SEHEMU YA 163
Magdalena hakuamini kama mtu aliekuwa mbele yake ni Roma , aliona ni kama miujiza na kujiuliza kwa wakati mmoja ni muda gani kafika ndani ya hili eneo , kwani ni sekunde chache mbele alionekana kukata tamaa kabisa , lakini sasa hivi tu anatokea mbele yake.
“Roma unafanya nini hapa?”Aliongea Magdalena huku akijinyanyua kivivu
“Unauliza niko hapa ulifikiri nimependa , Nyie kama jeshi la Tanzania mnapata faida gani kuingilia mambo ya Vaticann na Bunge la Kiza?”
“Sisi ni wanajeshi na tulipewa oda kutoka juu na ndio maana tuko hapa , lakini hata hivyo Bunge la Kiza ni mashetani”Aliongea Magdalena kwa sauti ndogo huku akisimama wima kabisa na Roma alimwangalia na kisha kutabasamu.
“Nafikiri hata wakubwa zako hawaelewi uhatari uliopo juu ya hawa watu wanaojiita ‘Blood Race’ inabidi nikitoka hapa niwaelezee”Aliongea Roma akiwa hana hata wasiwasi kabisa na muda huu Watu wa Vatican pamoja na na wa ‘Blood Race’ walikuwa wakimwangalia Roma kwa mshangao , unajua licha ya kwamba Lilith alimwita kama Hades , ila kwa mwonekano wa Roma hawakuwa wakiamini kabisa , kwani licha ya kuwa na taarifa zinazomuhusu Hades , hawakuwahi kumuona moja kwa moja.
“Kwanini umeniokoa?”Aliuliza Swali Mage akimwangalia Roma usoni , na Roma aliona swali hilo ni la kipuuzi.
“Kwahio ulitaka nikuache ufe , licha ya kwamba sikupenda kuingilia kinachoendelea hapa , ila nisingeweza kuona Rafiki wa mke wangu akiuwawa mbele ya macho yangu na isitoshe Taila linawezekana bado linakuhitaji , hata hivyo unabahati sana , ingekuwa ni miaka kadhaa nyuma nisingejihangaisha , ila kwakua sasa hivi na mimi ninafamilia lazima angalau nifanye jambo la kibinadamu”Aliongea Roma bila ya kuonyesha wasiwasi kabisa.
Magdalena uso wake ulionekana kukosa tumaini , ilionekana mrembo huyu alikuwa akitegemea jibu zuri kwa Roma, lakini sababu zilziokuwa zimetolewa zilikuwa hazijamridhisha , alijikuta akiangalia upande wa kulia kuwaangalia wanajeshi wake aliokuwa amefika ndano ndani ya hilo eneo na upande wake wa kulia alimuona Jumbe akiwa chini huku akionekana kujeruhiwa vibaya sana.
Mpaka kufikia muda huo Vatican walionekana kuzidiwa nguvu , lakini licha ya hivyo hawakuonekana kukata tamaa kabisa ,lakini pia upande wa Dark Parliament walionekana hawakuwa tayari kuwaacha Vatican , walikuwa na mpango wa kuwamaliza na kisha ndio waondoke na ‘Holy Grail’ , lakini sasa baada ya ujio wa Roma hapa ndani, pande zote mbili walikuwa wakiwaza ni upande gani Hades atasimama na waliamini upande wowote Hades atakao simama ndio utakaoshinda.
Magdalena sijui alimfanyia nini kwa Jumbe , lakini bwana huyo alionekana kupata nguvu na maumivu kupungua na sasa alikuwa amesimama na akimwangalia Roma.
“Bro bora hata umekuja kutusaidia maana tungekufa”Aliongea Jumbe huku akimwangalia Roma.
“Sijaja kusaidia mtu yoyote hapa na nikueleze tu sipo upande wa mtu yoyote , mimi nimekuja kuleta amani, usiongee maneno ya kipuuzi ukaniuzi maana naweza kukuua”Aliongea Roma kwa sauti ya kuwa siriasi kabisa na kumfanya Jumbe kunywea kwani ni kama alikuwa akifokewa.
Garbiel licha ya kupigana muda mrefu , hakuwa amedhurika sana , kwani alikuwa na baadhi tu ya majeraha na mikwaruzo kwenye mwili wake.
“Your Majesty’s ability is far beyond us. Are you possibly doing this for the Holy Grail as well?”(Mfalme uwezo wako ni mkubwa kuliko sisi , Kuna uwezekano wa wewe pia kupambana kwa ajili ya Holy Grail?”Aliongea Gabriel huku akimwangalia Roma aliekuwa kwenye mavazi ya suti kama alivyokuwa ametoka nyumbani.
“I can’t even confirm the authenticity of your Holy Grail, why would I be interested in it then? Furthermore, the term ‘eternity’ doesn’t hold any major meanings for me”
“Kwanza sina uthibitisho wowote wa kitu mnachopigania kuwa halali , kwanini niwe na matamanio nacho , Zaidi ya yote , kwangu neno ‘Umilele” halina maana kwangu”
“Sasa mfalme kama huna haja na ‘Holy Grail’ kwanini unaingilia?”Aliuliza Garbriel.
“Mimi ninachotaka ni amani itawale ndani ya hili eneo , mpaka sasa mmeua wanajeshi wengi wa Taifa ambalo ninaishi , na wanajeshi hawa ndio wanalinda usalama wa raia wa nchi hii, lakini hata hivyo mimi sina uadui wowote na Vatican pamoja na Dark Parliament , hivyo sitotaka kuona mapambano yanaendelea hapa , ninachowashauri muondoke mara moja na kilichotkea hapa kiishie hapa hapa”Aliongea Roma kwa msisitizo lakini kwa upande wa Gabriel hakuwa tayari , mpaka muda huo wanajeshi wake karibia wote walikuwa washapoteza Maisha na pili Holy Grail haikuwa kwenye mikono yake na aliona ni upuzi kuondoka pasipo kulipiza damu za wanajeshi wake.
“Mfalme mpaka sasa wanajeshi wetu karibia wote washakufa tayari sio haki kwa sisi kuondoka mikono mitupu”
“Gabriel sidhani kama wanajeshi wako wote wangekuwepo hai , ungekubali kuondoka pasipo kuwa na Holy Grail?”Aliongea Moses kwa kejeli.
“Since you guys aren’t willing to give up the stupid Holy Grail, let’s do it this way, hand it over to me and I’ll destroy it on the spot. It’ll be fair after that.”
“Nyie watu kwakua hakuna mmoja wenu ambaye yupo tayari kuachia hiko kikombe cha kipuuzi, tufanye hivi nipeni nikiharibu hapa hapa na itakuwa ni haki kwa kila upande”Aliongea Hades
“No Way”Aliongea Gabriel kupinga pendekezo la Roma , lakini Roma Hakujali.
“Do you guys think I’m here to listen to your opinions? Don’t irritate me anymore. When I take action myself, none of you will be benefited.”
“Mnafikiria nipo hapa kwa ajili ya kusikiliza maoni yenu , achene kunifanya nikasirike , nikiamua kuongea kwa vitendo hapa hakuna atakae faidika”Aliongea Roma kwa mkwala na kufanya pande zote kuwa na wasiwasi. Kwenye nyuso zao.
“Your Majesty mustn’t look down on us too much. Although Your Majesty is much stronger than most, I don’t think we’re free to be killed easily,”Aliongea Archimonde akimaanisha kwamba Roma asiwadharau kwani hawawezi kufa kizembe licha ya kwamba yeye ana nguvu.
Mpaka hapa Roma aliona kiburi kila upande na hakuona mtu yoyote ambaye alikuwa tayari kwa ajili ya kuachia hiko kikombe lakini pia hakutaka kukaa hapo msituni kwa muda mrefu kwani aliamini akichelewa Edna atamuacha na akaenda nyumbani peke yake , hivyo aliona anahitajika kukamilisha kila kitu na kuondoka zake.
“Kwa sababu hamtaki kutoa hiko kikombe kwa hiari yenu , basi nitamsachi mmoja mmoja na kukichukua kwa nguvu”Aliongea Roma na palepale akapotea alipokuwa amesimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Charlie na Charlie alitaka kumkwepa lakini Roma alikuwa na spidi kuliko yeye na alijikuta akipapaswa kwa spidi ya ajabu na Roma aliona Charlie hakuwa na hiko kukombe na alichokifanya ni kumtupia mbali Charlie kama mpira na kufanya watu wote kushangaa , kwani licha ya Charlie kuwa mwanamke lakini alikuwa na mwili mkubwa , walishngazwa na uwezo na nguvu za Roma kwa wakati mmoja.
Roma baada ya kukikosa kwa Charlie alimwangalia Moses aliekuwa mita kadhaa kutokea aliposimama na kumsogelea , lakini sasa ile anafika mahali aliposimaa Moses , hakuwepo , alikuwa amepotea kama jini na muda huo huo Nguvu kubwa sana ilimsukuma Roma na kumrushia nyuma na kujikuta akichuchumaa chini na kugusa Ardhi.
“Ni nguvu gani hii…!!!”Roma alijikuta akiwa kwenye mshangao , kwani hakuelewa ni nini kimepotea kwa muda huo kwani alihisi nguvu kubwa kuliko ya kwake.
“Moses…!!!!”Archimonde na wenzake wote walijikuta wakiita kwa nguvu baada ya kutokumuona Moses , licha ya kwamba walishangazwa na Roma kupotea na kuibuka kwa wakati mmoja , lakini swala la Moses kupotea liliwachanganya kwani walikuwa wakijua kabisa kuwa Moses hakuwa na uwezo huo.
Muda ule ule baada ya kupotea kwa Moses , wakati kila mtu akiwa kwenye mshangao , mara Ghafla mwanga hafifu kama wa moto ulitokea kutoka juu na hapo hapo Roma aliweza kushuhudia’ kikombe kikishuka kutoka juu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba , kikombe hiki hakikuwa kimeshikiliwa na mtu yoyoyte , ila kilikuwa kimesimama hewani , ilikuwa ni jambo la kushangaza mno kwa Roma na kwa kila mtu.
Roma alikuwa na uwezo wa ajabu mno , lakini likija swala la kugandisha kitu hewani hakuwa akiweza kwani hakuwa na uwezo wa kutumia ‘Space Laws’.
Lakini sasa mpaka muda huo alijiuliza Mioses kapotelea wapi , kwani yeye ndio aliekuwa na kile kikombe , lakini ajabu ni kwamba kikombe kilishuka chenyewe tena kwa namna ya ajabu huku bila ya Moses kuonekana tena.
Kila mmoja alishangazwa na jambo hilo , Lilith na yeye alikuwa kwenye mshangao , licha ya kwamba ‘Dark Parliament’ walikuwa ni watu wa kushuhudia baadhi ya matukio ya kutisha katika maisha yao , lakini tukio kama hilo lilikuwa la aina yake , kwani hakukua na aina yoyote ile ya nguvu ya ziada iliotokea kuashiria labda kama kuna mtu mwingine ameongezeka na hata Roma mwenyewe ambaye alikuwa na uwezo wa hali ya juu , hakuweza kutambua chanzo cha nguvu kubwa iliotokea.
Unachotakiwa kujua ni kwamba ‘Dark Parliament’Walikuwa wakihitaji hiko kikombe kutokana na kuamini kwamba kama watatumia kikombe hiko kitakatifu kunywea maji , basi wataweza kuishia Maisha marefu pasipo kufa na na hapa ndio maana Roma akasema kwamba yeye neno ‘Eternity’ kwake ni upuuzi na halina uhalisia wowote kama walivyokuwa wakiamini.
Roma baada ya kutoka kwenye mshangao , alisimama na kuchukua kikombe ambacho kilikuwa hewani na kukishika kwenye mikono yake bila wasiwasi wowote hukua akianza kukichunguza , ni kikombe cha zamani kama kilivyokuwa kikionyeshwa masaa kadhaa nyuma ndani ya ukumbi ule wa Mlimani City lakini hapa kwakua kilikuwa karibu , kilionekana kuwa na maandishi ambayo yeye mwenyewe licha ya kujifunza ligha nyingi hakuweza kutafsiri maana ya maandisihi hayo yaliokuwa yameandikwa kuzunguka sehemu ya juu.
“Umemuua Moses..!!!?”Aliongea Archimonde kwa hasira huku akimwangalia Hades , yeye hakuelewa kabisa hali iliokuwa imetokea na aliamini kabisa , aliekuwa amehusika na kifo cha Moses alikuwa ni Roma na ndio maana akamuuliza hivyo , lakini Roma wala hakugutushwa wala kushangazwa na Swali la Archimode.
“Sijahusika na kifo chake mimi , kaa ukilijua hivyo , lakini kilichotokea hapa pia sina maelezo nacho, na sasa kile mlichokuwa mkipigania kipo kwenye mikono yangu.”Aliongea Roma huku akiangalia kile kikombe , yaani kwake hakikuwa na maana kubwa kama watu waliokuwa wamezunguka walivyokwa wakikiangalia , yeye aliona kikombe hiko cha kawiada sana na hakukipa uzito wa aina yoyote ile.
Lilith alikuwa akikiangalia kikombe hiko kwa matamanio makubwa sana , alitamani kitue kwenye mikono yake na kisha apotee ndani ya hilo eneo , aliakuwa akiamini kama atakuwa na hiko kikombe basi anakwenda kuishi milele.