Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra


Great story
 
Leo hapa
 
Mkuu singanojr usitufanyie hivyo story yako ndefu sana unatuacha na arosto mpaka tumeahaanza kula methadone hamna ya story inapungua Kaka [emoji23][emoji23][emoji23]
 
SEHEMU YA 260

Edna alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu na kushindwa kujua ni maamuzi gani anapaswa kufanya , alijiona kaingia kikamilifu kwenye mtego wa mwanaume aliekuwa mbele yake.

Kwa upande wa mzee wa kichina ambaye ni babu yake Lanlan alionekana kumwangalia Edna kwa Kejeli, aliona kabisa mwanamke huyo hatokuwa na uwezo kabisa wa kumchukua Lanlan na kumucha Rom.

Mlezi pia wa Lanlan , Qiang hakujua ni maamuzi gani ambayo Edna atachukua na yeye macho yote yalikuwa kwa Edna.

Edna alichuchumaa na kisha akatoa nguo za Edna kwenye mkoba wake na kumvalisha.

“Lanlan Mama hawezi kukuacha tena, na usilie tena sawa?”Aliongea Edna na Lanlan alitabasamu baada ya kusikia maneno ya Faraja kutoka kwa mama yake.

“Lanlan anampenda sana mama yake”Alionea Lanlan na kumkumbatia Edna na Edna alijikuta akiguswa sana na maneno ya Lanlan.

“Kwahio ndio umeamua nini Miss Edna , muda unaenda?”Aliuliza yule mzee wakichina na kumwangalia Edna usoni.

“Hili swala limekuwa la ghafla sana kwangu, Lanlan nimefahamiana nae kwa siku chache lakini nahisi kabisa nina muunganiko nae ambaye siwezi kuelezea na inaniuma kumkosa hata kwa dakika”

“Huna haja ya kuelezea Zaidi , mpaka hapo nimeelewa kwamba unampenda sana mumeo kuliko Lanlan”Aliongea Yule mchina na kisha alimsogelea Lanlan.

“Lanlan twende nyumbani nimekuletea zawaidi ambayo utaipenda”Aliongea huku akimuweka begani Lanlna.

“Lakini Grandpa Lanlan anataka kukaa na mama yake , siwezi kuondoka”Aliongea huku akianza kulia akimwangalia mama yake.

“Lanlan niangalie usoni?”Aliongea yule mzee na Lanlan alitii na kumwangalia usoni babu yake , na haikueleweka mzee yule amemfanya nini lakini Lanlan alipitiwa na usingizi dakika ileile na kulaza kichwa chake kwenye kifua cha babu yake.

“Miss Edna nisamehe sana kama nimeongea maneno ya kukuuzi , usiwe na wasiwasi kabisa na Lanlan nitamtafutia mama yake ambaye yupo tayari kufanya chochote kwa ajili yake”Aliongea na kisha akainamisha kichwa chake kwa namna ya heshima mbele ya Edna na kisha akampa ishara Qiang aondoke.

“Subiri..”Aliongea Edna huku akishikwa na huzuni lakini mzee yule hakuangalia nyuma na aliondoka na dakika nne mbele hawakuonekana tena kwenye macho yake.

“Hey mrembo huna haja ya kuwa huzuni, nina mbegu nzuri sana kama utanikubalia ninaweza kukupatia ujauzito na ukazaa mtoto kama yule”Ilisikika sauti ya mwanaume nyuma ya Edna na kumfanya ageuke.

“Kwa hadhi gani uliokuwa nayo ,potea kwenye macho yangu”

“Hehe.. acha kujifanyisha wewe Malaya , umepokonywa mtoto hapa na nikikuangalia tu unaonekna kuwa kahaba ndio maana , acha maringo na twende nikakupe mambo”Aliongea yule mwanaume jamii ya mhindi mchanganyiko na mwafrika akiwa kifua wazi na bukta ilioloa maji na alionekana alikuwa akiogelea.

“Paah!!!”Kilikuwa ni kibao cha nguvu kilichotoka kwa Edna Kwenda kwa yule mwanaume.

“Nishakuambia ondoka kabla sijakufanya kitu kibaya”Alionea Edna huku akiwa na hasira mno , alikuwa akiumia kwa kumkosa Lanlan lakini hakuwa tayari kuvumilia kejeli kutoa kwa mwanaume aliekuwa mbele yake.

Bwana yule baada ya kuona kapigwa kibao , alionekana kukasirika mno na palepale alimpiga Edna bonge la kibao na kumfanya kudondokea kwenye maji ya baharini.

“Haaaa……!!!”Watu waliokaribu walishangazwa

“Oya braza unachofanya sio sahihi acha uzalilishaji”Aliongea mwanaume mmoja akitaka kumzuia yule mhindi kwa kutaka kumshika , lakini aliambulia teke lililompiga tumboni na kusinyaa na yule mhindi baada ya kuona amemuadhibu mwanaume kiherehere alimsogelea Edna alieloa kwenye maji huku damu zikimtoka puani na kumshika kwa ajili ya kumpiga ngumi nyingine lakini mkono uliishia hewani na kukuta sura ambayo haifamu.

“Crack!!!”

Kilikuwa kitendo cha fasta sana kilichofanyika na yule mwanaume palepale jina lake lilibadilika kutoka kuwa mtu hai na kuwa hayati.

“Khaa… jamani … uwiiii … kaua”Ilisikika sauti ya mwanamke na kufanya hata watu ambao hawakuwa wakifahamu tukio la udhalilishaji kusogea sehemu ya tukio.

“Edna…!!!”Aliita Roma na kumsogelea Edna ambaye alikuwa kwenye maji na kumbeba juu kwa juu kama mtoto.

“Mamaaaa….!!!!” Kundi lote lililokuwa limekusanyika lilitawanyika.

“Kuna nini?”

“Jini … jini …”Aliongea moja ya mwanaume aliekuwa akihema baada ya kusimama mita kadhaa kutoka kwenye tukio.

Ukweli kilichowafanya kutawanyika ni baada ya Roma kupotea ndani ya eneo lile ,ndio maana watu walichanganyikiwa mno na kuamini Roma alikuwa ni jini, watanzania wengi maswali kama hayo ya kupotea walikuwa wakiyashuhudia kwenye filamu , kama vile filamu ya Shumileta sasa kupotea kwa Roma kuliwafanya waamini ni jini.

******

TURUDI NYUMA KIDOGO

Roma alipumzika chumbani kwake kwa taribani lisaa limoja na nusu ndipo aliposhituka kutoka usingizini na kitu cha kwanza alichoshika ilikuwa ni simu yake, aliangalia saa na kuona amelala kwa lisaa na nusu.

Aliamka kivivu na kuingia bafuni na kuoga huku akiwa na mpango wa Kwenda nyumbani kwa Nasra mapema , hakutaka kulala huko huko kwani pia alikuwa na mpango wa Kwenda kwa Mrembo Rose kwani ni muda kidogo alikuwa hajawasiliana nae , lakini pia alikuwa akienda kumueleza juu ya swala la uwekezaji kwenye kammpuni yake mpya , hivyo akili yake ilikuwa na mipango miwili , mpango wa kwanza ni Kwenda kwa Nasra na kuweka mambo sawa na mpango wa pili ni Kwenda Mbagala Maji matitu kwa ajili ya kuonana na Rose.

Alitumia dakika kumi na tano tu kumaliza mpaka kuvaa na alitoka na ufunguo wa gari yake na kushuka chini sebuleni kwa ajili ya kuaga kama anatoka.

“Mama natoka kidogo”Aliongea Roma.

“Unarudi saa ngapi, tulijua unabaki ili tupate chakula cha Pamoja na Shangazi yako?”Aliongea Blandina na Roma alifikiria kidogo.

“Kama unaondoka inabidi kwanza umsubirie Edna ndio umuage uondoke”Aliingilia Blandina , hakutaka kumzuia kuondoka , ila alitaka kumzoesha Roma kumuaga Edna kila anapotoka , aliamini hio ndio mbinu ambayo inaweza kupunguza umbali uliokuwa kati yao , aliamini kama Roma ataaga na Edna kumruhusu basi itapunguza makasiriko ya Edna kwani atakuwa amemruhusu mwenyewe.

“Ngoja nimpigie simu”Aliongea Roma huku akitoa simu yake.

“Yaani Roma unatumia simu ya aina hio mpaka sasa hivi , kwanini usinunue mpya?”Aliuliza Jestina na Roma alitabasamu.

“Ni salama Zaidi kutumia simu za aina hii kuliko hizo kubwa”Aliongea Roma na kuweka simu sikioni na simu ilianza kuita takribani kwa dakika moja na haikupokelewa, alipiga kwa mara ya pili na haikupokelewa tena.

“Sh***T”Aliongea Roma chini chini na kutoka nje.

Roma alikumbuka asubuhi wakati akitoka na Edna aliwapa ishara Chiara na John ya kupumzika kwa siku hio kwanni atakuwa na mke wake , sasa ndio Roma alikumbuka na kujiona amefanya makosa kumuacha Edna na Lanlan kuwa peke yao pasipo kuwa na ulinzi

Roma baada ya kuona simu sasa haipokelewi alijawa na wasiwasi na hakuwa na mpango wa kutmia kabisa gari kwani Fukwe ya Coco haikuwa mbali , alitumia mbinu ya kuteleport.

Baada ya kufika Coco alijikuta akipandwa na Jazba baada ya kuona Edna akidhalilishwa na mwanaume kwa kupigwa kibao ambacho kilimdumbukiza kwenye maji ,na ilikuwa bahati yake kwani kama angechelewa Edna angepigwa ngumi takatifu ya uso.

“Mtu kama huyu ni kifo tu haina haja ya kumueleza kosa lake “Aliwaza Roma na palepale alimvunja shingo mwanaume wa kihindi ambaye hakutaka hata kumfahamu ni nani.

*****

Roma aliibukia kwenye gari ya Roll Royce ambayo Edna alikuja nayo hapo ufukweni na alimlaza kwenye siti Edna ambaye alikuwa amelala pasipo ya kuwa na fahamu , huku damu zikiwa zimegandiana kwenye pua zake , lakini pia nguo zake kuloana na maji ya baharini.

Roma baada ya kumuweka vizuri aliinua viganja vyake vya mkono kwa sentimita kadhaa Kwenda juu akimlenga Edna tumboni kwa dakika kama mbili hivi na palepale nguo za Edna zilianza kukauka kwa Spidi ya ajabu sana , huku pia damu ambayo ilikuwa imeganda kwenye pua zake ikipotea, ndani ya dakika tano Edna alirudi kwenye hali yake ya kwaida na alimwamsha.

“Wife pole sana”Aliongea Roma baada ya Edna kunyanyuka na kuketi kwenye kiti huku akijishangaa, kwani dakika kadhaa nyuma alikuwa baharini , akiwa amezungukwa na watu , lakini pia akishuhudia kitendo cha Roma kumuua mtu mbele yake , alikumbuka kila kitu na alishangazwa pia kuona nguo zake zimekauka na pia hakuwa akitoka damu tena.

Alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa na Roma alimwangalia mke wake huku akijiuliza Edna anawaza nini.

“Kulikuwa na haja ya kumuua?”Aliuliza Edna kwa sauti ndogo yenye unyonge na kujutia.

“Wife kama unakumbuka maneno yangu ya asubuhi vizuri basi nilichokifanya ndio sheria yangu , mtu kama yule ambaye alitaka kukudhalilisha adhabu kwake ni kifo hakuna namna”Aliongea Roma na kisha alitoa ufunguo kwenye mkoba wa Edna na kuwasha gari kurudi nyumbani.

“Yule mtoto Lanlan yuko wapi?”Aliuliza Roma na kumfanya akili ya Edna ianze kufikiria upya.

“ Babu yake kamchukua”Aliongea Edna kinyonge na kumfanya Roma kushangaa.

*****

Upande wa barabarani muda huohuo inaonekana gari aina ya Toyota Camry rangi nyeusi ikiwa imeegeshwa mita kadhaa kutoka kwenye moja ya jumba la kifahari ndani ya eneo la Osterbay huku mziki kwa mbaali ukisikika kutoka kwenye gari hio.

Dakika chache mbele alionekana kijana alievalia suruali ya Track , akija kwa kuhema kusogelea gari hio huku mkononi akiwa ameshikilia Camera kampuni ya Sony.

“Mbona unahema hivyo?”Ilisikika sauti ya kiume kutoka kwenye gari baada ya kioo kushushwa.

“Boss misheni imefeli”Aliongea yule mwanaume na mlango ulifunguliwa na kijana akaingia ndani.

“Unamaanisha nini misheni imefeli?”

“Salah is dead”

“What!…Salaah is what “

“ I mean dead , ameuliwa na mwanaume jini”Aliongea yule kijana na kumfanya mwanaume aliekuwa kwenye gari kukosa utulivu.

“Elezea vizuri nikuelewe , unanichanganya wewe mpumbavu”Kijana alielezea kilichotokea na kumfanya boss wake kushangaa mno.

“Umechukua picha tukio zima?”

“Ndio boss , si ndio ilikuwa kazi yangu kwenye huu mpango , nimechukua pia video tena HD na Edna na muuaji wamenaswa vyema” Aliongea na kisha akashika Kamera yake kwa mikono miwili huku akionekana kwenye mchecheto na kuwasha.

“Mbona hunipi nikiona hizo video unahangaika tun a hio Kamera” Aliongea yule mwanaume na kumwangalia yule dogo akihangaika na kamera yake.

“Hakuna picha , boss , inawezekana vipi hii wakati nilisevu kila kitu”Aliongea huku akitafuta picha baada ya kamera yake kuwaka lakini hakukuwa na kitu na kumfanya kupagawa.

“Acha kuchachawa inaonekana yule mpuuzi alijua kabisa unachukua video”Aliongea yule mwanaume.

“Boss unamjua?”

“Acha maswali mengi maana hayakusaidii , chuku pesa hii hapa kama malipo na poteaa kwenye macho yangu”Aliongea yule mwanaume kwa hasira na dogo baada ya kuona boss wake kakasirika haraka haraka alichukua pes ana kushuka kwenye gari na kupotea.

“Hahaha… Roma umenirahisishia kazi , ungekuwa na akili usingemuua Salah , Edna nikiri ulikuwa na akili nyingi sana ya kuolewa na Shetani Roma , lakini awamu hii nitahakikisha unatoa machozi ya damu,nimezaliwa upya na sio Abubakari mpuuzi wa kupanga mipango na kufeli”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli , lakini muda uleule simu yake ilianza kuita na aliangalia jina na kuona ni Matilda.

Haikueleweka Abubakari karudi lini Tanzania, ila ashaanza kumchokoza Roma.





SHEMU YA 261.

Edna hakutaka kumueleza Roma juu ya sharti alilopewa na babu yake Lanlan kabisa , alijiambia itakuwa siri yake , licha ya kwamba swala hilo lilikuwa likimuuma sana lakini alijikaza mbele ya Roma.

Simu ya Roma ilianza kuita mfululizo baada ya kukaribia nyumbani na kuichukua huku akiendesha gari na mkono mmoja na baada ya kuangalia jina alijikuta akishangaa kwani jina lilikuwa la Magdalena.Alimwangalia Edna na kisha akapokea

“Roma usiniambie wewe ndio umemuua Salah?”Aliuliza Magalena kwa hasira.

“Salah ndio nani?”Aliuliza

“Niambie umeua au hujaua?”Aliongea Magdalena kwa sauti ya ukali.

“Ndio leo nimeua ila sijamuua Salah mimi unaemtaja”Aliongea Roma na kumfanya Edna aliekuwa ametulia kumwangalia Roma kwa wasiwasi.

“Umefanya nini Roma , kwanini unapenda kuua bila tahadhari unajua Salah ni nani wewe?”

“Magdalena usinipigie kelele , mimi nimemuua mtu alienikosea na kutaka kumdhalilisha mke wangu , Sijui kinachokufanya uogope ni nini lakini nimeshamwadhibu na alichostahili , na toa salamu zangu za rambirambi kwa wafiwa”Aliongea Roma na kukata simu.

“Magdalena anasemaje, ni nani yule mwanaume”

“Sijajua na hata awe nani sijali, nilichofanya ni sahihi kwa mtazamo wangu”Aliongea Roma huku akiingiza gari getini na Kwenda kulisimamisha na giza lilikuwa lishaanza kutanda.

“Umeniweka kwenye nafasi mbaya , najua kuna watu waliokuwa wakirekodi kila kitu pale na picha zangu na zako zitasambaa mtandaoni”Aliongea Edna huku akianza kujawa na wasiwasi.

“Wife usijali mimi sio mjinga mpaka niruhusu watu kukurekodi , hakuna picha wala video kwenye kifaa chochote kimeweza kurekodi”Aliongea Roma na kisha akashuka kwenye gari.

“Unaenda wapi?”Aliuliza Edna baada ya kuona Roma anaingia kwenye gari yake nyingine.

“Ninaenda kumtembelea Nasra, nikitoka kwa Nasra nitaenda kwa Rose, Wife sitowahi kurudi leo”Aliongea Roma na hakusubiria hata jibu kutoka kwa Edna na aliwasha gari na kisha akashusha kioo.

“Wife nakupenda sana , najua una huzuni kwa Lanlan kuchukuliwa na babu yake, ila mimi mumeo nitajitahidi kuhakikisha unapata mtoto wa kwako, babe I love you and goodnight”Aliongea Roma na kisha akampa Edna busu la hewani na kutoa gari na Edna aliangalia mpaka inatoka nje ya geti na haikueleweka alikuwa akifikiria nini , ila alitoa mkoba wake kwenye gari na kisha kuanza kutembea kinyonge Kwenda ndani na akapokelewa na Blandina.

Blandina alimwangalia mke mwana na kujikuta moyo wake ukiwa kwenye majonzi , aliona mabadiliko aliokuwa nayo Edna.

“Edna umeonana na Roma?”Aliuliza Blandina na Edna aliitikia kwa kichwa na kisha alimsalimia Mama Theresa na Jestina na kisha alipiga hatua kuelekea juu kwenye chumba chake hku wote macho yakimwangalia Edna kwa chini alionekana kuwa mtu mwenye huzuni kwenye macho yao.

*******

Maongezi kati ya Pastor Cohen na Afande kweka yalisimama mara baada ya simu ya Afande kweka kuita na aliitoa kwenye mfuko wake wa koti na kumuomba msamaha Cohen kwa ajili ya kupokea simu hio.

Aliangalia jina juu ya kioo na lilisomeka Linda na Afande kweka alijikuta akishangaa kidogo na kisha akameza mate na kupokea.

“Za siku nyingi Afande” ilisikika sauti ya Linda kwenye simu.

“Salama Linda. Natumaini upo Tanzania?”

“Ndio Afande nipo hapa Tanzania na kabla sijarudi nchini Rwanda nataka muendelezo wa pale tulipoishia miaka ishirini iliopita, najua mpaka sasa una hasira na mimi kwa Kwenda nje ya mpango , lakini mpango ulifanikiwa licha ya njia tofauti, huna haja ya kunitenga ilihali mimi ni mshirika”Sauti ya Linda ilisikika na kumfanya afande Kweka avute pumzi.

“Unataka nini kutoka kwangu Lind?”

“Nahitaji kumjua X, lakini pia kuna kitu nilikuficha nahitaji pia kukueleza kabla sijarudi Rwanda”Aliongea na kumfanya Afande kweka kumwangalia Pastor Cohen.

“Linda kwasababu upo Tanzania litakuwa jambo la busara tuonane, naamini majibu yako yote ambayo nilishindwa kuyajibu miaka ile yanaweza kuwa na majibu sasa”Aliongea.

“Mheshimiwa kabla hatujaonana nataka kuweka kitu wazi”

“Ongea Linda”

“Mheshimiwa Jeremy amepata Ushahidi wa kila kitu juu ya ndege ya M Airline na awamu hii siwezi kabisa kuzuia swala hili lisiendelee na anapanga kuonana na vyombo vikubwa vya Habari kwa ajili ya swala hili kutangazwa na mheshimiwa kutoka Urusi ametoa ruhusa”Aliongea Linda na kumfanya Afande kweka kushangaa.

“Linda ngoja nakupigia muda huu”Aliongea Afande Kweka na kisha akakata simu.

“Kuna nini Komredi?”Aliuliza Cohen baada ya kufundua mabadiliko ya Afande kweka.

“Inaonekana Jeremy ashaanza kuchukua hatua juu ya kutangazia dunia kilichotokea mwaka 1998, hili litakuwa jambo la hatari kwa dunia na inaonekana Urusi wapo nyuma yake”Aliongea Afande Kwek ana kumfanya Pastor Cohen ashangazwe kidogo.

“Raisi wa Urusi mpango wake kwa sasa ni kuivamia Ukraine na nadhani anataka kutumia vyombo vya Habari kusambaza ukweli ili kutegeneza mtifuano kwa wanachama wote wa G20 ambao wanahusika na mpango LADO , huku akitumia mpango TASAC kwa mataifa ya Afrika kukaa kimya”Aliongea.

“Afande lakini mrusi ni mshirika wetu na pia kama taifa tumekuwa na ushirikiano mkubwa sana”Aliongea Afande na kumfanya Cohen kutabasamu.

“Kweka nakumbuka nilikupatia mpango LADO peke yake , lakini sikukupatia nyaraka ambayo inahusiana na Zeros Organisation?”Aliongea

“Zeros Organisation!? Ndio Komredi”

“Najua unaelewa kwamba mpango LADO ulikuwa chini ya Zeros organisation na taifa la Marekani peke yake?”

“Ndio nyaraka ilivyoeleza”

“Okey Kweka kuna mambo mengine huyafahamu mpaka sasa labda nikusaidie kuyatambua kabla hatujaachia majukumu yetu yote kwa Hades”Aliongea na kumfanya Afande Kweka kujawa na shauku.

“Zeros organisation ni taasisi ya siri sana ambayo imeundwa na mataifa yenye nguvu duniani, yaani G20 , hii Habari ushawahi kuisikia?”Aliuliza.

“Hapana ni jambo jipya kwangu Komredi”

“ Ndio hivyo unatakiwa kuelewa , kwamba Zeros ipo chini ya mataifa 20 hivyo mpango LADO pia ulikuwa chini ya mataifa 20, nadhani unakumbuka nilivyokupatia nyaraka ya mpango LADO nilikuambia kuwa nilizipata kwa kupitia njia zangu za siri?”

“Ndio nakumbuka”

“Unakumbuka pia nilipokupa picha ya Rahel Adebayo sikukupatia maelezo mengine licha ya kukuambia mtoto wake atakaemzaa ahusishwe kwenye mpango LADO?”

“Ndio pia nakumbuka , ulisema utanipatia maelezo baada ya mpango kukamilika”

“Basi muda huu lazima nikupatie maelezo yote , kiufupi miaka ile kabla sijakuambia mpango LADO na kukupatia nyaraka, Denisi mjukuu wako alikuwa ndani ya mpango tayari na nilitumia tu ugonjwa wake wa saratani kukushawishi , lakini ukweli ni kwamba Denisi alizaliwa na mwili wa tofauti sana katika mfumo wake wa vinasaba vya damu , swala ambalo lilimfanya Hades wa zamani kutaka aingie kwenye mpango LADO, hivyo hivyo kwa mtoto wa Raheli aliekuwa tumboni”Aliongea na kumfanya Afande kweka kushangaa.

“Kwahio miaka ile Komredi Denisi aliingia kwenye mpango LADO si kwasababu ya mimi kutaka apone uongjwa wake bali ni kwasababu ya damu yake na kila kitu kilikuwa kimepangwa hivyo na Hades wa Zamani?”

“Nadhani sasa unanipata , sikutaka kukudanganya lakini Hades wa zamani alinipatia maagizo nisikueleze chochote na nitumie ugonjwa wa Denisi kukushawishi, lakini hata hivyo Hades aliamini kama Roma angeshinda kwenye mpango basi ugonwa wake ungepona lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakupona kabisa ugonjwa wake , lakini sayansi iliukubali mwili wake na aliendelea kuishi licha ya kuwa na saratani ya ubongo”

“Unamaanisha Roma hakupona Saratani ya Ubongo?”

“Kwa maelezo ya Hades wa zamani Roma hakupona Saratani ya ubongo ila sayansi iliowekwa kwenye mwili wake ndio iliomuwezesha kuishi na ugonjwa wa Saratani na naamini mpaka sasa bado ana ugonjwa wake , hatahivyo jambo ambalo ninataka kukueleza Zaidi ni hili la raisi Jeremy”Alivuta pumzi na kuendelea.

“Zile nyaraka za mpango LADO walizosaini pasipo ya uelewa wao si bado unazo?”

“Ndio ninazo na nilimuonyesha Senga na kumuonya asije akamwambia Jeremy kwa namna yoyote ile”

“Basi ni vizuri , kwanza kabisa kabla sijakuelezea kuhusu namna tunavyokwenda kushirikiana na Urusi, huyu Linda tumuache kwanza amueleze Jeremy kilichotokea ili kumfunga miguu asiendelee na mpango wake”

“Lakini hili swala lina mkono wa mrusi huoni kwamba hata kama yeye asipofanya Urusi itafanya kwani Ushahidi wote wanao?”

“Sio kweli Urusi wana Ushahidi ambao The First Black aliruhusu wawe nao , Urusi linaweza kuwa taifa kubwa lakini kwenye intellijensia hawako vizuri kama ilivyokwa CIA na hiki ndio kinamfanya raisi Nipitu ashinwe kutekeleza mipango yake, kabla sijakueleza mpigie simu Linda aongee na Jeremy amueleze kila kitu kilichotokea na baada ya hapo atajumuika na wengine kwenye kikao chetu”Aliongea na Afande Kweka alimpigia Linda na kumpa ruhusa ya kumueleza Raisi Jeremy.

“Sasa Kweka inabidi nikuelezee kwanini kwa sasa hatupaswi kumhofia mrusi bali tunatakiwa kumhofia huyu mwanamke Athena na mpango wake wa kufufua Roho zilizolala”Aliongea.

“Nakusikiliza Komredi”

“Okey ni hivi..”
 
SEHEMU YA 264

Aliekuwa mlangoni hakuwa mwingine bali ni Ashley mtoto wa raisi Senga na Edna alishangaa kumuona Ashley kwenye ofisi yake asubuhi hio.

“Edna..!!!”Aliita Ashley na Edna alitabasamu na kutoka kwenye kiti chake na kumsogelea Ashley na kumkaribisha kwa kumkumbatia.

“Karibu sana Ashley , umerudi lini?”

“Nina siku mbili Tanzania”Aliongea Ashley kwa furaha kabisa

“Boss mimi nitaondoka kama hakuna maagizo mengine”

“Naomba uendelee kufatilia kinachoendelea ndani ya kampuni ya MAYA”Aliongea na Suzzane aliitikia na kisha alitoka kwenye ofisi akimwacha Profesa Ashley mtoto wa raisi Senga akiongea na Edna.

“Edna nadhani sasa hivi nikuite wifi”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kushangaa.

“Kwanini jamani”

“Edna usijifanye na wewe hupo tayari kutupokea kama wanafamilia ,mimi na Roma ni kaka na dada hivyo wewe ni mume wake na inakufanya kuwa wifi yangu haha..”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kucheka na kuona aibu kwa wataki mmoja.

Ashley na Edna wanafahamiana sana na sio kwasababu Raisi Senga alikuwa na ukaribu na familia ya Adebayo , bali Ashley na Edna walisoma shule moja ya IST kwanzia darasa la kwanza mpaka la saba, hivyo ni rahisi kusema kwamba Ashley , Mage , Magdalena na Edna walisoma shule moja na walikuwa marafiki wote kipindi cha utoto wao na ni Ashley ndio aliekuwa akiwaburuza darasani wanafunzi wote na nafasi ya pili ilikuwa ikishikiliwa na Edna.

“Edna nilikuja nyumbani nikaambiwa umekuja kazini ndio nikaona nije moja kwa moja kukuona kwani sina muda mrefu nataka kurejea Uingereza”Aliongea

“Mh! wewe nae na Uingereza yako , hujawahi kuipenda Tanzania wewe tokea uende masomoni”

“Sio kweli Tanzania naipenda , lakini mazingira yake na taaluma yangu ni vitu viwili tofauti , Serikali za wenzetu zinawapa sapoti sana wanasayansi kuliko hapa Tanzania”Aliongea na Edna alimuunga mkono.

“Sasa ni kipi ambacho unataka kuongea na mimi?”Aliuliza Edna.

“Hehe… kabla ya yote nilitaka kumuona mke wa kaka yangu kabla ya kurudi uingereza”Aliongea na kumfanya Edna kujisikia vizuri, kila mwanamke alieolewa mawifi wakikupenda basi unajiona kuwa na bahati ,na hio ndio ilikuwa kwa Edna , kupendwa na wifi yake Ashley hakuliona jambo baya, alijishangaa pia mambo yao na Roma yalivyoanza , lakini kadiri siku zinavyoenda mahusiano yao yanachukua sura mpya kila siku.

“Edna nimekuja kukuambia siri yangu ila nataka uniahidi kama hutomwambia Roma”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa.

“Niambie siri yako itakuwa siri yangu”

“Hehe. Umenikumbusha wakati tukiwa Watoto ulizoea kusema hivyohivyo lakini mwisho wa siku siri zangu ulimwambia mama yako”Aliongea Ashley na kumfanya Edna akumbuke na kuona aibu.

“Ule ulikuwa utoto , saivi mimi mkubwa na hata hivyo mama ndio mtu niliekuwa nikimwambia siri zangu na sasa hivi hayupo tena”Alionge akinyongea kidogo.

“Usijali Edna, mimi wifi yako nakupenda sana, Edna mimi nilijua kuwa wewe ni wifi yangu tokea siku uliokuja Ikulu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa kidogo.

“Unataka kumaanisha nini Ashley?”

“Namaanisha kwamba nilimfahamu Roma kabla yako hio ndio siri yangu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa Zaidi.

“Unasema kweli?”

“Ndio namfahamu Roma huenda kuliko unavyomfahamu wewe , mimi Roma nilimfahamu ni kaka yangu kabla hata hajaja huku Tanzania”Edna alishangazwana jambo hilo mno.

“Hebu nielezee vizuri”Aliongea.

“Usijali nipo hapa kukuelezea kila kitu ninachokijua kuhusu Roma”Aliongea Ashley na kumfanya Edna kujawa na shauku Zaidi, ijapokuwa alikuwa akitaka Roma ndio amwambie mwenyewe historia yake ya nyuma lakini swala la Ashley kumjua Roma lilimgusa na kutamani kujua.

“Kwa muonekano wako unaonekana Roma hajakueleza Maisha yake ya nyuma?”

“Ndio Ashley najua ana historia ya kipekee lakini sijawahi kupata kuijua”

“Mh ! Basi mimi nitakuelezea kwa upande wangu nilivyomfahamu Roma”Aliongea Ashley na Edna alikaa kitako kutaka kusikiliza histori ya Roma , alikuwa na hamu ya kujua Maisha ya nyuma ya Roma , lakini alikuwa akisita sana kumuuliza Roma mwenyewe.

********

Roma jana yake alienda kwa Nasra lakini alivyofika hakumkuta na alijaribu kumpigia simu lakini pia haikuwa ikipatikana , lakini hata hivyo hakuwa na wasiwasi na aliamua Kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Dorisi ili kumsalimia kwani ni muda kidogo hakuwa ameonana nae na alivyofika alimkuta na Dorisi alifurahishwa na ujio wa Roma na Roma alidumu nyumbani kwa Dorisi kwa masaa matatu mpaka alipoaga kuelekea Mbagala kwa ajili ya Rose , alikuwa amemkumbuka Rose hivyo alijiambia hawezi kumaliza siku pasipo ya Kwenda kumuona.

Na usiku ndio aliumalizia huko na asubuhi ya saa tatu ndio alionekana akiingia ndani ya nyumba yake anayoishi Pamoja na familia yake.

Roma baada ya kumaliza kuegesha gari moja kwa moja alitembea mpaka ndani na kumkuta mama yake akiangalia Runinga Pamoja na Bi Wema , lakini jambo lililomshangaza pia Mage na Magdalena walikuwepo.

“Roma wageni wako wanakusubiria”Aliongea Blandina baada ya kusalimiana na mtoto wake.

“Mama tutaongelea hapo nje”Aliongea Magdalena na kisha alitoka wa kwanza akimuacha Mage anaemkagua Roma.

Roma aligeuza na kisha alianza kutembea mpaka nje huku nyuma akifuatia Mage na walikuja kusimama kwenye bustani.

Mapacha hao walionekana warembo kweli kiasi cha kumfanya Sophia kukaa juu ya balcony na kuchungulia chini kile kinachoendelea , kwani yeye dakika kadhaa zilizopita ndio aliwapokea Mage na Magdalena sasa baada ya kuona wamekuja kwa ajili ya Roma alifikiria ni lazima watakuwa sehemu ya michepuko yake na ndio maana alishindwa na wivu kiasi cha kumpekea kupanda juu ya Balconi kuangalia kinacheondelea.

Roma alimwangalia Mage na kisha akamkonyeza na kumfanya Mage kuona aibu.

“Hivi Roma kwanini huna wasiwasi na sisi ndio tunaonekana kuwa na wasiwasi?”Aliuliza Magdalena huku akiweka kibesi.

“Magdalena usiniambie ni yaleyale ya Salah , mimi swala lile niliachana nalo muda uleule ulionipigia”Aliongea Roma na kumfanya hata Mage amshangae.

“Yaani umeua halafu unasema umeachana nalo , unajua hata mtu uliemuua kweli”Aliongea Magdalena.

“Magdalena kama unaona huyu mwanaume niliemuua ni wa spesho sana ni bora ukaniweka wazi ni nani haswa na kwanini unaogopa kuniambia”Magdalena alivuta pumzi.

“Ushawahi kusikia makampuni ya MAYA hapa Tanzania au popote ndani ya Afrika?”Aliuliza Magdalena na Roma hakuwa akifahamu kampuni ya MAYA kwani hakuwa mtu wa kufatilia sana Habari za watu ambao hawamhusu.

“Unaonekana haumfahamu basi ni hivi ni hivi mtoto uliemuua jana baba yake ndio mmiliki wa Makapuni ya MAYA”Aliongea.

“Maya Hubat ndio mmiliki wa makampuni hayo”

“Okey Magdalena tusema huyu Maya Hubat ni mtu mzito hapa nchini , mnachotaka mimi kufanya ni nini maana mimi sio Mungu niweze kurudisha uhai mtoto wake , mnaonaje mkienda moja kwa moja kwenye swali mlilokuja nalo”Aliongea Roma.

“Unachukulia mambo kwa wepesi sana..”

“Roma tunachotaka ni wewe kukana kuhusika kuwa muuaji wa Salah”Aliongea Mage na kumfanya Roma kwanza atabasamu.

“Kwanini napaswa kufanya hivyo?”

“Roma tunakusaidia ili kuepuka swala hili, unaweza ukachukulia poa swala la Salah ila Mzee Maya hagusiki kwa namna yoyote ile na anao uwezo mkubwa wa kukuangamiza na hata raisi mwenyewe hana uwezo wa Kwenda nae kinyume”

“Afande Mage huu ni msimamo wangu “

“Mimi Roma Ramoni nimemuua Salah nikiwa na akili zangu timamu kwa kumkosea heshima mke wangu kwa kitendo chake cha kumdhalilisha hivyo sipo tayari kukana adhabu ambayo nimeitoa kwani nitakuwa naenda kinyume na sheria nilizojiwekea, Ukifanya jambo na nafsi yako ikakuhumu basi jua umetenda dhambi , mimi nafsi yangu hainihukumu licha ya kwamba nimemuua Salah , hivyo haina haja ya kuhangaika”Aliongea Roma na kisha aliwaacha Mage na Magdalena wasijue cha kufanya lakini kabla ya Roma hajakaribia mlango wa kuingia mara alijikuta akisimama na kisha akageuka na kutabasamu kifedhuli , alihisi msuguano wa hewa ambao sio wa kawaida na sio kwake tu hata kwa Magdalena ilikuwa hivyohivyo.

“Denisii.!!!”Aliiita Sophia aliekuwa juu baada ya kumuona Denisi akiruka ukuta kama vile fisi na kutua kwenye eneo la Bustani.

ITAENDELEA

Haya Denisi huyo hapo , nini kitatokea
Nicheki watsapp 0687151346
 

Daaah genius sana singano jr hata sijui lini tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…