Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 79

Roma Alirudi zake kutoka kazini muda wa saa kumi za jioni, kwa namna ambavyo alionyesha kuchoka ungedhaniia alikuwa akifanya kazi ya maana huko kwenye kampuni, lakini ukweli ni kwamba siku hio alishindia kucheza gemu kama ilivyokuwa kawaida yake.

“Pole na kazi Mr Roma”Aliongea Bi Wema na Roma akatoa tabasamu la uchungu , maana alijua kabisa hana cha maana ambacho alikuwa akifanya ndani ya kampuni.

“Asante Bi Wema”Aliongea Roma na kisha akapandisha mdogo mdogo kwenda kwenye chumba chake akimuacha Bi Wema ambaye alikuwa anaagalia tamthilia za kikorea.

Edna alikuwa asharudi na Roma aliona gari yake , lakini kwa wakati huo Roma alishindwa kujua mke wake anafanya nini chumbani kwake , ila hakutaka kujali sana , licha ya kwamba alitamani muda kama huu anarudi kazini apokelewe na Edna na mabusu motomoto na kisha wapige kimoja apumzike , lakini Roma baada ya kufikiria hivyo aliona ni ujinga kwani alikuwa akimjua mke wake.

Aliwasha Tv na kuweka chaneli moja ya Kibrazili na kuangalia Warembo aina ya Red Indiani , kwa namna ambavyo channeli hio ilikuwa ikionesha iliamsha hisia za Roma na aliona ana uhitaji sana wa kitumbua.

“Nikimaliza kula naenda kwa Nasra”Aliwaza Roma na kisha akazima Tv na kujitupa kitandani kuutafuta usingizi.

Edna wakati Roma anarudi alimuona na ni kama alikuwa akimsubiria , kwani hata pale Roma alipoegesha gari lake na kuingia ndani alikuwa akimwangalia kwa juu , haikueleweka mrembo huyu alikuwa akifikiria nini , lakini uso wake haukuonesha kukasirika wala kutokuwa na furaha .

Ilipotimu saa moja kasoro Edna alishuka kwa ajili ya kumsaidia Bi wema kupika, Bi Wema kusema ukweli alikuwa ni mwenye kujisikia faraja na mabadiliko ya Edna.

Edna tokea alivyokuwa mdogo, hajawahi hata kulisogelea jiko na kama ukimuona akiingia jikoni , labda enzi hizo ni kwenda kumtafuta mama yake , kila kitu alikuwa akifanyiwa, na sio wakati akiwa mtoto tu , hata alipofikia ukubwani ilikuwa hivyohivyo na hili ndio jambo ambalo lilimfanya Bi Wema kumfurahisha baada ya Edna kubadilika , kwani Mwanamama huyu licha ya kwamba hakuwa akipendezwa na tabia ya Edna , lakini alishindwa kumwambia , alijiona ni kama mfanyakazi tu ambaye analipwa hivyo tabia ya Edna haikuwa ikimhusu , lakini pia alikuwa akimuonea huruma kwa wakati mmoja kutokana na kazi ngumu aliokuwa akifanya ya kusimamia kampuni.

Upande wa Roma haikueleweka alipitiwa na usingizi saa ngapi ,kwani alilala fofofo kiasi kwamba alikuwa akikoroma,bwana huyu alionekana alikuwa akifurahia maisha yake bila wasiwasi kabisa.

Saa moja kama na dakika mbili hivi simu yake ilianza kuita mfululizo na kumuasha kwenye usingizi wake ,alipapasa upande wa kushoto na kisha akaichukua na kuangalia jina la ,mpigaji na alikuta ni Diego.

“Kuna nini Diego?”

“Your Maajest ! ,Kuna watu ishirini walio na siraha wanaikaribia nyumba yako , tunataka ruhusa kutoka kwako ya kuingia kazini , vijana hawako mbali”Aliongea Diego na kumfanya Roma ainuke na kukaa kitako.

“Mmewatambua wanatokea wapi?”

“Ndio Mfalme Pluto , tumeweza kutambua wanatokea kambi ya jeshi Mbagala,wanaongozwa na Kapteni Elvice Temba wa kikosi cha Anga”aliongea Diego na Kumnfanya Roma akasirike na kuona huo ni uchokozi.

“Okey!Diego nitadili nao mwenyewe”Aliongea Roma na kisha akakata simu, aliivaa suruali ya Tracksuti na tisheti ya kubana ilioufanya mwili wake wa kimazoezi kujidhihirisha vyema na kisha alishuka taratibu kuelekea chini sebulenni.

Ile Roma anaangalia chini alimuonaAbubakari Hamadi ,Elvice pamojana wanaume wawili waliovalia mavazi ya kijeshi ,waliokuwa wameshikilia bunduki aina ya SMG.

Edna na yeye alikuwa ameketi kwenye masofa huku akiwa amezungukwa na wanaume hao , walionekana kuongea na yeye jambo, ambalo kwa upande wa Edna alionyesha sura iliojaa hasira.

Edna baada ya kumuona Roma amefika hapo sebuleni alijikuta akivuta pumzi ya ahueni , kwani watu waliokuwa mbele yake walionekana hawajafika hapo ndani kiamani kabisa.

Elvice na Abubakari walionyesha hali ya kuwa na wasiwasi mara baada ya Roma kujitokeza, lakini hawakutaka kudhihirisha hofi yao mbele ya Edna wala ya Roma , kwanza walikuwa na wanajeshi wengi wa kikosi cha Mbweha, ambacho kilikuwa kikiaminika kwa uwezo wake wa kimapigano likija swala la vita na hii yote ni kutokanana uzoefu wa kikosi hiko baada ya kwenda Sudani kulinda Amani.

“Edna nadhani mpaka sasa unaona ni nguvu ya namna gani ambayo ipo nyuma yangu , hawa unaowaona wote hapa ni wanajeshi na kwa amri yangu moja tu wameweza kunitii”Aliongea Elvice kwa kujiamini na kumfanya Roma kwanza atabasamu , huku sheteni akizidi kumpelekesha.

“Edna ,hatujaja hapa kwa vurugu , nia na madhumuni ya sisi kuja hapa nikutaka tuongee tuelewane na kisha tutaondoka kiamani kabisa”

“Hamjaja hapa kivurugu ?,Hebu acha kunichanganaya Elvice , mmevamia nyumbani kwangu ukiwa na watu wana siraha useme hamjaja kivurugu ,hili sitoacha lipite hivi hivi”aliongea Edna huku akianza kujiamini maana dakika chache zilizopita alionekana kukosa Amani baada ya kutokumuona Roma, alikuwa yupo sebuleni lakini alikuwa akijiambia Roma anafanya nini huko juu hashuki.

“Kwetu hawa wanajeshi ni namna ya kujilinda dhidi ya mumeo asifanye jambo lolote la kijinga , wakati tukiendeleza mazungumzo”Aliongea Elvice huku akimwangalia Roma, ambaye kila sekunde aliokuwa akiwaangalia viumbe hao alizidi kukasirika.

“Mnataka nini kutoka kwangu?”aliuliza Edna.

“Ni rahisi tu Edna, utarudisha asilimia 20 za hisa za kampuni ya JR na utalipwa kiasi cha pesa kwa gharama ya hisa hizo”Aliongea Elvice na kisha akampa ishara Abubakari na alielewa, kwani aliitoa karatasi iliokuwa kwenye mfuko wake wa nyuma iliokunjwa na kuiweka mbele ya Edna.

Muda wote haya wakati yakiendelea Bi wema pia alikuwepo kwa pembeni akiangalia , huku akiwa ni mwenye kujawa na hofu ya kile kitakacho tokea.

Lakini sasa wakati wanaendelea kumlazimisha Edna kusaini karatasi , mara Magdalena aliingia hapo ndani akiwa na Gwanda na alionekana kuwa na haraka sana.

“Agent flamingo , unafanya nini hapa?”aliuliza Elvice kwa mshangao , kwani hakuelewa ajenti Flamingo amefikafika je hapo ,kwani jambo lao lilikuwa la siri sana na ni watu wachache sana waliokuwa wakilifahamu.

Roma alimwangalia mwanadada huyu aliekuwa akifanana kwa asilimia mia moja na Mage kwa jinsi alivyokuwa akihema , alionekana kukimbia kwa kuwahi sana ndani hapo.

“Afande kanipa Amri ya kukuambia urudishe kikosi kambini haraka , na hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa”Aliongea Ajenti flamingo na kisha akawageukia wanaume waliokuwa wameshikilia siraha na kisha akawapa ishara ya kuondoka ma wale wanaume baada ya kusikia alietoa kauli ya kuacha kile wanachokifanya ni Afande Maeda, waliogopa na kushangaa kwa wakati mmoja , haikueleweka Elvice aliwashawishi vipi mpaka kuambatana nae.

Jamaa mmoja mnene mweusi , alimpa ishara mwenzake ya kwamba waondoke , huku wakimwangalia Elvice kwa macho makali na Elvice pia aliogopa kwa namna ambavyo mwanaeshi huyo alivyomuangalia.

Magdalena alijikuta akivuta pumzi ya ahueni mara baada ya hatua ya kwanza kumalizika , alimgeukia Roma na Edna.

“Roma na Edna naomba msamaha kwa niamba ya Afande Maeda kwa hili lililotokea leo , hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa yote yaliotokea leo”Aliongea Mage kwa heshima kiasi cha kumfanya Edna aone wasiwasi kwenye macho ya Magdalenda, aligeuza macho yake kwa Elvice na Abubakari.

Elvice alionyesha hali ya kuwa na wasiwasi sana , ni kama mtu ambaye hakutegema swala hili kuwafikia watu wakubwa , alimwangalia Abubakari ambaye na yeye alikuwa kwenye wasiwasi.

“Elvice sikutarajia unaweza kufanya jambo la kishenzi hivi , licha ya kwamba ulikuwa ukijinasibu kama rafiki yangu tokea tulipkuwa watoto , nimekasirika sana na siwezi kukusamehe , naomba muondoke kwenye nyumba yangu sasa hivi”Aliongea Edna huku akionyesha kuumizwa na matendo ya Elvice.

Ndio Edna licha ya kwamba alikuwa akijua Elvice hakuwa na nia nzuri kwake , tokea siku ya mkataba wa Yamakuza , lakini bado alikuwa akimchukulia kama rafiki ambaye walikuwa wote kwa pamoja na alikuwa anamheshimu kwa hilo , lakini kitendo cha kuungana na Abu kuja kuchafua Amani ndani ya nyumba yake kilimfanya kumuona Elvice ni msaliti na siku zote alikuwa akijinasibu kwa maneno bandia mbele yake ya kuwa rafiki.

Elvice na Abubakari waliangaliana na kisha wakamgeukia Ajenti Flamingo na wakapeana ishara ya kuondoka, wa kwanza kutangulia alikuwa ni Abubakari.

Magdalena baada ya kuona swala hilo limefanikiwa , aliinama kiheshima mbele ya Roma na Edna na kuanza kuondoka , lakini sasa ile Abubakari na Elvice wanakaribia Geti mara tu walishituka Roma huyu hapa akiwa mbele yao , na kwa Roma ni kama alitaka watoke ndani ili akawafanyizie nje.

Ubaridi uliwaingia wote wawili baada ya kushudia macho ya Roma ambayo leo hii hayakuwa ya kijani tu , bali yalikuwa yamebadilika Rangi kabisa na kutoa rangi hafifu ya kijani, ukimwangalia Roma macho yake unaweza kuyafananisha na Mbwa mwitu ambaye yupo kwenye kiasi cha juu kwa hasira.

Iilikuwa ni kitendo cha Ghafla tu walishikwa wote kwa pamoja kwenye shingo , kiasi kwamba Abu alitoa ukulele , kwani maumivu aliokuwa akisikia hayakuwa ya kawaida hata kidogo na aliona shingo yake inavunjika , lakini upande wa Roma ni kama hakujali makelele yao kwani aliwatupia wote kwa pamoja kwenye ukuta na wakaenda kujingonga vibaya sana na Elvice ndio aliekuwa wa kwanza kuzima huku damu zikianza kutoka puani.

Roma hakuridhika na swala hilo , aliona hawa wamezimia tu alitembea taratibu , huku akiwafuatwa huku mwili wake ukiwa umetuna kama amejaziwa upepo.

“Hades …No usimuue”Ilikuwa ni sauti ya Magdalena iliosikika na muda huohuo Edna na yeye ambaye hata kuvaa viatu amesahau ,alitoka kwa haraka , huku walinzi waliokuwa wakilinda ndani ya eneo hili wakiwa wamejawa na hofu kwa kile walichokuwa wakishuhudia kwa bosi wao.

Ajenti Flamingo baada ya kuona Hades anamsogelea Elvice kwa nia ya kuua, kama alipotea aliposimama na kuja kuibukia mbele ya Roma huku ule urembo wake ukibadilika na sasa Magdalena alionekana kama mwanajeshi mwenye mafunzo ya kichawi.

“Huwezi kunizuia ninachotaka kufanya”Aliongea roma kwa sauti nzito

“Inabidi uniue kwanza Hades kabla haujamfikia Elvice”

Aliongea Magdalena huku akionekana kujipanga kupigana na Hades.

Roma alitoa tabasamu la kifedhuli na hapo hapo alimpiga Magdalenda ngumi ya tumbo kw nguvu na kumfanya mwanadada kupaa na kwenda kutua mita kadhaa na alipokuwa amelala Abu karibu na chungu cha maua ,lilikuwa ni pigo ambalo liliacha kila mmoja Mdomo wazi ,Magdaleana hakuzimia kama ilibyokuwa kwa Abubakari na Elvice , aliinuka huku akiwa amejishika tumbo kwa maumivu makali aliokuwa anahisi.

Lakini ile anasimama vizuri ghafla tu ,Roma alipotea alipokuwa amesimama na ile anatokea tu alimbeba Ajenti Flamingo kwa spidi ya hali ya juu.

“BOOM’

Ulikuwa ni mlio wa kishindo kizito ambacho kilifanya hadi ardhi kutingishika mpaka ardhi ikachimbika na mchanga ukaruka juu , huku muda umeme ukakatika , na giza totoro.

Magdalena hakuelewa ni nini kimetokea, lakini pia alishangazwa na mtikisiko uliotokea dakika chache zilizopita, sio kwake tu kwa kila mtu hapo ndani alikuwa kwenye hofu kuu, hawakuelewa kishindo kilichokea dakika chache nyuma kilisababishwa na nini.

Ilipita kama dakika moja hivi kwa umeme wa jenereta kurudi na eneo likawa na mwanga , lakini ajabu ni kwamba Roma hakuonekana tena ,Edna alikuwa amekaa chini akiwa amenyoosha miguu kama mtu aliekosa tumaini na kuishi, huku akiwa sio mwenye kuelewa kile kinachoendelea,Bi Wema alikuwa ashapoteza fahamu muda mrefu,Derick alikuwa amepiga magoti huku akiwa ameshikilia moyo wake na vijana wake wengine wanaosaidiana katika ulinzi wakiwa hawaelewi chochote.

Muda ule ule wakati wakishangaa ,mlango wa geti ulifunguliwa kwa kasi na wakaingia wanaume wawili wote wakiwa kwenye mavazi ya gwanda za jeshi , na kwa haraka haaraka , walionekana kuwa ni wale wenye vyeo vikubwa Jeshini wakiwa wameambatana na wanajeshi wengine watano.

Ni kama sasa akili zilimrudia Magdalena kwani alisimama vizuri na kupiga saluti , na hii ilikuwa ni sheria , kama mwanajeshi umevaa gwanda unatakiwa kupiga saluti ,kama umevaa kawaida unatakiwa kubana t*ko tu.

“Ajenti Flamingo nini kimetokea?”

“Afande mpaka sasa sijapata kuelewa ni kimetokea dakika moja iliopita”Aliongea Magdalena na kufanya wanajeshi hawa wamwangalie Edna aliekuwa pembeni amekaa chini.

“Kanali angalia hali ya yule mwanamke anaongekana kuwa kwenye mshituko”Aliongea mwanajeshi huyu ambaye alionekana kuwa na cheo kikubwa Zaidi ya yule alieingia na pia wakati huo huo wanajeshi wengine walipewa ishara ya kuwaangalia Abubakari na Elvice ambao walikuwa wamelala bila fahamu.

“Ni nini kimechimba hapa?”Aliuliza Mwanaeshi huku Magdalena na yeye akisogelea sehemu ambayo imechimbika kwenda kiasi kwamba kama utasimamisha ndoo isingeonekana kwa juu, Mchanga pia ulikuwa umesambaa.

Lakini licha ya swali hilo Mage alishindwa kuelewa , Magdalena alichokuwa akikumbuka ni namna ambavyo Hades alimkwapua aliposimama na kumsogeza upande mwingine kwa ghafla sana na hapo hapo hakuelewa kilichoendelea licha ya kusikia mshindo mzito wa kama kitu ambacho kimedondoka kutoka juu.

“Hii ni nguvu iliotumika kuchimba hapa sio ya kawaida”aliongea Mwanajeshi huyu wakati akiwa amechuchumaa.
 
SEHEMU YA 80.

Ni baada ya tukio la kutisha ambalo limetokea ndani ya familia ya Edna , baada ya nusu saa hivi , hali ilirejea kama ilivyokuwa kawaida , lakini sio kwa ukawaida uliozoeleka na hii ni kutokana na kupotea kwa Roma, baada ya kishindo kizito kusikika na kupelekea mpaka ardhi ikachimbika.

Bi Wema alikuwa asharejewa na fahamu na alikuwa amelala kwenye sofa huku akionekana kukumbuka kilichotokea dakika chache zilizopita, Edna alikuwa amekaa karibu na Bi wema huku na yeye akijiuliza ni kipi ambacho kimetokea na Roma kaenda wapi baada ya umeme kukatika. Pamoja na kishindo kizito.

Edna alikuwa ni mwenye wasiwasi sana kiasi kwamba, haikueleweka kwenye moyo wake alikuwa akijisikiaje , licha ya kwamba hakuonesha mabadiliko ya kawaida , lakini alitamani kujua Roma ni wapi kaelekea baada ya tukio hilo ambalo halina maelezo ya kutosha.

Wakati Edna akiendelea kumuwazia Roma ni kipi kimemkuta upande mwingine Magdalena alisimamisha pikipiki yake ndani ya makao makuu ya jeshi lugalo na kisha akavua helmeti na kukimbilia ndani.

Na ile anaingia ndani ya ofisi ya Afande Maeda alikutana na sura tatu ambazo zilikuwa zimeketi kwenye masofa , sura ya kwanza ilikuwa ni ya baba yake Kanali Tobwe na sura ya pili ilikuwa ya Afande Maeda mwenyewe na Sura ya tatu ilikuwani ya Jenerali Athumani mstaafu.

“Ajenti Flamingo tunataka ripoti”

“Afande hali nimeshindwa kuielewa mpaka wakati huu ,ila niligundua jambo ambalo halipo sawa kwa Elvice”

“Unamaanisha nini kuhusu kutokuwa sawa , hao si waasi waliochukua wanajeshi na kwenda kumshambulia Hades?’

“Hapana Afande , hawakuwa kwenye akili zao timamu, walikuwa wanaongozwa na nguvu ambavyo nilishindwa kuitambua chanzo chake”Aliongea Ajenti Flamingo na kumfanya Afande Maeda kushangaa , anachomaanisha Magdalena , lakini sio kwake tu hata kwa Jenerali mstaafu na Kanali Tobwe hawakuelewa.

“Unamaanisha kuna nguvu za kichawi ambazo zilikuwa zikimuongoza Elvice , vipi kuhusu huyu Abubakari?”

“Nimeweza kugundua Elvice pekee,pamoja na wanajeshi wawili wakikosi cha Mbweha ndio ambao hakuwa kwenye akili zao timamu, macho yake yalikuwa yakidhihirisha nguvu ambayo sio ya kawaida na ilipotea mara baada ya kishindo kikuu kutokea na sikuelewa mpaka sasa nini kimetokea”

“Vipi kuhuu Hades?”

“Ametoweka mara baada ya kishindo kikuu Afande”Aliongea na kuwashangaza.

“Unaitafsiri vipi hio hali Ajenti ,Flamingo kwa namna ya sisi kuelewa”

“Siwezi kusema mengi juu ya hali hii Afande ila nina uhakika kuna mtu ambaye sio wa kawaida , aliengia nchini na kwa haraka ninaweza kusema aliwatumia Elvice kama njia ya kumsogelea Hades”Aliongea na kuwafanya wazee hawa kushangaa Zaidi.

“Hali ya Elvice ikoje kwa sasa?”

“Wote washapelekwa hospitalini ya jeshi kwa ajili ya matibabu”

Waliangaliana, huku wakionesha kutoelewa hali inavyoendelea, walimpa ruhusa Ajenti Flamingo kwenda kuendelea na kile ambacho alikuwa akikifanya.

“Nadhani tusubirie Hades atakapotokea”Aliongea Jenerali na kumfanya Afande Maeda na yeye atingishe kichwa kukubaliana na wenzake , lakini licha ya hivo alikuwa kwenye maswali mengi , alijiuliza kama alichongea Mage kitakuwa cha kweli ,huyo mtu mwenye nguvu alietokea ghafla tu kiasi cha kuweza kuwaongoza wanajeshi wake na kufanya uasi ni nani.

“Nadhani swala hili kwa sasa liwe siri na kama maneno ya Ajenti Flamingo ni ya kweli basi hatuna haja ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanajeshi wetu”

“Tunapaswa kuhakikisha hili kutoka kwa Elvice , atatueleza kile kilichotokea na kama kweli atakuwa hana kumbukumbu ya kile kilichokuwa kinaendelea dakika chache nyuma , basi tutaamini maneno ya Ajenti Flamingo ni ya kweli”.

Waliongea na kukubaliana wote kwa pamoja na walipiga simu hospitali lugalo kuhitaji taarifa ya Elvice.

Magdalena hakutaka kwenda nyumbani moja kwa moja ,alijua kwa namna yoyote ile Edna atakuwa kwenye mshituko mkubwa na anapaswa kuwa nao karibu , ukizingatia kwa namna tukio lilivyotkea watashindwa kua na Amani kabisa na ndio maana baada ya kutoka Lugalo kutoa ripoti ya tukio moja kwa moja aliendesha pikipiki yake kuelekea nyumani kwa Edna.

“Magdalena!!”Aliita Edna mara baada ya kufunguliwa mlango.

“Roma yuko wapi?”

“Edna hata mimi sijui alipoelekea , ila naamini atarudi”Aliongea Madgadela akimwangalia Edna ambaye alionekana kuwa na wasiwasi

Edna jibu liilionekana kutomridhisha kabisa , alitaka angalua maelezo ya kutosha kidogo , lakini Magdalena hakuonesha nia ya kumueleza kila kitu.

“Nitalala leo hapa Edna kukumpa kampani”Aliongea Magdalena huku akimwangalia Bi Wema ambaye hali yake sasa ilionekana kuwa ya kawaida,Edna alitingisha kichwa na kuona ahueni , lakini bado alitaka maelezo ya nini kimetokea , kwanini Roma kapotea ghalfla.

“Magdalena huna chochote cha kuniambia kuhusu nini kimetokea?”Aliuliza Edna mara baada ya Magdalena kuingia upande wa jikoni , mwanadada huyu alionesha hali ya kuwa na njaa na mpaka muda huo hakuona dalili ya wapiishi kuandaa chakula na aliona aingine mwenyewe jikoni , huku akiwa na mavazi yake ya kijeshi bado.

Muda huu ilikuwa ikienda kwenye saa tatu kasoro hivi za usiku tokea tukio la Elvice na Abubakari kutokea.

“Edna siwezi kuelewa kilichotokea , ila Elvice hakuwa kwenye akili zake za kawaida , alikuwa underifluence na nguvu ambayo nimeshindwa kuielewa chanzo chake”Aliongea Magdalena na kumshangaza Edna.

“Wewe umeuaje na kwanini nguvu hio iwe kwa Elvice?”

“Edna usiwe na wasiwasi ,Mumeo akirudi utamuuliza sawa ,hata mimi sielewi hali halisi ya kile kilichotokea , ila nina uhakika Mumeo atarudi”Aliongea Mage.

Ilikuwa ni saa nne na nusu hhivi za usiku ndani ya ofisi Maeda , aliingia mwanajeshi wa nyota tatu mweupe mrefu kwa wastani huku mkononi akiwa ameshikilia karatasi, jenerali hakuwepo Zaidi ya kuwepo kwa Afande Maeda na Kanali Tobwe.

“Afande Ripoti ikoje?”Aliuliza Afande Tobwe baada ya Afande Alvin Kingasa kutoa saluti.

Alvin Kingasa alikuwa ni mwanajeshi wa maswala ya kisaikolojia kutoka jeshi la wananchi na alikuwa akifanya kazi ndani ya hosipitali ya jeshi ya lugalo.

“Afande Ripoti inaonesha Elvice amepoteza kumbukumbu za muda mfupi uliopita nimejaribu kumdadisi mara ya mwisho ni wapi alipokuwepo na alinipa taarifa alikuwa nyumbani amepumzika baadayakushinda Bar na rafiki yake Abubakari usiku mzima wa jana wote.”

Afande Maeda aliridhishwa na ripoti hio na hakuona sababu ya kubakia hapo , aliagana na kanali Tobwe na kuainza safari ya kuelekea nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 82

BUDDAPEST- HUNGARY 1990

Ni asubuhi na mapema ndani ya mji mkuu wa Hungaria unaofahamika kwa jina la Budapest, mji ambao una wakazi Zaidi ya milioni moja, pembezoni mwa mto Danubi inaonekana familia nzima ya Mzee Kovac Smith ikiwa mezani kwa ajjili ya chai ya asubuhhi , wazungu wanaita Breakfast.

Jumla ya wanafamilia hawa ni Wanne , yaani Mzee Kovac mwenyewe ambaye ni tajiri maarufu ndani ya jiji hili la Buddapest , lakini pia alikuwepo Anna ambaye ni mke wa Kovac pamoja na watoto wao wawili , yaani Levente pamoja na dada yake Zoe.

Zoe na Levente walionekana kwenye mavazi yao ya shule huku mzee Kovac akiwa kwenye mavazi yake ya suti , akiwa ashajiandaa kwenda kwenye biashara zake , kwani mzee huyu alikuwa akimiliki kampuni yake ndani ya jiji hili la Buddapest.

“Levente mwalimu wako jana kanipigia simu , mara nyingi unaondoka kabla ya vipindi kuisha , nataka uniambie unaendaga wapi?”Aliongea Bi Anna kwa lugha ya kihungari, huku akiwamngalia Levente ambaye alikuwa na nywele zake za kujikunjakunja , ni kama alikuwa amevalishwa wigi na macho yake flani hivi ya rangi ya blue .

Levente alimwangalia mama yake na kisha akamgeukia baba yake ambaye alimpa ishara ya kumjibu mama yake kwa swali aliloulizwa , lakini licha ya kijana huyu kuulizwa swali hilo alionekana kukosa majibu.

“Dadi Levente kila siku anasoma hadithi za miungu ya Ugiriki”aliongea Zoe na kuwafanya wazazi hawa wamawangalie Levente.

Walikuwa wakijua moja ya hobi ya kijana Levente ni kusoma hadithi , tena hadithi ambazo zilikuwa zikihusiana na miungu ya kale , lakini licha ya wazazi hawa kujua hilo walichukulia tu jambo hilo kama hobi kwa mtoto wao.

“Levente what do you want to Acoomplish in the future”

“I want to revive the Greek God`s”Aliongea Levente akimaanisha kwamba anataka kufufua miungu ya kale ya Ugiriki baada ya kuulizwa na baba yake ni jambo gani anataka kukamilisha kwenye maisha yake ya baadae.

Jibu hilo lilimuacha mdomo wazi Mr Kovac , kwanza alishangazwa na jibu hilo kwani Levente ndio kwanza alikuwa na miaka saba, lakini wazazi hawa walichukulia swala hilo kawaida tu kwa mtoto kuota mambo ambayo hayawezekani kutokana na umri wake.

“Kama kweli unahitaji kufufua miungu ya Ugiriki unatakiwa kusoma kwa bidii”Aliongea Kovac ili tu kumfanya mtoto wake asome kwa bidii , kwani aliona ndoto yake haikuwa na uhalisia wowote, lakini mzee huyu pia alikuwa akiamini Levente atakuja kukamilisha jambo kubwa sana kwenye maisha yake kutokana na uwezo wake mkubwa wa akili, kiufupi Levente alikuwa ni Genius.

Utaratibu wa familia hii ni kabla ya Mzee Kovac kwenda kwenye majukumu yake lazima awapeleke watoto wake wote kwenye shule ambayo kila mmoja wao alikuwa akisomea na baada ya hapo ndio ataelekea kazini kwake , sio kama alishindwa kuwapa wafanyakazi ,bwana huyu kufanya hivyo , ila ni ile hali ya kupenda kufanya hivyo tu ndio iliomfanya Mzee huyu kuwapelekea watoto wake mwenyewe.

Zoe kalikuwa ni kasichana karembo kweli ukikaangalia m, unaweza kumfananisha na Rihana kwa muonekano wake , na macho yake yenye kiini cha rangi ya bluu , alikuwa ni kivutio sana kwa watoto wenzake , lakini pia kwa watu wazima na jambo hili lilimfanya Mzee Kovac kumpenda sana mke wake kwa kumletea duniani mtoto wa kike mzuri kiasi hiko, alijivunia kama baba kila alipokuwa akiongozana na watoto wake kwenda shuleni.

Mzee kovac aliwaacha watoto wake kama kawaida baada ya kuwafikisha sehemu husika , huku akimpa msisitizo Levente kutokipindia vipindi.

Baada ya kuhakikisha watoto wake washaingia darasani alipanda gari yake na kutokomea kazini katikati ya jiji.

Lakini baada ya dakika kama kumi na tano ya Mzee Kovac kupotelea na gari yake Levente alisogea upande wa Barabarani , kwani shule yao ilikuwa pembezoni mwa barabara iliokuwa ikiunganisha Budapest na baadhi ya sehemu zingine kama vile Bratislava na Slovakia.

Sasa Levente ile ya kufika tu barabarani ilisimama gari aina ya Trabant(Gari maarufu sana za miaka ya tisini ndani ya Budapest) na Levente aliingia ndani ya gari hio na ikaondolewa kwa spidi.

Ndani ya madakika chache tu , walikuwa wakiingia ndani msitu wa Gemence,msitu ambao ni sehemu ya mbuga ya wanyama inayofahamika kwa jina la Duna.

Gari aliopanda Levente ilikuja kusimama baada ya kutoka barabara kuu na kuingia upande wa kushoto kilometa moja, sehemu iliokuwa na nyumba ndogo tu ambayo kwa harakaharaka ungeiona ni nyumba ya chumba kimoja tu na jiko.

Levente mara baada ya kutoka akiwa na uniform zake alitingishiana kichwa na bwana mmoja mwenye ndevu nyingi mtu mzima ambaye ndie aliekuwa dereva na kisha bwana huyo akageuza gari na kuondoka , yaani kwa hali ni kama jamaa huyo alimleta tu Levente ndani ya eneo hilo .

Baada ya levente kuingia ndani ya kile kijumba alimsogelea mzee mmoja hivi mzee sana ambaye alikuwa na mindevu mingi ambayo ina mvi , kwa kumwangalia tu huyu mzee ungejua hana siku nyingi za kuishi duniani, nywele zake zote zilikuwa nyeupe na alikuwa akiota moto.

“Professor Banos , I am Here”Aliongea Levente na Babu ambaye alikuwa akiitwa Profesa Banos alitingisha kichwa kivivu sana.

Levente alitoa mikate iliokuwa kwenye begi lake , na haikujulikana aliiweka saa ngapi na kisha alimsogezea profesa Banosi na kumpatia , haikueleweka kwanini mtu anefahamika kwa jina la Profesa akaishi msituni na , msitu huu ulikuwa ukitisha kwelikweli ndani ya miaka hio , hakukua na sauti Zaidi ya ndege na baadhi ya wanyama waliokuwa wakiongea kwa lugha zao.

“Nenda kamalizie Projekti , hakikisha unafuata taratibu na hatua nilizokueleza”Aliongea mzee huyu kivivu kwa lugha ya kihungaria na Levente alitingisha kichwa na akageuka na kusogelea Zulia la mkeka lililotandikwa chini na kisha akafungua mlango wa mbao na kutumbukia ndani kwa kutumia ngazi.

Eneo la sehemu ambayo Levente ameingia halikuwa na mwanga mwingi , ila kulikuwa na taa zilizofungwa za umeme , haikujulikana chanzo cha umeme huo ni nini.

Lakini ndani ya eneno hili kulikuwa ni kama maabara ambazo muonekano wake ni ule wa kizamani kabisa na haikua ya kisasa sana, chini hakukuwa na sakafu ya kujengwa Zaidi ya mchanga , lakini mpangilio ulikuwa ni mzuri kwani kulia na kushoto kulikuwa na vifaa vingi vya Mbao halafu katikati kulikuwa na meza ndefu ambayo ilikuwa na madumu ya maj, hili eneo lilikuwa ni kubwa na kwa harakaharaka utatambua hili eneo ni Handaki.

Levente baada ya kusogea mita kadhaa mbele aliingia kwenye chumba kidogo upande wa kulia na ile anatoka alikuwa amebadilika , alivaa mavazi mengine mfano wa yale ya kidaktari (PPE) lakini muundo wa kizamani.

Kwa urefu na umri vilimfanya Levente kushangaza sana , kwani usingeamini mtoto kama huyo ambaye ndio kwanza ameingia darasa la kwanza , ndio mwenye kufanya mambo kama hayo , ilikuwa ikishangaza , lakini pia kuthibitisha uwezo wa akili wa Levente kwa wakati mmoja.

Eneo hili la handaki lilikuwa na kona nne ukitembea mpaka katikati unakutana na muunganiko wa sehemu nne zilizojengwa kwa muudno wa msalaba , na kwa jinsi palivyokuwa ni Dhahiri eneo hili lilijengwa miaka mingi sana kwani kwa juu kulikuwa na uozo na majani majani aina ya’Fern’.

Basi Levente mara baada ya kufika katikati alichukuwa kona inayoelekea magharibi na hapa ndipo alipoingia kwenye uwazi ambao ulikuwa na meza katikati ambazo zote zilikuwa na maboksi ambayo yalikuwa yamejengwa kwa mfumo wa kama vibanda vya kufugia kuku kwani pande zote nne zilikuwa zimezibwa na mbao lakini upande mmoja ulikuwa na uwazi uliokuwa na wavu na karatasi ngumu inayopitisha mwanga(Transparent)

Pembeni kutoka kwenye meza hii kubwa ambayo ilikuwa imejengezwa maboksi kwa juu kulikuwa na makabati yaliotengenezwa kwa muundo mzuri tu na kila kabati likiwa na mlango pamoja na kitasa pamoja na jina.

12 GOD`S( Zeus,Athena , Hermes , Hades ,Aphrodite, Demeter,Hera ,Dionysus,Appolo,Ares,Poseidon,Artemis)Hayo ndio majina yaliokuwa yameandikwa kwa kila mlango wa kabati hizo kwa jumla yake kumi na mbili huku chini yake ya hizo kabati kukiwa na neno ‘SPECIMENS’

Kwenye meza pia kulikuwa na jumla ya makabati kumi na mbili yaliokuwa na majina sawa kama ilivyokuwa kwenye makabati ya ukurani.

Sasa baada ya Levente kuingia hapa ndani kwanza alitabasamu na mwili wake ukamsisimka.

Ndani ya aya makabati ambayo yalikuwa kwenye meza kulikuwa na mapanya makubwa tu, kwa ukubwa wa panya buku.

Levente alipita kwa kila boksi huku akiangalia mapanya hayo kwa tabasamu kubwa , yaani kijana huyu alionekana kufurahishwa na uwepo wa mapanya ndani ya hilo eneo , alitembea taratibu mpaka alivyofika kwenye boksi la Ares.

“Ares leo nitaanza na wewe”Aliongea mtoto huyu anaekwenda kwa jina la Levente na kisha alisogelea kabati lililokuwa lipo hapo ndani kenye jina la Ares na kisha akalifungua na kutoa aina flani hivi ya unga mfano wa poda uliokuwa kwenye chupa na kisha akauweka kwenye kiganja cha mkono wake na akafungua kwa upande wa juu wa kibanda cha panya na kisha alimwaga ule unga na Panya lile lilianza kula kwa fujo ule unga wa poda na kumfanya Mtoto Levente kutabasamu , na ndani ya dakika chache tu Panya lile lilidondoka chini na kulala.

Baada ya levente kuona panya lenye jina la Ares limedondoka chini na kulala , aligeukia kabati kwa mara nyingine na akatoa vichupa viwili, kimoja kikiwa na jina la Al-Virus huku kikiwa na chata ya fuvu , na kijichupa kingine kikiwa na picha ya moto , huku chini kikiwa na jina la ‘Stabilizer’ majina yote yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kingereza.

Alivuta bomba kubwa kama zile za hospitalini na kisha baada ya hivyo alichukua kile kichupa kilichokuwa na majimaji na kisha akaweka sindano na kutoboa kwa upande wa juu na kunyonya yale maji kwenye kijichupa kile kiasi , kisha akaweka sindano ile na Bomba mezani.

Alitumia hatua za wali kutoa tena maji ya kwenye kijichupa(vials) kingine na kuweka mezani , na baada ya hapo akafungua kwa mkono kabati la panya alielala na kisha akamtoa na kumuweka mezani.

Licha ya kuwa mtoto lakini alikuwa hana hofu kabisa, na alionekana kujiamini kwa asilimia mia moja huyu mtoto wa kizungu, baada ya taratibu hizo , alichukua bomba la kwanza na kisha akamchoma panya yule na sindano ya Kirusi Al na baada ya hapo akachoma tena sindano ya ‘Stabilizer’ na baada ya kuridhika alimrudisha panya yule kwenye boksi na akafunga na kisha aliangalia saa ya mshale ya kizamani iliokuwa kwenye meza na ni kama alikuwa akihesabu dakika , ilichukua dakika kumi tu kupita , lile panya lilishituka , lakini awamu hii ililikuwa likiongezeka ukubwa kama vile tofu la unga wa ngano ambalo limetiwa hamira , yaani panya alikuwa ni panya buku lakini kadiri muda ulivyokuwa unaongezeka , alikuwa akizidi kuwa mkubwa kiasi kwamba Levente alikuwa na hofu, kwani aliona kama panya huyo anakwenda kupasuka.

“Come on Ares , Don’t bust … Come on Ares”Aliongea kijana huyu kwa sauti yake ya kitoto iliosikika ndani ya chumba hiki kwa dakika kadhaa , huku panya lile likizidi kuwa kubwa na sasa lilikuwa likilingana na sungura ambaye ana mimba ya watoto wengi , na tumbo la panya lile lilikuwa likicheza cheza kama spika inayopiga mdundo mzito huku likiwa limesimama sehemu moja bila kusogea.

Levente alionekana kuwa na wasiwasi kweli , alikuwa akiliangalia panya hilo kwa umakini sana , huku akihesabu kila dakika, kijana huyu mdogo aliendelea kuangalia saa kwa wasiwasi , huku panya lile lenye ukubwa wa sungura sasa lilikuwa limeacha kuongezeka lakini tumbo lake liliendelea kucheza cheza kama vile dundo la Singeli.

“Yeeee..ssss!, Yes, yes …..”Kijana huyu furaha ilimtawala huku akishangilia mpaka akakaa chini na kuinuka kwa wakati mmoja , wakati huu panya buku mwenye ukubwa wa Sungura tumbo lake lilikuwa limeacha kucheza sana na sasa lilienda kawaida.

‘Boom’

Ulikuwa ni mpasuko wa kikabati kilichokuwa na Panya lile ndani na kutoboa kwa nguvu na kwenda kugonga kwenye makabati ya upande wa pili kiasi kwamba mshindo wa nguvu ulisambaa kwenye chumba chote.

Kijana mdogo Levente alianza kuogopa kwani alikoswa koswa na Panya hili, ambalo sasa lilikuwa lipo bila ya kizuizi chochote,Levente baada ya kuona hali imebadilika kalianza kukimbia na kusimama upande wa kabati kwa nyuma karibu na mlango akiendelea kuangalia lile panya ambalo sasa lilikuwa likijipigiza kwa nguvu ukutani kama vile limepandwa na kichaa.

Lakini wakati huu sasa Levente wakati akiwa anafurahia na mafanikio hayo ,kwani ilionekana ndio kitu alichokuwa akitaka kitokee , mara alisikia shindo za viatu zilizokuwa zikija nyuma yake.

“Profesa Ban…..”Aliita lakini kabla hajamaliza.

“Paaa… Paaaa”

Ni risasi mbili zilizopigwa kwa wakati mmoja na kwenda kutua kwa kijana Levente na palepale vazi lake la kidaktari likachafuka kwa damu na huo ndio ukawa mwisho wa Mtoto Genius Levente.

Hakuwa mtu mmoja tu alieingia hapa ndani , walikuwa kama watano hivi huku wote wakiwa wamevalia mavazi meusi , huku wakiwa wameziba pua zao na mavifaa flani hivi kama yale ya wapiga mbizi ambayo yalionesha yalikuwa yakiwapa hewa safi.

“Chukua kila kitu kwenye makabati,Mnadakika moja tu”

Aliongea Bwana ambaye aliumtandika Levente kwa risasi na akasogelea lile panya na kulitandika na Risasi mfufulizo na palepale likalala chini likiwa linaonesha hali ya kufa na yule bwana aliekuwa na mabuti marefu meusi , ambayo yalieonesha kama ni ya kijeshi , alianza kuweka vitu kama sumaku kwenye meza ile ya mbao kwa kila boksi lenye panya na ile kumaliza tu na vijana wake watatu walikuwa washaweka kila kitu kwenye masanduku yao ya chuma waliokuwa wamebeba na kisha wakapeana ishara na kuondoka ndani ya eneo hili.

Nje kabisa Profesa Banosi alionekana kufa muda mrefu kwa kupigwa Risasi pia.

Wale watu ambao walikuwa na sare ambazo hazikueleweka ni watu waliotoka wapi, walionekana kuja na chopa yenye rangi za kijeshi ambayo bado ilionekana ikizungusha panga lake huku rubani akionekana akiwaangalia mabwana hawa waliokuwa wakiisogelea chopa kwa mwendo wa kujiamini kabisa.

Baada ya wote kuingia kwenye Chopa ilinyanyuliwa na kuacha upepo uliokuwa ukipeperusha miti na ile wanafika usawa wa juu tu.

‘Boom,Boom,Booom’

Ikawa ndio mwisho wa Profesa Banosi pamoja na kijana mdogo Levente na projekti yao , kijana akawa amekufa na ndoto yake ya kufufua miungo ya kigiriki , kwani walikuwa wamelipuliwa na mabomu ambayo yalifanya eneo hilo kutitia na kufunikwa na mchanga , ni kama walizikwa kabisa.

Hii ni historia iliotokea miaka hio ya Tisini ndani ya jiji la Budappest msitu wa Gemence , nini kilitokea baada ya hapo kwa Tajiri Kovac , Zoe na Bi Anna.

ITAENDELEA. JUMATANO

UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 100 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
asante kwa simulizi nzuri mkuu, Roma atarudi kweli, atafanikiwa kumkula Edna?
 
Duuuh mambo yanazidi kuwa ya moto
 
Back
Top Bottom