bottom