Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Hivyo ni vipande vya mbele boss kuanzia 180 mpaka 200 hizo flash back zipo
Pia mbn kama naona huyu Denisi yupo mara mbili yaaan jina la Roma la zamani na pia mtoto wa senga alie China ni Sawa au kuna error. Kila ukimtaja Denisi mwingine nakua napoteza connection
 
Pia mbn kama naona huyu Denisi yupo mara mbili yaaan jina la Roma la zamani na pia mtoto wa senga alie China ni Sawa au kuna error. Kila ukimtaja Denisi mwingine nakua napoteza connection
Kwa maelezo Denis(Roma) ni mtoto wa senga na yule first lady wa Kenya
 
Sasa katikati ya sherehe kuna Denisi mwingine ambae ni mtoto wa senga pia yupo China huko.
Dogo lake na Roma kapewa hilo jina kumuenzi mwanae aliyepotea na mama yake kwenye Ile ndege
 
Hivi ndio mpaka jumatano? Mbina mbali sana, hii ngoma ilitakiwa daily
 
Okey leo baadae nitaweka 4 episodes , alhamisi 4 episodes jumamosi 4 episode, ndio ratiba hio mpaka tuhitimishe

Ukitaka kusoma kwa kupitia watsapp wewe nicheki 0687151446
Umesema leo eee ?
 
SEHEMU YA 163

Magdalena hakuamini kama mtu aliekuwa mbele yake ni Roma , aliona ni kama miujiza na kujiuliza kwa wakati mmoja ni muda gani kafika ndani ya hili eneo , kwani ni sekunde chache mbele alionekana kukata tamaa kabisa , lakini sasa hivi tu anatokea mbele yake.

“Roma unafanya nini hapa?”Aliongea Magdalena huku akijinyanyua kivivu

“Unauliza niko hapa ulifikiri nimependa , Nyie kama jeshi la Tanzania mnapata faida gani kuingilia mambo ya Vaticann na Bunge la Kiza?”

“Sisi ni wanajeshi na tulipewa oda kutoka juu na ndio maana tuko hapa , lakini hata hivyo Bunge la Kiza ni mashetani”Aliongea Magdalena kwa sauti ndogo huku akisimama wima kabisa na Roma alimwangalia na kisha kutabasamu.

“Nafikiri hata wakubwa zako hawaelewi uhatari uliopo juu ya hawa watu wanaojiita ‘Blood Race’ inabidi nikitoka hapa niwaelezee”Aliongea Roma akiwa hana hata wasiwasi kabisa na muda huu Watu wa Vatican pamoja na na wa ‘Blood Race’ walikuwa wakimwangalia Roma kwa mshangao , unajua licha ya kwamba Lilith alimwita kama Hades , ila kwa mwonekano wa Roma hawakuwa wakiamini kabisa , kwani licha ya kuwa na taarifa zinazomuhusu Hades , hawakuwahi kumuona moja kwa moja.

“Kwanini umeniokoa?”Aliuliza Swali Mage akimwangalia Roma usoni , na Roma aliona swali hilo ni la kipuuzi.

“Kwahio ulitaka nikuache ufe , licha ya kwamba sikupenda kuingilia kinachoendelea hapa , ila nisingeweza kuona Rafiki wa mke wangu akiuwawa mbele ya macho yangu na isitoshe Taila linawezekana bado linakuhitaji , hata hivyo unabahati sana , ingekuwa ni miaka kadhaa nyuma nisingejihangaisha , ila kwakua sasa hivi na mimi ninafamilia lazima angalau nifanye jambo la kibinadamu”Aliongea Roma bila ya kuonyesha wasiwasi kabisa.

Magdalena uso wake ulionekana kukosa tumaini , ilionekana mrembo huyu alikuwa akitegemea jibu zuri kwa Roma, lakini sababu zilziokuwa zimetolewa zilikuwa hazijamridhisha , alijikuta akiangalia upande wa kulia kuwaangalia wanajeshi wake aliokuwa amefika ndano ndani ya hilo eneo na upande wake wa kulia alimuona Jumbe akiwa chini huku akionekana kujeruhiwa vibaya sana.

Mpaka kufikia muda huo Vatican walionekana kuzidiwa nguvu , lakini licha ya hivyo hawakuonekana kukata tamaa kabisa ,lakini pia upande wa Dark Parliament walionekana hawakuwa tayari kuwaacha Vatican , walikuwa na mpango wa kuwamaliza na kisha ndio waondoke na ‘Holy Grail’ , lakini sasa baada ya ujio wa Roma hapa ndani, pande zote mbili walikuwa wakiwaza ni upande gani Hades atasimama na waliamini upande wowote Hades atakao simama ndio utakaoshinda.

Magdalena sijui alimfanyia nini kwa Jumbe , lakini bwana huyo alionekana kupata nguvu na maumivu kupungua na sasa alikuwa amesimama na akimwangalia Roma.

“Bro bora hata umekuja kutusaidia maana tungekufa”Aliongea Jumbe huku akimwangalia Roma.

“Sijaja kusaidia mtu yoyote hapa na nikueleze tu sipo upande wa mtu yoyote , mimi nimekuja kuleta amani, usiongee maneno ya kipuuzi ukaniuzi maana naweza kukuua”Aliongea Roma kwa sauti ya kuwa siriasi kabisa na kumfanya Jumbe kunywea kwani ni kama alikuwa akifokewa.

Garbiel licha ya kupigana muda mrefu , hakuwa amedhurika sana , kwani alikuwa na baadhi tu ya majeraha na mikwaruzo kwenye mwili wake.

“Your Majesty’s ability is far beyond us. Are you possibly doing this for the Holy Grail as well?”(Mfalme uwezo wako ni mkubwa kuliko sisi , Kuna uwezekano wa wewe pia kupambana kwa ajili ya Holy Grail?”Aliongea Gabriel huku akimwangalia Roma aliekuwa kwenye mavazi ya suti kama alivyokuwa ametoka nyumbani.

“I can’t even confirm the authenticity of your Holy Grail, why would I be interested in it then? Furthermore, the term ‘eternity’ doesn’t hold any major meanings for me”

“Kwanza sina uthibitisho wowote wa kitu mnachopigania kuwa halali , kwanini niwe na matamanio nacho , Zaidi ya yote , kwangu neno ‘Umilele” halina maana kwangu”

“Sasa mfalme kama huna haja na ‘Holy Grail’ kwanini unaingilia?”Aliuliza Garbriel.

“Mimi ninachotaka ni amani itawale ndani ya hili eneo , mpaka sasa mmeua wanajeshi wengi wa Taifa ambalo ninaishi , na wanajeshi hawa ndio wanalinda usalama wa raia wa nchi hii, lakini hata hivyo mimi sina uadui wowote na Vatican pamoja na Dark Parliament , hivyo sitotaka kuona mapambano yanaendelea hapa , ninachowashauri muondoke mara moja na kilichotkea hapa kiishie hapa hapa”Aliongea Roma kwa msisitizo lakini kwa upande wa Gabriel hakuwa tayari , mpaka muda huo wanajeshi wake karibia wote walikuwa washapoteza Maisha na pili Holy Grail haikuwa kwenye mikono yake na aliona ni upuzi kuondoka pasipo kulipiza damu za wanajeshi wake.

“Mfalme mpaka sasa wanajeshi wetu karibia wote washakufa tayari sio haki kwa sisi kuondoka mikono mitupu”

“Gabriel sidhani kama wanajeshi wako wote wangekuwepo hai , ungekubali kuondoka pasipo kuwa na Holy Grail?”Aliongea Moses kwa kejeli.

“Since you guys aren’t willing to give up the stupid Holy Grail, let’s do it this way, hand it over to me and I’ll destroy it on the spot. It’ll be fair after that.”

“Nyie watu kwakua hakuna mmoja wenu ambaye yupo tayari kuachia hiko kikombe cha kipuuzi, tufanye hivi nipeni nikiharibu hapa hapa na itakuwa ni haki kwa kila upande”Aliongea Hades

“No Way”Aliongea Gabriel kupinga pendekezo la Roma , lakini Roma Hakujali.

“Do you guys think I’m here to listen to your opinions? Don’t irritate me anymore. When I take action myself, none of you will be benefited.”

“Mnafikiria nipo hapa kwa ajili ya kusikiliza maoni yenu , achene kunifanya nikasirike , nikiamua kuongea kwa vitendo hapa hakuna atakae faidika”Aliongea Roma kwa mkwala na kufanya pande zote kuwa na wasiwasi. Kwenye nyuso zao.

“Your Majesty mustn’t look down on us too much. Although Your Majesty is much stronger than most, I don’t think we’re free to be killed easily,”Aliongea Archimonde akimaanisha kwamba Roma asiwadharau kwani hawawezi kufa kizembe licha ya kwamba yeye ana nguvu.

Mpaka hapa Roma aliona kiburi kila upande na hakuona mtu yoyote ambaye alikuwa tayari kwa ajili ya kuachia hiko kikombe lakini pia hakutaka kukaa hapo msituni kwa muda mrefu kwani aliamini akichelewa Edna atamuacha na akaenda nyumbani peke yake , hivyo aliona anahitajika kukamilisha kila kitu na kuondoka zake.

“Kwa sababu hamtaki kutoa hiko kikombe kwa hiari yenu , basi nitamsachi mmoja mmoja na kukichukua kwa nguvu”Aliongea Roma na palepale akapotea alipokuwa amesimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Charlie na Charlie alitaka kumkwepa lakini Roma alikuwa na spidi kuliko yeye na alijikuta akipapaswa kwa spidi ya ajabu na Roma aliona Charlie hakuwa na hiko kukombe na alichokifanya ni kumtupia mbali Charlie kama mpira na kufanya watu wote kushangaa , kwani licha ya Charlie kuwa mwanamke lakini alikuwa na mwili mkubwa , walishngazwa na uwezo na nguvu za Roma kwa wakati mmoja.

Roma baada ya kukikosa kwa Charlie alimwangalia Moses aliekuwa mita kadhaa kutokea aliposimama na kumsogelea , lakini sasa ile anafika mahali aliposimaa Moses , hakuwepo , alikuwa amepotea kama jini na muda huo huo Nguvu kubwa sana ilimsukuma Roma na kumrushia nyuma na kujikuta akichuchumaa chini na kugusa Ardhi.

“Ni nguvu gani hii…!!!”Roma alijikuta akiwa kwenye mshangao , kwani hakuelewa ni nini kimepotea kwa muda huo kwani alihisi nguvu kubwa kuliko ya kwake.

“Moses…!!!!”Archimonde na wenzake wote walijikuta wakiita kwa nguvu baada ya kutokumuona Moses , licha ya kwamba walishangazwa na Roma kupotea na kuibuka kwa wakati mmoja , lakini swala la Moses kupotea liliwachanganya kwani walikuwa wakijua kabisa kuwa Moses hakuwa na uwezo huo.

Muda ule ule baada ya kupotea kwa Moses , wakati kila mtu akiwa kwenye mshangao , mara Ghafla mwanga hafifu kama wa moto ulitokea kutoka juu na hapo hapo Roma aliweza kushuhudia’ kikombe kikishuka kutoka juu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba , kikombe hiki hakikuwa kimeshikiliwa na mtu yoyoyte , ila kilikuwa kimesimama hewani , ilikuwa ni jambo la kushangaza mno kwa Roma na kwa kila mtu.

Roma alikuwa na uwezo wa ajabu mno , lakini likija swala la kugandisha kitu hewani hakuwa akiweza kwani hakuwa na uwezo wa kutumia ‘Space Laws’.

Lakini sasa mpaka muda huo alijiuliza Mioses kapotelea wapi , kwani yeye ndio aliekuwa na kile kikombe , lakini ajabu ni kwamba kikombe kilishuka chenyewe tena kwa namna ya ajabu huku bila ya Moses kuonekana tena.

Kila mmoja alishangazwa na jambo hilo , Lilith na yeye alikuwa kwenye mshangao , licha ya kwamba ‘Dark Parliament’ walikuwa ni watu wa kushuhudia baadhi ya matukio ya kutisha katika maisha yao , lakini tukio kama hilo lilikuwa la aina yake , kwani hakukua na aina yoyote ile ya nguvu ya ziada iliotokea kuashiria labda kama kuna mtu mwingine ameongezeka na hata Roma mwenyewe ambaye alikuwa na uwezo wa hali ya juu , hakuweza kutambua chanzo cha nguvu kubwa iliotokea.

Unachotakiwa kujua ni kwamba ‘Dark Parliament’Walikuwa wakihitaji hiko kikombe kutokana na kuamini kwamba kama watatumia kikombe hiko kitakatifu kunywea maji , basi wataweza kuishia Maisha marefu pasipo kufa na na hapa ndio maana Roma akasema kwamba yeye neno ‘Eternity’ kwake ni upuuzi na halina uhalisia wowote kama walivyokuwa wakiamini.

Roma baada ya kutoka kwenye mshangao , alisimama na kuchukua kikombe ambacho kilikuwa hewani na kukishika kwenye mikono yake bila wasiwasi wowote hukua akianza kukichunguza , ni kikombe cha zamani kama kilivyokuwa kikionyeshwa masaa kadhaa nyuma ndani ya ukumbi ule wa Mlimani City lakini hapa kwakua kilikuwa karibu , kilionekana kuwa na maandishi ambayo yeye mwenyewe licha ya kujifunza ligha nyingi hakuweza kutafsiri maana ya maandisihi hayo yaliokuwa yameandikwa kuzunguka sehemu ya juu.

“Umemuua Moses..!!!?”Aliongea Archimonde kwa hasira huku akimwangalia Hades , yeye hakuelewa kabisa hali iliokuwa imetokea na aliamini kabisa , aliekuwa amehusika na kifo cha Moses alikuwa ni Roma na ndio maana akamuuliza hivyo , lakini Roma wala hakugutushwa wala kushangazwa na Swali la Archimode.

“Sijahusika na kifo chake mimi , kaa ukilijua hivyo , lakini kilichotokea hapa pia sina maelezo nacho, na sasa kile mlichokuwa mkipigania kipo kwenye mikono yangu.”Aliongea Roma huku akiangalia kile kikombe , yaani kwake hakikuwa na maana kubwa kama watu waliokuwa wamezunguka walivyokwa wakikiangalia , yeye aliona kikombe hiko cha kawiada sana na hakukipa uzito wa aina yoyote ile.

Lilith alikuwa akikiangalia kikombe hiko kwa matamanio makubwa sana , alitamani kitue kwenye mikono yake na kisha apotee ndani ya hilo eneo , aliakuwa akiamini kama atakuwa na hiko kikombe basi anakwenda kuishi milele.
 
SEHEMU YA 164.

Roma hakuwa na wasiwasi kabisa na watu waliokuwa mbele yake , kwanza baada ya kuangalia kikombe hiko ambacho kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu alianza kukirusha rusha juu kama kamchezo.

“Mfalme Unapanga kufanya nini na hiko kikombe?”

“Mimi kwangu hakina thamani yoyyote na sina mpango nacho , lakini pia sitaki kuona mkiendelea kupigania juu ya hiki kitu , hivyo nitakiharibu mbele yenu ili kila mtu akose na aridhike”Aliongea Roma na hakusubiria jibu wala nini , alikishika kwa mkono mmoja kama bile ameshika yai na palepale ni kama kimesagwa sagwa , kwani kilichoonekana ni unga unga ulioonekana kwenye mikono yake na kumwagia chini na kufanya watu wote watoea macho , hawakuamini kitu cha thamani kubwa kama hivyo , Hades alikuwa amekiharibu kwa mkono mmoja , kitu ambacho kiliwafanya kutoka kwenye mataifa yao kuja mpaka Tanzania kwa ajili ya kukipata kwa gharama yoyote ile , sio hao wazungu tu walioshangaa lakini hata Magdalena ambaye muda wote alikuwa kimya alikuwa katika hali ya mshangao , hakuamini Roma alikuwa ameharibu , licha ya kwamba hakuwa na maelezo mengi juu ya Kikombe hiko , Zaidi ya kupewa maagizi kutoka kwa wakubwa zake.

“Unapata wapi ujasiri wa kuharibu ‘Holy Grail’, haya ni matusi kwa Mungu wetu na unmeukosea moja kwa moja uongozi wa Vatican”Aliongea Thomasi ambaye alikuwa kwenye maumivu baada ya kujeruhiwa , lakini baada ya kitendo cha Roma kuharibu kile kikombe swala hilo lilimgusa mno.

Lakini upande wa Roma wala hakujali kabisa , na alijipangusa mikono yake kama mtu anaejifuta na kisha akamwangalia Thomasi.

“Kama kweli hiki mnachokiita kikombe kitakatifu ni chenyewe na kimebeba nguvu ya Kimungu siamini kama ningeweza kukiharibu na mkono mmoja”Aliongea Roma.

“Holy Grail nguvu yake haipo kwenye madini yaliotengenezwa nacho , bali ni juu ya maana halisi iliopo nyuma yake ndani ya dini yetu”Aliongea Thimasi kwa hasira.

“Kwahio unatakaje , wewe amini unachoamini , ila unatakiwa kuelewa kwamba nishaharibu kikombe chenu na siwezi kukirudisha , kama mtaamua kuondoka ni juu yenu na kama mnataka kupigana na mimi , nipo tayari na niwatahadharishe tu , sijigambi ila nitahakikisha kama mtataka kupambana na mimi nitahakikisha mnakufa wote hapa”Aliongea Roma kwa msisititzo na kila mmoja alionekana kuamini maneno ya Roma , ukweli mpaka muda huo hawakuelewa nini kimemtokea Moses na waliogopa na wao pia kupotea kama mwenzao kwa kuambana na Roma

Vaticana walikuwa na hasira Zaidi baada ya kupoteza hiko kikombe , kwani kilikuwa ni cha kwao , lakini kwa upande wa Bunge la Kiza walikuwa hawajapteza kitu , wao walikuwa wakitaka kikombe hiko kwa ajili ya kukipeleka kwenye kambi yao kikawe kama alama ya kihistoria pekee na kutumia kuwekea damu ya Kafara.

Archimonde alimwangalia Lilith kuona ni hatua gani ataamua , alijiambia kama Lilith ataamua kupigana hata yeye atapigana, Lilith aliekuwa amesimama upande wa kushoto ghafla macho yake yaliokuwa meupe kiasi cha kufanya kiini cha macho kupotea yalirudi katika hali ya kawaida na kuwafanya hata baadhi ya wanajeshi wake waliokuwa katika mabadiliko kurudi katika hali zao za kawaida na kuwa kama binadamu wa kawaida.

“Mfalme Pluto naomba niombe msamaha kwa hali iliotokea leo na tutaondoka ndani ya hili Taifa na kurudi Ulaya”Aliongea Lilith kwa sauti yake nyororo.

“Lilith nikutakie safari njema”Aliongea Roma lakini Lilith ni kama hakuwa ameridhika na alitoka alipokuwa amesimama na kumsogelea Roma na kisha akamuinamia sikioni na alionekana kuna jambo ambalo alikuwa akimwambia na kumfanya Roma atabasamu kifedhuli na Lilith aliinua macho yake na kumwangalia Usoni huku akimkonyeza.

“Kama ndio unachotaka, basi sinabudi kukupatia unachotaka”Aliongea Roma na pale pale Lilith alimsogelea Roma usoni na ajabu walianza kupiga ‘French kiss’ na kuwafanya watu wote ndani ya hili eneo kushangazwa na kitendo hiko na , ni kama sasa walikuwa wameelewa ni nini Lilith aliongea na Roma baada ya kumnnogng`oneza.

Magdalena alijjikuta akipandwa na jaziba sana kwa tukio hilo , mpaka mwenyewe akajishangaa kwanini alikuwa na hasira , alijiuliza Roma anapata wapi ujasiri wa kumbusu huyo ‘Vampire’ , lakini pia wkati huo huo alikuwa akijiuliza ni kwannini alikuwa akipatwa na hasira wakati hakuwa na mahusiano yoyote na Roma.

“Eeh!...Ndio lazima nikamwambie Edna upuuzi wake ambao anaofanya hapa”Aliwaza Magdalena kwenye kichwa chake huku akigeuza shingo yake na kuangalia pembeni , hakupenda kabisa kushudia kile kilichokuwa kikiendelea.

“Okey! Lilith chukua watu wako muondoke , nishakamilisha ombi lako”Aliongea Roma baada ya kuachiana na Lilith na muda huo huo Lilith aliwapa ishara watu wake na wakapotea kimiujiza ndani ya hilo eneo akiwemo Archimonde na wenzake. Na waliobakia ni wale wa upande wa Wavatican.

“Vipi na nyie mnataka tuzipige au mnaondoka?”Aliuliza Roma na kuwageukia Gabriel na wenzake.

“Although I really want to try battling, it’s not the right time currently. We’ll leave Tanzania , but Your Majesty, please remember that you’ve destroyed our Holy Grail today.”Aliongea Gabrieli akionyesha kwamba hakuwa tayari kwa kupigana , lakini bado alikuwa na hasira juu ya Roma kuharibu Kikombe chao kitakatifu , ila hawakutaka kuleta fujo ,Gabriel aliwapa ishara watu wake na wakageuka na kuanza kupotelea gizani na waliokuwa wamebaki muda huo alikuwa ni Magdalena na Jumbe peke yao.

“Magdalena tuondoke”Aliongea Jumbe , lakini Magdalena hakumjali kabisa kwani muda wote alikuwa amemuangalia Roma.

“Jumbe unaweza kuondoka , nitaita wanajeshi kutoka Ruvu waje kusafisha hili eneo kuondoa Ushahidi”

“Hapana Magdalena siwezi kukuacha na huyu mtu hatari , anaweza akakudhuru”Aliongea Jumbe na kumfanya Magdaleana amwangalia kwa macho ya kumpuuza , alijiambia Jumbe hakuwa akifikiria vizuri , yaani mtu amuokoe halafu amdhuru.

“Magdalena nadhanni unapaswa kuondoka na mwenzako”Aliongea Roma .

“Hapana nina maswali yangu nataka kuuliza ndio niondoke”

“Maswali gani?”

“Nataka maelezo juu ya hawa watu wa ‘Dark Parliament’ umesema hatukua tukiwafahamu vizuri na utatuelekeza”Aliongea Magdalena na kumfanya Roma akumbuke kumbe alikwa amewaahidi kuwaleza juu ya hao watu wa kabila la Wanywa damu kutoka Ulaya.

“Kuhusu hilo ni litachukua muda kukujibu kwa sasa kwani lazima nikuelezee historia nzima , ila nikuambie tu Dark Parliament ni Watu jamii ya Vampire ambao walidhaniwa kupotea miaka mingi iliopita baada ya kutokomezwa na utawala wa Kirumi chini ya kiongozi mkuu wa kanisa yaani Papa , licha ya kwamba miaka hio Vampire ni jamii iliokuwa na nguvu ndani ya bala la Ulaya lakini Jeshi la Kirumi kwa wingi wao liliwashinda na wengine kukimbilia mafichoni na miaka kadhaa mbele wakaanzisha taasisi zao za siri za kiimani huku wakiwashawishi baadhi ya watumishi wa Mungu ndani ya Kanisa na kuwa upande wao”Aliongea Roma na kumfanya Magdalena kushangaa.

“Lakini licha ya hivyo Kundi hili halikuwa salama hata kidogo, kutokana na kuwindwa sana na hapo ndipo walipoingia makubaliano kwa kusaini mkataba wa makubaliano ambao ulikuwa ukiwaruhusu kuendelea kuishi pasipo kuudhihirisha uwepo wao duniani”

“Nimesikia Taasisi nyingi za siri ikiwemo hii ya Camarilla na SAVATH unaweza kuzungumzia juu ya hilo”

“Iko hivi Magdalena baada ya kusainni huo mkataba wa makubaliano waliishi kwa kutengeneza jamii zao za siri ikiwemo hio Camarilla pamoja na SAVATH na walitumia taasisi hizi kuwashawishi binadamu wa kawaida kujiunga nao”

“Kwahio Mkataba ulisainiwa kati ya watu hawa wa jamii ya Vampire na serikali gani?”

“Nishasema watu waliokuwa wakiwawinda enzi hizo ni Warumi , hivyo ni rahisi kusema kuwa waliosaini nao mkataba wa makubaliano ni Warumi pia, Magdalena ninachokuwambia hapa unatakiwa uelewe kuwa mpaka sasa hizi taasisi kama vile Camarilla ni taasisi kubwa sana duniani na ina wanachama wengi na moja ya ibada zao ni kutoa kafara ya damu, kwa kukurahisishia tu Archimonde na wenzake wapo kwenye kundi la SAVATH kundi hili wengi wao ni wale wanaotaka kutambulika uwepo wao ndani ya dunia , lakini wanakosa nguvu kutokana na kuwa wachache , ila kundi la Camarilla ndio wengi Zaidi duniani na kundi lanye nguvu na wanaoishi kwa siri sana huku wakiwa na ushawishi mkubwa sana kwenye serikali nyingi duniani mpaka kwenye Imani za kidini na kuhusu Holy Grail kuna siri kubwa sana ambayo ipo nyuma yake ambayo makundi haya yote wanaitaka hio siri ili kuweza kujiongezea nguvu Zaidi, na nimesikitishwa san ana Jeshi kutumika katika kuingilia haya mambo , kwani ni maswala ambayo hayakuwa yakilihusu kabisa na walitakiwa kukaa mbali , kwani mapambano ya hii jamii na Vaticani ni mapambano ya Nur una Giza ambayo hayakuwahi kukoma”

Aliongea Roma na kumfanya Magdalena, aamini maneno ya Roma na mpaka kufikia hatua hio , aliona wanajeshi wake wamekufa vifo vya bure kabisa na alijihisi hasira kwenye macho yake , kwani ukweli ni kwamba Vatican ndio walioomba msaada wa kuwasaidia kupata hiko kikombe huku wakiwashawishi kwa kuwaambia kuwa ni kitu hatari sana kama kitaingia kwa watu wabaya na ndio maana misheni ya kupata hiko kikombe akapewa Magdalena na kikosi chote cha Wachawi na mwishowe wakajikuta wanapoteza wanajeshi pasipo ya kuwa na sababu yoyote kwani mapambano hayo ya nguvu za kiimani hazikuwahusu.

“Mimi naondoka , nataka nimuwahi mke wangu kama hajarudi nyumbani niondoke nae”

“Okey nitamueleza Kamanda , siku nyingine tusiwe tunajiingiza kwenye maswala kama haya”Aliongea Magdalena.

“Kama umenielewa nadhani ni muda wangu sasa wa kuondoka”Lakini Magdalena akamzuia.

“Vipi kuhusu Holy Grail, ni kweli inaweza kumfanya mtu kuishi milele?”

“Sijui chochote juu ya tetesi hizo , ila mpaka sasa swala la kupotea kwa Moses ni swala ambalo linachanganya , lakini lenye uhatari Ambao unaweza usielewe hata nikikuambia hapa , Fanya kumuelezea tu kwa kifupi mkuu wako wa kazi juu ya kilichotokea leo hii”Aliongea Roma , lakini kwa upande wa Magdalena alionekana kutoridhika na aliona Roma hakuwa akitaka kujibu maswali yake makusudi kabisa.

“Vipi kuhusu Lilith .. kwanini ukafanya vile? Huogopi kama nitamwambia Mkeo kilichotokea hapa na muda mfupi uliopita mligombana kwa maswala haya haya”Aliuliza Magdalena huku akionekana kusita sita.

“Sikia Magdalena usije ukasema , kilichotokea hakikuwa na maana kubwa kati yangu na Lilith na hata hivyo sijawahi kupigana mabusu na Vampire”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu lake la Kifedhuli na kumfanya Magdalena abetue midomo na kuanza kuondoka na dakika moja zilikuwa nyingi kwa Magdalena kwani alipotea kabisa na Roma akabaki akiwa amesimama mwenyewe.

Upande wa huku mjini Edna hakuwa ameondoka , alikuwa amesimama eneo la maegesho akiendelea kumsubiria Roma , Mrembo huyu alikuwa na wasiwasi sana kwani ilikuwa ni Zaidi ya lisaa limepita pasipo kumuona Roma.

“Edna inabidi uelekee nyumbani Roma atarudi mwenyewe”Aliongea Mage huku akimwangalia Edna aliekuwa amesimama akizungusha zungusha shingo.

“Hapana nitamsubiri Mage , wewe unaweza kutangulia”Aliongea Edna.

Mage hata yeye mwenyewe alikuwa kwenye wasiwasi vilevile, ukweli licha ya kuja na dada yake kwenye hilo tukio , ila hakuwa akielewa kile kilichokuwa kikiendelea na hara pale Magdalena alivyoanza kushindana bei na Lilith hakuwa akijua ni nini kinaendelea na alikuwa kwenye mshangao kama watu wengine tu, lakini sasa kilichomshangaza Zaidi ni baada ya kupotea kwa Magdalena na kumuacha ndani ya eneo hilo pasipo kuonekana kwa zaidi ya lisaa limoja.

Alikuwa na wasiwasi licha ya kwamba alikuwa akijua dada yake hawezi kudhurika kutokana na kuwa mwanajeshi , lakini kilichomchanganya Zaidi ni kupotea pia kwa Roma , mrembo huyu hakujua ni nini kinaendelea , licha ya kwamba alikuwa polisi , lakini tukio lililotokea dakika chache zilizopita lilikuwa ni la kushangaza kwani hakuna mtuhumiwa yoyote aliekuwa amepatikana mpaka muda huo na hata polisi waliofika kuchunguza hawakuwa na majibu ya kueleweka licha ya kutoa taarifa ya hasara kubwa ambayo Mheshimiwa Kigombola alikuwa ameipara , baada ya vitu vingi kuibiwa.

“Wife hujaondoka bado , nilikuambia ukiona nachelewa uondoke”Aliongea Roma aliesimama nyuma ya Edna na Mage ambao walikuwa wamejiegemeza kwenye gari.
 
SEHEMU YA 165.

Edna alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa, alimkagua kwanzia chini mpaka juu na kuona hakuwa na tofauti yoyote na alijiambia moyoni huenda alikuwa kwenye mambo yake na yeye amesimama hapo muda wote kumsubiri.

“Ulitaka niondoke ili ubakie huku usiku mzima kama kawaida yako?”Aliuliza Edna kwa hasira

“Wife ndio maana nikakuambia utangulie , mimi ningekuja hata na usafiri wa kukodi”Aliongea Roma lakini Edna hakujibu kitu Zaidi ya kuingia kwenye gari na kuufunga kwa nguvu.

“Umeenda kupuyanga huko ndio unarudi , unamuacha mkeo anakusuburi muda wote bila taarifa”Aliongea Mage na kisha akageuka na kuanza kutembea kuondoka eneo hilo na kumfanya Roma amwangalie kwa sekunde na kisha akasogelea gari na kuingia siti ya nyuma. Na dereva aliewaleta aliwasha gari na kuingia barabarani kuelekea nymbani.

Ni siku nyingine , siku ya asubuhi Roma na Edna walikuwa mezani wakijipatia kifungua kinywa kwa ajili ya kuelekea kazini, Sophia na Bi Wema hawakuwepo mezani na hio ni kutokana na Sophia kuwa bado kalala na Bi Wema na yeye alikuwa na majukumu yake.

“Unakumbuka ahadi yako kuhusu kusimamia kampuni?”Aliuliza Edna ambaye alikuwa akinywa chai kwa mapozi ya kike na kumwangalia Roma aiekuwa bize akifakamia kipande cha mkate.

“Nakumbuka Wife, unaonekana kuwa na wasiwasi na mimi”

“Sina wasiwasi ,ninachokuambia sasa ni kwamba kampuni ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika”Aliongea Edna na kumfanya Roma amwangalie mke wake, alishangaa kwanni hakuwa hata na taarifa kuhusu kufunguliwa kwa hio kampuni hivi karibuni.

“Hayo maandalizi uliyafanya lini mke wangu , si wiki mbili zilizopita ulikuwa mgonjwa?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Edna.

“Nilikuwa hospitalini ndio , lakini haimaanishi kwamba na mambo mengine yanakwama”Aliongea Edna huku akijimiminia Maziwa nusu kikombe na kunywa kidogo na kisha kujifuta midogo na kitambaa.

“Tukitoka hapa nataka tuongozane tukaangalie mazingira ya kampuni , Siku mbili zijazo nataka unisindikize Kwenda Ufaransa na tukirudi tutaifungua kampuni rasmi”Aliongea Edna huku akiweka kikombe chini na kumfanya Roma amwangalie Edna.

“Ufaransa!!!”Aliuliza Roma kwa mshangao, ukweli mara baada ya kusikia Kwenda Ufaransa moyo wake haukukubaliana na hilo kabisa.

“Mbona umeshangaa , ni safari ya kibiashara tu , na nakwambia kama utakuwa tayari kunisindikiza kama hautokuwa tayari ni sawa pia”Aliongea Edna kwa sauti ndogo na kumfanya Roma afikirie kidogo.

“Nchi za Ulaya na Amerika ni nchi ambazo sipendi Kwenda maana watu wengi wananifahamu, lakini pia nina maadui wengi na sipendi kuua”Alijiwazia Roma kwa sekunde kadhaa na kisha akamwangalia Edna ambaye alikuwa akimwangalia usoni , akionekana kusubiria jibu lake.

“Bebi usiniambie ndio unatumia sababu ya kikazi , kumbe unataka twende Honeymoon?”

“Pffff”Edna alijikuta akipaliwa baada ya kusikia neno ‘HoneyMoon’, Ukweli Edna kwenye moyo wake alikuwa ashaanza kumuamini Roma kwa moyo wake wote na aliona anakila sababu za kumuamini , kwani Tokea wafunge ndoa ya Mkataba , licha ya Roma kuwa na tabia ya kuwa na wanawake wengi lakini kwake alikuwa akionesha utayari wa kumlinda kwa asilimia zote , Edna alifikiria mambo kadhaa yaliowatokea tokea apate kuoana na Roma na ni mengi ambao yalikuwa yametokea wakiwa Pamoja.

“Ni jambo zuri kama nitakuwa na mtu ninaemuamini katika biashara zangu , siku nikiwa sipo vizuri anaweza kunisaidia”Aliwaza Edna kabla ya kuzima taa na kuingia kwenye shuka na kuuchapa usingizi.

Unajua ukiwa mfanyabiashara mkubwa kama Edna swala la kusafiri sio swala la kupanga wiki au mwezi ni swala ambalo unaweza ukaamua Kwenda Marekani asubuhi na saa sita mchana upo kwenye ndege, Kwa mtu wa kawaida kusafiri lazima aanze kuipangia safari mwezi kabla , ila kwa mtu mwenye pesa akiamua kusafiri ni ndani ya muda tu ashapata tiketi na Visa ya kusafiria, hivyo hata Edna baada ya kuamka na kupokea simu kutoka kwa mfanyakazi wake aliekuwa akifahamika kwa jina la Chibu ,juu ya kampuni kubwa ya Luis Vuitton kutaka kuingia nae mkataba wa kibiashara unaohusiana na Malighafi mpya ambazo zilikuwa zikitengenezwa kwa mkataba wa kampuni ya Yamakuza, Maple na kampuni yake , aliona kuna haja ya Kwenda kuzungumzia hilo dili la biashara, lakini katika safari hio alijihisi anapaswa Kwenda na mume wake , haikueleweka kwanini alikuwa akiwaza hivyo , lakini aliamini uwepo wa Roma kwenye safari hio unahitajika.

“Unafikiria mambo mengi,ni safari ya kibiashara ,lakini mara nyingi sipendagi Kwenda Ufaransa mwenyewe”ALiongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.

“Unamaanisha nini hutaki Kwenda Ufaransa mwenyewe”

“Kama unataka kujua sababu inabidi twende Pamoja,na isitoshe uliniahidi utanisaidia kwenye baadhi ya mambo ,mbona unaonekana Kwenda kinyume na ahadi zako?”Aliongea Edna akiwa Siriasi na Roma kwakua alikuwa ni mtu mwenye uzoefu mkubwa ,katika akili yake kuna jambo ambalo ameligundua kutoka kwa Edna

“Okey ! Wife mimi Roma Ramoni siwezi kumkatalia mke wangu kwenye jambo Dogo kama hili , isitoshe tokea tufunge ndoa yetu hatujawahi kusafiri umbali mrefu , inaweza kuwa muda mzuri wa kuwa Pamoja Zaidi na kufahamiana kama mume na mke ”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie Machoni kwa sekunde kadhaa.

“Muda unaenda tunapaswa kuondoka”Aliongea Edna na kisha akanawa mikono na kuchukua mkoba wake na kutangulia na Roma alimalizia haraka na kisha kutoka mpaka nje.

“Uendeshe taratibu”Aliongea Edna akimpatia Roma ufunguo wa Benzi yake na Roma alitabasamu na kuipokea huku akijiambia kuwa na gari la kifahari ambalo lina spidi kubwa ndani ya Tanzania ni kupoteza pesa , yeye gari kama hizo alizoea kuendesha kwa spidi mpaka ya mwisho huko ughaibunu.

“Sawa Bosi”Aliongea Edna huku Roma akimfungulia mlango mke wake.

Dakika chache mbele kwa maelekezo ya Edna Gari ilikuja kusimama Morocco mita kadhaa kutoka yalipo makao makuu ya Airtel Tanzania.

Roma aliangalia jengo hili refu la kupendeza na kisha akamwangalia Edna na kutabasamu.

“Wife usiniambie kampuni unataka uifungue kwenye hili jengo?”Aliuliza Roma na Edna alimwangalia Roma kama vile mtu aliekuwa akijaribu kusoma hisia za Roma.

“Nimechagua ndani ya jengo hili kwasababu ni sehemu nzuri kutokana na aina ya Kampuni kuwa ya mambo ya Media na Entertainment”Aliongea Edna huku akianza kupiga hatua kuingia ndani kabisa ya jengo hili ambalo lilikuwa lina Zaidi ya Ghorofa ishirni Kwenda juu.

“Madam Karibu”Aliongea Suzzane huku akimwangalia Roma na kisha kumtingishia kichwa kama salamu , Suzzane hakuwa akimpenda kabisa Roma.

“Asante Suzzane ,Vipi maandalizi?”

“Kila kitu tayari Madam”Aliongea Suzzane baada ya wote kuingia kwenye Lift huku wakipishana na watu waliokuwa wakimshangaa Edna kwa kumhusudu , licha ya Edna kutokuwa maarufu lakini kuna baadhi ya watu pia walikuwa wakimfahamu na ukizingatia ndani ya jengo hilo pia kulikuwa na kampuni kubwa tu ya usafirisaji ya ‘AllyEXpress’.

Ndani ya dakika kadhaa tu Roma na Edna walikuwa ndani ya Ghorfa namba Kumi na nane.

“Madam kutokana na wataalamu walivyotoa ushauri , tumeamua kuifanya hii Floor kuwa ni Sehemu ya Ofice za wafanyakazi , Pamoja na Studio”Aliongea Suzzane huku akifunfua baadhi ya Vyumba vilivyokuwa na majina ya Vyeo vya kiofisi kama vile Chief Editor , Disigner Office , Content Manager na mambo megnine.

Baada ya Edna kuridhishwa na mpangilio wa Floor hio , walihamia Floor ya juu kabisa namba kumi na tisa , hii ni Floor ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya Redio Pamoja na Television Broadcasting Room`s lakini pia kulikuwa na Office ya Artist Manager na office zingine zilizokuwa zikihusiana na Mambo ya Media and Entartaiment Industry.

Floor ya mwisho kabisa , ilikuwa ni Floor ya viongozi wa juu kabisa wa Kampuni , ikiwemo Office ya Director , Business Manager , Exucutive Manager Pamoja na Chief Producer , lakini pia kulikuwa na Technical Room;s Pamoja na ukumbi wa mikutano.

Roma alishangazwa na maandalizi hayo na kwa kuangalia tu aliamini vitu vyote hivyo havikuwa vimepangwa ndani ya wiki , aliona mke wake huenda alikuwa ashaanza maandalizi tokea anamwambia juu ya swala hilo la Kampuni.

“Hii ndio itakuwa office ya Director”Aliongea Suzzane baada ya kufikia kwenye mlango upande wa kulia na kisha akaufungua na Roma na Edna wakaingia ndani, ilikuwa ni office mbili kwa moja (Two in One) yaani kulikuwa na ofisi ya Sekretary , halafu ukienda ndani Zaidi ndio unakuta ofisi ya Director mwenyewe.

“Roma unaonaje ofisi yako?”Aliongea Edna huku akiwa ameachia tabasamu kwenye uso wake , alionekana kuridhishwa na muonekano wa ofisi hio , na alijiambia moyoni hio ndio ofisi ya kukaliwa na mwanaume mwenye hadhi ya kuwa mume wake.

Suzzane alimwangalia Edna kwa mshangao , unajua licha ya kwamba alikuwa akisimamia maandalizi yote ya ufunguzi wa hio kampuni iliokuwa ikihusia Habari na Burudani , ila hakuwa akijua kuwa mtu aliekuwa akija kuongoza kampuni hio ni Roma , mwanaume ambaye yeye mwenyewe ndio aliehusika kumtoa Mbagala na kumleta kuonana na Edna , mwanaume ambaye hapo nyuma kazi yake ilikuwa ni kubeba mizigo , mrembo huyu alishangaa na kujiuliza Roma ana nini cha ziada mpaka bosi wake kumpa ofisi hio kubwa na cheo kama hicho , ikumbukwe kwamba mrembo huyu pia alikuwa akijua ndoa ya Edna na Roma haikuwa ya kimapenzi , kwani alikuwa akiujua mkasa wote uliotokea kati ya Edna na Roma,
 
SEHEMU YA 166

Roma alimwangalia Edna na kisha kutabasamu , kwa ukubwa wa hii ofisi aliona mke wake alikuwa akijitahidi kuipandisha hadhi yake , jambo ambalo kwake halikuwa kipaumbele sana , yeye alikuwa amekubali kuja kuongoza hio kampiuni kutokana na kwamba alikuwa ashaweka ahadi na hakuwa mtu wa kupenda sana kukaa kwenye maofisi makubwa kama hayo.

“Eniwei hii itakuwa sehemu nzuti kwa mimi kucheza gemu pasipo usumbufu”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake na kumsogelea Edna aliekuwa akiangalia upande wa nje wa jiji ambalo lilikuwa na pilikapilika na kumkumbatia kwa nyuma na kumfanya Edna ashituke , kwani Roma alifanya kitendo hicho mbele ya Suzzane , lakini Roma alikuwa akitegemea Edna angejaribu kujitoa ndio maana hakutaka kumpa nafasi.

“Bebi ofisi ni nzuri na kubwa , nitakuwa bosi”Aliongea Roma na kumbusu Edna shavuni na kisha akamwachia na kumfanya Edna kuwa mwekundu kama yai, hakuzoea kufanyiwa mambo ya kushitukiza kama hayo,alimwangalia suzzane na kujikuta akiona aibu kama mwanafunzi wa kidato cha tatu.

“Suzzane Asante kwa kazi kubwa uliofanya , nadhani baada ya vifaa vya kisasa vya mawasiliano tulivyoagiza kufika nchini kazi itakuwa imeisha kabisa na kuanzia wiki ijayo tutapanga ni tarehe ipi ya kuifungua”

“Asante bosi”

“Kuhusu jina la Kampuni na Muongozo wote kesho utapatiwa kwa ajili ya kuupitia na mtaweza kukutana na wasaidizi wako”Aliongea Edna huku akiwa amekalia kiti cha mzunguko ambacho Roma atakuwa anakalia alionekana kama mtu ambaye alikuwa akikijaribu.

Baada ya Edna kuridhika na ukaguzi wa maandalizi ya kampuni hio walishuka mpaka chini na kuingia kwenye gari kwa ajili ya kurejea makao makuu kuendelea na kazi na ndani ya muda mfupi tu, walikuwa washafika na Edna alielekea kwenye ofisi yake , huku Roma akielekea ndani ya idara ya PR.

Roma baada ya kuingia ndani ya eneo hili la kazi wenzake walionekana kuwa bize kweli na majukumu yao ya kazi , alisalimiana nao kama kawaida na kisha akaketi kwenye kiti chake, huku Recho aliekuwa akichezesha vidole kwenye tarakishi yake akimwangalia Roma kwa kutabasamu na kuendelea na kazi aliokuwa akiifanya.

Roma baada ya kucheza cheza gemu kwa dakika kadhaa, alionekana kuchoka na alikuwa amemkumbuka Nasra , alikuwa na siku kadhaa ambazo hakuwa ameonana na mrembo Nasra tokea siku ya mwisho walivyolala ndani ya hoteli ya Maple Grupu , siku ambayo Edna aliweza kutekwa na kundi la Yamata.

Roma alinyanyuka na kupiga hatua kutoka nje ya ofisi hio , huku akiacha baaadhi ya wanawake hawa warembo wakimwangalia kwa nyuma , walikuwa wakijiuliza Roma alikuwa akienda wapi , kwani haikuwa muda wa chakula.

Roma baada ya kuingia kwenye lift moja kwa moja ilipandisha mpaka Floor ya wafanyakazi wakubwa wa kampuni na alitembea mpaka ilipokuwa ofisi ya Nasra na kisha akagonga mlango na kuruhusiwa kuingia na Nasra alikuwa yupo Bize akiwa amekodolea macho kwenye tarakishi yake, huku akiwa amevalia miwanii ya kumkinga na mwanga wa bluu.

“Bebi…!!”Aliita Roma baada ya Nasra kumwangalia na kisha kujifanya kumpotezea.

“Mr Roma unashida yoyote unataka nikusaidie?”Aliongea Nasra akiweka sura ya Uprofesheno.

“Ndio ndugu mhasibu”Aliongea Roma huku akiiingia na kufunga mlango na funguo.

“Usifunge mlango na funguo”Aliongea Nasra kwa kuamrisha lakini Roma hakujali , baada ya kufunga mlango alimsogelea Nasra upande wa nyuma ya kiti chake.

“Roma nipo kazini kwasasa”Aliongea Nasra huku akiweka uso wa ukauzu na Roma aliona hali ya makasiriko kutoka kwa Nasra na alijiambia huenda ni kwasababu hakuwa amemtafuta kwa muda mrefu kidogo ndio maana mrembo huyu alikuwa akijifanyisha kununa.

“Romaa…!!!!”Nasra alijikuta akitoa mlio wa sauti baada ya Roma kupelekea mkono sehemu ambayo ilikuwa ndio kama ugonjwa kwa Nasra akiguswa hhio sehemu.

“Hehe….Bebi Nasra ukinibusu ndio naachia”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu la kifedhuli na na alionekana hakuwa na mpango wa kutoa mkono wake kabisa na Nasra licha ya kwamba mwanzoni alikuwa na hasira kutokana na kuingiliwa eneo lake la Kazi , lakini kitendo alichofanyiwa na Roma kilionekana kuzaa matunda.

“Roma… Toaa… bhaan,, Aiii..”Aliongea Nasra kwa kusista sita , lakini mrembo huyu alionyesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kujiuzia kwani alijikuta akisukuma kiti chake cha mataili na kikarudi nyuma na kujitoa kwa Roma na kumfanya Roma atabasamu.

“Roma hapa ni ofisini naomba uelewe”Aliongea Nasra na Roma aliona usiriasi wa Nasra na kuona aache kweli na kusogea na Kwenda kukalia sofa.

“Nimekumisi ndio maana”

“Kama umenimiss kwanini haukunipigia simu wala kunijulia hali, mwanaume mbinafsi wewe”Aliongea Nasra , ukweli mrembo huyu licha ya kwamba alikuwa akijua Roma ana mke ila siku zote alishindwa kujua kuwa Edna ndio aliekuwa mke wa Roma na hii yote ni kutokana na Tabia ya Nasra kutomfatilia kabisa Roma.

“Bebi nilikuwa bize , Wife alikuwa mgonjwa ndio maana”Aliongea Roma na Nasra alionekana kuelewa , aliona hayupo kwenye nafasi ya kulalamika kwani kwa Roma alikuwa mchepuko tu.

“Kuna jambo nataka kukuambia , nilikuwa nikisubiria unitafute mwenyewe”Aliongea Nasra na kumfanya Roma atake kujua ni nini Nasra anataka kuongea.

“Ni juu ya nini?”

“Ni kuhusu mama yangu , anataka kukuona”Aliongea Nasra na kumfanya Roma atoe macho.

“Unamaanisha unataka nikajitambulishe?”

“Ndio ninachomaanisha , mama yangu ananisumbua juu ya hilo na nishamwambia nina mpenzi,Mwisho wa mwezi ujao nataka kurudi kijijini Kwenda kumsalimia, hivyo naamini utanisindikiza”

Jambo ambalo Nasra alikuwa akiongea ni kwamba Roma alitakiwa Kwenda nyumbani kwa Nasra kwa ajili ya kujitambulisha ukweni.

“Bebi najua tokea tumeanza mahusiano yetu , sijawahi kukuuliza juu ya wazazi wako, kumbe wazazi wako wapo kijijini?”Aliongea Roma na kumfanya Nasra na yeye afikirie kidogo , ni kweli hakuwa amemueleza Roma juu ya Maisha yake yalivyokuwa tokea wanaanza kuonana na kuanza mahusiano yao na ni Zaidi ya mara nne washalala Pamoja na Roma ndio aliehusika hata kutoa usichana wake.

“Yeah! Ni Stori ndefu nitakuhadithia tukiwa na muda , ila ni kwamba ninae mama tu , baba sina kwani alishafariki, na tokea nitoke nyumbani miaka kumi na mbili iliopita sijawahi kurudi nyumbani Zaidi ya kuwasiliana na mama na kumtumia pesa ya matumizi tu , mwisho wa mwezi huu nataka nirudi nyumbani , lakini kanisisitizia lazima niende na wewe”Aliongea Nasra kwa sauti ndogo na kumfanya Roma afikirie kidogo.

Unajua Nasra ni kweli mama yake alikuwa akimsisitizia Kwenda kumtambulisha Roma kijijini , lakini tatizo kwa upande wake alikuwa akijua Roma ni mume wa mtu na hilo ndio lilimfikirisha Zaidi , lakini kutokana na Nasra kuwa katika Dini ya uislamu kwake hakuona shida kumpeleka Roma kama tu atakubali , lakini shida ilikuwa ni kwa Mke wake Roma ambaye hakuwa akimjua , hivyo aliishi kwa wasiwasi sana hata kuliweka hilo wazi mbele ya Roma.

“Okey nimekuelewa mpenzi wangu , unaonekana kuwa na wasiwasi mno”

“Kwahio umekubali tutaenda wote!?”

“Ndio nimekubali unafikiria nitaachaje sasa wakati mimi ndio mpenzi wako na nakupenda”Nasra alijikuta akitokwa na machozi , hakuamini Roma amekubali Kwenda nae kijijini kwa ajili ya kujitambulisha kwa mzazi wake , aliinuka alipokuwa amekaa na kumsogelea Roma na wakapeana ‘Deep Kiss’ kwa takribani dakika tatu nzima.

“Bebi unaonakena kufurahi?”Aliuliza Roma

“Yeah nimefurahi , Asante kwa kukubali Kwenda na mimi , nilikuwa nikiwaza sana juu ya hilo swala”

“Ulikuwa unawazia nini sasa , ulitakiwa uniambie kama kulikuwa na swala kama hilo”

“Wewe ulifikiri ni rahisi tu , kumbuka wewe ni mume wa mtu hivyo kuna ukomo wa mahitaji yangu kwako”Aliongea Nasra na kumfanya Roma amkumbuke Edna hapo hapo , na kukumbuka kuwa Nasra hakuwa akifahamiana na mke wake.

“Wewe ukiwa na shida yoyote niambie , ndio nina mke , lakini mimi ni mpenzi wako vile vile kama unashida wewe sema nitaangalia namna ya kukusaidia”Aliongea Roma na kumfanya Nasra kutabasamu. Na kumbusu Roma shavuni.

“Vipi mkeo lakini utamuaga vipi?”Aliuliza Nasra na kumfanya Roma kwanza akune kichwa

“Nasra unaonaje nikikutambulisha kwa mke wangu?”Aliuliza Roma.

“Lini!!?”

“Hata sasa hivi”Aliongea Roma na kumfanya Nasra ashangae na ombi hilo la Roma.

ALHAMISI TUTAONANA , NICHEKI WATSAPP 0687151346
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…