singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
- #461
Jioni ya leo nitawapostiaMkuu singanojr jumapili naona parefu sana tushushie hata episode moja leo [emoji42]
Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jioni ya leo nitawapostiaMkuu singanojr jumapili naona parefu sana tushushie hata episode moja leo [emoji42]
Balikiwa
tutashukuru ndugu
mkuu jioni ndo hii
YAH AWEKE DUDE...mkuu jioni ndo hii
[emoji848]SEHEMU YA 71
Abu alijikuta akitoa matusi ya nguoni mara baada ya kila benki ambayo alikuwa akiwasiliana nao kwa ajili ya mkopo kumwambia jibu linalofanana , alijikuta akichefukwa na Roho.
“Hawa wapuuzi wote naona wameambiana kutukazia , wase**ge kweli”Alitukana Abu huku akitoka kwenye ofisi yake na kuelekea upande ambao alimuacha Mzee Alex.
“Vipi Abu umefanikiwa?”Aliuliza Mzee Alex ambaye alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi , kwani kwa sura aliokuwa ameiona kwa Abu ilimwambia kila kitu.
“Mzee wananiambia jibu linalofanana , wanasema hawatoweza kutukopesha”Aliongea Abu na kumfanya Mzee Alex kukunja sura na hapohapo alitembea na fimbo na mkongojeo wake na kutoka ndani ya ofisi.
Mzee Alex aliona akafanye jambo hilo mwenywewe huku akidhania watu wa Benki watakuwa wamempuuza Abubakari na kwake watakuwa na heshima na kumpatia mkopo , lakini ajabu ni kwamba jibu lilikuwa ni lilelile , hakuna benki ambayo ilikuwa tayari kutoa kiasi cha bilioni 600 za kitanzania.
“Mr Alex tunajua umekuwa mteja wetu kwa muda mrefu sana , lakini hili swala la kinachoendelea kwenye kampuni yako ,linatuweka kwenye nafasi mbaya ya kufanyia kazi ombi lako , lakini kwakua wewe nni mteja wetu tunaweza kukuunganisha na mtu ambaye anaweza kukusaidia katika hili na yupo tayari kwa kuwekeza ndani ya kampuni yako licha kwamba hisa zinashuka , kama upo tayari nifanye nae mawasiliano na nikuunganishe”
Ilisikika sauti ya kirembo ambayo mwanzoni haikuwa imemsisimua mzee Alex lakini ilivyofika karibia mwisho , ilianza kumsisimua.
“Ndugu Meneja itakuwa vyema sana kama utanisaidia katika hilo nipo tayari kufanya kazi na huyo muwekezaji kama ataweza kutupatia keshi ndani ya muda mfupi”aliongea mzee huyu kwa pupa, lakini muda huohuo alifika Abu ambaye alikuwa anahema kama mtu aliekimbia mbio ndefu , Mzee Alex alimwangalia Abu na kujiuliza huyu mpumbavu anahema nini juujuu kama Bata.
“Miss Meneja nipo tayari kuonana na huyo muwekezaji”
“Sawa Mister Alex nipe dakika moja nifanye mawasiliano , halafu nipigie ndani ya dakika mbili”Sauti hio ya kirembo kutoka kwa Miss Meneja ilikatika kwenye masikio ya mzee Alex.
“Haya niambie wewe mpumbavu unahema kama Dubu, umeshindwa hata kuwa na sauti ya kuombea mkopo , ni nini utakikamiisha Abu kwenye maisha yako”Abu hakujali maneno ya Kejeli ya baba yake.
“Baba ni Edna!”Aliongea Abubakari na kumfanya Mzee huyu kushangaa.
“Unamaanisha nini?”
“Edna ndio anatufanyia uhuni baba, kuna taarifa nyingine ya sauti yangu ipo mtandaoni juu ya mpango wa mkataba feki”Aliongea Abuu na mzee Alex akampiga kikumbo Abu na kupita kuelekea kwenye chumba cha masoko ya Hisa.
“Ukiingiza kampuni kwenye mfumo wa hisa hii ndio , shida , yaani watu wapuuzi sana, taarifa haijathibitishwa lakini wanaenda nayo hivyohiyo”aliongea mzee Alex kwa hasira.
“Tunapaswa kufanya nini baba?”
“Nishapata muwekezaji ambaye yupo tayari kutupatia pesa ndani ya muda mfupi, nitaenda kukutana nae mimi mwenyewe na wewe utabaki hapa na wasiliana na Isack amefikia wapi kwenye maandalizi na waandishi wa habari”Aliongea mzee huyu na Abubakari alishangaa kwa taarifa ya baba yake kama ameshapata muwekezaji , alijiona kweli anasafari ndefu ya kumfikia baba yake , aliitkia kwa heshima.
Mzee Alex aliwasiliana na Benki na aliunganishwa moja kwa moja na mfanyabiashara huyo na kuambiwa wakutane hoteli ya Eunice hoteli iliopo Kimara.
“Endesha gari haraka wewe mpuuzi”
“Sawa Bosi”alijibu dereva wa mzee Alex huku akiwa makini na usukani akielekea Kimara.
Ndani ya madakika kadhaa tu walikuwa nje ya jengo hili la kisasa la hoteli ya hadhi ya nyota tano iliokuwa ikifahamika kwa jina la Eunice Hotel.
Baada ya mzee huyu kutoka kwenye gari , harakaharaka alitembea kuingia ndani ya hoteli hii, na watu waliokuwa wakimjua walimshngaa kwa mzee huyu kuwa na haraka isioyakawaida kwa siku ya leo.
Mister Alex alienda mpaka kwenye chumba maalumu cha VIP na kisha akaingia kama alivyokuwa amepewa maelekezo na muwekezaji na hapo ndipo alipokutana na kijana wa kizungu alievalia miwani yake na suti ya ‘Navyblue’ ,alikuwa ni kijana wa makamo umri sio chini ya miaka therathini hivi , alionekana kuwa profesheno kwa namna ambavyo alikuwa ameshikilia glass ya Wine.
“Welcome Mr Alex , it`s pleasure to meet you in person , I am Justin Bieber Assistant Managing Director of Athena Trading Company From Paris”Mzee kwanza alishangaa mara baada ya kusikia jina la Athena, mzee huyu ni kama alikuwa ashalisikia mahali lakini hakuwa na kumbukumbu vizuri.
Ndio mzee Alex hakuwa na taarifa kamili ya mtu anaefahamika kwa jina la Athena , kwani Abubakari alisahau kumpa maelekezo ya kutosha Mzee Alex juu ya mtu ambaye alikuwa akicheza na hisa za kampuni yao.
“Nimefurahi kukutana na wewe Mr Justin , unaonekana kijana mdogo lakini mwenye mafanikio makubwa”
“Asante Sana Mr Alex , nipo hapa kwa ajili ya kumwakilisha bosi , niseme kwamba kwa Zaidi ya miaka mine Bosi alikuwa ni mwenye kutamani kuwekeza ndani ya Tanzania na kutokana na nia yake amejikuta ni mtu wa kuvutiwa sana na Kampuni ya JR na moja ya sababu kubwa ni kutokana na malengo na mikakati ya kampuni ya JR ndani ya miaka ijayo , pamoja na uongozi thabiti”
Mzee Alex alijikuta kichwa kikivimba , kwanza alijisikia vizuri kwa kampuni yake kutambulika kimataifa kwani Ufaransa ni mbali sana , lakini pia alijisikia faraja kwa kuona kwamba makampuni makubwa kutoka Ufaransa yamevutiwa na malengo ya kampuni yake.
“Nimefurahishwa sana na jambo hili , kuona kampuni kama Athena kutoka Ufaransa kuvutiwa na uwekezaji wangu , niseme tu kwamba sisi kama JR group tuna malengo makubwa sana kwa baadae na ijapokuwa tunapitia kipindi kigumu kwa sasa lakini ni swala la muda tu kwa sisi kurudi kwenye mstari kwa spidi ya Roketi”
“Mr Alex mambo ya aina hio ndani ya kampuni ni kawaida , sana mnachotakiwa tu ni kusimamia mipango ya kampunni na kuhakikisha mnaimarisha uhusiano wa kampuni na wateja wenu hii ndio nguzo kubwa ya mafanikio kwa kampuni na naamini vitu hivyo mtavifanyia kazi na ndio maana nipo hapa kwa ruhusa ya bosi”
Wakati mzee Alex anaendelea kuongea na Muwekezaji kutoka kampuni ya Athena , meseji iliingia kwenye simu yake na aliitoa na kuangalia jina.
“Baba Hisa zinazidi kuporomoka , inabidi tupate kiasi cha pesa haraka” Mzee Alex aling`ata meno na kujisemea hili lipumbavu nitalifukuza kwenye kampuni yangu baada ya tatizo hili kuisha .
“Okey! Mr Justin ni kiasi gani ambacho unaweza kuwekeza kwetu?”Jamaa huyu kwanza alitabasamu na kisha akaangalia mkoba wake uliokuwa pembeni na kuchomoa karatasi na kisha akamkabidhi Mzee Alex.
Mzee macho yalimtoka , hakuamini kampuni ya Athena inapesa kiasi cha kutaka kuwekeza kiasi hiko cha pesa kwenye kampuni yake,Kilikuwa ni kiasi cha Dola bilioni moja.
“Mr Justin unamaanisha kwamba Bosi wako yupo tayari kuwekeza kiasi hiki kwenye kampuni yangu?”
“Ndio Mr Alex ,Au ni kidogo niongeze?”
“Hapana sijamaanisha hivyo hiki ni kiasi kinachotosha sana na nipo tayari kusaini mkataba”.
“Mr Alex unapaswa kusoma kwanza vipengele vya mkataba kabla ya kutia sahihi ili isije ikaleta shida mbeleni”Aliongea kijana huyu na kisha akatoa mkataba wa kiuwekezaji na mzee Alex kutokna na kuwa na haraka alipitia haraka haraka na kisha alitingisha kichwa baada ya dakika tano za kusoma.
“Mr Alex umeridhika na vipengele vya mkataba?”
Aliuliza Justine na kumfanya mzee huyu kufikiria kwa dakika kadhaa , kwanza kabisa alikuwa na hofu , kwani kiasi cha pesa ambacho muwekezaji anataka kuingiza kwenye kampuni kilikuwa kikubwa , aliona ni swala ambalo alihitaji kufikiria kwa muda lakini tatizo hakuwa na muda wa kufikiria , kwenye kampuni yake Mzee Alex alikuwa akimiliki asimilia sabini za hisa zote huku asilimia therathini ni wawekezaji wengine , kiasi cha Dola bilioni moja kama angeruhusu kiingie kwenye kampuni ni kama atakuwa ameuza asilimia therathini za hiza za kampuni kutokana na kushuka kwake.
“Hata kama akimiliki asilimia therahini ni bora , kwanza nitapata mtaji wa kupanua zaidi biashara kimataifa , lakini pia nitakuwa na asilimia arobaini za hisa za kampuni na kuendelea kuwa mmiliki mwenye hisa nyingi”aliwaza Mzee Alex na kisha akaangalia mkataba uliokuwa mbele yake huku Justine aliekuwa kwenye pozi la tabasamu akimwangalia mzee huyu.
“Mr Alex kama haujaridhika , unaweza kuchukua muda wako kusoma vipengele vya mkataba na kesho kutwa nitakuja kwa ajili ya kusaini kama utakuwa umeridhika mzee wangu”Aliongea Justine na sura yake ya upole , lakini mzee Alex baada ya kusikia kesho kutwa aliona mambo yanaweza kuwa mabaya Zaidi.
“Mr Justine nipo tayari kufanya biashara na Athena,”Aliongea mzee huyu na kisha akavuta karamu kwenye koti lake na kuchukua karatasi hio na kisha akatia sahihi yake kwa haraka.
Na bwana Justine na yeye akafanya hivyohivyo na kisha akachukua Tablet yake kwenye begi na kisha akafanya muamala wa dola bilioni na palepale pesa zikaingia kwenye kampuni ya JR.
NB:Taratibu zote za kusainishana mkataba kwenye simulizi hii ni za kutunga , sio uhalisia .
NITAENDELEA JUMATANO
UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 100 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA
NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
aseee hii simulizi hatari jmniSEHEMU YA 71

Tukae kwa kutulia sio[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3]tulia mkuu