SEHEMU YA 251
Mwanaume ambaye alikuwa ameingia hapo alikuwa ni mzungu mzee wa miaka sabini Kwenda themanini hivi , mwenye kipara ambacho sio cha kunyoa bali kile cha uzeeni.
Alikuwa amevalia koti la rangi nyeusi na suruali ya kitambaa , mzee huyo hakuwa peke yake bali alikuwa na kijana mwingine wa kizungu ambaye alionekana kuwa msaidizi wake,kijana ambaye alikuwa amevalia suti na kupendeza huku mkononi akiwa ameshikilia mkoba.
“Pastor Cohen!!!”Aliita Mellisa baada ya kugundua mtu aliekuwa mbele yake ni boss wake na sio kwa Mellisa tu ambaye alionyesha hali ya kuonyesha heshima bali hata pia kwa Zoe na Phill pamoja na Nadia.
“Komred sikutarajia kama utafika Tanzania bila taarifa?”Aliongea Afande kweka kwa bashasha kwa kutumia lugha ya Kingereza na mzee yule alitabasamu na walisalimiana kwa takribani dakika tano nzima..
Pastor Cohen alikaribishwa kuketi kwenye kiti ndani ya eneo hilo , huku upande wa kijana ambaye ameambarana nae alisisitiza kwamba atasimama na hakuna aliepinga juu ya hilo.
“Zenzhei huyu ndio Komred niliekua nakwambia nilikutana nae miaka mingi nyuma nilipokuwa nchini Sudani kusini , Ni Mchungaji raia wa Hungary, ndio mtu ambaye alinipa siri yote juu ya Project LADO”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Zenzhei atoe heshima yake kwa Mr Cohen.
Cohen ni mtoto wa kwanza wa Profesa Banosi kutoka taifa la Hungaria, Cohen baada ya kufikisha miaka kumi na moja ndipo alipochagua Maisha yake kuyaelekeza kwa Mungu tofauti na kile baba yake Banosi alichotegemea,kwani alidhania mtoto wake atamfuata yeye kuungana katika maswala ya sayansi , kwani kipindi Cohen ni mwanafunzi wa darasa la tano , Profesa Banos alikuwa tyari ni profesa ndani ya chuo kimoja ndani ya taifa la Hungaria, kabla hajaajiriwa chini ya kitengo cha sayansi , Zeros organisariona.
Sasa Maisha ya Cohen yalikuwa ni ya kusafiri sana , kwani licha ya kwamba alipenda maswala ya kumtumikia Mungu , lakini pia alipendelea sana kusafiri na kujifunza mambo mapya Pamoja na kusambaza neno la Mungu, sasa katika safari zake za kuzunguka dunia ndipo alipokuja kukutana na Afande Kweka nchini Sudani na kipindi hiko Cohen alikuwa si chini ya miaka sitini na kwa upande wa Afande Kweka yeye pia hakuwa chini ya miaka sitini ni rahisi kusema kipindi walipokutana walikuwa na umri sawa , japo kwa Afande Kweka alionekana kuwa mkubwa Zaidi ya Cohen na kwanzia hapo ndio urafiki wao na ukaribu ulipoanzia.
“Camillius do you believe in Science or God?”Aliuliza Cohen siku ambayo alikutana na Afande Kweka ndani ya moja ya kanisa huko Juba Sudani kusini.
“Pastor kwanini unaniuliza swali kama hilo?”Aliuliza Afande Kweka kwa mshangao.
“Camillius umeniambia kuwa mjukuu wako wa pekee yupo kwenye hatua za mwisho za uhai wake kutokana na ugonjwa wa Saratani ndio maana nakuuliza swali kama hili, kama je unaamini uwepo wa Mungu , au Sayansi?” Afande Kweka alijikuta akikuna kichwa , ukweli tokea aingie Jeshini hakuwahi Kwenda kanisani , lakini licha ya hivyo alikuwa akiamini uwepo wa Mungu , kwani alikuwa ni mkatoliki wa ukweli na hio ni kwasababu baba yake pia alikuwa mkatoliki, kwahio ni rahisi kwamba karithi dini kutoka kwa baba yake.
“I think I believe in both Science and God”Aliongea Afande kweka na kumfanya mchungaji Cohen kutabasamu na kunyanyuka mpaka upande wa kushoto ndani ya ofisi yake hii ya kikanisa na kuibua picha iliokuwa kwenye fremu , picha ambayo ilionekana kuwa yeye mweneyewe Pamoja na mzee mwingine na walionekana kwenye pozi la furaha.
“Huyu ni baba yangu”Aliongea Mchungaji Cohen , akimkabidhi picha Afande Kweka.
“He is Illuminat”Aliongea Cohen na kumfanya Afande Kweka kushangaa Zaidi
“Illuminat!?”
“Yes , he is , Have you heared about Illuminat?”
“Ndio, Ushawahi kusikia kuhusu Illuminat?”
“Occasionally , lakini niliamini ni hadithi za kufikirika tu”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Mchungaji Cohen kutabasamu.
“Umesema hadithi , ni hadithi za aina gani umeweza kusikia kuhusu Illuminat?”Aliuliza.
“Hadithi zinaelezea hawa Illuminat ni Ant-Christ(Mpinga Kristo) hivyo ndani ya kanisa ni kama maadui wa kanisa”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Cohen kushangaa kidogo na kushika kidevu chake kilichojaa ndevu nyingi huku akionekana ni kama mtu ambaye anatafuta neno rahisi la kuongea katika kichwa chake.
“Hizo hadithi ni za kweli na kama nilivyosema , baba yangu ni Illuminat , lakini sehemu ya hadithi hio haipo sawa”
“Kivipi Mchungaji”
“Illuminat are belivers too like my Father , they believe in Science like us who believe in God , actually they don’t Believe in God”
“Illuminat ni waumini pia kama ilivyo kwa baba yangu , wanaamini katika Sayansi kama ilivyosisi tunavyoamini katika Mungu”
“It’s the same Pastor , they don’t believe in jesus as son of God meaning they are Ant-Christ”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Mchungaji Cohen kutabasamu.
“Nilivyoongea ni sahihi , hawaamini uwepo wa Mungu nikimaanisha kwamba hawaamini katika Dini yoyote , Ukristo , Uislam , Uyahudi na dini zingine zote ambazo zinaamini katika Uwepo wa Mungu”Akavuta pumzi na kuendelea
“They Call themselves as Men of Science , Who are searching for the Answers , Answers to man`s destiny , Purpose and creations”
“Mchungaji umesema baba yako ni Illuminat hivyo moja kwa moja ni kwamba haamini katika uwepo wa Mungu kwa maelezo yako , vipi kuhusu wewe mtazamo wako kuhusu Sayansi kama mtumishi wa Mungu?”AliongeaAfande Kweka.
“Sayansi ni mtego ambao Mungu katuwekea wanadamu, Katika dini tunaamini kwamba Kuna uhalisia Zaidi ya kile tunachoweza kuhisi kwa milango ya fahamu zetu,uhalisia ambao sayansi haiwezi kuthibitisha ila sisi tunaamini hivyo, uhalisia ambao ni Zaidi ya Sayansi , hivyo ninachoamini ni kwamba yupo Mungu aijuae Sayansi yote”Aliongea Mchungaji Cohen kwa kingereza na kumfanya Afande Kweka kukubaliana nae.
“Camillius nafahamu wewe ni mwanajeshi na kule jeshini mnaitana Komredi kama sikosei , hivyo kwanzia leo hii nataka uniite Komredi ili niweze kukusaidia kwa shida aliokuwa nayo mjukuu wako”Aliongea .
“Sawa Komredi”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Mchungaji Cohen kutabasamu na kisha alinyanyuka na kusogelea kabati lililojengewa ukutani na kulifungua kwa ufunguo na kisha akatoa bahasha.
“Tunakwenda kuzungumza kama marafiki hivyo nichukulie kama si mchungaji ili iwe rahisi kwa wewe kunielewa , sawa Komredi?”Aliongea Cohen na Afande kweka aliitikia.
“Jambo ambalo ninakwenda kukueleza ni swala la siri sana na ni jambo ambalo litabakia kuwa siri kati yetu , wewe ni mwanajeshi na wanajeshi hawaendi kinyume na ahadi zao,lakini pia vilevile tokea ufike hapa nchini kwa ajili ya mazungumzo ya amani tumekuwa marafiki wa muda, hivyo nataka kukusaidia na kabla sijakuonyesha hizi nyaraka nataka ukiri kwamba unaahidi kutokumueleza mtu yoyote jambo ambalo tutaongea mahali hapa”
“Nakiri kwa vizazi vyangu vyote na mababu walionitanguliza sitotoa siri hii tunayokwenda kuzungumza”Alionga Afande Kweka.
“Good!, ?hizi nyaraka zinaweza kuwa zimebeba hatima au mwanzo wa Maisha mapya ya mjukuu wako Denisi kama ulivyomtaja kwa jina lake , kama ulivyosema kwamba unaamini katika Sayansi na Mungu basi nitakuelezea kilichopo humu ndani”Aliongea na kuweka ile fomu mezani na kukunja mikono yake kama mtu anaekusanya maneno.
“Its document provided to me via secret means with my late Father Banos , are concealed document about Science, I don’t have to read everything to you because I am only one supposed to undersrand what material contain in this document, the point is, there is fifty percent chance for your Grandson getting cured”
“Ni Nyaraka ambazo nilipatiwa kwa njia ya siri na marehemu baba yangu Banos, ni nyaraka za siri kuhusu Sayansi , sina haja ya kukueleza kila kitu kwasababu mimi pekee ndio niliekusudiwa kuelewa nini kipo kwenye hizi nyaraka pointi yangu ni kwamba , kuna asilimia hamsini ya mjukuu wako kupona kupitia hizi nyaraka”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kupatwa na mshangao na shauku ya kujua.
“Mchungaji , unasema kweli?”
“Ndio Kweka ninachozungumza ni kweli na hakika na unatakiwa tu kufanya maamuzi kabla ya March 8 “Aliongea na kisha alitoa karatasi moja kutoka kwenye nyaraka na kumpatia.
“My Secret Means provided me with this document also , its detailed information regarding Project LADO”
“Njia yangu ya siri imenipatia pia hii nyaraka ni taarifa ya inayohusiana na Projekti LADO”Aliongea na kisha akampatia Afande Kweka ile karatasi na akaanza kuisoma na dakika tano mbeleni jasho lilianza kumtoka , ni kama hakuamini kile alichokuwa akikisoma na hakuamini mtu ambaye anamkabidhi karatasi hio ni Mchungaji wa kanisa kubwa hapa Sudani ambaye anahubiri Amani kupitia kupendana binadamu kwa binadamu kama moja ya amri kuu ya Mungu, aliinua macho yake na kumwangalia Mchungaji Cohen.
“As I said, I am not an Illuminat, and that Project I can`t Prevent it from happening because I don’t want to compromise my safety and this Document”
“Kama nilivyosema mimi sio Illuminat nah io project siwezi kuizuia kutokea kwasababu siwezi kuhatarisha usalama wangu na wa hizi nyaraka”Alivuta pumzi na kisha akaendelea.
“Camillius maamuzi ni ya kwako , ulichoshikilia ni Top Secret ambayo mpaka sasa inakuweka kwenye hatari kubwa ya kuwinda na mataifa makubwa kama vile CIA , Mossad , M16 na mengineyo makubwa duniani ndani ya mataifa ishirini yote yenye nguvu duniani”Aliongea Cohen na kumfanya Kweka jasho kumtoka , licha ya kwamba alihudumu jeshi tokea alipomaliza la saba na kupigana vita ngumu kama ile ya Iddi Amini lakini hakuwahi kukutana na jambo zito kwenye Maisha yake kama hilo.
“Komredi natakiwa kufanya nini?”
“Umesema mjukuu wako ana miezi mitano tu ya kuendelea kuishi na upo hapa Sudani kwa ajili ya mazungumzo ya Amani ambayo yanaweza kudumu kwa mwaka mzima na usipate nafasi ya kumuona mjukuu wako, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unarudi Tanzania unaandaa mpango wa kumhusisha mjukuu wako kwenye hio Project”
“And then , nini kinafuata?”
“We believe in Science like My father did and wait for the result`s”
“Tutaamini katika sayansi , kama ilivyo kwa baba yangu na tutasubiria majibu”Aliongea Mchungaji Cohen na kumfanya Afande Kweka kufikiria kidogo na kisha akavuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Mimi mwanajeshi na mwanajeshi ameumbiwa maamuzi magumu , napaswa kufanya maamuzi magumu kama ipo asilimia hamsini ya kumsaidia Denis”Aliwaza Afande Kweka na kisha akamwangalia Mchungaji Cohen.
“Nipo tayari , kama ipo asilimia hamsini ya kumsaidia mjukuu wangu Denis basi nitafanya chochote”Aliongea na kumfanya Cohen kutabasamu.
“Maamjuzi ya busara Komredi , sasa inabidi uondoke na ukaanze utekelezaji wa mpango , kumbuka mambo mawili mpango ni kabla ya tarehe nane mwezi wa tatu , pili mpango huo asifahamu mtu yoyote Zaidi yako na una miezi sita mpaka sasa , swala la mwisho ni hili”Aliongea na kisha alitoa picha kwenye bahasha na kumpatia.
“Who is this woman?”Aliuliza kwa mshangao kwani picha hio hakuwa akiifahamu kabisa na mwanamke mrembo aliekuwa kwenye picha hakumtambua.
SEHEMU YA 252
“ Huyo mwanamke ni mjamzito , Anaitwa Rahel Adebayo ,ni mtanzania mwenzako”Aliongea Cohen
“Ndio Komredi , sijakupata vizuri”
“Ndio Camillius huwezi kunielewa ila ninachojaribu kukuambia ni kwamba mtoto atakaezaliwa na huyo mwanamke lazima awe kwenye mpango LADO”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushangaa Zaidi lakini Cohen hakujali.
“Ana ujauzito wa miezi miwili sasa na anatarajiwa kujifungua kabla ya tarehe 8 mwezi march , hivyo Camillius kazi ni kwako kuhakikisha mtoto anaezaliwa na huyo mwanamke anaingizwa kwenye mpango , nitakuja kukuelezea kwanini mtoto wa huyo mwanamke anatakiwa kuwa ndani ya mpango, ukishakamilisha kila kitu”Aliongea Mchungaji Cohen na kisha akatoa karatasi nyingine na kumwambia kuwa karatasi hio ni ya kusaini mkataba wa siri kati yake na yeye na Afande Kweka kwakua maji alikuwa ashayavulia nguo , ilibidi kufanya hivyo na kusaini.
“Mpaka hapa kila kitu kimekamilika ni wewe tu kuhakikisha mpango unafanikiwa”
“Sawa Komredi tutawasiliana hatua kwa hatua nitakapofikia”
“Camilius unatakiwa kuelewa kwamba mpango huu ni siri sana , hivyo utautimiza kwa akili zako wewe mwenyewe pasipo ya mimi kuhusika na nitakutafuta baada ya matokeo , unachotakiwa ni kuniamini mimi na kuamini katika Mungu na Sayansi kwa wakati mmoja”Aliongea na Afande kweka alikubali na wakaagana na mazungumzo hayo yalikuwa ni mwaka 1997 yaani miezi saba nyuma kabla ya tukio la kupotea kwa ndege ya M Airline.
“Kazi nzuri sana Cohen”ilisikika sauti nzito ya kiume chumba kizima bara baada ya Afande Kweka kutoka katika ofisi ya kitumishi siku hio hio mwaka 1997.
“Mfalme Pluto nimefanya kila kitu , lakini haujaniambia kwanini misheni ulionipa inamuhusisha Camilius Kweka na Rahel Adebayo”Aliongea peke yake na mutu wa nje angedhani Mchugaji Cohen ni chizi.
“Because Kweka`s Grandson and expected child of Rahel are only humans with which their DNA`s undergone Mutations”Sauti ilijibu.
“Lakini mpango huu umesema haukuhusu na upo chini ya Zeros , kwanini umeamua kuhusika?”
“Kama nilivyokuambia kwenye sayari yetu, mimi nilikuwa mwanasayansi na Athena ni familia ya wanasiasa na anachokifanya sasa ni kutaka kurudisha nguvu zetu upya jambo ambalo sipo tayari litokee,”
“Kwanini, wakati ni ndugu yako kutoka sayari moja?”
“Its simple I don’t want to be ruled again with that stupid family , I am King over myself here on earth , qualification that I lack back to our planet ,Athena She is from Royal Bloodline and she wil became devil if allowed to rule , so I must prepare someone with free soul”
“Ni rahisi , sitaki kutawaliwa tena na familia ile ya kipumbavu ,mimi ni mfalme juu yangu hapa duniani , sifa nilioikosa kwenye sayari yangu ,Athena ni mtoto katika familia ya kifalme na atakuwa shetani kama ataruhusiwa kutawala tena hivyo napaswa kuandaa mtu mwenye nafsi huru”
“Free Soul you mean..”
“Yes our soul `s are automatically under command from Athena`s Family , we are like slave to their family so if she come to her full Stregth, She will covet our soul`s and we will think like her and that is very dangerous”
“Ndio nafsi zetu moja kwa moja zipo chini ya maagizo kutoka kwaAthena , na sisi ni kama watumwa kwa familia yao , hivyo kama atapata nguvu zake zote , atatamani nafsi zetu na kutufanya tufikitie kile anachofikiria na hilo litakuwa jambo la hatari”
“So you are preparing people to fight her?”
“Kwahio unaandaa watu kupigana nae?”Aliuliza Cohen.
“Yes that is Plan I am creating new Hades , new Generation to oppose her, She is from Noble Family and I know for sure its going to be difficult to Defeat her but with determination and support I believe human will Prevail.”
“Ndio huo ndio mpango, ninamtengeneza Hades mpya , kizazi kipya ambacho kitapingana nae , nafahamu anatoka katika familia yenye utukufu mwingi hivyo itakuwa ngumu kumshinda , lakini kwa maamuzi na uwezeshwaji binadamu atashinda”
“I thought she is Smart”
“She is just Asshole for now , but when she comes to find all resoureces we lost and make all dormant soul`s active ,there is no chance for human again here, you guys will be Slave and Shell for their millenial survival”
“Ndio kwasasa ni mjinga mjinga , lakini atakapokuja kupata rasilimali zote tulizopoteza na kufanya Nafsi zilizolala kuinuka tena , hakutakuwa na nafasi tena kwa binadamu , mtakuwa kama watumwa na miili yenu itatumika kwa maelifu ya miaka yao ya kuishi”
“Why do you helping us , you don’t benefit from anything from human I suppose”
“Kwanini unatusaidia , haufaidiki chochote kutoka kwa binadamu nafikiri”
“Cohen you know nothing about us, we are sinner, deadly sinner and if my Brother`s and sister`s soul getting activated , The action that you translate as Sin now will become holy actions and what God did to our Planet will repeat here , so where do you think I will live, actualy there is a lot of benefit for slow development of human Mind, the more discoveries about Science the more human will be sinfull against God”
“Cohen hujui chochote kuhusu sisi , sisi ni watenda dhambi, watenda dhambi wakubwa sana , kama nafsi za kaka zangu na dada zangu zitainuka , matendo ambayo unayatafsiri kama dhambi kwa wakati huu , muda huo yatakuwa ni matendo matakatifu na alichokifanya Mungu kwenye sayari yetu kitajirudia na hapa duniani na unafikiri ni wapi nitaishi. Ukweli ni kwamba kuna faida kubwa sana kwa akili ya binadamu kupevuka mdogo mdogo , kadri binadamu anavyoendelea katika sayansi ndivyo atakavyozidi kutenda dhambi zidi ya Mungu”
“At least you guys trust in God”
“Angalau nyie watu mnaamini katika Mungu”
“There is always beginning of everything Cohen , we will talk again after the Plan”
“Kuna mwanzo wa kila kitu Cohen, tutaongea tena baada ya mpango”Iliongea na kisha sauti palepale ilipotea na Cohen alivuta pumzi na kuzishusha.
Naam huyo ndio Hades wa zamani alipokuwa akiongea na Mchungaji Cohen mwaka 1997 kabla ya mpango LADO
Haikueleweka ni namna gani Afande Kweka alikamilisha mpango wenyewe, lakini mafanikio yake ndio yanaonekana wazi ndani ya miaka hii sasa na hii inamthibitishia kwamba Afande Kweka ni mtu mwenye akili nyingi.,
********
Ni siku ya ijumaa Asubuhi Edna na Roma walionekana wakitoka Pamoja na kumfanya Blandina aliekuwa nje ya nyumba akifanya usafi kutabasamu, alitamani kuona Roma na Edna wakitoka mara kwa mara wakiwa Pamoja.
Siku hii ya ijumaa ilikuwa ni siku maalumu kwa Edna kutokwenda kazini , kwani alikuwa na barua ya mwaliko wa kuhudhuria kikao cha wafanyabiashara ambacho mgeni akiwa ni raisi wa Rwanda Mheshimiwa Paul Jeremy.
Sasa Edna hakutaka Kwenda peke yake , alimuomba Roma jana yake kumsindikiza Kwenda kwenye kikao hiko na Roma alikubali kwa furaha zote baada ya kuona mke wake anataka Kwenda nae kweney kikao hiko na ndio maana asubuhi hio walitoka Pamoja kwa kutumia gari aina ya Rolly Royce gari ambayo Edna hupenda kuitumia kwa shughuli maaliumu kama vile Kwenda kwenye mikusanyiko inayojumuisha matajiri wenzake.
“Wife uelekeo tafadhari”Aliongea Roma baada ya kutoa gari nje ya geti.
“Kikao kinafanyikia Mliman City”Aliongea Edna huku akiendelea kuangalia karatasi zilizokuwa kwenye mikono yake na ilionekana alikuwa akiendelea na kazi licha ya kwamba alikuwa akielekea kwenye kikao.
Roma aliendesha gari kwa raha zote huku kila baada ya dakika akigeuza macho yake kumwangalia Edna aliekuwa bize.
“Roma mbona unaniangalia sana , ukisababisha ajali je?”Aliongea Edna huku akimwangalia Roma.
“Babe hivi unajua uzuri wako hauchoshi kuangalia?”Aliongea Roma na kumfanya Edna kukosa utulivu kwa namna alivyosifiwa na kuona aibu kwa wakati mmoja , ila alihisi utamu ndani kwa ndani.
“ Kua makini na barabara , usije ukasababisha ajali”
“Niko makini mke wangu , siwezi kumsababishia mfanya biashara mkubwa ajali ilihali uchumi wa taifa hili unakutegemea”Aliongea Roma huku akiongeza mwendo na nusu saa tu walikuwa wakiingia mlimani City na magari mengi ya kifahari yalionekana ndani ya eneo hili , huku wanaume waliovalia suti wawili wawili wakitembea kuelekea ndani ya ukumbi.
Ulinzi ulikuwa mkali na kumfanya Roma ahisi uwepo wa kiongozi mkubwa ndani ya hili eneo , kwani licha ya kwamba alikuwa akijua kuwa wanakuja kwenye kikao cha wafanyabiashara wa jiji la Dar , lakini hakuwa akifahamu uwepo wa Rais wa Rwanda.
Kwa mssaada wa wahudumu waliovalia suti , Edna na Roma waliongozwa mpaka ndani ya ukumbi na kuonyeshwa siti ya mbele kabisa na kumfanya hata Roma ashangae kwanini wamepelekwa mbele ila hakujali.
Matajiri walikuwa wakimwangalia Roma na Edna waliotangulizana kwa macho ya kuhusudu na kumfanya Roma kuvimba , ila kuna baadhi ya matajiri alitamani kuwatoboa macho kwani aliona walikuwa wakimkodolea mke wake isivyokawaida na yeye hajapenda.
Zilipita takribani dakika kama kumi na tano tokea Edna aingine hapo ndani na kusalimiana na baadhi wa wafanyabiashara hatimae ving`ora vilisikika vikiingiia ndani ya eneo la Mlimani City nje kabisa ya ukumbi na dakika chache mbele maraisi wawili , yaani mheshimiwa Senga Pamoja na Raisi Jeremy walifika kwa Pamoja na kuungana na wasaidizi wengine kuingia ndani ya ukumbi huo , huku makachero wakionekana kuweka ulinzi kwa viongozi hao wakubwa.
Mheshimiwa Jeremy alioenakna kuwa na mchecheto kweli na kwenye ziara yake hii hakuwa peke yake bali alikuwa na mtoto wake Desmond ambaye alikutana nae hapa hapa Tanzania.
Upande wa kushoto walipokaa Edna ndio sehemu ambayo viti vya waheshimiwa vilipangwa yaani ni kama Edna aliwekwa karibu na Raisi Jeremy makusudi kabisa.
Wageni wote akiwemo Edna na Roma walisimama baada ya maraisi hao kuingia ndani ya ukumbi huu na kuongozwa moja kwa moja mpaka sehemu ambayo imeandaliwa kwa ajli yao.
“Bebi wife kuna kiongozi mwingine mkubwa anaefika ndani ya mkutano huu?”Aliuliza Roma akimwinamia Edna.
“Yeah , raisi Wa Rwanda anataka kuongea na sisi wafanyabiashara wa Tanzania”Aliongea Edna.
“Mh Raisi Wa Rwanda?”
“Ndio mbona unaonekana kushangaa, au unafahamiana nae pia ewe mfalme”Aliongea Edna .
“Haha..”Roma alijikuta akicheka mara baada ya kuona Edna anajaribu kumtania na Edna alimwangalia Roma machoni na kutabasamu , kitendo ambacho kilishuhudiwa na Desmond na alikunja sura kweli na muda huo huo na Edna aliinua macho yake na kuangalia mbele na yalitua kwenye sura ya raisi Jeremy aliekuwa akimwangalia kwa tabasamu na kumpungia mkono na kumfanya Edna kushangaa mno.
SEHEMU YA 253.
“Cohen kutana na msaidizi wangu wa muda mrefu , anafahamika kwa jina la Zenzhei ni moja ya binadamu wenye asili ya jamii ya Majini”Aliongea Afande kweka akimtambulisha Zenzhei baada ya kusalimiana nae.
“Nikiri sijawahi kuamini kabisa Habari zinazohusiana na majini , inaonekana licha ya uzee wangu mambo mengi siyafahamu bado , hahaha”Aliongea Mzee huyu wa kizungu kwa kingereza na kufanya kila mmoja kutabasamu.
“Hata mimi Pastor Cohen nimeshangazwa na utambuliso wake , nilikuwa nikisikia Habari za Hongmeng wakati nipo Brunei na nilichukulia kama hadithi tu , ila nimepata jambo jipya siku ya leo”Aliongea Mellisa.
“Zoe Kovac Right?”
“Yes Pastor Cohen” Aliongea na kumfanya Cohen kutabasamu na kutingisha kichwa chake na kuridhika na kisha Nadia alfonso na yeye alitambulishwa.
“Komredi tunamengi ya kuongea baada ya miaka mingi ya kutoongea , ila tumalize kwanza kikao”Aliongea Pastor Cohen na Afande kweka alikubnaliana nae.
“Mellisa umekutana tayari na Mr Roma?”Aliuliza Mchungaji Cohen
“Yes Pastor , nilikutana nae na kumueleza stori yangu , lakini tuliishia kwenye uadui”Aliongea na kufanya Mzee Kweka na Pastor Cohen kushangaa.
“Mmemueleza kuhusu Seventeen?”
“Yes We did Pastor”Aliongea Zoe na kumfanya Cohen kuvuta pumzi.
“Mmekosea na nilikosea pia kuwaonya juu ya hilo, lakini natumaini umemuonyesha alama uliokuwa ukiitafutia ufumbuzi”Mellisa alitingisha kichwa.
“Na ameitambua?”
“Ndio ameitambua na kunielezea ni ya uraia kutoka visiwa vya wafu”
“Vizuri sana kama mlifikia katika hatua hio, Mellisa sikutaka kukuelezea kuhusu hio alama kwani sikuwa na uhakika nayo , lakini kwasababu ya Hades mwenyewe kaitambua kama ni yenyewe basi naomba nikueleze aliekuwekea hio alama wewe pamja na Phill”
“Hata Phill anayo hio Alama Pastor?”Aliuliza Zoe kwa mshangao”
“Ndio ninayo , sijamaliza stori yangu namna nilivyoponyoka kwenye mikono ya CIA naamini inafanana kwa asilimia mia moja na yako Mellisa”
“Nawewe uliokolewa pasipo kufahamu na ulijikuta ukiwa wapi”
“Lesotho , I gaine my conscionsness in Lesotho”Aliongea Phill na kufanya kila mmoja kushangaa.
“Komredi nadhani nina mengi leo ya kuyasikia kwani mpaka muda huu sijaelewa hata moja”Aliongea Afande kweka na Mzee mchungaji Cohen alitabasamu.
“Ndio Afande, wapo Zaidi ya raia kumi na tano waliokumbwa na kazia ya kutafutwa na serikali ya Marekani chini ya Vitengo vyao vya kiusalamana kama vile CIA na Zeros chini ya Dhoruba nyekundu , kumi na tano wote walikamatwa lakini pia kuokolewa na kupelekwa mafichoni pasipo ya kujitambua na kuwekewa alama ya uraia kutoka Visiwa vya wafu na kati yao wawili ni Phill Pamoja na Mellisa”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kushangaa.
“Na nani aliekuwa akihusika ?”Aliuliza swali ambalo hata Melllisa na kila mmoja walitaka kusikia jibu lake na Cohen alivuta pumzi.
“Ni Hades?”Aliongea.
“Unamaanisha mjukuu wangu Roma?”Aliuliza Afande Kweka kwa mshangao.
“Hapana Afande , Hades wa zamani ndio aliehusika”Aliongea na kuwafanya Phill na Mellisa kushangaa mno.
Ukweli Cohen alikuwa na mengi sana ya kuwaeleza wanachama wake hao , hususani kwa Afande Kweka ambaye hakuwa akifaamu mambo mengi licha ya kumpa mpango wa kufanya miaka mingi nyuma pasipo ya kumueleza sababu na ndio maana alifika Tanzania kwa ajjili ya kuongea na Afande mwenyewe.
“Komredi nafikiri tuongee kwanza kabla ya kuendeleza hiki kikao kwa Pamoja kwani pia kuna wanachama wengine hapa hawapo , Mellisa nitakutambulisha kwa Ally Assad rafiki wa karibu sana na Hades anafika leo kutoka Saudi ni mwanachama mwenzetu”Aliongea Cohen na Mellisa na wenzake walikubali kwa kutii na kuwaacha Afande Kweka na Pastor Cohen kuongea.
“Komredi kwanza nikupe hongera sana sana kwa kutimiza mpango , najua tuliongea kwa simu mwaka ule baada ya ukamilishaji , lakini hatukuwahi kuonana moja kwamoja , nikupe hongera kwa mara nyingine”
“Asante sana Komredi nafikiri ni jambo jema umekuja ili unieleze kinachoendelea kabla sijaingia kaburini maana umri unanitupa mkono”
“Haha ,..Afande sio kweli unaonekana kuwa na Afya nzuri Zaidi yangu”
*******
Edna ndio wa kwanza kukwepesha macho baada ya kuona Raisi Wa Rwana anamuangalia sana m jambo ambalo hata Roma alilitambua na alijua sababu kwani alikuwa akijua Edna baba yake ni Raisi Paul Jeremy na Roma sasa alitambua kwanini waliwekwa mbele kabisa, aliamini ni mpango maalumu wa raisi huyo kumuona mtoto wake kwa ukaribu.
Licha ya hivyo Roma hakuepnda macho ya kifisi ya Desmond kabisa.
Unajua Roma baada ya kumuadhibu Desmond siku kadhaa zilizopita hakupata maelezo yoyote kutoka kwa Edna na hakufuatilia kabisa, lakini kumuona Desmond ndani ya hili eneo kidogo swala hilo lilimshangaza na kutaka kumjua vyema bwana huyo.
“Mke wangu yule mwanaume nilietaka kumuua juzi ni mtoto wa yule mzee”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa.
“Mh! Akikusogelea tena nitamuua”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie.
“Unapenda sana kuua eh?”
“Sipendi kuua lakini Imani yangu inaniambia ili kumaliza watu wahalifu na wachokozi ndani ya hii dunia adhabu ni moja tu, kifo”
“Basi utajikuta unaua dunia nzima kama unaamini kila mtu anaekukosea adhabu yake ni kifo”
“Hata sijali ikinibidi kufanya hivyo nitafanya kwani naamini pia hii dunia ina watu ambao sio wachokozi na wanajali Maisha yao Zaidi pasipo kuathiri wengine”Aliongea Roma na Edna hakutaka kuuliza swali lingine.
Wageni wakubwa wakubwa walipewa nafasi za kuongea maneno ambayo kwa upande wa Roma aliyaona ni porojo tu kwani hayakumvutia na alijiambia kama isingekuwa mke wake angeshaondoka muda tu.
Roma alimwangalia Raisi Senga ambaye alikuwa akimwangalia kwa macho ya chuki lakini kwake hakujali, na Edna pia aliona hilo, kuna muda Raisi Senga alikuwa akimwangalia Roma kama mtu anaemkagua na kisha kupotezea.
“Inaonekana baba yako hayupo tayari kukupokea”
“Ukinipokea wewe mke wangu inatosha , yeye hata sijali anipokee ama asinipokee kwanza sina mpango na familia yake mimi”
“Usiongee hivyo familia ni familia, umezunguka dunia nzima kwa miaka mingi lakini leo hii umejikuta upo Tanzania na hii yote ni kwamba asili yako ilikuwa ikikuita”Aliongea Edna.
“Unachoongea ni kweli mke wangu , lakini asili haijaniita bali wewe ndio ulioniita, Mungu alinipatia unabii nirudi Tanzania nije kukutana na mwanamke wa Maisha yangu na unabii wake kwangu unaonekana kuwa wa kweli kwani hata sikutumia nguvu kwani ulijileta tu mwenyewe na ukajaa..”Aliongea Roma lakini aliishia kusikilizia maumivu kwenye mguu wake kwani Edna alimpiga teke chini kwa chini.
Ajenda kubwa ya mkutano huo ni kuwaalika wafanyabiashara wa Tanzania Kwenda Rwanda kuwekeza na blah bla nyingi zilizotoka kwa Raisi wa Rwanda na baada ya takribani masaa nane ya hafla hio kuisha , mheshimiwa Jeremy alianza kupeana mikono na wafanyabiashara huku ulinzi pia ukiimariswa kwa kile ambaye alikuwa akisalimiana nae na Edna alikuwa ni mtu wa tano kusalimiana na Raisi Jeremy.
“Edna nikupe hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kwa hapa Tanzania katika kuchangia uchumi wa taifa hili”Aliongea kwa bashasha.
“Asante sana mheshimiwa kwa kutambua juhudi zangu”
“Haha.. Edna kila mtu anatambua juhudi zako , Afrika Mashariki kwa ujumla wanatamani kuwa na mfanyabiashara mkubwa kama wewe mwenye malengo makubwa na mimi pia ni mmoja wapo , Edna naomba uje Rwanda kuwekeza”Aliongea Jeremy kwa furaha mbele .
“Asante sana muheshimiwa natamani sana kuwekeza ndani ya taifa la Rwanda , lakini kwasasa macho yangu yote nimeyaelekeza mahali pengine ,Mungu kama akijalia basi nitafika nchini Rwanda na kuangalia Fursa za kiuwekezaji”Aliongea Edna na kumfanya Mheshimiwa kutabasamu.
“Asante sana Edna , muda wowote unakaribisha Rwanda ni nyumbani kwenu”Aliongea Raisi Jeremyna Edna alikubali ukaribisho.
“Mr Roma nimesikia Habari zako, kutoka kwa Raisi mwenzangu , nikupe hongera kwa kupata mwanamke mrembo kama Edna , unapaswa kujivunia”
“Mheshimiwa napokea pongezi zako kwa mikono miwili nasikia Rwanda ni nchi iliobalikiwa na warembo lakini sidhani kuna wa kumzidi mke wangu “
“Haha..nakubaliana na wewe”Aliongea na kisha akaachana na Edna na kuendelea kw wafayabiashara wengine
Ni nusu saa baadae Roma na Edna walitoka eneo la mlimani City kurudi nyumbani na walipitia barabara ya Sam Nujoma kuelekea Nwenge, Sasa wakati gari ya Edna inafika kwenye mataa ya Mwenge macho ya Edna yalitua kwenye abiria waliokuwa wakishuka kwenye daladala kituoni upande wa pili yake na moyo wa Edna ulipiga Kite.
“Lanlan…! Roma simamisha tafuta sehemu usimamishe gari”Aliongea Edna kwa kuropoka huku akigeuza macho nyuma kwani taa ya kijani ilikuwa ishawaka na Roma alikuwa ashaanza kuendesha kiasi cha kupita usawa wa kituo cha Mwenge.
“Edna kuna nini?”
“Simamisha gari pale “Aliongea Edna kwa amri na Roma ambaye akuwa akielewa kinachoendelea alisogeza gari mpaka pembeni na kusimamisha na Edna alichomoka kama mwanajeshi na kumfanya hata Roma kushangaa.