SEHEMU YA 64
Mzee Alex pamoja na wafanya biashara wengine waliokuwepo eneo la maegesho , walikuwa kwenye mshangao mkubwa sana , ni kama macho yao yaliku yakiwadanganya kwa kile walichokuwa wakikiona mbele yao , mtu ambaye dakika chache nyuma walimshuhudia kupigwa risasi alikuwa amembeba Seif begani , kwanini wasishangae.
“Jamani si tumeshudia akipigwa risasi huyu, au haikumpata?”Aliuliza mwanamama mmoja mnene aliekuwa ameshikilia simu yake kubwa ya I phone akiongea na mwanaume aliekuwa pembeni yake.
“Ni yeye si unaona shati limechafuka kwa damu , lakini inanishangaza kuona ni mzima”Alijibu mzee huyu.
Abuu alishindwa hata kuongea neno lolote Zaidi ya kumwangalia Roma anaemwingiza Seif kwenye gari , lakini muda huo huo Diego akiwa ameambatana na wazungu sita , wanajeshi wa Kikosi cha The Eagles waliingia ndani ya hili eneo na kumsogelea Roma.
“Sire!” Aliita Diego kwa mshangao mara baada ya kumuona Afshar kwenye gari.
“Diego nadhani mnataarifa za huyu muuaji?”
“Ndio Sir”
“Basi nadhani mnajua cha kufanya , mchukueni mpaka kambini , nitakuja kumhoji mimi mwenyewe .nikishamfikisha mke wangu nyumbani”
Aliongea na Diego alionekana kuelewa na haraka sana alimpa ishara Chiara na John kuondoka na Seif , huku na wao wakianza kuondoka eneo la hoteli hii , hawakutaka kukutwa na polisi ambao walikuwa njiani kufika eneo la tukio kwa kuchelewa.
Kila kilichokuwa kimetokea dakika kadhaa nyuma kilionekana kuwa kama muvi kwa macho ya watu wengi,waliokuwa wameshuhudia tukio hili kwanzia mwanzo mpaka mwisho.
Baada ya Roma kutoa maagizo , alimshika Edna mkono ambaye muda wote alikuwa akimwangalia Mume wake kama kiumbe ambacho ndio kwanza anakutana nacho leo kwa mara ya kwanza.
Edna alikuwa ni kama haelewi kile kinachoendelea na alimuona Roma kama mgeni kwenye macho yake , licha ya kwamba mrembo huyu alikuwa akijua Roma hakuwa wa kawaida , lakini hakudhania kama atakuwa ni Zaidi ya ule ukawaida aliokuwa akiujua,kwani kila siku alikuwa akishangazwa na jambo jipya kuhusu Roma.
Neema Luwazo na yeye alikuwa kwenye mshangao , alikuwa haelewi, kinachoendelea , licha ya kwamba tukio lote lilitokea kwenye majengo yake ya kampuni , lakini ni kama alikosa nguvu ya kutoa maagizo , kwani muda wote alikuwa ni mwenye kunyamaza na kuangalia kile kinachoendelea , mwanamama huyu alikuwa kwenye mshangao mkubwa.
“Abu tunatakiwa kufanya nini kwenye hali kama hii?””Aliuliza Mzee Alex aliekuwa ni kama haamini kinachoendelea na kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake , alikosa maamuzi ya hapokwa hapo , na ni mara ya kwanza pia kumuuliza kijana wake ni jambo gani linatakiwa kufanyika kwa wakati huo , lakini kwa Abuu alikuwa ni kama baba yake tu , kwani wote hawakujua ni hatua gani za kufuatwa kwa wakati huo.
“Baba hii ni hatari wakimhoji Seif na kututaja kama wahusika wa mpango mzima”Aliongea Abu na hapa ni kama alikuwa ameshituka.
“Mpigie Kigombola”Aliamrisha Mzee Alex huku akisogelea gari yake na kijana wake alimfungulia mlango , huku Abuu akiangalia Roll Royce ,gari alilopanda Edna na Roma likitokomea kwenye macho yake.
“Fu****ck!”Abuu alijikuta akigongagonga kioo cha gari yake kwa hasira , huku baadhi ya watu wakimshangaa , lakini sasa wakati hayo yanaendelea Azizi Mohamed alikuwa ndani ya maeneo hayo , na haikueleweka alikuwa wapi , kwani ndio kwanza alikuwa akitokeza kwenye mlango wa kutokea ndani ya jengo hili la Hoteli.
“Kuna nini kimetokea?”Aliuliza tajiri Azizi na kijana wake alievalia suti alimweleza kwa sauti ya chini na Mzee huyu aliachia cheko , lililofanya baadhi ya watu wamwangalie , lakini kama ilivyokuwa sifa yake , hakujali , alitembea kulisogelea gari yake na kuingia.
“Hii habari itamfurahisha Rafiki yangu Jeremy.. hahahaha”Huyu mzee Tajiri alionekana kufurahishwa sana na tukio hilo.
“Bosi!”Aliuliza Dereva baada ya kumuona bossi wake anacheka pasipo kuelewa ni nini kimchekeshacho.
“Hahahahaha ..Nipeleke nyumbani Sadiki nikalale mie”Aliongea mzee huyu na kisha Sadiki alitoa gari hio ya kifahari aina ya Range na kutoka nje ya hoteli hio.
Upande mwingine Mage na Magdalena walishuhudia tukio lote la Roma kutoka akiwa na Seif,Kwa Magdalena kwake ilikuwa ni afadhari kwani alikuwa mwanaeshi , ila kwa pacha mwenzake Mage hali ilikuwa mbaya.
“Magdalena mbona ni kama sielewi kinachoendelea , naielezeaje hii hali?”Aliongea Mage mwanadada huyu ,masikini alionekana kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja , hakuwa akielewa tukio zima lilivyotokea na mpaka kuisha.
“Usiumize kichwa sana Mage, Mume wa Edna sio wa kawaida”.
“Unamaanisha nini Magdalena?, sio wa kawaida kivipi?, mbona unaonekana kuna jambo unalijua unanificha”
“Siwezi kukuambia lolote Mage, ila jua sio mtu wa kawaida ,nimemsikia siku moja akisema wewe ni moja ya Askari wanaomchukia kwenye taifa hii , ila Mage nikwambie tu jitahidi kukaa nae mbali”Aliongea Magdalena wakati wakiwa kwenye Gari na kuzidi kumchanganya sana Mage.
“Mtu sio wa kawaida halafu nikae nae mbali , mimi ndio Mage , lazima nijue kila kitu , nitaanza kumfatilia kimya kimya” Aliwaza Mage , hakutaka kumuuliza sana dada yake maana alijua tabia yake ya kutotaka kuongea mara kwa mara hasa maswala ambayo yalikuwa yakihusu kazi yake.
Edna alionekana kuegamia kiti cha gari , huku akionekana kuwa na mawazo mengi kwa wakati mmoja , hakutaka kuongea chochote na Roma na hata Roma mwenyewe hakuwa akielewa mke wake alikuwa akifikiria nini na ndio maana hakutaka kumuuliza , aliendesha gari kimya kimta kuelekea nyumbani.
“Anaonekana kuwa na mshituko na najua ana maswali mengi , lakini siwezi kuanza mimi kumueleza , ila siku akitaka kujua historia yangu ya maisha yangu ya nyuma nitamueleza kila kitu”Aliwaza Roma wakati akiingia daraja la Kigamboni.
Edna aliekuwa ameegamia kwenye kiti alikuwa pia akiwaza kama alichokuwa akiwaza Roma.
“Sio kama nilivyomfikiria ,Anaonekana kuwa na historia kubwa sana kwenye maisha yake , lakini sitomuuliza mpaka atakaponiambia mwenyewe”Aliwaza Edna katika kichwa chake.
Wanandoa hawa walionekana kuwa na mawazo yanayotofautiana , Roma alikuwa akiwaza kumuambia Edna kila kitu kama tu ataamua kumuuliza,lakini wakati huo Edna anawaza pia kutomuuliza Roma chochote kuhusu maisha yake ya nyuma mpaka atakapomuambia mwenyewe.
Muda mchache mbele walifika nyumbani na Roma aliekuwa na shati lililokuwa na damu alitoka , huku Edna akiwa wa kwanza , alibeba mkoba wake mrembo huyu na kisha akakimbilia ndani na kumfanya Roma asimame amwangalie Edna, alishindwa kuelewa ni nini Edna anawaza kwa wakati huo.
“Mr Roma nini kimekukuta?”Aliuliza Bi wema kwa wasiwasi mkubwa baada ya kumuona Roma mgongo wake kutapakaa damu.
“Bi Wema kuna tatizo limetokea ila nitakueleza vizuri kesho , kuna mahali nataka kwenda , kuwa karibu na Edna anaonekana kuwa kwenye hali ambayo sio nzuri”Aliongea Roma na kisha akapanda mpaka chumbani kwake na kisha akaanza kuvua nguo.
Ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza na kusogelea kioo na kujiangalia kiupandeupande kwenye bega lake , lakini ajabu mgongo wa Roma ulikuwa na Tatuu kubwa tatu , bega la kulia na kushoto kulikuwa na tatuu mbili halafu chini ya mgongo usawa wa tumbo pia kulikuwa na tatuu.
Tatuu ya kwanza sehemu ambayo ndio risasi ilipita kulikuwa na tatu ya chata ya Zero’s Organisation, upande wa kulia kulikuwa na chata la The Eagles’s , upande wa chini usawa tumbo kulikuwa na chata kubwa ya Pete ambayo katikati ilikuwa na maneno ya kigiriki ‘AIDES’.
Jeraha la Roma lilonekan kuziba pamoja na risasi yake ndani ,Baada ya kujiangalia kwa muda alibadilisha mavazi yake na kuchukua ufunguo wa gari yake ya Aud na kisha akatoka.
“Bi Wema naweza kuchelewa kurudi”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema amshangae na kujiuliza huyu mwanaume anaenda wapi na usiku huo kwani ilikuwa ni saa nne na inaenda kwenye saa tano.
****
Upande wa village G,aliingia Scorpion na kumsogelea mheshimiwa Kigombola aliekuwa akiangalia runinga huku akisinzia sinzia.
“Kuna nini?”
“Mishenii imefeli”Aliongea Scorpion na kumfanya mheshimiwa Kigombola ashangae , lakini wakati huohuo simu yake iliokuwa kwenye meza ya kioo ilianza kuita kwa kucheza cheza na Mheshimiwa aliangalia na kisha akaichukua na alijikuta macho yakimtoka , kwan jina lililokuwa likisomeka kwa kwenye kioo ililikuwa ni la ‘First Black’.
“Kigombola habari za usiku?”Sauti ya First Black iliokuwa kwenye utulivi kama kawaida ilisikika upande wa pili na kwa Kigombola hata ile hali ya kuwa na usingizi ilikuwa imemuishia.
“Salama kabisa Rafiki yangu , nimeshangazwa na simu ya usiku usiku”.
“Ndio Kigombola simu hii ya usiku ni ya jambo muhimu sana”Aliongea na kumfanya Kigombola kushangaa.
“Nakusilikiza Mheshimiwa”.Kigombola alibadili jina kutoka rafiki yangu na kumuita Mheshimiwa na hii ilikuwa ni kawaida yake , kama hakukua na swala muhimu walikuwa wakiitana marafiki na kama kuna swala muhimu kikazi Zaidi alikuwa akimwiita The First Black Mheshimiwa, walikuwa wakiongea kwa kutumia lugha ya kingereza.
“Nadhani unakumbuka vifo vya raia wa Marekani vilivyotokea miaka kumi na moja nyuma”.
“Nakumbuka mheshimiwa ,tena nnilikuwa moja ya watu waliotuma salamu za pole”
“Ni vyema kama unakumbuka Kigombola , swala ni hili, mtu aliehusika kwenye tukio lile ni Afshar Bahman na leo FBI wapepata kujua yupo Tanzania , na kwa maelezo ya haraka haraka Afshar Bahman anashikiliwa na kikosi cha The Eagles ,Afshar Bahman kupotea kwake baada ya tukio lile hakukuwa kwa bahati mbaya na sitaki FBI wapate ukweli wowote kutoka kwa Afshar maana ni swala ambalo linaweza kuibua mgongano wa kisiasa ndani ya taifa langu”
“Mheshimiwa unataka nifanye nini?”
“Vijana wangu wapo njiani kuja Tanzania na watafika muda mfupi nchini Tanzania nataka uwaandalie mazingira ya kufanya kazi yao kwa ufanisi,nafikiri una nguvu kubwa serikalini , hivyo swala hili naomba liendee vizuri kusiwe na aina yoyote ya ‘Loopholes’,Narudia swala hili lazima lifanikiwe kwa namna yoyote ile ,Kigombola miseme tu kwa swala hili la Afshar unahusika moja kwa moja maana wewe ndio umemtoa Afshar kwenye mwanga baada ya kujificha ndani ya Tanzania kwa muda mrefu”
“Unamaanisha nini mheshimiwa , kwanini nahusika na swala hili?”
“Mtu aliekuja kwako na kujitambulisha kwa jina la Seif ni Afshar Bahman ninaemzungumzia na wanaintelijensia wangu wamenipatia hayo maelezo kwamba umempatia kazi ambayo imefeli na kupelekea kukamatwa na kikosi cha The Eagles , sitaki kuongea mengi juu ya kikosi cha The Eagles , lakini naamini swala nililokuambia litafanikiwa kwa asilimia mia moja”
Mzee Kigombola alijikuta akikunja ngumi kwa hasira na kujitukana , hakuelewa ni kwanini hakumjua Seif kama moja ya watu waliohusika na vifo vya watu Zaidi ya ishirini na tano nyuma.
“Nilitakiwa kujua kwanini Seif alizamia Tanzania , hili swala lake kuanzia mwanzo lilikuwa na maswali mengi ambayo yalihitaji majibu,I was being emotion na hili swala la Edna , hii yote ni kutokana na The Don kunipa presha ya kutatua njia ya ‘Safe Root’.