Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
DuhSEHEMU YA 104
Roma alimkaribisha kwanza Sophia mpaka kwenye masofa ya hapo sebleni , huku wakiwe mabegi pembeni, na wakati huu na Bi Wema alikuwa ashatoka jikoni na alikuwa ameketi sebuleni wakisubiri utambulisho kutoka kwa Roma.
Roma alimuelezea Edna kama alivyokuwa amepanga na Sophia , lakini kwa Edna alijikuta akishangaa , licha ya kwamba alionekana kuelewa lakini pia alibaki na maswali , kilichomfanya asiulize sana ni kutokana na kwamba hakuwa akimjua sana Roma kuhusu maisha yake ya nyuma na alichokuwa akijua tu ni kwamba Roma amelelewa huko Marekani na kuhusu taarifa za familia iliomlelea hakuwa nayo.
“Kwahio Sophia ni kama mdogo wako?”Aliuliza Bi Wema mara baada ya kuelewa utambulisho.
“Ndio Bi Wema ,Sophia ni mdogo wangu na ujio wake Tanzania ulikuwa wa ghafla sana, kwanza kanipigia akiwa tayari kashafika na sikutaka akaishi hotelini ukilinganisha na wema ambao familia yao imenitendea”Aliongea Roma kwa kudanganya na Sophia akamwangalia Roma na kujiambia kumbe Hades anajua kudanganya.
“Miss nadhani ni jambo zuri kama tutaishi na Sophia kwa muda , isitoshe Roma ni mumeo na ni sehemu ya familia”Aliongea Bi Wema Mzungu wa Roho.
Ukweli Bi Wema licha ya kwamba Edna na Roma walikuwa ni wanandoa wa mkataba lakini kwenye moyo wake alikuwa ashamkubali kabisa Roma kuwa mume wa Edna. Na alitaka na Edna pia amchukulie Roma kama mume wake , kitendo cha Roma kumleta Sophia hapo ndani ya familia alikipenda , aliona kama Edna ataendelea kukutana na baadhi ya familia ya Roma basi ukaribu wao utaongezeka.
Edna alimwangalia Roma ambaye alikuwa hana wasiwasi kabisa na kisha akageuza macho kwa Sophia na kumkagua juu hadi chini , Edna alimuona Sophia mrembo sana , na tofauti kati yake na yeye ilikuwa ndogo, na kwake ilikuwa afadhari baada ya kujua wawili hao ni kitu na mdogo wake,maana dakika kadhaa nyuma moyo wake uliogopa mpaka mwenyewe kushindwa kujielewa.
“Okey! Haina sababu ya Sophie kwenda kuishi sehemu nyingine wakati wewe ni sehemu ya familia yake”Aliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu.
“My Wife licha ya kwamba umrembo kuliko wanawake wote ndani ya dunia hii , lakini pia umebarikiwa busara”Aliongea Roma na Edna alitabasamu , licha ya kwamba alijua Roma anampamba tu kutokana na kukubali kwa Sophia aishi hapo , ila ndani ya moyo wake aijisikia vizuri kusifiwa mbele ya Sophia.
“Sister Edna nitakuwa mtiifu na nitahakikisha sikukasirishi”Aliongea Sophie na kumfanya Edna ashangae , kilichomfanya kushangaa ni kwamba kwenye maisha yaaake hakuwahi kuitwa dada na leo ilikuwa mara yake ya kwanza.
Bi Wema alijikuta akitoa tabasamu baada ya kumuona Edna alivyobadilika baada ya kuitwa dada, na alishindwa kumuelewa Sophie kafikiria nini kumuita Edna dada na sio Wifi , ila hakutaka kujali sana kwanza kwa jinsi Sophie alivyokuwa mzuri aliona ni sawa tu kwa hao wawili kuitana dada.
“Roma unaonaje ukimwandalia Sophia chumba chake?”
“Bi Wema chumba kipi kitamfaa??”
“Nitamwandalia mimi”Aliongea Edna na kisha alimwangalia Sophie kwa kumpa ishara amfuate , huku Roma na yeye akinyanyuka kusaidia kubeba mabegi kwenda juu.
Chumba cha Sophia kilikuwa kikiangaliana na chumba cha Edna , Roma aliingiaza Mabegi na kuwaacha dada na mtu wasaidiane kuandaa chumba.
“Kesho tutaenda kununua baaadhi ya vitu ambavyo unataka viwekwe kwenye chumba chako”Aliongea Edna na Sophie alimwangalia Edna.
“Thank you Sister”Aliongea Sophie na kumfanya Edna atabasamu , hakujua kwanini Sophie kaamua kumwita Dada ila alipenda, kwani alimuona Sophia kuwa M’cute’.
Saa tatu kamili Bi Wema alikuwa ashamaliza kupika na Edna alimsaidia kuandaa chakula mezani , Sophie na yeye alikuwa ashamaliza kuoga na kubadilisha mavazi na alishashuka chini na kukaa kwenye masofa , baada ya dakika kadhaa za kuandaa , mtaalamu Roma alishuka chini kwa ajili ya kula chakula kwani njaa pia ilikuwa ikimnyanyasa.
Bi Wema alitabasamu baada ya kuona familia imeongezeka mtu mmoja ,Mama huyu hakuwa akipenda familia kuwa na watu wachache , alipenda familia ya watu wengi.
“Sophie elimu yako ni ya levo gani?”Aliuliza Edna na Roma alimwangalia Sophie ,maana licha ya kwamba amemleta hapo ndani lakini hakuwa na taarifa zozote kuhusu elimu ya Sophia.
“Nina Masters ya Uchumi”
“Kweli!!”
“Ndio Sister Edna,Mbona kama hauniamini”
“Hapana nimeshangaa , unaonekana mdogo kwa levo ya elimu yako”
“Nina ‘skills’ nyingi ambazo zitakushangaza Sister”
“Kama zipi?”
“Nina Mkanda wa Bluu (Blue Belt) kwenye mchezo wa Kung Fu”Aliongea Sophie na kumfanya Roma atake kutema chakula alichokuwa akitafuna na Sophie alimwangalia Roma na kutabasamu.
“Blue Belt kwenye ‘Kung Fu’ ndio mkanda gani?”Aliuliza Edna kwani hakuelewa na Roma alitaka kumsikiliza Sophie atakavyojibu.
“Ni levyo ya kati ya mafunzo ya kimapigano ya kichina ni sawa tu kusema levo ya uvumilivu”Aliongea Sophie na kumfanya Roma amwangalie na Sophie ni kama alifanya makusudi alimwangalia pia.
“Ilikuwaje sikufikria hili kabla , haikuwa kawaida kwa Sophie kuweza kuvumilia lile baridi kwenye ile Mashua”Roma aliwaza.
Ukweli ni kwamba kwa namna ambavyo Sophie na Shirani walivyokuwa wamepakiwa kwenye ile mashua ,lakini pia na kwa jinsi ambavyo ‘Pasific Ocean’ ocean ilivyokuwa na baridi ukijumlisha na barafu ambazo Roma alitengeneza isingekuwa rahisi kwa mtu wa kawaida kuvumilia ile baridi, na ni mtu mwenye mazoezi maalumu tu ya kimwili ndio ambaye alikuwa na uwezo huo.
Roma palepale alitengeneza miale ya rangi flani kwenye macho yake na kummulika Sophia pasipo mtu yoyote kugundua na hapo ndipo alipothibitisha ni kweli Sophia alikuwa na uwezo wa kimapigano kwa levo aliosema.
“Kwa hio Miss Sophie unajua kupigana?”AliongeaBi wema ambaye muda wote alikuwa akisikiliza lakini mazungumzo yalivyofikia hapo alijikuta akikosa uvumilivu na kuuliza.
“Ndio Bi Wema nina uwezo wa kupambana na watu kumi kwa wakati mmoja ambao hawana mafunzo ya kimapigano”
“Mimi siamini”Aliongea Edna na kumfanya Sophie atabasamu.
“Nitakuonyesha picha tukimaliza hapa”Aliongea Sophie na kweli hakutaka kuamini pasipo kuona , kwani kwa mwonekano wa Sophie , aliona ni mdada mrembo sana kuwa na uwezo wa kimapigano.
“Ujuzi wako mwingine ni upi?”Aliuliza Edna.
“Najua pia kuimba na sio kujua tu napenda kuimba na ndio maana nimerudi Tanzania nataka nijikite kwenye usanii”Aliongea na kumfanya Edna awe ni kama haamini hivi.
“Kwahio umerudi tu kwa ajili ya kuwa msanii, na kwanini usiimbe Marekani ukaja Tanzania?”
“Kwasababu napenda Bongo Fleva”Aliongea na kumfanya Edna aelewe , aliona pia sio jambo baya kwa mtu kupenda kufanya kile anachopenda.
Baada ya kumaliza kula chakula Sophie alienda na kuleta picha na kuanza kumuonesha Edna na Bi Wema , walionekana tayari washazoeana na Roma aliekuwa akishuka kutoka juu akiwa ameshikilia funguo za gari yake aliishia kutabasamu moyoni.
“Mafunzo ya Kung Fu yanaonekana kumfanya Sophie iwe rahisi kuwafanya watu waliokaribu yake kumzoea”Aliwaza Roma na kuwasogelea .
Roma alitoa taarifa kama anatoka na Edna hata hakujisumbua kugeuka Zaidi ya kunyoosha mkono tu kuitikia na Roma hakujali sana , alipanga siku hi ya leo akamtembelee mchepuko wake Rose kwani ni muda kidogo hakuwa amemtembelea tokea watoke Kisarawe , aloitaka kujua ni nini kilitokea baada ya pale.
Dakika chache tu Roma alikuwa ndani nya Mbagala , alinyoosha moja kwa moja mpaka ndani ya eneo la Club B na kuegesha gari yake , leo hii ndani ya hili eneo kulikuwa na watu wengi kidogo kutokana na kwamba magari hapo ndani yalikuwa mengi kiasi cha kumfanya Roma ashangae kidogo , kwani ilikuwa sio wikiend.
Roma aliingia ndani ya hili eneo ambalo lilikuwa limechangamka huku likiwa na harufu mchanganyiko za bia na Marashi.
“Hubby!!!”Aliita Rose baada tu ya Roma kuingia hapa ndani, Rose alikuwa amependeza sana usiku huu , akiwa amevalia suruali yake ya kitambaa rangi ya samawati pamoja na blazia nyekundu iliokiacha kifua chake wazi.
“Bebi Rose nimekumisi sana”Aliongea Roma mara baada ya kukumbatiana na Rose pasipo kujali macho ya watu wengi yaliokuwa yakiwaangalia.
“Nimekumisi pia mpenzi”Aliongea Rose kwa sauti yake nyororo ambayo ilimsimua Roma na kisha wakaachiana.
“Kama umenimisi mbona huajanitafuta?”
“Namuogopa mkeo”Aliongea Rose na kumfanya Roma atabasamu .
“Rose mbona leo kuna watu wengi hapa kuna nini?”Rose alitabasamu na kisha akamwangalia Roma.
“Tunasherehekea ushindi leo , unaowaona hapa wengi ni vijana wangu,”Aliongea Roma huku Rose akimshika mkobo Roma na kumuongoza upande mwingine.
Club B ilikuwa ikipendwa pia na matajiri kutokana na mgawanyo wake , kwani ilikuwa pia na upande wa VIP(Very important person), upande huu wa VIP ulikuwa pia ukihusisha makutano ya kibiashara hususani wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao alikuwa wakitaka kuongea maswala ya kibiashara.
“Your Majest!!!”Roma alijikuta akigeuka mara baada ya kusikia sauti ambazo alikuwa akizifahamu na hii ni baada ya kuingia upande huu wa VIP akiwa ameambatana na Rose , lakini sasa Rose alijikuta akishangaa baada ya kuwaona mabwana hawa wa kizungu wakikakamaa kama vile wamemuona kiongozi mkubwa wa nchi.
The Eagles wote ni kama walikuwa wameambizana kwani kila mmoja alikuwa hapo ndani ,huku kwa wadada wakiwa na wanaume wa kibongo na kwa wanaume wakiwa na warembo wa kitanzania , Roma aliwaangalia mmoja mmoja na kugudua kuwa mtu pekee ambaye amekosekana ndani ya hilo eneo alikuwa ni Deigo na Btam.
“Bebi mbona wako hivyo”Aliuliza Roma huku akiwaangalia hawa vijana walivyobadilika ghafla.
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI:SINGANOJR
SEHEMU YA 105
Roma hakuona haja ya kumficha tena ili hali wanajeshi hawa wapo ndani ya hili eneo lakini pia Rose alikuwa ashaona namna ambavyo wanajeshi hawa wamebadilika , lakini pia aliona anasababu ya kumwambia Rose kutokana na kwamba yeye ndie aliemsadia makazi ya vijana wake hapa Tanzania pasipo kuuliza sana maswali.
“Mnaweza kuendelea na Starehe yenu vijana msinizigantie”Aliongea Roma na kuwafanya vijana hawa washushe pumzi kwani hawakuwa ni wenye kutegemea uwepo wa Roma maeneo hayo .
Ukweli ni kwamba The Eagles baada ya kufika Tanzania hawakupenda kujifungia ndani tu , walitamani pia kula bata kama binadamu wengine , na katika sheria za jeshi lao , hawakuwa pia wakizuiwa kula bata kisheria ,hivyo hawakuona tabu ya kutafuta warembo na wanaume pia, lakini sasa k katika kuchagua maeneo ya kula bata hawakutaka maeneo ambayo walidhania watagongana na Mfalme Pluto.
Na kwa kulijua hilo walianza kutafuta maeneo ya mbali na anapoishi Roma na katika tafuta yao walijikuta wakiangukia ndani ya Club B, huku wakidhania kuwa Roma hawezi kufika hayo maeneo , lakini pia walipendezwa na amsha asmha ndani ya Club hio.
“Darling ! Unamaanisha unamiliki wanajeshi?”
“Bebi Rose cha kushangaa nini sasa hapo , si kama wewe tu unavyomiliki kundi la Tembo”
“Hata kama mpenzi , lakini kumiliki wanajeshi sio jambo dogo , tena wakizungu lazima niwe na maswali”Aliongea Rose huku akiwa amemlalia Roma kwenye mapaja wakiwa wameketi kwenye masofa , huku Roma akicheza cheza na nywele za Rose.
“Unakumbuka mara yetu ya kwanza mimi na wewe kukutana?”
“Siwezi kusahau , nadhani ndio siku ya kipekee sana kwenye maisha yangu”
“Sasa ile ndio siku yangu ya kufika hapa Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa Mwanza na mtu wa kwanza kuongea nae hapa Tanzania ni wewe”Rose alishangaa hakuwa akilijua hilo.
“Kwahio ulitokea wapi?”
“Nilitokea Uingereza”
“kwahio hawa wanaeshi [ia wametokea Uingereza”
“Sehemu waliotokea ni mbali na Uingereza , siku moja nitakupeleka”Aliongea Roma na kumfanya Rose ajinyanyue na kumkumbatia Roma.
Rose hakutaka kuuliza maswali mengi , kwani alijiambia kwa kila nafasi ambayo Roma atakuwa anamkumbuka atakuwa anaitumia vyema kufanya nae mapenzi , ili hata wasipoonana kwa muda mrefu asiwe na hamu tena.
Walifanyana kwa Zaidi ya Masaa matatu na hii ilimfanya Rose kuchoka mno na hawakutakia kubaki hapo ndani Bar, walihamia nyumbani kwa Rose na Roma hakupanga kabisa kurudi nyumbani usiku huo.
“Vipi ulimalizaje swala la Baba yako?”Aliuliza Roma uda wa asubuhi mara baada ya kupiga cha asubuhi , sasa Roma alikuwa akinywa chai kabisa kwani hakuwa na mpango wa kurudi nyumbani , alipanga aende moja kwa moja kazini.
“Kundi lake kwa sasa lipo chini yangu , nimemfilisi mali zak zote , ila kwenye kumuua nilishindwa kwani licha ya kwamba ni adui yangu , lakini pia ni baba yangu”Aliongea Rose.
“Kwahio umeamua kufanya nini?”
“Mpaka sasa ninavyoongea yupo Kisiwa cha Heligoland”
“Unamaanisha Ujerumani?”
“Ndio babe”Roma alijikuta akishangaa kwani alikuwa akikifahamu hiki kisiwa sana kwa kuwa mbali.
“Nimeamua kumpeleka huko akaanze maisha upya , sijamuachia hata shilingi licha ya kuagiza vijana wakamuweke huko”
“Ni wazo zuri pia , nadhani atazeekea huko na hatoweza kupata nafasi ya kurudi Tanzania”
“Ndio na nimehakikisha hana aina yoyote ya mawasiliano na watu wa Tanzania kwenye kundi lake”Aliongea Rose na kumfanya Roma afikirie kidogo.
“Rose najua mpaka sasa biashara yako imekuwa kubwa na ukubwa wa biashara yako ndio wingi wa maadui, unaonaje ukitumia wanajeshi wangu”
“Lakini bebi sijui hata kwasababu gani umewaleta Tanzania kwanini niwatumie?”
“Sababu ya kuwaleta Tanzania ni kutokana na kwamba kitendo cha mimi kuwa karibu na nyie kinawaweka kwenye uhatari kutokana na upande wangu wa pili ambao watu wengi hamuufahamu na nikwambie tu , mpaka sasa nina maadu kila nchi ndani ya hii dunia”Rose alishangaa.
“Yeah! Usishangae , nina maadui wengi na ndio maana nimewaingiza The Eagles ndani ya Tanzania na madhumuni makuu ni ili wanisaidie kugundua watu wabaya wanaongia(Detect) ndani ya Tanzania”
“Mpenzi sijui historia yako ya nyuma , lakini mimi nipo tayari kukabiliana na maadui zako muda wowote, ila kwa mkeo sidhani kama ataweza”
“Ndio maana nimewaleta hapa nchini, kitendo cha mimi kuona na Edna ni Dhahiri sasa maadui zangu watakuwa wanafahamu udhaifu wangu na watamtageti, hivyo napaswa kumlinda pia”
“Kwahio umewaleta kwa ajili ya Edna tu?”Aliuliza Rose kwa wivu na Roma alitabasamu na kumfinya.
“Sijawaleta kwa ajili ya Edna pekee na ndio maana nataka wakusiadie hata kuwafundisha mapigano vijana wako ili wawe na ujuzi”Aliongea Roma na Rose aliitikia.
“Nitatafuta nafasi ya kukupeleka kwenda kuonana na mkuu wa kikosi ,Diego ,ili nikutambulishe”
“Sawa Mpenzi,Kunywa chai unaachelewa la sivyo mkeo hatokupandisha cheo”
“Bebi Rose mke wangu ashanipandisha cheo tayari”
“Kweli!!”
“Yeah!Anapanga kunifungulia kampuni niiongoze”Aliongea Roma na kumfanya Rose aone Edna anampenda sana Roma maana mpaka kuwaza kumfungulia kampuni sio swala dogo.
“Kwa hio Mpenzi ukishakabidhiwa hio kampuni si utakuwa na maamuzi ya juu kabisa?”
“Ndio , ila sinampango wa kufanya kazi nitagawa majukumu kwa wasaidizi wangu , mimi kukaa ofisini , kufanya vikao na kuandaa nyaraka kutanichosha sana , ni bora unipe kazi ya kuilipua Marekani”Rose alijikuta akitabasamu.
“Bebi unaonaje nikiwa muewekezaji kwenye kampuni yako?”
“Unataka kuwekeza?”
“Ndio ukweli ni kwamba licha ya kwamba kikundi changu kinajihusisha na Madawa ya kulevya , lakini hii biashara siipendi na napanga niache kabisa , licha ya kwamba jina la kundi langu litabaki na kikosi kizima , lakini nataka niwe tofauti na makundi mengine, nataka niwekeze kwenye biashara halali niachane na uuzaji wa madawa ya kulevya , lakini licha ya kwamba nina pesa nyingi , lakini mpaka sasa nimekosa mahali sahihi pa kuziwekeza zijiongeze , ila kwasababu unakwenda kukabidhiwa kampuni nataka tuunde umoja, nitawekeza kwa siri pasipo ya mkeo kujua”Aliongea Rose.
“Kwahio unataka kuwekeza?”
“Ndio najua biashara ya burudani kwa Tanzania kwasasa haipo sana vizuri , ila kama utakuwa na mipango mizuri na kuitangaza kimataifa itaweza kukua haraka na faida kuwa kubwa , licha ya kwamba inaweza isiwe rahisi lakini naamini itatengeneza faida” Roma alitingisha kichwa na kuona ni jambo sawa tu kwa Rose kuwekeza kwenye kampuni, kwani pia hio itafanya kampuni kuimarika kwa upande wa kifedha.
“Umefikiria vizuri inaonekana mpenzi wangu baadae untakuja kuwa mfanyabiashara mkubwa”Aliongea Roma na kumfanya Rose atabasamu.
“Roma nataka siku tupigane?”
“Hahaha.. Rose najua una mafunzo ya kimapigano , lakini hata nisitumie uwezo wangu na uunganike na kikosi chako hamuuwezi kupambana na mimi”
“Hubby! Unajua ni kiumbe gani kina nguvu sana duniani?”Aliuliza Rose na Roma alitingisha mabega kwamba hajui.
“Kiumbe chenye nguvu sana duniani ni Mwanamke , Sisi kila mwezi tunableed’ lakini bado tunaonakena kuwa na nguvu , hivyo hata tukipigana siwezi kukubali unishinde kirahisi”Roma alitabasamu
“Hehe… Bebi Rose unatakiwa kujua mpenzi wako mimi sio wa kawaida , wanaume wengine wanaweza kulinda nyumba ili wezi wasiingie ndani kuiba ila mimi nahakikisha nalinda heshima yangu kitandani”
“Muone sasa ..mimi sijui hayo ila ninachojua wewe mwanaume ambaye huna aibu”Aliongea huku akimpokonya kikombe.
Ilikuwa ni siku ya jumamosi asubuhi wanafamilia wanne yaani Bi Wema , Roma ,Sophie na Edna walikuwa mezani wakijipatia chai ya asubuhi nzito ambayo iliandaliwa na Sophia na Bi Wema.
Roma alionekana asubuhi hii kufurahia kweli chai hio , kwani alikuwa akila kwa spidi kubwa mno kiasi kwamba ni kama kuna mtu aliekuwa akishindana nae kula, Edna alijikuta akimwangalia Roma namna anavyokula na kujikuta akishindwa kuvumilia.
“Roma kula taratibu bwana , unakulaje kama mbuzi”
“Kama mimi ni mbuzi wewe utakuwa majani”Edna alijikuta akimpotezea kwani aliona ishakuwa tabia ya Roma , huku Sophia na Bi Wema waliokuwa pembeni wakiangalia wanandoa hawa walivyokuwa wakiongeleshana.
Sophia kwanza alishangazwa na maisha ya Roma na Edna , kwani hakutegemea wanandoa kuishi vyumba tofauti tokea afikie hapo , kuna muda alijiuliza labda ni kutokana na kwamba kuna migogoro kati yao , lakini alikaa Zaidi ya siku mbili kwenye hio familia na Roma na Edna hawakuonekana kulala pamoja na hili halikumhuzunisha ila lilimfurahisha, lakini sasa kwa macho yake jinsi alivyokuwa akimwangalia Roma na Edna aliona kuna kitu ambacho kinaendelea kwa hawa wanandoa , kwani licha ya kwamba walionyesha hali ya kuwa mbali kihisia ila aliona muunganiko ambao unaweza kuwa mgumu kwake kuuvunja na sio kwa Sophia tu ,hata Bi Wema alishaanza kuona tabia za mabadiliko za Edna tokea Roma afike hapo ndani kwenye familia , alimuona Edna akianza kubadilisha baadhi ya tabia zake ambazo alikuwa ashaanza kuzizoea na aliona kabisa Edna alikuwa akifanya makusudi tu lakini ana mapenzi na Roma.
Wakati Roma akiwa anaendelea kula pasipo kujali macho ya Edna , Simu yake iliingia meseji kwa kutetema ndani ya mfuko wake , aliitoa na kuangalia ni nani ambaye katuma ujumbe asubuhi hio siku ya jumamosi.
“Anko Roma leo usiku nafungua biashara kwa pesa ulionikopesha unaonaje ukiwa mteja wangu wa kwanza”Ilikuwani meseji kutoka kwa Yezi na Roma leo alimkumbuka, kwani zilikuwa zimepita takribani siku tatu tokea aonanae na Yezi, alitabasamu na kisha akaweka kijiko chini na kujibu.
“Okey saa ngapi utafungua, nije niweke Baraka”
“Saa mbili kamili”
“Okey nitafika”Alijibu Roma huku akitabasamu m hakuelewa kwanini anatabasamu , sasa wakati Roma anaendelea kuchati Edna alikuwa akimwangalia muda wote na kwa jinsi ambavyo alimuona Roma anachati, alijua tu ni mwanamke na hakujua ni mwanamke yupi kati ya wale aliokuwa akiwajua.
“Bi Wema naenda kazini , nitachelewa kurudi leo nina miadi na mtu usiku”Aliongea Edna huku akinyanyika na kuchukua mkoba wake.
“Miss lakini leo ni wikiend , tukuletee chakula mchana?”Aliuliza Bi Wema huku Roma akiendelea na kunywa chai yake bila habari hakuona utofauti wowote.
“Nitakula huko huko usiniletee na usiku msinihesabu”Aliongea na kutokomea nje na ni mvumo wa gari tu uliosikika kwenye masikio ya Bi wema na Roma pamoja na Sophie.
“Bro ila una mke ana wivu”Aliongea Sophie na kumfanya Roma amuangalie kwani hakuelewa alichokuwa anamaanisha.
“Unamaanisha nini Sophie?”
“Hahaha..yaani unashangaza kwakweli , unashindajwe kujua mabadiliko ya mkeo”
“Ndio Roma sidhani kama Edna ana miadi ya kuonana na mtu siku ya leo”Aliongea Bi Wema na kumfanya Roma asielewe vizuri.
“Mkeo alikuona unavyochatika na kisimu chako cha Bei Rahisi , huku ukiwa na tabasamu nje nje , yaani Roma unakichwa kigumu sijawahi pata ona”Aliongea Sophie na kumfanya Roma aelewe , hakujua kama kitendo cha kuchati kilimfanya Edna kuwa na wivu , lakini pia alijiuliza Wivu wa Edna umeanza lini.
SEHEMU YA 106
I990-CIA HQ USA ,VIRGINIA
Ilikuwa ni siku ya asubuhi ndani ya makao makuu ya CIA ambayo yanapatikana ndani ya jimbo la Virginia sehemu inayofahamika kwa jina la Lenley.
Sasa asubuhi hii ndani ya makao makuu haya alionekana bwana mmoja hivi wa kizungu aliekuwa akiingia ndani ya hili eneo akiwa na gari yake aina ya Benz , bwana huyu baada ya kushuka kutoka kwenye gari sehemu alipopaki , alifuatwa na bwana mwingine ambaye alikuwa akilingana nae kiumri , kwa makadirio ya miaka kama therathini hivi , utofauti wao kati ya mtu alieingia hapo ndani na aliemfata ndani ya eneo hilo la Maegesho ni unene , jamaa aliengia alikuwa ni ni mnene kidogo kutokana na mwili wake kuonesha ulikuwa ni ule wa mazoezi , lakini aliemfuata eneo la maegesho ya magari alikuwa ni mwembamba na hakua akionyesha kama mtu ambaye alikuwa ni wa kuchukua mazoezi.
“Mr Carlos ! Karibu sana kwa mara nyingine ndani ya makao makuu ya CIA , Naitwa ajenti Smith”
“Asante sana Mr Smith kwa kunipokea”
“Your Welcome , nifuate Director anakusubiria”Aliongea bana huyu huku akianza kutembea kuelekea ndani ya jengo hili kubwa ambalo kila mtu aliekuwwepo hapa ndani alikuwa bize na majukumu, ni eneo ambalo lina ulinzi mkubwa sana.
Carlos alionesha hali ya kukagua sana hili eneo , kwa muonekano wake ni kama alikuwa hajafika ndani ya hili eneo kwa muda mrefu sana , kwani alionesha hali ya kushangaa mabadiliko ya miundo mbinu.
“Kuna mabadiliko makubwa ndani ya hili eneo tokea nilivyoondoka kwenda Vietnam”
“You seems to be surprised?”
“Very Much”
“Since then we made a lot of Upgrade , All thanks to Mr President”Aliongea huku akifungua mlango mwingine upande wa kulia kwenye Korido hii ndefu iliokuwa na idara nyingi, jamaa huyu alievalia suti yake nyeusi alitabasamu na kumpa ishara ya kuingia na Carlosi akaingia.
“Carlos nice to meet you again after year`s”
“Nice To meet you too Powell”
“Karibu uketi”Aliongea Director mkuu wa kitengo cha intellijensia na kisha akaketi.
“Mr Smith nadhani kazi yako ishaisha na sasa nitaendelea na Carlos”
“Thank you Director”Aliongea Smith na kisha akatoka na kuwaacha Director na Carlos.
“Carlos kwanza ni kupe hongera sana kwa kazi kubwa uliokuwa unafanya Vietnam”
“Nashukuru sana Director”
“lakini pia nikupe pole , kwani baada ya kurudi ulipaswa kuwa likizo , lakini kutokana na kuwepo wa jambo la muhimu sana ,ambalo limetokea sikuwa na jinsi ya kukurudisha kazini, nadhani unafahamu kabisa kwamba kazi hii inahitaji kujitoa”
“Ndio naelewa Mr Powell na nadhani itakuwa vizuri sana kama utaenda moja kwa moja , kwani baada ya kupokea tu simu yako nilijua kuna jambo la muhimu na kama nisngetaka kulifanya usingeniona hapa, nadhani unanifahamu”
“Ndio nakuelewa kabisa Carlos”Aliongea bwana Poweli ambaye alikuwa mnene kidogo , mwenye nyywere nyeupe ambazo ziliashiria uzee , kwa haraka haraka alionekana kuwa na miaka sitini hivi kupanda, Poweli ni moja ya wafanyakazi wenye umri mkubwa sana kuhudumu ndani ya kitengo cha kijasusi cha CIA na hakuonesha dalili yoyote ya kustaafu.
“Okey Carlos nitakuomba usome hio karatasi kwa dakika chache kabla hatujaendelea na mazungumzo”Aliongea na kisha Carlos alichukua hio katatasi na kuanza kusoma.
“Pro Human Project !!”
“Ndio Carlos , hili ndio jambo ambalo unakwenda kulifanyia kazi nchini Bolivia”Aliongea na kisha akampatia karatsi nyingine.
“Ryan Fredrin ni moja ya watu ambao utakwenda kufanya nao kazi, kutokana na hio kambi kuwa msituni ndio maana tumekupendekeza”
“Misheni yangu ni ipi?”
“Unachotakiwa ni kuzamia ndani ya hii kambi pasipo kujulikana , ukishaingia kazi yako kubwa ni kuandaa mazingira kwa kazi ambayo ataifanya Ryani”
“And Then?”
“Kama Ryan akifanikisha wajibu wake hakikisha unamchukua mtoto , nina uhakika Ryani ataungana na mke wake kumlinda mtoto wao na pia wanaweza wakawa na mpango wa kukimbia na mtoto wao , hakikisha swala hilo halitokei, ukishampata mtoto hakikisha unamuua Ryani pamoja na Epholia”Carlosi alishangaa.
“Okey naomba kuuliza Poweli , kwa jinsi nilivyosoma hapa ni kwamba project hii inahusisha watoto kumi na mbili , kwanini mnataka mtoto mmoja tu huyu wa Ryan na Epholia?”
“Kwasababu hii project mheshimiwa 41 President alikuwa akiifatilia kwa muda mrefu sana tokea ikiwa kwenye Preliminary Stage(hatua za Mwnzo) na mafanikio yake mpaka sasa ni asilimia 8.3%, nadhani mpaka hapo unaelewa kwanini tunahitaji mtoto mmoja kati ya kumi na mbili?”Carlos alitikia kwa kichwa.
“Kwanini Ryani ahusishwe kwenye hii misheni , kwani ninaweza kwenda kumchukua mtoto pekee bila msaada wowote”Alitabasamu.
“Only parent can identify their Child without mistake. Hivyo hayahitajiki makosa, hatuna picha ya kumtambua mtoto wa Ryan, lakini tuna inntellijensia ya mtoto wa Epholia na Ryan kutengeneza asilimia 8.3 za mafanikio”Carlos alimuelewa vyema Director.
“Kwanzia muda huu misheni ishaanza na maandalizi yako ya safari yapo tayari , utaingia Bolivia kama Interpool Ajent , the Resr will depend with your efficiency , una wiki mbili tu tunahitaji taarifa kutoka kwako”
“Yes sir”Aliongea Carlos na kisha akatoka ndani ya ofisi hio.
Hii ni kabla ya kulipuliwa kwa kambi iliokuwa kule La Paz ,Bolivia kwenye ,msitu wa Amazoni.
Swali:Je Carlos alifanikiwa, tukio hilo linauhusiano gani na simulizi
Utaendelea ufahamu kadri simulizi inavyoendelea.
*****
Roma alijisikia aibu kwa namna ambavyo Sophie alikuwa amemshushua , ila hakutaka kufikiria sana , siku hii ya leo alipanga kubakia nyumbani tu.
Sophie na Bi wema walionekana kuzoeana kwa muda mfupi sana kwani walikuwa wakicheka na kumfanya Roma aliekuwa amejipumzisha chumbani kwake awasikie na aliishia kutabasamu tu kwa ujanja wa Sophia , kwani Sophia kwa kumuangalia alikuwa mpole ila akizoeana na mtu anakua muongeaji sana.
Chakula cha mchana Roma alishuka na kula kama kawaida na kurudi chumbani kuangalia runinga kupoteza poteza muda .
Licha ya Roma kutojali maneno ya Sophia juu ya wivu wa Edna lakini alikuwa akikumbuka kabisa , aliona kama maneno hayo yana ukweli basi huenda Edna ashaanza kumpenda , alikaa chumbani kwa kufikiria kwa masaa kadhaa na alijikuta akipotelea usingizini .
Roma alijikuta akija kushituka saa moja moja aliingia bafuni akaswaki na kuoga na akashuka mpaka chini sebuleni.
“Bi wema Edna asharudi?”Aliuliza Roma baada ya kumkuta Bi Wema aliekuwa bize kuangalia Runinga.
“Hajarudi bado”
“Bi Wema leo usiniwekee chakula”Aliongea Roma na kisha alipandisha juu na ndani ya dakika chache tu Bi Wema alimuona Roma akishuka akiwa amebadili mavazi , hakutaka kuuliza Roma anaenda wapi ila alikisia.
Roma alingia kwenye gari yake na kutafuta namba ya Edna na kupiga.
“Unasemaje?”Ilikuwa ni sauti ya Kibabe iliomfanya Roma atabasamu na ukauzu wa mke wake.
“Uko wapi?”
“Ofisini! Kuna nini?”
“Hakuna”Aliongea Roma na kisha akakata simu na kuwasha gari na kutoka.
Baada ya masaa kadhaa tu Roma alikuwa akiingiza gari sehemu ya maegesho kwenye kampuni ya Vexto , alimuona Chiara na John waliokuwa ndani ya eneo hili na kuwapa ishara waondoke na walitingisha vichwa vyao na wakawasha gari yao na kuondoka.
Edna alikuwa bize mno yaani haikueleweka alianza kufanyakazi saa ngapi kwani muda wote alikuwa amekodolea tarakishi yake macho huku akiwa amevaa miwani ya kumkinga na mwanga wa bluu.
Upande wa nje Monica pia alikuwepo na Roma ile anafika ndani ya hili eneo alimkuta mwanadada huyu akiwa amesinzia alionekana kuchoka kweli , na alimuonea huruma , hakutaka kumuamsha , alimpita na kuingia moja kwa moja ofisini kwa mke wake.
“Umekuja kufanya nini?”
“Edna Monica kalala , nenda kamwambie aende nyumbani , unamtesa mtoto wa watu hata kama unamlipa”Aliongea Roma huku akikaa kwenye masofa na Edna alijikuta akikumbuka kuwa Monica alikuwa amekuja nae siku hio na alikuwa amesahau kwani muda wote alikuwa amejichimbia kufanya kazi pasipo kupumzika.,aliangalia saa na kisha akatoka mpaka nje na kumuamsha Monica na kumwambia aende nyumbani.
“Malizia kuna sehemu nataka unisindikize”Aliongea Roma mara baada ya Edna kurudi na Edna alishangaa.
“Wapi nina majukumu mengi Roma”
“Wife kwanini wewe kila siku ni mwenye kuwa na majukumu unafikiri wengine hawana majukumu”Aliongea Roma na kumfanya Edna afikirie kidogo.
“Okey tunaweza kwenda nitamalizia nyumbani”Aliongea Edna na kumfanya Roma atoe tabasamu la uchungu.
Dakika chche mbele Roma alikuwa akiingiza gari ndani ya Kigamboni Pongoni Beach , mwanzo Edna aliwazia huenda Roma anamrudisha nyumbani , lakini walivyochukua barabara nyingine alishangaa kidogo lakini hakutaka kuuliza alisubiria kuona mwisho wake ni wapi Roma anampeleka.
“Wife leo ni siku yetu ya ‘Date’ aliongea Roma na kisha akamshika Edna mkono na kuanza kutembea kueleka upande wa Beach na hii ni baada ya kuegesha gari upande wa pili wa barabara.
Edna alitaka ajitoe kwa Roma ila alishindwa kwani Roma alimshika vizuri na alijiona hana ujanja Zaidi ya kufuata , watu walikuwa wakiawaangalia na kuishia kutabasamu , kwani licha ya giza , urembo wa Edna haukujificha.
Roma alijikuta akitabasamu mara baada ya kuona maboresho ambayo Yezi alikuwa ameyafanya kwenye kibanda chake cha chipsi na kutokana na leo ilikuwa ni wikiend watu walikuwa wengi wakipita pita eneo hili na Yezi aliekuwa bize, alikuwa akionekana kwenye macho ya Roma kwa umbali.
Yezi alikuwa bize mno na kumfanya roma atabasamu na kufurahishwa na juhudi za Yezi.
“Anko Roma !”Aliita Yezi baada ya kumuona na kuwasogelea.
“Sister Edna!!!”Aliita Yezi kwa mshituko
“Yezi!!!”Roma alishangaaa.
ITAENDELEA
NICHEKI WATSAPP 0687151346 NIKUPE UTARATIBU WA KUPATA MWENDELEZO , UNLESS OTHERWISE TUONANE JUMAPILI
Ndio mkuuMambo bulibuli singanor
singanojr naunga mkono hoja ya mkuu mweusi asili tupe zawadi ya Nyerere day kabla ya zile episodes
Kweli kabisa tunamuenzije baba wa Taifa bila kuangusha kitu siku ya leo...weekend imeqnza leosinganojr naunga mkono hoja ya mkuu mweusi asili tupe zawadi ya Nyerere day kabla ya zile episodes za weekend
Singanonr!! Naamini uko salama kabisa...utakuwa untest mitambo 123, tunajaribu...bila kutupia weekend inakuwa kama j4.kesho inshallah
Hadithi nzuri sana ila unavuta sana mkuu.eneo moja linachukua pakubwa sana.kwa mfano leo hujatundea haki kwa kweli.Yaaani ni kama picha ndio kwanza linaanza...daaah niko pale j5 nimekaa seat ya mbele.