Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Saa sita kamili mchana nitashushasinganojr nipo hapa mapema kabisa mtaalam wetu.
nipo hapa mkuu
mpaka jumapili ndugu daaaaah furaha ytu ni kusoma hii riwaya tu sasa mpka jumapili tutaishi kwa majonzi sanaSEHEMU YA 66.
“Mfalme Pluto kuna jambo halipo sawa kwa Afshar?”
“Unamaanisha nini Diego?”
“Anaonekana kutokuwa na kumbukumbu”Aliongea Diego na kumfanya Roma aongoze njia kuelekea upande wa chumba ambacho The Eagles walikifanya kama sehemu ya kufungia watuhumiwa kwa muda na kuwahoji.
Roma baada ya kumfikia Afshar , alimshika kidevu na kumuangalia machoni.
“Sh***t!, Poseidon yule fala , nilijua tu yupo hapa nchini kwa kazi maalumu na tamaa zake”Aliwaza Roma huku akionyesha hasira zake wazi na kumfanya Diego kushangaa.
“Your Majest Pluto ni nini tatizo”
“Kashafutwa kumbukumbbu , hakumbuki chochote”Aliongea Roma huku akimwangalia Seif ambaye alionekana kama hakuwa akijua kinachoendelea
“Poseidon anajifanya mjanja , ila dawa yake ipo jikoni tukikutana tena lazima nimfundishe adabu”Aliwaza Roma huku akionesha hali ya hasira kwenye macho yake,Poseidon alikuwa amemzidi akili.
“Diego hili swala la Afshar inaonekana kuwa kubwa na tushazidiwa akili , hana thamani tena na hata nikimuua haina maana kwangu, wasiliana na FBI , mfanye utaratibu wa kumkabidhi”aliongea Roma .
“Sawa mfalme Pluto”Aliongea Diego huku akionekana kutoridhishwa na kile kilichotokea .
“Kuna Ripoti nyingine Deigo?”
“Ndio mfalme Pluto , wakati ulipokuwa Japani majambazi walivamia nyumba yako na kwa bahati nzuri tuliweza kuwaintercept kabla hawajamfikia Malkia”Roma alishangaa kwani hio taarifa hana .
“Ni watu gani walioingia nyumbani kwangu?”
“Mfalme Pluto tulifanikiwa kuwadhibiti watatu kwa kuwaua na mmoja tukamuacha hai kwa ajili ya taarifa na katika mahojiano nae ametueleza mtu anaeitwa Elvice ndio aliewaagiza kufanya uvamizi huo”aliongea Diego na kumfanya Roma kupandwa na hasira.
“Unafikiri tukio la leo lina muunganiko na Elvice?”Aliuliza Roma.
“Mfalme Pluto tunauhakika kwa asilimia mia moja swala hili lina muunganiko”.
“Naamini pia hayupo Peke yake, nataka muchimbe taarifa za Abubakari Hamadi pia na mpate ushahidi wote”
“Sawa Mheshimiwa”.
“Kuna maendeleo yoyote ya misheni nilizowapa?”
“Mfalme kuna maendeleo makubwa , lakini bado tunaendelea kukusanya taarifa ili kufanya ulinganifu , nitakupa ripoti muda mchache , naomba utusamehe kwa kuchelewa kwetu”
“Hakuna shida Diego , mna muda wa kutosha wa kufatilia hilo ,,msifanye kwa haraka , nahitaji taarifa inayojitosheleza na ya uhakika”Aliongea Roma na Diego akapiga Saluti.
Bram alimchana Roma sehemu ya bega kwa utaalamu mkubwa na kisha akatoa risasi ,bwana huyu alioneakna sio mtaalamu tu katika maswala ya tarakishi , lakini pia alionekana kuiva katika swala la matibabu kwani ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza.
*****
Ilikuwa ni siku nyingine kabisa , siku ya jumapili na Roma ratiba zake zilikuwa zilezile , kuamka asubuhi na kufanya mazoezi kabla ya mambo mengine.
Muda wa saa mbili kamili alikuwa ashamaliza kujisafisha na sasa alikuwa akishuka chini sebuleni kwa ajili ya kupata kifungua kinywa kilichoandaliwa na Bi Wema.
Edna alikuwepo wakati Roma anashuka , na mrembo huyu leo alikuwa akimwangalia sana Roma wakati akiwa anasogea mezanni.
“Wife mbona unaniangalia sana?”aliuliza Roma huku akimwangalia mke wake na sura yake ya kipole asubuhi hii , alijikuta akikumbuka namna ambavyo Edna alikuwa akilia jana baada ya kupigwa risasi.
“Unaendeleaje na jeraha?”aliuliza Edna huku Bi Wema akimwangalia Roma usoni , alionekana alikuwa ashaambiwa na Edna kile kilichotokea.
“Wife usiwe na wasiwasi si unaniona nipo fiti”Licha ya jibu hilo Edna hakuonesha furaha.
“Siku nyingine usifanye kama jana”Roma alishangaa hakujua ni nini Edna alikuwa akimaanisha.
“Mke wangu sijakuelewa unachongea”
“Nipo siriasi Roma , usije ukafanya kitendo kama cha jana , sitaki deni kwenye maisha yangu”Aliongea Edna huku akianza kutirikwa na machozi na hakuendelea kukaa , alinyanyua mkoba wake kwani alikuwa ashajiandaaa tayari na kutoka nje.
Hali ile ilimshangaza sana Roma na hakuelewa ni nini kinaendelea kwa mke wake , alimwangalia Bi Wema na alionekana ni kama alikuwa akitaka maelezo.
“Mr Roma usiwe na wasiwasi , atakuwa sawa baada ya muda , kaniambia kilichotokea jana”Aliongea Bi Wema na kuendelea kunywa chai na Roma hakutaka kuuliza Zaidi na yeye aliendelea kunywa chai.lakini akili yake haikutulia kabisa.
****
Ni baada ya kama lisaa na nusu Edna alionekana akiingia ndani ya kituo cha kulelea watoto cha Son and Doughter Ophanage , mrembo huyu siku hii ya jumapili alionekana kutokuwa vizuri kimawazo.
Baada ya kuegesha gari yake alishuka na hapo hapo wattoto walimvaa na kumkumbatia , ni kama walikuwa wakimsubiria na Edna alijikuta mawazo yake yakipungua mara baada ya kuona watoto hawa.
Alibeba mmoja moja na kumuinua juu kwa furaha , lakini muda huohuo, watoto walimuona mwanadada mwingine mrembo aliengia hapo ndani na kumkimbilia huyu mwanadada hakuwa mwingine bali alikuwa ni Najma.
Edna baada ya kumuona Najma alitabasamu na kisha akamsogelea na wakakumbatiana kwa furaha.
“Edna unaonekana hauko sawa leo?”Aliongea Najma aliekuwa amevalia mavazi yake ya kiislamu , alionekana mrembo haswa.
“Kuna mambo yalitokea jana rafiki yangu”Aliongea Eda kwa kiufupi na muda huohuo walisogelewa na Mama Issa na wakasalimiana nae kwa furaha huku akiwakaribisha.
Lakini wakati wakiendelea kuongea kwa furaha , iliingia gari nyingine eneo la maegesho na akashhuka mwanamke mwingine mrembo na huyu hakuwa mwingine alikuwa ni Nasra , alikuwa amependeza kama kawaida yake ,huku na urembo wake ukizidi kumfanya kuonekana wa tofauti kati ya wanawake wengi.
Najma ndio aliekuwa wa kwanza kumkimbilia Nasra na kumkumbatia kwa furaha.
“Hey!Kumbe unafahamiana na Nasra?”Aliuliza Edna kwa mshangao.
“Ndio Edna muda mrefu sana na sisi ni kama mapacha” Edna alijikuta akishangaa Zaidi , hakuelewa wawili hao walikuwa wakifahamiana vipi na Nasra.
“Vipi kazi yako mpya ya ualimu Naj?”Aliuliza Nasra baada ya Edna kuanza kucheza na watoto ambao walikuwa hawataki kumuachia.
“Nimependa sana hapa Nasra , hasa ninapokuwa na watoto hivi najisikia faraja sana,Asante kwa kunitafutia kazi hapa” Aliongea Najma huku wakimwangalia Edna ambaye alikuwa bize na watoto na Nasra alitabasamu baada ya kumuona Rafiki yake kafurahi kwa kazi ya ualimu aliomtafutia ndani ya kito hiko cha Son and Daughter Orphanage.
“Edna anaonekana hayuko sawa leo”aliongea Nasra na kumfanya Najma amuangalie Edna.
“Itakuwa wamekorofishana na mume wake”Aliongea Najma.
“Sidhani , sema Edna nae msiri sana hataki kila siku nikutane na mume wake , sijui anachokificha kwa huyo mwanaume ni nini , au anaona nitamwiba”Aliongea Nasra na kumfanya Najma acheke.
“Najma leo si utanifundisha kupika pia?”Aliuliza Najma baada ya kuwasogelea Nasra na Najma.
“Ndio mnaonaje tukienda soko la Kiwangwa kununua mahitaji kabisa”aliongea Najma na Edna alitabasamu , ukweli ni kwamba Edna hakuwahi kwenda soko la kawaida , yeye mara nyingi ilikuwa ni SuperMarket.
“Namimi jamani , msinitenge”aliongea Nasra na kumfanya Najma amfinye.
“Nani kasema tunakutenga”Aliongea Najma.
Ndani ya dakika chache tu walikuwa ndani ya soko la Kiwangwa , lilikuwa soko dogo lakini lililokuwa limejaza vitu vingi na watu pia walikuwa wengi.
Lakini sasa ni kama wasichana hawa walikuwa kivutio kwa watu waliokuwa ndani ya hili eneo wakifanya manunusi na pia wale ambao walikuwa wakiuza bidhaa.
ITAENDELEA JUMAPILI SAA KUMI ZA JIONI
ENDELEA KULA MTORI NYASMA UTAZIKUTA CHINI
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 95 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA
NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346