SEHEMU YA 246
Edna alishangazwa na jibu la Najma lakini pia namna alivyokuwa anajiamini mbele yake na moja kwa moja aliona mapenzi ya dhati Najma aliokuwa nayo juu ya Roma mume wake.
“Najma nataka mimi na wewe tuwekeane ahadi”Aliongea Edna na kumfanya Najma kushangaa , hakujua Edna alikuwa akitaka kuwekeana ahadi gani na yeye ila alitaka kuisikia kabla ya kutoa maamuzi.
“Nataka unihakikishie kama Roma hatokutafuta Maisha yako yote usije ukamtafuta tena, mimi nitahakikisha namfunga miguu Roma kama mke wake na wewe uahidi mbele yangu, Suzzane akiwa shahidi kama hutokuja kumtafuta Roma wala kumsogelea tena”
“Sijakuelewa vizuri Edna unachomaanisha”Aliongea Najma na kumfanya Edna kufungua mkoba wake.
“Huu ni mkataba nilioandika usiku wa jana , ukisoma kila kitu utaelewa”Aliongea Edna huku akimkabizi Najma karatasi.
Najma alijikuta akitetemeka mara baada ya kusoma kilichokuwa kimeandikwa kwenye hio karatasi.
Edna alikuwa ameandaa mkataba wa ahadi ambao ulikuwa ukimtaka Najma kutomtafuta Roma kwenye Maisha yake yote wala kumsogelea kwa nia ya kutaka kuwa nae kimapenzi labda tu Roma mwenyewe afanye hivyo kwa hiari yake , huku upande wa Edna na yeye akiweka ahadi ya kwamba atahakikisha Roma hamtafuti Najma kwa vyovyote vile na ikitokea Roma kumtafuta Najma kwa hiari yake basi Edna hatokuwa na pingamizi tena na mkataba wa ahadi utavunjika rasmi na Najma kuwa huru kuwa na Roma kimapenzi.
Maelezo hayo sio ambayo yalimfanya Najma kutetemeka bali maneno ya chini yake mwishoni kabisa.
“Huna haja ya kuwa hivyo Najma , naelewa kabisa kwamba wewe na Roma mlikutana wa kwanza kabla yangu , hivyo sitaki kuwa mkatili , kama utasaini huo mkataba basi utapata faida mbili kama nilivyoeleza , kwanza nitagharamia matibabu ya kaka yako mpaka kubadilishwa figo , pili utapata ‘Scolarship’ ya kwenda kusomea nje ya nchi, najua una Diploma hivyo ni rahisi kudahiliwa kwa vyuo vya nje na masomo yako yatagharamikiwa na ‘Foundation’ iliochini ya kampuni yangu, Edna Foundation’”Aliongea Edna na kuendelea.
“Lakini pia kama itatokea umevunja mkataba kwa kumtafuta Roma basi gharama zote nitakazolipia inabidi ulipe mara mbili yake kama penati ya kuvunja mkataba kisheria”
“Edna.. uko siriasis juu ya hili?”Aliuliza Najma na kumfanya Edna atingishe kichwa kuashiria ni hakika.
“Nilichoandika hapo ni sahihi kabisa , kama utatia sahihi yako inamaanisha kwamba umekubaliana na mkataba wangu na kwanzia siku ya leo utakuwa kwenye kifungo cha kutumikia ahadi yako , na kaka yako atapatiwa matibabu kama nilivyosema na utachagua chuo chochote nje ya nchi na taasisi yangu itagharamikia masomo yako mpaka utakapomaliza”Aliongea Edna.
Najma alisoma upya karatasi iliokuwa kwenye mikono yake na kuingia kwenye mawazo na hata walivyofika mbele ya hospitalini ya Mloganzila hakuweza kutambua.
“Najma tupo hospitalini , fanya maamuzi sasa hivi”Aliongea Edna na kumgutusha Najma aliekuwa kwenye mawazo na Najma aliagalia jengo hilo la hospitali na kuanza kumfikiria kaka yake ambaye yupo kitandani akiugulia maumivu.
Upande wa Edna ukweli jana yake usiku alifikiria sana , licha ya kwamba alitamani kumsaidia Najma , lakini kama mfanyabiashara alitaka anufaike pia na ndio maana alikuja na wazo la kuandaa mkataba wa Najma kuacha kabisa kumfikiria Roma ili amsaidie kaka yake kupona , lakini wakati huo huo amsaidie Najma Kwenda nje ya nchi akaendelee na masomo , na aliamini kama Najma atamaliza kwenye chuo kikubwa huko duniani basi ingekuwa rahisi kutoka kwenye umasikini na hata kumpandisha hadhi yake, hivyo mkataba alioandika sio kwa ajili ya kumnyonya bali kumsaidia.
“Edna nipo tayari”Aliongea Najma na kumfanya Edna kutabasamu.
“Umefanya vyema Najma , Suzzane licha ya kuwa msaidizi wangu , lakini pia ni mwanaseria na atashuhudia makubaliano yetu”Aliongea Edna na kisha akatoa kalamu na kumpatia Najma kutia Saini kwenye nafasi ilioachwa wazi.
“Sina cha kupoteza , Roma hawezi kunipenda tena na kunioa , hivyo bora niyafikirie Maisha yangu kwa sasa ya baadae, najua Edna anajaribu kunisaidia kwa namna ya kipekee hivyo siwezi kumuangusha tena, nitakuja kumlipa wema wake siku nitakapofanikiwa”Aliwaza Najma na kisha alitia sahihi na akampatia kalamu Edna na kusaini pia na Suzzane nae akasaini.
Maongezi kati ya dokta mkuu wa hospitali yalikuwa yashafanyika na utaratibu huo ulifanywa na Suzzane hivyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuongea gharama tu na jopo la madaktari watakao husika na upasuaji.
Maongezi yalifanyika haraka haraka na Dokta Issay alifurahishwa na moyo mzuri wa Edna kumsaidia Juma na kumuona Najma kama mwanamke aliejaaliwa kuwa na marafiki wazuri.
“Najma unaonekana kuzaliwa na nyota kali sana , unatakiwa kujivunia ,wiki iliopita rafiki yako kakusaidia kiasi kikubwa cha pesa na leo hii pia Boss Edna hapa anakusaidia”Aliongea Dokta Issay na kumfanya Edna kushangaa lakini hakuuliza Zaidi ya kuagana na Dokta.
“Najma nafikiria unapaswa kumpigia Nasra simu , sijui nini kinachoendelea ila naamini ni rafiki mzuri kwako”Alimalizia Edna kuongea na Najma aliitikia kwa heshima , na Edna na Suzane waliingia kwenye gari na kumuacha Najma pasipo kujua kuwa Roma alikuwa akiwaangalia mita kadhaa kutoka waliposimama akiwa ndani ya gari.
*******
Roma baada ya kujua alichokifanya Edna hakuona haja ya kuendelea kubaki hapo hospitalini na hakutaka kabisa hata kuonana na Juma.
Aliondoka na kurudi kwenye kampuni ya mke wake na moja kwa moja alienda mpaka ndani ya ofisi ya Edna , alihitaji kujua ni nini kinaendelea.
Roma alimkuta Edna akiwa na baadhi ya mfanyakazi wa kampuni ambaye hakumtambua na aliacha wawili hao wamalize ndio aongee nae na mfanyakazi alionekana kupewa maelekzo na Edna yaliodumu kwa dakika kadhaa tu, na Roma aligundua mfanyakazi huyo ni moja ya viongozi wa moja ya kampuni za Edna ambazo zipo mikoani.
“Ngoja nikakutengenezee kahawa mke wangu kabla hatujaanza mazungumzo ya kina”Aliongea Roma huku akimwangalia Edna aliekuwa akijifanyisha kuwa bize na kupuuza uwepo wake.
“Haina haja , sema shida iliokuleta ofisini kwangu Mr Roma”Aliongea Edna , lakini Roma hakujali alitoka ndani ya ofisi ya Edna na kumuuliza Monica ni wapi anaweza kutengeneza kahawa na Monica ambaye hakuwa akimpenda Roma alimuonyesha kwa ishara upande wa kushoto .
“Dakika chache mbele Roma alirudi ndani ya ofisi ya mke wake na kisha kuweka kikombe mbele yake”.
“Mke wangu nikupendae kwa moyo wote , naomba upokee kahawa aliotegeneza mume wako kama ishara ya kukusapoti kwakile unachokifanya kwa taifa hili”Aliongea Roma huku akimwangalia Edna.
“Unaweza kusema sasa kilichokuleta”Aliongea Edna na kumfanya Roma afikirie kidogo , ukweli hakutaka kuongelea swala la kumuona Na Najma kule hospitalini kwani angeibua maswali.
“Edna nataka tuongee kilichotokea jana , sio kama unavyofikiria na sikupenda kukudanganya juu yangu na Najma , nilifanya hivyo…”
“Mr Roma, nipo kazini na naomba jambo lote ambalo utaongea ofisini kwangu liwe linahusiana na kazi tafadhari , Asante kwa kahawa na unaweza Kwenda kama huna jambo la ziada la kuongea”Aliongea Edna huku akiangalia tarakishi yake na kumfanya Roma avute pumzi.
“Alright kama hutaki tuongee tukiwa kazini basi tutaongea tukirudi nyumbani”Aliongea Roma na kisha aligeuka na kutoka ndani ya ofisini ya Edna.
Roma alienda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya Nasra , kuna mambo mawili matatu alitaka kuongea na mrembo huyo , kwani siku kadhaa nyuma hakuongea nae baada ya kujua kama Edna ni mke wake.
“Madam Nasra , Ninaweza kuingia?”Aliongea Roma baada ya kufnngua mlango na kumuona Nasra ambaye alionekana kuwa katika mawazo na Nasra aligeuza kiti na kumpa mgongo Roma.
Roma baada ya kuona hivyo , alijua mrembo huyo alikuwa na hasira na yeye hivyo aliona tiba pekee ni kumkumbatia na kumpiga busu na ndio alichofanya , lakini kwa Nasra alikuwa ni kama gogo , kwani hakutikisika.
“Bebi Nasra kama kuna shida ni bora ukaniambia kuliko kuninunia”Aliongea Roma na akageuza kiti cha Nasra na kumwangalia usoni , lakini ajabu mrembo huyo alikuwa akitoa machozi.
“Roma naomba nikuulize swali “Aliongea Nasra huku akimwangalia Roma usoni.
“Mhmh! Ongea Nasra na acha kulia maana machozi yako licha ya kukufanya uonekane mrembo lakini yananiumiza eti”Aliongea Roma huku akimfuta machozi Nasra kwa mkono.
“Nataka kujua nia yako ni ipi kuwa na mahusiano na mimi , huku ukijua Edna ni Zaidi ya ndugu yangu”Aliongea Nasra na kumfanya Roma asimama vizuri na kufikiria kidogo na mpaka hapo alijua kwanini mrembo huyo alionekana kutokuwa kwenye mudi nzuri.
“Nasra najua unaweza kuniona kama mwanaume mbinafsi na mwenye tabia mbaya, lakini kuhusu nilivyoanzisha mahusiano na wewe sikufikiria chochote zaidi ya kutaka kuwa na wewe, najua swala la Edna linaweza kuwa changamoto kwako na kukufanya uwaze , lakini nikuambie kwamba unawaza ujinga”Aliongea Roma na kumfanya Nasra amwangalie.
“Unasemaje nawaza ujinga , ilihali nimetembea na mume wa mtu”.
“Bebi Nasra unaonaje baadae nikija nyumbani kwako unipikie , nimemisi chakula chako na baada ya hapo tutaongea vizuri”Aliongea Roma.
“Siwezi kukaribisha mume wa mtu nyumbani kwangu tena , sitaki kumvunjia heshima Edna”
“Hehe.. tutaona kama unamaanisha hio baadae”Aliongea Roma na kisha alimsogelea Nasra na kumbusu shavuni na kutoka nje ya ofisi na ile anatoka kwenye korido macho kwa macho na Edna ambaye alionekana anatoka kwani alikuwa ametangulizana na Monica.
SEHEMU YA 247.
Edna alimwangalia Roma na kisha pasipo ya kuonyesha mabadiliko yoyote aliendelea na safari yake na kuingia kwenye lift na Roma alitabasamu na kisha alitembea mpaka kwenye ofisi ya Dorisi kwa ajili ya kumsalimia , lakini baada ya kufika ofisini kwake hakumkuta na aligeuza kuelekea kwenye idara anayofanyia kazi.
“Recho naona Ernest amekuwa na ukaribu mno na Benadetha?”Aliuliza Roma baada ya kufika kwenye meza ya Recho na hio ni baada ya kumuona Ernest Komwe, CEO msaidizi akiwa ndani ya ofisi ya Benadetha.
“Hehe.. unaona wivu kumuona mwanaume mwenzio akiongea na mrembo Benadetha?”
“Wewe nae na kakichwa kako kadogo , mimi nimeuliza na unaniuliza”Aliongea Roma na kumfanya Recho kumkagua Roma kwanzia juu mpaka chini ni kama kuna kitu anachokitafuta.
“Roma hivi wewe na Boss ni ndugu?”Aliuliza Recho na kumfanya hata Tina aliekuwa bize ainue macho yake na kumwangalia Roma.
“Kwanini unauliza hivo?”
“Unafikiri ni kawaida , kila mfanyakazi ndani ya hii kampuni anajiuliza swali la aina hio, umekuja si chini ya miezi mitatu , lakini sasa hivi mwenzetu ni Director , lakini mbaya Zaidi mnaonekana kuwa Pamoja”
“Sisi! , unaamaanisha mimi na Edna tunaoneka kuwa pamoja?”
“Ndio usichoelewa nini, mlienda Ufaransa Pamoja , lakini pia kwenye kusanyiko ile siku mlikuja Pamoja , tuna maswali ya kujua , si ndio Tina”
“Ndio Roma , tunataka utuambie ukweli leo , kama mna mahusiano tujue na kama hauna mahusiano nae utueleze mganga wako ni nani na sisi tukapate tiba”Aliongea Tina msambaa na kumfanya hata Roma kutamani kucheka na kushindwa kujua ajibu ni na aliishia kukuna kichwa.
******
Mheshimiwa Senga na Raisi mstaafu Kigombola walifikia kwenye makubaliano ya Yan Buwena kuendeleza tafiti za Marehemu Profesa Shelukindo , Raisi senga aliona hana haja ya kumzuia Mtangulizi wake katika hilo, lakini hakuacha kumpa tahadhadri ya kwamba Yan Buwen akifanya chochote ambacho kitafanya usalama wa raia kuwa hatarini basi hatovumilia juu ya hilo na mara moja Yan Buwen atakamatwa na vyombo vya sheria na Mheshimiwa Kigombola alimhakikishia Senga kwamba hakuna lolote ambalo linaweza kutokea na atakuwa karibu Zaidi na Yan Buwen.
Baada ya mheshimiwa raisi Senga kufanya kazi kwa muda mrefu mpaka muda wa chakula cha mchana , aliweza kupata smu kutoka kwa Senior.
“Ndio Senior”
“Senga nategemea kufanya ziara kwenye taifa lako ya siku mbili”Aliongea Senioit na kumfanya Senga kutabasamu.
“Nijambo jema kama utakuja Tanzania nadhani tutapata wasaa wa kuongea juu ya mipango yetu”
“Haswaa , hilo ndio linanifanya kuja Dar Es Salaam , nataka kumuona Edna pia Pamoja na mkwe wangu Roma”Aliongea na Senga alijikuta akibadili muonekano wake na ukawa usioelezeka anawaza nini.
“Senga najua unachofikiriria , ila tutaongea nikifika nchini Tanzania”
“Sawa Senior karibu sana , lakini bado hujanieleza mpango wako ni upi au unawaza kumuweka Edna wazi?”
“Hapana Senga , nataka unisaidie jambo moja kabla sijafanya safari yangu ya kuja Tanzania , nahitaji kuonana na wafanyanishara wakubwa ninaamini hio ni nafasi ya mimi kuonana na Edna”Aliongea Senior na kumfanya Senga afikirie kidogo.
“Okey Rafiki yangu , nadhani hilo linawezekana kabisa , nitawapa kazi wasaidizi wangu”
“Nitashukuru sana Senga , safari hii nitakuja kukuweka wazi mambo ambayo sikukueleza mapema , ili kuimarisha Zaidi uhusiano wetu lakini pia mipango yetu kwa maslahi mapana ya umoja wetu kitaifa”
“Ahsante Senior nategemea makubwa kutoka kwako”
“Haha.. sawa Senga nikutakie kazi njema”
“Ahsante Sana na wewe pia”Aliongea Senga na kukata simu.
“Ana mambo gani Senior anataka kuniambia au na yeye ni walewale wa kunificha , nakiri kwa sasa sina mtu wa kumuamini kabisa , napaswa kusimama mwenyewe, mwisho wa mwezi huu lazima niendele kwenye ibada ya mpasuko wa mwezi ili nijue namna ya kuongoza hili taifa na kudili na kila mmoja ambaye simuamini”Aliwaza Mheshimiwa senga.
“Mheshimiwa!!”Sauti ilimwita Mheshimiwa Senga aliekuwa kwenye mwazo na kuangalia mtu aliekuwa mbele yake, alikuwa ni Kabwe msaidizi wake.
“Nimeweza kufanya mawasiliano na Denisi na kumpatia ujumbe wa kurudi nyumbani haraka”Aliongea Kabwe.
“Shukrani Kabwe , unaweza Kwenda kama hakuna lingine muhimu”Aliongea mheshimiwa na kumfanya Kabwe kugeuka na kuondoka.
Senga licha ya kuonekana vyema kwa muonekano wa nje ila kwa ndani alikuwa akiungua , mke wake Damasi alikuwa amemchunia kutokana na Denisi kuwadanganya na Damasi alielekeza lawama zote kwake na aliona mke wake ana haki ya kumlaumu kwani siku zote alikuwa ni mwenye kufikiria uongozi pasipo kujali familia yake na matokeo yake Denisi anaamua kufanya kile anachoepnda pasipo ya yeye kuelewa.
Senga alikaa kwa dakika kadhaa na kisha alichukua simu yake na kupiga namba ambayo ilionekana kuwa ya nje ya nchi.
“Hello Dady”
“Hello My Daughter, unaendeleaje”
“Niko salama Dady how are you and mom?”
“We are fine my daughter, unarudi lini nyumbani?”
“Dady kuna tatizo…”
“Hapana tumekumiss mimi na mama yako”
“Ooh nikajua kuna tatizo , hujawahi kunipigia na kuniulizia narudi lini nyumbani baba, I real miss you and Mom too”Aliongea Ashley mtoto mkubwa wa Raisi Senga ambaye alikuwa ni mwanasayansi anaefanya kazi na Profesa Clark Stephanie.
“By the way Dady , how is Roma doing , do you keep in touch with him?”Aliuliza Ashley na kumfanya Senga kushangaa kidogo na moyo wake Kwenda kasi.
“ I don’t ,Why!, Unafahamiana na Roma?”Aliuliza Senga kwa sauti lakini hakukuwa na jibu upande wa pili na alishusha simu na kuangalia kama simu imekatwa , lakini aligundua bado ipo hewani.
“Ashley nimekuuliza swali”
“Dadii, Calm down , I was just asking if you are keeping in touch with him , you should if not dady, I know he is…”
“Baba,Punguza presha , nilikuwa na nauliza tu kama unawasiliana nae, unapaswa kufanya hivyo kama bado, najua yeye ni..”
“He is what Ashley , niambie umegundua nini?”
“Dady am sorry I Should have told you this soon , but I was worried and nor sure at the same time”
“Baba unisamehe , nilitakuwa kukueleza hili mapema , lakininilikuwa na wasiwasi na kutokuwa na uhakika kwa wakati mmoja”
Aliongea Ashley na kumfanya Senga kuvuta pumzi , kuna kitu amekingundua kwenye sauti ya Ashley.
“Niambei ni kipi unachotaka kunieleza, kinachokufanya kuwa na wasiwasi na kutokuwa na uhakika nacho kwa wakati mmoja Ashley”
“Nilifahamiana na Roma tokea naanza masomo yangu ya digrii, nilikutana nae Uingereza dady, I kept the truth hiden even when he was before you and mom, Dady forgive me, I had to pretend for some reason”Aliongea Ashley na kumfanya Senga kuvuta kidogo pumzi apate kupumua vizuri maana aliona ni mwendelezo wa maigizo kwa kila mtu anaemzunguka na aliwaza sijui na mke wake kuna jambo gani hajamwambia bado maana ndio kabakia.
“Ashley kuna mahusiano yoyote kati yako na Roma ?”Aliuliza Raisi Senga kwa wasiwasi.
“Dadiii…”
“Tell me everything Ashley”
“ Yes Dady,, we have been so far…”Aliongea Ashley na kumfanya Senga asiamini masikio yake na aliomba kile anachofikiria kisiwe sahihi.
“Dady sio kama unavyofikiria , I mean… I know he was my brother”Alimalizia Ashley.
“What..!! , You knew this even you”
“Dady I am so sorry , I know it`s not right for us to talk this over the phone , but I had the reasons, forced not to say anything when I Confirmed he was real my brother”
“Baba naomba unisamehe ,najua sio sahihi kuongelea kwenye simu , lakini nilikuwa na sababu , nililazimishwa kutoongea chochote , nilipothibitisha kama kweli ni kaka yangu”
“Ulilazimishwa nani mpaka ukashindwa kuniambia mimi na mama yako , kwanini kila mtu anafanya anavyotaka na hamnipi heshima yangu kama baba yanu”Aliongea Raisi Senga kwa hasira.
“Grandpa ndio alieniambia kwamba nisiongee chochote mpaka muda sahihi utakapofika”Aliongea Ashley na kumfanya Senga akose nguvu na alitamani apae akamtangwe risasi baba yake mzazi , kwani aliona michezo anayomfanyia imemzidi kimo.
“Huyu mzee kwanini ananizidi akili kwa kila kitu ninachokifanya , mimi ni nani kwenye Maisha yake mpaka kunifanyia mchezo mpaka na Watoto wangu”Aliwaza Senga kwa hasira huku akipangua mafaili yaliokuwa mezani na kumfanya katibu muhtasi wake kuingia baada ya kusikia vitu kudondoka.
*******
Ni muda wa saa kumi na mbili za jioni Edna alionekana akiwa ndani ya chumba chake akipangilia baadhi ya vitu vyake muhimu ambavyo alitoka navyo Kigamboni.
Wakati ekiendelea kuwa bize akipembua kitu kimoja kimoja na kukiweka katika sehemu husika , mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa na alionekana mrembo Mage akiingia ndani ya chumba hiko.
“Edna..!”Aliita Mage na kumfanya Edna aliekuwa akipanga vitu kwenye kabati kubwa kugeuka nyuma na baada ya kugundua ni Mage alimsogelea na kumkumbatia.
“Edna nimekumisije jamani , nilivyosikia mmerudi Osterbay nimekuja mbio mbio huku kabla hata sijatulia”Aliongea Mage na Edna alitabasamu.
“Ndio tumehamia huku kwenye nyumba kubwa , karibu sana”Aliongea Edna huku Mage akiketi kwenye kitanda kikubwa cha Edna.
“Usiniambie hio nayo ni staili siku hizi”aliongea Edna huku akimwangalia Mage kichwani , Edna licha ya kumzoea Mage siku zote kutokuwa na nywele ndefu , lakini hakuzoea kumuona na kipara.
“Nilikuwa jeshini”Aliongea Mage na kumfanya Edna kushangaa
“Jeshini!, uliacha Upolisi?”
“Nilitaka kuacha ila nimeghairi , mafunzo ya jeshi yamenishinda na kukimbia”Aliongea Mage huku akidanganya , kwani ukweli ni kwamba tokea aonjeshwe utamu na Roma hakuweza kuvumilia kubaki jeshini, alitamani kurudi ili amuone Roma , lakini pia hata Roma mwenyewe alikuwa ashamwambia aachane na jeshi , hivyo alijiambia yeye ni nani hata akatae kile ambacho bebi wake amesema.
“Hahaha.. nilijua upo ngangari kama Magdalena , kumbe mtoto soft”Aliongea Edna na kumfanya Mage kucheka.
“Hiki chumba kinanikumbusha tulivyokuwa wadogo , hakina mabadiliko makubwa”Aliongea Mage na kumfanya Edna kutabasamu.
“Kimejaa kumbukumbu nyingi sana za utoto wangu”Aliongea Edna huku Mage akiendelea kuangalia , lakini macho ya Mage yalivutiwa na karatasi iliokuwa karibu yake na aliichukua na kuishikilia mkononi huku Edna akimpa mgongo.
“MARRIGE CONTRACT” neno mkataba wa ndoa ndio ambalo lilimvutia sana Mage..
“Edna huu….. mkataba usiniambie ni wa kweli?”Aliongea Mage kwa mshangao mkubwa , ni kama kitu kilichokuwa kwenye mikono yake ni feki.
Edna aligeuka haraka haraka huku akijilaumu kusahau kuhifadhi karatasi za mkataba wa ndoa yake na Roma kwenye kabati.
Edna alimwangalia Mage alieshikilia karatasi na kushindwa hata ajibu nini kwani siri yake imefichuka.
SEHEMU YA 248.
LONDON—KENSIGNTON PALACE.
Ni ndani ya jumba la Kifalme ndani ya jiji la London Uingereza , anaonekana mrembo Ashley akiingia ndani ya jumba hilo akiwa amesindikizwa na walinzi wawili wa kike.
Ashley licha ya kwamba haikuwa mara yake ya kwanza kufika ndani ya hili eneo lakini hakuweza kuzoea mazingira ya ndani ya jengo hili na kama siku moja ataingia mwenyewe pasipo muongozo maalumu basi angeweza kupotea.
Mitindo ya kizamani ya upambaji wa jumba hili ndio moja ya vitu vilivyomvutia Zaidi Ashley.
Alitembea akiwa na mlinzi mpaka ghorofa ya tatu na kukaribishwa eneo la sebuleni na ‘House Keeper ‘ huku akiambiwa asubiri.
Dakika chache mbele baada ya kusubiri alionekana Profesa Clark Stephanie alievalia gaunni la Rangi nyeupe la maua maua na visendo vya rangi nyeupe akishuka kutoka juu ya ghorofa.
“Ashley you are here”Aliongea Profesa Clark na kumfanya Ashley kusimama na alisogeleana na Clark na kukumbatiana.
“Let us sit and talk, Shall we?”Aliongea Clark na Ashley aliitikia kwa kichwa na kuketi kwenye masofa hayo ya kifahari.
“Kwanini unataka kurudi Tanzania katikati ya project Ashley?”Aliuliza Profesa Clark huku akimwangalia Clark.
“Nina matatizo ya kifamilia. Profesa I told my father about Roma, I am so stupid , I should have told him in person not over the phone”Aliongea Ashley na kumfanya Clark kushangaa kidogo.
“Kwahio tatizo liko wapi kama ushamwambia tayari , hili ni jambo ambalo alipaswa kujua tokea miaka minne iliopita na mimi nilikuzuia kwasababu maalumu”
“Ndio naelewa Profesa , ulinieleza nikae kimya , lakini bado nahisi kuikosea familia yangu , Hususani baba inaonekana anafahamu tayari kuhusu Roma and he wasn’t surprised at all , it looks like he knew it from Grandpa….”Aliongea Ashley huku akionekana kujutia , mrembo huyu licha ya kwamba anayo PhD lakini bado alionekana sio mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza hisia zake.
“Ashley I kbow that feelings, and you should go and explain it, you are not going to concentrate with Project anyway with that situation”Aliongea Clark na kumfanya Ashley kutabasamu.
“Professor naweza kuelezea kila kitu kuhusu Roma , kuanzia siku ambayo nilitambua kuwa ni kaka yangu?”Aliuliza Profesa na kumfanya Clark afikirie.
“Ndio unaweza kuelezea , lakini ukumbuke tulimficha Hades juu ya uhusiano wako na yeye kwa muda mrefu”
“Naelewa Profesa , nampenda sana kaka yangu , ijapokuwa mama sio mmoja lakini tunashea damu moja, natamani kumuona Roma akimtambua baba”Aliongea Ashley na kumfanya Clark kumsogelea na kumshika mkono.
“Ashley unajua ni sababu gani nilikuchukua kipindi kile na kuwa mwanafunzi wangu na ukawa mtu wa kwanza kuingia kwenye maabara yangu?”Aliuliza Porfesa na Clark alitingisha kichwa kwamba hajui.
“Because you are Empaths”Aliongea Profesa akimaanisha kwamba Ashley ni mtu ambaye ana uwezo wa kuhisi maumivu na hisia za wengine wanaomzunguka.
“There is no static logic when it comes to family matter`s , all Decisions are always influenced with our own intuition and Intuition is common sense so you should do what feels right for your family”
“Hakuna mantiki maalumu likija swala la kifamilia , maamuzi yote yanaathiriwa na uangavu wetu wenyewe na uangavu ndio akili ya kawaida , hivyo unapaswa kufanya kilichobora kwa familia yako”Aliongea Profesa na Ashley alitabasamu na kisha waliagana.
*******
Mage alijikuta moyo wake ukijawa na furaha mno, hakuamini kama ndoa ya Edna na Roma ilikuwa ni feki , mrembo huyu licha ya kwamba alikuwa akimpenda Roma lakini alijawa na hatia kwani Roma alikuwa ni mume wa Edna , lakini leo hii ni kama alitua mzigo kwenye moyo wake baada ya kugundua kuwa Roma na Edna ndoa yao si kwasababu ya mapenzi bali ni ya kimkataba tu, alisoma vyema mkataba huo na aligundua ni kama mwezi tu uliokuwa umebaki kwa Roma na Edna kumaliza siku zao walizoahidiana kua Pamoja kama mke na mume..
Edna yeye kwasababu alimchukulia Mage kama rafiki yake , hakuona haja ya kumficha na alimweleza namna ambavyo walifunga ndoa na Roma , kwamba yote ilikuwa ni kumuepuka marehemu baba yake kumlazimisha kuolewa na mtu asiempenda.
“Edna niambie ukweli, Unampenda Roma?”Aliuliza Mage huku akimwangalia Edna kwa shauku.
“Kwanini unauliza hivyo?”
“Nataka kujua kama unampenda Roma licha ya kwamba umefunga nae ndoa ya kimkataba”Edna ukweli hakuwahi kujiuliza swali kama hilo na hata alipoulizwa alishindwa kuwa na majibu ya moja kwa moja.
“Sister Edna kuna hii kadi imeletwa kwa ajili yako”Aliongea Yezi aliengia chumba cha Edna na kufanya mazungumzo kati ya Mage na Edna kuvurugika.
Edna alichuku kadi iliokuwa ipo kwenye mikono yake na kuanza kuisoma , ilikuwa ni kadi iliokuwa ikionyesha mwaliko wa kuhudhuria kikao cha wafanyabiashara wakubwa nchini na Raisi wa Rwanda , mheshimiwa Paul Jeremy.
“Asante mdogo wangu”Aliongea Edna na Yezi alitabasamu
“Edna ngoja nirudi nyumbanni Baba na Mama wananisubiria, ndio kwanza nimerudi sasa hivi na sijawapa maelezo mazuri kwanini nimekimbia mafunzo ya jeshi”Aliongea Mage huku akinyanyuka na Edna aliafana na Mage na kuahidiana watatembeleana mara kwa mara kwani ni majirani.
“Safari yangu imejawa na bahati kubwa , nimefika tu nyumbani na nimegundua Edna na Roma hawaja oana kwa mapenzi, Roma ukishaachana na Edna utanioa mimi”Aliwaza Mage wakati akitoka kwenye geti la nyumba ya Edna.
Upande wa Edna baada ya Mage kuondoka aliingia kwenye mawazo, huku akiangalia karatasi ya mkataba wa ndoa, mrembo huyu alionekana kujiuliza maswali mengi na kukummbuka mengi ambayo Roma na yeye wamefanya.
Alijikuta akikumbuka kitendo walichofanya na Roma kule Kigamboni jana yake na alijikuta akitabasamu na kujionea aibu na kuuhifadhi mkataba ule kwenye Droo ya kabati.
*******
Kuanzia saa moja kamili mpaka saa mbiili na nusu Roma na Nasra walionekana kuhemeana kama vile ni mabeberu huku kila mmoja akionekana kutoa jasho jingi na shughuli iliofanyika hapo kitandani ilionekana pevu , na haikueleweka ule msimamo wa Nasra alioongea mchana uliishia wapi , kwani tunachoona mrembo huyu sio tu kumkaribisha Roma nyumbani kwake , lakini pia alimpatia kabisa na kitumbua.
“Bebi Nasra usiniambie ulijaza asali kabla ya mimi kuja?”Aliuliza Roma aliemkumbatia Nasra kwa nyuma huku wote wakiwa uchi.
“Ushaanza kuongea ujinga”Aliongea Nasra kwa aibu lakini na kufurahi kwa wakati mmoja kwani aliamini Roma atakuwa amefurahi.
“Hehe.. haina haja ya kuona aibu cha urembo”Aliongea Roma na kumbeba Nasra juu juu na kuzama nae bafuni na kilichosikika ni vicheko vya Nasra , na haikueleweka alikuwa akitekenywa au ni kipi kilichokuwa kikiendelea ,ila jambo moja la uhakika ni kwamba Nasra alikuwa ashayavulia maji nguo na hakuwa na budi kuyaoga , hakumuwaza tena Edna na alikuwa ni kama Dorisi tu, wote walijiambia watashea mwanaume mmoja yaani Roma au mfalme Pluto.
“Najma niambie kuhusu urafiki wako na Najma”Aliongea Roma na kumfanya Nasra kudondosha kijiko chini kwa mshangao.
“Roma una..”
“Nasra huna haja ya kupata mshituko, ndio nafahamiana na Najma, yeye na kaka yake ndio watu pekee waliokuwa kama ndugu kwangu nilivyofika hapa Dar”Aliongea Roma na baada ya kumaliza sentensi yake machozi yalikuwa yamemjaaa Nasra na Roma alishangazwa na hilo.
“Roma usiniambie mwanaume ambaye Najma anampenda ni wewe?”Aliuliza Nasra kwa wasiwasi na Roma hakuona haja ya kuficha na alimueleza ndio.
“Nasra subiri..”
“Roma naomba uondoke nyumbani kwangu”Nasra alibadilika ndani ya dakika chache huku akihisi kifua chake kupanda na kushuka kwa wakati mmoja.
“Roma naomba uongoke tafadhari..”Aliongea Nasra huku akikimbilia chumbani kwake na Roma alishangazwa na mabadiliko ya Nasra ,ila alishindwa kuendelea kukaa hapo ndani, aliona ni bora kuondoka na atakuja kumtafuta akishatulia.
Nasra alijikuta akilia ndani ya chumba chake kwa muda mrefu ,mpaka pale aliponekana akitoka akiwa na mkoba na funguo za gari na kwa jinsi alivyoonekana ni Dhahiri alikuwa akienda nyumbani kwa rafiki yake Najma..
Sasa wakati anaingia kwenye gari yake tun a kuliwasha , simu yake ilitoa mlio wa kuingia kwa ujumbe wa meseji na aliinua haraka hara na kisha kuangalia ujumbe huyo na alijikuta akinyong`onyea kwenye siti yake.
“Najma Am rel sorry sikufahamu , this is all because of Roma . Roma I hate you”Aliongea Nasra huku machozi yakimtoka.
SEHEMU YA 249
Ni muda wa saa mbili usiku , familia nzima ilikuwa mezani kasoro Roma peke yake ambaye aliaga tokea saa kumi na mbili kama anatoka na bado hakuwa amerudi.
Edna alikuwa akila chakula mdogo mdogo pasipo ya kuwa mchangiaji wa stori , alionekana kuwa mpole kuliko isivyokuwa kawaida , jambo hilo lilimfanya Blandina moyo wake kuuma , kama mama aliona Edna anateseka na kutokuwepo kwa Roma na alishindwa cha kufanya kumfariji Edna.
Wanafamilia walikula chakula mdogo mdogo huku stori za hapa na pale zikiendelea na Edna ndio aliekuwa wa kwanza kumaliza kula chakula na alirudi kwenye chumba chake cha kujisomea , chumba ambacho miaka kadhaa nyuma kilikuwa kikitumiwa na Bibi yake Pamoja na mama yake , ni chumba kikubwa kweli chenye vitabu vingi kuliko kile cha kule Kigamboni na vitabu vilionekana kupangiliwa kwa usafi wa hali ya juu.
Upande wa kushoto kulikuwa na tarakishi kubwa ya kampuni ya Apple na meza kubwa , kwa muonekano wake ni kama ofisi, na kama Edna ataamua kufanyia kazi zake hapo ndani basi isingeleta shida yoyote kwani kila kitu cha kiofisi kipo.
Moja ya sababu kubwa ambayo humfanya Edna kupotezea mawazo mabaya ni uwezo wake mkubwa wa akili , Edna ni mtu anaependa utulivu, ni aina ya watu wenye haiba ya ukimya na upole na mara nyingi hata jambo likimuudhi hatoongea chochote Zaidi ya kukaa kimya na kutafuta jambo la kufanya ili kumfanya kuwa bize, na Edna ndicho alichofanya baada ya kuingia kwenye chumba hiko , kwani alianza kufanya kazi ambazo hakuzimaliza ofisini kujiweka bize.
Nusu saa mbele mlango ulifunguliwa na alionekana Blandina aliebeba juisi na kuingia ndani ya chumba hiko na kumwangalia Edna aliekuwa bize na kazi.
“Edna mwanangu , unapendeza unavyoonekana kuwa bize na kazi”Aliongea Blandina huku akikagua chumba hiko na alimpatia na juisi.
“Ahsante mama”Aliongea Edna huku akitabasamum haikueleweka Blandina alitaka kuongea nini na Edna ila hakuweza kuongea na alimuacha Edna kuendelea na kazi huku akimwambia kuwa akichoka akapumzike asijitese kufanya kazi muda mrefu na Edna aliitikia kuwa atafanya hivyo , huku akijisikia vizuri, kwani aliona Mama mkwe wake anaonekana kumpenda na kumjali.
Saa sita kamili za usiku ndio muda ambao Roma alirudi na kabla hajaenda kwenye chumba chake alielekea kwanza kwenye chumba cha Edna na kujaribu kusukuma mlango na alitabasamu baada ya kugundua haujafungwa kwa Ndani.
Roma aliingia kwenye chumba hiki cha mke wake kimya kimya na kumwangalia Edna ambaye alionekana kuwa katika usingizi mzito, Roma alimfunika vizuri Edna na kisha alimwangalia usoni , alipendezwa na namna ambavyo Edna alikuwa amefumba macho na kuwa usingizini kwani alionekana kama mtoto.
“Nakupenda sana Edna mke wangu.., unaonekana kuwa mrembo Zaidi unapolala, Usiku mwema”Aliongea Roma kwa kunong`ona na kisha akambusu Edna kwenye paji la uso na kutoka nje ya chumba hiko, lakini ile anafunga mlango kwa nje , Edna alionekana hakuwa amelala na alimsikia Roma vizuri na kuishia kutabasamu na kufumba macho na kuendelea kulala.
Ukweli ni kwamba Edna baada ya kumaliza kufanya kazi zake na kurudi ndani ya chumba chake kwa ajili ya kupumzika hakulala , alikuwa macho mpaka wakati alipoona gari ya Roma ikiingia na kusimama maegeshoni ndio muda ambao alipanda kitandani kulala , kwani alionekana kuridhika baada ya kumuona mume wake kasharudi salama.
Sasa haikueleweka kama Roma asingerudi na kuendelea kutafuna kitumbua cha Nasra ingekuwaje, tushukuru kukasirika kwa Nasra kwani mrembo Edna aliweza kumuona mume wake akirudi kutoka kwa mchepuko wake na kupumzika.
********
“Najma naomba unisamehe rafiki yangu , sikufahamu kabisa kama The chosen one ndio Roma”Aliongea Nasra baada tu ya kufika Mbagala na Najma alikuwa na hasira mno kwani hakutaka kabisa hata kumkaribisha ndani rafiki yake.
Lakini licha ya hivyo Najma alikuwa ashaanza kumhurumia Nasra, ambaye alionekana kujutia na Najma pia aliona makosa ni ya kwake kwani licha ya kumpenda Roma na kumwambia Nasra kuhusu The Chosenn one lakini hata siku moja hakuwahi kumuonyesha Nasra sura ya Roma.
“Najma mwenyewe sikufahamu kama Roma ni mume wa Edna ndio nimefahamu juzi , kama ningejua mapema…”Aliongea Nasra na kuanza kulia , Nasra hakuwa tayari kukosana na Najma , alikuwa akimchukulia Najma kama ndugu yake wa pekee hapa mjini na ndio maana alikuwa tayari kufanya chochote kile kwa ajili ya kupewa msamaha , kwa upande wa Najma pia ilikuwa hivyo hivyo , licha ya kwamba alikuwa na hasira na Nasra lakini hakuwa tayari kumpoteza.
Nasra alieleza tokea siku ya kwanza anakutana na Roma kwenye usaili , lakini pia siku ambayo alijikuta akiwa uchi mbele ya Roma pasipo kutambua nini kilitokea na namna ambavyo mahusiano yake na Roma yalivyoanza na namna ambavyo hakuweza kutambua Roma ni mume wa Edna , mpaka siku ambayo pia Nasra alimpigia magoti Edna kwa ajili ya kumuomba msamaha , mrembo huyu alimweleza rafiki yake kila kitu na hio yote ni kutaka kumfanya Najma kumuamini tena.
Najma aliona ukweli katika maneno ya rafiki yake na hakuona haja ya kutokumsamehe , alimsogelea na kumkumbatia na wakaanza kulia Pamoja baada ya kusameheana.
Ni asubuhi Nasra alionekana akitoa gari yake ndani ya eneo la Bias akiitafuta barabara kuu kwa ajili ya kurudi nyumbani kwake na kujiandaa kwa ajili ya Kwenda kazini , njia nzima mrembo huyu alionekana kufikiria yale ambayo waliongea jana usiku na rafiki yake Najma.
Hakuamini kama Edna ameamua kumsaidia Najma kwa ajili ya kaka yake kupatiwa matibabu , hela ambazo Edna ametoa kwa ajili ya matibabu zilikuwa nyingi sana na ndio maana Nasra alijikuta akimfikiria Edna.
Ukweli ni kwamba Nasra hakufahamu kama kuna ahadi Najma na Edna wamekubaliana na Najma hakumueleza Nasra kutokana na kwamba mkataba wake na Edna ulikuwa ni siri na maelekezo hayo alipewa na Edna , hivyo aliamua kukaa kimya na kutokumuambia Nasra na ndio maana asubuhi hio Nasra alikuwa ni mwenye kujiuliza Edna ni kiumbe gani mwenye roho nzuri mpaka kutoka kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya matibabu ya kaka yake na Najma , alimuona Edna kama Malaika.
“Ngoja nikifika ofisini lazima nimpe shukrani zangu kwa kumsaidia rafiki yangu Najma”Aliwaza Nasra huku akizidi kukanyaga pedeli kuelekea Mikocheni nyumbani kwake.
*********
“Camillius wageni wetu washafika”Aliongea Zenzhei akimwamsha Afande kweka ambaye alionekana kupumzika ndani ya chumba chake.
“Asante Zenzhei , waelekeze chumba cha kukutania wageni ninakuja muda si mrefu , unaweza pia kuendelea na taratibu zingine”Aliongea Afande kweka na Zenzhei aliitikia na kutoka ndani ya chumba cha Afande Kweka kwa ajili ya kuelekeza wageni wake.
Ni ndani ya nyumba ya pili yake ndani ya uzio wa jumba hili analoishi afande kweka , mita kadhaa kuna nyumba nyingine ambayo mara nyingi Afande kweka hupenda kufanyia vikao ambayo vinahusu watu wengi lakini pia vya siri sana.
Sasa ndani ya jumba hili wanaonekana watu wanne jumla ambao ndio wageni wanaopaswa kuonana na Afande kweka , wageni hawa wa kwanza alikuwa ni Mellissa Luiz, wa pili ni Nadia Alfonso , wa tatu ni Zoe Kovac na mwingine ni mwanaume mzungu alievalia suti ya rangi ya samawati ambaye hakufahamika jina lake, ambaye kwa muonekano wake si chini ya miaka hamsini hivi.
Zenzhei Pamoja na wahudumu wa kasri hili la Afande kweka walionekana kuwa bize wakiwapa huduma wageni hawa ili kuwafanya wajisikie wapo nyumbani.
Baada ya kama nusu saa hivi alionekana afande kweka akiingia ndani ya ukumbi huo wa mikutano akiwa amevalia suti yake ya rangi nyeusi , licha ya kwamba alioekana kuwa mzee lakini afya yake ilikuwa imara kwani alitembea pasipo kutumia mkongojo.
“Karibuni sana wageni naitwa Camillius Kweka, ni Jenerali mstaafu wa jeshi la wananchi wa Tanzania, lakini pia mimi ndio baba kwa Raisi wa taifa hili”Aliongea Camillius akijitambulisha mbele ya wageni wake baada ya kukaa kwenye kiti.
“Tunashuru sana kukufahamu Afande Kweka , nitaanza kujitambulisha mimi”
“Kwa majjina nafahamika kama Mellisa Luiz ni jasusi mstaafu kutoka CIA na Dhoruba Nyekundu”Aliongea Mellisa kwa kingereza akijitambulisha na kisha akatambulisha kila mmoja alieambatana nae , lakini baada ya kufika kwa mzungu yule ambaye alionekana kuwa mtu mzima kama ilivyo kwa Mellisa , alimpa ishara ya kujitambulisha mwenyewe.
“Kwa majina nafahamika kama Phill Knight , I am Former undercover Agent with Zeros Organisation”Aliongea yule mwanaume kwa kujitambulisha kwa jina la Phill Knight akiwa ni jasusi mstaafu kutoka taasisi ya Zero.
“Karibu sana Phill Knight Tanzania , wote karibuni kwa mara nyingine Tanzania na huu ni mwanzo mzuri wa sisi kufahamiana , Comrade aliponipigia simu juu ya ujio wenu hapa Tanzania nilishangaa , lakini nimeshangazwa pia na namna mnavyoonekana kujiamini hii ni ishara kubwa kwa ushindi wa mapambano yetu tunayokwenda kuanza nayo”
“Huyu ni Zenzhei , ni msaidizi wangu lakini pia ni mwanachama mwenzetu , anaonekana kama binadamu wa kawaida , lakijni asili yake ni kutoka ulimwengu wa Majini kutoka miliki ya Hongmeng China, lakini pia ni moja ya Ninja waliopata mafunzo chini ya Yamaguchi”Aliongea Afande Kweka na kumfanya kila mmoja kushangaa.
“Afande kweka , sijawahi kumuona mtu kutoka jamii ya kijini kwenye mazingira ya kawaida ya dunia , kumbe stori juu ya miliki ya kijini ni kweli sio hadithi?”Aliongea Mellisa kwa namna ya kushangaa.
“Unaonekana kushangaa Miss Mellisa, Sio Hongmeng tu ndio miliki za kijini duniani , kwa ufupi ni kwamba Hongmeng ni kama sehemu tu ya taifa ndani ya ulimwengu wa Kijini na yapo makabila mengine yenye miliki katika ulimwengu wa Majini, Sisi kwa upande wetu Hongmeng ni kama walinzi wakuu ndani ya taifa la China”Aliongea Zenzhei na kumfanya Mellisa na wengine kuduwaa kwa mshangao ni Habari mpya kwao.
“Jamani nadhani leo hii hatupo hapa kwa ajili ya kuzungumzia miliki za kijini, ila ni kwa ajili ya kuongelea sehemu ya ajenda mlizofika nazo hapa nchini na kutaka kujadiliana na mimi”Aliongea Afande Kweka na Mellisa alitingisha kichwa.
“Afande kabla ya kikao chetu kuanza , nitajaribu kukueleza kwa ufupi ni kipi kilitokea miaka kumi na moja iliopita na kumfanya Phill Knight kuwa sehemu ya wanachama wetu”Aliongea Mallisa Luiz na kuanza kueleza stori ya Phill.
SHEMU YA 250
((((11 YEARS AGO(MIAKA KUMI NA MOJA ILIOPITA ANAELEZEA MELLISA)
Ni tarehe ishirini na tatu kuamkia ishirini na nne mwezi wa kumi na mbili ndani ya jimbo la Texasi jijjini Dallas , ndani ya makazi ya watu, sehemu inayofahamika kwa jina la Greenville Avenue muda wa saa sita usiku.
Mwanamama wa umri wa miaka arobaini hivi aliekuwa akifahamika kwa jina la Mary , alionekana akishituka kutoka usingizini , baada ya kulala muda mrefu, mwanamama huyu baada ya kishituka alijikuta akipapasa mkono wake upande wa kushoto pasipo kugeuka kwa nia ya kutafuta mwili wa mime wake Phill, lakini mwanamama huyu baada ya kupapasa juu na chini mkono wake haukuambulia kitu na hii ilimfanya anyanyuke na kukaa kitako na kugeuza macho yake kulia, na hapo alijikuta akitoa shuka taratibu baada ya kumuona mume wake aliekuwa amepitiwa na usingizi katika meza yake ya kusomea huku pembeni ilionekana Printer ambayo na yenyewe ilionekana kuwa imewashwa pamoja na tarakishi.
Bi Mary alionekana kumuonea huruma mume wake kwa kitendo cha kupotelea usingizi akiwa mezani anasoma,mwanamama huyu ambaye alikuwa amevalia nguo za kulalia alitembea kusogea upande ambao mume wake amelala kwenye meza ,na kabla hajamgusa ili aamke , mara Printer ilianza kutoa mlio wa sauti ya Kuprint karatasi.
Bi Mary alijikuta akighairisha zoezi lake na kisha kuchukua baadhi ya karatasi ambazo zilikuwa zikitemwa na Printer hio, karatasi ya kwanza ndio iliomshangaza mwanamama huyu:
Kwanza kabisa karatasi hio ilikuwa na ‘watermark’ ya neno ‘Confidential’ , ilionekana ilikuwa ni nyaraka ya siri ambayo Mume wake Phill alikuwa akiisubiria kiasi kwamba alijikuta akisinzia kwenye meza.
Bi Mary alijikuta akianza kutetemeka mikono kadiri alivyokuwa akisoma karatasi hio , huku mume wake akiwa bado amelala , mwana mama huyu alielewa kabisa taarifa hio ni nyeti , lakini kutokana na taarifa yenyewe kumshangaza alijikuta akiendelea kusoma, alimaliza katatasi ya kwanza akachukua nyingine akaimaliza , huku kila karatasi anayosoma ikimuacha mdomo wazi , alisoma nukta hadi nukta mwanamama huyu ambaye kazi yake kubwa ni kuuza maua.
Baada ya Bi Mary kumaliza kusoma , alijikuta mwili wake ukikosa nguvu , alichukua karatasi alizokuwa ameshikilia na akazirudisha kwenye mdomo wa Printer na baada ya kumaliza kusoma , alijikuta hata kile ambacho kimemsogeza kwenye meza aliolala mume wake Phill ,alisahau m alijongea na kurudi kwenye kitanda na kisha akajilaza na kujifunika shuka.
“Evidence regarding killing of Professor Banos and M-Airline Plane dissapearencce”
“Detailed Plan to Eliminate the World coming Enemy”
“Project LADO success Rate”
“Twelve Greek God`s to faight against the Wold Coming Enemy”
Hivyo ndio vichwa vya habari ambavyo Bi Mary alikuwa amevisoma na alikuwa akivifikiria akiwa ndani ya Blanketi huku machozi yakiwa yameujaza uso wake, hakuwamini kabisa kwa kile alichokiona.
Kulivyokucha Mary alijitahidi kuwa wa kawaida mbele ya mume wake amaye tayari alikuwa amevaa suti kwa ajili ya kuelekea kazini , ambayo Bi Mary siku zote alikuwa akijua mume wake alikuwa ni Mhandisi ndani ya kampuni ya kutengeneza magreda ya kuchimbia barabara.
Bi Mary aliwaangalia watoto wake watatu kwa namna ya kuwaonea huruma , na kisha akamgeukia mume wake Phill ambaye alionekana kutabasamu muda wote.
“Mary Yo seem to be off today , what the matter , Tomorrow is Christmas , why you are not happy like everyone else, Come on tell me”
“No Phill , I am fine ,Why?”
“Its nothing Mary if you are fine , then it`s okay , I will be off to work now”Aliongea bwana huyu na kisha alimsogelea mke wake na kumbusu shavuni na kisha akahamia kwa watoto wake wote ambao mmoja wa kike alikuwa na miaka kumi na mbili mwingine kumi na mmoja mine.
Baada ya dakika kadhaa za Phili kutoweka kwenye macho ya Mary , alikimbilia chumbani kwake na kuanza kutafuta zile karatasi sehemu ambazo alikuwa akiamini atazipata , lakini hakuweza kuzipata.
“Atakuwa ameenda nazo”Alijiongelesha huku akijilaumu kwanini hakupiga picha
“Pastor Edwardo , I have something very important to discuss with you”Aliongea akimaanisha kwamba anajambo la kuongea na mchungaji aliemtaja kwa jina la Edwardo na hii ni baada ya kusalimiana.
“Unaonaje mara baada ya mkesha wa leo , litakuwa jambo zuri , maana mchana wa leo ratiba zimebanana”Ilisikika sauti upande wa pili na Mary akakubaliana na Pastor.
“Sijui kama ninachofanya ni sahihi , lakini naamini ni vyema nikiongea na kiongozi wa dini , Phill sio wa kunidanganya mimi kwa Zaidi ya miaka ishirini tokea tuone, he is undercover agent with Zeros Organisation all this time?, Damn you Phill”Alijiongelesha mwanamama huyu huku akianza kutoa machozi ,alionekana taarifa ya jana usiku aliosoma ilikuwa ni kubwa kwake na yenye kumuumiza.
Usiku wa saa sita hivi kwenda saa saba za usiku ndipo tukio la kutisha lilipotokea na mkurdish Afshar alivyofanya yake ya kuwarushia risasi waumini wa kanisa la The Forgivven.
Upande wa Pastor na Mary walikufa wakiwa ndani ya chumba ambacho kilikuwa kinatumiaka kama ofisi ya mchungaji ndani ya kanisa hili la The Forgiven.))).
…………………
Afande Kweka alijikuta akishangazwa na stori hio sana na sio kwake tu hata kwa Zenzhei na Nadia pia walionekana kushitushwa na Habari hio.
“Kwahio bwana Phill baada ya kupoteza familia yako yote ni nini ambacho kilitokea?”
“Zeros organization wakishirikiana na CIA walinikamata na kunipeleka kwenye moja ya Blacksite na kuanza kunipa mateso makali ambayo sitoweza kuyasahau maishani , wakitaka nieleze kwanini nilidukua taarifa ambazo hazikuwa zikinihusu na ni nani ambaye nashirikiana nae ”Aliongea Phill na kumfanya Afande Senga kujawa na shauku.
“Unamaanisha kwamba taarifa ambazo Mary mke wako alisoma zilikuwa hazikuhusu , nilidhani wewe ni Undercover Agent kutoka Zeros Organisation?”Aliuliza afande Kweka na Phili alitabasamu.
“Ni kweli mimi nilikuwa ni Undercover ajent wa CIA , lakini pia wa Zeros Organisation , licha ya kwamba nilikuwa nikifanya kazi kwao haimaanishi kwamba nilikuwa na ruhusa ya kupata taarifa za kile ambacho kilikuwa kinaendlea ndani ya CIA Pamoja na Zeros kwani kazi zangu zilikuwa ni nje ya ofisi kama ujuaavyo Ajent wa CIA wengi”Aliongea.
“Unamaanisha nini?”
“Afande Kweka ninachomaanisha ni kwamba mkataba ambao ulinifanya nikachelewa kulala mpaka mke wangu kuupata na kuusoma haikuwa sehemu ya kazi yangu , bali kuna mtu kutoka ndani ya kitengo alinipa taarifa kwamba kuna siri kubwa anataka kunitumia”
“Mtu!!, Unamaanisha kutoka ndani ya Zeros au CIA?”
“Sifahamu ni kutoka kwa kundi lipi kwani yote nilikuwa nikifanyia kazi kwa wakati mmoja, ila mtu huyo nina uhakika alikuwa ndani kati ya idara hizo mbili na hakujitambulisha kwangu jina na aliniambia ni kutokana na usalama”
“Alikuwa akitaka nini kwako, na kwanini aliamua kukuchagua wewe na kukutumia nyaraka za siri”
“Aliniambia kwamba atanipa maelekezo mengine baada ya kusoma hizo nyaraka , lakini cha kusikitisha ni kwamba familia yangu na waumini wa kanisa la Forgiven waliteketezwa kwa kuuwawa kikatili kwa ajili ya siri hio feki”Aliongea na kumfanya Kweka kushangaa
“Kwanini unasema ni feki , ilihali ilipelekea vifo vya watu wengi kwa ajili ya kuzuia isisambae?”
“Afande Kweka hilo sifahamu mpaka sasa na ndio maana nipo hapa katika haya mazungumzo, nahitaji pia kujua kwanini watu walikufa licha ya taarifa ile kuwa asilimia hamsini ni uongo”
“Wewe ulitambua vipi kwamba taarifa hio ilikuwa ni feki?”
“Seventeen ndio alietuambia taarifa hio kuwa feki”Aliongea Mallisa na kumfanya Afande kweka kutoelewa , kwanza hakuwahi kusikia jina la Seventeen.
“Seventeen!!”
“Ndio Afande Seventeen ni mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na mjukuu wako Roma na ndio alietuambia taarifa hio kuwa feki lakini sio kwa asilimia mia moja, asilimia hamsini ya taarifa hio ni feki na nusu yake ni ukweli”Aliongea Mellisa na kumfanya Afande kweka kushangaa Zaidi.
“Mnaonaje mkiniambia hio asilimia ya ukweli ni ipi na huyo Seventeen ni nani kwa ujumla wake?”
1.Detailed Plan to Eliminate the World coming Enemy
2. Twelve Greek God`s to faight against the Wold Coming Enemy
“Hizo nyaraka mbili ni feki Afande , kwanza kabisa hakuna mpango wowote uliondaliwa kwa ajili ya kupambana na adui anaekuja kama ilivyoandikwa , lakini pia hakuna miungu kumi na mbili ambayo itapambana na Adui anaekuja , bali ilitakiwa kuandikwa kwamba One god to fight against eleven Greek gods”Aliongea Mellisa akimaanisha kwamba kati ya mungu mmoja atapamabana na miungu kumi na moja.
“Kama maelezo yako ni sahihi je huyo mmoja atakaeweza kupambana na miungo yote kumi na moja ni nani na kwanini mmojaapambane na wenzake?”Aliuliza Zenzhei ambaye alionekana kuwa katika mshangao pia.
“Ni Mfalme Pluto, Hades”
“Roma!, unamaanisha mjukuu wangu?”
“Ndio mjukuu wako ndie anaetakiwa kupambana na miungu yote kumi na moja kwani ni tishio kwa ulimwengu huu na ni yeye pekee ambaye anaweza kufanya hivyo”Aliongea Mellisa na kumfanya Afande Kweka kuvuta pumzi , bado alionekana kutoelewa.
“Kwanini mnaamini kwamba Roma ndio mtu pekee ambaye anaweza kupamana na hio miungu ambayo hata sielewi inahusiana na ninikwani nasikia stori zake tu na mmefahamu vipi kwamba Roma ndio muhusika kwa kupambana nah io Miungu?”
“Seventeen ndio alietueleza hivyo kwa Ushahidi mkamilifu”
“Ushahidi , unamaanisha kwmaba mmekuja na Ushahidi”
“Hpana afande , Roma mwenyewe ndio Ushahidi,,”Ilisikika sauti kutoka nje na kumfanya kila mmoja kugeuza shingo.
“Comrade!!”Aliongea Afande Senga akiwa katika hali ya mshangao , hakuamini rafiki yake wa miraka mingi alikuwa mbele yake.
ITAENDELEA MWAKANI , HAOOY NEW YEAR TO YOU ALL ,