singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
-
- #1,061
SEHEMU YA 194
Ni baada ya lisaa Edna na Roma walikuwa ndani ya hospitali moja ndani ya jiji la Paris huku kitandani akiwa amelala Harry , pembeni akiwepo mama yake Harry ambaye alikuwa amepewa taarifa ya uwepo wa mtoto wake hospitalini.
Harry alikutwa na ugonjwa wa kupungua Damu yaani Anaemia . licha ya vipimo vya daktari kuwa na ukakasi mwingi kutokana na hali ya ajabu aliokuwa nayo Haryy lakini aliishia kwenye hitimisho la Anaemia.
Mwanamke wa kizungu ambaye ni mama yake Harry alionekana kuwa kwenye majonzi mengi , kwani ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kwa mtoto wake kupata shida ya aina hio.
“Thank you so much. Our Harry had nothing wrong with him for the longest time, I really have no clue why he had such a sudden change.”
“Asanteni sana , Harry hakuwahi kupatwa na tatizo la kiafya kwa muda mrefu, nashindwa kuelewa ni nini kimemkumba ghafla”Aliongea mwanamke wa kizungu ambaye alikuwa mama yake Harry huku akiwaangalia Edna na Roma.
“Sio shida kubwa. Daktari alisema hatakuwa na matokeo mabaya yoyote. Ni kawaida kwa hali kama hizi kutokea kwa watoto. Unapaswa kuwa mwangalifu katika siku zijazo."Aliongea Roma , lakini kwa upande wa Edna alijua Roma alikuwa akidanganya kwani kilichompata Harry sio jambo la kawaida kabisa.
“Harry washukuru Uncle na Aunt , ndio waliokusaidia”Aliongea mama yake Haryy.
“Asante Uncle ,Asante dada”Aliongea Haryy akiwashukuru Roma na Edna kwa kumsaidia.
Edna na Roma kwakuwa walishamfikisha Harry sehemu husika, waliona hakuna lingine la kufanya hapo hospitalini ndio maana waliaga na kuondoka mpaka sehemu ambayo walikwa wameacha gari yao.
“Edna una mpango wa kukaa siku ngapi hapa Paris?”Aliuliza Roma.
“Kwanini unauliza?”
“Wewe nipe jibu?”
“Nimeamua kushiriki angalau kwa siku mbili kwenye maonyesho ya fasheni, vipi utanataka kurudi?”Aliuliza Edna pasipo kuelewa kuwa Roma alikuwa akiuliza kutokana na kwamba alikuwa na mpango wake kichwani wa Kwenda kuhudhuria mkutano wa siri unaofanyikia huko Le havre
“Nilitaka kujua tu mke wangu , hakuna kingine Zaidi”aliongea Roma huku akipotezea ile mada na muda huo huo walikuwa washalifikia gari lao lililowaleta hapo hospitalini.
Edna ndio aliekuwa wa kwanza kufungua mlango, lakini ajabu alijikuta akifunga kwa nguvu baada ya kuufungua na kumfanya Roma ashangae na kusogelea mlango huo na kuufungua na hapo ndipo alipoelewa kwanini Edna alikuwa amefunga mlango baada ya kuufungua , na hio ni kutokana na Stern na Alice walikuwa wakinyanduana kwenye gari paisipo ya kua na wasiwasi kabisa, na ilibidi Roma na yeye afunge mlango kusubiria wajiweke sawa ndio waingie.
“Jamani mtusamehe kwa kuwachelewesha , mnaweza kuingia sasa tushamaliza”Aliongea Alice bila aibu.
“Hata kama mnafanya mambo yenu pasipo kujali mazingira , hakikisheni mkimaliza upuuzi wenu mhakikishe mnasafisha , isije ikaonekana mke wangu ndio kaacha maharufu mabaya mabaya kwenye gari”Aliongea Roma baada ya kuingia kwenye gari , lakini kwa upande wa Edna alionekana kukosa utulivu , ukichanganya na harufu mbaya aliokuwa akiweza kuinusa kwenye pua zake.
Naam ilikuwa ni siku nyingine kabisa Asubuhi , Roma ilibidi aagane na Edna kwani hakuwa na mpango wa Kwenda kwenye maonyesho ya Fasheni bali alitaka aende kuhudhuria kikao cha siri , hivyo ilimbidi siku hio Edna kuondoka peke yake , Roma hakuwa amempa taarifa kamili Edna kama alikuwa anahudhuria kikao cha siri bali alitoa sababu nyingine kabisa ambayo wala Edna hakujihangaisha sana kufikiria juu ya sababu Roma aliotoa.
Edna ndie aliekuwa wa kwanza kutoka ndani ya jengo la hoteli na mpango wake siku hio ilikuwa ni kabla ya Kwenda kwenye maonyesho apitie hospitalini kwa ajili ya kumtembelea Harry kutokana na ahadi aliowekeana na mtoto huyo,
Stern na Alice ni kama walikuwa wakimsubiria Edna , kwani ile Edna anatoka kwenye mlango wa hoteli walimsogelea huku wakimuomba waongoke kwa Pamoja , Edna licha ya kutopenda kutumia gari moja na hao wapenzi , ila hakuwa na jinsi kwakua hakutaka kuonekana mtu mwenye Roho mbaya.
“Nitapitia kwanza Kumtembelea Harry kabla ya Kwenda kwenye maonyesho , kama halitawasumbua hilo tunaweza kuondoka wote”Aliongea Edna.
“Miss Edna wala hata usiwe na hofu , sisi tutakufuata popote pale unapoelekea”Aliongea Alice na Edna hakutaka kujishughulisha nao Zaidi ya kuingia kwenye gari na kumruhusu Dereva kuendesha mpaka maeneo ambayo angeweza kununua zawadi kwa ajili ya mtoto Harry , na kwakua Dereva alikuwa mzoefu , basi aliweza kuendesha gari mpaka sehemu husika , kwenye duka maalumu la mapambo mbalimbali Pamoja na maua , Edna alichagua mdoli mkubwa wa Sungura na kulipia na kisha aliamuru dereva kuendelea kuendesha mpaka Hospitalini.
Jambo ambalo Edna hakuwa amelijua kwa wakati huo ni kwamba kulikuwa na gari ambayo ilikuwa ikiwafuatilia tokea wanatoka hotelini na hata Edna alipokuwa ametoka kununua zawadi kwa ajili ya Harry Gari hio aina ya Bentley ilikuwa nyuma yao na baada ya wao kuondoka ile gari iliwaungia kwa nyuma na kuendelea kuwafatilia.
******
Upande mwingine kwenye bandari ya Le Havre , muda wa asubuhi sehemu ambayo meli kubwa ya Luois XVII ilipokuwa imesimamishwa , alionekana Fodessa akiwa na Boltoni wakiwa wamesimama , mbele kabisa ya meli hio walionekana walikuwa wakikaribisha wageni ambao walikuwa wakihudhuria kikao cha siri , kikao ambacho kilikuwa kikifanyika katika moja ya kambi ya kijeshi , iliokuwa ikipatikana ndani ya Le Havre.
Raia waliokuwa ndani ya hili eneo , licha ya kwamba walimuona Fodessa aliekuwa amevalia kombati ya jeshi , akipokea wageni , lakini hawakujishughulisha na kile kilichokuwa kikiendelea kabisa na walikuwa bize na majukumu yao yaliowafanya kuwa ndani ya eneo hilo la Bandari.
“Wamefika wageni wangapi mpaka sasa?”Aliuliza Fodesa huku akimwangalia Boltoni.
“Mpaka sasa wamefika wawakilishi wa kundi la Sea Eagles kutoka bahari ya Meditterranian , Dhoruba nyekund kutoka Marekani , Mossad , Zeros Organisation , Jaguar kutoka Amerika ya Kusini, Soviet Medal kutoka Urusi,Yamata Sect kutoka Japani….”Aliongea Boltoni huku ikionesha makundi mengi wawakilishi wake walikuwa tayari washafika.
“Kazi hii inaonekana kuwachosha sana , baada ya hiki kikao kuisha mtapatiwa likizo”Aliongea Fodesa huku akiangalia baadhi ya wafanyakazi wengine ambao wapo hapo kwa ajili ya kusimamia matayarisho ya kikao cha siri kinachoenda kufanyika.
Muda ule ule wakati wakiendelea kusubiria wageni , mara Mvua ilioambatana na wingu kubwa ilianza kunyesha na kumfanya Fodesa kushangaa , kwani muda mfupi tu ulipita hakuwa na dalili yoyote ya mvua.
“Kwanin inayesha Ghafla hivi?”
“Chief kuna wageni wanakuja”Aliongea Boltoni na pale pale walisogelewa na watu jamii ya Kijapani , mmoja akiwa ni mwanamke mwenye nywele ndefu , mtu mzima na mwingine akiwa ni msichana mdogo alievalia mavazi ya kitamaduni rangi ya bluu makadirio ya umri wa miaka kumi na tatu hivi , halafu mwingine alikuwa ni mwanaume aliekuwa amevalia joho la rangi nyeusi akiwa amelifunga na Kamba kiunoni , huku akiwa na Sime kubwa ndefu iliokuwa imefungwa kiunoni.
“Jamani tunaweza kuwatambua kwa majina yenu?”aliongea Fodesa.
“We’re from Takamagahara. I believe this is the first time I am meeting you. This one is Motakuto, I hope to get along well with you.”
“Tinatokea kundi la Takamagahara , Naamini hii ni mara ya kwanza kuonana , huyu hapa ni Motakuto , natumaini tutafahamina na kupatana vyema na nyie”Aliongea yule mwanamke mtu mzima akimtambulisha yule mtoto msichana mdogo kwa jina la Motukuto na kumfanya Fodesa amwangalie Boltoni kama mtu anaetaka maelezo.
“Chifu Takamahagara ni moja ya kundi kutoka Japani linaotumia nguvu za Zaida ni moja ya waalikwa ndani ya mkutano huu”Aliongea Boltoni na kumfanya Fodesa atingishe kichwa.
“Basi nafikiri Miss Motukuto hapa ndio anaekwenda kuwa mwakilishi wa kundi la Takamahagara?”
“Bwana Chifu umekosea , anaekwenda kutuwakilisha ni Jenerali mwenyewe”aliongea na kumfanya Fodesa kushangaa
“Yupo wapi huyo jenerali wenu?”
“Jeneral yule kule juu mlangoni?”Aliongea akinyoosha kidole na kumfanya Fodesa kugeuka na kweli alimuona mwanaume mwenye ndevu nyingi alievalia Keikogi(Mavazi flani ya kitamaduni ya kijapani) akiwa anawaangalia na kumfanya Fodesa ajiulize mtu yule kafikaje kule juu pasipo kupita kwao.
“Yule ndio Jenerali wetu , anafahamika kwajina la Nurarihyon, tunaomba mtuwie radhi kutokana na tabia ya jenerali wetu”Aliongea Motukuto.
“Hakuna shinda mnaweza kuendelea na kuingia kwenye meli”Aliongea Fodesa na kuwaruhusu wapite.
Kiufupi wageni wengi ambao walikuwa wamealikwa ndani ya huu mkutano walikuwa na sifa zao za kipekee sana, kuna waliokuwa walozi wa levo za juu kabisa ambao wamealikwa , kuna wapiganaji wakuu pia wamealikwa , makundi pia ya kimamluki pia yalikuwa yakihudhuria ndani ya mkutano huo, mbaya Zaidi ni ni kwamba ndani ya huu mkutano , kuna yale makundi ambayo yana uhasama na makundi mengine.
Zoezi la kupokea wageni lilikuwa kubwa mno kwani wageni walikuwa wengi sana ambao walikuwa wakihudhuria.
Baada ya kama masaa mawii ya kupita hatimae Roma aliekuwa akitembea kama analazimishwa akiwa alionekana akisogelea meli hio kubwa kwa ajili ya kuhudhutia , Fodesa na Boltoni ndio waliokuwa wakwanza kumuona