Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SEHEMU YA 94.
Roma ndio aliekuwa dereva usiku huu huku mke wake Edna aliekuwa amependeza akiwa amekaa pembeni ,Edna akiwa amevalia gauni la rangi nyeupe lenye maua kama michirizi huku kiunoni akafunga na mkanda wa rangi nyekundu, alikuwa amependeza , Roma nae mavazi yake yalikuwa ni suti kama kawaida na shati rangi ya bluu bila tai.
Roma aliendesha kwa maelekezo ya Edna mpaka wakaja kusimama kwenye jumba moja la Kifahari kubwa tu , na kwa kuangalia tu ndani ya eneo hili la Masaki huenda hilo jumba ndio ambalo ni kubwa sana kuliko nyumba zote ambazo wanaishi matajiri ndani ya huu mtaa.
Wakati Roma anasubiria geti la jumba hili kufunguliwa baada ya kupiga honi , nyuma yake aliona gari nyingine ya kifahari na ilionekana na yenyewe ilikuwa ikitaka kuingia ndani ya jumba hili , ilikuwa ni gari aina ya Porsche.
Geti lilifunguliwa taratibu na Roma aliingiza gari ndani ya jumba hili ambalo lilimshangaza sana Roma kwa madhanri ya hapo ndani , alipaki gari baada ya kuonyeshwa sehemu na mfanyakazi ambaye alionekana kama mlinzi na akaegesha gari yake , sehemu hii ilikuwa na magari mengi ambayo yapo ndani ya hili eneo , na jambo hili kwa harakaharaka lilimfanya Roma kugundua leo ndani ya hili jumba huenda kuna sherehe inayoendelea na sio kama alivyosema Edna kama anakuja tu kuonana na familia yenye nguvu ndani ya Tanzania.
Baada ya kugesha alishuka na kumfungulia Edna mlango na wakati huo huo ile gari iliokuwa nyuma yake pia ilikuwa eneo hilo la Maegesho na ile Roma na Edna wanapiga hatua kama mbili ,Dereva aliekuwa akiendesha gari hio alitoka na Wote Roma na Edna walimtambua , alikuwa ni Nadia Alfonso.
“Nadia alilazimisha tabasamu baada ya kuwaona Edna na Roma ambao kwa jinsi walivyokuwa wakionekana walidhihirisha uhusiano wao , yaani mume na mke.
“Mmependezana Edna”Aliongea Nadia baada ya kuwasogela na Edna alitabasamu na kumangalia Roma.
“Asante Nadia na wewe umependeza”Aliongea Edna huku Roma akimwangalia Nadia bila ya kuongea na Nadia alimwangalia Roma usoni ni kama alikuwa akisubiria Roma amsifie ila Roma hakufanya hivyo , alionekena akikumbuka baadhi ya mambo.
“Mr Roma hatujaonana tokea urudi Japani Hongera kwa kukamilisha jambo kubwa kwa kampuni”
“Asante sana Nadia , yote nimefanya tu kwa ajili ya mke wangu kipenzi”aliongea Roma huku akitabasamu na kumkonyeza Edna alietabasamu , ila kwa Nadia hakuonesha kufurahi kwa namna Roma anavyomwangalia Edna Zaidi ya kuweka abasamu bandia usoni.
Waliongozwa na mfanyakazi wa kike na kuzunguka upande wa pili wa jumba hili , hawakuingia ndani kama Roma alivyotegemea , Roma aliendelea kuangalia mandhari yakuvutia ya jumba hili.
“Nadia ,Edna karibuni”Aliongea mwanamama mmoja hivi maji ya kunde mtu mzima , makadirio ya miaka kama Arobaini na tano hivi , mwanamama huyu baada ya kuwasogelea macho yote yalikuwa kwa Roma , alimwangalia Roma kama vile alikuwa akimfananisha nah aa Roma alitambua hilo.
“Asante Mrs Mohamed”Alijibu Nadia na wakapeana mikono , alikuwa ni mwanamama ambaye alionekana mkarimu kwa jinsi alivyokuwa ameweka tabasamu usoni mwake.
“Mrs Mohamed huyu ni ndio mume wangu , anafahamika kwa jina la Roma Ramonni ,Roma huyu ni Mke wa Mohamedi tulikutana nae kwenye kusanyiko”Aliongea Edna akimtambulisha Roma.
“Unamaaisha huyu ndio mke wa yule tajiri Azizi?”
“Ndio Mr Roma naitwa Mama Nusra ,hongera kwa kupata mke mzuri kama Edna , Edna hongera nimefurahi kukutana na Mr Roma, Azizi alikuwa akiniambia kuhusu mumeo na nilitamani sana kumuona”Aliongea Mama huyu kwa furaha na kumfanya Nadia aliekuwa pembeni kuchukizwa na sifa za Mama Nusra.
“Nafurahi pia kukufahamu mama Nusra unaonekana kuwa mkarimu kweli na sikudhania Azizi atakuwa na mke kama wewe”Aliongea na kumfanya mwanamama huyu amwangalie usonni na kutabasamu.
“Ulidhania atakuwa na mke wa aina gani?”.
“Hehe..kwa anavyonekana ana hela ila Swaga hana hata mimi nimemzidi, kwanza anacheka kichafu na nilijua hatokuwa na mwanamke mrembo kama wewe ,Eti Mama Nusra umempendea nini yule mzee au ni kwasababu anapesa,”
Aliongea Roma na kumfanya Edna amfinye, maana aliona Roma anaanza kuongea ujinga lakini kwa Mama Nusra alijikuta akicheka , alionekana kujisikia vizuri sana kusifiwa kwa aina ya tofauti na Roma
Basi Edna na Roma waliongozwa mpaka upande wa Swimming Pooll , sehemu ambayo ilikuwa imepambwa , kulionekana kulikuwa na sherehe iliokuwa ikiendelea hapa ndani , kwani pia kulikuwepo na wageni japo hawakua wengi sana.
“Mr Roma.. hahahaha..tunaonana tena”Aliongea Tajiri Mohamedi , alionekana kufurahi sana kama kawaida yake na cheko lake.
“Sema Mzee unajua kucheka kichafu ,Mkeo anaweza kuingia kwenye kumi bora ya wanawake wenye huruma ndani ya Tanzania .. Anyway mimi na mke wangu tunafurahi kukutana kwa mara nyingine”Aliongea Roma na Tajiri huyu alichukulia maneno ya Roma kama sifa na alicheka tena.
“Edna kwa jinsi ulivyomzuri nilikuwa nikitegemea ,utatafuta mwanaume matawi ya juu , sikudhania utakuja kuangukia kwa mwanaume mbeba mizigo,Asie na pesa”Aliongea Tajiri Azizi na Roma alitabasamu aliona huyu mzee anamlipizia.
Wakati wakiwa wanaongea na Tajiri Azizi mara kuna mwanamke mremfu mrembo mno, mtu mzima aliwasogelea, Roma na uwezo wake wa kujua watu alijua kabisa mwanamke huyu hakuwa mtanzania.Edna alionesha kutomfahamu huyu mwanamke.
“Edna kutana na ‘First Lady’ kutoka Rwanda , Mke wa mheshimiwa Jeremy”aliongea Azizi na mwanamama huyu akaachia tabasamu na kumwangalia Edna huku akimpa mkono wa salamu.
“Nafurahi kukufahamu hakika ni kama watu wanavyokusigia , umrembo sana”Aliongea mwanamama huyu kwa kingereza na Edna alitabasamu.
“Nimefurahi pia kukutana na First lady kutoka Rwanda”Aliuongea Edna huku akiwa ametabasamu ,ila kwa Roma kuna kitu alikuwa akikiangalia kwenye uso wa huyu mwanamke , kitu ambacho mtu ambaye ni wa kawaida hawezi kukigundua , Roma aligundua huyu mwanamke anaefahamika kwa jina la ‘First lady’ hakuwa na tabasamu la dhati ni kama alikuwa akifosi na haikueleweka ni kwa namna gani aligundua.
Roma aligundua sherehe hii ilikuwa ni ya kumpongeza mtoto wa kiume wa tajiri Azizi aliekuwa amemaliza masomo yake ya ngazi ya Uzamili kutoka chuo cha Cambridge maana kulikuwa na maandishi juu ya jukwaa yalionakshiwa kwa maneno ya pongezi.
Baada ya kusalimiana na baadhi ya watu ambao wamealikwa hapa ndani , walionyeshwa meza yao ya kuketi huku wakiletewa vinywaji.
Meza aliokuwa amekaa Roma ilikuwa na jumla ya watu watatu , yaani yeye na Edna pamoja na Nadia, Edna na Nadia walionekana kuongea huku Roma akikagua mandhari ya hili eneo ni kama alikuwa akichunguza kila mtu aliekuwepo na ambaye alikuwa akiingia hapa ndani.
“Edna habari za siku”Ilikuw ani sauti iliowafanya Edna na Nadia waliokuwa wakiongea wainue macho yao na kumwangalia ni nani aliekuwa akiwasalimia na hata kwa Roma pia aligeuza shingo yake na kuangalia upande wa mtu aliesalimia.
“Denisi..!! ,Ni nzuri habari”Aliongea Edna , alikuwa ni Denisi mtoto wa raisi Senga, hata Roma alimkumbuka huyu bwana na tena alikumbuka kipindi wanaenda ikulu na Edna kuna jambo aliweza kuligundua kwenye uso wa Denisi.
“Salama kabisa , Umezidi kuwa mrembo Edna”Aliongea Denisi na leo hii alionekana kuchangamka kuliko ilivyokuwa kipindi c ha nyuma wakati Edna na Roma wapo ikulu.
Nadia alikuwa akimwangalia Denisi na Edna ni kama kuna jambo alikuwa akitafuta baina ya wawili hao , aliona wawili hawa walionekana kufahamiana kwa muda mrefu kidogo japo hakujua ni kivipi , hata kwa Roma alijua mke wake anaonekana kufahamiana na Denisi kwa muda mrefu.
Denisi p alionekana kufanya makusudi yaani licha ya kwamba Roma alikuwepo hapo kwenye Meza ila hakumsalimia na Roma hakujali ila alikerwa na namna ambavyo Denisi alikuwa akimwangalia Edna na pia namna ambavyo amemsifia ,Denisi alimwangalia Edna kwa macho ya kumtamani kabisa , licha ya kwamba wawili hawa wanaonekana kupishana umri kwani Denisi bado alikuwa mdogo kwa Edna.
Wakati Roma akiangalia namna ambayo Denisi akiongea na Edna mara alijikuta akizibwa uso na mikono laini na harakaharaka aligundua aliemziba ni mwanamke , ila alishindwa kung`amua mwanamke huyo ni nani.
“Ukinifahamu nakuachia”Ilimnong`oneza sauti masikioni na Roma alijikuta akikumbuka sauti hio lakini alishindwa kujua ni wapi aliisikia.
“Kwahio nisipokukumbuika utaendelea kuniziba hivihivi mpaka sherehe iishe”Aliongea Roma na aliemziba macho alimwachia na Roma hapo ndipo alipogeuka na kumuona msichana mrembo mwenye haiba ya utoto aliekuwa amemziba macho yake , alikuwa ni Donyi.
“Mungu wako hajajibu maombi yako tumekutana tena”Aliongea Donyi huku akivuta kiti na kuketi , alikuwa amependeza mno usiku huu.
Edna aliekuwa akiongea na Denisi alishuhudia tukio lote ,Roma kuzibwa macho na mwanamke mrembo ambaye alikuwa akimkumbuka vyema kwa kitendo cha kumkubatia Roma wakati wakiwa ndani ya jengo la My World Fashion Mall.
“Donyi Donyi unafanya nini hapa?”Aliuliza Roma.
“Na wewe unafanya nini hapa?”
“Wakubwa zako wakiuliza maswali jibu ,acha kuuliza maswali”Aliongea Roma akimfinya Donyi puani na kumfanya mwanadada huyu ampige Roma na kijibegi chake alionesha kutopenda Roma alichomfanyia.
“Unaniona kama mtoto?”
“Sio nakuoan kama mtoto , wewe ni mtoto na nikikukadiria unamiaka kumi na nane na umevunja ungo juzi tu”
“Looohh! Umekosea babu ,nina kumi na tisa”Aliongea Donyi na alionekana kumzoea kweli Roma kwa haraka , jambo ambalo lilimshangaza hata Nadia aliekuwa akiwaangalia.
“Hivi Anko jina lako unaitwa nani?”
“Naitwa Anko”Wakati Roma na Donyi wakiendelea kujibizana Sherehe ilianza na ni kama Roma alivyodhania , ilikuwa ni sherehe ya kumpongeza kijana wa kiume mkubwa wa Tajiri Azizi aliekuwa akifahamika kwa jina la Kassimu, lakini pia kulikuwa na tukio lingine la kumpongeza Mzee Atanasi, ambaye ametimiza miaka mia moja , Roma alishangazwa na jambo hili , licha ya kwamba Babu ambaye alipandihswa kwenye steji kuonekana mzee , lakini alikuwa ni mwenye afya yake nzuri..
Mzee Azizi alimpongeza kijana wake huku akiweka wazi kama mrithi wa mali zake, watu walimpongeza Atanasi na kwa jinsi kijana huyu alivyoonekana, alikuwa ni vijjana ambao walionekana kujiamini.
Kuna jambo ambalo Roma hakuelewa ila alipanga kumuuliza Edna wakati wa kurejea nyumbani.
Roma kwenye sherehe hii alipenda tukio moja tu na hilo lilikuwa ni muda wa chakula , yeye mambo mengine kwake hayakumvutia tofauti na Edna alieonekana kufurahi kuongea na baadhi ya wageni ambao walikuwa ni wafanya biashara wenzake.
Roma alikuwa ni kama mlinzi muda wote alikuwa akiangalia usalama wa Edna , licha ya kwamba alikuwa mita kadhaa tokea alipokuwa amesimama mke wake , lakini aliweza kugundua ni nani aliekuwa akimwangalia kwa macho mabaya Edna na aliweza kupata watu wawili ambao walikuwa wakimwangalia Edna kwa macho ambayo hakuyaelewa , wa kwanza alikuwa ni Denisi , huyu alionesha hali flani ya kimatamanio kwa Edna na kwa Roma alimuona Denisi kama mtu ambaye alikuwa ana mpango na Edna na hakuonesha kuheshimu Edna kama mwanamke ambaye ana mume , jambo ambalo kwake sio kama hakupenda wanaume kumwangalia Edna kwa macho ya kumtamani , alikua akijuwa mke wake ni mrembo hivyo kukodolewa macho na wanaume ni jambo la kawaida , ila macho ya Denisi yalizidi ila hakutaka kufanya lolote kwea wakati huo, aliona kuna siku lazima ambananishe tu.
Mtu mwingine aliekuwa akimwangalia Edna alikuwa ni mke wa Raisi Jeremy , alietambulishwa kwake kama First Lady huyu mwanamama Roma alimuona kama mtu ambaye hakuwa akimwangalia Edna kwa namna ya kumtakia mema , alimuangalia kwa namna flani hivi ambayo mwenyewe alitafsiri kama mtu mwenye kinyongo.
Wakati Roma akiwa ameshikilia wine yake, mara alikuja kushituliwa na mke wa Tajiri Azizi yaani Mama Nusra.
“Mr Roma kuna mtu nataka uonane nae ,nadhani hautojali nikikuiba kwa dakika”Aliongea mwanamama huyu na Roma alitingisha kichwa na kuongozana na Mama Nusra.
Waliingia ndani ya jumba hili kubwa ambalo kwa ndani lilikuwa likipendeza Zaidi ya nje ,kutokana na thamani za hali ya juu zilizokuwa zimetumika kama mapambo.
Aliongozwa mpaka kwenye chumba ambacho Roma aligundua kuwa chumba hiki sio sebule bali ni kama chumba cha kulala.
“Karibu Mr Roma”Roma alikaribishwa na Mama Nusra ndani ya chumba hiki ambacho kilikuwa ni Chumba kilichokuwa kinajitegemea , kwani kilikuwa na sebule kwa ndani ndogo na meza ya kusomea iliokuwa na tarakishi ya kampuni ya Dell, Roma macho yake yalipita harakaharaka kukagua chumba kizima na hapa ndipo alipoweza kuona picha kubwa iliotundikwa ukutani , picha hii ilikuwa ni ya Mzee Atanasi na Raisi wa kwanza wa Tanzania Julius Kambarage nyerere na wanaume wawili ambao Roma hakuwafahamu , ilikuwa ni picha ya pamoja mabayo kwa kuiangalia tu, ungegundua watu waliokuwa kwenye picha hio walionekana kuwa marafiki kutokana na mkao wao , walikuwa wameangaliana huku wakicheka.
NITARUDI WIKIEND JMOSI SAA 3 KAMILI USIKU
SIMULIZI INAENDELEA GRUPU NA WATSAPP INBOX KWA SPIDI YA 4G UNACHOPASWA KUFANYA NI KUCHIGIA KIASI KISICHOPUNGUA 2500 ILI NIKUUNGE A GRUPU , UKITAKA INBOX TU SPECIL BILA KUUNGWA GRUPU NI 3000.
NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
Inabidi leo atupie mzigo j5 mbali sana kiongozi.Hadithi nzuri sana ila unavuta sana mkuu.eneo moja linachukua pakubwa sana.kwa mfano leo hujatundea haki kwa kweli.
Sawa mkuu tunasibiri kwa hamunitawashushia mzigo Heavy baadae
Tunakusubiri mkuu mda ndio huu tupia vitunitawashushia mzigo Heavy baadae
Shukrani sana mkuuSEHEMU YA 116
Roma alimaliza taratibu zake zote baada ya kuamka na ni muda wa saa mbili kamili za asubuhi alishuka mpaka sebuleni kwa ajili ya kujipaitia kifungua kinywa kilichoandaliwa na BiWema.
“Bi Wema msimuamshe Edna muacheni alale mpaka atakaposhituka mwenyewe”Aliongea Roma mara baada ya kumsalimia Sophia na Bi Wema.
“Jana Miss na wewe mlirudi saa ngapi?”
“Tulirudi mapema tu , niliwakuta mnaangalia tamthilia yenu na siku taka kuwasumbua”Aliongea Roma na kila mtu akajiweka bize kuendelea kunywa chai ,huku Sophia akiibia ibia kumwangalia Roma , haikueleweka mrembo huyu alikuwa akifikiria nini.
Roma kama alivyopanga siku ya leo hakuwa kabisa na mpango wa kwenda kazini , alipanga kumpeleka Yezi kituoni ili akamsalimie Mama Issa, alipumzika kidogo kwenye chumba chake mpaka muda wa saa tatu kama na nusu za subuhi na alimpigia simu Yezi kwamba anamfuata sehemu ambayo amepanga na amkute amejiandaa.
Dakika chache mbele Roma alikuwa ashafika na alimkuta Yezi akiwa amesimama nje alievalia suruali yake ya jeans na jezi ya Yanga.
“Ingia twende Yezi”Aliongea Roma baada ya kusimamisha gari na kumuona Yezi amezubaa zubaa, huku pia wamama wa Kiswahili waliokuwa nje ya viubaraza vyao walihusudu gari ya Roma na kujiambia kwenye nafsi yao Danga lake Yezi ni bab kubwa.
Yezi ndio aliekuwa ametawala maongezi kwenye gari na kumfanya Roma kucheka , kwani alifurahishwa na baadhi ya stori za Yezi, na hii ilifanya safari yao kuchukua muda mfupi kuliko walivyotarajia , lakini baada ya kukaribia karibu na kituo hiki Yezi alijikuta akiwa kimya na kumfanya Roma amshangae.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi Yezi ,Mama Issa atafurahi sana kukuona siku hii ya leo”Aliongea Roma kumtia moyo Yezi , kwani aliona mabadiliko yake na Yezi alivuta pumzi na kuitikia kwa kichwa.
Roma ile anaingiza gari yake upande wa kushoto wa hiki kituo mita kama mia hivi kutoka getini, alisimamishwa na watu watatu, wote wakiwa kwenye mavazi ya suti ,wawili wakiwa ni wanaume na mmoja alikuwa ni mwanamke, Roma alishangaa kwanini kasimamishwa na watu hawa ilihali anataka kuingia kituoni.
“Tunaomba mgeuze gari mrudi na mtakuja siku ya kesho au mrudi baadae”Aliongea yule mwanamke na alionekana ndio aliekuwa ni kiongoza.
“Kwanini nirudi kesho wakati nimepanga kuja kituoni leo?”
“Mr kuna swala la kiusalama linaendelea hapa ndani na hamruhusiwi kupita”Aliongea yule mwanaume mmoja aliekuwa pembeni ya yule mwanamke, na kwa jinsi mwanaume yule alivyoongea Roma aligundua kuwa ni mkenya kutokana na rafudhi yake.
“Anko tutarudi kesho wanaonekana kuwa wanausalama”
“Yezi tulia tushakuja tayari na siwezi kurudi tena”Aliongea Roma huku akifungua mlango na kutoka nje na kuwafanya hawa wanausalama kuzidi kupandwa na hasira , maana waliona Roma analeta ngumu.
“Mr acha kujitafutia matatizo , tushasema eneo hili hauwezi kuingia siku ya leo mpaka kesho kutokana na itifaki za kiusalama”
“Kwahio unamaansha huko ndani kuna mtu mzito kutoka serikalini?”Aliuliza Roma akiwa hana hata wasiwasi.
“Mpaka hapo nadhani ushaelewa , hivyo geuza gari yako na uondoke usitulazimishe tutumie nguv”.Roma kwanza aliona hii ngumu na haikueleweka alikuwa akiwaza nini kwani alikuwa akikuna kichwa chake , aligeuka nyuma na kumwangalia Yezi ambaye alionekana kuwa na wasiwasi na hawa walinzi wote walikuwa wameshikilia Siraha za moto.
Wakati Roma akiwa amesimama pasipo kufanya jambo , ziliingia gari nyingine tatu eneo hili kwa upande wa nyuma na kuwafanya hawa walinzi wote waziangalie.
Gari moja ilikuwa nyeupe na mbili zilikuwa ni nyeusi moja ikiwa ni Mercedez Benz S-class na mbili zote zilikuwa ni gari kubwa aina ya V8, sasa barabara hii ya kuingia kituoni ilikuwa ni ndogo na ilikuwa ikiruhusu gari moja kwa wakati kupita na hivyo kitendo cha Roma kusimamisha gari yake ni kwamba alikuwa amezuia gari za nyuma yake kushindwa kupita.
“Kuna nini kinaendelea hapa?, tunataka kuingia kituoni mmezuia barabara”Aliongea bwana mmoja alievalia mavazi ya suti , alionekana alikuwa ni moja ya walinzi ambao wamekuja na gari hizo.
“Ajent Dondwe familia ya Mzee Atanasi imeshafika , nini tunapaswa kufanya?”Yule mwanamke alibonyeza kifaa chake sikioni na kuongea hayo maneno na ilionesha alikuwa akiwasiliana na waliokuwa ndani ya kituo, na baada kuongea hayo maneno alionekana kupewa maelekezo mengine na almpita Roma na kuelekea kwenye gari zilizokuwa nyuma , lakini kabla hata hajafika , alishuka mwanamama ambaye baada ya Roma kumwangalia tu alimfahamu, alikuwa ni Jestina mke wa tajiri Azizi , alijiuliza mwanamama huyu anafanya nini hapa.
“Madam unapaswa kurudi kwa siku ya leo , kuna itifaki za kiusalama zinazoendelea ndani ya hili eneo na haruhusiwi mtu yoyote kuingia kwa sasa”Aliongea yule Ajenti wa kike na kumfanya mwanamama huyu kushangaa , lakini macho yake pia alikuwa ameyaelekeza kwa Roma na yeye alijiuliza ni jambo gani ambalo limemleta Roma hapo kituoni.
“Kuna nini kinaendelea ambacho kinanifanya nisiingie ndani ya hiki kituo?”Aliuliza Jestina kwa mshangao na mpaka kufikia hali hio aliokuwa akiishuhudia , aliamini mpango wa kuonana na dada yake unakwenda kukwama.
“Lazima nionane na dada yangu kwa namna yoyote leo , najua hizi ni mbinu za kunizuia nisionane nae”Aliwaza mwanamama huyu huku akimwangalia Roma kwa sekunde na kisha akageuza na kwenda mpaka gari ya katikati , sio ile aliotoka ni ile ambayo ilikuwa ni ndogo aina ya Mercedez.
“Baba! Inaonekana walinzi wa raisi wa Kenya wanatuzuia tusionane na Blandina”Aliongea Jestina baada ya kioo kushushwa na ndani ya gari hio alionekana mzee Atanasi akiwa ameegamia kiti akiwa ameshikilia fimbo yake.
Upande wa ndani ya hiki kituo , ndani ya ofisi ya Mama Issa anaonekana Maina akiwa kwenye sura yake bandia huku akiwa amezungukwa na walinzi waliovalia suti nyeusi na mashati ya rangi yeupe , huku wakiwa wote wamevalia ‘Ear pieces’.
“Madam!, Mheshimiwa Raisi anataka urudi Kenya mara moja na hauruhusiwi kuongea na mtu yoyote ndani ya Tanzania mpaka utakapofika Kenya “Aliongea bwana mmoja hivi aliekuwa na mwili mkubwa kuliko wanausalama wote na alionekana ndio aliekuwa ni kiongozi.
“Siwezi kurudi Kenya pasipo kutimiza kile kilichonileta hapa, mwambieni hivyo Kamau”Aliongea Maina kwa hasira.
“Madam unafanya kazi yetu kuwa ngumu , tunaomba utoe ushirikiano”
“Nadhani hujayalewa maneno yangu , nishasema siwezi kutoka hapa pasipo kuoanana na mtu ambaye nimepanga kuonana nae na mtu yoyote asije akanigusa”Aliongea Maina na kufanya walinzi hawa waangaliane.
Walinzi hawa kazi yao waliona kuwa ngumu katika siku zote ambazo wamewahi kuhudumu kwa kumlinda mke wa Raisi Kamau, licha ya kwamba siku zote walinzi hawa walikuwa wakipokea maagizo kutoka kwa mke wa Raisi , lakini leo hii mara baada tu ya kuingia ndani ya kituo hiki , walipigiwa simu na mheshimiwa mwenyewe kutoka Kenya, akiwapa maagizo ya kumrudisha mke wake haraka nchini na haruhusiwi kuongea na mtu yoyote kwa usalama wake, na kwa maagizo hayo hata Mama Issa hakuruhusiwa kabisa kuongea nae na ndio maana hakuwepo kabisa kwenye hiko chumba cha ofisi.
Licha ya kwamba walinzi hawa hawakupewa maelekezo ya kutosha kutoka kwa muheshimiwa , lakini ilibidi watii oda ya raisi na mbaya Zaidi hakukuwa na maelekezo mengine ambayo yalikuwa yametolewa kwao na hii ilikuwa ni saa mbili za asubuhi muda mfupi baada ya Maina kufika hapo kituoni.
Sasa hawa walinzi walijitahidi kumueleza Maina juu ya agizo kutoka kwa mheshimiwa Raisi kumtaka Maina arudi nchini mara moja , lakini Maina hakutaka kurudi , alijua Kamau lazima atakuwa ashajua kuwa anakuja kuonana na familia yake na ndio maana alikuwa akitaka kuzuia jaribio hilo , hivyo aliona leo pasipo kutimiza azima yake anaweza asifanikiwe kabisa na ndio maana alileta ngumu na hii iliwafanya waljnzi hawa wapate ugumu wa kutekeleza maagizo , kwani licha ya kwamba walipewa oda , lakini pia walikuwa wakimheshimu mke wa raisi ,kwani walifanya nae kazi kwa muda mrefu sana hivyo unaweza ukasema kwamba walikuwa ‘Half loyal’ kwa Maina.
Baada ya Maina kuweka ngumu , hawa walinzi wa kitengo cha Secret service ilibidi wawasiliane na mheshimiwa kueleza kwamba madam hataki kurudi na jambo hili lilimkasirisha sana Mheshimiwa.
“Naona mnashindwa kufanya kazi yenu kwa weledi Njiro?”
“Hapana mheshimiwa Madam kagoma kutoa ushirikiano”
Kikawaida mke wa Raisi wa Kenya alikuwa akilindwa na walinzi wanne na ni hao ambao alikuwa akitembea nao kila mahali, na hawa walinzi alikuwepo Njiro ambaye ndio aliekuwa msaidizi wa karibu kabisa wa First Lady , lakini pia kuna walinzi wengine wawili wa kiume na msichana.
“Njiro ndani ya dakika therathini wanakuja Ajenti kutoka NIS wakiongozwa na Ajent Dondwe ,Hakikisha mke wangu haongei na mtu yoyote mpaka muda huo”Aliongea Mheshimiwa Kamau na kisha akakata simu.
NIS ni kitengo cha kijasusi cha Kenya kinachokwenda kwa kirefu cha National Intelligency Security na kitengo hiki kilikuwa na wanausalama wake ndani ya Tanzania kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wanausalama wa TISS kuwa ndani ya Taifa la Kenya.
Baada ya kama dakika arobaini na tano ndio Ajenti kutoka kitengo cha ujasusi cha Taifa la Kenya walifika ndani ya ofisi hii ya Mama Issa.
“Madam naitwa Ajenti Dondwe na hawa ni wenzangu , tupo hapa kwa ajili ya kuimarisha usalama , kwa maagizo tiliopewa ni kuhakikisha unatoka ndani ya hii nchi pasipo kuongea na mtu yoyote kwa ajili ya usalama wako”Aliongea Ajenti Dondwe mara baada ya kuingia ndani ya hii ofisi.
“Ajenti Dondwe nipo hapa Tanzania kwa ajili ya kikazi na mpaka sasa hakuna tishio lolote linalohatarisaha usalama wangu”
“Madam tunakuheshimu kama First Lady wa Taifa letu la Kenya , lakini wakati huo huo tunatii maagizo kutoka kwa raisi wa Kenya”Aliongea Dondwe akiwa siriasi.
“Ajenti Njiro hakikisha hakuna mtu anaesogelea kituo hiki kwa mita mia moja kutoka barabarani , utaungana na Ajenti niliokuja nao , nyie wawili mtabaki na mimi hapa ndani”Aluongea Dondwe na Ajenti Njiro alimwangalia Madam kwa huruma na kisha akatoka.
Kwahio licha ya kwamba Dondwe alipewa mamlaka ya kuhakikisha mke wa Raisi anarudi Kenya pasipo kuongea chochote , lakini hakuwa na mamlaka ya kumbeba kwa ulazima bila ruhusa yake , ingekuwa ni kuvunja itifaki za kiheshima kwa mke wa Raisi na ndio maana walitaka kutumia mbinu ya ushawishi kwanza na Mbinu hio haikudhaa matunda kwa takribani lisaa limoja mpaka Roma anafika hapa ndani ya kituo.
Baada ya Dondwe kupata taarifa ya ujio wa mke wa Tajiri Azizi akiwa na familia yake , uso wake ulizidi kuwa mweusi kutokana na wasiwasi , bwana huyu alikuwa na maelekezo ya kuzuia familia hio kukutana kwa namna yoyote na Maina, licha y a kwamba alishindwa kuelewa nini kinaendelea aliona ni wajibu wake kutii kile ambacho ameagizwa na mkuu wake wa nchi , Wakati akiendelea kuwaza cha kufanya simu yake ilianza kuita na kuitoa mfukoni.
“Dondwe mmefikia wapi mpaka sasa?”Aliuliza Mheshimiw Kamau aliekuwa kwenye hali ya wasiwasi.
“Madam Kagoma kabisa kutoa ushirikiano mheshimiwa , nahitaji amri yako nitumie nguvu”Aliongea Dondwe na kimya kikatawala kwa sekunde kama tano.
“Mpe Maina simu”Aliongea Kamau na Dondwe alifanya kama alivyoelekezwa .
“Kamau kwannini unanifanyia hivi?”
“Maina Jambo ambalo unataka kufanya linaniweka katika wakati mgumu , hebu nifikirie japo kidogo ni madhara gani yatatokea ukifanya hivyo”
“Kamau labda haujawahi kunifahamu , nilishafanya maamuzi tokea siku ya kwanza naingia ndani ya ikulu ya Wananchi wa kenya hii siku ikifika lazima niweke ukweli wote wazi”Aliongea Maina kwa hasira.
“Blandina mke wangu , najua mateso yako lakini hebu nifikirie kidogo kama kweli unanipenda , Please Blandina nipe muda wa miaka miwili”Licha ya mheshimiwa kuonekana kutumia kila mbinu ya kumshawishi Maina , lakini mwanamama huyu alishupaza shingo , alikuwa ashafanya maamuzi tayari mpaka kwa kufikia hapo.
“Kamau wewe ni mbinafsi sana, lazima nionane na familia yangu , niashachoka”Aliwaza Mke wa raisi baada ya kukata simu na Dondwe kuichukua na muda huo huo iliita tena.
“Dondwe mnaruhusa yangu tumieni njia yoyote hata kumzimisha”
“Sawa Mheshimiwa”Alijibu Dondwe na kisha alikata simu na kumuangalia mke wa Raisi.
“Madam naomba utoe ushirikiano wako , kabla hatua kali Zaidi hazijafanyika kuhakikisha unatoka ndani ya hili taifa”Aliongea Dondwe na Maina alijikuta akijawa na wasiwasi , aliomba hata malaika atokee amuokoe katika hio hali .
Dondwe baada ya kuona hakuna dalili ya Madam President kutii agizo, alimsogeleea.
“Unataka kufanya nini dondwe , nakuambia usije ukanigusa”
“Samahani madam”Aliongea dondwe na palepale akamfinya shingoni Madam President na akazima na akawapa ishara ajenti wenzake wambebe.
SEHEMU YA 117
Roma alielezwa kwa ufupi sana na mke wa Tajiri Azizi juu ya sababu ya wao kuja ndani ya hiki kituo kwa siku hii ya leo.
“Kwahio mmepanga kuonana na mke wa Raisi wa Kenya ndani ya hiki kituo?”Aliuliza Roma ili aelewe vizuri na mama huuyu alitingisha kichwa , licha ya kwamba amemuelezea Roma , lakini ukweli ni kwamba mwanamama huyu hakuwa na matumaini yoyote na aliona kama jambo hili likishindikana ampigie mume wake simu ili kumuomba msaada , licha ya kwamba hawakuwa wamempa taarifa juu ya jambo hilo.
“Kama mnamiadi nae basi nadhani hawa walinzi wanafanyakosa kubwa la kuwazuia”Aliongea Roma na kumfanya mwanamama huyu asimuelewe Roma alichokuwa akimaanisha.
Njiro aliekuwa amesimama mita kadhaa , alikuwa na wasiwasi mno , katika maisha yake ya kazi ya usalama hakuwahi kukutana na hali kama hio ambayo inamfanya kushindwa kuwa na maamuzi ya moja kwa moja , mwanamke huyu alikuwa kwenye dilema.
“Eti dada unaitwa Ajenti Nani?”Aliuliza Roma baada ya kumsogelea.
“Hupaswi kufahamu jina langu , unachopaswa ni kuondoka hapa”
“Wewe unaongea kama nani?”Aliuliza Roma lakini Njiro alishindwa kumuelewa.
“Unamanisha nini?”
“Namaanisha kwamba hapa ni Tanzania , hivyo huwezi kutuambia cha kufanya kwenye nchi yetu si Ndio Mrs Azizi?”Aliuliza Roma na kumfanya Jestina atingishe kichwa.
“Acha kibuli wewe mwanaume , nadhani haunitambui vizuri , kama unataka uondoke huna meno endelea kunigomea”Aliongea Njiro kwa dharau na kumfanya Roma atabasamu na kumpima huyu mwanamke kwa sekunde.
Yezi aliekuwa kwenye gari alikuwa akitetemeka sana , alitamani kumwambia Roma waondoke waache kuleta fujo na watarudi hata siku nyingine.
“Fyuu…!!!,, Fyuu.. Fyuu. Fyuu”Haikueleweka mara moja ni spidi ya aina gani aliotumia Roma kwani aliwapiga wanausalama wote shingoni ndani ya sekunde nne, jambo la kushangaza ni kwamba licha ya hawa wanajeshi kupigwa ndani ya sekunde nne , walidondoka chini wote kwa wakati mmoja wakiwa hawajitambui na ni Dhahiri kwamba hata kama watakaposhituka baadae hawataelewa ni nini kilitokea kwao.
Kila mmoja alieshuhudia kile kilichotokea alishangaa mno sio Yezi , sio mke wa tajiri Azizi , sio Mlinzi , sio mzee Atanasi , wote hawakuelewa nini kilichotokea Zaidi ya kuona kitendo cha Roma kupotea na ile anaibuka wanausalama wote walidondoka chini, ni rahisi kusema hawakuona tukio la Roma kuwagonga shingoni wale walinzi kwani alitumia spidi kubwa sana na ukizingatia pia Walinzi walikuwa wameachana kwa mita kama moja hivi umbali.
“Roma umewafanya nini?”Aliuliza Mrs Azizi kwa mshangao , lakini Roma hakuwa na jibu.
“Mrs Azizi nadhani sio muda wa maswali huu”Aliongea Roma na kuwabeba wale walinzi na kuwaweka pembeni ya barabara na kisha akaingia kwenye gari na kuendesha pasipo kumjali Yezi ambaye yupo kwenye mshangao.
Dondwe baada ya kumzimisha Maina na vijana wake kumbeba alibonyeza kitufe chake shingoni ili kuwasiliana na wanausalama wenzake wa nje , lakini ajabu alikosa mawasiliano na kuanza kuingiwa na wasiwasi.
“Nyie wawili mshikilieni vizuri mkamuingize kwenye gari , tunaondoka ndani ya hili eneo”Aliongea Dondwe huku akimpa ishara mwanausalama mmoja atoe siraha yake na awe makini , huku na yeye akitoa yake.
Ndani ya hili eneo , hapakuwa na mtu kabisa na ilionekana tahadhari zilikuwa zimechukuliwa , kwani haikuwa kama ilivyozoeleka licha ya kwamba leo ilikuwa ni siku ya katikati ya wiki , watoto wote walionekaa kuwa ndani ya majengo yao na hata Mama Issa pia hakuonekana.
Ile Dondwe anafungua mlango wa geti kwa kulisikuma ili kuruhusu gari za ndani zitoke alishangaa kumuona Roma aliekuwa amesimama na ilionekana alikuwa na yeye anataka kufungua geti.
“Mr Usalama! ,Mke wa Raisi yuko wapi wageni wake washafika”Aliongea Roma pasipo kujali huku akinyooshea vidole gari zilizokuwa nyuma ya gari yake ,Dondwe alijikuta akiangalia mbali Zaidi ya magari na hapa ndipo alipoweza kushuhudia vijana wake wakiwa chini pembezoni mwa barabara.
“Kacha Kacha”.Dondwe alikoki siraha yake huku akimnyooshe Roma.
“Nyoosha mikono juu na kaa pembeni , ukisogea hatua moja tu nakuchangua ubongo wako”Aliongea Dondwe lakini Roma hakujali yaani ni kama alimuona Dondwe kashikilia ‘toy’.
“Mr Usalama licha ya kwamba sipendi bunduki , lakini vile vile siziogopi , ninachotaka ni Amani itawale bila ya kutumia nguvu”Aliongea Roma na wakati huo huo gari zilizokuwa ndani zilisogelea geti na zenyewe zikitaka kutoka na akashuka na mwanausalama mwingine akiwa na siraha yake mkononi.
Mrs Azizi alijikuta akiwa ni mwenye wasiwasi kweli, hakuwa akiona kinachoendelea mbele kutokana na kwamba gari ya Roma ilikuwa imewazibia,Roma baada ya kuona Dondwe hayiupo tayari kumsikiliza alitumia sipidi ile ile ya mwanzo kumdhibiti Dondwe na mwenzake na baada ya kuona amefanikiwa , aliwatoa njiani na kisha akasogelea gari iliokuwa ikiwashwasha taa za mbele ikiashria inataka kutoka.
Wale walinzi kwa jinsi walivyoshuhudia namna ambavyo Dondwe na mwenzao walivyonyamazishwa na Roma walijikuta wakiwa kwenye mshituko na hawakuelwa ni jambo gani la kufanya wakiti huo.
Roma alimpa ishara dereva asogeze gari lake pembeni na kisha ashuke na dereva mwanausalama alitii, na kusogeza pembeni na kisha akazima gari na Roma akawapa ishara watoke kwenye gari.
“Okey! Madam President yuko wapi?”Aliuliza Roma lakini wanausalama hawa walishindwa kujibu na hii ni kutokana na kwamba walikuwa kwenye mshituko bado na kuogopa kwa wakati mmoja.
Ni baada ya nusu saa hali ndani ya kituo ilirudi kawaida na Mama Issa alionekana kuwa na furaha kubwa baada ya kuonana na Yezi , mwanamama huyu alikuwa amekaa na Yezi eneo la nje , sehemu ya kupumzikia kwenye majengo haya ya utawala huku wakiongea kwa furaha, kwa jinsi walivyokuwa wakiongea nni kama hakukuwa na tukio lililokuwa limetokea dakika kadhaa nyuma.
Wanausalama wote walikuwa wamefungwa na Kamba ngumu miguuni na mikononi na Roma , akisaidiana na mlinzi wa mke wa tajiri Azizi na wote walikuwa wanajitambua kwani ile Roma anamaliza kuwafunga aliwaamsha.
Dondwe na Njiro hawakuelewa ni nini kimetokea na walishindwa hata kuongea Zaidi ya kumwangalia Roma aliekuwa hana hata habari nao huku wakiwa na maswali mengi kwenye vichwa vyao , lakini sio maswali tu woga uliwajaa na wasiwasi kwa wakati mmoja , mpaka muda huo hawakujua Mke wa Raisi yuko wapi.
****
“Blandina nisikilize, kama hutaji nimwonyeshe hizi Picha Senga unatakiwa kukubali ninachokuambia”
“Kamau sikujua una roho ya kinyama namna hii?”
“Sina roho mbaya Blandina wewe ndio ulienilazimisha mimi kufanya haya yote , kumbuka tulipotoka mimi na wewe , nilikupenda wa kwanza , nikakufanyia kila kitu , lakini alipotokea tu Senga ukaamua kuniacha, unajua ni maaumivu gani nilipitia , huna haja ya kunilaumu kwa maamuzi yangu”
“Sikuwahi kukubalia Kamau kwa sisi kuwa wapenzi , kufanya kwetu mapenzi ilikuwa ni msukumo wa kimwili tu , lakini sikuwahi kukupenda Kamau na nilikuambia kabisa siku nikipata mwanaume ninaempenda tunaacha”
“Blandina kama haupo tayari uniambie sitaki kusikia ngonjera zako mabazo hazina ukweli , hii ni nafasi pekee niliokuwa nayo , nimetoka Kenya mpaka hapa Lampur kwasababu ya hii nafasi , siwezi kuichezea hata kidogo, kama hutaki niambie nimtumie Senga hizi picha , nadhani baada ya hapa mtaendelea kupendana sana”
“Usinifanyie hivyo Kamau, Sitaki kumsaliti Senga najua tuna hisitoria mimi na wewe lakini hayo yashapita naomba usimtumie Senga hizo picha”
“Sikia Blandina nafanya yote haya kwasababu nakupenda sana naomba kesho ughairishe kwenda China tutumie nafasi ya kesho na kesho kutwa na baada ya hapo nitakuacha na maisha yako, Blandina na nakuapia hizi picha nitafuta kama utakubali na sitokusumbua”
“Siwezi kufanya hivyo , Denisi ni mgonjwa na taratibu za kiusafiri zishafanyika tayari , siwezi kughairisha”
“Najua Denisi ni mgonjwa na ndio maana kesho ataondoka na Bite na wewe utabaki , ila sikulazimishi Blandina ,nikuambie tu muda utakao ingia kwenye ndege ndio muda ambao nitahakikisha hizi picha zinamfikia Senga”
Naam hayo ni mazungumzo ambayo yalikuwa yakifanyika ndani ya mgahawa mmoja katikati ya jiji la Kual Lampur , mazungumzo haya yalikuwa ni kati ya Blandina na Kamau Kamau na ilikuwa ni miaka Zaidi ya Ishirini iliopita wakati Blandina akiwa nchini Malaysia kwa ajili ya matibabu ya Denisi.
Baada ya siku kupita baada ya mazungumzo hayo kufanyika yaani saa saba mchana ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa uliokuwa ndani ya jiji hili la Kual Lampur , alionekana Blandina pamoja na mwanadada mmoja hivi mrefu mwemambamba ,Maji ya kunde aliekuwa akifahamika kwa jina la Bite wakiingia ndani ya jengo la wasafiri lililokuwa na maandishi makubwa ya ‘Departure’. Blandina alikuwa amemshikilia mkono mtoto mdogo wa miaka kama mitano hivi.
“Denis utatangulia na Mama Mdogo Bite, sawa mwanangu”
“Hapana mama twende wote”
“Nisikilize Denisi Mama yako ,utaenda na Mama mdogo kama tulivyoongea jana sawa?”Aliongea Blandina huku akimgusa Denisi kichwani kwa kumbembeleza.
“Bite nina dharula inayonitaka kubaki hapa Malaysia ile kesho nitafika , naomba utangulie ,taratibu zote za mapokezi zishafanyika kwa upande wa China”
“Sawa ila inabidi iwe kesho kweli , Denisi ni mgonjwa na anakuhitaji wewe Zaidi kuliko mtu yoyote”Aliongea Bite na kumfanya Blandina ajisikie vibaya, alikuwa ni mwenye huzuni mno kumuachia Denisi kwenda China peke yake.
“Nisamehe mwanangu , najua hali yako kwa sasa sio mbaya , ila nafanya haya yote kulinda ndoa yangu , nakupenda sana Denisi”Aliwaza Blandina wakati akiwaangalia Bite na Denisi wakitokomea kwenye mlango kuelekea kupanda ndege ya Shirika la M Airline.
“Blanidna hupaswi kuwa na mawazo tena , baada ya leo kesho utasafiri kwenda kumuona mwanao”Blamdina alijikuta akigutushwa na sauti ilio nyuma yake , sauti aliokuwa akiijua vyema kama ni ya Kamau.
Blandina hakutaka kuongea neno , alijikuta chozi likimtoka huku akitangulia mbele kutoka ndani ya jengo hili la uwanja wa ndege,moyo wake ulikuwa ukimuuma mno mpaka yeye alijishangaa.
Bite alijikuka akichangamka mara baada ya kukutana na mwanamke wa kiafrika ambaye alikuwa amekaa siti ya pembeni na yeye , mwanamke ambaye alikuwa amebeba mtoto mdogo.
“Mnaenda China kufanya nini?”Aliuliza yule mwanadada ambaye alijitambulisha kwa jina la Regina.
“Ni kwa ajili ya Denisi , ni mgonjwa “Alijibu Bite.
“Pole jamani , nini Zaidi?”
“Ana saratani ya Ubongo”Alijibu Bite na kumfanya mwanamama Regina amuonee huruma Denisi, alishangazwa na mtoto mdogo namna hio kuwa na saratani ya Ubongo.
“Na wewe mtoto wako anaitwa nani?”
“Lorraine”Alijibu huku akitabasamu.
“Una katoto kazuri mno”.
“Asante”Wadada hawa wawili yaani Regina na Bite waliacha kuongea mara baada ya kuambiwa wafunge mikanda kwani Ndege inataka kupaa.
Regina alikuwa na yeye akielekea nchini China akiwa na mtoto Lorraine na Bite alikuwa akielekea nchini China kumpeleka Denisi kwenye matibabu.
“Blandina najua unaniona kama mnyama , lakini baada ya tukio linaloenda kutokea muda mfupi ujao utanishukuru” Aliwaza Kamau Kamau wakati akiwa na Blandina kwenye Taxi. Na hio ilikuwa ni miaka Zaidi ya ishirini nyuma.
Kamau Kamau alionekana kujua kuna jambo ambalo linaenda kutokea muda mchache unaokuja , je kama ni kweli alifahamu vipi kutokana na tukio lenyewe na ilikuwaje Blandina akabakia kwake.
ITAENDELEA NEXT EPISODE MUDA WOWOTE KABLA YA SAA TATU
SEHEMU YA 118
Mheshimiwa Raisi Kamau alionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno na hii ni baada ya kukosekana hewani kwa Dondwe na kumfanya kutofahamu ni nini kinaendelea nchini Tanzania.
Bwana huyu alijilaumu sana kumruhusu Maina kwenda Tanzania pasipo kuchukua tahadhari zozote.
Ukweli ni kwamba baada ya Maina kupanda ndege na baada ya masaa mawili kupita ndipo mheshimiwa alipopewa ujumbe na Deo kuwa inawezekana Madam anaenda kuonana na mke wa tajiri Azizi.
Baada ya mheshimiwa Kamau kupata hii taarifa , alitafuta namna ya kuhakikisha taarifa hio na hapo ndipo alipompigigia mtu wake aliempandikiza ndani ya familia ya Tajiri Azizi na ni kweli alipewa taarifa kwamba Mke wa Tajiri Azizi yaani Jestina alikuwa na ratiba ya kwenda kituo cha kulelea yatima cha Son And Daughter Orphanage, na mpaka hapo ndipo Kamau alipopata kujua jambo ambalo Maina alikuwa akilifanya , alishangaa sana na kuona ni kwanini Maina hakumshirikisha.
“Inanipasa kutulia naamini Blandina anataka tu kuonana na familia yake , na hatoongea Zaidi ya anayoyajua , napaswa kumuamini”Aliwaza Mheshimiwa Kamau huku akichukua maji kwenye glasi na kunywa kidogo ili kujituliza , lakini licha ya kujiambia maneno hayo bado bwana huyu alikosa utulivu kwenye akili yake.
*****
“Mheshimiwa Maina amefanikiwa kuonana na familia yake leo”Aliongea Linda mlinzi wa raisi Jeremy na kumfanya mzee huyu kutabasamu.
“Iliwezekana vipi Kamau akashindwa kumzuia mke wake?”
“Kwa taarifa za watu wetu nchini Tanzania wanasema raisi Kamau alijitahidi kuzuia , ila alishindwa kutokana na Roma kuingilia”Jeremy alitoa macho na kumwangalia Linda ni kama hajasikia vizuri.
“Ilikuwaje Roma akawa ndani ya hiko kituo?”
“Mpaka sasa sijapata taarifa Zaidi Mheshimiwa”.
“Hili swala sikudhania litatokea mapema hivi nadhani ni muda sasa wa kuanzisha mpango wangu niliokuwa nao miaka mingi , lakini bado namuonea huruma Senga”Aliongea Jeremy.
“Lakini Mheshimiwa Naamini Mheshimiwa Kamau hakuna anachokifahamu kuhusu mpango LADO”
“Linda unachoongea ni kweli na mimi nataka kuamini hivyo na nimekuwa nikijitahidi miaka na miaka kuamini hivyo , lakini mienendo ya Kamau haijawahi kunifanya nimwamini , kumbuka Kamau ndio mtu pekee aliekataa kuingia kwenye mpango TASAC licha ya kumlazimisha”
“Naelewa Mheshimiwa lakini bado naona ni swala ambalo linakosa muunganiko , maana swala la kupotea kwa ile ndege ni swala ambalo ni zito mno kwa mtu kama Kamau kulifahamu”Aliongea Linda na kumfanya Mheshimiwa Jeremy awaze kidogo.
“Nadhani swala hili tuangalie DS ya Tanzania watalitolea vipi maamuzi swala la Blandina, Endelea kufuatilia ni sababu gani Roma alikuwepo kwenye kituo cha Son And Daughter Orphanage”
“Sawa Mheshimiwa” Aliongea Linda na kisha akatoka.
DS ni kirefu cha maneno ya ‘Deep State’ au kwa Kiswahili unaweza kusema Serikali ya ndani,DS ni kikundi cha watu ndani ya nchi ambacho kinakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi ya kisela katika Nyanja zote , hawa DS ni rahisi kusema wanauwezo wa kuamua ndani ya taifa raisi awe nani kutokana na nguvu yao na mara nyingi wanafanya kazi kwa siri sana.
******
Edna alijikuta akijishangaa kulala muda mrefu mno kuliko isivyokuwa kawaida , saa saba na nusu mrembo huyu alishituka kutoka usingizini na kuanza kukumbuka ni muda gani alilala maana alikuwa na nguvo alizovaa jana yake.
“Ni Roma yule Shetani Sijui alinifanyia nini?”Mrembo huyu alionekana kukumbuka tukio lililotokea , alikumbuka namna ambavyo Roma alimkumbatia kwa nyuma na kwanzia hapo hakuelewa nini kiliendelea.
Edna alijinyanyua kivivu kitandani na kuangalia saa kupitia simu na hapa ndipo aliposhituka , hakuamini ilikuwa ni saa saba mchana , kwani licha ya kwamba alijua amelala muda mrefu , lakini hakujua kuwa siku ilikuwa ikikaribia kuisha , alikumbuka simu yake nyingine iliokuwa kwenye mkoba wake na kuitoa haraka na kuangalia ni nani kapiga na kweli kulikuwa na ‘missed calls’ nane kutoka kwa Monica lakini pia kulikuwa na ujumbe wa maandishi.
“Madam muwekezaji Yan Buwen kutoka China keshafika nchini , Nakupigia hupatikani nimesogeza ratiba ya wewe kuonana nae saa moja za leo jioni”
Ulikuwa ujumbe kutoka kwenye simu ya Edna hakukuwa na jumbe nyingine za muhimu Zaidi na kumfanya mwanamke huyu kuvuta pumzi ya afadhali.
“Miss umeamka?”Ilikuwa ni sauti ya Bi Wema aliekuwa akiandaa chakula mezani na kwa harufu tu ya chakula ilimfanya Edna kuhisi njaa.
“Nimelala sana Bi Wema leo , kwanini hamkuniamsha?”
“Roma alituambia tusikuamshe mpaka utakapo amka mwenyewe na sisi tuliona ni sawa maana ulifanya kazi sana wiki hii pasipo kupumzika”Aliongea Bi Wema na Edna hakubadili muonekano wake , ila alikuwa akiwazia ni nini Roma alimfanya mpaka kulala muda mrefu, alijua Roma sio mtu wa kawaida lakini hakudhania kama anaweza kumfanya pia mtu kulala muda mrefu.
“Miss Mbona haukuniambia kama Yezi amepatikana?”Aliongea Bi Wema na kumfanya Sophia ajiulize Yezi ni nani.
“Ndio Bi Wema nilisahau , mambo yalikuwa mengi ,Roma ndio kakuambia?”
“Ndio kaniambia leo asubuhi na kampeleka kituoni kuonana na Mama Issa”Edna alishangaa kwasababu hakuwa na hio taarifa.
******
Upande mwingine ndani ya hoteli ya Serena alionekana bwana mmoja hivi wa Kichina aliekuwa amevalia taulo la rangi nyeupe ndani ya hoteli hii akiwa ameshikilia glasi ya wine huku akiwa amevalia miwani yake , kwa kumuangalia tu bwana huyu utafahamu umri wake haukua ukizidi miaka Arobaini.
Wakati bwana huyu akiangalia mandhari ya nje yajiji hili , simu yake ya chumba iliita mfululizo na kumfanya ageuke na kuisogelea na kisha aliipokea.
“Mr Yan Una mgeni eneo la mapokezi anafahamika kwa jina la Scorpion”Aliongea mwanadada wa mapokezi na kumfanya Bwana huyu atabasamu na kisha alijibu kwa Kingereza kama amruhusu aje.
Baada ya kama dakika tano aliingia mlinzi wa kike wa mheshimiwa Kigombola aliekuwa akifahamika kwa jina la Scorpion , alikuwa amevalia mavazi yake ya suti nyeusi akiwa na miwani ya jua , licha ya mwanadada huyu kuwa na sura ngumu lakini leo hii alipendeza.
“Karibu sana Sciorpion , ni muda mrefu hatujawahi kuonana tokea uje Tanzania”Aliongea Yan Buwen huku akitabasamu lakini Scorpion hakutoa aina yoyote ya tabasamu mlinzi huyu alikuwa kauzu hatari.
“Umekuja Tanzania kufanya nini Yan Buwen?”Aliuiza Scorpion kwa sauti ya kibabe.
“Nadhani unajua kwanini nipo hapa Tanzania mpaka muda huu”
“Kama umekuja kwa ajili ya jiwe la Kimungu sahau , washalichukua Yamata”
“Hahaha..Scorpion Baada ya kuja Tanzania naona uwezo wako wa akili umeshuka kwa Zaidi ya asilimia hamsini , Watanzania wamekudumaza kama walivyodumaa”Aliongea Yan Buwen kwa kejeli.
“Unamaanisha nini?”
“Yamata wamepewa jiwe feki , hivi unamchukuliaje Hades wewe, ndio maana nakuambia uwezo wako umedumaa , ulivyokuwa chini yangu haukuwa hivyo Scorpion”Aliongea Yan Buwen na kumfanya Scorpion ashangae.
“Una uhakika ni jiwe feki?”
“Ndio maana nipo hapa Tanzania, The Don anataka hilo jiwe kwa namna yoyote na niimekuita tuonane ili unisaidie kuandaa mpango wa kupata jiwe hilo”.
“Mpango Gani unapanga ili hali unajua hatuna uwezo wa kupambana na Hades”
“Hatuna haja ya kupambana na Hades ,The Doni mwenyewe atapambana nae”Aliongea Yan Buwen kwa tabasamu na alionekana kuwa na shauku kubwa.
“Sasa kama The Don ndio anakwenda kupambana na Hades tunaandaa mpango wa nini?”Aliuliza Scorpion na Yan Buwen alikunywa kidogo kinywaji chake halafu akatabasamu.
“Yapo mambo mengi haufahamu Scorpion na siku sio nyingi utakuja kugundua angalau nusu yake , ujio wangu hapa Tanzania ni kutaka kuhakikisha kama jiwe hilo lipo hapa au Hades kalificha nje ya Tanzania , hio ndio sababu ya mimi kufika hapa Tanzania , lakini pia nadhani mpaka sasa haujafahamu kwanini The Don alikupa maagizo kukaa karibu na mheshimiwa Kigombola?”Scorpion alitngisha kichwa kuonyesha hajui.
“Okey ukikamilisha kazi nitakayokupa siku ya leo, nitakuambia kila kitu”Aliongea na kisha akanyanyuka na kutoa picha na kumpatia Scorpion”
“Nahitaji kusikia kifo cha huyo mtu kabla ya kesho asubuhi”Aliongea Yan buwen na Scorpion aliangalia hio picha na kisha akavuta pumzi.
“Kwahio hili ni dili , nakamilisha kifo cha huyo mtu na utaniambia kwanini The Don kanileta Tanzania”.
“Hahaha…Scorpion , hupaswi kuwa na wasiwasi licha ya kwamba naonekana kama mtu ambaye siaminiki , lakini kuhusu hilo nitakutimizia , Ndani ya dunia hii ni mimi pekee ambaye namfahamu The Don kwa kumuona Hata raisi wa Marekani anamsikia tu … hahahaha”
ITAENDELEA MONDAY.
Kaka hujaniunga kwenye group kaka.NICHEKI WATSAPP 0687151346 KUOATA UTARATIBU WA MWENDELEZO , SISI HUKU WATSAPP TUPO SEHEMU YA 170
Tupomnaosema niweke mwendelezo wikiend hii mjitokeze
tupomnaosema niweke mwendelezo wikiend hii mjitokeze