Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 63

John alikimbia mpaka chini kwenye bustani za jengo hili na kuhakikisha, lakini hakukuua na dalili zozote za Afshar kuonekana , jambo hili lilimshangaza sana.

“How this possible!?”Alijiuliza huku akiwa sio mwenye kuamini kama Afshar kapotea , aliamini lazima atakuwa katika mazingira hayohayo.

Upande wa ndani ya ukumbi hali ilikuwa mbaya , lile kusanyiko lilikuwa limeharibika ,Chiara alikuwa fasta sana , baada ya kuona Edna Analia pasipo kufanya lolote alimsogelea.

“Madam tunapaswa kumpeleka hospitalini”Aliongea Chiara kwa kingereza na kumfanya Edna aliekuwa haoni vizuri kwa machozi amwangalie na akili yake kuanza kufanya kazi, alikuwa akilia huku akitaja jina la Roma , alijua mwanaume aliekuwa chini alikuwa amepigwa risasi kwa ajili ya kumlinda yeye.

Watu walio majasiri walizunguka na wale waliokuwa na waoga kama makunguru walianza kutawanyika,Chiara alimbeba Roma na kumuweka begeani , licha ya kuwa mwanadada lakini alidhihrisha uwanajeshi wake.

Tukio la mzungu kumbeba Roma na kumtoa liliwaacha Mzee Alex pamoja na Abuu kwenye maswali mengi, na ni kama Abuu sasa akili yake ilikuwa ikija na kupotea ,alianza kukumbuka maneno ya Elvice juu ya wanajeshi wake aliowaagiza kuingia kwenye nyumba ya Edna kumteka kudhibitiwa na wazungu.

“Unafikiri atapona?”Aliuliza Mzee alex aliekuwa nyuma ya Abuu na kumfanya bwana huyu ageuke kwa mshituko.

“Hata kama yupo hai , tunaenda kummalizia hukohuko”Aliongea abuu alieawa na Faraja moyoni.

“Ila bado kuna jambo sijaelewa hapa , huenda yale maneno naanza kuyaamini , huyu bwana sio wa kawaida , unajua alikuwa mbali na Edna lakini nilishangaa yeye ndio amepigwa na Risasi sio Edna”Aliongea Mzee Alex huku akimwangalia Abu ni kama alikuwa akitafuta sapoti kwa maneno aliyoyasema.

“Ulikuwa huamini baba , lakini naamini saivi umeanza kuelewa mkasa niliopitia , ila hata hivyo yashaisha haya Roma huu ndio mwisho wake na Edna anaenda kuwa wangu”Aliongea na Mzee alex alitabasamu na kumpigapiga Begani na kuondoka na fimbo yake ya kutembelea.

Magdalena na Mage walikuwa ndio wa kwanza kutoka nje ya jengo ukumbi huku wakionesha dhamira ya kumkamata Sniper , na wao walifika mpaka kwenye bustani na kumkuta John ambaye alikuwa bize kuhangaika kutafuta.

Chiara baada ya kumfikisha Roma kwenye Gari na nyuma nyuma akiwa Edna pamoja na Neema ambao wote walionekana kuwa na wasiwasi , huku aliekuwa kweye wasiwasi Zaidi alikuwa ni Edna, Chiara alimuweka Roma kwenye siti ya Gari.

“Chiara hapa panatosha , utakaa karibu na Edna nakuja kumchukua”Aliongea Roma aliekuwa amenyanyuka na kumfanya Edna atumbue macho na haikuwa kwa Edna tu hata kwa Neema.

“Roma!”Aliita Edna ambaye alikuwa akifuta kamasi na machozi kwa wakati mmoja na sasa ni kama alipata ahueni , ila bado hakuwa akiamini kama aliekuwa mbele yake ni Roma

“Hehe…My wife nani kakuambia nakufa kizembe hivyo mumeo , nilikuwa nikisikia unavyolia , unaonekana unanipenda sana,siwezi kufa nani atakulinda”Aliongea Roma huku akijishika eneo la Bega ambalo damu zilianza kupungua kutoka na kisha akavua koti la suti na kuliweka kwenye gari na hapo shati alilokuwa amevaa lililonekana kuwa na damu ambazo zimesambaa kiasi.

Lakini Edna alionekana kutoridhika , alijua Roma alikuwa na maumivu na anajikaza ,licha ya kwamba yeye na Neema wote walikuwa kwenye mshangao wa kuamka kwa ghafla kwa Roma.

“Mke wangu utabaki na Chiara atakupa Ulinzi hapa mpaka nitakaporudi , ngoja nikamkamate alieataka kukuzuru na utaamua tumpe kifo cha aina gani”

Aliongea Roma na kisha kuanza kupiga hatua , huku watu wakimshangaa kumuona Roma kaamka, hawakuelewa nini kimetokea kwani mtu ambaye walidhania kuwa mfu anaonekana kuwa hai tena.

Mahesabu yangu yalienda kama nilivyotaka , nigekosea kidogo tu huenda ingenipata kwenye uti wa mgongo”Aliwaza Roma akikatisha upande wa kulia kuelekea lilipo jengo la Apartment.

“Your Majest!”Aliita John na kufanya Magdalenda na Mage wageuke kumwangalia Roma aliekuwa akitembea kama hakijatokea kitu na hapa ndipo macho ya Mage yalimtoka.

“John imekuwaje?”

“Ni Afshar Bahman Sir”Aliongea John na kumfanya Roma ashangae.

“Afshar Bahman?, yule gadi wa miaka kumi na moja nyuma?”Aliuliza Roma na kumfanya John atingishe kichwa kwa ishara ya ndio.

“Sasa yuko wapi?”

“Kapotea Ghafla baada ya kujirusha kutoka ‘floor’ ile ya ishirini”aliongea na Roma akaangalia juu na kisha akatabasamu ni kama mtu ambaye ameona kitu.

“Endelea kutoa ulinzi hapa nakuja” Aliongea Roma kisha akwapita Mage na Magdalena waliokuwa wakimshangaa na Roma aliwakonyeza lakini kitu na pacha wake walishindwa kuongea , waliishia kuangalia Shati la Roma lilivyokuwa limechafuka kwa damu.

Roma baada ya kuingia kwenye jengo hili ambalo ni kama halikuwa na wapangaji , ila walikuwepo na wamejifungia katika vyumba vyao , alipandisha na lift mpaka Floor ya kumi na kisha akatoka na kutembea mpaka ‘Apartment’ namba kumi na moja iliokuwa na mlango upande wa kushoto kwake na kisha akasimama.

*****

Upande wa ndani ya ‘Apartment’ namba kumi na moja alionekana jamaa mmoja ambaye alikuwa upande wa jikoni , akiwa bize na maswala ya upishi, alikuwa ni mwanaume mzungu aliekuwa na nywele fupi , ukimwangalia kimakadiro si chini ya miaka therathini,alikuwa amevaa suruali ya Truch Suit , pamoja na Tishen ya kata mikono yenye picha ya Mike Tyson.

Alichukua vttunguu ambavyo alikuwa amevikata harakaharaka na kisha akaweka mafuta kwenye kikaangio baada tu ya kumaliza alipasua mayai manne na kuweka kwenye kikaangio hiko na kuweka mayai.

“Chwaaa…. Chwaa,,,,”

Ulikuwa ni mlio wa mkaango , huyu bwana wa kizungu alionekana kuwa vyema sana katika swala la upishi , kwani alivyokuwa akizungusha yai muundo wa chapatti iliokuwa kwenye kikaangio ungesema ‘Yes’ huyu ndio mzungu anaejua kupika.

Baada ya bwana huyu kuona pishi lake lipo tayari , aliweka kwenye sahani na kisha akazima gesi na kutoka hadi eneo la Sebuleni.

Ajabu ni kwamba eneo la Sebuleni alikuwepo Seif, akiwa amefungwa na mabendeji kwenye miguu na mikononi pia na kwenye tumbo lake alikuwa amezungushiwa Pazia ambalo lilikuwa limefungwa kwenye mguu wa sofa kwa chini, Seif alikuwa mzima na alimwangalia mzungu aliekuwa mbele yake na katika akili yake alijua mtu huyu lazima atakuwa ni FBI tu maana ndio watu aliokuwa wakimtafuta.

Bwana huyu wakizungu alionekana kutomjali Seif , aliwasha Tv na Rimoti na kisha akaweka sahani yake kwenye meza ya kioo na kuendelea kula mayai yake ya kukaanga.

Lakini muda huohuo mlango uligongwa na kisha alitabasamu na kumwangalia Afshar.

“Ulietaka kumuua yupo mlangoni”Aliongea kwa kingereza na kumfanya Afshar atoe macho na bwana huyu alitabasamu na kisha akasogelea mlango.

“Hahahaha.. Hades! Naona umewahi kuliko nilivyotarajia”Aliongwa bwana huyu kwa kingereza na kumfanya Roma atabasamu.

“Nilijua tu Mpishi wa kimataifa upo Bongo ,uwepo wako niliunusa wakati naingia na Gari ndani ya haya maeneo”

Aliongea Roma na alionekana kumfahamu sana bwana huyu aliemwita mpishi wa kimataifa na wakati huo Afshar aliefungwa na mabendeji akitoa macho kama kabanwa na mlango.

“How this possible?”Aliwaza kwenye akili yake maana alikuwa akikumbuka kabisa alimpiga Roma risasi za mgongoni , alijiuliza inawezekanaje aonekane kama hajajeruhiwa , maana Afshar alimuona Roma akiwa mzima , licha ya ushahidi wa damu tu katika shati yake.,

“Poseidon , siui unafanya nini Tanzania , lakini nimekuja kuchukua mtu wangu alietaka kumuua mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Poseidon arudi kukaa kwenye Sofa na kisha akala kidogo , upande wa Roma licha ya kumuona bwana huyu aliemwita Poseidon hakuonesha kubadilika , yaani hakuwa na furaha sana , alikuwa kawaida tu kama vile mtu huyo alikuwa akionana nae mara kwa mara.

“Hades nimefulia sana , sina hata hela ya kula, kuna mshikaji kanipa tu hifadhi kwenye hii ‘Apartment’ kupitia AirBnB, unaonaje ukinilipa kama malipo ya kumuokoa mtu wako alietaka kujiua”Aliongea mwanaume ambaye sasa tunamfahamu kwa jina la Poseidon na namna alivyokuwa akiongea alionyesha kweli hana hela , lakini pia ungeshagaa mzungu huyu kukosa hela maana katika jamii nyingi za kiafrika ni mara nyingi sana kwa mzungu kukosa hela , japo wanafulia.

“Poseidon sijakuomba unisaidie kumuokoa , kwasababu nitamuua , ni vilevile tu kwanini nikupatie pesa, pambana na shida zako , mimi mwenywe nalishwa na mke wangu, hela natoa wapi,halafu huyu fala hapa anataka kumuua”.

Afshar ambaye alikuwa akiwaelewa Hades na Poseidon , sasa alikuwa amepata mwanga namna ambavyo aliokolewa, kwani wakati anajirusha alihisi nguvu isio ya kawaida ikimvuta kupitia usawa wa dirisha na aliposhituka tu yupo ndani ya hiki chumba.

“They are God`s”Aliwaza Seif kwa mshangao akimaanisha watu waliokuwa mbele yake ni Miungu baada ya kusikia jina la Pseidon na Hades , Seif alionekna kuwa na baadhi ya taarifa zinazohusu Miungu watu .”Hawa ndio tuliokuwa tukiwasikia jeshini , kumbe ilikuwa kweli , nilikuwa nikidhani ni hadithi za kufikirika “Aliendelea kuwaza huku akizidi kuogopa na kujiona kaingia cha kike.

“Hades acha zako ,unajifanya kama hunijui, ukiwa ndani ya nchi yako, hatujaonana muda mrefu Tokea tusaini The God`s treaty ulitakiwa sasa unikaribishe kwa shangwe,inakuwaje wewe pekee ndio huoneshi kunimisi”Aliongea Poseidon akionekana ni mwenye kulalamika

“Kwanza unafanya nini Tanzania , si nilisikia upo China wewe umefungua mgahawa?”Aliuliza Roma

***

Upande mwingine Abu na mzee Alex walitoka mpaka nje chini kabisa ya maegesho , wakwanza kutoka alikuwa ni mzee Alex ambaye alionekana kuwa na furaha sana usiku huu kwa kufanikisha jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza vichwa muda mrefu na sasa aliona kilichobaki ni kuhakikisha anapata kampuni ya Edna.

Lakini sasa alijikuta akishangaa mara baada ya kumuona mzungu ,Edna pamoja na Neema Luwazo waliokuwa wamesimama kwenye magari , wakati akijiuliza nini kinaendela alisogelewa na kijana wake na kisha akamwambia jambo kwa sauti ya chini na kumfanya mzee huyu aanze kupumua kwa kasi,, sijui alikuwa ameambiwa nini.,lakini aligeuza na kurudi ndani kwa spidi na fimbo yake ya kutembelea.

Edna na Neema Luwazo walijikuta wakimshangaa mzee huyu , kwani alionekna kama alikuwa amechanganyikiwa.

Baada ya dakika chache tu Abu alietangulizana na Mzee Alex walionekana kurudi kwa spidi.

“Hehe.. wife mtu wetu tumemkamata”.Aliongea Roma aliekuwa amemuweka Begani Seif akiwa kwenye mabendeji , akiwa mzima ,Seif aliishia kumwangalia Abuu. Huku Abu akijiona kama akili yake haifanyi kazi vizuri.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 64

Mzee Alex pamoja na wafanya biashara wengine waliokuwepo eneo la maegesho , walikuwa kwenye mshangao mkubwa sana , ni kama macho yao yaliku yakiwadanganya kwa kile walichokuwa wakikiona mbele yao , mtu ambaye dakika chache nyuma walimshuhudia kupigwa risasi alikuwa amembeba Seif begani , kwanini wasishangae.

“Jamani si tumeshudia akipigwa risasi huyu, au haikumpata?”Aliuliza mwanamama mmoja mnene aliekuwa ameshikilia simu yake kubwa ya I phone akiongea na mwanaume aliekuwa pembeni yake.

“Ni yeye si unaona shati limechafuka kwa damu , lakini inanishangaza kuona ni mzima”Alijibu mzee huyu.

Abuu alishindwa hata kuongea neno lolote Zaidi ya kumwangalia Roma anaemwingiza Seif kwenye gari , lakini muda huo huo Diego akiwa ameambatana na wazungu sita , wanajeshi wa Kikosi cha The Eagles waliingia ndani ya hili eneo na kumsogelea Roma.

“Sire!” Aliita Diego kwa mshangao mara baada ya kumuona Afshar kwenye gari.

“Diego nadhani mnataarifa za huyu muuaji?”

“Ndio Sir”

“Basi nadhani mnajua cha kufanya , mchukueni mpaka kambini , nitakuja kumhoji mimi mwenyewe .nikishamfikisha mke wangu nyumbani”

Aliongea na Diego alionekana kuelewa na haraka sana alimpa ishara Chiara na John kuondoka na Seif , huku na wao wakianza kuondoka eneo la hoteli hii , hawakutaka kukutwa na polisi ambao walikuwa njiani kufika eneo la tukio kwa kuchelewa.

Kila kilichokuwa kimetokea dakika kadhaa nyuma kilionekana kuwa kama muvi kwa macho ya watu wengi,waliokuwa wameshuhudia tukio hili kwanzia mwanzo mpaka mwisho.

Baada ya Roma kutoa maagizo , alimshika Edna mkono ambaye muda wote alikuwa akimwangalia Mume wake kama kiumbe ambacho ndio kwanza anakutana nacho leo kwa mara ya kwanza.

Edna alikuwa ni kama haelewi kile kinachoendelea na alimuona Roma kama mgeni kwenye macho yake , licha ya kwamba mrembo huyu alikuwa akijua Roma hakuwa wa kawaida , lakini hakudhania kama atakuwa ni Zaidi ya ule ukawaida aliokuwa akiujua,kwani kila siku alikuwa akishangazwa na jambo jipya kuhusu Roma.

Neema Luwazo na yeye alikuwa kwenye mshangao , alikuwa haelewi, kinachoendelea , licha ya kwamba tukio lote lilitokea kwenye majengo yake ya kampuni , lakini ni kama alikosa nguvu ya kutoa maagizo , kwani muda wote alikuwa ni mwenye kunyamaza na kuangalia kile kinachoendelea , mwanamama huyu alikuwa kwenye mshangao mkubwa.

“Abu tunatakiwa kufanya nini kwenye hali kama hii?””Aliuliza Mzee Alex aliekuwa ni kama haamini kinachoendelea na kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake , alikosa maamuzi ya hapokwa hapo , na ni mara ya kwanza pia kumuuliza kijana wake ni jambo gani linatakiwa kufanyika kwa wakati huo , lakini kwa Abuu alikuwa ni kama baba yake tu , kwani wote hawakujua ni hatua gani za kufuatwa kwa wakati huo.

“Baba hii ni hatari wakimhoji Seif na kututaja kama wahusika wa mpango mzima”Aliongea Abu na hapa ni kama alikuwa ameshituka.

“Mpigie Kigombola”Aliamrisha Mzee Alex huku akisogelea gari yake na kijana wake alimfungulia mlango , huku Abuu akiangalia Roll Royce ,gari alilopanda Edna na Roma likitokomea kwenye macho yake.

“Fu****ck!”Abuu alijikuta akigongagonga kioo cha gari yake kwa hasira , huku baadhi ya watu wakimshangaa , lakini sasa wakati hayo yanaendelea Azizi Mohamed alikuwa ndani ya maeneo hayo , na haikueleweka alikuwa wapi , kwani ndio kwanza alikuwa akitokeza kwenye mlango wa kutokea ndani ya jengo hili la Hoteli.

“Kuna nini kimetokea?”Aliuliza tajiri Azizi na kijana wake alievalia suti alimweleza kwa sauti ya chini na Mzee huyu aliachia cheko , lililofanya baadhi ya watu wamwangalie , lakini kama ilivyokuwa sifa yake , hakujali , alitembea kulisogelea gari yake na kuingia.

“Hii habari itamfurahisha Rafiki yangu Jeremy.. hahahaha”Huyu mzee Tajiri alionekana kufurahishwa sana na tukio hilo.

“Bosi!”Aliuliza Dereva baada ya kumuona bossi wake anacheka pasipo kuelewa ni nini kimchekeshacho.

“Hahahahaha ..Nipeleke nyumbani Sadiki nikalale mie”Aliongea mzee huyu na kisha Sadiki alitoa gari hio ya kifahari aina ya Range na kutoka nje ya hoteli hio.

Upande mwingine Mage na Magdalena walishuhudia tukio lote la Roma kutoka akiwa na Seif,Kwa Magdalena kwake ilikuwa ni afadhari kwani alikuwa mwanaeshi , ila kwa pacha mwenzake Mage hali ilikuwa mbaya.

“Magdalena mbona ni kama sielewi kinachoendelea , naielezeaje hii hali?”Aliongea Mage mwanadada huyu ,masikini alionekana kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja , hakuwa akielewa tukio zima lilivyotokea na mpaka kuisha.

“Usiumize kichwa sana Mage, Mume wa Edna sio wa kawaida”.

“Unamaanisha nini Magdalena?, sio wa kawaida kivipi?, mbona unaonekana kuna jambo unalijua unanificha”

“Siwezi kukuambia lolote Mage, ila jua sio mtu wa kawaida ,nimemsikia siku moja akisema wewe ni moja ya Askari wanaomchukia kwenye taifa hii , ila Mage nikwambie tu jitahidi kukaa nae mbali”Aliongea Magdalena wakati wakiwa kwenye Gari na kuzidi kumchanganya sana Mage.

“Mtu sio wa kawaida halafu nikae nae mbali , mimi ndio Mage , lazima nijue kila kitu , nitaanza kumfatilia kimya kimya” Aliwaza Mage , hakutaka kumuuliza sana dada yake maana alijua tabia yake ya kutotaka kuongea mara kwa mara hasa maswala ambayo yalikuwa yakihusu kazi yake.

Edna alionekana kuegamia kiti cha gari , huku akionekana kuwa na mawazo mengi kwa wakati mmoja , hakutaka kuongea chochote na Roma na hata Roma mwenyewe hakuwa akielewa mke wake alikuwa akifikiria nini na ndio maana hakutaka kumuuliza , aliendesha gari kimya kimta kuelekea nyumbani.

“Anaonekana kuwa na mshituko na najua ana maswali mengi , lakini siwezi kuanza mimi kumueleza , ila siku akitaka kujua historia yangu ya maisha yangu ya nyuma nitamueleza kila kitu”Aliwaza Roma wakati akiingia daraja la Kigamboni.

Edna aliekuwa ameegamia kwenye kiti alikuwa pia akiwaza kama alichokuwa akiwaza Roma.

“Sio kama nilivyomfikiria ,Anaonekana kuwa na historia kubwa sana kwenye maisha yake , lakini sitomuuliza mpaka atakaponiambia mwenyewe”Aliwaza Edna katika kichwa chake.

Wanandoa hawa walionekana kuwa na mawazo yanayotofautiana , Roma alikuwa akiwaza kumuambia Edna kila kitu kama tu ataamua kumuuliza,lakini wakati huo Edna anawaza pia kutomuuliza Roma chochote kuhusu maisha yake ya nyuma mpaka atakapomuambia mwenyewe.

Muda mchache mbele walifika nyumbani na Roma aliekuwa na shati lililokuwa na damu alitoka , huku Edna akiwa wa kwanza , alibeba mkoba wake mrembo huyu na kisha akakimbilia ndani na kumfanya Roma asimame amwangalie Edna, alishindwa kuelewa ni nini Edna anawaza kwa wakati huo.

“Mr Roma nini kimekukuta?”Aliuliza Bi wema kwa wasiwasi mkubwa baada ya kumuona Roma mgongo wake kutapakaa damu.

“Bi Wema kuna tatizo limetokea ila nitakueleza vizuri kesho , kuna mahali nataka kwenda , kuwa karibu na Edna anaonekana kuwa kwenye hali ambayo sio nzuri”Aliongea Roma na kisha akapanda mpaka chumbani kwake na kisha akaanza kuvua nguo.

Ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza na kusogelea kioo na kujiangalia kiupandeupande kwenye bega lake , lakini ajabu mgongo wa Roma ulikuwa na Tatuu kubwa tatu , bega la kulia na kushoto kulikuwa na tatuu mbili halafu chini ya mgongo usawa wa tumbo pia kulikuwa na tatuu.

Tatuu ya kwanza sehemu ambayo ndio risasi ilipita kulikuwa na tatu ya chata ya Zero’s Organisation, upande wa kulia kulikuwa na chata la The Eagles’s , upande wa chini usawa tumbo kulikuwa na chata kubwa ya Pete ambayo katikati ilikuwa na maneno ya kigiriki ‘AIDES’.

Jeraha la Roma lilonekan kuziba pamoja na risasi yake ndani ,Baada ya kujiangalia kwa muda alibadilisha mavazi yake na kuchukua ufunguo wa gari yake ya Aud na kisha akatoka.

“Bi Wema naweza kuchelewa kurudi”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema amshangae na kujiuliza huyu mwanaume anaenda wapi na usiku huo kwani ilikuwa ni saa nne na inaenda kwenye saa tano.

****

Upande wa village G,aliingia Scorpion na kumsogelea mheshimiwa Kigombola aliekuwa akiangalia runinga huku akisinzia sinzia.

“Kuna nini?”

“Mishenii imefeli”Aliongea Scorpion na kumfanya mheshimiwa Kigombola ashangae , lakini wakati huohuo simu yake iliokuwa kwenye meza ya kioo ilianza kuita kwa kucheza cheza na Mheshimiwa aliangalia na kisha akaichukua na alijikuta macho yakimtoka , kwan jina lililokuwa likisomeka kwa kwenye kioo ililikuwa ni la ‘First Black’.

“Kigombola habari za usiku?”Sauti ya First Black iliokuwa kwenye utulivi kama kawaida ilisikika upande wa pili na kwa Kigombola hata ile hali ya kuwa na usingizi ilikuwa imemuishia.

“Salama kabisa Rafiki yangu , nimeshangazwa na simu ya usiku usiku”.

“Ndio Kigombola simu hii ya usiku ni ya jambo muhimu sana”Aliongea na kumfanya Kigombola kushangaa.

“Nakusilikiza Mheshimiwa”.Kigombola alibadili jina kutoka rafiki yangu na kumuita Mheshimiwa na hii ilikuwa ni kawaida yake , kama hakukua na swala muhimu walikuwa wakiitana marafiki na kama kuna swala muhimu kikazi Zaidi alikuwa akimwiita The First Black Mheshimiwa, walikuwa wakiongea kwa kutumia lugha ya kingereza.

“Nadhani unakumbuka vifo vya raia wa Marekani vilivyotokea miaka kumi na moja nyuma”.

“Nakumbuka mheshimiwa ,tena nnilikuwa moja ya watu waliotuma salamu za pole”

“Ni vyema kama unakumbuka Kigombola , swala ni hili, mtu aliehusika kwenye tukio lile ni Afshar Bahman na leo FBI wapepata kujua yupo Tanzania , na kwa maelezo ya haraka haraka Afshar Bahman anashikiliwa na kikosi cha The Eagles ,Afshar Bahman kupotea kwake baada ya tukio lile hakukuwa kwa bahati mbaya na sitaki FBI wapate ukweli wowote kutoka kwa Afshar maana ni swala ambalo linaweza kuibua mgongano wa kisiasa ndani ya taifa langu”

“Mheshimiwa unataka nifanye nini?”

“Vijana wangu wapo njiani kuja Tanzania na watafika muda mfupi nchini Tanzania nataka uwaandalie mazingira ya kufanya kazi yao kwa ufanisi,nafikiri una nguvu kubwa serikalini , hivyo swala hili naomba liendee vizuri kusiwe na aina yoyote ya ‘Loopholes’,Narudia swala hili lazima lifanikiwe kwa namna yoyote ile ,Kigombola miseme tu kwa swala hili la Afshar unahusika moja kwa moja maana wewe ndio umemtoa Afshar kwenye mwanga baada ya kujificha ndani ya Tanzania kwa muda mrefu”

“Unamaanisha nini mheshimiwa , kwanini nahusika na swala hili?”

“Mtu aliekuja kwako na kujitambulisha kwa jina la Seif ni Afshar Bahman ninaemzungumzia na wanaintelijensia wangu wamenipatia hayo maelezo kwamba umempatia kazi ambayo imefeli na kupelekea kukamatwa na kikosi cha The Eagles , sitaki kuongea mengi juu ya kikosi cha The Eagles , lakini naamini swala nililokuambia litafanikiwa kwa asilimia mia moja”

Mzee Kigombola alijikuta akikunja ngumi kwa hasira na kujitukana , hakuelewa ni kwanini hakumjua Seif kama moja ya watu waliohusika na vifo vya watu Zaidi ya ishirini na tano nyuma.

“Nilitakiwa kujua kwanini Seif alizamia Tanzania , hili swala lake kuanzia mwanzo lilikuwa na maswali mengi ambayo yalihitaji majibu,I was being emotion na hili swala la Edna , hii yote ni kutokana na The Don kunipa presha ya kutatua njia ya ‘Safe Root’.
 
SEHEMU YA 65

“Nini kimetokea Scorpion?”Aliuliza Kigombola baada ya kukata simu.

“Kwa maelezo ya Abubakari mheshimiwa ni kwamba Roma sio mtu wa kawaida , Risasi zimempata lakini hajafa na mbaya Zaidi anasema Seif amekamatwa na Roma na inaonekana anaenda kufanya nae mahojiano maana bado yupo hai”aliongea Scorpion ka wasiwasi na mheshimiwa , hasira zilizochanganyika na mshangao zilijionyesha katika macho yake.

“Unaweza kwenda”Aliongea huku akinyanyuka na kwenda maka kwenye ‘Water Dispenser’ na kumimina maji kwenye glass na kunywa yote , akachukua maji mengine na kunywa tena.

“Nimekuwa mjinga sana, hii yote ni kutokana na kuzungukwa na watu wapumbavu kama Alex na Bakari hawana mawazo mbadala Zaidi ya kutikia ndio tu”Aliwaza mheshimiwa na kisha akareea sehemu aliokuwa ameketi na kupiga simu.

“Nataka taarifa zote zinazihusu kikundi cha The Eagles sasa hivi , nadhani hapo kitengoni mnazo taarifa zake”.

“Ndio mheshimiwa taarifa ipo na naomba radhi kwa kuchelewesha taarifa hii kukutumia”

“Cut the bullshit , nitumie taarifa now”Akakata simu , huku akionekana kuchafukwa na roho na ndani ya dakika chache tu Taarifa ilitumwa kwa njia ya watsapp , alifungua faili na kuanza kusoma na macho yalimtoka.

“Umuhimu wangu kwenye hili taifa naona sasa hivi umeshuka kiwango cha kudharauliwa , kwanini taarifa muhimu kama hii sikuwa nayo”Aliongea muheshimiwa huku akiendelea kupitia , taarifa aliokuwa akisoma ilikuwa ikimuhusu Roma kukodi wanajeshi wa The Eagles.

“Hili ndio kosa namba moja nililofanya , niliridhika na taarifa ile ya Harvard,nilitakiwa kumchimba Roma vizuri na kumjua kiundani ,nilikuwa nikipambana na mtu ambaye sikuwa nikimjua vyema”Aliwaza mheshimiwa huyu , alionekana hakuwa na taarifa kamili zilizokuwa zikimhusu Roma , lakini pia mheshimiwa aliona watu wa Kitengo walifanya makusudi kutompitishia taarifa zinazohusu The Eagles.

“Hii Taarifa bado haiitoshelezi naamini kuna Zaidi ya hii , The Eagles ni kundi kubwa , haiwezekani Roma kuwa na uwezo wa kuwakodi, kwa namna ambavyo anataka ni pesa nyingi sana zinatumiak kukodi hawa wanajeshi”Aliendelea kuwaza mheshimiwa , taarifa ambayo alikuwa ametumiwa , ilikuwa ikionesha Roma kukodi wanajeshi kutoka kikundi cha The Eagles kuja Tanzania , taarifa hio haikuonyesha kama Roma ndio aliekuwa mmiliki wa kundi hilo.

Kiufupi ni kwamba mheshimiwa Kigombola hakuw ana uelewa wowote juu ya Roma kuitwa Hades au Pluto.

****

Upande wa Mbweni ndani ya jumba la kifahari alilokuwa akiishi Meja jenerali wa JWTZ Maeda Mkwizu alikuwa ameketi sebuleni akiwa ameshikilia simu yake kubwa ya Sumsung S 22 huku akiperuzi, bwana huyu alikuwa akiangalia baadhi ya picha ya za matukio zilizokuwa zikimuonesha Roma kumuweka Seif Begani, Roma kupigwa risasi , picha ambazo haikueleweka zilipigwa saa ngapi. Wakati akiendelea kuangalia picha hizo , mara simu yake iliita na jina lilisomeka KITENGO, alipokea na kuweka simu sikioni.

“Nipe habari Hamduni?”.

“Afande nimempa taarifa kama ulivyoelekeza”.

“Safi hakikisha hapati taarifa kamili inayomuhusu Hades , fanya kila anachoelekeza lakini unipatie taarifa kwanza”

“Sawa Afande”Aliongea mwanaume aliefamika kwa jina la Hamduni na kisha simu ilikatwa

“Kuna mipaka ya jeshi na siasa , ambayo haiwezi kuvukwa na nitahakikisha nalinda mipaka hii kwa namna yoyote ile”Aliwaza Afande Maeda.

*****

Upande mwingine ndani ya jengo la Apartment alionekana Poseidon kalala kwenye sofa huku akiwa hana habari , akiangalia chaneli iliokuwa ikionyesha mapishi , bwana huyu alionekana ni wale watu ambao hawakuwa wakichoka kujifunza , licha ya kwamba alikuwa akifahamika kama mpishi bora duniani.

Eitani Rof ndio jina la Poseidon lililokuwa maarufu Zaidi , Eitan ni jina la mpishi maarufu ambaye alikuwa akifahamika duniani kote , na hii ni baada ya kushinda tuzo ya mpishi bora wa dunia kwa miaka mine mfululizo.

Umaarufu wa Eitan ulianzia nchini China baada ya bwana huyu kufungua mgahawa uliopata umaarufu nchini humo uliofahamika kwa jina la ‘Taste of Angels’,licha ya bwana huyu kuwa maarufu nakufahamika kwa jina la Eitan Rof lakini ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu kwa jina la Poseidon.

Poseidon ni jina linalotoka katika historia ya Ugiriki ya kale yaani Mungu wa Bahari ,tetemeko la Ardhi na Farasi ,katika historia ya Ugiriki ya kale Poseidon anafahamika kama moja ya Miungu ambayo ilikuwa na sifa ya kukasirika haraka.

Wakati bwana huyu akiendela kuangalia Runinga , mara simu yake ilianza kuita , aliangalia jina na lilisomeka ‘Master’.

“Umefanikisha kazi?”Lilikuwa ni swali baada tu ya kupokea.

“Asilimia mia moja , nataka pesa zangu ndani ya muda mfupi”

“Una uhakika hata kumbuka chochote?”

“Master maswali mengi sitaki , sijawahi kufeli kwenye kazi yangu ashasahau kila kitu mpaka sasa”

“Hela zako zishatumwa kwenda kisiwa cha Sychelles , dakika chache zijazo utatumiwa taarifa za akaunti”.

“Good! Master tutaonana kukiwa na dili tena”Na simu ikakatwa.
 
SEHEMU YA 66.

“Mfalme Pluto kuna jambo halipo sawa kwa Afshar?”

“Unamaanisha nini Diego?”

“Anaonekana kutokuwa na kumbukumbu”Aliongea Diego na kumfanya Roma aongoze njia kuelekea upande wa chumba ambacho The Eagles walikifanya kama sehemu ya kufungia watuhumiwa kwa muda na kuwahoji.

Roma baada ya kumfikia Afshar , alimshika kidevu na kumuangalia machoni.

“Sh***t!, Poseidon yule fala , nilijua tu yupo hapa nchini kwa kazi maalumu na tamaa zake”Aliwaza Roma huku akionyesha hasira zake wazi na kumfanya Diego kushangaa.

“Your Majest Pluto ni nini tatizo”

“Kashafutwa kumbukumbbu , hakumbuki chochote”Aliongea Roma huku akimwangalia Seif ambaye alionekana kama hakuwa akijua kinachoendelea

“Poseidon anajifanya mjanja , ila dawa yake ipo jikoni tukikutana tena lazima nimfundishe adabu”Aliwaza Roma huku akionesha hali ya hasira kwenye macho yake,Poseidon alikuwa amemzidi akili.

“Diego hili swala la Afshar inaonekana kuwa kubwa na tushazidiwa akili , hana thamani tena na hata nikimuua haina maana kwangu, wasiliana na FBI , mfanye utaratibu wa kumkabidhi”aliongea Roma .

“Sawa mfalme Pluto”Aliongea Diego huku akionekana kutoridhishwa na kile kilichotokea .

“Kuna Ripoti nyingine Deigo?”

“Ndio mfalme Pluto , wakati ulipokuwa Japani majambazi walivamia nyumba yako na kwa bahati nzuri tuliweza kuwaintercept kabla hawajamfikia Malkia”Roma alishangaa kwani hio taarifa hana .

“Ni watu gani walioingia nyumbani kwangu?”

“Mfalme Pluto tulifanikiwa kuwadhibiti watatu kwa kuwaua na mmoja tukamuacha hai kwa ajili ya taarifa na katika mahojiano nae ametueleza mtu anaeitwa Elvice ndio aliewaagiza kufanya uvamizi huo”aliongea Diego na kumfanya Roma kupandwa na hasira.

“Unafikiri tukio la leo lina muunganiko na Elvice?”Aliuliza Roma.

“Mfalme Pluto tunauhakika kwa asilimia mia moja swala hili lina muunganiko”.

“Naamini pia hayupo Peke yake, nataka muchimbe taarifa za Abubakari Hamadi pia na mpate ushahidi wote”

“Sawa Mheshimiwa”.

“Kuna maendeleo yoyote ya misheni nilizowapa?”

“Mfalme kuna maendeleo makubwa , lakini bado tunaendelea kukusanya taarifa ili kufanya ulinganifu , nitakupa ripoti muda mchache , naomba utusamehe kwa kuchelewa kwetu”

“Hakuna shida Diego , mna muda wa kutosha wa kufatilia hilo ,,msifanye kwa haraka , nahitaji taarifa inayojitosheleza na ya uhakika”Aliongea Roma na Diego akapiga Saluti.

Bram alimchana Roma sehemu ya bega kwa utaalamu mkubwa na kisha akatoa risasi ,bwana huyu alioneakna sio mtaalamu tu katika maswala ya tarakishi , lakini pia alionekana kuiva katika swala la matibabu kwani ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza.

*****

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa , siku ya jumapili na Roma ratiba zake zilikuwa zilezile , kuamka asubuhi na kufanya mazoezi kabla ya mambo mengine.

Muda wa saa mbili kamili alikuwa ashamaliza kujisafisha na sasa alikuwa akishuka chini sebuleni kwa ajili ya kupata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Bi Wema.

Edna alikuwepo wakati Roma anashuka , na mrembo huyu leo alikuwa akimwangalia sana Roma wakati akiwa anasogea mezanni.

“Wife mbona unaniangalia sana?”aliuliza Roma huku akimwangalia mke wake na sura yake ya kipole asubuhi hii , alijikuta akikumbuka namna ambavyo Edna alikuwa akilia jana baada ya kupigwa risasi.

“Unaendeleaje na jeraha?”aliuliza Edna huku Bi Wema akimwangalia Roma usoni , alionekana alikuwa ashaambiwa na Edna kile kilichotokea.

“Wife usiwe na wasiwasi si unaniona nipo fiti”Licha ya jibu hilo Edna hakuonesha furaha.

“Siku nyingine usifanye kama jana”Roma alishangaa hakujua ni nini Edna alikuwa akimaanisha.

“Mke wangu sijakuelewa unachongea”

“Nipo siriasi Roma , usije ukafanya kitendo kama cha jana , sitaki deni kwenye maisha yangu”Aliongea Edna huku akianza kutirikwa na machozi na hakuendelea kukaa , alinyanyua mkoba wake kwani alikuwa ashajiandaaa tayari na kutoka nje.

Hali ile ilimshangaza sana Roma na hakuelewa ni nini kinaendelea kwa mke wake , alimwangalia Bi Wema na alionekana ni kama alikuwa akitaka maelezo.

“Mr Roma usiwe na wasiwasi , atakuwa sawa baada ya muda , kaniambia kilichotokea jana”Aliongea Bi Wema na kuendelea kunywa chai na Roma hakutaka kuuliza Zaidi na yeye aliendelea kunywa chai.lakini akili yake haikutulia kabisa.

****

Ni baada ya kama lisaa na nusu Edna alionekana akiingia ndani ya kituo cha kulelea watoto cha Son and Doughter Ophanage , mrembo huyu siku hii ya jumapili alionekana kutokuwa vizuri kimawazo.

Baada ya kuegesha gari yake alishuka na hapo hapo wattoto walimvaa na kumkumbatia , ni kama walikuwa wakimsubiria na Edna alijikuta mawazo yake yakipungua mara baada ya kuona watoto hawa.

Alibeba mmoja moja na kumuinua juu kwa furaha , lakini muda huohuo, watoto walimuona mwanadada mwingine mrembo aliengia hapo ndani na kumkimbilia huyu mwanadada hakuwa mwingine bali alikuwa ni Najma.

Edna baada ya kumuona Najma alitabasamu na kisha akamsogelea na wakakumbatiana kwa furaha.

“Edna unaonekana hauko sawa leo?”Aliongea Najma aliekuwa amevalia mavazi yake ya kiislamu , alionekana mrembo haswa.

“Kuna mambo yalitokea jana rafiki yangu”Aliongea Eda kwa kiufupi na muda huohuo walisogelewa na Mama Issa na wakasalimiana nae kwa furaha huku akiwakaribisha.

Lakini wakati wakiendelea kuongea kwa furaha , iliingia gari nyingine eneo la maegesho na akashhuka mwanamke mwingine mrembo na huyu hakuwa mwingine alikuwa ni Nasra , alikuwa amependeza kama kawaida yake ,huku na urembo wake ukizidi kumfanya kuonekana wa tofauti kati ya wanawake wengi.

Najma ndio aliekuwa wa kwanza kumkimbilia Nasra na kumkumbatia kwa furaha.

“Hey!Kumbe unafahamiana na Nasra?”Aliuliza Edna kwa mshangao.

“Ndio Edna muda mrefu sana na sisi ni kama mapacha” Edna alijikuta akishangaa Zaidi , hakuelewa wawili hao walikuwa wakifahamiana vipi na Nasra.

“Vipi kazi yako mpya ya ualimu Naj?”Aliuliza Nasra baada ya Edna kuanza kucheza na watoto ambao walikuwa hawataki kumuachia.

“Nimependa sana hapa Nasra , hasa ninapokuwa na watoto hivi najisikia faraja sana,Asante kwa kunitafutia kazi hapa” Aliongea Najma huku wakimwangalia Edna ambaye alikuwa bize na watoto na Nasra alitabasamu baada ya kumuona Rafiki yake kafurahi kwa kazi ya ualimu aliomtafutia ndani ya kito hiko cha Son and Daughter Orphanage.

“Edna anaonekana hayuko sawa leo”aliongea Nasra na kumfanya Najma amuangalie Edna.

“Itakuwa wamekorofishana na mume wake”Aliongea Najma.

“Sidhani , sema Edna nae msiri sana hataki kila siku nikutane na mume wake , sijui anachokificha kwa huyo mwanaume ni nini , au anaona nitamwiba”Aliongea Nasra na kumfanya Najma acheke.

“Najma leo si utanifundisha kupika pia?”Aliuliza Najma baada ya kuwasogelea Nasra na Najma.

“Ndio mnaonaje tukienda soko la Kiwangwa kununua mahitaji kabisa”aliongea Najma na Edna alitabasamu , ukweli ni kwamba Edna hakuwahi kwenda soko la kawaida , yeye mara nyingi ilikuwa ni SuperMarket.

“Namimi jamani , msinitenge”aliongea Nasra na kumfanya Najma amfinye.

“Nani kasema tunakutenga”Aliongea Najma.

Ndani ya dakika chache tu walikuwa ndani ya soko la Kiwangwa , lilikuwa soko dogo lakini lililokuwa limejaza vitu vingi na watu pia walikuwa wengi.

Lakini sasa ni kama wasichana hawa walikuwa kivutio kwa watu waliokuwa ndani ya hili eneo wakifanya manunusi na pia wale ambao walikuwa wakiuza bidhaa.

ITAENDELEA JUMAPILI SAA KUMI ZA JIONI

ENDELEA KULA MTORI NYASMA UTAZIKUTA CHINI

ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 95 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
mpaka jumapili ndugu daaaaah furaha ytu ni kusoma hii riwaya tu sasa mpka jumapili tutaishi kwa majonzi sana
 
Back
Top Bottom