Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 167

Mage licha ya kwamba alikuwa akionekana kawaida mbele ya Roma , lakini ukweli ni kwamba mrembo huyo hakuwa kawaida kabisa, haikueleweka ilianza lini , lakini Mage alikuwa amebadilika sana yale Maisha ya kutumia viungo bandia kwa ajili ya kujiridhisha alikuwa ashaacha na swala ambalo lilikuwa limemfanya kuacha juu ya kutumia vifaa hivyo ilikuwa ni Roma.

Mage alikuwa akimuwaza Roma kila siku , licha ya kwamba Roma alikuwani mpenzi wa rafiki yake wa utotoni yaani Edna , lakini alishindwa kuhimili hisia zake , mwanzoni kwake alihisi ni chuki ambazo alikuwa nazo juu ya Roma ndio zilizokuwa zikimfanya kumuwazia Roma , lakini kadri siku zilivyokuwa zikienda aliamini haikuwa chuki bali ni mapenzi aliokuwa nayo juu ya Roma , yaani chuki zikageuka mapenzi,

Siku ya jana yake ndio alipohakikisha hisia zake kikamilifu na kuaminni kwamba alikuwa na mapenzi na Roma , kilichomfanya kuhakikisha hilo ni wakati baada ya Roma kupotea ndani ya ukumbi Pamoja na dada yake , kitendo kile kilimfanya mrembo huyu kuwa na wasiwasi mno na wasiwasi wake haukuwa kwasababu huenda Roma angekuwa kwenye matatizo , Hapana , bali wasiwasi wake ulikuwa ni kwamba huenda Magdalena pacha wake alikuwa na Roma na wanafanya mambo ya kimapenzi na hata baada ya Roma kurudi hakuridhika kabisa, kwanza alijiuliza Magdalena yuko wapi mpaka Roma kujitokeza peke yake, lakini wasiwasi wake ulijaa Zaidi baada ya dakika kadhaa kutumiwa ujumbe na Magdalenda kwamba arejee nyumbani kwani yeye ashafika.

Ilikuwa ni muda wa saa mbili za asubuhi gari ya Porsche ilisimama ndani ya eneo la Osterbay, gari hii ikiendeshwa na mwanadada mrembo Polisi Mage , baada ya kupiga honi kwa dakika moja hatimae geti lilifunguliwa na Mage akaingiza gari ndani.

“Karibu sana Miss”Aliongea mlinzi wa getini mara baada ya Mage kutoka kwenye gari na Mage aliitikia kwa kichwa na kuzunguka upande wa Buti na kutoa sanduku kubwa la kuhifadhia nguo.

“Mage..!”Ilikuwa ni sauti ya Magdalena iliokuwa ikitokea nyuma na kumfanya Mage ageuke nyuma na kumuona dada yake aliekuwa amevalia Track Suit akiwa nyuma yake na kwa jinsi alivyomuona alijua tu anatoka kuchukua mazoezi ya kukimbia na muda huio alikuwa ndio anarudi.

“Dabi Chukua hilo begi”Aliongea Mage na akimwamrisha mlinzi wa geti kuchukua Begi alilokuwa ameshikilia Mage na mlinzi kwa haraka haraka alitii na kubeba hilo begi na kuelekea ndani.

“Naona umeamua kurudi nyumbani”Aliongea Magdalena huku akimsogelea Mage.

“Ndio nimechoka kuishi mwenyewe nimeamua kurudi”Aliongea Mage huku akiladhimisha tabasamu huku akimkagua Magdalena , alikuwa ni kama aliekuwa akimfananisha dada yake na mtu, na hata Mage alishangazwa na namna ambavyo Mage alikuwa akimwangalia.

Ukumbuke kwamba Mage na Magdalena licha ya kuwa na kazi tofauti , lakini walikuwa wakifanana sana na kilichokuwa kikiwatofautisha pekee ilikuwa ni mtindo wa nywele , kwani Magdalena hakuwa na nywele ndefu na Mage alikuwa na nywele ndefu alizozibana kwa nyuma.

“Nimefurahi umerudi pacha.. twende ndani baba na mama watakuwa wanatusubiri”Aliongea Magdalena na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jumba hili ambalo lilikuwa la kifahari kweli.

“Jana ulirudi saa ngapi na kwanini ulipotea wewe Pamoja na Roma?”aliuliza Mage kabla hata hawajafikia mlango na kumfanya Magdalena kusimama na kumwangalia Mage.

“Kuna jambo lilitokea ni la kikazi Zaidi na lilikuwa likihusiana na kile kikombe”

“Vipi kuhusu Roma na yeye alipotea kwasababu hio hio”

“Ndio Mage ila yashapita na sitaki kuyaelezea Zaidi”Aliongea Magdalena na kuingia ndani huku akimuacha Mage akisimama nje.

Damn it ! hii yote ni kutokana na mimi kuwa dhaifu”Alijiwazia Mage huku akikunja ngumi , kwani hakuwa ameridhika na majibu ya dada yake , alijona yeye kama dhaifu na ndio maana mambo mengi hakuwa akiyajua.

“Mage..!!!,Jamani karibu”Aliongea Mama P huku akiwa ameshikilia chupa ya chai na alionekana alikuwa akiandaa kifungua kinywa muda huo , na alifurahishwa sana baada ya kusikia kuwa Mage karudi nyumbani na siku zote lilikuwa ndio hitajio lake kubwa , hakupenda namna ambavyo Mage alikuwa akiishi peke yake kwenye Apartment.

“Asante Mum”Aliongea Mage huku wakikumbatiana kwa furaha na muda huo huo alionekana Afande Tobwe aliekuwa akishuka kutoka juu akiwa amevalia suti na kushikilia mkoba mkononi.

“Dadiii…”Aliongea Mage na kumkimbilia baba yake na kumkumbatia na kumfanya Magdalena awaangalie baba na mwana na kisha akapandisha juu kwa ajili ya kujisafisha mwili , ili arejee mezani kwa ajili ya kifungua kinywa.

“My Daughter Welcome Back Home”aliongea Afande Tobwe na kumfanya Mage atabasamu huku wakitembea wote kuelekea mezani.

“Mwana na Baba wamekutana hii nyumba itachangamka sasa na wengine kukosa nafasi”Aliongea Mama P huku akitabasamu.

“Ushaanza wivu wako na utakonda awamu hii..”Aliongea Afande Tobwe na kumfanya Mama P Kucheka kwa nguvu na wote wakaketi mezani.

Mage alioenakana kujidekeza sana mbele ya Afande Tobwe kuliko isivyokuwa kawaida na alionekana kuwa tofauti na dada yake Magdalena.

“Dadii.. nimerudi nataka kujiunga na Jeshi”Aliongea Mage na kumfanya Afdne Tobwe atamani kujimwagia juisi na hata Magdalena pia alishangazwa na maneno ya pacha wake na sio kwa Magdalena tu pia kwa Mama P alishangaa mno.

“Mage mbona unanitisha , kwanini Ghafla tu unataka kujiunga na jeshi?”Aliuliza Afande lakini muda huu Mama P alikuwa akimwangalia mwanae na kuna vitu vingi alikuwa ameviona kwa Mage na hata namna ambavyo alikuwa akiongea , alikuwa amebadilika.

“Nataka kuwa na nguvu kama Magdalena ,mambo mengi siyajui kwasababu mimi ni dhaifu…”Aliongea Mage na palepale akamwangalia Magdalena na kuanza kutoa machozi na kunyanyika na kukimbilia juu na kuwafanya wanafamilia kushangaa na mtu wa kwanza kunyanyuka na kumkibilia Mage alikuwa ni Mama P.

Mama P ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona Mage akikosa ujasiri na kujiita Zaifu na kulia mbele yao , aliamini kuna jambo ambalo limemtokea mtoto wake na moyo ulimuuma mno , kwani mara nyingi hakuwa akimfatilia Mage kwa ukaribu na kujua maendeleo yake.

*******

Ukweli Nasra pia alikuwa ashawaza siku ambayo ataweza kuonana na mke wa Roma , hakujua ingekuwaje , kwani alikuwa akijua vizuri mambo ya wake kutopenda michepuko.

“Naomba tupange siku utanitambulisha tu”Aliongea Nasra na Roma alitabasamu na kukubaliana na nae.

Baada ya Roma kutoka ndani ya ofisi ya Nasra alirudi sehemu anayofanyia kazi kwa ajili ya kuendelea na shughuli ya kucheza gemu ili kupoteza muda na hatimae kurejea nyumbani.



Upande wa ofisini kwa Nasra baada ya Roma kuondoka , simu yake ya mezani ilianza kuita na aliiichukua na kuipokea.

“Sawa Boss”Aliitikia Nasra na kisha akanyanyuka na kutoka nje ya ofisi yake na alionekana kuchukua uelekeo wa ofisi ya Bosi Edna.

“Boss nimefika”Aliongea Nasra baada ya kuingia ndani ya ofisi ya Edna, Ofisi ambayo leo hii ilikuwa na mabadiliko kidogo kutokana na kuwa na maua mengi yaliokuwa yamepambwa ofisi nzima.

Ukweli ni kwamba baada ya siku kadhaa nyuma kwa Kampuni kuingia kwenye tatizo la kushuka kwa Hisa za kampuni , lakini pia taarifa mbaya ambayo ilikuwa ikisambaa mtandaoni , iliokuwa ikihusiana na Edna , lakini pia taarifa za kuugua kwa Edna , wafanyakazi wengi wa kampuni walikuwa na wasiwasi na bosi wao sana kutokana na kuugua kwake , lakini wakati huo walimuona Edna kama shujaa baada ya hali kutengemaa na tatizo kuonekana kama vile halijatokea na hayo maua yote yaliokuwa yamepambwa kwenye ofisi ya Edna yametoka kwa wafanyakazi wa kampuni hio , walionekana kumkubali sana Bosi Edna kwa juhudi zake alizokuwa akifanya kwa kampuni, kwao Edna alikuwa sio bosi tu , lakini walimuona kama shujaa, na hii yote ni kutokana na namna Edna alivyokuwa akiwajali wafanyakazi wake , kuanzia mazingira ya kazi , mpaka mishahara yao, Edna alikuwa CEO wa kuigwa , licha ya kuwa kauzu , lakini alikuwa akijali kila mfanyakazi na alihakikisha kila mfanyakazi jasho lake linathaminiwa na kampuni , Edna hakuwa mnyonyaji na alikuwa msikilizaji na mtu wa kutoa maamuzi na alikuwa akisimamisa sheria na haki katika kufanya kwake maamuzi na hilo lilimjengea heshima kubwa tokea apewe kampuni hio kutoka kwenye mikono ya mama yake.

“Nasra nitahitaji uidhinishe kiasi cha bilioni mbili kwenda Vexto Media and Entertainment”Aliongea Edna.

“Sawa bosi lakini nadhani kutokana na malengo ya kampuni na uendeshaji wake kitakuwa kiwango kidogo sana , nilipiga mahesabu na kuona Bilioni tano ndio zinaweza kutosha”

“Nalifahamu hivyo ndio maana nataka kuidhinisha kiasi hiko , nataka nione hatua atakazochukua Director kuendesha kampuni na kiasi kidogo cha pesa na isitoshe mpaka sasa tunakampuni lakini juu ya uendeshaji hatujapanga”Aliongea Edna na kumfanya Nasra kushangaa kidogo.

“Boss unapanga nani kuwa Director?”Aliongea Nasra na Edna alifikiria kidogo.

“Napanga kumuachia Roma Ramoni awe Director”Aliongea na kumfanya Nasra kutoa macho kwa mshangao , ilikuwa ni taarifa mpya kwake.
 
SEHEMU YA 168

“Mbona umeshangaa hivyo Nasra unafikiri hawezi?”Aliuliza Edna na kumfanya Nasra kurudia katika hali ya ukawaida.

“Hapana Boss nimeshangaa , maana kaanza kazi juzi na kupandishwa cheo mpaka kuwa Director , si jambo dogo”

“Ni kweli unayosema , lakini Roma amefanikisha jambo kubwa ka kampuni kuliko wafanyakazi wote waliofanya kazi hapa miaka na miaka , hivyo naona anafiti kwenye hio nafasi”Aliongea Edna na kumfanya Nasra atabasamu, ukweli alirufahi sana moyoni na kujiambia yes atakwenda kumtambulisha mume wake mtarajiwa kama Director na sio mfanyakazi wa kawaida kwenye kampuni.

“Nimefurahi..”Aliongea Nasra huku akijizuia.

“Kweli”

“Ndio kama mfanyakazi mwenzake nimefurahi kwa ajili yake”Aliongea Nasra akijirekebisha na Edna alimwangalia kwa dakika kadhaa na kisha akageukia tarakishi yake.

“Ni hivyo tu Nasra”Aliongea Edna.

“Edna…”Aliita Nasra na klumfanya Edna amwangalie , ukweli ni kwamba mara zote Nasra akitaka kuongea jambo nje ya kazi ataacha kumuita Edna kama Boisi na ataita jina lake.

“Kuna nini Nasra unachotaka kuniambia , niambie”

“Um… Mwisho wa mwezi huu napanga Kwenda nyumbani kumuona mama”Aliongea Nasra na kumfanya Edna kutoa macho na kisha tabasamu likatangulia.

“Umeamua hatimae Kwenda kutembelea kijijini kwenu baada ya muda mrefu?”

“Ndio…!Mama amenilazimisha niende , lakini pia anataka kumuona mkwe”Aliongea Nasra kwa sauti ndogo lakini kwa upande wa Edna moyo ulipiga Paah , baada ya kusiikia neno Mkwe, lakini alijiuzuia kutoonesha mshangao wake.

“Okey Nasra litakuwa jambo jema, hata hivyo umri unaenda,Nadhani baada ya safari hio utanitambulisha nimfahamu Shemeji yangu”Aliongea Edna huku akilazimisha tabasamu na Nasra aliona aibu kidogo.

“Nitakutambulisha lazima , utakuwa mtu wa pili kumfahamu”Aliongea Nasra nae na akatabasamu na kumruhusu Nasra kuondoka baada ya Sekretari wa Edna kuingia akiwa na faili mkononi.

Kilichomfanya Edna moyo wake kupata mshituko ni kutokana na kwamba alikuwa akijua fika kuwa mtu ambaye alikuwa ni mpenzi wa Nasra ni Roma , sasa swala la Nasra Kwenda kumtambulisha mchumba wake ukweni aliamini kabisa Roma ndio anaenda kutambulishwa.

“Inamaana Roma ashapanga Kwenda kujitambulisha nyumbani kwa Nasra”Alifikiria Edna huku akijihisi moyo wake kuuma hatari.

******

“Mama Theresia vipi kuhusu mpango tuliopanga?”Alikuwani Jestina aliekuwa kwenye simu akiwa nyumbani kwake baada ya Tajiri Azizi kuondoka na alikuwa akimpigia kujua ni lini Mama Theresia anakwenda kutimiza ahadi yake ya Kwenda kuonana na Raisi Senga , ili kumueleza juu ya uwepo wa Blandina nchini Kenya.

“Jestina , inaonekana Baba alikuwa akifahamu juu ya kukutana kwetu na hata kuonana na Roma , leo nimetoka nyumbani na amenieleza kila kitu kuhusu Denisi na ameniambia mpango wetu hatupaswi kuutekeleza “Ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Jestina kukunja sura kwa hasira.

“Unamaanisha nini hatuwezi kuutekeleza?”

“Jestina baba kaniambia hili swala linapaswa kufanyika kwa hatua na hata yeye anatamani kumuona Roma akirudi kwenye familia mapema na nimemuelewa na kuona kaongea jambo la maana ,Jestina najua unataka kumsaidia Dada yako , lakini nadhani hili swala tumwachia baba yangu kwa muda , isitoshe ukweli utatoka tu”Aliongea Mama Thereisa na kumfanya Jestina kufikiria kidogo.

“Okey! Nimekuelewa Mama Theresia”Aliongea Jestina na kukata simu kinyonge , ukweli hakuwa na amani kabisa , aliamini dada yake alikuwa akiteseka.

Hapana lazima nitafute njia ya kumsaidia dada yangu , hata kama hawataki nitahakikisha ukweli unakuwa wazi”Aliwaza Jestina huku akijilaza kitandani.

Upande mwingine wa nyumbani kwa Afande Kweka , alionekana akipokea simu yake iliokuwa ikiita na kuweka sikioni.

“Comrade it been a long Time..”Ilisikika sauti upande wa pili ikiongea kwa lugha ya Kingereza.

“Ndio Komredi ni Zaidi ya miaka ishirini hatujawahi kuwasiliana tokea tuachane nchini Thailland”

“Ndio Komrade naomba unisamehe kwa kutokutafuta kwa muda mrefu”

“ Asante sana Komredi , nilikuwa nikisubiria simu yako miaka na miaka na ndio maana sikuwahi kubadilisha namba yangu ya mawasiliano”

“Haha..Comrade umefanya jambo la maana kutokubadilisha , lakini hata ungebadilisha ningepata namna ya kuwasiliana na wewe nadhani unakumbuka kuwa mimi na wewe tuna siri ambayo inaendelea kati yetu”

“Hahaha…Naelewa Komredi na nadhani umenitafuta muda muafaka , licha ya uzee wangu huu , ila mawazo hayajawahi kuniishia juu ya maamuzi niliofanya miaka ya nyuma”

“Haha..Komredi ulinipinga sana kipindi kile , lakini nadhani sasa hivi unapaswa kunipa heshima yangu”

“Hahaha,,,Komredi unayo heshima yangu tokea siku nilivyoshuhudia matokeo kwa macho yangu , ni matokeo makubwa kweli”

“Komredi ninayofaraha kama umefurahishwa na matokeo na simu hii ni kwa ajili ya kujua namna ulivyoyapokea matokeo”

“Komredi niseme kwamba asante sana , nimefurahishwa kwa namna kubwa sana na matokeo , shukrani zote ziende kwako”

“Haha Koimredi hupaswi kunishukuru hivvyo , kila mtu alifanya sehemu yake na matokeo ndio yamekuwa haya … ila Komredi nimekupigia kwa jambo la Ziada kutokana na matokeo”

“Komredi nipo tayari kusikiliza jambo hilo”

“Komredi nadhani unakumbuka kuwa kulikuwa na watu wakubwa nyuma yangu kipindi kile wakati nakulazimisha kufanya maamuzi?”

“Ndio nakumbuka Komredi”

“Ni Vyema kama unakumbuka Komredi , jambo lenyewe ni kwamba wakuu wanataka kuona kama Matokeo hayana dosari ya aina yoyote”

“Unamaanisha nnini Komredi?”

“Namaanisha unapaswa kuyaweka karibu Matokeo, Nafasi nzuri ndani ya taifa litakuwa jambo zuri Zaidi , tunataka kuona Matokeo yakiwa karibu kabisa na familia yako , ikiwezekana pia matokeo kuwa karibu na Mzaa chema”Ilisikika sauti ya upande mwingine , watu hawa wawili yaani Mzee Kweka na mtu aliekuwa akiitana na Komredi walionekana kuongea kwa Kodi ya neno Matokeo.

“Nimekuelewa Komredi unachomaanisha na nikuahidi ,swala hili nilikuwa nikisubiria tu simu yako , ili kufanya maamuzi”

“Komredi nashukuru kwa kunielewa , wakuu wanataka jambo hili kufanyika mapema kwani ‘Adui wa Zamani anakuja”Mzee Kweka alishangaa.

“Komredi nilifikiria tishio juu ya Adui lishakuwa ‘Neutralized”

“Hpana Komredi , Adui anatarajiwa kurudi na ni hatari sana kwa dunia na ndio maana tunataka majaribio ya Matokeo kukamilika kwa haraka sana na wakuu wanafatilia kila kinachoendelea , hivyo kazi kwako Komredi” Mzee Kweka alifikiria kidogo.

“Sawa Komredi , swala hili naomba nilifanyie kazi ndani ya mwezi mmoja nitakuwa na majibu ya kuridhisha”

“Sawa Komredi , nitakupigia baada ya mwezi”

“Okey Komredi” Hatimae simu ilikatwa na muda huo huo aliingia Zenzei.

“Camilius nimesikia kila kitu”Aliongea Zenzei na kumfanya Mzee Kweka kulazimisha tabasamu.

“Zenzhei nadhanni ni muda wa Senga kujua kila kitu”

“Camilius unamaanisha kila kitu?”

“Simaanishi kila kitu namaanisha taarifa muhimu anazopaswa kujua”Aliongea Afande Kweka.

“Nini napaswa kufanya Camilius?”

“Awamu hii nitalifanyia hili kazi mwenyewe”

“Okey Camilius ila tutakuwa Pamoja katika hili”Aliongea Zenzhei na kumfanya Afande kweka kutabasamu na kutingisha kichwa.
 
SEHEMU YA 169

Wanasemaga utu uzima dawa na hii ndio ilionekana kwa Mama P , mabadiliko aliomuona nayo Mage yalikuwa yakimwambia kila kitu kuwa Mage alikuwa kwenye Mapenzi, kwani alivyokuwa amemzoa Mage sivyo , lakini swala likabakia huyo mwanaume Mage alietokea kumpenda ni nani.

“Mage hebu niambie nini kimekupata ili niweze kukusaidia”Aliongea Mama P mara baada ya kuingia ndani ya chumba cha Mage na kumkuta akiwa halii kama mwanzo bali muda huu alikuwa amejiinamia chini kama mtu anaekagua usafi wa sakafu, lakini licha ya kuulizwa hakuwa tayari kusema , kwanza ataanzaje maana mwanaume ambaye ametokea kumpenda alikuwa mume wa mtu na sio wa mtu tu , ni mume wa rafiki yake wa utotoni , hivyo swala hilo akiliweka wazi ni Dhahiri hata mama yake atamshangaa.

“Mage niambie kwanini unajiita dhaifu ?”Aliuliza Mama P kwa mara ya pili na awamu hii Mage alinyanyua macho yake na kumwangalia Mama yake.

“Nataka kujiunga na Jeshi Mum”Aliongea Mage kwa sauti ndogo , yaani kwa alivyokuwa akionekana Mage hapa usingedhania ni yule ambaye alikuwa na mikwala mingi akiwa eneo lake la Kazi.

“Unataka kujiunga na jeshi ! ni sababu ipi ambayo imekufanya kutaka kujiunga na jeshi , maana wewe mwenyewe ndio uliochagua Kwenda kusomea upolisi”Aliongea Mama p Huku akikaa kwenye kitanda , alikuwa akimdodosa mtoto wake ili angalau kupata mwanga lakini Licha ya Hivyo Mage hakuwa na sababu ya moja kwa moja.

“Okey kama unashindwa kuniambia sababu , niambie ni mwanaume gani umempenda?”Lilikuwa ni swali lililomfanya Mage amwangalie mama yake kwa mshangao.

“Usishangae mimi ni mama yako na nakujua sana Mwanangu , umebadilika sana,Mara ya mwisho nilisikia ulikuwa ukienda Date, nataka uniambie ni hatua gani ulifikia , nieleze Mage ndio nitaweza kukusaidia , mwanaume huyo ni nani , ni wa familia ipi hapa Dar na anafanya kazi gani?”Aliuliza Mama P

“Mama ni kweli kuna mwanaume nampenda…”Aliongea Mage kwa sauti ndogo mno ya kutojiamini , lakini sauti iliosikika kwa Magdalena ambaye alikuwa yupo nje ya mlango akisikiliza maongezi ya Mama yake na pacha yake Mage.

“Ni mwanaume gani kampenda Mage?”Ni swali lililoibuka katika kichwa cha Magdalena , lakini kadiri alivyokuwa akifikiria alijikuta moyo wake ukienda spidi spidi , hali ambayo hakuwa ameelewa , ni kama alikuwa ashapata jibu mpaka muda huo.

Mama P alijikuta akitoa tabasamu , kwanza baada tu ya kusikia kauli hio kutoka kwa Mage , alinyanyuka na kumkumbatia Mage , hakuamini kabisa kama Mage alikuwa ashapenda , mwanamama huyu siku zote alikuwa na wasiwasi sana juu ya Watoto wake kukosa wanaume , kwani tokea awalee hakuwahi kuwashuhudia hata wakitaniana na mwanaume kimahaba na hili lilimtiaa wasiwasi kwani aliona umri wao ulikuwa ukienda na kuna muda alitamanni hata kuwatafutia wachumba yeye mwenyewe kwenye familia za kitajiri ndani ya Osterbay , lakini aliogopa kwani mambo hayo yalikuwa yashapitwa na wakati , lakini pia hakutaka kuwauzi , lakini licha ya hivyo moyo wake yeye na mume wake ulishindwa kutulia kabisa na kuogopa moja kwa moja , lakini leo hii Mage anamwambia kuwa amempenda mwanaume , kwanini asifurahie,

Nitahakikisha huyo mwanaume anaempenda Mage kwa namna yoyote ile , hata kama ni kumpatia pesa”Aliwaza Mama P huku akiendelea kumkumbatia Magreth.

“Ana shida gani dada yako?”Aliuliza Afande Tobwe baada ya Magdalena kurudi Sebuleni na Magdalena alitabasamu kidogo.

“Sijasikia vizuri”Aliongea Magdalena , lakini Afande Tobwe alikuwa ashajua mtoto wake anamdanganya ,ila hakutaka kuuliza Zaidi , alijiambia atazipata taarifa kwa mke wake.

“Mgdalena muda si mrefu tutaenda kuanza mafunzo ya kikosi chetu maalumu cha wanajeshi ambao watapata mafunzo kutoka kwa Roma na jeshi lake,nataka ulisimamie hilo hatua kwa hatu na kuhakikisha swala hili linafanikiwa”Aliongea Afande Tobwe m huku akinyanyuka kwa ajili ya kuelekea kazini kwani muda ulikuwa umeenda.

“Utaniagia kwa mama yako”Aliongea Afande na Magdalena akatikira kwa kichwa.

******

Kwakua Roma hakuwa amekuja na Gari , ilibidi Edna aondoke na Roma kuelekea nyumbani, na sasa mrembo huyu alionekana akiwa ndani ya maegesho ya gari akimsubiria Roma , ambaye alikuwa ashamtaarifu kwa kumtumia ujumbe wa meseji.

Uzuri ni kwamba eneo ambalo Edna alikuwa akiegesha gari lake ni tofauti kabisa na sehemu za wafanyakazi wa kawaida wa kampuni , na hivyo hakuna mtu ambaye alikuwa akijua Bosi wao kampakia nani kwenye Gari.

Ndani ya dakika kadhaa tu Roma alionekana akija ndani ya B2 Parking Lot , akiwa na tabasamu bashasha akimwangalia mke wake.

Edna alikuwa akimwangalia Roma huku vitu vingi vikipita kwenye akili yake , alikumbuka maneno ya Nasra masaa kadhaa yaliopita na alitamani amuulize Roma , ila aliona hana haja ya kumuuliza , lakini bado moyo wake ulikuwa ukiuma.Aliamini kama ni kweli Roma alikuwa akienda kujitambulisha nyumbani kwa Nasra basi watakuja kuona baada ya mkataba wao wa ndoa kuisha na alianza kuona Roma hakuwa akimchukulia kama mke wake halisi na alikuwa akimjali Nasra kuliko yeye , Edna alizuia sana hasira zake na kugeukia mlango wa Dereva na kuingia ndani ya gari kabla hata Roma hajamfikia, na Roma aliishia kutabasamu na kisha akaingia upande wa siti na kuketi.

“Wife unaonaje hii?”Aliuliza Roma

“Nini..!”

“Tunavyorudi hivi nyumbani wawili , mke na mume na hata kuendesha gari kwa zamu , asubuhi ilikuwa mimi sasa hivi ni zamu yako , Hehe..Wife mapenzi yetu ni ya aina yake watu wanapaswa kutuonea Gere”Aliongea Roma kama kawaida yake akiingizia utani , lakini Edna alikuwa kauzu mno, Roma aliona mabadiliko ya Edna ila hakutaka kuyawazia.

Nusu saa mbele walifika nyumbani na Bi Wema alifurahishwa na kuwaona wawili hao kurudi Pamoja na alitamani kila siku iwe kama hivyo, Bi Wema alikuwa akiogopa sana kushuhudia Edna akiishi Maisha ya upweke kama Mama yake na ndio maana siku zote alitaka kuona Edna na Roma wanapatana na kuwa mke na mume kimapenzi na kulala chumba kimoja na hatimae kuwa na Watoto.

Roma baada ya kuingia chumbani kwake simu yake ilianza kuita na aliitoa na kuangalia mtu aliekuwa akipiga na jina lilikuwa ni la Afande Maeda , alipokea na kuweka sikioni.

“Ndio Afande”

“Habari za saa hizi Mr Roma”

“Salama kabisa Afande kuna jipya?”

“Nimekupigia kukumbushia lile swala la mafunzo ya wanajeshi wetu huko Mirambo , wiki ijayo tunatarajia kuanza mafunzo na tunataka uwepo kwenye ufunguzi”.

“Hakuna shaka Afande”

“Asante sana Mr Roma nakutarajia siku hio , nikutakie jioni njema”Smu ilikatwa.

Nilikuwa nishasahau mimi”Aliwaza Roma huku akivua koti lake la suti na kulitundika kwenye kabati la nguo.

******

Naam ilikuwa ni siku nyingine kabisa siku ya asubuhi Roma alikuwa akiegesha gari lake ndani ya Kampuni.

Roma baada ya kutoka kwenye gari yake , alitembea na kuingia ndani ya Lift a alikutana na Benadetha aliekuwa kwenye Lift na alionekana na yeye ndio alikuwa akiingia kwenye kampuni.

Roma alitabasamu na kisha na yeye akaingia ndani ya lift.

“Hongera!”Aliongea Benadetha baada ya kusalimiana na Roma , lakini Roma alishangaa Benadetha kumpa hongera .

“Benadetha unanipa hongera ya nini tena?”

“Acha kujifanyisha Roma wakati unajua ninachomaanisha”

“Niambie sijui unachomaanisha ndio maana nauliza”Aliongea Roma lakini kwa Benadetha aliona Roma alikuwa akijifanyisha tu.

“Namaanisha hongera kwa kupandishwa cheo na kuwa Director wa kampuni mpya inayokwenda kuanzishwa”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma akumbuke sasa na kuishia kujikuna kichwa.

“Aaa…Benadetha ni jambo la kawaida sana , kwanza nilikuwa nishasahau ndio maana”Aliongea Roma na ukweli alikuwa akimaanisha , ila ilikuwa ngumu kwa mwanamke kama Benadetha kukubaliana nae , kwani alikuwa akimjua sana Roma utendaji wake wa kazi , na pia isitoshe ni wafanyakazi wengi ambao wanatamani kuwa katika nafasi kama ya Roma , sasa Roma kusema ni jambo la kawaida kwake aliona Roma anajaribu kuwa ‘Humble’ Ila moyoni yupo ‘Excired’ na furaha juu.

Roma ile wanatoka kwenye Lift ni kama alikuwa akisubiriwa kwani Monica alikuwa amesimama kama mwanajeshi ,Roma baada ya kumuona Moinica alivyosimama alijikuta akitabasamu na kujiambia ‘Miss Airport’ ana vituko sana , maana staili yake ya usimamaji ilimchekesha.

“Mr Roma naomba unifuate”Aliongea Monica na pasipo hata ya kusubiri jibu alianza kupiga hatua kuondoka ndani ya hilo eneo.
 
SEHEMU YA 170

Roma hakujiuliza sana maswali ni wapi alipokuwa akitakiwa kumfuata Monuca , ila akili yake ilikuwa ishafanya kazi tayari na alijua tu , alikuwa akiendelea ndani ya ofisi ya CEO.

Dakika chache walikuwa nje ya mlango wa ofisi ya Edna na wa kwanza kuingia alikuwa ni Monica

“Boss!, Roma is here”Aliongea Monica kwa Kingereza.

“Alright you may go out now”Aliongea Edna akimaanisha kwamba anaweza kutoka sasa.

Ndani ya hii ofisi licha ya Edna kuwa bize , lakini hakuwa peke yake , kwani upande wake wa kulia walionekana watu wawili wakiwa wameketi kwenye asofa , mmoja akiwa ni mhindi na mwingine akiwa ni mwanamke mrembo rangi ya chocolate. Mwanaume alionekana kuwa si chini ya miaka Therathini hivi akiwa amevalia miwani yake ilionakshiwa na rangi ya Dhahabu , na pia mwanamke alikuwa mkubwa vile akiwa amevalia suti yake rangi ya Bluu na blazia nyeupe inayonekana , wote walionekana kujiamini.

“Roma hao watakuwa ni wasaidizi wako kuanzia siku hii ya leo , Daudi na Wendy huyu ndio Director wenu”Aliongea Edna na pale pale wale wanaume walinyanyuka kiheshima na kumsogelea Roma.

“Director naitwa Daudi ninayofuuraha kukutana na wewe”Aliongea kwa heshima akimsalimia Roma.

“Naitwa Wendy Rabani nimefurahi kukufahamu Director”Aliongea yule mwanamke na Edna alitoka kwenye kiti chake huku akiwa amshikilia karatasi mbili na kumsogelea Roma na kumpatia.

“This will be the highlight of Vexto Media and Entertainment in the next few years. We’re mainly getting into music, television, advertisements, etc to utilize our resources, advantages and fame, to create a first class entertainment conglomerate in the country, or even the world”

“Huu ndio muongozo wa Vexto Media and Entertainment ndani ya miaka michache ijayo . Tunakwenda kuingia kwenye kiwanda cha Mziki , Televisheni , Matangazo N.k , Tutatumia Rasilimali , Faida na umaarufu wetu kutengeneza Burudani ya kiwango cha kwanza ndani ya taifa na hata duniani kote”Aliongea Edna kwa kingereza safi huku akiwaangalia Daudi na Wendy.

“Roma you will take charge of core decision-making in Vexto Entertainment. Daudi and Wendy will be your effective assistants, being executive manager and business manager respectively”

Edna aliendelea na kusema kwamba Roma ataongoza kampuni ya Vexto , huku Daudi akiwa ni Meneja Mtendaji na Wendy akiwa ni Meneja wa Maswala ya Kibiashara, kwa namna ambavyo Edna alikuwa akiongea utasema kwamba Roma hakuwa akifahamiana nae , alikuwa siriasi na alikuwa pia akijiamini na kila neno lililomtoka lilikuwa katika mpangilio na Kingereza cha kisomi.

Roma aliishia kujikuna kichwa , licha ya kwamba alikubaliana na mke wake juu ya kuongoza kampuni hio , lakini bado hakuwa akikubaliana kabisa na swala hilo , aliona ni swala ambalo litamfanya kuwaza sana, lakini Edna hakumjali kabisa aliwageukia Daudi na Wendy.

“You two are considered the elders in the company. Bearing enough working experience, I assign you to be Roma’s assistants. I hope that you can give him guidance and opinions. Although he has good potential, he lacks working experience when it comes to practicality. You guys may need to put in more effort for this”

“Nyie wawili mnatambulika kama wakongwe kwenye kampuni , kutokana na uzoefu wenu mkubwa nawapa kazi ya kuwa wasaidizi wa Roma , natumaini mtampa muongozo mzuri na ushauri , Japokuwa ana uwezo mkubwa ila hana uzoefu mkubwa likija swalla la kivitendo , hivyo mnatakiwa mfanyie juhudi hilo”Aliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu huku akimwangalia Edna na kujiambia huyu mwanamke ndio yeye pekee anaemuweza.

Ukweli huyu Daudi na Wendy ni wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni na walikuwa wakifanya kazi ndani ya tawi la Kenya na waliitwa nchini kusimamia kampuni hio mpya kutokana na uzoefu wao mkubwa kazini.

“Rest assured, Boss Edna. Your arrangements naturally have your reasons. We know what to do”Aliongea Daudi

“Since Director Roma can gain Boss Edna’s recognition at his age, he must be unique in some ways. I hope that we can learn from each other in the future, and improve the company from its already good condition.”

“Kutokana na Director Roma kupata utambuzi katika umri wake huu , naamini ni wa kipekee , na natumaini tutaweza kujifunza kwa kila mmoja wetu na kuendea kuboresha kampuni kutoka kwenye hali hii nzuri iliopo “Aliongea Wendy na Edna alitabasamu , Wendy aliongea kwa kujiamini kabisa na alinekana msomi kweli wa ngazi za juu na ilikuwa tofauti kwa Roma, Roma yeye licha ya kuwa na cheti cha Harvard ila kilikuwa ni cha kufoji tu kwa kutumia Koneksheni zake na ukweli hakuwa amesoma hata darasa la kwanza Zaidi ya kujifunza lugha tu alivyokuwa kwenye mafunzo ya Uninja chini ya Zeros Organisation , hivyo alihusudu namna Wendy na Daudi walivyokuwa wakionesha ujuvi wa mambo na namna walivyokuwa Profesheno na Edna alionekana hakufanya makosa kabisa kuwachagua na kuwa wasaidizi wa Roma.

Edna alikuwa akijua Roma ni mtu mzito sana huko duniani kutokana na umiliki wake wa pesa nyingi , lakini hata hivyo hilo hakutakaka bisa kulizingatia , yeye hakuwa akipendezwa na Maisha ya Roma namna anavyoishi na alipanga kumfanya kuwa Siriasi.

“Eti niko Special…haha.. Ingekuwa ni kwenye kuua ningeona maana ya Pointi zao lakini kuongoza kampuni sina uspecial wowote”Aliwaza Roma kwenye akili yake , huku Daudi na Wendy wakimwangalia.

Ukweli ni kwamba Edna pia alikuwa ameshawaambia mafanikio ya Roma aliokuwa ameyafanya kwenye kampuni , katika dili la Yamakuza ndio maana wawili hao waliamini Roma atakuwa ni Giniasi na wana mengi ya kujifunza kutoka kwake.

Baada ya maelekezo hayo kutoka kwa Edna Daudi na Wendy waliondoka kwa ajili ya kuandaa mazingira ya ufunguzi wa kampuni wiki zijazo ,ila Roma hakutoka alimsogelea Edna kwenye meza yake.

“Mke wangu Mtiifu , kuwa na huruma na mimi , kwanini tusitafute mtu tu wa kuongoza kampuni , sitamani kabisa kupewa mkampuni niuongoze”Aliongea Roma kama kawaida yake , licha ya kuonekana hakuwa siriasis , ila ni ukweli Roma alikuwa akimaanisha hakuwa na uwezo wowote wa kuongoza kampuni kwakua hana Elimu hio.

“Kwanini , mbona unaongeka kuwa kigeugeu?”Aliongea Edna huku akiendelea kuangalia tarakishi yake.

“Sina uzoefu wa kutosha ndio maana , naweza nikaua kampuni yako”

“Hilo lisikupe shida kabisa , unachotakiwa ni Kwenda asubuhi kazini na kukaa kwenye kile kiti chako cha kibosi na kufanya maamuzi baadhi ya maswala makubwa ya kikampuni , kuhusu uendeshaji Daudi na Wendy nawaamini wafanya kila kitu , hutakiwi hata kujihangaisha”Aliongea Edna kwa msisitizo.

“Sawa , ila nimezoea sehemu yangu ya kazi ndani ya PR”

“Kucheza gemu ndio kuzoea!, Sasa nakuambia hivi kama ukienda kinyume na ahadi yako nitahakikisha wapenzi wako wote ndani ya hii kampuni nawafukuza,”Aliongea Edna kwa hasira na kumfanya Roma ashangae.

“Usishangae nina uwezo huo , kampuni hii ni ya kwangu na namiliki hisa Zaidi ya asilimia tisini hivyo ninaweza kufanya chochote, ili mradi tu ukubaliane na kuongoza kampuni , usisahau kuna yule rafiki yako injinia nitamfukuza pia”Aliongea Edna.

“Kama ni hivyo je ushafanya maamuzi ya kuishi na mimi milele kama mume na mke?”Aliuliza Roma na yeye akiwa siriasi na kumfanya Edna apepese macho kama mtu ambaye hakuwa ametegemea hilo swali.

“Ninachofanya hapa ni kutumia Rasilimali watu katika kampuni yangu , kuhusu mambo mengine nitaangalia na utendaji wako wa kazi…”Aliongea Edna kwa sauti ndogo na ya kusita sita .

“Okey Wife kama huogopi kupoteza hela zako nitakuwa Director”

“Hata usijali nitakuwa makini na kila kinachoendelea kwenye kampuni”

“Okey wife , ila nina ombi moja”

“Mh..”

“Nataka niwee na uwezo wa kurudi ndani ya kampuni muda wowote na nafasi yangu ndani ya PR iendelee kuwepo”Aliongea Roma na kumfanya Edna afikirie kidogo na kisha akamwangalia Roma.
Anataka kuwa karibu na wanawake zake”Aliwaza Edna kabla ya utingisha kichwa na kukubaliana na Roma.
 
SEHEMU YA 171

Naam ni siku nyingine kabisa , siku ambayo Roma na Edna walikuwa wakielekea Ufaransa , Roma alikuwa tayari ashajiandaa na sasa alikuwa eneo la Sebuleni akiwa amesimama na Sophia aliekuwa akimuweka Tai vizuri , Roma alitabasamu na kumuona Sophia kama mwanamke ambaye yupo tayari kufanya vitendo ambavyo vilitakiwa kufanywa na Edna mke wake.

“Uitumie hio nafasi vizuri”Aliongea Sophia na kumfanya Roma amwangalie.

“Unamaanisha nini Sophia?”

“Unaenda na Sister Ufaransa , hakikisha unafanikisha wajibu wako kama mwanaume”Aliongea Sophia na kumfanya Roma atabasamu , alikuwa ashajua ni jambo gani Sophia alikuwa akimwambia.

“Naona ushakata tamaa ya kuwa mke wangu”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la kifedhuli.

“Utajua kama nimekwama au sijakwama”Aliongea Sophia na kisha kutoka aliposimama Roma baada ya kumuona Edna aliependeza akishuka kutoka juu , Edna leo hii hakuwa amevalia kama bosi , bali alivaa kama mwanamke anaeenda ‘Vacation’ , alikuwa amevalia suruali ya Jeans ya Bluu na Tisheti kubwa nyeupe iliokuwa na maandishi makubwa ya ‘Perfect Girl?’ Roma aliishia kutabasamu na hata Sophia alitabasamu baada ya kuona Edna kavaa hayo mavazi na kumuoneshea Dole gumba na kumfanya Edna atabasamu na Roma alimsaidia Edna kubeba mkoba wake wa nguo.

“Wife umependeza , leo hauonekani kama Bosi wa kampuni kubwa”Aliongea Roma na Edna alitabasamu na kisha alitembea uelekeo wa jikoni kwa ajili ya kumuaga Bi Wema , lakini kabla hata hajafika Bi Wema alitokea.

Bi Wema alikuwa na furaha ajabu tokea siku Edna alivyomwambia juu ya safari yao ya Kwenda Ufaransa na Roma , aliamini mpaka hapo Roma ashindwe mwenywe tu , ila kila kitu kishajilengesha na alitarajia siku Edna akirudi hapa ajiandae kwa ajili ya kuweka maizingira ya Chumba cha Edna kwa ajili ya Roma kuhamia Rasmi.

Baada ya dakika kama hamsini hivi Roma walikuwa washafika ndani ya uwanja wa Ndege wa JNIA kwa ajili ya safari yao ya kuelekea Ufaransa, Ndege ambayo walikuwa wakitegemea kusafiria , ilikuwa ni ya Shirika la Emirates.

Edna na Roma ndio waliokuwa wakionekana kuwa wa umri mdogo ndani ya Daraja la kwanza ndani ya ndege hii , na kama ujuavyo Daraja la kwanza mara nyingi halina siti nyingi sana , lakini pia ni ghali sana kupanda ndege na kununua tiketi ya Daraja la kwanza , na mara nyingi abiria waliokuwa wakisafiri na Daraja la kwanza ni wale wazee wenye pesa ambao walikuwa na afya sizisokuwa imara.

“Unajua natamani kukupiga kibao jinsi unavyonikodolea macho”Aliongea Edna na hii ni baada ya Roma kuangalia namna Tisheti ya Edna ilivvytuna , waswahili wanasema mtoto saa sita , hii ndio ilivyokuwa kwa Edna Tisheti ambayo alikuwa amevaa ilimkosha sana Roma na alijjikuta akishindwa kujizuia kabisa na kukodolea manyonyo ya mke wake na sura ya kifisi. Roma alijiambia kama isingekuwa ukauzu wa mke wake , angekuwa ashapeleka mkono na kuyagusa.

Jana yake wakati akiwa anaiwazia safari , alijiambia itakuwa ni safari ndefu kwakua hata pata hata upenyo wa kucheza cheza na warembo wanoahudumu kwenye ndege, lakini kwa jinsi mke wake alivyovaa , alijiambia hii safari sio ndefu kama alivyodhania.

“Babe Edna yaani unaonekana mrembo mno siku ya leo , Siku zote sikupata nafasi ya kuangalia kwa ukaribu hivi, ila kwasababu safari yetu itakuwa ndefe hivi , yaanni nitaangalia mpaka nichoke mwenyewe”Edna alijikuta akiona aibu kwa maneno ya Roma.

“Huna aibu yaan..”Aliongea Edna , ukweli hakuwa akipenda namna Roma alivyokuwa akimwangalia na alikasirika na kufurahi kwa wakati mmoja na hata yeye hakujielewa kwani moyo wake ulikuwa ukidunda isivyokawaida.

Upande wa kulia kwao kulikuwa kumekaa wazungu wawili wa umri mkubwa hivi kama miaka sabini , mwanamke na mwanaume na walikuwa wakiwaangalia Edna na Roma na kisha kutabasamu na kuongea kwa Kihispania Lugha ambayo Edna hakuwa akiifahamu , lakini kwa muonekano wa hao wazungu alijua kabisa wanawaongelea na alimgeukia Roma baada ya kukumbuka Roma ni Gwiji wa Lugha.

“Wanaongea nini?”Aliuliza Edna.

“Yule mwanamke kasema sisi ni wapenzi tuliobarikiwa na yule mwanaume kasema , Nilijua watu Weusi hawapo Romantic kabisa , kumbe wako vizuri tu kama sisi Wazungu”Alitafsiri Roma huku akiweka tabasamu lakini Edna aliwaangalia wale wazungu na wakamwangalia na kutabasamu na akaona aibu.

“Unanidanganya , unaninyanyasa na uongo wako kisa sijui kihispania sio?”

“Unafikiri mimi Muongo wamesema hivyo , kama ningetaka kubadilisha maneno ningesema tu , ‘Oh Yule mwanamke ni Mrembo sana na anaendana sana na yule mwanaume , inaonekana Mungu pekee ndio kawakutanisha na ninavyoona pale yule mrembo ndio kaanza kumtongoza mwanaume , huoni mwanaume alivyokuwa na mwili uliojengeka kimazoezi ugonjwa wa wanawake wengi”

“Nyamaza..”Aliongea Edna hakutaka kusikiliza Zaidi na Roma alinyamaza kweli , huku Edna akiinua mkono wake uliokuwa na saa ya Patek Phillipe saa ya Gharama kubwa na unaambiwa saa hio bei yake ni sawa na Range Rover Sport.

“Ni Zaidi ya lisaa tokea kuanza safari..”Aliongea Edna na kisha akaegamia Siti hio ya ndege.

****

Wakati Edna na Roma wakiwa angani kuja Ufaransa , ndani ya jiji la Paris kwenye jengo moja lililokuwa katikati ya jiji , jengo ambalo lilikuwa likitambulika kama makao makuu ya Polisi jiji Parisi chini kabisa ya vyumba vya Ardhini kuna ofisi iliokuwa ikifahamika kwa jina la Ofisi Namba Saba.

Ni ofisi ambayo ilikuwa na tarakishi nyingi na kwa haraka araka utafahamu ni kwamba hapa ndani ni ‘Monitoring Room’, Ofisi ilikuwa na takribani watu kumi waliokuwa wakichezesha vidole vyao kwenye Skirni huku wakiangalia maeneo yote ya jiji zima la Paris.

Muda huo huo wakati wazungu hao wanaendelea kuchezesha vidole vyao kwenye tarakishi zao mlango wa chuma ulisikika ukifunguliwa na akaingia bwana mmoja mzungu umri wa miaka Arobaini hivi mwenye uwalalaza alievalia mavazi ya kipolisi bwana huyu anafahamika kwa jina la Depney, baada ya kuingia ndani ya hiki chumba alisogelewa na mwanaume mmoja kwa heshima kabisa na kuinamisha kichwa chake kwa ishara ya heshima.

“Chief, is there anything you need?(Chifu kuna kitu chochote unataka?”.

“Where’s Fodessa?”Aliuliza kwa sauti yake nzito kweli akimaanisha Fodessa yuko wapi.

“Chief Msaidizi alikwenda kukusanyika na viongozi wa mashirika ya watumia nguvu za giza na vikundi vya mamluki kutoka Amerika Kusini na Asia Magharibi. Ninaamini atarudi hivi karibuni”Aliongea kwa kifaransa.

“Humph. Il est étonnamment libre. Est-ce que l'accueil des dirigeants étrangers de la pègre est son travail maintenant”

“Siku hizi anaonekana kuwa na muda mwingi wa kujiachia , mpaka kazi ya kukutana na Mamluki imekuwa kazi yake ya kuwakaribisha nchini”Aliongea kwa Kifaransa, lakini muda huo huo mlango ulifunguliwa na mwanaume aliekuwa amevalia sare za jeshi la polisi , huku akiwa ameshilia kofia mkononi akiingia , alikuwa na nywele nyeupe tunaina Blonde hair

“Kaimu Chifu mkuu wa Ofisi namba saba Foddessa, Ninaripoti”Aliongea yule mwanaume huku akikakamaa mwili.

“Ulikuwa wapi?”

“Nilienda kwenye kikao cha siri kilichokuwa kikihusisha wageni wa kijeshi kutoka kundi la Panther (Panther Mercenary Group) na kundi la Bahari Mfu..”Kabla hajamalizia alijikuta akipokea bonge la Teke kutoka kwa Dipney. Ambalo lilimkusanya Mzima mzima na kutua chini na Dipney hakuishia hapo tu baada ya kuona katua chini kama Mende alimkanyaga kwenye kifua na buti lake la kijeshi.

“Unasema….Kupokea Mamluki ,,, hivi unaelewa kuwa wakati unapokea Mamluki wako nilikuwa nikifokewa na Mheshimiwa Raisi kama Mbwa”Aliongea Dipney huku macho yake yakiwa mekundu mno na kuna jambo ambalo lilionekana halikuwa sawa ndani ya Paris , kwani sio kawaida kwa mkuu wa jeshi la Polisi kufokewa kama mtoto na Raisi.

“Mwanaharamu. Unafikiri una umuhimu wowote hapa?! Hebu niambie! Tangu kuanzishwa kwa hii Idara na Charles de Gaulle, ambayo sasa ni sisi Ofisi ya Saba katika Kurugenzi kuu ya Usalama chini ya DGSE, tumekuwa na mashujaa wengi na majasusi wabobezi ! Lakini nikuambie wewe, Fodessa, hautawahi kuja kuwa mmoja wao!”Aliongea kwa Hasira huku akimuongezea na buti na kufanya wafanyakazi waliokuwa hapo ndani kujifanya hawajasikia chochote na kujiweka bize.

“Fodessa nikukumbushe tu kwamba ni usaliti uliofanywa na mababu zetu enzo hizo ndio maana mtu kama wewe ukazaliwa , wewe ni NAZI na unanuka usaliti wa Damu ya Kijerumani na kama nisigeshurutishwa kukupandisha vyeo , ungebakia tu kuwa komandoo wa kawaida ndani ya jeshi na sio ndani ya kitengo hiki muhimu ndani ya Taifa”

Sasa mpaka hapa unatakiwa kuelewa kitu kimoja kwanza kabisa DGSE ni kirefu cha Directorate-General for External Security hili ni shirika la kijasusi la Ufaransa kama yalivyo mashirika mengine ya kijasusi kama vile CIA .

Ofisi namba saba licha ya ofisi hii kuwa ndani ya jengo la makao makuu ya jeshi la polisi , lakini ofisi hii ilikuwa ikijitegemea kwani ilikuwa ikichukua maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa DGSE lakinni wakati huo huo kushirikiana na jeshi la Polisi la Ufaransa , nia na madhumuni ya kuundwa kwa idara hii ni kwa ajili ya kulipa nguvu jeshi la polisi katika kugundua wahalifu ndani ya jiji la Paris, hii idara ya Ofisi namba saba ni kama vile useme Shrikika Tanzu la CIA(Central intelligence Agency) lifahamikalo kwa jina la NSA(National Security Agency) ( rejea kitabu changu cha masaa mawili ya kumbukumbu.) lakini idara hii pia ikifanana sana na FBI ya kule Marekani kwani zote zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nchi inakuwa salama kwa mtu anaeingia na anaetoka.

“I, Fodessa, will never forget Director’s kindness in my entire life.”Aliongea kwa kingereza huku akimaanisha kwamba hatokuja kusahau matendo ya kikarimu ya Dipney.

“Utajua mwenyewe , siwezi kukuachia ukafanya uchunguzi wa wa chanzo cha tukio la Kigaidi liliotokea na vikao vya siri vinavyoendelea hapa Parisi lakini pia Utambulizi halisi wa Apollo, siwezi kupoteza kazi kwa ujinga wako mimi”Aliongea kwa Kifaransa. Akiwa na msisitizo , lakini Fodessa aliishia kujikung`uta vumbi.

KITAKACHOTOKEA SIO POA

TUKUTANE WIKIEND
NICHEKI WATSAPP 0687151346 KAMA UNAHITAJI KUSOMA KWA NJIA YA WATSAPP
 
Wahusika ni wengi mno hadi sasa wananichanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…