Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 197

Kila mmoja hapo ndani hakuelewa kwanini Roma alikuwa akisaidia watu kutoka upande wa Dark Parliament ,Sauroni mwenyewe alikuwa halewi bosi wake alichokuwa akifikiria , ila hakutaka kuuliza.

Lilith baada ya kuona Roma amekubali kumsaidia alijikuta hata nguvu kurudi upya huku akimshikilia vyema baba yake ambaye alipata mapigo ya kutosha kutoka kwa Kadinali Cruff.

“Are you really Pluto, the new Hades?”

“Ni kweli wewe ndio Pluto , Hades mpya”Aliuliza kadinali Cruff.

“Haina haja ya kunifahamu Kadinali, japokuwa sikupaswa kuwa upande wowote kwenye mapambano yenu , lakini nahisi nguvu kubwa ya uovu ndani yako”Aliongea Roma na kumfanya Gabriel amwangalie Roma kwa mshangao , hakujua ni kwanini Roma kaongea maneno hayo.

“Kijana acha kujigamba , ijapokuwa wewe ni sehemu ya Miungu watu kumi na mbili ,lakini huwezi kushindana na Nguvu ya Mungu”Aliongea Cruff lakini Gabriel aliekuwa akijua moto wa Roma ilibidi aingilie.

“Roma kaa nje ya hili la sivyo utapoteza kitu unachokipenda kwenye dunia hii”Aliongea Gabriel na kumfanya Roma kushangaa

“Unataka kumaanisha nini Gabriel”

“Hahaha… Hades tulijua tu utaingilia kwenye mipango yetu kama ulivyofanya kule Tanzania na tulivyofahamu uwepo wako hapa Ufaransa tulichukua tahadhari zote”Aliongea Cruff lakini Roma alishindwa kuelewa anamaanisha nini na kutokana na kutopenda kutishiwa amani palepale alipotea alipokuwa amesimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Cruff.

Lakini Kadinali na yeye hakuwa mzembe , ni kama alimtegemea Roma kwani ile Roma anaibuka na yeye alipotea na kuibuka mita mbili mbele

“Unajigamba sana kijana , Hebu onja kwanza joto la Jehanamu”Aliongea Cruff.

“Fireeeeee…!!!!” Aliongea Kadinali na palepale ulilipuka moto kama bomu na kumfunika Roma kiasi cha kumpekekea kutoonekana na kufanya hata Sauroni aliekuwa nyuma kuinuka kwa wasiwasi,

Moto ule ulidumu kwa dakika kama mbili hivi kabla ya kuisha na ile unazima alionekana Roma aliekuwa amesimama vilevile alivyokuwa mwanzo pasipo ya kuwa na jeraha lolote.

“Cruffy nishakwambia kabla ya kupambana na mimi lazima ujitakase kwanza la sivyo huniwezi kuniunguza na huu moto wako”Aliongea Roma na kumsogelea Cruff kwa spidi ya mwanga na ile anamfikia alimsomba mzima na Kwenda kutua nae kwenye ukutani na kumgonganisha kwa nguvu kiasi kwamba eneo lilitengeneza mtetemoo wa ardhi , huku akionekana kumshikilia kwenye shingo.

“Unajua kwanini nimeamua kuwa upande wa Dark Parliament?”aliongea Roma huku macho yake yakitoa mwanga wa Kijani , lakini Cruff alishindwa kujibu kwani alikuwa amekabwa vilivyo kwenye shingo.

“Miaka miwili nyuma wanajeshi wa Vatican walinishambulia wakati nilivyokuwa Rome, pasipo ya kuwa na kosa lolote wala kuwachokoza , nilitoa msahamaha , lakini inaonekana mnataka kurudia kosa”Aliongea Roma na Cruff hakutaka kufa kizembe alitumia uwezo wake wakuita nguvu , lakini haikuelewa Roma alimzibiti na nguvu ya aina gani , kwani kaditi alivyokuwa akiita nguvu , alishindwa kabisa kuipata.

“Roma usimuue Kadinali”Aliongea Gabriel kwa sauti akimwamrisha Roma.

“Sina sababu ya kumuacha hai, nachukia sana vitisho”Aliongea Roma.

“Una sababu ya kumuacha hai Roma , Mkeo Edna yupo kwenye mikono yetu”Aliongea Gabriel na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia Gabriel kwa hasira, ni kama hakuwa amemsikia vizuri.

“Unataka kumaanisha nini?Aaliongea Roma huku baadhi ya watu kama kumi waliobaki kwenye hili eneo wakimshangaa Gabriel ,h awakuelewa alikuwa akimaanisha nini.

Lakini Gabriel wala hakuongea chochote Zaidi ya kutoa kijisimu kidogo(Burner phone) , kama vile funguo ya gari na kuweka sikioni

“We’ll abandon our original plan. Cardinal Cruff has been defeated. Proceed with what you were going to do,”

“Tutaachana na mpango wa kwanza ,Kadinali Cruff kashindwa , endeleeni na kazi mliopangiwa”Aliongea kwa kupitia simu na kisha akakata na kumgrukia Fodesa ambaye muda wote alikuwa amejibanza kwenye kona , na haikueleweka kwanini muda wote hakuwa amekimbia na kuungana na watu wengine waliokuwa wamekimbilia kwenye meli, Fodesa alioenaka kuwa na roho ngumu kweli.

“Fodesa kuna tarakishi yoyote maneno ya karibu?”aliuliza Gabriel na kumfanya Roma amwangalie , hakujua ni kitu gani Gabriel walikuwa wamefanya kwa mke wake Edna.

“Ndio kuna tarakishi ambazo zipo ndani ya chumba cha mawasiliano”Aliongea Fodesa na Gabriel alitabasamu.

“Hades kuna jambo ninataka kwanza kukuonesha na ukishaona nadhani utafanya maamuzi aidha ya kutupatia teknolojia na kufuata maelekezo yetu au kumpoteza mkeo”

“Mimi sina shida , twende ukanionyeshe hiko unachotaka kuonyesha”aliongea Roma huku akianza kutembea yeye na kuachana na Kadinal Cruff.

Na ndani ya dakika kama mbili hivi , waliingizwa kwenye chumba kingine kikubwa ndani ya jengo hili ambalo lilikuwa limeharibiwa pakubwa kutokanana mtifuano uliotokea, ilikuwa ni sehemu ya mawasiliano ndani ya hii kambi.

“Deputy Director Fodessa, please turn on the monitor and switch to satellite mode,”Aliongea Gabriel huku akimwamrisha Fodesa kuwasha Tarakishi na kuunganisha na mawasiliano ya satilaiti.

Baada ya Fodesa kuunganisha mawasiliano ya Satilaiti palapale Skinri zote za komputa zilizokuwa zimefungwa ukutani zilionyesha eneo la baharini paisipo kuonekana kwa mtu yoyote kwenye hizo Skrini , lakini dakika moja mbele hatimae watu waliokuwa kwenye meli ya kivita, walionekana kwenye Skrini, walikuwa ni wanaume wengi waliovalia kombati za jeshi , huku wakiwa na chata ambalo Roma alikuwa akilikumbuka , walikuwa ni moja ya wanajeshi waliowateka siku ambayo walifika Ufaransa ,Sun Gold Totem, wanajeshi hawa walikuwa wapo kwenye meli ya kivita wakiwa wamesimama eneo ambalo mara nyingi kwenye meli za kivita ndege hutua na kuruka angani.(Deck)

Roma wakati akiendelea kuangalia kwa kukagua watu wote waliokuwa kwenye meli , hatimae walionekana wanajeshi wengine ambao walikuwa wamebeba watu begani ambao walikuwa wamefungwa na Kamba na baada ya kusogea kwenye Deck waliwashusha kama mizigo.

“Harry!!”Fodesa ndio aliekuwa wa kwanza kumtambua mtoto wake na Roma pia baaada ya kuangalia kwa umakini aliweza kuona sura ya Stern, Alice Pamoja na Mke wake Edna waliokuwa wamefungwa na wote walionekana kutokuwa kwenye kumbukumbu.

“Gabriel hii maaana yake nini, inamaana Vatican mmeamua kuungana na Apollo kuhujumu usalama wa dunia?”Aliuliza Fodesa kwa hasira kwani alikuwa tayari alishaelewa wanajeshi waliokuwa wakionekana kwenye Skrini walikuwa ni wa kundi la Apollo

Lakini Gabiel wala hakutaka kumsikiliza Fodesa Zaidi ya kufyura na kuendelea kuangalia kwenye Skrini na palapale kilionekana kivuri kikisogelea mbele , sehemu ambapo Edna na wengine wamewekwa chini.

Kile kivuli baada ya kusogea mbele kilifanya kuziba Skrini yote kwa ukubwa wake , alikuwa ni mwanaume alievalia mavazi ya kijeshi huku akiwa na alama kubwa ya ‘Sun Gold Totem’ kwenye kifua chake , kichwani alikuwa amevalia helmeti kubwa kama yale waliokuw awakivaa wanajeshi wa Kirumi hapo kale.

Kwa jinsi ilivyokuwa , ilionekana kabisa wanajeshi hawa walikuwa wamefunga Kamera ambazo zilikuwa na uwezo wa kunasa na sauti upande wa pili.

“I believe some of you may recognize me, but let me introduce myself… I am Apollo.”

“Najua wengi wenu huenda mkawa mnanifahamu , lakini ngoja nijitambulishe.. kwa jina naitwa Apollo”Aliongea kwa sauti nzito ilioweza kusikika na kila mtu aliekuwa ndani ya chumba hiki.

Kumbuka hapa ndani walikuwepo watu ambao hawakuwa wakizidi kumi , kwani wengine wote walikimbia , waliokuwa wamebaki ni Fodesa , Roma , Cruff , Gabriel na Lilith na baba yake na wanajeshi wengine wa The Eagles akiwemo Sauron.

“This must come as quite a shock to you I imagine, as to why I’m related to the Vatican, but I don’t think it warrants a discussion as of now. Let’s just leave it at mutual interests…that’s all.”

“Nadhani mpo kwenye mshituko mkubwa kwanini nina uhusiano na Vatican , lakini sio swala la kuzungumza kwa sasa na tutaliacha kwa manufaa ya pande zote mbili, ni hivyo”Aliongea kwa sauti nzito

“Haha…Ijapokuwa siamini kama kweli wewe ni Apollo, ninatamani kujua kwanini umeungana na Vatican, au ni kwasababu mnataka kuwa moja ya dini inayoweza kutawala Ulimwengu wote?’Aliongea bwana mmoja alieingia muda huo huo na haikueleweka alikuwa wapi , alikuwa ni Ajenti kutoka kundi la Dhoruba Nyekundu.

Baada ya Apollo kusikia yale maneno wala hakuongea chochote ,Zaidi ya kutoa ishara kwa wanajeshi wake waliokuwa kwenye hio meli ya kivita na palepale alisogezewa upinde flani wa Mshale wa kisasa kabisa ambao ulikuwa ukitumiwa kwenye karne ya kumi na saba huko Ujerumani.

Unachotakiwa kuelewa kuna utofauti wa upinde wa mshale inayotumika kwenye mataifa ya Asia na iliotumika Ulaya , kama ushawahi kuangalia muvi ya kizungu ya Arrows , basi utakuwa unanipata vyema.

Kilichokuwa kikifanyika upande wa baharini kilikuwa kionekana vyema , licha ya kwamba kulikuwa na giza kwani ilikuwa ni usiku kama wa saa nne , lakini taa kubwa kwenye meli ziliwafanya Roma na wengine kuona kila kinachoendelea.

Apollo baada ya kukabidhiwa ule upinde na mshale aliseti vizuri na kisha akalenga hewani na kufanya Fodesa na wengine wasijue anataka kufanya nini, kwani ilionekana sehemu waliokuwepo na kambi hii ya jeshi kulikuw ana umbali mrefu , kwani kama wangekuwa karibu na kambi Rada za jeshi la Ufaransa zingeweza kuwanasa.

“Foolish humans. Since you doubt my identity and capability, I’ll show you the difference between people and gods”

“Binadamu wapumbavu , kwasababu mnawasiwasi na ubini wangu Pamoja na uwezo wangu , nitawaonyesha tofauti iliopo kati ya Binadamu na Miungu”Aliongea Apollo na palepale akaachia mshale hewani na hakuna alielewa ni jitu gani ambacho Apollo alikuwa akikifanya , lakini dakika mbili mbele chumba kilianza kutoa mlio wa hatari kama Alarmu na kufanya eneo lote lijae mwanga mwekundu na Fodesa alibonyesha haraka haraka kuangalia Anga karibu na kambi na hapo ndipo alipotoa mshangao , kwani waliona kitu mfano wa Kimondo kikishuka kwakasi usawa wa jengo na dakika chache mbele , kilisikika kishindo cha aina yake kilichoacha mtikisiko eneo lote

Hakuna mtu alie elewa ni nini kimefanyika , lakini walibakia kwenye mshangao pekee.

“Apollo unataka nini kutoka kwetu , kwanini umemteka mke wangu?”aliuliza Fodesa kwa wasiwasi

“Mmeamini sasa?’

“Taja shida yako”

“Hahaha…. Hades sikutegemea kama unaweza kuhudhuria mkutano huo wa siri na ukaharibu mpango wangu , lakini hakuna kinachoharibika kabisa maana nilichukua tahadhari mapema”Aliongea Apollo huku akimpotezea Fodesa na swali lake.

“Persephone is now in my hands. I believe this warrants a discussion and hopefully the start of a good partnership… Ooh! Without forgetting your other woman is also in my Hand”

“Persephone yupo kwenye mikono yangu naamini nitamtumia kama kibali cha kuanza kwa uhusiano wangu mimi na wewe..Ooh bila kusahau mwanamke wako mwingine yupo kwenye mikono yangu”Aliongea Apollo na palepale akatoa ishara na muda ule ule alionekana mwanamke akiwa ameshikiliwa na wanajeshi akieletwa ndani ya eneo hilo, aliekuwa amefungwa kitambaa mdomoni , alieonekana uwa na kumbukumbu.

“Nadia…!”Roma alishangaa hakuelewa imekuwaje na Nadia akawa ndani ya hilo eneo kwani alikumbuka huyo mwanamke alikuwa Tanzania.
 
SEHEMU YA 198

Roma hakujua ni kwa namna gani Nadia aliweza kuingia kwenye mikono ya Apollo , lakini hata hivyo Apollo alimuona Nadia kama mwanamke wake , jambo ambalo sio kweli kwani Roma hakuwa na uhusiano wowote na Nadia.

“Ushirikiano gani unataka kutoka kwangu?”aliuliza Roma

“Mtu pekee ambaye ninapenda kuwa na ushirikiano nae ni wewe Hades , kama utakuwa upande wangu ,nitakufanya utawale Bara lote la Ulaya , huku tukizidi kujipanua Zaidi duniani kote”aliongea Apollo.

“Hahah…Apollo…” Wakati wengine wakiwa kwenye wasiwasi Roma aliachia cheko kiasi kwamba mpaka machozi yalikuwa yakimtoka na haikueleweka alikuwa akicheka nini.

“Unacheka nini Hades?”aliuliza Apollo

“Hapana … nimefurahishwa na ndoto zako kubwa”Aliongea Roma

“Hades huu ulimwengu umeoza , Bila ya kufanya ubatizo wa Damu juu ya watu wanaopenda pesa , hakuna binadamu ambaye anaweza kutoka kwenye vifungo ,Hades sisi ndio wenye jukumu la kuwasaidia hawa binadamu , Because we are Gods,’ whether or not you understand is none of my business; I don’t expect anyone to understand it. All I want to know is whether you accept it,”Aliongea Apollo akimaanisha kwamba haijalishi Roma anakubaliana na yeye au la , ila anataka kujua msimamo wake.

“Okey! Unataka nishirikiane na wewe kivipi?”Aliongea Roma na kufanya kila mtu hapo ndani kumwangalia kwa wasiwasi, kwani walielewa Kama Roma ataungana na Apollo , basi Fodesa Pamoja, Lilith na wengine wasingepona.

“Ninachotaka kutoka kwako ni kutowadhuru Gabriel , Kadinal Cruff Pamoja na Fodesa , nina mpango nae hapo baadae”Aliongea Apollo na kumfanya Fodesa kushangaa.

“Una,,unataka nini?”Aliuliza

“Nataka uelekekee kwenye maabara ya kambi na uchukue ‘End Button’ ambayo mtaweza kuitumia mkiwa nje na kisiwa”Aliongea Apollo na kiumfanya Fodesa kushangaa mno, lakini wenzake hawakuelewa Apollo anamaanisha nini akisema ‘End Button’.

“Fodesa End Button ndio nini?”Aliuliza Lilith.

“Ni kama swichi ya kulipua mabomu ya nyuklia yaliotegeshwa ndani ya hii kambi”Aliongea Fodesa kwa wasiwasi na kila mmoja akashangaa , kwani mpaka hapo walielewa Apollo alikuwa akitaka kuilipua kambi yote.

Ndio asilimia kubwa ya kambi nyingi ambazo zilikuwa zikimilikiwa na majeshi ya nchi kubwa kama vile Marekani , Ufaransa na Ujerumani wanatega mabomu ya siri kwenye kambi zao , maana ya kuweka mabomu hayo ni kwa ajili ya usalama , kwa mfano kama Adui akaingia na kuteka kambi , kinachofanyika ni kubonyeza tu na kisiwa chote kinapotelea baharini , ijapokuwa athari za mabomu ya nyuklia zinaweza zikawa kubwa , lakini zisingesambaa eneo lote la ufaransa ni kilimita kadhaa kutoka kwenye kambi.

“Hades watu wote ambao wapo kwenye hiko kisiwa ni kama kunguni tu kwako , nahitaji uwaue kwa namna unayoona inafaa wewe mwenyewe ili ni utangazie ulimwengu juu ya utawala wangu”Aliongea Apollo.

“Labda kwenye ndoto …”Aliongea Naurinyhyon kutoka kundi la Takamagahara na kupotea aliposimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Fodesa na kumuwekea panga kwenye shingo kwa ajjili ya kummaliza na muda wote huyu jenerali wa kundi hili haikueleweka alikuwa amejificha vipi kwani uwepo wake ni kama haukuonekana kwa waliokuwa hapo ndani na walishangaa akiwa amemuwekea Panga lake Fodesa.

“Nikimmaliza Fodesa hakutakuwa na uwezekano wa kupata kitufe cha kulipua nyuklia na hii kambi itabaki salama”aliongea Jenerali.

“Hebu kuwa na subira”Aliongea Roma na kumsogelea jenerali Nauryhyon na kumvuta nyuma.

“Hades unataka alipue hiki kisiwa kwa maagizo ya huyo mpumbavu”Aliongea kwa hasira

“Mfalme Pluto Apollo ametuambia kwamba sisi Vatican ndio wenye jukumu la kutengeneza ulimwengu mpya , ulimwengu wenye nuru ya bwana ,Mbali na dhambi hivyo hapa kisiwani sisi tunapaswa kuondoka na wewe utabaki kwa ajili ya kumaliza kazi”aliongea Gabriel.

“Fodessa fanya kama ninavyokuambia acha woga, Hades na wewe muda wa mazungumzo ushaisha nataka ufanye maamuzi sasa hivi , la sivyo mkeo atakuwa halali yangu”

Roma hakumjibu Apollo Zaidi ya kumgeukia Fodesa , alitaka kujua Fodesa atafanya maamuzi gani ,kwani hata yeye mke na mtoto wake walikuwa chini ya Apollo.

“Fodesa unafikiri ni maamuzi gani tunapaswa kufanya?”Aliuliza Roma na Fodesa baada ya kuulizwa swali hili alisogelea Ukuta na kisha kupiga ngumi nzito ukutani kwa hasira mno kiasi cha kupelekea mikono yake kuvuja damu huku aking`ata meno kwa hasira.

“I won’t detonate the bomb!”Fodesa alitoa maamuzi kwamba hayupo tayari kulipua mabomu na kufanya kundi lote kumwangalia kwa mshangao , walimuona Fodesa kama mtu jasiri , kwani mpaka hapo alikuwa akimaanisha kwamba yupo tayari kukosa familia yake , ili tu asiruhusu mabomu kulipuka , yaani kwa maneno marahisi alikuwa akiweka maslahi ya taifa mbele ya familia yake.

Sasa Fodesa alikuwa ashaonyesha msimamo wake , aliebaki alikuwa ni Roma kutoa na yeye maamuzi yake , kama yupo tayari kumlazimisha Fodessa kulipua mabomu ili amuokoe Edna au aungane na Fodesa na kuruhusu Edna na wengine kufa.

“Wewe mjinga sana Fodesa , hili taifa litakusaidia nini”Kadinali Cruff aliongea kwa hasira , lakini Fodesa hakumjibu chochote Zaidi ya kusogea mpaka mbele kabisa na kuangaliana na Appollo kupiia Monita.

“I refuse, Apollo. You won’t be able to control me using my wife and son! I, Fodessa, am unlike the despicable, corrupt scums who would act in the name of God!,”

“Ninakataa , Apollo, Hauwezi kuniendesha kwa kumtumia mke wangu na mtoto wangu , Mimi Fodesa sipo kama hao Wapuuzi na mafisadi ambao wapo tayari kufanya jambo lolote baya kwa kutumia jina la Mungu, ”Aliongea Fodesa na akaendelea

“Tena mimi ni Mfaransa ambaye nimezaliwa na mchanganyiko wa Mjerumani Pamoja na Mfaransa , watu wanaweza kuniona kichaa , lakini nipo tayri kufanya jambo lolote kwa ajili ya nchi yangu”Aliendelea kuongea Fodesa kwa msisitizo huku macho yakiwa mekundu, alionekana yupo tayari kwa ajili ya kuwatoa kafara mtoto wake na mke wake kwa ajili ya taifa.

Kila mtu alieweza kusikia maneno ya kijasiri kutoka kwa Fodesa , wengine walimheshhimu na wengine wakajawa na majuto makuu ya kumtegemea wakiwemo Gabriel.

“Hahaha… Fodesa , Fodesaaa, unafikiri kuna kinachobadilika kisa tu hutaki kunipatia Switch na kulipua hio kambi”Aliongea kwa kejeli na kisha akaingiza mkono kwenye kombati yake ya jeshi na kuchomoka na Rimoti ya rangi nyeusi ndogo sana inayofiti kwenye kiganja cha mkono na kisha akamuonyesha Fodesa.

“Umee..umewezaje kuipata..”aliongea Fodesa huku akirudi kinyume nyume kwa mshangao.

“Hahaha… msinichukulie poa unafikiri hayo mabomu yanaendeshwa na Rimoti moja tu iliopo hapo kambini, nilitaka kukusaidia tu kama sehemu ya shukrani zangu kwako , lakini unaonekana kutonielewa”Aliongea Apollo.

“Hades , Kwasababu Fodesa hayupo tayari na ashachagua upande wake , ni zamu yako kufanya maamuzi, utawaondoa watu wote wa Vatican kutoka kwenye hio kambi na uhakikishe wengine wanabaki”Aliongea Apollo na kufanya hata Sauroni amwangalia Roma ana maamuzi gani juu ya hilo , ukweli hakuna ambaye alikuwa na uwezo wa kushindana na Roma hapo ndani , hivyo waliona Roma akiamua kuwabakisha kisiwani , uwezo huo anao kwa asilimia mia moja , hivyo Maisha yao yalikuwa kwenye mikono ya Hades , lakini licha ya hivyo walikuwa na asilimia ndogo sana ya kupona kwani mke wa Hades Madam Persephpne yupo kwenye mikono ya Apollo , hivyo ilikuwa ni kitendo cha Roma kuchagua kumuokoa mke wake au kuwaokoa wao.

Roma aligeuka na kuwaangalia Gabriel na Kadinali Cruff ambao muda wote macho yao yalionyesha ushindi na kisha aliwasogelea.

“Haha, Your Majesty Pluto, you are making the right choices.” Aliongea Kadinali Cruff , licha ya kwamba alipokea kipondo dakika chache nyuma , lakini alikuwa yupo tayari kuungana na Roma kwa ajili ya mpango wao mkubwa wa kutawala Dunia yeye Pamoja na mwehu Apollo.

“Unauhakika…. “Aliongea Roma mara baada ya kumfikia Kadinali , lakini kabla Kadinali hajaongea neno , macho ya Roma yalibadilika palepale na kua ya Njano kama vile ni Roboti na pasipo ya Kadinali kutegenea Roma alikunja ngumi na kumtandika nayo Kanidali utosini.

“Pwaaa..!!!”

Ni kama tikiti lililipasuka kwa kupigwa na kitu Kizito ndio kilichotokea kwa kadinali kwani palepale ubongo wake wote ulisambaa eneo zima , huku vipande vipande vya Nyama vikitapakaa na kufanya kila mtu kutoa macho kwani hawakuwahi kuona tukio kama hilo kwenye Maisha yao , Kilikuwa ni kifo cha kikatili mno.
 
SEHEMU YA 200

Kila mmoja alitegemea Roma kuwaondoa wavatican hapo kambini , lakini ajabu alimpasua Kadinali Cruff kichwa chake , watu waliokuwa kwenye hofu,akiwemo Fodessa ,tumaini jipya lilirudi na kuona Roma kawachagua.

“You..yo..Dare to..”Aliongea Gabriel huku akirudi nyuma kwa wasiwasi mno , lakini Roma hakumjali ,kwanza alitoa tabasamu lake la kishetani na kumwangalia Gabriel.

“Pumbavu .. ulifikiri ningemuacha hai huyu mpuuzi mwenzako ,Mungu alimpangia kufa kwa mkono wangu , hivyo nimetimiza unabii tu”Aliongea Roma huku akijifuta damu iliosambaa kwenye uso.

“Kama mpango wenu ni kutaka ushirikiano wangu, mngeniambia kutoka mwanzo kuliko kunisumbua, kunitishia amani na kutumia watu wangu wa karibu kwa ajili ya kunipata”Aliongea Roma na kufanya wale wengine wote kufurahia kwa maamuzi Roma alioyafanya , hawakuweza kutegemea kama Roma anaweza Kwenda kinyume na Apollo.

“Hades! Do you know what you’re doing?! The life of your woman is in my hands! I could end her life anytime I want to!”

“Hades!Unaelewa unachokifanya ,Maisha ya mkeo yapo kwenye mikono yangu , ninaweza kuyakatisha muda wowote ninaotaka”Aliongea Apollo baada ya kushuhudia tukio la kichwa cha Kadinal Cruff kupasuliwa kama yai.

“Hehe…naelewa na unaonekana kuwa na bahati sana , kwani ninao wanawake wengi , lakini naona wakwanza kuingia kwenye mikono yako ni mke wangu”Aliongea Roma kama mtu anaepumua kwa afadhali baada ya kazi nzito na muda huu macho yake yalikuwa kawaida , ila alikuwa na matone ya damu kwenye uso.

“You don’t seem to think I am ready to take matters into my own hands. Hades, as a god, I won’t hesitate to kill Persephone at all.”

“Unaonekana kutokufikiria kama hili swala siwezi kulifanya mimi mwenyewe kwa mikono yangu ,Hades mimi kama mungu , siwezi kusita sita kumuua Persephone”

“Hahaha… Wewe ni mpumbavu , unafikiri simfahamu Apollo .. acha kujidanganya wewe ni feki”Aliongea Roma na kufanya hata Fodesa aliekuwa kwenye wasiwasi asimame vizuri na kumwangalia Roma.

Wote walijiuliza kama maneno ya Roma kwamba mtu aliekuwa mbele yao sio Apollo bali ni feki ni ya ukweli.

“Hades sina haja ya kukuthitishia mimi ni Apollo , ninaweza kuwarushia mishale kadhaa kutoka hapa nilipo na kuuwa baadhi yenu , na nasema hivi mkeo anakufa na baada ya hapo nalipua kisiwa chote”

“Haha.. Sawa ila ukumbuke hata ulipue hiki kisiwa sitoweza kufa kwasababu ya bomu la nyuklia”Aliongea Roma kwa kejeli.

“Ninachokuambia ni hivi , nilikuwa nikikufahamu tokea mwanzo wewe ni feki na nilikuwa nikikuchora tu tokea siku nafika hapa Paris, Wewe ni mjinga kwani hata kama ni maigizo umefeli ,huwezi ukasikia Miungu watu wakajitangaza tangaza hovyo, kwanza hawahitaji msaada wakitaka kufanya jambo lolote lile , unachofanya ni kupanikisha vyombo vya usalama , lakini huna lolote” Aliongea Roma na kuendelea kushangaza watu waliokuwa wapo hapo ndani.

“Hades , sitaki maneno mengi , nipe jibu moja, upo tayari kwa ajili ya kufanya kazi yangu au kuwaacha hawa wanawake wako wafe kwenye mikono yangu?”

Lakini Roma hakujibu alitaka kumuonyesha Apollo jibu lake kwa vitendo , na palepale alipotea na ile anaibuka alikuwa nyuma ya Gabriel , lakini ni kama Gabriel alitegemea kwani alivuta siraha yake ya kivita maarufu kama Lance of Longinus na kusogea mbele na kuirudisha kwa kasi kuelekea usawa wa Tumbo la Roma , lakini ni kama Roma alitaka amuache afanye kile anachotaka , kwani ile siraha mfano wa mkuki ilitua tumboni , lakini haikupita ni kama ilifika mwisho , kwani kadri aliyyokuwa akiisukuma iingie tumboni kwa Roma haikupita , ni kama chuma kinapokutana na chuma.

Ukumbuke Lance of Longinus ni mkuki ambao ulitumika kumchoma Yesu ubavuni wakati wa kusurubiwa kwake katika biblia , na inasemekana siraha hii baada ya tukio hilo ilitunzwa kama ukumbusho ndani ya Vatican , lakini haikueleweka kwanini Gabriel alikuwa akiitumia, kwani siraha hii ambayo pia inafahamika kwa jina maarufu kama vile Spear of Destiny, ni moja ya hazina za siri za Vatican.

Roma alitabasamu kifedhuli na palepale alimpiga Teke Gabrieli kwa nguvu kubwa na Kwenda kutua kwenye mlango wa chuma na kutokana nguvu aliotumia ni kama ya kungongwa na gari aina ya Fuso na Gabiel alikuwa mfu palepale huku ile siraha baada ya Gabriel kufa ilipotea kwenye mikono yake.

“Kwanini anaua kikatili namna hio?”Aliuliza AJenti wa kundi la Dhoruba nyekundu.

“His Majesty Pluto is simply too strong. It isn’t his intention to cause a scene like this. All he did was exert a little bit of power. What you see is just the terrifying result that follows.”

“Mfalme Pluto ana nguvu kubwa sana , sio nia yake kusababisha haya , ila alichokifanya ni kutumia nguvu kidogo tu na kinachofuatia ni matokeo ya kutisha”Aliongea Sauron.

“Okey!Pluto mpaka kufikia hapa nadhani maongezi yetu yamefikia ukomo na hakuna maelewano , nitafanya kile nilichodhamiria kwa watu wako hawa”Aliongea Apollo aliekuwa kwenye hasira , licha sura yake kutokuonekana kwasababu ya kuvaa Helmet , lakini kwa sauti yake tu ilionekana alikuwa ni mwenye hasira na palepale aligeuka na kumsogelea Edna aliekuwa hajitambui akipigwa na ubaridi wa baharini na haikueleweka walikuwa wamewekewa madawa gani, kwani kwa upepo wa baharini Pamoja na baridi wangezinduka.

“Hades unamuacha amuue mkeo…!!!”Aliongea Lilith kwa wasiwasi kweli , licha ya muda wote kuwa kimya , lakini mpaka kufikia hapo alikosa uvumilivu na hakuelewa Roma alitaka kufanya nini.

“Hehe.. nikajua wewe ndio mmoja ya wanawake wanaombea mke wangu afariki mchukue nafasi yake”Aliongea Roma akimwangalia Lilith.

“Hades hata kama sijawahi kukutana na mkeo , lakini kushuhudia kifo chake sio jambo zuri”Aliongea Lilith , lakini Roma alimpotezea.

“Okey!, Nyie wengine mnaweza kuondoka hapa na mniache , naamini bomu linaweza kulipuka muda wowote”aliongea Roma akiamrisha watu wote waondoke.

“Mfalme Pluto kwanini sasa umeua Wavatican ilihali unajua atalipua hiki kisiwa , inamaana gani sasa”aliongea yule ajenti wa Dhoruba Nyekundu.

“Unafikiri ningefanya nini , tayari rimoti ipo kwenye mikono yake , hivyo isingekuwa na maana ya kuwaacha hai”

Kundi la Takamagahara ndio watu pekee walioondoka ndani ya hilo eneo na kuwaacha wengine akiwemo Lilith na baba yake.

Apollo baada ya kufika mita mia moja kutoka alipolazwa Edna aliomba upinde wake wa mshale na kisha akaseti vizuri na kuvuta huku akimwangalia Edna ambaye hakuwa akijitambua.

“Goodbye, Persephone. You shall blame your foolish husband for this,”Aliongea Apollo na kisha akaachia mshale na kumfanya Lilith na baba yake kutoangalia kitendo kile , lakini kwa upande wa Roma alikuwa akiangalia na Nadia pia aliekuwa ameshikiliwa na wanajeshi wa Apollo alifumba macho, hakutaka kushuhudia Edna akifa mbele yake.

Fodesa ndio aliekuwa wa kwanza kushangaa kile kilichokuwa kikiendelea , kwani sehemu ambayo Edna alikuwa amelala ni kama vile alikuwa ndani Puto la Plastic liliomfunika kwa juu ,lililokuwa na rangi ya njano huku likitoa mwanga kama wajua kwakucheza cheza na kutoa mvuke kwa wakati mmoja.

“It`s Divine Shield”Aliongea Fodesa akimaanisha kwamba ni ngao ya kimungu.

Apollo hakuelewa ni nini kimetokea , kwani wakati anarusha ule mshale ulidunda kwenye pira ambalo limemfunika Edna kudondokea pembeni.

“Ni nini hiki…”Aliongea Apollo huku na wanajeshi wake wakisogea nyuma kwa mshangao.

Upande wa Roma huku kisiwani hakuwa na wasiwasi kabisa , ni kama alitegemea tukio lile kutokea lakini pia haikueleweka kama ndio kamkinga Edna kwa kutumia Ngao ya kimungu.

Apollo aliekuwa akitetemeka mikono alivuta tena mshale na kupiga tena kuelekea sehemu ambapo amelala Edna , lakini ilikuwa vile vile mshale ule haukupita Zaidi ya kudunda kwenye ngao ya Rangi ya njano ambalo lilionekana kama kioo na kudondokea pembeni na ikumbukwe mshale aliokuwa akitumia Apollo sio wa kawaida , kwanikama unakumbuka alirusha hewani na ukafika kisiwani na kuleta tetemeko,lakini ulionekana kudunda mbele ya Devine Shield.

“I refuse to believe that it can’t be penetrated!!”

“Nakataa ,siamini kama mshale hauwezi kupita kwenye hii ngao”Aliongea Apollo.

“Hehe..it can’t be done. Although you are very strong, and the weapon in your hand is comparable to a Devine weapon, you’re still no god.”

“Hehe...hauwezi kupita.. ijapokuwa unanguvu nyingi na siraha yako inaweza kulinganishwa na siraha ya kiuungu , lakini bado wewe sio sehemu ya Miungu”Aliongea Roma kwa kejeli.

“What’s this?! Tell me, what is this?!”Aliongea Apollo huku akitetemeka na hii ilimfanya sauti yake kubadilika na kusikika kawaida tofauti na mwanzo ambapo sauti yake ilikuwa nzito, Fodesa ndie aliekuwa wa kwanza kuitambua sauri hio.

“Director Depney!!”Alimaka Fodesa na kuita hilo jina akimwita Apollo feki mkurugezi wa Ofisi namba saba , directo Depney.
 
SEHEMU YA 201

Fodesa masikio yake yalikuwa vizuri sana na katika Maisha yake asingeshindwa kutofautisha Sauti ya Depney hata kidogo , alikuwa na uhakika ni sauti yake.

“Director , siamini kama ni wewe”Aliongea kwa mshangao.

“Haha..Ooh kumbe ni wewe Director Depney,Unaonekana kuwa na muda wa kuchezea mpaka kuanzisha kamchezo ka kujifanyisha wewe ni Apollo , Nakusikitikia mpango wako umefeli”Aliongea Roma huku hali ya chumba ikibadilika kutoka kwenye hofu mpaka kwenye mshangao, mwanzoni walikuwa wakifahamu kama Director alikuwa na udhuru ,ndio maana alishindwa kuhudhuria yeye mwenyewe , lakini kumbe ndio aliekuwa akiwahangaisha vyote hivyo na kupelekea watu kufa.

Depney baada ya kuona kakamatika , ilibidi avue lile helmeti na kulitupia pembeni na kisha akasogea mbele tena , licha ya kwamba alikuwa amegundulika na siri yake , lakini hakuonyesha kuwa na hofu.

“Director kumbe ni wewe kweli… ndio maana ukaniambia ni kukaimu nafasi yako kumbe ulikuwa na lako kichwani”Aliongea Fodesa huku akishindwa kuzuia hisia zake za mafadhaiko.

“Najuta kukusapoti takataka kama wewe , unaongea kuhusu ushindi kutoka kwa wanajeshi wetu , lakini wewe ni mwanaharamu mchanganyiko wa kinazi ,huna tofauti na msaliti vilevile”aliongea Depney alimkejeli Fodesa.

“Pluto nilikuchukulia poa na nakiri hilo ndio kosa langu , sikudhania kama utaweza kunigundua mapema , ila hakuna kinachoharibika , rimoti ya kulipua mabomu ipo kwenye mikono yangu, licha ya kwamba sijui umewezaje kumuwekea ngao mkeo na nikashindwa kumu,a ila sidhani kama unaweza kupona kwenye bomu la nyuklia”

“Duh! Nilishasau kama unarimoti kwenye mikono yako Depney , mimi nimsahaulifu sana na ndio kawaida yangu kwasababu hata mke wangu ana akili kuliko mimi, lakini licha ya hivyo toke siku nilivyosikia kuhusu Apollo na ile siku tulivyotekwa nilijua kabisa Apollo ni mtu ndani ya jeshi la Ufaransa “

“Ooh! nina shauku ya kujua uliwezaje kufahamu yote hayo , kwasababu sina haraka ya kuwalipua tufanye kama kauli yako ya mwisho kabla ya kifo chako”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

“Kwanza kabisa kilichonifanya nikagundua kuwa serikali inahusika ni namna ambavyo tulitekwa , Msitu wa Rommilly upo karibu sana na mjini , hivyo kwa vyvyote vile usalama wa taifa wasingeweza kushindwa kujua mateka wamepelekwa wapi, kitu cha pili kilichofanya nigundue ni Siraha ambazo magaidi walikuwa wakitumia, lakini pia namna ulivyoweza kuchagua tageti zako, kama kweli ungekuwa ni Apollo halisi usingehangaika na taifa la Ufaransa bali ungeenda moja kwa moja kutishia mataifa makubwa kama Marekani , lakini kwakua ulikuwa ndani ya jeshi na usalama wa Taifa la Ufaransa uliona mpango wako unaweza kufanikiwa ndani ya Ufaransa”Aliongea Roma na akaendelea.

“Kwa ninavyoona mpango wako ni kutaka kuwa raisi wa Ufaransa Pamoja na mwenyekiti wa EU kwani ni zamu ya Ufaransa kutoa kiongozi mwaka huu”Aliongea Roma.

Unachotakiwa kuelewa katika umoja wa mataifa ya ulaya EU, mwenyekiti anatoka katika kila taif kwa mfuatano wa muda maalumu ,ni kama ilivyo kwa SADC hapa Afrika basi hata kwa Ulaya, hivyo mwaka huo ilikuwa ni zamu ya Ufaransa kutoa mwenyekiti wa EU.

Sasa Roma baada ya kuunganisha matukio yote aliamini kabisa Apolo feki kachagua mwaka huo kwa makusudi maalumu , kwanza ni kumtoa raisi kwenye kiti chake kwa kumuua huku akisingizia jambo hilo kufanywa na sehemu ya Miungu watu yaani Apollo, lakini wakati huohuo pia aliweza kuchangua mwezi ambao Onyesho la Fasheni la wiki lilikuwa likifanyika hapo Ufaransa na hii ingemfanya kutoshitukiwa kwani katika onyesho hili ni matajiri wengi ambao huwa wanahudhuria , hivyo ni rahisi kwa dunia kuona ni magaidi ndio yamefanya tukio hilo , hivyo kwa Apollo feki kutoshitukiwa kuwa ndani ya serikali , yaani kiufupi yale matukio ya kulipua baadhi ya kambi za jeshi za NATO Pamoja na EU ni geresha tu ya kutaka kujifanyisha ana nguvu na yupo tayari kufanya chochote na Apolo feki aliweza kufanikiwa kutokana na kwamba alikuwa ndani ya kitengo cha usalama wa taifa hivyo siri zote alikuwa akizifahamu.

Mpango wa Depney ulikuwa ni mzuri , lakini alichokosea ni kumdharau Roma, halafu pia kosa kubwa ni kujiita Apollo , Roma ni sehemu ya miungu kumi na mbili iliotengenezwa hapa duniani kwa kusudi maalumu la kiusalama , hivyo yeye alikuwa akimjua Apollo halisi ndio maana aliweza kugudua mapema kuwa Apollo aliekuwa mbele yake ni feki.

“Hivyo nakiri kabisa kuwa mpango wako licha ya kuwa mzuri , lakini ulikuwa na matobo mengi na ulichokosea pia ni kujiamini sana na kujikweza lakini pia kuwaamini sana washirika wako ,Wavatican”Alimalizia Roma

“Kwahio unataka kusema nini kama umeweza kujua mpango wangu? , unachotakiwa kuelewa mpaka sasa hivi mpango haujafeli na nitaanza kulipua hiko kisiwa na nikishamaliza nitammalizia na mkeo, na ili uone kama namaanisha nitaanza na hawa wapenzi”aliongea Depney kwa kejeli na kisha akawasogelea Stern na Alice na kisha akachukua mshale wake ambao haukuwa na nguvu za kawaida kutokana na kufanyiwa matambiko, na alimwelekezea Alice kwa kutaka kuanza nae.

Lakini kabla hajatimiza azima yake Stern aliekuwa amejilaza chini alinyanyuka kivivu na kumfanya Depey kushangaa , kwani alichokuwa akijua ni kwamba kemikali aliotumia kwachoma mateka wake ilikuwa ikidumu kwa mud amrefu sana , hivyo kuamka kwao kungechukua muda , lakini ajabu Stern aliamka muda huo.

“Depney usimuue”Aliongea Fodesa kumzuia lakini Depney aliona aanze kwanza na Stern ambaye ashazinduka na ndipo ammalizie Alice.

“Hades nimesikia porojo zako muda mrefu mno , hivi unajua ni baridi kiasi gani ambalo lipo huku baharini, Inawezekana vipi mtu mmoja kuongea pumba muda wote huo, Persephone hayupo kama sisi , yeye ni rahisi kushikwa na baridi” Alionea Stern huku akisogea mbele pasipo kumjali Depney anaedhamiria kumuua na akaendelea kuongea.

“Sasa ngoja nikugee siri kwanini mkeo hakupi mzigo, ni kwasababu unaongea sana, wewe unatakiwa Kwenda moja kwa moja kwenye dhumuni lako , hivyo hivyo ungefanya kwa huyu mpuuzi hapa , tunachelewa kwenda kula kwa ajili porojo zako unajua ni muda gani tumelazwa hapa?”Aliongea Stern akiwa siriasis awamu hii.

“Hehe..mbona sasa wewe ndio unaeonekana kuongea sana kuliko mimi”Alijibu Roma huku akiweka tabasamu la kejeli.

Lakini Depney alikasirika Zaidi baada ya kuona Stern na Roma wanaongea pumba nay eye mwenyewe akajishangaa kwanini alikuwa akiwasikiliza..

“Ushamaliza kuongea sasa nitakupeleka kuzimu , wewe mpumbavu”Aliongea Depney na palepale alivuta mshale na kuachia, lakini upande wa Stern hakusogea , ila alionekana kama anaongea maneno flani kimya kimya kama ya kunuia jambo flani na muda ambao Fodesa anaachia mshale ndio muda ambao ngao kama aliofunikwa nayo Edna ilitokea mbele ya Stern na Risasi iligonga kwa nguvu na haikumpata Stern kwani ilizuiwa na Divine Shield.

“Depney weweni mjinga sasa , hivi unafikiri Hades anaweza kumkinga mke wake kwa umbali aliokuwepo,ni mimi ndio niliemuwekea ngao baada ya wewe kutaka kumpiga na mshale wako wa kipuuzi”Aliongea Stern na kumfanya Depney atoe jicho

“You… You’re not Stern! Who are you really?!”Aliongea Depney akirudi nyuma kwa woga, mwanzoni aliamini Roma ndie aliehusika na kumkinga Edna na ngao ili asidhurike lakini kumbe alikuwa ni Stern , ndio maana alitaka kujua jina halisi la Stern.

“Wewe ni mjinga sana Depney, kichwa chako kimejaa funza , yaani inashangaza mpuuzi kama wewe unataka kuanzisha vita , eti nataka kutawala Dunia yote , What Stupid Excuse …nilikuacha muda mrefu nione kama mpango wako unaweza kufanikiwa , lakini unaonekana kuwa Zaidi ya mjinga , kama ulikuwa unajua mpango wako utafeli usingetumia jina langu maana unaninajisi”Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kwa Stern kuongea kwa hasira , kwani siku zote alionekana kutokuwa mtu siriasis ambaye alichukuliwa kama chukizo Pamoja na dada yake kwa kitendo cha kuwa wapenzi ilihali ni ndugu.

Upande wa Depney alikuwa kwenye mshituko mkubwa hakuelewa kile kilichokuwa kinatokea

“You… you are… you are…”Aliongea Depney pasipo kumaliza Setensi yake huku akijikokota kurudi nyuma.

“So you finally got it, That’s right, I am real A… po… llo.”

“Naona sasa unaelewa , Ndio mimi ni Apollo halisi”Aliongea Stern


JUMAPILI ITAENDELEA 0687151346 WATSAPP NITAFUTE
 
Mkuu shukran sana aiseee dah[emoji4][emoji39][emoji39][emoji39] ngoma inazidi kupamba moto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…