SEHEMU YA 67
Edna alionekana ile hali ya mawazo aliokuwa nayo kumpotea kabisa, kwa mara ya kwanza Edna alikuwa akifanya manunuzi katika soko la kawaida , kwake ilikuwa ni jambo jipya katika maisha yake , lakini pia lilikuwa jambo ambalo lilimfanya kufurahi.
Kwa namna Edna alivyokuwa akiongea na Najma usingedhania ni yule mwanamke kauzu , hapa Edna alionekana kuwa mwanamke muongeaji , kwani alichangia baadhi ya topic na kucheka na kufurahi, jambo ambalo lilimfanya hadi Nasra ashangae , kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Edna akiwa anafuraha namna hio na kujiachia bila wasiwasi.
Warembo hawa licha ya watu kuwashangaa hapo sokoni , lakini hawakujali sana , walijali kile walichokuwa wakikifanya , Najma alimuelekeza Edna kila kitu ambacho alikuwa akinunua kazi yake katika upishi , jambo ambalo lilimfanya Edna atikie kwa kichwa , kwake kila jambo ambalo alikuwa akiambiwa lilikuwa ni jipya.
Baada ya kumaliza manunuzi waliingia kwenye gari na kutoweka eneo la hapo sokoni na kuelelekea mahali ambapo Najma alikuwa akiishi , na haikuwachukua muda mrefu kufika , kwani Najma alikuwa akiishi nje kidogo na kituo cha kulelea watoto , kwenye nyumba ambazo pia zilikuwa za kituo hiko , ilikuwa ni sehemu ya kisasa kweli , kutokana na muundo wa majengo hayo , Najma alikuwa akikaa Ghorofa ya Sita kwenye Apartment ya vyumba viwili sable na jiko.
Edna aliingia ndani ya chumba cha Najma na kuvaa Traucksuit ya Najma ili asichafue mavazi yake na kisha akapewa na Khanga kujifunga kiunoni na kumfanya Edna kuonekana kama mama wa nyumbani,kwa namna alivyovaa na hata yeye alipojiangalia kwenye kioo alijikuta akitabasamu , kwani ilikuwa ni kama mara yake ya kwanza kuvaa aina hio ya mavazi.
“Unaonekana kama Mama Edna , umependeza na ulivyokuwa mrembo shost;”Aliongea Najma na kumfanya Edna atabasamu na kujisikia vizuti kusifiwa na rafiki yake.
Najma alikuwa ni wale wanawake waliokulia kwenye mazingira ya kujitegemea kupika , hivyo alikuwa vizuri sana kwa mapishi aina mbalimbali na hii ilikuwa rahisi kwake kumuelekeza Edna, na Edna pia alifurahi kwani Najma hakumchukulia kama Bosi , alimchukulia kama rafiki wa levo sawa na yake na hii iliwafanya wawili hawa kujisikia huru kwa kila mmoja.
“Nimekulia katika familia ya kufanyiwa kila kitu na wafanyakazi, nakiri kuna vitu vingi ambavyo nimekosa kuvijua kama mwanamke”Aliongea Edna wakati akimwangalia Najma anavyokata kitunguu.
“Edna huna haja ya kuwaza aina ya maisha uliokulia , cha msingi kila kitu ambacho hukukifanya ni rahisi kujifunza na utakuwa mke bora”Aliongea Najma na Edna alitabasamu.
“Ana roho nzuri halafu mrembo , atakayebahatika kuwa na Najma atakuwa na mke bora”Aliwaza Edna.
Baada ya Najma kumuelekeza kila kitu Edna sasa ilikuwa zamu yake kuanza kupika , aliingia jikoni na kufanya taratibu taratibu kwa umakini wa hali ya juu na kumfanya Najma aliekuwa pembeni atabasamu , kwani alimuona Edna kama mtoto, lakini pia alifurahi kuwa na aina ya rafiki wa namna hio,Najma alitokea kumpenda Edna ghafla na pia kwa Edna hivyohivyo, alikuwa ashapenda kuwa karibu na Najma , kwake ndio rafiki yake wa kwanza ambaye alijisikia kuwa nae huru.
“Edna unaonaje ukipika kingi umpelekee na mumeo?”Aliongea Najma na kumfanya Edna amkumbuke Roma na namna alivyoondoka asubuhi.
“Nitampelekea”Aliongea huku akitabasamu
Saa kumi na mbili na nusu Edna aliingia ndani ya maegesho na kuzima gari lake , huku akionesha hali ya kuridhika baada ya kuona gari zote mbili za Roma zipo.
Roma siku hii ya jumapili hakutoka Zaidi ya kubakia nyumbani , alicheza gemu mpaka muda wa saa nane na kushuka chini kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya kula na kushiba alirudi chumbani kwake na kuwasha runinga huku akiweka chaneli ya CNN na moja ya habari iliomvutia ni habari iliokuwa ikimuonesha malkia wa Wales katika ziara yake ya kikazi nchini Australia.
“Catherine licha ya umri kusogea , lakini bado anaonekana kuwa mrembo”Aliwaza Roma huku akichoshwa na Taarifa ya habari na kuzima runinga na kisha akajitupa kitandani.
*****
Ni usiku wa saa saba za usiku ndani ya jiji la Milan nchini Italy mwaka 2010 ndani ya hosteli za kanisa moja Maarufu ndani ya jiji hili , anaonekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya chumba ambacho hulala wageni , wanaofika kuomba hifadhi wanapoingia ndani ya jiji la Milan,hususani wale ambao hawana msaada.
Sasa ndani ya chumba kimoja anaonekana mwanaume mmoja akimlazimisha mwanamke kufanya nae mapenzi,lakini mwanamama huyo akionekana kutotaka kufanya tendo hilo na mwanaume anakasirishwa na namna ya mwanamke kukataa, wakati mwanaume na mwanamke wanazidi kusumbuana anaingia mtoto wa kike ambaye anaonekana kuwa katika hali ya usingizi na mtoto anaita jina la mama yake kwa nguvu kiasi cha kumgutusha mwanaume ambaye anamlazimisha mwanamke kufanya mapenzi.
“Clark nenda kwenye chumba chako haraka”Aliongea mwanamke kwa hasira , alionekana kutotaka mtoto wake ashuhudie kile ambacho anafanyiwa na mwanaume , lakini mtoto huyu ambaye kwa makadirio ya umri alikuwa si chini ya miaka kumi na tatu anakataa kuondoka na kusogea mpaka kitandani na kumvuta mwanaume shati lake na mwanaume anakasirika sana na kumpiga mtoto bonge la kibao ambacho kinampelekea mtoto kuzirai palepale , mwanamke anogopa na kulia kwa wakati mmoja.
“Pastor pleas..!!”Mwanamke anaomba kuachwa akaangalie hali ya mtoto wake , lakini mwanaume ambaye mwanamke anamuita kwa jina la Pastor anaoneakana kutomsikiliza na kumshika mwanamke vizuri na kumdondosha kitandani na kuanza kuchana mavazi ya mwanamke mpaka kumbakisha na nguo ya ndani, mwanaume anaefahamika kwa jina la Pastor anafakamia ziwa la mwanamke na kuanza kulinyonya kwa pupa huku mwanamke akitoa kilio huku akitaja jina la Clark , mwanaume baada ya kuridhika kunyonya Ziwa alivuta nguo ya Ndani na kuivua na kisha anashusha suruali yake na kutoa mwichi wake wa rangi nyeupe na kisha analengesha katika sehemu za mwanamke huku akiwa amemshika mikono vyema kiasi cha kumfanya mwanamke kutoweza kufurukuta , Baada ya mwanaume anaeitwa Pastor kuona amekaa katika mkao mzuri wa kutimiza haja ya mwili wake, huku akisahau jina lake la Pastor analengesha tararibu, huku mwanamke akifumba macho na alionekana kutotaka kumwangalia mwanaume anaeitwa Pastor machoni kwa kitendo cha kumbaka , lakini mwanaume ile anataka kuingiza dudu lake mara mwanamke anashituka, mara baada ya maji ya moto kumdondokea na kumloanisha kwenye paji lake la uso na sehemu za mwili , lakini anashangaa hayakuwa maji kama alivyodhania bali zilikuwa ni damu , mwanamke anajikuta akitoa yowe la Woga , lakini wakati uleule anajikuta kufumbwa mdomo.
“Shii…”Mwanamke anajikuta akifumbua macho yake kiuoga na kumwangalia mtu ambaye amemfumba mdomo na kushangaa ni kijana mdogo lika la mwanae akiwa ameshikilia upanga mrefu ukatao kuwili ukiwa na damu.
“Who are you?”Lilikuwa ni swali la kiuoga kutoka kwa mwanamke mara baada ya kushuhudia maiti ya Pastor iliokuwa chini ikitapatapa kwa kushindana na kifo.
“Hupaswi kujua , kwani nawewe lazima ufe , sitakiwi kuacha shahidi nyuma”aliongea Mwanaume kijana kwa sauti nzito na kumfanya mwanamke kuogopa sana na kujitoa katika mikono ya mwanamke kijana na kukimbilia alipolala mtoto wake wa kike na kumbeba na kumuweka mapajani , huku mwanamke akiwa uchi , lakini kijana mwanaume hakuonesha hali ya huruma yoyote katika macho yake , kijana ambaye alikuwa na ngozi ya kiafrika.
“Tafadhari naomba usiniue , nitakupa chochote utakachotaka”aliongea mwanamke kwa pupa huku akitoa machozi na akisahau kama alikuwa mtupu , lakini licha ya maneno yake kwa mwanaume kijana yalionekana kutokuwa na maana yoyote na aliangalia upanga wake na kisha akamsoglea mwanamke kwa matayarisho ya kuua.
Mwanaume kijana alionesha hali ya kutokua na huruma kwenye macho yake, kwani aliinua upanga wake juu, lakini kabla ya kutekeleza azima yake mara mwanamke alimwamuru asubiri.
“Wait!!!!”Aliongea mwanamke na kijana mwanaume alimwangalia mwanamke huku akisita kufanya lile alilokusudia na mwanamke ananyanyuka na kukimbilia mkoba wake uliokuwa na nguo na kisha akatoa kitu kama Cheni iliokuwa na kidani cha Duara , kidani ambacho kilikuwa kikionekana kuwa cha Dhahabu tupu na kumkabidhi mwanaume huku akitetemeaka mikono.
“Huu ni uthibitisho wa mimi ni nani , Tafadhari naomba usiniue mimi na mtoto wangu, nitakupa chochote”Aliongea mwanamke na kumfanya mwanaume kijana aliekuwa katika sura ya usiriasi aangalie kile ambacho mwanamke alikuwa akimpa.
“You’re a Princes Catherine who Declared Dead?”Aliuliza mwanaume kwa mshangao huku akishika kile kidani.
“Roma, Roma Amka”Ni sauti ambayo Roma alikuwa akiitambua na kumfanya kushituka kutoka hali yake ya usingizi uliojaa ndoto na kumwangalia Edna aliekuwa amesimama pembeni kwenye kitanda.
****
Edna baada ya kurudi , alisalimiana na Bi Wema na moja kwa moja akaelekea jikoni na kuweka mfuko wake uliokuwa na Hotpot la chakula alichotoka nacho Kiwangwa Bagamoyo.
“Umetuletea nini Miss?”aliuliza Bi Wema kwa shauku na Edna akatabasamu.
“Ni chakula , nilishinda kwa rafiki yangu Kiwangwa leo ,alikuwa akinifundisha kupika”Aliongea Edna huku akionekana kuwa na furaha tofauti na alivyotoka asubuhi.
“Unaonekana kuzoeana na Rafiki yako sana eh , unaonekana kuwa na furaha Edna?”
“Ndio ana roho nzuri sana , nimetokea kumzoea kuliko watu wote niliokutana nao nje ya familia” Aliognea Edna na bi Wema alijikuta akitabasamu , kwake aliona ni hatua nzuri kwa Edna kutengeneza marafiki na hii itamsaidia kupunguza tabia yake ya kujifungia ndani muda wote , lakini pia itambadilisha na kuwa kama mwanamke sio kama CEO.
Edna alirudi jikoni na kusadiana na biWema kuongezea chakula kwa ajili ya usiku.
“Mr Roma leo hajatoka kabisa , kajifungia siku nzima”Aliongea Bi Wema na Kumfanya Edna afikirie kidogo na kisha akatabasamu na kuendelea kusaidia kupika.
Mpaka inatimia saa mbili Edna na Bi Wema walikuwa washamaliza kupika na Roma hakuwa ameshuka Sebuleni bado na Bi Wema aliona hii ni nafasi nzuri kwa Mke kwenda kumuasha mume wake kwa ajili ya chakula.
“Edna kamuamshe mumeo kwa ajili ya chakula”aliongea Bi Wema mara baada ya kuketi kwenye meza na Edna aliitikia kwa kichwa na kisha kupandisha juu , huku Bi Wema aliekuwa chini akitabasamu , alijiona ni mwanamke mwenye mbinu.
Edna alifika kwenye mlango wa Roma na kusimama , kwake tokea Roma afike hakuwahi kuja kugonga huo mlango na ilikuwa kama ni mara ya kwanza kwake kufanya hivyo , baada ya kusimama kwa sekunde kadhaa aligonga mlango kwa Zaidi ya mara tatu , lakini hakukuwa na majibu, jambo lililomfanya apatwe na wasiwasi na akafanya maamuzi ya kusukuma mlango na kuingia ndani , lakini ajabu alimuona Roma akiwa amelala kwenye kitanda akiwa hana habari.
Edna alijikuta akiangaza kulia na kushoto kuangalia chumba cha Roma ambacho kilikuwa kimejaa harufu ya kiume na kupendezwa na mpangilio wa chumba cha Roma , alisogea mpaka kitandani na kumwangalia Roma aliekuwa amelala fofofo.
Edna alijikuta akishangazwa na mgongo wa Roma uliokuwa una michoro ya ‘tatoo’ kubwa ambazo michoro yake hakuwahi kuiona katika maisha yake , lakini pia alizidi kushangaa sehemu ambayo Roma alipigwa risasi , hapakuonesha alama yoyote ya jeraha au kuacha kovu.
“How Thiss Possible?”
SEHEMU YA 68
Edna alizidi kukodolea mgongo kwa umakini kama mtu ambaye hakuwa akiamini na alitaka kuthibitisha Zaidi kama kitu anachoangalia ni kweli , lakini kila kitu kilikuwa vilevile , hakukua na jeraha lolote Zaidi ya Tatoo za ajabu ambazo hakuzielewa, zikiwa kwenye mgongo wa Roma, aliangalia Pete yenye neno ‘Aides’ kwa makini na kwa sekunde kadhaa na baada ya hapo ndipo akili yake ilirudi na kuona aache kukodolea na kumuamsha Roma alieshituka .
“Edna..!!!”Aliita Roma baada ya kumuona Edna aliesimama akimwangalia.
“Chakula tayari , nimegonga haufungui”Aliongea Edna na kisha akageuka na kuanza kutembea na Roma alimwangalia Edna mpaka alivyotoka nje kabisa.
“Leo nimelala sana hadi nimeota miaka iliopita nilivyokutana na Catherine”Alijiwazia Roma na kuvaa tisheti na suruali ya Track na kisha akashuka chini.
Edna alimwangalia Roma kwa kuibia ibia , ni kama mrembo huyu hakuwa akimjua Roma na ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona , alikumbuka tukio la Kunduchi kwa kila kitu kilichotokea , akaunganisha na namna ambavyo Mwili wa Roma usivyokuwa na jeraha lolote la ushahidi kama alipigwa Risasi , akaunganisha na michoro ya ajabuajabu alioiona kwenye mwili wa Roma na kujikuta akiwa ni mwenye kujawa na maswali megni , lakini licha ya kuwa na maswali kedekede hakuwa tayari kuuliza swali ili kupata majibu.
“Anabadilika macho Rangi , anapona haraka ,ana michoro ya ajabu ,anatembea kwa spidi huyu mwanaume ni nani kwanini haniambii chochote”Aliwaza Edna huku akiendelea kula.
“Nimemisi sana chakula cha aina hii Bi Wema , ni kitamu nilikuwa nikipendelea sana kula nikiwa Mbagala”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema atabasamu.
“Kapika Miss Edna”Aliongea Bi Wema na kumfanya Roma amwangalie Edna aliejifanyisha kuwa bize kula.
“Wife usiniambie ndio unavyonilipa kwa kukuokoa jana hivi?”Aliongea na matani yake na kumfanya Edna akose utulivu moyoni , lakini wakati ule ule simu ilianza kuita na kumfanya anyanyuke na kuisogelea.
Mpigaji wa simu alikuwa ni ATHENA ,Edna alisogea mpaka eneo la masofa na kusimama na kuongea ni kama hakuwa akitaka Bi Wema na Roma wamsikie.
“Boss tupo tayari kuachia bomu”Ilisikika sauti upande wa pili.
“Okey! Hakikisheni hakuna makossa yanafanyika , lazima mpango wetu ufanikiwe kwa asilimia mia moja”
“Sawa Bosi”Baada ya Edna kuongea hivyo alikata simu na kurudi kuendelea kula , huku Roma akimwangalia Edna na Edna hakujali macho ya Roma.
****
Ilikuwa ni siku nyingine ,Siku ya Jumatatu , siku ambayo watu wengi kama kawaida , hawakuwa wakiipenda siku hii kutokana na sababu zao , muda huu wa saa moja kamili ndani ya jumba la kisasa Makongo juu alionekana kijana Abuu akiwa amelala , huku siku hii ikionekana sio ya kawaida kwake , kwani kwa mazoea yake ni kwamba muda wa saa moja kamili tayari ashakuwa macho na alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kwenda kazini , lakini siku hii ye leo alionekana kulala muda mrefu.
Wakati bwana huyu akiendelea kulala , mara simu yake ilianza kuita mfululizo kiasi cha kumuamsha bwana huyu na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Isaack , CEO msaidizi, kabla ya kupokea aliangalia saa ya ukutani na kuona muda haukua umeenda sana licha ya kwamba alikuwa amelala muda mrefu.
“Kuna nini Isaack?”
“Boss .. hali sio shwari?”
“Unamaanisha nini?”aliongea Abuu huku usingizi ukimkata moja kwa moja.
“Hisa za kampuni zimeshuka isivyokawaida baada ya soko kufunguliwa”Aliongea Isaack na kumfanya Abuu akate simu na kuingia kwenye ‘Platform’ ya biashara za soko la hisa na kuangalia Chati ya kampuni yake na hapo ndipo macho yalipomtoka kwani ,kampuni yake imefungua na gepu kubwa chini ya mstari wa ‘Dow Jones’ , lakini licha ya kufungua chini bado soko lilionekana kushuka.
Alijikuta akiamka haraka na kukimbilia bafuni na kujisafisha haraka haraka na kurudi ndani na kuvaa haraka sana , alitumia dakika kumi mpaka kumaliza na kisha akatoka na kuingia kwenye gari yake.
“Shi**t kuna mtu anacheza na soko la hisa za kampuni yetu”Aliongea huku akikanyaga pedeli.
Ndani ya dakika chache tu alikuwa ashafika maegeshoni chinin ya jengo hili kubwa la kampuni .
Ndani ya kampuni hii , wafanyakazi walionekana kuwa bize kweli, wengi walionekana kushughulika na tatizo lililojitokeza siku hii ya jumatatu asubuhi , ule uchomvu wa wikiend waliokuwa nao wote ulikuwa umewaishia na sasa walikuwa wakifanyakazi kwa juhudi zote.
Abuu moja kwa moja alienda kwenye Idara inayohusika na usimamaiaji wa hisa za kampuni na alivyoingia hapa ndani , vijana waliokuwa wakihusika na kazi hio walikuwepo wakiwa bize kuangalia namba zilizokuwa zikionekana kwenye skrinni hizo kubwa huku wakichezesha vidole vyao kwenye tarakishi na walionekana waliikuwa wakifanya juu chini kurudisha soko katika hali ya kawaida.
“Isack nilezee hali halisi”Aliongea Abuu ambaye leo hii hata tai alikuwa amesahau.
“Kuna hii taarifa ndio inayofanya Hisa kushuka , japo ipo kwenye uvumi , lakini wafanyabiashara wanaichukulia kama moja ya taarifa sahihi na kuwafanya watupe hisa zetu sokonni kwa bei ya hasara”Aliongea Isack huku akimuonesha Abuu taarifa.
Taarifa ambayo ilikuwa ikisambaa mtandaoni ilikuwa ikionesha kampuni ya JR grupu walikuwa wakijihusisha na biashara ambazo ni haramu , ndio taarifa ilionekana kwenye kishikwambi alichoshikilia Abu.
“Nani katoa hii habari?”Aliuliza Abu.
“Mr Abubakari , hio sio swali la kuuliza maana taarifa hii tayari ipo mitandanoni na inaathiri soko pakubwa , tunatakiwa kufanya kitu, Nashauri tutoe taarifa ya kukataa uvumi unaoenea”
“Fanyeni hivyo sasa mnasubiri nini?”Aliongea Abu kwa hasira na ndani ya madakika kadhaa tu taarifa hio ilitolewa na uzuri ni kwamba wafanya biashara wengi wa hisa wanachanzo kimoja cha kupokea taarifa hivyo ukitoa taarifa ni rahisi kwa wafanyabiashara hao kuiona.
“Boss !”aliita kijana mmoja aliekuwa akihangaika na tarakishi yake,lakini wote walishangaa kile walichokuwa wakiona kwenye Skrini , kwani licha ya kutoa taarifa hio soko lilishuka tena.
“Nini kinaendelea?”.
“Athena kauza kiasi kikubwa cha pesa kwa hasara na kufanya soko lishuke tena chini”Aliongea kijana huyu na Abuu alimwangalia Isaack.
“Nilishindwa kupata mawasiliano na huyu Athena mpaka sasa”Aliongea Isaack ambaye ni kama alijistuikia.
“Tumieni kiasi chote cha pesa tulichonacho kununua hisa zisiende chini’
“Abu , sio kama napinga maamuzi yako lakini hatuwezi kutumia kiasi chote cha kampuni kushindana na watu wengi , tutabakiwa watupu.
“Fanya kama nilivyoelekea , zipo benki ambazo zinaweza kutukopesa”Aliongea Abuu na vijana walivuta pesa yote benki na kuingiza sokoni na hii ni mbinu ya kuadanganya wafanyabiashara wadongo kwamba soko linapanda.
Upande wa pili ni kama walikuwa wakisubiriwa na Athena kuingiza hela zao ndani ya soko , kwani mwanzoni Athena alikuwa ameweka asilimia kumi na moja ya hisa zake , lakini baada ya JR kuweka pesa zao kwa minajiri ya kununua hisa zao , Athena akauza tena kwa bei ya hasara kwa asilimia kumi na mbaya Zaidi ni kwamba Athena alionekana kukubalika kwa wafanyabiashara kwani kitendo cha kuuza tu watu na wao ni kama waliambiwa wauze m waliuza hisa kwa bei ya hasara na kufanya soko lizidi kushuka.
Wakati huo huo aliingia Mzee Alex aliekuwa anahema hapondani ya chumba na kufanya Abu amwangalie baba yake kwa wasiwasi.
“Abubakari nini kinaendelea?”Aliuliza mzee huyu kwa wasiwasi , kwani kwenye maisha yake tokea aanzishe kampuni yake hakukuwahi kutokea tukio kama hilo na hio ilikuwa ni mara ya kwanza.
“Chairman , kuna mtu anaonekana kucheza na soko la hisa zetu kiasi kwamba kutumia taarifa ya uongo inaysambaa mtandaoni , na kuuza hisa zetu kwa hasara na hii imefanya watu kumuamini sana na hivi sasa soko linaendelea kushuka , licha ya kwamba tumeingiza kiasi kikubwa cha pesa sokoni kununua hisa zetu ili kuzipandisha thamani , lakini bado inaonekana kutotosha.
“Mnafikiri ni kiasi gani cha pesa ambacho kinaweza kukabiliana na hio hasara”Aliuliza Mzee Alex na vijana walipiga mahesabu.
“Bilioni 500 Boss”aliongea kijana na kumfanya mzee huyu amwangalie Abu , ni kama walikuwa wakijiuliza ni kwa namna gani wanaweza kupata kiasi hiko cha pesa ili kurudisha soko.
“Chairman! Naamini kabla hatuja weka pesa Zaidi sokoni , tuagalie ni namna gani tunaweza kukanusha kwa ushahihidi kwamba taarifa inayosambaa mtandaoni sio ya kweli”Aliongea Isaack na Mzee huyu aliona ni kweli , lakini alitaka yote yafanyike kwa pamoja.
“Abu wasiliana na benki ya ABSA watukopeshe Bilioni 600 haraka sana , Isaack wewe itisha mkutano wa waandishi wa habari na mimi mwenywe nitaongea na waandishi wa bahari kama kampuni yetu haihusiki na tuhuma zinazoendelea mtandaoni”Aliongea mzee Alex na Abu na Isaack kila mmoja alitoka kwenda kutimiza maagizo.
“Mr Abubakari , tunatambua JR kama moja ya wateja wetu wa muda mrefu , lakini tumekuwa tukiangalia mwendendo wa soko la hisa ya kampuni yenu kwa Zaidi ya siku zote tatu na hakukua na mipango chanya ya kampuni kuimarisha hali inayoendelea na leo jumatatu hali imezidi kuwa mbaya, hivyo kwa heshima na taadhima tunakataa ombi la kutoa kiasi cha shilingi bilioni 600”Ilikuwa ni sauti ya mwanadada mrembo iliokuwa ikisikika kwenye masikio ya Abuu na kumfanya bwana huyu atoe tusi na licha ya kusikia sauti hio kuwa nzuri siku zote aombapo mkopo , lakini leo hii kwa mara ya kwanza aliona mwanamke huyo alikuwa akizungumza kama mwanaume.
*****
Edna alifika mapema kazini na kusalimiana kikauzu na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni na kisha akaelekea ofisini kwake, baada kama ya nusu saa alifika Roma Ramoni na gari yake aina ya Aud na kisha akapaki na kuingia ndani ya ofisi yake , huku kichwani akiwa na mawazo ya kwenda kucheza gemu.
Leo hii wafanyakazi wa kampuni walikuwa wakimwangalia kwamacho ambayo hayakuwa ya kawaida , kwani walikuwa wakijua mafanikio alioyafanikisha kwa kampuni.
Mtu wa kwanza kumshobokea Roma mara aada ya kufika ndani ya kampuni alikuwa ni Recho , leo mwanadada huyu alikuwa amejipodoa kuliko isivyokawaida , na mbaya Zaidi ,alikuwa amevalia nguo fupi mno kiasi kwamba hata wafanyakazi wenzake walikuwa wakishangaa inakuwaje mwanadada huyu leo kuvaa aina hio ya mavazi , lakini hakuna aliekuwa akijali sana ukizingatia kampuni ilikuwa na wafanyakazi wa kike kwa asilimia kubwa.
Roma alisalimiana na Benadetha aliekuwa bize kutoa maelekezo kama kawaida , na Benadetha alimsalimia Roma na kuendelea na mishe zake.
“Handsome !Mambo?”Alisalimia Recho kwa mapozi na kusogeza kiti chake kabisa karibu na meza ya Roma huku akimrembulia Roma, huku kijisketi kikiacha mapaja wazi kitendo kilichomfanya Roma ameze mate mengi.
“Poa! Mrembo mambo”
“Safi za Japani?”
‘Njema kabisa, umekua mrembo sana leo Recho kuliko siku zote”Aliongea Roma huku akiweka mkono kwenye paja la Recho na Recho aliuangalia mkono wa Roma na akatabasamu.
“Kawaida tu mbona”.
“Hapana hii ya leo sio kawaida , halafu unanukia vizuri mno”
“Asa..nte. eh” Aliongea Recho huku akishikwa na msisimko wa ajabu baada ya Roma kupelekea mkono karibu na ua la mwanadada huyu na kusugua na hakukua na mtu aliekuwa akijua kile kinachoendeleana Recho alijizuia kutoa sauti.
Recho nguo yake ya ndani ilikuwa imeshaloa muda mrefu sana , na alitamani mechi kwa muda huo huo na Roma alitabasamu kifedhuli baada ya kuona kampatia Recho.
“Ukome kunitega?” Aliwaza Roma lakini muda huo huo alikuja Miss Aiport na Roma alimuona wakati akiingia hapo ndani na kuacha alichokuwa akifanya na kugeukia tarakishi yake na hata kwa Recho pia , lakini jicho lilikuwa limemshuka mwanadada huyu kiasi kwamba hakuwa akijielewa kabisa na pia alikuwa mwekundu.
Miss Aiport au Monica baada tu ya kufika kuna mazingira hakuyaelewa , alimwangalia Roma kwa macho makali na kisha akamgeukia Recho na kuangalia kimini chake na kujikuta akichefukwa na Roho.
“Unaitwa na bosi”Aliongea mwanadada huyu na kisha aligeuza na kuanza kutembea kwa haraka haraka huku akiacha sauti za viatu nyuma na kuwafanya wafanyakazi hawa wa kitengo cha Public Relation kumwangalia na kisha kuendelea na kazi yake.
Roma alinyanyuka na kisha akamkonyeza Recho na kuondoka
SEHEMU YA 69
Roma aliingia ofisini kwa mke wake na kumkua Edna aliekuwa bize kama kawaida , lakini Edna alipomuona Roma alimpa ishara ya kukaa na Roma hakutaka kuongea sana alikaa huku akimwangalia Edna.
Baada ya kama dakika chache kupita Edna alionekana kumaliza kile alichokuwa anafanya na kisha akachukua ufunguo wa gari na kumpatia Roma.
“Kanisubiri maegeshoni , kuna sehemu tunaenda”Aliongea Edna huku akimkabidhi Roma ufunguo wa Gari , Roma alimwangalia mrembo huyu na kisha akatabasamu na kuuchukua kisha akatoka.
Roma alishuka mpaka kwenye eneo la maegesho ya magari ya viongozi wa juu wa kampuni na kisha akalisogelea gari la mke wake na kufungua mlango na kisha akaingia.
“Gari inanukia hii”Aliwaza Roma huku akinusa harufu ya perfume ya Jasmine inayonukia kwenye gari ya mke wake.
Aliwaza ni safari gani alikuwa akielekea na mke wake asubuhi hio , kwani haikuwa kawaida kuondoka wakiwa kazini pamoja , ndani ya kama dakika kumi na moja hivi,Edna alievalia vazi lake la Pink refu na suruali nyeupe alitokea , alikuwa akitembea kimadaha na kujiamini mno na kumfanya Roma amwangalia mwanamke huyu kwa jinsi alivyokuwa mrembo.
“Endeesha uelekeo wa kibaha”Aliongea Edna huku akikaa na kuchukua kishikwambi chake akiandelea kiufanya kazi.
Roma alifurahishwa na urahisi wa gari hii ya mke wake , ilikuwa ikitembea kama haitaki hivi.
Ndani ya madaika kadhaa tu walikuwa wapo kibaha kimya kimya.
“Wife wapi nielekee au ninyooshe Chalinze moja kwa moja?”
“Hapana ukifika kibaha kwa Mathaisi kunja kulia kuingia sehemu inayofahamika kama Mji wa Kisasa”Aliongea Edna na Roma akaitikia kwa kichwa kwa maelekezo ambayo alikuwa amepewa na kuendelea kuendesha..
Barabara ya kuelekea Mji wa kisasa ,ilikuwa bora sana , ilikuwa imejengwa kwa utaalamu wa hali ya juu a na jambo hili lilimfurahisha Roma sana na kujisikia vizuri wakati wa kuendesha gari.
Ndani ya dakika chache tu walikuwa nje kabisa ya Uzio wa Mji wa kisasa na mlinzi alionekana kujua gari hio kwani alifungua geti na kupita.
“Mke wangu tunafanya nini hapa?”Aliuliza Roma huku akiwa anaangalia majengo haya ghorifa kumikumi yalioenda hewani , ni majengo ambayo yalikuwa yamejengwa kwa ustadi wa hali ya juu sana , huku kukiwa na mazingira tulivu mno , eneo la maegesho ndani ya mji huu magari yalikuwa ya bei kubwa pekee na hii ilionyesha kwamba watu waliokuwa wakiishi ndani ya haya majengo ya Apartment hawakuwa wanyonge kipesa.
“Haya ni majengo ya Kampuni yangu , hivyo ni sahihi kwa mimi kuwa hapa”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae kwani ni majengo mengi yaliokuwa hapo ndani Zaidi ya kumi na yote yakiwa yameenda hewani , aliishia kujisemea mke wake anapesa.
Baada ya kukata kushoto upande mwingine walikuja kusimama kwenye jengo ambalo kimuundo lilikuwa tofauti na mengine, na hili lilionekana kupendeza sana.
“Madam!”Aliita mwanamke mmoja mrembo ambaye alimfanya Roma amshangae na huyu mwanadada hakuwa mwingine bali ni Suzzane na Roma alikuwa akimkiumbuka vyema kwani ndio aliemfuata Mbagala kwa mara ya kwanza.
Suzzane alimwangalia Roma kwa macho yakutompenda na Roma hakujali na wote kwa pamoja waliingia kwenye Lift na ndani ya dakika kadhaa walikuwa ghorofa namba 15 ghoofa ya mwisho.
Baada ya kutoka , walisogelea mlango mwingine ambao Suzzane alitumia ‘Fingerprint’ pamoja na Jicho kuufungua mlango huo na ukafunguka na hapa ndipo Roma aliposhangazwa na muonekano wa hapa ndani.
Ilikuwa ni sehemu ambayo ilikuwa na mpangilio kama wa idara ya kijasusi lakini pia na kampuni kwa wakati mmmoja , mbele kabisa kulikuwa na bango kubwa lililoandikwa kwa jina la ATHENA.
“Wife hapa ni wapi?”Aliuliza Roma akimwangalia Edna ambaye alikuwa akitembea kwenye Korido ndefu na kisha wakasimama kwenye mlango wa chumba , Suzzane alitumia utaratibu uleule wa awali kufungua chumba hicho na wakaingia hapa ndani na hapo ndipo Roma alipozidi kushangaa Zaidi baada ya kukuta vijana wakizungu na kiafrika kuwabize na tarakishi ambazo zimefungwa kwa ustandi wa juu , huku tarakishi hizo zikionyesha chati za Masoko ya hisa duniani ambayo namba zake zilikuwa zikishuka na kupanda na vijana walionekana kuwa bize . utadhani walikuwa wanadukua taarifa flani.
“Madam karibu”Aliongea kijana ambaye alikuwa amevaa kanzu na koti jeusi na kibarakashia , mweeupe hivi.
“Amiri kutana na mume wangu Roma Ramoni”aliongea Edna na kufanya vijana waliokuwa bize, kugeuka wote kwa pamoja , ni kama walikuwa hawajasikia maneno hayo kutoka kwa bosi wao na hata kwa Amiri mwenyewe alishangazwa na bwana aliekuwa mbele yake , kwani alikuwa akimfahamu Roma kama mfanyakazi aliefanikisha saini ya mkataba wa Yamakuza kwa faida kubwa, lakini sasa alivyotambulishwa alishangaa , hakuamini bosi wake mrembo ana mume wa aina hio.
“Roma huyu ni Amiri Director wa kitengo changu cha ATHENA”Roma alishangaa huku akimwangalia Bwana Amiri.
“Nafurahi sana na imekuwa heshimwa kwangu kukutana na wewe mume wa Bosi”.
“Hata mimi”Aliongea Roma kwa kifupi na kumwangalia mke wake na Edna alijua Roma alikuwa na maswali mengi na ndio maana alikuwa akimwangalia, lakini hakutaka kuongea kwanza alimwangalia Amiri.
“Mpango wetu unakwendaje?”
“Ni kama tulivyotegemea Madam , mpango unaenda vizuri sana”Aliongea Amiri kwa heshima.
“Okey , leo nipo hapa mpaka swala hili naliona mwisho wake na nitakuwa na mume wangu hapa”Aliongea Edna na kisha akamgeukia Roma huku Amiri akiitikia kwa kichwa na kurudi alipokua amesimama.
“Mke wangu nadhani uanze sasa kunipa maelekezo ya kutosha”
“Ndio maana nimekuleta hapa Roma”Aliongea Edna .
“Hiki ni kitengo cha siri cha kampuni kinaitwa ATHENA kama ulivyoona jina lake , Mama ndio alieanzisha kitengo hiki miaka mitano nyuma baada ya kumaliza ujenzi wa mji huu wa kisasa , kazi ya kitengo hichi nikukusanya taarifa zote muhimu ambazo zinamchango chanya na hasi kwa kampuni , kwa zile taarifa chanya zinafanyiwa kazi kama fursa kwa kampuni na kwa zile hasi tunaangalia ni namna gani ya kuzifanya kuwa chanya ili zithiathiri maendeleao ya kampuni.
“Hawa unaowaona wote hapa ni ‘Traders’ ambao kampuni imewaajili kwa kuwatoa kwatika mataifa mbalimbali , wengi wao hapa ni wajuzi katika maswala ya masoko ya Hisa ambao wamemaliza katika vyuo vikubwa duniani , ni waajiriwa ambao wanapewa mshahara mkubwa Zaidi kuliko mfanyakazi yoyotea wa Vexto na hii yote ni kutokana na kazi yao kuwa ya masaa mengi , na jengo hili lote ni la kwao , wanaishi hapa na kupata huduma zote muhimu”Roma alishangaa.
“Kwa hio mke wangu hawa wote ni wataalamu wa maswala ya masoko ya kimatiafa pekee?”
“Hapana hapa wapo ambao pia ni wahandisi wa maswala ya Computer , wapo wataalamu wa udukuaji pia wa kiwango cha kimataifa”Alivuta Pumzi na kisha kuendelea.
“Hii ni sehemu ambayo imetumia uwekezaji wa hali ya juu sana na uwepo wa kitengo hiki hapa Tanzania haufahamiki kwa mtu yoyote Zaidi ya hawa wafanyakazi , mimi , Marehemu mama na Wewe ni mtu watatu”Aliongea Edna na kumfanya Roma ajisikie vizuri , kwani kwa hatua hii aliona Edna alikuwa akimwamini na ndio maana amemleta hapo ndani.
Baada ya maelekezo hayo mafupi Edna aliwasogelea vijana waliokuwa wapo kazini na kuendelea kuangalia kile kinachoendelea.
“Amiri nataka ile record ya sauti ianze na pia nataka msambaze taarifa ya sauti ya Abubakari kutaka kunisainisha mkataba feki na kampuni ya Yamakuza”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae.
“Edna unamaanisha nini kusema mkataba feki , inamaana ulijua mapema kama mkataba ni feki?”Aliuliza Roma kwa mshangao na Amiri alimgeukia Roma.
“Ndio Mr Roma mkataba wa Yamakuza tulikuwa tunajua ni Feki na ndio maana Madam akakataa kuhusuika kwenda kutia sahihi”
Roma alijikuta akishangaa mno swala hilo , hakujua kabisa kama mke wake siku zote hizo alikuwa amekaa na siri hio moyoni , na swala zima la kwenda Japani alikuwa anajua kama tulikuwa wakienda kusaini mkataba feki.
“Edna inamaana yale yote tuliokuwa tunapitia Kule Jaoani ulikuwa ukijua kama yatatokea?”Aliuliza Roma .
“Roma najua unajihisi kama nilikuongopea , lakini nilifanya yote kwa makusudi maalumu”
“Huna haja ya kujielezea Edna , lakini ulichofanya sio vizuri , hivi unajua ni kidogo tu Dorisi angedhurika baada ya siisi kushambuliwa , je nisingekuwepo ingekuwaje?”Aliuliza Roma huku akiweka uso wa siriasi ambao Edna hakuwahi kuuona.