SEHEMU YA 113
Roma ilibidi amtoe Amina kwenye kifua chake kwani aliona mwanadada huyu ni kama anataka kumng`ata sasa lipsi za midomo yake ,Fayezi na mzee Kanani ni kama hawakuwa wakiamini kile ambacho kilikuwa kinatokea , waliona mpaka kufikia hatua hio jambo lishakuwa gumu , Fayezi aliwaangalia wawili hawa na hata ile hali aliokuwa nayo ilimpotea kwenye macho yake .
“Mr Rma nadhani mpaka kufikia hapo , unaonesha haupo tayari kushirikiana na sisi juu ya hili jambo?”Aliuliza Fayez.
“Sio kwamba sitaki kutoa ushirikiano , lakini huwa mara nyingi sina tabia ya kumuangalia mtu machoni na kuongea uongo hususani kwenye swala zito kama hili ,Mtu anahitajika kufahamika katika jamii kwa sifa nzuri lakini wakati huo huo mtu anapaswa kutofautisha kati ya aibu na heshima, Amina ni mwanamke ambaye ametoa usichana wake hivyo hili sio swala la kutaka kuzimwa na pesa na kuchukuliwa kirahisi , wewe ni mwanaume unatakiwa kuelewa kanuni za maisha ndogo ndogo kama hizi”
“Kama ningekuwa simpendi Amina nisingeweka juhudi kuzuia jambo ambalo amefanya na kulisahau hili jambo katika kichwa changu na kutaka kuendelea nae”
“Haha..Unajidanganya Fayezi kwanini unataka kuficha ,Unataka katangazia watu kwamba hili jambo halijatokea wakati kila kitu kimetendeka , ulichofanya wewe ni kumsafisha kwenye macho ya watu wengi, ilihali wewe mwenyewe unakubali kwamba alitenda hili jambo , kama kweli unampenda usingeficha chochote bali ungekubali kama amefanya lakini licha ya kufanya kwake umeamua kumkubali hivyo hivyo kama binadamu asiekamilika, hayo ndio mapenzi ya dhati , ila kwa ulichofanya mimi nakuona kama mwanaume unaempenda Amina kutokana na uzuri wake wa nje tu , lakini sio kila kitu kuhusu yeye”Mrembo Amina alijikuta akiguswa na maneno ya Roma.
“Roma kwa jinsi unavyo ongea unanifanya nikupende Zaidi na tukafanye tena”Aliongea Amina pasipo kumjali baba yake wala Fayezi.
“Tulia mtoto mzuri hatuwezi kufanya muda huu”
“Mr Roma unapaswa kumheshimu Amina kama mchumba wangu , acha kuongea maswala yako ya kipuuzi”
“Wewe Fayezi bwana ni mwanaume wa kushangaza sana , ninachofanya hapa ni kujaribu kukufungua akili , huyu mrembo hakupendi hivyo kubali ukweli na ukaendelee na maisha yako , wanawake wapo wengi ambao watakufaa”
“Nasema hivi mimi labda sio Fayezi , nitahakikisha unashuhudia namuoa Amina, nina nguvu na pesa za kufanya hivyo”Roma alitabasamu.
“Hizo ni pesa zako na hazina maana yoyote kwangu wala kwa huyu mwanamke , na kama zingekuwa na maana kwako na kwake nadhani mpaka sasa tusingekuwa tunazungumza haya , lakini kama bado unataka kumuoa huyu mwanamke siwezi kuingilia , lakini unapaswa kuongea nae kwanza siku akikubali basi sitokuwa na namna ya kuingilia”
“Wewe mjinga,Mbona unaongea kwa kujiamini sana , unafikiri hatuwezi kukufanya chochote?, nakuambia hivi mimi Feisal Kanani ilimradi nina nguvu na pesa nitakufanya kitu ambacho hutokuja kusahau katika maisha yako”Aliongea tajiri Feisal kwa hasira , alishindwa kuvumilia kuangalia mambo yanayotendeka kwenye macho yake.
“Baba huruhusiwi kumfanya chochote Roma”Aliongea Mrembo huyu akimkingia kifua Roma , lakini Roma alijikuta akitabasamu na kumrudisha mrembo Amina nyuma yake na kumsogelea mzee.
“Mzee nikuambie tu , mimi sio tajiri kama nyie wa kuendesha magari na kulindwa na watu wengi lakini pia kuabudiwa kutokana na pesa zenu , mimi ninaweza kua masikini kwenye maisha yangu , lakini siwezi kuruhusu mtu anichokoze , kama kuna jambo unataka kufanya kwangu nakukaribisha, usiongee sana , msemo wangu katika maisha ninao ukubali ni ule unaosema , mwanaume anatambulika kwa juhudi za mikono yake sio kwa maneno yanayotoka kwenye midomo yake”Mzee alijikuta akichemka kwa hasira , hakuwahi kukutana na mtu anaejiamiani kama Roma kwenye maisha yake , alishindwa kufanya chochote na aliona ni kama atapasuka kwa hasira , na alijikuta akishikilia kifua chake.
“Nadhani hunijui vizuri mimi ,, nakuambbia nitakukomesha”
“Mzee nachukia kutishiwa amani sana kwenye maisha yangu ,labda nikuambie tu mwanao nilimbanjua , tena sio kwa goli moja nimepiga goli Zaidi ya tatu na wote tulifurahia tendo na tulitumia Zaidi ya masaa kama nane kumaliza , sasa hebu niambie je unauwezo wa kuchakata kama wangu?,mimi Roma Ramoni siogopi mtu , ukitaka tuliamshe tuliamshe ukinishinda nitakubali nimeshindwa lakini nikikushinda ukubali kushindwa”Mzee alijikuta akipandwa na presha na kuanza kupumua kwa tabu na kidogo tu adondoke ila alidakwa na mabodigadi wake na kumuingiza kwenye gari.
“Mr Roma ninaenda ila nitarudi kivingine”Aliongea Fayezi lakini kabla hajageuka Roma alikuwa ashamfikia na kumkaba shingoni na kufanya mabodigadi wamzingire , Fayezi alianza kutapatapa kwani mikono ilikuwa imemkaba kiasi cha kukosa pumzi , alimpiga piga ngumi Roma , lakini ni kama alikuwa akipiga gogo Roma hakuhisi maumivu yoyote.
Mabodigadi walishindwa kufanya chochote kutokana na namna ambavyo Roma amemshikilia Fayezi , ni kama walikuwa wakimuogopa Roma.
“Amina ukinipa ruhusa nimuue ili asikusumbue tena , nammaliza hapa hapa”
“Hapana Roma naomba usimuue mwachie aende zake”Aliongea Amina kwa woga , kwani aliona Fayezi anakaribia kufa na Roma alitabasamu na kumrushia kwa mabodigadi wake.
“Sipendi kutishiwa kwenye maisha yangu, nilikupa nafasi ya kunifokea unifokee kwa kumchukua mchumba wako lakini hukufanya hivyo ,lakini kunitishia ni jambo lingine kwenye maisha yangu , Na ushukuru Amina kakuokoa la sivyo nisingekuachia uhai wako , hivyo usie ukamsumbua tena maana haumdai chochote, ondoka”Aliongea Roma na Fayezi hakutaka kubakia hapo , aliingia kwenye gari akiwa na hasira na akaondoka.
Roma baada ya kumaliza kuongea hivyo ,alianza kupiga hatua kuondoka , huku akimuacha Amina aliesimama akishindwa kuelewa afanye nini , alijua mpaka hatua hio Roma amemsaidia sana hivyo hakupaswa kumfuata tena , kwani anajua ana mke.
“Kwaheri Roma,Mungu akipenda tutaoana”Aliongea Amina huku akifuta machozi kwenye macho yake na Roma alimwangalia mrembo huyo na kumkonyeza na hakutaka kubaki tena hata sekunde , alitaka awahi kazini.
*****
Jestina alijikuta akiumia sana baada ya kujua kuwa dada yake Blandina yupo hai muda wote huo Zaidi ya miaka ishirini pasipo yeye na familia yake kujua , alijilaumu kwa kutofika ndani ya kituo hiki.
“Kwahioo nia yake ya kufungua kituo hiki , ilikuwa ni kama njia kwa dada na sisi kuungana tena?”
“Naweza kusema hivyo Mrs Azizi, Blandina alikuwa akifanya maombi sana kila siku ili mmoja ya wanafamilia kuja kutembelea hiki kituo , ili apate kuonana na ninyi”Aliongea Mama Issa na kumfanya mwanamke huyu azidi kububujikwa na machozi , aliona ni roho yake ya kibinafsi ambayo ilimfanya asikumbuke kuja kutembelea hiki kituo.
Jestina hakutaka kukaa chini hata kwa dakika moja , aliomba mawasiliano ya Blandina kwa ajili ya kuwasiliana nae na Mama Issa alimpatia bila shida yoyote.
“Hii ndio namba ambayo aliandaa kwa ajili ya nyie kuwasiliana”Aliongea mama Issa na kumkabidhi namba hio.
“Asante sana mama Issa , naomba niondoke sasa , nitakuja tena baada ya kuwasiliana na dada yangu”Aliongea huyu mwanamama huku akifuta machozi na kuweka kikaratasi kile kwenye mkoba wake na kuondoka ndani ya kituo hiki.
Mama issa alijikuta akikaa chini na kuanza kulia kwa kwikwi , haikueleweka ni kwanini mwanamama huyu alikuwa akilia.
Baada ya Jestina kufika nyumbani , haraka haraka aliingia kwenye chumba cha baba yake ,Mzee Atanasi , alikuwa akitaka kumueleza kila kitu alichopata kujua siku hio ya leo.
“Kuna nini Jestina mbona unahema hivyo?”Aliuliza Mzee Atanasi baada ya kukaa kwenye kitanda , kwani alikuwa amelala , na muda huu Tajiri Azizi hakuwepo.
“Baba….hiii..hiiii”Mwanamama huyu alijikuta akianza kulia pasipo kuongea na kumfanya mzee huyu aone kuna jambo ambalo halikuwa sawa , alikuwa akijua Jestina siku hio alimuaga kwenda kutembelea kituo cha Son And Daughter Orphanage, lakini alishangazwa na namna ambavyo amerudi.
“Jestina niambie nini kimetokea , kulia kwako kunaniweka kwenye hali ya Sintofahamu, nishakuambia siku zote unapaswa kuwa imara , kwanini unaruhusu hisia zikutawale”AliongeaMzee huyu kwa kufoka baada ya kuona Jestina Analia tu bila kuongea.
“Babani Blanidna baba…”Aliongea na kuchukua mkoba wake na kutoa barua na kisha kumkabidhi Mzee Atanasi , lakini kwasababu mzee huyu hakuwa akiona vizuri alimwambia Jestina Asome hio barua.
Mpaka Jestina anamaliza kusoma barua hio ni kama mzee huyu hakuwa akiamini kile alichokisikia , ilikuwa ni barua ya kuumiza mno kwa mwanafamilia yoyote ambaye alikuwa akimpenda Blandina.
“Blandina ni mjinga , anakaaje miaka yote hio bila kutuambia yupo hai , anajua ni namna gani nilikuwa nikiumia kwa kifo chake , Mshenzi sana huyu mtoto,sikutegemea kama atafanya ujinga kama huu”Aliongea mzee Atanasi huku hasira zikiwa kwenye macho yake.
“Baba usiwe hivyo , inatupasa kufurahi yupo hai , ni kosa letu pia baba”
“Jestina naomba uniache na sitaki kumsikia, kama kweli Blandina ni mwanangu asingefanya maamuzi ya kipuuzi namna hio , naomba uniache na usije ukalitaja jina lake mbele yangu tena , kama alichagua kukaa miaka ishirini pasipo kutuambia kama yupo hai , aishi hivyo hivyo na sitaki kumuona kwenye familia yangu”Aliongea kwa hasira huyu mzee , alikuwa mzee , lakini alionyesha alichukizwa sana na maamuzi ya Blandina na Jestina aliona amuache baba yake , kwani kwa hasira aliomuona nayo , hakuwahi kuishuhudia kwenye maisha yake yote tokea akiwa mdogo.
Licha ya Jestina kuona baba yake kakasirika , hakutaka kutulia kabisa , alijiambia lazima siku hii ya leo aisikie sauti ya Blandina kwa namna yoyote ile , alijua baba yake anahasira tu za muda mfupi na muda ukipita atatulia… haraka haraka alikimbilia kwenye chumba chake na kutoa simu yake na kuanza kuingiza ile namba aliopewa na kupiga na kisha akaweka sikion, na alishukuru baada ya kusikia namba ile inaita.
*****
Roma saa tano kama na nusu ndio muda ambao alifika kazini , hali ya kampuni ilionekana kuwa tulivu mno, ni hali ya hewa ya ubaridi na marashi ya aina tofauti yaliomfaya bwana huyu kufurahi.
Baada ya kuingia ndani ya idara ya PR aliwakuta wenzake wakiwa bize , Recho alimuona Roma na kumsalimia na hakukua na stori nyingi, alikaa kwenye kiti chake na kuvuta pumzi , licha ya kwamba alionekana kuwa sawa kwa nje , ila alijua Edna saivi atakuwa na hasira nae na hivyo akili yake ilikosa utulivu,Roma hakutaka kufikiria sana , aliamua kutulia kwenye kiti chake na kuegamia , leo hii hakuwa hata na hamu ya kucheza gemu.
Saa kumi kamili alitoka na gari yake na kurudi nyumbani na alipokelewa vizuri na Bi Wema lakini kwa Sophia alimwangalia Roma na kushindwa kumuelewa , kwani tokea jana yake ndio anarudi muda huu , alishangaa ni mwanaume wa aina gani anaweza kutoka na kuiacha nyumba yake na kurudi jioni , lakini hakutaka kujali sana.
Ukweli ni kwamba licha ya taarifa ya Amina kusambaa mtandaoni lakini picha za Roma zilifichwa na pia jina lake halikuandikwa Zaidi ya Amina peke yake alieonekana , hivyo hata Sophia na Bi Wema hawakuwa wakijua kile kinachoendelea , walichokuwa wanajua ni Roma kulala nje ya Nyumbani kwa usiku mzima, na walihisi ni lazima itakuwa alilala kwa mwanamke , lakini kwa Bi Wema hakujali sana , aliona tabia za Roma zilikuwa zikisababishwa na Edna mwenyewe kwa kutomjali mume wake, mwanamama huyu aliamini kama Edna angekuwa anamhudumia Roma kwa kila kitu , basi Roma angetulia nyumbani , hivyo matendo ya Roma hakuyawazia sana.
Edna hakurudi kabisa mpaka inafika saa mbili na alimpigia simu Bi Wema kama atachelewa kurudi , ana kazi ofisini na Bi Wema alishangaa, ila hakutaka kuuliza sana , alimsihi tu asisahau kula.
Roma na yeye baada ya kujua hilo , hakutaka kuliwazia sana , alijua Edna alikuwa na hasira hivyo alikuwa akifanya hivyo kumuepuka , ili wasionane na hakutaka kufanya jambo lolote kwa muda huo , aliona ataharibu Zaidi , alichoamini tu ni kwamba Edna atakuwa salama kwani wanajeshi wake wanampa ulinzi.
SEHEMU YA 114
BOLIVIA 1990.
Katika jambo ambalo Carlos , alikuwa amekosea ni kumuacha Ryani kumtoka kwenye macho yake, alijitukana kwa makossa aliokuwa amefanya kwani Ryani alionyesha kumzidi akili.
Misheni ya Carlos kuingia ndani ya Kambi hii ambayo ilikuwa ikiendesha project ya Pro Human ilifanikiwa kwa asilimia mia moja , na bwana huyu kutokana na utaalamu wake uliotukuka katika maswala ya kijasusi , aliweza kujipenyeza na kukubalika kama moja ya walinzi ndani ya hii kambi na alimfanya Mellisa Luiz Meneja wa hio ‘project’ kumuamini na haikuwa kumuamini tu , lakini pia alimfanya akawa mpenzi wake na hapa ndipo kosa la Melisa alilokuwa amefanya kwani Carlos alitumia udhaifu wa Mellisa wa mapenzi yake kwake na kumpa cheo kikubwa cha ulinzi ndani ya kambi hii na kufanya misheni yake kukamilika kwa asilimia mia moja.
Baada ya siku kadhaa za Carlos kutoa maendeleo ya misheni yake kwa Director Powel kwa njia ya siri , aliweza kupewa maagizo mengine ya kuhakikisha anatega mabomu ndani ya hio kambi ndani ya siku moja.
“Kazi yako ni kutega mabomu ambayo yataweza kuilipua hio kambi yote pasipo kuacha aina yoyote ya ushahidi Carlos , kuhusu namna ya kupata mabomu hayo , itakuwa juu yako , tumia utaalamu wako kutengeneza mabomu hayo , una siku nne tu , siku inayofuatia mtapokea ugeni ndani ya kambi yenu na hio ndio itakuwa siku ya kukamilisha misheni”
“Ugeni gani Director??”
“Atakuja Ryani akiwa na sura ya mjukuu wa Profesa Banosi , afahamikae kwa jina la Coheni , hakikisha unafanya nae ‘Eye Contact’ na atakupa maelekezo namna ya kukamilisha misheni na baada ya hapo utajua nini unapaswa kufanya”Aliongea Director na kisha akakata simu., na hio ilikuwa ni siku nne kabla ya Cohen na Mr Anderson kufika ndani ya kambi ya Pro Human kwa kutumia usafiri wa Chopa.
“Mellisa There is Problem , which need your attention?”Aliongea Carlos alieshikilia bunduki lake huku akiangaliana na Cohen.
“What ,Which Problem??”Aliuliza Merlisa huku akitangulia mbele na muda ule ule Cohen alimpa ishara Carlos ya vidole vinne akimaanisha kwamba anazo dakika nne za kukamilisha misheni, na Mr Anderson hakuelewa kilichokuwa kikiendelea kwani macho yake yote yalikuwa kwa vichanga ambavyo vilikuwa vikionekana kwenye Skrini.
Muda ambao Merlisa alikuwa akiingia kwenye chumba kilichokuwa ni cha kuongezea Camera ,Cohen alimsogelea Mr Anderson na kumpiga kitaalamu kwenye shingo yake na akamuweka chini akiwa hajitambui
“Upande wa Chumba cha kuongozea Kamera baada ya Merlisa kuingia ndani ya hiki chumba , alijikuta akipigwa na mshangao , kwani vijana wote walikuwa wamelala chini wakiwa hawajitambui huku kamera za Ulinzi kupitia Skirni za hapo ndani zikionesha maeneo yote ya nje na ndani ya eneo hili.
“Upo chini ya ulinzi Merlisa”Aliongea Carlos kwa sauti nzito ambayo Merlisa hakuwa amewahi kumsikia nayo Carlos na ni kama hakuwa akiamini kwani alijikuta akigeuka.
“Carlos..!!!”Aliongea kwa mshangao Merlisa huku akionesha hali ya wasiwasi katika macho yake.
“Usishangae Merlisa , mimi ni Carlos ndio Ajenti kutoka CIA na nipo kwenye misheni ya kuharibu kila mnachotengeneza hapa ndani”Aliongea Carlos kwa lugha ya kingereza na kumfanya mwanamama huyu kutoa machozi , alikuwa ametokea kumpenda sana Carlos kwa muda mfupi,lakini sasa baada ya kujua mwanaume aliekuwa mbele yake , alimhadaa na hakuwa akimpenda kama alivyokuwa anamwambia ila yupo kwenye misheni aliumia.
Carlos hakutaka kuongea sana na Merlisa , alimpa Amri ya kusogelea tarakishi moja iliopo hapo ndani ili kuingia kwenye mfumo wa ulinzi wa kambi hio , ili afungue mlango wa chumba ambacho vitoto vichanga vilikuwa vimehifadhiwa , na hii ilikuwa ni kumruhusu Ryani akamchukue mtoto na kutoka ndani ya hio kambi.
Merlisa hakutaka kuleta shida kabisa , aliona nia ya Carlos kumdhuru na ndio maana alitii.
“Carlos hatutakiwi kufanya hivi ni hatari mno kama watoto wale wakitoka uraiani , pasipo hatua za kiusalama juu yao kuchukuliwa “
“Shut the F*ck up Merlisa , Do as I say , Open the Door”Aliongea Carlos kwa hasira na Merlisa alianza kutetemeka , alikuwa akiogopa kufa na ndio maana alianza kucharanga batani za tarakishi na ndani ya dakika kadhaa tu , ilitokea Ramani ya eneo lote la kambi na kumfanya Carlos atabasamu.
“Make it Hury Merlisa this is no Joke”Aliongea Carlos
“Hapana CIA hawajui hatari iliopo kama vile vichanga vitatoka uraiani , lazima nitafute namna”Aliwaza Merlisa na hakutaka kuleta ubishi , alifungua mlango.
Ryani aliekuwa kwenye sura ya Coheni baada ya kuona mlango umefunguka haraka haraka alitembea kwenye yale makabati ya vichanga vilivyokuwa vikirusha rusha miguu kwa nguvu mno ambayo sio ya kawaida kwa mtoto mchanga, Alihesabu vitoto vyote kumi na mbili na baada ya kifikia kwenye sanduku lililokuwa na jina la ‘The First Goddess’Alitabasamu na kilichomshangaza Ryani ni kwamba kati ya vichanga vyote kumi na mbili , mtoto wake pekee ndie embaye hakuwa akirusha miguu.
“Carlos huwezi toka hai ndani ya hii kambi unajidanganya tu , ulinzi ni mkali sana”Aliongea Merlisa
“Thanks for your Concern Merlisa , but we are not Done yet”
“Unataka nini tena Carlos?”
“Nataka u’activate All the Bomb’s, kwenye hii kambi”Aliongea Carlos na kumfanya Merlisa atoe macho.
Ukweli ni kwamba Carlos baada ya Director kumpa maelekezo ya kutengeneza mabomu , alimuelewa kwani aligundua kuwa Director Powel alikuwa akiongea kwa Code.
Katika akili ya kawaida , kwa Projekti kubwa kama hii Carlos aliaminni lazima kuna tahadhari ambazo zimechukuliwa pale mpango utakapo feli , aliamini lazima kutakuwa na mabomu ambayo yametegwa ndani ya hii kambi kama tahadhari ya kiusalama , ili kama wanachokitengeneza kikiwazidi nguvu , wanachokifanya ni kulipua tu kambi, hilo alielewa sana Mtaalamu Carlos na hivyo ndivyo pia alivyowezakufungua kodi ya Director powel , ya kutengeneza mabomu’, kwa mtu wa kawaida asingeelewa , ila kwakua Carlos alikuwa na mafunzo ya juu ya kijasusi , basi aliweza kumuelewa Powel.
Merlisa mpango wake ulikuwa ni kulipua mabomu yaliokuwa yapo kwenye hio kambi lakini kitendo cha kupewa amri na Carlos kufungua hayo mabomu basi hakuona shida kabisa kufanya hivyo m alichokifanya ni kucharanga batani za tarakishi na ndani ya dakika chache tu Ramani ya mabomu yote mazito yalionekana.
“Do you really want to Activate The Bomb’s? ,If you hit ‘Enter ‘The Bomb`s will go off in 60 second”Ulikuwa ujumbe uliosomeka kwenye Skrini ya tarakishi hii na Merlisa alimwangalia Carlos.
“Merlisa nakupenda sana na neno lolote la kimapenzi nililokuambia ni la dhati kabisa , lakini mimi ni Ajenti siruhusiwi kupenda , kabla hujabonyeza hiko kitufe nataka kukupa sekunde therathini za kujiokoa kabla ya mabomu hayo hayajalipuka”Aliongea Carlos na kumfanya Merlisa ashindwe kujua ni nini anamaanisha.
“Nitatoka na kufunga ule mlango wa kutokea baada ya kubonyeza hiko kitufe nitaufunga kwa nje , kwa uzoefu wangu kufungua kile kitasa bila ufunguo itakuchukua sekunde therathini pekee na mpaka hapo utakuwa na sekunde nyingine therathini za kutoka kwenye hii kambi kabla ya mlipuko”Aliongea Carlos na kisha alisogea kinyume nyume mpaka kwenye mlango huku siraha yake akimuelekezea Merlisa na ile anafika kwenye mlango alimuamrisha Merlisa kubonyeza ‘Enter’ huku Carlos akiangalia Skrini za ukutani maana na zenyewe zilikuwa zimekunganishwa na Tarakishi ambayo alikuwa akitumia Merlisa, na Merilisa alifumba macho kwa sekunde kama mtu ambaye alikuwa akisali na kisha akabonyeza kitufe cha ‘Enter; na palepale Carlos alitoka na kufunga mlango na kukimbia.
Carlos alifanikiwa kutoka kabla ya mlipuko lakini kwa kuchelewa na hii ni kutokana na kwamba mlango ambao alitakiwa kutumia kutokea , ambao ulikuwa ndio njia ya Rahisi kutoka kabisa ya uzio, mlango huo ulikuwa umefungwa kwa nje na alijua huenda atakuwa ni Ryani , kwani muda mchache uliopita alimpa ishara ya kutumia njia ya Mashariki ya kambi hii.
Misheni ya Carlos ikawa imefeli , kwani licha ya bwana huyu kutumia chopa kumtafuta Ryan , lakini hakumuona kabisa na Ryani alimzidi ujanja Carlos.
Hio ilikuwa nni miaka ya tisini wakati tukio hili likitokea huko nchni Bolivia kwenye msitu wa Amazoni , Ryani na mke wake Epholia walitokomea kusiko julikana na mtoto ambaye alikuwa akitengenezwa kuwa ‘Pro Human aliepewa jina na Project hio kama ‘The First Goddess’ Yaani Mungu wa kike.
Je huyu mtoto yuko wapi na ukumbuke Merlisa alisema ni hatari kwa huyu mtoto kuingia kwenye jamii ya Binadamu wa kawaida.
ITAENDELEA
SEHEMU YA 115
KENYA –NAIROBI.
Mke wa Raisi Kamau Kamau , aliekuwa akifahamika kwa jina la Maina alikuwa ameketi eneo la sebuleni akiangalia Runinga ndani ya ikulu , licha ya mwanamama huyu kuangalia kile kilichokuwa kikioneshwa na chaneli maarufu kutoka Marekani , lakini alionyesha kukosa umakini kabisa, baada ya kuona haelewi alizima runinga ile na kunyanyuka na kulisogelea Friji lililokuwa hapo sebuleni na kutoa chupa ya Wine na akaifungua na kuijaza kwenye glass na kisha alitembea kuelekea upande wa kushoto akiwa maeshikilia Wine yake mkononi,wakati huu alikuwa na sura yake bandia iliokuwa ikifahamika kwa wananchi wengi wa Taifa la Kenya.
Na wakati huu ilikuwa ni saa tisa hivi za jioni , baada ya mwanamama huyu kuingia kwenye hiki chumba , alichukua simu yake kubwa ya I phone na aliona ujumbe uliokuwa ukitoka kwa Mkuu wakituo cha kulelea Yatima cha Tanzania.
“Nimefanikiwa kukabidhi”Ilikuwa ni meseji ilioandikwa kwa namna hio na mwanamama huyu alijikuta akifumba macho na kuangalia juu kwasekunde kama sitini hivi na ile anashusha uso wake chini , macho yake yalijawa na machozi baada ya kuyafumbua.
“Kamau Utanisamehe sana ,Huu ndio wakati wa mimi kutoka kwenye hiki kifungo”Aliongea mwanamama huyu na kisha akasogelea kabati lililokuwa ndani ya hiki chumba kikubwa kama cha mfalme na kufungua mlango wa kushoto , sehemu ambayo ilionekana kuhifadhia baadhi ya vitu vyake muhimu kama vile vibanio vya nywele na mikufu ya thamani , alitoa mkufu mmoja wenye kidanui chenye herufi ya nembo D na kisha akaishika mkononi na kisha alisogelea mkoba mweusi alioutundika kwenye kabati na kisha akaufungua na kutoa simu ndogo ana ya Nokia tochi na kurudi kitandani.
Maina baada ya kufika kitandani alifungua kile kidani kwa kukibanjua katikati na ikadondoka laini chini kwenye sakafu na mwanamama huyu aliinama na kuiokota na kisha akafungua ile simu ndogo na kuingiza ile laini na kuwasha ile simu.
Baada ya Maina kumaliza kuwasha tu ,simu ile ilianza kuita hapo hapo na mwanamama huyu aliangalia simu iliokuwa ikiita bila kupokea , alikuwa ni kama mtu ambaye alikuwa akijishauri kupokea ama asipokee , kwani hakuonekana kuwa na uhakika kwenye macho yake.
“Blandina umejiandaa kwa Zaidi ya miaka ishirini kwa ajili yah ii siku , hupaswi kuogopa , pokea simu”Ilikuwa ni suati ambayo ilikuwa ikimshawishi kwenye kichwa chake , ambayo ilionekana kuwa na nguvu sana kuliko ile ambayo ilikuwa ikimkataza, simu ilikatika, lakini baada ya dakika moja ilianza kuita tena na mwanamama huyu alivuta pumzi na kuweka sikioni.
“Hello!!”Ilikuwa ni sauti ambayo mwanamama huyu alikuwa akiijua sana , licha ya kwamba ilikuwa miaka mingi sana bila ya kusikia hio sauti , lakini hakuwahi kabisa kuisahau Zaidi ya kuimisi tu , mwanamama huyu alijikuta akishindwa hata kuongea neno.
“Blandina najua unanisikia ni mimi mdogo wako Jestina”Ilikuwa ni sauti upande wa pili , iliosikika na kumfanya mwanamama huyu kuanza kutoa machozi mfululizo yaliokuwa yakitambaa mpaka kufikia kwenye shingo yake.
“Jestina najua ni wewe , mimi ni Blandina dada yako , sipo sehemu nzuri ya kuongea , Alhamisi ya wiki hii naomba tuonane ndani ya kituo cha Son and Daughter orphanage Bagamoyo , muda ni saa nne kamili za asubuhi”
Aliongea Maina kwa kujikaza na kisha akakata ile simu na kuizima kabisa na akaifungua na kutoa ile laini na kusogelea mlango wa chooni na akaitupa ile laini na akarudi na kiuchukua kile kidani na akakifunga kama mwanzo na kisha akarudi na kukihifadhi kwenye kabati.
Upande wa ofisini ndani ya ikulu hii ya wananchi wa Kenya , Mheshimiwa Raisi Kamau Kamau , alikuwa akiendelea na majukumu yake kama kawaida akiwa na umakini mkubwa , bwana huyu alionesha kuna nyaraka muhimu ambazo alikuwa akizisoma na kuzisaini mpaka pale mlango wake ulipofunguliwa na katibu muhtasi wake.
“Mheshimiwa Mr Deo anataka kuonana na wewe”Aliongea mwanadada moja mrefu ambaye alikuwa ni katibu muhtasi,
“Laila unaweza kumruhusu haina shida”Aliongea Kamau kwa lugha ya Kingereza na Laila aliitikia kwa kichwa na kisha akatoka ,na ndani ya dakika chache tu , aliingia bwana mmmoja hivi alievalia mavazi ya suti , mrefu mweusi alienyoa kipara, alikuwa ni kijana wa miaka kama Therathini hivi.
“Nipe ripoti Deo”
“Mheshimiwa kuna meseji kutoka Tanzania imeingia katika mfumo wetu”Aliongea Deo na Mheshimiwa alimpa ishara Deo amsogeleee kwenye meza yake na Deo alimpa mzee huyu kishikwambi alichokuwa ameshikilia mkononi mheshimiwa.
“Nimefanikiwa kukabidhi”Ulikuwa ndio ujumbe uliosomeka kwenye kishkwambi , uliokuwa ukitoka kwa Mkuu wa kituo cha kulelea Yatima cha Son and Orphanage kwenda kwa Maina.
“Unaonaje?”Aliuliza Mheshimiwa.
“Unaonekana ujumbe ambao una Zaidi ya maana”
“Hata mimi naona hivyo Deo , lakini ni jambo ambalo nitalithibitisha mimi mwenyewe”Aliongea Mheshimiwa na Deo aliitikia na kisha akatoka.
“Lazima kuna jambo mke wangu anapanga kulifanya , ila nitajua,Maina huwezi kunizidi akili, mimi ndio Kamau utaishi na mimi mpaka siku mmoja wtu atakapotangulia mbele za haki”Aliwaza Mheshimiwa Kamau Kamau na kisha akarudisha macho yake kwenye karatasi zilizokuwa kwenye meza yake na kuendelea na kazi yake aliokuwa akiendelea kufanya.
“Mume wangu Alhamisi nitaelekea Tanzania”Aliongea Maina usiku baada ya kufanya tendo la ndoa na sasa walikuwa wamepumzika huku Maina akichezea chezea kifua cha Kamau.lakini kwa upande wa Kamau hapo hapo ujumbe wa meseji uliibuka kwenye kichwa chake na kengele ya hatari iligonga.
“Kuna nini mke wangu?”
“Nahitaji kuonana na watoto wa kile kituo, ni muda sasa sijafika hata kutembelea mume wangu”Aliongea Maina na kumfanya Kamau afikirie kidogo , ukweli hakuwa na tabia ya kumzuia mke wake likija swala la kutembelea watoto, kwani tokea Blandina aanze kujificha kwa sura Bandia Furaha kubwa ya blandina ni kuona watoto na ndio maana Mheshimiwa alijitahidi sana kumsapoti maina katika jitihada zake za kufungua vituo vya kulelea watoto yatima, aliona ni jambo pekee ambalo anaweza kumfanyia mke wake kama moja ya malipo kwa namna ambavyo amevumilia miaka na miaka kuishi na sura bandia mbele za watu.
“Sawa mke wangu,sina haja ya kukuzuia , ila ujue tu nakupenda sana”Aliongea Kamau na kumfanya Maina apatwe na wasiwasi kidogo , lakini aliishia kutabasamu na kujikunja kama mtoto kwenye mwili wa mume wake.
*****
Zilipita siku mbili yaani Jumatatu , jumanne na sasa ilikuwa ni jumatano kwa Roma, bwana huyu tokea tukio la kulala na Amina lipite mke wake alikuwa amezidisha kumchunia kwa asilimia mia moja , Edna hakutaka kabisa kuongea na mume wake , kwanza Edna hakuwa akirudi nyumbani muda ambao ulikuwa umezoeleka kwake kurudi na siku nyingine alikuwa akilala kabisa kazini jambo ambalo liliwashangaza sana Bi Wema na Sophia kwa mabadililo ya Edna.
Roma licha ya kujua mke wake alikuwa hataki kabisa hata kuongea na yeye na alikuwa akimkwepa makusudi , hakutaka kulazimisha , aliendelea na mishe zake kama kawaida.
Saa moja kamili za jioni Roma alikuwa Pongoni Beach akiwa na Yezi, Roma alikuwa akimenya viazi na Yezi alikuwa akikaanga na kupakua na kuweka kwenye kabati la kuhifadhia.
Yezi alikuwa akimwangalia Roma kwa namna ambavyo yupo siriasi na kujikuta moyo wake ukiwa wa moto, hakuelewa ni kipi alichojisikia moyoni mwake , lakini alikuwa akijisikia vizuri kuwa na mtu ambaye alikuwa akimsaidia na kumjali.
“Anko Aunt Edna anaendeleaje?”Aliuliza Yezi baada ya kumaliza kazi yake na kukalia kindoo karibu na Roma.
“Kaninunia, siku ya tatu leo haniongeleshi”Aliongea Roma akiwa kawaida na Yezi alishangaa kidogo.
“Yaani Anko unapata mke mzuri kama Aunt Edna halafu unamuuzi mpaka anakununia”Roma alijikuta akitoa tabasamu la uchungu , nikweli kabisa kwa jinsi Edna alivyokuwa mrembo mtu yoyote lazima angesema kama Yezi,ila kulikuwa na mambo ambayo watu hawakuwa wakijua
“Ni mambo ya mahusiano , kununiana kupo tu “Aliongea Roma akipotezea mada , ukweli aliamini Edna hasira zake zitaisha zenyewe tu na watarudi kuwa kama kawaida , licha ya kwamba Roma hakuwa akitegemea kitu kikubwa kutoka kwa Edna lakini namna mke wake alivyokuwa akimueuika , alikuwa akijisikia vibaya.
“Yezi nadhani unakumbuka kuwa kesho tunaenda Kiwangwa kumuona Mama yako?”Aliongea Roma.
“Ndio anko Roma nina shauku kweli ya kumuona Mama Issa”
“Kama unashauku kwanini hukurudi muda wote unamtesa mama wa watu?”
“Nilikosa ujasiri”Aliongea Yezi na Roma akatabasamu , alimuelewa Yezi anachomaanisha hivyo hakutaka kuongea Zaidi.
Roma alimsaidia Yezi mpaka muda wa kuondoka na kumsindikiza mpaka sehemu ambayo Yezi amepanga na kisha akarudi nyumbani kwa ajili ya kulala, ilikuwa ni saa nne kama na nusu wakati akiingia nyumbani na gari ya Edna haikuwepo na alijua tu huyo mwanamke atakuwa yupo bado kazini , lakini wakati anaanza kupiga hatua kuelekea ndani geti lilifunguliwa na gari ya Edna ilionekana kuingia na Roma baada yakuiona gari ya mke wake inaingia , alisimama , alitamani kuongea nae hata kidogo kabla ya kwenda kulala.
Edna alishuka kwenye gari , akiwa na mkoba wake , mrembo huyu alionyesha hali ya kuchoka mno, kiasi kwamba Roma alimuonea huruma na kujiona mwenye hatia , hakujua kilichokuwa kikiendelea kwenye akili ya Edna.
Edna alimpita Roma baada ya kumtingishia kichwa kama salamu, lakini Roma palepale alimsogelea Edna na kisha akamkumbatia kwa nyuma.
“Roma naomba uniachie , usivuke mpaka”Ilikuwa ni sauti ya kibabe ya Edna , lakini Roma hakujali , alimshika Shingo Edna na palepale Edna alilegea kwenye mikono ya Roma , alionekana tayari ashalala na haikueleweka Roma kamfanyia nini.
Roma alimbeba na kumuingiza ndani , na sebuleni walikuwepo Bi Wema na Sophia wlaiokuwa wakiangalia tamthilia ya kifilipino , na walionekana walikuwa wamenogewa sana , kwani walishindwa hata kujua Roma alipita hapo sebuleni.
Roma aliingia kwenye chumba hiki cha mke wake na kumpeleka Edna mpaka kitandani na kumlaza vizuri , alimtoa kijikoti cha suti alichovaa Edna na kumbakiza na blazia.
Roma baada ya kumaliza alimshika Edna kwenye uso wake kwa kumuwekea kiganja na akafumba macho kwa takribani dakika kumi na kisha akatoa kile kigana na kumfunika na shuka vizuri .
“Endless resorve restoration Energy ,utaamka kesho saa saba mchana , mpaka hapo utakuwa umepumzika vya kutosha na unaweza kuendelea kuninunia mke wangu , ila sitaki kukuona ukichoka namna hii”Aliongea Roma akimwangalia namna Edna alivyokuwa usingizini na kujikuta akivutiwa Zaidi na namna mke wake alivyolala.
Roma kuna jambo wakati alipoingia hakulioana na sasa alikuwa ameliona na kumfanya Acheke , jambo lenyewe ni kwamba Mdoli aliomzawadia Edna ulikuwa umening`inizwa ukiwa umefungwa Kamba shingoni kwenye uzio wa balconi kwa nje, yaani ilikuwa ni kama Edna alikuwa akiuonyonga huo Mdoli.
“Hahaha..”Roma alijikuta kicheka kwa namna ambavyo mdoli huo umenyongwa, hakutaka kuutoa , alichofanya ni kuangalia kwa dakika kadhaa na kisha akamgeukia Edna na kutabasamu na kisha akatoka na kwenda kwenye chumba chake.
“Kesho ni Alhamisi nikiamka nimpeleke Yezi Kiwangwa”Aliongea Rma baada ya kuoga na kujilaza kitandani.
ITAENDELEA KESHO.