Mwislam by choice
JF-Expert Member
- Sep 23, 2017
- 361
- 471
Singano mwakani ndo huu mzee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante mkuuAisee mkuu kwanza nikupe pongezi kwa hiki kigongo na ahsante kwa bonge la burudani mungu akulinde mkuu
Ratiba itaendelea vile vile , jumanne ,alhamisi na jumapili , baadae jioni nashusha ya kuanzia mwakaSingano mwakani ndo huu mzee
Safi sana mkuu.endelea na utaratibu wako arosto zetu zisikutowe kwenye mstari.Ratiba itaendelea vile vile , jumanne ,alhamisi na jumapili , baadae jioni nashusha ya kuanzia mwaka
Sent using Jamii Forums mobile app
Ratiba itaendelea vile vile , jumanne ,alhamisi na jumapili , baadae jioni nashusha ya kuanzia mwaka
Sent using Jamii Forums mobile app
SEHEMU YA 254
Roma ilibidi atafute sehemu nzuri Zaidi kusimamisha gari , kwani sehemu ambayo alisimamisha haikuwa kwa ajili ya megesho, alitembea mita mia mbili hivi karibu na kiwanda cha Shelys na kusimamisha gari pembeni na kisha akashuka na kuanza kutembea kwa miguu kurudi nyuma.
Upande wa Edna kitendo cha kushuka kwenye gari tu ni kama Lanlan alihisi uwepo wake kwani aliangalia upande wa Edna na kumuona na kuanza kumkimbilia jambo ambalo lilimtia wasiwasi sana Edna kwani aliona anaweza kudondoka barabarani na kugongwa na gari.
Spidi ya Lanlan ya kukimbia ni kama yupo kwenye mashindano ya Marathon kwani alitoka kama Mbwa baada ya kumuona Edna na kumkimbilia na kufanya hata wapita njia washangazwe na uwezo wa mtoto mdogo kukimbia.
“Maa,…mmiii” Lanlan alijirusha kama mshale na kumfanya Edna kuyumba kutaka kudondoka kwani nguvu aliotumia lanlan kumvaa ilikuwa ya aina yake.
Watu baadhi walisimama na kuwashangaa Edna na Lanlan baada ya kukumbatiana na Edna alijisahau kabisa yupo barabarani, kwenye Maisha yake alikuwa akihisi kabisa kuwa mama kamili hisia ambazo hakuwahi kuzipata kabisa , yaani kwake Lanlan alimuona kama mtoto wake kamili na sio wa kupita tu.
“Miss samahani kwa usumbufu wa Lanlan”Ilisikika sauti mbele ya Edna na kuinua macho na kumuona mwanamke wa kichina ila Edna hakujiabu Zaidi ya kumwangalia Lanlan.
“Lanlan mmekuja kufanya nini mjini?”Aliuliza Edna kwa kingereza na kumfanya Lanlan kuanza kutoa machozi.
“Mom!, Grandpaa kanikimbia na kuniacha mwenyewe … na wewe pia naomba usiniache kama zamani tena , Lanlan hataki kuishi peke yake tena hiii.. hiiii”Aliongea Lanlan na Edna alihisi moyo wake ukimuuma ajabu ni kama ni kweli alikuwa amemuacha Lanlan.
“Lanlan nyamaza acha kusumbua watu , tuondoke”Aliongea Qian xing , mlezi wa Lanlan na kumfanya Lanlan ajifiche nyuma ya Edna.
“Miss nani unaitwa?”Aliuliza Edna akimwangalia mlezi.
“Qiang Xing ,ni mlezi wa Lanlan amekuwa akisumbua toke amara ya mwisho mlipoonana kule kituoni na nimekuja nae kwa kumdanganya namleta kwako kwani haachi kulia halafu babu yake ameondoka bila taarifa”Aliongea yule mdada wa kichina na kuanza kutoa machozi kama mtoto mdogo na kumfanya Edna kushangaa.
“Wife japo sijui huyu mtoto umemtoa wapi , ila sio vizuri kuendelea kusimama hapa , mnaonaje tukitafuta sehemu ya tulivu na kukaa”Aliongea Roma ambaye alimsogelea Edna.
Ukweli Roma hakuelewa kinachoendelea kwani aliona Ednna akikumbatiana na mtoto ambaye hakuwahi kumuona , licha ya kwamba alimuona mtoto huyo kuwa mzuri na kufanana na Edna kwa kiasi flani ila hakupendezwa na jambo hilo, lakini Zaidi ni kwamba watu walikuwa wakiwashangaa na ndio maana alimsogelea ili kumtoa eneo hilo.
Edna aligeuka na kuangalia mazingira na kuona ni kweli watu walikuwa wakiwaangaliana na kuona aibu kidogo na kuyaona maneno ya Roma ni sahihi.
“Qiang Xing unaonaje tukienda kuongelea kwenye gari na kutafuta sehemu ya kutulia”
“Mom Lanlan ana njaa ,tunakoenda kuwe na chakula, Lanlan anapenda nyama”
“Wewe mtoto ni nani unawaza chakula tu?”Aliuliza Roma akiangalia kitoto kilichoshikilia mikono ya Edna.
“Mom who is this uncle?”
“He is bad guy I know , don’t mind him , what do you need to eat?”
“Napendelea kula nyama wa kukaanga , ya kuchoma au kubanika”Aliongea Lanlan kwa furaha na kumfanya Edna atabasamu na kumfanya Roma aliekuwa nyuma ashangae kwani kwanza kabisa hana maelezo juu ya mtoto huyo na hakujua amefahamiana vipi na Edna kwani wanaonekana wamezoeana sana kiasi kwamba ni kama wana miaka mingi ambayo wameishi pamoja , ila hakutaka kuuliza alitaka kwanza wafike kwenye gari kwani jua lilikuwa kali pia.
Mlezi wa Lanlan baada ya kufikia Gari ya Edna alijikuta akiwa na wasiwasi , hakua mjinga gari iliokuwa mbela yake ilikuwa ya pesa mbaya sana ambayo hakuwahi kuwaza kupanda kwenye Maisha yake yote.
“Qiang Xing ingia”Aliongea Edna ambaye alikuwa ashaingia kwenye gari tayari na Lanlan na hata kwa Roma pia alikuwa ashaingia upande wa dereva,Mwanamke huyo japo ya kuonekana kuwa na wasiwasi , lakini aliingia hivyo hivyo.
“Wife tunaenda moja kwa moja nyumbani?”Aliuliza Roma baada ya kuingia barabara ya Sellasie kutoka Morocco na kumfanya Edna aliekuwa akiongea na Lanlan kwa furaha afikirie kidogo.
“Utasimiamisha kwenye mgahawa wa Best Bite”Aliongea Edna na Roma aliangalia kioo cha juu na kumwangalia Edna ambaye hakuwa na Habari nae na alijikuta akivuta pumzi na kwasababu hakuwa akifahamu mgahawa huo alitumia ramani ya gari na dakika chache tu Roma aliweza kuona bango la njano na kuingiza gari eneo la Maegesho na kusimamisha.
Edna na Lanlan Pamoja na mlezi walishuka wa kwanza na akafuatia Roma mwenyewe aliekuwa na njaa kwani hakula chakula kilichoandaliwa kwenye kikao na hio yote ni baada ya Edna kulazimisha kuwahi kuondoka.
“Qiang Xing!, mama yake Lanlan yuko wapi na kwanini ulikuwa unalia nini kimetokea kwa babu yake?”Aliuliza Edna baada ya kukaa na kuagiza chakula na Qiang alivuta pumzi, ni yeye peke yake ambaye hakuonyesha hali ya utulivu na alionyesha kuwa na wasiwasi na ni kama watu waliokuwa mbele yake akuwa akiwaamini.
“Wife kabla haujaendelea ni bora ukanieleza huyu mtoto umekutana nae wapi?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Lanlan ambaye hakuwa na habari nae.
“Nilikutana nae kule kituoni kwa Zaidi ya mara mbili ya kwanza ni kabla hatujaenda Ufaransa na ya pili ni juzi nilivyoenda na mama”Aliongea na Roma sasa alielewa.
“Qiang huna haja ya kuwa na wasiwasi , sisi ni watu wazuri na isitoshe nampenda Lanlan hivyo siwezi kumzuru kuwa na amani na nielezee”Aliongea Edna na kumfanya Qiang kidogo kutulia.
“Lanlan hana mama”
“Aunt Qiang Lanlan ana mama na mama hawezi kumuacha Lanlan tena”Lanlan aliingilia baada ya kusikia maelezo ya mlezi wake.
Kwa maelezo ya Qiang ni kwamba yeye mwenyewe hamfahamu mama yake Lanlan na anachoelewa tu ni kwmaba mama yake Lanlan anafanana sana na Edna ,akaendelea kusema kwamba alikutana na Babu yake Lanlan na Lanlan mwenyewe huko china jimbo la Hubei na kipindi ambacho alikutana na Babu yake Lanlan, yeye alikuwa hana kazi maalumu na biashara yake kubwa ilikuwa ni kuuza maua.
“Wakati nakutana na Master, Lanlan alikuwa na miaka miwili pekee”
“Na sasa Lanlan ana miaka mingapi?”
“Ana miaka mitatu Kwenda minne”Alijibu
“Na ikawaje mkawaTanzania , lakini pia kwa muonekanao wa Lanlan anaonyesha hana asili ya China na babu yake ni mchina kama ulivyosema”
“Ni kweli hata mimi swali hilo nilikuwa nikimuuliza Master juu ya asili ya Lanlan , lakini hakuwahi kuniambia Zaidi ya kunionyesha picha ya Mama yake Lanlan na naweza kusema Tanzania ni taifa la saba kutembea nikiwa na Master na Lanlan”
“Taifa la Saba?” Edna alishangaa lakini pia kuvutiwa na maongezi kiasi kwamba alisahau kuwa chakula kishaletewa muda mrefu tu.
“Ndio taifa la Saba ,kwa maelezo ya Master anasema amemleta Lanlan hapta Tanzania kwani anaamini anaweza kumpata baba yake, lakini jambo la kishangaza ni Zaidi ya wiki sasa babu yake Lanlan hajarudi na Lanlan anasumbua tokea akuone anaona wewe ndio mama yake na mimi nimekosa maamuzi na nimejikuta kuwa katika mawazo”Aliongea na kuanza kutokwa na machozi , alionyesha hisia zake zipo karibu mno.
“Okey Qian tunapaswa kula kwanza tutaongea Zaidi”Aliongea Edna huku akirudisha macho yake chini kumwangalia Lanlan lakini alijikuta akipigwa na butwaa.
“Hurray!!!!,Mom nimemshinda Anko..”Aliongea Lanlan kwa furaha mno.
Jambo Edna ambalo hakuwa amelifahamu ni kwamba baada ya muhudumu kuleta chakula aina ya Chipsi nyama sahani nne na kuziweka mezani ,Roma alichukua sahani yake na Lanlan pia alichukua sahani yake Pamoja na uma na wakaanza kula ,Sasa jambo ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba spidi ya Lanlan kula aliona ni kubwa kuliko yake na kushangazwa , lakini hakutaka kuongea chochote alichokifanya aliinua macho na kumwangali Lanlan usoni na Lanlan aliekuwa akitafuna nyama alimwangalia Roma usoni na wote walirudisha macho yao kwenye sahani na kuanza kula haraka haraka kama vile wanashindana pasipo ya Edna na Mlezi wa Lanlan kujua kinachoendelea.
Sasa Edna hili swala hakuwa akijua kwamba linafanyika kwani alikuwa akimsikiliza Qiang na upande wa Roma yeye hakuvutiwa na maongezi ya Qiang kwani aliona hayamhusu hivyo aliingia kwenye mashindano ya kula na Lanlan.
Lanlan ndio wa kwanza kumaliza sahani yake na akafuatia Roma na wakaangaliana usoni kwa mara nyingine kama vile simba dume na simba jike na kisha macho yao yakageukia chakula cha Edna na Qiang na waliwaangalia usoni na kuwaona wako bize kuongea na Roma ndio aliekuwa wa kwanza kuvuta sahani ya Edna na kuiweka kwake na Lanlan baada ya kuona Anko kavuta sahani ya Edna alivuta ya mlezi wake na pambano likaanza upya.
Kilichomfanya Roma kushindwa ni namna ya ukataji nyama wa Lanlan na umma, alikuwa mikono yake ni kama ilikuwa imefungwa mota.
“Mh!!!, huyu mtoto sio wa kawaida”Aliwaza Roma na kuanza kula kwa spidi , lakini alikuwa amechelewa kwani Lanlan alikuwa ashamaliza kula na kushangilia na muda huo ndio Edna alikuwa akirudisha macho yake kwenye meza na kukuta sahani zote nne zikiwa tupu , huku baadhi ya watu waliokaa karibu yao wakiwaangalia Roma na Lanlan, walishuhudia kilichokuwa kikiendelea lakini wote macho yalikuwa kwa Lanlan.
SEHEMU YA 255
Edna aligeuza macho kwa Roma na kumwangalia na Roma alitingisha mabega na kumfanya Edna amgeukie Lanlan.
“Lanlan umemshinda uncle kufanya nini?”Aliuliza Edna.
“Mom, Lanlan amekula chukula sahani mbili na Uncle sahani mbili , Lanlan ndio wa kwanza kumaliza , Lanlan amekuwa mshindi”Aliongea Lanlan kwa kingereza na kumfanya Edna asiamini kama Lanlan anaweza kumaliza chakula sahani mbili na aliamini ni Roma ndio amekula sahani zote tatu.
“Wife usiniambie anataka kunisingizia nimekula sahani zote tatu , mimi nimekula mbili na huyu mtoto anaependa kuongea kwa nafsi ya pili umoja amekula mbili na nikweli kanishinda”Aliongea Roma na kuchukua juice na kunywa kwa kutumia mrija pasipo kujali macho ya Edna.
“Miss Edna huna haja ya kushangaa Lanlan ni mlaji mzuri wa chakula anaweza kula sahani hata tatu za vipande vya nyama”
“Sahani tatu umesema?”
“Mom , Lanlan anapenda kula na Lanlan bado hajashiba”Aliongea Lanlan na kumfanya Roma acheke.
“Hey Chubi umejifunzia wapi kula?”Aliongea Roma na Lanlan alionekana kutopenda kuitwa jina la Chubi kwani alimwangaliakwa macho makali.
“Anko mimi sio Chubi , Mimi ni Lanlan na Lanlan anapenda jina lake”Aliongea Lanlan kwa kingereza na kumfanya Edna kutabasamu , alishangazwa na kufurahi kwa wakari mmoja lakini hakuelewa kwanini Lanlan anongea kwa nafsi ya pili umoja yaani sehemu ambayo alipaswa kusema mimi anaweka jina lake , lakini alifurahishwa pia kwa wakati mmoja.
“Lanlan hupaswi kula chakula kingi sana kwani wewe ni mwanamke”
“Mom ,Lanlan anapenda kula na Lanlan hajashiba”Aliongea mtoto Lanlan na kumfanya Edna atabasamu na kufikiria kidogo , lakini liishia kumpa ishara mhudumu kuwasogelea.
“Tuletee chakula sahani tatu zingine”Aliongea Edna.
“Sawa Madam”Alijibu mhudumu.
“Leta sahani nne”Aliongea Roma.
“Wewe si umeshiba , sahani mbili hazitoshi”
“Wife usiniambie baada ya kupata haka kachibi Girl ushaanza kunibagua mumeo , hata mimi sijashiba “Aliongea Roma.
*******
“Kwahio Komredi unamaanisha mtoto wa Raheli na yeye aliishi?”Aliuliza Afande Kweka kwa mshangao baada ya kupewa nusu Habari ya kilichoendelea baada ya ndege ya M Airline kupotea.
“Ndio alipona na alipewa jina la Seventeen , huku Roma akipewa jina la Thirteen kabla hajakutana na Hades wa zamani na kumrithisha jina lake”Aliongea na kumfanya sasa Afande Kweka kuelewa.
“Ni kipi kilitokea haswa?”
“Maelezo yote sina , ila kwa nusu ukweli ninachofahamu ni kwmaba Mfalme wa Zamani yaani Hades anamwandaa Roma mjukuu wako kwa ajili ya kupambana na mwanamke shetani afahamikae kwa jina la Athena, kama nilivyokueleza kuwa hao wote ni jamii ya viumbe vilivyotawala miili yetu kutoka sayari nyingine”Aliongea na kumfanya Afande kweka kwanza kukuna kichwa , hakuwahi kusikia jambo la aina hio katika Maisha yake, ni jambo la kwanza na kwake aliona ni kama hadithi za SinganoJr tu na hazina ukweli.
“Kwahio unamaanisha kuna mamia ya roho zilizolala na mpango wa huyo Athena ni kuziamsha hizo Roho?”
“Kila nilichosema Camilius ni cha kweli , mwanzoni hata mimi sikuwa nikiaminni lakini nilipokutana na Hades na uwezo wake wa kuongea na mimi kama Malaika ndio niliamini”
“Samahini naomba kuuliza?”Aliongea Zenzhei na Cohen alimpa nafasi ya kuuliza.
“Ni kipi ambcho kimetokea kwenye sayari yao mpaka wakaja kwenye sayari yetu na sayanri yao ni ipi na kwanini wameishi miaka mingi sana pasipo kufanikisha mipango yao ya kurejesha Nafsi zao tatizo ni nini?”Aliongea Zenzhei.
Ukweli ni kwamba Zenzhei na Afande Kweka walichokuwa wakielwwa ni kwamba miungu ya kigiriki waliokuwa wakiisikia kutoka kwa watu ni ya kutengengezwa na binaadamu kupitia maabara na hawakufahamu kama ni viumbe ambavyo vilishuka miaka mingi iliopita na kufika hapa duniani na kutawala miili ya binadamu, hivyo kila kitu ni kipya kwao.
“Kuhusu jina la Sayari yao sijalifahamu mpaka sasa , lakini ninachowfaamu ni kwamba sayari yao ilikuwa na mazingira kama ya duniani na namna ambavyo walikuwa wakiishi pia ni kama Maisha yetu ya hapa duniani , utofauti mkubwa ni kwamba kwenye sayari yao maendeleo ya teknolojia yamekuwa kwa kasi sana kutokana na uwezo mkubwa waliojaaliwa kiakili na Muumba wao na hii ikapelekea wengi wa raia kutokubali uwepo wa Mungu na kuanza kuasi na kufanya vitendo vichafu, kwa maneno marahisi ni kama kilichotokea Sodoma na Gomora ndio kilichotokea kwenye sayari yao , kwani Mungu aliwaaangamiza na walioweza kukimbia wakakimbia na waliokufa wakafa na waliokimbia ndio walifika hapa duniani,Hivyo ndivyo Hades alivyonisimulia”Aliongea na kumfanya Zenzhei kushangaa.
“Kwanini walipewa majina ya miungu ya kale ya Ugiriki?”Aliuliza Zenzhei.
“Hata mimi hilo swali najiuliza lakini sikupewa majibu mpaka sasa na Roma hili ni swali lake na anapaswa kutujibu kwani yeye ndio alierithi kila kitu kutoka kwa Hades wa zamani hivyo ni lazima atakuwa anaelewa kila kitu”Aliongea Cohen
“Mchungaji huyu Seventeen yeye kwa sasa yuko wapi kama aliweza kufanikiwa katika Project?”
“Seventeen hata mimi sijawai kuonana nae , lakini watu ambao wameweza kukutana nae ni Zoe Kovac peke yake ndani ya visiwa vya Maldives na baada ya hapo walipotezana”
Ukweli ni kwamba Afande Kweka swala la mtoto Lorraine likuwa likimtekenya kwa ndani , licha ya kwamba siri hio amekaa nayo miaka mingi lakini alitamani kabla hajafa amueleze Rahel , lakini swala hilo halikutimia kwani Rahel alikufa mapema , lakini bado alikuwa na hatia na kuhitaji kumueleza Jeremy , lakini alihisi swala hilo linaweza kuleta migogoro na ndio maana alikaa kimya.
“Komredi nawiwa sana juu ya swala la Lorraine na pacha wake?”Aliongea Afande kweka.
“ Komredi halafu kwanini hukuniambia kuhusu pacha wa Loraine , swala hili nimelifahamu juzi tu baada ya Roma kurudi Tanzania?”
“Ni kweli Komredi sikukueleza , lakini kipindi narudi Tanzania katika harakati za kukamilisha mpango ndio niligundua Rahel alikuwa amebeba mapacha na kwakweli nilishukutu sana baada ya jambo hilo , na kuona mpango wangu kuwa rahisi sana kutekelezeka na niliamini pia hata wewe ulikuwa na taarifa za kutosha juu ya hilo ndio maana nilikaa kimya”AliongeaAfande Kweka.
“Sikuwa na taarifa kwasababu mimi sikuwa kiongozi wa mpango , nilichokuwa nafanya ni kupokea maagizo tu kutoka kwa mfalme Pluto wa zamani , hivyo swala la uwepo wa Edna nililifahamu juzi tu ,lakini hakuna kinachoharibika nadhani sikulifahamu kwakua halikuwa na shida kwenye mipango yake”
“Nisamehe sana Komredi kwa kutokukutaarifu , jambo ambalo linaniumiza ni hii siri kuna upande unaniambia nimwambia Raisi Jeremy juu ya kilichotokea kwa Lorraine”
“Kweka naona sasa unazeeka rafiki yangu, hili ni swala ambalo hapaswi kuambiwa mpaka tuwe na uhakika wa mahali huyu Seventeen alipo , kwasasa tutaangalia mipango tuliokuwa nayo lakini pia kuanza kumshawishi Roma kujiunga na sisi na kumtambulisha kwa wanachama wengine”Aliongea Cohen na Afande kweka alitingisha kichwa kukubaliana nae.
*******
Upande wa uwanja wa kimataifa wa Dar es salaam muda mchache baada ya ndege ya shirika la Emirates kutua , anaonekana mwanaume wa kiarabu alievalia kanzu na kiremba kichwani kutoka ndani ya jengo la Terminal namba tatu upande wa wanaowasili.
Baada ya kutoka nje aliona mtu alieshikilia bango lililoandikwa jina lake, Sheikh Ally Assad ndio jina ambalo lilosomeka kwenye bango na mzee yule ambaye ukimwangalia kwa makadirio ya umri hakuwa chini ya miaka sabini.
“Asalam Alaykum, Habari yako”Aliongea kwa Kiswahili kilichojaa tamathari za kiarabu na alieshikilia bango alitabasamu.
“Alaykum Asalam , karibu Tanzania Sheikh, naitwa Felix nipo hapa kwa ajili ya kukupokea”Alikuwa ni kijana ambae siku za nyuma alionekana ndani ya hospitali ya Aghakhani katika wodi ya Matrida akiwapa onyo la kwamba wasimfatilie Roma tena Pamoja na Edna na hio ilikuwa ni baada ya Mzee Alex kurushwa juu ya ghorofa na Roma , sasa Felix yule ndio aliekuja kumpokea Sheikh Assad.
“Asante sana kijana kwa kunipokea”Aliongea na Felix alichukua mkoba wa mzee yule na kisha alimuongoza njia mpaka upande wa maegeso ya magari na alisogelea gari aina ya Range Rover na kisha alimfungulia mlango Sheikh na kuingia na kisha gari iliondolewa taratibu.
Dakika chache baada ya gari ile kuondoka ndani ya mlango huo huo wa jengo la wanaowasili alionekana Yan Buwen akiwa Pamoja na Denis Senga waliovalia mavazi ya kibishoo na kwa jinsi walivyokuwa wakionekana ni kama walikuwa wakija kufanya show ndani ya jiji la Dar kwani walionekana kupendeza.
“Finally I am home”Aliongea Denis huku akinusa hewa ya jiji la Dar na Yan Buwen alimwangalia na kisha akafyura na kuendelea kutembea mbele.
“Mr Denisi”Ilisikika sauti ya wanaume watatu waliowasogelea na mmoja wao alikuwa ni Kabwe moja ya wasaidizi wa karibu wa Raisi Senga.
“Ndio Kabwe , mbwa wa baba kutoka ikulu , za siku nyingi”Aliongea Denis kwa dharau huku akimwita Kabwe mbwa kutoka Ikulu lakini kwa Kabwe hakujali.
“Mr Denis tumeagizwa na mheshimiwa kwa ajili ya kukupokea na kukupeleka moja kwa moja ikulu”Aliongea Kabwe na kisha Denisi alimgeukia Yan Buwen.
“You should go, but don’t forget what is plan”Aliongea Yan Buwen na kisha akaanza kupiga hatua na ile anafika eneo la maegesho ni kama alikuwa akisubiriwa kwani aliingia kwenye gari mmoja aina ya BMW nyeusi na kisha ikaondoka na kumuacha Denisi akiangalia gari ile kwa mbali na kutabasamu.
“Roma ama zako ama zangu , nisharudi na nakuja kukuonyesha kwamba wewe ni mdogo sana kwangu , nishapata taarifa zote za babu anachokipanga juu yako jambo ambalo sitoruhusu litokee ,nitakuuwa na nitachukuwa wanawake wako wote na nitafanya nao Three some”Aliwaza Denisi na kisha akamwangalia Kabwe aliekuwa amesimama kikakamavu na kisha alitoa tabasamu la kejeli na kuwapa ishara waongoze njia, yaani hakuwaza kama alikuwa na kesi ya kujibu kwa mama na baba yake, alionekana kujiamini kukiongezeka kwa asilimiamia moja.
ALHAMISI INAENDELEWA
0687151346 NAMBA YA WATSAPP
Alhamisi ndo Leo singanojr a.k.a Roma RamoniSEHEMU YA 254