Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Duh
 
SEHEMU YA 107

Edna alijikuta akishindwa kujizuia na kumsogelea Yezi na kumkumbatia , huku Roma akiwaangalia , alijikuta wakati huo huo akikumbuka stori ya Yezi kutoroka kituo cha kulelea watoto .

“Yezi hivi unajua ni kwa kiasi gani tulikutafuta baada ya kutoroka kituoni”Aliongea Edna na kumfanya Yezi ashindwe kujibu na kuishia kulia kwa kwikwi.

Ukweli ni kwamba Yezi kuna kipindi maisha yalikuwa magumu sana kwake na kutamani kurudi , lakini alishindwa kutokana na namna ambavyo aliondoka , ule ujasiri wa kurudi ulimpotea kabisa.

Roma baada ya kusikia hivyo ndio alipata kujua sasa Yezi alikuwa ametoroka kituo cha kulelea Yatima cha Son And Daughter Orphanage.

“Aunt Edna Am Soryy najua wewe na Mama Issa mlikuwa na wakati mgumu baada ya mimi kuondoka”

“Sasa kama ulijua tutakuwa kwenye wakati mgumu kwanini umeondoka , unajua ni kiasi gani Mama Issa amekuwa ni mwenye kukuwazia tokea utoroke”Yezi alishindwa hata kujibu ,alijiona ni mwenye hatia .

Edna alishindwa kumgombeza Zaidi Yezi, kwani ilikuwa imepita kama mwaka mmoja tokea Yezi atoroke , aliangalia mazingira ya biashara ya Yezi na kujikuta akimuonea huruma, aliona ni maisha magumu sana Yezi alipitia ukilinganisha pia yeye ni msichana.

“Umefahamiana vipi na Yezi?”Aliuliza Edna huku akimwangalia Roma na Yezi alidakia swali hilo na kujibu kwa kuelezea tukio zima.

“Kumbe ile siku hakuwa kwa wanawake wake , nilimuwazia vibaya”Aliwaza Edna.

“But Aunt hujanieleza huyu Anko ni nani kwako?”.

“Ni Mke wangu Yezi , inaonekena kukutana kwetu kulikuwa na sababu”Aliongea Roma baada ya kuona Edna anasita sita , ila Yezi alishangaa hakujua yule dada tajiri mwenye moyo mzuri ambaye alikuwa akiwasaidia watoto Yatima pasipo kujitangaza, lakini pia mwanadada ambaye alikuwa aliekuwa amkimjua kama tajiri ukijumlisha pia na urembo wa Edna, alishangaa Roma mwanaume wa kawaida kumuoa Edna.

“Hongera Anko , Aunt Edna ni mwanamke mwenye Roho nzuri sana na nni mrembo”Aliongea Yezi na kumfanya Edna aone aibu kidogo kusifiwa ila alijisikia vizuri.

Edna alionesha furaha yake ya wazi baada ya kukutana na Yezi kwa mara nyingine tokea atoroke kwenye kituo cha Son And Daughter Ophanaage ,Yezi almwelezea Edna maisha yake yote ambayo alikuwa akifanya tokea alivyotoka kituoni huku akificha kumwambia juu ya kupelekwa polisi mara kadhaa, lakini pia kujiaunga na kundi la watoto watukutu la Sherif,Roma hakutaka kuingilia mazungumzo hayo, aliacha wawili hao waongee.

Na kwa jinsi Edna alivyokuwa akionekana , ilionesha alikuwa akimpenda sana Yezi , kwa kiasi kikubwa sana.

“Vipi kuhusu Shule?”.

“Aunt Edna ushasahau nilitoroka kabla ya majibu ya kidato cha sita kutoka?”Aliongea Yezi na kumfanya Edna akumbuke na kuona amueliza swali la kijinga.

“Matokeo yako yalikuwaje, au hukufuatilia?”

“Nilifaulu kwa division Two”

“Vipi kuhusu mpango wa kwenda chuo?”

“Nilikuwa nikifikiria kujiunga chuo , lakini nilipata ugumu kurudi kituoni kufatilia vyeti vyangu”Aliuongea Yezi na Edna aliona lazima Yezi angepata ugumu , kwani kwa namna ambavyo Yezi aliondoka, kwa mtu yoyote ingekuwa ngumu kurudi tena pasipo kuwa na hatia

Edna licha ya kuona biashara ya Yezi kuwa ndogo , lakini pia mazingira kutoyapenda alishindwa kumwambia Yezi asifanye hio biashara , alimuona Yezi ni mtu mzima tayari hivyo kumwambia kipi cha kufanya wakati huo ilikuwa umepita , alitaka Yezi afanye kile ambacho anaona ni sahihi, na yeye mwenyewe atamsaidia kimawazo tu ili afanye maamuzi sahihi , kwani kwa jinsi ambavyo Yezi alimsimulia maisha yake yalivyokuwa aliona kabisa Yezi amekuwa mtu mzima ambaye amepitia changamoto za kimaisha hivyo atakuwa tayari na ukomavu wa akili katika kufanya maamuzi yanayohusu maisha yake..

“Kwahio ndio ulikuwa ulinileta kuonana na Yezi?”

“Ndio Wife , asubuhi alinitaairifu anafungua biashara yake upya , hivyo nilitaka tukamuunge mkono kama wateja wake wa kwanza”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie , alimuona Roma kuwa na Roho nzuri.

“Nilidhania asubuhi anachati na wanawake zake , nimemuwzia vibaya kwa mara mbili mfululizo”Aliwaza Edna

“Uliwezaje kumsaidia Yezi pesa na akapokea?”

“Kwanini unauliza hivyo?”

“Humjui Yezi wewe, tokea aliuvyokuwa mdogo sheria yake ilikuwa ni moja, hakupenda kupokea msaada kabisa kutoka kwa watu hususani pesa”Roma aliona maneno ya Edna kuwa na ukweli kwa namna ambavyo Yezi alizikataa pesa zake ile siku.

“Wife hio chukulia kama siri yangu na Yezi”Aliongea Roma na kumfanya Edna avute mdomo na kupotezea.

“Nimefurahi kuonana na Yezi leo, nilitokea kumpenda sana wakati akiwa ndani ya kituo”Aliongea na wakati huu walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kupata chakula cha usiku pamoja na Yezi.

“Mke wangu hata mimi nimeona ulivyokuwa na furaha,unaonaje ukinizawadia hata busu sasa mumeo”Aliongea Roma na kumfanya Edna akose utulivu huku akianza kukumbuka ndoto yake ya siku kadhaa zilizopita

“Nataka unisadie kumshawishi Yezi arudi shule , lakini pia umpeleke akaonane na Mama Issa kwani amekuwa ni mwenye kumuwazia sana na amekuwa akiangalia picha yake mara kwa mara na nilimuonea huruma”Aliongea akiipotezea topiki

“Mama Issa anaonekana kumpenda sana Yezi?”

“Hata kama ni wewe ungempenda, Yezi aliokotwa nje ya kituo na mama Issa akiwa mdogo sana na alimlea mwenyewe mpaka kufikia umri mkubwa ni rahisi kusema ni mtoto wake kabisa , kwanini asimuwazie”

“Sasa kwanini alitoroka?”

“Yezi baada ya kuelezwa ukweli na Mama Issa namna ambavyo aliokotwa kwenye geti la kituo alianza kubadilika na hata sisi wenyewe hatukujua nini kilimpata mpaka kuamua kutoroka , lakini hayo yashapita nataka akaonanae na Mama Issa mwenyewe na wewe utachukua jukumu la kumpeleka”

Roma hakutaka kumpinga mke wake , aliona atii maagizo.

****

Saa saba mchana siku hii hii ya Jumamosi ,ndani nya kituo cha Son And Daughter Orphanage, alionekana Mke wa Tajiri Mohamedi akishuka kwenye Gari aina ya V8 nyeusi akiwa amevalia gauni lake refu lenye rangi nyeupe na nyeusi kama pundamilia na mkoba wake rangi ya khaki.

Muda huo huo wakati Mwanamama huyu akiwa amesimama kwenye hili eneo la Maegesho alisogelewa na Mama Issa na baadhi ya viongozi wa kituo hiki na kwa jinsi walivyomsogelea ni Dhahiri kabisa walikuwa na taarifa ya ujio wa mama huyu na sasa wapo hapo kwa ajili ya kumpokea.

“Karibu sana Mrs Azizi naitwa Tabea Singano Wengi wananifahamu kwa jina la Mama Issa ni mkuu wa hiki kituo”Aliongea Mama Issa huku akipeana mkono.

“Nafurahi sana kukufahamu mama Issa , mara nyingi nilikuwa nikisikia hiki kituo, kumbe ni kikubwa hivi?”Aliongea huku akigeuza macho kulia na kushoto akiangalia majengo ya kituo hiki.

“Ndio ni kituo kikubwa sana ambacho kina kila aina ya Huduma , Karibu sana ndani ya kituo chetu , tumejisikia furaha sana kusikia ujiio wako”Aliongea Mama Issa kwa ukarimu.

Mrs Azizi alimgeukia Derava wake na kumpa ishara a kwamba watoe mizigo.

“Mama Issa nimekuja na mizigo kwa ajili ya kuwasaidia watoto , najionea hata aibu kutofika ndani ya hiki kituo tokea kuanzishwa kwake , lakini naamini utakuwa ni mwanzo mzuri wa mimi kufika mara kwa mara , nimekuwa nikitembelea vituo mbalimbali , lakini nimeshindwa kufika hapa , imekuwa ajabu kweli mpaka najishangaa”Aliongea huku akitabasamu

“Huna haja ya kuzungumza hivyo , wahenga wanasema kila jambo na wakati wake na wewe kufika mahali hapa ni muda sahihi na haujachelewa kabisa , katibu sana”

Baada ya kukaribishana Mama Issa aligawa majukumu kwa ajili ya kushushwa mizigo aliokuja nayo Mrs Azizi , na wakapiga picha ya kumbukumbu na baada ya hatua hio ya kwanza kwa kila mhisani anayefika ndani ya kituo hicho kutoa msaada , hatua inayofuatwa ni kutembezwa ndani ya kituo hiko na kukutanishwa na watoto hawa wanaolelewa , Mrs Azizi alijiambia kuwa kwenye vituo vyote vya kuelelea watoto Yatima ametembelea, hiki kituo ndio kikubwa Tanzania nzima na chenye mazingira mazuri , alifurahishwa na uwepo mpaka wa ‘Swimming pool’.

“Mke wa Raisi wa Kenya amejitahidi kwakweli nampa hongera yake, ni kituo kikubwa sana”

“Ni kweli Maina amekuwa msaada mkubwa kwa jamii nyingi za kiafrika na mimi pia nampa pongezi yake kwa hilo , kwani tokea kuanzishwa kwa kituo hiki ni watoto wengi wamesaidiwa na kwa sasa wanamafanikio makubwa”Aliongea Mama Issa huku wakaongozana mpaka ofisi ya Mama Issa ilipo kwa ajili ya kupewa maelezo ya namna utaratibu wa kituo hiko huendeshwa kama ilivyodesstuli.

Waliingia ndani ya hii ofisi ya Mama Issa , lakini ajabu ni kwamba leo ile picha ya mwanamama iliokuwa ukutani haikuwepo, kama siku ile ambapo Roma alikuja hapo kwa Mara ya kwanza, na haikueleweka kwannini ilikuwa imetolewa.

“Mrs Azizi kama nilivyosema hujachelewa kabisa na ujio wako leo ni wakati sahihi kabisa, na kukaribisha tena ndani ya kituo chetu, nilikuwa nikiusubiria ujio wako Zaidi ya miaka ishirini na hatimae umefika ,na ndio maana nasema ni wakati sahihi”Mrs Azizi hakuelewa anachomaanisha Mama Issa.

“Ni kweli ulikuwa ukinisubiria?,Mbona naona kama kuna jambo lingine kwenye macho yako Mama Issa unataka kuniambia”

“Ni kweli kabisa umepatia, kuna jambo ambalo nataka kukuambia ,ni jambo lakni pia naweza kusema ni maagizo niliopatiwa miaka ishirini iliopita”

“Maagizo, miaka ishirini iliopita!!??”Alishangaa lakini Mama Issa hakujali alinyanyuka kwenye sofa na kusogelea meza yake na akavuta mtoto wa meza na kutoa ufunguo na kisha akasogelea kabati lililokuwepo hapo ndani upande wa kushoto lenye mlango wa mbao na kisha akalifunua na kutoa bahasha za zamani sana za kuhifadhia barua na kutoka nayo.

“Hii ni barua yako niliopewa miaka ishirini iliopita , siku ya kufunguliwa kwa hiki kituo na Madam Maina”

Mke wa tajiri Mohamedi aliangalia barua hio kwa wasiwasi , alijiuliza kama barua hio ilitakiwa kumfikia yeye kwanini hakukabidhiwa mpaka leo hii, na ni kweli barua hio ilikuwa yakwake kwani hata jina lake la Jestina lilionekana pia juu ya bahasha.

“Kwanini haukunipatia hii barua mpaka imepita miaka mingi kiasi hiki?”

“Hayo ndio maagizo niliopewa , nilitakiwa kukukabidhi siku ambayo utafika ndani ya hiki kituo cha kulelea watoto ,hata mimi Madam amenishangaza kwa maagizo hayo , lakini niliamini kuna jambo kubwa ambalo lipo kwenye hio barua”Aliongea na kumfanya Mama huyu kujawa na shauku kubwa sana ya kujua nini kimeandikwa kwenye hio barua.

“Naruhusiwa kuisoma hapa hapa , au kuna maagizo mengine?”Aliongea kwa wasiwasi

“Unaweza kuisoma hapa hapa , barua hio mpaka sasa wewe ndio mmiliki”Aliongea Mama Issa, na mke wa Tajiri huyu anaefamika kwa jina la Jestina , hakutaka kusubiria hata sekunde kujua ni nini kipo kwenye hio barua, aliifungua haraka haraka na kuanza kuisoma.

Jestina kadri alivyokuwa akisoma hio barua ilimfanya atetemeke mikono huku machozi yakiujaza uso wake , mwanamama huyu alionekana kitu ambacho alikuwa akisoma kilikuwa ni cha kuhuzunisha mno.

“Blandina dada yangu…hihiii,”Mwanamama huyu alijikuta akikosa uvumilivu kabisa na kuachia kilio cha kwikwi na kumfanya Mama Issa amsogelee na kumkumbaitia huku akimpigapiga begani kwa namna ya kumfariji, ni kama mwanamama huyu alikuwa akijua kilichokuwa kikiendelea.

Mwanamama huyu alijikuta akinyamaza na kuinua tena barua na kuanza kusoma , ni kama hakuwa akiamini alichokuwa akikisoma kwenye hio barua, lakini aliishia kujishika moyo wake na kuanza kulia tena, alionekana kuwa kwenye maumivu makali.



SEHEMU YA 108

MIAKA ISHIRINI ILIOPITA.

Ilikuwa ni mchana wa siku ya jumatano , siku ya sikukuu ya Eid al-Fitr saa saba mchana alionekana Blandina akiwa ndani ya Eneo la Bagamoyo Kiwanga, hii siku ilikuwa ndio ya ufunguzi rasmi wa kituo cha kulelea watoto cha Son and Daughter orphanage, licha ya kwamba tayari kituo hiki kilikuwa tayari kishaanza kulelea , lakini ufunguzi wake rasmi haukuwa umefanyika na siku hio ya jumatano ndio sherehe ya ufunguzi ilikuwa ikifanyika rasmi na mheshimiwa Raisi Mkapa ndio aliekuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kituo hiki.

Sherehe za ufunguzi wa hiki kituo hazikudumu muda mrefu , kwani baada ya wageni walioalikwa ndani ya hili eneo kutoa shukrani kwa Blandina aliejitolea kuenga majengo hayo ya kituo, hakukua na cha Ziada na asilimia kubwa ya watu waliokuwa wamealikwa ndani ya hiki kituo walikuwa ni wafanyabiashara na wanasiasa na sherehe hizo pia ziliambatana na Harambee kubwa iliofanyika kwenye hii siku , harambee ambayo ilikuwa ni ya kuchangia maendeleo ya kituo hicho na jambo hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Baada ya Sherehe kuisha Blandina aliongozana na Mama Issa mpaka ofisini kwa ajili ya maongezi na baadhi ya maelekezo.

“Ndio narudi Kenya hivyo Rafiki yangu”Aliongea Blandina.

“Ila Blandina sikubaliani kabisa na maamuzi yako ambayo unataka kufanya , kwaninni unaificha familia yako kama upo hai?”

“Tabea ni Zaidi ya miaka mitatu sasa nimewaficha , muumuzi yangu yananiumiza lakini kwa sasa sina jinsi”

“Huna jinsi kivipi Blandina, utaishi hivyo mpaka lini kwa kujificha , ni sababu gani inakufanya ujifiche ambayo hutaki kuniambia”

“Nitakueleza rafiki yangu kila kitu siku moja , ipo sababu kubwa ya mimi kufanya haya maamuzi”

Mama Issa alimwangalia Blandina kwa huzuni , kwani licha ya kwamba alisoma na Blandina miaka ya nyuma , lakini baada ya wao kumaliza masomo yao hawakupata kuonana tena kwa miaka , mpaka siku walivyokutana kwa bahati Nairobi, wakati Mama Issa akirudi Tanzania akitokea Nchini Uswisi alipokuwa akifanya kazi ,chini ya shirika la UNICEF.

Mama Issa hakujua kabisa maisha ya nyuma ya rafiki yake Blandina na hata pale Blandina alipompa mpango wake wa kujenga kituo cha kulelea watoto nchini Tanzania na akitaka yeye akisimamie kituo hiko hakutaka kupinga kwani pia kwa wakati huo hakuwa na kazi , lakini pia alikuwa na ndoto pia za kusaidia watoto wasiojiweza na wale ambao wapo kwenye mazingira magumu , lakini licha ya pendekezo hilo kutoka kwa Blandinda, Mama Issa alimuona Blandina kama mtu ambaye alikuwa amebadilika na hata pale mwanamama huyu alipokaa chin na kumuuliza Blandina, nini kinaendelea ,na Blandina kumueleza nusu ya ukweli, alijikuta akishangaa.

Blandina alimueleza mama Issa kama familia yake ilikuwa ikijua amefariki na ajali ya ndege na hawajui kama yupo hai , lakini pia akamwambia kuwa anataka ibakie hivyo hivyo na hapa ndipo mwanamama huyu aliposhangaa na kutakakujua sababu ni nini ya kutaka watu wake wakaribu kujua hivyo ilihali alikuwa hai , lakini Blandina hakutaka kumueleza , na kumuahidi siku moja atamuambia ni kipi kilitokea mpaka yeye kutotaka kufahamika kuwa yupo hai.

“Tabea najua una maswali mengi juu ya maamuzi yangu , lakini siwezi kukuambia kwa sasa ni ipi sahabu , hii ni barua siku mdogo wangu akifika hapa kituoni kwa ajili ya kutembelea hiki kituo ambacho tumekianzisha nataka umkabidhi hii barua, na ndio siku ambayo nitakuambia kila kitu kwanini nipo kama nilivyo, Tabea naomba unitunzie hii siri”Aliongea Blandina huku akitokwa na machozi na Tabea alimuonea huruma , alijua kuna kitu kikubwa kinachoendelea kwenye maisha ya rafiki yake ambacho ni cha kuumiza na hakuwa na jinsi kukubali ombi hilo.

“Kwahio asipokuja utaishi hivyo hivyo na siri yako miaka yote?”

“Hii ndio ahadi yangu naweka leo na wewe Tabea”Aliongea na kisha ni kama alikumbuka jambo Fulani na kutoa barua nyingine mbili kwenye begi lake na kumpatia.

“Hizi ni barua za wanafamilia wangu Tabea , yoyote atakaekuja kutembelea hiki kituo mpatie barua moja kati ya hizi kutokana na jina lake , hii ndio ahadi naweka kwako , kama wasipokuja mpaka naingia kaburini basi naamini itakuwa ni majaliwa ambayo Mungu amenipangia na kama watakuja itakuwa pia ni majaliwa ,lakini pia ndio siku ambayo sitaishi kwa kujificha tena”Tabea alishangazwa na maneno yake huku akichukua barua hizo, nah ii ni siku ambayo ilikuwa ni ya ufunguzi wa hiko kituo miaka ishirini nyuma

Tabea aliiishi kwa kusubiria mwanafamilia yoyote ndani ya familia ya Tajiri Azizi waje kutembelea kituo hicho , lakini hakuna ambaye aliweza kufika kwa takribani miaka ishirini , kuna muda mwanamama alikosa uvumilivu na kutaka kwenda kukabidhi barua hizo , lakini kila akikumbuka ahadi aliokuwa amewekeana na rafiki yake alishindwa kabisa.

Kituo kilizidi kuneemeka na kuongezeka ukubwa ,kilizidi kusaidia watoto wenye uhitaji wakiwa wadogo mpaka wakati ambao walifikia umri wa kujitegemea , wahisani wa kutoa msaada walikuja ndani ya hiki kituo kwa wingi akiwemo Tajiri Marium Bibi yake na Edna lakini familia pekee ya Blandina haikuweza kufika, hata baada ya miaka ambayo Blandina mume wake anashinda kiti cha uraisi nchini Kenya hakuna familia yoyote iliowahi kufika ndani ya hiki kituo , Blandina alisubiria familia yake kufika ili ajiweke huru aache kuishi kwa kujificha , lakini waapi , Tabea na yeye aliishi kwa kusubiria familia ya Atanasi ije kutembelea kituo ili siri imtoke moyoni , lakini waapi , wanafamilia hao ni kama kuna nguvu ambayo ilikuwa ikiwafanya wasifike ndani ya hiko kituo , kwani hata magari yao yalikuwa yakipita kabisa nje ya kituo hiko.

Blandina akaishi kwa miaka Zaidi ya ishirini bila kutambulika kama yuko hai na familia yake ilikuwa ishamsahau kabisa na walishamfanyia hata matanga na kubakia kama kumbukumbu.

Blandina kuna muda alitaka kwenda kuonana na familia yake kabla ya Baba yake kuiaga dunia , alihofia sana huyu mwanamama kama baba yake atafariki kabla ya wao kuonana na kujitambulisha kwake kama yu hai , lakini ahadi yake aliojiwekea kwenye moyo wake ilikuwa na nguvu kiasi kwamba alishindwa kuchukua hatua kabisa, Dhamiri na kiapo alichojiwekea mwanamama huyu ni kama Mungu alikikubali kwa asilimia mia moja na ahadi hio ikamfunga..

Naam baada ya miaka Zaidi ya ishirini imepita na sasa ile siku ambayo Tabea alikuwa akiisubiria ilikuwa imefika na leo siku ya Jumamosi hatimae anatua siri ambayo ameitunza kwa miaka mingi kwenye kifua chake .

****

Ilikuwa ni usiku wa jumapili Saa mbili za jioni Roma alionekana ndani ya gari yake aina ya Audi maeneo ya Moroco,Roma usiku huu hakutaka kubaki kabisa nyumbani kutokana na kwamba siku nzima alikuwa tu nyumbani hakutoka , leo hii bwana huyu kwenye kichwa chake alikuwa amepanga apate sehemu ya kutuliza kichwa usiku huu, na mchana yote alikuwa akitafuta mtandaoni ni sehemu gani nzuri kwa ajili ya bata la usiku na sehemu aliokuwa amepata ilikuwa ni Maisha Basement Club , club ambayo ilikuwa ikipatikana ndani ya Makumbusho ndani ya jengo la LAPF tower.

Baada ya kuendesha kwa dakika kama kumi hivi hatimae aliingiza gari yake ndani ya hili eneo, na watu siku hii walionekana kuwa wengi sana jambo ambalo lilimfurahisha kwani hakutaka eneo tulivu , alitaka eneo ambalo litamrusha roho,Warembo kama kawaida walimuangalia Roma kwa macho ya Matamanio kwani waliona gari nzuri aliokuja nayo.

Ndani ya club hii walionekana warembo mbalimbali waliovalia nusu uchi walioo kuwa wakiingia na wale ambao walikuwa wakitoka.

Baada ya kuzama ndani kabisa ya Club hii kubwa tu ndani ya jiji la Dar aliangalia upande wa kushoto na kulia kuona ni sehemu gani kukaa , huku akisikilizia makelele ya mziki yaliokuwa hapa ndani huku watu waliokaa zaidi ya wawili kwa jinsia zote wakiendelea kuburudika.

Roma alipenda sana hili eneo kwa kusukuma muda uende kisha arudi nyumbani , leo hii hakuwa na mpango kabisa wa kuwa na mwanamke , alipanga apate bia mbili tatu na kisha aondoke.

Alichagua upande wa kulia wa hii bar , sehemu ambapo haakuwa na watu wengi sana na kisha akaketi na dakika moja tu baada ya kukaa alikuja muhudumu na Roma aliagiza Heinken na muhudumu huyu wa kiume alitabasamu na kuondoka kuleta kinywaji alichoagizwa.

Ndani ya dakika chache tu Roma alikabidhiwa kinywaji chake huku akinywa taratibu bila habari huku akichora baadhi ya watu waliokuwa wakiingia hapa ndani na ni kama kuna kitu alichokuwa akitafuta.

Sasa ile wakati anamaliza bia yake na kumuita mhudumu kwa ajili ya kumuongeza bia nyingine ,mara aliingia mwanamke Shombe Shombe wa Kiarabu ndani ya hili eneo na kufanya hali ya hewa ibadilike kwani wanaume wote waliokuwa hapa ndani walimkodolea macho kutokana na urembo wa mwanamke huyo.

Yule mwanadada ni kama alikuwa akijua ni wapi anaelekea , kwani alinyoosha moja kwa moja mpaka upande ambao yupo Roma huku akiwa na tabasamu , kwa muonekano wake ni kama alikuwa akiwaambia watu kama nina miadi na mtu, na Roma alimwangalia mrembo huyu kwa macho ya kujiuliza mbona kama anamfuata yeye na makisio yake yalikuwa ni kweli , kwani yule mrembo ambaye alikuwa amevaa kinguo kifupi cha plastiki na kufanya umbile lake alilojaaliwa nalo kuonekana vizuri kwa wanaume hawa na kuamsha matamanio yao kusogea moja kwa moja mpaka kwenye meza yake na kisha akaketi, na hakujali namna ambavyo Roma alikuwa akimwangalia.
 
SEHEMU YA 109

“Hi!”Alisalimia yule mrembo mara baada ya kumfikia Roma na Romaa alitikia huku akimwangalia huyu mwanamke kwa kumchunguza , alionekana mrembo kwenye macho ya Roma , lakini kwa jinsi ambavyo amevaa ilionesha huyu mwanamke alikuja hapo ndani kuuza , hivyo ndio namna ambavyo Roma alimuona.

“Utapendelea nini miss?”Aliuliza mhudumu ambaye alimhudumia Roma dakika kadhaa zilizopita , aliuliza kwa lugha ya Kiswahili.

“Brandy Alexanda or Alexandra” Huyu mwanadada alimjibu kwa lugha ya kingereza safi kile cha kumungunya , na kwa Roma alijjua tu huyu mwanadada kwa rafudhi yake atakuwa ameishi sana Uingereza kutokana na namna yake alivyokuwa anaongea , alikuwa akiongea kama Mzawa.

“Whaat….What!”Mhudumu alionesha hali ya kutokuwa vizuri kwenye swala zima la kuongea kingereza , kwani hakumuelewa yule mwanadada mrembo.

“Amesema leta bia yoyote yenye chapa ya Alexanda au Alexardra”Alirekebisha Roma kwa Kiswahili na Mhudumu alimshukuru Roma kwa kumsaidia maana alikuwa akitoka jasho.

Ndani ya sekunde chache tu Mhudumu alirudi akiwa ameshikilia ‘cocoa colored cocktail’ na kumpatia huyu mwanadada na akapokea na akamgeukia Roma na kumpa tabasamu mwanana.

“Sorry about that, I’ve been overseas for the last few years, so I don’t know how to call for drinks in this country. However, not many people know the name Alexandra, looks like Mister is well-educated when it comes to drinks.”

“Samahani juu kilichotokea , nilikuwa nje ya nchi kwa miaka mingi kidogo hivyo sijui namna ya kuagiza kinywaji ndani ya hili taifa, Hatahivyo sio watu wengi ambao wanajua kutamka Alexandra ,Inaonyesha Mr umeelimika kidogo likija swala la Vinywaji?”Aliongea Mrembo huyu kwa kingereza safi na kumfanya Roma Atabasamu , alipendezwa na namna mrembo huyu alivyokuwa akiongea na alikumbuka mbali.

“To commemorate the King of Britain Edward the 7th and Queen Alexandra’s marriage, that cocktail was made as a present for the queen. Many women like the taste of that drink. If a man has the heart to understand women, then for a man to know all this is nothing special.”

“Kuadhimisha ndoa ya Mfalme wa Uingereza Edward wa 7 na Malkia Alexandra, kinywaji hiko ilitengenezwa kama zawadi kwa malkia. Wanawake wengi wanapenda ladha ya kinywaji hicho. Ikiwa mwanamume ana moyo wa kuelewa wanawake, basi kwa mwanamume kujua haya yote sio kitu cha kipekee sana”Aliongea Roma huku akiinua chupa yake na kugonga Chears

“But amongst the men who entered this place, you’re the only man who didn’t go looking for a woman.”

“Lakini kati ya wanaume walioingia mahali hapa, wewe ndiye mwanaume wa pekee ambaye hauna mwanamke.”Aliongea huyu mrembo na kumfanya Roma azungushe kichwa kuangalia watu waliokuwa hapa ndani na kuona ni kweli yeye pekee ndio aliekuwa yupo peke yake na hii ilimfanya kujua ni kwannini huyu mrembo alikuja moja kwa moja mpaka kwenye meza yake.

“Even if I didn’t look, didn’t you come over?”

“Sijaenda kutafuta lakini si tayari umekuja?”Aliongea Roma huku akitabasamu na mwanadada huyu alitabasamu pia na kisha akanyoosha mkono wake.

“Naitwa Amina”Roma alijikuta akitabasamu na kwa jinsi alivyomuona huyu mwanamke alijikuta akivutiwa nae na ule mpango wake aliokuwa nao wa kutotafuta mwanamke usiku huu aliutupilia mbali na kujiambia huyu mwanamke usiku huu hamuachi , anafaa kwa matumizi ya usiku huo.

“What a unique introduction.Naitwa Roma Ramoni”

“Your introduction is even more special, but at least it’s much more interesting than other men I met this night, Congratulations, you’ve aroused my interes”

Utambulisho wako pia unaonekana kuwa wa kipekee Zaidi na angalau unavutia kuliko wa wanaume wote ambao nimeweza kukutana nao usiku huu , Hongera umeyaamsha matamanio yangu”Aliongea huyu mrembo kwa namna ya kutongoza flani hivi

“What interest?, You want to know my body is made of? If you’re willing to trade at an equal price, perhaps we can reach a mutual understanding”

“Matamanio gani?,Unataka kujua mwili wangu umeumbwaje , kama upo tayari kuniuzia kwa bei ya kawaida , huenda tukafikia maelewano”Aliongea Roma ila mrembo huyu hakukasirika.

“I suspect that such words may not be from the true you, and that’s what sparked my interest. To simply put, I wanted to see if the man in front of me could meet the requirements to be my intimate male companion.”

“Amina ,the truth in this world doesn’t exist, if you’re willing to, I feel that you should make a judgement based on the sharp intuition you ladies have”

“Amina, neno ukweli katika ulimwengu huu halipo, ikiwa uko tayari, nahisi unapaswa kutoa uamuzi kulingana na hisia za kimaamuzi ambazo mnazo nyie wanawake”Kwa jinsi Roma alivyomuona huyu mrembo ni Dhahiri kabisa alikuwa hapa ndani kwa ajili ya kutafuta mwanaume , lakini anashindwa kuongea moja kwa moja.

“Could you explain? I don’t really understand what you mean, Mr. Roma.”

Roma kwanza alitabasamu hakuelewa ni kii huyu mrembo hakuwa akielewa mpaka kufikia hatua hio , aliona ni kama alikuwa akijifanyisha tu.

“Amina! Unajua ni nani aliegundua Redio?”

“Mtu yoyyote aliesoma lazima atakuambia ni Marconi”Alijibu lakini mrembo huyu alimuona Roma kama mtu ambaye hakukubaliana na jibu.

“Kwahio unamaanisha nimekosea?”

“Kulingana na nchi nyingi za magharibi, ni kweli Marconi ndiye aliyevumbua redio. lakini, katika vitabu vya kiada vya Urusi ya Kisoviet ya Zamani , ilikuwa ni Popov; huko Ujerumani, ni Hertz; Bara la Amerika, ni Dreyfus. Ili kukurahisishia tu, Popov wa Urusi alikuwa amefanikiwa kutafiti teknolojia ya redio miaka kadhaa kabla ya Marconi, lakini kwa sababu alihitaji ufadhili wa kiasi cha rubles(hela ya Urusi) 1000, jeshi la Urusi lilikataa moja kwa moja uvumbuzi wake. Na baada ya miaka Kadhaa mbele Marconi alipokea Tuzo ya Nobel Prize baada ya kutangaza kugundua Redio”

“Roma ingawa sijui maneno unayoyasema ni kweli au La , ila hakuna mwanaume ambaye nishawahi kukutana nae anaongea kwa Swaga kama wewe”Aliongea huku akimkonyeza Roma na Roma alitabasamu.

“Kwahio vipi sasa , unakubali au?”

“Congratulations, tonight I’m yours.”

“Hehe..Happy to serve you”Aliongea Roma na kujiona mshindi baada ya kufanikiwa kupata hio pisi na aliona usiku wake unakwenda kuwa wa maana sana.

Wakati sasa Roma anamalizia bia yake ili aondoke na mrembo Amina akajivinjari nae usiku , waliingia wanaume wanne ndani ya hii Bara huku wakiangalia kulia na kushoto na ile wanaangalia mbele waliona walichokuwa wanakitafuta na kusogea kwa spidi mpaka kwenye meza aliokaa Roma.

“Amina Bosi ametuagiza urudi nyumbani sasa hivi na tupo hapa kwa ajili ya kukuchukua”Aliongea mwanaume mmoja hivi mwenye mwili wa mazoezi na alionekana kama bodigadi, alievalia suruali nyeusi cchini kama za jeshi na tisheni ya kubana kifua chake , alikuwa amevimba kifua kwa mazoezi makali.

Mrembo huyu aliwaangalia mabaunsa hawa huku akiwa amejawa na wasiwasi kwenye macho yake na kisha akamgeukia Roma.

“Mr Roma utanicha niondoke na hawa watu au utanitoa mahali hapa ukaufurahie urembo wangu usiku kucha?”Aliongea kwa kingereza chake na Roma akaweka chupa ya bia yake chini na kisha akatoa kiasi cha pesa kwa bia aliokuwa ametumia mrembo huyu na ya kwake na kuweka mezani na kuzuia na chupa na kisha akatabasamu, alijiambia ni mwanaume mjinga pekee anaeweza kuacha mrembo kama huyo aliejirengesha kwake.

“If Miss Amina can bless me with a kiss, I believe tonight we would have such a great time that it would be remembered for a lifetime”

Aliongea Roma na Amina alionekana kuwa romantic kweli kwani alimsogelea Roma na kumbusu shavuni na kumfanya Bodigadi yule kupandwa na hasira na kumsogelea Roma huku akidhamiria kumtoa Amina, lakini Amina hakujua namna ambavyo alibadilsihwa upande na Roma.

“Wewe mpuuzi unakitaka kifo”Aliongea lile baunsa na kurusha ngumi kuelekea usoni kwa Roma , lakini ni kama Roma alimtegemea , kwani ile inamfikia usawa wa uso, alidaka mkono wake sehemu ya muunganiko wa kiganja na mkono na kabla bwana yule hajarusha teke Roma alimkunja kwa nguvu kiganja cha mkono wake na kukipindisha kueleka upande mwingine na kumfanya baunsa atoe ukulele.

Mrembo Amina alijikuwa akishangazwa na tukio hilo , Wale wengine baada ya kuona mwenzao ameshikiliwa kwa namna ile na kutoa ukulele walisogea kwa kasi kwa ajili ya kumchangia Roma, lakini kabla hawajamfikia , Roma alimyanyua kwa nguvu yule Baunsa na kuwarushia wale na kuwafanya wote wadondoke nae huku kuvunjika kwa viti hapa ndani kukisambaa na kufanya watu waanze kusogea.

Roma hakutaka kuleta vurugu Zaidi ,alijua walinzi watakuja muda si mrefu , alimshika Amina mkono na kuwakwepa wale mabaunsa na kutoka nje haraka huku watu wakiwashangaa , lakini wakimshangaa Zaidi Roma kwani kwa namna ambavyo alimrusha yule bodigadi ni kama mpira.

“You belong to me, and not the other way around. Obediently stay in your seat and buckle up, don’t delay what’s important”Aliongea Roma kwa kumuamrisha Amina na kisha akaliwasha gari.

Mabaunsa yalinyanyuka harakaharaka na kukimbilia nje , lakini walikuwa wamechelewa kwani ile wanatoka gari ilikuwa ikitokomea barabarani upande wa Moroco , waliifukuzia na Roma aliwaona kwenye kioo namna ambavyo wanakuja na akatabasamu , alichukua barabara ya Magomeni na ndani ya dakika chache tu aliwaacha mbali sana baada ya kufika makutano ya barabara ya Karume na Kariakoo , aliendelea kuendesha gari huku mrembo huyu akimshangaa Roma na kuzidi kuvutiwa , alionesha kupenda wanaume wenye nguvu.

Roma baada ya kuendesha gati kwa madakika kadhaa alikuwa akiingia daraja la kuingia kigamboni , alilipia ushuru na kupita na alikuwa na mpango wa kutafuta Hoteli , Kwa jinsi alivyomuona mrembo huyu , aliona hapaswi kuchukua hoteli ya kawaida , kuna Hoteli aliokuwa akiikumbuka iliokuwa karibu na Nyumba ya Rose ,ndio alipanga kwenda ndani ya hoteli hio.

Dakika chache mbele alikuwa ndani ya Cloud Hotel , ilikuwa ni hoteli nzuri ya kisasa ambayo ilikuwa ikivutia kwa kiasi kikubwa , Roma alibenjua mkebe wa Gari na kutoa hela za Dola alizokuwa amehifadhi na kisha alifungua mlango na wakatoka baada ya kuegesha gari sehemu maalumu.

Roma baada ya kukabidhiwa chumba chao na kuingia ndani alijikuta akipandwa na mzuka hatari , kiasi kwamba huyu mrembo alijikuta akishindwa kujizuia na kucheka

“There’s no need to be in such a rush, right? It’s not like I’m going to run away tonight.”

“Haina haja ya kuwa na haraka sana , sio kama nitakukimbia usiku huu “

“You demoness, isn’t this fire caused by you?”Aliongea Roma huku akimkumbatia kwa nyuma.

Moto ulionekana kuwapanda kweli , ila kwa Roma aligundua ugeni kwa huyu mrembo hakujua kwanini mrembo aneonekana kutokuwawa mzoefu hivi hakuwa mtundu kwenye mapenzi.

Baada ya kuvuana nguo , alimbeba juu juu na kisha akaelekea nae bafuni na umtumbukiza kwenye ‘bath tub’ na Roma akafuatia, na ndani ya madakika walikuwa kwenye kitanda hiki kikubwa cha sita kwa sita

“Wewe ni bikra?”Aliuliza Roma baada ya kuona ugumu.

“Endelea tu usijali sana Mr Roma”Aliongea Mrembo huyu na Roma hakujali , alijiambia si umetaka mwenyewe ngoja ni kuoneshe.

Ilikuwa ni muda wa Asubuhi ,Roma akiwa amelala wakiwa wamekumbatiana na mrembo Amina , Mara mlango wao uligongwa kwa nguvu kiasi cha kumfanya Roma ashituke na kupandwa na hasira na kujiuliza mpuuzi gani huyo anagonga mlango namna hio.

“Wewe Mbakaji Fungua , Utaozea jela nakuambia”Ilisikika sauti ya kibabe nje na kumfanya Roma aone wanaogonga hawana heri , Amina alikuwa ashaamka na yeye na Roma alimgeukia na kumwangalia na Amina akamtingishia Mabega kuashiria haujui kinachoendelea na Roma alijifunga taulo na kuusogelea mlango.

Unajua nini kitarokea

ITAENDELEA.
 
Yaaani ni kama picha ndio kwanza linaanza...daaah niko pale j5 nimekaa seat ya mbele.
 
Yaaani ni kama picha ndio kwanza linaanza...daaah niko pale j5 nimekaa seat ya mbele.
Hadithi nzuri sana ila unavuta sana mkuu.eneo moja linachukua pakubwa sana.kwa mfano leo hujatundea haki kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…