Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Mamida Bado mpaka muda wa BBC pendwa ya wakati ule
 
SEASON 8
SEHEMU YA 211
BEIJING- CHINA.
Naam ni muda wa saa sita usiku katikati ya jiji la Beijing nchini China , inaonekana Gari aina ya Mercedes-Benz G55 AMG nyeusi ikisimama katikati ya jiji mbele ya hoteli maarufu ya Hilton Hotel.
Baada ya gari hii ya kifahari kusimama walinzi waliokuwa ndani ya eneo hili ambao walikuwa wakisinzia , hamasa yao ya kazi ilirejea upya baada ya ujio wa ghafla wa gari hii ya kifahari ndani ya hoteli yao , ijapokuwa kwa uzoefu wao wa kazi ni magari mengi ya kifahari ambayo wameweza kuyashuhudia yakifika mara kwa mara ndani ya hoteli hio, lakini kwa Gari ilioingia muda huo wa usiku ilikuwa ya kifahari zaidi walioweza kuipokea kwa siku hio.
Baada ya gari kusimama sehemu husika ,dereva aliekuwa akiendesha gari hio ,Mzungu, alishuka haraka haraka na kisha akazunguka upande wa kulia na kufungua mlango na kumruhusu mwanaume wa makamo kushuka ndani ya gari hio.
Ni mwanaume aliedhihirisha ujana , alievalia suti ya Armani ya rangi nyeusi Pamoja na tai ya rangi ya bluu , huku saa ya gharama kubwa ya rangi ya dhahabu ikipendezesha Zaidi muonekano wake.
“You may stay here. I’ll go up alone,”Aliongea kwa kumpa maelekezo Dereva aliekuja nae ndani ya hoteli hio akimwambia asubiri hapo ataelekea juu ya jengo hilo mwenyewe.
“Okey!Boss”Alijibu Dereva huku akiinamisha kichwa chake kwa ishara ya heshima Pamoja na walinzi waliokuwa ndani ya hili eneo.
Mwanaume huyu alipiga hatua kuelekea juu kw akitumia ngazi kuingia ndani ya hoteli hii , huku kila baada ya hatua kama nne alionekana kuweka suti yake vizuri, licha ya kwamba anaonekana kujiamini lakini alionyesha wasiwasi ambao sio wa kawaida.
“Sir, may I be of any assistance?”Aliongea mwanamke wa kachina alivalia sare za uhudumu wa hoteli hio ,akiwa amesimama wima kumpa heshima mgeni aliekuwa mbele yake , huku akimuuliza ni msaada gani anapaswa kumsaidia.
“I would like to check into my room. I believe I have it reserved”
“Ningependa kuingia kwenye chumba changu, Natumaini kimeandaliwa”
“Sure. May I ask for your name please?”Aliuliza mhudumu huyu wa kichina kwa sauti yake nyororo na kingereza kilichonyooka.
“Yan Buwen”Alitaja mwanaume yule jina lake na kumfanya mhudumu kuangalia tarakishi yake kwa sekunde kadhaa.
Ndio alikuwa ni Yan Buwena ambaye tumemuaona chini Tanzania, Mwanasayansi ambaye amefika Tanzania na kusababisha kifo cha Profesa Shelukindo kwa kumtumia Scorpion, muuaji aliepata mafunzo kutoka kundi la Yamaguchi ambaye kazi yake ndani ya Tanzania ni kumlinda Raisi Kigombola.
“Mr Yan, our presidential suite Numbered 001 is yours. Please take the elevator to the sixty-eighth floor. Here’s your access card.”Aliongea yule mhudumu akimwambia Yan Buwen kama chumba namba moja cha Presidential Suite ni cha kwake na achukue lift mpaka Floor namba sitini na nane, huku akimpatia kadi ya kufungulia mlango ,Platinum Gold.
“Thank You”Alijibu Yan Buwen na kuelekea upande wa Lift kuelekea juu kabisa ya jengo hili refu sana la Hoteli ndani ya Beijing , ni jengo ambalo huwezi ukalikuta hapa Tanzania kwa urefu Kwenda juu na ndio lililokuwa likimilikiwa na kampuni kubwa ya Hilton inayojihusisha na maswala ya mahoteli.
Ndani ya dakika kama tano Lift iliokuwa imembeba Yan Buwen ilikuja kusimama ndani ya Floor namba sitini na nane na kumruhusu Yan Buwen kutoka na kusogelea chumba namba moja ndani ya Floor hii.
Yan Buwen baada ya kufika kwenye mlango uliokuwa na kibao cha namba moja , alisimama na kuanza kujiweka sawa muonekano wake kuanzia nywele mpaka suti yake kwa takribani dakika tano nzima kabla ya kufungua mlango , na kwa mtu yoyote angemuona kwa kitendo ambacho anafanya angemshangaa.
Baada ya kujihakikisha yupo sawa alishika kadi kwa mkono wa kulia na kisha aliichomeka sehemu husika kwenye mlango na akashika kitasa na kuusukuma mlango na kusababisha taa za chumba hiko cha kifahari kuwaka baada tu ya kuingia ndani na kudhihirisha mandhari murua kabisa iliosababishwa na samani za kisasa zilizokuwa zimepangiliwa ndani ya chumba hiko.
“You’re half an hour late.” Ilisikika sauti kutoka kwenye kona ya chumba hiki na kumfanya Yan Buwen mwili wake kusisimka na kumeza mate mengi kabla ya kugeuka na hii yote ni kutokana na sauti ya kirembo iliojaa chumba kizima.
Upande wa kushoto wa chumba upande wa sebuleni anaonekana mwanamke mrembo wa kizungu , mwenye nywele nyeusi ndefu zilizofungwa kwa nyuma , alievalia gauni la kupendezesha mwili rangi nyeusi, aliekaaa kwenye sofa huku mkononi akiwa ameshikilia Glass ya mvinyo mwekundu na alikuwa akinywa huku macho yake yote yakiwa nje ya dirisha akiwa ni mwenye kuangalia mandhari ya jiji.
Alikuwa ni mwanamke mrembo kuliko neno lenyewe , licha ya mwanga hafifu uliotolewa na taa za chumba hiki kumulika, lakini ilitosha kusema kwamba mwanamke aliekuwa mbele ya Yan Buwen alikuwa ni mrembo kama Malaika.
Yan Buwen aliesimama mita kadhaa aliishia kuhusudu uzuri wa mwanamke aliekuwa mbele yake huku akiendelea kumwangalia kwa macho ya matamanio.
“I… got into an emergency on the way here. I didn’t mean to be late.”
“Ni…nilipata dharula njiani , sijafanya makusudi kuchelewa”Aliongea Yan Buwen huku akionyesha hali ya kukosa utulivu.
Ukweli ni kwamba Yan Buwen sio kweli kama alipata dharula ya kumfanya achelewe , ila wakati yupo njiani akija ndani ya hoteli hii, aliona suti ambayo alikuwa amevaa mara ya kwanza haijamkaa vyema , hivyo ilimlazimu kutafuta suti nyingine.
Mwanamke aliekuwa mbele ya Yan Buwen alionekana kutojali kabisa sababu ambazo Yan Buwen ametoa , bali alimgeukia na kumwangalia machoni huku akikucha nne kimadaha na kufanya macho yake ya kizungu kuonekana vyema, na kwa mapozi yake ya kike ilikuwa ni kama adhabu kwa mtazamaji.
“Nipe maendeleo ya majaribio ya Specimen niliokupatia?”Aliongea.
“Mpaka sasa majaribio yanaendelea vizuri , maelekezo yako yanaonekana kuwa na msaada mkubwa , nimefanikiwa kufanya mnyumbulisho wa Specimen na naamini ndani ya miezi kadhaa tutaweza kupata matokeo sawia na mwonekano wake halisi wa sasa , hata kuzidi”
“Sijali muda utakao tumia , ninachotaka ni matokeo ya kuridhisha, sitarajii uniangushe katika hili, usinifanye juhudi zangu nilizotumia kupata hizo Specimen ziende bure”
“Siwezi kukuangusha kabisa , nitakamilisha kila kitu ulichoniagiza bila matatizo yoyote , I’ve also discovered a possibility for the gene mutation through my experiment results. If my past research proves to be right, I believe the future you wish to witness will come true. We’ll soon be unstoppable!”
“Nimeweza pia kugundua uwezekano wa mabadiliko ya jeni kupitia matokeo ya majaribio yangu , kama utafiti wangu utathibitisha kuwa sahihi , naamini kesho ulioitarajia kuiona itawezekana kabisa , muda si mrefu tutakuwa hatushikiki”
“Not us, but me… I want to make it clear right now that you are nothing but a tool to me.”
“Sio sisi, bali mimi…nataka niweke jambo moja wazi kwako lieleweke , kwangu mimi wewe ni kama chombo tu na hakuna Zaidi ya hapo”Aliongea mwanamke na kumfanya Yan Buwen hali aliokuwa nayo ya mchecheto kupotea , lakini alirudisha tabasamu.
“Nipo tayari unitumie kama chombo upendavyo .. nitahakikisha naendelea kuwa wa faida kwako”
“Yan Buwen… better not stare at me this way with your stupid eyes. I am fully aware of the pointless intentions you hold. In my eyes, you’re just a dog with a smarter brain than most. I have no interest in dogs.”
“Yan Buwen… ni bora ukaacha kuniangalia kwa namna hio na macho yako ya kipumbavu , nifahamu nia yako isiokuwa na maana uliobeba zidi yangu , kwenye macho yangu wewe ni mbwa mwenye ubongo wenye akili kuliko wengine , Sina matamanio na mbwa”Yan Buwen lilimshuka ni kweli alikuwa akimwangalia mrembo aliekuwa mbele yake kwa macho yasio ya kawaida.
“Nitakuwa makini siku nyingine ..naomba unisamehe”Aliongea Yan Buwen lakini mwanamke aliekuwa mbele yake wala hakumjali kabisa na aliangaliwa kama vile ni funza.
“Nimepata taarifa una mpango wa kumsingizia Hades juu ya kifo cha Profesa Shelukindo?”
“Ndio,, ndio .. nilikuwa na mpango huo mimi na mheshimiwa raisi mstaafu wa Tanzania”
“Nadhani sijakupa maagizo ya namna hio?”
“Licha ya kwamba tulipanga kumsingizia , lakini hakuna namna ambayo Hades angeweza kushikiliwa juu ya hilo , serikali ya Tanzania inayo mpango mkubwa juu yake”
“Hahaha….unaonekana mjinga eti ,unafikiri watanzania ni wapumbavu kama unavyowafikiria na wanaweza kudanganyika na mchezo unaotaka kufanya, usijifanye una akili kuliko wengine wakati upo wa kawaida tu , hakikisha haufanyi makosa, nina jua madhumuni yako”Yan Buwen alijikuta akikosa neno la kuongea kwani mtu aliekuwa mbele yake licha ya kuwa mwanamke mrembo ila alikuwa akimuogopa.
“Yan Buwen ninachokuambia ni kuweka umakini kwa yale ninayokuambia tu , sitaki mambo ya kipuuzi yajitokeze ,nikifanikiwa kuangamiza ulimwengu wa majini naamini pia unaweza ukanufaika kiduchu, na nitakuacha ufanye unachoweza kufanya, hata kama utamuua Hades itakuwa juu yako”Aliongea mwanamke huyu mrembo na kumfanya Yan Buwen kutingisha kichwa kama ameelewa na yule mrembo alinyanyuka alipokaa na kuwea Glass yake chini na kutembea kimadaha mpaka lilipodirisha na kisha akamgekia Yan Buwen.
“Godstone Pamoja na Teknolojia ya Thanatos vimehifadhiwa humu ndani kwenye chumba cha usalama , vichukue vyote kwa Pamoja na urudi navyo Tanzania , najua unafahamu unachopaswa kufanya , sitaki uendelee kubaki hapa China kwa muda mrefu”Aliongea yule mwanamke mrembo na palepale mwanga mkali wa kung`aa sana kama wa mwezi ulimdhingira mwanamke na kumfanya Yan Buwen macho yake kushindwa kuhimili na kuyafumba na ile anayafumbua mwanamke yule hakuonekana tena ndani ya chumba chake kwani alishatoweka kimaajabu.
Yan Buwen mara baada ya kugundua mrembo aliekuwa mbele yake kapotea alikimbilia dirishani kuangalia chini na hakuambulia chochote ,hata harufu yake haikuweza kusikika ndani ya chumba hiko , kitu pekee ambacho kilibaki kama Ushahidi ni Glass ya mvinyo iliokuwa nusu kwenye meza.
Naam huyu ndio The Doni A.k,a Athena.





SEHEMU YA 212
Naam ilikuwa ni siku ya jumanne ndani ya jiji la Dar muda wa saa nne za mchana alionekana Roma aliekuwa kwenye gari yake akipita Bagamoyo Road , ndani ya gari alionekana Diego na wanajeshi watatu wa kikochi cha The Eagles wakisonga mbele kuelekea upande wa Bagamoyo.
Siku hii ya jumanne ilikuwa ni siku ya Roma kutimiza ahadi ya kuhudhutia ufunguzi wa mafunzo ya kijeshi kwa vikosi maalumu, licha ya kwamba mafunzo hayo alipanga kuwaachia wanajeshi wake wa The Eagles kuyasimamia , lakini kwa siku hio ya ufunguzi alipanga mwenyewe kuwepo.
Masaa kadhaa mbele , hatimae waliweza kufika ndani ya kambi ya Mirambo na kupokelewa na Afande Tobwe aliekuwa amevalia gwanda za kijeshi.
“Karibuni sana Afande”Aliongea kwa bashasha Afande Tobwe huku akisalimiana na Diego Pamoja na wanajeshi wengine wawili.
“Diego nadhani mnamkumbuka?”Aliuliza Roma na Diego na wenzake wasingeweza kumsahau Afande Tobwe kwani siku yao ya kwanza kufika Tanzania ndio aliewazuia uwanja wa ndege na kuwataka Kwenda nae kambini.
Roma alikagua eneo lote la kambi hii ambalo limezungkwa na msitu mkubwa na alionesha hali ya kuridhika, baadhi ya wanajeshi walionekana wakichukua mazoezi huku wengine wakiwa wapo kwenye shughuli za kawaida za kila siku kama vile kufyeka majani marefu na kufanya usafi.
“Mfalme Pluto kwanini umetupangia kazi ya namna hii , wanajeshi wa hapa wanaonekana kutokuwa na msingi mzuri”Aliongea Diego huku akikuna kichwa chake na Roma alitabasamu.
“Diego ngoja uwaone kwanza ndio uanze kutoa maoni yako”Aliongea Roma kwa kutabasamu na kuendelea kufuatishana na Afande Tobwe.
Utambulisho ndani ya kambi ulikuwa mfupi sana , kwani baada ya Roma kutambulishwa kwa viongozi wa juu wa kambi moja kwa moja walienda kwenye eneo la mikusanyiko kwa ajili ya kukutana na wanajeshi ambao walitakiwa kuanza mafunzo.
“Ndio hawa Mr Roma ,wapo katika muundo wa timu mbili na kila timu ina jumla ya wanajeshi ishirini, tumetumia kigezo cha uwezo wao jeshini kuwadahili kwa ajili ya mafunzo haya maalumu, tunatumaini baada ya mafunzo haya watakuwa na uwezo wa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi maalumu cha makomandoo”Aliongea Kanali Tobwe huku akimtambulisha Roma kwa wanajeshi waliokuwa mbele yake waliosimama wima kijeshi kwa kujipanga mstari.
Roma alianza kupitisha macho yake kwa kila mwanajeshi kwa ajili ya kumkagua , licha ya kwamba alikuwa amesimama mbali na wanajeshi hao , lakini haikumzuia kuawaangalia mmoja mmoja, asilimia kubwa ya wanajeshi wote waliokuwa mbele yake walikuwa ni wanaume na wanawake walikuwa ni wachache sana.
Wakati Roma akiendelea kuangalia , alijikuta macho yake yakitua kwenye sura anayoifahamu na kushangaa uwepo wake.
Mtu alieweza kumtambua alikuwa ni Mage , licha ya kwamba alikuwa amenyoa nywele zake zote na kuwa na kipara, ila aliweza kumtambua na kujiuliza huyu mwanamke anafanya nini hapo kambini kwani alikuwa akijua ni polisi, na kwa Afande Tobwe na yeye aliweza kuona mshangao wa Roma ila alipotezea na kisha akasogea mbele kidogo kwa ajili ya kutoa utambulisho.
“Huyu ni Mr Roma Ramoni , ndio atakua mkufunzi wenu mkuu, ila kutokana na majukumu yake kuwa mengi hatakuwa na uwezo wa kuwa hapa kambini , bali wanajeshi wake hawa watatu wenye uwezo mkubwa ndio mtakuwa nao kwa miezi yote miwili ya mafunzo, Afande Diego, Adeline na Mollin ni wanajeshi kutoka jeshi la The Eagles , watawafundisha mbinu zote za kijeshi zinazowapa sifa duniani kama sehemu ya jeshi lenye nguvu kwa muda wote wa mafunzo , mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha mnatii na kutii na kutii maagizo yote kutoka kwao “
Wakati Afande Tobwe anaendelea kutoa maelezo , Roma alisogea mpaka sehemu waliosimama wanajeshi hawa na kuanza kukagua mmoja mmoja mpaka alipofika sehemu ambayo amesimama Mage.
“Unafanya nini hapa?”Aliuliza Roma , lakini Mage ni kama vile hajamsikia kwani alizidi kusikiliza kile kinachongelewa na viongozi wake wa jeshi.
“Nakuuliza tena unafanya nini hapa?”Aliongea Roma kwa sauti na kufanya wanajeshi waliokuwa pembeni kukosa utulivu na kujiuliza ni jamboo gani linaendelea kati ya mkufunzi mkuu na mwanafunzi.
Roma mwenyewe hakelewa kwanini Mage kaamua kujiunga na mafunzo hayo , kwani licha ya kuwa na wanawake wachache waliokuwa ndani ya hili eneo , lakini ni Mage pekee ndie ambaye alidhihirisha uzuri wa kipekee na hii ni kama ilimfanya kuwa na wivu kwa mwanamke mrembo kama Mage kuchangamana na sura ngumu kama hizo za kiume..
“Mwnaafunzi namba kumi na tisa kutoka kikosi namba mbili, mafunzo maalumu , salamu kwako mkufunzi mkuu”Aliongea Mage huku akipiga saluti baada ya kuona Roma anamuuliza maswali mengi na kwa jinsi Mage alivyokuwa akiongea ilimfanya Roma atamani kucheka , licha ya kwamba siku zote Mage alionekana kuwa siriasi akiwa eneo lake la kazi , ila mambo ambayo anayafanya yalimshangaza na kumfurahisha kwa wakati mmoja, maana hapa ni kama Mage hajawahi kukutana na Roma hapo kabla.
“Mage ni maigizo gani unafanya , nimekuuliza unafanya nini hapa na unajifanyisha kutokunifahamu, Wewe si polisi kwanini umeacha kazi yako na kujiunga na mafunzo ya jeshi?”Lakini licha ya maswali ya Roma ,Mage aliekuwa ‘mguu pande’ alikuwa amesimama pasipo kuongea chochote huku macho yake yote yakiwa mbele.
“Mkufunzi mkuu huna haja ya kumuuliza maswali mengi , Mage anaonekana kutopenda hata kuongea na wewe”Ilisikika sauti upande wa pili ya kiume na kumfanya Roma akasirike na kuweka sura ya mbuzi na kumgeukia mwanaue mwenye mwili uliojengeka kimazoezi.
“Wewe ni nani mpaka kutaka kuingilia mazungumzo yangu?”Aliongea Roma huku akimkodolea macho kwa ukaribu mwanajeshi aliekuwa amesimama karibu na Mage.
Licha ya kwamba muda huo wanajeshi hao walikuwa wakipokea maagizo kutoka kwa Diego na pia Afande Tobwe kuwepo juu sehemu maalumu ya kusimama , Roma hakujali kabisa na hata wakati alipokuwa anaongea na Mage , Afande Tobwe aliona hilo.
Siku chache nyuma Afande Tobwe baada ya Mage kurudi nyumbani na kumwambia kwamba anataka Kwenda jeshini swala hilo lilimshangaza na hata pale aliposikia sababu kubwa ya Mage kutaka Kwenda jeshi ni kwasababu ya mwanaume alishangaa mno na kutokana na uwezo wake wa kipelelezi aliweza kugundua Roma Ramoni ndio mwanaume ambaye mtoto wake huyo wa kike katokea kumpenda na jambo hilo alilihakikisha baada ya kumuuliza Magdalena na baada ya Magdalena kutingisha kichwa kama ni kweli Kanali Tobwe aliingia kwenye tafakuri nzito kwanzia siku hio na hata mke wake Mama P hakumueleza kuhusu mwanaume ambaye Mage katokea kumpenda alikuwa ni mume wa Edna , aliona lingeleta mgogoro katika familia lakini licha ya hivyo alionekana kuwa na maamuzi yake kichwani.
“Mwanafunzi namba kumi na sita , kwa jina la Baga , kutoka kikosi namba mbili , mafunzo maalumu , Mkufunzi mkuu naamini kwamba huwezi kumlazimisha Komredi Mage kuongea na wewe kama hataki kufanya hivyo”Aliongea Afande Baga pasipo kuwa na wasiwasi kabisa , alionekana kujiamini mbele ya Roma.
“Afande Baga kama nitamlazimisha kuongea na mimi utanifanya nini?”Aliongea Roma kwa sauti na kufanya wanajeshi wote kukosa utulivu kwani Roma aliongea waziwazi kiasi kwamba mpaka Afande Tobwe na Diego na wengine waliweza kusikia.
“Mkufunzi mkuu naomba swala hili tulimalize kwa mimi kupambana na wewe”Aliongea Afande Baga pasipo ya kuwa na wasiwasi na kumfanya Roma atabasamu.
“Unajiamini vipi kama unaweza kumshinda mtu ambaye ametambulishwa kama mkufunzi wako?”Aliuliza Roma.
“Mkufunzi mkuu , hata kama nitashindwa kukushinda , lakini siwezi kuogopa kupambana na wewe,nitakushikisha adabu”Aliongea na Baga Palepale alisogea mbele na kujitayarisha kimapambano, na Roma baada ya kuona staili ambayo Baga kaka alijikuta akitabasamu na kumgeukia Afande Tobwe
“Afande Tobwe naona staili yake ya kusimama ni ya kipekee , naamini pia mlitumia vigezo vya aina hii katika kuwachagua?”
“Ndio kila mwanajeshi tulieweza kumchagua katika wengi anamiliki aina ya mapigano ya kipekee , hatuna mpango wa kuwajengea mbinu mpya za kimapigano ila tunataka kuwaendeleza na uwezo wao wa kipekee ili kurahisisha mafunzo”Alijibu Afande Tobwe.
“Staili yako ya usimamaji ni kama ile ya wanamichezo wa mieleka lakini kwa namna ulivyosimama inaonekana kama staili ambayo watu wengi hudhamiria kufanya mapigo ya kuua moja kwa moja , kwakua umeyataka mwenyewe hakikisha unapigana kwa uwezo wako wote”Aliongea Roma
Baga baada ya kuruhusiwa kwa ajili ya pambano palepale alimsogelea Roma kwa spidi ya kasi kweli na kurusha ngumi kuelekea usawa wa macho na Roma aliikamata ngumi yake kwa nguvu na Baga kadri alivyokuwa akivuta mkono wake alishindwa na ilimbidi kutumia ngumi ya upande wa kushoto wa mkono wake na Roma aliikamata pia na baada ya Baga kuona mikono yake imeshikiliwa pasipo kuachiliwa ilibidi amsogelee Roma karibu kwa nguvu huku wakikutanisha mabega.
Baga baada ya kukutanisha mabega na Roma huku akimsukuma pasipo yakua na mafanikio palepale aliinua mguu wake juu kwa kudhamiria kumpiga Roma tumboni kwa kutumia Goti.
“Kuwa makini ”
Mage alijikuta akimtahadharisha Roma kwa pigo lile na Roma ni kama alikuwa akifanya makusudi kwani alimuacha Baga kumpiga kisawa sawa na kumfanya Roma kutabasabu baada ya kusikia sauti ya Mage.
“Haha.. kumbe anaongea”Aliongea Roma akimwangalia Baga aliekuwa akijipanga kuleta pigo lingine , lakini Roma palepale alisimama vizuri na kwa kutumia vidole viwili tu alimpiga Baga kwenye paji la uso.
Lilikuwa ni pigo la kitoto sana lakini lenye athati kubwa sana kwa Baga , kwani alirudishwa nyuma kwa nguvu isiokuwa ya kawaida na kutua chini kama mzigo kwa kutumia mgongo kiasi kwamba alijipigiza vibaya sana chini na kufanya watu wote waliokuwa ndani ya hili eneo kushangazwa na kitendo kile , kwani waliweza kuona namna ambavyo Roma alitumia vidole viwili kumpiga Baga.
Baga mwenyewe alielala chini hakuelewa hata ni nini kilichotokea na alimwangalia Roma kwa mshangao.
Roma baada ya kuonga Baga anamshangaa alimpa mkono akimpa ishara ya kusimama .
“Nashukuru kwa namna ulivyokuwa jasiri , lakini unachotakiwa kuelewa ni kwamba wewe ni binadamu na sio punda, Punda ni jamii ya mnyama na mnyama siku zote yuko tayari kwa lolote na asiweze kujizuia, lakini binadamu hupaswi kua kama mnyama , ukiona adui yako ana nguvu kuliko wewe na bado ukataka kujilinganisha nae na ukaishia kufa , basi huna tofauti na mnyama, rudi kwenye timu yako”Aliongea Roma na Baga ambaye alikuwa kwenye mshituko alirudi kusimama na wenzake.
Mage baaada ya kusikia maneno ya Roma alihisi kabisa Roma ameongea maneno yale kwa ajili yake na alijjikuta akianza kutoa machozi bila sababu ila Roma baada ya kuona machozi ya Mage wala hakujali Zaidi ya kuendelea kuongea.
“Sitohudhuria kwenye mafunzo haya mara kwa mara kwasababu wote mnaonekana kama kunguni kwangu , haina haja ya kukasirika kwasababu nimewatukana ila huo ndio ukweli na hata kwa kunguni hivyo hivyo pia ana kibonde wake anaemuona mdogo kuliko yeye , hivyo kama hamtaki siku nyingine kupigwa na vidole viwili kama Baga hakikisheni mnafanya mafunzo kwa kadri mnavyoelekezwa na kwa juhudi kubwa”
“Diego nitawapa mlolongo wa namna ya mafunzo kufanyika na baada ya hapo mtaendele na utaratibu ambao mtaona unafaa wenyewe , kwanzia muda huu mtaanza mafunzo yenu rasmi na mafunzo ya leo hayatakuwa juu ya uzito wala ustahimilivu , bali zoezi la leo litakuwa ni namna ya kujiokoa”Aliongea Roma na palepale wanajeshi wote waliokuwa wamezunguka eneo lile akiwemo Afande Tobwe walidondoka chini , kasoro wanajeshi wa The Eagles tu , Diego , Molin na Adeline ndio ambao hawakua wameathirika na Roma alitoa tabasamu na kuwaangalia.




SEHEMU YA 213
Haikueleweka Roma alikuwa amewafanyia nini , lakini wanajeshi hawa walionekana kuwa macho lakini viungo vyao havikuweza kufanya kazi , lilikuwa ni jambo la kushangaza ambalo Roma alifanya kwa wanajeshi wenye mafunzo takribani ya arobaini wote.
“Msiniangalie kwa macho ya mshangao , nishasema zoezi la laeo ni kijifunza namna ya kujiokoa , haijalishi huwezi kutembea , lakini kwasababu upo hai unatakiwa ujaribu bahati yako ya kujiokoa , kwa mtu atakae weza kufika upande ule wa pili wa msitu basi atakuwa ameweza kufanikiwa zoezi la leo”Aliongea palepale na wanajeshi walijihisi nguvu zao kurudi na Roma alitumia kingereza kuongea na Diego na palepale Diego aliekuwa mita kadhaa kutoka waliopokuwa wamelala wanajeshi alipotea na ile anakuja kuibka alikuwa mbele ya mwanafunzi namba moja na kumchapa Buti.
Na wengine baada ya kuona tukio hilo waliamka haraka haraka na kuanza kukimbia kwani kwa namna ambavyo Diego alimwadhibu mwenzao waliona pasipo kukimbia itakuwa ni zamu yao kupata pigo la namna hio.
Dadkika chache mbele wanajeshi wote waliiokuwa kwenye mafunzo maalumu walipotelea msituni na kuanza kukimbia kwa kujiokoa huku wakifukuzwa na Adeline Mollin , Pamoja na Diego.
“Kwa uwezo ambao wanautumia wanajeshi hawa wa The Eagles nimeamini sisi kama jeshi tuko nyuma sana”Aliongea Afande Tobwe huku wote macho yakiwa msituni.
“Wanajeshi wangu wote wanamafunzo maalumu ya Martial Art ambayo yanawafanya kuweza kukimbia kwa spidi kubwa , hii yote inawezekana kutokana na uwezo wa mtu anavyoweza kutumia nguvu za kiasili alizozaliwa nazo kwenye mwili wake, muda mwingine inaweza kuonekana kama uchawi lakini kwa mafunzo maalumu ni jambo linalowezekana”Aliongea Roma.
“Inaonekana itachukua muda mrefu Zaidi kwa wanafunzi wetu kuweza kufikia levo za wanajeshi wako”Aliongea mkuu wa kambi ya jeshi
“Hio itategemea na juhudi za kila mmoja”Alijibu Roma .
“Mr Roma naomba muda wako niweze kuzungumza jambo binafsi na wewe”Aliongea Afande Tobwe na Roma alitingisha kichwa na wakasogea pembeni.
“Najua unaweza kuwa na mshangao kwanini nimemruhusu Mage kufanya haya mafunzo”
“haina haja ya kelezea kila kitu kinajielezea..”Aliongea.
“Nyie vijana mna mambo sana.., ukweli mpaka sasa hivi sijaelewa moja kwa moja ni kipi kimetokea kati yako na Mage ,lakini nimeweza mpaka sasa kuelewa baadhu ya mambo”
“Nafikiri ulipata uelewa huo kwasababu wewe ni baba”
“Sio kweli , mwanzoni sikuwa nikielewa kinachoendelea Mage alivyoniambia anataka kujiunga na jeshi, ila kwa kupitia Magdalena niliweza kufahamu baadhi ya vitu”
“Kati ya Mage na Magdalena naweza kusema kwamba siku zote Magdalena ndio alieweza kuzaliwa na uwezo mkubwa Zaidi kuliko dada yake Mage na hii imekuwa ni athari kubwa kwa Mage , kwani tokea ni mdogo Mage alikuwa na juhudi nyingi sana ili kutaka kumzidi dada yake lakini mwisho wa siku aliishia kushindwa na hii ilimpelekea Mage kuwa na hasira za karibu sana na kuwa mkali sana lakini upande mwingine Mage ni moja ya Watoto wenye moyo mwepesi mno kuliko hata kwa Magdalena , ubabe wake wote upo nje tu, ni mwigizaji mzuri likija swala la kujifanyisha yupo imara lakini akiwa peke yake hubadilika kabisa”Aliongea Afande Tobwe.
“Wakati Mage alipoleta swala la kutaka kujiunga na jeshi kwangu lilinishangaza sana na hata mama yake lilimshangaza na sikuwa tayari kumruhsuu kwa namna yoyote ile kujiunga na jeshi , lakini nilipopata kujua sababu kutoka kwa dada yake nilishangaa , licha ya kwamba nilijua mmekutana mara kadhaa tokea unafika hapa nchini, lakini sikudhania kabia Mage anaweza akakupenda mwanaume wa aina yako”Aliongea na kumfanya Roma akune kichwa chake.
“Mr Roma sitaki Watoto wangu wote wawili kuwa wanajeshi , hii kazi ni hatari na ninaweza kuwapoteza wote kwa Pamoja , hivyo naomba unisaidie jambo moja”
“Ni kusaidie nini Afande”
“Mage yupo hapa kwasababu anahisi unamuona kama kiumbe dhaifu ambaye huwezi kuwa nae katika mahusiano na anachofanya ni kuhakikisha gepu ambalo lipo kati yenu kupungua , hivyo kwakua anakupenda na ni maamuzi ambayo amefanya yeye mwenyewe mimi kama baba yake nitamsapoti kwa namna yoyoyte ile , hivyo naamini kwasababu anakupenda bado, mrudishie angalau mapenzi kidogo aliokuwa nayo juu yako”
“Haha..sema nyie wazee mnanifurahisa sana tokea nifike hapa nchini , wewee na Balozi Ramadhani hamna tofauti kubwa , mnajua fika nina mke lakini bado mnataka niweze kuwa na Watoto wenu”
“Ni kweli lakini kama unao uwezo wa kuwaonyesha mapenzi wote kwa Pamoja , kwanini swala la Mage lishindikane , unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wote kwa Pamoja unawapa sehemu ndogo katika moyo wako, Wote hapa tunajua fika una wanawake wengi tofauti na mkeo”
“Mimi sio kama Ramadhani , yeye amefanya maamuzi yake kwasababu kuna faida anaitafuta kutoka kwako , yeye na familia yake , lakini sio kwa upande wangu ninachokifanya ni kuangalia furaha ya Watoto wangu na naongea kama baba anaefanya kila linalowezekana kuhakikisha Watoto wake wapo salama”Aliongea Afande Tobwe , lakini Roma kabla hajajibu, simu yake iliokuwa mfukoni iliita na baada ya kuangalia jina la mpigaji aliona ni Bi wema na alipokea haraka haraka na kuweka sikioni.
“Mr Roma kuna mgeni wenu hapa nyumbani anawasubiri”
“Unamaanisha nini kwamba anatusubiri Bi Wema?”
“Kwasababu anataka kuongea na wewe pamoja na Miss Edna”Aliongea Bi wema na kumfanya Roma ashanage ni mgeni gani hiyo ambaye anataka kuongea nae Pamoja na mke wake.
“Okey Bi Wema nipo njiani , kama ataweza kusubiri kwa masaa kadhaa nitafika hapo muda si mrefu”Aliongea Roma na akakata simu.
“Afande Tobwe , mimi nadhani sina cha kufanya hapa tena , nina mgeni ananisubiri nyumbani hivyo nitaondoka”Aliongea Roma.
“Hakuna Shida Mr Roma mpaka hapa sisi kama jeshi tunashukuru kwa kutimiza ahadi yako”Aliongea na Roma aliagana na maafande wengine na kuelekea upande alioacha gari yake.
Na ndani ya dakika chache tu alikuwa barabarani akielekea jijini Dar Es salaam.
*******s
VATICAN -ITALY.
Ni ndani ya ofisi kubwa ya kisasa iliopambwa kwa michoro mbalimbali ya kirumi , huku asilimia kubwa ya mwonekano wa ofisi hii kuonekana kupangiliwa na samani zilizokuwa katika rangi ya shaba Pamoja na dhahabu.
Mbele kabisa ya ofisi hii kulikuwa na meza kubwa ya kisasa iliokuwa na msalaba katikati juu ya meza huku ikiwa na vitabu vingi vilivyokuwa vimepangiliwa , pamoja na tufe lililokuwa likionyesha ramani ya dunia.
Upande wa kushoto wa ofisi hii kulikuwa na vinyago mfano wa sanamu mbalimbali vya kuchonga vilivyonakshiwa pia kwa rangi ya dhahabu , kimoja kikionyesha mwanaume aliepigiliwa misumari kwenye msalaba yaani Yesu na sanamu lingine pia lililikuwa likimuonyesha mama yake Yesu aliemshikilia mtoto, picha pia kubwa ya Papa wa kwanza kuliongoza taifa la Rome miaka mingi iliopita ilikuwa imetundikwa ukutani.
Kwa muundo wa ofisi hii ni Dhahiri kwamba haikuwa ofisi ya mtu wa kawaida kabisa ndani ya jiji lote hili takatifu la Vatican , kwani ofisi hii ilikuwa ikipatikana upande wa kaskazini mwa Vatican yaani upande wa St Peter Basilica.
Kwa upande wa nje kabisa wa jengo la ofisi hii iliokuwa kwenye jengo refu Zaidi kuliko yote ndani ya jiji hili takatifu la Vatican , kibao juu ya mlango kilisomeka kwa jina la ‘Papacy’.
Papacy ni neno linalowakilisha ofisi ya papa ndani ya Vatican , hivyo ofisi ambayo tuliiona kuwa na mpangilio mzuri na wa kipekee ilikuwa ni ofisi anayokaa kiongozi mkuu wa kanisa la kikatoliki duniani yaani Papa.
Naam ni dakika chache tu alionekana Papa aliekuwa kwenye mavazi yake ya kitamadni ya siku zote , Cassock choir Dress, akiwa akitembea kuelekea upande wa ofisi yake huku kila sister na mapadiri wenye vyeo vikubwa aliokuwa akikutana nao njiani humsalimia kwa kubusu pete yake iliokuwa kidoleni , pete ambayo ilikuwa ikiashiria mamlaka.
Ndani ya dakika chache Papa Andre Keish alisimama nje ya ofisi yake na kuvuta pumzi kabla ya kusukuma mlango na kuingia ndani ya ofisi yake na kwa jinsi ambavyo alionyesha hali ya kuwa na wasiwasi ni kama vile ofisi hio haikuwa ya kwake.
“Your Holliness…!!!”ilisikika sauti nzuri ya kike mara baada tu ya Papa kuingia ndani ya ofisi yake hii na alinyoosha mkono wake wa kulia uliokuwa na pete kuelekea kwenye kiti ambacho wageni hukalia kila wanapokuja kumtembelea na palepale , mwanga mkali kama wa jua ulisambaa chumba kizima na kumfanya Papa afumbe macho.
“Minerva… nimeitikia wito wako wa kutaka kuonana na mimi,nina ratiba iliobanana kwa siku ya leo ya kuongoza kusanyiko la watakatifu wa bwana”Aliongea Papa kwa Lugha ya kilatin na palepale mwanamke mrembo ambaye alikuwa amevalia sale za rangi nyeupe kama zile ambazo Masister huvaa….
“Your Holliness , We need to talk about future of the church and World”Aliongea Minerva , mwanamke mrembo ambaye kila mwanaume ambaye angemuona angemmezea mate kwani kadiri ulivyokuwa ukimwangalia ni kama uzuri wake ulizidi kuongezeka maradufu.
Mwanamke huyu hakuwa mwingine bali ni yule ambaye tulimuona akiongea na Yan Buwen usiku wa jana yake, mwanaume ambaye pia alikuwa akitambulika kama The Doni.
 
SEHEMU YA 214
Athena kwa historia ya Ugiriki ya kale alikuwa ni mungu wa vita , busara na ulinzi , katika miungu yote kumi na mbili katika historia yao, Athena pekee ndie aliekuwa akiongoza kwa akili nyingi sana.
Kwa upande wa Rumi kabla ya kuja kwa Christ Yesu, Minerva pia alikuwa na sifa zinazofanana na za Athena na wagiriki na waroma walikuwa wakiwaona kama mtu mmoja.
“Minerva unataka kuongea nini?”Aliuliza Papa Adre Kleish baada ya kukaa kwenye kiti chake na Athena bila ya wasiwasi alitumia kidole kimoja kuchora alama ya Zero na baada ya kumaliza alitumia mkono wake kupitisha mkono sehemu ambayo amechora alama ile na ilionekana ni kama mkono wake unamezwa na hewa lakini alipouvuta nje aliibuka na HollyGrail.
“Mtakatifu!,kikombe cha ukumbusho alichotumia Mesiah in last Supper”Aliongea Minerva na Papa alisimama kwa kutaka kushika kile kikombe kama mtu asieamini lakini Athena alikivuta nyuma.
“Minerva that is our sacred Treasure, You stole it from us”
“Minerva hio ni hazina yetu takatifu , Uliiba kutoka kwetu?”
“Your Hollines you are mistaken , I did not Stole it but I Secured it From Dark Parliament”
“Mtukufu umekosea ,sijaiba bali nilikilinda kutoka kwenye mikono ya Bunge la Kiza”
“Minerva wewe ni mtoto wa Mungu na Bwana yupo tayari kukupokea baada ya kukutakasa Dhambi zako zote , naomba urudishe hazina ya kanisa kwetu na ahadi zake zitatimia kwako”Aliongea Andre na kumfanya Athena kutabasamu.
“Hazina hii itakaa kwenye mikono yangu mpaka nitakapo pata majibu ninayo yataka Andre”
“Majibu Gani?”
“Nahitaji kujua siri ambayo ipo nyuma ya HollyGrail na muunganiko wake na Prior of Sion”
“Why must I?”
“Because I have been the Protector of this City for Centuries , I need to know the Codes Andre , I have my own limit in Diplomatic conversation , I will be Back when you have made Decision”Aliongea Athena akimaanisha kwamba anahitaji kujua siri iliopo nyuma ya HollyGrail huku akijinasibu ya kwamba alikwa mlinzi wa Vatican kwa karne na Karne na ameshachoshwa na mazngumzo ya kidimplomasia.
Unafikiri mpango wa Athena ni nini haswa…… na siri anayoitaka ni ipi.
******
Kutokana na mwendo ambao Roma alikuwa akiutumia haikumchukua muda mrefu kufika ndani ya jiji la Dar eneo la Tegeta na baada ya takribanni dakika arobaini na tano zingine ziliweza kumfikisha Kigamboni.
Roma baada ya kufunguliwa geti moja kwa moja aliingiza gari haraka na Kwenda kuliegesha katika eneo maalumu na kutoka, kwa jinsi magari yalivyoongezeka aliona kweli kuna ugeni hapo nyumbani na hata gari ya mke wake pia ilikuwa ishafika.
Sebuleni hapakuwa na mtu , lakini ile anashangaa alimuona Edna aliejiufunga khanga akiwa amebeba kikombe cha chai akipandisha ngazi Kwenda juu.
“Njoo kwenye chumba changu cha kujisomea tunasubiriwa”Aliongea Edna baada ya kusimama na Roma alitingisha kichwa na kuanza kupiga hatua kuelekea juu , huku akishangaa ni mgeni gani ambaye kamfanya Edna kutengeneza kahawa na kujifunga khanga kiunoni kama vile mama wa nyumbani kwani muda huo Roma alijiambia mke wake angekuwa kazini akiendelea na majukumu yake , lakini sasa hivi hali aliokuwa akiona ni tofauti kabisa.
Roma baada ya kuingia kwenye chumba cha Edna cha kujisomea alionekana mzee mmoja akiwa ameketi kwenye masofa huku akiwa amekunja nne na kushikilia moja ya kitabu katika vitabu vingi vinavyomilikiwa na Edna.
Roma kwanza hakumfahamu huyo mzee kwani hakuwahi kumuona mahali popote, Edna alieshikilia kikombe alikiweka mezani na kumkaribisha mzee..
“Roma umefika!... niliomba nitegenezewe kahawa na mkwe wangu hahaha…”Aliongea Mzee huyu kwa bashasha na alionekana hakuwa na wasiwasi kama vile yupo kwake.
“Wewe ni nani mpaka ujione huru kama hapa ni kwako?”Aliuliza Roma aliesimama mlangoni na mzee yule baada ya Roma kuuliza swali la namna hio alisimama na kisha akatabasamu.
“Mimi ni babu yako Camilllis Kweka ndio maaa….”Kabla hajamaliza Sentensi yake Roma kama upepo alikuwa ashamfikia na kumshika shingo na kumning`niza hewani na Afande Kweka alianza kutapatatapa.
Edna aliekuwa amesimama akiwa katika mshangao baada ya kusikia maneno ya Afande Kweka , alishangaa Zaidi na woga kuongezeka baada ya kumuona Roma amemning`iza mzee wa watu hewani.
Edna alikuwa akijua jambo ambalo Roma analifanya ni la hatari kwani alikuwa akielewa nguvu iliokuwa nyuma ya Mzee Kweka ndani ya taifa hili , licha ya mzee huyo mtoto wake kuwa raisi , lakini pia alikuwa akiogopwa sana jeshini na maamuzi yake yalikuwa yakiheshimiwa sana.
“Romaa…”Edna alijikuta akili yake ikirudi na kumkimbilia Roma na kumshika shati aache kile ambacho anakifanya.
“Unakuja nyumbani kwangu .. halafu unajifanya ni kwako na unaanza kuongea upuuzi wa ubabu babu”Aliongea Roma kwa hasira huku akizidi kumnyonga Afande kweka na alionekana hakuwa tayari kubembeleza.
“Roma muachie tafadhari... nakuomba”Edna alikuwa akiogopa kiasi kwamba hata machozi yalianza kujitengeneza kwenye macho yake.
“Swaaaaash!!!!”
Ulikuwa ni kama upepo uliomsukuma Roma na Kwenda kutua kwenye mlango huku akimwachia Afande kweka aliedondoka chini huku akianza kukohoa mfulilizo.
“Mr Roma naomba utulie tafadhari..”Aliongea Zenzhei aliembana Roma ukutani na kwa jinsi Roma alivyoshikiliwa ilikuwa ni ngumu sana kwake kuchoropoka kwenye mikono ya Zenzhei na jambo hili lilimshangaza sana.
“You Are cultivator ?””Aliuliza Roma kwa mshangao na kumfanya Zenzhei kutabasamu na kumwachia.
“Ndio Mr Roma mimi ni Cultivator kutoka katika miliki ya kijini kutoka china ,Hongmeng”
“Hongmeng..!!!, Your From Hongmeng?”Roma alijikuta akishangaa mno hakuwahi kufikiria kama atakuja kukutana na raia wa China kutoka Hongmeng”
“Lakini kwanini unatoa ‘Aura’ kama Ninja wa kundi la Yamaguchi?”
“Mr Roma hilo ni swala ambalo mimi na wewe tutakaa na kuzungumza ila kwa sasa unapasa kumsikiliza Camilius”Aliongea Zenzhei na kumfanya Roma akumbuke kuna mtu alietaka kumuua nyuma yake , ukweli alikuwa ‘Excited’ baada ya kukutana na mtu kutoka Hongmeng.
Hongmeng katika utamaduni wa Taifa la China watu hawa hufahamika kama walinzi wakuu wa taifa, licha ya kwamba Hongmeng ni kama jina linalotambulisha utamaduni kama vile neneo Hegemony , lakini kwenye tamaduni za kichina Hongmeng maana yake ni ‘Concealment’ au Siri kwa Kiswahili chake , sasa Hongmeng ni jamii ya siri ambayo ipo China ambayo ipo kwa mfumo wa hadithi yaani ni kama hapa Tanzania mtu akuambie ziwa Tanganyika kuna njia ya kuelekea ulimwengu wa majini ndio hivyo hivyo kwa upande wa China kuna jamii(realm) ya kijini ambayo kwao wanaitambua kama Hongmeng ,sasa kilichomshangaza Roma ni kwamba watu wote wa jamii ya Hongmeng huwezi ukawakuta kwenye ‘Mundane world’, yaani ulimwengu wa kawaida wa kuchanganyika na watu ni kama hivyo hivyo kwa majini kutopenda kuchanganyika na binadamu ndio hivyohivyo kwa Hongmeng , Katika hadithi nyingi za kichina inasemekeana kundi hili la watu kutoka Hongmeng wana nguvu za kichawi ambazo sio za kawaida kabisa , sasa hapa nitakueleza kwanini majini wanatofautiana nguvu.
Edna hakuelewa kinachoendelea na alishangaa kuongezeka kwa Zenzhei hapo ndani kwa ghalfla tu , japo alishukuru kupitia mchina huyo Roma alimuachia Afande kweka lakini alikuwa na wasiwasi , lakini mrembo huyu alikuja kuchanganyikiwa Zaidi baada ya kusikia namna mchina huyo alivyokuwa akiongea.Edna alimsaidia mzee Camilius kukaa kwenye sofa na kurudi nyuma
“Mzee inabidi ujielezee vizuri la sivyo utaondoka hapa ukiwa maiti”Aliongea Roma akiweka uso wa usiriasi na ilibidi Edna amsogelee na kumwambia atulie.
Na mzee Camillius alikaa vyema na kisha kutabasamu huku akishika shingo yake inayouma na kumpa ishara Zenzhei kumsogelea.
q



WATSAPP 0687151346 NICHEKI KWA KUPATA YTARATIBU WA MWENDEKEZO
 
Duuuuh chuma roma sasa nae zamu yake kukutana na wababe wake
 
Mkuu singanojr ,huyu Raheli ni wa babati yetu hii hii ya Manyara au kuna Babati nyingine?😂.. Atakuwa mburu wa Dareda au Bashnet huyu,maana kama namkumbuka kumbuka,😂..yani sura yake kama inakuja halafu inakataa😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…