Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Kuna story nafuatilia humu jf ila hii ni the best. Bonge la story keep it up mzee! hongera kwa utunzi
 
Du! Karibu siku inageuka hatujapata muendelezo mkuu
 
SEHEMU YA 72

Roma alibakia kukaa chini tu kuangalia kile ambacho mke wake Edna alikuwa akifanya,kwa namna ambavyo Edna alikuwa akitoa maelekezo, alijiwazia kwenye kichwa chake kwamba itamchukua muda mrefu kumuelewa Edna.

Roma hakutaka kujisumbua sana na michakato iliokuwa ikiendelea hapa ndani , yeye alichokifanya ni kurudi kwenye sofa la hapa ndani na kisha aliuchapa usingizi , jambo ambalo lilimfanya Edna ageuke na kumwangalia na ile anageuka aligonganisha macho na Amiri na Edna akaishia kutabasamu na wakaendelea na kile walichokuwa wakifanya.

“Boss Meneja wa Benki X anapiga, mpango unaonekana kwenda kama tulivyopanga”Aliongea Amiri na kumfanya Edna atabasamu.

“Hio ni kazi ya Adrin”Aliongea Edna na Adrini ambaye alikuwa nimzungu alievalia Headphone kichwani alishituliwa na kuambiwa hatua inayofuata ni ya kwake”Kwa namna ambavyo mambo yalikuwa yakienda hapa ndani yalionekana kupangwa muda mrefu kwani Adrin mzungu alikuwa akijua cha kufanya , aliongea na Meneja wa Benki na kisha akaunganishwa na mzee Alex , na hapo Adrin Mzungu alikubaliana na Mzee Alex kuonana nae ndani ya Eunice Hotel Kimara.

“Boss uko tayari kuingiza kiasi cha Bilioni moja kwenye kampuni ya JR?”Aliuliza Amiri ni kama alikuwa na wasiwasi na kile ambacho anakifanya Edna.

“Nishafanya maamuzi Amiri , nataka mnunue hisa za kampuni kwa asilimia ishirini”Aliongea Edna akimaanisha kwmba wanunue sehemu ya umiliki wa kampuni ya JR kupitia mtandao kwa asilimia ishirnini.

Adrin alitoka na kuainza safari ya kuelekea Eunice hoteli kwa ajili ya dili la uwekezaji ndani ya kampuni ya JR.

Mpango wa Edna ulikuwa rahisi sana , kwanza kabisa Athena Trading Company ni kampuni halisi ambayo Edna alikuwa akiimiliki kwa siri , na kampuni hii ilifunguliwa na mama yake Edna huko nchini Ufaransa mwaka 2014 ndani ya jiji la Parisi , kampuni hii ilikuwa ikihusika na maswala ya Masoko ya Hisa Duniani(Hedge fund management), ni kampuni ambayo ilikuwa ikijiendesha kwa thamani ya dola bilioni moja(Tirioni moja kwa hela za kitanzania) na Adrin Mzungu alikuwa ni Managing Director msaidizi (MD) wa kampuni hii na haikueleweka kwanini Mama yake Edna alifungua kampuni hii kwa siri , kwani haikuwepo kwenye Orodha ya kampuni matawi ya Vexto(Utaelewa baadae ni swala linalohusiana na mkataba wa Mama yake Edna na familia ya Adebayo) .

Sasa kilichofanyika ni kwamba Kampuni ya JR ilikuwa imeruhusu asilimia therathini pekee kuingia kwenye mzunguko wa soko la Hisa na hii Mzee Alex ameifanya ili kuzuia watu wa nje kumzidi umiliki ndani ya kampuni yake , na hapa ndipo Edna alipotafuta njia sasa ya kupunguza asilimia Sabini ambazo mzee Alex anamiliki ndani ya kampuni na mpango ulikuwa ni kuhakikisha anaingiza kiasi cha pesa kikubwa ambacho ni sawa na asilimia therathini, na aliona mbinu za kuingiza kiasi hicho pasipo kutumia pesa nyingi ni kuhakikisha anashusha thamani kwanza ya hisa za kampuni ya JR kutumia ushahidi aliokuwa nao , na hii ni kutokana na kwamba wafanyabiashara ndani ya masoko ya hisa wanaangalia ni taarifa gani ni chanya kwa kampuni na hasi kwa kampuni na athari zake ni zipi kwa hisa za kampuni , kama taarifa ni chanya basi hisa za kampuni zitaongezeka thamani na kama ni hasi hisa za kampuni hupungua thamani , na hapa Edna baada ya Roma kusaini mkataba Japani na JR kutolewa kwenye mkataba huo, hisa zilishuka thamani na hapa ndipo kampuni ya Athena ilianza kununua hisa kwakiasi kikubwa huku wakifanya mchezo wa kuwachanganya(Stock manipulation strategy) wanunuaji Hisa wadogo wa kampuni kwa wakati mmoja, na baada ya kuona zoezi hilo limefanikiwa akatoa tena taarifa hasi mtandaoni na kufanya hisa za kampuni ya JR zishuke thamani Zaidi na kufikia malengo yake na hapo ndipo alipochonga mchongo na benki kwa ajili ya kutotoa mkopo , haikueleweka alitumia mbinu gani mpaka kufanya benki kumtii , sasa kitendo cha Mzee Alex kukosa mkopo na benki kuunganishwa na kampuni ya Edna ya Athena ulikuwa ni mtego ambao mzee Alex kama angekuwa na ufahamu na kile kinachoendelea angekimbia.

Edna kwenye asilimia therathini za hisa ambazo zipo kwenye soko alinunua kwa asilimia ishirini na baada ya Mzee Alex kusaini kiasi cha bilioni moja dola kuingia kwenye kampuni, ni sawa na kusema ameruhusu asilimia therathini kati ya sabini alizokuwa akimiliki na kubakiwa na asilimia arobaini tu , hivyo Edna akijumlisha asilimia therathini ya uwekezaji na ile ya Soko anayomiliki ni sawa na kusema anamiliki kampuni ya JR kwa asilimia Hamsini na yeye kuwa mmiliki mkubwa katika kampuni na hii inamfanya kuwa na nguvu ya kufanya maamuzi , yaani Mzee Alex licha ya kwamba kampuni ni ya kwake lakini kitendo cha kusaini tu bilioni moja kuingia kwenye kampuni , alitoa umiliki wa kampuni kwa Edna bila yeye kujielewa.

“Cling!” Ni mlio wa meseji kutoka Swiss bank ulioingia kwenye simu ya Edna ya I phone.

“Muamala umethibitiwa , kiasi cha Dola bilioni moja kimetumwa kwenda akaunti Xxxx jina JR Group of Companies”

Edna alijikuta akirukaruka kama mtoto kwa furaha baada ya meseji hio kuingia kwenye simu yake , hii ilikuwa na maana kwamba Mzee Alex amekubali kuachia asilimia therathini za hisa zake kwenda kwa Edna pasipo yeye mwenyewe kujua , lakini wakati huohuo Edna akimiliki asilimia Ishirini za hisa za JR.

“Hongera sana Madam kwa kuipata JR Group”Waliongea wafanyakazi wote wa ATHENA na kumpongeza kwa kupiga makofi.

*****

KIGALI

First Lady au mke wa mheshimiwa Raisi Jeremy , alionekana kwenye chumba cha kufanyia masaji, , mwanamama huyu alionekana kufurahia huduma ambayo alikuwa akifanyiwa na mwanadada ambaye alikuwa mtaalamu wa kazi hio.

Wakati akiwa amenogewa kiasi cha kufumba macho mara mfanyakazi wa kike aliingia na kumshitua kiasi cha kukasirika kwa jambo hilo

“Madam simu yako inaita”

“Jina linasomeka nani?”

“Mtanzania”alijibu mwanadada huyu alievalia suti kwamba jina la mpigaji ni Mtanzania na baada ya First lady kusikia jina hilo alinyanyuka haraka sana na kuipokea simu.

“Nipe ripoti”

“Kuna Taarifa mbaya Madam”Ilisikika sauti upande wa pili ya kike.

“Ongea”

“Edna kafanikiwa kuwa mmiliki mkubwa wa kampuni ya JR”Mwanamama huyu alijikuta akishangaa .

“Okey! Sio taarifa mbaya kama unavyofikiria”Aliongea

“Unamaanisha nini Madam?”

“Ni hivyo tu , endelea kunijuza kwa kila kinachoendelea”

Na simu ikakatwa na mwana mama huyu alitembea kusogelea kioo na kujiangalia shepu yake huku akionekana kuwaza, alijizungusha kwa dakika kadhaa kwa kujitathimini , alikuwa ni mwanamke mzuri mwenye shepu nzuri sana na kwa kumuangalia tu ungejisemea Mheshimiwa Jeremy anafaidi.

“Rahel ulikosea sana kuzaa na kuiba moyo wa Jeremy ili hali mimi ndio mke wake , nitalipiza kisasi kupitia mwanao Edna , sijaridhika kabisa na kifo chako” Aliwaza mwanamama huyu , alionekana kufanya jambo baya kwa Rahel ,lakini licha ya hivyo hakuwa ni mwenye kuridhika na sasa anataka aendeleze kisasi kupitia Edna.

Upande mwingine ndani ya ofisi ya Mheshimiwa Jeremy , alionekana kuwa bize na majukumu yake kama ilivyokawaida kwa raisi huyu katika utendaji wake kazi uliotukuka , wakati akiendelea kupiga kazi , aliingia Linda Mlinzi wake wa siku nyingi.

“Mheshimiwa nina taarifa njema”

“Niambie Linda”

“Ajenti wetu kanipatia taarifa kutoka Tanzania”aliongea Linda na kumfanya Mzee Jeremy aegamie kwenye kiti ni kama alikuwa kujiandaa kusikiliza taarifa hio njema kutoka kwa Linda.

“Nipe Utamu Linda”Aliongea Mzee Jeremy na kumfanya Linda kucheka.

“Edna sasa ni mmiliki kwa asilimia Hamsini wa kampuni ya JR”

“Wow! That is indeed good News Linda”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akiachia tabasamu mwanana na kumfanya Linda kutabasamu pia.

“Linda tell me honestly,How Do you Think, I mean Edna?”

“I think she is Cute”

“Hahahahaha… That is Right .. she is Cute Daughter of mine Hahaaa”Mzee Jeremy alijikuta akiachia cheko ambalo lilimfanya Linda kutabasamu.

*****

Roma alikuwa muda wote akisikia kila kilichokuwa kikiendelea hapo ndani , alikuwa amelala lakini masikio yake yalikuwa kwa Edna , alitaka angalau kumfahamu mke wake kwa namna yake mwenyewe , hata pale aliposikia kicheko kilichoashiria furaha kwa Edna alijikuta pia akifurahi na hata yeye mwenyewe alishindwa kujua ni kwanini kafurahi.

Roma alinyanyuka alipokuwa amelala na kisha akamsogelea Edna ambaye alikuwa akiangalia skrini za hapo ndani na kisha akamkumbatia kwa nyuma na kupitisha mikono kwa mbele, na kumbusu Edna shavuni na kumfanya mwanadada huyu kushituka , ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanyiwa hivyo na mwanaume na hii ilimfanya sura yake kubadilika na kuwa nyekundu m huku akiona aibu , kwani kitendo kilifanyika mbele ya wafanyakazi.

“Bebi mpango wako umefanikiwa kwa asilimia mia mpaka naiona furaha yako, unaonaje tukienda kusherekea usiku wa leo mpaka asubuhi”Aliongea Roma na kufanya vijana wagune , ila kwa Edna aliona aibu mno , alitamani ardhi ipasuke atumbukie, hakuelewa Roma ni mtu wa aina gani kukosa aibu.
 
SEHEMU YA 73

Mzee Alex baada ya kuagana na Adrin moja kw amoja alirejea ndani ya kampuni.

Abuu alikuwa akiongea na waandishi wa habari kuhsu kukanusha taarifa iliokuwa ikisambaa mtandaoni na waandishi hao walifanya kazi yao vizuri sana.

Hali ya kampuni ilionekana kuimalika baada ya Mzee Alex kufanikisha kiasi kikubwa cha pesa , Abubakari alimuona baba yake kama shujaa likija swala la biashara.

Mzee Alex hakutaka kuongea mengi mbele ya Abu Zaidi ya kumgonga gonga begani na kumwambia aendelee na kazi huku , akiagiza kitengo cha ‘Public Relation’(PR) kufanya kazi yao vyema kuhakikisha uhusianno wa kampuni na wateja unaimarishwa , lakini pia majibu yote na malalamiko ya wateja yanatatuliwa kwa wakati.

Mzee Alex alirudi nyumbani kwake Masaki kwenda kupumzika baada ya swala hilo lililomuumiza kichwa kulitatua kwa asilimia mia mmoja , huku akijiona shujaaa.

Dereva alimuendesha bosi wake kwa umakini mkubwa na ndani ya dakika chache walikuwa washafika na mzee huyu alifika nymbani kwake , na ile anatoka kwenye gari , aliona ongezeko la gari ya kifahari lililokuwa hapo ndani , gari aina ya Roll Royce.

Matrida naona leo kanikumbuka baba yake”aliwaza Mzee huyu , alionekana kulitambua gari hio kama la mwanamke anaefahamika kwa jina la Matrida.

Baada ya kuingia tu ndani alijikuta akisikia vicheko vya wasichana vikitokea sebuleni, mzee huyu alijiambia kuzaa wanawake ni mzigo , kwani yeye anahangaika na maswala ya kampuni lakini watoto wake walikuwa wakila bata.

Sebuleni alikuwa ameketi Mwanadada mrembo wa kuvutia mno maji ya kunde , mwenye shepu namba nane , alionekana kwa kumwangalia tu umri wake haukua chini ya miaka ishirini na Tano , alikuwa yupo na mdogo wake anaefahamika kwa jina la Queen , utofauti wa Matrida na Queen ni unene , Queen alikuwa mnene kidogo na Matrida alikuwa mwembamba kwanzia tumboni mpaka kwenye kiuno huku kunakoendelea ni shepu nene , iliomfanya mwanadada huyu kuzidi kuvutia.

“Dadi..!!”Aliita Matrida baada ya kumuona baba yake na kumsogelea na kisha akamkumbatia kwa mbwembwe zote , walikuwa ni watoto wa kisasa ambao kukumbatia na kubusu wazazi wao ni kama salamu na ishara ya upendo .

“Leo umenikumbuka baada ya kunichunia kwa kipindi kirefu”Aliongea Mzee.

“Nani wa kulaumiwa Baba, umekuwa wa kutudharau ndani ya familia , huna haja ya kulalamika , na nimekuja tu baada ya kuona kampuni inaenda ndivyosivyo”.

“Matrida na Queen nishawaambia nyie kuleni bata tu , ila maswala ya kampuni ni maswala ya mimi na kaka yenu Abu kufikiria”Aliongea Mzee Alex na kumfanya Matrida abenue mdomo na kurudi kwenye sofa na mzee Alex hakuwa ni mwenye kujali.

“Unajigamba sana na huyo Abu, ila kunasiku utaona hata sisi tunapaswa kuwa kwenye nafasi sawa kama Abu kwenye familia”Aliongea Matrida na kisha akachukua ufunguo wa gari kwenye meza ya kioo na kisha akamkumbatia mdogo wake na kumpiga busu Queen ambaye kwa mavazi ambayo amevaa ungejiuliza ni tamaduni gani unatumika ndani ya familia hii.

“Matrida ushakua mtu mzima sasa , nahitaji umlete mwanaume umtambulishe kwangu”Aliongea Mzee Alex na Matrida akasimama.

“Usijali baba nikimpata nitamtambulisha kwako”Aliongea Matrida na kisha akaondoka.

“Nawewe ulete mwanaume sio unajipanua panua tu hapa ndani , hata sikuelewi”Aliongea Mzee Alex baada ya kumgeukia Queen.

“Dadiii..!!!”Alilalama Queen kwa sauti huku akiweka kigauni chake vizuri , lakini mzee Alex hakumjali alichapa mwendo kuelekea juu.

Upande wa nje , baada ya Matrida kuingia kwenye gari yake , alitoa simu yake kubwa ya Oppo Reno 7 Pro na kisha akapangusa kwa dakika na kuweka sikioni , alionekana alikuwa akimpigia mtu.

“Edna you have to keep your Promise ,I am next CEO of JR Group”

“Ofcourse , Everything has been Running Smooth so far due to your support Matrida ,I will keep my Promise”Ilisikika sauti ya mrembo Edna upande wa pili na kumfanya mwanadada huyu kutabasamu.

“Thank you”

Na kisha simu ikakatwa na Matrida aligeuka nyuma na kuangalia Ghorofani upande ambao alikuwa akijua ndio ofisi ya baba yake ilipo, lakini pia chumba cha baba yake.

“Utanisamehe sana Baba , ila haya ni maamuzi niliofanya kwa ajili yako na familia yetu kwa ujumla , nisingeweza kuona kampuni inaenda kwa familia ya Adebayo kwa ujinga wa Abubakari”Aliwaza mwanadada huyu na kisha akawasha gari yake na kuondoka taratibu.

Kwa msiomjua Matrida ni mtoto wa kwanza wa mzee Alex ,Matrrida ni msomi kutoka chuo kikuu cha Durban South Afrika, alikosomea maswala ya Banking and Finance kwa ngazi ya shahada na baada ya kumaliza alijiendeleza na masomo yake ya juu ndani ya chuo kikuu cha Georgetown Universitiy kilichopo Washinton Dc Marekani.

Matrida alikuwa ni moja ya watoto wa mzee Alex ambao waliokuwa na akili nyingi ukiachana na mdogo wake Queen ambaye darasani hakuwa akifanya vizuri na alisoma pia chuo cha Yale akichukua kozi ya Bachelor of Art in Social Media(Mafunzo ya Sanaa upande wa mitanado ya kijamii)

Matrida baada ya kurudi Bongo alijiingiza kwenye penzi zito na gavana wa benki kuu ya Tanzania bwana Musa Omari , huyu Musa Omari ndio alimtafutia Matrida kazi ndani ya benki hio na kupewa cheo cha juu cha umeneja ndani ya benki kuu ya Tanzania,Tawi la Mwanza.

Licha ya kazi hio ,Matrida hakuwa na furaha kabisa,Matrida tokea mdogo hawakua wakipatana kabisa na Abubakari Hamadi tokea aingie kwenye familia yao , sio kwake tu hata kwa mdoggo wake Queen vilevile hawakuwa wakimpenda kabisa Abubakari , mtu pekee ambaye alikuwa akimpenda Abu alikuwa ni mama yao, Mama Matrida alimpenda Abuu kutokana na kwamba mume wake alikuwa akimpenda kijana huyo na pia kwakua mumewe hakuwa na uwezo wa kumzalisha tena.

Matrida kitendo cha baba yake kuwabagua katika kuongoza kampuni kilimuuma sana, kwani kwake aliona swala hilo ni kama ubaguzi wa kijinsia na hii ilimfanya mwanadada huyu kutopatana kabisa na Baba yake na hata mama yake alipofariki alihamia moja kwa moja jijini Mwanza na kuendelea na maisha yake ,huku akimtembelea mzee wake mara chache sana.

Lakini waswahili wanakuambia ‘Kimya kingi kina mshindo mkuu’

*****

Roma alimuendesha mke wake taratibu wakirejea kazini kwani muda haukua umeenda sana, wakati wanafika Mbezi ndio simu ya Edna ilipoanza kuita na jina kusomeka ‘Matrida’.

Roma alimsikia mke wake namna ambavyo alikuwa akiongea na simu hio na kujiuliza ni jambo gani lingine mwanamke huyu anapanga kwenye kichwa chake, hakuweza kupata kuelewa kichwa cha mke wake kinafikiria nini , kwani kwa namna ambavyo anamuona Edna ni kama alionekana kuwa na mpango mwingine anataka kuanzisha.

“Wife nini kinaendelea baada ya mafanikio ya leo?”Aliuliza Roma na Edna alimwangalia Roma huku akikumbuka shambulio alilofanyiwa kwa kushitukiza madakika kadhaa nyuma.

“Nitamtoa Abubakari kwenye nafasi yake ya CEO lakini pia nitamtoa Mzee Alex kwenye nafasi yake ya mwenyekiti wa kurugenzi ya bodi , kutokana mpaka sasa mimi ndio mwenye hisa nyingi”

Aliongea Edna na Roma kuona huo ni mpango mkubwa , aliona mke wake anajitengenezea maadui , kwani kumtoa mtu aliejenga kampuni yake miaka mingi kwenye umiliki sio jambo jepesi na hakuna mtu yoyote duniani atakae kubali swala hilo kirahisi pasipo kulipiza.

“Lakini sio swala la kujiamulia Edna , kuna wanabodi wengine ambao pia swala hilo lazima walipitishe na pia mzee Alex mwenyewe lazima akubaliane na hilo”

“Nililielewa hili swala tokea mwanzo na ndio maana nina mpango wa kumtumia mtoto wake wa kike”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae.

“Kivipi mke wangu?”

“Mzee Alex ana mtoto wa kike mkubwa , ndio huyu alionipigia dakika kadhaa zilizopita, naweza kusema kwamba mpango huu ulifanikiwa kupitia yeye kuwa na nafasi kubwa ndani ya benki kuu, na hii ikawa rahisi kushawishi benki kutotoa mkopo kwa JR Group”

“Kwa hio unamaanisha kwamba huyo mtoto wake ni mfanyaazi wa BOT na katumia nafasi yake kushawishi benki ndogo za kibiashara kutotoa mkopo kwa JR, ili wewe dili lako lipate kufanikiwa?”Aliitikia Edna kwa kichwa.

“Sasa huyu Mtoto haoni kwamba anakupa umiliki wewe , ni faida gani anayoipata?”

“Faida ipo,Kwanza kabisa nimemuahidi atakuwa CEO baada ya Abu , pili anamiliki asilimia tano ndani ya kampuni ya Baba yake ,tatu makubaliano yangu na yeye ni kuacha kampuni ya JR kuendelea kufahamika kama mali ya familia na pia kutoiunganisha na Vexto, lakini hayo yote yatawezekana kutokana na uwezo wa Matrida kumalizia sehemu iliobaki”

“Unamaanisha nini sehemu iliobaki , wakati kila kitu kishaisha mpenzi?”

“Matrida anatakiwa kumshawishi baba yake kuachia asilimia zote arobaini kwenda kwa Matrida na hii itamfanya kuwa na asilimia arobaini na tano za hisa na kuwa mmiliki mkubwa baada yangu”

Roma hakutaka kuuliza Zaidi , kwani aliona milolongo yote hio ni maswala ya kuumiza kichwa tu , aliona hayo ngoja amuachie Edna aendelee nayo , huku akijiambia yeye atadili na matokeo ya maadui wa Edna watakaojitokeza.

“Bebi tukale kwanza kabla ya kuelekea kazini”

“Sawa”Alijibu Edna kivivu hata yeye alikuwa akiwaza hivyohivyo , hakutaka kurudi kazini akiwa na njaa , isitoshe pia alikuwa amekamilisha jambo kubwa kwa siku hio .
 
SEHEMU YA 74

Roma Alikuja kusimamisha gari Makongo juu, Edna alishangazwa na Roma kumleta hayo maeneo , lakini hakujali sana , alitaka kuona mwisho wake.

Baada ya Roma kusimamisha gari ,alishuka na Edna pia hivyohivyo , jua siku ya leo halikuwa kali sana na kulikuwa na dalili ya mvua.

“Wife tutatembea kidogo mpaka hapo mbele , kuna mgahawa mzuri tu”

“Sasa kwanini usingesimamishia gari hapo?”

“Edna hivi lini ushawahi kuchukua mazoezi hata ya kutembea?”Aliuliza Roma na Edna hakuweza kujibu hilo swali , kwani ni kweli katika maisha yake hakuwa ni mwenye kuchukua mazoezi , hata ya kutembea , alikuwa ni mwenye kutembea na usafri kila mahali na hata kazini hakuwa akipanda ngazi , alikuwa akitumia Lift.

“Unatakiwa kuchukua mazoezi kwa ajili yaAfya yako na huu ni mwanzo , tutatembea mpaka kwenye mgahawa na kurudi kwa mguu pia”Aliongea Roma na Edna alishindwa aongee nini , kwani hata kama angegoma alikuwa akimjua Roma na isitoshe alikuwa na ufunguo.

Mtaa huu haukua na watu wengi sana kama maeneo ya Tegeta, lakini watu waliokuwepo ndani ya huu mtaa hawakuaacha kumkodolea Roma na pisi yake kali.

Dakika chache mbele kama kumi na tano hivi waliweza kufika ndani ya mgahawa mmoja maarufu kwa kuuza nyama za kuchoma unaofahamika kwa jina la ARIFU, haikueleweka Roma alipafahamu vipi hapo mpaka kujua huo mgahawa na Edna alitamani kumuuliza Roma lakini alishindwa.

Waliingia ndani ya mgahawa huu , huku wateja wa mgahawa huu wakiwaangalia , hii sehemu ilikuwa na makelele mengi na kumfanya Edna asiipende , lakini kwa Roma yeye aliona kawaida tu , kwani kwanza alikuwa amezoea kula sehemu kama hizi na pia alifanya makusudi kumleta Edna ndani ya eneo hili la mgahawa.

Mbele kabisa ya mgahawa huu kulikuwa na mdoli mkubwa mweupe uliowekwa mbele ya mlango na kufanya eneo hili kupendeza Zaidi , ilionesha mmiliki wa hapa ndani alikuwa mwanamke.

Roma leo alishangazwa sana na Zogo ambalo lipo ndani ya hii sehemu kwa siku ya leo , huku kwa mbele wakionekkana wazungu na baadhi ya wabongo wakiwa wamezunguka meza.

“Roma..!”Ilikuwa ni sauti ya kike ambayo ilimfanya Roma kugeuka na baada ya kukutanisha macho na mwanamke mtu mzima hivi mweupe shombeshombe alievalia Aproni alitabasamu.

“”Mama Aisha nimekuja kukutembelea na mke wangu leo”Aliongea Roma na kumfanya mwanamama huyu mtu mzima kushangaa na kumwangalia Edna , ni kama hakuwa akiamini kama Roma ana mke kama huyo.

“Jamanii! Umepataje mke mzuri kama huyu Roma?”Aliuliza Mama huyu huku akimshika Edna mikono na kumfanya Edna atabasamu na kujisikia vizuri ,kwake hii ni mara ya kwanza kwa Roma kumtambulisha kama mke na ndio kilichomfanya kujisikia vizuri.

Roma na Mama Aisha mmiliki wa Mgahawa huu , walionekana kufahamiana sana , jambo ambalo lilimfanya hata Edna kutaka kujua ukaribu wao ukoje.

“Mama Aisha pale ni nini kinaendelea?”Aliuliza Roma baada ya kuona kuna zogo sana , kwa watu waliozingira meza na mama Aisha akatabasamu.

“Kuna mchezo wa kushindana kula nyama unaendelea pale, nimejaribu kutoa shindano leo kama kuvutia wateja”Aliongea Mama Aisha na kumfanya Roma na Edna watabasamu kwa pamoja.

“Mshindi anapatiwa zawadi gani?”

“Unataka ukajiunge nini?.Mshindi ni chakula bure kwa wiki nzima”Alijibu na Roma alitoa macho.

“Mama Aisha na mimi nataka kushindana kwenye hilo shindano , lakini nikishinda sitaki chakula maana itakuwa ngumu mimi kuja mpaka huku , unaonaje huo mdori hapo , nikishinda inakuwa zaiwadi ya mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae na Mama Aisha alitabasamu.

“Kwakua leo ni siku ulionitambulisha kwa mkeo, basi nakubaliana na ombi lako, isitoshe mdoli wangu ni mzuri na unaendana na mkeo”aliongea Mama Nasra na kumfanya Roma atabasamu na kisha akamwangalia Edna na kumkonyeza , lakini Edna aliishia kushangaa na matendo ya Roma.

Roma alimshika mkono Edna na kwenda mpaka upande ambao kuna meza na mama Aisha alimtambulisha kama mshiriki wa shindano kwa siku hio na akajitokeza mtu kwa nia ya kutaka kushindana na Roma na Roma alimwangalia mshindani wake na kutabasamu , lakini pia hata kwa mwenzake alimwangalia Roma na kisha akamdharau na kuona huyu lazima amshinde.

“Nikishinda pambano , sitaki nyama za bure wala chakula , bali nitachukua ule mdoli kama zawadi kwa mke wangu”

Aliongea Roma kwa sauti na kufanya kundi la watu wamwangalie Edna na kisha wakashangilia kwa kupiga makofi na kumfanya Edna atabasamu kwa Aibu , ila kwa Roma hakuwa kabisa na aibu Zaidi ya kumkonyeza Edna.

Sahani tano za vipande vya nyama ya ng`ombe ya kuchoma vilipangwa na dakika za kumaliza sahani zote zilikuwa ni kumi na tano , zilikuwa ni dakika chache sana ambazo Mama Aisha alikuwa ameweka kama moja ya sheria za Pambano ,Roma alimuona mwanamama huyu kufanya jambo hilo makusudi ili watu wasishinde , ila alijiambia leo lazima ashinde kwa namna yoyote ile ili kumpa zawadi mke wake.

Baada ya maandalizi ya pambano kuanza,Mtoto wa mama Nasra alitoa sauti kuashiria pambano kuanza na hapo hapo Roma na Mshindani wake Shombeshombe walianza kula kwa haraka sana ,Roma alikuwa akila taratibu kitendo kilichofanya washabiki kushangaa na staili ya kula , ni kama Roma alikuwa akimpa nafasi ya ushindi bwana Shombeshombe.

Edna licha ya kwamba mwanzoni aikuwa hakubaliani na shindano hilo ,kwani aliaona kama jambo la aibu , lakini sasa Roma ashaingia kwenye mchezo na alitaka awe siriasi , alitaka kumpiga kibao ale , haraka mwenzake anamshinda.

“Roma kula bhna ,,, atakushinda”Aliongea Edna baada ya kukosa uvumilivu na Roma alimwangalia na kisha akatabasamu na kumkonyeza.

Na muda huu watu walikuwa wakimshangilia Shombeshombe kwa kumaliza sahani ya kwanza , na walimuona Roma kama hatoweza kumfikia kwa namna yoyote ile , Roma aliona shabiki yake alikuwa ni mke wake pekee.

Roma baada ya kuona mpinzani wake kafikisha sahani ya kwanza na ya pili kufikia nusu , alianza kuchukua nyama mbilimbili na kutumbukia mdomoni , yaani Roma alikuwa akitafuna mara moja ilikuwa imepita , spidi ambayo alikuwa akitumia haikuwa ya kawaida na jambo hili likamuacha Edna na watu wa hapo ndani kwa mshangao na ndani ya dakika moja na nusu Roma alikuwa ashamaliza Sahani ya kwanza na sasa alikuwa akienda ya pili.

Shombeshombe alimwangalia Roma kwa namna anavyokula haraka na kujikuta akitumbua macho na kusahau kama yupo kwenye pambano , alishangazwa na ulaji huo wa Roma na kujiuliza huyu ni mnyamaa au ni binadamu , ile anakuja kushituka ,Roma alikuwa akimalizia sahani ya tatu.

Mashabiki wote walihama kwa Shombeshombe na kuja upande wa Roma huku Edna akiwa ni mwenye kushangaa m kwa mambo ambayo Roma alikuwa akiyafanya.

Ndani ya dakika saba tu Roma alimalizia nyama ya mwisho na kisha akamwangalia mke wake na kumkonyeza , Mama Nasra aliekuwa pembeni yake alijikuta akishangazwa na uwezo huo wa Roma , alikuwa ni kama mtu aliekuwa mbele yake hajawahi kukutana nae .

Watu walishangilia huku wakimwangalia Roma kwa macho ya kiulizo na kujiuliza ni mtu gani huyu anaweza kula nyama kwa kuitafuna mara moja na kumeza.

“Mama Aisha siku nyingine unapaswa kuweka zenye mifupa”Aliongea Roma aliekuwa akimalizia kutafuta nyama ya mwisho , huku shombeshombe na wengine wakiendelea kumwangalia Roma.

“Hahaha… umenishangaza sana leo”

Aliongea Mama Aisha kuku akielekea mlangoni kutoa mdoli uliokuwa kwenye mlango,mwanamama huyu alionekana kujutia kuweka Mdoli wake rehani , lakini alikuwa ashaweka ahadi , alichukua ule mdoli na kisha akampatia Roma ambaye alikuwa akitabasamu na kisha baada ya Roma kupewa mdoli wake alimkabidhi Edna.

“Wife Zawadi yangu kwako kama mumeo”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushindwa kuzuia tabasamu , ni kweli zawadi hio ilikuwa ya thamani Zaidi kwa Edna.

Na hata Roma mwenyewe siku nyingi alikuwa akiwaza ni zawadi gani ambayo napaswa kumpatia Edna , lakini alishindwa kung`amua , kwani mke wake alikuwa na kila kitu , kama ni maua alikuwa nayo yamejaa na yote yamenunuliwa na pesa , sasa yeye baada ya kuona pambano hilo na Mdoli mlangoni aliona hio ndio nafasi nzuri kwa kumpatia Edna zawadi.

Mama Aisha aliwapa chakula cha bure kizuri na baaada ya wawili hao kula kumaliza walitoka ndani ya mgahawa hupo wa ARIFU kutembea kueleka walipokuwa wameacha gari.

Edna alionekana kama mtoto kwa namna ambavyo alikuwa amebeba mdoli wale wa Rangi nyeupe na masikio ya pink.

“Umefahamiana vipi na yule mama?”Alivunja ukimhya Edna mara baada ya wawili hawa kuingia kwenye gari na kuanza safari ya kurudi .

“Nilikutana nae Mikumi nikiwa njiani kuja Dar, alikuwa ameharibikiwa na gari yake njiani nikamsaidia kuitengeneza na akanipatia lift kama malipo”.

“Wewe huko Mikuni ulikuwa upo kwenye gari au ulikuwa unatembea?”

“Nilikuwa natembea , sikuwa hata na hela”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa.

“Na wewe ulikuwa ukitokea wapi?”

“Nilikuwa nikitoka Mwanza wife”Edna alishangaa Zaidi.

“Kwa hio unamaanisha ulitembea kutoka Mwanza Mpaka Mikumi”

“Hehe..Wife unashangaa nini , hujawahi kusikia watu wanatembea kutoka Kigoma huko mpaka Dar”Aliongea Roma na kumfanya Edna aone ni kweli , lakini bado alibakia na maswali.

*****

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa ya asubuhi , Abu alionekana akiingia kazini kama kawaida , lakini siku hii akionekana kuwahi tofauti na siku zingine.

Baada ya kuegesha gari yake , moja kwa moja aliingia kwenye Lift ya jengo hili kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi yake.

“Boss..!!”Aliita Isack aliekuwa na wasiwasi na kumfanya Abuu aliekuwa akitembea kwenda kwenye ofisi yake asimame na kumwangalia.

“Kuna nini?”

“Kuna Jambo ambalo halipo sawa”

“Kivipi?”

“Nimejaribu kufatilia muwekezaji ambaye Chairman jana alisaini nae makataba ndani ya kampuni yetu”

“Sasa nini hakipo sawa?”

“Muwekezaji anatoka kampuni ya Athena Trading Company”Aliongea Isack na kumfanya Abu atoe macho huku akichukua kishikwambi mbacho Isack ameshikilia mkononi , na baada ya Abu kuangalia kwa umakini alijikuta akitetemeka mikono.

“Ni macho yangu , au hii ni sahihi Isack?”

“Ni Sahihi kama unavyoona ,mpaka sasa Athena ana asilimia hamsini za hisa ndani ya kampuni na ni rahisi kusema ndio mmiliki wa JR group mpaka sasa”Aliongea Isack na Abu alishindwa kuongea chochote , alionekana kuchanganyikiwa na alichokifanya ni kughairisha safari ya kuingia kwenye ofisi yake na kurudi alikotoka.

Ndani ya madakika kadhaa hivi Abubakari Hamadi CEO alionekana akiingia Masaki nyumbani kwa baba yake , huku akionekana mwenye haraka kweli.

Ndani ya sehemu ya kuegesha magari kwa muda Gari ya RollRoyce ilionekana hapo ndani , lakini kwa Abu alishindwa hata kuona.

Nyumba ilionekana kutulia mno na hili halikumpa Abuu shida , alienda moja kwa moja mpaka ilipo ofisi ya baba yake Mlezi na ile anafungua tu mlango , alimuona Mzee Alex akiwa hayupo peke yake , bali alikuwepo Matrida mtu ambaye hawakua wakipatana kabisa ,Matrida alimgeukia Abu na kutabasamu , huku Mzee Alex akimwangalia Abu na kusikitika na kisha akaendelea na kile alichokuwa akifanya , Mzee huyu alikuwa akisaini karatasi ambayo hakuwa akijua inahusiana na nini.
 
SEHEMU YA 75

MIEZI SITA NYUMA

Ilikuwa ni miezi sita nyuma kabla ya Edna kukutana na Roma , wakati mwanadada huyu anaingia kwenye kampuni yake siku ya asubuhi , alikutana na mgeni ambaye hakuwa akimfahamu mpaka pale mgeni huyo alivyojitambulisha kwake.

“Miss Edna nina furaha kukutana na wewe ana kwa ana , ni mrembo kama sifa zako zinazosambaa kwenye ulimwengu wa kibiashara”Aliongea mgeni huyu na Edna akatabasamu na ukweli ni kwamba Edna alikuwa ashazoea namna ambavyo watu kumsifia na alichukulia kawaida tu.

“Kana nilivyokuambia majina yangu naitwa Matrida Alex , mimi ni mtoto mkubwa wa mzee Alex , mmiliki wa kampuni ya JR grupu”Aliongea mwanadada huyu na kumfanya Edna ashangae kidogo.

“Ndio Miss Matrida , naamini ujio wako umebeba jambo kubwa”

“Ni kweli na nitaenda moja kwa moja,nia ya kufanya nije hapa ni kutokana na kwamba nataka kuchukua nafasi ya uongozi wa juu wa kampuni ya JR na kumtoa Abubakari”

“Sababu za kutaka hivyo , kwani naamini Abubakari kapata Baraka zote kutoka kwa baba yako”Matrida alifikiria kidogo na kisha akamwangalia Edna kwa jinsi alivyokuwa akiongea , alipendezwa na mwanamke mwenzie kwa namna ambavyo alikuwa akiongoza kampuni kubwa kama hio ndani ya Taifa la Tanzania.

“Sababu kubwa mimi ni mtoto kihalali wa Mzee Alex , lakini pia yule mzee amekuwa ni mwenye kutudharau wanawake….”Alianza kuelezea namna ambavyo Mzee wake hakutaka kuwapa nafasi yoyote katika kampuni.

Edna alijikuta akivuta pumzi na kumuonea huruma kwa wakati mmoja , aliona maamuzi ya Mzee Alex kuwabagua watoto wake kijinsia ni swala ambalo kwenye jamii halikubaliki .

“Kwa hio Matilda unataka nikusaidie nini?”

“Nitakusaidia kuipata JR Grupu”Aliongea na kumfanya Edna ashangae.

“Huwezi kunipatia JR Group bure naamini kuna kitu unataka kutoka kwangu’

“Ni kweli kuna jambo nataka kutoka kwako na ili mimi kukusaidia lazima unihakikishie jambo moja”

“Nakusikiliza”Aliongea Edna huku akikunja nne.

“Endapo nitakusaidia kuipata JR grupu nataka niwe CEO wa kampuni , lakini pia nataka Kampuni ya JR ibaki kutambulika kama mali ya kifamilia , lakini pia nataka niwe sehemu ya umiliki wa kampuni ya JR ili kuweza kuwa na nguvu kama CEO”Aliongea Matilda na kumfanya Edna afikirie kidogo.

“Mpango wako ni upi?”Aliuliza Edna .

“Kwasasa mpango sina , ila naamini unampango wa kutaka kuingia kwenye kampuni ya JR”.Aliongea Matilda na kumfanya Edna atabasamu.

“Matilda mimi kama mfanyabiashara niseme kweli , kampuni ya JR inamsingi mzuri kibiashara na pia natamani kuwa moja ya wawekezaji ndani ya kampuni yenu , lakini kwa sasa mipango yangu yote nimeielekezea kwa kuipanua Vexto kimataifa , lakini kwakua umekuja kwa ajili ya kuomba msaada juu ya mimi kuichukua JR, kwasasa siwezi kukuahidi chochote , ila naamini mpango utajitokeza hivi karibuni na nitaangalia ni namna gani ya wewe kuweka msaada wako”Aliongea Edna na kumfanya Matilda avute pumzi , aliona ni hatua nzuri alipiga kuisogelea kampuni ya baba yake.

Baada Miezi kupita , siku ambayo Dorisi na Roma kwenda japan , Edna alimtafuta matilda kwa simu na kumueleza akae tayari kwa msaada ambao ataomba kutoka kwake.

“Nimekupigia kukujulisha ile nia yako , kwanzia sasa kuwa macho kwa msaada ambao nitaomba kutoka kwako , nimeambatanisha na faili ambalo litakusaidia katika kumshawishi baba yako kukupa kampuni kwenye mikono yako”Aliongea Edna na kisha akakata simu.

****

Wakati Abu anaamka kwa ajili ya kuelekea kazini , nyumbani kwa Mzee Alex, Matilda alikuwa akiingia nyumbani hapo kuonana na baba yake.

Queen alikuwa amelala hivyo mwanadada huyu hakujisumbua kumuamsha , alichofanya ni kwenda moja kwa moja mpaka ilipo ofisi ya baba yake na hii ni kutokana na kwamba mwanadada alikuwa akijua wakati huo kuwa baba yake atakua ashaamka , kwani mzee Alex alikuwani wale wazee ambao hawakuwa wakilala kwa muda mrefu.

“Matilda kuna nini ambacho umekileta asubuhi asubuhi?”Aliuliza Mzee Alex na Matilda alisogea mpaka kwenye meza ya baba yake na kumpatia fomu aliokuwa ameishikilia mkononi na mzee huyu aliekuwa na wasiwasi alifungua fomu hio, huku akimshangaa mtoto wake , kwani ni kwa mara ya wanza kuwa siriasi namna hio mbele yake.

Mzee Alex alijikuta akianza kutetema mikono , baada ya kusoma karatasi hio.

“How This possible?”Aliongea mzee huyu huku macho yake yakianza kuonesha uwekundu.

“Baba ulikosea sana kumpa kampuni Abu na kutudharau sisi watoto wako, hata kama tulikuwa wa kike angalau ungetupa hata nafasi kwenye kampuni”Aliongea Matilda huku akionyesha hasira zake waziwazi.

“Kwa hio haya yote yaliokuwa yakiendelea , ilikuwa ni mipango ya Edna , huku wewe ukimsaidia?”

“Sio kumsaidia Edna baba , nimefanya haya yote kulinda kampuni , hebu baba fikiria huu ushahidi ungetoka kwenye mitandao , hali ingekuwaje”Aliongea Matilda kisha akampatia Flashi na mzee huyu kwa namna ya kutetemeka alichukua flashi ile na kuchomeka kwenye tarakishi yake na alichoona kwenye tarakishi hio kilimfanya kuanza kukosa pumzi.

“Raheli , utakake usitake , lazima kampuni iruhusu madawa yangu ya kulevya kupitia kwenye kampuni yako”

“Alex , labda niwe mfu ila swala unaloongea hapa ni upuuzi ambazo sitokuja kufanya”.

“Paah…!,Wewe ni mwanamke Rahel , huwezi kushindana na wanaume na nitahakikisha jambo langu linafanikiwa”

Ni sauti na video iliokuwa ikionyesha kwenye flashi hio na kumfanya mzee huyu atumbue macho , hakujua kama Raheli alikuwa na ushahidi wa aina hio ambao alikuwa ameuficha miaka na miaka mpaka kifo kilipomkuta.

Mzee huyu alichoka , aliona ni kweli mtoto wake kafanya jambo kubwa kuzuia ushahidi huo usitoke.

“Unataka nifanye nini Matilda ?”

“Huna haja ya kufanya jambo kubwa ninachotaka ni jambo dogo tu , asilimia arobaini za hisa zako za kampuni nataka uzihamishie kwangu sasa hivi , pili ujiuzuru kwenye nafasi yako ya uwenyekiti wa bodi , tatu Abu atatoka kwenye nafasi ya CEO wa kampuni na mimi nitachukua majukumu ya kampuni , na nikuhakikishie tu baba , licha ya Edna kumiliki asilimia kubwa ya hisa za kampuni, siwezi kumruhusu kubadilisha umiliki wa kampuni kwenda kwa familia ya Adebayo , JR itabaki kuwa mali ya familia ya Alex”Aliongea kwa uchungu na kumfanya mzee huyu amwangalie mtoto wake huyu na kujikuta akijutia maamuzi yake alioyafanya kwa kuwadharau.

Mzee aliinuka na kisha akasogea mpaka upande wa dirishani , sehemu ambayo inapicha kubwa ya mlima kilimanjaro na kisha akaitoa picha mbao na hapo kulionekana ‘Safebox’, aliingiza namba za nywira tarakimu nane na kisha kiboksi hiko kikafunguka na mzee alitoa karatasi na kisha akarudi kwenye meza yake na kukaa tena , aliangalia karatasi alioshikilia mkononi kwa muda na baada ya hapo alitoa peni yake na kusaini ,

Wakati huohuo Abu ndio aliingia hapo ndani na kumuona baba yake akiwa na Matilda , alitembea taratibu huku akimwangalia Matilda alieachia tabasamu la kejeli.

Mzee Alex hakutaka kuongea lolote na Abu, aliendelea kusaini karatasi kama nne hivi na baada ya kumaliza , alimpa ishara ya Matilda kusogea .

“Make me Proud Matilda”Aliongea Mzee huyu na kumkabidhi karatasi hizo na kisha akaegamia kiti chake na kufumba macho na Matilda alitoka huku akiwa haamini kama mambo yamekuwa marahisi hivyo.

“Baba..!”Aliita Abubakari kwa sauti na mzee Alex alimpa ishara ya Abu kuketi kwenye sofa la pembeni kwanza amuache.

Upande wa Matilda , baada ya jambo lake kufanikiwa kama alivyopanga, alienda kumuamsha mdogo wake na kumwambia kila kitu , jambo lililomfanya Queen nkutoa ukulele wa furaha , kiasi kwamba sauti ilijaa nyumba nzima.

*****

Ilikuwa ni asubuhi nyingine kwa Edna na Roma kuliona jua , wanandoa hawa ambao hawakuwa wakilala kwenye chumba kimoja.

Edna aliekuwa anajipaka mafuta aliangalia mdoli wake uliokuwa kwenye kitanda na kisha akatabasamu , haikuelewa ni kipi ambacho kilikuwa kikimfurahisha mwanadada huyu,huenda alikuwa akikumbuka Roma alivyokuwa akifakamia nyama pasipo kuzitafuna.

Edna baada ya kujipaka poda yake na kumaliza ,alichukua mkoba wake na kushuka taratibu kuelekea chini kwa ajili ya kunywa chai kuelekea kazini.

Roma na Bi wema walionekana kuwepo tayari kwenye meza , na walikuwa wakimsubiri, Edna alimwangalia Roma.

“Morning Bi Wema”

“Morning Edna”

“Za asubuhi Roma?”Alisalimia Edna na kumfanya Roma kutabasamu , lakini sio kwa Roma tu hata kwa Bi Wema , alitabasamu na kuona mabadiliko makubwa kwa Edna , kwani mara nyingi sio mwenye kumsalimia mume wake.

“Safi mke wangu , umeamkaje?”

“Safi”Alijibu , lakini wakati huo huo mara kengelele ya mlango wa nyumba yao ilitoa mlio, kuashiria kuna mgeni na Roma ndie alienyanyuka na kusogelea mlango kwa ajili ya kufungua.

Roma alipata kumuona mwanaume ambaye alikuwa kwenye mavazi ya suti , ambaye hakuwahi kumuona na kujiuliza huyu mtu ni nani wa kuja kusumbua watu asubuhi asubuhi.

Nina taarifa kwa ajili ya Miss Edna”Aliongea mwanaume na Roma alimpisha na bwana huyu mweusi aliingia.

“Rasi…!!, kuna nini?”Aliuliza Edna mara baada ya kumuona mwanaume huyu nakumtambua.

“Miss , kuna taarifa mbaya nimeleta asubuhi na nimeshindwa kupiga simu”

“Ni Taarifa gani hio?”Bwana huyu alionekana kuvuta pumzi za kijasiri.

“Miss mzee ametutoka leo asubuhi”Aliongea Rasi na kumfanya Edna atumbue macho , baada ya kusikia baba yake Mzee Adebayo amefariki asubuhi hio.
 
SEHEMU YA 76

Roma na Bi Wema wote walishangazwa na kuhuzunishwa na taariFa hio iliowafikia asubuhi hio,Edna alijikuta akijongea mpaka kwenye sofa na kukaa, hakuwa akitoa machozi lakini alionekana kuwa kwenye uchungu wa kumpoteza mzazi wake.

Ndio Edna na Baba yake hawakuwahi kuwa na ule ukaribu wa utoto na Ubaba na hii yote nikutokana na siri ambayo Edna hakuwa akiijua uu ya baba yake,Mzee Adebayo hakuwahi hata kumshika mkono Edna tokea anazaliwa mpaka kuwa mkubwa.

Na maisha ya Edna na Mzee Adebayo , yalikuwa ni ya kugombana ,kila siku jambo ambalo lilimfanya Edna asimpende kabisa baba yake , hata pale Edna alivyomshuhudia Roma kumdhuru baba yake hakuona hatia hata kidogo , kwake aliona anastahili , na tokea siku ile Edna hakuwahi kusikia habari yoyote kutoka kwa baba yake na pia hakujali kujua , hayo ndio maisha ya Edna na Mzee Adebayo , lakini licha ya hivyo Edna bado alimchukulia Mzee Adebayo kama baba yake mzazi na hakumpuuza.

“Kipi kimesababisha kifo chake?”Aliuliza Roma.

“Nadhani hamkuwa na taarifa , ila siku chache zilizopita mzee alipatwa na ukichaa wakati akiendelea na matibabu ndani ya hospitali ya Aghakani , na haikueleweka ilikuwa vipi , ila leo asubuhi tulimkuta akiwa amefariki pembeni ya jengo la hospitalini , na kwa uchunguzi uliofanyika inaonesha alijirusha gorofani”Aliongea Rasi.

“Mwili wake kwa sasa upo wapi?”

“Bado upo Hospitalini umehifadhiwa”Aliongea Rasi na kila kitu Edna alikisikia kwani Roma ndie aliekuwa akiuliza.

“Rasi wasiliana na Babu kuhusu taarifa za msiba, atakupa utaratibu”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae , hakuwa na taarifa ya uwepo wa Babu kwenye maisha ya Edna ndio maana alikuwa akishangaa ,lakini Roma hakujilaumu kwa kutokujua , kwani tokea aingie ndani ya familia ya Edna hakuwahi kumuuliza kuhusu baadhi ya ndugu zake.

“Sawa Madam”Aliongea Rasi na kisha akageuka na kutoka nje , kwani lililokuwa limemleta hapo ndani , lilikuwa limekwisha kufanyika.

“Edna sijawahi kusikia ukimtaja babu yako” Aliongea Roma akikaa kwenye masofa na Bi Wema alimuangalia Roma na kuona ngoja amjibu yeye.

“Mzee Adebayo baba yake yupo hai na ni Jenerali wa jeshi mstaafu, haujasikia kuhusu taarifa zake kutokana na kwamba MissEdna na babu yake hawajawahi kupatana kama ilivyokuwa kwa baba yake”

“Kunasababu gani ya Edna kutopatana na Babu yake?”Aliuliza Roma na Bi Wema akamwangalia Edna aliejinamia chini.

Kwa maelezo ya Bi Wema , Mzee Athumani ambaye ndie babu Yake Edna , alimtelekeza Mariam (jina la bibi yake Edna) wakati akiwa na ujauzito wa Adebayo , na hii ilimfanya bibi yake Edna kumchukia Mzee Athumani kwa kitendo cha kumtelekeza akiwa mjamzito na kwenda kuoa mke mwingine.

Bibi yake Edna licha ya Adebayo kuwa mtoto wa Athumani hakutaka kumuingiza kwenye familia ya Athumani na alichokifanya miaka hio ni kumuita jina la Jedi Adebayo na kwanzia hapo familia yao ikafahamika kama ya Adebayo.

Hivyo ni rahisi kusema kwamba Edna asingempenda mtu ambaye bibi yake alikuwa akimchukia , Edna na Bibi yake walikuwa wakipatana sana Enzi hizo za uhai wake na hii ilichangia pakubwa kwa Edna kumchukia Mzee Athumani.

Licha ya kwamba mzee huyu baada ya kustaafu katika jeshi , alijitahidi kuweka ukaribu na Edna ili amtambue kama babu yake , ila Edna hakutaka kabisa mazoea nae na aliweka mstari kabisa wa ukomo kati yake na Babu yake kindugu.

Mzee Adebayo baada ya kuona mama yake hampendi Mzee Athumani baba yake mzazi na pia kitendo cha kutomrithisha kampuni kama mtoto wake, aliweka ukaribu na Mzee Athumani kama kisasi cha kumkasirisha mama yake , na hii ndio ilioongeza ukaribu baina yao, hivyo ni rahisi kusema kwamba Adebayo anatambulika ndani ya familia ya Athumani na msiba ulikuwa ukiwahusu kwa asilimia kubwa.

Wakati Bi Wema akiendelea kumuelezea historia hio ya kuchanganya Roma, simu ya Edna ilianza kuita na jina lilisomeka ‘Mzee Athunani’, aliangalia simu yake na kisha akapokea kinyonge.

“Edna pole sana , nimepata sasa hivi taarifa ya kifo cha mwanangu Adebayo na nimeona utakuwa kwenye uchungu mkubwa kumppoteza baba yako na ndio maana nimeona nikupigie simu kukupa pole , na pia kukuambia tuko pamoja na Ramadhani atahakikisha taratibu zote za msiba zinafanyika”Aliongea Mzee huyu.

“Sawa nashukuru”Aliongea Edna na kisha kukata simu , alionekana hakutaka mazungumzo mengi.

“Anasemaje?”Aliuliza Bi Wema.

“Balozi Ramadhani atasimamia taratibu za msiba”alijibu Edna na kuendelea kumshangaza Romana kumwangalia Bi Wema.

“Ni yule ambaye aliomba muongee kwenye kusanyiko , ni balozi nchini Japani”Aliongea Edna kinyonge na kumfanya Roma ashangae Zaidi.

“Inamaana Edna na Sophia ni ndugu , sasa kwanini Balozi anataka nimuoe Sophia ilihali anajua Edna na Sophia ni ndugu”Aliwaza Roma hhuku akishindwa kuelewa kwa wakati mmoja , ila Roma aliona hayo ayaweke kiporo kwanza aangalie swala muhimu kwa wakati huo.

Edna na Roma walitoka kwa pamoja kwenye Gari moja kuelekea hospiali ya Aghakani, Edna alitaka kuona mwili wa baba yake kabla haujapelekwa nyumbani kwa ajili ya taratibu zingine za kuupumzisha.

“Za saa hizi ndugu?”Roma aliekuwa eneo la nje kwenye hospitali hii ya Aghakani alifuatwa na bwana mmoja hivi mhindi , ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kidaktari, wakati huu Edna alikuwa akiongea na baadhi ya wasaidizi wa Mzee Adebayo na Roma aliwapa nafasi ya wao kuongea.

“Salama”

“Niwape pole za msiba , numekuona ukiingia hapa na Miss Edna na kwa taarifa nilizopewa ni kwamba wewe ni mume wake , nimeona nikufuate kwani kuna jambo ambalo nataka tuongee”Aliongea Dokta na kumfanya Roma ashangae.

“Lina husiana na nini Labda?”

“Ni swala nyeti kidogo na ndio maana nilivyokuana uko peke yako nikakusogelea , ni juu ya Mzee Adebayo”Aliongea.

“Okey , nimekuelewa , tunaongea wapi , hapa au ofisini”

“Ofisini itakuwa vyema Zaidi”aliongea Daktari huyu na kisha akageuza kuelekea ofisini kwake huku Roma akifuatia.

“Dokta nieleze , swala ambalo umesema ni nyeti?”Aliongea Roma mara baada ya kuketi na Dokta alivuta faili moja kwenye shelf na kulifungua na kisha akatoa karatasi na kumpatia Roma.

Roma alijikuta akishangazwa na taarifa hio iliokuwa kwenye karatasi hio.

“Hii taarifa ni sahihi?”

“Ndio Mister , ni taarifa sahihi kabisa”

“Kwanini unanionesha hii taarifa?”Aliuliza Roma.

“Nadhani mpaka hapo ushaelewa taarifa hio kama ikijulikana italeta madhara gani kwa Mkeo”

“Ndio maana nikakuuliza kwanini umenionesha hii taarifa , unataka nini , ongea acha kuzunguka zunguka?”Aliongea Roma huku akianza kukosa utulivu na hasira kuanza kuonekana na huyu dokta wala hakutishwa na kupaniki kwa Roma alitabasamu.

“Napanga kuitunza hio taarifa na ibakie kuwa siri yangu mimi kama daktari ambaye nilikuwa nikimtibia Mzee Adebayo kwa kipindi chote , hivyo ili taarifa hii iwe siri nataka cha kuniziba mdomo”Aliongea akimaanisha kwamba anataka kiasi cha pesa ili kutoivujisha taarifa hio , Roma alijikuta akikasirika sana na swala hili , alichukia sana watu wa aina hio katika maisha yake, wanaotumia udhaitu wa wengine kwa ajili ya faida.

“Okey nishakuelewa unataka kitu cha kuziba mdomo, niambie ni kiasi gani unataka?”

“Bilioni moja na nusu tu itanitosha”Aliongea Mhindi huyu kwa kujiamini , alijua ni kiasi kidogo sana kwa Roma kutoa ukilinganisha na utajiri ambao Mke wake alikuwa akimiliki , lakini pia aliona Taarifa hio ni kubwa sana na ingeweza kuleta madhara makubwa kwa Edna kama jamii ingeifahamu.

Ilikuwa ni kitendo cha haraka sana alichofanya Roma , kwani tayari alikuwa amemshika Shingo daktari huyu wa kihindi na kumning`iniza hewani kwa mkono mmoja.

“Nachukia watu wa aina kama yako na siku zote nimekuwa wakutoa adhabu ya kifo kwa watu kama wewe,maana hamna mchango wowote kwa dunia”Aliongea Roma huku macho yake yakianza kubadilika Rangi na kuwa ya kijani na kumfanya Dokta azidi kutapatapa , alikuwa akinyongwa na mkono mmoja , na alijitahidi kujitoa kwenye mikono ya Roma lakini alishindwa kabisa kujitoa kwake ,na kifo alikiona kile kinakuja.

Roma alionekna leo hakudhamiria kuua , maana baada ya kuridhika na kumkaba dokta huyu mhindi alimtupa chini kama furhushi , na kisha akachukua ile karatasi na kuichanachana.

“Siku ukifungua mdomo wako na ukatoa hii taarifa , nitatekeleza kifo chako kwa Staili ambayo hata shetani mwenyewe atashangaa”

Aliongea Roma huku akiwa ameshika Kidevu cha Dokta huyu ambaye alikuwa akihema kwa shida kwenye Sakafu , na Roma hakuridhika , baada ya kumpiga biti Dokta Mhindi, alimpiga kibao cha uso kwa namna ya kumziba , na Dokta aliona nyota nyota , kwenye maisha yake hakuwahi kuwaza kukutana na aina hio ya mtu, harufu ya mkojo ilianza kusambaa ndani ya hiki chumba.

“Umenielewa?”Aliuliza Roma huku akimwangalia dokta huyu ambaye Pua zake zilikuwa zikitoa Damu mfululizo , na bwana huyu kinyonge alitingisha kichwa kuashiria ameelewa.

Muda huohuo ambao Roma alikuwa akimpiga Biti Dokta mpaka kupelekea mkojo ,mlango ulifunguliwa na Edna aliingia na kushangazwa na hali iliokuwa hapo ndani , aliinua macho yake kwa Roma na kuwaza ni jambo gani Roma anafanya.

“Edna umejuaje nipo humu?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Edna ambaye macho yake yalikuwa kwa Dokta Mhindi aliekuwa akitokwa na damu.

“Ni nini kunaendelea Roma ,Mbona dokta yupo hivyo?”

“Kuna jambo nilikuwa namuelekeza mke wangu , usiulize mengi ni maswala ya kawaida tu ,kama ushamaliza tuondoke”Aliongea Roma kwa sauti ya siriasi na kumfanya Edna amwangalie Roma machoni na alimuona macho yake yapo kawaida , alijua kuna jambo ambalo linaendelea hapa ndani ,lakini alishindwa kuuliza.

Roma alimsukumia Edna nje na alirudi ndani kwa spidi na kisha akamsogolea Dokta mhindi na kumpiga teke la tumbo na kumfanya Dokta huyu ajikunje kwa maumivu makali huku machozi yakimtoka.

“Onyo mara moja ukirudia ni kifo ,Ole Wako”

“Romaa..!!”Aliita Edna aliefungua mlango kwa mara nyingine akijiuliza ni nini tena Roma anafanya.
ITAENDELEA JUMAPILI MCHANA
UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 100 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
SIMULIZI ZANGU ZILIZOKAMILIKA AMBAZO ZIPO FULL NI
  1. WARAKA WA RAISI KABLA YA KIFO
  2. BOOK OF ALL NAMES
UNAWEZA KUPATA SIMULIZI ZANGU ZOTE KWA 3000 TU LIPIA KWA NAMBA HIZO HAPO JUU
SIMULIZI ZINAZOENDELEA KWENYE GRUPU NI
  1. MASAA MAWILI YA KUMBUKUMBU
  2. MY FREEDOM(UHURU WANGU)
  3. NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
Hizo zote zinaendelea kwenye grupAu ukichangia kuanzia 2000 kuendelea utatumiwa zote
 
Niko muhimbili hapa nimepata mtoto wa Kiume nimempa jina Roma

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23] Kwanza nikupe hongera Mkuu kwa kutuletea jembe kwenye hii dunia[emoji4][emoji4][emoji4] ila sasa siku akikua akaulizia historia ya jina lake utamwambia mwamba singanojr ndo alisababisha au utahifadhi hii story ajr asome mwenyewe[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom