SEHEMU YA 197
Kila mmoja hapo ndani hakuelewa kwanini Roma alikuwa akisaidia watu kutoka upande wa Dark Parliament ,Sauroni mwenyewe alikuwa halewi bosi wake alichokuwa akifikiria , ila hakutaka kuuliza.
Lilith baada ya kuona Roma amekubali kumsaidia alijikuta hata nguvu kurudi upya huku akimshikilia vyema baba yake ambaye alipata mapigo ya kutosha kutoka kwa Kadinali Cruff.
“Are you really Pluto, the new Hades?”
“Ni kweli wewe ndio Pluto , Hades mpya”Aliuliza kadinali Cruff.
“Haina haja ya kunifahamu Kadinali, japokuwa sikupaswa kuwa upande wowote kwenye mapambano yenu , lakini nahisi nguvu kubwa ya uovu ndani yako”Aliongea Roma na kumfanya Gabriel amwangalie Roma kwa mshangao , hakujua ni kwanini Roma kaongea maneno hayo.
“Kijana acha kujigamba , ijapokuwa wewe ni sehemu ya Miungu watu kumi na mbili ,lakini huwezi kushindana na Nguvu ya Mungu”Aliongea Cruff lakini Gabriel aliekuwa akijua moto wa Roma ilibidi aingilie.
“Roma kaa nje ya hili la sivyo utapoteza kitu unachokipenda kwenye dunia hii”Aliongea Gabriel na kumfanya Roma kushangaa
“Unataka kumaanisha nini Gabriel”
“Hahaha… Hades tulijua tu utaingilia kwenye mipango yetu kama ulivyofanya kule Tanzania na tulivyofahamu uwepo wako hapa Ufaransa tulichukua tahadhari zote”Aliongea Cruff lakini Roma alishindwa kuelewa anamaanisha nini na kutokana na kutopenda kutishiwa amani palepale alipotea alipokuwa amesimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Cruff.
Lakini Kadinali na yeye hakuwa mzembe , ni kama alimtegemea Roma kwani ile Roma anaibuka na yeye alipotea na kuibuka mita mbili mbele
“Unajigamba sana kijana , Hebu onja kwanza joto la Jehanamu”Aliongea Cruff.
“Fireeeeee…!!!!” Aliongea Kadinali na palepale ulilipuka moto kama bomu na kumfunika Roma kiasi cha kumpekekea kutoonekana na kufanya hata Sauroni aliekuwa nyuma kuinuka kwa wasiwasi,
Moto ule ulidumu kwa dakika kama mbili hivi kabla ya kuisha na ile unazima alionekana Roma aliekuwa amesimama vilevile alivyokuwa mwanzo pasipo ya kuwa na jeraha lolote.
“Cruffy nishakwambia kabla ya kupambana na mimi lazima ujitakase kwanza la sivyo huniwezi kuniunguza na huu moto wako”Aliongea Roma na kumsogelea Cruff kwa spidi ya mwanga na ile anamfikia alimsomba mzima na Kwenda kutua nae kwenye ukutani na kumgonganisha kwa nguvu kiasi kwamba eneo lilitengeneza mtetemoo wa ardhi , huku akionekana kumshikilia kwenye shingo.
“Unajua kwanini nimeamua kuwa upande wa Dark Parliament?”aliongea Roma huku macho yake yakitoa mwanga wa Kijani , lakini Cruff alishindwa kujibu kwani alikuwa amekabwa vilivyo kwenye shingo.
“Miaka miwili nyuma wanajeshi wa Vatican walinishambulia wakati nilivyokuwa Rome, pasipo ya kuwa na kosa lolote wala kuwachokoza , nilitoa msahamaha , lakini inaonekana mnataka kurudia kosa”Aliongea Roma na Cruff hakutaka kufa kizembe alitumia uwezo wake wakuita nguvu , lakini haikuelewa Roma alimzibiti na nguvu ya aina gani , kwani kaditi alivyokuwa akiita nguvu , alishindwa kabisa kuipata.
“Roma usimuue Kadinali”Aliongea Gabriel kwa sauti akimwamrisha Roma.
“Sina sababu ya kumuacha hai, nachukia sana vitisho”Aliongea Roma.
“Una sababu ya kumuacha hai Roma , Mkeo Edna yupo kwenye mikono yetu”Aliongea Gabriel na kumfanya Roma ageuke na kumwangalia Gabriel kwa hasira, ni kama hakuwa amemsikia vizuri.
“Unataka kumaanisha nini?Aaliongea Roma huku baadhi ya watu kama kumi waliobaki kwenye hili eneo wakimshangaa Gabriel ,h awakuelewa alikuwa akimaanisha nini.
Lakini Gabriel wala hakuongea chochote Zaidi ya kutoa kijisimu kidogo(Burner phone) , kama vile funguo ya gari na kuweka sikioni
“We’ll abandon our original plan. Cardinal Cruff has been defeated. Proceed with what you were going to do,”
“Tutaachana na mpango wa kwanza ,Kadinali Cruff kashindwa , endeleeni na kazi mliopangiwa”Aliongea kwa kupitia simu na kisha akakata na kumgrukia Fodesa ambaye muda wote alikuwa amejibanza kwenye kona , na haikueleweka kwanini muda wote hakuwa amekimbia na kuungana na watu wengine waliokuwa wamekimbilia kwenye meli, Fodesa alioenaka kuwa na roho ngumu kweli.
“Fodesa kuna tarakishi yoyote maneno ya karibu?”aliuliza Gabriel na kumfanya Roma amwangalie , hakujua ni kitu gani Gabriel walikuwa wamefanya kwa mke wake Edna.
“Ndio kuna tarakishi ambazo zipo ndani ya chumba cha mawasiliano”Aliongea Fodesa na Gabriel alitabasamu.
“Hades kuna jambo ninataka kwanza kukuonesha na ukishaona nadhani utafanya maamuzi aidha ya kutupatia teknolojia na kufuata maelekezo yetu au kumpoteza mkeo”
“Mimi sina shida , twende ukanionyeshe hiko unachotaka kuonyesha”aliongea Roma huku akianza kutembea yeye na kuachana na Kadinal Cruff.
Na ndani ya dakika kama mbili hivi , waliingizwa kwenye chumba kingine kikubwa ndani ya jengo hili ambalo lilikuwa limeharibiwa pakubwa kutokanana mtifuano uliotokea, ilikuwa ni sehemu ya mawasiliano ndani ya hii kambi.
“Deputy Director Fodessa, please turn on the monitor and switch to satellite mode,”Aliongea Gabriel huku akimwamrisha Fodesa kuwasha Tarakishi na kuunganisha na mawasiliano ya satilaiti.
Baada ya Fodesa kuunganisha mawasiliano ya Satilaiti palapale Skinri zote za komputa zilizokuwa zimefungwa ukutani zilionyesha eneo la baharini paisipo kuonekana kwa mtu yoyote kwenye hizo Skrini , lakini dakika moja mbele hatimae watu waliokuwa kwenye meli ya kivita, walionekana kwenye Skrini, walikuwa ni wanaume wengi waliovalia kombati za jeshi , huku wakiwa na chata ambalo Roma alikuwa akilikumbuka , walikuwa ni moja ya wanajeshi waliowateka siku ambayo walifika Ufaransa ,Sun Gold Totem, wanajeshi hawa walikuwa wapo kwenye meli ya kivita wakiwa wamesimama eneo ambalo mara nyingi kwenye meli za kivita ndege hutua na kuruka angani.(Deck)
Roma wakati akiendelea kuangalia kwa kukagua watu wote waliokuwa kwenye meli , hatimae walionekana wanajeshi wengine ambao walikuwa wamebeba watu begani ambao walikuwa wamefungwa na Kamba na baada ya kusogea kwenye Deck waliwashusha kama mizigo.
“Harry!!”Fodesa ndio aliekuwa wa kwanza kumtambua mtoto wake na Roma pia baaada ya kuangalia kwa umakini aliweza kuona sura ya Stern, Alice Pamoja na Mke wake Edna waliokuwa wamefungwa na wote walionekana kutokuwa kwenye kumbukumbu.
“Gabriel hii maaana yake nini, inamaana Vatican mmeamua kuungana na Apollo kuhujumu usalama wa dunia?”Aliuliza Fodesa kwa hasira kwani alikuwa tayari alishaelewa wanajeshi waliokuwa wakionekana kwenye Skrini walikuwa ni wa kundi la Apollo
Lakini Gabiel wala hakutaka kumsikiliza Fodesa Zaidi ya kufyura na kuendelea kuangalia kwenye Skrini na palapale kilionekana kivuri kikisogelea mbele , sehemu ambapo Edna na wengine wamewekwa chini.
Kile kivuli baada ya kusogea mbele kilifanya kuziba Skrini yote kwa ukubwa wake , alikuwa ni mwanaume alievalia mavazi ya kijeshi huku akiwa na alama kubwa ya ‘Sun Gold Totem’ kwenye kifua chake , kichwani alikuwa amevalia helmeti kubwa kama yale waliokuw awakivaa wanajeshi wa Kirumi hapo kale.
Kwa jinsi ilivyokuwa , ilionekana kabisa wanajeshi hawa walikuwa wamefunga Kamera ambazo zilikuwa na uwezo wa kunasa na sauti upande wa pili.
“I believe some of you may recognize me, but let me introduce myself… I am Apollo.”
“Najua wengi wenu huenda mkawa mnanifahamu , lakini ngoja nijitambulishe.. kwa jina naitwa Apollo”Aliongea kwa sauti nzito ilioweza kusikika na kila mtu aliekuwa ndani ya chumba hiki.
Kumbuka hapa ndani walikuwepo watu ambao hawakuwa wakizidi kumi , kwani wengine wote walikimbia , waliokuwa wamebaki ni Fodesa , Roma , Cruff , Gabriel na Lilith na baba yake na wanajeshi wengine wa The Eagles akiwemo Sauron.
“This must come as quite a shock to you I imagine, as to why I’m related to the Vatican, but I don’t think it warrants a discussion as of now. Let’s just leave it at mutual interests…that’s all.”
“Nadhani mpo kwenye mshituko mkubwa kwanini nina uhusiano na Vatican , lakini sio swala la kuzungumza kwa sasa na tutaliacha kwa manufaa ya pande zote mbili, ni hivyo”Aliongea kwa sauti nzito
“Haha…Ijapokuwa siamini kama kweli wewe ni Apollo, ninatamani kujua kwanini umeungana na Vatican, au ni kwasababu mnataka kuwa moja ya dini inayoweza kutawala Ulimwengu wote?’Aliongea bwana mmoja alieingia muda huo huo na haikueleweka alikuwa wapi , alikuwa ni Ajenti kutoka kundi la Dhoruba Nyekundu.
Baada ya Apollo kusikia yale maneno wala hakuongea chochote ,Zaidi ya kutoa ishara kwa wanajeshi wake waliokuwa kwenye hio meli ya kivita na palepale alisogezewa upinde flani wa Mshale wa kisasa kabisa ambao ulikuwa ukitumiwa kwenye karne ya kumi na saba huko Ujerumani.
Unachotakiwa kuelewa kuna utofauti wa upinde wa mshale inayotumika kwenye mataifa ya Asia na iliotumika Ulaya , kama ushawahi kuangalia muvi ya kizungu ya Arrows , basi utakuwa unanipata vyema.
Kilichokuwa kikifanyika upande wa baharini kilikuwa kionekana vyema , licha ya kwamba kulikuwa na giza kwani ilikuwa ni usiku kama wa saa nne , lakini taa kubwa kwenye meli ziliwafanya Roma na wengine kuona kila kinachoendelea.
Apollo baada ya kukabidhiwa ule upinde na mshale aliseti vizuri na kisha akalenga hewani na kufanya Fodesa na wengine wasijue anataka kufanya nini, kwani ilionekana sehemu waliokuwepo na kambi hii ya jeshi kulikuw ana umbali mrefu , kwani kama wangekuwa karibu na kambi Rada za jeshi la Ufaransa zingeweza kuwanasa.
“Foolish humans. Since you doubt my identity and capability, I’ll show you the difference between people and gods”
“Binadamu wapumbavu , kwasababu mnawasiwasi na ubini wangu Pamoja na uwezo wangu , nitawaonyesha tofauti iliopo kati ya Binadamu na Miungu”Aliongea Apollo na palepale akaachia mshale hewani na hakuna alielewa ni jitu gani ambacho Apollo alikuwa akikifanya , lakini dakika mbili mbele chumba kilianza kutoa mlio wa hatari kama Alarmu na kufanya eneo lote lijae mwanga mwekundu na Fodesa alibonyesha haraka haraka kuangalia Anga karibu na kambi na hapo ndipo alipotoa mshangao , kwani waliona kitu mfano wa Kimondo kikishuka kwakasi usawa wa jengo na dakika chache mbele , kilisikika kishindo cha aina yake kilichoacha mtikisiko eneo lote
Hakuna mtu alie elewa ni nini kimefanyika , lakini walibakia kwenye mshangao pekee.
“Apollo unataka nini kutoka kwetu , kwanini umemteka mke wangu?”aliuliza Fodesa kwa wasiwasi
“Mmeamini sasa?’
“Taja shida yako”
“Hahaha…. Hades sikutegemea kama unaweza kuhudhuria mkutano huo wa siri na ukaharibu mpango wangu , lakini hakuna kinachoharibika kabisa maana nilichukua tahadhari mapema”Aliongea Apollo huku akimpotezea Fodesa na swali lake.
“Persephone is now in my hands. I believe this warrants a discussion and hopefully the start of a good partnership… Ooh! Without forgetting your other woman is also in my Hand”
“Persephone yupo kwenye mikono yangu naamini nitamtumia kama kibali cha kuanza kwa uhusiano wangu mimi na wewe..Ooh bila kusahau mwanamke wako mwingine yupo kwenye mikono yangu”Aliongea Apollo na palepale akatoa ishara na muda ule ule alionekana mwanamke akiwa ameshikiliwa na wanajeshi akieletwa ndani ya eneo hilo, aliekuwa amefungwa kitambaa mdomoni , alieonekana uwa na kumbukumbu.
“Nadia…!”Roma alishangaa hakuelewa imekuwaje na Nadia akawa ndani ya hilo eneo kwani alikumbuka huyo mwanamke alikuwa Tanzania.